Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 559 | 560 | (Page 561) | 562 | 563 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kitambi ni ile hali ya tumbo kuwa kubwa na kuchomoza kwa mbele na wakati mwingine kufikia hatua ya kuniníginia.

  JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA

  Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati ya bilioni 50 hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.
  Kwa wanawake seli hizo zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

  Kwa upande wa wanaume seli hizo zinapatikana sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia. Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:
  i. Njia ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi
  ii. Na njia ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

  SABABU ZA KUPATA KITAMBI
  Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika mwili wa mwanadamu, hali inayo sababishwa na mtu kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

  VYAKULA VINAVYO CHANGIA KULETA KITAMBI
  Vyakula vinavyochangia kuleta kitambi ni pamoja na :
  i. Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama nyekundu (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama ya kuku wa kizungu ( iwe ya kuchemsha, kukaanga ama kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa mafuta (chips) pamoja na pizza.
  ii. Vyakula vyenye wanga mwingi kama vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate mweupe.
  iii. Vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi iliyo ongezwa ( added sugar ), kama vile soda na keki.
  iv. Vyakula vilivyo tengenezwa kwa ngano na sukari kama vile keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate mweupe nakadhalika
  v. Pamoja na vinywaji vilivyo tengenezwa kwa kutumia ngano kama vile bia za aina mbalimbali na kadhalika.
  Vyakula vilivyo tajwa hapo juu, vikitumiwa bila kuzingatia kanuni za mlo kamili, huchangia kuleta tatizo la kitambi. vi. Sababu nyingine ni kutofanya mazoezi ya mwili na viungo ( physical exercises ) kwa muda mrefu.

  JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI
  Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips).

  Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40 kwa wanaume na >88 cm au 35 kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake. BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.

  Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu. Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

  MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI
  Tumekwisha ona hapo juu jinsi kitambi kinavyo patikana na vyakula pamoja na sababu nyinginezo zinazo sababisha kutokea kwa kitambi, sasa tutazame mambo yatakayo kufanya uwe katika hatari ya kupatwa na kitambi.

  Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mambo yafuatayo huwaweka watu katika hatari kubwa ya kupatwa na kitambi :
  1. Ulaji mbovu wa chakula; Ulaji mbovu wa chakula ni ulaji usio zingatia kanuni za mlo kamili. Hapa mtu hufululiza kutumia chakula cha aina fulani pekee bila kuzingatia aina nyinginezo za chakula. Mfano; mtu anaweza kuwa anakula mlo ufuatao : Asubuhi : Mchemsho ama supu ya ngíombe , chapatti tatu na soda moja. Mchana : Ugali nyama choma anashushia kwa maji na soda. Jioni : Mchemsho wa kuku na bia mbili nakuendelea. Usiku : Chips mayai au chips kuku au chips mishikaki na bia. Mtu huyu akiendelea na utaratibu huu kwa muda mrefu, ni lazima atapatwa na kitambi.
  2. Ulaji mfululizo wa vyakula vyenye mafuta mengi
  3. Ulaji mfululizo wa vyakula vyenye wanga mwingi .
  4. Ulaji mfululizo wa vyakula vyenye sukari iliyo ongezwa ( added sugar ).
  5. Ulaji mfululizo wa vyakula vya ngano.
  6. Ulaji mfululizo wa vinywaji vyenye ngano na sukari.
  7. Kutofanya mazoezi ya mwili na viungo ( physical exercises ).

  Mhusika anapokuwa katika makundi yote yali yotajwa hapo juu, hali huwa mbaya zaidi.

  NJIA ZA KUONDOA KITAMBI Kuwa na kitambi ni lugha ya mwili ( body-language ) inayo leta ujumbe kwako kwamba ì Mwili wako haupo salama tena ì
  Kama una kitambi maana yake una mafuta yasiyo hitajika mwilini, mwili wako unatumika kuhifadhi mafuta usiyo yahitaji.

  Hali hii kitabibu imaanisha kwamba, ogani nyinginezo zilizomo ndani ya mwili wako zinao gelea kwenye mafuta( fats ) yasihotika yaliyomo ndani ya mwili wako, jambo linalo kuweka katika hatari kubwa sana ya kushambuliwa na magonjwa hatari kama vile shinikizo kubwa la damu, kiharusi na kisukari na kwa kutaja machache.
  Hivyo basi ili kuondokana na hatari hiyo, yakupasa kupambana kuondoa hayo mafuta yasiyo hitajika mwilini mwako.

  NJIA ZA KUONDOA KITAMBI.
  Unaweza kuondokana na kitambi kwa kufanya diet pamoja na mazoezi ya mwili na viungo.
  Vilevile unaweza kuondoa kitambi na kupunguza mafuta mwilini kwa kutumia dawa asilia ya kuondoa kitambi na kuondoa mafuta yasiyo hitajika mwilini.
  DAWA ASILIA YA KUONDOA KIAMBI NA MAFUTA MWILINI.
  Hii ni njia ya uhakika kabisa ya kuondoa tatizo la kitambi pamoja na mafuta yasiyo hitajika mwilini. Unaweza kuondoa tatizo la kitambi pamoja na kupunguza mafuta mwilini kwa kutumia DAWA ASILIA IITWAYO YA MKATAA KITAMBI. Dawa hii ni ya asili kabisa ì Pure Herbal ì, ambayo haijachanganywa na kemikali yoyote, haina side effect kwa mtumiaji na inaondoa kabisa tatizo la kitambi ndani ya siku kumi na nne.

