Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

MSIKITI WA GADDAFI DODOMA WAMSHUKURU MEMBE

$
0
0
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani (kulia) akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati), kwa waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani humo jana, wakati waumini hao walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. Kushoto ni Diwani wa Kwadelo, Alhaj Omary Kariati. 
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), kwa waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani humo jana, wakati 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati waumini hao, walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiagana na  waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati waumini hao walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani.


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akibadilishana mawazo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani, wakati waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma, walipomwita jana kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), Mkoani humo, Zidikheri Swedy Kheri.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani (kushoto), wakishiriki katika chakula cha usiku kilichoandaliwa na waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiagana na viongozi wa dini ya kiislam mkoa wa Dodoma jana,  wakati waumini wa Msikiti wa Gaddafi, walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi.


YAMOTO BAND KUPIGA SHOW MBILI KABAMBE NDANI YA "USA" NOVEMBER 28 -HOUSTON TX | DECEMBER 5 -WASHINGTON DC

$
0
0
*** INFOS- 301-661-6207 | 713-373-6525 | 240-605-1870***

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AWAPA FUTARI WATOTO YATIMA

$
0
0
  mail.google.comZ
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimia na baadhi watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya malezi aliowaalika kupata futari katika viwanja vya ikulu-Juni 29, 2015. picha na Freddy Maro  .mail.google.comV
mail.google.com
Baadhi ya watoto yatima kutoka katika vituo mbalimbali vya malezi mkoa wa Dar es Salaam wakipata futari katika viwanja vya ikulu.

WASANII WAOMBA KUPUNGUZIWA KODI KWENYE VIFAA VYA MUZIKI.

$
0
0
1 Msanii G Nako kutoka Kundi la muziki wa kizazi kipya la Weusi akiimba sambamba na msanii mchanga ambaye hakufahamika mara moja kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.  

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Kundi la Weusi Nick wa Pili (Kushoto) akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa inayofanyika kwa mwezi mara mbili siku ya Jumatatu makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto kwake ni wasanii wanaounda kundi hilo John Simon aka Joh Makini na G Nako na Afisa kutoka BASATA Bi. Elineca Ndowo. 

1 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mitaji na Misaada kwa wasanii kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi. Elineca Ndowo (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) kuhusu masuala mbalimbali kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ambayo huandaliwa kwa mwezi mara mbili ziku ya Jumatatu na Baraza hilo. Wengine katika picha kulia kwake ni Wasanii G Nako na John Simon maarufu kama Joh Makini wanaounda kundi la muziki wa kizazi kipya la Weusi. 


Baadhi ya wasanii nchini wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Fedha kufikiria kupunguza au kufuta kabisa ushuru wa forodha unaotozwa kwenye vifaa vya muziki wanavyoagiza kutoka nje ili kukuza Sanaa na kusaidia mamilioni ya vijana ambao wamejiajiri kupitia sekta hiyo.


Akizungumza kwa niaba ya wasanii mapema wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mmoja wa wasanii anayeunda kundi la muziki wa kizazi kipya la Weusi Nick wa Pili alisema kwamba, kwa sasa sekta hiyo ni kimbilio la ajira kwa vijana wengi kwa hiyo Serikali haina budi kupunguza kodi kwa zana mbalimbali zinazotumiwa na wasanii ili kurahisisha uzalishaji, kukuza tija na uchumi.


“Wasanii wengi kwa sasa wanakwenda kufanya video na kutengeneza muziki nje ya nchi. Hii inatokana na teknolojia yetu kuwa chini ya wenzetu. Naamini Serikali ikipunguza kodi katika vifaa hivi na kuwawezesha wataalam tulionao basi nchi zote jirani zitakimbilia kwetu” alisema Nick.

Aliongeza kwamba vipaji vya wasanii vipo vingi lakini kutokana na uzalishaji duni wa kazi za muziki na hata filamu wasanii wamejikuta wakishindwa kushindana ipasavyo nje ya nchi na mara nyingi kutumia gharama kubwa katika kufuata teknolojia hizo za juu nchi za nje na hivyo kuikosesha serikali mapato.

“Wasanii wanakwenda kulipa zaidi ya milioni arobaini kwa video moja tu nje ya nchi, hizi fedha zinakwenda kukuza uchumi wa nchi zingine. Naamini kama Serikali ikijenga mazingira mazuri ya kiteknolojia na zaidi kushusha gharama hizi basi nchi yetu itafaidika zaidi na Sanaa” alizidi kusisitiza Nick.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mitaji na Misaada kwa wasanii kutoka BASATA Bi. Elineca Ndowo alisema kwamba sekta ya Sanaa nchini inazidi kukua na hivyo lazima wasanii nao wafikirie kufanya kazi kisasa na kwa kufuata taratibu zote ili kuipa serikali uhakika katika kupanga kulingana na hali halisi.


