Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

TBL YAPATA TUZO YA NSSF YA MWAJIRI BORA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cavin O'Flaherty (wa pili kulia), akipokea tuzo ya mwajiri bora wa kwanza katika idara ya matekelezo ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutoka kwa Meneja Kiongozi wa NSSF mkoa wa Temeke, Bw. Chieldrick Komba, Dar es Salaam jana. Wengine kulia ni Meneja wa Huduma za TBL, Alois Maleck Qande (wa pili kulia), Afisa Uhusiano Doris Malulu (kulia) na baadhi ya maofisa wa NSSF (waliosimama kushoto.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cavin O'Flaherty (wa nne kulia) na Meneja wa Huduma za TBL, Alois Maleck Qande (wa tatu kulia) wakionyesha tuzo za ushindi wa kwanza wa mwajiri bora walizopewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wengine ni baadhi ya maofisa wa NSSF na TBL.
 TUZO ZENYEWE
WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

WAZIRI WA ARDHI WILLIAM LUKUVI AZINDUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU ZINAZOJENGWA NA NHC WILAYANI MASASI

$
0
0
New Picture (4)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akiweka jiwe la msingi katika nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi ambazo ujenzi wake utakamilika mwezi Oktoba mwaka huu.

New Picture (5)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akipewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio.
New Picture (3)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimia viongozi wa NHC mara baada ya kuwasili eneo la Napupa Masasi kuzindua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC. Anayemuongoza Mh. Waziri ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi.
New Picture (7)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na hadhira iliyofurika katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi.Alizitaka taasisi zinazotoa huduma ya umeme na maji kutekeleza majukumu yao ili kupunguza gharama za uuzaji wa nyumba zinazojengwa na waendelezaji wote wa makazi.

New Picture (8)
Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi.
New Picture (6)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi. Akitoa taarifa ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi kwa Waziri wa ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi aliyefika katika mradi huo wenye nyumba 54 na kuuzindua.
New Picture
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi Bi Beatrice Dominic akitoa taarifa ya usimamizi wa ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi alipozuru Masasi na kuzindua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC.
New Picture (1)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na wazee aliyowahi kufanya nao kazi Wilayani Masasi mwaka 1975 akiwa Katibu wa Vijana wa Wilaya, baada ya kukutana nao Ikulu ndogo Mjini Masasi.
New Picture (2)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi,akionyeshwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi Bi. Bi Beatrice Dominic mali na magari yaliyounguzwa na vijana wa Masasi kutokana na vurugu zilizowahi kutokea huko nyuma na kuunguza pia jengo la Ofisi ya ardhi ikiwemo nyaraka zote. Hadi sasa Halmashauri hiyo haina Ofisi za kutosha kufanyia kazi na wala usafiri wa kusaidia utendaji wa kazi wenye tija.

MBOWE,NDESAMBURO,JAFARY MICHAEL WATIKISA MJI WA MOSHI

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Railway mjini Moshi .
Mwenyekiti wa Chadema taifa,Freman Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Philemon Ndesamburo walipokutana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Railway mjini Moshi,wengine ni Mwenyekiti wa BAWACHA mkoa wa Kilimanjaro ,Helga Mchomu .
Mamia ya wananchi waliohudhulia mkutano huo ,wakimsikiliza mstahiki Meya,Jafary Michael (hayuko pichani).
Msatahiki Meya wa manispaa ya Moshi Jafary Michael akizungumza katika mkuta huo.
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Philemon Ndesamburo akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Railway.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akimkaribisha Mwenyekiti wa Chadema taifa ,Freman Mbowe kuhutubia wananchi katika viwanja vya Railway mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Chadema taifa,Freeman Mbowe akiwahutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Railway mjini Moshi.
Mbowe akiagana na wananchi waliohudhuria mkutano huo .
Mwenyekiti wa Chadema taifa,Freeman Mbowe akisalimiana na wananchi waliojirtokeza katika mkutano huo.
Mbowe akisindikizwa na wananchi wakati akiondoka katika iwaja ya Railway. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

NAPE AKIHUTUBIA MJINI GEITA

WAZIRI BERNARD MEMBE APATA WADHAMINI GEITA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita Juni 21.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho. Picha zote na John Badi.SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati mwenye miwani) akishangiliwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita Juni 21.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho. Kushoto kwake ni Katibu wa CCM wilaya ya Geita, Robert Balingo.SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipongezwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita Juni 21.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.SONY DSC
SONY DSC
Waendesha baiskeli wakiusindikiza msafara wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (hayupo pichani) baada ya kuwasili wilayani Geita Juni 21.2015,kwa ajili ya kutafuta wadhamini wa kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.

KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA CCM (NEC) YA ZANZIBAR

$
0
0
06
Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa taarifa za Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halamashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC),kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,mbele ya Mwenyekiti Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) wengine Makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kushoto)na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilali.03
Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halamashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) wakipitia agenda mbali mbali zilizotayarisha katika kikao hicho cha siku moja kabla ya kuanza katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.05
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiendesha kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halamashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC),kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,(kushoto)Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilali.02 
Wajumbe wa kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halamashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) wakipitia agenda mbali mbali zilizotayarisha katika kikao hicho kabla ya kuanza   wakati Mwenyekiti wake akiwa    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,

01
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama wakati alipowasili katika Viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM  Kisiwandui Mjini Unguja leo, kushiriki katika kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halamashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC), [Picha na Ikulu.]
04 
Wajumbe wa kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halamashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) wakipitia agenda mbali mbali zilizotayarisha katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,wakati Mwenyekiti wake akiwa    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.  07
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halamashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) wakisikiliza taarifa za na Agenda za kikao zilizotolewa na Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai mbele ya Mwenyekiti  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.

