Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 49537 articles
Browse latest View live

ACACIA KUKUSANYA DOLA 200,000 KWA AJILI YA UFADHILI WA ELIMU KWA WATOTO MASKINI, NI KUPITIA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
 KAMPUNI ya ACACIA inayojishughulisha na uchimbaji na utafutaji madini, imezindua kampeni ya kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, leo Jumatatu Juni 22, 2015, ambapo fedha hizo zitakwenda kusaidia sekta ya elimu kwenye maeneo yanayozunguka migodi mitatu inayomilikiwa na kampouni hiyo ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwenye lango la Machame,iliyo shirikisha watu 21, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Brad Gordon, alisema, kampuni yake ilianzisha mpango ujulkikanao kama “CAN EDUCATE”, ikimaanisha tunaweza kujieleimisha, imeamua kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, ili kusaidia elimu na kampuni inimekuwa ikifanya hivyo kila mwaka.

“Lengo ni kukusanya dola za Kimarekani 200,000, zitakazosaidia jamii inayokaa kuzunguka maeneo ya migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo” alisema Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa Kmapuni, Asa Mwaipopo.
Na kuongeza kuwa kuna watoto wengi wanashindwa kendelea na elimu ya sekondari na ile ya chuo kikuu, sio kwa sababu za uwezo mdogo wa kimasomo, bali ni ukosefu wa fedha za kuendelea na elimu. 

Acacia imeamua kushiriki katika kuwasaidia watoto hawa ili watimize ndoto zao. Alimaliza Mwaipopo. Pichani, Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya ACACIA, Brad Gordon, (Wapili kushoto), akiongoza timu ya watu 21 wakiwemo wafanyakazi, marafiki na familia za wafanyakazi wa kampuni hiyo ,kupanda Mlima Kilimanjaro kwenye lango la Machame mkoani Kilimajaro Jumatatu Juni 22, 2015, kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini.(Habarin na K-VIS MEDIA, picha na Dixon Busagaga)
 Kundi la watu 21, wakiwemo, wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro Juni 22, 2015
 Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (katikati), akiwa na Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo, (kushoto), akizungumza muda mfupi kabla ya kuongoza timu ya wapanda mlima Kilimanjaro kwa nia ya kukjsuanya fedha hizo
Brad, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Necta Pendaeli Foya (katikati)

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA APOKELEWA KWA SHANGWE JIMBONI KWA NGELEJA LEO,AKAGUA MRADI MKUBWA WA MAJI

$
0
0
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifafanua jambo alipokuwa akihutubia umati wa watu waliofurika kumsikiliza  katika uwanja wa CCM Wilaya ya Sengerema ambapo aliwaambia wakazi hao Chama Cha Mapinduzi kitasimamia haki na misingi kwani ndio chama pekee kinachojali watu.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wapo kwenye ziara ya Kukagua na kuimarisha uhai wa chama,Kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,katika Mikoa ya Kagera,Geita na sasa mkoani Mwanza.
 Mbunge wa Jimbo la Sengerema Ndugu William Ngeleja akihutubia wakazi wa Sengerema mjini kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni rasmi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Sengerema mjini kwenye uwanja wa CCM wilaya ambapo aliwaambia moja ya sababu kubwa ya kuporomoka kwa vyama vya upinzani nchini ni kutotaka kubadili viongozi na kubaki na viongozi wale wale ambao tangia 1995 mpaka leo wameshindwa kuleta mabadiliko kwenye vyama vyao na kuendelea kushindwa kwenye chaguzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Nyamazugo kutoka kwa Mhandisi wa Maji mkoa wa Mwanza Ndugu Antony Sanga. Mradi huo mpaka kukamilika utakuwa na uwezo wa kutoa lita milioni 15 hivyo kuzidi mahitaji ya Sengerema ambayo ni lita milioni 8 kwa sasa,awamu ya kwanza ya mradi huo unategemewa kukamilika mwezi wa 8 mwaka huu na awamu nyingine inategemewa kukamilika mapema mwaka 2016.Pichani kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 kivuko kipya cha SUMAR III kitakachokuwa kinatoa huduma kati ya Sengerema na Mwanza kupitia feri ya Kamanga.
  Mbunge wa Jimbo la Sengerema Ndugu William Ngeleja akizungumza jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (pichani kati) wakati wa uzinduzi wa kivuko kipya cha SUMAR III kitakachokuwa kinatoa huduma kati ya Sengerema na Mwanza kupitia feri ya Kamanga. 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa kivuko kipya cha SUMAR III kitakachokuwa kinatoa huduma kati ya Sengerema na Mwanza. 
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua hali ya Soko Kuu la Halmashauri ya mji wa Sengerema, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza leo. Soko hilo limelalamikiwa na watumiaji kuwa na uchafu uliokithiri katika maeneo mbalimbali vikiwemo vyoo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimhoji Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kujua imekuwaje hadi hali ya soko kuwa mbaya, alipokagua vyoo na kushuhudia hali mbaya

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Sengerema, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata mpya ya Nyamizeze, Sengerema ambao walitaka kumsalimia .
Wakazi wa Sengerema mjini wakifuatilia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa CCM wilaya mkoani Mwanza
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa watu waliofurika kumsikiliza katika uwanja wa CCM Wilaya ya Sengerema ambapo aliwaambia wakazi hao Chama Cha Mapinduzi kitasimamia haki na misingi kwani ndio chama pekee kinachojali watu.

