Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

BODI YA UTALII TANZANIA (TTB), YAANDAA ONESHO LA SITES KUFANYIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY OKTOBA MOSI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu Onesho la Sites litakalofanyika Oktoba Mosi hadi 3, 2015 Ukumbi wa Mlimani City. Kushoto ni Ofisa Mauzo Mkuu wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Lima Dsilva na  Meneja Huduma wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Dawit Mekonnen. 

 Meneja Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Sebastian (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni   Ofisa Mauzo Mkuu wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Lima Dsilva na  Meneja Huduma wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Dawit Mekonnen, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi na Ofisa Uhusiano Mkuu wa TTB, Geofrey Tengeneza.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.



Na Dotto Mwaibale

KAIMU Mkurugenzi Mwendeshaji, bodi ya Utalii nchini, Devotha Mdachi, alisema ufinyu wa bajeti ya matangazo katika sekta ya utalii unasababisha  sekta hiyo, kutofanya vizuri ukilinganisha na nchi nyingine.

Mdachi aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akitolea
ufafanuzi wa onesho la utalii nchini, linalotarajia kufanyika Oktoba mosi hadi 3 mwaka huu linalojulikana kama Sites.

Kaimu mkurugenzi huyo alisema kuwa bajeti finyu iliyotengwa na Serikali katika kutoa matangazo ya utalii wa ndani ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine zinavyojitangaza duniani.

Pia, alisema kutokuwa na ofisi za bodi ya utalii katika kila mkoa
na kutokuwa na Shirika la Ndege la Taifa kusababisha utalii wa ndani kuwa mdogo.

“Wenzetu wa Kenya bajeti yao ya matangazo ya utalii ni kubwa
ukilinganisha na sisi kwani wao wametenga bilioni 36 katika
matangazo, lakini sisi bajeti yetu ya matangazo ni finyu sana ambapo ni bilioni 2.3,” alisema Mdachi

Kwa upande wake, Meneja huduma za utalii nchini ambaye
pia ni Mratibu Mkuu bodi hiyo, Sebastian Philip alisema onesho hilo litakutanisha wafanyabishara wa hapa nchini kutoka kwenye masoko ya utalii, hivyo ni vema watanzania kutumia fursa hiyo kuhakikisha kunaleta soko kubwa la utalii nchini.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com


MBUNGE WA SINGIDA MJINI MO DEWJI AWAAGA WANANCHI WAKE,KUTOGOMBEA TENA JIMBO LAKE

0
0
IMG_7558
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_7562   
"Tulifanikiwa kujenga wodi ya macho, ndani ya hospitali yetu ya mkoa. Tulifanikiwa kuchangia ujenzi, wa zahanati za Mungumaji, na Manga ambazo zimekamilika! na zahanati ya kijiji cha Ititi ambao bado ujenzi unaendelea." alisema.

Pamoja na ujenzi huo pia alielezea mafanikio ya kusaidia baiskeli kwa walemavu na kufunga solar panel, pamoja na majokofu ya kutunzia dawa, kwenye zahanati za Manga na Unyambwa!
Akifafanua zaidi katika sekta ya elimu alisema kwamba walijenga vyumba vya madarasa, kuweka matangi ya maji ya kuvunia maji ya mvua, vyoo, na kusambaza madawati katika shule mbali mbali za msingi na sekondari jimboni Singida mjini.

Aidha alichangia vitabu zaidi 1000, vya masomo ya sayansi na sanaa, kwa shule zetu zote, za serikali ndani ya manispaa, ya Singida na tulifanikiwa, kuwapeleka wanafunzi wa shule ya msingi Ukombozi kwenye ziara ya kujifunza bungeni.

Akizungumzia sekta ya maji walifanikiwa kuchimba visima viwili kwenye mtandao wa Suwasa na vingine 45 ndani ya baadhi ya vitongoji vyetu vya manispaa ya Singida. Aidha alisema alifanikiwa kusukuma mradi wa visima 10, unaofadhiliwa na benki ya dunia, akisisitiza kuwa wakati akiingia mwaka 2005 upatikanaji wa maji safi na salama ulikua asilimia 23 na sasa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 81.

Pia alisema amefanikiwa kuisukuma serikali, kujenga barabara za kiwango, cha changarawe ndani ya manispaa na kufanya manispaa kuwe na barabara zinazopitika kwa kipindi chote!
IMG_7530
Mkazi wa Singida mjini akimwomba Mbunge wake asiache ngazi kwa maana bado wanamuhitaji baada ya kutangaza kutogombea tena.

Akiwashukuru wananchi wa Singida alisema kwamba: "kuwatumikia ninyi imekuwa ni tunu kubwa sana niliyo-barikiwa katika kipindi hiki cha miaka 10, na najisikia kuwa nimependelewa kwa kujifunza mambo mengi yanayohusu Singida na uongozi bora, na hususan mapungufu yake, ikiwemo mimi mwenyewe."

Alisema dhamira yake kwa wananchi haitokani na nafasi yangu kama mbunge ama mwanasiasa, akisisitiza kuwa dhamira yake ya uzaliwa inayotokana na mapenzi aliyonayo kwao na imani aliyonayo juu ya uwezo wa kuijenga Singida.

"Mapenzi yangu na imani yangu kwenu hayapimiki, na ninapenda kuwahakikishia leo kuwa, haya yatajitokeza katika njia nyingine nyingi tu." Alisema pamoja na kutokugombea katika muhula wa tatu, lengo lake kuu la kutumikia wananchi wa Singida linabaki pale pale.

