Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

WAZIRI MEMBE ASHIRIKI MAZISHI YA MUFTI ISSA SHABAN BIN SIMBA

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe  akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Mufti mkuu Issa Shaban Bin Simba wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Nguzo Nane mjini humo Juni 16.2015.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe  akitoa neno kwa umati wa waombolezaji katika msiba wa Mufti mkuu Issa Shaban Bin Simba nyumbani katika Mtaa wa Majengo mjini Shinyanga, baada ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Nguzo Nane mjini humo Juni 16.2015.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe  akisindikizwa na Askofu Liberatus Sangu baada ya kumaliza mazishi ya marehemu Mufti mkuu Issa Shaban Bin Simba nyumbani katika Mtaa wa Majengo mjini Shinyanga Juni 16.2015.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe  akisalimiana na wananchi baada ya weka udongo kwenye kaburi la marehemu Mufti mkuu Issa Shaban Bin Simba wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Nguzo Nane mjini humo Juni 16.2015.

JK AONGOZA MAELFU YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA SHEIKH MKUU

$
0
0



Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, likitolewa nyumbani kwake, tayari kwa safari ya kwenda msikitini kuswaliwa na baadae kwenye mazishi, yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ugongo kwenye Kaburi la Marehemu Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, aliezikwa leo Juni 16, 2015 kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.
Masheikh kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wakimzika Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban bin Simba, aliezikwa leo Juni 16, 2015 kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akiweka ugongo kwenye Kaburi la Marehemu Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, aliezikwa leo Juni 16, 2015 kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiweka ugongo kwenye Kaburi la Marehemu Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, aliezikwa leo Juni 16, 2015 kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa Mazishi ya Marehemu, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, Mbaraka Simba wakati kwenye Makaburi ya Waislam ya Nguzo Nane, Mkoani Shinyanga leo Juni 16, 2015.

KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA WILAYA YA BUKOMBE MKOAN GEITA.

$
0
0
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukivuka mto kuelekea katika kijiji cha Ilyanchele wilayani Bukombe wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika wilaya hiyo kuelekea katika kijiji hicho hata hivyo msafara huo haukuweza kuvuka mto mkubwa wa Ilyamchele na magari  kutokana na kutokuwepo kwa daraja linalounganisha kijiji hicho ambapo leo ndiyo limewekwa  jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo  na Ndugu Abdulrahman Kinana.

Baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo Kinana pamoja na msafara wake walivuka mto huo kwenye daraja la miti lililotengenezwa kwa nguvu za wananchi.  kisha alipanda pikipiki na kuelekea katika mkutano mdogo na wananchi wa kijiji cha Ilyanchele ambacho kimo katika msitu wa akiba  kata ya Nyamonge wilayani Bukombe mkoani Geita.


Kinana yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza ambapo baada ya kumaliza ziara yake mkoani Kagera sasa anaendelea na ziara hiyo katika mkoa wa Geita kabla ya kumalizia ziara yake mkoani Mwanza akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akivuka na wananchi katika daraja hilo.
Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia mjini Bukombe,mkoani Geita
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubi Wananchi katika mkutano wa hadhara mjini, Bukombe wakati wa ziara yake mkoani Geita.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akitema chehe katika mkutano wa hadhara mjini, Bukombe wakati wa ziara yake mkoani Geita.
Katibu wa NEC Itikadi  na Uenezi Nape Nnauye akiunguruma katika mkutano wa hadhara mjini Bukombe



Wananchi wakimlaki Katibu Mkuu Kinana kwenye mkutano wa hadhara mjini Bukombe,
Wananchi wakimlaki Katibu Mkuu Kinana alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Bukombe.
 Katibu Mkuu Ndugu Kinana akishiriki kufitisha fremu ya mlango katika vyumba vya madara ya Shule ya Sekondari ya Busonge, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akishiriki kutega mzinga wa nyuki katika Kata ya Iyogelo, wilayani Bukombem Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana  akiwahutubia wachimbaji wadogo wadogo wa madini katika Kata ya Uyovu, wilayani Bukombe, Geita.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wadogo wakitafuta dhahabu wilayani Bukombe.
 Ndugu Kinana akizungumza na wajasiliamali wa uuzaji wa samaki na dagaa katika Soko la Uyovu katika Kata ya Uyovu, wilayani Bukombe.
Wananchi wa Kijiji cha Ilyamchele wakisindikiza kwa ngoma msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Nape Nnauye
 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa chumba cha darasa katika Shule ya Msingi ya Ilamchele, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita.
Sehemu ya chumba cha darasa cha Shulre ya Msingi Ilyamchele, katika Kata ya Namonge, wilayani Bukombe. Ndugu  Kinana baada ya kuona hali hiyo, aliitisha harambee ya ujenzi wa shule hiyo, isiyokuwa na walimu wataalamu
 Ujenzi wa vyumba viwili vya darasa katika Shule ya Msingi ya Ilyamchele ukiendelea, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitumia usafiri wa pikipiki alipokuwa anakwenda Kijiji cha Ilyamchele, Kata ya Namonge ambako aliendesha harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ilyamchele akiwa katika ziara wilayani Bukombe, Geita, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Wananchi wakivuka daraja la Ilyamchele wilayani Bukombe, Geita

Wananchi wakivuka daraja la Ilyamchele wilayani Bukombe, Geita
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akivunja muwa na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Bukombe wakati akirejea mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Ilyanchele.
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akichagua muwa na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Bukombe wakati akirejea mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Ilyanchele.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizindua ujenzi wa wa dara la Ulyamchele,wilayani Bukombe mkoani Geita.
 Gari lililombeba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye likivuka katika moja ya mito katika Kijiji cha Ilyamchele, wilayani Bukombe.
 Msafara wa Komredi Kinana ukivuka katika moja ya mio iliyopo Barabara ya Ilyamchele
Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la CCM  Tawi la Busonzo, wilayani Bukombe 