NAPE AKIHUTUBIA WAKAZI WA SENGEREMA

WIZARA YA HABARI UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO YAMUAGA RASMI MTALAMU WA KUPIGA PICHA KUTOKA SHIRIKA LA (JICA) LA JAPAN

$
0
0
4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akitoa shukrani kwa mwalimu wa picha  kutoka Japan  Mitsuhiro Matsuda  katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Ofisini kwake Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
3
Afisa habari Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Ramadhani Ali akitoa maelezo ya mafunzo yaliyoendeshwa na Mtaalamu wa Japan  Mitsuhiro Matsuda katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizara  ya  Habari Mnazimmoja  Zanzibar.
5
Mtaalamu wa kupiga picha kutoka Shirika la JICA la Japan Mitsuhiro Matsuda akizungumza katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizara ya Habari Mnazimmoja Zanzibar.
2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akiangalia baadhi ya picha za wanafunzi waliopata mafunzo ya  mwalimu  kutoka Shirika la JAICA  la Japan  Mitsuhiro  Matsuda katika hafla  ya kumuaga  iliyofanyika  Wizara Habari Mnazimmoja baada ya kumaliza muda wa miaka miwili ya kutoa mafunzo ya kupiga picha Zanzibar.
6
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akimkabidhi zawadi  Mitsuhiro Matsuda zilizotolewa na Idara ha Habari Maelezo Zanzibar katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizara ya Habari Mnazimmoja  Zanzibar
7
1
Picha ya pamoja ya Mitsuhiro Matsuda na baadhi ya wanafunzi wake waliopata mafunzo ya miaka miwili ya kupiga na kusafisha picha katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mnazimmoja Zanzibar.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE AANZA ZIARA NDANI YA JIMBO LA MISUNGWI AKITOKEA SENGEREMA MKOANI MWANZA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Msafara wake wakiingia kwenye kivuko cha Mv Misungwi katika feri ya Busisi mara baada ya kumaliza ziara yake wilaya ya Sengerema mapema leo asubuhi kuelekea wilaya ya Misungwi tayari kwa kuendelea na ziara yake ndani ya jiji la Mwanza
 Mbunge wa Jimbo la Sengerema,Mh.William Ngeleja (wa pili kulia) kwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana wakitazama kivuko cha Mv Sengerema iliyokuwa ikielekea katika feri ya Kigongo walipokuwa ndani ya Mv Misungwi,wakielekea wilaya ya Misungwi kuendelea na ziara ndani ya jiji la Mwanza
 Mbunge wa Jimbo la Sengerema,Mh.William Ngeleja (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana walipokuwa ndani ya kivuko cha Mv Misungwi,wakitokea wilaya ya Sengerema kuelekea wilaya ya Misungwi kuendelea na ziara ndani ya jiji la Mwanza
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh.William Ngeleja, kivuko cha Mv Sengerema wakati kilipokuwa kinapishana na kivuko cha Mv.Misungwi mapema leo asubuhi,shoto ni Katibu wa CCM Mkoa  Bwa.Miraj Mtaturu

BALOZI SIMBA APONGEZWA NA ILIYOKUWA IDARA YAKE KWA KUTEULIWA KUWA NAIBU KATIBU MKUU

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Elibariki Maleko katika hafla fupi ya kumpongeza Balozi Simba kwa kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Kabla ya uteuzi huo Balozi Simba alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati. Hafla hiyo ilifanya katika Hoteli ya Southernsun Jijini Dar es Salaam 
Balozi Simba akitoa neno la shukrani kwa Watumishi wa Idara ya Mashariki ya Kati wakati wa hafla hiyo.
 Balozi Simba  (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Idara ya Mashariki ya Kati. 
Picha na Reginald Philip

SIMBACHAWENE ATAKA USHIRIKIANO ATEKELEZE MAJUKUMU YA WIZARA

$
0
0
  Waziri wa Nishati na Madini,  George Simbachawene, akizungumza na wananchi wa  Kijiji cha Mwilowe, Wilaya ya Mpwapwa, baada  kuzuia msafara wake   wakati  alipopita  katika Kijiji hicho wakati wa ziara ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili unaofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO). Wanakijiji hao walimweleza Waziri kuwa kijiji chao pia kiunganishwe na umeme.