  JINSI DAWA YA MKATAA KITAMBI INAVYO FANYA KAZI.
  1. Huyeyusha mafuta yasiyo hitajika mwilini.
  2. Husaidia kupunguza hamu ya chakula.
  3. Inazuia kutengenezwa kwa seli za mafuta ( fat cells ) katika mwili wa mwanadamu. Unapokula chakula chenye mafuta mengi, dawa hii asilia hupambana kuyafanya mafuta hayo yasitengeneze seli za mafuta mwilini mwako. Hali hii huuepusha mwili wako kuhifadhi mafuta yasiyo hitajika mwilini.
  4. Husaidia kupunguza uzito wa mwili kwa haraka sana endapo itatumika pamoja na diet ya kabechi.

  UFANISI WA DAWA.
  Ufanisi wa dawa hii ni wa asilimia mia moja. Dozi ya dawa hii hutumika kwa muda wa siki ishirini na moja.

  MATOKEO YA DAWA:Dawa hii huondoa kabisa kitambi ndani ya siku kumi na nne.

  BEI YA DAWA : Dawa hii inaoatikana kwa kiasi cha SHILINGI ELFU HAMSINI TU (Tshs. 50,000/=)

  MAHALI TUNAPO PATIKANA.
  Tunapatikana jijini DAR ES SALAAM, katika eneo la TABATA -MAKOKA karibu na SHULE YA SEKONDARI YA MT.ANNUARITE.

  KWA WATEJA WASIO WEZA KUFIKA OFISINI KWETU.
  Kwa wateja wasio weza kufika ofisini kwetu Tabata, tunao utaratibu wa kuwafikishia dawa mahali popote walipo ndani ya jiji la Dar Es salaam.

  KWA WATEJA WA NJE YA DAR ES SALAAM.

  Kwa wateja waliopo nje ya Dar Es salaam, tunawatumia dawa kwa njia ya MABASI.
  Kwa wateja wa ZANZIBAR tunawatumia dawa kwa njia ya boti.

  KWA WATEJA WA NJE YA NCHI:
  Kwa wateja wa nje ya nchi, tunatumia dawa kwa njia ya POSTA au DHL.
  WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA : 0766 53 83 84
  TUTEMBELEE: www.neemaherbalist.blogspit.com

  0 0

  Meneja wa benki ya Exim Tanzania  tawi la Zanzibar Bw. Mwinyimkuu Ngalima akimkabidhi seti ya jezi mwakilishi kutoka timu ya soka yaa Kid Boys ya visiwani humo ikiwa ni sehemu ya udhamini wa mashindano yaliyolenga kuibua vipaji vya mchezo huo yaliyohitimishwa kwenye Uwanja wa Abeid Amani Karume, wilayani Mwanakwerekwe hivi karibuni.
  Waziri wa Kazi na Huduma za jamii, Zanzibar  Mh.Ali Suleiman (mwenye suti ya kaki) akikabidhi kikombe cha ushindi kwa Nahodha wa timu ya soka ya Feza ambayo ilifanikiwa kuibuka mshindi kwenye mashindano yaliyolenga kuibua vipaji vya mchezo huo yaliyohitimishwa kwenye Uwanja wa Abeid Amani Karume, wilayani Mwanakwerekwe hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa kutoka benki ya Exim Tanzania (wadhaamini) pamoja na waandaaji wa mashindano hayo.

  Baadhi ya Maofisa kutoka benki ya Exim Tanzania, wakisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Kid boys ya visiwani Zanzibar kabla ya kuanza kwa mchezo uliozikutanisha timu hiyo dhidi ya timu ya Feza ya visiwani humo pia kwenye mashindano yaliyolenga kuibua vipaji vya mchezo huo yaliyohitimishwa kwenye Uwanja wa Abeid Amani Karume, wilayani Mwanakwerekwe hivi karibuni. Timu ya Feza ilibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Kid boys.

  Zanzibar, Benki ya Exim Tanzania imeahidi kuunganisha nguvu zaidi na mamlaka za kimichezo visiwani Zanzibar katika kuhakikisha sekta ya michezo visiwani humo inakua zaidi.

  Hatua hiyo ya benki ya Exim ilitangazwa na Meneja wa tawi la benki hiyo visiwani humo Bw.Mwinyimkuu Said Ngalima wakati wa kilele cha mashindano ya soka yaliyolenga kuibua vipaji vya mchezo huo yaliyohitimishwa kwenye Uwanja wa Abeid Amani Karume, wilayani Mwanakwerekwe kwa udhamini wa benki hiyo.

  “ Kutokana na jitihada zinazoonyeshwa na mamlaka za michezo sambamba na Serikali tumeona na sisi pia tuna haja ya kuunga mkono jitihada hizi hasa katika kuibua vipaji ikiwa ni sehemu ya mpango wetu wa kushirikiana na jamii.’’ alisema Bw. Ngalima.

  Benki hiyo ilikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi tofauti ikiwemo seti mbili za jezi kwa timu zilizoingia fainali, zawadi kwa mchezaji bora, goli kipa bora na muamuzi bora. Pia benki hiyo ilitoa zawadi kwa mchezaji aliyeonyesha kipaji zaidi.