"Naomba nitoe ahadi kwenu! nitaendelea kushirikiana, na kada wa CCM, mtakaomchagua, kwenye nafasi hii ya ubunge katika shughuli zote za maendeleo ya jimbo letu! kwani dhamira yangu, ya kushirikiana nanyi, kujiletea maendeleo, haikuwa lazima mimi niwe mbunge, bali ilitokana na mapenzi yangu, kwa Singida na watu wake! "
IMG_7549
Mwanamama huyu akiwa haamini macho yake huku machozi yakimlenga lenga baada ya kusikia Mbunge wake kutogombea tena ubunge wa jimbo la Singida mjini.

IMG_7533
Watoto hawa machozi yakiwalenga na kuonyesha huzuni baada ya kumsikia mbunge wao akitangaza kuachia ngazi jimbo la ubunge wa Singida mjini.
IMG_7533IMG_7535
Wananchi wa Singida wakisikiliza hotuba ya mbunge wao.
IMG_7536IMG_7567
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na mkazi wa kijiji cha Kinyampembe kata ya Meria ambaye ni mlemavu wa macho na miguu aliyefahamika kwa jina moja tu la Kangariga wakati wa hafla ya mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka ya ubunge wake, ambapo aliitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena jimbo la Singida mjini jana katika viwanja vya People's Club.
IMG_7402
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akiingia jukwaani na dancers wake kuwapa burudani wananchi wa Singida mjini.
IMG_7588
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akitumbuiza wananchi wa Singida mjini wakati wa mkutano mkubwa wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo hilo.
IMG_7428
Pichani juu na chini ni Diamond Platnumz na ma-dancers wake wakishambulia jukwaa.
IMG_7440
IMG_7445
Umati wa wananchi wa Singida ukiwa uchizika na burudani ya Diamond Platnumz.
IMG_7447
IMG_7453
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote na dancers wake wakitia mbwembwe kwenye show ya kukata na shoka katika viwanja vya People's Club, Singida mjini.
IMG_7454
Chibu Dangote akishambulia jukwaa na dancers wake.
IMG_7471
IMG_7476
IMG_7478
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote katika hisia kali kuwapa raha maelfu ya wananchi wa Singida mjini.
IMG_7481
Umati wa maelfu ya wananchi wa Singida mjini uliokusanyika katika viwanja vya People's Club kusikiliza taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya ubunge wa Mh. Mohammed Dewji.
IMG_7610
IMG_7617
IMG_7626
Vijana wakimshangilia Chibu Dangote.
IMG_7629
Kijana wa Singida mjini (mwenye vest) akiimba jukwaa moja na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote.
IMG_7642
IMG_7633
Ngolololo...cha ngololo now, show me how the do ngololo...Chibu Dangote akionyesha madoido yake kwa wananchi wa Singida mjini.
IMG_7645
Shangwe za wananchi wa Singida mjini.
IMG_7675
Chibu Dangote akiwapa mikono wakazi wa Singida mjini wakati akiwaaga mara baada ya kutumbuiza.
IMG_7712
Kijisehemu cha maelfu ya wakazi wa Singida mjini waliojitokeza katika mkutano uliotishwa na Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji ambaye amewaaga rasmi.
IMG_7716
Kwenye moja na mbili alihusika DJ, Rommy Jones (kulia) akishow love na mmoja wa ma-dancers wa Diamond, Moses Iyobo.
IMG_7728
Videographer wa MO kutoka Sofia Production, Yusuf Kissoky akichukua matukio muhimu ya kumbukumbu.
IMG_7735
Msafara wa Mh. Mohammed Dewji na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ukiondoka katika viwanja vya People's Club.

Na Modewjiblog team, Singida
MBUNGE wa Singida mjini na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema hatagombea ubunge wa jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa miaka 10 na kuwezesha maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na afya.

Mbunge huyo alisema hayo akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa People's Club (MB) wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo.Katika utekelezaji huo ametumia shilingi bilioni 5.
Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia kuongeza shule za sekondari kutoka mbili hadi 15, kuwapo kwa vituo vya afya na kupeleka shule watu wenye mazingira magumu elfu 15.
Alisema ametekeleza majukumu yake ya kusukuma maendeleo katika jimbo lake la uchaguzi kwa ushirikiano mkubwa na kufanikisha vipaumbele vya wakati huo ikiwamo elimu na Afya
Alisema kwamba kujiondoa kwake katika siasa za jimboni kunatokana na majukumu ya biashara zake kuwa makubwa pamoja na kutaka kuwa karibu na familia yake baada ya miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.
"Ukichukulia kuongezeka kwa-mvi kichwani, ukilinganisha wakati wa awamo ya kwanza, nafikiri ni busara sasa kutimiza majukumu haya ya familia ambayo niliyabania nafasi yake kwa kipindi cha miaka 10.
"Pia siyo siri kwamba majukumu ya biashara zangu yamebadilika katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. ukuaji wa biashara zangu umeambatana na kuongezeka kwa majukumu, hususan mahitaji ya muda zaidi.
Mtazamo huu wa kuipa biashara muda zaidi ni muhimu sana kwa sababu mafanikio yangu kwenye biashara ndiyo yaliyoni-wezesha kuwatumikia, na yatakayo-niwezesha kuendelea kuwatumikia wananchi wa Singida kwa vitendo." alisema.
Akizungumzia sekta ya afya alisema wananchi wa Singida walifanikiwa kukabiliana vilivyo na ugonjwa hatari wa Malaria kwa kugawa vyandarua zaidi ya vyandarua 6000 kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
"Kwa kusambaza vyandarua hivi, tulifanyikiwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa asilimia hamsini" alisema akishangiliwa.
Aidha alishirikiana na mamlaka husika kupambana na ugonjwa sugu wa mtoto wa jicho kwa kupeleka madaktari bingwa na kufanya kambi kwenye hospital ya mkoa, waliotoa huduma ya upasuaji wa jicho na kutoa miwani kwa zaidi ya wananchi 1,000.

