Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AMALIZA ZIARA YAKE JIMBO LA MISUNGWI,KESHO KUVAMIA JIMBO LA KWIMBA MKOANI MWANZA

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa pili kushoto), akishiriki kupalilia katika shamba la dengu la mwanakijiji cha Manawa, Kata ya Misasi, Luhoyo Mwilima (Wa tano kulia), akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, leo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana,Leo aliendelea na ziara yake katika jimbo la Misungwi linaloongozwa na Mh. Charles Kitwanga ambaye pia ni naibu Waziri wa Nishati na Madini akitembelea maeneo mbalimbali na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015, inayotekelezwa na serikali ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ili kuzipatia ufumbuzi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikatiza katika kijiji cha Mahando,mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya CCM tawi la Kijiji cha Mahando, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza leo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimueleza jambo Mbunge wa Jimbo la Misungwi Dkt.Charles Kitwanga,walipokwenda kuwasalimia Mama Lishe na kuzisikiliza changamoto zao na namna ya kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine.


Wananchi wa kijiji cha Nyang'homango wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipowahutubia katika kijiji hicho ,wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezo Nape Nnauye akiwahutubia na kuwasalimia wakazi wa kijiji cha Nyang'homango waliokusanyika kwa wingi ,ikiwemo pia kumsilikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana
Mbunge wa jimbo la Misungwi Dkt.Charles Kitwanga akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Nyang'homango.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akisindikizwa kwa ngoma ya Sungusungu, alipokuwa akienda kuzindua Ofisi ya CCM na kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Mahando, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na Uhai wa Chama katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza leo. 
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Misungwi,Mh.Charles Kitwanga pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Mkoa Ndugu Miraji Mtaturu wakiwapungia mkono na kukaribishwa na wananchi, alipokuwa akienda kuzindua Ofisi ya CCM na kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Mahando, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na Uhai wa Chama katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kijiji cha Mahando, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza leo. Baadaye Kinana aliwataka, kuitumia ofisi hiyo kama kitegauchumi.
Mmoja wa Kiongozi cha Mama Lishe,tawi la Misungwi,Mama Easther Daudi akisoma risala yao fupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana ambaye alikuwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mbunge wa Jimbo la Misungwi Dkt.Charles Kitwanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana,Leo aliendelea na ziara yake katika jimbo la Misungwi linaloongozwa na Mh. Charles Kitwanga ambaye pia ni naibu Waziri wa Nishati na Madini akitembelea maeneo mbalimbali na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015, inayotekelezwa na serikali ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ili kuzipatia ufumbuzi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Misungwi Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi amesema Chama cha Mapinduzi CCM kinaishauri Serikali kuutoa na kuurudisha kwa wadau  muswaada wa sheria ya habari ambao umepelekwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa kwa, kuwa wadau wanaulalamikia na wanataka kushirikishwa kuujadili ndipo uende bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa kama sheria uli iweze kusainia na Rais.

Ameongeza kuwa “Sheria zinazotungwa ni kwa ajili ya wananchi hivyo Chama cha Mapinduzi kinaishauri serikali kuwa,  kama wadau wanaulalamikia muswaada huo,ni vyema ukarudhishwa kwa wadau ili ujadiliwe upya kwa pamoja,Serikali na wadau ndipo upelekwe  Bungeni  ukajadiliwe na kupitishwa kama sheria”

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Wilaya ikiwemo pia  kupokea taarifa ya chama na serikali.

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AWATUNUKU NISHANI WATUMISHI WA UMMA WALIOLILETEA SIFA TAIFA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Nishani ya Jamhuri ya Muungano Daraja la Kwanza kwa kuwa mwaminifu na kujitolea moja kwa moja kulipatia Taifa sifa kubwa katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiulinzi na kijamii wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
N2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Liberata Rutegaruka Mulamula Nishani ya Jamhuri ya Muungano Daraja la Kwanza kwa kuwa mwaminifu na kujitolea moja kwa moja kulipatia Taifa sifa kubwa katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiulinzi na kijamii wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
N3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Martin Turuka Nishani ya Utumishi mrefu na Maadili mema Daraja la kwanza kwa kuwa mtumishi wa umma kuanzia ngazi ya ukurugenzi na kutumikia Taifa si chini ya ishirini mfululizo na kuonyesha maadili mema wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.

