Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 552 | 553 | (Page 554) | 555 | 556 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akifungua Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma leo mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel.
   Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma wakiwa katika mkutano huo ulifanyika leo mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza wakati akifungua  Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma leo mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel. Kulia kwake ni baadhi ya waandishi wa habari wakifutilia hotuba yake kwa umakini.
   Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mathias B. Kabunduguru akizungumza katika Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma leo mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel.
  Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) kufungua Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma leo mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel.

  0 0

  Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church Eliud Isanja (wapili kushoto) akiwa katika mahafali ya chuo cha Bibilia kinachomilikiwa na kanisa hilo.watatu kushoto ni Mgeni Rasmi Kwa upande wake Askofu Mwangalizi wa  Kanisa hilo Israel Maasa

  Na woinde shizza ,Arusha
  Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church Eliud Isanja  amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba na kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo  ya taifa.

  Isanja aliwaasa Watanzania kutozembea nafasi hiyo muhimu na badala yake waitumie fursa hiyo  itakayoleta  mabadiliko yanayotarajiwa na wengi.

  Akizungumza katika mahafali ya Wahitimu wa Diploma ya masomo ya Biblia amesema kuwa Tanzania inahitaji Viongozi waadilifu na wenye bidii.
  “Watu wasipige tu kelele barabarani bali wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi bora watakaoliongoza taifa hili” Alisema Isanja

  Kwa upande wake Askofu Mwangalizi wa  Kanisa hilo Israel Maasa ambaye alikua mgeni wa heshima katika mahafali hayo amewataka watanzania kuwa makini na wagombea wanaowagawa Watu kwa misingi ya ukabila na udini na kutowachagua  kwani wataathiri umoja na mshikamano wa kitaifa.

  Wilfred Pallangyo ameeleza kuwa ni wakati wa Watanzania kuwatambua viongozi watakaofaa kuliongoza taifa na kuwapa nafasi hiyo pasipokufanya makosa pia kuepuka vitendo vya rushwa hasa tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.

  Alisema kuwa  Tayari zoezi la uandikishaji limeanza katika baadhi ya mikoa na linategemewa kukamilika nchini kote  ili kukamilisha uchaguzi utakaoanza Octoba mwaka huu,vuguvugu la uchaguzi tayari limeanza tumeshuhudia hekaheka za wagombea wa Urais.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Ndg Halima Maulid Salum, akimkabidhi seti ya Komputer  Ndg Faiza Abass kwa ajili ya Kitengo Shirikishi Pemba, kwa ajili ya kuwekea kumbukumbu ya wagonjwa wanaoripotiwa kupitia Kitengo hicho, Vifaa hivyo vimetolewa na Taasisi ya Tanzania Helth Promotion Support , makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya hoteli ya Maszosns  shangani Zanzibar anayeshuhudia katikati Mkurugenzi Mtendaji wa THPS Dr. Redempta Mbatia

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid Salum, akimkabidhi Seti ya Komputer Daktari wa Kituo cha Afya Mnazi Mmmoja Ndg John Maida, kwa ajili ya kutunzia Kumbukumbu katika Kituo chao, msaada huo wa Kumputer umetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya THPS,Komputer hizo zimekabidhiwa kwa Vituo vinane Unguja na Pemba makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya hoteli ya Mazsons Shandani Zanzibar.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid Salum, akimkabidhi Seti ya Komputer Daktari wa Kituo cha Afya Pemba Ndg, Badran Sultani Issa, kwa ajili ya kutunzia Kumbukumbu katika Kituo chao, msaada huo wa Kumputer umetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya THPS,Komputer hizo zimekabidhiwa kwa Vituo vinane Unguja na Pemba makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya hoteli ya Mazsons Shandani Zanzibar.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid Salum, akimkabidhi Seti ya Komputer Daktari wa Kituo cha Afya Unguja, Ndg Ahmed Hani Mohammed, kwa ajili ya kutunzia Kumbukumbu katika Kituo chao Shirikishi , msaada huo wa Kumputer umetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya THPS,Komputer hizo zimekabidhiwa kwa Vituo vinane Unguja na Pemba makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya hoteli ya Mazsons Shandani Zanzibar.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid Salum, akimkabidhi Seti ya Komputer Daktari wa Kituo cha Afya Chakechake Pemba Bi Mgeni Seif, kwa ajili ya kutunzia Kumbukumbu katika Kituo chao, msaada huo wa Kumputer umetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya THPS,Komputer hizo zimekabidhiwa kwa Vituo vinane Unguja na Pemba makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya hoteli ya Mazsons Shandani Zanzibar.
  Mkurugenzi  Mtendaji wa THPS, Dr.Redempta Mbatia, akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa maelezo ya THPS, jinsi nanavyofanya kazi zake. 
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Ndg Halima Maulid Salum, akifungua mkutano wa siku moja kwa Madaktari wa Vitengo vya Shirikishi vya Ukimwi, Ukoma na Kifua Kikuu, kutunza data katika Vituo vyao iliowajumuisha Madaktari kutoka  Vituo 8 vya Unguja na Pemba , ulioandaliwa na Taasisi ya Tanzania Helth Promotion Surppot , yaliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar, kulia Mkurugenzi  Mtendaji wa THPS, Dr.Redempta Mbatia
  Washiriki wa warsha ya siku moja kutathimi mafanikio ya Utunzaji wa Data katika Vituo vya Afya Shirikishi vya Unguja na Pemba, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Bi Halima Maulid Salum akifungua warsha hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.
  Ofisa wa THPS Zanzibar akifuatilia warsha hiyo ya Madaktari wa Vituo vya Afya Kitengo Shirikishi wakati wa  mkutano huo wa siku moja kutathimini mafanikio ya Utunzaji, uliofanyika hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar.
  Washiriki wa warsha ya siku moja kutathimi mafanikio ya Utunzaji wa Data katika Vituo vya Afya Shirikishi vya Unguja na Pemba, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Bi Halima Maulid Salum akifungua warsha hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.
  Mkurugenzi  Mtendaji wa THPS, Dr.Redempta Mbatia, akizungumza kabla ya kukabidhi seti za kumputer kwa vituo vya afya vinane vya Unguja na Pemba kwa ajili ya kutunzia kumbukumbu katika vituo vyao.
  DR Mdahoma akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa Msaada wa Komputer kwa Ajili ya kuwekea Kumbukumbu katika Vituo vya Afya vya Unguja na Pemba, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya hoteli ya mazsons shangani Zanzibar.
  Naibu Katibu Mku Wazara ya Afya Zanzibar Halima Maulid Salum akitowa shukrani kwa msaada huo wa Seti za Kumputer uliotolewa na THPS kwa ajili ya Vituo vya Afya Vinane vya Unguja na Pemba ili kuweza kutunza kumbukumbu zao za kila siku.
  Madaktari wa Vitengo Shirikishi katika Vituo vya Afya Unguja na Pemba wakishuhudia ukabidhiwaji wa misaada ya Styei za Komputer kwa Vituo hivyo kwa ajili ya kutunzia kumbukumbu katika vituo vyao wakiwa katika bustani ya hoteli ya Mzsons shangani Zanzibar wakati wa makabidhiano kabla ya kuaza kwa mkutano wa kutathimini uwekaji wa kumbukumbu. uliofanyika katika hoteli hiyo
  Madaktari wa Vitengo Shirikishi katika Vituo vya Afya Unguja na Pemba wakishuhudia ukabidhiwaji wa misaada ya Styei za Komputer kwa Vituo hivyo kwa ajili ya kutunzia kumbukumbu katika vituo vyao wakiwa katika bustani ya hoteli ya Mzsons shangani Zanzibar wakati wa makabidhiano kabla ya kuaza kwa mkutano wa kutathimini uwekaji wa kumbukumbu. uliofanyika katika hoteli hiyo

  0 0

  Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty hati ya makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty hati ya makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam.Picha ya pamoja kati ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na maofisa wa kampuni ya TBL mara baada ya hafla ya makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, hafla hiyo ilifanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam. Picha ya pamoja kati ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na maofisa wa kampuni ya TBL mara baada ya hafla ya makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, hafla hiyo ilifanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es SalaamMkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akiwa katika hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akiwa katika hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam.

  Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota kulia akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akiwa katika hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota kulia akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akiwa katika hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota kulia akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akiwa katika hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota kulia akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akiwa katika hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam.Mmoja wa maofisa wa TTCL kitengo cha mawasiliano (Multiprotocol Label Switching Virtual Private Network - MPLS VPN) akitoa ufafanuzi na faida za matumizi ya mfumo wa huduma za mawasiliano ya sauti, intaneti pamoja na data wa TTCL. Mmoja wa maofisa wa TTCL kitengo cha mawasiliano (Multiprotocol Label Switching Virtual Private Network - MPLS VPN) akitoa ufafanuzi na faida za matumizi ya mfumo wa huduma za mawasiliano ya sauti, intaneti pamoja na data wa TTCL.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akiiwakilisha kampuni yake katika hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akiiwakilisha kampuni yake katika hafla hiyo iliyofanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akisaini hati ya makabidhiano na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ya mradi wa kuiunganisha kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya Bia Tanzania jana jijini Dar es Salam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Peter Ngota akishuhudia.Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akisaini hati ya makabidhiano na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ya mradi wa kuiunganisha kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya Bia Tanzania jana jijini Dar es Salam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Peter Ngota akishuhudia.
  Baadhi ya maofisa wa kampuni ya TBL wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, hafla hiyo ilifanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam. Baadhi ya maofisa wa kampuni ya TBL wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL) jana jijini Dar es Salam, hafla hiyo ilifanyika ofisi za TBL Ilala jijini Dar es Salaam.[/caption] Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imekabidhi mradi wa kuiunganisha matawi 12 ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika huduma za mawasiliano ya sauti, intaneti pamoja na data ili kuviwezesha vituo hivyo kufanya kazi katika mfumo wa kisasa kimawasiliano jambo ambalo litaboresha utendaji kazi wa kampuni hiyo. Akikabidhi mradi huo leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya TTCL, Peter Ngota alisema kwa sasa wamekamilisha kuyaunga kimawasiliano ya kisasa matawi 12 ya kampuni ya bia Tanzania ambayo ni pamoja na tawi kuu la Dar es salaam (HQ), Arusha, Moshi, Mwanza, Ubungo, Mwenge, Konyagi, Masaki, Bukoba, Shinyanga, Iringa na tawi la Tanga. Alisema mfumo huo wa mawasiliano unaunganisha makao makuu ya ofisi na matawi yake ambayo yako maeneo tofauti nchini kwa lengo la kurahisisha utoaji na upokeaji wa Taarifa (Data) huku ukiwa salama tofauti na mifumo mingine. "...Katika mfumo huu wa Multiprotocol Label Switching Virtual Private Network (MPLS VPN), Tanzania Breweries Ltd inapata huduma ya sauti, intaneti pamoja na data. Kwa huduma hizi TBL sasa iendelee kwa kasi kuboresha mifumo ambayo itasaidia kuongeza tija katika utendaji kazi wake na kwa wateja kwa ujumla," alisema Ngota. Ofisa huyo Mkuu wa Masoko na Mauzo aliongeza kuwa kwa sasa TTCL ni kampuni pekee yenye mtandao wa Mkongo (Fibre) ambao umesambaa nchi nzima huku ukiwa chachu ya kuleta mabadiliko katika kutoa huduma kwa wananchi na utendaji kazi wa jumla wa makampuni mbalimbali. TTCL imekuwa nguzo muhimu kwa Taasisi za kifedha (Kibenki), Balozi, Mashirika, Wizara na taasisi za serikali, makampuni ya kimataifa na binafsi katika kuboresha utendaji na uendeshaji wa shughuli zao kisayansi na kukidhi viwango vya kimataifa. TTCL pia imefanikiwa kuunganisha wateja mbalimbali ikiwa ni pamoja taasisi na ofisi za serikali; TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wizara ya Fedha, Kampuniya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Bima la Taifa (NIC). Alisema huduma hiyo ya mkongo pia imerahisisha kazi katika Hospitali ya Muhimbili, Mwananyamala, Temeke, MOI, Bugando, KCMC pamoja na Hospitali za Mkoa nchi nzima ikiwemo Zanzibar pia zinaendelea kuunganishwa kupitia Mkongo wa TTCL kwa huduma bora za kiafya kupitia afya mtandao. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty akipokea mradi huo alisema tayari wameanza kuona mafanikio makubwa baada ya kuanza kutumia mfumo huo huku ukisaidia kukua kwa biashara yao tofauti na awali. Aidha alisema kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea kukua kila uchao kampuni hazina budi kufanya kazi kwa kutumia teknolojia mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa kazi na ubora hali itakayochangia kukua pia kwa biashara zao. "...Tayari tumeanza kuona mafanikio tangu kuanza kutumia huduma hii na tunaamini tutapata mafanikio zaidi, kwa sasa unaweza kutofautisha na ilivyokuwa kabla ya kuanza kutumia MPLS VPN," alisema O'Flaherty.*Imeandaliwa na mtandao: www.thehabari.com ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com Click here to Reply, Reply to all, or Forward 5.57 GB (37%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 0 minutes ago Details 11 more Joachim Mushi's profile photo Joachim Mushi Friends Show details

  0 0

  naibu waziri wa maliasili na utalii mahamod mgimwa ambye pia mbunge wa jimbo la mufindi kasikazini.
   hapa mabingwa wa kombe hilo wakishangia ushindi pamoja na mgeni rasmi pamoja na viongozi mbalimbali.
  mratibu wa mashindano hayo aliyetangaza kustahafu kuratibu mashindano hayo.


  na fredy mgunda,iringa

  akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya kombe la muungano mratibu wa kombe hilo DAUDI YASSIN alimpongeza mbunge wa mufindi wa jimbo la mufindi kasikazini ambaye pia ni naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMOD MGIMWA kwa kisaidia kutoa zawadi.


  YASSIN alisema kuwa tulipungukiwa baadhi ya zawadi kutokana na kombe hilo kufanyika bila ya kuwa na mdhamini wa kudumu hivyo aliamua kumtafuta mbunge huyo na kumuomba awasaidie baadhi ya zawadi kutokana na kukwama kwake.


