Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI KIJIJI CHA MAGOZA, MKURANGA

$
0
0
 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akikata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa gharama ya sh. mil 56, katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda, Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Karu Karavina na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (wa pili kulia).
 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto kwake) pamoja na Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, Karu Karavina (kushoto) wakifurahi baada kukabidhi mradi wa  kisima cha maji kwa wananchi wa Kijiji cha Magoza, wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL gharama ya sh. mil. 56.

 Akina mama wakicheza kwa furaha wakati wa hafla ya kukabidhiwa kisima chas maji na TBL
 Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akitoa utambulisho wakati wa hafla hiyo


 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akimtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda, wilayani Mkuranga, Pwani, wakati wa hafla ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kilichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 56 kijijini hapo. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.

 Mmoja wa akina mama akifurahia baada ya kuteka maji kwenye kisima hicho

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akielezea mikakati ya kuisaidia jamii katika uboreshaji wa sekta ya maji nchini kutoka  sehemu na faida inayopatikana katika mauzo ya vinywaji vyao
Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo wa kisima.
 Wakifunua pazia kuzindua mradi huo wa kisima
 Mgeni rasmi, Benjamin Majoya akifungua maji ya bomba badaa ya kuzindua kisima hicho
 Steve Kilindo wa TBL, akinywa maji baada ya kuzindua kisima hicho

Akina mama wakazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda,Mkuranga, wakiwa wamebeba ndoo za maji waliyoteka katika Kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kijiji hicho kwa gharama ya sh. mil. 56. Hafla ya TBL kukabidhi kisima hicho cha maji ilifanyika mwishoni mwa wiki.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA KUANZA ZIARA KESHO KUELEKEA KAGERA, GEITA ,MWANZA

$
0
0
Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza mapema leo jijini Dar na Waandishi wa habari, alieleza kuwa wataondoka jijini Dar kesho kwa basi maalumu, ambapo watasimama njiani katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na mengineyo kwa ajili ya kusalimia wananchi.
 Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisisitiza jambo zaidi kwa Waandishi wa habari, kuhusiana na ziara hiyo itakayoanza kesho.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana anatarajia kuanza ziara ya siku 28 kesho katika mikoa mitatu ya Kagera, Geita na Mwanza kukamilisha mikoa yote 30 nchi nzima.

Ziara hizo zenye malengo ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama zimekuwa na mafanikio kwa kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakumba wananchi hasa wa mikoani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo, Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema wataondoka jijini Dar kesho asubuhi kwa basi maalumu, ambapo watasimama njiani katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na mengineyo kwa ajili ya kusalimia wananchi.

“Ziara rasmi itaanza June 4 katika Wilaya ya Nyakanazi mkoani Kagera, lakini kesho tutakunywa chai Morogoro chakula cha mchana tutakula Dodoma halafu tutasalimia wananchi katika Mikoa ya njiani kama Singida, Nzega na tumepanga kulala Kahama mkoani Shinyanga, tukiamka ziara ndio itaanza rasmi,” alisema Nape.

Aliongeza kuwa katika ziara hiyo watatembelea majimbo yote ya uchaguzi hivyo amewataka wana-CCM na wananchi wengine kujitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu katika ziara hiyo ya kihistoria.

“Hii ni ziara ya kihistoria kwa sababu ya mambo matatu, kwanza tutatembelea visiwa vyote vya Ukerewe ambavyo ni nadra kutembelewa na viongozi, pili huu ni mwaka wa uchaguzi kuna masuala mengi yanahitaji ufafanuzi,” alisema.

Akitaja ratiba ya ziara hiyo Nape alifafanua kuwa, “Kuanzia Juni 5 mpaka Juni 15 tutakuwa Mkoa wa Kagera, Juni 16 mpaka 21 tutakuwa Mkoa wa Geita na Juni 22 mapaka Julai 2 tutakuwa Mwanza kuhitimisha ziara ya nchi nzima kwa mkutano mkubwa wa kihistoria.”

Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu faida za ziara hizi Nape alisema kuna masuala mengi ya kimaendeleo yalisimama lakini alipopita Katibu Mkuu Kinana ufumbuzi umepaikana, akitolea mfano mashamba yaliyobinafsishwa bila kufuata utaratibu alisema Rais Jakaya Kikwete, amefuta hati nyingi za mashamba ya wawekezaji na kurudishwa kwa wananchi.

“Kuna baadhi ya maeneo kulikuwa na zahanati zimeshajengwa lakini hakuna vibali, nimepata taarifa kuwa vibali vimeshapatikana na huduma zinaendelea, kulikuwa na matatizo ya ardhi za wananchi kuchukuliwa na wawekezaji katika maeneo ya Tanga, Arusha, Babati na maeneo mengine lakini kila kitu kipo sawa sasa na wananchi wanamshukuru Kinana,” alisema.

Aliongeza kuwa, “Nisisitize kuwa tumesema tutaondoka na basi maalumu kwa sababu kama kuna mwingine atafanya hivyo atakuwa ametuiga, mkumbuke hili wazo la kuondoka na basi ni la Katibu Mkuu.”.

Ikiwa ziara hizi zitamalizika salama Julai 2 mwaka huu, Kinana atakuwa Katibu Mkuu pekee wa CCM tangu kuanzishwa kwake Februari 5, 1977 kuzunguka nchi nzima kuangalia uhai wa chama na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.

Programu ya kukuza ajira zenye staha kwa vijana kuzinduliwa jijini Dar es Salaam juni 5, 2015

$
0
0



Washiriki wa mkutano wa asasi za Vijana ILI kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Frank Shija, WHVUM.
 Mratibu wa Programu ya kukuza Ajira zenye Staha Dar es Salaam, kupitia Elimu ya Biashara na Maendeleo ya Ujasiriamali Bw. Dominic Ndunguru akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa program hiyo jana jijini Dar es Salaam. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT)  na Youth For Africa (YOA).
 Mshauri wa maswala ya Sera na Miradi ya Maendeleo wa Tanzania Youth Vision Association Bw. Elly Ahimidiwe Imbyandumi akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano wa kutathmini utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha katika jiji la Dar es Salaam (YEID jana katika ukumbi wa Kituo cha Vijana cha Don Bosco cha jijini Dar es Salaam.Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT)  na Youth For Africa (YOA).
 Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa akielezea jambo wakati wa mkutano wa asasi za Vijana kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) mradi huo unalenga kuwajengea uwezo  vijana ili waweze kujiajiri na kuajirika. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT)  na Youth For Africa (YOA).
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa asasi za vijana wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa mkutano wa asasi za Vijana uliofanyika jana jijini Dar es Salaam ili kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) mradi huo unalenga kuwajengea uwezo  vijana ili waweze kujiajiri na kuajirika. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT)  na Youth For Africa (YOA). 

WASIFU WA MAREHEMU KAMISHNA MKUU MSTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA - ONEL E. MALISA

$
0
0
 Marehemu alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.  Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kidia mwaka 1951 – 1954 na baadae Shule ya Msingi Kidia Juu (Kidia Upper Primary School) mwaka1955 – 1958.   

Alihitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Nne mwaka 1974 katika Shule ya Sekondari Mawenzi akiwa mtahiniwa wa kujitegemea (Private Candate). Aidha, alisoma Cheti cha Sheria Chuo Kikuu cha D’Salaam mwaka 1975 – 1976 na baadaye Shahada ya Kwanza ya Sheria Chuo Kikuu cha D’Salaam mwaka 1977 – 1980. 

Marehemu ajiunga na Jeshi la Magereza mwaka 1964 baada ya kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Chuo Ukonga, D’Salaam yaliyofanyika kuanzia Januari - Julai, 1964.  Ndani ya utumishi, alipata fursa ya kuhudhuria Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili (Advance Course) Chuo Ukonga, D’Salaam kuanzia Aprili – Julai, 1967 na Mafunzo ya Uongozi wa Juu (Gazetted Course) kuanzia Februari – Mei, 1974.

