Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MAJINA YA WASHINDI WA TUZO ZA KTMA 2015 HAYA HAPA

$
0
0
1. KIKUNDI BORA CHA MWAKA - BONGO FLEVA - YAMOTO BAND
2. KIKUNDI BORA CHA MWAKA TAARAB - JAHAZI MODERN TAARAB
3. BENDI BORA YA MWAKA - FM ACADEMIA
4. MSANII BORA CHIPUKIZI - BARAKA DA PRINCE
5. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA (WAITE) -MRISHO MPOTO FT. FELLY KANO
6. WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA - NITAMPATA WAPI - DIAMOND PLATINUMZ
7. WIMBO BORA WA AFRO POP - MWANA ALI KIBA
8. VIDEO BORA YA MWANAMUZIKI YA MWAKA - MDOGOMDOGO - DIAMOND PLATINUMZ
9. MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA BENDI - ENRICO
10. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA BONGO FLEVA - NAHREEL
11. MTUNZI BORA WA MWAKA- HIP HOP - JOH MAKINI
12. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI - JOSE MARA
13. MTUNZI BORA WA MWAKA BONGO FLEVA - ALI KIBA
14. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB- MZEE YUSSUF
15. MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIUME - ALI KIBA
16. MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIKE - VENESSA MDEE
17. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB - MZEE YUSSUF
18. MWIMBAJI BORA WA KIUME BONGO FLEVA - ALI KIBA
19. MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB - ISHA MASHAUZI
20. MWIMBAJI BORA WA KIKE BONGO FLEVA - VANESSA MDEE
21. WIMBO BORA WA TAARAB (MAPENZI HAYANA DHAMANA)- ISHA MASHAUZI
22. WIMBO BORA WA MWAKA (MWANA)- ALI KIBA
23. WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI (WALEWALE) -VIJANA WA NGWASUMA
24. WIMBO BORA WA R&B (SIKSIKII)- JUX
25. RAPA BORA WA HIP HOP - KIPI SIJASIKIA ( PROF J FT. DIAMOND PLATINUMZ)
26. MSANII BORA WA HIP HOP - JOH MAKINI
27. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI (SURA YAKO) - SAUTI SOL

WAZIRI BERNARD MEMBE APATA UDHAMINI ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akishuhudia mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitia saini kumdhamini kwenye fomu yake ya kugombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, katika ofisi ya CCM wilaya ya Kaskazini ‘B mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar jana, ambapo alipata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote mine ya Unguja. Katikati ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM  wilaya hiyo, Haji Machano Haji. Picha zote na John Badi
5
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati), akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kati, Ally Yusuf Salim zilizojazwa na wanachama wa CCM mkoa wa Kusini Unguja jana kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote minne ya Unguja. Kushoto ni Katibu wa CCM Kata ya Jumbi, Christina Athony.
2
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akilakiwa na  wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Mjini Unguja, baada ya kuwasili kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Aman kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote minne ya Unguja.
3
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati) akifurahia jambo pamoja na  wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Mjini Unguja, kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Aman jana waliofika kumdhamini ili awanie Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1500 katika mikoa yote minne ya Unguja.