N4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha akimvisha Balozi wa Tanzania nchini Burundi Rajabu Hassan Gamaha Nishani ya Utumishi mrefu na Maadili mema Daraja la kwanza kwa kuwa mtumishi wa umma kuanzia ngazi ya ukurugenzi na kutumikia Taifa si chini ya ishirini mfululizo na kuonyesha maadili mema, wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
N5Mwalimu Rosalia Marmo Massay akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete baada ya kuvishwa nishani ya Utumishi mrefu na maadili mema Daraja la Pili kwa kufanya kazi bora na maadili mema yanayostahili kuigwa na wengine kwa muda usiopungua miaka ishirini wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
N6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha CPL Liberatus Tibaitirwa Ndyetabula nishani ya Ushupavu inayotolewa kwa majeshi ya ulinzi na Usalama na watu wengine kwa vitendo vya ushupavu, wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
N7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi waliovishwa nishani mbalimbali leo Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Jaji MkuuMohamed Chande Othman na kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
N8
N9Mtoto huyo akimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete picha aliyoipiga.
N10Mtoto wa Mmoja ya viongozi waliovishwa nishani akipiga picha ya pamoja iliyomjumuisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi waliovishwa nishani
………………………………………………………………………..
Na Hassan Silayo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewavisha nishani mbalimbali watumishi wa Serikali kwa kutambua mchango wao kitaifa. 
Rais Kikwete amefanya hivyo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya sheria ya mamlaka ya Rais (sura ya 9) kamailivyorekebishwa mwaka 2002 fungu la 4 kama ilivyotangazwa katika tangazo la serikali namba 227.

Nishani zilizotunukiwa leo ni Nishani ya Jamhuri ya muungano Daraja la Kwanza, Nishani ya Utumishi mrefu na Maadili mema Daraja la kwanza, Nishani ya utumishi mrefu na Maadili mema Daraja la pili na Nishani ya Ushupavu. 
Nishani hizo zinatunukiwa kwa watumishi ambao sifa zao zimekidhi mmatakwa ya nishani husika 

Boss Mkuu wa Usalama wa Taifa Rwanda Emanuel Karenzi Karake Akamatwa London

0
0

London,Uingereza,

Mkuu wa usalama wa taifa wa nchi ya Rwanda Major Gen.Emanuel Karenzi Karake amekamatwa na wanausalama katika uwanja wa ndege wa Heathrow nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita,kwa kutuhuma za mauaji ya kivita mwaka 1994 na baada ya mwaka huo pia.

Major Gen.Karenzi Karake aliwekwa kizuwizini na baadaye  kufikishwa katika mahakama ya Westminister,amri ya kukamatwa kwa mkuu huyo wa idara ya ujasusi (NISS) ya Rwanda kunatokana na ombi la mahakama ya nchi ya Spain ambayo imeorodhesha watu wapatao 40 kuhusika na makosa ya kivita nchini Rwanda ,mashataka yalifunguliwa 2008 kufuatia uchunguzi uliofanywa na kikosi cha mahaka ya spain kinachoongozwa na Andreu Melles .

Mkurugenzi mkuu huyo wa usalama wa taifa wa Rwanda Bw.Karenzi Karake mwenye umri wa miaka 54 bado yupo kiziwizini na anatagemea kupandishwa Kizimbani tena siku ya Alhamisi.

TRA YAKUTANA NA BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA KUIJADILI SHERIA MPYA YA KODI

0
0
Afisa Mwandamizi Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akiwasilisha Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 kwa viongozi wa Baraza la Maaskofu Tanzania na kuwaeleza jinsi ilivyoziongelea jinsi ilivyozieleza Taasisi za Dini hasa katika masuala ya ulipaji kodi, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
3
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakimsikiliza Bi. Rose Mahendeka alipokuwa anawasilisha Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
45
Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo la Tabora akichangia kwenye moja ya maeneo ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
6
Father Longino Rutagwelera wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino tawi la Mtwara akichangia kwenye moja ya maeneo ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
7
 Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Fr. Raymond Saba akiongea na wajumbe wa Baraza hilo waliohudhuria mkutano huo uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
9
Afisa Mwandamizi Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akiwaeleza jambo wajumbe wa baraza la Maaskofu Tanzania wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Na Hassan Silayo-MAELEZO.

