Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUUNDA KITENGO MAALUMU KWAAJILI YA USHIRIKI WA WATANZANIA KATIKA SERA YA NISHATI NA MADINI

$
0
0
 Msimamizi wa masuala ya ushiriki wa watanzania wa wizara ya nishati na madini Neema Apson akizungumzia jinsi wizara ya nishati na madini inavyoshiriki katika kuhakikisha taarifa zinawafikia wananchi kwa usahihi kuhusiana na mafuta na gesi katika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo. pia wizara hiyo itaunda kitengo maalumu kwaajili ya kusimamia masuala ya gesi na mafuta na kuwajulisha wananchi kushiriki vyema katika nishati zitolewazo hapa nchini.
 Mkuu wa Biashara wa British Concil Hugh Penrhyn Jones akizungumza katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo.
 Mratibu wa kitengo cha uwajibikaji wa makampuni na mazingira-kituo cha sheria na haki za binadamu,Wakili Flaviana Charsles akiuliza swali katika mkutano wa kujadili masuala ya mafuta na gesi pamoja na changamoto zake kwa jamii katika mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wadau wa maendeleo ya mafuta na gesi wakimsikiliza mtoa maada katika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo.(Picha na Avila Kakingo)

BENKI YA CRDB KUANZA KUUZA HISA STAHILI JUNI 26

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na baadhi ya wanahisa wa benki hiyo kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa hisa stahili za benki hiyo unaoanza Juni 26 hadi Julai 16. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akifungua mkutano wa wanahisa wa benki hiyo katika Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akizungumza wakati wa mkutano wa wanahisa uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi yaWakurugenzi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika mkutano huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na baadhi ya wanahisa wa benki hiyo kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa hisa stahili za benki hiyo unaoanza Juni 26 hadi Julai 16. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya maofisa wa benki hiyo pamoja na wanahisa wakimsikiliza Dk. Charles Kimei.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB. 
 Wakurugenzi wa Benki ya CRDB na wanahisa wakiwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB na mameneja wa matawi wakiwa katika mkutano huo.

Meza Kuu.

 Dar es Salaam, Tanzania
BENKI ya CRDB, imetangaza kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa Hista Stahili kwa wanahisa wake, unaofunguliwa Juni 26 na kuhitimishwa Julai 16, ili kuongeza mtaji wake wa uendeshaji.

Hisa Stahili ni zile za ongezeko zinazotolewa au kuuzwa kwa wanahisa wa benki hiyo kwa mfumo wa hisa moja mpya kwa kila hisa tano anazomiliki.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mauzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema kuwa baada ya maazimio ya wanahisa wake wote katika Mkutano Mkuu uliopita.

“Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, imeidhinisha kuingiza sokoni hisa mpya 435,306,432 kwa ajili ya wanahisa wake ambapo kila hisa moja itauzwa kwa shilingi 350, hivyo kusanyo tarajiwa la mtaji mpya litakuwa ni sh. 152,357,251,200,” alisema Dk. Kimei.

Alibainisha kuwa fedha hizo zitakazopatikana baada ya mauzo ya hisa zitatumika kwa mambo kadhaa, ikiwamo uboreshaji wa njia za kutolea huduma kwa wateja wa benki hiyo.

“Mwanahisa atakayekuwa na sifa za kupokea kupokea hisa hizi ni yule tu atakayekuwa kwenye kumbukumbu za vitabu vya benki mpaka kufikia Alhamisi Juni 18 mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya mwisho ukusanyaji kumbukumbu hizo,” alifafanua Dk. Kimei.

Aliongeza kuwa CRDB inahitaji kuongeza mtaji wake ili kufikia malengo yake ya kibiashara, ikiwamo upanuzi wa mtandao na ununuzi mitambo ya uendeshaji.


“CRDB imeona hii ndio njia sahihi na bora zaidi, kwani licha ya kuongeza mtaji, pia inatoa fursa kwa wanahisa wetu kuongeza hisa zao sambamba na umiliki wao wa benki hii,” alibainisha Dk. Kimei.