UPENDO KILAHIRO KUMPIGA TAFU BONNY MWAITEGE

0
0
MUIMBAJI  mahiri wa muziki wa Injili Tanzania anayeshika kasi katika anga la muziki huo Afrika Mashariki na Kati, Upendo Kilahiro anatarajia kumsindikiza mwenzake Bonny Mwaitege anayetarajia kuzindua albamu tatu mfululizo, uzinduzi unaotarajia kufanyika Agosti 2.  

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, Kilahiro ataungana na Kwaya ya Wakorintho wa pili ya Mufindi mkoani Iringa.
Msama alisema Kwaya hiyo ni mojawapo  ya watakaomsindikiza mwimbaji huyo kwa sababu hivi sasa sambamba na Kilahiro.

“Uzinduzi  wa  albamu tatu za Bonny Mwaitege unatakiwa kufanyika kwa maandalizi ya hali ya juu ambayo yanafanyika kwa mfumo  wa kisasa,” alisema Msama na kuongeza. “Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi mkubwa  hasa hatua za mwisho za rekodi ya albamu hizo inayomaliziwa  jijini Mwanza na baadaye Nairobi,” alisema Msama.

Msama alisema sambamba na muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa albamu hizo. Aidha Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa kupata neno la Mungu kupitia muimbaji huyo.  Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo.

AFRIKA KUSINI YAKABILIWA NA TABIANCHI KWENYE MIJI YAKE MIKUBWA

0
0
DSC_1900Mkufunzi na mtafiti, Daktari John Odindi, kutoka chuo kikuu cha KwaZulu-Natal, Durban nchini Afrika Kusini (kulia) katika mahojiano maalum na mwandishi wa Habari mwandamizi wa blog ya modewjiblog.com, Andrew Chale kwenye mkutano wa wanasayansi juu ya mabadiliko ya tabianchi, unaoendelea kwenye ukumbi wa Makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa (Picha na Mpiga picha maalum).

Na Andrew Chale, Modewjiblog
[Paris, Ufaransa] Watafiti kutoka chuo kikuu cha KwaZulu-Natal, Durban nchini Afrika Kusini wamewasilisha mada juu ya mabadiliko ya tabianchi kuhusiana na ongezeko la joto kwenye miji (urban temperature increase) ya Durban, East London na Port Elizabeth kwenye nchi hiyo.

Mada iliyowasilishwa na Daktari John Odindi katika mkutano mkubwa wa wanayasansi juu ya siku za usoni na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ‘Our Common Future Under Climate Change’ unaofanyika kwenye makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa. Mkutano huo wa siku nne (Julai 7-10) unawajumuisha wanasayansi zaidi ya 2500 kutoka pembe zote duniani.
Akizungumza katika mahojiano maalum, Dk. Odindi ambaye ni mkufunzi na mtafiti anasema hali ya ongezeko la joto ni kubwa na kupitia utafiti huo wanashauri jamii kuchukua hatua dhidi ya kukabiliana nayo.

“Utafiti wetu tuliowasilisha ni tumeangalia namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi dhidi ya joto katika miji hii kwani linakuwa kubwa kutokana na ongezeko la makazi mengi ya watu, viwanda na shughuli za kila siku za wananchi” alibainisha Dk. John Odindi.
Dk. John Odindi anashauri uhifadhi na utunzaji wa mazingira ya asili ikiwemo mimea, chemichemi za maji ya asili na mito kulindwa kwani vitu hivyo ndivyo vinavyosaidia kupunguza hali ya joto mijini.

Hivyo ansema kupitia mkutano huu wa Wanasayansi, kuelekea mkutano mkuu wa 21 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiriko ya Nchi (COP21) utakaofanyika Paris , Desemba mwaka huu, anatumai kwamba mataifa yatajumuika kutafuta muafaka za kupunguza kiwango cha joto duniani.

Pia anabainisha kuwa, nchi ya Afrika Kusini imejidhatiti katika kukabiliana na hali hiyo ya tabianchi katika ongezeko la joto mijini kwani mkutano wa COP17, ulifanyika katika jiji la Durban, Afrika Kusini. Mada hiyo inaenda sanjari na matakwa ya mataifa mbalimbali juu ya kukabiliana na kiwango cha hali ya joto na nyuzi mbili (to reduce temperature level by 2 degrees).
19494771666_060632cea2_oBaadhi ya wanasayansi hao wakiwa katika mkutano huo unaendelea katika ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa.. (Picha kwa hisani ya Christophe Maitre, INRA).