NAPE AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUSHIRIKISHWA WADAU WA HABARI KABLA YA SHERIA KUPITISHWA NA BUNGE

0
0

Niambie Live Show EP7

0
0
 Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii.
Na mgeni mwalikwa ni Dotto Malongo
Ni Niambie Live....
KARIBU

WANAHABARI WASHINDANA KUTAMBUA LADHA ZA BIA ZA TBL DAR

0
0
 Mpishi Mkuu / Brew Master Kiwanda cha Bia cha TBL, Dar es Salaam, Bw. Benjamin Budigila (kulia), akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo baada ya semina ya siku moja kuhusu matumizi ya pombe kupita kiasi.
 Mpishi Mkuu / Brew Master Kiwanda cha Bia cha TBL, Dar es Salaam, Benjamin Budigila akiwaonyesha waandishi wa habari jinsi wanavyotumia mtandao wa Komputa kuhakiki viwango katika suala zima la uzalishaji wa vinywaji wa kampuni hiyo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mush, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shindano maalumu la kutambua harufu na radha ya aina ya Bia zinazotengenezwa na TBL.

 Matokeo yakitangazwa
 Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza kwa makini, Mpishi Mkuu / Brew Master Kiwanda cha Bia cha TBL, Dar es Salaam, Benjamin Budigila
 Meneja uzalishaji wa TBL, Bw. Charles Nkondola akikabidhi zawadi ya bia aina ya Kilimanjaro Twist kwa mshindi wa tatu wa kutambua aina ya ladha ya Bia za  Kampuni ya Bia Tanzania (TB)L, Aloyce Ndeileko wa This Day, iliyofantika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
 Wanahabari wakisikiliza kwa makini masharti ya ushindi ya muomnjaji bora wa ladha za bia za TBL

 Mhariri wa Business Times, Mnaku Mbani akiangalia glasi zenye aina mbalimbali ya Bia, wakati wa shidano la kutambua aina ya bia.

 Meneja wa Maabara ya Kampuni ya Bia Tanzania Tanzania, Bi. Conchesta Ngaiza (kulia), akizungumza na waandishi wa habari walipofika kwenye maabara ya kiwanda hicho, baada ya semina ya siku moja kuhusu matumizi ya pombe kupita kiasi.

Afisa Uhusiano wa TBL, Editha Mush akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki semina ya siku moja, Waandishi hao pia walitembelea mitambo mbalimbali ya kiwanda cha uzalisha bia cha TBL.
 Mpigapicha wa Uhuru, Christopher Lissa akiwa tayari kwa mashindano ya kutambua aina ya Bia za TBL.
Meneja Usalama na Afya wa kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Bw. Renatus Nyanda akiwaelekeza waandishi wa habari kuvaa vifaa maalumu vya usalama kwa ajili ya kufanya matembezi kuangalia kazi mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo.

news alert: Mbunge wa Geita (CCM) Mhe. Donald Kevin Max afariki dunia

0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Geita (CCM) Mheshimiwa Donald Kevin Max (58)(picha) amefariki dunia. 

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) kwa Waheshimiwa Wabunge wote pamoja na umma kwa ujumla,  Mhe. Max amefariki dunia tarehe 23 Juni, 2015 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. 

Kwa mujibu wa taarifa hii, taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia kadri zitakavyopatikana ikiwa ni pamoja na ratiba ya Mazishi. 
“BWANA ametoa, BWANA ametwaa, 
Jina la BWANA  lihimidiwe.” Amina.


Imetolewa na:

Ofisi ya Bunge,

Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na

Uhusiano wa Kimataifa,


DODOMA


Bayport Financial Services yamfuta machozi Latifa Said

0
0
Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, kushoto akimkabidhi hundi Latifa Juma yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake Juma Said, aliyekuwa Mchapa Vitabu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar es Salaam. Kulia ni mume wa Latifa, anayeitwa Bakari Msumi. Picha zote kwa Hisani ya Bayport Financial Services.

Bayport Financial Services yamfuta machozi Latifa Said


TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, leo jioni imemkabidhi hundi ya Sh Milioni tatu (3,000,000), mjasiriamali Latifa Juma, ikiwa ni sehemu ya mafao yake baada ya mzazi wake Said Juma, kuwa mteja wa Bayport kwa kupitia huduma yake ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao iliyoanzishwa mapema mwaka jana.

Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya Bayport Financial Services, Morocco, jijini Dar es Salaam, huku akisindikizwa na mumewe Bakari Msumi. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema kwamba marehemu Said Juma alikuwa mteja wao, huku akijiunga pia katika huduma ya bima, ambayo leo imemnufaisha mtoto wake.

Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, kushoto, akiwa kwenye makabidhiano ya hundi Latifa Juma yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake Juma Said, aliyekuwa Mchapa Vitabu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar es Salaam. Kulia ni mume wa Latifa, anayeitwa Bakari Msumi. Picha zote kwa Hisani ya Bayport Financial Services.


