Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 556 | 557 | (Page 558) | 559 | 560 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajab Rutengwe akiwa ameshika mwenge wa Uhuru baada ya kupokea kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Said Magalula
   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajab Rutengwe (kushoto) akiwa amekumbatiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Said Magalula baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru.

   Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Bw. Juma Khatibu  Chum akifungua kitambaa kama ishara ya kuzindua zoezi la uandikishaji wapiga kura Wilayani Mvomero lililofanyika  katika Kijiji cha Salawe Kata ya Kibati.
  : Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Juma Khatib (katikati) akipewa maelezo ya  zoezi la uandikishaji wa wapiga kura litakavyoendeshwa, muda mfupi baada ya kuzindua zoezi hilo. (Kulia mwenye tracksuit) ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Betty Mkwasa.


  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA, Bi. Marion Moore (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya bidhaa mpya ya mkopo maarufu kama ‘Executive Loan’, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Pamoja naye, kushoto ni Meneja Mauzo Kanda Bw. Haule Stephen na Mshauri Mkuu wa masoko Bw. Andrew Omusambayi.

  TAASISI ya kifedha, Faidika imezindua bidhaa mpya ya mkopo maarufu kama ‘Executive’ inayolenga kuwezesha upatikanaji rahisi wa mkopo usiokuwa na dhamana kwa wafanyakazi wa serikalini wa mpaka shilingi milioni 30. 

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Afisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA, Bi. Marion Moore alisema mkopo huo mpya ni moja kati ya bidhaa ya kipekee nchini yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wafanyakazi toka serikalini.

  “Bidhaa yetu ya mkopo wa Executive, ni bidhaa itolewayo haraka, yenye ubunifu na rahisi katika upatikanaji wake na ya kipekee katika soko la Tanzania. Ni mkopo ambao utawawezesha wafanyakazi wengi toka serikalini kupata fedha na kuweza kuinua viwango vyao vya maisha kwa kujihusisha na miradi mikubwa mbali mbali.   Viwango vya mikopo hii ni kuanzia shilingi milioni kumi mpaka thelathini ambapo marejesho yake yananzia miezi sita mpaka miezi sitini,” alisema Moore. 

  “Bidhaa ya mkopo ya ‘Executive’ ni bidhaa ya kipekee kwa soko la Tanzania, kutokana na kwamba mteja atakiwi kutoa dhamana yoyote ili kupatiwa mkopo. Inachukua masaa 48 tu kwa mteja kupatiwa fedha za mkopo,” aliongeza.

  Naye Meneja Masoko wa Kanda wa FAIDIKA, Bw. Haule Stephen alisema kuwa muombaji anatakiwa kutoa stakabadhi mbili za mishahara ya miezi miwili iliyopita, taarifa ya kibenki ya akaunti kuanzia miezi miwili na kuendelea, Kitambulisho cha kazi na picha moja ya pasipoti, ili kujipatia mkopo huo. Na kuongeza kuwa viwango vya mikopo ya FAIDIKA vimekua kutoka kuanzia shilingi milioni kumi na kufikia shilingi milioni ishirini.  

  “Dhumuni letu ni kuona viwango vya maisha vya watanzania vinakua kupitia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha,” alisema Bw. Stephen.  

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Profesa John Nkoma akifungua mkutano na waandishi wa Habari na kuzungumzia umuhimu wa kusajili namba za simu za Mkononi na Mfumo mpya wa kusajili namba na kuhakiki kutumia Teknolojia mpya ya Kielekroniki.
   Mwenyekiti wa umoja wa makampuni ya mawasiliano Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bwana Rene Meeza akitamka Rasmi Uzinduzi wa usajili mpya wa simu za mikononi kwa kutumia Teknolojia mpya ya kutumia smart phone kutumia Programu ya KYC
  Muwezeshaji katika mkutano na waandishi wa habari akiendelea
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi hati wa NIDA Thomas William akizungumza umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha Taifa ambapo ndicho kitakuwa kitambulisho rasmi katika kusajili Namba mpya za simu na kuhakiki kwa wale ambao tayari wamejisajili.
   Mfumo mpya wa Kielekroniki kutumia Smart Phone kwa Program ya KYC inavyofanya kazi.
  Mkutano ukiendelea 
  Picha na Fredy Anthony wa Blogs za Mikoa.

  Mfumo mpya wa Usajili wa Namba za Simu (Sim Card registration)  kwa kutumia Teknolojia mpya ya Kigitali Kupitia Smart Phone kwa Programu ya KYC umezinduliwa Rasmi leo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ukiwahusisha Makampuni ya simu, NIDA, Polisi na TCRA.

  Akizungumza katika Mkutano huo wa uzinduzi wa Huduma hiyo ya kisasa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma amesema kuwa mwanzo kulikuwa hakuna changamoto sana juu ya laini za Simu lakini kwa sasa zaidi ya laini za simu 32,000,000 zilizo sajiliwa, Pia alizungumzia umuhimu wa kujisajili ikiwa ni pamoja kwa usalama, kutunza amani pia kusaidia mamlaka kuwa na kumbukumbu za watu ambao wamejisajili..

  Nae Mwenyekiti wa umoja wa makampuni ya mawasiliano Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bwana Rene Meeza  alielezea kwa kina namna ya mfumo huo mpya utakavyofanya kazi ambapo katika usajili mpya wa Kielekrinki kutakuwa na kusajili kwa kutumia kitambulisho cha Taifa ambapo zoezi kupata vitambulisho vya Taifa kwa wananchi Tanzania Linaendelea.

   Alielezea Mfumo huo mpya wa Sim Card registration kuwa unakwenda kwenda kwa kutumia Smartphone ambayo itakuwa na Programu ya KYC ambapo mteja atasajiliwa ndani ya simu hiyo kuanzia kuandika Majina yake, Atapigwa Picha, Kitambulisho chake kitapigwa picha kama ni Feki Mashine Simu haita kipiga picha, pia Mteja ataweza kutia Saini yake pale pale kwenye simu. Aliongeza kuwa Mfumo huo utapatikana kwa Mawakala wa Makampuni husika wa Simu za mkononi. 

