Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 49516 articles
Browse latest View live

UN TANZANIA YAKUSANYA MAONI KUHUSU UTENDAJI WAKE NCHINI NDANI YA SABASABA, KARUME HALL

$
0
0
IMG_5730
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza Mkurugenzi wa kampuni ya Events World, Dimo Debwe Mitiki, jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”. (Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
IMG_5736
IMG_5779
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza mmoja wa wananchi aliyetembelea la Umoja huo jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania.

IMG_5793
Laurean Kiiza (kushoto) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akimsimia Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige kuwasilisha maoni (GeoPoll) yake moja kwa moja kwenye simu ya kiganjani, alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
IMG_5772
Mdau wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Lemmy Hipolite (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, jinsi alivyowezeshwa na Umoja huo kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupata elimu inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa kuuza michoro hiyo ndani ya banda la Umoja wa Mataifa.
IMG_5710
Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, akionyesha baadhi ya kazi zake kwa wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
IMG_5764
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo ya maeneo mbalimbali yaliyofanikiwa katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDAP) kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa na kutaka kufahamu shughuli mbalimbali za UN Tanzania.
IMG_5744
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimkabidhi makabrasha na vipeperushi mbalimbali vya Umoja Mataifa, Mwandishi wa Michuzi blog, Chalila Kibuda aliyetembelea banda hilo kwenye maonyesha ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_5701
Sophia Mataro (wapili kushoto) kutoka Shirika la UNESCO Tanzania, akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwa mmoja wa wananchi alitembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
IMG_5717
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na kituo cha Televisheni cha Channel Ten kilichotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba yanaoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
IMG_5802
Timu ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa "Delivering as One" wanaotoa huduma kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama “Sabasaba” yanayoendelea kurindima jijini Dar es Salaam.
IMG_5738
Muonekano wa nje wa banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Na Modewji blog team
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania limetoa nafasi ya kipekee kwa watanzania kutoa maoni yao wakati wa kipindi hiki cha maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam, yaliyoanza kurindima Juni 28, huku wakikusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi juu ya utendaji wake kwa wanaotembelea kwenye maonyesho hayo kila siku.
Aidha, katika kupokea maoni hayo, UN imeweka utaratibu wa moja kwa moja kwa wananchi kufika kwenye banda lao na kutoa maoni yao, ambayo yanaenda moja kwa moja kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.
Njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kuingia http://gpl.cc/UN2
Kupitia linki hiyo, mtumiaji anaweza kutumia simu yake ya smartphone, laptop na vifaa vingine vya kielektroniki.
Njia nyingine ni ya kutumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Na kwa njia ya tatu ni kuwasilisha namba ya simu na majina na ujumbe unaotaka na UN wataufanyia kazi.
Aidha, maoni hayo yatakuwa yakipokelewa kwa kipindi chote cha SabaSaba, hivyo wananachi wameombwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao ya nini UN wakifanye nchini pamoja na mambo mengine.

Uzinduzi wa Bonaza Kombe la Masauni Viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar.

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Hamad Masauni akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Kikwajuni Bondeni iliolazimika kuchukua kipigo cha mabao 2--1 katika mchezo wa ufunguzi wa Bonaza hilo linalofanyika usiku katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, Mhe Hamad Masauni akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Kisimamajongoo iliotoa kipigo cha mabao 2--1 katika mchezo wa ufunguzi wa Bonanza hilo linalofanyika usiku katika viwanja vya Mnazi mmoja Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Hamad Masauni akizindua michuano ya Bonaza la Kombe la Masauni, yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku na kushirikisha timu mbalimbali za vijana ili kukuza vipaji vya mchezo huo Zanzibar. 
Viongozi wa meza kuu wakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa Bonaza la Kombe la Masauni yanayofanyika usiku katika viwanja vya malindi mnazi mmoja.
Kikosi cha timu ya Kisimajongoo kinachoshiriki Bonaza la Kombe la Masauni wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo wao wawa ufunguzi uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku. timu hii imeshinda katika mchezo huo 2--1


Kikosi cha timu ya Kikwajuni Bondeni kilichokubali kipigo cha mabao 2--1 dhidi ya timu ya Kisimajongoo. 


Wapenzi wa mchezo wa mpira wakifuatilia michezo wa Bonaza ya Kombe la Masauni yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja 

Kocha wa timu ya Kisimajongoo akitowa maelezo kwa wachezaji wa timu yake ikiwa tayari iko mbele kwa mabao 2--1
Kocha wa Timu ya Kikwajuni Bondeni akitowa maelekezo kwa wachezaji wa timu yake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza.