 Wananchi wa Kijiji cha Mwilowe wakizuia msafara wa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakitaka kijiji hicho pia kiunganishwe na nishati hiyo. Waziri alikua katika ziara ya kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini unaofadhiliwa na wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).
 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akiangalia mfano wa mashine ya kusaga inayotumia umeme  wa mota aliyotengenezwa na Kijana katika Kijiji cha Lukole. Simbachawene aliahidi kumsaidia Kijana hiyo kuweza kufikia lengo lake.
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizindua Albam ya  nyimbo ya Kwaya ya Mtakatifu Agustino katika Kijiji cha  Kingiti, Kigango cha Kingiti, wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Pili.
 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akionesha Album ya nyimbo ya Kwaya ya Mtakatifu Agustino katika Kigango cha Kingiti, kijiji cha Kingiti baada ya kuzindua Albam hiyo. Simbachawene alizindua album hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Pili.
Waziri wa Nishati na Madini, George simbachawene akishiriki kucheza ngoma ya Kabila la Wagogo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Umeme Vijijini, Awamu ya Pili katika Kijiji cha Malolo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma.
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akimkabidhi baskeli , Diana Kalenza, katika kijiji cha Idodoma, Wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa  Umeme vijijini, Awamu ya Pili. Kwa mujibu wa Simbachawene baiskeli hiyo imetengenezwa na SIDO, Dar es Salaam.
Mmoja wa wananchi katika kijiji cha  Malolo akiimba wimbo  mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati wa ziara ya Waziri katika Kijiji chicho. Wimbo huo uliokuwa na ujumbe wa kumwomba waziri   kukiunganisha Kijiji hicho. Aidha, wimbo huo  ulieleza namna  wanakijiji hao  watakavyotumia nishati hiyo kwa maendeleo yao. 

Na Asteria Muhozya, Mpwapwa
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amewataka wananchi kuwapa ushirikiano viongozi wa Wizara hiyo ili waweze kutekeleza kikamilifu majukumu yao kutokana na kusimamia rasilimali  muhimu  zinazobeba uchumi wa nchi.

Simbachawene aliyasema hayo kwa nyakati tofauti  wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini unafadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), na kutekelezwa na Shirika la Umeme   Nchini (TANESCO), katika vijiji vya Kinusi, Nzugilo, Idodoma, Malolo na Lukole, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma.

“Tuko kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Tunataka mshuhudie mafanikio makubwa ya usambazaji umeme vijijini. Serikali inatambua umuhimu wa nishati hii kwa maendeleo,na tutahakikisha kuwa, tunavifikia vijiji zaidi katika Awamu ya Tatu”, alieleza Simbachawene.

Simbachawene aliongeza kuwa, Mradi wa  usambazaji Umeme Vijijini ni endelevu na kuongeza kuwa, hivi sasa , serikali imezifikia takriban Kata na Tarafa  nyingi nchini na kuongeza kuwa, serikali itahakikisha inayafikia maeneo mengi zaidi yakiwemo yale yenye huduma muhimu za kijamii zikiwemo zahanati, shule na visima vya maji.

Aidha, alisema wizara yake iko kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote kuhakikisha kwamba wananufaika na rasilimali anazozisimamia bila kujali itikadi za vyama na hivyo kuwaomba wananchi kuonesha ushirikiano wakati serikali inapotekeleza Mradi huo wa usambazaji umeme Vijijini.

“Tuo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si kwa kuangalia  itikadi za vyama.Tutawatumikia wananchi wote bila kupokea rushwa kwa kuwa tunao uwezo wa kuwatumikia , nia tunayo, tunachotaka ni ushirikiano wenu”, alisema Simbachawene.

Katika hatua nyingine Simbachawene amepiga marufuku uchimbaji wa madini katika vyanzo vya maji na kueleza kuwa, wote watakaobainika kuchimba madini katika vyanzo hivyo, watafutiwa leseni zao za uchimbaji madini.

“ Sheria ya madini, kanuni na taratibu zake haziruhusu kuchimba madini katika vyanzo vya maji, kwa yeyote atakaebainika kuchimba madini katika vyanzo hivyo, tutamfutia leseni kwa kufuata taratibu na kanuni hizo”,alisistiza Simbachawene.

SOS WAADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA KWA MWANZILISHI WA VIJIJI VYA WATOTO DUNIANI

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
Watoto wametakiwa kujaliwa kwa kila namna ili kuwaanda kuwa taifa bora kutokana na misingi ambayo imewekwa kwa watoto hao.

Akizungumza na leo katika maadhimisho ya kuezi  kuzaliwa kwa mwanzilishi Vijiji vya Watoto SOS,Herman Gmeiner,Mkurugenzi wa Kijiji cha SOS,Anglolwisye Mwollo-ntalima,amesema  kuwa kila juni 23 kila mwaka wanaadhimisho kuzaliwa kwa Gmeiner.
Mwollo-ntalima amesema kuwa kutokana na mwanzilishi huyo kwa sasa Rais wa SOS ni mtu aliyetokana na SOS na kizazi hicho kinaendelea kuwepo.


Amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Nijali mimi ambayo dunia nzima imeadhimisha siku hiyo kwa kumkumbukA Mwanzilishi wa SOS.

Katika maadhimisho  ya SOS ,Kampuni ya Kontena ya Maersk Line imetoa msaada wa komputa katika kijiji cha watoto ili waweze kutumia kutokana na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano.

