Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 566 | 567 | (Page 568) | 569 | 570 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dk. Florence Turuka (wa pili kulia) akionyesha ripoti ya Dunia ya mwaka 2015 kuhusu uwekezaji mara tu baada ya kuizindua kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia  ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Nakuala Senzia (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya TIC,  Prof. Lucian Msambichaka (wa pili kushoto) na Mjumbe wa kamati ya Bodi ya TIC, Dr Frances Shao.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dk. Florence Turuka (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),  Prof. Lucian Msambichaka kwa pamoja wakizindua ripoti ya Dunia ya mwaka 2015 kuhusu uwekezaji kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Nakuala Senzia (wa kwanza kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi waripoti ya Dunia ya mwaka 2015 kuhusu uwekezaji mara tu baada ya kuizindua kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Pembeni yake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dk. Florence Turuka (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),  Prof. Lucian Msambichaka (Katikati) na Mjumbe wa kamati ya Bodi ya TIC, Dr Frances Shao.
  Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa TIC waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa ripoti ya Dunia ya mwaka 2015 kuhusu uwekezaji iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali kuhusu uwekezaji zilizoambatana na uzinduzi huo.
  Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa TIC waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa ripoti ya Dunia ya mwaka 2015 kuhusu uwekezaji iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali kuhusu uwekezaji zilizoambatana na uzinduzi huo.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
                                                   JESHI LA POLISI TANZANIA
  RPC.                                                                                                       Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                   
  Namba ya simu 2502572                                                                                            S. L.260,
  Fax - +255252503734                                                                                                   
   MBEYA.
  E-mail:-  rpc.mbeya@tpf.go.tz                                                                      
  tanpol.mbeya@gmail.com

  TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 25.06.2015.
  MTU MMOJA AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA WATU WASIOFAHAMIKA.


  ·      MTU MMOJA MKAZI WA MBALIZI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE MOSHI.


  KATIKA TUKIO LA KWANZA

  MTU MMOJA MKAZI WA CHALANGWA WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOFREY MWAMBONA @ ANKI (28) AMEKUTWA AMEUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA KUTOLEWA KOROMEO.

  MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UMETELEKEZWA KANDO YA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA MNAMO TAREHE 24.06.2015 MAJIRA YA SAA 23:59 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHALANGWA, KATA YA CHALANGWA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

  INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA AMETOKA GEREZANI HIVI KARIBUNI ALIPOKUWA AKITUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUBAKA WATOTO WATATU NA ALIKUWA AMETOKA KWA RUFAA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MSAKO UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


  TAARIFA ZA MISAKO:

  MTU MMOJA MKAZI WA MBALIZI NJE KIDOGO YA JIJI LA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUSAJO MWAMPOSA (29) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE MOSHI (GONGO) UJAZO WA LITA 12.

  MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 24.06.2015 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA HUKO MTAA WA NDOLA, KATA YA UTENGULE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA UPIKAJI/UUZAJI WA POMBE HIYO ILI WAKAMATWE NA HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

  Imesainiwa na:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Italy Nchini Tanzania, Luigi Scotto, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 25, 2015 kwa ajili ya mazungumzo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Italy nchini Tanzania, Luigi Scotto,  wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 25, 2015 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Ballozi wa Italy nchini Tanzania, Luigi Scotto (wa pili kushoto), baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 25, 2015. Kushoto ni Mkurugenzi  wa Idara ya Ulaya na Marekani, Balozi Joseph Sokoine (kulia) ni Msaidizi wa Balozi wa Italy, Michelangela Adamo. Picha na OMR

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  WATANZANIA walioko Ughaibuni wanatakiwa kuelezwa vitu ambavyo vitawafanya watanzania nchini kutambua umuhimu wa watu katika masuala mbalimbali ikiwemo uchumi.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari  Maelezo  jijini ,Dar es Salaam,Mratibu wa Watu Waishio Ughaibuni (Diaspora),Majjid Mjengwa amesema kutokana na kutambua uwepo watu milioni mbili wako  nje nchi ambao wanatakiwa kushirikishwa katika masuala mbalilmbali yanayoendelea nchini.
   
  Mjengwa amesema kutokana na kuona hilo amebuni kipindi cha Diaspora katika kituo cha TBC kwa ajili ya kuelimisha watanzania juu watu wanaoishi  nje  ya nchi  juu ya faida kwa watu hao.
   