Niambie Live Show.....Father's Day Special

$
0
0

Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki hii mada ni SIKU YA KINABABA DUNIANI.
Na mgeni mwalikwa ni Mayor Mlima
Ni Niambie Live....
KARIBU

NAIBU WAZIRI WA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI ,ANGELA KAIRUKI ATEMBELEA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)MKOA WA KILIMANJARO

$
0
0

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angela Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa shirika la nyumba la taifa mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya nyumba za NHC zilizoanza kufanyiwa ukarabati.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angela Kairuki akikagua nyumbaza NHC zinazofanyiwa ukarabati zilizoko eneo la Rau.
Naibu Waziri Kairuki akizungumza jambo na Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro ,Sheakh Kombo.
Ofisi za Shirika la Nyumba la Taifa mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza na wafanyakazi wa shirika laArdhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angela Kairuki,kulia kwake ni Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro Sheakh Kombo,
Baadhi ya wafanyakazi wa NHC mkoa wa Kilimanjaro.
Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro ,Sheakh Kombo akizungumza wakati akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Naibu Waziri,Kairuki akifurahia jambo na Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro,Sheakh Kombo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

TANAPA WAKABIDHI MRADI WA UJENZI WA DARAJA KATIKA VIJIJI VYA SINGANA SUNGU WILAYA YA MOSHI VIJIJINI.

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akikata utepe katika daraja hilo kuashiria uzinduzi rasmi wa dara.
RC Gama akipita pamoja na viongozi wengine kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika dara hilo
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kandaya Kaskazini.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akizungumza wakati wa kuzindua rasmi mradi wa daraja uliofadhiliwa na Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya wakazi wa vijiji vya Singa na Sungu wilaya ya Moshi.
Daraja linalotenganisha vijiji vya Singa na Sungu wilaya ya Moshi vijijini ambalo kwa sasa limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo kufika kwa urahisi katika hosptali ya Kibosho.
Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro,Remida Ibrahim akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya mradi huo pamoja na kufanya utambulisho kwa viongozi.
Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Erastus Rufunguro akizungumza katika makabidhiano hayo.

BENKI YA CRDB TAWI LA MLIMANI CITY YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA NA JUMBO JUNIOR ACCOUNT

$
0
0

Baadhi ya Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water Front wakitoa misaada katika kituo cha kulelea watoto wa chini ya miaka minne(4) yatima katika kituo cha Msimbazi Chidrens Home kilichopo Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam jana.

Crediti manaja wa Benki ya CRDB, tawi la Water front, Isaya Lyimo akimpa maelekezo Sista wa kituo cha watoto yatima cha Msimbazi Chidrens Home kilichopo Msimbazi Centre, Sista Anna Marandu mara baada ya wafanykazi wa tawi hilo kutoa msaada wa vitu mbalimbali jijini Dar es Salaam leo. kulia ni Meneja wa Tawi la Water Front Donath Shirima.

watoto wa shule ya Dar es Salaa Interanational school. (DIT) wakifurahia mchezo uliokuwa ukichezwa.

WAZAZI WAMEASWA KUWAPOKEA VIJANA WAO WALIOAMUA KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
 Na mwandishi wetu.
Wazazi wameaswa kuwa tayari kuwapokea Vijana au watoto wao walioamua kuacha matumizi ya dawa za kulevya ili kuwalinda na vishawishi vinavyoweza kutoa nafasi ya kuwarejesha tena kwenye matumizi ya Dawa hizo pamoja pombe haramu.

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi ametoa wosia huo wakati wa kuwapokea Vijana Sita wa Kijiji cha Fujoni walioamua kuacha kutumia Dawa za kulevya na kupata mafunzo watakayoyatumia kuwasomesha wenzao kuachana na Dawa hizo hapo katika Skuli ya Fujoni Wilaya ya Kaskazini “ B “.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema wapo Wazazi na Familia  Nchini ambao bado wanaendelea  na tabia ya kuwatenga Vijana wao walioathirika na Dawa za kulevya kwa kuchelea kufanyiwa matendo ya maudhi kama wizi.

Alisema tabia hiyo inafaa kuachwa kwa vile kama haikutafutiwa ufumbuzi  inaweza kuzalisha zaidi Vijana wanaotumbukia katika matumizi ya Dawa za kulevya na hatimae kuwa na kundi kubwa la  walevi ndani ya Jamii ambao ni nguvu kazi ya Taifa.

Balozi Seif alionyesha furaha yake kutokana na ujasiri  mkubwa ulioonyeshwa na vijana hao wa kuamuwa kuacha matumizi ya Dawa za kulevya na kujitolea kuwa mfano kwa wenzao wenye tabia hiyo.

Wakati huo huo Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif ameukabidhi Uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } shilingi Milioni 5,000,000/-  kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kibanda cha Maji katika Kijiji cha Kinduni. 

Ujenzi wa Kibanda hicho una lengo la kuimarisha miundo mbinu ya upatikanaji wa huduma za Maji safi na Salama ndani ya Kijiji hicho chenye changamaoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

 Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na mmoja kati ya Vijana sita walioamua kuachana na matumizi ya Dawa za Kulevya katika Kijiji cha Fujano hapo katika Viunga vya vya Skuli ya Fujoni. Kati kati yao ni Mwakilishi wa Umoja wa kusaidia mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya na Pombe Tanzania Bwana  Abdulrahman Mohammed Abdulla.
  Mwakilishi wa Umoja wa kusaidia mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya na Pombe Tanzania Bwana  Abdulrahman Mohammed Abdulla akielezea mikakati ya taasisi yake katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya hapa Nchini.
Balozi Seif akizungumza na baadhi ya Wananchi mara ya kukabidhiwa Vijana Sita walioamua kuachana na matumizi ya Dawa za kulevya waliokuwa wakipata mafunzo kwenye Kituo cha Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Sheha wa Shehia ya Fujoni Bwana Said Mgeni Bakari na wa kwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini “ B “ Nd. Hilika Khamis na Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi.
Kijana Ayoub Hussein Ayoub Mmoja kati ya Vijana sita walioamua mkuachana na matumizi ya Dawa za kulevya akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake kuushukuru uongozi wa Jimbo la Kitope kwa kusaidia mbinu na uwezeshaji uliowachangia wao kuacha dawa hizo.
Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi shilingi Milioni 5,000,000/- Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Gharu hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa kibanda cha maji katika kijiji cha Kinduni.

ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI LUKUVI MKOANI LINDI

$
0
0
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisalimiana na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya siku mbili amapo atasikiliza na kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali yenye migogoro katika mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mama Mwantum Mahiza akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika mkoa huo kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mh William Lukuvi mara baada ya Waziri Lukuvi kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mama Mwantum Mahiza muda mfupi baada ya Mama Mahiza kutoa taarifu fupi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa shirika la nyumba la Taifa Mkoa wa Lindi Bw Mussa Patric Kamenda badaa ya mkurugenzi huyo kutoa taarifa kwa Mheshimiwa Waziri jinsi shirika hilo linanvyotekeleza miradi mbalimbali katika mkoa huo.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi (kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mama Mwantum Mahiza (kushoto) kuhusu ujenzi wa nyumba unaofanywa na Shirika la nyumba la Taifa mkoani Lindi. Katikati ni mfanyabiashara wa mkoa wa Lindi Bw Kassim Abdallah ambaye amenunua mojawapo nyumba ambazo zimejengwa na shirika la nyumba la Taifa.
Waziri wa ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akitoa malelekezo kwa Bwana Mussa Patric Kamenda Mkurugenzi wa shirika la nyumba la Taifa Mkoa wa Lindi   namna bora ya kutumia viwanja kwa ujenzi wenye manufaa kwa kulunufaisha shirika hilo.
Picha na Clarence Nanyaro.

BENKI YA NMB YAZINDUA RASMI FAMILIA YA KADI ZA BENKI “MASTERCARD DEBIT” ZINAZOKUBALIKA KIMATAIFA

$
0
0
 Wadau wa benki ya NMB pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumiwa rasmi na benki hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback, akiwahutubia wadau wa Benki ya NMB wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi hiyo mpya ambayo itaanza kutumiwa rasmi na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa bodi, benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard iliyozinduliwa rasmi na benki hiyo katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. (Kulia) ni Afisa wa Master Card kanda ya Afrika ya kati Bw. Michael Mieback aliyehudhuria mkutano huo.
  Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker (katikati) pamoja na Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback, (kulia) wakiteta jambo kabla ya uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumika katika benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa rasmi na wateja wa benki hiyo hivi karibuni. (Anayeangalia kulia) ni Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Prof. Joseph Semboja. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam.
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya NMB, Prof. Joseph Semboja mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam rasmi kwa kuzindua huduma mpya ya Mastercard iliyoanzishwa na benki hiyo.(Katikati) ni Mkurugenzi mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker.
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin W. Mkapa (kushoto) akisalimiana na Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati Bw. Michael Mieback (kulia) mara tu alipowasili katika uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itayoanza kutumiwa rasmi na wateja wa benki hiyo. (Katikati) ni Mkurugenzi mkuu wa benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker.
Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam . 
 Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumika hivi karibuni kwa wateja wake. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam. 
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa akihutubia wadau wa benki ya NMB kabla ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Mastercard ya benki ya NMB ambayo itatumika rasmi kwa wateja wake hivi karibuni. Hafla iliyofanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro Hotel.
Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara tu baada Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin W. Mkapa kuzindua rasmi huduma mpya ya NMB Mastercard. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency, jijini Dar es Salaam.


Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa (katikati) pamoja wakurugenzi wa Benki ya NMB wakikishangilia kikundi cha sanaa kilichotumbuiza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumika kwa mara ya kwanza kwa wateja wake. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania, 16 June 2015 –National Microfinance Bank (NMB), Benki inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi nchini, imezindua rasmi familia ya kadi za benki “MasterCard Debit”, zikiwemo Tanzanite, Titanium  kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Kadi ya “First world Rewards”.  

Familia hii ya kadi hizi za benki zitahudumia wateja aina mbalimbali, ikiwemo asilimia kubwa ya wateja (Tanzanite), wateja wa kipato cha kati (Titanium) na wale wateja wa kipato cha juu (World Rewards) ikitoa huduma na faida mbalimbali mahususi kwa walengwa.
“Pamoja na ukuaji wa kasi katika sekta ya malipo kwa njia ya elektroniki, wateja wetu wanazaidi kutafuta njia za haraka, salama na zenye unafuu kutumia katika malipo. Kukabiliana na wimbi hili, tumezindua familia hii ya kadi zinazokubalika kimataifa, na hivyo kurahisisha upatikanaji wa pesa zao kwa usalama popote walipo, Tanzania au nje ya nchi” alisema Ineke Bussemaker, Mkurugenzi mtendaji wa NMB.
Wamiliki wa kadi hizi za ‘MasterCard’ wataweza kutoa Fedha kutoka mashine za Miamala ya fedha duniani kote zenye alama ya “MasterCard Acceptance” ya fedha. Pia wataweza kulipia bili, kulipia umeme na Salio za simu, pamoja na kununua bidhaa mtandaoni kutoka maduka mbalimbali makubwa ndani na je ya nchi.
“Kadi za “MasterCard debit” zinakubalika na mamilioni ya wafanya biashara kutoka nchi Zaidi ya 210, ikiwa na maana kuwa wanaosafiri kwa ajili ya mapumziko au biashara wataweza kupata pesa zao popote pale, kwa urahisi kama wakiwa nyumbani” alisema Michael Miebach, Raisi, Mashariki ya kati na Africa, MasterCard. 
“muhimu Zaidi, kila muamala wa kitaifa na kimataifa unalindwa na usalama wa “masterCard SecureCode pamoja na EMV chip na Teknolojia ya PIN” ambazo hutoa usalama wa ziadakila mara mteja anatumia kadi yake mtandaoni au katika duka la kawaidia.”
NMB pia inakuwa Benki ya kwanza Tanzania kuzindua kadi ya “MasterCard World Rewards”. Kadi hii inawapa fursa wamiliki kupata huduma za kipekee za kiamisha kama vilie ofa za ndege, malazi, kukodisha gari, vyakula, manunuzi, michezo na burudani kupitia “Mastercard priceless Cities and Priceless Africa Programmes”.
“Hapa NMB tunaamini ni muhimu kufahamu mahitaji na matakwa ya wateja wetu, na kuwazawadia kutokana uaminifu wao. Tunayofuraha kuwa benki ya kwanza Tanzania kutambulisha mpango huu wakimapinduzi unaotoa zawadi kwa wateja wetu wa kipato cha juu huduma mbalimbali za kipekee za kimaisha, kupitia matawi yetu yaliyopo tayari na tawi letu jipya kabisa la “Private banking” litakalo hudumia wateja wetu wa kipato cha juu” alisema Bussemaker.
Wamiliki wa kadi za “Worlds Rewards” wataweza kujipatia poinyti za uaminifu kila mara wanapotumia kadi zao. Pointi hizi za uaminifu zinaweza kukombolewa kwenye mashirika ya ndege zaidi ya 800 dunia nzima, kampuni za kukodisha magari an hoteli maarufu Zaidi ya 160,000 duniani.  
Wamiliki wa kadi zilizo kwenye familia hii, wataenedlea kufurahia huduma nyinginezo za NMB zikiwemo “NMB App, NMB Internet Banking, NMB E-Statement na NMB Mobile”.

