Katibu Mkuu wa CCM,Ndg Kinana akisisitiza jambo.
Umati wa wakazi wa Chato mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa stendi ya Zamani.Katibu Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inabidi ifute kodi kandamizi zinazowazuia wananchi kurahisisha maisha yao.
Umati wa wakazi wa Chato mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa stendi ya Zamani.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg Kinana akisisitiza jambo
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana ukipokelewa katika kijiji cha Kasenga,ukitokea mkoani Kagera,tayari kwa kuanza ziara ya siku 6 mkoani Geita.
Ndugu Kinana akisalimiana na wananchi wa Kasenga,wilayani Chato mkoani Geita ikiwe ni sehemu ya mapokezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi ofis mpya ya CCM katika kata ya Kasenga,wilaya ya Chato mkoani Geita.
Muonekano wa ofisi hiyo ya CCM
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi mara baada ya kuwasha mtambo wa maji uliojengwa Chato Mlimani kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji utakaohudumia wakazi wa mji huo leo, wakati wa ziara yake katika mkoa wa Geita .
Kinana anaendelea na ziara hiyo ya kikazi mkoani humo baada ya kumaliza ziara kama hiyo mkoani Kagera jana, Kinana anaendelea na ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, kukosoa na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi kwa maisha na maendeleo yao kwa ujumla akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pichani kushoo na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakisoma bango lenye maanidishi lililobebwa na baadhi ya vijana
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Paulina Sabinati mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
Katibu Mkuu wa CCM akizungumza na Wanachama wa Mshikamano Saccos wapatao zaidi ya 400,ampapo pia alikabidhi mikopo kwa wanachama wa saccos hiyo wapatao 20,kiasi cha shilingi milioni 78
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mkuu wa wilaya ya Chato Ndugu Rodrick Mpogole, viongozi wa CCM wilaya ya Chato pamoja na mafundi wa Tanesco akishiriki kutandaza waya za umeme katika mradi wa umeme vijijini REA katika kijiji cha Mkungo,wilayani Chato mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Makurugusi kuhusiana na mpango wa kupata umeme katika kijiji chicho,ambapo kijiji chao kimerukwa na kuachwa bila kuweka umeme,hiuvyo Wananchi hao wamemuomba Ndgugu Kinana kuhakikisha anawasaidia na wao wanapata umeme katika kijiji chao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana tano na wananchi hao mara baada ya kuwaahidi kuongea na Waziri wa Nishati na Madini ili kijiji hicho kiwekewe umeme vijijini REA, ambapo wanakijiji hao walijawa na furaha mara baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa kiongozi huyo wa juu wa CCM.
Umati wa wananchi wa Chato mjini wakishangilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyeanza ziara ya siku sita mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa nyumba ya daktari katika kijiji cha Ihanga wilayani Chato.
Wananchi wakinyanyua mikono yao juu juu kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Chato mjini ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Chato ikiwa siku yake ya kwanza ya ziara mkoani Geita baada ya kumaliza ziara ya siku 10 mkoa wa Kagera.Katibu Mkuu wa CCM anazunguka nchi nzima kukagua,kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM akiwa ameambatana Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nnape Nnauye..
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Diwani wa kata ya Biziku Bw. Magomamoto Zanzibar akijinadi na kueleza namna alivyotekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM katika kata yake.