RAIS WA SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA ADDO NOVEMBER MWASONGWE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE IRINGA MJINI KWA TIKETI YA CCM

$
0
0
Ndugu wanahabari leo tarehe 21 Juni 2015 nimekuiteni kuwaeleza juu ya Nia yangu ya kugombea Ubunge Iringa Mjini kwa ticket ya CCM. 
Sababu ninayo Nia ninayo na uwezo ninao kwa wananchi wangu wa Iringa na Tanzania kwa ujumla. Natambua ya kua uongoZi ni Mzigo… Uongozi ni kipaji na uongoZi ni kubeba Majukumu ya kuwaongoza wengine na siyo Ubwana au Ubwanyenye Kama dhana hii inavyoharibiwa na wengi.
Ndugu wana Habari Uongozi ni Wito… Mimi nimezaliwa hospitali ya serikali ya Mkoa Iringa na kukulia Frelimo kata ya Mivinjeni na nimekua Kiongozi tangu nikiwa Mtoto pale Sokoni Iringa Kanisa Kuu na baadae kuwa Kiranja Prefect nikiwa Wilolesi Shule ya Msingi Hali hiyo iliendelea nikawa Waziri Katika wizara mbali mbali miaka yote mitatu nilipokua Chuo Kikuu baada ya Kumaliza Masomo yangu ya Sheria CCM makao Makuu walinileta Iringa Kama Katibu wa Wilaya kazi ambayo nayo ilininoa vilivyo.
 Ndugu wana Habari kazi hiyo haikuishia hapo… Katika kujifunza uongozi Mungu amenibariki kuwa Msaidizi wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Kama Mzee Makamba, George Mkuchika na Jaka Mwambi Mpaka baadae Mwenyekiti wa Chama Changu CCM aliporidhia kuanzishwa kwa taasisi ya wasomi yaani vyuo Vikuu ambapo nilipelekwa kuongoza na nikiwa huko niliweza kujenga takribani matawi yote ya vyuo Vikuu Nchi nzima kwa kuhakikisha wana kuwa na Uongozi na ofisi zao ushahidi ni hapa kwetu Iringa nilifungua matawi matatu na kujenga ofisi za Mkwawa na Tumaini. Nimepitia mafunzo mbali mbali ya Chama tangu mwaka 2006 Katika Chuo Kikuu cha CCM Ihemi na kufaulu kwa distinction jambo ambalo linanipa unyenyekevu kuwatumikia Wananchi wangu wa Iringa.
Ndugu wana Habari nimejiunga na CCM tar 31.12.1998 Tawi la Tandamti Frelimo kwa Balozi wangu Mzee Mlosi (Mungu amuweke mahala pema) hivyo ni karibu miaka 14 nipo ndani ya Chama Changu na ninaona ninayo haki na wajibu kuwaongoza wana Iringa wenzangu ambao najua changamoto zao zinazowakabili Katika Chama na Nje ya Chama.
Ndugu wanahabari kwa kutumia uzoefu nilionao hapo juu vilevile Kama Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Rais wa WanamuZiki wa Injili Tanzania, Wakili (Advocate) na kada wa CCM Mume wa Mke Mmoja na watoto watatu, hii Kabisa ni ishara kubwa kuwa ninao uwezo wa kupambana na changamoto za Iringa Mjini na Nchi yangu kwa Ujumla.

Changamoto tuliZonazo… Ndani ya Chama…., bila kupepesa maneno natambua mpasuko uliopo na ambao umesababishwa na Viongozi wa juu wa Chama Wilayani na Mkoani hapa na wengine wamepewa nafasi za serikali lakini bado wamekipasua Chama kwa makundi hivyo mtu Pekee atakayeleta Umoja na mshikamano ni Mimi Addo November Mwasongwe ambaye sina kundi na nipo Tayari kuongoza watu wote, mtu wa watu Mpenda watu ambaye Nafahamu taratibu za Chama Changu ndio maana Mpaka leo sijafanya vurugu yeyote jimboni Kama wanavyofanya wenzangu ambao mnawajua..na mmewaona wakijipitisha kila kukicha.
Mara Zote napata sana Faraja ninapokumbuka Kauli inayosema Kizuri Chajiuza Kibaya Chajitembeza Natambua changamoto ya ofisi bora za CCM na usafiri kwa kila Kata na Hilo nitalichukua Kama jukumu langu binafsi Kama mjumbe wa Kamati ya Siasa pale mtakaponipa ridhaa ya Ubunge. Natambua kuwa mafunzo ya uongozi tanatakiwa kuanzia ngazi za shina Mpaka Kata na Wilaya.Changamoto za Wananchi 1.Miundo Mbinu na Umeme jambo hili litakua kipaumbele kuhakikisha maeneo yote yanafikika kwa Lami hii inaweZekana kwa kupata Mbunge safi ambae ni mie na madiwani safi,2. Iringa kuwa kitovu cha Utalii Kama ilivyo Arusha.
Wote tunatambua kuwa Mbuga ya Ruaha ndiyo kubwa kuliko Zote Duniani hivyo ni jukumu letu kuitangaza na kuweka vivutio vya utalii Kama vile Mahoteli makubwa Tour Guide Offices jambo ambalo litakuza uchumi wa Iringa kwa kupitia Utalii na kutoa ajira kwa wana Iringa na wengine wengi. 
3. Kuwamilikisha wananchi wetu ardhi zao ili wasiweze kudhurumiwa lakini waweze kukopea inapobidi kwa maendeleo Yao 4. Kukuza Michezo na Sanaa kuwa na uwekezaji wenye tija wa Sanaa na Michezo jambo litakalotoa ajira ya kudumu na kukuza uchumi wetu, 5. Matibabu ya uhakika kwa wazee wanawake na wasiojiweza 6.
Utawala bora na uwajibikaji 7. Wananchi kupata mikopo nafuu ya Nyumba 8. Kupiga Vita ukimwi na malaria 9. Kukuza Kilimo na kutafuta Masoko ya uhakika ya maZao yetu 10. Kukuza Elimu na kutoa Motisha kwa Vijana wetu walioko kuanzia Shule za Msingi na Sekondari ili tujipatie vijana wenye uwezo mkubwa kwa maendeleo ya Taifa na hili halitawezekana bila walimu bora wanaolipwa vizuri 11.
Uongozi wa Vitendo 12. Kukuza Miundo Mbinu hasa usafiri wa Anga kwa kurekebisha Airport yetu ili kuharakisha maendeleo na Utalii.13. Rasilimali ziwanufaishe wananchi wetu 14. Kukemea Rushwa na Ufisadi ifikie hatua ikibidi tuapishwe kwa Jina la Mwenyezi Mungu kuwa Kati ya Sisi Wagombea yeyote anayetumia pesa kuhonga Katika uchaguzi huu basi na afe kwa Jina la Mwenyezi Mungu kwenye hili tusilete mzaha tujiulize hawa wanaotumia pesa watazirudishaje?? Kwa Njia ipi 15. Wanawake, wazee Vijana na Watoto kuwa na Mfuko wao maalum wa kuwakwamua 16. Lugha ya Kiswahili kuitumia kama mtaji kwa kuanzisha madarasa yatakayowaleta watalii kuja kujifunza Kiswahili na ikibidi watu wetu kwenda Nje ya Nchi kufundisha Kiswahili jambo litakalonipa sana Faraja 17.
Kuziba pengo Kati ya asiye Nacho na mwenye nacho. 18. Kupunguza Kabisa kero ya Maji na gharama ya maji mwananchi wa kawaida apate maji pasipo Shaka 19. Kuwa na usafiri wa Ambulance ikibidi kila Kata ili kunusuru maisha hasa Akina Mama wanaokwenda kujifungua Hospitali. 20. Kukaribisha wawekezaji wenye tija kwa maendeleo ya wote. Ndugu zanguni ninayo mengi mema kwa Jimbo langu na Taifa langu na Ni matumaini yangu ya kuiona Iringa kwa jicho la Mwenyezi Mungu yaani Iringa ambayo Mungu anataka Iwe Kama alivyoikusudia na Kila Mmoja aweze kuridhika nayo. Inawezekana Kila Mmoja Akitimiza wajibu wake, Mjenga Nchi ni Mwananchi. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Iringa, Mungu akiwa Upande Wetu Ni Nani aliye juu yetu??? Tujipe moyo Tutashinda Pamoja. Addo November Mwasongwe, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania,

KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA


WASANII KUTUMIKA KUELIMISHA UMMA MENEJIMENTI YA MAAFA

$
0
0
Askari wa Jeshi la Zima moto nchini, Josephat John akieleleza matumizi ya Kizimamoto wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, mjini Dodoma tarehe, 21 Juni, 2015.2
Afisa Tawala, Ofisi ya Waziri Mkuu, Leah Kibassa, akifanya mazoezi ya kutumia kizima moto wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi hiyo, mjini Dodoma.3
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu  Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya (mwenye tai) akishuhudia, Salma Juma akikabidhiwa Kizima moto kilichonunuliwa na washiriki wa mafunzo ya menejimenti ya maafa wa Ofisi hiyo mjini Dodoma tarehe, 21 Juni, 2015,  Kwa lengo la kuhamasisha watumishi wa Ofisi hiyo kukabili majanga ya moto.4
 Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mafunzo ya majanga ya moto  wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa mjini Dodoma.
………………………………………………………
Na. Mwandishi Maalum
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa inaandaa mkakati wa elimu kwa umma wa menejimenti ya maafa ambao utawatumia watu maarufu nchini wakiwemo wasanii wa sanaa mbali mbali kwa lengo la kufikisha elimu kwa umma ya menejimenti ya maafa. 
Akiongea wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki hii, Brig.Jen, Mbazi Msuya alibainisha kuwa jamii ikielimishwa kikamilifu juu ya menejimenti ya maafa athari za maafa zinapunguzika.
“Tunaposema menejimenti ya maafa tunazingatia, kuzuia, kukabili maafa na kurejesha hali ya awali baada ya maafa kutokea. Kwa mantiki hii kama tunavyo elewa Wasanii wanao uwezo wa kufikisha ujumbe kwa haraka, lugha nyepesi, kwa watu wengi na kwa ujumbe mmoja, hili ndo linalotusukuma kufikiria kutumia hawa watu katika kutoa elimu ya menejimenti ya maafa kwa jamii yetu” alisema Msuya.
Msuya aliongeza kuwa nchi yetu imekuwa ikikumbwa na majanga ya asili na yale yanayosababishwa na binadamu, ambapo majanga yanayosababishwa na binadamu kwa kiwango kikubwa jamii inaweza kuyakabili tu ikiwa elimu ya menejimenti ya maafa hayo imemfikia kila mwanachi. Hivyo kwa kuwa wasanii wengi msingi wa kazi zao za sanaa huaksi yanayojiri katika jamii yao hivyo hii itakuwa ni fursa kwao kuijengea jamii uwezo wa kuyakabili maafa.
“Athari za Majanga yanayosababishwa na binadamu kama moto yanaweza kuzuilika ikiwa menejimenti ya majanga hayo itatolewa kwa umma. Wananchi wakielimishwa umuhimu wa kuwa na vizima moto majumbani mwao na katika vyombo vya moto wanaweza kukabili majanga ya moto na hili litawezekana kwani tayari tunayo mikakati ya mawasiliano ya kukabiliana na maafa ” alisisitiza Msuya.
Ofisi ya waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu maafa tayari imeshaandaa Mkakati wa Mawasiliano wa kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara, Shinyanga na Dodoma lengo ikiwa ni kila mkoa nchini kuwa na mkakati huo utakowezesha menejimenti ya maafa kwa jamii ya watanzania. Aidha mkakati huo unabainisha kila mdau wa maafa wajibu wake katika menejimenti ya maafa wakiwemo wasanii.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO YAPUNGUZA MAAMBUKIZI YA MALARIA KWA ASILIMIA NANE

$
0
0
Nyumba ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Mkuyuni ambayo imefunguliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ndugu Juma Khatib Chum ili watumishi hao waweze kuishi karibu na Kituo hicho.
Na. Andrew Tangazo Chimesela (Morogoro)
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, imefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa asilimia 8 ukilinganisha na maambukizi ya ugonjwa huo mwaka 2014.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Dkt. Mwanahamisi Yahya ambaye ni Kaimu mganga wa kituo cha Afya cha Mkuyuni Wilaya ya Morogoro wakati akiwasilisha taarifa ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ndugu Juma Khatib Chum.
Dkt. Mwanahamisi amesema, mapambano dhidi ya malaria Katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ni moja ya Kipaumbele kinachotiliwa mkazo na Halmashauri hiyo kupitia Idara ya Afya, jitihada zilizoleta matokeo chanya ya kushusha maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia Nane.
“Hali ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria katika Halmashauri yetu imeshuka kwa asilimia Nane kutoka asilimia 56 mwaka 2014 hadi asilimia 48 mwaka 2015”, matokeo haya yametokana na jitihada za Halmashauri ikishirikiana na wadau mbalimbali ”.aliongeza Dkt. Yahya.