Kuhusu NMB
National Microfinance Bank (NMB) ndio benki ya biashara  inayoongoza kwa huduma zote kamilifu hapa Tanzania ikitoa huduma mbalimbali za kibenki kwa kundi la wateja linalowakilisha vyema Tanzania nzima. Benki hii hutoa huduma kama za akiba, mialama pamoja na huduma za ufadili kwa watu binafsi, kuanzi kampuni ndogo hadi za kati, serikali, kilimo biashara pamoja na makampuni makubwa na taasisi. NMB pia ina jukumu muhimu katika sekta ya kilimo pamoja na maghala hapa nchini kupitia SACCOS na Amcos.

Katiaka Ubinafsishaji mwaka 2005, benki ilikuwa na wateja takribani 600,000, idadi hiyo ikiongezeka na kufikia millioni 1.8. Benki haikuwa na Mashine ya muamala (ATM) hata moja miaka mitano iliyopita, leo hii inamiamala Zaidi ya 600, ambayo ni asilimia 40 ya mashine zote Tanzania kwa ujumla. Benki inamatawi zaidi ya 170 na inapatikana katika asilimia 95 ya wilaya zote za kiserikali Tanzania. Nia ya benki hii ni kufikia asilimia 100 ya wilaya zote Tanzania

Fuatilia ukurasa wetu Twitter @NMBTanzania na upande wa Facebook NMB Tanzania

Kuhusu MasterCard
MasterCard, www.mastercard.comni kampuni ya teknolojia katika ulimwengu wa malipo ya kielektroniki. Sisi tunaendesha mfumo wenye kasi zaidi duniani katiaka masuala ya miamala ya fedha, kuunganisha wateja, taasisi za fedha, wafanyabiashara, serikali na biashara katiaka nchi zisizopungua 210. Bidhaa hizi za MasterCard pamoja na huduma zake hufanya shughuli za kibiashara za kila siku kama vile ununuzi, kusafiri, kuendesha biashara na kusimamia fedha - rahisi, salama zaidi na zenye ufanisi zaidi kwa kila mtu. Fuatilia kurasa wetu wa Twitter: @MasterCardMEA na @MasterCardNews, kujiunga na majadiliano Beyond the Transaction Blog na jiunge kupata habari za kina MEA Engagement Bureaua.

WAZIRI BERNARD MEMBE APATA UDHAMINI WA KISHINDO KATIKA MKOA WA ARUSHA

$
0
0
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliofurika nje ya Ofisi ya CCM ya Wilaya ya Arusha jana kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500. Picha zote na John Badi.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akiwasalimia  wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliofurika nje ya Ofisi ya CCM ya Wilaya ya Arusha jana kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati) akiagana na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliofika kumpokea nje ya Ofisi ya CCM ya Wilaya ya Arusha jana kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500.

HUAWEI TANZANIA NA WIZARA YA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUUNGANA KATIKA KONGAMANO LA TEKNOHAMA NCHINI

$
0
0

Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu kuungana na kampuni ya Huawei katika kongamano la Teknohama, kulia ni Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala.
Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala kiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu kuungana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika kongamano la Teknohama kushoto ni Mkurugenzi wa ICT katika wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba
Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba (Kushoto) wakishikana mkono na Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala kuashilia kuungana katika kongamano la Teknohama.

Kampuni ya Huawei Tanzania ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Technolojia jana ilitangaza kuwepo kwa kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference katika ukumbi wa Julius Nyerere Convential Center JNICC tarehe 18 na 19 Juni 2015.

Kongamano hilo litajadili hali ya sekta ya tecknohama kwa sasa,sera mpya zitakazowekwa na kuweka ajenda ya jinsi ya kukuza sekta hiyo nchini.pia kongamano hilo litaainisha jinsi nchi itafikia malengo yake ya milenia kupitia tecknohama.

Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Dk. Ally Simba alisema, “tumefurahi sana kwamba Wizara na kampuni ya Huawei Tanzania zitashirikiana katika kongamano hilo,ambapo tutajadiliana kwa undani ukuaji na maendeleo katika sekta ya ICT.Na kwa upande wa Wizara tutaelezea sera mpya na mipango tulioweka ili kuhakikisha maendeleo ya sekta”.