  Alimalizia kwa kusema kuwa Mfumo huo mpya utatumika kwa kuanza kusajili namba mpya za simu kwa Kutumia kitambulisho cha Taifa kama ndio Kitambulisho Rasmi ingawa viambulisho vyengine kama Hati ya kusafiria itaweza kutumika, Pia mfumo huo utatumika kuhakiki Namba za simu ambazo tayari zimesajiliwa.

  Pia  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi hati wa NIDA Thomas William alizungumza umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha Taifa na Kushukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Makampuni ya Simu kwa kuanzisha Mfumo huo mpya ambao utarahisisha kazi na kuongeza ufanisi zaidi


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi Makaje Goso, wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya maziko yanayotarajia kufanyika leo jioni. Katikati ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakia Bilal.Picha zote na OMR
  2
  Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi Makaje Goso, wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya maziko yanayotarajia kufanyika leo jioni. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
  3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, wakati alipofika kwenye Ofisi za Bakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha marehemu Simba.
  4
  Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, wakati alipofika kwenye Ofisi za Bakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha marehemu Simba.
  5
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Ofisi za Bakwata, Kinondoni kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha Marehemu Simba, leo Juni 16, 2015. Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
  7
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Viongozi katika Kisomo cha kumuombea Marehemu Mufti Shaaban Bin Simba, kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kweny Viwanja vya Ofisi za Bakwata zilizopo inondoni, jijini Dar es Salaam.
  8
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa Kisomo cha kumuombea marehemu Bin Simba, kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kweye Viwanja vya Ofisi za Bakwata Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
  9
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki swala maalumu ya kuswalia Jeneza (halipo pichani) na baadhi ya viongozi wa kitaifa wakati wa kisomo maalumu kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kwenye Viwanja vya Ofisi za Bakwata zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumuombea marehemu.

  0 0

  1
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimian na baadhi ya wananchi wa Mpanda waliofika kwenye ofisi ya CCM ya Wilaya  ya Mpanda  kushuhudia na kumdhamini  ilia pate sifa za kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Juni 15, 2015.
  2
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wanaCCM wa kijijini kwake Kibaoni wilayani  Mlele Juni 15, 2015 wakati alipokwenda kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya  Kibaoni  kabla ya kudhaminiwa  na wana CCM wa kata hiyo  katika  nia yake ya kutafuta uteuzi wa CCM  wa kugombea urais katika uchaguzi uja.
    4
  Baadhi ya wananchi wa Mpanda waliofika kwenye ofisi ya CCM ya wilaya ya Mpanda kumdhamini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika nia yake ya kuwania uteuzi wa CCM kugombea nafasi ya rais wa Tanzania Juni 15, 2015.
  56
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wanaCCM waliofika kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya Kibaoni kumdhamini katika nia yake ya kuwania uteuzi wa CCM katika kugombea nafasi ya urais Juni 15, 2015. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  …………………………………………………….
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ambaye pia ametangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) amepata wadhamini 9,141 baada ya kuhitimisha zoezi hilo katika mkoa wa Katavi.
  Hadi jana mchana alikuwa amekwishapata wadhamini 4,243 kwa kuzuru vituo viwili tu vya Inyonga na Mpanda Mjini. Lakini hali ilibadilika alipofika kijijini kwao Kibaoni kwenye ofisi CCM kata ya Kibaoni ambako alikuta maelfu ya watu wakimsubiri ili wasaini fomu za kumdhamini.
  Akitangaza idadi ya watu walijitokeza kumdhamini Waziri Mkuu, Katibu wa CCM wilaya ya Mlele, Bw. Sidael Goroi alisema kuwa tarafa za Mpimbwe na Mamba ambazo ziko kwenye Bonde la Ziwa Rukwa zimetoa wadhamini 3,450 wakati tarafa ya Nsimbo imetoa wadhamini 1,448 na kufanya jumla ya wadhamini 4,898 kwa jana jioni tu. Tarafa ya Mpimbwe ambako Waziri Mkuu anatoka ina kata tisa zikiwemo za Kibaoni, Mwamapuli, Ikuba, Usevya, Mbede na Majimoto.
  Mapema jana asubuhi, katika kituo chake cha kwanza cha Inyonga, yalipo makao makuu ya wilaya yake ya Mlele, Waziri Mkuu alipata wadhamini 1,440. Alirejea Mpanda saa 9 mchana ambako katika ofisi ya CCM Wilaya alipata wadhamini 2,803 na kufanya jumla ya wadhamini 4,243 kwa vituo hivyo viwili.
  Akitoa nasaha zake kwa wakazi hao jana jioni (Jumatatu, Juni 15, 2015), Waziri Mkuu aliwashukuru wote waliomdhamini huku akiwaomba waendelee kumuombea safari zote zilizo mbele yake na zoezi zima liende vizuri kwani suala la urais siyo lelemama bali ni la kumtanguliza Mungu.
                                                                                Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu Pinda alisema: “Suala la urais si la kufa na kupona bali ni la kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwanza. Kila mgombea anapaswa amuombe Mungu kwamba kama itampendezea na kumuona anafaa ndipo amchague yeye (mtangaza nia).”
  “Ndiyo maana mara zote huwa nawaambia wenzangu kwamba hakuna haja ya kutukanana wala kupakana matope. Huwa nawaambia tusikwaruzane wala tusitukanane kwa sababu hakuna ajuaye Mwenyezi Mungu amemuandaa nani miongoni mwetu,” alisema.
   Aliwataka wananchi na viongozi wa wilaya hiyo watoe ushirikiano kwa wagombea wengine watakaofika wilayani humo kuomba wadhamini.
  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, JUNI 16, 2015.

