Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

JANUARI MAKAMBA ATUA BUKOBA LEO, APATA MAPOKEZI MAKUBWA NA KUZOA WADHAMINI LUKUKI

$
0
0
Mh. Januari Makamba baada ya kusalimiana na Wakazi waliojitokeza kwenye Makao makuu ya CCM ameelekea katika Hospitali ya Mkoa kuwaona wagonjwa mbalimbali na Baada ya hapo ameelekea Wilayani Misenyi kwenda kusalimia Wakazi wa huko na Kuwaomba wamdhamini kwa kuweka saini fomu zake za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho cha CCM.
Mh. Januari Makamba Akitia saini Katika kitabu cha wageni Ofisi za CCM

January Akizungumza na wakazi wa Bukoba waliojitokeza kumsikiliza katika katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kagera leo.


Wakazi wa Mji wa Bukoba wakimsikiliza Mh. January Makamba kwa makini leo hii jumatano.



Mh. January Makamba na mkewe, Ramona Makamba(kulia) baada ya kuwasili mkoani hapa Kagera kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho cha CCM. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Mh. January Makamba na mkewe, Ramona(kulia) mara baada ya kushuka kwenye Ndege leo hii Jumatano asubuhi juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Mh. January Makamba akisalimiana na Katibu wa Vijana Mkoa wa Kagera
Mh. January Makamba akisalimiana na Wanafunzi wa Sekondari waliokuwa  Uwanjani hapo ambao bila Shaka walikuwa wanasoma masomo ya Ndege inavyoruka na kutua na mengineyo kiujumla leo jumatano juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mh. January Makamba akisaini kwenye kitabu cha Wageni kwenye Uwanja Ndege Bukoba.
Mh. January Makamba na mkewe, Ramona wakiteta jambo kwa furaha.
Msafara wa Bodaboda kuelekea Mjini kwenye mzunguko na kugeuka kwenye Makao makuu ya CCM Mkoa wa Kagera



Mjini Bukoba, Bodaboda wakimsindikiza Mh. Januari Makamba



Makamba akisalimia Wakazi wa Mji wa Bukoba walijitokeza kwa wingi
January Makamba ameendelea na Ziara yake ya Kusaka Wadhamini katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania na leo hii jumatano juni 24, 2015 yupo hapa Mkoani Kagera akiomba Uzamini. Mh. January Makamba amepokelewa na wakazi wengi wa Mkoa wa Kagera wakiwemo Vijana walijitokeza kwa wingi kumpokea. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

MAASKOFU WABARIKI UZINDUZI WA ALBAMU YA BONNY MWAITEGE

$
0
0
VIONGOZI wa dini wakiwemo Maaskofu na Wachungaji wa Makanisa mbalimbali hapa nchini wamebariki uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji mahiri wa muziki wa Injili hapa nchini Bonny Mwaitege, unaotarajia kufanyika Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama sababu za viongozi hao wa dini kutoa baraka kwa albamu hizo ni kutokana na umahiri wa muimbaji huyo.
Msama alisema amepokea baraka hizo kutoka kwa viongozi hao wa dini kwa sababu uzinduzi huo unashirikisha albamu tatu kwa pamoja, jambo ambalo linaonesha ni ukomavu na umahiri katika kufanikisha neno la Mungu ipasavyo.
“Uzinduzi wa Bonny Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu viongozi wa dini mbalimbali wametia baraka kwa maneno matakatifu ambayo yatafanikisha ufikishwaji wa neno la Mungu kwa jamii ipasavyo,” alisema Msama.
Msama alisema baraka hizo za viongozi wa dini zinakwenda sambamba na maombi ya kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchini ambao utahusu urais, Wabunge na Madiwani.
“Viongozi wa dini ndio wanafanikisha tunu ya amani tuliyonayo, hivyo wameongeza chachu ya maombi ya amani hiyo tuliyoachiwa na baba wa Taifa, Mwalim Julius Kambarage Nyerere,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema hivi sasa wanaendelea na maandalizi ya kurekodi albamu hizo jijini Mwanza ili kupata ladha nzuri ya nyimbo hizo za kumuimbia na kumtukuza Mungu.
“Waandaaji wanaendelea na kazi yao ya kufanikisha kurekodi albamu hizo ambazo zitakuwa na ubora wa aina yake kwa sababu umahiri wa watendaji wake ambao ni wa kampuni yake ya Video Productions. Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili kujiandaa kupata kazi bora ya muimbaji huyo ambaye anashika anga la muziki huo Afrika Mashariki na Kati.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU-JUNI 24, 2015