Mkurugenzi wa Maersk Line,Morten Juul amesema anatambua kazi inayofanywa na SOS  katika kuwatunza watoto kwa unagalifu.
Mkurugenzi wa kijiji cha watoto cha SOS hapa nchini, Angolwisye Mwollo-Ntallima akicheza na watoto katika siku ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa  SOS duniani,ambayo hufanyika kila Juni 23 kila mwaka, iliyofanyika katika kijiji cha SOS- Ubungo jijini Dar es Salaam leo.  
Mwalimu mkuu wa watoto wadogo wa kituo cha  SOS ,Agnes Mlema akizungumza leo katika siku ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa  SOS duniani,ambayo hufanyika kila Juni 23 kila mwaka, iliyofanyika katika kijiji cha SOS- Ubungo jijini Dar es Salaam leo.  
Baadhi ya watoto wakicheza ngoma leo katika kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS Ubungo jijinio Dar es Salaam.
Nkurugenzi mkuu wa Maersk Line, Morten Juul  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa kituo cha SOS pamoja na viongozi wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wa kompyuta katika kituo hicho leo jijini Dar es  Salaam.(Picha na Chalila Kibuda Globu ya jamii)

NHIF YAZOA VIKOMBE VYA UBUNIFU KATIKA MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

$
0
0
 Rais mstaafu Alhaj Ali Hasan Mwinyi akimkabidhi kikombe cha ushindi wa ubunifu katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma, mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa mfuko wa taifa wa  bima ya afya,Ali Othman katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyofikia kilele leo  katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Picha ya pamoja wakiwa na vikombe vya ushiindi vya ubunifu katika maonyesho ya utumishi wa umma yaliyofikia kilele leo  katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 wafanyakazi wa NHIF wakiwa na vyeti na vikombe vya ushindi wa ubunifu katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyofikia kilele leo  katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

GEPF YAWAKIVUTIO KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

$
0
0
Wananchi wakipata maelekezo kutoka kwa mwakilishi wa mfuko wa GEPF,  katika monyesho ya utumishi wa umma yaliyokiwa yakifanyika katyika viwanja vya Mnazi moja jijini Dar es Salaam.

TFDA WAFUNGA MONYESHO YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUWA NA BANDA BORA

$
0
0
 Mneja wa mawasiliano wa Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza akiwa na kikombe cha ushindi katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa TFDA wakiwa katika picha ya pamoja wakifurahia kikombe katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
wafanyakazi wa TFD wakiwa na vyeti pamoja na vikombe vyao vya ushikndi katika kilele cha maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja   jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMENUEL MASSAKA.

Airtel yazindua ofa ya LUKU

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea na waandishi wa Habari leo katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel nchini kupata Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money, kushoto ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel na (Kulia) Steven Kimea Meneja wa Airtel Money.
Meneja wa Airtel Money Steven Kimea (Kulia) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel nchini kujipatia nyongeza ya Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money, anayefwata kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo katika ofisi ya Airtel jijini Dar es Salaam. 

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika la umeme la (TANESCO) imezindua ofa kabambe itakayowazawadia wateja wake nchi nzima Unit za bure za Luku pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money

Ofa hii mpya ina lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme na pia kuwazawadia wateja wa Airtel wanaonunua unit za LUKU kupitia huduma ya Airtel Money

Akiongea kuhusu ofa hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackosn Mmbandoalisema” Wateja wetu watazawadia unit LUKU za ziada Bure mara tu watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money. Tunaamini ofa hii inaendana na mahitaji na mwendendo wa maisha ya watanzania. 

Kwa sasa manunuzi ya umeme kupitia njia nyingine si tu yanaleta changamoto za kusafiri umbali mrefu na kupoteza muda mwingi kupata huduma bali husababisha watu kukaa foleni ndefu kusubiri kununua umeme. leo Airtel tunatoa ofa hii kwa wateja wetu na kuwawezesha kununua LUKU kwa urahisi wakiwa majumbani mwao pamoja na kunawazawadia kwa kuwapatia unit za Luku za ziada za bure”.

Aliongeza kwa kusema “ Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu zinazokithi na kutatua mahitaji ya wateja wetu , tukiwa na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 45,000 nchini , wateja wetu wanafaidika na huduma ya mikopo, huduma za kuhamisha pesa, kutoa na kuweka pesa na nyingine nyingi.