  "niliamua kumtafuta mbunge wetu ili atusaidie kwa kuwa tulikuwa tumepungukiwa kwenye upande wa zawadi hivyo mgunge huyo naye hakusita akatusaidia" alisema DAUDI YASSIN
  baada ya hapo nilisikia minong'ono ya wananchi waliokuwepo  uwanja hapo walimsifia mbunge huyo kwa kijitolea na kuwasaidia waandaaji wa mashindano hayo kutokana na waandaaji kuto kamilisha baadhi ya zawadi.

  lakini wananchi hao ambao ni wapenzi wa michezo waliendelea kumuongea mbunge wao kwa kusema amekuwa akitolea mara kwa mara katika matatizo mbalimbali ya wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa bado ana wajali na kuwapenda.

  hata hivyo baadhi ya wananchi waoshabikia chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)walisema kuwa licha ya wao kuwa katika chama hicho lakini bado wanaukubali na kuupokea mchango wa mbunge huyo ambaye amekuwa akisaidia maendeleo katika jimbo hilo.

  niliamua kutafuta mbuge huyo kwa njia ya cm ili kujua kwanini ameamua kuwasidia wananchi wake kipindi hiki cha uchaguzi alijibu hivi "hiyo sio mara ya kwanza kufanya hivyo nimekuwa nikifanya mara kwa mara kwa lengo la kuleta maendeleo ya katika jimbo hilo"alisema mgimwa


  MGIMWA aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kuendelea kumuunga mkono wakati wa kuleta maendeleo na kuacha na itikadi ya vyama,inatakiwa tukae pamoja ili tuweze kuleta maendeleo kwa kuwa akifanya pekee yake ataweza kuleta maendeleo hivyo ushirikiano kwa pamoja ndio njia sahihi ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo.   

  0 0

   Meneja Mradi wa Kilimo cha Shayiri TBL Dk. Basson Bennie akitoa elimu kwa wakulima na wadau mbalimbali namna sahihi ya kuandaa, kupanda zao la Shayiri wakati wa Siku ya Mkulima wa Shayiri iliyofanyika juzi wilayani Monduli mkoani Arusha.
   Afisa Ugani Nyanda za Juu Kusini, Makambako, Iringa Njombe, Rukwa na Mbeya Paul Antapa mwenye fulana nyekundu akimkaribisha Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoani Arusha Jowika Kasunga wakati wa Siku ya Wakulima wa Shayiri iliyofanyika Monduli Juu pembeni yao ni Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Edith Mushi.
  Meneja wa Kiwanda cha TBL Arusha Salvartory Rweyemamu akibadilishana mawazo na Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga wakati wa Siku ya Mkulima wa Shayiri iliyofanyika juzi kwenye mashamba ya wakulima hao yaliyopo Kata ya Monduli Juu.

   Baadhi ya wakulima wa Shayiri wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye Siku ya Mkulima wa Shayiri na  Wataalamu mbalimbali wa kilimo walioalikwa na Kampuni ya Bia nchini TBL.
   Baadhi ya wakulima na wadau wa Kilimo cha Shayiri wakifuatilia maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Kilimo cha Shayiri kutoka TBL Dk. Basson Bennie alipokuwa akitoa elimu ya namna sahihi ya kuandaa shamba kabla ya kupanda wakati wa Siku ya Mkulima wa Shayiri iliyofanyika Monduli mkoani Arusha.
   Baadhi ya wakulima na wadau wa Kilimo cha Shayiri wakifuatilia maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Kilimo cha Shayiri kutoka TBL Dk. Basson Bennie alipokuwa akitoa elimu ya namna sahihi ya kuandaa shamba kabla ya kupanda wakati wa Siku ya Mkulima wa Shayiri iliyofanyika Monduli mkoani Arusha.
   Afisa Ugani Nyanda za Juu Kusini, Makambako, Iringa Njombe, Rukwa na Mbeya Paul Antapa akimsaidia kufungua bomba la dawa Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Monduli Juu Barick Kivuyo baada ya kukabidhiwa mabomba 10 na Kiwanda cha TBL, katikati yao ni Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga aliyekuwa mgeni rasmi kwenye Siku ya Mkulima wa
  Shayiri iliyofanyika wilayani hapa.
   Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoani Arusha Jowika Kasunga akijaribu kuponyeza udongo ili kuonyesha tofauti kati ya udongo wa shamba unaotakiwa na usiotakiwa wakati wa utoaji elimu kwa wakulima kwenyeSiku ya Mkulima wa Shayiri iliyofanyika Monduli Juu mkoani Arusha na kuwandaliwa na Kampuni ya Bia ya nchini (TBL)
   Meneja Mradi wa Shayiri Dk. Basson Bennie akijaza maji kwenye chupa za plastiki kwa ajili yakuwaonyesha wwakulima wa shayiri namna ya kupima udogo wa shambani.
  Baadhi ya wadau na wakulima wa Shayiri wakifuatilia maelezo kutoka kwa mtalaamu hayupo pichani wakati wa Siku ya Mkulima wa Shayiri iliyofanyika wilayani Monduli juzi na kuandaliwa na
  Kampuni ya Bia nchini (TBL).

  0 0
 • 06/12/15--02:05: Article 18

 • 0 0

  IMG_0984
  Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakikagua mitaala ya kufundishia kwenye ofisi za walimu katika shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo huku Afisa Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith Mackenzie (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa ugeni huo.
  (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

  Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
  MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Alvaro Rodriguez ametaka serikali za tawala za mikoa na serikali za mitaa kuwezeshwa zaidi ili kuweza kuwatumikia wananchi.

  Aliyasema hayo wakati alipozuru kijiji cha Chasimba mwishoni mwa juma akiwa na Balozi wa Hispania Luis Cuesta Civis kuona miradi ya maendeleo inayofadhiliwa kwa pamoja kati ya serikali ya Tanzania, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Hispania.

  Mratibu huyo alisema kwamba mafanikio makubwa yanayoonekana katika kijiji cha Chasimba ni matokeo ya ushirikiano mzuri wa wadau wa maendeleo na wanakijiji.

  Alisema ushirikiano huo ni muhimu katika kutokomeza umaskini uliokithiri katika jamii.

  Alisema pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo wangelipenda kuona serikali za mitaa zinawezeshwa zaidi ili kuweza kusaidia jamii kama inavyofanyika sasa katika kijiji cha Chasimba.

  Kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji kadhaa nchini vinavyofaidika na mpango unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF, ambao nao unachangiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo.

  Alisema anapenda kuona kwamba maisha ya wakazi wa kijiji hicho yanabadilika na kuwa kama ya mama Kicheko ambaye ameondoka katika umaskini uliokithiri baada ya kutumia vyema mradi uliofikishwa kijijini hapo.

  Alitoa wito kwa wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kusaidia kuwezesha serikali za mitaa na mashirika yanayoapambana na umaskini nchini kuwezesha miradi ya kuondoa umaskini kufanikiwa.

  Bi. Kicheko ambaye mwaka mmoja uliopita alikuwa hohehahe kwa sasa anatengeneza sabuni, ameboresha nyumba yake kwa kuiwekea bati na ana kula mlo zaidi ya mmoja sasa.

  Katika ziara hiyo, Mratibu huyo alitaka kujua wananchi wa Chasimba katika miaka mitano hadi saba ijayo wanataka kuwaje na kujibiwa kwamba wanataka kuwa na hali bora zaidi ilivyo sasa na kuanzisha viwanda vidogo.


  0 0

  Na Mwandishi Wetu.

  Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Januari Makamba amewaomba wanachama wenzake wa CCM walioko Njombe kutochukulia suala la ugombea kwa ushabiki kiasi cha kuzua mtafaruku ndani ya chama, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wake.