“Sekta ya Sanaa inakua, lazima tuisaidie Serikali kuipa takwimu sahihi na moja ya njia ya kuhakikisha hili ni kwa wasanii kujisajili, kusajili kazi zao na kuhakikisha taarifa sahihi na kwa wakati zinapatikana. Hili litarahisisha upangaji wa mipango” alisema Bi. Ndowo.


Jukwaa la Sanaa la BASATA ni programu ambayo hufanyika kwa mwezi mara mbili siku ya Jumatatu na hutumika kama jamvi la kuwaelimisha wasanii na kuwakutanisha kwa pamoja katika kubadilishana uzoefu na mawazo kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo sekta yao.  

KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA

UZINDUZI WA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA SHINYANGA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bwana Michael Mhando akitoa taarifa fupi kuhusu mpango wa huduma ya madaktari bingwa unaoendeshwa na NHIF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bwana Alli Nassoro Rufunga akizungumza na wananchi na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga waliokuja kupata huduma kabla ya kzindua rasmi mpango huo.
 Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliokuja kupata huduma za madaktari bingwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Michael Mhando akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga vifaa tiba vitakavyotumika katika zoezi hilo la siku tano.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akisalimiana na mmoja  wa madaktari bingwa Dokta Vicencia Sakware ( Mtaalamu wa Dawa za Usingizi na Wagonjwa Mahututi)
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akiagana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bwana Michael Mhando na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri wa KItaalamu Dokta Frank Lekey baada ya uzinduzi wa huduma za madaktari bingwa.
 
Akizungumza kuhusu mpango huo wa kupeleka madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bwana Michael Mhando amesema Mfuko unatekeleza mpango huo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kupeleka huduma bora za matibabu kwa wananchi wote. 

Ameongeza kuwa utekelezaji wa mpango huo unakusudia kuwapunguzia wananchi wamikoa ya pembezoni gharama za kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa ambazo ziko mbali na maeneo wanayoishi.

Hadi sasa mpango huo umeshatekelezwa katika mikoa ya Lindi, Kigoma, Rukwa, Katavi, Pwani, Tabora, Mara Manyara na Mtwara na kuwanufaisha zaidi ya wananchi 7800.
 
Katiba hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amewapongeza madaktari  bingwa hao kwa moyo wao wa kujitolea na kuwataka wengine kuiga mfano wao. Aidha amemwagiza Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa vifaa tiba  vilivyotolewa na NHIF viendelee kutunzwa ili viwanufaishe wananchi wengi zaidi.

Bwan Rufunga pia amewahimiza wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujiunga  kwa wingi katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waondokane na unyonge wa kutibiwa kwa kutumiwa fedha taslimu  na badala yake watibiwe kwa kutumia kadi za CHF.

WAZIRI NYALANDU AZINDUA KAMPENI MPYA YA KUWAHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA JIJINI MWANZA LEO

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akiwa amekata utepe kuashiria uzinduzi wa usafiri wa boti (Majini) katika suala zima la kurahisisha  kuhamasisha kampeni ya Uhamasishaji Watanzania Kutembelea Hifadhi za Taifa,hafla hiyo imefanyika mapema leo asubuhi ndani ya Yatch Club,jijini Mwanza,kulia ni  Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi 
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akiwa amekata utepe kuashiria uzinduzi wa usafiri wa magari (nchi kavu) katika suala zima la kurahisisha  kuhamasisha kampeni ya Uhamasishaji Watanzania Kutembelea Hifadhi za Taifa,hafla hiyo imefanyika mapema leo asubuhi ndani ya Yatch Club,jijini Mwanza
Picha ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa kampeni ya Uhamasishaji Watanzania Kutembelea Hifadhi za Taifa,hafla hiyo imefanyika mapema leo asubuhi ndani ya Yatch Club,jijini Mwanza.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza mapema leo asubuhi ndani ya Yatch Club wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni ya Uhamasishaji Watanzania Kutembelea Hifadhi za Taifa,hafla hiyo imezinduliwa jijini Mwanza .
 Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza mapema leo asubuhi ndani ya Yatch Club wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni ya Uhamasishaji Watanzania Kutembelea Hifadhi za Taifa,hafla hiyo imezinduliwa jijini Mwanza.

 Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza mapema leo asubuhi ndani ya Yatch Club wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni ya Uhamasishaji Watanzania Kutembelea Hifadhi za Taifa,akiwa amezungukwa na baadhi ya Wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali ambao watahusika kwa namna moja ama nyingine kushiriki kuhamasisha watu mbalimbali katika suala zima la kutangaza utalii wa ndani. 