  Amesema katika kipindi hicho kitatoa mwanga kwa watu wa ughaibuni na watanzania nchini juu kushirikiana katika masuala mbalimbali.
   
  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa,Rosemary Jairo amesema kuwa ubunifu wa mjengwa wa kipindi cha Diaspora kitasaidia kuelimisha watanzania juu maana wakishajua itakuwa ni rahisi kupata uraia pacha.
   
  Amesema watanzania wengi hawajui faida ya kuwa na watu nje ya nchi katika masuala ya uchumi wanawezaje kuchangia kuleta maendeleo.
  Jairo amesema kuna watanzania  wanafanya kazi ughaibuni wanafanya vizuri hali ambayo wanaweza kufanya katika nchi yao.
  Mratibu wa Kipindi cha Diaspora,Maggid Mjengwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kipindi cha Diaspora kitachoanza kuruka katika kituo cha TBC hivi karibuni katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo,Kushoto ni Mkurugenzi wa Diaspora Intiative,Emmanuel Mwachullah,Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Rosemary Jairo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Rosemary Jairo akizungumza na waandishi wa habari juu ya watu wanaoishi Ughaibuni katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es Salaam,kushoto ni Mratibu wa Kipindi cha Diaspora,Maggid Mjengwa picha na Chalila Kibuda)

  0 0

   Mafundi wakitoa mizigo kwaajili maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
  Mwonekano wa nje katika viwanja vya sabasaba ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja hivyo.
   Gari likiwa limebeba takataka katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
    Mabanda ya maonyesho ya sabasaba yakiendelea kufanyiwa kukarabati kwaajili ya maonyesho yatakayoanza Juni 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
  Wazee wa kilimo kwanza wakiwa katika maandalizi ya maonyesho ya sabasaba.
   Wanawake nao katika harakati za kuweka mazingira ya kupendeza katika mabanda ya maonyesho ya sabasaba leo jijini Dar es Salaam.
  PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.


  0 0

  IDADI kubwa ya waimbaji  wa nyimbo za Injili Tanzania wameonesha nia ya kumsindikiza mwenzao, Bonny Mwaitege anayetarajia kuzindua albamu yake Agosti 2 mwaka huu.

  Uzinduzi huo unaotarajia kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambao utashirikisha albamu tatu za muimbaji huyo zinazoendelea kurekodiwa jijini Mwanza.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama hivi sasa utaratibu wa kurekodi albamu hizo unaendelea jijini Mwanza. Msama aliyezungumza na Mwandishi wa gazeti hili jijini Mwanza alisema amepokea maombi ya waimbaji mbalimbali hapa nchini ambao wanahitaji kuwa pamoja na mwenzao huyo.

  Msama alisema kwa kuwa bado wanaendelea na hatua za mwisho za kufanikisha kazi hizo, wanajipanga kushirikisha idadi kubwa ya waimbaji watakaomsindikiza mwezao. Aidha Msama alisema sambamba na waimbaji hao kutaka kupanda jukwaani siku hiyo, pia mashabiki wa muziki huo hapa nchini wanahitaji uzinduzi wa albamu hiyo ushirikishe pia waimbaji raia wa Afrika ya Kusini.

  0 0

   Miss Universe Tanzania 2014 Caroline Bernard leo amekabidhi
  msaada pamoja na kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike katika shule ya msingi Msimbazi Mseto.
  Huu ukiwa ni mwendelezo wake katika kufanya kazi za kijamii, Caroline ambaye ndiye aliyetwaa taji la Miss Universe Tanzania 2014 ataendelea kulitumikia taji lake kama mrembo mtawazwa
  ingawa alishindwa kwenda kushindana kimataifa kutokana na sababu za kiafya.
  Caroline alishindwa kwenda kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa2014 na badala yake kwenda mshindi wa pili Nale Boniface mara baada ya kuumia kidole cha mguu wiki chache kabla ya mashindano. Mpaka atakapokabidhi taji baaadae mwaka huu, Caroline ndo ataendelea
  na taji lake ndiye atakayemvisha mtaji mshindi wa 2015.
  Msaada alioutoa caroline ni pamoja na vitaulo vya kinamama (hygiene pads) vya kujihifadhia wakati wa hedhi na karatasi ya kujisafishia maarufu kama tissue. “Nimelenga kushughulika na watoto wa kike hasa wa shule ya msingi darasa la sita na la saba kwani hawa ndio wanaotakiwa kujitambua zaidi hususani mabadiliko yao ya kimwili huanzia hapa.”Alisema mrembo Caroline.mmm
  Miss Universe Tanzania ilianza mashindano yake mwaka 2007 na mshindi wake alikuwa Mwanamitindo Flaviana Matata na aliweza kuitoa kimasomaso nchi yetu ya Tanzania kwa kushika nafasi ya Sita kidunia.Mwaka uliofuata, 2008 mrembo Amanda Ole Sululu alimrithi
  Flaviana Matata na kuvaa taji la Miss Universe Tanzania 2008 akifuatiwa na mrembo Illuminata James mwaka 2009, kisha Hellen Dausen mwaka 2010.
   Baadae taji lilichukuliwa na Nelly Kamwelu 2011 na mwaka jana 2012 taji lilinyakuliwa na mrembo Winfrida Dominic. Mwaka 2013 taji lilienda kwa mrembo Betty Boniface na hatimaye kumuachia mikoba mrembo Caroline
  Bernard Miss Universe 2014