Dkt. Yahya amesema, Kituo cha Afya cha Mkuyuni na Zahanati zilizopo katika Tarafa ya Mkuyuni vimeendeleza mapambano dhidi ya Malaria kwa kutoa Elimu kwa akimama Wajawazito ili kuzuia maambukizi ya malaria kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Jitihada nyingine zilizofanywa katika kupunguza mambukizi ya Malaria kushirikiana na Wadau mbalimbali ni pamoja na kuhamasisha jamii kutumia kikamilifu vyandarua vilivyotiwa viwatilifu na kusafisha mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu wanaosababisha malaria.
Aidha, Dkt. Yahya alitaja lengo la mapambano dhidi ya Malaria kuwa ni kupunguza maambukizi, magonjwa na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria katika jamii kwa kutoa Elimu na huduma Bora za Afya kupitia vituo vya Afya na Zahanati.
Sambamba na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Ndugu Juma Khatib Chum kupokea Taarifa hiyo ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria, alifungua nyumba ya mtumishi wa kituo cha Afya cha Mkuyuni iliyojengwa kwa gharama ya shilingi 135,000,000.00.
Miradi mingine ya maendeleo iliyopitiwa na mwenge huo ni pamoja na mradi wa utunzaji mazingira Kijiji cha Kiloka, mradi wa maji na usafi wa mazingira wa Kijiji cha Changa na mradi wa Ufugaji bora wa nyuki uliopo kijiji cha Kikundi. 
Miradi mingine ya maendeleo iliyopitiwa na Mwenge huo ni mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Mtego wa SImba, mradi wa mashamba ya Kikundi cha Vijana wakulima wa mahindi na mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Vicoba Kikundi cha Upendo. 
Mwenge wa uhuru umeingia siku yake ya tatu kukimbizwa katika Mkoa wa Morogoro ambapo leo umekimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na kupitia miradi saba ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi 323,142,000.00.

MBUNGE WA KIGAMBONI DK.FAUSTINE NDUGULILE AZINDUA MASHINDANO YA DIWANI CUP KATA YA KISARAWE TWO MANISPAA YA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile (wa pili kulia), akizungumza na wachezaji wa timu za Dubu na Tumaini (hawapo pichani), wakati akifungua mashindano ya  kombe la umoja na mshikamano maarufu kama Diwani Cup yaliyoanza uwanja wa Kibamande eneo la Mwasonga Manispaa ya Temeke Dar es Salaam jana. Kulia ni mlezi wa mashindano hayo,  Diwani wa Kata ya Kisarawe II,  Issa Zahoro.
Mlezi wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kisarawe II,  Issa Zahoro, akikagua timu ya Dubu kutoka eneo la Mwasonga.
 Mlezi wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kisarawe II,  Issa Zahoro, akikagua timu ya Tumaini kutoka katika kata hiyo.
Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile

Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile, akiwasalimia mashabiki wakati akiwasili kufungua mashindano hao.
Mashabiki wakifuatilia mashindano hayo.
Wazee wa Kata hiyo wakifuatilia kwa karibu mashindano hayo.
Timu ya Tumaini ikiomba dua kabla ya kuanza mashindano hayo.
Timu ya Tumaini katika picha ya pamoja.
Timu ya Dubu katika picha ya pamoja.
Waamuzi wanaochezesha mashindano hayo.
Timu na waamuzi wakielekea kukaguliwa.
Mchezaji wa timu ya Tumaini, Tamimu Mussa (kushoto), akimtoka Josephat Kalinga wa timu ya Dubu.
Mashabiki wakifuatilia mashindano hayo.
Hapa ni kazi tu uwanjani.
Hapa mchezaji mdogo kuliko wote kutoka timu ya Dubu, Mwishehe Omary akipewa zawadi ya sh.10,000.
Mchezaji aliyeng'ara katika mashindano hayo akipokea zawadi ya sh.10,000.

Na Dotto Mwaibale

MASHINDANO ya  kombe la umoja na mshikamano maarufu kama Diwani Cup yamezinduliwa rasmi katika eneo la kisarawe II,kwa timu za dubu kupepetana dhidi ya timu ya Tumaini zote za kata hiyo.

Akizindua mashindano hayo yaliyofanyika Kiwanja cha Kibamande kilichopo eneo la Mwasonga, Mbunge wa Kigamboni Faustine ndugulile alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,

"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Ndugulile
    
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Ayubu Mkonde aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa ikiwakilisha kata hiyo katika mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.

Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kisarawe II,  Issa Zahoro alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa eneo la Kisarawe II.ambapo katika mchezo wa ufunguzi timu ya Dubu ilishindwa kutambiana dhidi ya timu ya Tumaini kwa kutoka uwanjani bila ya kufungana. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AANZA ZIARA MKOANI MWANZA,AMALIZANA NA KAGERA NA GEITA

$
0
0
 
  Katibu Mkuu wa CCM ndugu Kinana (kulia) akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya  katika Kata ya Nyehunge Kijiji cha Isaka, Jimbo la Buchosa, wilayaniSengerema, Mwanza leo.
  Katibu Mkuu wa CCM ndugu Kinana  akitoka akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya  katika Kata ya Nyehunge Kijiji cha Isaka, Jimbo la Buchosa, wilayaniSengerema, Mwanza leo. 
 Wananchi  wakimshangilia Mbunge wa jimbo la Buchosa,Mh.Charles Tizeba,alipokuwa akizungumza nao kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndgugu Kinana kuwasalimia Wananchi  katika Kijiji cha Bupandwa, Jimbo la Buchosa.

  Ndugu Kinana akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Bupandwa, Jimbo la Buchosa.
 Ndugu Kinana akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la msingi katika Jengo la Ofisi ya CCM Tawi la Katwe,jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana na mradi wa maji katika Kijiji cha Rumeya, Buchosa Wilayani Sengerema.
  Ndugu Kinana akihutubia katika Kijiji cha Nyakarilo, Jimbo la Buchosa, Sengerema.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi wa kata ya Bukokwa,jimboni Buchosa wilaya ya Sengerema mkaoni Mwanza,pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
  Kinana akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji  katika Kijiji cha Kalebezo, Kata ya Nyehunge, Jimbo la Buchosa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kalebezo, Kata ya Nyehunge, Buchosa baada ya kuzindua mradi wa maji.
 Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Charles Tizeba akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kalebezo, Kata ya Nyehunge, Buchosa baada ya kuzindua mradi wa maji.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara iliofanyika kwenye kijiji cha Nyehunge jimbo la Buchosa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema katika jimbo la Buchosa,alipokuwa akiuliza swali .

nana ambaye yupo katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ameanza ziara mkoani Mwanza, baada ya kumaliza ziara katika mikoa ya Kagera na jana Mkoa wa Geita.