  Makamba ameyasema hayo alipokuwa akiwashukuru wanachama wenzake waliojitokeza kumdhamini ili kupata ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.


  "Najua katika kipindi hiki, ambacho wanachama wengi tumejitokeza kuwania nafasi hii kila mtu ametengeneza kundi la wafuasi ambao wengi wanadhani kwamba kuwa kundi la mtu mmoja basi wewe ni adui wa kundi jingine. Hili ni kosa, sote tunania njema na nchi hii, tujenge mazxingira ya kutooneana haya baada ya kupatikana kwa mgombea mmoja kwa kuungana mkono bila kuchafua wengine", alisisitiza Makamba.


  Makamba ameonya pia kuhusu kuchafuana kwa watangaza nia, wenyewe kwa wenyewe ambako kutasababisha kazi nyingine kubwa ya kuanza kumsafisha mgombesa atakayesimamishwa na chama muda utakapofika.


  Leo mchana Makamba anatarajiwa kupokea wadhamini mkoani Songea na baadae kuelekea Mbeya mjini ambako pia atafanya zoezi hilo.

  Mh January Makamba akicheza ngoma pamoja na wanachama wa CCM wilayani Njombe waliojitokeza kumdhamini.


  0 0

  Na Mwandishi wetu.
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeonya kwamba haitamvumilia mtendaji ye yote wa Serikali  au Taasisi zake za Umma atakayebainika anazorotesha ufanisi wa kazi pamoja na kuendeleza makundi katika sehemu za kazi.

  Onyo hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Idara ya upigaji chapa na Mpiga chapa Mkuu wa Serikali baada ya kuangalia utendaji kazi wa fanyakazi hao katika sehemu mbali mbali za Kiwandi hicho hapo Maruhubi Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

  Balozi Seif alisema yapo mambo yanayofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi za Umma ambayo hayapendezi kwa vile yanazorotesha ufanisi wa kazi kutokana na baadhi yao kupenda majungu na uvivu wa uwajibikaji.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alionya kwamba wapo watendaji katika Kiwanda cha Uchapaji wenye tabia ya kuendeleza uvivu jambao ambalo linawavunja moyo wenzao walioamua kufanyakazi kwa juhudi. Hivyo watendaji hao wanapaswa kujirekebisha mara moja.

  Alifahamisha kwamba tabia hiyo mbaya inaiumiza Serikali Kuu iliyoamua kutumia fedha nyingi  za kigeni katika kuimarisha miundo mbinu ya kisasa ya Kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha katika kiwango chaTeknolojia ya  kisasa.

  “ Pamoja na changamoto zinazokukabilini katika utendaji wenu wa kazi lakini Serikali kamwe haitosita kumchukulia hatua mtendaji ye yote atakayeonyesha tabia ya kuanzisha makundi na uvivu katika kazi “. Alisema Balozi Seif.

  Aliwaeleza wafanyakazi hao wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali  waelewe kwamba wanawajibika katika eneo muhimu kwa Taifa jambo ambalo wanahitajika kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifafanua kwamba Ofisi yake inayosimamia Kiwanda hicho iko katika matayarisho ya kuandaa Rasimu itakayoiomba Serikali Kuu kukifanya kiwanda hicho mabadiliko ya kuwa Mamlaka inayojitegemea.

  Alisema hatua hiyo itasaidia kuiongezea mapato Taasisi hiyo yatakayokidhi huduma za uendeshaji kamili pamoja na mafao ya wafanyakazi waoenbdesha  Kiwanda hicho.

  Mapema Wafanyakazi hao walielezea changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ambazo zimekuwa zikichangia kupunguza ari yao ya kjazi.

  Walisema tatizo la usafiri kwa watendaji wanaomaliza kazi nyakati za usiku limekuwa mtihani mkubwa wa muda mrefu, posho  kwa muda wa ziada pamoja na ukosefu wa mafunzo kweza kuzimudu vyema mashine za kisasa wanazotumia.

  Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya changamoto hizo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohammed alisema kwamba Wizara hiyo itaomba ruhusa ya Serikali Kuu kununua Gari itakayosaidia kupunguza changamoto ya usafiri kwa watendaji hao.

  Dr. Khalid alisema tatizo la posho za ziada kwa watendaji hao zimekuwa zikilipwa na Wizara  kwa mujibu wa maombi yhanavyopelekwa licha ya kwamba Taasisi hiyo imekuwa ikitumia fedha za ziada za Idara nyengine katika kununulia mali ghafi za kuchapisha kazi muhimu za Taasisi za Serikali.

  Akigusia suala la mafunzo Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kuwa Wizara ina mpango wa kuwapeleka mafunzoni wafanyakazi watano wa  Kiwanda hicho kwenye kwenye mashine zinazofanana na zile wanazotumia ili wapate uzoefu.
   Makamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia harakati za matengenezo ya Vitabu vya Baketi katika Kiwanda cha Uchapaji Maruhubi wakati alipofanya ziara fupi ya Kutembelea kiwanda hicho.Kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bibi Hanat mohammed Aboud.
  Mkuu wa Kitengo cha Kompyuta katika Kiwanda cha uchapaji Maruhubi Nd. Moh’d Abass Rajab akimuonyesha  Balozi Seif aina za michoro tofauti  inayosarifiwa katika uchapaji wa vitabu na majarida mbali mbali yanayopelekwa  na wateja kuchapishwa kwenye kiwanda hicho.
  Picha na –OMPR – ZNZ.


  0 0
 • 06/12/15--03:21: Article 14
 • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 96
  TAREHE 12 JUNI, 2015
  MEYA MWANZA KUFUNGA U13 KESHO
  Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kesho jumamosi atafunga rasmi mashindano ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13.

  Sherehe ya kufunga mashindano hayo itafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa9 kamili alasiri .

  Kwa takribani wiki moja sasa mashindano hayo yamekuea yakiendelea jijini Mwanza katika viwanja vya Alliance na CCM Kirumba.

  Lengo la mashindano haya ni kuibua vipaji kwa ajili ya kupata timu ya Taifa ya awali itakayojiandaa na fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019 fainali zitafakazonyika nchini Tanzania.

  Katika kutambua na kujiunga na watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) siku hiyo ya tareje 13/06/2015, TFF itajiunga na familia ya walemavu wa ngozi katika kuadhimisha siku yao kimataifa na kuonyesha bango maalum leney kuelimisha umma juu ya ubaya wa uovu wa kuwaumiza na kuwaua  wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (pichani) , amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Iringa kwenda Zanzibar kutaka kugongana uso kwa uso na ndege nyingine dakika moja kabla ya kutua.

  Waziri Membe akiwa na ujumbe wake wa watu wanane, walikuwa wakisafiria ndege ya kukodi kampuni ya 5H NEG Precition Aviation ikirushwa na rubani Mathew Mhahiki, ambaye ameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilodai “ni kwa rehema za Mungu tumepona ajali hii.” 

  Akizungumza na mwandishi wetu aliyeko katika ziara yake, rubani Mhahiki alisema: “Lazima kuna tatizo katika control center hata hivyo tayari nimeongea nao na wameniomba samahani na kudai walipitiwa, maana kwa hali ilivyokuwa ni kwamba tungegongana wakati wa kutua maana nimeshangaa tu kuona ndege hii hapa ndiyo maana nikaamua kumkwepa mwenzangu nikapanda juu.”