$
0
0
01
03
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano la Nne la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 24, 2015.02
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoma kwa Profesa Nerey Mvungi wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam juu ya Ubunifu wake wa kutengeneza mfumo wa kidigitali wa kusaidia kupambana na ajali barabarani  kabla hajafungua Kongamano la Nne la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 24, 2015
mail.google.com
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoma kwa kijana Godfrey Magila wa Magilatech Company Ltd.  juu ya Ubunifu wake wa kutengeneza mfumo wa teknolojia ya mawasiliano rahisi  kabla hajafungua Kongamano la Nne la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 24, 2015
PICHA NA IKULU

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII LAZARO NYALANDU APATA WADHAMINI WILAYANI MASASI, MTWARA

$
0
0
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisalimiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Masasi, Mtwara, jana, wakati alipofika kuomba udhamini kwa wanachama wenzake, akiomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Mbele ni Katibu wa CCM wilayani humo, Mwanamasudi Msafiri Pazi.2
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akikabidhiwa fomu na Katibu wa CCM Wilaya ya Masasi, Mwanamasudi Msafiri Pazi, baada ya kudhaminiwa na wana-CCM zaidi ya 97. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Kazumari Malilo, kwenye Ofisi za CCM wilayani humo.
3
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akikabidhiwa fomu na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Masasi, Polle Polle, baada ya kudhaminiwa na wana-CCM kwenye Ofisi za Chama hicho.
4
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisalimiana na kijana wa Chipukizi wilayani Masasi, Raheli, wakati alipofika kuomba udhamini kwa wanachama wa CCM, jana, ambapo zaidi ya 97 walijitokeza kumdhamini.
5
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza na wanachama wa CCM waliojitokeza kumdhamini katika harakati zake za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu ujao, jana. Kushoto ni Mjumbe wa NEC, Polle Polle na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilayani Masasi, Kazumari Malilo.

MAWAKALA WA FORODHA NCHINI WAASWA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA HIMAYA MOJA YA FORODHA YA AFRIKA MASHARIKI (SINGLE CUSTOM TERRITORY)

$
0
0
1
Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi akiongea na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na kuwataka mawakala wa Tanzania kujisajili katika mfumo wa uondoshaji wa Himaya moja ya Forodha(SINGLE CUSTUM TERRITORY) ili kuwezesha uondoshwa wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika kwani mifumo huo na watanzania tayari zinawasiliana mpaka sasa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kushoto ni Naibu Kamishna wa Forodha Dkt. Patrick Mugoya.
2
 Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga akiongea na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na wawakilishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo aliipongeza serikali kupitia Mamlaka hiyo katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa mawakala wa forodha na kuiasa kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ili kuiwezesha serikali kupata mapato kwa maendeleo ya Taifa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kulia ni Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi.
3
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakimsikiliza Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

4
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakichangia wakati wa mkutano uliokutanisha Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
5
………………………………………………….
Habari Picha Na Hassan Silayo-MAELEZO
Mawakala wa Forodha nchini wameaswa kujisajili katika mfumo wa uondoshaji mizigo wa Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki (Single Custom Territory) utakao anza kutumika hivi Karibuni.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi wakati mkutano na Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA)
Bw. Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha nchini hawana budi kufanya hivyo ili kuwezesha uondoshwaji wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika.
“Sasa tunaelekea katika matumizi ya Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki yaani Single Custom Territory ili kuwa na uwezo wa kupata huduma kwa kutumia mfumo huo pindi matumizi yatakapoanza mapema ili kuondoa usumbufu utakaoweza kutokea”. Alisema Bw. Kabisi
Bw. Kabisi aliongeza kuwa mpaka sasa ni makampuni mawili (2) ya mawakala waliojisajili mpaka sasa.
Aidha Bw. Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha hawana budi kuendelea kuwa waamifu ili waendelee kuongoza katika makusanyo ya fedha kwa mwaka ujao ambapo kwa mwaka huu wamechangia kwa asilimia 40 ya mapato ya serikali.
Naye Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga alisema kuwa wataendelea kushirikiana na Mamlaka la Mapato Tanzania (TRA) katika kuhakikisha wanaifanya idara ya forodha inafanya vizuri katika makusanyo ya fedha.
Pia Bw. Ngatunga aliitaka serikali kuendelea kushughulikia changamoto mabalimbali zinazoikabili idara hiyo ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu na kuendelea kuongoza katika makusanyo ya mapato ya serikali.