SIARA LEONE WAZURU NHIF KUJIFUNZA JINSI YA KUNDESHA MFUKO HUO KATIKA NCHI YAO

0
0
 Waziri wa Kazi na Hifadhi ya Jamii wa Siara leone,Dk.Mathew Teamba (Mwenye Tai nyekundu) akiwa Wajumbe nchi hiyo  waliokuja kutembelea  Mfuko wa  Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ili kujifuza na kwenda kutekeleza katika nchi yao  hafla hiyo imefanyika katika  ofisi za Makao Makuu  leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa uanachama wa NHIF,Twahiru Hauke  akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Kazi Maalum wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Siera leone,Mohamed Godoe walipotembelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Kazi na Hifadhi ya Jamii wa Siara leone,Dk.Mathew Teamba (Mwenye Tai nyekundu) akipewa maelezo na Msimamizi wa Mifumo ya Komputa  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jinsi ya kuhifadhi  nyaraka za wananchama wa NHIF  walipotembelea  leo ofisi za Makao Mkuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo jijini Dar es Salaam.4
 Mkurugenzi wa Masoko wa NHIF ,Rehan Athuman akizungumza na waandishi wa habari juu ya ugeni waliopokea kutoka  nchini Siara leone leo katika ofisi za Makao Makuu ya NHIF jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Hifadhi ya Jamii wa Siara leone,Dk.Mathew Teamba akizungumza na waandishi wa habari juu ziara ya kutembelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF walipofika katika Makao Makuu ya leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

SIKU YA PILI YA WARSHA YA WADAU JUU YA MIPANGO YA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIA NCHI

0
0
 Bwana Masinde Bwire kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira akiwasilisha mada juu ya mabadiliko ya Tabia Nchi kwenye warsha ya Wadau kuhusu mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
 Profesa Kangarawe akiwasilisha mada katika warsha hiyo mjini Bagamoyo.
 Sehemu ya Wadau waliohudhuria wrsha hiyo wakifuatilia kwa makini uwasilishaji mada juu ya mabadiliko ya Tabia Nchi.
Wajumbe waWarsha hiyo wakiwa katika magrupu kwa ajili ya kujadili kile walichofundishwa katika warsha hiyo.

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA UKUMBI MPYA WAMIKUTANO WA CCM, MJINI DODOMA LEO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Kikwete, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo mjini Dodoma, leo Julai 9, 2015.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Kikwete, akibonyeza kitufye cha kengere kuashiria uzinduzi rasmi wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo maeneo ya ..... mjini Dodoma, leo Julai 9, 2015.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Kikwete, na Balozi wa China nchini Tanzania, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo mjini Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Julai 9, 2015.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, Katibu Mkuu wa CCM Bara, Abrahman Kinana, baada ya kuzindua rasmi ukumbi huo leo, mjini Dodoma.
Picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali baada ya uzinduzi huo.

 
 Rais Jakaya Kikwetena baadhi ya Viongozi, wakitembelea kukagua ukubi huo baada ya uzinduzi.
Picha ya pamoja baada ya kutembelea kukagua ukumbi huo. Picha na OMR

AIRTEL FURSA YATUA MWANZA

0
0
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na vijana
wa Mwanza wakati wa uzinduzi  wa warsha maalum kwa vijana  ya'Airtel
Fursa'  kutoka Airtel Tanzania yenye lengo la kuwawezesha Vijana
wajasiliamali nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji
Mwanza.
 Baadhi ya vijana wa mwanza wakifuatilia kwa makini mafunzo yalikuwa
yakiendeshwa na Airtel Fursa yenye lengo la kuwawezesha vijana kupata
mafunzo kwenye usimamizi wa fedha, upatikanaji wa mikopo, kufungua
akaunti ya benki na mambo muhimu katika kuendesha biashara. Warsha
hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji Mwanza.
 Meya Stanslaus Mabula akiongea na vijana Mwanza wakati wa uzinduzi  wa
warsha maalum kwa vijana  ya'Airtel Fursa'  kutoka Airtel Tanzania
yenye lengo la kuwawezesha Vijana wajasiliamali nchini iliyofanyika
katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji Mwanza.
 Mtaalamu wa maswala ya kijamii na ujasiliamali bw, Fidelis Madaha
akifundisha mada ya Masoko katika warsha ya Airtel fursa iliyofanyika
katika ukumbi wa halmashauri ya jiji jana. Airtel inaendesha warsha
hizo kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata mafunzo kwenye usimamizi
wa fedha, upatikanaji wa mikopo, kufungua akaunti ya benki na mambo
muhimu katika kuendesha biashara.

ATHARI ZA MADINI YA ZEBAKI KATIKA MWILI WA BINADAMU

0
0
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya  Makamu wa Rais Anjelina Madete(katikati)  akifungua mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka ofisi hiyo, Joseph Kihaule na  kushotoni Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren.
 Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Joseph Kihaule (kushoto)akisisitiza jambo wakati akiongoza mkutano wa Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam, kulia ni Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren.
Issaria Mangalili akitoa mada juu ya mikataba mbalimbali inayohusu kemikali mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.
 Mhandisi Peter Nyangombe (wa pili kushoto) akitoa mada juu ya Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.
 wadau wa mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana wakijadiliana  jambo  kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.
 Picha ya pamoja kati ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya  Makamu wa Rais Anjelina Madete(wa pili kushoto)  mara baada ya kufungua mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka ofisi hiyo, Joseph Kihaule na  (wa pili kulia) ni  Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa mazingira kutoka ofisi hiyo, Rogathe Kisanga.
Picha na Magreth Kinabo – Maelezo

MEMBE ASISITIZA UMUHIMU WA VIWANDA

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.), akiongea kwenye muhadhara kabla ya Mtoa mada mkuu Prof. Justin Yifu Lin hajaongea katika muadhara uliokuwa unazungumzia umuhimu wa viwanda nchini ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje.
Makamu wa Rais wa zamani wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin akitoa mada yake juu ya uwanzishaji wa viwanda nchini Tanzania katika muadhara ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya (Kulia), na kushoto ni Balozi Mstaafu Mhe. Elly Mtango wakisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Lin (hayupo pichani). 
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza kwa makini Prof. Lin (hayupo pichani), Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Nigel Msangi, Kushoto ni Afisa Mawasiliano mwandamizi wa Mambo ya Nje Bw. Ally Mkumbwa nao wakifuatilia kwa makini Muhadhara uliokuwa ukiendelea.