  0 0

  8
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake ya mwisho kwenye mkutano wa 15 wa Umoja wa wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi (OAFLA) uliofanyika  kwenye Ukumbi wa Sandton jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini -Juni 15,2015.
  …………………………………………………………………..
  Na Anna Nkinda – Johannesburg, Afrika ya Kusini
   Asilimia 73 ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) yanayotokea  miongoni mwa vijana Barani Afrika huwapata wasichana  huku asilimia 15 ya vijana wote  ndiyo wanaotambua hadhi yao ya VVU na hivyo kusababisha  tatizo hilo kuendelea kuwa  kubwa.
  Hayo yamesemwa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwenye mkutano wa 15 wa Umoja wa wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi (OAFLA) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Sandton Convention Centre mjini Johannesburg Afrika ya Kusini.
  Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema tatizo la VVU na Ukimwi bado ni kubwa miongoni mwa vijana wa kike na kama wataendelea kuambukizwa kwa kiwango hicho kutakuwa na muda mrefu wa kupambana na maambukizi kwa wenzao ambao hawajaambukizwa na kutahitajika muda mrefu wa matumizi ya dawa za kufubaza VVU ambazo ni ghali.
  “Ushauri wangu kwenu ni kuongea juhudi zaidi ili kupaza sauti za watoto wetu wa kike ambao wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa VVU, kufanya mapambano dhidi ya Ukimwi kuwa  ni agenda ya kudumu ya OAFLA kila tutakapotayarisha mipango yetu ya taarifa mapambano dhidi ya VVU ni muhimu kujumuishwa”, alisisitiza Mama Kikwete.
  7
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake ya mwisho kwenye mkutano wa 15 wa Umoja wa wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi (OAFLA) uliofanyika  kwenye Ukumbi wa Sandton jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini -Juni 15,2015.

  Kwa upande wa elimu Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema upatikanaji wa elimu bora kwa mtoto wa kike kutafungua fursa za kuweza kuboresha afya, kipato chake na hatimaye kujiongezea uwezo wake binafsi na familia kwa ujumla.
  Alisema, “Tunatambua kwamba kwa kadri mtoto wa kike anavyokaa muda mwingi shuleni ndivyo anavyoweza kuepuka uzazi katika umri mdogo, vifo vinavyotokana na matatizo ya uzazi na umaskini”.
  Mama Kikwete alisema ili kukabiliana na changamoto hizo Taasisi ya  WAMA  imeendesha kampeni ya mtoto wa mwenzio ni mwanao;Mkinge na Ukimwi kwa njia za upashanaji habari, mafunzo na uraghibishi kwa kutoa  mafunzo ya stadi za maisha na ujinsia kwa vijana wa rika mbalimbali ili kuwawezesha kuepuka ujauzito na maambukizi ya VVU.
  “Tumetekeleza afua mbalimbali za kusaidia kutokomeza maambukizi mapya ya VVU kutoka kwa Mama Kwenda kwa mtoto (EMTCT), kushirikiana na jamii za wafugaji ili kuepuka desturi zinazochochea vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi katika umri mdogo, tohara kwa wasichana na unyanyasaji wa kijinsia na kutekeleza kampeni ya kupima na kutibu mabadiliko ya awali ya saratani ya shingo ya kizazi”, alisema Mama Kikwete.
  Akiwakaribisha wake hao wa Marais, Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mama Thobeka Madiba Zuma alisema muda umefika kwa wao  kuonyesha majukumu yao  katika Bara la Afrika kwa kuungana  kwa pamoja na viongozi wa jamii zao ili waweze  kuondoa unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake zikiwemo mila kandamizi, kusimamia ili wanawake wapate haki za uchumi, afya ya uzazi na kulinda haki za  wazee, walemavu na watoto.
  “Vijana wapate elimu ya afya ya uzazi huduma ya kuzuia  maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ipatikane kwa urahisi kwa wanawake walio na maambukizi hii itasaidia  wanawake kujifungua watoto  wasio na maambukizi na hivyo kutokuwa na maambukizi katika vizazi vijavyo”, alihimiza Mama Thobeka.
  Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS) kutoka Umoja wa Afrika (AU) na Tume ya kushughulikia Uchumi ya Afrika (ECA) Rosemary Museminali alisema kama jamii itaamua kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali pamoja na mashirika binafsi ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi inawezekana kwa kiasi kikubwa kumaliza maambukizi ya VVU.
  Rosemary alisema,  “Katika nchi za Afrika msichana mmoja kati ya wasichana 10 wenye umri wa chini ya miaka 15  ana mtoto, wasichana hawa wanatakiwa kuwa  shule na kubeba vitabu na siyo kubeba watoto pia wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya VVU
  Mkutano huo wa wake wa marais wa Afrika ulienda sambamba na mkutano wa 25 wa wakuu wa nchi na viongozi wa Serikali wa Afrika uliomalizika  leo mjini Johannesburg.

  0 0

  1
  Jokate (kushoto) akizungumza katika mkutano wa jukwaa la sanaa. Katikati ni katibu mkuu wa Chama cha  Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli na mbunifu mkongwe wa mavazi, Asia Idarous.
  2
  Mbunifu mkongwe wa mavazi nchini, Asia Idarous (kulia) akisisitiza jambo katika mkutano wa jukwaa la sanaa. Katikati ni Katibu mkuu wa Chama cha  Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli na msichana mwenye vipaji vingi, Jokate Mwegelo.
  3
  Katibu mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli (Katikati) akizungumza katika mkutano wa jukwa la wasanii, kulia ni Mbunifu mkongwe, Asia Idarous na msichana mwenye vipaji vingi, Jokate Mwegelo.
  4
  Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza akifafanua jambo katika mkutano huo.
  5
  Msanii mkongwe wa maigizo na filamu nchini, Mzee Jangala akifuatilia mkutano wa jukwaa la sanaa.
  6
  Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza akionyesha kipaji chake cha kupiga zeze na kuimba kwa kushirikiana na wasanii wengine waliohudhuria mkutano wa Jukwaa la Sanaa.

