Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

TAZAMA MH. MEMBE ALIVOTIKISA JIJI LA MBEYA


ALI KIBA NA ABDU KIBA WALIVYOWARUSHA WASHINGTON DC..WAKISINDIKIZWA NA AJ UBAO

$
0
0
ALI KIBA NA MBWEMBWE ZAKE SASA
ALI KIBA NA ABDU KIBA WAKIWARUSHA









                                                     JE UNAWAJUA HAWA
    ABDU KIBA ....ALI KIBA..NA PROMOTA "DMK GLOBAL " KABLA YA SHOW KUANZA





                                                        WADAU NDANI YA VIP





                     SUNDAY SHOMAY AKIW BACK STAGE NA THE KIBA SQUARED





                                                                     MAMBO YA VIP
                                                                           MAMBO YA VIP


 

              MWANAMUZIKI AISHIYE WASHINGTON "AJ UBAO " ALIFUNGUA SHOW


                                         PROMOTA DMK NA MWANAMUZIKI AJ UBAO


                                                             PROMOTA J&P








WAANDAAJI "DMK GLOBAL


MZEE YUSUF KUTANGAZA NIA NDANI YA DAR LIVE KESHO

HABARI YA UTAFITI WA KUIWEZESHA ZNZ KUWA NA VYANZO VYA NISHATI WAFANYWA

$
0
0
Na Rahma Khamis – Maelezo Zanzibar.  
                 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na azma yake ya kukamilisha Mradi wa Utafiti wa Nishati mbadala ili kujuwa uwezekano wa Zanzibar kupata Umeme wake wa uhakika.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla  Shaaban katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  Chukwani  wakati akitoa Hutuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2015 /2016.

Amesema Wizara yake imekamilisha kazi ya kupatikana  kwa Mkandarasi  kutoka katika Kampuni ya (AGMIN ya Italy )kwa Ujenzi wa Minara ambapo kwa sasa ameanza kazi zake.

Aidha amefahamisha kuwa Mshauri Elekezaji wa ukusanyaji wa taarifa pamoja na kutaarisha Ripoti ya upembuzi  sahihi ( Feasibility Study) ameshapatikana ambapo kazi yao inatarajiwa kumalizika Mwaka ( 2017).

Itakumbukwa kuwa Zanzibar bado inategemea Nishati ya Umeme kutoka Tanzania Bara na kwamba kama Utafiti huo utatoa Matokeo mazuri kuna uwezekano wa Zanzibar kuwa na Vyanzio vyake vya Umeme badala ya kutegemea Bara.

Waziri Shabani amesema katika utekelezaji huo Wizara imeweza kushiriki katika mikutano mbalimbali iliyofanyika ndani na nje ya Nchi ikiwemo kuhudhuria katika mkutano wa kuitangaza Tanzania katika utekelezaji wa masuala ya Nishati (Den Hague-Uholanzi).

Akielezea kuhusu utekelezaji huo amesema  kuwa ni kushiriki katika Maonesho na Warsha ya Nishati Mbadala iliyo fanyika Kahama na Tanzania, na kushiriki Vikao vya Jumuia ya Afrika Mashariki katika masuala ya Nishati na Umeme (Nairobi Entebe) sambamba na mkutano mkuu wa Mafuta na Gesi wa Afrika Mashariki (EAPCE 2015) uliofanyika Kigali –Ruwanda.

Hata hivyo amesema katika kuhakikisha Nishati ya Mafuta inapatikana Nchini Wizara inaendelea kufuatilia shughuli za kusimamia upatikanaji wa Mafuta pamoja na utekelezwaji wa Ratiba za uagizaji wa Mafuta Nchini kwa Makampuni manne makubwa (GAPCO,UP,ZP na PUMA).

Aidha  amefahamisha kuwa katika kulisimamia suala hilo dosari za uagizwaji wa Mafuta ya Petrol zimejitokeza baina ya Mwezi wa Februari na Machi ambazo zilichangiwa na kuchelewa kwa Meli ya Mafuta ya pamoja (Bulk Consignment) inayoleta Mafuta Nchini Tanzania.

Sambamba  na hayo Waziri Shaaban amesema kutokana na hali iliyojitokeza ni kiashirio tosha cha kusisitiza umuhimu wa kuwepo kwa Taasisi maalum ya kushuhulikia Sekta Binafsi ya kuendesha Biashara hiyo kwa kutumia sheria.
Waziri Shaaban ameliomba Baraza la Wawakilishi limuidhinishie Jumla ya Shl. Bilion 35 na Milioni 949 kwa ajili ya Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati kwa mwaka wa Fedha 2015-16.  
                                                            
                               IMETOLEWA NA  HABARI MAELEZO –ZANZIBAR.

UNFPA-TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA TUME YA MIPANGO YAENDESHA WARSHA MKOA WA MARA

$
0
0
Mgeni Rasmi Bw. Ibrahim D. Kalengo, Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambae anamwakilisha Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa ajili ya warsha hiyo kufunguliwa rasmi.2
Mwezeshaji Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya vijana katika mipango ya maendeleo ya mkoa na wilaya.3
Washiriki wa warsha kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini mwezeshaji.4
Afisa kutoka UNFPA anaeshughulikia maswala ya vijana Bi. Tausi Hassan, akisisitiza jambo kwa washiriki wa warsha kuhusu program za vijana katika shirika la UNFPA.5
Washiriki wa warsha kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa warsha hiyo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wameandaa warsha kwa ajili ya kuhamasisha na kuwajengea uwezo watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Musoma warsha inafanyika katika ukumbi wa Afrilux Hotel tarehe 11 na 12 Juni 2015. Kituo hiki kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu.
Washiriki wa warsha ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.

