Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

ZANTEL PARTNERS & DONATES TO TANZANIA ALBINO SOCIETY (TAS)

$
0
0
 Zantel CEO  Pratap Ghose handing over a dummy cheque to TAS chairman

Albinism is a genetically inherited disorder resulting from inability to produce melanin, a dark pigment that colors skin, hair and eyes; this situation leaves the affected people colored hence becoming different from others. For some time now Tanzanians have been witnessing a wave of brutal killings of people with albinism, commonly known as albinos.

Albinos in Tanzania have been facing serious problems of being killed and stigmatization, the killings have been driven by the belief advanced by some witchdoctors that the body parts have properties that confer wealth and good luck, a lot of progress has been made in this cause already by the government, NGOs and business communities.
 Zantel Marketing Director Ms. Progress Chisenga shakes hand with TAS Chairman Mr. Ernest Kimaya

As Zantel, we feel this is a critical moment for Tanzanians, and we want to be part of this important communications campaign to help end Albinism related deaths in Tanzania by using our core capacity as a telecom company to get the message out.

As part of our corporate social responsibility, ZANTEL is supporting TAS, in areas of public education, visibility and a donation, embarking in a journey together with Tanzania Albino Society to organize a campaign geared to promote awareness on albinism to our customers

ZANTEL is investing in educating the public on matters pertaining albinism by sending bulk SMS to our customers and using our various media programs.

ZANTEL will also provide different platforms to ensure visibility of Albinism messages through our staff meetings and other company events.
Zantel CEO Pratap Ghose shaking hands with a member of TAS. Last but not least, ZANTEL is also donating 5 million Tanzanian shillings to support the organization operations in the country.

APPRECIATION

$
0
0

The family  of the late Judge(Rtd) Anthony Bahati  of  Oysterbay - Dar es-salaam  would like to express  our heartfelt thanks   to relatives, friends, neighbours, and well wishers who  joined us throughout the difficult  period  of nursing and later  bereavement of our beloved father  who passed away on the 28thMay,2015 at Muhimbili National Hospital (MNH) and was peaceful laid  at Kinondoni grave yard  on the  2nd June,2015.

The family sincerely valued your spiritual, moral and material support extended to us during our difficult moments. It is our sincere wish to mention all who participated in all errands in one way or another but the list is too long, for those who are not   mentioned here, we humbly valued your participation and contribution hence kindly accept our appreciation. Specifically, the family would like to mention the following;

The State House, the  First Lady  Mama Salma Kikwete,Hon. Mizengo Pinda, the Prime Minister, the Principal Judge, Judges and staff of the High  the Court, retired  judges, Chairman of the Law Reform Commission, Regional Commissioner   of  Dar-es  salaam, Coast,Morogoro and Arusha, Regional Administrative  Secretaries of Dar-es salaam  and Coast Region, Chief Court  Administrator, doctors and nurses at Muhimbili National Hospital, Tanganyika Law Society, Regional Commissioner-Dar-es salaam, Saint Peter’s Church Parish priest, Don Bosco choir-from Tabata Kimanga, UDSM class of 1968 Faculty of Law,Jumuiya  ya Moyo Mt. wa  Yesu-Oysterbay, National Social Security Fund(NSSF),ADEM,SWISSPORT,LRCT  and  Judge (rtd)  Stephen  Ihema.

We also extend our appreciations to all MZIWA members.
There will be a requiem mass on Saturday 4thJuly, 2015 at 11:00 am at St. Peters Church-Oysterbay. 

Thereafter we cordially invite you to join us for lunch at Oysterbay- Mzinga way No. 14 from 12.45pm.

                “ A tree is known by its fruit; a man by his deeds.’’
   ‘ 'A good deed is never lost; he who sows courtesy reaps friendship     and who plants kindness gathers love’’. Saint Basil. 

POLISI ARUSHA KUWAFANYIA USAILI ASKARI WATARAJIWA

$
0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus Sabas  
Na woinde shizza,arusha.


Jeshi la Polisi Mkoani hapa linatarajia kuwafanyia usaili vijana wa Mkoa huu waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014 ambao wamechaguliwa kupitia tovuti ya Tamisemi ambayo ni www.pmoralg.go.tz.  Wanaotarajia  kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Polisi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus Sabas aliyasema hayo ofisini kwake leo asubuhi ambapo alisema zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku mbili mfululizo yaani kuanzia tarehe 06.07.2015 na tarehe 07.07.2015 katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi za Mkoa huu.