  Waziri Membe alisema: “Nina uzoefu mkubwa wa kusafiri na ndege mahali pengi duniani, hali hii ilikuwa ni ajali na labda sasa tungekuwa dead bodies, lakini ninajua Mungu yuko upande wetu katika safari hii ya uhakika, lakini pia izingatiwe nimekuja kufanya kazi ya Mungu.” 

  “Katika safari hii tutashuhudia mambo mengi sana, lakini kwa kuwa kila ninapotaka kuondoka nyumbani ama hotelini mara nyingi nimekuwa nikimtanguliza Mungu maana bila Mungu hii ilikuwa ni mwisho wa maisha yetu tuliokuwa kwenye ndege hii.”

  Waziri Membe alikuwa amealikwa mjini hapa na Umoja wa Akimama wa Kikristu (Umaki) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar waliokuwa wakifanya mkutano wao mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano akitokea Iringa ambako alikwenda kutafuta udhamini wa chama ili kumwezesha kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM.

  Akiwa uwanjani hapo, Waziri Membe alikutana na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba aliyekuja hapa Zanzibar kutafuta wadhamini ambapo makada hao walipata nafasi ya kuzungumza. 

  Akiwa katika mkutano huo, Waziri Membe alisema: "Miongoni mwa mambo yanayonikera ndani nafsi yangu ni kuona mwanamke bado anaachwa nyuma, hili halipendezi, ni lazima tuhakikishe wanawake wanapata elimu ya ufundi stadi maana mwanamke akiwezeshwa hasa katika eneo hili la elimu wanaweza hata kushinda wanaume wengi.”

  “Ni lazima kina mama wawezeshwe kujiajiri ili msiwategemee kina baba kwa kila jambo lakini pia ili kufikia malengo hayo ni lazima tuwape elimu kina mama.”

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mteule wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Burundi Mhe,Rajab Gamala alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha jana,[Picha na Ikulu.]

  0 0


  Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wana CCM waliofika kumdhamini pamoja na wananchi wengine, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wana CCM 9516 kwa mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo safari yake ya kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kimteue kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
  Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea majina kutoka kwa Naibu Katibu wa CCM Wilaya ya Tabora Mjini, Bi. Hidaya Rashid yenye idadi wanachama wa CCM 9516 waliomdhamini ili aweze kuteuliwa na Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
  Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM waliofika kumdhani pamoja na wananchi wa Mji wa Tabora, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015.
  Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Mzee Juma Nkumba, aliewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani Tabora miaka ya nyuma.

  Mh. Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Wazee wa Mji wa Tabora.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa ya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.
   Wanahabari wakiwa katika mkutano na Bwana Makonda.
  Waandishi wa habari kutoka vyombombalimbali wakichukua taarifa hiyo.

  Dotto Mwaibale

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema atachukua sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kuwalipa wanasheria watano watakao kuwa wanafanya kazi ya kusikiliza na kuwasaidia wananchi wenye migogoro ya ardhi.

  Makonda alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika wilaya yake ya Kinondoni Dar es Salaam leo asubuhi.

  "Kama nilivyobadilisha mfumo mzima wa PF3 ndivyo ninavyofanya kwenye ardhi nimechukua hatua mahususi kuchukua sehemu ya mshahara wangu na kuajiri jumla ya wanasheria watano watakao wasaidia wananchi hasa wanyonge kupata haki zao juu ya madai yao mbalimbali yahusuyo ardhi" alisema Makonda.

  Alisema wanasheria hao watachukua asilimia 75 ya mshahara wake kwa kazi hiyo hivyo mwananchi wa Wilaya ya Kinondoni hatatakiwa kulipa hata senti tano atakapokuwa amekwenda kupata huduma hiyo.

  Makonda alisema kuwa kuanzia Jumatatu ya Juni 15, 2015 wanasheria hao watakuwepo ofini kwake watakaofanya kazi saa zote kwa lengo la kusaidia ili wapate uelewa wa kisheria juu ya haki zao zozote kuhusu umiliki wa ardhi.

  Makonda alisema heshima aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete ya kumteua kuwa mkuu wa wilaya hiyo kwake anatafsiri kama changamoto kubwa ya kuhakikisha anashughulikia kwa kina matatizo ya msingi ya wilaya hiyo.

  Alisema katika wakati huu huwezi kutaja changamoto kubwa tatu za wilaya hiyo ukaacha kutaja migogoro ya ardhi na kuwa kwa ufafanuzi zaidi unaweza kurejea hotuba yake ya Februari 28, 2015 wakati akianza kazi mambo aliyoyataja na kuyapa kipaumbele ambapo alitenga kila siku ya Ijumaa kuwa ni siku ya kukutana na watu wenye migogoro ya ardhi ili kuitatua.

  Makonda alisema ili kumaliza changamoto hiyo ya migogoro ya ardhi kama si kuipunguza kwa kiwango cha juu kila mkazi wa wilaya hiyo anatakiwa kuchukua kopi ya hati au nyaraka yoyote ile inayompa uhalali wa kumiliki ardhi, shamba au kiwanja na kopi hizo zipelekwe kwa ofisi ya mtendaji wa kata kwani kuanzia Julai 2, 2015 yeye na timu ya watu wa ardhi atahamishia ofisi yake kwenye kata hizo kwa ajili ya kuzihakiki nyaraka hizo.

  Alisema pindi watakapo baini kuwa kiwanja kimoja kina zaidi ya mmiliki mmoja watamtafuta mmiliki halali kupitia vyombo walivyonavyo na atakayebainika ameghusi atachuliwa hatua.

  Alisema lengo la kuhamishia ofisi yake kwenye kata ni kufuta kabisa uzoefu wa kusikitisha wa wananchi mmoja kugundua kwamba kiwanja chake kinamilikiwa na mtu mwingine baada ya kumwaga roli la mchanga ama tofali. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com- simu namba 0712-727062)


  0 0


  Monica  Mbega  (kulia) akifurahi pamoja na wana CCM Iringa mjini ambao   walijitokeza kumdhamini  kuwa mgombea wa nafasi ya  urais   kupitia CCM.
  Monica Mbega akionyesha orodha ya  wadhamini  wake

  Hata  mimi nimechukua fomu ya  Urais :Naibu  meya  wa Manispaa ya  Iringa ambae ni diwani  wa kata ya  Ilala Bw  Gervas Ndaki akifurahia kushika mkoba  wenye fomu ya  CCM ya  kuomba kuwa mgombea  wa nafasi ya  Urais  wa Jamhuri ya  Muungano  wa Tanzania ,fomu ya Monica Mbega  baada ya mgombea  huyo  kufika mjini Iringa  kusaka  wadhamini 30
  .........................................................
   Na  Matukiodaima Blog
  WAKATI mbio za makada  wa chama  cha mapinduzi (CCM)  waliotia nia ya  kuomba  kuteuliwa  kuwa wagombea wa nafasi za urais zikiendelea  kushika kasi kwa  kila mgombea kutumia mbinu yake ya  kuwafikia wana CCM kuomba udhamini , aliyekuwa mbunge wa  jimbo la Iringa mjini .

  Monica Mbega leo  ameingia wilaya ya Iringa mjini mkoani hapa  kuomba udhamini na kupata  wajumbe 33  huku akiwataka  watanzania kutoaminishwa na mbwembwe  za  watia nia wenzake wanazofanya mikoani na  kuwa yeye ndie Rais wa awamu ya tano baada ya Dr Jakaya Kikwete  na  kuwataka  watia  nia wenzake wamuunge mkono.