KINANA AWASILI WILAYA YA KYERWA, ATAKA MIRADI YA MAENDELEO ISIMAMIWE NA HALMASHAURI SIYO SERIKALI.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitembelea shamba la ndizi na kahawa la  mkulima wa Kahawa na Ndizi Ndugu Eustace Kubalienda Kishunji katika kijiji cha Mabila,wilayani Kyerwa mkoani Kagera

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa Kahawa na Ndizi Ndugu Eustace Kubalienda Kishunji ambaye ni mmiliki wa shamba la Ndizi,, Amesema shamba hilo  lina  miche 345 ambayo huvuna magunia 25 na ana shamba la migomba ambalo humpatia mavuno ya  mikungu  kwa mwezi 45.

Mzee Kishunji ambaye anaishi katika kijiji cha Kikukuru kata ya Mabira ameweza kusomesha watoto wawili katika vyuo vikuu vya Dar es salaam na Dodoma na amejenga nyumba ya kisasa yenye thamani kubwa ya fedha kutokana na kilimo bora cha kisasa.


Katibu Mkuu Kinana yuko ziarani katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye

 Mkulima bora wa migomba na kahawa katika Kijiji cha Mabira, Mzee Eustus kishunju Ntibalienda (kulia) akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuhusu alivyoweza kufanikiwa katika kilimo cha mazao hayo, Katibu Mkuu alipomtembelea mkulima huyo,  akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo. 

 Sehemu ya soko la biashara la kisasa na la kimataifa linalojengwa Kigorogoro,mpakani mwa Tanzania na Uganda.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (pichani kati) akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh.John Mongella wakijadiliana jambo mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Kigorogoro, alipowasili katika kijiji hicho kukagua ujenzi wa soko la kisasa na la Kimataifa katika kijiji hicho leo.

Hhata hivyo Kinana ameonesha kusikitishwa baada ya kujulishwa kuwa ujenzi wa mradi huo, unaohitaji sh. bilioni 1.5 umesimama kutokana na serikali kuu kukosa fedha.

        Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, amesema ni vema miradi muhimu ya maendeleo iwekwe chini ya usimamizi wa halmashauri ya eneo linalohusika badala ya serikali kuu. 

       Amesema, utaratibu wa kuifanya miradi ya aina hiyo kuwa chini ya usimamizi wa serikali, umekuwa ukileta matokeo mabaya ikiwemo kusimama kwa ujenzi wa miradi.


       Kinana amesema hayo leo, baada ya kukagua ujenzi wa kitu kikubwa cha biashara, katika Kata ya... wilayani Kerwa mkoa ni Kagera ambacho ujenzi wake umesimama tangu mwaka juzi kwa maelezo ya kukosekana fedha.


      "Jamani jengo kama hili lilitakiwa lisimamiwe na Halmashauri ya eneo hili, lakini kusimamiwa na wizara ni kupoteza muda, hivi kweli ni rahisi mkaguzi atoke Dar es Salaam, kuja hadi huku kukagua ujenzi tu wa jengo hili, hasa ikizingatiwa kuwa miradi kama hii ni mingi?" alihoji Kinana.


 Wananchi wa Kijiji cha Kigorogoro katika Kata ya Murongo wilayani Kyerwa mkoani Kagera wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCm, Abdulrahman Kinana akipowasili kuwahutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Kibingo Wilayani kyerwa mkoani Kagera.
 Wananchi wa kijiji cha Isingiro wakimshangilia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,alipopanda jukwaani na kuwasalimia.
 Wananchi wa kijiji cha Isingiro wakimsikiliza Katibu Mku wa CCM,Ndgu Kinana alipokuwa akiwahutubia
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibingo, Kata ya Kaisho, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Wananchi wa Kijiji cha Isingiro wakishangilia jambo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa Wilaya mpya ya Kyerwa,Mh.Edward Ole Lenga,pichani katini Mkuu wa wilaya ya KaragweMh. Deodatus Kinawiro
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza jambo mara baada ya kupolewa katika wilaya mpya ya Kyerwa,katika kijiji cha Nkwenda,wilayani humo. 
 Kabla ya kuanza ziara yake katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alianza kazi kwa kuzungumza na wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCm ya wilaya hiyo.

  Katibu NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia Wananchi wa kijiji cha Nkwenda,wilayani Kyerwa mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nkwenda,Kinana alipita kijijini hapo kuwasalimia wananchi waliokuwa  na shauku kubwa ya kumuona Katibu Mkuu huyo.

Rais Kikwete awasili Arusha kuongoza maadhimisho ya Siku ya Albino

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Albino Tanzania Bwana Ernest Kimaya akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) muda mfupi baada ya kuwasili jana  jioni.Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa wa Albino itakayofanyika leo katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid. Kushoto ni Bwana Godson Mollel mwenyekiti wa Chama cha Albino Mkoa wa Arusha. Picha na Freddy Maro

Dkt Mwele: Kutoka binti mwenye ndoto kuwa mtafiti hadi mwanasayansi wa kimataifa hadi muwania Urais2015

$
0
0

Mapema wiki hii, mwanasanyansi wa kimataifa Mtanzania, mwanamama Dokta Mwelecele (Mwele) Malecela, alitangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania kwa kuomba ridhaa ya kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi CCM. Dokta Mwele ambaye hadi wakati anatangaza uamuzi huo ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), ana historia ya kipekee ambayo nilibahatika kuifahamu kupitia chapisho moja lililopo katika blogu hii. Hata hivyo, chapisho hilo ambalo lilisomwa na maelfu ya watu, lilikuwa katika lugha ya Kiingereza. Makala hii ni marudio ya chapisho hilo kwa lugha ya Kiswahili. Maelezo hayo yanatoka mdomoni mwa Dkt Mwele mwenyewe ila mie nimetafsiri tu kwa Kiswahili.
Ajira yangu katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ni hadithi ya bahati yenye matokeo mazuri ambayo awali haikuwa katika nia yangu. Nilijiunga na taasisi hiyo mwaka 1987 baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika stadi ya wanyama na tabia zao (BSc in Zoology) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1986. Baada ya usahili mzito, nilipangiwa kufanya kazi Kituo cha Amani (Amani Centre), hususan kushughulikia ugonjwa unaofahamika kama Bancroftian Filariasis. 