MAADHIMISHO YA MIAKA 90 YA SKULI YA NDIJANI YAFANYIKA WILAYA YA KATI MKOA WA KUSINI UNGUJA

$
0
0
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna (wa pili kushoto) akipata maelezo wakati alipotembelea maonesho katika maadhimisho ya miaka 90 ya Skuli ya Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kwa niaba ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheini leo (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,Picha zote na Ikulu.2
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi Asma Abdalla Khamis darasa la kumi na mbili Ndijani kuhusu utengenezaji wa Mafuta ya mgando ambayo utengenezaji wake unatokana na Nta,mafuta ya Nazi na Mawardi wakati alipotembelea maonesho katika maadhimisho ya miaka 90 ya Skuli ya Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kwa niaba ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheini leo (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Ahmada Hija.3
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Chara Stivin Bakari ambao hutoa misaada mbali mbali kwa Watu wenye ulemavu wakati alipotembelea maonesho katika maadhimisho ya miaka 90 ya Skuli ya Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kwa niaba ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheini leo Juni 14, 2015.4
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Chara Stivin Bakari wenye ofisi zake Mazizini Mkoa wa Magharibi   wakati alipotembelea maonesho katika maadhimisho ya miaka 90 ya Skuli ya Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja   leo akimuwakilisha Rais wa Zanzibar katika sherehe hizo.
5
Baadhi ya wazee na wananchi wa Kijiji cha Ndijani na Vitongoji vyake waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 90 ya Skuli ya Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna alipozungumza nao leo wakati akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Skuli hiyo.6
Baadhi ya wazee na wananchi wa Kijiji cha Ndijani na Vitongoji vyake waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 90 ya Skuli ya Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna alipozungumza nao leo wakati akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Skuli hiyo,
7
Baadhi ya wazee Akina mama na wanafunzi wa Skuli ya Bembela ya Mjini Magharibi walioalikwa katika katika sherehe za maadhimisho ya miaka 90 ya Skuli ya Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna alipozungumza nao leo wakati akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Skuli hiyo
8
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna  akitoa hutuba katika sherehe za maadhimisho ya miaka 90 ya Skuli ya Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Skuli hiyo (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Dkt.Idriss Muslim Hija na (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Kati Mhe Vuai Mwnyi.

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AHUDHURIA IBADA MJINI DODOMA-JUNI 14,2015

$
0
0
01
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakishiriki  katika ibada ya kwanza  ya Jumapili kwenye kanisa Katoliki la Paulo wa Msalaba  mjini Dodoma Juni 14, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
03
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakisalimiana na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Dodoma, Mhashamu Mathias Isuja baada ya ibada ya kwanza katika kanisa la Paulo wa Msalaba mjini Dodoma Juni 14, 2015.
04
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiwa katika picha ya pamoja na wanakwaya baada ya kuhudhuria ibada ya kwanza katika kanisa Katoliki la Paulo wa Msalaba mjini Dodoma Juni 14, 2015.
05
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na wanakwaya baada ya ibada ya kwanza katika kanisa la Mtakatifu Paulo wa  Msalaba mjini Dodoma Juni 14, 2015.
06
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Huruma ya mjini Dodoma baada ya kushiriki katika ibada  ya kwanza kwenye kanisa Katoliki la Paulo wa Msalaba mjni Dodoma Juni 14, 2015.

KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO, ZITTO KABWE AWAHUTUBIA WAKAZI WA MKOA WA TABORA

$
0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwahutubia wakazi wa mji wa Tabora juzi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Town School, mara baada ya kuzindua Azimio la Tabora lililouhishwa kutoka azimio la Arusha.
2
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Samson Mwigamba,  akiwahutubia wakazi wa mji wa Tabora juzi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya ,Town School, mara baada ya kuzindua Azimio la Tabora lililouhishwa kutoka azimio la Arusha.
3
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Anna Mghira, akiwahutubia wakazi wa mji wa Tabora juzi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya ,Town School, mara baada ya kuzindua Azimio la Tabora lililouhishwa kutoka azimio la Arusha.
5
Wakazi wa mji wa Tabora wakifuatilia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Town School, mara baada ya kuzindua Azimio la Tabora lililouhishwa kutoka azimio la Arusha.
1

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AZINDUA TAMASHA LA MICHEZO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda  Amezindua Tamsha la Michezo na afya lenye lengo la kuboresha afya ambalo limeandaliwa na kampuni ya Fern (T) Ltd Lililofanyika leo 14 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.Lengo kubwa la tamasha hilo ni kuwakutanisha watu wa rika mbalimbali ili kufurahia na kuweka miili yao sawa kwa afya bora.