  …………………………………………………………
  Na Mwandishi wetu
  Msichana mwenye vipaji lukuki nchini, Jokate Mwegelo amewataka wasanii kuwa wabunifu ili kupata mafanikio katika sanaa na shughuli zao za kila siku.

  Jokate alitoa wito huo wakati akitoa mada katika Jukwaa la Sanaa la lililoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kushirikiana na chama cha  Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz).
  Alisema kuwa sanaa ina wigo mpana sana na kila msanii anatakiwa kuwa mbunifu ili kujiweka tofauti  na msanii mwingine na kujipatia fedha kwa kutumia ubunifu wake.

  Kwa mujibu wa Jokate, yeye aliamua kupitia kwenye fani ya urembo na mwaka 2006 alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Miss Tanzania. Alisema kuwa aliamua kutumia umaarufu wake kujipatia maendeleo pamoja na ukweli kuwa alisomea mambo ya siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  “Elimu yangu ya mamo ya siasa haina nafasi kwangu, nilianza kuwa mshehereshaji (MC) katika shughuli mbalimbali, nikaingia katika fani ya ubunifu wa mabavi (Kidoti Fashion), nikaanzisha kidoti club ili kupata marafiki ambao tutazungumza lugha moja,” alisema Jokate.
  Mrembo huyo hakuishia hapo kwa kuingia katika fani ya utangazaji wa vipndi hasa Chanel O, uigizaji wa filamu, utengenezaji wa nywele, ndala na sasa mwanamuziki.

   “Hii yote ni kutafuta ‘chaneli’ za kupata fedha, nimefanikiwa na sasa nina makubaliano yenye thamani ya Sh 8.5 bilioni na kampuni ya Kichina, Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti,” alisema.
  Mbali ya Jokate, mbunifu maarufu nchini, Asia Idarous naye aliwataka wasanii kuwa waaminifu na kujitangaza katika shughuli zao ili kupata maendeleo.
  Idarous  alisema kuwa msanii ambaye atakuwa mbunifu na kipaji cha hali ya juu, hataweza kupata maendeleo kama atakosa sifa ya uaminifu ambayo mara nyingi uendana na nidhamu katika kazi.
  “Mimi nilianza kazi ya ubunifu wa mavazi miaka ya 1980, mpaka leo nafanya kazi hii, wabunifu wengi (hata Jokate) amepitia kwangu, siri kubwa ya mafanikio haya ni uaminifu na nidhamu katika kazi, nimefanikiwa kuanzisha Vazi la Khanga nchini Marekani na Lady in Red, leo hii ni maarufu,” alisema Idarous.
  Katibu Mkuu wa Chama cha  Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli alitoa wito kwa wasanii chipukizi kufuata nyayo za Jokate na Idarous ili kuweza kufanikiwa katika kazi zao za sanaa.
  Bumbuli alisema kuwa ni vigumu kupata mafanikio katika sanaa bila kuweka wazi kipaji chako hadharani na hapo ndipo vyombo vya habari vitakuona na kuanza kuandika habari zao.

  0 0

  1
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Madaktari wa Kichina waliopo Zanzibar waliofika kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wao wa kazi katika Hospitali mbali mbali Unguja na Pemba (wa pili kulia) Balozi Mdogo wa China Nchini Tanzania anyefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie Yunliang,
  [Picha na Ikulu]
  ????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi Mdogo wa China Nchini Tanzania anyefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie Yunliang wakati akiongoza ujumbe wa Madaktari wa Kichina waliopo Zanzibar waliofika kumuaga Rais (hawapo pichani) baada ya kumaliza muda wao wa kazi katika Hospitali mbali mbali Unguja na Pemba,

  0 0

  ????????????????????????????????????Na Kijakazi Abdalla Maelezo Zanzibar
  ……………………………….
  Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imesema kuwa meli ya MV Mapinduzi 11 inatarajiwa kuwasili Zanzibar wiki ya mwisho wa mwezi julai,2015
  Hayo yameelezwa na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Juma Duni Haji wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo 2015/2016 huko  katika Ukumbi wa Baraza la WawakilshiChukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar
   Amesema kuwa ujenzi wa meli hiyo upo hatua za mwisho kukamilika ambapo meli inaendelea kufanyiwa vipimo na majaribio ya baharini pamoja na majaribio mengine muhimu ya vifaa na mitambo viliomo katika meli hiyo.
   Aidha amesema kuwa iwapo mambo yatakwenda vizuri katika vipimo na majaribio hayo meli hiyo itaanza safari kutoka Korea ya Kusini hadi Zanzibar tarehe 25/Juni 2015 na kuwasili Zanzibar wiki ya mwisho wa mwezi Julai ,2015.
   Aidha amesema kwa upande wa Shirika la Bandari linahudunia meli katika bandari za Unguja na Pemba pamoja na kusimamia usalama wa  usafiri ndani na maeneo ya bandarini
   Aidha amesema kuwa shirika limehudumia jumla ya meli za kigeni 144 zenye uzito wa GRT 1,914,246, meli za ndani 2,927pamoja na vyombo vya kienyeji 3,283 pamoja na kuhudumia jumla ya tani 145,226 za mzigo mchanyiko na makontena 44,601 pamoja na mzigo wa majahazi tani 106,934.
   Sambasamba na hayo Waziri huyo ameiomba Serikali liidhinishe jumla ya sh 189,108,700,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwa mwaka 2015/2016,ambapo Wizara itatekeleza progamu nne ikiwa ni pamoja na matumizi ya kawaida, matumizi ya kazi za maendeleo na mikopo kutoka kwa washirika wa Maendeleo.