Nilishawahi kusikia kuhusu ugonjwa huo nilipokuwa mwanafunzi UDSM chini ya uangalizi mzuri wa Mhadhiri Dokta Parkin lakini sikujua nini nitafanya kuhusiana na ugonjwa huo. Kichwani mwangu, nilitamani kufanya kazi kuhusu ugonjwa wa malaria ambao kwa wakati huo nilidhani ulikuwa eneo la kuvutia kiutafiti. Kwahiyo, lazima Nikiri kwamba nilifadhaika kujikuta nashughulikia ugonjwa wa Bancroftian Filariasis badala ya malaria, ambayo ilikuwa na nyenzo nyingi kwa maana ya vifaa na ufadhili. Hata hivyo, niliambiwa bayana kuwa lazima nishughulikie kufufua shughuli ya ugonjwa huo wa Bancroftian Filariasis hapo Amani.



Nikiwa mtu ninayependa kukabiliana na changamoto, nikaanza safari ndefu ya kupita Milima ya Usambara, kuelekea sehemu hiyo  inayoitwa Amani.Safari ilikuwa katika mlolongo wa kupanda na kushika vilima kama mawimbi vile hadi wakati flani sikuona watu wala makazi. Hofu yangu ilipunguzwa na mandhari mazuri, misitu ya kupendeza, na hewa ilivyokuwa mwanana kadri tulivyopanda milima. 

Nilipofika Amani, hofu yangu ilinirudia tena, nikijiuliza iwapo ningemudu kweli kumudu maisha katika sehemu hiyo ambayo ilikuwa kama mafichoni kwa wakati huo. Nilijifariji mwenyewe kwa kujikumbusha kwamba sehemu hiyo tayari ilikuwa na wanasayansi kadhaa, na wamemudu kuishi hapo, Kwahiyo nami ningeweza pia. Baba yangu alikuwa na msemo maarufu, ‘Ni juu yako kumudu mazingira yanayokukabili,’ na hivyo ndivyo nilivyoamua kufanya.



Baada ya wiki kadhaa za mafunzo ya kuelewa mazingira, hatimaye nilipangiwa kufanyakazi katika maabara ya minyoo (helminthology laboratory) ambapo nilijifunza kuhusu parasaiti aitwaye Wuchereria Bancrofti, ambaye ndiye anayeeneza ugonjwa wa Bancroftian Filariasis. Nikajifunza kutambua hatua za awali za mzunguko wa maisha ya parasaiti huyo na mwingine aitwaye Onchocerca Volvulus. Nikajifunza kupasua mbu kwa ajili ya ucuhunguzi wa lava wa maambukizi na utambuzi wa mabara wa parasaiti mbalimbali, kama vile wa kichocho (schistosomes), minyoo ya tumboni (hookworks), trikurisi (Trichuris), nk. 

Wakati huo, dunia yangu ilikuwa dunia ya minyoo, na watu walioniinghiza katika dunia hiyo walikuwa miongoni mwa wajuzi wa mabara na wasaidizi wa mabara, ambao walinipatia mafunzo bora kabisa. Nathamini mafunzo hayo kwa sababu yamesaidia sana kunifanya kuwa mtu niliye sasa. Mmoja wa wasaidizi wa mabara alipendelea kunikumbusha kwamba alianza kazi mwaka niliozaliwa. Haikujalisha walivyonichukulia kama mtoto, nilichukua kila walichoniambia, na nilifurahia kila dakika. Kuna Nyakati familia yangu ilikuwa na wasiwasi kuhusu maendeleo yangu.Niliwapigia simu zile za zamani za mkonga kuwajulisha kuwa nilikuwa naendelea vema na kwa hakika ninapenda mahala hapo.




Kazi zangu za awali zilijumuisha kuchunguza uhusiano kati ya parasaiti wa eosinophilia na helminth. Pia nilichunguza matokeo ya majaribio ya maangamizi ya malaria katika maambukizi ya Bancroftian Filariasis. Pia nilifanya kazi na marehemu Profesa Chris Curtis kudhibiti mbu aina ya Culex katika mji wa Muheza kwa kutumia dawa za kuua wadudu za polystyrene beads.


Baadaye nilikwenda London, Uingereza kufanya Shahada ya Uzamili na ya Uzamifu katika Taasisi ya Magonjwa ya Kitropiki ya Chuo Kikuu cha London, ambapo nilifanyia kazi maambukizi ya filarial kwa paka. Paka hao walikuwa kwa ajili ya majaribio ya uchunguzi ambao ulikuwa muhimu kwa uelewa wa maambukizi ya filarial. Kazi niliyofanya ilikuwa kupata uelewa jinsi parasaiti wanavymudu kukwepa mfumo wa kinga ya mwili wa kiumbe aliyeambukizwa, na matokeo ya uchunguzi wangu yaligundua  kuwa kuna molekyuli za kiprotini (immunoglobulins) ambazo zilikuwa zikiwakinga parasaiti husika. Hii ilisaidia kuongoza uelewa kuhusu watu wenye maambukizi ya filarial lakini hawaonyeshi dalili za wazi.


Baada ya kurudi nyumbani, nilijihusisha na kuandaa utafiti wa kuelewa kitu ambacho kwa lugha ya kitaalam kinachoitwa immunoepidemiology ya maambukizi ya ugonjwa wa mabusha.Utafiti huo uliofanyika Kingwende, Kenya na Masaika, Tanzania. Machapisho kadhaa ya kitaaluma yalitokana na utafiti huo uliotuwezesha kufahamu zaidi kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa mabusha, ambao ungetuwezesha kutafuta mbinu bora za udhibiti.