Aidha alisema zoezi hilo litaanza kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 10:00 Jioni huku tayari majina ya vijana waliochaguliwa na maelezo yake yameshabandikwa katika ofisi za Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa wilaya ya Arusha Mjini huku wilaya za Longido, Arumeru, Monduli, Karatu na Ngorongoro majina yao yatabandikwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri husika za wilaya hizo.


Waombaji watatakiwa wawe na vyeti vyote vya masomo (Academic Certificate(s)/Result Slip(s) & Leaving Certificate(s) na nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (original Birth Certificate) huku Hati ya Kiapo cha kuzaliwa haitakubaliwa pia atatakiwa kuwa na namba za simu ambayo itasaidia kumjulisha endapo atachaguliwa.


Aidha Kamanda Sabas alisema kwamba kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili huku atatakiwa kuwa na kalamu ya wino kwa ajili ya usaili wa kuandika bila kusahau kuzingatia tarehe na muda kuanza usaili.

Kamanda alimalizia kwa kusema kwamba, Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye ili mradi awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili.

DC MAVUNDE AZINDUA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU MPWAPWA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Adv. Anthon Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpira wa Miguu kuwania Kombe la DC na kushirikisha timu 24 kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo jana.
Timu za Mpwapwa Academy na Kota FC zikizubiri kukaguliwa na mgeni rasmi. Katika mchezo huo wa ufunguzi Kota FC wqalishinda goli 3-2.
DC akikaribishwa kusalimiana na wachezaji.
Mdhamini wa michuano hiyo ya DC Cup 2015, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Anthony Mavunde akisalimia wachezaji wa Kota FC.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Anthony Mavunde akisalimia wachezaji Mpwapwa FC
Wachezaji wa Mpwapwa FC wakiwa tayari kuanza pambano lao.
DC Mavunde akipata maelezo kutoka kwa viongozi wa mpira Mpwapwa.

TUWAONEE HURUMA - LAKE ZONE ALL STARS (NEW AUDIO)

MSAADA WA VIFAA KWA WANANCHI WA JIMBO LA RAHALEO

$
0
0
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akimkabidhi Seti ya Komputer Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo,kwa ajili ya matumizi ya Chuo hicho vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar,  akimkabidhi Vyerehani Mkuu wa Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo Zanzibar Bi Hawa Seif Amour, kwa ajili ya matumizi ya Wanafunzi wa Kituo hicho,vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akimkabidhi Seti ya Komputer Mkuu wa Chuo cha Ualimu Rahaleo Ndg Ussi Said Suleiman, kwa ajili ya matumizi ya Chuo hicho vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.
Wanafunzi wa Skuli ya msingi Rahale wakimpokea Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar alipowasili katika viwanja vya Skuli hiyo kukabidhi Vifaa viliotolewa na Mwakilishi wa Rahaleo kwa Wananchi wa jimbo hilo.




Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar, akimkabidhi Seti ya Vifaa vya ufundi gereji Kijana Zuberi Issa Ford,kwa ajili ya matumizi ya kazi zao za ufundi wa pikipiki  vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Rahaleo kuhudhuria hafla ya kukabidhi Vifaa kulia Mwakilishi wa Rahaleo na kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Rahaleo Ndg Daudi Amani Bakari
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa kwa Wananchi wa Jimbo lake iliofanyika katika Skuli ya Msingi Rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar, akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Rahaleo na wanafunzi wa skuli hiyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vilivyotolewa na Mwakilishi wa  Jimbo hilo Mhe. Nassor Salim Jazira.
Wanafunzi wa skuli ya msingi rahaleo wakimsikiliza Mhe Waziri Zainab akitowa nasaha zake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa 

Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo wakifuatilia nasaha za Mhe Waziri Zainab wakati akizungumza na Wananchi wa jimbo la Rahaleo katika hafla ya kukabidhi vifaa,
         Wazee wa Kamati ya Jimbo la Rahaleo wakimsikiliza Waziri Zainab Omar akiwahutubia.
                                         Walimu wa Skuli ya Rahaleo wakifuatilia hafla hiyo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akimkabidhi fedha Mkuu wa Chuo cha Ualimu Rahaleo Ndg Ussi Said Suleiman, kwa ajili ya kuogezea kusajili Chuo chao NACTE,fedha hizo ikiwa ahadi alioyowaahidi Viongozi wa Chuo hicho kwa ajili ya kufanya usajili wa Taifa.
Mzee wa kamati ya Jimbo la Rahaleo Ali Vuai Mussa akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa kwa wananchi wa jimbo la rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Zaiba Omar, na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Kamati ya Jimbo la Rahaleo, baada ya hafla hiyo ya kukabidhi vifaa. ilofanyika katika skuli ya rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Zaiba Omar, na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo, baada ya hafla hiyo ya kukabidhi vifaa. ilofanyika katika skuli ya rahaleo Zanzibar.