  Fainali hiyo ilivutia mashabiki wengi wakiwemo viongozi wa serikali wilayani humo na maeneo jirani wakiongozwa na Waziri wa Kazi na Huduma za jamii, Mh.Ali Suleiman ambapo hadi mwisho wa mchezo timu ya Feza iliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wapinzani wao timu ya Kid Boys.

  Akizungumza mara tu baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi Mh. Suleiman mbali na kuipongeza benki ya Exim kwa udhamini wa mchezo huo pia alitoa wito kwa mashirika na taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi ili kusaidia sekta ya michezo visiwani humo.

  0 0


  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika nje ya jengo la CCM mkoa mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, June 18, 2015 alipokuja kutafuta wadhamini ambapo alipata jumla ya wadhamini 33,780 mkoani Kilimanjaro.
  Kiongozi wa dini ya kiislam akimuombea Lowassa.

  Kiongozi wa dini ya kikristo akimuombea Lowassa.

  Edward Lowassa akiingia huku akisindikizwa na mamia ya watu mkoani Kilimanjaro.

  Baadhi ya wakazi wa mkoani Kilimanjaro waliokuja kumlaki Edward Lowassa.


  Mheshimiwa Edward Lowassa akiwahutubia wananchi wa mkoani Kilmanjaro waliokubali kumdhamini.

  Edward Lowassa akisalimiana na Lenard Minja.

  Edward Lowassa akisaini daftari la wageni ndani na jengo la CCM mkoa, Kilimanjaro.

  Mamia ya wakazi wa mkoani Kilimanjaro waliokuja kumdhamini Edward Lowassa.

  Mamia ya wakazi wa mkoani Kilimanjaro waliokuja kumdhamini Edward Lowassa.
  Wakazi wa mkoani Kilimanjaro waliokuja kumdhamini Lowassa.


  Na Joshua Fanuel.
  KILIMANJARO Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa aliyeianza safari ya matumaini katika uwanja wa michezo wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha Mei 30, 2015 kwa kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumteua kugombea urais wa Tanzania.


  Jana June 18, 2015 aliwasilili mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro kusaka wadhamini ambapo kwa taratibu za katiba mgombea anatakiwa kupata jumla ya wadhamini 450 katika mikoa 15 ya Tanzania.

  Mheshimiwa Edward Lowassa amepata wadhamini  kutoka katika majimbo yafuatayo, Moshi Vijijini 11564, Rombo 6615, Hai 1854, Siha 9860, Moshi Mjini 1184, Same 1600, Mwanga 1103. Jumla ya wadhamini ni 33,780 kutoka katika mkoa wa Kilimanjaro.

  Katika kuwashukuru wakazi wa mkoani Kilimanjaro waliomdhamini na wale walioacha shuhuli zao na kwenda kuungana nae katika safari ya matumaini, Lowassa alisisitiza kuwa anauchukia umasikini na akipewa ridhaa ya kuongoza nchi hii atahakikisha anatokomeza umasikini, pia aliwaahidi wakazi wa Kilimanjaro kuwa mwezi wa kwaza wa utawala wake ataanza na mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha amefufua viwanda vilivyofungwa ili vijana waweze kupata ajira.

  Aliendelea kuwasisitizia kwa wale wenye sifa za kujiandikisha waweze kujiandikisha mapema kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili siku ya uchaguzi ikifika waweze kufanya maamuzi kwani wanachi ndio wenye maamuzi ya kuchagua kiongozi wanaomuhitaji.

  Pia Mhesimiwa Lowassa alisema endapo atachaguliwa kuiongoza nchi ya Tanzania atahakikisha nchi nzima kuanzia viongozi mpaka wananchi wanakimbia mchakamchaka katika kufikia malengo na kwa yeyote ambaye hatakua tayari kukimbia mchaka mchaka katika kuleta mafanikio atamuweka pembeni na kupisha wale walio tayari kwa mchaka mchaka kuendelea kuijenga nchi ya Tanzania.
  Kawaida:

  0 0

   
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wazee na Viongozi wa Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ kabla ya kuzungumza nao kujadili tatizo la migogoro ya Ardhi.
   Baadhi ya Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ wakimsikiliza Balozi Seif hayupo pichani wakati wa kujadili changamoto zinazowakabili za migogo ya Ardhi { Hifadhi ya Misitu } ndani ya Shehia hizo.Wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Kusini Bi Kibibi Mwinyi Hassan.
  Balozi Seif akizungumza na Wazee na Viongozi wa Muyuni “A “ na Muyuni “ B “ baada ya kupokea changamoto zinazowakabili za migogoro ya ardhi. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkopa wa Kusini Unguja Dr. Idriss  Hijja na Kushoto yake ni Mwenyekiti wa Kikao hicho Diwani Mstaafu wa Muyuni Bwana Abdulla  Hija Abdulla.  Picha na – OMPR – ZNZ.  Na Othman Khamis Ame
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haipendelei kuona Wananchi katika baadhi ya shehia wanalumbana na kufikia hatua ya kuhitilafiana katika mambo ambayo wakiamua kukaa pamoja katika kuyajadili kwa njia ya vikao  yanaweza kurekebishika bila ya kutumika nguvu za Serikali Kuu.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wazee na Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “B” katika kikao cha kujadili matatizo yaliyojitokeza baina ya Wananchi dhidi ya viongozi wao wa shehia hizo.