Wakati huohuo, nilihusika na kuandaa mpango wa kimkakati kwa ajili ya mradi wa kutokomeza mabusha  nchini Tanzania. Hii ilifuatiwa na azimio la Shirika la Afya Duniani Mei 1997 ambalo lilisisitiza kuangamizwa kwa ugonjwa huo.Uaandaji wa mpango huo madhubuti ulifuatiwa na kuteuliwa kwangu kubwa mkurugenzi wa mradi unaohusu maradhi hayo mwaka 2000. Mwaka huohuo, mradi wa kupambana na ugonjwa wa mabusha ulianzishwa katika kisiwa cha Mafia, na mchango wangu kutoka maabara hadi kwenye eneo ambapo utafiti unatafsiriwa kwa vitendo ulitimia kamili. Kuna msemo wa Kiswahili kwamba safari moja huanzisha nyingine. Kwa upande wangu, hakujawa na mwisho wa safari hii bali ni vituo tofauti tu ninaposimama kidogo lakini naendelea mwelekeo huohuo.


Mradi huo wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha ulizidi kuimarika na sasa unafanya kazi katika wilaya 53 na umewafikia watu MILIONI 13. Huku msukumo sasa ukiwa kwenye magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika, njia zilizotumika katika mpango wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha zimepanuliwa na kujumuisha ugonjwa wa kichocho, minyoo wanaosambaa kupitia udongo na trakoma. Kwa kiasi kikubwa, usaili wangu katika makao makuu ya NIMR uliniandaa kwa ajira ya utafiti na udhibiti wa ugonjwa wa mabusha lakini kama ilivyo katika maeneo mengine ya maisha, sikujua hilo kwa wakati huo. Nilipata fahari kubwa pale Rais Jakaya Kikwete alipotangaza kuwa ataanzisha mfuko maalum kwa ajili ya ugonjwa huo kuwasaidia watu wanaosumbuliwa nao. Rais alitoa tangazo hilo katika Mkutano wa kimataifa wa masuala ya afya jijini Arusha, na hii imesaidia kupanua uelewa wa madhila yanayowakabili wahanga wa ugonjwa huo nchini Tanzania na kwingineko barani Afrika. Matokeo kutoka kituo cha uangalizi Tandahimba yanaonyesha  mradi wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha umefanikiwa kupunguza maambukizi katika wilaya hiyo, na hiyo itakuwa sehemu ya kwanza ya mafanikio ya kuingilia kati maambukizi kwa upande wa Tanzania Bara.

[IMG_7940.jpg]
 Je hii habari inayoelezea mafanikio? Ni habari kuhusu binti mdogo aliyekuwa na ndoto za kuwa mtafiti; kuhusu msichana aliyepanda vilima vya Amani kusaka ndoto yake, na ya mwanamke ambaye sasa anaishi katika ndoto hiyo kwa kufanya tafiti na kuchangia katika kukabiliana na ugonjwa ambao amekuwa akijishughulisha nao kwa takriban maisha yake yote. Labda hayo ndio mafanikio. Au waonaje?


Nina deni kubwa kwa watu wengi walioniwezesha kufanikisha safari hii, hususan baba yangu Dokta John Malecela na marehemu Mrs Ezerina Malecela ambao walinihakikikisha kuwa "ndiyo, waweza kutimiza ndoto yako."

Hapa chini ni machapisho mbalimbali ya kitaaluma 


Malecela M.N. Baldwin C.I and Denham D.A (1994) Hosts antigen on the surface of microfilariae of Wuchereria bancrofti and Brugia pahangi.

Transactions

Awarded prize for best presentation


Baldwin C.I., Medieros F, Malecela M.N. and Denham D.A (1994) Humoral responses in cats repeatedly infected with Brugia pahangi. Parasite 1,1S


Malecela (1995): Microfilariae and the immune response in cats repeatedly infected with Brugia pahangi. Ph.D. thesis, University of London.


P.E.Simonsen, D.W Meyrowitsch, W.G.Jaoko,M.N.Malecela, D.Mukoko, E.M.Pedersen, J.H. Ouma, R.T.Rwegoshora, N.Masese, P.Magnussen, B.B.A Estambale and E.Michael (2001) Bancroftian Filariasis infection,Diseaese and Specific Antibody Response Patterns in a high and a low endemicity community in East Africa. Parasite Immunology 23: 373-388


Michael E., Simonsen P.E., Malecela M., Mukoko D., Pedersen E.M., Rwegoshora R.T., Meyrowitsch D.W, Jaoko W.G., (2001)Transmission intensity and immunoepidemiology of bancroftian filariasis in East Africa. Parasite Immunology No 23. Pp 373-388


Paul Simonsen,Peter Bernhard, Walter Jaoko, Dan Meyerowitsch, Mwele N.Malecela-Lazaro, Pascal Magnussen and Edwin Michael (2002) Filaria Dance sign and subclinical hydrocele in two East African communities with Bancroftian filariasis. Transactions of the Royal Society of Tropical Medicine and Hygiene


Simonsen,P.E, Meyerowitsch, D.W, Jaoko W.G., Malecela, M.N., Mukoko, D., Pedersen, E.M., Ouma,J.H., Rwegoshora, R.T., Masese.N Magnussen, P., Estambale, B.B.A & Michael E. (2002) Bancroftian filariasis infection disease and specific antibody responses patterns in a high and low endemicity community in East Africa. American Journal of Tropical Medicine and Hygiene Vol 66(5) pp550-559


Simonsen P.E Meyrowitsch D.W., Mukoko D, Pedersen E.M., Malecela-Lazaro M.N., Rwegoshora R.T., Ouma J.H., Masese, N. , Jaoko W.G., Michael E., (2004) The effect of repeated half-yearly mass treatment on Wuchereria bancrofti infection and transmission in two East African communities with different levels of endemicity. American Journal of Tropical Medicine and Hygiene No 70 pp. 63-71