Upendo Nkone kumsindikiza Bonny Mwaitege

$
0
0
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Tanzania, Upendo Nkone amekuwa wa kwanza kujitokeza kusindikiza uzinduzi wa mwenzake Bonny Mwaitege, utakaofanyika Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,  Alex Msama Nkone amekuwa wa kwanza na ameonesha nia ya kumsindikiza Mwaitege kwa sababu ya ubora wa uzinduzi huo. “Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi mkubwa  hasa hatua za mwisho za rekodi ya albamu hizo inayomaliziwa  jijini Mwanza na baadaye Nairobi,” alisema Msama.

Msama alisema Mwaitege anatarajia kuzindua albamu  tatu  ambazo zitashika anga la muziki huo hapa nchini kwa sababu ya ubora. Msama alisema sambamba na muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa albamu hizo.

Aidha Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa kupata neno la Mungu kupitia muimbaji huyo.  Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo.
 

BONANZA LA MASAUNI CUP LAENDELEA ZANZIBAR

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Abdalla Bulembo wa kwanza kushoto Mbunge wa Kikwajuni Mhe Hamad Masauni na Kada wa CCM Abass Bahari wakijiandaa kuelekea kukagua timu hizo wakati wa Bonaza hilo linaloendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja usiku kwa micxhezo miwi kila siku.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Muembeladu kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa Bonaza katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar, Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Rahaleo,kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa Bonaza katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar, Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar. 
Kikosi cha timu ya Muembeladu kinachoshiriki michezo ya Bonaza la Kombe la Masauni.
           Kikosi cha timu ya Rahaleo,kinachoshiriki michezo ya Bonaza la Kombe la Masauni.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akizungumza na wanamichezo wakati wa mchezo wa Bonaza Kombe la Masauni na kuwataja vijana kukuza michezo ndio mafanikia yao kujipatia ajira, Michezo huleta amani na utulivu katika nchi. Na kuahidi timu itakayoshinda katika mchezo huo ataizawadia shilingi laki moja. kwa bahati mbaya timu hizo zimetoka sare na kukabidhiwa kila moja shilingi 50,000/- baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa sare ya 2--2  
Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimiliki mpira huku mchezaji wa Rahaleo akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo wa Bonaza Masauni Cup.

Wachezaji wa Rahaleo na Muembeladu wakiwania mpira katika mchezo wa Bonaza Masauni Cup linalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku. 
                           Mchezaji wa timu ya Muembeladu akiondoa mpira.
Wapenzi wa mchezo wa soka Zanzibar wakifuatilia michezo ya Bonaza ya Kombe la Mbunge wa Kikwajuni Mhe Hamad Masauni. Masauni Cup.Bonaza
                     Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimpita mchezaji wa timu ya Rahaleo.
Kocha wa timu ya Rahaleo akitowa maelekkezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wao na timu ya Rahaleo uliofanyika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya 2--2
Kocha wa timu ya Muembeladu akitowa maelekkezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wao na timu ya Rahaleo uliofanyika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya 2--2
                                                      Kizazaa golini kwa timu ya Rahaleo
Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimpita mchezaji wa timu ya Rahaleo akiwa chini, wakati wa mchezo wao wa Bonaza Kombe la Masauni timu hizo zimetoka sare ya 2--2
Golikipa wa timu ya Rahaleo Saleh Machupa akiokoa mpira golini kwake wakati wa mchezo wao Bonaza Kombe la Masauni inayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni ili kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar.

Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Ethiopia wazindua kiwanda cha Kudhibiti Malaria Pwani

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua rasmi kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo.Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiangalia uzalishaji wa viuadudu vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn muda mfupi kabla uzinduzi wa kiwanda cha kudhibiti malaria Mkoani Pwani leo. (picha na Freddy Maro).