Tamasha hilo Limepambwa na burudani kwa ajili ya kuwaburudisha watu na wataalamu mbalimbali waliobobea kwenye sekta ya ufundishaji juu ya ufanyaji mazoezi na wataalamu wa afya watakuwepoa kwa ajili ya kutoa ushauri wa afya na lishe.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda  Akiteta Jambo na Mratibu wa tamasha hilo, Dimo Debwe Mitiki.Katika jitihada za kuijengea jamii ya kitanzania tabia ya kufanya mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya zao, kampuni ya Fern (T) Ltd Iliona ni vema Kuandaa  tamasha la kimichezo lililoambatana na mazoezi pamoja na burudani kwa ajili ya watu wa kada mbali mbali.
 Lengo kubwa la tamasha hilo ni kuwakutanisha pamoja watu wa kariba mbalimbali na umri tofauti kufurahi pamaja na kuweka miili yao fit na kuongeza kuwa, watakuwepo wataalamu mbalimbali waliobobea kwenye sekta ya ufundishaji juu ya ufanyaji mazoezi na wataalamu wa afya watakaotoa ushauri mbalimbali wa afya na lishe.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Alipata nafasi ya Kupima Afya yake kwenye Tamasha hilo kutoka kwa Wataalamu wa Afya na Lishe walioendesha zoezi hilo bure..Kwa siku za hivi karibuni watu wengi wamekuwa wakifuatilia sana masuala ya afya kitu ambacho kimepelekea kuibuka kwa vikundi vingi/vilabu vingi vya mazoezi. Kutokana na kutokuwepo kwa muundo rasmi unaowakutanisha watu hawa wapenda mazoezi Fern imetambua na kuona fursa hiyo kupitia Tamasha Hilo..
  Washiriki wa Tamasha hilo Kutoka maeneo Mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaaam  wamepata Nafasi ya Kufanya Mazoezi ya Jogging Pamoja na Mkuu wa Wilaya.Washiriki wa tamasha hilo kuwa ni pamja na Joging clubs zaidi ya 100 kutoka wilaya zote 3 za mkoa wa Dar es Salaam; Temeke,Kinondoni na Ilala, makampuni na Taasisi mbalimbali wakiwemo, CRDB Bank, TCDC, SMART TELECOMMUNICATION, PSI ,washiriki wengine ni pamoja na Gyms kama vile AZURA, THE GYM, GENESIS HEALTH CENTRE, POWER ON FITNESS, HOME GYM NA UNIVERSAL GYM, wasanii wa tasnia ya Filamu na Muziki nchini.Wahiriki walikusanyika viwanja vya leaders kuelekea Coco beach na kuzunguka maeneo ya kinondoni kisha kurudi tena Leaders na baada ya watu kurudi leaders waliendelea na mazoezi ya viungo
Zoezi hili likimalizika litafuatiwa na kipindi cha dondoo za lishe na afya kutoka kwa kwa wataalamu waliobobea ambapo watu watapata fursa wa kujifunza mambo kadhaa yahusuyo afya,” alifafanua .
 Tamasha hilo lililokuwa la aina yake limewavutia watu mbalimbali
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akiongea na Mmoja wa Watoto walioshiriki Tamasha hilo leo
 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akishiriki Kufanya Mazoezi Mbalimbali Katika Tamasha hilo lililofanyika Katika Viwanja vya Leaders

LOWASSA AENDELEA KUVUNA WANACHAMA NDANI YA MKOA WA KATAVI.

$
0
0
  Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu zenye majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Katavi leo Juni 14, 2015, waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Bi. Elizabert Kashira. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkomo maelfu ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Mpanda, waliofurika kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi leo Juni 14, 2015.Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwashukuru wanaCCM wa Mji wa Mpanda waliofurika kwenye waliofurika kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi leo Juni 14, 2015, mara baada ya kukabidhiwa fomu za kumdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi. 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na wanaCCM wa Mji wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa wakati alipofika kutafuta udhamini wa kupewa ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya wanCCM 4045 wamemdhamini.

BM HAIR & BEAUTY CLINIC WAZINDUA HUDUMA MPYA JIJINI DAR

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akikata utepe kuzindua huduma mpya za BM Hair and Beauty Clinic huku akisaidiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele leo jijini Dar es Salaam. Kwa sasa wamefikisha miaka 14 kwa kutoa huduma zenye ubora tokea imeanzishwa.   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akionyesha grasi juu yenye kinywaji pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele kuashiria kuzinduliwa kwa huduma mpya.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimia na wafanyakazi wa BM Hair and Beauty Clinic mara baada ya kuzindua huduma za kipekee ijulikanayo kwa jina la (Premier Services) iliyofanyika Kinondoni jijini Dar es Salaam. Pembeni kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele.