LOWASSA ATUA KIGOMA LEO

$
0
0
Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Noverty Kibaji akizungumza wakati akimuelezea Mh. Lowassa, idadi ya wanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Noverty Kibaji (kushoto) akimkabidhi, Mh. Edward Lowassa, majina ya wanaCCM wa Kigoma Mjini waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Mh. Lowasaa akionyesha majina ya WanaCCM wa Mkoa wa Kigoma waliomdhani ili aweze kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC), Daniel Nsanzugwanko (kulia) amkabidhi Mtangaza nia, Majina ya wanaCCM wengine waliomdhani.
Wananchi wa Mji wa Kigoma wakiwa wamejipanga kando ya Barabara kuu ya Kutoka Ujiji, kumpokea Mtangaza nia ya Kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mtangaza nia ya Kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkoani wana CCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kumlaki kwenye Ofisi Kuu za CCM mkoani hapo.
Mh. Lowassa akisani kitabu cha wageni kwenye Ofisi Kuu za CCM Mkoani Kigoma leo, Kulia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC), Daniel Nsanzugwanko.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dkt. Aman Kaborou, muda mfupi kabla ya kupokea idadi ya majina ya wanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amedhaminiwa na wanaCCM 11,250 Mkoani Kigoma, leo Juni 13, 2015.
Wazee kwa vijana wakimshangilia Mh. Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinganga, Hamis Mngeja akizungumza machache mbele ya hadhara ya wanaCCM wa Mkoa wa Kigoma.

Umati wa WanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma, ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma, kuja kumuona Mh. Edward Lowassa (anaeonekana kule mbele) wakati alipofika kuomba udhamini wa wanachama wa CCM, ili aweze kupata ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhaminiwa na wanaCCM 11,250 wa Mkoa wa Kigoma, leo Juni 13, 2015.

Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM wa Mkoa wa Kigoma.

WASIFU WA BERNARD KAMILIUS MEMBE

$
0
0
Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe. 

Kwa kabila, Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.

Elimu:
1962 – 1968: Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.
1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi
1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora
1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais
1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika maswala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor Political Science and International Relations)
1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika katika ofisi ya rais
1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa (Masters- Economics, International Relations and International Law)
1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi za mambo ya ulinzi na usalama
Mafunzo:
Kati ya mwaka 1975 na 1976 Ndugu Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ambapo vijana wote waliohitumu kidato cha Sita walitakiwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya Jeshi, Ndugu Membe aliajiriwa katika Ofisi ya Rais, Utawala bora.
Mwaka 1978, Ndugu Membe alipata Mafunzo ya sheria za Jinai na usalama wa nchi, nchini Uingereza. Aidha, mwaka 1980, Ndugu Membe alipata mafunzo ya siasa, katika Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Kivukoni, Dar es Salaam.
Familia:
Mwaka 1986, Ndugu Bernard Membe alifunga ndoa Takatifu na Dorcas Richard Masanche, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam. Ndugu Membe na mama Dorcas wamejaliwa kupata watoto watatu, Cecilia, Richard na Denis.
Siasa:
Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.

Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.

Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyakuwa anashikilia wadhifa huo - Dr Asha Rose Migiro - kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo. Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.

Mafanikio:
Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.

Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. 

Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.

Uchumi: Bernard Membe amesimamia vema utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya uchumi ili kuwezesha Tanzania kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuininua hali za wananchi wake. Ni katika kipindi chake, nchi imeshuhudia uwekezaji mkubwa katika eneo la viwanda, gesi, makaa ya mawe, kilimo na utalii. Chini ya uongozi wa Ndugu Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilipata tuzo ya utendaji bora iliyotolewa na sekta binafsi kwa kutambua mchango mkubwa wa Wizara katika kukuza sekta binafsi Tanzania.

Kudumisha mahusiano kimataifa: Katika kipindi chake, Tanzania imefanikiwa kuipaisha Diplomasia yake katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kutembelewa na viongozi mbalimbali mashuhuri kama, Marais George W. Bush na Baraka Obama wote wa Marekani, Xi Jinping wa Uchina, Joachim Gauck wa Ujerumani, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Piere Nkuruzinza wa Burundi, Joseph Kabila wa DRC, Philipe Nyusi wa Msumbiji, Mwana wa Mfalme wa Malkia wa Uiengereza, na Mwana wa Mfalme wa Japan.

Pia chini ya uongozi Ndugu Bernard Membe Tanzania imefanikiwa kupanua wigo wa mahusiano yake Kaimataifa kwa kufunguwa Balozi mpya katika nchi za Malaysia, Brazil, Comoro, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait. Aidha, Wizara imefanikiwa kufungua upya Ubalozi wa Tanzania the Hague, Uholanzi uliofungwa mwaka 1994. Kadhalika Balozi Mpya za Brazil, Oman, Uturuki, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Namibia zilifunguliwa hapa nchini.

Kutambuliwa:
Kwa kutambua mchango wake katika kurejesha hali ya amani na utulivu katika Visiwa vya Comoro, mwaka 2008, Bernard Membe alikuwa miongoni mwa watanzania waliotunukiwa Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro na rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Uozefu:
2006 – hadi sasa: Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2008 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Africa, Addis Ababa, Ethiopia.
Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kutoka muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini, SADC
2006 – 2011: Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM
2006 – 2011: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.
2006 – hadi sasa: Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa
2013 – hadi sasa: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Madola Commonwealth
2014 – hadi sasa: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amekuw mjumbe wa kamati za usuluhishi katika migogoro kwenye nchi za Sudan ya Kusini, Madagascan na katika mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.
Pia Tanzania imefanikiwa kushiriki katika zoezi la Uangalizi wa chaguzi kwa niaba ya SADCC katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagasca, Kenya, Comoro na Afrika ya Kusini.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA MJI WA AVIC, ‘AVIC TOWN’ ULIOPO KIGAMBONI DAR ES SALAAM .