  0 0

  Kama ulipitwa na uzinduzi wa filamu ya Mpango mbaya iliyochezwa na washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 uliofanyika katika ukumbi wa mlimani city mwishoni mwa wiki nakuacha gumzo unaweza kutazama hapa matukio yaliyojili katika uzinduzi huo.

  0 0

  Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Lydia Bukumbi akiaga mwili wa Robert Tillya.
  Mwandishi wa Global Publishers, Mayasa Mariwata akiuaga mwili wa mfanyakazi mwenzake kwa simanzi.
  Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (wa kwanza kulia), Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka (wa tatu kulia) na Ofisa Utawala wa Global, Soud Kivea (wa pili kushoto) wakiwa na simanzi wakati wa zoezi la kuaga mwili wa Robert Tillya.

  Elvan Stambuli akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Global Publishers Ltd.

  Wafanyakazi wa Global wakiongozwa na Imelda Mtema (wa kwanza kushoto) kuaga mwili wa Robert.
  Wafanyakazi wa Global, ndugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili wa Robert kwa simanzi nzito.
  Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist akiaga mwili wa Robert kwa huzuni.
  Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli akiaga mwili wa marehemu.
  Mhariri wa Championi Jumatano, Phillip Nkini akiaga mwili wa Robert.
  Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard Manyota akiuweka vizuri mwili wa Robert tayari kwa zoezi la kuaga.
  Mwili wa Robert Tillya ukipelekwa kwenye gari.

  Waombolezaji wakijiandaa kuingia kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Kilimanjaro.
  MWILI wa aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Robert Tillya hatimaye leo umeagwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa maziko.
  Marehemu Tillya alikuwa dereva wa Global na alifikwa na mauti Jumamosi iliyopita alfajiri baada ya kupata ajali maeneo ya River Side, Ubungo jijini Dar.
  Mamia ya waombolezaji wakiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, wafanyakazi wa Global, ndugu, jamaa na marafiki waliungana katika Hospitali ya Mwananyamala kumuaga mpendwa wao majira ya saa tano asubuhi.
  Marehemu Tillya alizaliwa Novemba 18, 1981 na ameacha watoto wawili wa kiume na wa kike.
  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Tillya mahali pema peponi. AMEN. 
   (PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)

  0 0

   Wahitimu wa shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone wakiwa kwenye picha ya pamoja
   Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone, Bi Usia Nkoma Ledama akizungumza jambo wakati wa mahafali ya tatu ya shule hiyo
   Mwalimu Debby Ndulla(wa kwanza kushoto) akiwatambulisha walimu wa Shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone ambao ni Mwalimu Tatu(wa pili kutoka kushoto) akifuatiwa na Mwalimu Revina(katikati), Mwalimu Doroth(wa pili kutoka kulia) pamoja na Mwalimu Aika(kulia)
   Mwalimu Debby Ndulla(wa kwanza kushoto) akiwatambulisha wadada wanaowalea watoto wadogo wa shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone.
   Mwalimu Debby Ndulla(kushoto) akimtambulisha Kaka Tobi mbele ya wazazi pamoja na walezi wa watoto waliofika kwenye mahafari ya Tatu ya shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone
   Kaka Tobi akiwapungia mikono wazazi pamoja na walezi wa watoto(hawapo pichani)
   
   Wanafunzi wa dalasa la Lantana katika shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone wakitoa burudani wakati wa mahafari ya tatu ya shule hiyo yaliyofanyika leo
   Wanafunzi wa dalasa la Lilies katika shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone wakitoa burudani wakati wa mahafari ya tatu ya shule hiyo yaliyofanyika leo
   Wanafunzi wa dalasa la Lavender katika shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone wakitoa burudani wakati wa mahafari ya tatu ya shule hiyo yaliyofanyika leo
   Bwana na Bibi Seyvunde wakizungumzia maendeleo ya mtoto wao ambaye alikuwa ni mmoja wa wahitimu leo.

  Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone, Bi Usia Nkoma Ledama(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast Gerald Hando(katikati) pamoja na Mwalimu Debby Ndulla(kushoto) 
   
   Baadhi ya wazazi pamoja na walezi waliofika katika mahafari ya watoto wao wakifuatilia yanayoendelea.
  Picha hizi chini ni wakati wa kukabidhiwa vyeti kwa wanafunzi hao waliohitimu leo
      Wazazi pamoja na walezi wakichukua matukio

  0 0

  Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa Bi Mboni Mhita  kushoto  akiwa na wajumbe wa kamati ya  ulinzi na usalama wilaya hiyo ya  Mufindi  katika  kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya  wilaya ya  Mufindi
  Baadhi ya  ndugu  wakichukua mwili wa ndugu  yao baada ya  kuutambua

  Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Bi Mboni Mhita (kushoto)  akimfariji  mmoja kati ya  majeruhi wa ajali ya  basi la Another G na lori  iliyoua 23 na kujeruhi 34 jana  ,wengine pichani ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya  Mufindi (picha na matukiodaimaBlog)


   Na MatukiodaimaBlog.
  MIILI yote  23  ya ajali  ya  basi  aina  Coster  mali ya kampuni ya  Another G lenye  namba  za  usajili  T 927 CEF aina ya  mitsubishi fuso iliyokuw3a ikifanya    safari  zake  kati ya Iringa – Njombe ambalo  liligoganga na   uso kwa  uso na lori  lenye namba za usajili T 916AQM  likiwa na  Tela lenye namba za usajili T 965 BEH Scania  imetambuliwa na  ndugu  zao.