Alisema mapema mwaka huu mteja wao alifariki Dunia, hivyo baada ya kupata taarifa hizo tuliamua kufuatilia na kukutana na mtoto wake Ratifa, ambaye hapana shaka fao hili linaweza kumuendeleza zaidi na zaidi. “Bayport Financial Services kama kawaida yetu tumekuwa na lengo la kuwakomboa wateja wetu kwa kuwapatia mikopo mbalimbali kama vile mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa ikiwamo huduma yetu mpya ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, bila kusahau fao la Bima ya Elimu ambalo lina umuhimu mkubwa.

“Naomba Watanzania wote waweke utaratibu wa kujiunga na bima hii ambayo malipo ya kila mwezi kwa fao la Bronze ni Sh 3500 tu, huku mafao yake yakiwa ni Sh 1,800,000, huku Makato ya bima ya Silver yakiwa ni Sh 7,000 na fao lake ni Sh 3,700,000 na Gold akilipwa mteja Sh 7,500,000 wakati makato yake yakiwa ni Sh 12,000 tu kwa mwezi,” alisema Ruth.

Naye Ratifa aliwashukuru Bayport kwa huduma zao nzuri, huku akisema mafao ya baba yake yatachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha yake na mama yake, hususan kwa kuendeleza ujenzi wa nyumba yao.


“Ninachotaka kufanya ni kuendeleza ujenzi wa nyumba yetu ili mimi na mama yangu tuishi vizuri, baada ya kufiwa na baba yetu, ambaye leo tumepewa kiasi hicho cha pesa,” alisema.

Naye mume wa Ratifa, Bakari Msumi, alisema hajawahi kuona taasisi yenye huduma nzuri kama Bayport Financial Services, hasa baada ya kuhakikishiwa malipo ya mafao yam zee wao bila usumbufu wowote, jambo ambalo ni nadra kwa taasisi nyingi nchini.


“Awali hatujafahamu kama tunaweza kupata bila usumbufu, ajabu ni kuona sisi tunapigiwa simu hatua kwa hatua, kuelekezwa njia za kupita, hususan baada ya kuitwa katika makabidhiano ya hundi,” alisema Msumi na kuwapongeza Bayport, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia huduma zote zinazotolewa na Bayport.

Aidha, utaratibu wa malipo ya huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao umepangwa kulipwa kila mwaka, ili kuhakikisha kuwa mafao hayo yananufaisha walengwa, hususan kwa wale wanaoendelea na masomo katika shule na vyuo mbalimbali nchini.

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2015 CHAFANA

0
0
Tuzo zilizokabidhiwa Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma jana tarehe 23 Juni, 2015.
 Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi  (wa pili kutoka kushoto) akitembelea mabanda katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana. Anayemuongoza ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (watatu kutoka kushoto).
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akihutubia wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.
 Moja kati ya washindi wa tuzo za Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 wakifurahia tuzo waliyoipata wakati wa kilele za Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Watumishi wa Umma na wananchi waliohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakimsikiliza mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi (hayupo pichani) jana.
 Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi akizungumza na watumishi wa Umma na wananchi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akimkabidhi tuzo mmoja wa wawakilishi wa taasisi zilizopata tuzo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.

KAMATI ZA MAAFA ZA TAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO WA MENEJIMENTI YA MAAFA

0
0

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Kagera, Fikira Kisimba (katikati)
akifuatilia mafunzo ya menejimenti ya maafa wakati wa mafunzo kwa
waratibu maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015, (mwenye miwani) ni
Mkurugenzi msaidizi (Mipango na Utafiti), Idara ya Uratibu maafa Ofisi
ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho.
Mwakilishi wa  Mkuu wa Polisi wilaya ya Bukoba, Mkaguzi John Kayunga
akifafanua masuala ya menejimenti ya maafa katika Jeshi la Polisi
mkoani Kagera wakati wa  mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa waratibu
maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015.
Mratibu maafa wilayani Muleba Mkoani Kagera, Ruth Ishabakaki
akifafanua masuala ya menejimenti ya maafa wilayani Muleba wakati wa
mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa waratibu maafa mkoani Kagera
tarehe 24 Juni, 2015, mafunzo hayo yameratibiwa na Idara ya Uratibu
maafa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Baadhi ya waratibu Maafa mkoani Kagera wakifuatilia mafunzo ya
menejimenti ya maafa kwa waratibu hao tarehe 24 Juni, 2015, mafunzo
hayo yameratibiwa na Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
Mratibu Maafa, Idara ya uratibu maafa,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Benedict
Kisaka akitoa mafunzo ya menejimenti ya maafa wakati wa mafunzo kwa
waratibu maafa mkoani Kagera tarehe 24 Juni, 2015.