  Balozi Seif Ali Iddi alisema tabia ya baadhi ya wananchi hasa Vijana kutumia njia ya mkato katika maamuzi yao ya  kurejesha Kadi za uanachama ni udhaifu unaofa kuepukwa kwa vile hauwezi ukatoa suluhu ya tatizo linalolalamikiwa na Wananchi hao.

  Alisema maisha ya amani na utulivu ndio yanayotegemewa  na Serikali Kuu kuendelea kushamiri ndani ya Shehia hapa nchini ambazo zinawajibika kufanya kazi kwa umakini.

  Balozi Seif alieleza kuwa  Sheha wa Shehia yoyote ile hapa Zanzibar ni mtumishi wa Serikali kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar asiyepaswa kuhusika na vitendo vinavyoashiria vurugu ndani ya eneo lake.

  Mapema  Diwani Mstaafu wa Wadi ya Muyuni Bwana Abdulla Hijja Abdulla ambae ndie mwenyekiti wa Kikao hicho alielezea matatizo mengi yanayowasumbuwa Wananchi hao wa Muyuni  “ A “ na Muyuni “ B “ hasa lile la hifadhi ya msitu ambalo waliamuwa kuianzisha kwa hatma yao ya baadaye.

  Bwana Abdulla alisema uchelewaji wa kuchukuliwa hatua  za kisheria katika ngazi za Shehia, Wilaya na Mkoa dhidi ya  watu waliomua kuvamia hifadhi hiyo ndilo tatizo kuu lililoibua mtafaruk kati ya Wananchi hao wa Uongozi wa Shehia hizo.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Kusini Nd. Khamis Jabir Makame alisema alilazimika kulitembelea eneo la Mgogoro wa Ardhi katika eneo la Hifadhi ya Muyuni  muda mfupi uliopita ili kujionea hali halisi ya kile kinacholalamikiwa.

  Nd. Jabir alikieleza kikao hicho kwamba akiwa pamoja na Viongozi wenzake wa Wilaya alibaini kuwepo kwa miti ya kudumu iliyooteshwa kwa muda mrefu katika eneo hilo pamoja na Miti ya matunda ambayo tayari imeaanza kuzaa.
  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

  0 0


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 100
  TAREHE 19 JUNI, 2015
  TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza na timu ya Taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainaili za wachezaji wa ndani CHAN 2016.

  Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kuanzia majira a saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

  Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo wa awali ili kujiweka katika mzingira mazuri ya kusonga mbele, kabla ya mchezo wa marudaino utakaofanyika baada ya wiki mbili jijini Kampala.

  Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema vijana wake wako katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti katika mchezo huo.

  Endapo Stars itaitoa Uganda katika hatua ya awali, itafuzu katika hatua ya pili ambapo itacheza dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan, na mshindi wa mchezo huo moja kwa moja atafuzu kwa fainali za CHAN 2016 nchini Rwanda.

  Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili leo mchana jijini Dar es salaam kisha kuelekea kisiwani Zanzibar tayari kwa mchezo huo wa kesho dhidi ya Taifa Stars.

  TWFA KUFANYA UCHAGUZI AGOSTI 15
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA), George Mushumba ametangaza uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika agosti 15, 2015 kujaza nafasi mbalimbali.

  Kwa mamlaka aliyonayo anapenda kutangaza uchaguzi mkuu wa TWFA leo kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi, uchaguzi huo utafanyika tarehe 15, Agosti 2015 katika nafasi zifuatazo:
  1. Mwenyekiti
  2. Katibu Msaidizi
  3. Mweka Hazina
  4. Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.       

  Fomu za kuomba nafasi hizo zitaanza kutolewa tarehe 19-23 Juni 2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.

  Kalenda ya Uchaguzi wa TWFA imeambatanishwa:

  JEDWALI NAMBA MOJA (1)
  KALENDA YA MATUKIO YA UCHAGUZI YA TWFA

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Nasir Abu Jaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 19, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Nasir Abu Jaish, anayemaliza muda wake wa kazi nchini wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 19, 2015 kwa ajili ya kumuaga
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Nasir Abu Jaish, anayemaliza muda wake wa kazi nchini,  wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 19, 2015 kwa ajili ya kumuaga. Picha na OMR

  0 0


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Bw. Clement Mshana, wafanyakazi wake na waandishi wote kwa ujumla kufuatia kifo cha mtangazaji na mwandishi mwandamizi wa TBC Bi. Florence Dyauli.
  “Pokea rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na mwandishi mwandamizi na mahiri Bi. Florence” Rais amesema.

  “Mbali na uandishi na utangazaji wake mahiri, Bi. Florence alikua mzalendo wa kweli aliyetumikia taasisi hii ya serikali kwa uadilifu na upendo wa kweli, tutamkumbuka na tutaukosa mchango wake. 

  Ni wajibu wetu kumuombea mapumziko mema kwa mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa mchango wake alioutoa kwa moyo wa dhati”. Amesema Rais Kikwete na kuongeza kuwa: 

  “Hakika Florence tutamkumbuka, nawapa pole wafanyakazi wote wa TBC na waandishi wote kwa kuondokewa na mwenzao katika tasnia ya Habari”. Rais ameongeza.