Aliendelea kwa kuwahakikishia Watanzania kwamba Wizara imejikita katika kukuza sekta ya Teknohama.aliongeza kwamba Makamo wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anategemewa kuwa mgeni rasmi,huku pia ,Waziri na Katibu Mkuu wa Wizaraya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia na Balozi wa China nchini Tanzania watakuwepo.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Bwana Samson Majwala alisema, “tunaishukuru sana Wizara kwa kukubali kuungana nasi katika kuandaa kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference nchini Tanzania,na tunawahakikishia Watanzania wote kwamba kongamano litapendeza.

Tutakua na wataalam kutoka nyanja tofauti za Teknohama kutoka serikalini na kampuni ya Huawei ambao watatuelimisha kuhusu mitindo mipya katika sekta hiyo.Sisi kama Huawei tutaelezea mipango tuliyonayo ya kuboresha sekta hii nnchini Tanzania”.

Katika kongamano hilo,Huawei watazindua bidhaa zao mpya za Oceanstor V3 na Fusonq.Pia kutakua na gari maalumu la kufanya maonesho,gari hilo kwa kila mwaka linafanya ziara katika mabara yote duniani,na kwa mwaka wa 2015 litazuru bara la Afrika haswa Afrika kusini na Afrika Mashariki,Tanzania ikiwemo ya nchi itakayopita.

WIZARA YA HABARI YAKAMILISHA UBORESHAJI TOVUTI YA WANANCHI, SASA IKO HEWANI

$
0
0
Hussein Makame-MAELEZO.


WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari- MAELEZO, imekamilisha kazi ya kuboresha Tovuti ya Wananchi na sasa iko hewani.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Wizara hiyo, Mkurugenzi wa MAELEZO Assah Mwambene, aliwataka wananchi kuitumia tovuti hiyo kupitia anuani ya www.wananchi.go.tz kuwasilisha hoja zao Serikalini ili ziweze kupatiwa majibu .

 “Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari- MAELEZO, imekamilisha kufanya  maboresho ya tovuti ijulikanayo kwa jina la Tovuti ya Wananchi” alisema Mwambene na kuongeza:

“Lengo letu sasa ni kutaka wananchi badala ya kuhangaika sana, akiwa sehemu yoyote ya nchi hii anaweza kuuliza swali kupitia mtandao wa intaneti kwa anuani ya www.wananchi.go.tz


Alisema mwananchi akiingia kwenye tovuti hiyo atakutana na sehemu ya kuweka hoja yake kuuliza swali, kutoa maoni, kutoa pongezi, kuwasilisha malalamiko yake na moja kwa moja yatapokelewa na MAELEZO na kufanyiwa kazi.


“Mwananchi anaweza kuandika swali moja kwa moja kwenye taasisi anayotaka swali lile liende, kwa mfano kama anataka swali lile liende Wizara ya Ardhi anaweza akaandika” alisema Mwambene na kuongeza:

“Sisi tutapata taarifa kwamba ameleta swali na tutalipeleka kwenye taasisi husika na tutaangalia na kuona je swali hilo limejibiwa ama halijajibiwa”.

Mwambene alifafanua kuwa kila siku MAELEZO itajua ni wizara gani ama taasisi gani ya Serikali imepelekewa swali gani na swali hilo limejibiwa au la.



Alisema tovuti hiyo ni chombo muhimu katika mabadiliko ya sayansi na teknolojia na itamfanya mwananchi asilazimike kutembea kutoka kwenda wizara moja hadi nyingne ama taasisi ya Serikali kushughulikia malalamiko yake.


Alitoa mfano kuwa hata mwananchi akitaka kujua jinsi ya kupata viza au huduma nyingine inayotolewa na Serikali ataweza kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi sana kupitia tovuti hiyo ya Wananchi.


“Baadaye kuna jambo lingine ambalo bado tunalifanyia tathimini, ni suala la kwamba wanaanchi wanaweza kutumia simu zao za mkononi kutuma maswali na kupokea majibu” alisema Mwambene.


Alibainisha kuwa tathimini hiyo ikikamilika hivi karibuni, watatoa namba ambayo mwananchi anaweza kutumia ujumbe mfupi wa simu ya mokononi kutuma hoja yake Serikalini na kupatiwa majibu kupitia njia hiyo.


“Ni tovuti ambayo tunapenda wananchi waitumie ili kupunguza gharama na muda mwingi sana kwa mfano mtu kusafiri, kupanda gari kwenda wizarani au taasisi ya umma kufuatilia shida yake.Hivyo anaweza kutumia simu yake ya mkononi” alisema Mwambene na kuongeza:


“Lengo letu ni kwamba wananchi waone kama hiyo ni fursa muhimu ya mawasiliano na waone kuwa sasa hivi wanaweza kutuandikia ujumbe kuuliza swali au malalamiko na yatatufikia na kufanyiwa kazi”.

Mwambene alisema Wizara imejipanga vya kutosha kuhakikisha kwamba Serikali inawasiliana na wananchi wake kwa kusikiliza shida zao na kuzipatia majibu.


“Hii ni Serikali ya wananchi na lazima tuwasiliane na wananchi kwa njia yoyote ambayo ni rahisi kuwafikia na Serikali imeona hii ni njia rahisi zaidi kuwafikia kupitia mtandao huu wa Tovuti ya Wananchi” alisema.



Tovuti ya Wananchi imewahi kufanya kazi katika miaka iliyopita na baadaye ilisimama lakini  sasa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeifanyia marekebisho makubwa na iko hewani. 