TAASISI ZA ULINZI NA USALAMA ZAPATIWA MAFUNZO

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Major General G.S Milanzi kulia akiongea na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Helmas Mwansoko kushoto kabla ya Prof. Mwansoko kutoa Mhadhara juu ya Utamaduni unavyochangia katika usalama na ulinzi wa Nchi kwa Viongozi wa Ulinzi na usalama wa ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi za umma.Mhadhara huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.d2
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Helmas Mwansoko akitoa mada kwa Viongozi wa Ulinzi na usalama wa ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi za umma juu ya Utamaduni unavyochangia katika usalama na ulinzi wa Nchi .Mhadhara huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.d3
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Helmas Mwansoko akitoa mada kwa Viongozi wa Ulinzi na usalama wa ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi za umma juu ya Utamaduni unavyochangia katika usalama na ulinzi wa Nchi .Mhadhara huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.Picha na Benjamin Sawe

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YANG’ARA KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA SABASABA

$
0
0
Mmoja wa wakina mama kutoka Kikundi cha Wachimbaji  Madini Wanawake Tanzania, (Tanzania  Women  Mining Association) Shamsha  Diwani (katikati) akitoa maoni yake  mara baada ya kutembelea banda la Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi Nchini ( TANSORT) kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere  jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi Nchini ( TANSORT) Dorcus Moshi (katikati) akiwaelimisha   watoto waliotembelea banda hilo  aina za madini yanayopatikana nchini Tanzania.

Baadhi ya wananchi wakiangalia aina za madini  ya mawe katika banda la  Wakala wa Jiolojia Nchini (GST), kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere  jijini Dar es Salaam.
Banda la Wizara ya Nishati na  Madini  kama linavyoonekana pichani kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere  jijini Dar es Salaam
.
Afisa Uokoaji kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Evarist Mwanakatwe (kulia) akielezea kazi ya uokoaji inavyofanywa na mgodi huo pindi yanapotokea maafa.

Mfano wa mtambo  wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji katika banda la Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ulikuwa kivutio kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Afisa Uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Evarist Mwanakatwe (katikati) akielezea mikakati ya mgodi huo katika  uimarishaji wa usalama katika shughuli za madini.
Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Philipo Mathayo (kushoto) akielezea sera ya madini  katika kuimarisha shughuli za uchimbaji madini nchini. 
Afisa Mawasiliano katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Suzan Mwita (kushoto) akitoa maelezo kwa maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini waliotembelea banda la mgodi huo.

Afisa Mazingira katika Mgodi wa Dhahabu (GGM) Paskazia Mwesiga (kushoto)  akitoa elimu  juu ya utunzaji wa mazingira katika mgodi huo kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere  jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Steven Lowoko  akiwaonesha wananchi jinsi umeme wa maji unavyozalishwa kupitia mfano wa mtambo wa kuzalisha  maji kwenye banda la TANESCO
Meneja Utawala Mfawidhi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) (Kulia) akielezea mafanikio ya mgodi huo kwenye banda la GGM.
Wataalam katika Wakala wa Ukaguzi wa  Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la TMAA.

ZOEZI LA UANDIKISHAJI LAENDELE VYEMA ZANZIBAR.

$
0
0
Na Rahma Khamis-Maelezo Zanzibar  .
         
Zoezi la uandikishaji katika Daftari la Wapiga kura kwa Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja limeendelea vyema ambapo Wananchi katika Mkoa huo wamejitokeza kwa wingi. Aidha hali ya Amani na Utulivu imetanda katika zoezi hilo jambo ambalo limewanya Maafisa wa Tume ya Uchaguzi kufanya kazi yao kwa wepesi.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kituo cha uandikishaji Shehia ya Binguni Wilayani huko, Khamis Kombo wakati akitoa maelezo kuhusiana na zoezi hilo lililoanza rasmi leo.

Amesema katika uandikishwaji huo wananchi wengi Wake kwa waume wamejitokeza ili kutimiza haki yao ya msingi ya Kidemokrasia. Aidha amefahamisha kuwa kundi kubwa la Watu wanaojiandikisha katika Zoezi hilo ni Vijana wapya waliotimza sifa za kuandikishwa.

Kwa upande wake Sheha wa Shehia hiyo Ali Yussuf Mussa amefahamisha kuwa watu wamejitokeza bila wasiwasi ili kutimiza lengo la zoezi hilo. Amesema changamoto kubwa iliyojitokeza ni baadhi ya Vijana kutojua Shehia zao za kujiandikisha na ambapo waliwaelekeza vyema na kupata haki yao.