MAONYESHO YA 39 YA KIMATAIFA YA BIASHARA KATIKA VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Wananchi wakiangalia kifaa kilichotengenezwa na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa ajili kusoma kiwango cha maji kwa  bei  uliyoweka na fedha yake unatumbukiza kisha maji yanaanza kutoka walipotembelea maonyesho ya 39  ya Kimataifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Madhari ya maonyesho ya 39  ya Kimataifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakiwa katika Harakati za kutembelea mabanda  ya maonyesho ya 39  ya Kimataifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Ofisa wa JKT akionyesha wananchi  jinsi wanavyofuga kwa kisasa katikamaonyesho ya 39  ya Kimataifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. (picha na Emmanuel Massaka).

UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA KOREA WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
 Mmoja wa wafanyabishara wa nishati kutoka Korea akiangalia  vinyago kwenye banda la  Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) kwenye Maonesho  ya Kimataifa ya  Sabasaba (Dar es Salaam International  Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

 Afisa wa Huduma kwa Wateja kutoka Shirika la  Umeme Nchini (TANESCO)  Lucas Kusare ( wa pili kutoka kulia) akiwaonesha  wafanyabiashara wa nishati kutoka Korea mfano wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa njia ya maji katika  Banda la  TANESCO kwenye Maonesho  ya Kimataifa ya  Sabasaba (Dar es Salaam International  Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

Mtaalam kutoka Idara ya Madini Mhandisi Rayson Nkya (Katikati) akimwonesha  Makamu wa Rais wa Kampuni  ya  Energy and Minerals  Resources Development  Association ya Korea,  Dk. Song Jae Ki (Kulia) moja ya machapisho  ya Wizara ya Nishati na Madini kwenye Maonesho  ya Kimataifa ya  Sabasaba (Dar es Salaam International  Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni   Godfrey Fweni kutoka  Idara ya Madini ya Wizara hiyo.

Mtaalam kutoka Idara ya Nishati,  Yusuph  Msembele (Katikati) akimwonesha mmoja wa wafanyabiashara kutoka  Korea (kulia, anayepiga picha machapisho hayo) machapisho ya Idara ya Nishati.

Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Korea (Kulia) akiangalia vinyago katika banda la Kituo cha Jimolojia  Tanzania (TGC) Kushoto ni Afisa Utawala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Matiko Sanawa.

Washirki kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Maonesho  ya Kimataifa ya  Sabasaba (Dar es Salaam International  Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.



INTRODUCING Alikiba Chekecha Cheketua Official Video

ACACIA YAKUSANYA SHILINGI MILIONI 800 ZA KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU, BAADA YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
 MKUU wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Glorious Luoga, (Katikati), akinyanyua juu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 800, baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampouni ya Acacia, Brad Gordon, (kushoto), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye lango la kushukia kutyoka kilele cha  Mlima Kilimanjaro, Mweka, Juni 28, 2015,  Fedha hizo ambazo ni kwa ajili yab kusaidia sekta ya eli kwa watoto kutoka familia duni, zimetokana na wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki, kupanda Mlima Kilimanjaro kwa nia ya kuchangisha fedha chini ya mpango wa kampuni hiyo wa "CanEducate".

Kampuni ya Uchimbaji Acacia, inayojishughulisha na uchimbaji na utafutaji madini, , imekusanya zaidi ya shilingi milioni 800 kupitia upandaji wa hisani wa mlima Kilimanjaro ambao unalenga kuchangisha fedha za kusaidia sekta ya elimu nchini chini ya mpango wa “CanEducate”, uliobuniwa na kampuni hiyo miaka mitano iliyopita.

Timu ya wafanyakazi, marafiki na wanafamilia wa Kampuni ya Acacia wapatao 21 wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon, wamerudi kutoka safari ya kupanda mlima Kilimanjaro iliyowachukua siku sita.
Kupitia mpango huo wa CanEducate, mpango ambao unatoa ufadhili wa elimu kwa watoto wanaotoka familia duni, zinazoishi maeneo yanayozunguka migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo, ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi, Acacia imeanza utaratibu wa kila mwaka wa kualika wafanyakazi, marafiki na wahisani kuchangisha fedha kwa njia hiyo ya upandaji mlima.



Akizungumza na wandishi wa habari kwenye lango la kushukia la Mweka, Afisa Mtendaji Mkuu wa Acacia amesema ni jambo la kujivunia kuona kampuni imefikia lengo la kukusanya kiwango cha dola 200,000, sawa na shilingi za Kitanzania Milioni 800, kupitia zoezi hili, fedha ambazo zitakuwa na matokeo makubwa sana  kwa kugusa maisha ya watoto wengi nchini Tanzania.




“Tayari tumekwisha fikia lengo la kukusanya dola 200,000 huku michango zaidi ikiendelea kumiminika. Tunayaasa makampuni na watu binafsi kuendelea kuchangia kwani zoezi lipo wazi hadi mwisho wa mwezi Julai,” alisema Brad.