MOROGORO WAJITOKEZA KWA WINGI KUMDHAMINI WAZIRI BERNARD MEMBE

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (mwenye miwani), akilakiwa na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofurika nje ya viwanja vya ofisi ya CCM ya Morogoro Mjini Juni 24.2015, wakati akitafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini.Picha zote na John Badi.SONY DSC
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofurika nje ya viwanja vya ofisi ya CCM ya Morogoro Mjini Juni 24.2015, wakati akitafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini.

CCM ZANZIBAR YALAANI CUF KUSUSIA VIKAO VYA BARAZA

$
0
0
1
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Waandishi wa Habari katika Afisi kuu CCM Kisiwandui ambapo amelaani hatua ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF kugomea Vikao vinavyoendelea vya Baraza la Wawakilishi hapo Jana.2
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukuwa maeelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Afisi kuu CCM Kisiwandui. Vuali amelaani hatua ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF kugomea Vikao vinavyoendelea vya Baraza la Wawakilishi hapo Jana. 

RAIS KIKWETE NA DKT. REGINALD MENGI IKULU, DAR ES SALAAM

$
0
0


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa  Vyombo vya Habari (MOAT) Dkt Reginald Mengi wakiongea na kubadilishana mawazo Ikulu, Jijini Dar es salaam katika hafla ya kutunuku nishani  kwa watumishi wa umma na wananchi waliofanya vyema na kwa uadilifu kwenye sehemu zao za kazi. Dkt Mengi alikuwa mmoja wa watu mashuhuri walioalikwa
hapo Ikulu. PICHA NA IKULUJ

4TH GLOBAL ANIMAL HEALTH CONFERENCE 2015

$
0
0
 mail.google.com
Director of Veterinary Services, Ministry of Livestock and Fisheries Development Mr Abdu Hayghaimo delivers his keynote speech when he was opening a 4th Global Animal Health Conference 2015 in Dar es Salaam yesterday organized by the federation Health forAnimals (formerly known as IFAH) with the support of the Organising Committee partners and funded by the Bill and Melinda Gates Foundation.
m
A cross-section of participants of the 4th Global Animal Health Conference 2015 in Dar es Salaam yesterday organized by the federation Health forAnimals (formerly known as IFAH) with the support of the Organising Committee partners and funded by the Bill and Melinda Gates Foundation.

Article 4

Airtel yatoa 20m/- kufuturisha Vituo vya watoto yatima nchini

$
0
0
 Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akiongea na waandishiwa wa habari katika hafla ya makabidhiano ya hundi kwa Bakwata, kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima hapa nchini vyenye thamani ya sh. Milioni 20 , Kulia ni Sheikh Mohamed Khamis Said mwakilishi wa Bakwata.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akikabidhi hundi yenye dhamani ya sh.milioni 20 ya msaada wa vyakula kwa BAKWATA kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima hapa nchini, akipokea (Kulia) Sheikh Mohamed Khamis Said mwakilishi wa Bakwata.