Article 23

ZIARA YA KATIBU WA CCM NDUGU KINANA WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimsikiliza kwa makini, Diwani wa Nyakafulwa, Mathias Nyororo, aliyekuwa akifafanua kutoanza kwa mradi wa maji kijiji cha Masumwe, licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa fedha za mradi huo miezi sita iliyopita. Iikuwa ni baada ya wananchi kulalamika kutopata maji katika kijiji hicho katika mkutano wa hadhara ambao Kinana aliufanya katika kata ya Masumbwe,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Masumbwe wilayani Mbongwe,mkoani Geita.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kumwaga zege katika zahanati ya kijiji cha Kasheko kata ya Lulembera wilayani Mbogwe mkoani Geita. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa wodi ya akina mama inayojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya Lugunga
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipaka rangi moja ya nyumba za walimu zinazojengwa kwa nguvu za wananchi katika sekondari ya Mbogwe kata ya Bwela.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lugunga,wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na Wana CCM katika katika kata ya Mang'ombe kwenye kikao cha Halmashauri kuu Wilaya pamoja na kupokea taarifa ya chama na serikali
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mganga Mkuu wa kituo cha afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe,Dkt John Mgosha,alipokagua kituo hicho na kuwasha umeme wa REA kituoni hapo,kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.Kinana na ujumbe wake yupo katika ziara ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010-2015 inayotekelezwa na serikali. 
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhisiana na kazi zinazofanywa na vikundi vya wajasiliamali-Wanawake mjini Masumbwe wilayani Mbogwe,Ndugu Kinana alikagua miradi mbalimbali ya vikundi hivyo vya wajasiliamali.
 Baadhi ya Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara uliokuwa ukifanyika katika uwanja wa Masumbwe,wilayani Mbogwe mkoani Geita.
 Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Masumbwe wilayani Mbogwe.

PICHA NA MICHUZI JR-MBOGWE, GEITA

NASSAR ATUMIA HELKOPTA KUHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI.

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Jshua Nassar akizungumza na wananchi katika kata ya Shambarai Burka wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo kuhasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftarai la kudumu la wapiga kura.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.
Mbunge Joshua Nassar akitelemka kutoka katika helkopta wakati alipofika katika kata ya Shambalai Burka kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha.
Mbunge Nassar pia alitumia mkutao huo kuwaonesha wananchi magari mawili ya kubeba wagonjwa aliyotoa kwa ajili ya Halmashauri ya wilaya ya Arumeru.
Magari mawili ya kubebea wagonjwa yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwa ajili ya watu wa jimbo hilo.
Mbunge Nassar akiwaapisha wananchi ikiwa ni moja ya hamasa kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Mbunge Nassar akiondoka katika uwaja huo mara baada ya kumalizza mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akisalimiana na rubani wa Helkopta wakati anaanza ziara ya kuhamaisha zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa BVR.
Mbunge Nassar akifunga mikanda tayari kwa kuanza ziara.
Mbunge Joshua Nassar akitelemka kutoka katika helkopta wakati alipofika katika kata ya Shambalai Burka kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha.
Baaadhi ya wananchi wakiwa wamembeba Mbunge Joshua Nassar mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Shambarai Burka.
Mbunge Joshua Nassar akisalimiana na mmoja wa watoto waliojitokeza kumpokea.
Kundi la kina mama pia walikuwa miongoni wananchi waliojitokeza kumpokea Mbunge Nassar.
Mbunge Joshua Nassar akiwa na viongozi wengine wa Chadema wilaya ya Arumeru.
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Arumeru ,Gadiel Mwenda akizungumza katika mkutano uliofanyika kata ya Shambarai Burka kuhamasisha wanachi kujitokeza katika zoezi la uandikishwaji.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

TANAPA WAKABIDHI MRADI WA UJENZI WA BWENI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NURU YA WILAYANI SIHA.

$
0
0

Bweni la wanafunzi lililojengwa kwa ufadhili wa hifadhi za taifa (TANAPA) katika shule ya sekndari Nuru wilayani Siha.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza katika hafla hiyo juu ya dhana ya ujirani mwema inayofanywa na Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) kwa jamii zinazozunguka hifadhi za taifa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akikata utepe katika Bweni hilo .

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Nuru iliypo wilayani Siha alipowasili kwa ajili ya makabidhiano na ufunguzi wa Bweni la wananfunzi lililojengwa kwa ufadhili wa hifadhi za taifa Tanzania (TANAPA).
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo.
Baadhi ya wanafunzi katika shule ya sekondari Nuru wakimsikiliza RC Gama (hayupo pichani).
Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa akizungumza katika hafla hiyo.
Mku wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa ndani ya Bweni hilo.
Wananfunzi katika shule hiyo wakimsikiliza mkuu wa Mkoa marabaada ya kufungua rasmi Bweni hilo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

KONGAMANO LA UPATIKANAJI WA FEDHA ZA NDANI ZA MAENDELEO LAFANYIKA JIJINI ARUSHA

$
0
0
CDF 1
Mratibu Mkazi Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) na Mwakilishili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ambaye alikua mgeni rasmi katika Kongamano la upatikanaji wa fedha za ndani za maendeleo akitoa hotuba yake kwa washiriki kutoka Halmashauri za wilaya nchini lililofanyika jijini Arusha.
CDF 2
Mkuu wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) nchini na Meneja wa LFI duniani, Peter Malika akizungumza wakati Kongamano hilo.
CDF 4
Mkurugenzi wa Huduma(Tamisemi), Denis Bandisa akizungumza wakati Kongamano ambalo pamoja na mambo mengine alizitaka halmashauri nchini kubuni vyanzo vya ndani vya mapato badala ya kutegemea wafadhili.
CDF 5
Washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi wakifatilia kwa makini mada katika Kongamano hilo.