MKUTANO MKUBWA WA AMANI NA UPENDO KUFANYIKA LEO JIJINI ARUSHA

$
0
0
SAM_3390
SAM_3402Askofu Solomon Mwagisa ambaye ni katibu wa mkutano wa Amani na Upendo utakaofanyika leo jijini Arusha katika viwanja vya reli kwanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni akielezea namna walivyojiandaa na mkutano huo,kushoto ni Askofu Mkuu wa makanisa ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini kati Solomon Massangwa(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_3404Askofu Mkuu wa makanisa ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini kati Solomon Massangwa akizungumza na wanahabari jana jijini hapa kuhusu mkutano huo mkubwa wa Amani na Upendo ambapo alisema kuwa ni muhimu kwa kila mtu kuhakikisha Amani inakuwepo huku akisisitiza kuwa bila Amani hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika pasipo Amani
SAM_3407Paul Malisa mwakilishi wa Askofu mkuu Josephat Lebulu wa kanisa Katoliki Arusha ,Paroko wa Parokia ya mtakatifu Theresia Arusha mjini akizungumza na wanahabari juu ya mkutano huo ambapo alisema kazi walionayo ni kuhakikisha wanapigia debe Amani hasa katika kipindi hichi kuelekea uchaguzi mkuu
SAM_3401Eng.Tunzo Muzava ambaye ni mratibu wa mkutano huo akizungumza na vyombo vya habari jana alisema kuwa Muhubiri mkubwa wa kimataifa kutoka Marekani Will Graham anatarajiwa kuhubiri katika mkutano huo huku kwaya zaidi ya 200 kutumbuiza,Mkutano huo unashirikisha makanisa yote ya Arusha

WATANZANIA WAASWA KUJITOKEZA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA WANAHABARI WANAOSUMBULIWA NA MAGONJWA SUGU

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda akitoa wito kwa watanzania wote wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kushiriki katika harambee hiyo itakayofanyika katika viwanja vya Leaders club,siku ya Jumamosi Julai 4,2015 wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene.Kulia ni wajumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe na Angela Msangi
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha mshikamano katika Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaosumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa.Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Grace Nakson
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa ambaye ni mjumbe wa kamati ya kuratibu Harambee ya kuwachangia wanahabari wanasumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa  akiwahamasisha wanahabari wote nchini kuungana katika harambee hiyo kwa kuihamasisha jamaii kushiriki katika tukio hilo muhimu. Kushoto  ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo  ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson.
 Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa kuhamasisha kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo  ugonjwa sugu wa saratani
. Mjumbe wa Kamati ya Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo  ugonjwa sugu wa saratani Bi. Angela Msangi akiwahamasisha wanahabari kujitokeza kwa wingi katika harambee hiyo na pia kutumia taaluma yao kuihamasisha jamii kujitolea katika kufanikisha lengo la harambee hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe.
PICHA NA FRANK MVUNGI-MAELEZO

UONGOZI WA WIZARA YA UCHUKUZI WAKUTANA NA UJUMBE KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA GUANG DONG WA NCHINI CHINA LEO ASUBUHI WIZARANI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Ndege cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing (kushoto), akimpatia zawadi Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire, leo asubuhi baada ya ugeni huo kukutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi leo asubuhi.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing wakati ujumbe huo ulipokutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Wizara na ujumbe kutoka Kiwanja cha ndege cha Guang Dong kutoka nchini China, wakati ulipotembelea Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi. Ujumbe umeonyesha nia kuwekeza katika Viwanja vya Ndege vya Tanzania.
(Habari Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)     

FILAMU YA HAMU YA MAFANIKIO ‘DESIRE TO SUCCEED’ IMENDULIWA JANA

$
0
0
 Na Bakari  Issa Madjeshi,Globu ya jamii.
Filamu ya Kiswahili ijulikanayo kama  Hamu ya Mafanikio ilizinduliwa rasmi  jana na Benki ya DCB katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Filamu hiyo imeandaliwa na DCB Commercial Benki kwa kushirikiana na Kampuni ya ConsNet,yenye lengo la kuelimisha na kuhamasisha  wateja, wadau na umma kwa ujumla juu ya umuhimu na faida za kufanya shughuli za kibenki na DCB ambazo zinabadili maisha ya wateja kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo amesema moja ya changamoto zilizopo katika sekta ya benki ni jamii kukosa elimu ya kutosha juu ya huduma za Kibenki,hivyo mbali na kujitangaza, DCB imeamua kutoa elimu ya kibenki  kupitia Filamu hiyo.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia amewashukuru waandaaji wa Filamu hiyo,ikiwa  Bodi ya Filamu nchini pamoja na wasanii wote walioshiriki kuigiza filamu hiyo  kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Pia ametoa wito kwa wasambazaji wa Filamu hiyo kuifanya  kazi  yao kimakini ili kutimiza malengo na madhumuni ya kuandaa Filamu hiyo.
Washiriki katika Filamu hiyo ni pamoja na Tito Zimbwe,Rose Ndauka,Jackline Pentezel,Abdul Mhema,Hidaya Njaidi, Gojak na Wasanii wengine wengi. Baada ya kuzinduliwa Filamu hiyo itaonyeshwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo City Centre,Magomeni,Arnautoglu,Mnazi Mmoja,Tabata,Ukonga,Chanika,Mabibo na Kariakoo kwa nyakati tofauti kuanzia Julai mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Filamu ya Hamu ya Mafanikio 'Desire to Succeed' iliyozindulia katika ukumbi wa  Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia akizungumza katika hafla  ya uzinduzi wa Filamu hiyo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana ambapo alitoa wito kwa wasambazaji wa Filamu hiyo kuifanya  kazi  yao kwaumakini ili kutimiza malengo na madhumuni ya kuandaa Filamu hiyo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo (kulia) kwa pamoja wakionyesha DVD za Filamu hiyo.
Baadhi ya  washiriki na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Filamu hiyo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam,Juni 25,2015.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AKUTANA NA TADWU LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na Umoja wa Madereva  Tanzania (TADWU)juu ya usajili waliopata ambao utafanya waweze kuingia mkataba wa waajiri wao na kuweza kujiunga katika mfuko wa bima ya Afya  uliofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam, Kushoto  ni Mwenyekiti wa Umoja huo,Clement Masanja, kulia ni  Katibu Mkuu  wa chama hicho Abdallah Lubala.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda akikabidhi Katiba ya Umoja wa Madereva  Tanzania (TADWU) kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo Abdallah Lubala katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya madereva wakifurahia kupata umoja huo utakaoweka wazi juu ya ajira ya kazi zao katika katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda akiagana na madereva katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.( PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA MALAWI KATIKA SHEREHE ZA UHURU WA MSUMBIJI