Airtel Tanzania imetoa Tsh Milioni 20 kwa Jumuiya ya Waislamu kupitia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa lengo la kufuturisha vituo kumi vya kulelea watoto yatima nchini. 
Akikabidhi hundi kwa Naibu katibu Mkuu wa Bakwata Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Hawa Bayumi alisema vituo vitakavyopata msaada huo ni pamoja na Kigogo Fresh orphanage cha Ilala, IHSANI orphanage cha Temeke, Almadina center kinondoni.
Pia kwa Arusha ni Kiboa Islamic orphanage, Nusuru yatima orphanage Bukoba, Nuru orphanage Mbeya, Zam zam orphanage Dodoma, Maua Daftari Foundation Zanzibar, Chuno orphanage center Mtwara na Makorora Yatima center cha Tanga ambapo kila kimoja kitapatiwa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni2. 
“Airtel Tanzania kama inavyofanya miaka mingine leo pia inaungana na ndugu na jamaa zetu waislamu kuadhimisha mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa kuwakumbuka watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia hivi vituo ili nao waweze kushiriki mfungo wa Ramadhan.” alisema. 
Aliongeza kuwa Airtel imekuwa ikitoa misaada kama hii kwa makundi mbalimbali katika jamii kila mwaka na kusisitiza kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Airtel watajumuika na watoto hawa katika mwezi huu ili na wao pia wajiskie kama sehemu ya jamii. 
“Tunapenda kutoa rai kwa mashirika mengine pia yawakumbuke hawa watoto na kuwasaidia ili wajisikie kama sehemu ya jamii,” alisema. 
Akipokea hundi hiyo, Naibu katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mohamed Khamis Said aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo na kusisitiza kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa na kuhakikisha watoto wanaolelewa katika vituo hivi wanapata mahitaji muhimu hasa katika mwezi huu wa Ramadhan. 
“Tunashukuru mno kwa niaba ya vituo hivi na tunatoa wito kwa mashirika mengine pia yajitokeze na kutuunga mkono ili tuweze kufikia yatima wengi zaidi na kuwapa faraja katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan” alisema.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA KWIMBA MKOANI MWANZA LEO

$
0
0
Sehemu ya Umati wa wakazi wa wilaya ya Kwimba na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara,Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu,Ndugu Kinana alikemea tabia ya wapinzania kuwahadaa vijana nchini kuwa wakiingia madarakani wataweza kuwatekelezea kila kitu,aidha aliwataka vijana wa kitanzania kuacha kabisa kuhadaika na baadhi ya Wanasiasa ambao wamekuwa wakiwapotosha na kuamini kila kitu kitapatikana bila kufanya kazi na kujituma.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani Kwimba, ambapo aliitaka jamii wakiwemo mabalozi wa mashina kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO), ili kuepusha mauaji dhidi yao.
Wananchi wilaya ya Kwimba wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo.
 Mbunge wa Jimbo la Kwimba,Mh., Shanif Mansoor akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo. 
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa  CHADEMA katika Kijiji cha Ilula kata ya Ilula wilayani Kwimba,ndugu AmaraMateremki  akizungumza baada ya kuamua kukihama chama hicho na kuijunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akionesha baadhi ya kadi za wafuasi wa chama cha CHADEMA kuhamia CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akikabidhi msaada wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu Mjini Ngudu. Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor pichani shoto.
Mmoja wa viongozi kutoka kikundi cha akina mama kiitwacha UAMSHO akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana mara baada ya kukabidhiwa vyerehani vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor .
 Balozi Specioza Balele wa CCM Shina namba 12, akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipomtembelea wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba katika Mji wa Ngudu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiongea kwa balozi wa shina namba 12,Balozi Specioza Balele wa CCM Shina namba 12, alipomtembelea wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba katika Mji wa Ngudu.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kwimba Ndugu Petro Ngh'ingi wakati wa mapokezi kwenye kijiji cha Mwamaya kata ya Hungumalwa Pichani kati ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba Bi.Tabu Lugwesa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor wakati wa mapokezi kwenye kijiji cha Mwamaya kata ya Hungumalwa wilaya ya kwimba mkoani Mwanza.
 Walinzi wa Jadi wa kisukuma maarufu kwa jina la Sungusungu wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mavazi ya jadi ya walinzi wa Kisukuma maarufu kama Sungusungu.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa kata ya hungumalwa waliojitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kijiji cha Mwamaya, Kwimba mkoani Mwanza.
 Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor akihutubia wakazi wa kijiji cha Mwamaya wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamaya waliojitokeza kwa wingi kumpokea kwenye wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasha umeme kama ishara ya kuwasha umeme  kwenye nyumba ya Ndugu Charles Lusana mkazi wa kijiji cha Mwamaya kata ya Hungumalwa,Kwimba mkoani Mwanza.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Ndugu Charles Lusanamkazi wa kijiji cha Mwamaya kata ya Hungumalwa mkoani Mwanza mara baada ya zoezi la kuwasha umeme kukamilika
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia kikundi cha ngoma za utamaduni Idibuili wakati alipotembelea kijiji cha Hungumalwa kuona na kushiriki ujenzi wa Zahanati.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilula Hamala Materemki, kata ya ilula wilani Kwimba aliyejiuzulu na kuamua kujiunga na CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Diwani ya kata ya Hungumalwa Shija Marando wakati wa kuona na kushiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hungumalwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Hungumalwa wakati wa kuona maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya kijiji.Wengine pichani ni Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor na Diwani wa Kata ya Hungumalwa Shija Marando.
 Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor akishiriki ujenzi wa zahanati ya Hungumalwa wilayani Kwimba.