  Mbega ambae  alilazimika  kusubiri wajumbe 30   wa  kumdhamni  kwa  zaidi ya masaa manne katika ofisi ya CCM wilaya ya  Iringa  mjini  alitoa kauli  hiyo wakati  akizungumza na  wanahabari juu ya safari  yake  hiyo ya  kutaka  kwenda Ikulu na kudai  kuwa amelazimika  kuzuia  viongozi  wa CCM wilaya ya  Iringa kutomuandalia  mbwembwe  zozote wala wapambe wa kumshangilia  wakati  wa safari  yake  hiyo ya  kutafuta  wadhamini.

  Alisema  kuwa kuwa anamtegemea  Mungu  zaidi katika  safari yake  hiyo ya kwenda Ikulu na ndio maana  hakupenda  kuweka makisio ya gharama  za safari nzima ya mchakato huo wa kuelekea  kupokea kijiti kwa Rais Dr Kikwete na  hivyo ndio  sababu ya  yeye  kuzunguka  bila ya mpambe zaidi ya dereva  anayemuendesha pekee.

  " Naomba  niwaelezeni  wazi  kuwa sina mgombea  wa  kumuunga mkono kati ya  wote  waliojitokeza  zaidi ya 30 kwani naamini  kuwa namba   moja kati ya  wote  hao waliojitokeza ni  Monica Ngenzi Mbega   ninasema   hivyo  kwa  kuwa  nchi ya  sasa inahitaji mwamanke kuongoza  kwani  mwenye  kuweza  kuvunja makundi ni mwanamke sio mwanaume tena .....mwanamke ni mwepesi  wa  kusamehe  sio mtu wa makundi hivyo kama hivyo  ndivyo ukitanguliza  upendo makundi hayatakuwepo ila  wapo  wenye visasi vya kutoka mwaka 2005 ila sio mimi ....mimi nimetanguliza upendo  zaidi....mimi  ni mama nitaiunganisha  nchi na  changamoto  inayomkabili Rais wa awamu ya tano ni  jinsi na kuiunganisha  nchi na mimi ndie pekee  wa kuunganisha nchi hii"

  Alisema  kuwa  iwapo  watanzania  wataunganishwa  kuwa  wamoja kuna  uwezekano  wa nchi  kuachana na utegemezi na hivyo  wananchi  wake kuwa  wamoja na  kuweza kushiriki kujiletea maendeleo yao  chini ya rais wao Mbega .

  Hivyo  alisema  kuwa iwapo chama  chake  kitamteua  na watanzania  wakamchagua  na  kuingia Ikulu  wategemee Tanzania  mpya  yenye amani ,upendo na mshikamano na uchumi  bora  kwa  kila mtanzania  kuongeza pato  binafsi .

  Mbega  alisema  kuwa tayari  Rais wa nchi  Dr  Kikwete  amepata  kuueleza  umma kuwa misaada ambayo  nchi  inapata  kutoka kwa  wahisani mingine ina masharti magumu  na ndio maana  ya baadhi ya miradi kushindwa  kukamilika kwa  wakati na  kuwa iwapo yeye ataingia  Ikulu atajaribu kukwepa misaada  hiyo na  kulijenga Taifa  linalojitegemea lenyewe  ili kuto kuwa na miradi isiyo kamilika kutokana na masharti magumu ya  wahisani .

  Alisema  kuwa  kikubwa  kilichomsukuma kuchukua  fomu  ya  kutia nia kuomba  kuteuliwa  kuwania Urais ni uzalendo  wake  katika Taifa wenye shauku  la  kuliongoza Taifa la Tanzania kama mwanamke  wa kwanza  toka  nchi ipate  uhuru  wake mwaka 1961 bila ya  kuongozwa na mwanamke na  kudai kuwa hakuna  mgombea  wa CCM ambae anajambo lake  binafsi la  kufanya  zaidi ya kutekeleza  ilani ya uchaguzi ya CCM.

  "Falsafa  yangu ni kusahihisha  changamoto zinazoonekana  katika  kutekeleza  ilani hatujaweza  kufanikiwa hili ....mheshimiwa Rais Dr Kikwete  tunaona jinsi anavyotekeleza ilani katika  sekta  mbali mbali ila  utasikia  katika  vikao  vya kamati  kuu  wakati akitoa taarifa ya  utekelezaji  kuwa kuna changamoto mbali mbali ambazo zimekwamisha  utekelezaji wa ilani hivyo  mimi nitaanzia kutekeleza  changamoto kwanza .....kwani bajeti  inayotengwa ndio inapaswa  kusimamiwa  kwanza  mwelekeo mzima  wa serikali yangu ni  kuona tunapata Taifa la watu  wanaojitegemea wenyewe"

  Katika  hatua nyingine Mbega ambae aliangushwa nafasi ya  ubunge  mwaka 2010 na mbunge Peter Msigwa (Chadema)  alisema  kuwa bado ana nguvu  ya  kurudi  kugombea ubunge  jimbo la Iringa mjini na kumshinda mbunge  wa sasa mchungaji Msigwa kwani bado nguvu  za  kurejesha  jimbo hilo  CCM anazo japo hana mpango wa ubunge zaidi ya  kutimiza dhamira yake ya  kuingia Ikulu kama Rais aliyokuwa nayo toka mwaka 2005 na  alishindwa  kuingia mwaka 2010 kwa  kumheshimu Rais Dr  Kikwete pekee ila  sasa ni zamu  yake .