Mchezaji wa timu ya Kisimajongoo na Kikwajuni Bondeni wakiwania mpira wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Bonaza la Kombe la Masauni Zanzibar.
Kizaaza golini kwa timu ya Kisimajongoo wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Bonaza la Kombe la Masauni, yanayofanyika usiku katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar. 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA, ANAYEMALIZA MUDA WAKE

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa India Nchini Tanzania, Debnath Shaw, anaye maliza muda wake wa kazi nchini wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga rasmi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa ajili ya kuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

SIMBA SPORT CLUB YAANDIKA HISTORIA, WAZINDUA KADI MPYA

$
0
0
Afisa MtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula  Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu Wakiwa wameshika Mfano wa Kadi ya Club Hiyo waliyoizindua  Leo.
Klabu ya Simba leo hii imeandika historia kwa kuzindua Kadi Mpya za Wanachama ambazo zinamwezesha  kila Mwanachama wa  Simba  kupata  bima  ya maisha  hadi  Tsh 250,000 ikiwa atafiwa  na  mwenza au mtoto au yeye  mwenyewe  kupitia  bima  ya  maisha   iitwayo Simba Pamoja. Pia Simba  leo hii imezindua  Kadi za watoto yaani Simba Cubs. 
Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Akimkabidhi Mtoto  Iqram Ally Kadi ya Simba Cubs waliyoizindua leo wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula (kulia) Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange.

Akizungumza wakati wa uzinduzi Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Simba inaendeleza falsafa yetu ya utendajii  kifanya kazi ‘’maneno machache vitendo vingi’’, baada ya kuboresha upatikanaji wa taarifa kupitia mtandao kwa kuzindua tovuti yenye taarifa na huduma mbalimbali ndani yake, leo tumewaita  hapa  kuandika historia mpya kwa wana Simba na hususani wale wanaota ka kuwa wanachama wa Simba’’.

Aliongeza  kusema ‘’ Simba inapenda kuwajulisha kuwa sasa mpenzi wa Simba anayetaka kuwa mwanachama anaweza kuomba kupata kadi ya wanachama kupitia tovuti ya Simba yaani www.Simbasports.co.tz . Napenda mtambue hii ni historia katika  ukanda huu kuweza kutumia  teknojia kufikia wanachama, Sisi  ni wakisa  sana  tunaona  mbele!.
AfisaMtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula (Kulia) Akielezea Jambo  Akiwa Ameambatana na Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Wakati wa Uzinduzi wa Kadi Hiyo ya Simba Sport  Club Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu.

Kwa  upande wake Afisa Mtendaji  Mkuu  wa EAG Group ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati  ya masoko na  biashara Imani  Kajula  alisema
‘’ Uanzishwaji  wa  Kadi  ya  Simba Cubs itawawezesha watoto sio tukutambuliwa  kuwamemba  wa  Simba, bali  pia  kupata  punguzo   kubwa au kuingia  bure  kwenye  matukio  yanayo  andaliwa  na  Simba Sports Club. Pia  maduka  mbalimbali  yatatoa  punguzo  kwa  watoto  wenye  Simba Cub Card.

Wote  mna  jua fika  kuwa  mapenzi   hujengwa, Simba ina lengo la kujenga msingi  imara  wa kuendeleza  wanachama  na  wapenzi wake’’.

WAZIRI MKUU AHIMIZA WANANCHI KUEPUKANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KWA KUPIMA AFYA ZAO NA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA

$
0
0
1nh
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na umati wa watu waliokisanyika katika banda la NHIF juu ya umuhimu wa watu kupima afya zao mara kwa mara na kuzingatia kanuni bora za maisha ili kuepuka maginjwa yasiyoambikiza ambayo mengi husababishwa na unene uliokithiri.
2nh
Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kuhusu huduma zinazotolewa na banda la NHIF katika Maonesho ya Wiki ya Serikali za Mitaa viwanja vya Mashujaa Mtwara.
nh3
Msururu wa wananchi wa Mtwara wakisubiri zamu zao kupima afya zao wakati Mzee aliyejitokeza kupima akipatiwa huduma.
.....................................................................
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda leo ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maadhimisho ya wiki ya Serikali za Mitaa viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara na kuhimiza wananchi kuzingatia afya bora ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza kama Sukari na Shinikizo la damu.  

Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu juu ya huduma zitolewazo katika banda hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando alisema NHIF anaungana na Serikali katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuhimiza wananchi kupima afya zao na kuishi mtindo bora wa maisha unaozingatia lishe bora na mazoezi. 

Alisema 'Mfuko umejiwekea utaratibu wa kupima afya bure kwa wananchi kila unaposhiriki maonesho mbalimbali ili kuwajengea wananchi tabia hiyo na kuonesha umihimu wa suala hilo ili kuepuka madhara makubwa ya afya na vifo ambavyo vingeweza kuepukika'Kwa upande wake Meneja wa NHIF Mtwara Bi. Joyce Sumbwe alisema tangu maonesho hayo yaaenze tarehe 24 Juni watu 1,800 wameshapimwa afya zao na 32% kati yao wamepatikana na unene uliokithiri ambao ni chanzo kikubwa cha magonjwa hayo. 