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Malawi Profesa Peter Mutharika wakitoka katika uwanja wa michezo wa Machava jijini Maputo Msumbiji baada ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya uhuru wa Msumbiji-Juni 25,2015. (picha na Freddy Maro)
3
Askari wa Msumbiji wakishuka na mwavuli wakati wa sherehe za uhuru.1
Ndege zikipita na kuchora rangi za bendera za Msumbiji jana wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Uhuru wa msumbiji.2

NAPE AMALIZA MGOGORO WA WAFANYAKAZI WA UHURU PUBLICATIONS LTD

$
0
0
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto), akiagana na wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kuapata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wa pili kushoto), akifurahia jambo na wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kupata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (mwenye miwani nyuma), akifurahia jambo na wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kupata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wa pili kushoto), akiagana na Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Ramadhan Mkomwa baada ya kikao na wafanyakazi wa kampuni hiyo, waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kupata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.

Wanafunzi Feza Schools washinda kimataifa 'Genius Olympiad'

$
0
0
Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete (kulia) ambaye alishinda medali ya dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata wakizungumza na waandishi wa habari. Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete (kulia) ambaye alishinda medali ya dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata wakizungumza na waandishi wa habari.Mwanafunzi Veronica Samuel Ndomba akielezea (kulia) katika picha na abendera ya nchi yake mara baada ya ushindi katika mashindano ya Genius Olympiad hivi karibuni. Mwanafunzi Veronica Samuel Ndomba akielezea (kulia) katika picha na bendera ya nchi yake mara baada ya ushindi katika mashindano ya Genius Olympiad hivi karibuni.Picha ya Mwanafunzi Prince Mwemezi Muzamil Katunzi aliyoipiga na kushinda katika mashindano ya Genius Olympiad. Picha ya Mwanafunzi Prince Mwemezi Muzamil Katunzi aliyoipiga na kushinda katika mashindano ya Genius Olympiad.Wanafunzi wa Shule za Feza Tanzania walioshinda mashindano ya taaluma kimataifa ya 'Genius Olympiad' katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao.Wanafunzi wa Shule za Feza Tanzania walioshinda mashindano ya taaluma kimataifa ya 'Genius Olympiad' katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao.

Mwanafunzi Yahya Mhata ambaye kwa pamoja wamebuni mfumo huo, ameuelezea kuwa ni mzuri na rafiki wa mazingira huku ukiweza kuhifadhi kumbukumbu za mawasiliano kwa uhakika tofauti na ule wa kadi za makaratasi ambao wengi hupoteza kadi hizo na kujikuta wakipoteza mawasiliano muhimu. 

 Wanafunzi wengine wa Shule za Fedha ambao ni Prince Mwemezi Muzamil Katunzi, Goodluck Komba, Sajjad El-Amin na Veronica Samuel Ndomba ambao kila mmoja ameshinda medali za fedha katika makundi ya ushindani tofauti chini ya usimamizi wa mwalimu Metin Er wa Masomo ya Biashara, Fedha International School walieleza kunufaika na mashindano kitaaluma na upeo. 

 Mwanafunzi Mwemezi Muzamil Katunzi, ambaye aliwasilisha picha yenye ujumbe wa mazingira na kushinda alisema picha hiyo aliipiga eneo la viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam ikielezea namna binadamu wanaathiri mazingira kwa kuchoma moto hovyo na kuleta matatizo mengine duniani. Kwa upande wao wanafunzi Goodluck Komba na Sajjad El-Amin waliwasilisha andiko la mradi wa kutengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi taka ambao ulishika nafasi ya tatu katika mashindano ya Genius Olympiad yaliyofanyika jijini New York. 