  “Salaam pia ziwafikie ndugu na jamaa wa Bi. Florence ambao msiba huu ni mkubwa sana kwao na unawagusa sana, naelewa machungu waliyonayo na huzuni, hata hivyo kwa pamoja ni wakati wa kuzidi kumuombea Marehemu katika safari yake ya mwisho”. 

  Rais amesema na kuwatakia roho ya subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwao.

  Bi. Florence ambaye amefariki jana  18 Juni, 2015 jijini Dar-es-Salaam alizaliwa Julai 27, 1961. Bi. Florence alianza kazi katika Radio ya Taifa, Radio Tanzania Dar-es-Salaam (RTD) na baadaye  Televisheni ya Taifa (TVT) na kwa sasa TBC .

  Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amina.
  Imetolewa na:
  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
  Ikulu-DSM
  19 Juni, 2015

  0 0

  Wafanya biashara wadogo huamini kwamba kua na tovuti ni kitu kinachofanywa na wafanya biashara wakubwa na inaitaja gharama nyingi kutengeneza. Hilo sio kweli. Gharama ya kuwa na website ni ndogo sana ukilinganisha na faida utakazo zipata baada ya kuwa nayo. Faida ya kuwa na tovuti ni pamoja na; Biashara yako kuaminika kitaifa na kimataifa. Biashara zote zilizo halisi na zinazoaminika hua na tovuti. 

  Tovuti yako itasaidia kuhalalisha biashara yako. Kuwa na tovuti pia itakusaidia kujitangaza kwa bei rahisi sana kuliko utangazaji wa magazeti, radio, mabango na mwingine wowote.  Kwa kuwa tovuti ipo mtandaoni masaa 24 na mahali popote hivyo basi wateja wako wataweza kukuona mahali popote watakapo kuwa na kwa muda wowote. 

  Pamoja na hayo mabadiliko yoyote yatakayo tokea kwenye biashara yako yanaweza kusambazwa kiurahisi kwa wateja wako. Ukiongeza bidhaa unazo uza, ukiongeza au ukibadalisha huduma unazozitoa nk. wateja wako wanapata huu ujumbe kiurahisi bila gharama zozote kwako.  

  Kutengenezea tovuti ya biashara yako, tumia wasajili wa tzNIC wenye vibali vinavyokubalika: http://www.tznic.or.tz/index.php/registrars/accredited-registrars.
  Au, unaweza kwenda moja kwa moja kwenye tovuti ya tzNIC. Kama una maswali zaidi tembelea kurasa zao za Facebook na Twitter

  0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiweka shada katika kaburi la mpigania uhuru na muasisi wa taifa la India Mahatma Ghandi jijini New Delhi India leo asubuhi
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India kwa sherehe za ukaribisho wake rasmi nchini India kwa ajili ya ziara yake ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika asubuhi ya leo, Ijumaa, Juni 19, 2015.


   Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu wa IndiaMheshimiwa Narendra Modi, na Rais Wa IndiaMheshimiwa Pranad Mukherjee wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Rais kikwete kuwasili katika ikulu ya India kwa mapokezi rasmi

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono  na Rais wa India, Mheshimiwa Pranad Mukherjee (kushoto) na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Narendra Modi katika sherehe za kumkaribisha nchini India kwa ziara rasmi ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika Ikulu ya India mjini New Delhi, asubuhi ya leo.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Majeshi ya India liliandaliwa kwa ajili ya kumkaribisha kwa ziara rasmi ya Kiserikali nchini India katika sherehe za ukaribisho zilizofanyika asubuhi ya leo.
  Picha na Freddy Maro

  0 0


   Masanja Mwinamila (44) mara baada ya kufikishwa katika kituo cha Polisi Wilaya ya Nzega Juni 15, 2015.
   Mtoto Margreth Hamisi Machiya (6) aliyenusurika kuuzwa akiwa hai na mjomba wake.
  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Juma Bwire akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo Juni 16, 2015.

  Na Daniel Mbega, Nzega.
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Nzega leo hii imemhukumu Masanja Mwinamila (44), mkazi wa Kitongoji cha Kona Nne, Kijiji cha Ugembe II, Kata ya Mwakashanhala, Tarafa ya Puge wilayani Nzega katika Mkoa wa Tabora kwenda jela miaka 10 kwa kosa la kuteka mtoto mwenye albinism, Margreth Hamisi (6).

  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Saraphine Nsana, alitoa hukumu hiyo baada ya mshtakiwa kusomewa shtaka na kukiri kutenda kosa hilo.

  Ilielezwa mahakamani hapo kwamba, mnamo Juni 15, 2015 majira ya saa 3:00 usiku katika Kijiji cha Ugembe II, Kata ya Mwakashanhala wilayani Nzega, mtuhumiwa alimteka binti huyo kwa lengo la kwenda ‘kumuuza’ ili ajipatie fedha (kiasi kimehifadhiwa).

  Hii ni mara ya kwanza kwa kesi inayohusisha utekaji nyara, kujeruhi na mauaji dhidi ya watu wenye albinism kuchukua muda mfupi zaidi, kwani ndiyo kwanza kesi hiyo ya Jinai Namba 116/2015 imefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kutolewa hukumu.