Aidha amesema katika Shehia yao hakuna Viashiria vyovyote vya uvunjifu wa Amani kama ilivyodaiwa katika Mkoa wa Mjini magharibi na kwamba watu hufuata taratibu na kuandikishwa kwa wepesi.

“Mpaka sasa tunashkuru katika shehia yetu hali ni shuari licha ya mvua kunyesha kwa wakati ule zoezi hilo lilidorora kidogo kutokana na unyeshaji huo lakini kwa sasa zoezi linaendelea kwa salama na amani bila ya matatizo yoyote .’alisema Sheha wa Binguni.Hata hivyo Sheha huyo ametoa wito kwa Wananchi wote wenye sifa za kuandikishwa ambao hawajajitokeza wajitokeze ili kutimiza haki yao ya kidemokrasia.

Amesema hiyo ni fursa pekee kwa kipindi hiki na kwamba yoyote atakayekosa  itamlazimu kusubiri kwa kipindi cha miaka mitano kupata haki hiyo.
                           
          IMETOLEWA NA HABARIMAELEZO -ZANZIBAR

WIZARA YA AFYA ZNZ YAKABIDHIWA MAGARI YA MSAADA TOKA UENGEREA

$
0
0
Na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar .

Shirika la Shistosomiasis Control Initiative (SCI) la Uengereza limetoa Msaada wa Magari mawili aina ya Toyota Double Cabin kwa Wizara ya Afya Zanzibar kupitia kitengo chake cha Maradhi yasiyopewa umuhimu (NTD).



Akikabidhi msaada huo leo Mwakilishi wa Shirika hilo Dkt. Khalfan Abdallah Mohamed amesema lengo la Msaada huo ni kuiwezesha Zanzibar kupiga hatua katika mapambano yake na Maradhi hayo ambayo yanawaandama watu wengi.

Maradhi hayo ni pamoja na Matende, Minyoo,Kichocho ambayo ni vigumu kupata Misaada ya matibabu kutoka kwa Wafadhili wa jumuiya za kimataifa.

“Ni rahisi sana kuomba Msaada wa Maradhi kama UKIMWI kwa vile yanapewa kipaumbela na Wafadhili lakini maradhi mengine kama Minyoo au Matende ni vigumu sana kumshawishi mfadhili akasaidia” alisema Mwakilishi huyo wa SCI.

Amesema Gari hizo ni kwa ajili ya kazi za kitengo cha Maradhi yasiyopewa umuhimu na kwamba zitatumika zaidi katika zoezi la ulishaji Dawa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amelishukuru Shirika la SCI kwa mashirikiano ya muda mrefu na Wizara ya Afya kupitia kitengo cha NTD kinachoendesha zoezi la ulishaji Dawa Mashuleni na katika jamii kwa ujumla.

Aidha ametowa wito kwa Mashirika mengine ya maendeleo kuunga mkono jitihada za Wizara ya Afya Zanzibar katika kupambana na Maradhi mbalimbali ambayo yanadhoofisha afya za Wazanzibari kupitia Vitengo mbalimbali.

Waziri Mahmoud amezipokea gari kwa niaba ya Waizara ya Afya na kuliahidi Shirika la SCI kuzitunza ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Gari hizo mbili zitagawiwa ambapo Unguja itabakia moja na Pemba kupelekwa moja ili kusaidia mapambano ya Maradhi yasiyopewa umuhimu.

Imetolewa na Maelezo Zanzibar

MATUMIZI MABAYA YA ARDHI TISHIO KWA UHIFADHI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu 

Na Woinde Shizza,Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi
mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi
yamekua tishio kwa  maeneo uhifadhi hivyo kupelekea uvamizi wa maeneo
hayo na kutumiwa kwa shughuli za ufugaji na kilimo kinyume cha
utaratibu.

Nyalandu amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa kati ya
Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) uliofanyika jijini
hapa,amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu  utakaorithiwa na
vizazi vijavyo  mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi
kuzingatiwa.

Waziri huyo amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya uhifadhi
ikiwemo Hoteli na kumbi za starehe unaathiri shughuli za uhifadhi
hivyo amewataka wadau wa utalii kugawanya uwekekezaji  kwa kuwekeza
nje ya hifadhi.


“Mtu anayefikiria kujenga miji ndani ya hifadhi anakua hajapiga hesabu
vizuri  lazima tutawanye  uwekezaji hoteli zijengwe nje ya hifadhi”
Alisema Nyalandu.