  Kwa  mujibu  wa  mkuu  wa wilaya ya Mufindi ambae ni  mwenyekiti wa kamati ya  ulinzi na  usalama ya  wilaya  Bi Mboni Mhita kuwa  ndugu  wa marehemu  hao  waliokufa katika ajali  waliweza  kutambua  miili ya ndugu  zao jana na leo na   kuwa hadi  sasa hakuna mwili  ambao bado kutambulia na  hivyo kuvishukuru  vyombo  vya habari kwa  kushiriki kuhabarisha  juu ya ajali  hiyo  na wananchi  ambao  waliitikia na  kufika  kutambua miili   hiyo .

  Akizungumza na  mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz  leo  mkuu  huyo  wa  wilaya Bi Mboni  alisema  kuwa  jitihada  kubwa zimeonyeshwa na  vyombo  vya habari  vya ndani ya mkoa  wa Iringa na nje ya  mkoa ikiwemo mitandao ya  kijamii katika  kuhabarisha  umma na ndio  sababu ya utambuzi  wa miili  hiyo  kufanikiwa mapema baada ya habari kuenezwa vilivyo.

  Pia  mkuu  huyo wa wilaya   alipongeza  uongozi  wa JKT Mafinga   na uongozi  wa kitaifa  wa jeshi   hilo kwa  kujitolea  kusaidia mazishi  ya  vijana wake  ambao walikuwa wakielekea JKT Mafinga kwa ajili ya  kuripoti kwa kuanza mafunzo ya jeshi na   baadhi yao  kufa katika ajali  hiyo  huku baadhi  wakijeruhiwa kwani alisema ni  vigumu kwa taasisi  kujitolea  kusaidia mtu ambae hana mkataba  nae.

  Aidha  mkuu  huyo  wa  wilaya aliwaomba  wananchi wote  nchini ambao ndugu  zao walipoteza maisha katika ajali ya basi la Majinja lililoua  watu  zaidi ya 50 katika  eneo la Changalawe  mjini Mafinga  kufika kituo  cha  polisi Mafinga kwa ajili ya kutambua  na kuchukua mizigo ya  ndugu  zao  waliopoteza maisha katika ajali hiyo na kuwa mali  zote za marehemu hao zimehifadhiwa salama.
  Hata  hivyo  mkuu  huyo  wa  wilaya ya  Mufindi Bi Mboni alivitaka  vyombo  vya   usalama  barabarani katika  wilaya ya Mufindi  kuendelea na mkakati  wake wa  kuwabana madereva wanaovunja  sheria  za  barabarani na kuwachukulia hatu kali kama  njia ya  kupunguza ajali  hiyo.

  Alisema askari  hao  pia  wanapaswa  kukagua ubora  wa  vyombo  vya usafiri vyote na  vile ambavyo havina  ubora  ni heri  kuvifungia  hadi vitakapoboreshwa  kuliko  kuruhusu vyombo  vya  usafiri  chakavu  kufanya kazi  ya usafirishaji  wa abiria .

  Kuhusiana na wajibu  wa  shirika la viwango Tanzania (TBS) mkuu  huyo wa wilaya  alishauri kuwepo na mkakati makini wa TBS  kukagua  ubora  wa vyombo  vya usafiri vinavyoingizwa  nchini kwani mabasi  mengi ya abiria  siti   zake zimeshikiliwa na ngundi ya mbao na baada ya kutokea ajali siti hizo  hung'oka na kama abiria amefunga mkanda hulazimika kuchomoka na siti yake .

  Alisema katika ripoti ya ajali ya kwanza ya basi la Majinja  iliyotokea Machi  mwaka huu na kuua watu zaidi ya 50   kamati ya uchunguzi  ilibaini hilo na  kuwa  mwenye uwezo wa  kukagua  viwango  vya vyombo  hivyo  vya usafiri ni TBS kwa kushirikiana na wadau wengine kama Sumatra   na jeshi la polisi  kupitia kitengo  cha usalama barabarani.

  Wakati  serikali ya  wilaya ya  Mufindi kupitia mkuu  huyo wa  wilaya ikishauri TBS na  washirika  wake  kuweka mkakati wa kukagua   viwango  vya vyombo   hivyo  vya usafiri baadhi ya  wananchi   wilaya ya  Mufindi na mkoa wa Iringa wamekuwa na maoni  tofauti kwa  kulitaka jeshi la polisi kitendo  cha askari wa usalama barabarani kuanza kusindikiza mabasi hayo yanayotoka  usiku mkoani Njombe na Iringa ili  kuhakikisha abiria   hawazidi katika mabasi hayo ya usiku.

  Zacharia Sanga  mkazi  wa Mafinga  wilaya ya Mufindi na John Lumwesa mkazi  wa Iringa mjini  walisema kuwa  kimsingi mabasi hayo  yanajaza  abiria  kupita  kiasi na kutembea kwa mwendo mkali  zaidi kutokana na nyakati za usiku  askari  wa usalama barabara  kutokuwepo.

  Hivyo walitaka  askari  wa usalama barabarani  kuendelea kuwepo na tochi hadi usiku ili  kuthibiti ajali mbaya kama  hiyo ambayo mbali ya  kuwa ni uzembe wa dereva  wa basi ila kukosekana kwa askari  wa usalama barabarani  usiku ni  moja ya  sababu.

  Mganga  mkuu  wa  Hospitali  ya  wilaya ya  Mufindi Dr  Godluck  Mlimbila  alisema  kuwa hali za majeruhi 34 waliokuwa  wamelazwa katika  Hospitali   hiyo zinaendelea  vizuri na  kuwa mbali ya  wale  wanne ambao  hali  zao  zilikuwa mbaya  zaidi na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya   mkoa wa Iringa katika Hospitali  hiyo hadi jana majira ya saa 8 mchana  ni majeruhi kati ya 8 na 10  pekee  ndio ambao  walikuwa  wakiendelea na matibabu   huku  wengi  wao wakiwa  wameruhusiwa baada ya hali  zao  kuendelea  vema .