Mmoja ya wafanyakazi wa BM Hair & Beauty Clinic, Neema Mushi akimpa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda juu ya huduma wanazozitoa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele akimpa maelezo machache Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda juu ya bidhaa na huduma wanazotoa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akionyeshwa na kupewa maelezo juu vifaa mbali mbali vya kisasa vinavyopatikana ndani ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele.
Tukizungumzia suala la vifaa vyenye ubora BM Hair & Beauty Clinic inaongoza na sasa imeongeza huduma zake.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiondoka eneo la tukio mara baada ya kumaliza kuzindua huduma mpya za BM Hair & Beauty Clinic. 
Wafanyakazi wa BM Hair & Beauty Clinic wakishangilia mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele na wafanyakazi wa BM Hair & Beauty Clinic.

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA 25 WA KAWAIDA WA UMOJA WA AFRIKA JIJINI JOHANNESBURG LEO

$
0
0
2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongzi wengine wa Umoja wa Afrika wakiimba wimbo wa umoja huo katika ukumbi wa Sandton Convention Centre Jijini Johannsburg, Afrika Kusini, wakati wa ufunguzi wa mkutano wao wa 25 wa kawaida leo June 14, 2015.3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Zanzibar Dkt.MwinyihajiMakame Mwadini na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba  katika ukumbi wa Sandton Convention Centre Jijini Johannsburg, Afrika Kusini, wakati wa ufunguzi wa mkutano wao wa 25 wa kawaida wa Wakuu wa nchi anachama wa Umoja wa Afrika leo June 14, 2015
4
Wajumbe wakati wa ufunguzi wa mkutano wao wa 25 wa kawaida wa Wakuu wa nchi anachama wa Umoja wa Afrika leo June 14, 2015.PICHA ZOTE NA IKULU

Wanazuoni wakutana kujadili suala la 'Msimamo Mkali katika Dini' Maana, Matukio, Sababu na Suluhisho.

$
0
0
  Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini la Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Shehe Abdallah Ndanga (kushoto), akizungumza wakati wa kongamano kuhusu ‘Msimamo Mkali katika Dini, Maana, Matukio, Sababu na Suluhisho’ lililowashirikisha viongozi kutoka zaidi ya misikiti 100 , viongozi wa taasisi za kiislamu, wanazuoni, na vijana wanaoendesha harakati za kiislamu katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kushoto kwake ni baadhi wa viongozi wa umoja huo; Shehe Suleiman Amrani Kilemile, Shehe Muharram Juma Doga na Shehe Ibrahim Hamadi.
 Baadhi ya washiriki wa kongamano la siku moja lililokuwa likijadili kuhusu ‘Msimamo Mkali katika Didi, Maana, Matukio, Sababu na Suluhisho’  lililoandaliwa na Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania na kufanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo akitoa mchango wake wa mawazo kuhusu mjadaala uliokuwa ukiendelea.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wakipiga picha ya kumbukumbu. Ilielezwa kuwa suala la msimamo mkali katika dini linapingana na imani na mafundisho sahihi ya uislamu likichangiwa pia na ukosefu wa elimu sahihi ya dini ya kiislamu.

INTRODUCING New Video: Yamoto Band ~ Nisambazie Raha

WAZIRI BERNARD MEMBE AHANI MSIBA WA MAREHEMU SALMIN AWADH SALMIN MJINI UNGUJA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimpa mkono wa pole Bi. Mwaka Mohamed ambaye ni mjane wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM), marehemu Salmin Awadh Salmin aliyefariki mapema Februari mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba nyumbani kwake, Mkoa wa Mjini Unguja, Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akitoa mkono kwa familia ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM), marehemu Salmin Awadh Salmin aliyefariki mapema Februari mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba nyumbani kwake, Mkoa wa Mjini Unguja, Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akitoa ubani kwa Bi. Mwaka Mohamed ambaye ni mjane wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM), marehemu Salmin Awadh Salmin aliyefariki mapema Februari mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba nyumbani kwake, Mkoa wa Mjini Unguja, Zanzibar.