Alisema kuwa kwa sasa Tanzania ina jumla ya Jumuiya za Hifadhi za
Wanyamapori (WMAs) 21 ambazo ni kilometa za mraba 36237.7 na jumuiya
nyingine  17 ziko katika hatua mbalimbali za uanzishwaji,amezitaka
jumuiya hizo kuhakikisha kuwa zinawashirikisha wananchi katika
kuhifadhi na kunufaika kwa mujibu wa sera ya wanayama pori ya mwaka
1998.

Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza watalii nchini Wilbard  Chambulo
alisema kuwa ili uhifadhi uweze kufanikiwa lazima wanakijiji wawe na
hati miliki za maliasili ili waweze kuzitunza vyema.
Chambulo anaeleza kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika uhifadhi ni
nguzo muhimu sana kwa uhifadhi  itakayosaidia kuwa na utalii endelevu
kwa vizazi na vizazi.

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA CHIFU KINGALU WA 14 WA WALUGURU, NA KUSIMIKWA KWA CHIFU KINGALU 15 KIJIJINI KINOLE, MOROGORO

$
0
0
u
Mama Salma Kikwete akimpa pole na pia kumpongeza Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru  wa Mkoa wa Morogoro Chifu Kingalu wa 15  baada ya kusimikwa rasmi kijijini Kinole mkoani Morogoro leo Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo na hatimaye mazishi ya kaka yake Marehemu Chifu Kingalu wa 14.
k
Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru wa Mkoa wa Morogoro Chifu Kingalu wa 15  akiongea machache baada ya kusimikwa rasmi kijijini Kinole mkoani Morogoro leo Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo na hatimaye mazishi ya kaka yake Marehemu Chifu Kingalu wa 14.
l
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  Kiongozi mpya wa kabila la Warugulu wa Mkoa wa Morogoro Chifu Kingalu wa 15  baada ya kusimikwa rasmi kijijini Kinole mkoani Morogoro leo Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo na hatimaye mazishi ya kaka yake Marehemu Chifu Kingalu wa 14.
PICHA NA IKULU
 t
Mama Salma Kikwete akimpa pole na pia kumpongeza Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru  wa Mkoa wa Morogoro Chifu Kingalu wa 15  baada ya kusimikwa rasmi kijijini Kinole mkoani Morogoro leo Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo na hatimaye mazishi ya kaka yake Marehemu Chifu Kingalu wa 14.

WILLIAM NGELEJA AREJESHA FOMU ZA URAIS MJINI DODOMA

$
0
0
mail.google.com
MBUNGE wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja, akirejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia CCM kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho mjini Dodoma,
mail.google.comm
MBUNGE wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja akibadilisha mawazo na wabunge wenzake, Ezekiel Maige (Msalala) na Dk. Delay Peter Kafumu (Igunga), wakati aliporejesha fomu kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.