Akiwa mkoani Mwanza atafanya kazi ya kuimarisha uhai wa chama, kusimamia, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi  ya CCM, pamoja na kusilikiza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema katika jimbo la Buchosa,Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa kwa
furaha na Mbunge wa Jimbo la  Sengerema, ambaye pia ni mmoja wa wana CCM waliochukua fomu ya kuomba kuwania urais ndani ya chama hicho, William Ngeleja alipowasili katika Kata ya Nyamadoke, Jimbo la Buchosa,, wilayani Sengerema, kuanza ziara rasmi katika majimbo yote ya Mkoa wa Mwanza leo.

Ndugu Kinana ambaye yupo katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ameanza ziara mkoani Mwanza, baada ya kumaliza ziara katika mikoa ya Kagera na jana Mkoa wa Geita.

Akiwa mkoani Mwanza atafanya kazi ya kuimarisha uhai wa chama, kusimamia, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi  ya CCM, pamoja na kusilikiza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la  Sengerema, ambaye pia ni mmoja wa wana CCM waliochukua fomu ya kuomba kuwanua urais ndani ya chama hicho, William Ngeleja, alipowasili wilayani Sengerema.

KAIMU MKURUGENZI BOHARI YA DAWA (MSD), AZUNGUMZIA UFUNGUAJI MADUKA YAO KARIBU NA WANANCHI

$
0
0

 Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), akimuelekeza jambo Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kulia), katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (kushoto), akizungumza na John Chale kuhusu kazi mbalimbali zinazpfanywa na MSD baada ya kutembelea banda la MSD katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja mwishoni mwa wiki
 Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kushoto), akiwaelekeza jambo wananchi waliotembelea banda la MSD katika maonyesho hayo.
 Vifaa tiba mbalimbali na vitanda vinavyoonyeshwa na MSD katika maonyesho hayo.
Kitanda kikiwa kwenye soko kwenye maonyesho hayo.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI Kuu ya Dawa (MSD),imejipanga  kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kufungua maduka yao kwenye mikoa minne nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD Cosmas Mwaifwani katika mahojiano ya maonyesho ya Utumishi wa Umma yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Mwaifwani alisesema lengo ni kuziondolewa usumbufu hospitali kuagiza dawa kwenye ofisi ya kanda mara zinawaishia ghafla na maduka hayo yatakuwa ndani ya hospitali au karibia na hospitali.

Ametaja mikoa ambayo wanaanzia kufungua maduka hayo  ni Mbeya,Dar es Salaam,Mwanza na Arusha ambamo yatakuwa yanafanyakazi saa 24.

“Tumeamua kusogeza huduma karibu na jamii kwa kufungua maduka katika mikoa hiyo aidha,ndani ya hospitali au karibu na hospitali kuzirahisishia kuzinunua pindi wanaishiwa na dawa kabla ya kuziagiza”,alisema Mwaifwani .

Akizungumzia mafanikio alisema wamepata  muarobaini ya kuwadhibiti wezi wa dawa za serikali kwa kuziwekea nembo maalum.

Alisema tayari  zoezi hilo lishaanza ambapo hadi sasa dawa 42 zishawekewa nembo hizo zijulikanazo kama (GOT), na jitihada bado zinaendelea kwa dawa nyingine.

Mwaifwani alisema  jitihada bado zinaendelea kufanywa na MSD kuendelea kuziweka nembo zaidi dawa nyingine za kawaida ambayo jumla yake ni 630,na zile za mradi msonge jumla yake 613.

“MSD bado inaendelea kuweka dawa za serikali nembo ili kudhibiti wizi wizi na tumeanza na aina hizo 42 bado tunaendelea kuweka nyingine zilizobakia”,amesema Mwaifwani.

Amezitaja baadhi ya dawa zilizowekewa nembo kuwa ni pamoja na Magnesium, Amoxilin, Ciproflaxin, paracetamol, Dixlophenac,  Clotromoxin na nyinginezo.  (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

LOWASSA AZIDI KUJIZOLEA MAPOKEZI MAKUBWA KILA ANAKOKWENDA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka na swala la kukatwa jina lake katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa Tanzania.

Lowassa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM zaidi ya elfu 52.

"Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu". alisema Lowassa.

 Lowassa aliwasili Mkoani Ruvuma mapema mchana wa leo akitokea Mkoani Iringa kwaajili ya kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais kwa tiketi ya chama hicho, ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na kupelekea kufunga barabara kuu ya mjini, hali iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya kibambaza cha jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza hao.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma waliokuwa wamesimama nje ya Ofisi za CCM Mkoa huo, mjini Songea leo Juni 21, 2015, wakati alipofika kwa ajili ya kupata udhamini utakaomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma. 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Chifu wa Kabila ya Wangoni, Chifu Ally Yussuf Songea (97). Chifu huyo alikwendwa kwenye uwanja wa Ndege wa Songea kumpokea Mh. Lowassa.
Wakinamama wa Mkoa wa Ruvuma wakimfurahia Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
Mmoja wa Wazee wa Mkoa wa Ruvuma, Mzee Ally Jaibu Rashid akitoa neno kwa niaba ya Wazee wa Ruvuma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na Wazee wa Mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiondoka kwenye viwanja vya CCM Mkoa wa Ruvuma.

MFUKO WA PESHNI WA PSPF WATOA ELIMU KWA MADEREVA TAXI WA WILAYA YA ILALA NA MADEREVA KUJIUNGA NA MPANGO WA HIARI

$
0
0
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma  akitoa maelezo ya kina kuhusu faida na huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujionga alipokuwa akiongea na madereva wa taxi wa wilaya Ilala jijini Dar 
 Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akizungumza na madereva wa taxi wa wilaya ya Ilala(Hawapo pichani) kuhusu kutii sheria za barabarani na kuwasisitiza kujiunga na mfuko wa Peisheni wa PSPF.

 Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa azungumza jambo na madereva wa taxi wakati wa mkutano wao uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Tambaza jijini Dar
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akijibu maswali ya baadhi ya madereva 
 
 
 
 Madereva wa Taxi wa wilaya ya Ilala wakiuliza maswali kwa Maofisa  wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati wa mkutano wao
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akiwaelekeza madereva wa Taxi jinsi yakujiunga na mfuko huo
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka akimpa maelezo mmoja wa madereva wa Taxi wilaya ya Ilala aliyeamua kujiunga na mfuko wa Peisheni wa PSPF
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akimtolea ufafanuzi kuhusu faida za mfuko wa PSPF wakati wa mkutano wao uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Tambaza jijini Dar

Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka(kushoto) akimuonesha mmoja wa madereva ili aweke alama ya dole gumba kwenye fomu za Uchangiaji wa Hiari
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka akielezea jinsi ya ujazaji fomu za Uchangiaji wa Hiari kwa baadhi ya madereva waliovutiwa kujiunga na mfuko wa Peisheni wa PSPF
Baadhi ya Madreva wa Taxi wilaya ya Ilala wakiendelea kufuatilia kkwenye mkutano wao



Na Mwandishi Wetu
Madereva taxi katika wilaya ya Ilala jijini dar es salaam wapokea elimu kutoka kwa mfuko wa pensheni wa PSPF na kuweza kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha wanawekeza katika mfuko huo kwa manufaa yao hapo baadae kutokana na kazi zao wanazozifanya kila siku za udereva kuwa ni kazi za kawaida na kuona kuwa Pspf ndio kimbilio kwa madereva hao

Akizungumza wakati wa mkutano huo Afisa masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Ismail Juma amesema wameamua kuungana na madeeva Tax ili kuweza kuwapa elimu katika suala la kuwekeza na kufaidika na mafao mbalimbali yanayo tolewa na PSPF kwani Pindi watakapo jiunga na mfuko huo wataona matunda mengi hasa kutokana na kuwa ni watu ambao wanategemewa na familia hivyo kama Pspf wana mafao ambayo wataweza kujikwamua kama mafao ambayo wanaweza kuwasomesha watoto,vilevile fao la uzazi hata fau la nyumba pia ujiungapo na mfuko huu utafaidika na wala hauto jutia 

Mkuu wa kitengo cha elimu wa jeshi la polisi,kikosi cha usalama barabarani makao makuu , Abel Swai wakati akitoa elimu ya usalama barabarani amewaasa madereva wote nchini hususani kwa madereva walio weza kufika katika mkutano huo wa madereva tax kuweza kuwekeza katika mifuko ya jamii ni jambo muhimu hasa ukizingatia kwa hali ya sasa maisha kuwa ya kawaida na uchumi wanchi yetu kuporomoka amewaomba madereva kutumia fursa zinazo tolewa na mfuko wa pensheni wa PSPF ili wawe na akiba ya mafao yao pindi kazi zinapo isha na hata kuweza kufaidika na mambo mbalimbali katika mfuko huo

Pia mkaguzi msaidizi wa polisi kanda maalumu ya dare s salaam Josephat Sylvery Tirumanywa amewasisitiza madereva kutii sheria za barabarani maana wamepewa dhamana ya kuwasafirisha abiria kwa amani na upendo ,hivyo kati ya jeshi la polisi na madereva husaidiana kufanya kazi kwa umoja na hivyo kuweka mahusiano mazuri katika kufanikisha nchi yetu iajengwa na sisi watanzania kwa kuendeleza upendo na amani pindi tuwapo barabarani,aliongeza kuwapa shukrani mfuko wa pensheni wa Pspf kwa hatua ya kuwahamasisha watu mbalimbali kuweza kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha mabadiliko ya wananhi mbalimbali yanatokea kimaisha ,elimu,afya na mengine mengi.

Miongoni mwa madereva waliohudhuria katika mkutano huo wameupongeza  mfuko wa pesheni wa PSPF kwa kuweza kuwajali kwa kuwapa elimu juu ya mfuko huo pia wameahidi kushiriki vilivyo katika kujiunga na mfuko huo ili  kuhakikisha maisha yao yanaenda sambamba na hadhi ya jina na ubora wa kazi zinazofanywa na PSPF,
”kwani tumeiona fursa kutoka PSPF hivyo hatuna budi kujiunga na mfuko huu kwani fursa ni kuthubutu,kuhiari, kutendana kuamua  na uamuzi tulio uchukua ni kujiunga na PSPF kwa manufaa ya kwetu pia ya taifa kwa ujumla “pia wawasisitiza kuendelea kueneza elimu katika mkoa wa dar es salaam wote na hata nje ya mkoa ili watu watambue fursa zinazo tolewa na PSPF.


MAONESHO YA UTALII YA SANGANAI/HLANGANANI–(WORLD TOURISM EXPO) ZIMBABWE YAFUMBUA MACHO WATANZANIA

$
0
0
IMG_4145
Pichani juu na chini ni Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vyake nchini Tanzania kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali vikiwemo vya utalii nchini Zimbabwe waliofika katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya nane ya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) kupata taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii wa Tanzania yaliyomalizika jana jijini Harare katika ukumbi wa hoteli ya Rainbow Towers.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
IMG_4137IMG_4168
Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) akibadilishana mawazo na wananfunzi wa Belvedere Technical Teachers College nchini Zimbabwe, Francisca Chipuriro (kushoto) na Natalie Takavarasha (katikati) wakati walipotembelea banda la Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za utalii wa Tanzania na vivutio vyake siku ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers.
IMG_4185
Wageni mbalimbali waliovutiwa na vivutio vya utalii nchini Tanzania wakiendelea kumiminika katika banda la Tanzania na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) ambapo hivi sasa Shirika la ndege la Fastjet limeanza safari zake jijini Harare kupitia Lusaka hadi Dar es Salaam kwa gharama nafuu kabisa itakayowezesha wananchi wa Zimbabwe kufanya safari za Tanzania kwa gharama nafuu kabisa.