LOWASSA AENDELEA KUSOMBA WADHAMINI KWA KISHINDO JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Jiji la Arusha waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa ulipo mbele ya Ofisi za CCM Mkoa huo, leo Juni 24, 2015, wakati alipofika kwa ajili ya kupata udhamini utakaomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Mh. Lowassa akiwaaga WanaCCM wa Mji wa Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (wa tatu kulia) sambamba na Mkewe Mama Regina Lowassa, wakiongozana na viongizi mbali mbali wa Chama wa Mkoa wa Arusha waliofika kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA, wakati akitokea Mkoani Dodoma kuhudhulia vikao cha Bunge na kupigia kura bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimjulia hali Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM, Mathias Manga, aliyejeruhiwa kwa risasi jana usiku na watu wasiofahamika, wakati walipokutana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa KIA, Mkoani Kilimanjaro leo Juni 24, 2015.
Sehemu ya Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaoishi maeneo ya jirani na Uwanja wa Ndege wa KIA wakimshangilia Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa wakati walipomsimamisha ili aweze kuwasalimia leo Juni 24, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Sioi Sumary.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya madakrari wa kigeni wanaotoa huduma kwenye hospitali ya Kanisa na International Evangelical Church, lililopo katika Kijiji cha Sakila, Wilayani Arumeru jijini Arusha. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Eliud Isanja.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungua mkoni ikiwa ni ishara ya kuwasalimia waumini wa Kanisa na International Evangelical Church, waliomualika leo Juni 24, 2015 ili aweze kuzungumza nao pamoja na kufanyiwa ibada maalum ya kumuombea.
Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelical Church, Askofu Eliud Isanja akizungumza jambo wakati akimtambulisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa kwa waumini wa kanisa hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Waumini wa Kanisa la International Evangelical Church (hawapo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Mkewe, Mama Regina Lowassa kabla ya kufanyiwa Ibada maalum ya kumuombea Mh. Lowassa katika Kanisa la International Evangelical Church, lililopo katika Kijiji cha Sakila, Wilayani Arumeru jijini Arusha.
Sehemu ya Maaskofu wa Kanisa la International Evangelical Church, wakimuombea Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa, leo Juni 24, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelical Church, Askofu Eliud Isanja.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwa safarini kuelekea Jijini Arusha, mara msafara wake ukasimamishwa na WanaCCM wa Mji wa Maji ya Chai Wilayani Arumeru waliotaka kumsalimia.
Dereva wa Daladala uzalendo ukamsinda kwenye usukani na kuamua kukaa Dirishani ili aweze kumuona Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa alishuka kwenye gani na kuungana na WanaCCM hao.
Msafara wa Mh. Lowassa ulizuiwa tena eneo la Tengeru, Jijini Arusha baada ya WanaCCM wa Mji huo kufunga barabara ili waweze kuzungumza na kipenzi chao.
Mh. Lowassa akiwapungia mkono WanaCCM hao wa Mji wa Tengeru waliokuwa wamefurika kwa wingi barabarani.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mwenyekiti wa CCM jijini Arusha, Ndg.Onesmo Ole Nangole pamoja na WanaCCM wengine, wakati wakielekea kwenye Uwanja wa Msikiti Mkubwa, kulikoandaliwa shughuli nzima ya kukabidhiwa fomu za kumdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya WanaCCM 120, 335 wa jiji la Arusha wamemdhamini Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Jiji la Arusha waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Msikiti Mkubwa uliopo mbele ya Ofisi za CCM Mkoa wa Arusha, leo Juni 24, 2015. Jumla ya WanaCCM 120, 335 wa jiji la Arusha wamemdhamini Mh. Lowassa.
Baadhi ya Wazee wa Kabila la Kimasai wakimbariki Mh. Lowassa katika Safari yake ya Matumaini.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM wa Mkoa wa Arusha waliomdhamini ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Ferouz Bano, ambapo WanaCCM wapatao 120, 335 wamemdhamini Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akikabidhi sehemu ya fomu hizo kwa Mkewe Mama Regina Lowassa. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM jijini Arusha, Ndg.Onesmo Ole Nangole.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia WanaCCM wa Mkoa wa Arusha waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Msikiti Mkubwa uliopo mbele ya Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha, leo Juni 24, 2015.
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Mh. Goodluck Ole Mideye akiwasalimia wanaCCM wa Mkoa wa Arusha.
Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Namelock Sokoine akiwasalimia WanaCCM wa Arusha.
Umati wa Watu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Hamis Mngeja akisalimia.
Sehemu ya WanaCCM wa Mkoa wa Arusha wakionekana ni wenye Furaha na Imani Kubwa na Mh. Lowasaa.
Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Arumeru, Mathias Manga akisalimia.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisikiliza jambo kutoka kwa Mkewe, Mama Regina Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM jijini Arusha, Ndg.Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia kuzungumza na WanaCCM wa Mji wa Arusha.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimpa pole Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM, Mathias Manga, aliyejeruhiwa kwa risasi jana usiku na watu wasiofahamika, wakati alipomwita jukwaani kuwasalimia WanaCCM wa Arusha.