Wengi wa wananchi waliojitokeza walionekana kutokujia kuwa wanatembea na shinikizo la damu na walishauriwa kwenda kituo cha afya ili kuanza matibabu. Naye Meneja Masoko na Elimu kwa Umma Bi. Anjela Mziray alitoa wito kwa wananchi kujiunga na NHIF ili kumudu gharama za matibabu ambazo ziko juu na magonjwa huja bila taarifa hata wakati ambapo mtu hana fedha mfukoni. Alisema suluhisho ni kwa wananchi wote kujiunga na Bima ya afya.

TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA ( TFF)

$
0
0
Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam.

CECAFA YATOA RATIBA YA KAGAME 2015.

Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kwa sapoti yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.

Lengo la CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza michezo mingi na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru CECFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na kuahidi TFF itahakikisha michuano hiyo inafanya nchini katika hali ya amani na usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa michuano hiyo.

Timu zilizothibtisha kushiriki michuano hiyo ni Yanga, Azam (Tanzania), APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Al Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia), Malakia (Sudani Kusini), Adama City (Ethipia) na KCCA (Uganda).

Wakati huo Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangza ratiba ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA.

Mechi ya ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudia wenyeji Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya Somalia.

 Ratiba ya michuano hiyo imeziweka timu hizo katika makundi matatu ambapo kundi A lina timu za: Yanga (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djbiout), KMKM (Zanzibar) na Khartoum-N (Sudan)

Kundi B: APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi) na Heegan FC (Somalia), Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda)

Timu tatu zitakazoshika nafasi ya juu kutoka kundi A, timu mbili za juu kutoka kundi B & C, na mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B & C zitaingia katika hatua ya robo fainali.
  
 BENDERA AIPONGEZA TFF
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dokta, Joel Bendera ameipongezs TFF kwa kuandaa mashindano ya ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13),  na maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika za vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Bendera amesema hiyo ndiyo njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio pia amepongeza juhudi za Chama cha Soka mkoa wa Manyara na TFF kwa kuandaa kozi za makocha na waamuzi, akisema huo ndiyo uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani Manyara.

Aidha aliwaasa makocha kutumia mbinu za kisasa za ufundishaji soka walizozipata kwenda kuendeleza vipaji vya wachezaji watakaowafundisha.

Pia Bendera amewahakikishia wakazi wa Manyara atahakikisha wanaandaa vipaji vitakvyowawezesha kuwa na timu bora itakayowakilisha mkoa wa Manyara.


ACCREDITATION FOR ALL AFRICAN GAMES:
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limetangza kufunguliwa kwa maombi ya vitambulilsho kwa wandishi wa habari kwenye fainali za michezo ya Afrika zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo- Brazaville.

Waandishi wa habari wanaotajiwa kwenda kufanya kazi kwenye michuano hiyo wanaombwa kufanya maombi ya vitambulisho (Accrediatation) kuanzia Juni 29 mpaka Julai 7 mwaka huu.

Link ya kufanya maombi hayo ni @CAF_Online
Accreditation for African Games Congo 2015 draw




TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA SH. MIL. 65 RUFIJI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji , Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifungua maji ya bomba mara baada ya makabidhiano ya kisima kilichochimbwa na TBL kwa gahrama ya shilingi mil. 65 katika Kijiji cha Mwaseni Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani. Makabidhiano hayo yalifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo, wakiwatwisha  ndoo za maji akina mama wa Kijiji cha Mwaseni, Mibuyu Saba mara baada ya kukabidhi kisima cha maji kilichochibwa na TBL kwa gharama ya shilingi mil. 65, wilayani RufijiMkoa wa Pwani. Hafla hiyo ilifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki. 
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo, wakiwatwisha  ndoo za maji akina mama wa Kijiji cha Mwaseni, Mibuyu Saba mara baada ya kukabidhi kisima cha maji kilichochibwa na TBL kwa gharama ya shilingi mil. 65, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani. Hafla hiyo ilifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki. 

Na Mwandishi wetu , Rufiji
MKUU wa wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu  amewataka wakazi wa kijiji  cha mwaseni  Mibuyu saba kulinda miradi  mbalimbali ya maendeleo hili kuweza  kupunguza tatizo la umaskini katika  eneo hilo.

Babu alisema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji hicho wakati wa makabidhiano ya Kisima kirefu cha maji safi kilicho chimbwa na Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya wakazi eneo hilo

“Kisima hiki ni sehemu ya miradi ya maendeleo ambayo imekuwa ikifadhiliwa na TBL katika jamii hivyo sio kitu cha itikadi kila mtu anapaswa kukitunza na kulinda kwa ajili ya kupunguza mzigo wa 
kwenda kufata maji mbali kwa wakina mama waishio hapa” alisema Babu.

Babu aliongeza kuwa mbali ya kuchota maji tu lazima kijiji kiweke utaratibu wa kuakikisha kuwa kila mmoja anachangia huduma kidogo hili kuweza kufanya huduma hiyo kuwa endelevu na sio ikiaribika kusubiri kutafuta mfadhili tena.