Huduma ya Airtel Timiza inayotoa mikopo isiyo na dhamana kupitia simu za mkononi ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma za kisasa zenye ubunifu kwa watanzania.” aliongeza Mmbando

MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA-JUNI 23,2015

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe wakati wa kupiga kura bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Bungeni mjini Dodoma Juni 23,2015 ( Kulia), Mbunge wa Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Anna Chilolo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akipiga kura ya ndio wakati bunge lilipokuwa likipitisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Bungeni mjini Dodoma ( Kulia), Mbunge wa Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Anna Chilolo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mh. Mussa Azan Zungu wakati wa kupiga kura bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Bungeni mjini Dodoma leo-juni 23, 2015.1
Waziri wa Fedha, Saada  Mkuya akihitimisha Hoja ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha, Bungeni Mjini Dodoma Juni 23, 2015.(Picha zote na ofisi ya Waziri Mkuu)
2
Waziri Mkuu, Mizengo  Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Mpanda Kati, Said Arfi,  Bungeni mjini Dodoma.
4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Asiye na Wizara Maalum, Profesa Mark Mwandosya na Mbunge wa kigoma Mjini Peter Serukamba kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na wabunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah (kushoto) na Al Shymaa Kwegyir wakitoka kwenye kumbi wa Bunge mjini Dodoma.

CHAMA CHA WASAMBAZAJI WA FILAMU TANZANIA WASITISHA KUKUNUNUA STIKA ZA TRA NA KUPELEKA FILAMU ZAO BODI YA FILAMU KWAAJILI YA KUFANYIWA UKAGUZI

$
0
0
Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania,Bw Moses Mwanyilu akionyesha baadhi ya filamu ambazo zinauzwa nchini bila kupata kibali kutoka bodi ya filamu Tanzania na kutokuwa na stika za ushuru za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakielezea changamoto zao kuhusiana na filamu za kitanzania kulazimishwa kukaguliwa na bodi ya filamu na kuwekwa stika za TRA ilhali filamu za nje hazifanyiwi hivyo na kupelekea filamu za kitanzania kutokuwa na ushindani sokoni.
Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania,Bw Moses Mwanyilu akionyesha filamu kutoka nje ambayo inasemekana kuwa na maadili yasiofahaa kutazamwa na watoto chini ya miaka 18 ambayo inaendelea kuuzwa nchini huku ikiwa haijakaguliwa na bodi ya filamu wala haina stika za TRa kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza watayarishaji na wauzaji wa filamu za kitanzania ambazo zimekuwa na mlolongo mrefu hadi kuingia sokoni.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kuandika kile kinachozungumzwa.
Mjumbe wa chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Saleh Abdallah akizungumzia kauli moja waliyokubaliana kama wasambazaji kuwa Kuanzia tarehe 1 Julai 2015 wao kama watayarishaji na wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania wamesitisha swala la kupeleka filamu zao bodi ya filamu kwaajili ya kukaguliwa wala kununua stika za TRA mpaka pale mamlaka husika zitakapokaa chini na kujadiliana kuhusu swala hili.
……………………………………………………….
HABARI PICHA- NA  LUKAZABLOG
Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu.
Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.
Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.

Article 14


KONGAMANO LA HUAWEI CLOUD CONFERENCE LAFANYIKA DAR ES SALAAM

$
0
0
Katibu mkuu wa Wizara ya Sayansi Pro. Patrick Makungu  Md of Huawei Tanzania Bw. Zhan Yongquan anayeshuhudia ni balozi wa china nchini Tanzania, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na technolojia na waziri wa afya wa Zanzibar. bw kombo, wakisaini mkataba wa makubaliano kati yao  ikiipa nafasi kampuni ya Huawei Tanzania kua moja ya washauri wa mambo ya TEHAMA nchini.
2
Waziri wa Wizara ya Sayansi pro. Makame Mbawara akielezea Data Center iliyojengwa hapa Tanzania kwa waandishi wa habari. Pembeni yake ni Director wa ICT Dr. Ally Simba,3
Mr. Jiang Xin (Product Manager wa Huawei Enterprises) akielezea Data Center.