TANGAZO LA MSIBA TANZANIA NA MAREKANI

$
0
0
11261405_1439531623036433_198071232238341808_o
DR. ALI MZIGE wa Mikocheni, Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha Dada yake MRS MARIAMU -MWAJUMA MUSISA (NEE MZIGE) kilichotokea Raleigh, North Carolina Marekani tarehe 21-06-2015. Mwili wa marehemu utaletwa Tanzania kwa ajili ya mazishi.

Tutatoa taarifa zaidi mwili utakapowasili. Kwa mawasiliano tafadhali mpigie Yussuf Mhiro 0754-609-338 / 0714-979-014.Usoma taarifa hii tafadhali wajulishe ndugu jamaa na marafiki wa Ukoo wa Humbi Ziota na Musisa. Au Kaka wa Marehemu DR. ALI A. MZIGE 0713 410 531, 0754 495 998.
Inna Lillahi, wa inna ilaihi ra'ajiun.

JENNIFER MGENDI KUZINDUA VIDEO YAKE YA WEMA NI AKIBA


WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MUUNGANO SAMIA SULUHU HASSAN ATOA WITO WA KUTUNZA MALI ASILI NA MAZINGIRA

$
0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa wito wa kutunza mali asili na mazingira kwa sababu ni urithi kwa vizazi vijavyo. Aliongea hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa  idadi ya watu duniani inazidi kuongezeka hivyo basi ni jukumu la kila mmoja kuacha kukata miti hovyo, kuacha kuchoma misitu na vitu vyote vinavyosababisha uharibifu wa mazingira kwa sababu upo uhusiano wa karibu sana kati ya umaskini na uharibifu wa mazingira.

 'Uharibifu wa mazingira huongoza kusababisha umaskini' alisema Bi Samia.
Aidha alisisitiza kuwa matokeo yataonekana iwapo  maazimio yaliyopendekezwa katika Azimio la Gaborone yatatiliwa maanani. 

Mkutano huo wa  Wadau wa Azimio la Gaborone umeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Serikali ya Botswana. Wadau mbalimbali wa mambo ya mazingira kutoka Wizara na Taasisi za Serikali wamehudhuria Mkutano huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone juu ya utunzaji Mazingira jijini Dar es Salaam.
 Mtoa mada katika Mkutano huo Bwana Carlos Manuel Rodriguez akiwasilisha mada katika mkutano huo.
 Sehemu ya Wadau wa Mkuatano huo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano huo.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wadau waliohudhuria Mkutano huo.

News alert: bei mpya za usajili makampuni na majina ya biashara Brela kuanzia Tarehe 1 Julai.