  Jitihada za Polisi
  Mafanikio ya kukamatwa kwa Masanja Mwinamila akiwa katika harakati za kutaka kumuuza mtoto Margreth Hamisi, ambaye ni mpwa wake, yametokana na umakini wa Jeshi la Polisi nchini ambapo maofisa wake wa Kikosi Kazi cha Taifa waliweka mtego na kufanikiwa kumnasa mtuhumiwa kabla hajamdhuru mateka wake.
  Tukio hilo limefanikisha kuubomoa mtandao hatari wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kwani ni takriban wiki tatu tu tangu maofisa usalama walipofanikiwa kuwanasa watu wengine sita wakiwa katika harakati za kuuza mifupa inayodhaniwa kuwa ya binadamu (albino) mjini Kahama Mei 22, 2015 ambapo tayari wamekwishafikishwa mahakamani pamoja na wengine watatu waliokamatwa baadaye.
  Matukio hayo mawili makubwa yaliyotokea katika kipindi hicho yamedhihirisha namna serikali kupitia jeshi hilo na vyombo vingine vya usalama inavyoshughulikia mitandao hiyo hatari usiku na mchana ili kuhakikisha Watanzania wote wanaishi kwa amani na usalama.


  0 0

   Mkurugenzi wa Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Stephen Kilindo (kulia), akikabidhi mfano wa hundi ya Dola 24,000 za Kimarekani kwa Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita, Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga na wafugaji wa mbuzi wa maziwa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Mwanza. Fedha hizo zimetolewa na Kampuni SABMiller tanzu ya TBL.
   Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorice Malulu (kulia), akifafanua jambo kuhusu msaada uliotolewa na Kampuni hiyo kwa ACE Afrika kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Mwanza. Wengine ni Meneja wa Fedha na Utawala wa ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita (kushoto) na Mkurugenzi wa Sheria TBL, Stephen Kilindo.
   Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kupokea mfano wa hundi ya Dola 24,000  za Marekani zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga katika mikoa ya Arusha,

  Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kupokea mfano wa hundi ya Dola 24,000 za Marekani zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga katika mikoa ya Arusha, 

  0 0

   
   Wanahisa, Bodi ya Wakurugenzi na MenejimentI ya ECOBANK  wakishiriki Mkutano Mkuu wa mwaka  wa benki hiyo uliofanyika katika  Ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre uliofanyika jijini Dar es Salaam  19 June 2015. 

   Wanahisa, Bodi ya Wakurugenzi na MenejimentI ya ECOBANK  wakishiriki Mkutano Mkuu wa mwaka  wa benki hiyo.
  Bodi ya Wakurugenzi na MenejimentI ya ECOBANK  wakishiriki Mkutano Mkuu wa mwaka  wa benki hiyo
   Wanahisa na MenejimentI ya ECOBANK  wakishiriki Mkutano Mkuu wa mwaka  wa benki hiyo.
   Mkutano ukiendelea
  Wanahisa, Bodi ya Wakurugenzi na Menejiment ya ECOBANK  wakishiriki Mkutano Mkuu wa mwaka  wa benki hiyo

  0 0

  Na Mwandishi wetu,Globu ya Jamii
  KUONGEZEKA kwa ndoa za utotoni inatokana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kuendelea kutumika wakati hali yake ni mbaya kwa watoto wakike kushindwa kufikia ndoto zao.
  Akizungumza na katika mdahalo wa Nijali uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Regency ,Mratibu wa Utetezi Taifa ,SOS Tanzania/Zanzibar ,John Batista amesema  kuongezeka kwa mimba za utotoni inatokana na sheria ya ndoa kuendelea kutumika.
  Amesema kuwa kuendelea kwa mimba za utotoni pamoja kuolewa kunatokana sheria kutamka kuwa mtoto anaweza kuolewa kwa miaka 14 kwa ridhaa ya wazazi.
  Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu (UNFPA) inaonyesha watoto 1,3822 ambao wamezaliwa katika mwaka 2005  na 2010 ifikapo 2030 watakuwa wameolewa chini ya miaka 18.
  Katika ripoti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaonyesha wasichana 8000 wanapata ujauzito wakiwemo wanafunzi wa Shule ya msingi 3000 na ,sekondari 5000.
  Mratibu wa C-SEMA,Michael Kihongoh amesema kampeni hii ni endelevu na waandishi wametakiwa kuweka kipaumbele kupigania sheria ya ndoa ya mtoto kuondolewa kabisa ili watoto wa wakike waweze kulindwa.
  Amesema kuwa watoto wa kike wako katika hatari ambapo elimu inatakiwa kutolewa kwa jamii ikiwemo malezi kwa waoto wa kike wasiweze kuingia katika vishawishi.
  Mratibu wa Utetezi Taifa, SOS Tanzania/Zanzibar, John Batista, akizungumza katika Mdahalo wa Nijali uliolenga ndoa za utotoni na mimba za utotoni  kwa kushirikisha Chama cha Waandishi wa Habari za Watoto, (TAJOC) na wengine, uliofanyika leo katika Hoteli Regency jijini Dar es Salaam.
   Mshauri Mkuu Mwandamizi na Msimamizi wa Huduma ya Simu kwa Mtoto wa C-SEMA, Fatuma Ahmad akizungumza na waandishi wa habari katika mdahalo wa Nijali uliofanyika katika leo Hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam.
   Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Watoto (TAJOC), Chalila Kibuda akizungumza na waandishi wa habari katika mdahalo wa Nijali uliofanyika katika leo Hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam.
  Washiriki wa Mdahalo wa Nijali  ulioshirikisha Chama cha Waaandishi wa habari za Watoto (TAJOC) na wadau wengine uliofanyika leo katika Hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mwenyekiti  wa  Chama cha Wajane Tanzania, Rose Sarwatt akizungumza na waandishi  wa habari hawapo pichani  juu maazimisho siku ya wajane Duniani itakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jeshini jijini Dar es Salaam Juni 23 mwaka huu. 