Aidha, ameongeza kuwa kwa kila dola moja itakayochangwa na wafadhili, pia Kampuni ya Acacia itaongeza dola moja na hivyo kufanya jumla ya fedha zitakazoelekezwa kusaidia sekta ya elimu kupitia mpango huu kufikia kiasi cha dola 400,000 kwa mwaka huu.



Kwa kuzingatia kuwa inagharimu kiasi cha dola 75 kwa mwaka kupeleka mwanafunzi shuleni nchini Tanzania, fedha zilizokusanywa zina uwezo wa kusaidia wanafunzi zaidi ya 2,000 wasioweza kumudu gharama za masomo hususani kutokea jamii jirani na migodi ya Acacia yaani Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara iliyoko mkoani Shinyanga na Mara.



Mpango wa CanEducate ulianza mwaka 2010 kwa kuwanufaisha wanafunzi takribani 158 katika maeneo ya Bulyanhulu na hadi mwisho wa mwaka 2014 mpango umekuwa hadi kufikia kuwanufaisha wanafunzi zaidi ya 1,800 katika maeneo ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara na wanafunzi hawa wameonyesha ufaulu mzuri katika shule mbalimbali katika mitihani yao ya Taifa.



Mlima Kilimanjaro,, unatambulika kuwa  mlima mrefu zaidi barani Afrika nan i wa tatu duniani ambao kufikia kilele cha Uhuru mita 5,895 ni hatua ya juu barani Afrika. Kampuni ya Acacia ina mtazamo kuwa  Elimu humfanya binadamu kuwa huru sababu ambayo inaufanya mpango wa CanEducate kufaa kukusanya  fedha kupitia kupanda mlima hadi kufikia kilele cha Uhuru Peak.



Waweza kuchangia Elimu kupitia upandaji mlima huu wa hisani, kupitia tovuti ifuatayo;

http://caneducate.ca/kili-climb.html

 Brad, (kushoto), akikabidhi hundi hiyo kwa Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga
 Brad, akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo, akiwa
 Brad Gordon, (wakwanza kulia), akiongoza timu ya watu 21, wakiwemo wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki, kushuka Mlima Kilimanjaro wakitokea kileleni, kwenye lango la Mweka
 Furaha baada ya kufanikiwa kufika Kilele cha Mlima Kilimanjaro na kurejea salama
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Acacia, Brad  Gordon, (Katikati), Makamu wa Rais wa Acacia anayeshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, (wakwanza kulia), Meneja Mkuu wa uendelezaji wa kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo, (wapili kulia), Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga, (watatu kulia),wakiwa katika picha ya pamoja na watu 21 waliofanikiwa kupanda Mlima Kilimanjaro
 Brad, akipongezana na Deo
Deo akitoa shukrani baada ya timu ya watu 21, walioongozwa na Brad, kufanikiwa kupanda na kurejea salama kutoka kilele cha mlima Kilimanjaro

UTT-PID na SUMA JKT kujenga nyumba za kisasa za kuuza kwa askari na maofisa wa jeshi na umma

$
0
0
2015-06-26 15.13.03Mtendaji Mkuu wa UTT-PID, Dr. Gration Kamugisha (kushoto) akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu Lt-Colonel, Felix Samillan baada ya kutiliana saini ya mkataba wa kujenga nyumba za kisasa za kuuza kwa askari na maofisa wa jeshi na umma mradi unaotarajiwa kujengwa Chalinze

Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) kwa kushirikiana na Taasisi ya SUMA JKT imesainiana mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa nyumba za kisasa za kuuza kwa askari na maofisa wa jeshi na Umma, tukio lililofanyika Juni 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam.Katika tukio hilo, Taasisi ya UTT PID iliwakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu Dr. Gration Kamugisha na Taasisi ya SUMA JKT iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu Lt-Colonel, Felix Samillan huku mradi huo ukitegemea kuanza katika kipindi cha mwaka mpya wa fedha wa serikali Julai mwaka huu.

Aidha, nyumba zinazotarajiwa kujengwa zitakuwa ni za vyumba viwili na vitatu katika miundo mbalimbali na za kuvutia ambazo zitakuwa za mfumo wa kisasa kwa kuishi kifamilia pia. Katika mkataba huo utatanguliwa na ujenzi wa nyumba za mfano katika eneo la Chalinze na mara baada ya ujenzi huo kukamilika, Nyumba za mradi zitajengwa kwa walengwa wote watakaokuwa wameomba na kukidhi vigezo muhimu vya kupata nyumba hizo.

UTT-PID inafanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.

Pia wanaendesha miradi ya viwanja maeneo mbalimbali nchini ikwemo Bagamoyo, Chalinze Mkoa wa Pwani, Lindi, Kagera, Korogoro na mikoa mingine mingi.