Mwanafunzi Komba alisema mradi wao ni rafiki wa mazingira na ukitumika utaokoa sehemu kubwa ya uharibifu wa mazingira. Kwa upande wake msichana pekee aliyeshinda katika mashindano hayo, Veronica Samuel Ndomba alisema andiko lake lilishinda kwenye kipengele cha 'Mazingira Yetu' na aliandika kuonesha namna elimu ya mazingira inaweza kutolewa na kulinda uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa katika shughuli mbalimbali za binadamu.

 Naye msimamizi wa wanafunzi hao, mwalimu Metin Er alisema kundi hilo la wanafunzi mbali na kujijenga kimaarifa kwa wanafunzi hao wameiletea sifa Tanzania kwani kwani mashindano hayo ya kitaaluma yalishirikisha nchi mbalimbali zikiwemo USA, Romania, Nigeria, Tunisia, Holland, Turkmenistan, Kazakhstan and Russia. Shule za Fedha International School zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma kitaifa na kimataifa jambo linaloendeleza umaarufu wa shule hizo kila uchao. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

TANAPA KUTOA TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA UTALII NA UHIFADHI JIJINI MWANZA JUMATATU JUNI 29, 2015

$
0
0
k
Meneja  Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (Tanapa),Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makao makuu ya shirika hilo leo jijini Arusha juu ya utoaji Tuzo za umahiri wa uandishi wa habari za Utalii na Uhifadhi utakaoaofanyika  Jumatatu ,Juni 28,2015 jijini Mwanza.l
Waandishi wa habari kutoka taasisi mbalimbali jijini Arusha wakiondoka Makao Makuu ya Tanapa baada ya kumaliza mkutano huo.
Na Filbert Rweyemamu,Arusha
Shirika la Hifadhi za Taifa nchini(Tanapa)litatoa Tuzo za umahiri wa Uandishi bora wa Habari na Makala zinazohusu Utalii na Uhifadhi  nchini kwa waandishi wa Habari nchini ikiwa ni kutambua mchango wako katika kukuza sekta hiyo nchini.  Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Arusha,amesema maandalizi yote yamekamilika na utoaji Tuzo utafanyika jijini Mwanza,Jumatatu,Juni 28,mwaka huu.

Amesema idadi ya washiriki imekua ikiongeza kila mwaka hasa waandishi wa  kutoka nje ya miji mikubwa kama Dar es Salaam,Arusha na Mwanza hali inayoonyesha mashindano haya kukua. “Tumeshuhudia mwaka huu waandishi wengi kutoka mikoa ambayo awali haikushiriki lakini wakati huu wapo waandishi wa Redi za kijamii ambao kazi tumezipokea,”
Washindi wanatarajiwa kujipatia fedha taslimu na kupata safari za mafunzo katika moja ya nchi za Sadc.

Shelutete amesema kwa kipindi cha miaka minne washindani wamekua wakichaguliwa kutoka vyombo vya habari vya Runinga(TV)Radio na Magazeti lakini mwaka ujao wigo utapanuliwa na kujumuisha Mitandao ya Kijamii na Wapigapicha.

CHAMA CHA ACT CHATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI EDSON KAMUKARA.

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
……………………………………………………
CHAMA cha Alliance ForChange and Transparance( ACT- Wazalendo.)kinachozingatia msingi wa utu, undugu na uzalendo kwa Taifa,kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mwandishi wa Habari Edson Kamukara.
Kutokana na msiba huo Chama kinatoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu, ndugu jamaa na marafiki,waaandishi wa Habari na wafanyakazi wote wa Hali Halisi Publishers kwa kuondokewa na mtu ambaye mchango wake kwa Taifa ulikuwa unahitajika kwa kiasi kikubwa hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu katika nchi
Tunawaombea kwa mungu wawe na uvumilivu na kuzidi kumuombea marehemu apate pumziko la amani.
Kichama tumempoteza mtu aliyekuwa akituelekeza upungufu wetu kupitia kalamu yake hali iliyotufanya tujirekebishe kila tunapobaini ukweli wa ukosoaji wake.
Tunazidi kumuombea kwa Mungu ampe faraja katika utangulizi wake huu, huku tukiwa na mengi mema ya kujifunza kutoka kwake.
Imetolewa na
Samson Mwigamba
Katibu Mkuu Taifa ACT-Wazalendo
Juni 26,2015