NIAMBIE LIVE SHOW WIKI HII (TEASER)

UN YAISIFU TANZANIA KUWA MSTARI WA MBELE KUTETEA ALBINO

$
0
0
UN 6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akihutubia wananchi waliohudhiria maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UN 1
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini, Alvaro Rodriguez akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya wenye Ualbino yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UN 3
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini, Alvaro Rodriguez akipongezwa na Rais Jakaya Kikwete baada ya kutoa hotuba yake katika Maadhimisho ya Siku ya wenye Ualbino yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UN 4
Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya wenye Ualbino yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UN 5
Mwenyekiti wa wenye ulemavu wa ngozi nchini(TAS), Ernest Kimaya akitoa nasaha zake.

UN 7
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kebwe Steven Kebwe akitoa nasaha zake.
UN 8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Jakaya Kikwete akiwapongeza watoto wenye Ualbino wanaofadhiliwa na USAID chini ya mpango wa Tuwalee.
UN 13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque baada ya maadhimisho hayo, kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda.
UN 12
Baadhi ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa na watu wenye nia mbaya.(Picha na modewjiblog)
Na Mwandishi wetu, Arusha

MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodgriguez amepongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kushawishi dunia siku ya kukumbuka watu wenye ulemavu wa ngozi duniani.

Alisema dhana ya Juni 13 ilianzia Tanzania kwa mshikamano kati ya serikali ya Tanzania na mashirika yasiyo ya kiserikali kama Shirika la Under the same sun (TAS).Alisema kutokana na bidii walizoonesha Novemba 18,2014, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha siku hiyo kuadhimishwa duniani kote kila ifikapo Juni 13.

Akihutubia kabla ya rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi kuzungumza, Rodgriguez alisema dunia inapaswa kuangalia kwa makini maisha ya walemavu wa ngozi na kuzuia ukatili dhidi yao.

Alisema pamoja na haja ya kuongeza ufahamu wa watu juu ya masuala ya ualibino na maalbino ni vyema jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kwamba kila mwanamke, mwanamume na mtoto wanatendewa kwa usawa na kwa heshima. Alisema kutokana na haja hiyo Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanyakazi na serikali ya Tanzania kuboresha maisha ya watu wake kwa kusaidia kuimarisha mfumo wa mahakama, masuala ya wakimbizi na masuala ya utoaji haki.

Alisisitiza kuwa kuwapo kwa haki, usawa na utu kutahakikisha kuwapo kwa amani na usalama kwa jamii zenye ulemavu wa ngozi.

Alisema kwa sasa kuna woga mkubwa kwa jamii ya ulemavu wa ngozi kutokana na chuki, unyanyapaa, mashambulizi ya kutisha, mauaji na kugeuzwa kuwa bidhaa huku wakiuuawa kwa sababu za matambiko ya kutafuta utajiri. Mratibu huyo alisema kwamba taifa na jamii ya binadamu wote wanatakiwa kushirikiana katika kuzuia ukatili kwa wenye ulemavu na pia kuwasaidia kukabilina na mazingira yao magumu hasa upatikanaji wa vifaa vya kuwakinga na madhara ya jua.

Alitaka pia jamii kuelimishwa kuhusu mtiririko wa vinasaba vinavyosababisha ulemavu wa ngozi na kupambana na ubaguzi na tishio la maisha kwa kutoa mafunzo mbalimbali. Aidha alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kazi na wanachama wa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali na Serikali kuimarisha haki za binadamu .
UN 10
Baadhi ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa na watu wenye nia mbaya.
UN 11
Baadhi ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa na watu wenye nia mbaya.

Article 22

$
0
0
Tazama ripoti hii fupi kuhusu matembezi ya SUSAN G. KOMEN RACE FOR THE CURE mwaka 2015 hapa Washington DC


ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WACHANGIAJI DAMU SALAMA DUNIANI KWA PAMBANO LA MPIRA WA MIGUU KATIKA KIWANJA CHA AMANI