 
Balozi Simba akichangia mada katika muadhara uliokuwa ukiendelea.
Muhadhiri Chuo cha Diplomasia Bw. Innocent Shoo akiuliza swali.
Afisa Mambo ya Nje Bi. Felisita Rugambwa naye akiuliza swali katika muhadhara.
Dkt Lin akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kulizwa.
Picha ya juu na chini ni watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje nao wakisikiliza mada kwa makini.
KKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akitoa neno la shukrani kwa Prof. Lin, kwa niaba ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya kumalizika kwa muhadhara huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo huku akisikilizwa na Prof. Lin (Kulia) na Mhe. Membe (Katikati). 
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Diaspora Bi. Rosemary Jairo akizungumza jambo kwa Prof. Lin (kushoto) na Katibu Mkuu Balozi Mulamula.
Picha na Reginald Philip
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, amesema upatikanaji wa gesi ni nyenzo muhimu ya uendelezaji wa viwanda vya kati ili kutengeneza ajira na kuharakisha maendeleo ya nchi.
Mhe. Membe alipongeza uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu za Afrika itakapohamishia baadhi ya viwanda vyake, akazitaka taasisi za uwekezaji na uendelezaji wa viwanda kuweka mikakati madhubuti ya kutumia fursa hiyo kikamilifu.
Mhe. Waziri alisema hayo leo wakati wa mhadhara wa aliyekuwa Mchumi Mkuu na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar Es Salaam, uliohudhuriwa na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na wadau wengine.
Alisema uendelezaji wa viwanda lazima utiliwe mkazo katika mpango wa Tanzania kuingia uchumi wa kati 2025. "Tuache kukimbilia viwanda vikubwa vinavyohitaji mitaji mikubwa, ambayo hatuna.

Tuchague viwanda vya kati vitakavyoajiri watu wengi kwa uwekezaji wa wastani."
Mhe. Membe alisema uendelezaji wa viwanda usambae nchi nzima ili kuvutia vijana kuishi vijijini badala ya kukimbilia mijini. "Sasa hivi nchi yetu ina viwanda takriban 3,000 lakini zaidi ya theluthi mbili viko Dar Es Salaam. Lazima umeme upelekwe vijijini kuleta uwiano wa maendeleo ya viwanda," alisisitiza.
Katika mhadhara wake, Prof. Lin alisema nchi nyingi zinazoendelea zilifanya maamuzi yasiyo sahihi kuhusu viwanda. "Nchi nyingi zilifuata kile kinachoitwa Muafaka wa Washington na kuanzisha viwanda vikubwa kwa maelekezo ya nchi tajiri, ambavyo viliwashinda kuendesha kwa kuwa vilihitaji uwekezaji mkubwa sana."
Alisema nchi za Asia zilizoendelea kwa haraka ni zile zilizoamua kuzingatia mazingira halisi na kwenda hatua kwa hatua katika kuanzisha viwanda. "Hii iliimarisha uchumi wao na kuukuza."
Prof. Lin alisema serikali zina wajibu wa kusimamia uendelezaji wa viwanda kwa kuweka sera sahihi, kuhimiza uwekezaji kwenye uzalishaji wa bidhaa zenye masoko ya uhakika na kusaidia sekta binafsi ishiriki kikamilifu.
Akiongelea Tanzania, Mchumi huyo wa Kichina alisema ingawa gharama za ajira ziko chini, gharama za uendeshaji ziko juu, hivyo hazivutii uwekezaji. Alisema moja ya sababu kubwa za Shilingi ya Tanzania kushuka thamani ni uuzaji mdogo wa bidhaa nchi za nje.

WAANDISHI WA HABARI WACHANGISHA MILIONI 31 KUSAIDIA WENZAO

0
0

Mwenyekiti wa Kampeni iliyolenga kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu yakiwepo ya saratani, (MEDIA CAR WASH FOR CANCER) , Benjamin Thompson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kiasi cha fedha kilichopatikana katika harambee ya jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi Milioni 31 zilipatikan ikiwa ni ahadi na taslimu. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa. Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kampeni iliyolenga kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu yakiwepo ya saratani, (MEDIA CAR WASH FOR CANCER) , Benjamin Thompson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kiasi cha fedha kilichopatikana katika harambee ya jijini Dar es Salaam leo, ambapo kiasi cha shilingi Milioni 31 zilipatikan ikiwa ni ahadi na taslimu. Pamoja nao ni Wajumbe wa Kamati hiyo Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa (kulia) na Judicate Shoo.Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa katika mkutano huo hii leo. Kutoka kushoto ni Mroki Mroki, Leah Samike, Judicate Shoo, Mwenyekiti Benjamin Thomson, Zamaradi Kawawa, Angela Michael Msangi, Grace Nakson na Somoe Ng'itu. Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.