Na. Mwandishi Maalum 
Kamati za kuratibu maafa katika ngazi ya serikali za mitaa zimetakiwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ya menejimenti ya maafa ili kuweza kujenga jamii yenye uwezo wa kuzuia na kukabili maafa yanayotokea katika maeneo yao.
 
Akifungua mafunzo ya waratibu wa maafa mkoani Kagera, tarehe 24 Juni, 2015,  Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo, Fikira Kisimbaalieleza kuwa nguvu ya uwezo wa jamii kuweza kukabili maafa itapatikana iwapo kamati za kuratibu maafa katika ngazi za serikali za mitaa zitawajibika wakati wote kwa kutokuwa zinasubiri uratibu wa  maafa yanapotokea . 

“Tunazo kamati za maafa kuanzia ngazi za vijiji , vitongoji, kata , wilayani hadi mkoani lakini kamati hizi zinasikika sana wakati maafa yanapotokea hali ambayo si nzuri katika hatua za menejimenti ya maafa, kwani tunaposema menejimenti ya maafa tunazingatia, kuzuia, kukabili  maafa na kurejesha hali ya awali baada ya maafa kutokea” alisema Kisimba.

Kisimba aliongeza kuwa mkoa wa Kagera umekuwa ukikumbwa na maafa ya upepo mkali ambapo alibainisha kuwa wilaya ya Muleba imewahi kupatwa na maafa hayo pamoja na maafa ya Kimbunga katika kisiwa cha Goziba lakini wilayani Misenyi magonjwa ya mlipuko yamekuwa yakijitokeza hivyo kamati husika zikiwajibika athari za maafa haya zinapunguzika.

Awali akiongea katika mafunzo hayo, Mkurugenzi msaidizi (Mipango na Utafiti), Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho alizitaka kamati za  serikali za  mitaa  na vijiji mkoani humo kuhusisha maafa na mipango yao ya maendeleo, ili kuhakikisha jamii inakuwa na uwezo wa kupunguza athari za maafa hayo.

“Ili kamati za maafa ziweze kuwajibika ipasavyo hatunabudi Mipango ya maendeleo katika serikali za mitaa ihusishe maafa ili jamii iwe na uwezo wa kukabiliana na maafa wakati janga linapotokea na wakati wa kurejesha hali. Kamati za ”  alisisitiza Mrisho.

Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Idara ya Uratibu Maafa itaendelea kutoa elimu na kushirikisha Wadau ili kuimarisha uwezo wa nchi katika kujenga uwezo wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na athari za maafa yanapotokea.

MAHAKAMA YA TANZANIAYAENDELEA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA HAKI

0
0
 Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania (wa kwanza kushoto), Bw. Waleed Malik, Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia (wa pili kushoto), Bi. Neema Ndunguru, Mkurugenzi wa Mazingira ya Biashara (PDB) pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Dunia wakiwa meza kuu wakati wa Kikao cha majadiliano katika ya Mahakama na Wadau wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kupata maoni juu ya maboresho ya huduma za Mahakama. (IMG. 7436)
 Mmoja wa wadau walioshiriki katika warsha hiyo akitoa maoni yake katika majadiliano hayo. (IMG. 7449)
 Washiriki wakiwa katika kazi za makundi wakitoa maoni juu ya Mpango Mkakati wa Mahakama wenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma zake.  (IMG. 7465) (Picha na Mary Gwera, Mahakama).

Na Mary Gwera

KATIKA mwendelezo wa maboresho ya utoaji wa huduma ya haki nchini, Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukutana na wadau pamoja na Washirika mbalimbali wa maendeleo ili kupata maoni yao juu ya uboreshaji wa huduma zake.