$
0
0
1
Waziri wa Kilimo na Mali Asili Dkt. Sira Ubwa Mamboya akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa ya Jangombe na Kimbunga ya Tazari kabla ya kupambana katika mchezo maalum wa maadhimisho ya siku wachangiaji damu salama katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar. Wa kwanza (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
2
Meneja wa Mpango wa Damu Salama Zanzibar Dkt. Mwanaheri  Ahmed Abdulrahim akizungumza na wananchi na wanamichezo katika maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama katika kiwanja cha Amani Mjini Zanzibar.
3
Wachezaji wa Timu ya Kimbunga ya Tazari ya Mkoa wa Kaskazini Unguja wakishangiria ushindi wao baada ya kuilaza timu ya Taifa ya Jangombe mabao 3-2 katika pambano maalum la siku ya wachangiaji damu salama liliofanyika Uwanja wa Amani.
4
Waziri wa Kilimo na Mali Asili Dkt. Sira Ubwa Mamboya akimkabidhi ngao mmoja wa wachangiaji  bora wa damu salama Abdalla Muhd Kassim kwa niaba ya wenzake watatu ambao wamechangia mara 40 kila mmoja.
5
Waziri wa Kilimo na Mali Asili Dkt. Sira Ubwa Mamboya akimkabidhi kombe la ushindi Nahodha wa timu ya Kimbunga Shaaban Ramadhan Kangeta baada ya kuilaza Taifa ya Jangombe Mabao 3-2 katika pambano la siku ya wachangiaji damu salama liliofanyika uwanja wa Amani.
6
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama Dkt. Sira Ubwa Mamboya  na viongozi wa Wizara ya Afya na baadhi ya wachangiaji damu salma kutoka Taasisi mbali mbali na watu binafsi katika maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama yaliyofanyika Uwanja wa Amani Zanzibar

WAZIRI LUKUVI AHIMIZA MPANGO SHIRIKISHI KUENDELEZA ARDHI KATA YA MAKONGO KWA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU.

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na akizungumza na wananchi wa Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya Mpango Shirikishi wa kuendeleza ardhi na makazi ya wananchi kwa kushirikiana na Serikali.
3
Diwani wa Kata ya Makongo Deusdedith Mtiro akimkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na ujumbe alioambatana nao wakati wa ziara ya kikazi iliyokuwa na lengo la kuongea na wananchi wa Kata ya Makongo leo kuhusu namna bora ya kuwashirikisha wananchi katika kuendeleza ardhi ndani ya kata hiyo kwa maendeleo endelevu na yenye manufaa kwa pande zote mbili yaani wananchi na Serikali.
2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angellah Kairuki akisisitiza namna mabaraza ya ardhi yanavyopaswa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa, wakati wa mkutano wa Waziri wa wizara hiyo na wananchi wa kata ya Makongo leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Makongo Deusdedith Mtiro.
4

5
Mkazi wa Makongo juu Bi Ritha Mbotto akimuuliza swali Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo pichani) wakati mkutano na wanchi wa kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwandishi wa habari wa TBC Edward Kondela.
6
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiteta jambo na Naibu Waziri wake Angellah Kairuki wakati wa mkutano na wananchi wa kata ya Makongo leo jijini Dar es salaam.
7
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Makongo wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na ujumbe wake wakati wa mkutano na wananchi wa kata ya Makongo leo jijini Dar es salaam.
89
…………………………………………………
(Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

SERA YA MAENDELEO YA VIJANA NA HARAKATI YA KUWAKOMBOA VIJANA NCHINI

$
0
0
Na: Genofeva Matemu, na Benjamini Sawe
Serikali iliandaa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana mnamo mwaka 1996; Utekelezaji wa Sera hii umekabiliwa na changamoto mbalimbali za kitaifa na za kidunia.
Katika milenia hii ya Sayansi na teknolojia, vijana wa kiume na kike ni rasilimali kubwa zaidi kwa sasa na siku za baadaye; wanatoa msukumo wa kuleta mageuzi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa katika sayari hii yenye mabadiliko ya haraka duniani.
Mazingira ya dunia, kijamii, kiuchumi na kisiasa yameathiri hali ya vijana nchini Tanzania, Uhamiaji wa vijana kutoka maeneo ya vijijini kwenda mijini umeongeza mzigo wa huduma za Umma mijini na miundombinu ya kijamii hivyo kuleta ukuaji wa haraka wa sekta isiyo rasmi na ongezeko la matukio ya ajira mbaya kwa vijana.
Vijana wengi nchini wanafanya kazi kwenye sekta za kilimo, uvuvi, madini, ufugaji wa wanyama na viwanda vidogovidogo kama vya useremala, sonara, biashara ndogondogo za kuuza nguo za mitumba, matunda na vyakula vya aina mbalimbali.