………………………………………………………..
Kampuni ya Huawei Tanzania ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  wameandaa kongamano la kwanza la sekta ya TEHAMA (ICT) ijulikanayo kama Huawei Cloud Conference kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC). 
Kongamano hili liliwakutanisha wadau wote wa TEHAMA (ICT) nchini, wakiwemo wa serikali na wa sekta binafsi na lilizinduliwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lv Youquin, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Patrick Makungu pamoja na usimamizi wa makampuni shirika ya Huawei Tanzania kutoka; Airtel, Viettel, Tigo, Vodacom, na TTCL.
Katika Kongamano hilo la mada “Rahisisha Teknolojia, Rahisisha Biashara” ilizungumziwa hali ya sasa ya sekta ya TEHAMA, sera zake pamoja na kupanga jinsi ya kuiendeleza sekta hii nchini ili kufikia malengo ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ya millenia ya 2025 ambayo ni kuendeleza Tanzania kupitia TEHAMA. 
Katika kongamano hili kampuni ya Huawei Tanzania (ambao ni wabunifu wakubwa wa bidhaa na huduma za TEHAMA) pamoja na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia walitia sahihi mkataba wa makubaliano kati yao huku ikiipa nafasi kampuni ya Huawei Tanzania kua moja ya washauri wa mambo ya TEHAMA nchini.
Baada ya kutia sahihi, Kampuni ya Huawei Tanzania ilielezea mipango yake ya kuendeleza na kukuza mawasiliano nchini Tanzania kwa kukuza sekta ya TEHAMA na kutoa elimu serikalini, mashuleni na kwa wananchi wote kwa ujumla kuhusu sekta iyo.
Tanzania imekua ikifanya kazi kwa karibu sana na Kampuni ya Huawei Tanzania na kwa mda wote kampuni hii imeshirikiana na wizara kwa karibu sana. Utiaji sahihi wa makubaliano ya kushirikiana katika shughuli za TEHAMA ni ushuhuda tosha wa jinsi Huawei Tanzania inavyojali sekta ya TEHAMA nchini na itaendeleza kukuza teknolojia hiyo nchini. 
Akizungumza katika Kongamano hilo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technolojia, Prof. Makame Mbarawa alisema, “TEHAMA inachangia sana katika maendeleo ya Uchumi ya nchi kwani inawezesha mambo kufanyika kwa ufanisi zaidi. Wizara na serikali kwa ujumla imekuwa na mahusinao mazuri na Kampuni ya Huawei Tanzania, na tumesha shirikiana katika miradi mingi. Pamoja na ubunifu wake katika sekta ya TEHAMA, Huawei imechangia sana katika mambo mbali mbali nchini Tanzania. Kufikia kwenye Mkataba wa Makubaliano kati ya Wizara na Huawei ni ishara ya ubora wa kazi ambayo kampuni hii, na itaendeleza ubadilishinaji wa teknolojia kati ya Huawei na Tanzania. Huawei imechangia pakubwa katika ukuaji wa sekta ya TEHAMA nchini Tanzania.
Naye Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lv Youquin alisema, “ Kwa mda mrefu Tanzania na China wamekua na mahusiano mazuri hususan baada ya ujio wa raisi wa china bwa. Xi Jinping mwaka 2013; Kampuni nyingi za kichina zimekuja Tanzania kuwekeza na kukuza nchi. Kama kiongozi wa mambo ya TEHAMA duniani, Huawei imewekeza nchini Tanzania kwa Zaidi ya miaka 17 na kwa muda wote huo imetoa ajira nyingi kwa watanzania pamoja na kuwekeza kwenye shughuli za kijamii nchini, na kuwa mfani wa kuiga katika maswala ya kidiplomasia kati ya Tanzania na China.
Katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Patrick J Makingu aliwapongeza Huawei kwa mchango wao katika kujenga Tanzania bora kupitia TEHAMA na kuwasihi makampuni mengine ya TEHAMA kuiga mfano wa Huawei. Aliendelea kwa kusema, “Huawei imekuwa ikijikita katika kutafuta suluhisho mpya katika sekta ya TEHAMA duniani. Awali mwaka huu, Huawei ilihusika katika Kongamano la Mobile World Congress mjini Barcelona nchini Uhispania ambapo walikuwa moja kati ya mashirika makubwa kufanya maonyesho ya bidhaa zake mpya na sisi kama Wizara tunajivunia kufanya kazi nao”.
Naye Mtendaji Mkuu wa Huawei Tanzania Bw. Zhang Yongquan alisema “Kampuni ya Huawei Tanzania imekuwepo nchini kwa takribani miaka 17 na imejishughulisha katika shughuli mbalimbali za kujenga nchi ikiwepo shughuli za kijamii hususani kwenye michango vyuoni na mahospitalini. Bw. Zhang Yongquan, aliendelea kwa kusema “Tunashukuru serikali ya Tanzania pamoja na wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa kuendelea kuiunga mkono kampuni yetu”. 
Katika kongamano hilo, kampuni ya Huawei Tanzania ilizindua bidhaa zake mpya Oceanstor V3 and Fusioncube. Pia imeonyesha Truck yao inayozunguka nchi mbalimbali kila mara moja kwa mwaka ikianzania nchini China, na kwa mwaka huu truck hili linazunguka kusini na magharibi mwa bara la Afrika. 
Kampuni ya Huawei Tanzania inaongoza katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Tanzania na imekua ikishirikiana na wadau wengine wa mawasiliano kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel na TTCL katika kuchangia ukuaji wa watu binafsi kwenye hii sekta (ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).

CUF watoka nje ya Baraza la Wawakilishi

$
0
0
Na Kijakazi Abdalla / Maryam Kidiko -Maelezo Zanzibar .

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha Mapinduzi wamesikitishwa na kitendo cha wawakilishi wenzao wa Chama cha Wananachi (CUF) kutoka nje  ya kikao kilichojadili mswada wa kupitisha matumizi ya Serikali kwa mwaka 2015/2016.

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud amesema kuwa kitendo kilichafanywa na Wajumbe  wa CUF kutoka nje ya Baraza  sio cha busara na hakileti sura nzuri ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa..

Amesema  uamuzi waliochukuwa wajumbe hao ni kukitia aibu chama hicho na kuwanyima haki wananchi waliowachagua kuwaingiza ndani ya Baraza.

Waziri Aboud amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zazibar ina nia thabiti ya kufanya uchaguzi kwa njia ya haki kwa wanannchi wote na sivyo kama wnavyofikiria wawakilishi  hao.