  0 0

  m
  Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima ( AFP) Said Soud akizungumza na Waandishi wa Habari hawapopichani  akizungumza kulaani kitendo cha Chama cha Wananchi (CUF) kutoka katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  kulia ni Afisa wa Habari  wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ali Issa na kushoto ni  Shaibu Masoud Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha  Wakulima (AFP). 
  mail.google.com
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakipokea maelezo kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP)Said Soud  katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

  0 0  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
  index
  TAARIFA KWA UMMA.
  TAHADHARI YA UGONJWA WA NIMONIA INAYOTOKANA NA CORONA VIRUS
  …………………………………………………..
  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, inapenda kutoa tahadhari ya ugonjwa wa nimonia inayotokana na kirusi kiitwacho Corona virus. Mnamo tarehe 21 Mei 2015, Wizara ilipokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) juu ya kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa wa Nimonia unaosababishwa na kirusi cha “Coronavirus”, Korea ya Kusini.
  Ugonjwa huu unaenezwa na kirusi kiitwacho “Middle East Respiratory Syndrome Coronavirus (MERS Cov).” Dalili kuu za ugonjwa huu ni homa kali, kukohoa na kushindwa kupumua kwa ghafla, na hatimaye kupata Nimonia. Dalili nyingine ambazo zinaweza kutokea ni pamoja na kupata maumivu makali ya tumbo pamoja na kuharisha. Kipindi kati ya kupata maambukizi mpaka kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 10. Ugonjwa huu hutibiwa kufuatana na dalili zilizojitokeza. Mpaka sasa hakuna chanjo maalum kwa ajili ya ugonjwa huu.
  Virusi hivi, kutokana na tafiti zinazoendelea hubebwa na wanyama hususan ngamia na tafiti hizi zimeonyesha uwepo wa virusi hivi kwenye ngamia katika nchi za Egypt, Oman, Qatar na Saudi Arabia. Mara mgonjwa apatapo ugonjwa huu, uambukizo kwenda kwa mtu mmoja hutokea iwapo mtu huyu atakuwa karibu na mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huu na kugusa majiimaji au makamasi hasa wakati wa kukohoa au kupiga chafya. Vilevile uambukizo huweza kutokea iwapo mtu akigusa mazingira ambayo yamechafuliwa na majimaji au makamasi ya mgonjwa aliyedhibitishwa na ugonjwa huu.

  Ugonjwa wa Corona virus uligundulika kwa mara ya kwanza mwezi Septemba 2012 katika nchi za Mashariki ya kati huko Saudi Arabia. Ugonjwa huo umeendelea kusambaa katika nchi za Mashariki ya kati zikiwemo za Jordan, Qatar, na Falme za Kiarabu (UAE). Katika bara la Ulaya, ugonjwa huu umethibitishwa kutokea nchi za Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza na barani katika nchi ya Tunisia. Ugonjwa huu umeendelea kuwepo kwenye nchi hizi kwa kiwango kidogo kuanzia mwaka 2012 hadi Aprili 2015.