WANAHABARI WAPEWA SEMINA KUHUSU WIKI YA USALAMA BARABARANI YA UMOJA WA MATAIFA DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua semina hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi.
 Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi (kulia), akizungumza katika semina hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed kufungua semina hiyo. 

 Ofisa Mradi wa Usalama Barabarani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Marry Kessy (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa mada kwenye semina hiyo.
 Mkaguzi wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Mossi Ndozero (kulia), akitoa mada kwenye semina hiyo.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Safe Speed Foundation, Henry
 Bantu akizungumza kwenye semina hiyo.
 Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mary Kitambi akitoa mada kuhusu sekta ya Afya inavyokabiliana na changamoto za utoaji huduma kwa wagonjwa wanaopata ajali.
 Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
 Semina ikifunguliwa.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye 
semina hiyo.
 Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.


Dotto Mwaibale

WATOTO 1, 86, 300 wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ajali za magari duniani hivyo kuwa changamoto kubwa ya usalama barabarani.

Hayo yalibainishwa na Ofisa Mradi wa Usalama Barabarani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Marry Kessy wakati akitoa mada kwa wanahabari kwenye semina ya siku moja ya wiki ya umoja wa mataifa ya usalama barabarani iliyofanyika Dar es Salaam leo.

"Hii ni changamoto kubwa duniani na hapa nchini kwani kati ya watoto hao idadi kubwa ya wanaopoteza maisha katika ajali hizo ni watoto wa kiume" alisema Kessy.

Mkaguzi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani, Mossi Ndozero alisema kumekuwa na changamoto nyingi zinazotokana na masuala ya usalama barabarani ikiwemo ukiukwaji wa sheria za barabarani unaosababishwa na binadamu.

Ndozero aliwataka watumiaji wa vyombo vya moto kuwa makini wawapo barabarani na kufuata sheria jambo litakalo saidia kupunguza changamoto hiyo ya ajali kama sio kuisha kabisa.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Safe Speed Foundation, Henry Bantu alisema maendeleo ya dunia yamesababisha ongezeko la magari barabarani hususan nchini Tanzania hivyo kuongeza ajali za barabarani.

Bantu aliwataka watanzania kujenga utamaduni wa usalama barabara ambao hatuna jambo litakalo saidia kupunguza ajali kwa kusaidiana na wadau wengine.


Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mary Kitambi alisema ajali zinazotokea nchini zimechangia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa hivyo kuwa changamoto katika hospitali mbalimbali nchini kutokana na wodi kutokidhi ongezeko la wagonjwa na vifaa tiba.

Alisema kilele cha maadhimisho ya wiki ya umoja wa mataifa ya usalama barabarani yatafanyika Julai 15 mwezi huu Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam.

Asya Idarous Khamsin na Titty wanakuletea futari ya pamoja ndani ya Terrace Lounge, Msasani City Mall, siku ya Jumapili 12

0
0
TX4A9780 Mama wa mitindo hapa Tanzania maarufu kwa jina la Asya Idarous Khamsin na Titty wanakuletea futari ya pamoja ndani ya Terrace Lounge, Msasani City Mall, siku ya Jumapili 12, July 2015 kwaanzia mida ya saa kumi na mbili kamili hadi saa mbili usiku. Jipatie kadi yako kwa shilingo 25,000/= tu! kwani 15000/= ni special kwaajili ya Dinner yako, inayobaki ni sadaka itakayo tumika kununulia Khanga zitakazo pelekwa Hospitalini kwa wagonjwa wanawake siku ya IDD. Hivyo kwa moyo wa kujitolea nyote mnakaribishwa kushiriki katika zoezi hili, pia kwa mawasiliano zaidi piga namba o784263363 au 0754273472.Futari

IGP MANGU AZINDUA NA KUKAGUA MIRADI YA POLISI TABORA, TANGA NA SINGIDA

0
0
7
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Tabora wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Ludovick Mwananzila na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe.Suleiman Kumchaya.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).
2
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Polisi Tabora wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Tabora.IGP pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
3
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Polisi Dkt.Nyanda wakitoka kukagua Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Polisi Tabora baada ya kuizindua wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo..IGP pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
4
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiweka jiwe la msingi katika jengo la Kikosi cha usalama barabarani mkoani Tabora wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo ambapo pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa huo.Kulia ni Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Kamishna msaidizi wa Polisi, Juma Bwire.
5
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akikagua ujenzi unaoendelea wa Kituo cha Polisi na Makazi ya Askari Wilayani Ikungi mkoani Singida wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Katikati ni ni kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi Thobias Sedoyeka na Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Ikungi.
6
Kamanda wa Kikosi cha Ujenzi cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi, Richard Malika akimtembeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu kuangalia ujenzi wa kituo cha Polisi wilayani Lushoto mkoani Tanga wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.

SEHEMU YA HOTUBA YA JK WAKATI WA UFUNGUZI WA JENGO LA KISASA LA MIKUTANO DODOMA

0
0

WAZIRI WA KAZI ATEMBELEA BANDA LA NSSF KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

0
0



Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume, akitoa maelezo kwa Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka, alipotembelea banda la NSSF wakati wa Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akitembelea banda la NSSF.
 Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la NSSF. Kulia ni Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Sadi Shemliwa (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume wakati alipotembelea banda la NSSF katika Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Sadi Shemliwa (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume wakati alipotembelea banda la NSSF katika Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watoto wakipata zawadi za madaftari walipotembelea banda la NSSF.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande akipata maelezo kutok kwa Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Salim Khalfan alipotembelea banda la NSSF kujionea shughuli zinazofanywa na shirika hilo.