Amesema wakati huu ambapo tunaelelekea katika  uchaguzi mkuu wa mwezi wa Oktoba  ilikuwa si busara kuchukuwa hatua hiyo  kwa vile  hawakutumia sheria bali walitumia  siasa zaidi.


Wakichangia mswada huo baadhi ya wawakilishi   CCM wamewataka wananchi waliowachagua wawakilishi wa CUF  kuwakataa katika uchaguzi wa mwezi Oktoba  kwa vile wameshindwa kuwawakilisha vizuri katika vikao vya Baraza hilo tokea walipoingia mwaka 2010.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CUF wametoka nje ya Baraza kwa madai  ya kutoridhika na zoezi zima la uandikishaji wapiga kura linaloendelea Wilaya ya Magharibi A.

Akitoa taarifa baada ya kuanza kikao cha asubuhi cha Baraza hilo   huko Chukwani, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, mjumbe wa CUF Juma Duni Haji  alisema kuwa wameamua kutoka nje kutokana na kutokuwa na imani na zoezi  la uandikishaji wapiga kura linavyoendeshwa.

Alidai kuwa  baadhi ya wanachama wa CUF wenye sifa  ya kuandikishwa wamekuwa wakunyimwa haki hiyo na wamekuwa wakipigwa na askari wa vikosi vya SMZ wakati wakiwa njiani kwenda  kujiandikisha.

“Tumeshuhudia  askari  waliovaa  ninja (kufunika nyuso) wenye silaha katika mitaa wakiwakimbiza wananchi wanaokwenda kujiandikisha kupiga kura,” alilalamika Juma Duni.

Pamoja na wajumbe hao kutoka nje ya Baraza,  Wajumbe wa Chama cha Mapinduzi CCM waliendelea  kujadili na kupitisha  mswada  wa matumizi ya fedha kwa mwaka 2015/2016  .

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR. 

NHC YAFANYA UHAKIKI WA VIKUNDI VYA VIJANA KATIKA MKOA WA LINDI NA MTWARA

$
0
0
Uhakiki wa vikundi vya vijana vilivyopewa msaada wa mashine na NHC ili kujiajiri na kusaidia wananchi kupata matofali ya kujengea nyumba bora umeanza katika Mikoa mbalimbali ukianzia na Mkoa wa Lindi na Mtwara. 

Katika hali isiyotarajiwa Mkoa wa Mtwara ambao kwa muda mrefu umekuwa ukililia kuletewa maendeleo umeshindwa kutumia fursa ya msaada wa mashine kwa vijana waliyopewa na NHC hali iliyolifanya Shirika kutwaa baadhi ya mashine ili zipewe vikundi vingine vinavyofanya vizuri Fuatilia kupitia habari picha hizi ili ufahamu kilichojiri katika mikoa hiyo ya kusini mwa Tanzania. Leo uhakiki huo unaendelea Mkoani Ruvuma.
New Picture
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Bw. Nicholous Kombe akimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akimshukuru kwa Halmashauri hiyo kusaidia kikundi cha vijana kwa kuwawezesha fedha na udongo kwa ajili ya kutengeneza matofaliya kufungamana. Katikati ni Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu.
New Picture (2)
Jengo la Ofisi ya kikundi cha vijana cha Narunye(hakuna kutegeana) katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini likiwa limeonwa na Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kama inavyoonekana. Kikundi hiki kimeshaanza kupata maombi mengi ya matofali kutoka kwa wananchi wanaohitaji.
New Picture (1)
Kikundi cha vijana cha Ruangwa Materials Group katika Halmashauri ya Wilaya Ruangwa kimeshatengeneza matrofali kwa kutumia mashine ya msaada kutoka NHC. Halmashauri ya Wilaya hiyo imeamua kuyatumia matofali ya vijana hawa kujengea zahanati na majengo mengine yanayohitajika katika Halmashauri zikiwemo nyumba za Waalimu.