SULEIMAN NYAMBUI AWAAGA WATANZANIA AKISONONEKA

$
0
0
M
Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui (kulia) akikabidhiwa suti ya michezo yenye bendera ya Tanzania kutoka Meneja Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally atakazozitumia wakati akifubndisha riadha nchini Bunei barani Asia ambako amepata mkataba wa kufundisha riadha kwa miaka miwili. (Picha na Peter Mwenda).N
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports,Abbas Ally akimkabidhi zawadi ya suti Katibu Mkuu wa zanmani wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suliman Nyambui anayekwenda kufanya kazi ya kufundisha riadha nchini Bunei,Asia.
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) aliyeachia wadhifa huo, Suleiman Nyambui ameiasa Serikali kuwa ikitaka kurudisha heshima ya michezo kama zamani ni lazima irudishe vipindi vya michezo (Physical Education PE) kuanzia shule za msingi.
Nyambui ambaye amejing’atua kuendelea na madaraka yake ya Ukatibu Mkuu wa RT baada ya kuingia mkataba wa kufundisha riadha kwa kipindi cha miaka miwili nchini Brunei barani Asia, alisema Tanzania kama haitarudisha michezo katika programu zake hakutakuwa na ushindi.

Alisema Serikali ikiweka mikakati ya michezo na kutenga viwanja vyenye ubora vya kuchezea tutaendelea kuwa wasindikizaji katika michezo yote ya riadha, soka, netiboli, ngumi na mingine ambayo kila wachezaji wakishiriki hakuna ushindi unaopatikana kulinganisha na zamani ambako wao waliwika.

Nyambui alisema Tanzania imejaliwa kuwa na wachezaji wenye vipaji na baadhi ya maeneo yanayofaa kwa ajili ya kujenga viwanja na kuweka kambi za mazoezi kwa timu za taifa kama Tanga,Mbulu, Arusha, Singida, Njombe, Makambako na Mbeya ambako hali ya hewa inaruhusu wachezaji kufanya mazoezi kwa nguvu.
Alisema kutofanyika mashindano ya michezo katika ngazi za wilaya inawanyima wachezaji wengi wenye vipaji kuonesha uwezo wao wa kujituma kutumikia taifa katika michezo kwa sababu hawaonekani.
Akipokea zawadi ya suti na vifaa vya michezo vyenye bendera ya Taifa kutoka Kampuni ya Isere Sports, Nyambui alisema Serikali pia inatakiwa kuwasaidia waagizaji na wauzaji wa vifaa vya michezo wapunguziwe ushuru ili wauze vifaa hivyo kwa bei nafuu.

Nyambui aliyewahi kuwa mshauri wa ununuzi wa vifaa vya michezo wa Kampuni ya Isere alisema katika kipindi cha miaka miwili atakayokuwa nje ya Tanzania bado ataendelea kutoa ushauri kwa watanzania wa njia nzuri ya kujikwamua.

MASIKINI MAMA HUYU KWA MAUMIVU ANAYOYAPATA AOMBA KUKATWA MGUU.

$
0
0
JAMII imeombwa kutoa msaada wa hali na mali kwa BI GRACE KAIZA mkazi wa Igoma jijini Mwanza ambaye ameomba mukatwa mguu wake kutokana na Saratani ( Kansa) katika mguu huo.

Akizungumza na *JEMBE Habari* Bi. Grace Kaiza amesema amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu jambo lililomuathiri kwa kiasi kikubwa kiafya na hata kiuchumi.


Akielezea namna tatizo hilo lilivyompata amesema lilianza kama uvimbe katika mguu wake kisha kufanyiwa upasuaji mara kadhaa lakini haikusaidia na ndipo alipobainika kuwa na ugonjwa huo.

Ameongeza kutokana na ugonjwa huo amekuwa akipata maumivu makali mno yanayo mliza hasa nyakati za usiku hali inayomfanya kushindwa kulala.
Naye msamalia mwema ambaye pia nimjumbe wa serikali ya mtaa wa NYAKATO MAHANGO Jijini Mwanza BI KHADIJA YASIN amesema kuna haja ya kumsaidia BI GRACE kutokana na shida anazopata. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA KISA NA MKASA.

Fedha inayohitajika ili kuweza kumsaidia BI GRACE Aaondokane na tatizo alilonalo ni kiasi cha shilingi milioni mbili za kitanzania, ambazo zitamwezesha kuondolewa mguu kabla haujaleta madhara zaidi.