  0 0

  mail.google.comRais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudani ya Kusini Mhe. Riek Machar Teny Dhurgon baada ya kufanya naye mazungumzo mafupi walipokutana jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini, Jumatatu jioni Juni 15, 2015 baada ya Mkutano wa 25 wa Kawaida wa  Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU), ambapo Mhe Machar alimuomba Rais Kikwete aendelee kuwa mwenyeji wa mikutano ya mazungumzo ya amani kati ya vikundi vitatu vinavyosigana vya nchi hiyo. Kulia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
  PICHA NA IKULU

  0 0

   Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wea Monduli, Mh. Edward Lowassa, akitoa hotuba ya shukrani kwenye makao makuu ya CCM mkoa wa Sin gida, baada ya kupata wadhamini kufuatia kucvhukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa, ameweka rekodi mpya baada ya kupata wadhamini 22, 758. Tangu aanze kutafuta wadhamini mapema mwezi huu
   Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia  wana CCM na wakazi wa Manispaa ya Singida, waklati akiondoka makao makuu ya CCM mkoani Singida, Juni 16, 2015, baada ya kupata wadhamini.
   Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wana CCM na wakazi wa Manispaa ya Singida, waklati akiondoka makao makuu ya CCM mkoani Singida, Juni 16, 2015, baada ya kupata wadhamini.Picha na K-VISD MEDIA  0 0

   Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akimpa pole Mjane wa Marehemu, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, nyumbani kwake Majengo, Mkoani Shinyanga leo Juni 16, 2015. Mufti Simba alifariki dunia Juni 15, 2015 kwenye hospitali ya TMJ Mikocheni Jijini Dar es salaam.

   Mawaziri Wastaafu Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Mh. Fredrick Sumaye walipokwenda  kumpa pole Mjane wa Marehemu, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, nyumbani kwake Majengo, Mkoani Shinyanga leo Juni 16, 2015. Mufti Simba alifariki dunia Juni 15, 2015 kwenye hospitali ya TMJ Mikocheni Jijini Dar es salaam.

  0 0

  2
  Mshindi wa mbio za Acacia Tufanikiwe Pamoja Lake Zone Cycle Challenge, Masunga Duba aliyeinua mikono akishangilia mara baada ya kumaliza mbio hizo akiwa mbele ya wenzake. Mshindi huyo anatoka mkoa wa Shinyanga.
  3
  Makamu wa rais wa Kampuni ya Uchimbaji wa dhahabu ya Acacia, Deo Mwanyika (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya Acacia, Mishel Ash, (wa pili kutoka kushoto) ambaye pia ni kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu
  4
  Washindi wa mbio za wanawake (kilometa 80). Aliyesimama katikati ni Martha antony ambaye ndio aliibuka mshindi wa kwanza, akifuatiwa na Laulensia Luzuba, (mwenye mtoto) aliyekuwa mshindi wa pili na Veronica Saimon (wa kwanza kushoto) aliyejinyakulia nafasi ya Tatu.
  5
  Washiriki wa mbio za Acacia tufanikiwe pamoja lake zone cycle challenge wakimenyana vikali wakati wa mashindano hayo.

  6
  Afisa mkuu wa uendeshaji wa kampuni ya Acacia Mishel Ash akimvisha medali mshindi wa mbio hizo Martha Antony wakati wa Hafla ya Kutoa zawadi kwa washindi.

  1
  Mmoja wa washiriki wa mbio hizo akinywa maji wakati wa mashindano hayo.
  ………………………………….
  Na Mwandishi wetu
  Washiriki wa mbio za baiskeli zijulikanazo kama “Acacia Tufanikiwe Pamoja Lake Zone Cycle Challenge” kutoka mikoa ya Shinyanga na Mwanza wameendelea kuudhihirisha umma wa wakazi wa kanda ya ziwa na watanzania kwa ujumla kuwa mpaka sasa hawana mpinzani baada ya washiriki wa mbio hizo kuibuka kidedea katika fainali za kumtafuta mshindi wa kanda hiyo.
  Washiriki wa mikoa hii miwili wamejinyakulia nafasi zote za juu na hivyo kuwashinda wenzao wa mikoa mingine ya Kanda ya ziwa ikiwemo Kagera, Mara, Geita na Simiyu.

  Katika mbio za wanaume za umbali wa kilometa 156.6 kutoka Kahama mpaka Tinde na kisha Kurejea Kahama, mshindi wa mwaka jana Masunga Duba (Mwanza) aliibuka tena kidedea huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Lupilya Hamis(Shinyanga) na nafasi ya tatu ikimuendea Kulwa Tuki(Shinyanga), washindi hawa wamejinyakulia kitita cha pesa taslimu Sh1,500.000/- kwa mshindi wa kwanza, Sh1,200.000/= mshindi wa pili na Sh800,000/= kwa mshindi wa tatu.

  Kwa upande wa mbio za wanawake za umbali wa kilometa 80, kutoka Kahama mpaka Mwakata Kisha kurejea Kahama, timu ya mkoa wa Mwanza imedhihirisha kuwa wao bado ni mabingwa kwa kuibuka tena washindi wa mbio hizo, huku mshindi wa mbio za Mwaka jana Martha Antony, akiibuka mshindi wa kwanza akifuatiwa na Laulensia Luziba na nafasi ya tatu ikienda kwa Veronica Simon. Washindi hao wamepata zawadi ya pesa taslimu Sh1,200.000/= kwa mshindi wa kwanza, Sh800,000/= mshindi wa pili na Sh600,000/= mshindi wa tatu.