New Picture (3)
Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu akitoa mawaidha kwa kikundi cha vijana cha Narunye kilichopo katika Wilaya ya Lindi vijijini baada ya kutembelea kikundi hicho kukagua kazi zake.Vijana hawa wanajihusisha pia na utunzaji mazingira.
New Picture (4)
Baada ya Wakurugezi wa Halmashauri za Kilwa na Lindi Vijijini kutokuwa karibu na vikundi vya vijana, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC na Meneja wa Mkoa wa Lindi waliweza kufanya mazungumzo nao ya kina na hatimaye wamekubali kuwasaidia vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC katika Halmashauri zao ili waweze kujiajiri. Kulia ni Bi. Oliver Vavunge ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilwa Bi. Maimuna Mtanda.
New Picture (5)
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Bw. Daniel Kaluse hakuwa nyuma kutembelea kikundi cha Vijana na Maendeleo kilichopo eneo la Mitwero nje kidogo ya Manispaa hiyo ili kuwapa moyo na kufahamu maendeleo yao akiwa ameandamana na ujumbe wa NHC.
New Picture (6)
Meneja wa NHC Mkoa wa Mtwara Bw. Joseph John akitoa taarifa ya Mkoa kwa Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC ya maendeleo ya vikundi vya vijana waliosaidiwa mashine na NHC . Katika taarifa yake Meneja huyo alisikitishwa na vijana wa Mkoa wa Mtwara kushindwa kutumia kikamilifu msaada huo na akalaumu Halmashauri za Mkoa huo kushindwa kushiriki kikamilifu katika programu hiyo ya kusaidia vijana.
New Picture (7)
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akikemea na hatimaye kukinyanganya mashine kikundi cha Likonde katika Manispaa ya Mtwara kwa kuifungia stoo mashine waliyopewa msaada na NHC bila kufanya kazi iliyokusudiwa ya kufyatua matofali. Mashine hiyo itapewa kikundi kingine ili itumike kikamilifu.
New Picture (8)
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akiwa Wilayani Tandahimba akikagua matofali yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana cha Maendeleo Group kilichopewa msaada wa mashine na NHC. Kikundi hiki kinasubiri kulipwa na Halmashauri matofali hayo yanayotarajiwa kujengea nyumba za waalimu.
New Picture (9)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Bw Dennis Mwaitete akielezea mkakati wa Halmashauri yake wa kusaidia vijana ulivyo alipotembelewa na ujumbe wa NHC uliokuwa ukihakiki vikundi vya vijana Mkoani Mtwara.
New Picture (10)
Kikundi cha vijana cha Umoja Lekanelo kilichopo Wilaya ya Newala kilichoshindwa kutumia kikamilifu mashine ya msaada kilichopewa na NHC kiliweza kupokonywa mashine hiyo jana. Wilaya ya Newala ina shughuli za madini na kilimo cha korosho kiasi cha kuwafanya vijana kushindwa kujihusisha kikamilifu na mradi wa kufyatua matofali.
New Picture (11)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Marx Kamaoni akizungumza na ujumbe wa NHC uliofika Ofisini kwake kuhamasisha Halmashauri za Wilaya kusaidia vikundi vya vijana vilivyopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali na NHC.
New Picture (12)
Vyombo vya habari vimehusishwa katika uhakiki huu na hapa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Newala Bw. Marx Kamaoni akiongea na waandishi wa habari kuelezea mkakati wa Halmashauri yake kusaidia vijana.
New Picture (13)
Kikundi cha Vijana cha For Energy Group kilichopo Wilayani Masasi kilitembelewa na baada ya kuridhishwa na utendaji wake NHC ilikiongezea mashine mbili zilizopokonywa vikundi vingine vilivyoshindwa kuzitumia Wilayani Newala na Masasi Vijijini. Hii ni nyumba iliyojengwa na kikundi hicho Wilayani Masasi.
New Picture (14)
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akivionya vikundi vya vijana vya Nayoden na Mangaka Wilayani Nanyumbu waliokula fedha ya mtaji waliopewa na NHC ambapo aliamuru kuchukuliwa kwa mashine zao na kuwapa muda wa kujiandaa. Aliwataka kuziomba mashine hizo kwa maandishi watakapokuwa tayari kuzitumia. Mashine hizo zilifungiwa Ofisi ya Kata ya Mangaka kwa muda wa miezi nane wakisubiri kupata fedha nyingine kutoka NHC.
New Picture (15)
Mashine iliyopokonywa vijana wazembe Wilayani Nanyumbu ikipandishwa katika gari baada ya vijana hao kuzembea kuitumia na kuifungia Ofisi kwa muda mrefu.

CLIP FUPI YA NAPE : GOLI NI GOLI

RAIS KIKWETE AMTUNUKU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MBARAK ABDULWAKIL NISHANI YA UTUMISHI MREFU NA MAADILI MEMA DARAJA LA (I)

$
0
0
1
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam.Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.2
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, baada ya kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu.8
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kushoto) akiwa na baadhi ya Watunukiwa wakiwa katika hafla hiyo wakati wakisubiri kutunukiwa.9
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kwenda nyuma mstari wa kwanza) akiwa na baadhi ya Watunukiwa wakiwa katika hafla hiyo wakati wakisubiri kutunukiwa. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.3
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Ernest Mangu (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil baada ya kutunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I) na Rais Jakaya Kikwete, katika sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu,4
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) John Minja (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil baada ya kutunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I) na Rais Jakaya Kikwete.
5
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil baada ya kutunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I) na Rais Jakaya Kikwete.
6
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akiteta jambo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR), Joyce Mends-Cole katika Ukumbi Mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtunukia Katibu Mkuu huyo, Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I).
7
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) John Minja (kulia) na Mkurugenzi wa Sera na Mipango, wa Wizara hiyo, Haji Janabi, nje ya Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtunuku Katibu Mkuu huyo, Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I).
   10
Rais Jakaya Kikwete (wanne kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Watunukiwa wa Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la Kwanza. Wakwanza kulia mstari wa nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Viewing all 49537 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>