Pamoja na ukweli kwamba vijana hawa wamejiajiri lakini bado wanakumbana na matatizo mengi katika kutekeleza shughuli zao; matatizo hayo ni pamoja na ukosefu wa mtaji wa kufanyia kazi, vifaa na ujuzi wa kiufundi au stadi muhimu za maisha.
Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 1996 imewezesha utekelezaji wa program mbalimbali za maendeleo ya vijana ambazo ni pamoja na stadi za kujenga uzoefu kwa ajili ya uwezeshaji wa kiuchumi, maadili mema, mwenendo na utendaji bora, ushiriki wa vijana na utoaji wa huduma rafiki kwa vijana.
Hata hivyo Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 inalenga masuala ya maendeleo ya vijana katika uwezeshaji wa kiuchumi, mazingira, ukuzaji wa ajira, ushiriki wa vijana katika masuala mbalimbali kwenye jamii, VVU na UKIMWI, jinsia, Sanaa na utamaduni, michezo, afya ya uzazi kwa vijana na masuala ya maisha ya familia.
Katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imejizatiti kutoa elimu ya uhamasishaji, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, ujuzi, na stadi za maisha kwa vijana wote nchini kwa kukutana na vijana katika kila Halmashauri na kutoa elimu inayowasaidia vijana kujitambua hivyo kutumia fursa mbalimbali walizonazo kujiendeleza.
Kwa kuanzia Vijana kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mbeya, Dodoma,Kilimanjaro, Singida, Kigoma, Manyara, Arusha na Mara wamefikiwa na Wizara ya habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika harakati za kuwakomboa vijana kifikra na kiuchumi ili kuondokana na kundi la vijana lisilokuwa na mwelekeo katika jamii.
Wizara inaendelea kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishajimali, kusajili vikundi hivyo na hatimaye vikundi hivyo kujiunga katika SACCOS za vijana zilizoanzishwa, ikizingatiwa kuwa hii ni mojawapo ya kigezo muhimu cha kikundi kuweza kupewa Mkopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mfuko wa Maendeleo ya vijana una changamoto mbalimbali zikiwemo: Fedha zinazotengwa kwa ajili ya Mfuko kuwa kidogo ukilinganisha na mahitaji ya Vijana, Vijana wengi kutokuwa na mwamko wa kurejesha fedha kwa wakati, Maandiko ya Miradi mingi inayowasilishwa kutokidhi vigezo ili kuweza kukopesheka. 
Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ni kwa ajili ya Vijana wote nchini, kila kijana anayo haki ya kunufaika na Mkopo kutoka katika Mfuko huu. Vijana wanatakiwa kukopa na kurejesha na siyo kama wengine wanavyohusisha fedha hizi na masuala ya kisiasa wakidhani ni takrima. Pia, wanatakiwa kuzingatia masharti/ vigezo vilivyopo katika mwongozo wa Mfuko pindi wanapoandaa Maandiko ya Miradi yao.
Serikali imelenga kuendelea kuboresha Mfuko huu ili kuwa na fedha za kutosha na kuweza kuwafikia vijana wengi nchini, hii itasaidia vijana wengi kujiajiri wao wenyewe na kutengeneza ajira kwa vijana wengine. 
Katika kutekeleza azma ya kusaidia Vijana, jumla ya shilingi Bilioni 6 zimetengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya kusaidia mfuko wa Maendeleo ya Vijana, ambapo Vijana kutoka Halmashauri mbalimbali nchini wamepatiwa mikopo yenye unafuu, riba kidogo na upatikanaji wake ukiwa ni wa urahisi.