CDF 6
Washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja, Kongamano hilo limefanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Na Mwandishi wetu, Arusha
MFUKO wa Umoja wa Mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), umeitisha kongamano la siku mbili la upatikanaji wa fedha za ndani kwa maendeleo.
Kongamano hilo linahusisha wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa nchini Tanzania na linashirikisha watu 110.
Pamoja na wakurugenzi hao, wapo na wawakilishi kutoka Serikali Kuu na wawakilishi walioteuliwa kutoka serikali za mitaa za Uganda, Senegal na Benin.
Kwa mujibu wa taarifa ya UNCDF, nia ya kongamano hilo ni kuonesha mafanikio ya mfumo wa ukusanyaji wa fedha za ndani kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi ya kibiashara katika nchi za Tanzania na Uganda.
Taarifa hiyo imesema kwamba baada ya kujifunza mafanikio hayo washiriki watajadiliana na kujipanga kwa ajili ya utekelezaji wa mfumo huo katika nchi zao wanaokotoka ili kupiga hatua mbele katika uendelezaji wa miradi bila kutegemea fedha za nje.
Akizungumza wakati wa ufunguzi Katibu Mkuu Tamisemi, Jumanne Sagini alisifu kazi inayofanywa na programu ya uwezeshaji wa fedha za ndani kwa maendeleo ( Local Finance Initiative- LFI) chini ya sekretarieti ya UNCDF kwa ubunifu wake unaowezesha kupatikana kwa mitaji ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na serikali za mitaa.
Aidha alielezea dhamira ya serikali ya kutumia mfumo huo ulioasisiwa na UNCDF kwa kuufanya uwe wa kitaasisi zaidi ili kuweza kusaidia kutekeleza mipango ya maendeleo na uwekezaji ya serikali za mitaa.
Akizungumzia umuhimu wa kongamano hilo, Mgeni rasmi, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez, aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kufuata mfumo wa utafutaji wa fedha za ndani kwa ajili ya kukuza uwekezaji katika miundombinu ya kibiashara inayoleta mabadiliko kwa umma.
Rodriguez alisema katika hotuba yake kwamba kwa kuwezesha mfumo wa UNCDF LFI kwenye serikali za mitaa ndio jibu la uhakika la uwekezaji wenye mafanikio endelevu kwa taifa zima.
Aidha alisema mpango huo wa LFI ambao umekuwepo nchini kwa miaka mitatu na kuwezesha kuleta mabadiliko katika jamii, unafaa kumilikiwa na jamii ili kuwezesha mafanikio ya juu katika uwekezaji.
Mratibu huyo alisema kwamba Umoja wa Mataifa kupitia UNCDF utaendelea kufanyakazi na serikali ya Tanzania,kwa kuwa wanaamini kwamba vita dhidi ya umaskini itafanikiwa kwa kuhamisha mitaji na kuipeleka katika ngazi za chini kwa maendeleo ya wananchi.
Kongamano hilo ambalo ni mwendelezo wa uwezeshaji na kubadilishana uzoefu na elimu kwa lengo la kuwezesha miradi ya umma na binafsi inayochagiza maendeleo kujengwa; katika siku ya kwanza ya kongamano hilo washiriki wataoneshwa miradi iliyotekelezwa manispaa ya Busia Uganda na Kibaha nchini Tanzania.
Manispaa ya Busia imejenga kituo cha malori, ushuru wa forodha na maeneo ya kufanyia biashara, wakati Kibaha wamejenga kituo cha kisasa cha mabasi na soko.
Timu ya wataalamu wa UNCDF watawafundisha washiriki kwa siku 2 kuhusu miradi ya maendeleo, awamu za malipo ya fedha na mikakati ya kupata fedha na malipo na mbinu za kupunguza hatari za kibiashara.
Akisisitiza umuhimu wa kongamano hilo Mkuu wa UNCDF nchini na Meneja wa LFI duniani Peter Malika alisema kwamba kongamano hilo linatoa nafasi kwa watumishi wa serikali za mitaa na wengine kujifunza namna mpya ya kupata mitaji kwa kutumia vyanzo vya nyumbani ili kufadhili miradi ya miundombinu ya kiuchumi inayohitajika kwa ajili ya kutoa fursa za ujasiriamali , biashara, uwezeshaji, ajira, kuboresha maisha ya watu, ukusanyaji kodi na utoaji huduma.
Kongamano hilo la siku 2 ni miongoni mwa juhudi kadha za UNCDF za kuwezesha serikali za mitaa kufikia maendeleo endelevu na kuleta athari chanya kwa jamii ili kuondoa umaskini.

SHIRIKA LA OXFAM LAKABIDHI VITUO VYA KUSINDIKA NA KUHIFADHI MAZIWA KWA WANAWAKE WA VIJIJI VINNE VYA WILAYA YA NGORONGORO

$
0
0
Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro John Kulwa Mgalula akikata utepe kama ishara ya kuzindua  rasmi kituo cha kuhifadhia na kusindika maziwa.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro John Kulwa Mgalula akijalibisha Jokofu linalotumia umeme wa jua wakati wa uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro John Kulwa Mgalulawa kwanza kushoto akioneshwa baadhi ya vifaa ambavyo walikabidhiwa vituo hivyo na Shirika la Oxfam Tanzania.
Baadhi ya Wanakikundi cha NOSOTWA kutoka kijiji cha Engaresero.
Stellah Julius kutoka Oxfam akizungumza  na wanakikundi cha NOSOTWA kutoka kijiji cha Engaresero. 
 Mwenyekiti wa kikundi cha NAPONU akishukuru Oxfam kwakujengewa kituo cha kisasa cha kuhifadhi na kusindika Maziwa.
 Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro John Kulwa Mgalula Wanakikundi cha NOSOTWA kutoka kijiji cha Engaresero.
 Miriam Lembilika akishukuru kwa kuletewa vituo hivyo kijijini kwao.
Wanakikundi cha NYUWAT kutoka kijiji cha MALAMBO wakifurahia jambo.
  Afya imezingatiwa hiki ni moja ya vyoo ambavyo vipo katika vituo hivyo.
Wanakikundi cha NAPONU kutoka kijiji cha PINYINYI.
 Picha ya pamoja na wanakikundi wa NYUWAT kutoka kijiji cha MALAMBO


Shirika lisilo la Kiserikali la Oxfam hapo jana lilikabidhi vituo vya kusindika maziwa kwa wanawake wa vikundi vinne kutoka vijiji vya Engaresero, Pinyinyi, Malambo na Piyaya vilivyoko katika wilaya ya Ngorongoro.

Akipokea vituo hivyo kwa niaba ya wanavikundi hao, Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro John Kulwa Mgalula, alisema ana imani vituo hivi vitawasaidia wanawake kukua kiuchumi na kuepuka kuwa tegemezi kwani wanawake wengi wamekuwa na sifa ya uvumilivu, uangalifu wa hali ya juu na kwamba mara nyingi wao hufanya vitu kwa uaminifu.