Akziungumza wakati wa kukabidhi kisima hicho Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano kutoka TBL, Stephen Kilindo alisema kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha fedha shilingi milioni 65 za kitanzania na kukabidhiwa kwa wana kijiji hao.

Alisema kuwa kisima hicho kirefu ambacho kimesambaza mabomba manne ya kutolea maji kitaweza kuhudumia watu 1700 waishio katika eneo hilo na maeneo ya jirani.

Kilindo alisema TBL kama mdau wa maendeleo na shirika ambalo uwepo wake inategemea watanzania imeamua kuchimba kisima hicho kama ni sehemu ya kurudisha kile wanacho kipata kwa wananchi hili waweze kufurahia miasha kama ilivyo katika nchi zingine duniani.

“Tanzania kilamahala kuna maji kinachohitajika ni uwezeshaji hivyo sisi kama TBL tumeliona hilo ndio maana tumeamua kujenga visima kila mahali palipo kuwa na mahitaji ya maji hapa nchini” alisema Kilindo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mwaseni Mibuyu Saba, Hasan Abdallah alishukuru  TBL kwa msaada huo mkubwa katika kijiji chake kwa kusema kuwa wameweza kutatu changamoto kubwa katika eneo ambayo inaweza kuwa chachu ya maendeleo mingine yote.

Alisema kuna mashirika mengi sna lakini TBL kwa moyo wao wameweza kuona tatizo la mwaseni na kulibeba kama lao hivyo awana neon zaidi ya shukrani katika kampuni hiyo.

LOWASSA ARUDISHA FOMU LEO MJINI DODOMA, ATEMA CHECHE KWA WANAOMTUHUMU

$
0
0



WAZIRI Mkuu Mstafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

 Mh. Lowassa ambaye alikuwa amesindikizwa na Wenyeviti wa CCM wa mikoa 12 kutoka bara na visiwani, aliwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma majira ya saa 8:30 mchana wa leo Julai 1, 2015, na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi. 

Baada ya kukabidhi fomu hizo, Mh. Lowassa, alikutana na waandishi wa habari na kusoma taarifa yake fupi, ambapo alionya wale wote wanaoeneza habari potofu kuwa yeye ni mla rusha, watoe ushahidi, wapi amekula rushwa, na ni  kiasi gani, za nani na wapi, Awataka Watanzania kupuuza habari hizo na kwani yeye ni muadilifu na hana shaka na hilo. Alisema, yeye ana fedha kiasi gani za kuwapa Wana CCM 874,297, waliojitokeza kumdhamini.

 "Maneno hayo sasa basi, natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi huo autoe hadharani vinginevyo waache kueneza uvumi na uongo" Alisema Mh. Lowassa.  Alisema yeye anachukia umasikini, na kwamba endapo chama kitamteua na hatimaye Watanzania kumchagua kuwa Rais wa awamu ya Tano, atahakikisha anatimiza dhamira yake ya kuwaondolea Watanzania umasikini.


 Mh. Lowassa, ambaye alisindikizwa na Vigogo wa chama hicho akiwemo, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, na Mzee Pankrans Ndejembi wakiwemo wenyeviti wa CCM 12 kutoka Tanzania Bara na Visiwani, amehitimisha zoezi hilo baada ya kuzunguka mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani, na mara zote amekuwa akipata idadi kubwa ya wana CCM na wananchi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM mahala alikopita, ikiwa ni pamoja na wengine kujipanga barabarani na kumpungia mikono
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) akizipanga vyema fomu zake ili azikabidhi kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi (kushoto), wakati alipofika kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015. Mh. Lowassa amerudisha fomu hizo, baada ya ziara yake ya nchi nzima kutafuta saini za WanaCCM wa kumdhamini ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015, ambapo jumla ya WanaCCM 874,297 walimdhamini.Kushoto kwa Mh. Lowassa ni Mkewe, Mama Regina Lowassa.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi fomu za wanaCCM waliomdhamini ili aweze kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi wakionyesha fomu hizo kwa wanahabari wakati wakikabidhiana, kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kurudisha fomu za wanaCCM waliomdhamini ili apare baada ya ziara yake ya nchi nzima kutafuta saini za WanaCCM wa kumdhamini ili aweze kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.


NI MSIBA TENA JAMBO CONCEPTS (T) LTD, WACHAPISHAJI WA GAZETI LA JAMBO LEO

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Jambo Concepts (T) Ltd, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti na Jarida la Jambo Brand, limempoteza mfanyakazi wake mwingine wa idara ya masoko, Kinai Mtinda (pichani), baada ya kufariki dunia saa 7 usiku wa kuamukia leo katika Hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Msiba na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa kaka yake Mbezi Beach na taratibu zingine kuhusiana na msiba huo zitatolewa baadae.

Marehemu Kinai ameacha watoto wawili.