  Mbio hizo ambazo zimeandaliwa na Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) kwa udhamini wa kampuni ya uchimbaji wa Madini ya Acacia, inayomiliki migodi ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi, yote ikiwa mikoa ya kanda ya ziwa, kupitia mpango wake wa Tufanikiwe Pamoja ikiwa ni mara ya pili sasa ambapo mashindano ya mwaka huu yameonyesha mafanikio makubwa kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanyika.
  Akizungumza na washiriki wa mashindano hayo Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpyesa, ambaye alikua mgeni rasmi wa fainali hizi, amesema ana imani kuwa mashindano hayo yatasaidia kuibua vipaji ambavyo vitauletea sifa mkoa wa Shinyanga, Kanda ya ziwa na hata taifa kwa ujumla kwani baiskeli kwa maeneo hayo ndiyo jadi yao.
  Awali akimkaribisha Mkuu wa wilaya kuzungumza na washiriki hao, Makamu wa Rais wa Acacia Deo Mwanyika amesema kampuni ya Acacia imekuwa ikifanya shughuli za uchimbaji unaojali na ndio maana iliona vyema kuweka udhamini wake pia katika mchezo wa baiskeli, “toka tuanze huu sasa ni mwaka wa pili na tunayaona mafanikio makubwa kwani hata maeneo ambapo mchezo huu ulikuwa hauchezwi sasa unachezwa, hali ambayo imeongeza hamasa na idadi ya washiriki.”
  Aidha Makamu wa Rais huyo wa Acacia amesema mipango ya kampuni kwa sasa ni kuona pia inashiriki katika kuendeleza michezo mingine ikiwemo na soka.

  0 0

   Makamu wa Rais,Dk.Mohamed Gharib Bilal akiwasili katika Msikiti wa Kinondoni  kwa ajili ya ibada  kuswalia mwili wa aliyekuwa Mufti Alhaj  Sheikh Shaaban Issa Bin Simba iliyofanyika katika Msikiti wa Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya waislaam wakiwa katika msikiti wa kinondoni katika ibada ya kuswalia mwili wa aliyekuwa Mufti Alhaj  Sheikh Shaaban Issa Bin Simba iliyofanyika katika Msikiti wa Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya waombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mufti Alhaj  Sheikh Shaaban Issa Bin Simba wakiwa katika majonzi  katika ofisi ya Makao Makuu ya Bakwata,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
   Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe akimpa pole Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu kufuatia na msiba aliyekuwa Mufti Alhaj  Sheikh Shaaban Issa Bin Simba katika msikiti wa Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.)  0 0

  Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kulia), akimuelekeza jambo mwananchi aliyetembelea banda la MSD katika maonyesho hayo yaliyoyoanza leo na kufikia tamati baada ya wiki moja
  Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akimuelekeza jambo Mwanahabari aliyetembelea banda la MSD katika maonyesho hayo. Katikati ni Ofisa Udhibiti Viwango na Ubora wa MSD, Betia Kaema.
  Ofisa Udhibiti Viwango na Ubora wa MSD, Betia Kaema (kushoto), akizungumza na mwananchi aliyetembelea banda la MSD.
  Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya akiwa ndani ya banda la MSD.
  Vifaa tiba vikioneshwa katika banda hilo.
  Muonekano wa banda la MSD katika maonyesho hayo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

  0 0


  Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (kushoto), akionesha Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa wizara hiyo, Dk.Fidelis Myaka.
  Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Raphael Daluti Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam leo asubuhi.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Mhandisi Raphael Daluti (katikati), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo.

  Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa wizara hiyo, Dk.Fidelis Myaka (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
  Mtafiti Mkuu wa Kilimo wa Costech, Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mada fupi kuhusu maendeleo ya bioteknolojia katika uendelezaji wa Sekta mbalimbali hususan ya kilimo.

  Kaimu Mkurugenzi wa Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia (Costech), Dk.Nicholas Nyange (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
  Wadau wa sekta ya kilimo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Wanahabri wakichukua taarifa hiyo.
  Wadau wa sekta ya kilimo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
  Waziri Zambi na viongozi wengine wakiwa meza kuu.
  Uzinduzi ukiendelea.

  Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.

  Dotto Mwabale

  NAIBU Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi amesema Tanzania haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia katika uendelezaji wa Sekta mbalimbali hususan ya kilimo.

  Kauli hiyo aliisema wakati akizindua Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam leo asubuhi.

  " Jukumu letu ni kushirikiana na wadau wote kuhakikisha tunakuwa na matumizi salama na endelevu ya bioteknolojia ili kuiondolea wasiwasi jamii kuhusu dhana iliyopo ya athari zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa" alisema Zambi.

  Alisema kutokana na mantiki hiyo, Serikali imeweka mikakati mbalimbali katika kushughulikia masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya mwaka 2010 yenye lengo la kujenga uwezo wa kutumia teknolojia hiyo kwa kuzingatia faida zilizojidhihirisha katika kuboresha afya ya wanyama na binadamu, kilimo, viwanda na mazingira.

  Zambi alisema sera ya taifa ya kilimo ya mwaka 2013 inatamka kwamba uelewa mdogo wa umma kuhusu matumizi ya bioteknolojia unachangia kuwepo kwa upokeaji mdogo wa teknolojia hiyo kwa madhumuni ya kuongeza matumizi ya mbinu za bioteknolojia ya kilimo katika uzalishaji, tija na kipato kwenye sekta ya kilimo.

  Kaimu Mkurugenzi wa Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia (Costech), Dk.Nicholas Nyange alisema teknolojia hiyo mpya ya uzalishaji wa mazao ni muhimu sana hapa nchini katika sekta ya kilimo.

  Mtafiti Mkuu wa Kilimo wa Costech, Dk.Emmarold Mneney alisema changamoto kubwa waliyonayo watafiti hapa nchini ni pesa na kuwa wanahitajika kutoka katika utafiti wa ndani na kutoka nje kama wafanyavyo wenzao wa nchi za Uganda, Kenya ambao tafiti zao zimefanikiwa katika kilimo cha mahindi, pamba na mohogo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

older | 1 | .... | 556 | 557 | (Page 558) | 559 | 560 | .... | 1897 | newer