BIMA YA RESOLUTION YAFUTURISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

0
0
 Picha ya baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kufutari katika ukumbi wa hoteli Serena, futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution.
 Baadhi wa waumini wa dini ya kiislam wakimsikiliza mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir, na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salim wakiwaongoza wa umini wa Dini ya kiislamu katika mwezi Mtukuru wa Ramadhani kuchukua futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 kushoto ni  Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir wakifutari na Shehe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh, Alhadi Mussa Salim katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Alhamisi 9 Julai 2015: Kampuni ya Bima ya Resolution leo hii imeaanda hafla ya kufuturisha wateja wake katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hafla ilihudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa Bin Salum.

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa kampuni hiyo ya bima kushirikiana na wateja wake katika iftar kwa lengo la kuwaleta karibu wateja wao na kuwashukuru kwa ushirikiano wa mwaka hadi mwaka.

"Tunawashukuru sana kwa kuhudhuria hafla hii na tunawapongeza kwa uvumilivu wenu katika mwezi huu mkuu wa Ramadhan.” Meneja Mkuu wa Resolution Insurance nchini Tanzania, Bwana Oscar Osir alisema.

Katika hafla hiyo Shiekh Mkuu aliwakumbusha waumini wote umuhimu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

“Ningependa kuwahimiza Waislamu wenzangu kutia maanani amri wakati wa Mwezi Mtukufu. Tuonesha upendo na uvumilivu kwa wote, kusameheana na kuwasaidia wale ambao hawana uwezo wa kujisaidia” Sheikh Alhad alisema.

"Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu kwani ndiyo inatupa motisha ya kuendelea kuwapa huduma bora zaidi. Katika shughuli za kuwapa Huduma zilizo bora zaidi na zinazoweza kuwahudumia ukiwa hapa nchini na hata sehemu yeyote duniani. Ningependa pia kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuwapa bidhaa bora na kuwasikiliza ili tutimize mahitaji yenu", alisema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Resolution Insurance Bi Zuhura Muro.



 Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir, akiwatambulisha wageni waliaalikwa wa dini ya kiislam waliojumuika na Bima ya Resolution katika futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Shehe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh, Alhadi Mussa Salim akizungumzia mara baada ya kufutari futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bima ya Resolution,Zuhura Muro akiwashukuru waumini wa dini ya kislam kwa kujumuika pamoja na Bima ya Resolution katika kufutari iliyo andaliwa na Bima ya Resolution katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam jana.

SHEREHE YA KUMUAGA (SEND OFF) TUMPALE JOHN MWAISANGO, YAFANA KATIKA UKUMBI WA MKAPA JIJINI MBEYA .

0
0
Tumpale John Mwaisango(kulia) Bi. Harusi mtarajiwa akiwa pamoja na Mume wake Mtarajiwa Jeofrey Daniel Shipela (kushoto) katika nyuso za Furaha wakati wa sherehe za kumuaga .
Hivi ndivyo ukumbi ulivyo ulivyokuwa
Bibi Harusi Mtarajiwa Tumpale John Mwaisango akiwa anaingia ukumbini 
Bi Harusi mtarajiwa Tumpale John Mwaisango akimpa zawadi Mume wake Mtarajiwa Jeofrey Shipela wa kwanza kulia ni mpambe wa Bwana harusi mtarajiwa Venance Matinya
 Bi. Harusi Mtarajiwa Tumpale John Mwaisango (kushoto) Akikata keki kulia ni Mpambe wake Monica
 Bi. Harusi Mtarajiwa Tumpale John Mwaisango (kushoto) Akimlisha keki Mpambe wake Monica
Baba Mdogo wa Tumpale John Mwaisango akitoa neno kwa Binti yake na neno la Shukurani
Daniel Shipela (Kushoto) Baba Mzazi wa Bwana Harusi Mtarajiwa Jeofrey Shipela na Mama Mkubwa wake Elizabeth Njeje (kulia) wakitambulishwa
Mbele kwa Mbwembwe za aina yake na kwa umahili Mkubwa Bwana Charles Mwaipopo akifungua Shampeni , wakati wa Sherehe hiyo
Bibi Harusi Mtarajiwa akimrisha Chakula bwana Harusi Mtarajiwa 
Kutoka kulia ni Fredy Anthony Njeje, Grace Mwasote na Njuguna Karanja Marafiki wakubwa wa Joseph Mwaisango wakiwa katika Sherehe 
Baba Mchungaji ambaye ni Baba yake Mdogo wa Tumpale akimpa Mkono wa Pongezi 
Mbele ni Baadhi ya kaka zake na Bibi Harusi Mtarajiwa wamewakajeee...
Joseph Mwaisango kaka Mkubwa wa Tumpale John Mwaisango akimkabidhi zawadi mdogo wake Bibi Harusi Mtarajiwa , Fedha ambazo zitamsaidia ambapo anaenda kuanza Maisha na kumuaga rasmi.
Baadhi ya watu walikuwepo katika Sherehe hiyo
Huyo anaondoka baada ya kumaliza Sherehe
Bibi Harusi Mtarajiwa Tumpale John Mwaisango kuelekea katika Sendoff yake aliona bora asherekee pia na watoto yatima na waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu cha Nuru hapa akiwapa zawadi
Baadhi ya Vitu ambavyo alipeleka katika kituo hicho
 Huko Nyumbani pia kulikuwa na Sherehe ya kumuaga Binti Tumpale Mwaisango, Hapa Baba Mdogo akitoa Neno la Shukurani
 Sherehe ikiendelea Nyumbani