  Ongezeko la ugonjwa huu limejitokeza zaidi kuanzia tarehe 20 Mei, 2015 katika nchi ya Jamhuri ya Korea. Hadi tarehe 20 Juni, 2015, watu 167 walikuwa wamethibitishwa kuwa na ugonjwa huo wa nimonia ya Corona Virus na 24 kupoteza maisha. Vile vile nchi za Thailand na China kumekuwa na mgojwa mmoja kila nchi.
  Hadi sasa hakuna mgonjwa yoyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na virusi vya Corona virus hapa nchini. Kwa kuwa magonjwa hayatambui mipaka ya nchi ni vyema tuchukue tahadhari dhidhi ya Ugonjwa huu.
  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeandaa mikakati ya kuzuia ugonjwa huu usiingie hapa nchini ikiwa ni pamoja na;
  • Kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa magonjwa (Surveillance) hususan katika vituo vitano maalum vilivyopo nchini vinavyofanya ufuatiliaji wa magojnwa ya neumonía (Influenza sentinel surveillance sites).
  • Kuongeza kasi ya ufuatiliaji kwa vituo vya kutolea huduma kote nchini. Aidha Wizara imeagiza kupitia waganga wakuu wa mikoa kutoa taarifa /ongezeko la wagonjwa watakaoonyesha dalili za ugonjwa huo hususan kwa wagonjwa ambao wamesafiri kwenye nchi ambazo zina ugojnjwa huu. Ainisho sanifu (Standard case Definition) imetolewa kusaidia mtaalamu wa afya kuweza kutambua ugonjwa huu. Aidha kasi hii ya ufuatiliaji inaangalia iwapo kuna ongezeko la Nimonia kali au mafua kulinganisha na majira ya wakati huu kwa miaka mingine.
  • Kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu maeneo ya mipakani hususan kwa wasafiri watokao nje ya nchi hususani watokao nchi za Mashariki ya Kati, pamoja na Bara ya Ulaya na Afrika, kwa kutumia mifumo ile ile iliyowekwa kwa wagonjwa ya kuambukiza kama Ebola ambayo yaweza kuingia nchini kupitia mipaka yetu. Ufuatiliaji huu hufanyika bila kusababisha usumbufu usio wa lazima kwa wasafiri.
  • Kuendelea na upimaji wa sampuli zinazohisiwa kuwa na ugonjwa huu. Aidha Maabara ya taifa imejengewa uwezo wa kupima virusi vya Corona virusi. Sampuli zilizopimwa kuanzia April mpaka Juni 2015 zimethibitisha kuwa hakuna ugonjwa huo hapa nchini.
  • Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania bara. Aidha taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli ikiwa ni pamoja na vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu.
  • Kutoa elimu wa jamii kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipakani kuhusu dalili za ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga na maambukizi ili endapo ugonjwa huo utatokea uweze kutolewa taarifa mapema.
  • Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya na mipakani wa namna ya kutambua na kujikinga dhidi ya maambukizo ya ugonjwa huu pamoja na uchukuaji wa sampuli iwapo mgonjwa atapatikana huku wakizingatia kanuni za usafi (Infection, Prevention and Control)
  • Wizara inasisitiza kuwa hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili kwa wasafiri watakaokwenda au kurudi katika maeneo tajwa yaliyothibitishwa kuwa na ugonjwa huu.
  Hitimisho
  Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa nchini.
  Ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya hewa iwapo mgonjwa atokohoa au kupiga chafya bila kujikinga au pia kugusa sehemu zenye ugonjwa huo na kujigusa mdomomi au puani. Kwa kuzingatia hali hiyo, wizara inapenda kutoa tahadhari kwa wananchi juu ya umuhimu wa kunawa mikono vizuri kwa sabuni na maji mara kwa mara na pia kuzuia mdomo na pua kwa kitambaa au karatasi laini (tissue paper) wakati unapokohoa au kupiga chafya.
  Mpaka sasa hakuna kizuizi cha kusafiri kutoka nchi moja hadi nyingine. Hata hivyo inashauriwa kwamba mtu yeyote anayesafiri kwenda Mashariki ya Mbali na nchi za Asia afahamu kuwa kuna hatari ya ugonjwa huu na kwamba anatakiwa atoe taarifa mapema kwenye taasisi za huduma za afya iwapo ataona dalili kama hizi wakati akiwa safarini au wakati amewasili toka nchi ambazo zina ugonjwa huu.
  Vilevile, wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.
  Imetolewa na;
  Kitengo cha Mawasiliano Serikali – Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
  Juni 25,2015