UMOJA WA MATAIFA WAHUDHURIA MAONYESHO 39 YA KIBIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mtaalamu wa Mawasilano wa Umoja wa Mataifa Tanzania (UN), Hoyce Temu akizungumaza na MICHUZI BLOG baada ya kutembelea banda la umoja wa mataifa,katika maonyesho ya kimataifa ya 39 ya kibiashara yanayoendelea kufanyika katika viwanja Mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu wa Mawasilano wa Umoja wa Mataifa Tanzania (UN), Hoyce Temu akifanua juu ya namba mbalimbali zitakazo tumika kwa wananchi ili kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na umoja wa Mataifa-Tanzania, katika viwanja vya Mwalimu nyererejijini Dar es Salaam.
Afisa habari wa kituo cha umoja wa mataifa (UNIC),Usia Nkoma Ledama akifafanua kuhusina na matumizi ya madawa ya kulevya na jinsi umoja wa mataifa kitengo cha madawa ya kulevya jinsi wanavyopambana  mara baada ya timu ya Michuzi blog kutembelea banda la Umoja wa matafa(UN) katika maonyesho ya 39 ya kibiashara yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa kuchora kitengo cha sanaa wa (ILO), Paulina Kijazi katika banda la Umoja wa mataifa akizungumza na mwananchi  juu ya masuala mbalimbali kuhusiana na Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya sabasaba katika viwanja vya Mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakipata maelekezo katika banda la umoja wa mataifa-Tanzania, katika maonyesho yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu nyerere.

WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA LEO WAMEHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA

$
0
0

Hakimu Mwakalinga siku alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Leo amehukumiwa tena kunyongwa mpaka kufa katika mauaji ya mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila.


Na Daniel Mbega

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya leo hii imewahukumu kunyongwa mpaka kufa watu wanne kati ya watano waliomuua Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).


Waliohukumiwa kunyongwa mpaka kufa ni Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga na Gerard Korosso Kalonge (wakazi wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje), na Leonard Msalage Mwakisole na Hakimu Mselem Mwakalinga (wakazi wa Kiwira wilayani Rungwe).


Mshtakiwa wa nne, Mawazo Philemon Figomole, ameachiliwa huru na mahakama hiyo baada ya ushahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasi na shaka kwamba alihusika katika mauaji hayo.


Akisoma hukumu ya kesi hiyo ya mauaji yenye kumbukumbu Namb. KIW/IR/49/2008 na PI 5/2013, Jaji wa Mahakama Kuu Dk. Revila, amesema mahakama imejiridhisha pasi na shaka na ushahidi wa upande wa mashtaka kwamba washtakiwa hao wanne walitenda kosa hilo na hivyo wanastahili adhabu hiyo.



Hii ni kesi ya saba ya mauaji ya albino kutolewa hukumu ambapo mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 15 wamehukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Ililezwa mahakamani hapo kwamba, mnamo Februari 5, 2008 majira ya saa 12:00 na saa 1:00 jioni huko katika Kijiji cha Ilolo, Kata ya Kiwira, tarafa ya Ukukwe, wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, washtakiwa hao walimteka nyara kijana Henry Mwakajila, ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Ukukwe na kisha kumuua.

Wakati wa mwenendo wa kesi, ilielezwa na mashahidi wa upande wa mashtaka kwamba mshtakiwa wa kwanza Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga ambaye ni mganga wa jadi, mkazi wa Kijiji cha Mbembati, Wilaya ya Ileje, alikutwa na utumbo unaodhaniwa kuwa wa binadamu na ulipopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ukathibitika kwamba ni utumbo wa marehemu Henry.


Mshtakiwa wa pili, Gerard Korosso Kalonge wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje alikutwa na vidole vinne na mifupa kumi (10) vyote vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu na baada ya uchunguzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali ilibainika kwamba ni viungo vya marehemu Henry Mwakajila.

Ilielezwa pia kwamba, washtakiwa Leonard Msalage Mwakisole, Mawazo Philemon Figomole na Hakimu Mselem Mwakalinga ndio waliodaiwa kumteka nyara mtoto huyo na kumuua, kisha kupeleka viungo kwa mganga wa kienyeji Asangalwisye Kayuni.


Mshtakiwa wa tano, Hakimu Mselem Mwakalinga, tayari alikwishahukumiwa kunyongwa katika kesi nyingine ya mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, John Mwankenja, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake. Hukumu ya kesi hiyo namba 131/2012 ilitolewa Novemba 13, 2013 ambapo inaelezwa kwamba watuhumiwa walitenda kosa hilo Mei 19, 2011 katika kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Ingawa watuhumiwa walikuwa wanne, lakini Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya chini ya Jaji Samwel Karua iliwahukumu kunyongwa mpaka kufa mshtakiwa wa kwanza Hakimu Mwakalinga na mshtakiwa wa pili Daudi Mwasipasa kwa maelezo kwamba walihusika moja kwa moja na mauaji hayo ya kukusudia.


Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili yeye alitiwa hatiani kutokana na kosa la kumhifadhi mtuhumiwa namba moja baada ya kutoka kufanya mauaji wakati mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela alitiwa hatiani kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika katika mauaji hayo ingawa hakusika na kitendo hicho moja kwa moja, hivyo wote wawili walihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.


Hata hivyo, Myovela tayari alikwishahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria. 


Inadaiwa kwamba, chanzo cha mauaji hayo ya John Mwankenja, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rungwe, kilitokana na kiongozi huyo kufahamu kwamba hao ndio waliomuua mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila, hivyo aliuawa ili kupoteza ushahidi.


Imeandaliwa na mtandao wa www.brotherdanny.com

Mfuko wa uwekezaji wa pamoja wazinduliwa nchini

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Core Securities Limited, Bw. George Fumbuka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Umande Unit Trust (UTT), mfuko wa uwekezaji wa pamoja utakaowawezesha wakezaji wengi kukusanya mitaji yao kwa pamoja ili kupata mtaji mkubwa zaidi. Ameambatana na Meneja uendeshaji wa kampuni hiyo Bw. Jonathan Swalala (Kulia) na Meneja Mahusiano ya Wawekezaji, Bi. Sandra Felician (kushoto). UUT ni mfuko wa pili wa pamoja kusajiliwa nchini, kufuatia mfuko ulio chini ya serikali unaojulikana kama Dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT). 
Meneja uendeshaji wa kampuni ya Core Securities Limited, Bw. Jonathan Swalala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Umande Unit Trust (UTT), mfuko wa uwekezaji wa pamoja utakaowawezesha wakezaji wengi kukusanya mitaji yao kwa pamoja ili kupata mtaji mkubwa zaidi. Ameambatana na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw. George Fumbuka (wa pili kushoto) na Meneja Mahusiano ya Wawekezaji, Bi. Sandra Felician (kushoto). UUT ni mfuko wa pili wa pamoja kusajiliwa nchini, kufuatia mfuko ulio chini ya serikali unaojulikana kama Dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT).

Kampuni ya Core Capital Securities imezindua mfuko wa uwekezaji wa pamoja uitwao Umande Unit Trust, utakaowawezesha wakezaji wengi kukusanya mitaji yao kwa pamoja ili kupata mtaji mkubwa zaidi.

UUT ni mfuko wa pili wa pamoja kusajiliwa nchini, kufuatia mfuko ulio chini ya serikali unaojulikana kama Dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa UUT Bw. George Fumbuka alisema kuwa wawekezaji wamepatiwa njia nyingine iliyo salama na rahisi zaidi itakayowawezesha kuwekeza fedha zao.

“Faida ya uwekezaji hutokana na ukubwa wake, yaani mtaji mkubwa huzaa faida kubwa zaidi. Lakini pia hutokana na kusambazwa kwake katika mirija kadha wa kadha ya uwekezaji,” alisema.


“Mwekezaji akitukabidhi mtaji wake, fedha huwekezwa katika mipango mikubwa ambayo mwekezaji mmoja mmoja asingeweza kuifikia. Ni wakati umefika watanzania wachangamkie fursa hii ya uwekezaj wa pamoja ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini,” alifafanua.

Bw. Fumbuka alisema kuwa mfuko huo utawekeza katika mafungu matatu lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya watu kutoka kwenye makundi mbalimbali.

“Fungu la kwanza litajulikana kama Umande Capitalisation Fund, fungu hili litawafaa vijana na wafanyakazi wanaotaka kufaidika na kukua kwa mtaji wao kulingana na soko la hisa. Katika fungu hili, asilimia 95 zitawekezwa katika hisa za makampuni yenye dalili nzuri ya kukua na asilimia tano iliyobaki itawekezwa katika amana za muda mfupi zenye kuzalisha riba nzuri,” alibainisha.

Aliongeza kuwa fungu la pili ni Umande income Fund linalowafaa wanaotaka usalama wa mitaji yao huku wakipata faida ya kutosha ambapo asilimia 75 zitawekezwa katika dhamana za serikali na asilimia 25 katika hisa ili kupata faida itokanayo na kukua kwa soko la hisa la Dar es Salaam.

Alisema kuwa fungu la tatu linajulikana kama Umande Balanced Fund ambapo asilimia 60 itawekezwa kwenye hisa za makampuni na asilimia 40 kwenye dhamana za serikali na mabenki.


Alisema kuwa ofa ilifunguliwa tarehe 18 Mei 2015 na Itakamilika 24 Julai 2015, ambapo katika kipindi hicho kila kipande kitauzwa kwa shilingi 100.