IMG_4229
Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii zinazofanywa na kampuni yake kwa wageni waliofika katika banda la Tanzania wakati wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare.
IMG_4241
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (wa pili kulia) akitoa maelezo yaliyomo kwenye vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini Tanzania kwa wageni waliotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho nane ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.
IMG_4191
Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel ya nchini Tanzania, Joseph Waryoba (kulia) akipata picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Zambia, Felix Chaila aliyembelea banda la Tanzania wakati wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers ambayo yamemalizika juzi.
IMG_4195
Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travelnchini Tanzania, Joseph Waryoba katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tanzania Travel Company ambayo pia imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.
IMG_4205
Timu kutoka Tanzania ambayo imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare ikiongozwa na Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba, Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (kulia).
Na Modewjiblog team, Harare
TIMU ya watanzania walioenda kuhudhuria maonesho ya utalii nchini Zimbabwe wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza uendeshaji wa sekta ya utalii.
Walisema katika ziara yao hiyo wamegundua kwamba Wazimbabwe kuanzia wanapompokea mgeni hadi anapofika hotelini wanaonesha kujali hali ambayo mgeni hawezi kusahau hata kidogo.
Aidha amesema kwamba hata mipangilio ya kwenda kwenye vivutio inafanyika katika hali ambayo huwezi kusahau hata kidogo.
Kutokana na mazingira hayo, wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza namna ya kupokea na kuishi na wageni na kuwatengenezea taswira ambayo hawatakaa wakisahau.
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wamodewjiblog yaliyofanyika mjini Harare siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers jijini Harare.
Solomon amesema ingawa hali ya Tanzania si mbaya, watendaji katika viwanja vya ndege na mahotelini wanaweza kuangalia namna Wazimbabwe wanavyojali kazi zao na tabasamu zao nyakati zote kwa wageni .
“Si kwamba kwetu kuna shida lakini unaona watu wanavyojituma hapa” alisema Esther Solomon na kuongeza kuwa aliona jinsi walivyojipanga vizuri na wafanyakazi walikuwa na uelewa wa hali ya juu.
Esther aliongoza kundi la watu watano wa Kitanzania walioalikwa na mamlaka ya utalii Zimbabwe (ZTA) kuhudhuria maonesho hayo.Tanzania iliweka banda lake pia katika maonesho hayo ya siku tatu yaliyomalizika juzi.
Makampuni ya mawakala wa utalii aliyoambatana nayo katika safari hiyo ni pamoja na Tanzania Travel Company, Cordial Tours and Travel, Mberesero Tented Camp na Best Northern Tours and safaris .
Alisema safari yao Zimbabwe pamoja na ushiriki wao katika maonesho pia walifika katika maeneo mbalimbali ya kitalii nchini yakiwemo maporomoko ya Victoria.
Aidha walipewa nafasi ya kukagua sehemu za malazi kwa ajili ya wageni.
Alisema katika maonesho hayo wamefanikiwa kupata wageni wengi wanaoulizia namna ya kufika Tanzania na pia ushirikiano wa makampuni katika sekta ya utalii.
“ Watu wengi wamekuja kututembelea. Na wengi ni watu weusi. Mwamko wao wa kutembelea vivutio ni mkubwa.” Alisema Esther na kuongeza kuwa wamebaini kwamba ipo haja ya watanzania kuhimizwa kutembelea vivutio kwani hata nchini Zimbabwe wanaotembelea vivutio ni wananchi wenyewe.
Alisema wengi waliofika katika banda la Tanzania waliulizia namna ya kufika visiwa vya Zanzibar na pia mbuga za Tanzania.
Aidha mawakala wengi waliulizia namna ya kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha utalii katika bara la Afrika.
Asilimia 80 ya watalii nchini Zimbabwe wanatoka bara la Afrika na waliobaki ndio wanatoka nje ya bara hili.

UHALIFU MTANDAO KUELEKEA UCHAGUZI 2015

$
0
0

Nianze makala hii kwa kupongeza jitihada za dhati za serikali ya awamu ya Nne katika uwekezaji wake kwenye sekta ya TEHAMA Nchini. Ni wazi kabisa nchi yetu imepiga hatua kubwa katika maswala ya TEHAMA kulinganisha nan chi nyingi Afrika. Mifano michache ni pamoja na kuhama kutoka analogia kulekea Digitali, Mkonge wa taifa, Kupatikana kwa Khala Mtandao la taifa, kuaandikisha upigaji kura kimtandao na mengineyo mengi.


Aidha, Jitihada kama vile kupatikana kwa sharia mtandao, kupatikana kwa vitengo vinavyo shughulikia uhalifu mtandao,  wakala za serikali mtandao na mengineyo yamekua ni hatua ya kipekee iliyoweza kutoa matumaini kwa watanzania kutoka kwa serikali ya awamu hii ya Nne inayo ongozwa na Dk. Jakaya Kikwete.


Jitihada hizi njema naona bado kuna ya kufanyika zionyeshe matunda na zibaki salama kwa muda mrefu. Nimeyasema hayo kufuatia kauli yangu niliyoitoa, Nilipo sema serikali ina jukumu la kuwekeza zaidi katika maswala ya usalama mitandao ili kuweza kubakisha salama jiihada hizi za TEHAMA kwani isipo fanywa hivyo kuna hatari kubwa mbele yetu kimtandao iyakayo pelekea jitihada hizi kuingia dosari kubwa.


Hatari za kimtandao zitakazo pelekea kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wetu, siasa zetu, tamaduni na jamii yetu kwa kwa ujumla wake. Napo zungumzia uchumi nipamoja na upotevu mkubwa wa fedha unaosababishwa na uhalifu mtandao ulio athiri taasisi za fedha na mawasiliano nchini. Kumekua na wimbi kubwa la wizi wa fedha kimtandao hii ni mjumuisho wa pesa kutoka mabenki pamoja na pesa zinazo potea kutokea kwenye miamala ya simu.


Moja ya changamoto iliyo sikika kwenye kikao nilichoshiriki kilicho husisha nchi ya  ujerumani na Tanzania ni pamoja na lalamiko kutoka kwa mshiriki kuelezea kua kupitia mtandao alipoteza pesa zake na kumekua na ugumu kuzipata pesa hizo. Nilitolea ufafanuzi hilo kwa kueleza kua tatizo ni kubwa na kama hakuna jitihada za dhati kudhibiti hili basi kuna hatari ya uchumi wetu kupitia uhalifu huu mtandao kuporomoka.


Aidha, Naomba nijikite zaidi kwenye Uchaguzi mkuu ujao Oktoba – Ni wazi kabisa kuanzi uandikishaji hadi taratibu nyingine za kuelekea uchaguzi mkuu umehamishiwa katika mtandao. BVR (Biometric Vote Registration) mfumo mtandao unaotumika kuandikisha wapiga kura ambao kwa ujumla wake ni mfumo wwa kimtandao.