Akiongea na Waandishi wa Habari mapema jana, katika Warsha iliyoandaliwa na  Mahakama ikishirikisha Ugeni kutoka Benki ya Dunia na Wawakilishi kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka, TRA, Umoja wa Taasisi za Kifedha,MOAT, TIRA, TCRA n.k iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam, Bw. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania alisema Mahakama imekuwa katika mchakato wa maboresho na washirika mbalimbali wa Maendeleo na wadau wa utoaji haki ili kuboresha huduma zake.
“Mikakati hiyo ya maboresho ni sehemu ya mpango wa miaka mitano (5) ya maboresho ya Mahakama ambapo unaenda sambasamba na maboresho ya miundombinu ya majengo ya Mahakama, matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nk” Alisema Kattanga
Mtendaji alisema maoni yanayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali wa Mahakama utasaidia kubadili mtazamo mbaya wa wananchi walionayo kuhusiana na Mahakama na hivyo kusaidia kujitathmini na kubadili mfumo wake wa utoaji wa huduma. 
Aliongeza kuwa maboresho hayo yataenda sambasamba na kubadili mfumo wa ushughulikiaji wa malalamiko kuhusiana na mashauri mbalimbali na kurahisisha taratibu mbalimbali za kisheria zitakazowezesha wananchi kupata urahisi katika ufunguaji wa mashauri.
Kwa upande wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu-Ethiopia, Mhe. Dkt. Menbere Tseha Tadesse, ambaye ni miongoni wa Wawakilishi kutoka Benki ya Dunia (World Bank), alisema kasi ya jitihada mbalimbali zilizowekwa na Mahakama ya Tanzania katika kuboresha huduma zake inatia moyo.
Alisema ufanisi wa Mpango Mkakati wa Mahakama utategemea maoni ya wadau mbalimbali wa Mahakama ili kupata njia bora za kuboresha huduma zake kwa wananchi.
Naye, Bw. Henry Mwanyika, Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), alisema amefurahishwa na uamuzi uliofanywa na Mahakama wa kujitathmini utendaji wake ambao umekuwa shirikishi, akiongeza kuwa uamuzi huu utawezesha Mahakama kupata maoni ya wadau ya nini kifanyike katika kuboresha huduma zake kwa wananchi.
“Kwa kweli nimefurahishwa sana na uamuzi wa Mahakama wa kutushirikisha sisi wadau katika mpango wake wa maboresho na tunahaidi kushirikiana nao bega kwa bega katika jitihada hizo,” alieleza.

WANAHABARI WASHINDANA KUTAMBUA LADHA ZA BIA ZA TBL, DAR

0
0
 Afisa wa TBL, Bw. Benjamin Budigila (kulia), akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo baada ya semina ya siku moja kuhusu matumizi ya pombe kupita kiasi.
 Afisa wa TBL, Bw. Benjamin Budigila akiwaonyesha waandishi wa habari jinsi wanavyotumia mtandao wa Komputa kuhakiki viwango katika suala zima la uzalishaji wa vinywaji wa kampuni hiyo.
 Meneja uzalishaji wa TBL, Bw. Charles Nkondola akikabidhi zawadi ya bia aina ya Kilimanjaro Twist kwa mshindi wa tatu wa kutambua aina ya ladha ya Bia za  Kampuni ya Bia Tanzania (TB)L, Aloyce Ndeileko wa This Day, iliyofantika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

 Wanahabari wakisikiliza kwa makini masharti ya ushindi ya muomnjaji bora wa ladha za bia za TBL
 Matokeo yakitangazwa
 Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza kwa makini, Afisa wa TBL, Bw. Benjamin Budigil
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mush, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shindano maalumu la kutambua harufu na radha ya aina ya Bia zinazotengenezwa na TBL.
 Mhariri wa Business Times, Mnaku Mbani akiangalia glasi zenye aina mbalimbali ya Bia, wakati wa shidano la kutambua aina ya bia.
 Msimamizi wa Maabara ya Kampuni ya Bia Tanzania Tanzania, Bi. Conchesta Ngaiza (kulia), akizungumza na waandishi wa habari walipofika kwenye maabara ya kiwanda hicho, baada ya semina ya siku moja kuhusu matumizi ya pombe kupita kiasi.

Afisa Uhusiano wa TBL, Editha Mush akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki semina ya siku moja, Waandishi hao pia walitembelea mitambo mbalimbali ya kiwanda cha uzalisha bia cha TBL.
 Mpigapicha wa Uhuru, Christopher Lissa akiwa tayari kwa mashindano ya kutambua aina ya Bia za TBL.
Afisa Usalama na Afya wa kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Bw. Renatus Nyanda akiwaelekeza waandishi wa habari kuvaa vifaa maalumu vya usalama kwa ajili ya kufanya matembezi kuangalia kazi mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo.

DENMARK YAIMARISHA SEKTA YA UTAMADUNI NA UBUNIFU TANZANIA

0
0
PROGRAMU mpya za utamaduni na ubunifu zinatoa fursa kubwa ya uanzishaji  wa shughuli za kitamaduni zenye kuimarisha sekta ya ubunifu wenye mwelekeo kiuchumi.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania,Bw. Johnny Flentoe akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa program mpya ya CKU.
 