Mkurugenzi aliyashukuru mashirika ya Oxfam waliofadhili ujenzi wa vituo hivi pamoja na PALISEP waliotekeleza mradi huu kwa jitihada mbalimbali ambazo yamekuwa yakifanya katika wilaya ya Ngorongoro ili kuwakuza wanawake kiuchumi huku akitaja miradi mingine iliyofadhiliwa na Oxfam kuwa ni pamoja na ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula, ujenzi wa majosho, pamoja na ujenzi wa vyanzo vya maji.

Akikabidhi vituo hivyo, Stellah Julius kutoka Oxfam alisema, “Baada ya kufanya utafiti uliowashirikisha wanawake wa vijiji hivi vinne walituambia kwamba wanahitaji vituo vya kusindika na kuhifadhia maziwa. Tumewajengea vituo hivi mvitumie kwa maendeleo yenu.” Stellah pia aliipongeza serikali na wadau mbalimbali kwa kutoa ushirikano mkubwa uliopelekea kufanikisha ujenzi wa vituo hivyo ikiwemo kutoa maeneo ya ardhi ya vijiji hivyo vinne.

Aidha Stellah aliwataka wanavikundi hao kuwa wabunifu wa namna ya kujiendeleza kibiashara na kuepuka kutegemea mashirika na taasisi ambazo zipo kwa muda tu.

Naye Mkurugenzi wa shirika la PALISEP Robert Kamakia alisema shirika lake limewajengea uwezo wana vikundi hao kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na mbinu mbalimbali za kibiashara pamoja na kuwafundisha namna za kutunza maziwa kwa usafi.

Kwa upande wake Thomas Nade, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ngorongoro aliwataka wanavikundi hao kusajili vikundi vyao mapema ili vitambulike kisheria na waweze kunufaika kwa namna mbalimbali ikiwemo kupatiwa mikopo na kufungua akaunti ya benki.


Wanawake kutoka vijiji hivi vinne wanatarajia kunufaika kwa kujipatia kipato kutokana na kuuza maziwa na siagi.

Akionyesha furaha yake, Mariam Lembilika kutoka kijiji cha Malambo alisema, “Mimi kama mwanamke ambaye nina watoto watano na sina mume natarajia kutumia kipato kutokana na biashara hii kusomesha watoto.”

Naye Mary Saigulan kutoka kijiji cha Engaresero alisema, “Tutauza maziwa na siagi na kujipatia fedha nyingi ambazo zitatusaidia kuanzisha miradi mingine na kutuwezesha kujitegemea“

Ujenzi wa vituo hivi vinne umegharimu takribani shilingi za kitanzania milioni 120 na kila kimoja kina jokofu linalotumia umeme wa jua, mashine za kusindika maziwa, madumu ya kuhifadhia maziwa, vipima joto, vipimo vya kupimia ubora wa maziwa, tenki la maji pamoja na mashimo mawili ya vyoo na bafu.

Vikundi hivyo vya NOSOTWA (Engaresero), NAPONU (Pinyinyi), NYUWAT (Malambo) na NASERIYAN (Piyaya) vina wana kikundi wapatao 30 kila kimoja.

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UBUNIFU

$
0
0
Ofisa Mwandamizi wa Maendeleo ya Jamii, Idara ya Kuondoa Umasikini katika Wizara ya Fedha, William Ghumpi akimpatia Kitabu cha Taarifa ya Utekelezaji wa Malengo ya Milenia 2014, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana. Wapili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma. (Picha na Kassim Mbarouk).

Na Salma Ngiwilizi – Maelezo
SERIKALI imewataka watumishi wa umma nchini kuonyesha ubunifu na weledi  katika utendaji kazi wa majukumu yao mbalimbali ili kuweza kukidhi matarajio ya wananchi.

 Aidha  imewasisitiza watumishi  wa umma wanawake  kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na ufanisi  ili kuonyesha uwezo  wao na uhodari   katika kutekeleza majukumu  yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana  na Kaimu Katibu Mkuu  wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma HAB Mkwizu wakati  akifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  Mhe. Celina Kombani yanatoendelea kwenye  viwanja vya Mnazi  Mmoja.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni chachu ya kuwawezesha Wanawake  kuongeza Ubunifu na Kuboresha utoaji wa Huduma kwa Umma”.

Serikali imetoa miongozo mbalimbali ya kisera inayokusudia kumpa mwanamke wa nchi  hii fursa sawa ya kuchangia maendeleo ya nchi yetu.

Baadhi ya miongozo hiyo ni pamoja na Sera ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996, Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000, na mwongozo wa anuai za jamii mwaka 2010.

 Alisema  hadi sasa utekelezaji wa miongozo hii umeleta matokeo chanya ambapo nchi yetu inajivunia kufikia mafanikio kadhaa , ambayo ni pamoja kuongezeka kwa idadi hya wanawake katika ngazi  za maamuzi Serikalini kutoka asilimia 26 mwaka 2005 na kufikia  asilimia 34 mwaka 2014.

“Wale waliopata nafasi walizopewa au kupata kutokana na juhudi zao. Ujuzi au uzoefu wao wanazitendea haki kwa kusimamia vizuri wale walio chini yao na kutoa huduma bora iliyotukuka kwa wananchi,” alisisitiza.

 Aliongeza kuwa  mafanikio  mengine ni kujenga uwezo wa watumishi wanawake kupata sifa za ziada ,kuongeza ubunifu na kuboresha upatikanaji wa huduma na Serikali imekuwa ikitoa ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili kwa wanawake katika Vyuo Vikuu vya hapa nchini. 

Hivyo katika kipindi cha miaka 10 jumla ya watumishi wanawake 251 walipatiwa ufadhili na kuhitimu masomo yao katika shahada mbalimbali  za uzamili.

 Alitoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia,sekta binfasi na vyombo vya habari kuendelea kutoa mchnago katika kuhimarisha Utumishi wa Umma  katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images