Kwa yeyote atakayeguswa na taarifa hii anaweza kuwasiliana na BI GRACE kwa ajili ya kumsaidia kupitia namba za simu 0768 264 182 

RAIS KIKWETE AONGOZA SIKU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA DUNIANI MJINI BAGAMOYO – JUNI 26, 2015

$
0
0
R
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa mawasiliano kuhusu athari za magonjwa mbalimbali hatarishi kupitia simu ya mkononi akiwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif  Selemani Rashid na Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA)  Bw. Peter Masika  kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Dunia, katika Viwanja vya Taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mjini Bagamoyo leo Juni 26, 2015. 
PICHA NA IKULU
B
Wasanii wanafunzi wa Mwaka wa tatu wakichezaa igizo la athari za  madawa ya kulevya mbele ya Rais Kikwete wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Dunia yaliyofanyika katika Viwanja vya Taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mjini Bagamoyo leo Juni 26, 2015
D   Z
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipena mikono na timu za michezo zilizoshinda michezo ya waathirika wa madawa ya kulevya walio katika matibabu kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Dunia ni katika Viwanja vya Taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mjini Bagamoyo.

TUME NEC YAAHIRISHA KWA MUDA WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA MFUMO WA BVR DAR ES SALAAM NA PWANI

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) YATOA SALAAM ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA MSIBA WA EDSON KAMUKARA

$
0
0
 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa kifo cha aliyekuwa mmoja wa waandishi wa habari mahiri na mhariri wa gazeti la mtandaoni, Mwanahalisi Online, Edson Kamukara, kilichotokea ghafla jana jioni katika mazingira yanayodaiwa kuwa ni ajali ya moto.


Kumwelezea Edson Kamukara ambaye kabla ya kuhamia Mwanahalisi Online linalomilikiwa na Hali Halisi Publishers, alikuwa Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima, akiwa ametokea Gazeti la Jambo Leo ambalo alijiunga nalo akitokea Gazeti la Majira, katika nafasi hii ya salaam za pole yenye ukurasa mmoja, linaweza kuwa jambo gumu sana.


Marehemu Kamukara alikuwa mmoja wa waandishi makini na mahiri ambao tasnia ya habari ingeweza kujivunia kuwa nao (wakiwa hai) kwa muda mrefu, hususan katika changamoto kadhaa ambayo taaluma hiyo adhimu inapitia kwa sasa nchini Tanzania.


Katika salaam hizi, CHADEMA kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano ambayo kutokana na majukumu yake ya kila siku ilifanya kazi kwa ukaribu wa kitaaluma na kikazi na Kamukara, inaweza kutaja sifa nne kati ya nyingi alizokuwa nazo Kamukara;

1.     Uthubutu wa kukataa rushwa na kusimamia maadili ya taaluma.

2.     Kupenda kazi yake.

3.     Nidhamu ya kazi.

4.     Uwezo wa kutimiza majukumu yake kazini.


Mbali ya kumsaidia kupata zawadi katika mashindano ya tuzo za umahiri wa uandishi wa habari, chini ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), tunaamini sifa hizo pia zilimfanya Kamukara awe miongoni mwa waandishi vijana walioweza kuaminiwa na kukabidhiwa majukumu ya uhariri katika vyombo vya habari vikubwa akiwa na umri mdogo, baada ya kuwa ameandaliwa na kuiva kuchukua nafasi muhimu katika kutimiza uandishi wa habari unaowajibika kwa umma.



Zinahitajika kurasa kadhaa kuweza kumwelezea Edson. Kwa masikitiko makubwa CHADEMA kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano, kinatoa salaam za pole na rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa kwa namna moja au nyingine na msiba huu wa Kamukara.


Salaam hizi za pole pia ziwafikie wafanyakazi wenzake katika Kampuni ya Hali Halisi Publishers wamiliki wa Gazeti la Mwanahalisi Online kwa kuondokewa na mtumishi mwenzao ambaye tunaamini hadi mauti yanamkuta si tu walifanya naye kazi lakini waliishi naye vizuri.


Aidha chama kinatoa salaam za pole kwa tasnia nzima ya habari nchini hususan kwa waandishi wa habari kwa kuondokewa na mwandishi mwenzao katika wakati ambao mchango wake ulikuwa bado ukihitajika katika mapambano ya kitaaluma na kikazi.


Tunaungana pia katika maombolezo ya msiba huu na wapenzi wote wa kazi za Kamukara ambao wengi wao hususan baada ya kuwa wamesoma makala yake kwenye Gazeti la Mawio toleo la Alhamis wiki hii (jana) ambako alikuwa akiandika mara kwa mara, watakuwa bado hatawaki kuamini kuwa Edson Kamukara katutoka na hatuko naye tena katika ulimwengu huu wa kimwili.


Wakati tukimwombea mapumziko ya amani huko aliko Edson Kamukara, tunamwomba Mwenyezi Mungu awatie nguvu wafiwa wote na kuwajaalia ujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu na moyo wa subira katika wakazi huu wa majozni mazito.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.