Mfuko huu ulianzishwa mwaka 1993, chini ya kifungu namba 17(1) cha The Exchequer and Audit Ordinance (Cap 439) No 21 of 1961, lengo likiwa ni kuwasaidia vijana ili wapate mikopo yenye masharti nafuu.
Katika ziara yake ya kukagua miradi ya vikundi vya Vijana wa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi hivi karibuni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga amewashauri vijana kuchangamkia fursa hiyo ambayo haimuhitaji mkopaji kuwa na dhamana isiyo hamishika bali kuwa na uaminifu wa kurejesha mkopo huo utakaotolewa kupitia vyama vya kuweka na kukopa SACCOS.
“Vijana wanatakiwa kuhamasishwa kuunda na kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na kuunda SACCOS za vijana ili waweze kupatiwa mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa ajili ya kuongeza mitaji na kupanua uzalishaji”. Anasema Bi. Nkinga.
Afisa Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bibi. Subira Mfanga anabainisha kuwa vijana nchini wanahitaji elimu ya ziada kubadilisha fikra zao kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia vijana kutambua kuwa fursa za ajira zinasababishwa na wao wenyewe kwa kuwa waaminifu, kuchukua mkopo unaotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kurudisha mkopo huo kwa wakati ili kuweza kutoa fursa kwa vijana wengine kufikiwa na mkopo huo.
Bibi Mfanga anaongezea kuwa zoezi lililofanywa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwafikia vijana wa Halmashauri ya Mwanga ni lulu kwa vijana wa Wilaya hiyo kwani limewasaidia vijana kujielewa hivyo kuacha kutumika vibaya katika makundi yanayoleta uhasama ndani ya jamii bali wajikite zaidi katika uwekezaji kwa kuanzisha miradi endelevu, yauhakika na inayotekelezeka. 
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Deogratius Yenza amesema kuwa viongozi wa Mkoa wa Dodoma wako bega kwa bega na Vijana wa Mkoa huo kwani vijana ndio sehemu kubwa ya nguvu kazi ya Taifa wanahitaji kujengewa ujuzi, kushauriwa, na kufanyiwa tathmini ya miradi wanayoombea mikopo ili iweze kuleta tija na hamasa kwa vijana wengine kuiga mfano wa vijana wa Dodoma.
Aidha Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo Vijana Bi. Venerose Mtenga amesema kuwa walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 watakaoruhusiwa kuomba mkopo na kurejesha mikopo hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ambapo muda wa maandalizi utakuwa wa miezi mitatu tu na riba yake itakua asilimia kumi (10%) kwa mwaka ambapo kikundi kitalazimika kulipa tozo ya asilimia 15 iwapo kitashindwa kurejesha mkopo katika muda uliopangwa.
Akifafanua jambo wakati wa semina ya kuhamasisha vijana wa Mkoa wa Mbeya Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima amewataka vijana kutambua yakua miradi itakayopewa mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana itaibuliwa na vikundi vya vijana wenyewe na andiko la miradi litawasilishwa kwa Afisa Maendeleo ya vijana wa Halmashauri husika ambapo ataitembelea miradi hiyo iliyowasilishwa kwake ili kuthibitisha uhai wake na uwezo wa miradi kurejesha mkopo na kuwasilisha miradi hiyo kwa Afisa wa Mkoa ambaye baada ya kuipitia ataituma Wizarani kwa hatua zaidi.
Hata hivyo, vijana waliopata nafasi kushiriki semina mbalimbali zilizotolewa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wameiomba Serikali kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanakuwa endelevu na yanawafikia vijana nchini kote ili kuwawezesha vijana kufahamu umuhimu wa Mfuko huo, upatikanaji wa fedha, pamoja na sifa za upatikanaji wa fedha kutoka mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Jitihada zote hizo zinalenga katika kufikia malengo na mikakati mbalimbali ya kukuza ajira kwa Vijana nchini kama zilivyoainishwa kwenye Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, Sera ya Ajira ya mwaka 2008, Mpango Kazi wa Taifa wa Ajira kwa Vijana wa mwaka 2007, MKUKUTA II na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025.
Tanzania kama sehemu ya dunia inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana walioko katika mazingira hatarishi pamoja na umuhimu wa kuhakikisha kuwa vijana wanahusishwa kikamilifu katika malengo ya maendeleo kama Taifa la kesho.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AAGA UMOJA WA AFRICA,ATUMIA KISWAHILI

WIZARA YA HABARI VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO YATOA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MUFTI SHAABAN ISSA BIN SIMBA

$
0
0

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo chaSheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.

Katika salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi  Oktoba mwaka huu. 

Waziri huyo ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole  , unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake.


“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo chaSheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja” amesema .


Amesema Waziri Mukangara: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu.


Aidha, kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema peponi roho ya marehemu … Amina.”


Imetolewa na;


Idara ya Habari(MAELEZO)


15 Juni,2015

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images