Kifo cha Mtinda kinakuja ikiwa ni siku chache tangu afariki dunia Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Ramadhani Kibanike mwishoni mwa mwezi uliopita. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe Amina.

AIRTEL SMARTFONIKA YAMFIKIA MTANGAZAJI EPHRAIM KIBONDE WA CLOUDS FM

$
0
0
 Ofisa Mauzo wa Airtel, Salma Juma akimuelekeza jambo Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde kabla ya kumsmartfonika simu ya kisasa mapema wiki hii katika duka la  wazi la Airtel lililopo Game Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga.
 Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga (kulia), akimsmartfonika simu Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde.
 Ofisa Mauzo wa Airtel, Rehema Hoza (katikati), akimkabidhi Kibonde kifaa cha kutunzia umeme 'Powerbank'. Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga.

 Maofisa mauzo wa Airtel wakiwa katika duka la wazi Game Mlimani City.
 Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
 Meneja Mawasiliano wa Airtel, Jackoson Mmbando, akimuelekeza jambo, Kibonde baada ya kusmartfonika simu hiyo ya kisasa.
 Ofisa Mauzo wa Airtel, Eveline Amos (kushoto), akiwaelekeza jambo, Kibonde na mteja mwingine waliofika katika duka la wazi lililopo Game Mlimani City.
 Maofisa Mauzo wa Airtel wakiwahudumia wateja katika duka hilo la wazi.
  Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
Wateja wakiwa duka la wazi Game Mlimani City.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Simu ya Airtel imeendelea kuwa smartfonika watu maarufu kwa kuwapatia zawadi za simu kwa awamu tofauti kama walivyojiwekea utaratibu huo.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema kwa wiki hii mpango huo wa smartfonika umemdondokea Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephrahim Kibonde ambapo amepata zawadi ya simu ya kisasa yenye uwezo mkubwa.

"Tumejipanga vizuri katika mpango huu wa kuwasmartfonika watu maarufu wakiwemo wa sanii na wadau mbalimbali katika wakati tuliopanga" alisema Mmbando.

Mmbando alisema pamoja na kuendelea kuwasmartfonika walengwa hao sasa mpango mzima utakuwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yaliyoanza mapema wiki hii katika viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mmbando ametumia fursa hiyo kuwataka wateja wa Airtel kutembelea banda lao lililopo katika viwanja hivyo ili kupata huduma mbalimbali pamoja na kujipatia simu za aina mbalimbali kwa bei nafuu. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

DEGE ECO - VILLAGE WASHIRIKI MAONYESHO YA SABASABA, WAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KUNUNUA NYUMBA

$
0
0
Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam ya Saba Saba.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zishakamilika.
Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni.

Mradi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.

Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wa kazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.
 Wafanyakazi wa Dege Eco - Village akimhudumia wateja wao aliyefika katika banda lao.
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village wakiwahudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Muonekano wa Banda lao lililopo viw
 
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village akimhudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village amkimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya kununua nyumba.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village (katikati) akiwaonyesha wafanyakazi wa kampuni hiyo namna walivyoweza kufanya vyema katika mauzo ya nyumba.
Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.

Rais Kikwete afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Ikulu Dar es salaam

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni, mara baada ya kufanya mazungumzo nae.

MABIBO BEER YAIDAI TUME YA USHINDANI SHILINGI TIRIONI MOJA, YASEMA IMEKWAMISHWA KUJENGA VIWANDA VITATU NCHINI

$
0
0
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kupinga uamuzi wa Tume ya Ushindani (FCC)  na kuidai fidia hiyo ya Shs. 1 trilioni kutokana na hasara wanayoipata kwa kuruhusu bia ya Windhoek kuingia katika soko la Tanzania kiholela.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira (katikati), akizungumza katika mkutano huo na kusema bia halali iliyopo kwenye soko ni ile yenye namba MB 66 na inayosambazwa na kampuni hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Mabibo, Anic Kashasha na Wakili, Stephano Kamala.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kampuni ya Mabibo, Anic Kashasha (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Wakili wa Kampuni hiyo, Respicious Didace na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira.
Wakili, Stephano Kamala (kulia), akizungumza katika mkutano huo. (PICHA ZOTE KWA HISANI YA BLOG YA HABARI ZA KIJAMII)