  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi  Ombeni Sefue (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi     (kulia) juu ya shughuli mbalimbali za PSPF, wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Utumishi) Bw. Habib Mkwizu  (kushoto) na Bw. Joseph Lyimo, ambaye ni Afisa wa PSPF. Mheshimiwa Sefue alitembelea banda la PSPF katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi juu ya shughuli mbalimbali za PSPF,  kulia ni Michael Tarimo, Afisa wa PSPF. Mheshimiwa Sefue alitembelea band la PSPF katika maonesho hya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

   Bw. Max Mbise akitoa maelezo juu ya shughuli mbalimbali za PSPF kwa wateja waliotembelea banda la PSPF katika maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyamalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

   Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi akitoa maelezo kwa mmoja wa wanachama wa PSPF waiotembelea banda la PSPF katika maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyamalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi akitoa maelezo kwa wanachama wa PSPF waiotembelea banda la PSPF katika maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyamalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.


    


  0 0

  h
  Mkurugenzi wa kampuni ya Azam Hussein Moh’d Said akiwaelezea Waandishi wa Habari juu ya safari ya Boti hiyo Kilimnjaro V  zitakavyokuwa kati ya Zanzibar na  Dari-esaalam . ( Pcha zote Na Miza Othman Maelezo Zanzibar).j
  Captain wa Boti ya Kilimanjaro (V)  Thomas akiwapa maelezo Waandishi wa Habari namana anavyoendesha Boti hiyo.k
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakipanda katika Boti ya Kilimanjaro v iliyozinduliwa jana ambayo inatarajiwa kufanya safari zake hivi karibuni kati ya Zanzibar na Dar-esaalam.l
  Muonekano wa boti ya Kilimanjaro V.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akionyesha fomu zilizojazwa na wanaCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya 1,500 kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Shesha (kulia) katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni Juni 25.2015. Kushoto ni mkewe Mama Dorcas Membe.  Picha zote na John Badi
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM zaidi ya 1,500 walimdhamini.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiagana na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM 1,500 walimdhamini.

  0 0

  Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi amkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete katika uwanja wa Michezo wa Michezo wa Machava jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za miaka 40 za Uhuru wa Msumbiji.Msumbiji ilipata uhuru wake tarehe25 June mwaka 1975 kutoka kwa mkoloni Mreno.(picha na Freddy Maro).


  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akizungumza wakati akiwashukuru wanaCCM wa Mkoa wa Manyara, waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Lowassa amepata wadhamini 42, 405 , Mjini Babati Mkoani Manyara leo, Juni 25, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akipokea fomu ya udhamini kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Babati Mjini, Daniel Ole Porokwa, leo Juni 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 42, 405 wa Mkoa wa Manyara.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimsalimia Kijana Jacob Jeremiah ambaye ni mlemavu wa miguu, alipokutana nae nje ya Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Manyara, iliopo Mjini Babari leo Juni 25, 2015, wakati akiwa katika ziara ya kusaka wadhamini  watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.


  0 0

   Vijana 20 kutoka Sumve wakionyesha kadi zao za Chadema kabla ya kuzikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za Chadema kutoka kwa vijana 20 waliojiunga na CCM na wanachama wapya zaidi ya 1520 walipewa kadi zao za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Sumve. Katika ziara yake kwenye jimbo la Sumve Katibu Mkuu wa CCM amepokea kadi 48 kutoka Chadema ikiwa 28 zilizorudishwa katika kijiji cha Goloma kata ya Mwadu.
   kadi za Chadema kutoka kwa vijana 20 waliojiunga na CCM na wanachama wapya zaidi ya 1520 walipewa kadi zao za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Sumve.
   Wananchi wa Kata ya malya wakionyesha Bango kubwa lenye ujumbe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana lenye madai ya kudhulumiwa viwanja ambavyo tangia walipie miaka mitatu sasa hawajapata viwanja,Katibu Mkuu wa CCM alikuwa njiani kuelekea Nyambiti ndipo wananchi hao walimsimamisha barabarani na kutoa kero zao.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungunza na wakazi wa kata ya Malya ambao wanadai viwanja vyao walivyovilipia miaka mitatu iliyopita,lakini mpaka sasa wananchi hao hajakabidhiwa,Ndugu Kinana ameipa muda wa miezi miwili  na ushehe kuwa ifikapo septemba 1,2015 ,Halmashauri ya wilaya ya Sumve ihakikishe imelitatua tatizo hilo na wananchi kupewa viwanja vyao. Katibu Mkuu wa CCM alikuwa njiani kuelekea Nyambiti ndipo wananchi hao walimsimamisha barabarani na kutoa kero zao. 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Sumve,Mh Richard Ndassa,mara baada ya kuzindua  huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji cha Mwabilanda  wilayani Kwimba.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia sehemu ya kunyweshea maji mifugo katika kijiji cha Kishilili, ambapo Ng'ombe zaidi ya 800 hupata huduma ya maji safi na salama katika mradi ambao pia husaidia kaya 102 kupata maji safi na salama katika kisima kinachotumia mfumo wa jua (solar power).
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchanganya zege wakati wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mwashilalage.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Nyambiti.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wakazi wa Sumve wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano Sumve wilayani Kwimba.
   Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe. Richard Ndasa akiwasalimu wakazi wa Sumve waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Sumve ambapo aliwahakikishia ahadi za CCM zitatekelezwa.
   wakazi wa kata ya Sumve waliofika kwenye mkutano huo wa hadhara.