Imetolewa leo Ijumaa, Juni 26, 2015 na;

Idara ya Habari na Mawasiliano

CHADEMA





ZIARA YA KATIBU MKUU NDANI YA JIMBO LA MAGU LEO,KESHO KURINDIMA JIMBO LA NYAMAGANA JIJINI MWANZA.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu kushoto wakionyesha magwanda yaliokabidhiwa kwao aiyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wilaya ya Magu,Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi kutoka CHADEMA.Zaidi ya wananchama 53 kutoka vyama vya upinzani walijiunga na CCM wakiwemo Chadema 28 na ACT 12 na wengine kutoka vyama vingine.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea magwanda ya aliyekuwa  Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu  Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi, kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizokuwa  za wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo na vyama vingine mara baada ya wanachama hao kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi cha Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza.

Katibu Mkuu huyo amempokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu  Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi , Kinana yuko katika ziara ya kikazi  ya mkoa Mwanza akimalizia mkoa wa mwisho wa Tanzania baada ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani akipita katika majimbo yote, wilaya zote hapa nchini  na nusu ya Kata na vijiji kwa muda wa miaka miwili akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.

Kinana amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku akihimiza uhai wa CCM ambapo pia  katika ziara hiyo amekuwa akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye . 
Baadhi ya Kadi za wafuasi wa vyama mbalimbali walizoamua kuachia ngazi na kuhamia chama CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo wakifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa utumiaji wa maji hayo katika mji wa Magu. 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Magu. Katika Kikao hicho Katibu Mkuu wa CCM amewajia juu Viongozi wanaotumia vibaya nafasi zao kwa kujifanya maarufu zaidi ya Chama alisema "Hakuna mtu maarufu zaidi ya CCM huku akisema kuna watu wanaona kama wamekiteka hiki chama nyara na kukiweka kwenye kikapu na kuzunguka nacho, Hatutokubali hilo litokee" aliendelea kusema bora mtu aende upinzani kulikoni kuwa na sisi halafu anatuumiza. 

 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo akizungumza na wananchi kuhusu kuiagiza mamlaka ya Mapato TRA na kikosi cha Usalama Barabarani kuenda katika wilaya kwa ajili ya kutoa huduma za utoaji wa leseni za uendeshaji vyombo vya moto na kukusanya kodi mbalimbali za vyombo vya moto ili kupunguza urasimu wa huduma hiyo ambazo zimekuwa zikipatikana kwenye miji mikuu ya mikoa peke yake.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Magu mjini,aliyekuwa akitoa kero yake kubwa ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo,katika mkutanno wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa saba saba
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akijibu hoja mbalimbali zilizokuwa zimeulizwa na baadhi ya wakazi wa mji wa Magu mapema leo jioni katika mkutanno wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa saba saba
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibeba tofari mara baada ya kushiriki kufyatua wakati alipokagua shughuli za kikundi hicho katika kijiji cha Irungu wilayani magu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akzungumza jambo mara baada mara baada ya kukabidhi mashine kwa vijana wafyatua matofali katika kijiji cha Nyigoro-Ilungu wilayani Magu,ambapo vijana hao walipata tenda ya kujenga Nyumba ya Bibi Asteria Selemani inayojengwa na Mwanaye Zakaria Andrew katika kijiji cha Irungu wilayani Magu Anderw amekipatia tenda ya kufyatua matofali ya kujengea nyumba hicho kikundi cha vijana ambacho  kimefadhiliwa mashine ya kufyatua matofali na Shirika la Nyumba Tanzania NHC.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa maji wa Wilaya ,Injinia Rutta Merchades alipotembelea chanzo cha maji Nyanguge wilayani Magu.
 Wakazi wa Nyanguge wakisubiri maji kuzinduliwa na katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya mkoa wa Mwanza ya kukagua ,kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa mradi wa Maji Nyanguge.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji kama ishara ya kuzinduliwa kwa huduma za maji Bi.Yustina mkazi wa Nyanguge.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsalim fundi Raina Lucas anayeshiriki ujenzi wa jengo la x-ray katika kituo cha afya Kisesa.
 Pichani ni moja ya jengo la X-Ray linalojengwa  katika kituo Afya Kisesa wilayani Magu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu  Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Kisesa mapema jioni ya leo alipokuwa akimaliza ziara yake ndani ya jimbo la Magu.

Vibe magazine is Now for Free

$
0
0


A prominent entertainment monthly magazine The Vibe which published by ABC Bros  was re launched and now will be distributed free to the readers. This will make it Tanzania’s number 1 FREE entertainment Youth Magazine
The magazine Editor in Chief Allan Rwechungura said that since the magazine was launched,it has achieved the objectives and now is  leading entertainment magazine in Tanzania. “On behalf of Vibe Magazine team, I deeply appreciate your support and its great to know that we can count on you ”.
Rwechungura said from this month the Vibe Magazine will be distributed  for free to its readers and advertisers, which means the increase number of readership and more exposures for advertisers,  “We promise to bring more news on entertainment, sports as well as other issue relevant to entrepreneurship skills targeting to empower and educate Tanzanians youths,hope our readers will enjoy more”
He said the magazine will be distributed in prime locations in the country,in saloons/barbershops, in colleges and universities as well as remote areas to enable many readers to get entertainment news,and also will be available online.