Na Daniel Mbega
KAMPUNI ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd imesema inakusudia kuifikisha mahakamani Tume ya Ushindani (FCC) ikidai fidia ya Shs. 1 trilioni kutokana na kukiuka mkataba baina ya kampuni hiyo na Kampuni ya Bia ya Namibia (NBL - Namibia Breweries Limited) unaoipa Mabibo haki ya kipekee ya kusambaza bia ya Windhoek nchini Tanzania.
Mbali ya kusudio hilo, kampuni hiyo pia imeiomba Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa uamuzi uliochukuliwa na Baraza la Ushindani (FCT) mwezi Aprili 2015 kuhusu haki ya Mabibo ya kuagiza na kusambaza bia za Windhoek kipekee katika soko la Tanzania.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira, alisema anashangazwa ni kwa vipi vyombo hivyo viwili vimekuwa vikikiuka sheria na kuinyima haki kampuni hiyo hata baada ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kutoa hukumu.
Rugemalira alisema kwamba, mnamo mwezi Aprili 2015, FCT ilitoa uamuzi unaotafsiriwa kwamba kwamba mkataba baina ya Mabibo NBL ambao ulisajiliwa kwa matakwa ya Sheria ya Alama za Biashara na Huduma, haukuwa halali kisheria.
"Si FCC wala FCT yenye mamlaka yakutengua uamuzi halali wa Mahakama kutafsiri sheria na katiba ya Tanzania. Katika kufungua shauri lake katika Mahakama ya Rufaa tarehe 24 Juni 2015, Mabibo imeiomba Mahakama kuthibitisha kwamba mwenendo wa Mabibo ni sahihi kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003, kama Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilivyoamua mwaka 2010 na kuwa FCC na FCT walifanya kinyume cha mamlaka zao za kisheria na kikatiba na kujipa uwezo wa kutengua maamuzi ya Mahakama za Tanzania" alisema Rugemalira.

Rugemalira alisema kwamba, Mabibo inataka fidia hiyo kutoka FCC na washirika wake kwa sababu amri isiyo halali ya FCC imeruhusu mwendelezo wa uagizaji wa bia ya Windhoek na wasambazaji wasioruhusiwa hivyo kuharibu biashara ya Mabibo na mkondo wa uadilifu wa bidhaa ya Windhoek katika soko la bia Tanzania.
Awali,  Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya kampuni hiyo, Anic Kashasha, alisema kitendo kilichofanywa na vyombo hivyo viwili vimeitia hasara kubwa kampuni hiyo na kuchelewesha hatua ya ujenzi wa viwanda vitatu vya kuzalisha bia hiyo.
"Tumepanga kujenga viwanda vitatu nchini - Kagera, Kilimanjaro na Tanga - lakini kwa hali ya sasa jitihada hizi zinakwama kwa sababu mauzo ya bia ya Windhoek hapa nchini ni kiasi cha asilimia 0.05 tu ya soko la jumla badala ya asilimia 5 ambayo imekusudiwa katika soko hilo.
"Kwa miaka kadhaa sasa tumeendelea kuumia kutokana na uamuzi huu wa vyombo hivi ambao sasa umefanya waagizaji wengine wasambaze bia ya Windhoek huku sisi wenye haki tukiumia," alisema Kashasha.
Akitoa ufafanuzi wa kisheria, Mwanasheria wa kampuni hiyo Respicious Didace, alisema FCC na FCT hawana haki ya kisheria ya kukiuka hukumu halali ya mahakama kwani, kisheria hakuna chombo chochote kinachoweza kutengua uamuzi wa mahakama isipokuwa mahakama yenyewe kwa kufanya marejeo au mahakama ya juu.
"Mahakama yenyewe inaweza kutengua hukumu hiyo kwa kufanya marejeo (review) au mahakama ya juu yake, lakini hakuna chombo kingine chochote kinachoweza kupinga amri halali ya mahakama," alisema Didace.
Kwa miaka kadhaa sasa Kampuni ya Mabibo imekuwa ikilalamikia hatua ya vyombo hivyo viwili katika biashara kuinyima haki yake ya msingi na kusisitiza kwamba ni vyema kuzingatia dhana ya utii wa sheria bila shuruti.
“Kuna amri ya Mahakama ambayo inazuia mtu yeyote kuingiza na kusambaza Windhoek katika soko hapa nchini bila kuomba na kupata kibali kutoka Mabibo. Amri hii ni halali na inapswa ifuatwe,”  alisisitiza Rugemalira. 
Rugemalira alisisitiza kuwa bia ya Windhoek inayopaswa kuuzwa katika soko la Tanzania lazima iwe na alama ya MB66 na kwamba inasambazwa na kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited pekee. 

Alvaro Rodriguez afunga Mkutano kujadili Afya na Vifo kwa Mtoto Tanzania

$
0
0
Washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania ikifuatilia majadiliano wakiwa katika picha ya pamoja. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo. Washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania ikifuatilia majadiliano wakiwa katika picha ya pamoja. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baadha ya hafla ya kufunga mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baadha ya hafla ya kufunga mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania.Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baadha ya hafla ya kufunga mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baadha ya hafla ya kufunga mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza alipokuwa akifunga mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza alipokuwa akifunga mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania.Baadhi ya Washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania, wakiwasilisha kazi baada ya mijadala ya makundi.Baadhi ya Washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania, wakiwasilisha kazi baada ya mijadala ya makundi.Meza kuu ikipokea maswali toka kwa washiriki wa mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania.Meza kuu ikipokea maswali toka kwa washiriki wa mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini TanzaniaBaadhi ya Washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania, wakiwasilisha kazi baada ya mijadala ya makundi. Baadhi ya Washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania, wakiwasilisha kazi baada ya mijadala ya makundi.[/caption]  [caption id="attachment_59059" align="aligncenter" width="600"]Baadhi ya Washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania, wakiwasilisha kazi baada ya mijadala ya makundi.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania, wakiwasilisha kazi baada ya mijadala ya makundiBaadhi ya wawasilisha mada toka meza kuu wakijibu maswali ya washiriki wa mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania.Baadhi ya wawasilisha mada toka meza kuu wakijibu maswali ya washiriki wa mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania.Mratibu wa mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania (kushoto) akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez kabla ya kufunga mkutano huo. Mratibu wa mkutano uliojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania (kushoto) akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez kabla ya kufunga mkutano huo.Sehemu ya washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania ikifuatilia majadiliano. Sehemu ya washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania ikifuatilia majadiliano.