“Tunatarajia vipande vianze kuuzwa au kununuliwa kutoka kwa meneja mnamo 27 Julai 2015. Tukiwa tunasonga mbele, UUT tumejipanga kutambulisha bidhaa na huduma bora zaidi katika soko lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya makundi tofauti tofauti katika jamii,” alisema

Mfuko wa Pensheni wa LAPF WASHIRIKI Maadhimisho ya Wiki ya Serikali za Mitaa Mtwara

$
0
0
 Mfuko wa Pensheni wa LAPF umeshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Serikali za Mitaa Mtwara katika viwanja vya mashujaa. LAPF inawakaribisha wakazi wa Mtwara na Watanzania wote kutembelea banda lao ili uweze kupata  huduma mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufahamu juu ya huduma mpya zinazotolewa na LAPF kama vile mkopo wa kujikimu, Mafao ya Uzazi na Mkopo wa Elimu. Pia wanachama watapata fursa ya kuangalia taarifa za michango yao kujiunga  na LAPF na kupata vitambulisho bandani.Pichani ni maafisa wa LAPF wakitoa huduma kwa wanachama waliotembelea banda hilo.




TEMBELEA OFISI YA GLOBAL EDUCATION LINK (GEL) ILIYOPO SABA SABA UJIPATIE NAFASI YA KUSOMA CHUO NJE YA NCHI

$
0
0
Msimamizi wa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Haroun Weggoro akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Afisa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Makungu Joseph akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao  iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Kantante Cornerio akihudumia wateja waliohudhuria katika ofisi yao iliyopo iliyopo maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel (Kushoto) akiwa na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, David Nsimba (katikati) wakizungumza na mteja aliyewatembelea ofisini kwao katika maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya wafanyakazi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Doreen Luzuki akiwakaribusha wateja walitembelea ofisini kwao katika maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Global Education Link wakiwa na nyuso za furaha kusubiri wageni.
Muonekano wa Ofisi ya Global Education Link iliyopo ndani ya viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

CBA YAIBUKA BINGWA MASHINDANO YA SOKA YA MABENKI NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

$
0
0
 Wacheaji wa CBA Tanzania na Mkombozi wakiwa wamejipanga kukaguliwa kabla ya mchezo kuanza
 Wacheji wakionyeshana ubae uwanjani
**********
Timu ya soka ya Benki ya CBA Tanzania  imeichapa timu ya Benki ya Mkombozi FC kwa magoli 3-2 na kufanikiwa kuondoka na kombe la ligi ya mabenki na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mwaka huu sambamba na kitita cha shilingi milioni moja taslimu katika fainali zilizofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Vinara wa mabao waliong’ara katika mchezo huo ni Jessy Nyambo wa CBA FC David wasongwa wa Mkombozi FC.



Pia timu ya Benki ya Mkombozi ambayo iliibuka na ushindi wa pili ilijinyakulia kitita cha shilingi laki nane na kombe .



Akizungumza wakati wa fainali hizo Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoa wa Dar es Salaam Emanuel Kazimoto,  alisema kuwa mashindano hayo ya taasisi ni muhimu kwa kuwa yanaziunganisha taasisi mbalimbali kuwa na ushirikiano katika kazi na wafanyakazi kuweza kujenga miili yao kupitia kufanya mazoezi na aliahidi kuwa watazidi kuunga mkono mashindano ya aina hii na kuzishauri taasisi hizo kubuni mashindano ya aina mbalimbali yatakayoshirikisha wafanyakazi wengi zaidi.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania,Julius Mcharo alisema amefurahishwa na ushindi ambao vijana wake wamepata na kuongeza kuwa wataendelea kushiriki na kudhamini michezo mbaimbali kwa kuwa  wanaamini kuwa michezo inaleta mshikamano na kujenga umoja ikiwemo pia kuimarisha afya.



Meneja Masoko wa Benki ya Mkombozi Grace Mboya,alipongeza timu zote zilizoshiriki mashindano hayo na kusema kuwa kinachotakiwa ni kujiimarisha zaidi ili yazidi kuongezeka ubora kwa kushirikisha timu za taasisi zote zilizopo katika sekta ya fedha.


Baadhi ya wachezaji wa timu hizo ambao ni wafanyakazi wa enki hizo wamesema kuwa mashindano hayo yameweza kuwakutanisha na kuweza kufahamiana zaidi na pia ni moja ya mazoezi ya kujenga miili yao.Michuano hiyo iliyoanza Mwezi April 2015 na kufunguliwa na Naibu Waziri wa Fedha,Mwigulu Nchemba yameshirikisha timu za soka za mabenki na mashirika ya hifadhi ya jamii.



Mkurugenzi wa CBA Tanzana Julius Mcharo akibadilishana mawazo na Meneka Masoko wa Benki ya Mkombozi grace Mboya wakati wa  mechi ya fainali baina ya timu iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Karume ambapo CBA imenyakua ubingwa
 Baadhi ya wafanyakaz wa CBA Tanzania na Mkombozi wakishangilia uhamasisha timu zao uwanjani
Mkurugenzi wa CBA Tanzana Julius Mcharo akibadilishana mawazo na Meneka Masoko wa Benki ya Mkombozi grace Mboya wakati wa  mechi ya fainali baina ya timu iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Karume ambapo CBA imenyakua ubingwa
 Mkurugenzi wa CBA Tanzania Julius Mcharo akiongea na wachezaji baada ya kumalizika mchezo huo.