$
0
0
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mki wa Avic, ‘Avic Town’, uliofanyika leo Juni 13, 2015 Kigamboni jijini Dar es Salaam.Picha zote na OMR.2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lyu Youqing (kulia), Makamu wa Rais wa ‘Avc International’, Dkt. Cheng Baozhong (kushoto) kwa pamoja wakikata utepe kuzindua ramsi Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Avoc ‘Avic Town’, uliozinduliwa leo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lyu Youqing (kulia), kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la Msingi la uzinduzi ramsi wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Avoc ‘Avic Town’, uliozinduliwa leo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lyu Youqing (kulia), Makamu wa Rais wa ‘Avc International’, Dkt. Cheng Baozhong (wa pili kushoto) kwa pamoja wakifurahia baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Avoc ‘Avic Town’, uliozinduliwa leo Kigamboni jijini Dar es Salaam
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kuzindua ramsi Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Avic ‘Avic Town’ uliofanyika leo Juni 13, 2015, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia mandhali ya jiko katika moja kati ya nyumba zilizojengwa katika eneo hilo, wakati alipokuwa akitembelea nyumba hizo baada ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Avic ‘Avic Town’ Kigamboni.
11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mradi huo kukagua mara baada ya kuuzindua leo Kigamboni.
12
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika  picha ya pamoja na baadhi ya viongozi baada ya uzinduzi huo.

TUME YA HAKI ZA BINADAMU, UNESCO WATAKA JAMII KUTAMBUA WATU WENYE ALBINISM

$
0
0
XXKamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dkt. Kevin Lothal Mandopi akielezea namna ya tume hiyo ilivyo mstari wa mbele kuelimisha Umma dhidi ya vitendo na ukatili kwa watu wenye Ualbinism nchini kwa wadau na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam mapema leo Juni 13.2015.

Na Andrew Chale, modewjiblog
Tume ya Haki za binadamu na Utawala bora nchini, leo Juni 13,2015, imeungana na watanzania wote kuadhimisha siku ya Kimataifa ya uelimishaji umma kuhusu Ualbino na haki za watu wenye Ualbino ambapo imeitaka jamii kutambua haki na wajibu wa kuwalinda na kuwathamini.

Akisoma taarifa maalum kwa wadau mblimbali na waandishi wa habari waliojitokeza jijini Dar Es Salaam, Kamishna wa tume hiyo, Dkt. Kevin Lothal Mandopi alieleza kuwa jamii inayo wajibu wa kuwathamini watu hao wenye albinism kwani nao ni kama binadamu wengine na wana haki sawa.

Kamishna Mandopi katika taarifa hiyo alibainisha kuwa, mpango wa elimu kwa umma umelenga kubadilisha fikra, mtazamo na imani potofu juu ya watu wenye ualibinism. “Ni dhahiri kuwa iwapo jamii itaelewa dhana nzima ya Ualbinism na kubadili fikra na dhana potofu dhidi ya watu hawa, kuna uwezekani mkubwa wa kukomesha kabisa matendo maouvu dhidi ya ndugu zetu wenye Ualbinism” alieleza Kimishna Mandopi.
UNS
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwa msisitizo juu ya jamii ya watanzania kuchukua hatua ya kuwalinda watu wenye Ualbinism nchini wakati wa tukio maalum la maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma kuhusu Ualbino, iliyoandaliwa na tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini. 

kushoto kwake ni Wakili wa Serikali na Mratibu wa masuala ya Albinism nchini, Bi Beatrice Mpangala. Kwa upande wake Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Zulmira Rodrigues alisisitiza jamii nchini kuongeza upendo pamoja na kuachana na imani potofu inayosababisha kukithiri kwa vitendo hivyo hapa nchini.


Pia alibainisha kuwa, imefika wakati sasa wa kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ilikutambua wenye Ualbinism ilinao waishi na kupata haki sawa kama binadamu wengine.

“Wajibu wetu ni kuwathamini na kuwalinda watu wenye Ualbinism, tumetembea maeneo mbalimbbali ikiwemo Kanda ya Ziwa katika vituo maalum vya watoto wenye Albinism, Ni wakati wa kuendelea kutoa elimu ili watoto hao watoke huko ili waishi na jamii kama wengine” alisisitiza Bi. Zulmira.
UNESCO2
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwa msisitizo juu ya jamii ya watanzania kuchukua hatua ya kuwalinda watu wenye Ualbinism nchini wakati wa tukio maalum la maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma kuhusu Ualbino. kulia ni maafis wa taasisi hiyo ya UNESCO na kushoto kwake ni Wakili wa Serikali na Mratibu wa masuala ya Albinism nchini, Bi Beatrice Mpangala.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi Marry Massay alizitaka mamlaka husika ikiwemo za Serikali na watu binafs, vyombo vya habari na jamii kwa pamoja kutoa elimu ya uelimishaji umma kuhusiana Ualbinism ilikuendelea kuwa Tanzania yenye amani na upendo kama ilivyojizolea sifa ndani na nje ya mipaka yake.
E
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi Marry Massay akisisitiza umma kuchukua hatua dhidi ya mapambano kwa watu wenye Ualbinism kwa kuwalinda pamoja na kutoa elimu sahihi ya mapambano ikiwemo kuachana na imani potofu dhidi ya jamii hiyo.
Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Bi. Neema Ringo, alibainisha kuwa, ofisi yake imekuwa mstari wa mbele kufuatilia kesi mbalimbali ikiwemo dhidi ya jamii ya wenye Albinism huku akiwataka wananchi kujitokeza kutoa ushahidi pamoja na kufuatilia kesi hizo mara kwa mara.
Kwa upande wa wadau wengine walitaka Serikali kuwa mstari wa mbele kushikamana na jamii hiyo yenye ualbinism ilikutokomeza kabisa imani potofu iliyojijengeka kwa watu ikiwemo kutoa elimu kwa ngazi zote mara kwa mara.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ndiye mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kimataifa ya kuongeza ufahamu juu ya Ualbino ambayo yameandaliwa na Chama Cha Albino Tanzania, jijini Arusha.
tumeeee
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Bi. Neema Ringo,akitoa wito kwa wadau mbalimbali (Hawapo pichani) Kujitokeza katika kesi kutoa ushahidi hasa wakati wa kesi dhidi ya vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye Albino nchini.ambapo alieleza kuwa wamekuwa na changamoto dhidi ya mashahidi hivyo ni wakati sasa wa wananchi kujitokeza kufuatilia kesi hizo ikiwemo mashahidi kujitokeza.
MCHANGIA
Mmoja wa wadau waliojitokeza kwenye maadhimisho yaliyoandaliwa na tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, akichangia maoni yake dhidi ya hatua za kufanyika ili elimu ifike kwa jamii ikiwemo kuwatumia watu mbalimbali hasa ngazi za chini wakiwemo Wenyeviti, madiwani na wakuu wa Wilaya na Mikoa.
WW
Mmoja wa mdau wa masuala ya haki za binadamu, ambaye ni mlemavu, akichangia mada kwenye kwenye maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
P
Taswira katika mkutano huo wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ukiendelea ukumbini hapo...!