Kutokana na utendaji wake wa kazi, marehemu aliwahi kutunukiwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:-

·        Afisa Magereza Daraja la Tatu mwaka 1964
·        Afisa Magereza Daraja la Pili mwaka 1965
·        Afisa Magereza Mkuu Daraja la Nne mwaka 1967
·        Afisa Magereza Mkuu Daraja la Tatu mwaka 1971
·        Mrakibu Msaidizi wa Magereza mwaka 1975
·        Mrakibu wa Magereza mwaka 1976
·        Mrakibu Mwandamizi wa Magereza mwaka 1978
·        Kamishna Msaidizi wa Magereza mwaka 1982
·        Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza mwaka 1984
·        Kamishna wa Magereza mwaka 1992
·        Kamishna Mkuu wa Magereza mwaka 1996 – 2002


Aliwahi kufanya kazi katika vituo mbalimbali vikiwemo Gereza Butimba -  Mwanza, Isanga - Dodoma, Wami Vijana - Morogoro, Chuo cha Usalama Moshi,  Gereza Songwe - Mbeya, Chuo Ukonga - D’Salaam na Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, D’Salaam.

Aidha, marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Magereza kama ifuatavyo:-

·        Mkufunzi Mkuu Chuo Ukonga mwaka 1975
·        Mkuu wa Chuo Msaidizi, Chuo Ukonga mwaka 1981
·        Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1983
·        Mkurugenzi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1984
·        Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Makao Makuu mwaka 1992
·        Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza mwaka 1996 – 2002 alipostaafu kazi.
 
Marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa utumishi wake.  Baadhi ya mambo aliyoyafanya ni kama ifuatavyo:- 

·        Alianzisha na kuimarisha mahusiano baina ya Jeshi la Magereza na Magereza ya nchi nyingine Afrika na duniani. 
·        Alikuwa mmojawapo wa Makamishna wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Nchini (Law Reform Commission)
·        Alikuwa mshauri kwenye Maboresho ya Jeshi la Magereza pamoja na Sera ya Taifa ya Magereza.
·        Kama hatua ya kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani aliweza kushauri  na kusimamia kutungwa kwa Sheria zifuatazo:-

-      Sheria ya Bodi ya Parole
-      Sheria ya Huduma kwa Jamii (Community Service)

Nishani alizotunukiwa akiwa kazini ni:-

·        Nishani ya mstari wa nyuma
·        Nishani ya Utumishi mrefu
·        Nishani ya Utumishi uliotukuka

Hata baada ya kustaafu kazi, marehemu aliendelea kutoa mchango wake kwa kushauri mambo kadhaa pamoja na kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya Jeshi na Taifa.  Kutokana na mchango wake huo alitunukiwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2015.
Kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza, tunatoa salamu nyingi za rambirambi kwa Mke, Watoto na Ndugu wa Marehemu kwa msiba huo mkubwa uliotufika.




MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMINA

KONGAMANO LA KWANZA LA WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKONI TANZANIA LAFANYIKA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Equality for  Growth (EfG), JaneMagigita akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Dar es salaam leo.
Ofisa Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar es Salaam leo. Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Japhet Makongo akizungumza na Wanawake wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo.
Wafanyabiashara wanawake Masokoni wakiwa kwenye Kongano hilo.

Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Sarah Mambea na Brenda Kharono.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo, kutoka kulia Mussa Mlawa,Susan Sitta na Munaa Abdalah.


Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (Repoa), Samwel Wangwe amewataka watanzania kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanawake kwani wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa.

Akizunguza Dar es Salaam leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kwanza la wanawake wafanyabiashara sokoni Tanzania, Wangwe alisema ni muhimu kuhakikisha wafanyabiashara hao wanawezeshwa na kuwajali katika uzalishaji na uendeshaji wa biashara zao.

Alisema kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo kutoa changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya kisera.

"Wafanyabishara wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa kutokana na uwepo wa asilimia 43 ya wajasiriamali wanawake Tanzania," alisema Wangwe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, alisema  lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wanawake wafanyabiashara walio sokoni kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwajengea mshikamano na kujadili masuala muhimu yanayowahusu katika biashara zao.