Kwa mujibu wa balozi wa Denmark nchini Tanzania,Bw. Johnny Flentoe, amesema kwamba Tanzania inautajiri mkubwa wa kiutamaduni ambao unaweza kutumiwa kuchangia pato la taifa GDP.

 “Bado tasnia ya sanaa na ubunifu ambayo ingeliweza kuchangia katika uchumi na kuwapatia kazi vijana haijatumika ipasavyo. Kutokana na hilo kipaumbele cha programu hii mpya ni kuwezesha vijana kutumia sanaa na ubunifu kukuza ajira,” anasema balozi Johnny Flentoe.
Mshairi Jasper Sabuni akifanya kazi ya 'spoken words' wakati wa uzinduzi wa program mpya ya CKU.

Juni 5, 2015, Ubalozi wa Denmark ukishirikiana na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU) umezindua program mpya ya utamaduni na  maendeleo Tanzania ( Tanzania Culture and Development Programme ).

Programu hiyo imelenga kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo watanzania watajipambanua kupitia kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni na kujipatia kipato.
Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi wa program mpya ya CKU Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
CKU inatekeleza program hiyo kupitia kwa washirika wake likwemo Tamasha la Kimataifa la Filamu (Zanzibar International Film Festival (ZIFF), kupitia mradi wao wa Village Panorama ambao unalenga kuonyesha filamu za kuelimisha maeneo ya vijijini huko Zanzibar.

Taasisi nyingine ni Culture and Development in East Africa (CDEA), ambao watafanya utafiti wa namba sanaa ya muziki na filamu inavyochangia katika pato la taifa, wakati taasisi ya Soma Book Café ikiindesha mashindano ya uandishi na usomaji wa vitabu.

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wao watanufaika na program hiyo kwa kupatiwa vifaa vya muziki vya kufundishia huku Nafasi Art Space ambacho ni kituo cha sanaa kikiboreshwa na kupata uwezo wa kutumika kama kituo kikubwa cha sanaa za maonesho.  
Meneja wa CKU Afrika Mashariki, Christoph Lodemann akitoa maelezo mafupi juu ya program mpya ya Tanzania

“Sanaa ina uwezo mkubwa wa kuwezesha majadiliano na kupaza sauti ya umma. Ndio maana Denmark inawezesha kuwapo kwa jukwaa ili wananchi waweze kujieleza wenyewe kupitia sanaa. Kwa kukuza vipaji vya wasanii wapya nchini Tanzania, Denmark inatoa mchango wake mkubwa kwa wasanii na wabunifu,”  anasema meneja wa CKU Afrika Mashariki Christoph Lodemann.

Denmark inawezesha shughuli za sanaa,utamaduni  na ubunifu wa kisanii nchini Tanzania kama mchango wake katika juhudi za kukuza uchumi wa taifa hili.

MKWASA AITA 26 TAIFA STARS

0
0
Kocha Mkwasa (kushoto) na msaidizi wake Hemed Morocco wakiongea na waandishi wa habari.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 104
TAREHE 24 JUNI 2015

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemtambuisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari.

Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha hao wazawa wanaoanza kazi kesho kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala.

Mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, Mkwasa amesema anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi hiyo ya kuingoza Taifa Stars na msaidizi wake Hemed Morocco, na kuomba watanzania kuwapa sapoti.

Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.

Aidha Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.

Wachezaji walioitwa ni makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).

Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).

Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).

Viungo wa pembeni: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano “Messi” (Simba).

Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).

Wachezaji Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoingia kambini kesho.

Katika hatua nyingine Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd Mgoyi.

Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

NACTE YAVIFUTIA USAJILI VYUO VITATU (3) NA KUVISHUSHA HADHI VYUO KUMI NA SITA (16)

0
0
NACTE yavifutia usajili vyuo vitatu  (3) na kuvishusha hadhi vyuo  kumi na sita (16)
Dar es Salaam, 24 Juni 2015 Katika jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo  vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dkt. Adolf B. Rutayuga alisema kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya vyuo husika kushindwa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na NACTE.

“Kwa kutumia Sheria ya Bunge Sura Na. 129 na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujitetea na kufanya marekebisho yaliyobainishwa,” alieleza.

Kaimu Katibu Mtendaji huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Ushauri na Malezi ya Taasisi na Vyuo vya Ufundi NACTE aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi vilivyopewa maelekezo ya kufanya marekebisho vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yabainishwa. Hata hivyo alisema hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake.