WAZIRI BERNARD MEMBE AKUTANA NA WASANII WA FILAMU MKOA WA MOROGORO

$
0
0
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wasanii wa tasnia ya filamu mkoa wa Morogoro jana, wakati alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini. Picha zote na John Badi
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa tasnia ya filamu mkoa wa Morogoro jana, wakati alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini.

TPB YAZINDUA HUDUMA MAALUMU YA AKAUNTI KWA VIKUNDI VISIVYO RASMI

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEC), Beng’I Issa, (kushoto), akikata utepe kuzindua huduma maalum ya akaunti ya vikundi visivyo rasmi, jana.

KATIKA  jitihada za kuwafikia Watanzania mbalimbali Benki ya Posta Tanzania (TPB) imezindua akaunti maalum kwa ajili ya Vikundi Visivyo Rasmi. Uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mtendaji  wa Shirika la Uwezeshaji Tanzania, Beng’I Issa katika viwanja vya Shule ya Msingi Osterbay, Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema, sasa makundi mbalimbali yasiyo rasmi yanaweza kufungua akaunti na Benki ya Posta na kuweza kupatiwa mikopo ya riba nafuu ya kuwawezesha katisha shughuli zao za ujasiriamali. 
‘Tunaposema akaunti za vikundi visivyo rasmi, ni vikundi kama vile jogging, vilabu mbalimbali vya michezo, wasuka nywele, wasuka mikeka n.k., aliongeza Moshingi.

Makundi mengi yamejitokeza katika kufungua akaunti hizi za vikundi visivyo rasmi, na hadi sasa akaunti takribani 340 zimefungulia kwa makundi yasiyo rasmi, alisema Moshingi. Kwa wiki benki inafungua akaunti zaidi ya 16 kwa makundi haya, na tunapenda kuwahamasisha makundi haya yajitokeze kwa wingi, ili waweze kunufaika na akaunti hii, alisema Moshingi.

Kwa upande wake Beng’i Issa, alitoa pongezi kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kubuni akaunti hiyo maalum kwa makundi hayo. ‘Makundi mengi yanatamani sana, kupata huduma za kibenki kwa ajili ya shughuli zao za kila siku, ila kutokana na uwezo sababu zilizo nje ya uwezo wao wanashindwa kupata huduma hizo’, alisema Issa. Sasa makundi haya yajitokeze kwa wingi katika kufungua akaunti hii Benki ya Posta iliwaweze kupata huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo, mikopo n.k aliongeza Issa.

Benki ya Posta Tanzania ni miongoni mwa mabenki yanayokuwa kwa kasi nchini, ikifuata sera ya financial inclusion, yaani kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za kifedha hapa nchini. 
 
Benki hii hivi sasa ipo katika mchakato wa kubadilisha sharia iliyoanzisha Benki ya Posta Tanzania, Sura ya 301, ili kukidhi matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha na kanuni zake (The Banking and Financial Institution Act, 2006 and its Regulations), ambayo imeweka masharti kwa benki zote nchini kusajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni, sura 212. Mchakato huu wa kubadilisha sharia hiyo uko Bungeni hivi sasa na uko katika hatua nzuri, na unalenga kuiwezesha Benki ya Posta Tanzania kukidhi matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha na Kanuni zake. 
 
Akizungumza mchakato huu, Moshingi alisema mara baada ya kukamilika kwake, benki yake itaweza kujiimarisha zaidi na kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake, katika wigo mpana zaidi.
 Wajasiriamali, wakiwa wamekamata kadi ya ATM ya benki ya Posta, baada ya benki hiyo kuzindua, huduma ya akaunti maalum kwa vikundi visivyo rasmi, jijini Dar es Salaam

 Katibu Mtendaji wa NEC, akizungumza wakayi wa uzinduzi huo
Maafisa wa juu wa benki hiyo, wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo

UTUMISHI YAWAAGA WATAALAMU 12 WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA HAPA NCHINI

$
0
0
 Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw.Koji Ueda akielezea namna alivyofanya kazi katika shule ya Sekondari Sogesca iliyoko mkoani Mwanza,katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.
 Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi. Haruka Ota akielezea namna alivyofanya kazi katika Maktaba Kuu ya Taifa,wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo. 
 Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw.HAB Mkwizu katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi.Sekiko Masui aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw.HAB Mkwizu ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla ya kuwaaga iliyofanyika ofisini kwake leo. Wengine ni watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images