……………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
MBUNGE wa Sengerema, William Ngeleja, amesema amepata fundisho kubwa katika harakati zake za kuwaomba udhamini ili ateuliwe kuwania urais na kwamba, limemuongezea shauku kubwa ya uongozi.
Ngeleja, ambaye amepata kuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, amesema yuko tayari kuwatumikia watanzania iwapo CCM kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera.
Akizungumza wakati akirejesha fomu za kuomba kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, Ngeleja alisema anatambua nafasi anayoimba ni nyeti na kwamba, amejipima na anatosha kubeba mikoba ya JK.
Alisema kazi ya kutafuta wadhamini katika mikoa mbalimbali nchini, Ngeleja alisema wakati wa zoezi hilo amejifunza mambo mengi na ambayo yamemfanya kuendelea kuifahamu nchi kijiografia na changamoto zake.
“Nipo tayari na shauku yangu ya kuliongoza taifa imezidi kupamba moto wakati wa zoezi la kuzunguka kuomba udhamini kwenye mikoa yote nchini. “Nimeona na kujifunza mengi na nimepata fursa ya ya kuona maendeleo makubwa yaliyofanywa na serikali yetu katika nyanja zote na changamoto ambazo bado zinatukabili kama taifa,” alisema Ngeleja.
Alisema watanzania wana shauku kubwa ya kupambana na umasikini na kwamba, nimejionea mwenyewe namna ambavyo watu wana shauku kubwa ya kupambana na umasikini.
“Unajua sisi wabunge mara nyingi tumekuwa na majukumu makubwa ya majimboni na mara nyingi tathmini tunayoifanya ya maendeleo kwa nchi yetu inatokana na kile kinachofanyika majimboni kwetu, lakini zoezi hili la udhamini limenipa fursa ya kuona kinachoendelea nchi nzima.
“Kila tulikopita tuliwakuta wananchi wanashiriki kwenye miradi ya ujenzi wa maabara za shule, madarasa ya shule, zahanati, watoto wanakwenda ama kutoka shuleni,” alisema Ngeleja.
Aliongeza kuwa jambo lingine ambalo amejifunza wakati wa kazi ya kusaka wadhamini ni kuwa Tanzania bado ni ya wakulima na wafanyakazi, ingawa makundi ya wavuvi, wafugaji, wajasiriamali, wafanyabiashara, wana michezo na wasanii nayo ni makundi makubwa katika jamii.
Ngeleja aliwaahidi wanachama wenzake wa CCM kuwa ili nchi ifanikiwe kupunguza umasikini na kufikia hadhi ya uchumi wa kati ifikapo au kabla ya mwaka 2025, ni lazima uwekezaji mkubwa ufanywe kwenye sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda, michezo na tasnia ya sanaa, ambazo zinaongoza kutoa ajira kwa zaidi ya asilimia 75 ya watanzania.
Kuhusu kilimo, Ngeleja alisisitiza kuwa ni muhimu kurejeshwa kwa hadhi ya kilimo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo, uchumi wa nchi ulibebwa na sekta hiyo hususan mazao ya biashara kama pamba, mkonge, korosho, karafuu, kahawa na michikichi.
Mgombea huyo kijana ambaye anatajwa kuwa ni miongoni mwa wachapakazi mahiri, ameendelea kujinadi kupitia kauli mbiu yake ya Maono Sahihi, Mikakati Thabiti, Matokeo Halisi (MMM).
“Kauli mbiu hii inabeba vipaumbele vinne ambavyo ni ujenzi wa uchumi imara, uimarishaji wa utawala bora, huduma za jamii na miundo mbinu,” alisema.
 Aidha, amejinadi kuwa na weledi wa hali ya juu kuhusu sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya maendeleo ya uchumi wa taifa lolote duniani.
Kuhusu uimarishaji wa CCM, Ngeleja ameendelea kuwaahidi wana CCM wenzake kwamba akifanikiwa kuwa akifanikiwa kupeperusha bendera na kushinda, ataendeleza maboresho yanayofanywa sasa na chama chake ili kulingana na kile cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, ambacho kina miradi ndani na nje ya nchi.

RAIS KIKWETE ASHUHUDIA KUSIMIKWA KWA KIONGOZI MPYA WA WALUGURU CHIFU KINGALU WA 15 KIJIJINI KINOLE, MOROGORO

$
0
0
01
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia kusimikwa kwa Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 katika kijijini Kinole mkoani Morogoro Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki jana Jumatano jijini Dar es salaam na kuzikwa leo kijijini hapo.
02
Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 akitolewa nje baada ya kusimikwa rasmi kuwa kiongozi wa kabla hilo kijijini Kinole mkoani Morogoro Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki jana Jumatano jijini Dar es salaam na kuzikwa leo kijijini hapo.
03
Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 akichomeka fimbo yake ya Uchifu kabla ya kuketi  meza Kuu na Rais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kusimikwa rasmi kuwa kiongozi wa kabla hilo kijijini Kinole mkoani Morogoro Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki jana Jumatano jijini Dar es salaam na kuzikwa leo kijijini hapo. PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AZINDUA KIWANDA CHA KUULIA MAZALIA YA MBU