  Pia  alisema   CCM bado ina nguvu zaidi katika  jimbo la Iringa mjini na Tanzania kwa ujumla na iwapo  suala la upendo  likawatangulia  watia nia wote pale  wanapokosa  kuteuliwa kuungana kwa upendo  kumuunga mkono aliyeteuliwa kamwe suala la wapinzani  kushinda  litabaki  kuwa ni ndoto.
  Na Matukiodaima Blog , Iringa WAKATI mbio za makada wa chama cha mapinduzi (CCM) waliotia nia ya kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi za urais zikiendelea kushika kasi kwa kila mgombea kutumia mbinu yake ya kuwafikia wana CCM kuomba udhamini , aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega jana ameingia wilaya ya Iringa mjini mkoani hapa kuomba udhamini na kupata wajumbe 33 huku akiwataka watanzania kutoaminishwa na mbwembwe za watia nia wenzake wanazofanya mikoani na kuwa yeye ndie Rais wa awamu ya tano baada ya Dr Jakaya Kikwete na kuwataka watia nia wenzake wamuunge mkono. Mbega ambae alilazimika kusubiri wajumbe 30 wa kumdhamni kwa zaidi ya masaa manne katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa mjini alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari juu ya safari yake hiyo ya kutaka kwenda Ikulu na kudai kuwa amelazimika kuzuia viongozi wa CCM wilaya ya Iringa kutomuandalia mbwembwe zozote wala wapambe wa kumshangilia wakati wa safari yake hiyo ya kutafuta wadhamini. Alisema kuwa kuwa anamtegemea Mungu zaidi katika safari yake hiyo ya kwenda Ikulu na ndio maana hakupenda kuweka makisio ya gharama za safari nzima ya mchakato huo wa kuelekea kupokea kijiti kwa Rais Dr Kikwete na hivyo ndio sababu ya yeye kuzunguka bila ya mpambe zaidi ya dereva anayemuendesha pekee. " Naomba niwaelezeni wazi kuwa sina mgombea wa kumuunga mkono kati ya wote waliojitokeza zaidi ya 30 kwani naamini kuwa namba moja kati ya wote hao waliojitokeza ni Monica Ngenzi Mbega ninasema hivyo kwa kuwa nchi ya sasa inahitaji mwamanke kuongoza kwani mwenye kuweza kuvunja makundi ni mwanamke sio mwanaume tena .....mwanamke ni mwepesi wa kusamehe sio mtu wa makundi hivyo kama hivyo ndivyo ukitanguliza upendo makundi hayatakuwepo ila wapo wenye visasi vya kutoka mwaka 2005 ila sio mimi ....mimi nimetanguliza upendo zaidi....mimi ni mama nitaiunganisha nchi na changamoto inayomkabili Rais wa awamu ya tano ni jinsi na kuiunganisha nchi na mimi ndie pekee wa kuunganisha nchi hii" Alisema kuwa iwapo watanzania wataunganishwa kuwa wamoja kuna uwezekano wa nchi kuachana na utegemezi na hivyo wananchi wake kuwa wamoja na kuweza kushiriki kujiletea maendeleo yao chini ya rais wao Mbega . Hivyo alisema kuwa iwapo chama chake kitamteua na watanzania wakamchagua na kuingia Ikulu wategemee Tanzania mpya yenye amani ,upendo na mshikamano na uchumi bora kwa kila mtanzania kuongeza pato binafsi . Mbega alisema kuwa tayari Rais wa nchi Dr Kikwete amepata kuueleza umma kuwa misaada ambayo nchi inapata kutoka kwa wahisani mingine ina masharti magumu na ndio maana ya baadhi ya miradi kushindwa kukamilika kwa wakati na kuwa iwapo yeye ataingia Ikulu atajaribu kukwepa misaada hiyo na kulijenga Taifa linalojitegemea lenyewe ili kuto kuwa na miradi isiyo kamilika kutokana na masharti magumu ya wahisani . Alisema kuwa kikubwa kilichomsukuma kuchukua fomu ya kutia nia kuomba kuteuliwa kuwania Urais ni uzalendo wake katika Taifa wenye shauku la kuliongoza Taifa la Tanzania kama mwanamke wa kwanza toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 bila ya kuongozwa na mwanamke na kudai kuwa hakuna mgombea wa CCM ambae anajambo lake binafsi la kufanya zaidi ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM. "Falsafa yangu ni kusahihisha changamoto zinazoonekana katika kutekeleza ilani hatujaweza kufanikiwa hili ....mheshimiwa Rais Dr Kikwete tunaona jinsi anavyotekeleza ilani katika sekta mbali mbali ila utasikia katika vikao vya kamati kuu wakati akitoa taarifa ya utekelezaji kuwa kuna changamoto mbali mbali ambazo zimekwamisha utekelezaji wa ilani hivyo mimi nitaanzia kutekeleza changamoto kwanza .....kwani bajeti inayotengwa ndio inapaswa kusimamiwa kwanza mwelekeo mzima wa serikali yangu ni kuona tunapata Taifa la watu wanaojitegemea wenyewe" Katika hatua nyingine Mbega ambae aliangushwa nafasi ya ubunge mwaka 2010 na mbunge Peter Msigwa (Chadema) alisema kuwa bado ana nguvu ya kurudi kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini na kumshinda mbunge wa sasa mchungaji Msigwa kwani bado nguvu za kurejesha jimbo hilo CCM anazo japo hana mpango wa ubunge zaidi ya kutimiza dhamira yake ya kuingia Ikulu kama Rais aliyokuwa nayo toka mwaka 2005 na alishindwa kuingia mwaka 2010 kwa kumheshimu Rais Dr Kikwete pekee ila sasa ni zamu yake . Pia alisema CCM bado ina nguvu zaidi katika jimbo la Iringa mjini na Tanzania kwa ujumla na iwapo suala la upendo likawatangulia watia nia wote pale wanapokosa kuteuliwa kuungana kwa upendo kumuunga mkono aliyeteuliwa kamwe suala la wapinzani kushinda litabaki kuwa ni ndoto. MWISHO Picha namba 1; Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega akionyesha fomu yenye orodha ya wana CCM 33 wa mkoa wa Iringa waliomdhamini katika safari yake ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM jana mjini Iringa (picha na Francis Godwin) Picha namba 01 ;Naibu meya wa Manispaa ya Iringa ambae ni diwani wa kata ya Ilala Bw Gervas Ndaki akifurahia kushika mkoba wenye fomu ya CCM ya kuomba kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,fomu ya Monica Mbega baada ya mgombea huyo kufika mjini Iringa kusaka wadhamini 30 (picha na Francis Godwin) Picha namba 3 Monica Mbega (kulia) akifurahi pamoja na wana CCM Iringa mjini ambao walijitokeza kumdhamini kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia CCM (picha na Francis Godwin)

  Monica  Mbega  akisisitiza  kuwa hakuna zaidi  yake
  Monica Mbega  akizungumza na  wanahabari  mjini Iringa  leo baada ya  kudhaminiwa na wanachama  zaidi ya 33
  Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza akitoa taarifa ya  idadi ya  wana CCM waliomdhamini Mbega
  Mbega  akifurahia  orodha  ya  wana CCM waliomdhamini
  Baadhi ya  wadhamini wa  Mbega  Iringa
  Kada wa CCM mama Mwalusamba  akimuombea dua Monica Mbega
  Wadhamini wa Mbega  Iringa

  0 0


   Mh January Makamba akihutubia wanachi na wanachama wa CCM mkoani Ruvuma mara baada ya kabidhiwa fomu yenye sahihi za wanachama waliomdhamini.  Mh January Makamba akihutubia wanachi na wanachama wa CCM mkoani Ruvuma ndani ya ukumbi wa ofiswi kuu ya chama hicho mkoani Ruvuma. kuanzia kushoto ni mke January Makamba, Ramona Makamba, katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma, Verena Shumbusho na kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa, Odo Mwisho.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho akimkabidhi fomu yenye majina na sahihi za wanachama waliomdhamini mh. January Makamba. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Ruvuma.


  MBUNGE wa Bumbuli, January Makamba amewataka makada wote waliomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya urais ndani ya Chama  kuwa wanakiacha chama hicho kuwa salama baada ya mchakato huo kukamilika.

  January, aliyasema hayo baada ya kupokea orodha ya wanachama wa chama hicho, katiaka Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa Ruvuma jana, ambapo wanachama 3500 walijitokeza kumdhamini.

  Alisema hivyo kwa vile kuna wapo waomba ridhaa ambao wanadai kuwa endapo hawatateuliwa katika nafasi hiyo kuna hatari chama kikasambaratika.

  Alisema, chama hicho kinahitaji kupata mgombea ambaye atahakikisha kuwa nama hicho kinabaki salama na kwambapia atawaongoza watanzania wote bila kujali dini wala kabila zao, akibainisha kuwa yeye ndio sahihi katika kudumisha hayo.

   ”Mimi siamini siasa za kupakana matope kwani wote ni wanachama wa chama kimoja na mwisho wa siku tutapata mgombea mmoja na tutahitajika kumpigia kampeni”alisema Jamuary.