  Maadhimisho hayo yatalenga  kusaidia wajane kisheria, kupata elimu pale wanapo kwama  kushawishi  jamii kuandaa wosia ili kupunguza  au kuondoa usumbusu. Kulia ni  Katibu Chama cha Wajane Tanzania John Shabani  mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa idala ya Habari MAELEZO leo Jiji Dar es Salaam.
   Katibu Chama cha Wajane Tanzania John Shabani  akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu  kutoa fursa ya kuzungumzia matatizo yanayowakumba wajane hasa wanawake na watoto wao ili kurejesha haki zao na kupambana na umaskini kwa kuwezeshwa.Kushoto ni
  Mwenyekiti  wa  Chama cha Wajane Tanzania, Rose Sarwatt.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika kikao mkutano wa chama cha wajanae hapa nchini mkutano ulifanyika katika ukumbi wa idala ya Habari MAELEZO leo Jiji Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka.)

  0 0

   January Makama akiweka saini kitabu cha wageni alipotua  mkoani Tabora kusaka wadhamini. Kulia ni mkewe na kushoto ni mmoja wa viongozi wa CCM mkoani humo
   January akilakiwa na wazee wa Tabora 
   Mke wa January akimpigia debe mumewe mjini Tabora
   January akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga na kutoa shukrani kwa wananchi wa Tanga kwa kujitokeza kwa wingi kumdhamini na kumsikiliza


  0 0

   .Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya kushoto Akishirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa World Lung Foundation(wa pili kushoto)Dr Nguke Mwakatundu kukata utepe wakati wa Uzinduzi wa Nyumba za Watumishi wa Afya katika kituo cha Afya Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.
   Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya  akikata utepe Ikiwa ni Ishara ya ufunguzi wa Nyumba zilizo jengwa kwa hisani ya WLF kwa ajili ya watumishi wa Afya katika kituo cha Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.
   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  Kanali Mstaafu Issa Machibya akikagua moja ya Nyumba za Watumishi wa Afya zilojengwa kwa hisani ya WLF Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  Kanali Mstaafu Issa Machibya(wa tatu kushoto)akifatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WLF Dr Nguke Mwakatundu katika picha ya pamoja na Baadhi ya wataalamu wa Afya Wilayani Uvinza Mkoani.

  0 0

  Mkurugenzi Idara ya Uratibu Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mjini Dodoma, tarehe, 19 Juni, 2015.02
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho akisisitiza jambo wakati akitoa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mjini Dodoma.03
  Washiriki wa  mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo na  Mkurugenzi Idara ya Uratibu Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery    (mwenye tai nyekundu waliokaa) Mjini Dodoma.

  …………………………………………
  Na. Mwandishi wetu.
  Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa imeandaa mafunzo ya kujikinga na maafa kwa watumishi wa umma ili wapate uelewa wa mbinu za kujiandaa na kukabiliana na maafa hususan katika sehemu zao za kazi.
  Akiongea wakati wa Ufunguzi wa mafunzo ya menejimenti ya maafa mjini Dodoma, Tarehe 19, Juni 2015, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu aliyewakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, Obbey Assery, alieleza kuwa wameanza kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu na watumishi wengine watajengewa uwezo wa Menejimenti ya maafa.
  “Tumeanza na ofisi yetu na baadae watumishi wengine watapata mafunzo haya ili tuweze kuwajengea uelewa na ujuzi wa kukabili maafa husususan katika sehemu zao za kazi. Kumekuwepo na majanga ambayo huwapata watumishi wa umma wakiwa kazini kama vile; moto, matetemeko na ajali lakini kwa kuwa na uelewa wa menejimenti ya maafa hayo tunaweza kuwa na uwezo wa kukabili na kupunguza athari za maafa hayo” alisema Asserry.
  Awali akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kufungua Maonesho hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Msuya amesema kuwa pamoja na kuwajengea uwezo wa menejimenti ya maafa watumishi hao, alibainisha kuwa kila mshiriki hana budi kuifikisha elimu hiyo aliyoipata kwa jamii inayomzunguka.
  Washiriki wa mafunzo hayo wanafundishwa kuhusu ; Dhana ya Menejimenti ya Maafa Mfumo wa Menejimenti ya Maafa Nchini, Huduma ya Kwanza kwa Jamii Uratibu na Udhibiti wa eneo la Maafa na Kujianda na Kukabiliana na dharura ya Moto.
  Mafunzo hayo yameendeshwa na Idara ya Menejementi ya Maafa ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na wawezeshaji wengine kutoka Jeshi la Polisi, Jeshi la Zima Moto na Uokoaji pamoja na Taasisi ya Ultimate Security Ltd, kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo Duniani (UNDP) kupitia miradi inayoratibiwa na Ofisi hiyo ya Menejimenti ya Maafa na Mfumo wa taarifa za tahadhari za mapema nchini.