BENKI YA CRDB YAVUTIA WENGI MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
BENKI ya CRDB imewataka Watanzania kutembelea banda lao ili kupata huduma mbalimbali za Fedha.

Akizungumza katika Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Ofisa wa benki hiyo, John Titus amesema kuwa banda lao linashughulika na kufungua akaunti na kumuhudumia mteja.

Aliongeza kuwa Benki ya CRDB pia imeweka Mobile  Branch ambayo hufanya kazi zote zinazofanywa na benki hiyo ikiwemo huduma za kuweka fedha na kutoa.

Titus alisema pia wanahuduma ya Jumbo ambayo ni akaunti kwa ajili ya watoto.

Alisema akaunti hiyo huwapa watoto fursa ya kuwekezewa fedha zitakazowasaidia katika masomo na maisha yao ya baadae.

Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za Fedha katika Mobile Branch katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Barabara ya Kilwa.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za Fedha katika Mobile Branch katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Barabara ya Kilwa.
Gari aina ya Passo ambayo itakabidhiwa kwa mshindi wa mwezi Juni katika viwanja vya Sabasaba.
Ofisa wa Benki ya CRDB, David John akitoa ufafanuzi kuhusu Huduma ya Simbanking kwa mteja aliyefika katika banda la CRDB katika maonyesho ya Sabasaba.
Mteja akipata huduma katika banda la CRDB.
Mteja akiweka sahihi baada ya kufungua akaunti. 
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Pamela Haule akitoa huduma kwa Hawa Hashimu ambaye aliyefika kufungua akaunti katika Viwanja vya Sabasaba.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Pamela Haule akitoa huduma kwa wateja waliofika katika banda la benki ya CRDB.
Ofisa wa Benki ya CRDB, John Titus (katikati) akimuhudumia mteja wa benki hiyo aliyefika katika banda la benki hiyo, Gerald Stanslaus katika maonyesho ya Sabasaba.
Wateja wakipata huduma katiba banda la CRDB.
Mteja akiweka Passworld baada ya kufungua akaunti. 
Wateja wakipa huduma katika Mobile Branch.

NYALANDU AREJESHA FOMU ZA URAIS

$
0
0
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akirejesha fomu za wadhamini kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajabu Luhavi, jana, baada ya kukamilisha kazi ya kuomba udhamini kwa mikoa yote nchini.02
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhavi. Kulia ni mkewe Faraja na kushoto ni Luhavi.01
MKE wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Faraja, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhavi ofisini kwake katika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wakati Nyalandu aliporejesha fomu zake za kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya urais.03
BAADHI ya wanachama wa CCM waliomsindikiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma, jana. 
04
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakipongezwa na sehemu ya umati uliojitokeza kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wakati akirejesha fomu.0506
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakishangiliwa na mamia ya wanachama wakati wakiondoka ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, jana baada ya kurejesha fomu za kuomba urais.

Dogo Jembe azungumzia mikakati wa rasilimali na afya

$
0
0
Yule mgombea mwenye umri mdogo zaidi ambaye siku za karibuni amejizolea
umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii tangu achukue fomu ameanza
kumwaga sera zake ambapo leo anazungumzia kuhusu ambavyo Watanzania
wanatakiwa wafaidike na rasimali pia mipango ya kuboresha huduma za afya.