  January, alisema kama wagombea watapakana matope katika mchakato huo wa kuomba ridhaa kwa wanachama, anaamini wakati ukifika wa kumfanyia mteule utakuwa mgumu kwani itakuwa siyo rahisi kumfanyia kampeni ambaye tayari umekwisha kumpaka matope.

  “Niwaombe muwapime wagombea ambao wameonekana wakiomba nafasi hiyo kwa mbwembwe kwani hatawatakapopata nafasi hiyo wataongoza kwa mbwe jambo ambalo wananchi hawalihitaji”alisema Jamnuary.

  January, alisema kuwa chama hicho kiko makini na hakitamteua mgombea kwa woga kama inavyodaiwa na baadhi ya wagombea  kwamba wasipochaguliwa chama hicho kitasambaratika jambo ambalo siyo sahihi.

  Alisema kuwa anaamini kuwa chama hicho kitamteuwa mgombea ambaye ni muadilifu, atakuwa rahisi katika kumnadi kwa wananchi.

  Akizungumzia, mkoa wa Ruvuma, January, alisema mkoa huo hivi sasa unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la umeme na upande wa hospitali ya Mkoa.

  Alisema kwa vile matatizo hayo anayatambua, pindi atakapopewa ridhaa na chama na kuchaguliwa kuwa rais atahakikisha mkoa huo unaingizwa katika gridi ya Taifa kama ilivyo kwa mikoa mingine.

  Katika hatua yingine, juzi mkoani Njombe, January alipata wadhamini 84.

  January, alisema anaamini atakapokuwa rais atakuwa na uwezo wa kuamua mambo makubwa yanayolihusu taifa ukilinganisha na nafasi aliyosasa kwani inamopaka katika maamuzi ya kushughulikia mambo mbalimbali ya Taifa. 


  PICHANI JUU NA CHINI:    Mh January Makamba na mkewe, Ramona Makamba wakipeana mikono na wanachama wa CCM mkoa wa ruma waliofika katika ukumbi wa  mikutano katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Ruvuma.


  Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma, Verena Shumbusho akiwakaribisha mkoani Ruvuma Mh January Makamba na mkewe, Ramona Makamba.

  0 0

  NA MASANJA MABULA -PEMBA 
  …………………………………
  MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BALOZI ALI ABEID KARUME AMESEMA KUWA IWAPO CHAMA HICHO KITAMWANI NA KUMCHAGUA KUWA MGOMBEA WA KITI CHA URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO ATAHAAKIKISHA KWAMBA ANAYAVUNJA MAKUNDI YOTE YA WAGOMBEA .
  AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA WA CCM WILAYA YA WETE , BALOZI AMESEMA KUWA KAZI YA KWANZA ATAKUWA NI KUWASHIRIKISHA WANACHAMA WA CCM WALIOJITOKEZA KWENYE MCHAKATO HUO KUUNDA  SAFU IMARA YA UONGOZI .
  AIDHA AMESEMA KUWA ANATAMBUA KWAMBA KILA MGOMBEA ANAKUNDI LAKE NA KUONGEZA KWAMBA KWA UPANDE WAKE KUNDI ANALOLITEGEMEA NI CHAMA CHA MAPINDUZI .
  AMEAHIDI KUWAFUATA NA KUSHAURIANA NA WANACHAMA WENZAKE AMBAO WANAMAKUNDI HASA KATIKA KIPINDIN HICHI CHA KINYANGANYIRO CHA KUOMBA RIDHAA YA CHAMA KUPITISHWA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS  NA KUWASHAWISHI KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA LAKINI YA CHAMA KIMOJA CHA CCM
  “NATAMBUA KUWEPO NA MAKUNDI YA WAGOMBEA NDANI YA CHAMA , LAKINI IWAPO MIMI WATANIAMINI NITAHAKIKISHA KWAMBA MAKUNDI NINAYAVUNJA NA KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI AMBAYO ITAWASHIRIKISHA WAGOMBEA WOTE WALIOINGIA KWENYE MCHAKATO HU ” ALIFAHAMISHA .

  KATIKA HATUA NYINGINE BALOZI ALI AMESEMA KUWA IWAPO ATAPITISHWA NA CHAMA CHAKE KUGOMBEA NAFAI HIYO ATAHAKIKISHA KWAMBA ANATENDA HAKI NA KUBADILISHA UCHUMI WA NCHI KWA KUIMARISHA ELIMU YA UJASIRIAMALI ILI KUWAFANYA VIJANA KUWEZA KUJIAJIRI WENYEWE .
  AMEELEZA KWAMBA IWAPO ATACHAGULIWA KUWA RAIS WA NCHI HATAKUWA NA KINYONGO NA MTU KWA KUWA HANA UGOMVI NA MTU KWAMBA ATALIPA KISASI NA ATAWATUMIKIA WANANCHI WOTE WA UADILIFU
  NAYE BIZAINAB KHAMIS SHOMAR AMEWAAMBIA WANACHAMA HAO WA CCM KUWA BALOZI ALI AMEAMUA KUWANIA NAFASI HIYO YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BAADA YA KUTIMIZA MASHARTI , SIFA NA VIGEZO KUMI NA TATU AMBAZO ZIMEWEKWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI .

  AMESEMA KUWA BALOZI ALI HAKUBAHATISHA KUINGIA KWENYE MCHAKATO HUU KWANI AMETIMIZA SIFA NA MASHARTI YAALIYOWEKWA NA CHAMA HICHO NA NA HIVYO KUWA NA KILA SIFA YA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA .

  “BALOZI ALI AMETIMIZA VIGEZO NA MASHARTI YALIYOWEKWA NA CHAMA CHETU NA NDIYO MAANA AKAAMUA KUINGIA KWENYE MCHAKATO HUU , HIVYO NI WAJIBU WENU KUMDHAMINI KWANI NI MTU ANAYEJIAMINI NI MWADILIFU”ALIELEZA ZAINAB. 
  HII NI MARA YA PILI KWA BALOZI ALI ABEID AMAN KARUME KUWANIA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMBAPO MWARA YA KWANZA ILIKUWA MWAKA 2005.

  0 0

    Baadhi  ya wazee wa Dodoma waliofika kwenye ukumbi wa Halmashauri kuu ya taifa ya CCM kumsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza baada  ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya watu waliofika kwenye Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kumsikiliza wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma.
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza baada ya kuchukuwa   fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma. Kulia ni mkewe mama Tunu Pinda
  Sehemu ya wageni wakimsikiliza Mhe Pinda  wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya watu waliofika kwenye Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kumsikiliza wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma

  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri  wa Fedha Mh.Saada Mkuya Salum akiwa na katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Servacius Likwelile pamoja na Msajili wa Hazina Nd.Lawrence Mafuru wakipokea hundi ya mfano ya shilingi Bilioni 3 kutoka Puma Energy Tanzania Limited. Kushoto kwa Mh.Waziri ni Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Limited Nd. Philippe Corsaletti.

   Mh.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwashukuru watendaji wakuu wa Puma Energy Tanzania Limited kwa kuwasilisha kwa Serikali gawio la faida la shilingi Bilioni 3. Mawasilisho hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha,Mjini Dodoma. Kulia kwa Mh.Waziri ni Dr.Servacius Likwelile,Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali. 

older | 1 | .... | 552 | 553 | (Page 554) | 555 | 556 | .... | 1897 | newer