  0 0


  Mhariri  wa Mwana Halisi Online, Edson Kamukara (pichani), amefariki Dunia kwa ajali ya moto nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam leo hii majira ya saa moja kasorobo jioni, baada ya kulipukiwa na jiko la gesi, habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Polisi wameuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuhifadhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa kifo chake.


  Ofisa Uhusiano wa NMB, Viccent Mnyanyika akimkabidhi zawadi marehemu Edson Kamukara wakati wa uhai wake kwenye wa utoaji wa tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) zilizofanyika Aprili 24 mwaka huu.

  Globu ya Jamii inaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake, marafiki na majirani katika msiba huu. Mola na aiweke mahala pema Roho ya Marehemu,
  AMINA

  0 0

                                                                                                                                   
                  

  A team of 21 Acacia staff, friends and family led by Chief Executive Officer, Brad Gordon, are embarking on the journey of a lifetime to reach Uhuru Peak; the summit of Mount Kilimanjaro, to raise funds for education.


  Through its CanEducate, a charity that provides educational sponsorships to impoverished and at-risk children in developing countries including Tanzania, the company targets to raise $200,000.


  As it costs $75 a year to send a student to school in Tanzania, the targeted donation has the potential to help 2000 students in communities surrounding Acacia mine sites of Buzwagi, Bulyanhulu and North Mara, who fail to attend schools due to income constraints.


  Elaborating further, Brad said for less than a month, donations were going on so well hoping to attain the target, and that the company was set to match individual donations by a dollar for a dollar.


  “I am sure that the final figure is going to have an incredible and positive impact on the lives of children in Tanzania. If you haven’t done so yet, there is still time to give. We need those crucial dollars to get us to our target and to give the team 200,000 reasons to make it to the top,” he added.


  The CanEducate initiative started in 2010 covering 158 students at Bulyanhulu and by the end of 2014 the programme had grown to cover 1,800 students across Bulyanhulu, Buzwagi and North Mara and has delivered some of the best performers in various schools in the National Form 4 examinations.


  Mount Kilimanjaro, in Tanzania, is the highest freestanding mountain in the World and Uhuru Peak, at 5,895m is the highest point in Africa. Uhuru means freedom and Acacias believes education brings freedom through choice, which is why CanEducate is the perfect recipient of funds raised through the climb.


  Notes to the editor


  Acacia is the leading gold producer in Tanzania with three producing mines, all located in northwest Tanzania, together with several exploration projects at various stages of development, including exploration land holdings in the highly prospective greenstone belts in Western Kenya and Western Burkina Faso.


  Acacia Mining plc is a UK public company with its headquarters in London. We are listed on the Main Market of the London Stock Exchange under the symbol ACA and have a secondary listing on the Dar es Salaam Stock Exchange in Tanzania.If you wish to support this noble course, please do so at the following link: http://caneducate.ca/kiliclimb.html.  By Dixon Busagaga ,Michuzi blog representative Northern zone.  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Wizara na ujumbe kutoka Kiwanja cha ndege cha Guang Dong kutoka nchini China, wakati ulipotembelea Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi. Ujumbe umeonyesha nia kuwekeza katika Viwanja vya Ndege vya Tanzania. (Habari Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).                                                                               

   Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing wakati ujumbe huo ulipokutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Ndege cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing (kushoto), akimpatia zawadi Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire, leo asubuhi baada ya ugeni huo kukutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi leo asubuhi.


older | 1 | .... | 566 | 567 | (Page 568) | 569 | 570 | .... | 1903 | newer