$
0
0
T13
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiangalia uzalishaji wa viuadudu vya  mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi leo.T14
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiangalia uzalishaji wa viuadudu vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi leo.(Picha na Freddy Maro).J8
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakifungua jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
J9
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria, leo mkoani Pwani.
J10
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, leo mkoani Pwani.
J11
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda wakati wa Halfa ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria, leo mkoani Pwani, Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
J12
Balozi wa Cuba nchini Tanzania Bw. Jorge Luis Lopez akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichojengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Cuba na Tanzania, ambapo aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika masuala balimbali ya maendeleo leo mkoani Pwani.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichogharimu kiasi cha bilioni 61.5 za kitanzania, ambapo alipongeza mradi huo kwani utasaidia kuondoa ugonjwa wa malaria nchini, pia aliipongeza sekta ya afya kwa kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na malaria kwa asilimia 71 na wagonjwa wenye kuugua malaria kwa asilimia 51 kwa kipindi cha mwaka 2004-2014 leo Mjini Kibaha.
J2
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria ambapo aliipongeza serikali ya Tanzania katika kutekeleza Mradi huo utakaosaidia katika kupambana na vita dhidi ya malaria nchini Tanzania na Afrika kwa Ujumla, leo Mjini Kibaha.
J4
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria ambapo alishukuru na kupongeza uzinduzi wa kiwanda hicho kwani kitakuwa ni mwarobaini katika mapambano dhidi ya malaria kwa mkoa wa pwani na afrika kwa ujumla,leo Mjini Kibaha.
J5
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Abdalah Kigoda akiongea katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria na kuahidi kushirikiana kwa karibu na shirika la maendeleo ya taifa (NDC) katika kutekeleza majukumu ya kiwanda hicho ili kutekeleza agizo la Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika vita dhidi ya malaria kupitia Mradi huo, leo Mkoani Pwani.
J6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
J7
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo laTaifa (NDC) Dkt. Chrisant mzindakaya akimkabidhi zawadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
…………………………………………………………………..
 VICTOR MASANGU, KIBAHA-PWANI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete amesemaSerikali ina mpango wa nchi nzima wa kupulizia dawa kwa ajili ya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria  lengo ikiwa ni kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo hususani kwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Dokta Kikwete ameyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichopo eneo la TAMCO wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.
Raisi Kikwete alisema Serikali imekua ikipambana na ugonjwa huo  kwa kutumia dawa za malaria za Mseto na baadae Vyandarua vyenye dawa za kuua wadudu wa ugonjwaambavyo vilisambazwa kwa nchi nzima huo lakini bado haijafanikiwa kuuondosha kabisa hapa nchini pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika.
Alisema Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2007 hadi asilimia 10 mwaka 2012, ambapo pia idadi ya wagonjwa imepungua kutoka asilimia 51na vifo vimepungua hadi asilimia 71 kutoka mwaka 2004 hadi 2014..
Aidha Dokta Kikwete aliwataka wananchi kuendelea kutumia vyandarua vyenye dawa ili kuepuka kupata maambukizi ya ugonjwa huo na kuondokana na dhana potofu kuwa vyandarua hivyo vinasababisha madhara hususani kwa wamnaume.
Kwa upandewake Waziri wa Viwanda na Biashara Abdallah Kigoda alisema mikakati ya serikali ni kuongeza viwanda mama kwa ajili ya kukuza uchumi na kupunguza kasi ya ugonjwa wa malaria ambao umekua kikwazo cha maendeleo kwa wananchi.
Waziri huo pia alibainisha kuwa Serikali ina mikakati ya kufufua bandari za nchi kavu na majini ikiwa sambamba na kuboresha miundombinu ya reli ili kuwezesha kufika kwa urahisi kwenye maeneo ambayo yalikua vikwazo kwa wawekezaji wanaolenga kujenga viwanda na kuongeza fursa mpya ya ajira kwa watanzania hususani vijana ambao wataongeza pato la Taifa.
Waziri Mkuu wa Ethiophia na mwenyekiti wa kupambana na malaria barani Afrika HaileMariam Desalegn ataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo inaendelea kwa nchi za Afrika.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya NDC Christopher Mzindakaya alisema kuwa hadi sasa kiwanda hicho kimewaajiri wafanyakazi 145 na kimegharimu kiasi cha shilingi bilion 61.5 hadi kukamilika kwake pia kitakua na uwezo wa kuzalisha lita za ujazo milioni sita kwa mwaka.

SEHEMU YA HOTUBA YA KINANA MWANZA MJINI

Jenifer Mgendi azindua dvd yake ya wema ni akiba

$
0
0
Mmoja wa Waimbaji mahiri wa nyinbo za Injili, Jenifer Mgendi akiimba mbele ya wapenzi na washabiki wa nyimbo zake katika uzinduzi wa  dvd yake ya Wema ni akiba,uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar .
Wa pili pichani ni  Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Dr Barnabas Mtokambali akiionesha dvd ya Jennifer Mgendi ya Wema ni akiba baada ya kuizindua Jumapili iliyopita. Kulia ni Katibu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Mchungaji Ron Swai.
Baadhi ya Watumishi wa Mungu wakiiombea baraka dvd ya Wema ni akiba wakiongozwa na Dr Barnabas Mtokambali.
 Jenifer Mgendi akiiimba kwa hisia katika uzinduzi huo. 
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images