CHAMA CHA WAFANYAKAZI MADEREVA TANZANIA (TADWU), CHAMKABIDHI MLEZI WAO MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA RASIMU YA MKATABA WA MABORESHO YA MASLAHI YAO.

$
0
0
 Mlezi wa chama cha wafanyakazi madereva Tanzania (TADWU), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na madereva kabla ya kukabidhiwa rasimu ya maboresho ya maslahi ya madereva hao na cheti cha utambulisho wa chama hicho Dar es Salaam jana. Kulia ni  Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah Lubara na Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah Lubara (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, rasimu ya mkataba wa maslahi ya madereva waliyokuwa wakiidai serikali kwa muda mrefu Dar es Salaam jana.

Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda cheti cha utambulisho wa chama chao kipya kitakachoitwa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU) baada kuundwa rasmi ambacho kitazindulia Julai Mosi mwaka huu.
 Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Said (kulia) akizungumzia yaliyomo kwenye rasimu hiyo na maboresho ya maslahi yao.
 DC Makonda akisalimiana na madereva baada ya kumaliza kwa mkutano huo.
 Madereva wakiwa wamesimama wakisubiri kusalimiana na mlezi wao DC Paul Makonda.
 Ni usikivu kwa mlezi wao wakati akihutubia.
 Mkutano ukiendelea.
 Hapa ni furaha tupu kwa madereva hao.
 Madereva wakiwa kwenye mkutano huo.
 Madereva wakishangilia hutuba ya mlezi wao Paul Makonda.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea


Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Madereva nchini nchini kimemkabidhi mlezi wao Mkuu wa Wlaya ya Kinondoni Paul Makonda rasimu ya mkataba uliobeba maboresha ya maslahi waliokuwa wanaidai kutoka kwa wamiliki pamoja na Serikali.

Katika hatua nyingine madereva hao Julai Mosi mwaka huu wanatarajiwa kuzindua chama chao ambacho kitaitwa Chama cha Madereva Wafanyakazi Tanzania (TADWU).

Hatua ya kutengeneza rasmu hiyo hiyo imekuja baada ya kikao walichokaa Juni 21 mwaka huu ambapo lengo lilikuwa ni kuwashinikiza waajiri kuwapa mikataba ya kudumu wakiwa kazini ikiwa ni pamoja na likizo za uzazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Said alisema rasimu ya mkataba huo imebeba maboresho ya maslahi yao waliyokuwa wanadai.

Alisema madai hayo ni pamoja na bima ya maisha , mazishi yenye staha, muda wa kazi kisheria, matibabu, na nauli ya kwenda kazini.

"Leo tuna chama cha wafanyakazi madereva Tanzania , pia tumepewa mkataba hivyo nawatangazia madereva wote kuwa tumepata  chombo cha kuzungumzia tofauti na ilivyokuwa awali.

Kwa sasa imebaki kujadili na serikali kuhusu kuboreshwa kwa mishahara hivyo napenda kuwatangazia madereva kuwa tumepata mikataba tuliyohitaji miaka mingi,"alisema.

Katibu huyo aliongeza kuwa chama hicho hakitasita kumchulia hatua za kisheria mmiliki atakayekiuka sheria hizo na kuongeza hakitasitakumpeleka kwenye vyombo vya sheria kama walivyokuwa wanawafanyia mwanzoni.

Akikabidhiwa mkataba huo kwa chama hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema mahali walipofikia madereva hao kwa sasa ni jambo la kuleta maendele makubwa.

Alisema watanzania wanatakiwa kutambua kuwa madai hayo si kwa ajili ya madereva peke yao  bali ni kwa ajili ya taifa zima na kwamba kutatuliwa kwa changamoto hiyo kutapunguza ajali zinazoendelea kutokea nchini.

Makonda alisema asilimia kubwa ya madereva wamekuwa wakipata ajali kutokana na kuchoka hivyo wanaposinzia usahau kuwa wanaendesha vyombo vya moto hivyo kusababisha ajali.

Katika hatua nyingine Makonda alisema kuwa asilimia 80 ya waandishi wa habari hawana mikataba ya kudumu na kwamba ni changamoto hivyo aliwataka kwenda kuonana nae ili kupata ushauri wa namna ya kuwawezesha kuhakikisha wanapewa mikataba ya ajira na waajiri wao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)






Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images