Kuna hatari kubwa ya Mifumo hii kuathirika kimtandao na kusababisha kupatikana kwa taarifa zisizo sahihi endapo wahalifu mtandao wataweza kuingilia na kufanya marekebisho wa namna ya ufanyaji kazi wake. Hii inaambapatana na Matumizi mabaya ya mitandao kuelekea uchaguzi ambapo inaweza kusababisha kuyumbisha amani iliyoko Nchini. Nimelizungumza hili kwa kirefu sana kama inavyoweza kusomeka kwa ku "BOFYA HAPA"



Ikumbukwe Wahalifu mtandao wamekua hawalali waki tafuta njia mpya za kuleta maafa mtandao na ndio maana hata baada ya kumaliza kikao maalum cha wana usalama mitandao tulipokutana Jijini Johannesburg, Ambapo Kwa ufupi taarifa yake inaweza kusomeka kwa ku "BOFYA HAPA" – Palitokea uhalifu mtandao ulio itikisa nchi ya Marekani na baadae kwenye Mahojiano yangu na kituo cha BBC nikaweza kutolea ufafanuzi walau kwa uchache ya wapi tunajikwaa kama tulivyo kubaliana mkutanoni. Unaweza kusikiliza mahojiano hayo kupitia Video inayo onekana hapa.



WITO: Naomba niendelee kutoa wito katika swala zima la ushirikiano kwani taifa au kundi Fulani peke haliwezi kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao unao endelea kukua kwa kasi. Aidha, Kuendelea kukuzwa kwa uwezo watu wentu wa ndani hasa wanao shughulikia uhalifu mtandao nchini pamoja na kukukuza uelewa wa matumizi salama mitandao kwa watumiaji.



Aidha, Kupatikana kwa Chombo maalum kitakacho unganisha nguvu za vitengo kadhaa vilivyopo ili kupatikana nguvu ya pamoja kufikia malengo ya kuweka taifa letu salama pamoja na kuongeza uwekezaji katika usalama wetu wa mitandao Nchini.

AIRTEL FURSA’ TUNAKUWAWEZESHA YAMUWEZESHA FUNDI NGUO, BETHA BENEDICT MKAZI WA BUNJU JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
????????????????????????????????????
Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kulia), akizungumza wakati wa hafla ya kukabdhi mashine ya cherehani yakushonea nguo kwa fundi wa kushona nguo, Betha Benedict mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” (katikati), Betha Benedict aliyewezeshwa na mpango huo, na kushoto ni mama yake Betha Benedict.
????????????????????????????????????
Mama yake Betha akiishukuru Kampuni ya Airtel kwakumuwezesha Mwanae kwakupitia mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha”
????????????????????????????????????
Mratibu wa Chuo cha (MTCD) Dogodogo kinachotoa mafunzo kwa Vijana waishio katika mazingira magumu kuanzia Umri wa miaka 10-16, Bw.Issa Buzohera naye akishukuru Kampuni ya Airtel kwa mpango huo.
????????????????????????????????????
Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (wa pili kulia ), akimkabidhi zawadi ya mashine ya kushonea ‘cherehani’, Betha Benedict (wa pili kushoto), mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakwezesha”. Kushoto ni mama yake Betha na kulia ni Meneja wa Airtel, Fadhili Mwasijeba.
????????????????????????????????????
Betha Benedict akioneshwa na Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi vifaa vinavyotumika katika mashine ya kushonea nguo cherehani.
????????????????????????????????????
Baada ya makabidhiano ikawa ni furaha kwa ,Betha pamoja na vingozi wa kampuni hiyo.
????????????????????????????????????
Betha Benedict (kulia), akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Airtel mara baada ya kuwasili nyumbani kwake kwaajili ya kumkabidhi zawadi (katikati), Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi.
????????????????????????????????????Betha Benedict (kusoto) akisalimiana na Afisa Uhusiano na Matukukio wa Airtel, Dangio Kaniki (katikati), mama yake Betha Benedict.
????????????????????????????????????
Picha ya pamoja.
…………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
AIRTEL Tanzania kwa kupitia mpango wake mpya wa Airtel
Fursa-Tunakuwezesha imemkabidhi kijana Betha Benedict vifaa
mbalimbali vya kushonea na mashine ya kushonea nguo ‘cherehani) ambavyo vitamsaidia katika biashara yake ya kushona nguo na kumuongezeaa kipato chake.

Betha ambaye ni mkazi wa Bunju alikabidhiwa vifaa hivyo juzi na Kampuni ya simu ya Airtel ambapo awali alikuwa akitumia cherehani kimoja na kuwa na changamoto ya ufanyaji wa kazi yake hiyo ya ushonaji.

Akizungumza baada ya makabidhiano, Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema mpango huu ulibuniwa ili kuwawezesha vijana na kuwakwamua kiuchumi.

Alisema Betha amepitia changamoto nyingi kupitia kazi yake hiyo ya ushonaji kwani ndiye anayeitunza familia yao mama pamoja na wadogo zake hivyo fursa hiyo aliyoipata itamuwezesha asonge mbele kimaisha.
“Betha ni kijana wa pili kufaidika na mpango huu na kama tulivyosema hapo awali mpango huu unawalenga vijana ambao tayari wanajihusisha na miradi mbalimbali kama Betha na wanatakiwa kutuma maombi yao,” alisema na kusisitiza kuwa mpango huo hauwalengi wanaotaka kuanzisha miradi.

Alimtaka Betha atumie vifaa hivyo vizuri iliaweze kujiendeleza
zaidi na kuwa mfano mzuri kwa vijana ili kuutangaza vizuri mpango huu.
Bayumi aliwataka vijana wachangamkie fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango huu unawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao.

“Program hii inahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini,” alisema.
“Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma
ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao
kwa kupitia barua pepe .

airtelfursa@tz.airtel.com<mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>. ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtelwww.airteltanzania.com<http://www.airteltanzania.com/>,”

KINANA ALIPOHUTUBIA MKOANI GEITA

MEMBE AHUDHURIA MSIBA WA MTOTO WA JENERALI MSUGURI NA KUHANI MSIBA WA JOHN NYERERE BUTIAMA MKOANI MARA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri wakati wa ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri, Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri wakati wa ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri (wa tatu kulia), Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akijadiliana jambo na Mama Maria Nyerere baada ya  shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri, katika ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri, Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua. Kulia ni Mbunge wa Mchinga (CCM), Saidi Mtanda.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati alipokwenda nyumbani hapo kuhani msiba wa mtoto wa Baba wa taifa, Marehemu John Guido Nyerere, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bw. John Guido Nyerere aliyefariki Mei 9 mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015.
Picha na John Badi
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images