  0 0

   Waziri wa Fedha wa Tanzania, Bi Saada Mkuya(wa tano kutoka kushoto waliokaa) na Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano wa Zambia(wa sita kutoka kushoto),wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika hafla ya kusaini makubaliano ya kurahisisha uchukuzi wa abiria na mizigo. Leo mchana mjini Dodoma.Kushoto kwa Waziri Mukanga ni Naibu Waziri wa Fedha wa Tanzania, Bw Adam Malima.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akisistiza jambo kabla ya tukio la kusaini makubaliano ya Kurahisisha Uchukuzi wa mizigo na abiria kati ya  nchi hizo mbili, leo mchana katika ukumbi wa St Gasper, mjini Dodoma.
   Waziri wa Fedha, Bi Saada Mkuya akijadili jambo na Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano wa Zambia, Bw. Yamfwa Mukanga, kabla ya kusaini makubaliano ya kurahisisha uchukuzi wa abiria na mizigo, leo mchana katika ukumbi wa St Gasper mjini Dodoma.
   Waziri wa Fedha wa Tanzania, Bi Saada Mkuya, na Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano wa Zambia, Yamfwa Mukanga wakisaini hati ya makubaliano ya kurahisisha uchukuzi wa mizigo na abiria katika nchi hizo mbili, , leo mchana katika ukumbi wa St Gasper mjini Dodoma huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha Tanzania, Adam Malima( wa kwanza kulia waliokaa), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile (wa tatu kutoka kulia waliosimama), Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa pili kutoka kulia waliosimama) na wataalam kutoka Tanzania na Zambia.

  Baadhi wa wadau wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano wa Zambia, Bw. Yamfwa Mukanga (hayupo pichani),   wakati akitoa hotuba yake kabla ya kusaini makubaliano ya kurahisisha uchukuzi wa abiria na mizigo kati ya Tanzania na Zambia, leo mchana katika ukumbi wa ST Gasper mjini Dodoma leo mchana. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)     

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka (kushoto), akimkaribisha Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano wa Zambia, Yamfwa Mukanga, wakati alipofika mjini Dodoma kusaini makubaliano ya kurahisisha uchukuzi wa Mizigo na abiria kati ya nchi hizo mbili. Makubaliano hayo yamesainiwa leo mjini Dodoma katika ukumbi wa St. Gasper kati ya Serikali ya Tanzania na Zambia.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Suleiman Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari katika banda la mamlaka hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na TAA pamoja na miradi yao.
   Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Laurent Mwigune (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu shughuli zinazofanywa na TAA.
   Kamanda Msaidizi wa Kikosi cha Zimamoto Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Kamishna Msaidizi, Mpemba Magogo (katikati), akizungumza na waandishi habari kuhusu kazi za uokoaji pale unapotokea moto. Kulia ni Koplo, Brian John wa Kikosi hicho cha Zimamoto.
   Koplo, Brian John wa Kikosi hicho cha Zimamoto katika uwanja huo akionyesha zana zake za kazi za kuzimia moto.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Suleiman Suleiman (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wake kwenye banda lao.
   Wafanyakazi wa idara mbalimbali wa TAA wakiwa katika picha ya pamoja katika maonyesho hayo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Suleiman Suleiman akiondoka baada ya kuzungumza na wanahabari.


  Na Dotto Mwaibale

  MAMLAKA  ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imesema  upanuzi wa jengo la tatu wa awamu ya pili katika viwanja vya ndege nchini unatarajia kukamilika mwakani, utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 7.5 kwa siku.

  Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo asubuhi na Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi Suleiman Suleiman, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Alisema mwanzoni viwanja hivyo vilikuwa na uwezo wa kuchukua watu milioni 1.5 kwa siku, lakini kwa sasa uwezo wake ni watu milioni 2.5, hivyo kukamilika kwa mchakato huo kutarahisisha kusafiri kwa urahisi kwenda sehemu yoyote ya nchi iwe ndani na nje.

  "Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza utaufanya kuwa wa kimataifa, ndege zitakuwa zikitoka Mwanza na kwenda Ulaya hadi mataifa mengine, itapunguza gharama za usafirishaji na kumsaidia mwananchi wa kawaida kumudu gharama," alisema.

  Aliongeza, ili kudhibiti uingizwaji wa madawa ya kulevya katika viwanja vya ndege, wameweka kamera maalumu zitakazosaidia kutambua mizigo ambayo si salama.

  Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Kikosi cha  Zimamoto na Uokoaji katika viwanja hivyo, Mpemba Magogo, alisema Watanzania wanatakiwa kutambua kuwa, usalama upo katika maeneo hayo, hivyo wasiwe na hofu.


  Alisema kuna baadhi ya changamoto kama kukua kwa teknolojia hivyo, inatakiwa uwanja huo kuwa na vifaa vya kisasa vya kutosha. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)


  0 0


older | 1 | .... | 559 | 560 | (Page 561) | 562 | 563 | .... | 1897 | newer