Soma Hotuba Ya Rais Kikwete ya Kuagana Na Kuvunja Bunge La Kumi, 2015

0
0

Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika 2015 Yazinduliwa

0
0
Kulia ni Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura Paez akifafanua sehemu ya Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 kwa wanahabari jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Kushoto ni Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC), Stella Vuzo. Kulia ni Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura Paez akifafanua sehemu ya Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 kwa wanahabari jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Kushoto ni Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC), Stella Vuzo.Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura Paez akifafanua sehemu ya Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 kwa wanahabari jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. 
Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura Paez akifafanua sehemu ya Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 kwa wanahabari jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura Paez akifafanua sehemu ya Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 kwa wanahabari jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura Paez akifafanua sehemu ya Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 kwa wanahabari jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015. Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015Kulia ni Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura Paez pamoja na Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC), Stella Vuzo wakiwa wameshika nakala ya Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 mbele ya wanahabari. 
Kulia ni Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura Paez pamoja na Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC), Stella Vuzo wakiwa wameshika nakala ya Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 mbele ya wanahabari.
Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015. Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015.Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015. Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015.Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015. Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015.Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC), Stella Vuzo akifafanua jambo wakati Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 ilipokuwa akifafanuliwa kwa wanahabari jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC), Stella Vuzo akifafanua jambo wakati Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 ilipokuwa akifafanuliwa kwa wanahabari jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

KUTOKANA na hali ya huduma ya miundombinu ya usafirishaji kuwa duni na ya aghali imeshindwa kukuza biashara na uchumi katika kiwango kinachotegemewa katika mataifa mengi ya barani Afrika. Sekta ya huduma ya miundombinu ambayo ni kichocheo kikubwa katika kukua kwa uchumi imeshindwa kuleta mageuzi ya kutosha.

 Taarifa hiyo imebainishwa katika Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 iliyozinduliwa Jijini Geneva na kusoma katika baadhi ya mataifa ya Afrika. Akifafanua ripoti hiyo nchini Tanzania, Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura Paez alisema huduma za miundombinu ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya 2016-2030 na kujenga jukwaa kwa ajili ya ukuaji mpana barani Afrika.

 Alisema katika ripoti hiyo inayotoa mwangaza wa uchumi wa Afrika imebainisha huduma za miundombinu kama vile maji na afya zinahusishwa zinahusishwa na malengo muhimu ya maendeleo endelevu katika kufikia matokeo ya maendeleo ya kijamii na endelevu. Alisema huduma kama vile umeme, mawasiliano ya simu na usafiri huchangia katika tija pia huamuwa ushindani wa makampuni ya Afrika. "Afrika inawakilisha asilimia 15 ya idadi ya watu duniani lakini inatoa asilimia 2.2 tu ya huduma za mauzo ya nje kimataifa, hali hii inaonesha kutotumika kikamilifu kwa sekta hiyo," anafafanua Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi akizungumzia ripoti hiyo ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015.

 Aliongeza kuwa ripoti ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015 inasisitiza umuhimu wa mataifa ya Afrika kukabiliana na changamoto za mapungufu mbalimbali katika udhibiti wa sera, ambayo yamechangia kukosekana kwa ufanisi wa kuweza kutumia kikamilifu sekta ya huduma kuchochea maendeleo ya kiuchumi. Ripoti hiyo pia inabainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2009-2012 sekta ya huduma barani Afrika ilikuwa kwa kiwango cha asilimia 4.6 ikilinganishwa na asilimia 5.4 katika nchi zinazoendelea. Sekta ndogo za kihuduma zilizokuwa kwa kasi zaidi zilikuwa usafiri, uhifadhi na mawasiliano. 

Hata hivyo sekta ya huduma katika Afrika iliongoza ukuwaji wa pato la taifa katika chi 30 kati ya nchi 54 katika kipindi cha 2009-2012, huku kati ya nchi 45 ambapo pato la sehemu ya huduma lilipanda, 30 zilipata tatizo la kupungua kwa uzalishaji viwandani kuanzia kipindi cha 2001-2004 hadi kipindi cha 2009-2012. Aidha alisema baadhi ya nchi za Afrika zimeendeleza huduma za viwanda vyao kwa mafanikio na hata zinapeleka huduma zake katika masoko ya Afrika huku akizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na Mauritius na Nigeria ambapo zinafanya vizuri sekta ya huduma za kifedha na kibenki. 

Alisema kibiashara katika sekta ya usafiri wa anga nchi za Ethiopia, Kenya na Afrika ya Kusini zinafanya vizuri huku huduma za elimu ni Uganda, huduma za mawasiliano ya simu Misri na huduma za Bandari ni nchi ya Djibouti na Kenya. Baada ya ufafanuzi huo ripoti imeshauri masuala kadhaa ikiwemo kuwa na kanuni ya ufanisi wa huduma ya miundombinu. 

Alisema pamoja na hayo mataifa mengi yapo chini katika uhuru udhibiti sekta zote na mifano ya viwango vya kimataifa vya udhibiti wa miundombinu havitumiki barani Afrika ilhali vyombo vingi vya udhibiti vipo katika hatua za awali za maendeleo na bajeti ya kawaida na mara nyingi hata hukosa wafanyakazi wenye sifa. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images