WANAWAKE WATAKIWA KUJIAMINI KATIKA NAFAZI ZAO ZA UONGOZI -KAIRUKI

$
0
0
 Katibu mtendaji wa uongozi institue,Profesa Joseph Semboja  akizungumza katika mkutano wa kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya uongozi uliofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanawake walioshiriki mkutano wa kuwajengea uwezo katika masuala ya uongozi uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Nabu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angela Kairuki akizungumza na wanawake katika mkutano wa kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya uongozi uliofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
NAIBU  Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angela Kairuki amewataka wanawake kujiamini katika nafasi za uongozi wanazozipata katika kuweza kufikia asilimia ya 50 kwa 50.
Hayo aliyasema katika mkutano wa wanawake ulioandaliwa na uongozi Instute,Kairuki amesema katika kuelekea katika uchaguzi mkuu wanawake wajitokeze katika nafasi mbalimbali ili kuweza kubadilika.
Amesema katika ngazi mbalimbali za maamuzi katika bodi zilizopo nchini ni idadi ndogo za wanawake ikilinganishwa na wanaume hali ambayo sasa inatakiwa kuweka kupaumbele katika bodi kuwa na uwakilishi wa wanawake.
Kairuki amesema sasa ni wakati wa mabadliko kwa wanawake kuonyesha uwezo katika kazi mbalimbali na kujenga mazingira ya kujiamini katika kazi iwe  nafasi za ukurugenzi na kazi nyinginezo za serikali na sekta binafsi.
Nae Katibu Mtendaji wa Uongozi Institute,Profesa Joseph Semboja amesema wameanza program hiyo katika kuwainua wanawake katika nafasi za uongozi katika kuweza kufikia malengo ya asilimia 50 kwa 50.
Sembomja amesema wanawake katika kuelekea uchaguzi mkuu ni fursa kwao kujitokeza kutokana na mafunzo mbalimbali wanayopata kutoka kwa wanawake waliokatika nafazi za uongozi.

Zantel yasaidia Chama Cha Maalbino Tanzania kutoa elimu kwa umma.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Bwana Ernest Kimaya. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya ushirikiano na kampuni ya Zantel leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose na Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bi Progress Chisenga,
   Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya ushirikiano wao na chama cha Maalbino Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bi Progress Chisenga, na Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya

 Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imekisaidia Chama cha Maalbino Tanzania katika mpango wake wa kusambaza elimu juu ya ulemavu wa ngozi kwa jamii pamoja na msaada wa jumla ya shilingi milioni 5 ambao unalenga kusaidia uendeshaji wa shughuli zake hapa nchini.

Zantel kwa kushirikiana na Chama Cha Maalbino kitajikita kutoa elimu hii kwa kusambaza ujumbe mfupi kwa wateja wake pamoja na kutumia vipindi vyake inavyodhamini ili kupeleka ujumbe kwa jamii kiujumla.

Pamoja na hiyo pia, Zantel inajipanga kutumia mikutano ya wafanyakazi pamoja na matamasha ili kuhakikisha ujumbe kuhusu ulemavu wa ngozi unawafikia watu wengi zaidi.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Pratap Ghose alisema mchango huo katika kuwawezesha Chama cha Maalbino ni sehemu ya huduma za kampuni yake kwa jamii.

“Tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu miongoni mwa wanajamii, na kwa hakika hatua kubwa imepigwa katika kupambana na tatizo hili tayari, na sisi kama Zantel tunaamini kwa kutumia uwezo wetu kama kampuni ya simu tunaweza kushiriki kulimaliza tatizo hili la mauaji ya ndugu zetu’ alisema Pratap.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Tanzania ina jumla ya watu wenye ulemavu wa ngozi 5,200 na wengi wao wanaishi kanda ya ziwa, na toka mwaka 2009 jumla ya kesi 155 zinazohusu walemavu wa ngozi zimeripotiwa kwa vyombo vya sheria kwa mujibu wa taasisi ya Under the Same Sun.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya, ameipongeza kampuni ya Zantel kwa mchango wao akisema utasaidia sana katika juhudi zao za kupigania haki za walemavu wa ngozi nchini.

‘Watu wenye ulemavu wa ngozi ni kama binadamu wengine wa kawaida, hivyo tunaiomba jamii isiwatenge ndugu zetu hawa’ alisema Kimaya.

Bwana Kimaya pia aliomba wadau wengine wajitokeze kuwawezesha walemavu wa ngozi waweze kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo.


“Jamii yetu ya walemavu wa ngozi ina matatizo mbalimbali, hivyo tunazidi kuwaomba watu binafsi, serikali pamoja na makampuni mbalimbali wazidi kujitokeza kusaidia kundi hili la jamii’ alisisitiza Kimaya.

Chama cha Maalbino Tanzania kilianzishwa mwaka 1978 kikiwa na lengo la kulinda na kuwezesha watu wenye ulemavu wa ngozi nchini na kinahudumia zaidi ya wanachama 1,200. 

BENKI YA CRDB YASAIDIA KAMATI YA AMANI YA DINI

$
0
0

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum wakionyesha hundi ya shilingi milioni 12 kwa ajili ya maandalizi ya futari iliyoandaliwa na Kamati ya Amani ya viongozi wa Madhehebu ya dini itakayofanyika Ijumaa Julai 3 kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum  akitoa shukrani zake baada ya kupokea hundi ya sh. milioni 12 kutoka benki ya CRDB.
 Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa  akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi milioni 12 kwa ajili maandalizi ya Futari iliyoandaliwa na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini. Kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.  
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mbalali, Chibby Chibby akiwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mbalali, Chibby Chibby akibadilishana mawazo na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.
Picha ya pamoja.
Viewing all 49516 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>