 
“Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa kwa makosa yafuatayo, moja kumalizika kwa muda wa  Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); pili kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; tatu kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukuliwa hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na nne taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbali mbali,” alifafanua

Vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja na Dar es Salaam College of Clinical Medicine cha jijini Dar es Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali, Ndatele School of Medical Laboratory Sciences cha Dar-es-Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali na Institute for Information Technology  cha jijini  Dar es Salaam pia chenye namba za usajili REG/EOS/014

Taassi/vyuo vilivyoshushwa hadhi  baada ya kushindwa kutiza mashart ni pamoja na Sura Technologies – Dar es Salaam,  Institute of Management and Information Technology – Dar es Salaam, Techno Brain - Dar es Salaam, Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya, Mbozi School of Nursing – Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi, KCMC AMO Anaesthesia School – Moshi, Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi.

Vingine ni, AMO Training Centre Tanga – Tanga, CATC – Songea, CATC – Sumbawanga, COTC Maswa – Shinyanga, COTC – Musoma, Dental Therapists Training Centre – Tanga, Ngudu School of Environmental Health Sciences – Kwimba na KCMC AMO General School – Moshi.

Kuhusu NACTE
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)wakati wa kutangaza ubora wa elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo  vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mitaala wa baraza hilo Twilumba Mponzi na Msaidizi wa katibu Mtendaji Alex Nkondola.
 Wakurugenzi wa Manejimenti ya NACTE wakiwa kwenye mkutano pamoja na waandishi wa habari uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
 Mwandishi wa habari kutoka kituo cha EAT, Noah Laltaila akimuuliza swali Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga kwenye mkutano  uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo  vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
Baadhi ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE) uliohusu kutangaza ubora wa elimu unaotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo  vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.

MASHINDANO YA KILIMANJARO AMBASSADOR KUFANYIKA JULAI 24 MWAKA HUU

0
0
 Baadhi ya warembo watakawo wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika Julai 24 katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi wakiwakipewa maelekezezo na mwalimu  Omary Bokilo leo katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya warembo watakawo wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika Julai 24 katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi wakiwa katika picha ya pamoja leo katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.
 Katibu mtendaji wa Rick Plan co.Ltd, Sebu Panya akizungumza  kuhusiana na mashindano ya   wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika Julai 24 katika katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi leo
 katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Rick Plan co.Ltd, Jaquline Chuwa na Mkuu wa itifaki  wa Rick Plan co.Ltd, Angeris Faber.

Mkurugenzi wa Rick Plan co.Ltd, Jaquline Chuwa akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari leo  kuhusiana na mashindano ya   wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika Julai 24 katika katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshikushoto ni Mkuu wa itifaki  wa Rick Plan co.Ltd, Angeris Faber.  
PICHA NA EMMENUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA KAIMU MUFTI MKUU WA TANZANIA SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIRY IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila  Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza  Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu  na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila Ikulu jijini Dar es salaam leo.

VIJANA WAKIWA KATIKA KUSAKA MKATE WA KILA SIKU

0
0
Kutafuta liziki ni kwa kila mtu ila tofauti ni kwa namna gani jamaa kama alivyokutwa na kamera yetu leo katika eneo la Kinondoni B jijini dar es salaam.
Mjasiliamali akimuuzia mteja wake mara baada ya kuegesha gari lake pembeni kama alivyonaswa na kamera yetu leo katika eneo la kariakoo jijini Dar es Salaam leo. (PICHA NA EMMENUEL MASSAKA)

KIBAKA AIPATA JOTO YA JIWE LEO JIJINI DAR

0
0
 Askari wa kampuni ya G1 Security wakimrekebisha mtuhumiwa wa wizi ambaye jina lake halikufahamika mara moja,alinaswa akiwa katika harakati za kutaka kufanya uhalifu  katika Jengo la PAlM RESIDENCE jijini  Dar es salaam.
 Mtuhumiwa wa wizi ambaye alikusudia  kufanya uhalifu  katika Jengo la PAM RESIDENCE jijini Dar es Salaam akitolewa nje na Askari wa kaampuni ya G1 Security.
 Mtuhumiwa wa uharifu katika jengo la PAM RESIDENCE jijini Dar es Salaam.
 Askari wa kaampuni ya G1 Security wakuwa na mtuhumiwa  ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakiwa nje ya jengo  PAM RESIDENCE jijini Dar es Salaam.
Mtuhumiwa wa wizi  ambaye jina lake halikupatikana mara moja akihojiwa na Askari wa kaampuni ya G1 Security juu ya jiwe alilokuwa nalo kwenya mfuko  picha na EMMANUEL MASSAKA.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images