Airtel Fursa Yatumia zaidi ya milioni 3 kumpiga tafu mjasiliamali mwingine - Airtel Fursa wiki hii kuwafaidisha mamia ya vijana Mwanza

$
0
0
 Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kulia), akiwa na kijana Mariam Mrisho (wa pili kulia) aliyewezeshwa na Airtel Fursa-Tunakuwezesha vifaa mbalimbali na jokufu kwa ajili ya kumsaidia katika biashara yake ya mama lishe na kutengeneza vitafunwa na juisi Dar es Salaam jana. Wa tatu kushoto ni mama wa Mariam Mrisho, Amina Lugome. Wengine ni ndugu zake Mrisho.
 Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (katikati), akimkabidhi jokofu kijana Mariam Mrisho (wa pili kulia) mkazi wa Kinondoni aliyewezeshwa na Airtel Fursa-Tunakuwezesha vifaa mbalimbali kwa ajili ya kumsaidia katika biashara yake ya mama lishe na kutengeneza vitafunwa na juisi Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia kushoto ni Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki. Wengine ni ndugu zake Mrisho.
 Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kulia), akimkabidhi mtungi wa gesi kijana Mariam Mrisho (wa pili kulia) aliyewezeshwa na Airtel Fursa-Tunakuwezesha vifaa mbalimbali na jokufu kwa ajili ya kumsaidia katika biashara yake ya mama lishe na kutengeneza vitafunwa na juisi Dar es Salaam jana. Wa tatu kushoto ni mama wa Mariam Mrisho, Amina Lugome. Kushoto ni Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
 Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kulia), akimkabidhi seti ya glasi kijana Mariam Mrisho (wa pili kulia) aliyewezeshwa na Airtel Fursa-Tunakuwezesha vifaa mbalimbali na jokufu kwa ajili ya kumsaidia katika biashara yake ya mama lishe na kutengeneza vitafunwa na juisi Dar es Salaam jana. Wa tatu kushoto ni mama wa Mariam Mrisho, Amina Lugome. Kushoto ni Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
 Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akipiga makofi pamoja na jamaa zake na Mariam Mrisho wakati  wa hafla ya kumkabidhi vifaa hivyo. Kwa habari kamili ya hafla hii BOFYA HAPA

TIB officially transformed to TIB Development Bank Limited and TIB Corporate Finance Limited

$
0
0
The Bank of Tanzania (BoT) has issued two licenses to TIB Development Bank Limited and TIB Corporate Finance Limited, which is a designated Commercial Bank subsidiary of the former.

TIB Development Bank Managing Director, Peter Noni told the press yesterday at the 39th Dar es Salaam International Trade Fair that the licenses have been issued by BoT in June 2015 for the Development and Corporate bank to engage in development financing and commercial banking activities respectively. He said TIB Development Bank is currently seeking to raise Sh. 390 bn/- to reach sh 500bn/- in its five-year plan for loaning in development projects.

According to him despite the inadequacy of capital, after the transformation TIB Development Bank has continued to disburse loans to its customers  with expectation of doubling it to 200bn/- this from 100bn/- disbursed last year.
“The government has been injecting capital to increase its capacity to finance more development projects and it is currently injecting 30bn/- annually to boost the bank’s financing capacity,’’ he said

He added that the bank had earmarked agro-processing activities because over 70 per cent of the population is engaged in farming activities. “Agriculture accounts for 38 per cent of our bank’s loan profile,’’ he mentioned.


Some of the areas that has benefited from TIB Development Bank loans include sugar farms and factories, cotton, coffee processing, cashes nut processing, packaging and even storage.

Other sectors are tourism by 14 per cent, manufacturing by 11 per cent, manufacturing by 11 per cent, real estate is 9 per cent. Oil, gas and electricity get up to 9 per cent while trade is 9 per cent.In the oil and gas sector, the bank has issued 26million US dollars to Wentworth Resources Limited, the company dedicated to oil and gas exploration to invest in gas transmission infrastructure. To the Tanzania Railway Limited (TRL), the bank has injected 12bn/- as working capital and 18 million US dollar for remanufacture of locomotives.

TIB Development Bank that is a wholly state-owned institution was created in 2013 following the transformation of former Tanzania Investment Baank into a two-tier group incorporating a development finance institution and a corporate bank. With the current status as per BoT certification given to TIB Development Bank and TIB Corporate Banking, the bank hopes to reduce the burden of government institutions and agencies depending on Treasury to implement their development projects.

“This is a great achievement of President President Kikwete who initiated the project and is now retiring after it is completed. We are optimistic that once it is fully funded, it will support various development activities,’’ he said
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images