JANUARY MAKAMBA ATEMA CHECHE RUVUMA, AONGOZA KWA KUPATA WADHAMINI

RAIS KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA WATU WENYE ALBISM DUNIANI

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na baadhi ya watoto wenye albinism mara baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa Sheikh amri Abeid mjini Arusha leo ambapo aliongoza maadhimisho ya siku ya watu wenye Albinism Duniani.
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na baadhi ya watoto wenye albism katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya watu wenye albinism Duniani. picha na Freddy Maro.

INTRODUCING VIDEO | SAMATA A - WANABOA


KINANA AITAKA SERIKALI KURAHISISHA UTOAJI WA LESENI KWA WAFANYABIASHARA,MADEREVA WA MAGARI NA BODABODA

$
0
0
 Wananchi wa Ngara mjini wakishangilia jambo katika mkutano wa hadhara wa CCM
 KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa mji wa Ngara Mjini kwenye mkutano wa hadara,Nape Nnauye alisema kuwa hakuna sababu ya Watanzania kuingia kwenye mpasuko kwa sababu ya mchakato wa katiba mpya na kuashauri ni vema mjadala ukafungwa kwenye nyumba za ibada. Amesema inasikitisha unapoona baadhi ya viongozi wa dini badala ya kuhubiri neno la Mungu na kuwaunganisha Watanzania wanatumia nafasi yao kuwagawa wananchi kwa sabababu ya Katiba mpya.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrhaman Kinana akiwahutubia wananchi wa Ngara mjini,Kinana ameitaka Serikali kurahisisha utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara , madereva wa magari na bodaboda badala ya kuacha watu wanasumbuka kutafuta leseni umbali mrefu tena kwa gharama kubwa.



Kinana amesema kuwa  moja ya ombi la wananchi hao ilikuwa ni kuomba kurahisishiwa kupata leseni ili kuondoa usumbufu wanaoupata sasa.

Alisema Serikali lazima iweke mazingira mazuri ya kutoa leseni kwa wananchi wakiwamo wafanyabishara na madereva bodaboda huku akieleza hakuna sababu ya kutumia gharama kubwa kwa ajili ya leseni.
 
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Chanjo ya  watoto kuzuia maambukizi ya magonjwa katika kata ya Nyakisasa kijiji cha Kashinga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ngara mkoani Kagera,lengo la ziara hiyo likiwani ni kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na ktibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa CCM  kutoka mkoa wa Kagera.
 Baadhi ya akina mama na watoto wao wakisubiri watoto wao kupatiwa chanjo katika zahanati ya kijiji cha Kashinga wilayani Ngara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi hawapo pichani wakati alipozindua chanjo ya watoto katika zahanati ya Kashinga akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Ngara leo wa tatu kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM na katikati ni  Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongella
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika zahanati hiyo. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wa CCM wilayani Ngara wakishiriki kwa pamoja katika ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Munjebwe, Rulenge.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Rulenge.
 Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CHADEMa wakikabidhi kadi zao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana,na kutangaza kujiunga na chama chama CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi mbalimbali za waliokuwa wanachama wa Chama cha CHADEMA mara baada ya kurejesha kwake na kujiunga na CCM katika mji wa Rulenge.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ngara Mama Constansia Buhie wakizikusanya kadi  mbalimbali za wafuasi wa upinzani na kuzikabidhi kwa viongozi hao wa CCM,ikiwa ni ishara ya kujiunga na chama hicho cha CCM
 Baadhi ya kadi zilizorejeshwa kwa Kinana na wananchi hao na kujiunga na CCM.
 Kwaya ya akina mama wa Rulenge wakiimba wimbo maalum wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza  Mzee Godwin Magambo wakati alipowasilisha malalamiko yake ya ardhi 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mhandisi wa kampuni ya kichina ya TKPE Bw.Ton Minyang wakati alipokagua ujenzi wa  Mtambo wa umeme  vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya Kabanga wilayani Ngara. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua kkikundi cha akina mama wajasiriamali cha mjini Ngara kabla ya kuhutubia mkutano wake na wananchi mjini humo leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata keki kuashiria uzinduzi wa kikundi hicho cha akina mama wajasiriamali.

WAZIRI BERNARD MEMBE ATEMBELEA KABURI LA HAYATI ABEID AMAN KARUME MJINI ZANZIBAR

$
0
0
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati alipotembelea chumba ambacho muasisi wa Mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume aliuawa kwa risasi wakati akicheza bao, katika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja Juni 13.2015 jioni, ambapo Waziri Membe yupo Zanzibar kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
Picha zote na John Badi
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mkonge (kulia), wakati alipotembelea chumba ambacho muasisi wa Mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume aliuawa kwa risasi wakati akicheza bao, katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja Juni 13.2015 jioni, ambapo Waziri Membe yupo Zanzibar kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa tatu kushoto) akishiriki katika dua ya kumuombea muasisi wa mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume, wakati alipotembelea kaburi lake lililopo katika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja Juni 13.2015 jioni, ambapo Waziri Membe yupo Zanzibar kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati mbele) akifurahia jambo na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waasisi wa mapinduzi ya Zanzibar, baada ya kutembelea kaburi la muasisi wa mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume lililopo katika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja Juni 13.2015 jioni, ambapo Waziri Membe yupo Zanzibar kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.

RAIS KIKWETE AWASILI AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA 25 WA UMOJA WA AFRIKA

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa mara walipowasili katika hoteli ya Sun Internatioal Maslow Hotel, Sandton, Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa Mkutano wa 25 wa kawaida wa Umoja wa Afrika.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa na Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba   mara walipowasili katika hoteli ya Sun Internatioal Maslow Hotel, Sandton, Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 25 wa kawaida wa Umoja wa Afrika.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa wa Ubalozi  wa Tanzania  nchini Afrika Kusini mara walipowasili katika hoteli ya Sun Internatioal Maslow Hotel, Sandton, Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 25 wa kawaida wa Umoja wa Afrika.

PICHA NA IKULU.

biashara matangazo...Design Mpya ya Tshirts za Kitaa wear zapatikana sasa

$
0
0
Design Mpya ya Tshirts Bei 25,000/= per peace 
Designer ; Mike Mwakatundu 
Shop ; Kitaa Wear 
Kwa Mawasiliano Email; mwakatundu.m@gmail.com 
+255 754 310 202 +255 713 292 212 
 NB Unaletewa mpaka Nyumbani/Ofisini 
 Kama upo interested na bidhaa nyingine zaidi hizo hapo chini tembelea blog yetu www.dukaletu.blogspot.com 
 Ili kuwajua watengenezaji waagizaji wa bidhaa mbalimbali, mahoteli, usafiri , address sahihi za watu mbalimbali maarufu hapa nchini tembelea blog yetu www.tanzaniasocialmedia.blogspot.com





NSSF YAWANUFAISHA YATIMA NA WAHUDUMU WA WAGONJWA MAHOSPITALINI

$
0
0
Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha, Darul-Arqam, Ustaadh Hemed Jaffar. Hafla hiyo ilifanyika Tandika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Mkaguzi wa NSSF mkoa wa Temeke, Ummy Kimario na kushoto ni Ofisa wa Huduma kwa Wateja, Carolyne Newa. 

Ofisa Mkaguzi wa NSSF mkoa wa Temeke, Ummy Kimario (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa madaftari kwa mtoto, Ally Abdallah.
Ofisa Mkaguzi wa NSSF mkoa wa Temeke, Ummy Kimario (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa madaftari kwa mtoto, Ally Abdallah.
Viongozi wa NSSF mkoa wa Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Darul-Arqam cha Tandika jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Jumiiyatul Akhlaaqul Islaam (J.A.I), ya jijini Dar es Salaam akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya kusaidia taasisi hiyo ambayo inatoa huduma za kijamii pamoja na kuwahudumia wagonjwa bila kujali imani wala jinsia. 

Baadhi ya vyakula vilivyotolewa na NSSF kwa kituo hicho.
 Baadhi ya maofisa wa NSSF mkoawa Temeke.
Maofisa wa NSSF mkoa wa Temeke wakiwa katika ofisi za JAI muda mfupikabla ya kutoa msaada wa vifaa tiba.


Mhasibu Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdulkarim Kisuguru akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi misaada ya vifaa tiba katika Taasisi ya Jumiiyatul Akhlaaqul Islaam ya jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mafao ya Matibabu NSSF, Dokta Zakia Mohamed akifafanua jambo kuhusu vifaa tiba walivyokabidhi katika taasisi hiyo.
Sehemu ya msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na NSSFkwa taasisi ya JAI.
Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mwenyekiti Kamati ya Utendaji ya Taasisi ya Jumiiyatul Akhlaaqul Islaam, Ahmed Hassan Bakar (wa pili kushoto) na Naibu Mwenyekiti, Aman Soud Aman.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Jumiiyatul Akhlaaqul Islaam ya jijini Dar es Salaam akiagana kwa furaha na Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (kulia) baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Picha ya pamoja.
 Picha ya pamoja.

Mhasibu Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdulkarim Kisuguru akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi misaada ya vyakula pamoja na vifaa vya shule katika Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu cha, Darul-Arqam cha Tandika jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika Mazingira cha Darul-Arqam cha Tandika jijini Dar es salaam akizungumza wakati hafla ya kupokea misaada kutoka NSSF.
 Baadhi ya watoto wanaolelea katika kituo cha Darul-Arqam cha Tandika jijini Dar es salaam wakiwa katika haflaya kupokea msaada wa vyakula na vifaa vya shule vilivyotolewa na NSSF. 
 Maofisa wa NSSF wakiwa katikahafla hiyo.
 Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (wa pili kulia) akiwa na baadhiya maofisa wa NSSF mkoa wa Temeke walipofikakutoa msaada katika kituo cha Darul-Arqam.
 Maofisa wa NSSF mkoa wa Temeke.
  Maofisa wa NSSF mkoa wa Temeke wakiwa katika hafla hiyo.
Kijana aliyewahi kuishi na kusoma katika katika Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika Mazingira cha Darul-Arqam, Idd Abasi  akitoa ushuhuda wake kwa viongozi wa NSSF mkoa wa Temeke. Kijana Idd kwa sasa anasoma Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam akichukua masomo ya BSC, LMV.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images