Alisema kongamano hilo limehusisha wanawake 200 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, na mkoani Tanga katika Wilaya ya Lushoto huku wakiongozwa na kauli mbiu isemayo 'Sauti ya Mwanamke Sokoni'.

Alisema kauli hiyo inalenga kumkomboa mwanamke mfanyabiashara kwa kumjengea uwezo kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia katika kuendesha shughuli biashara za shughuli za soko. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712-727062).

Mfuko wa Pensheni wa PSPF Wakabidhi Msaada kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar.

$
0
0
 
Ofisa wa Mfuko wa Pensheni PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akimkabidhi msaada wa Magogoro Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ame Perera kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya mvua na kuharibikiwa na mali zao, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngome chumbini Zanzibar.
 OFISA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akitowa maelezo kwa niaba ya Mkufugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa Magodoro kwa wananchi wa Jimbo la Chumbuni waliopata janga la mvua za masika katika shehia tatu za jimbo hilo, Chumbuni. Karakana na Muembemakumbi Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Perera Ame Silima akitowa shukrani kwa uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao kwa Wananchi wa Jimbo lake wakati wa makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngombe chumbuni Zanzibar.Mhe Mbunge akiishukuru PSPF kwa kutumia sehemu ya pato lake kwa kusaidia Jamii.
Sheha wa Shehia ya Karakana Ndg Bakari Makame akitowa shukrani kwa niaba ya wananchi wake kwa Msaada wa Magodoro yaliotolewa na Mfuko wa PSPF kwa kujali wananchi wakati wa maafa  na kutowa shukara hizo kwa Uongiozi huo wakati wa makabidhiano ya msaada huo yaliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Mabanda ya Ngome Chumbuni Zanzibar.
  WANANCHI wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya mvua hivi karibuni.
Wananchi wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya mvua hivi karibuni.

NINATAKA URAIS WA MIAKA MITANO-SITTA

$
0
0
 Mheshimiwa Sitta akisimikwa kuwa Mjukuu Mkuu wa ukoo wa Fundikira katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Unyanyembe Itetemia mkoani Tabora jana.
 Mheshimiwa Samweli Sitta akiwa na viongozi wenzake wa CCM alipokuwa akitangaza nia ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mheshimiwa Samweli Sitta akitangaza nia mbele ya umati wa wananchi katika uwanja wa Ikulu ya Unyanyembe katika manispaa ya Tabora. 

Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii, Tabora.


Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema kuwa anataka ubunge wa miaka mitano kuweza kuivusha nchi katika kutokana na mambo yanayoonekana ikiwamo muungano,udini ,ungezeko la vijana.


Sitta ameyasema hayo leo wakati akitangaza nia ya kugombea urais katika mkutano uliofanyika katika viwanja  vya Ikulu ya Chifu Fundikira Kata ya Itetemia  mkoani Tabora.


Amesema mtu  yeyote makini ana nafasi ya Urais, hana budi   kuyapima mazingira ya taifa katika miaka mitano ijayo na kuzielewa changamoto zitakazokuwepo katika kipindi cha uongozi anachokusudia kuongoza.


“Maoni yangu kipindi cha miaka mitano ijayo kina mwelekeo wa mifarakano katika  masuala ya muungano wetu; kutetereka  kwa mshikamano wetu kunatokana na chokochoko  za siasa za ushindani, udini  na  kupanuka kwa  tofauti ya kipato, ongezeko la kundi kubwa  hususani la vijana mijini  lisilo  na uhakika wa ajira na haya yote yanaashiria ongezeko la uhalifu”amesema Sitta.


Amesema anamini kutokana na  mchanganyiko wa uzoefu  wa uongozi, unamuwezesha kukusanya  nguvu chanya za Watanzania ili kuyatanzua matatizo yanayotokana na changamoto zilizopo kwa kipindi cha sasa.


Sitta amesEma kugombea nafasi ya Urais wa nchi yetu si jambo jepesi.Linahitaji tafakuri ya kina ukizingatia kuwa nafasi hiyo ya uongozi inabeba matumaini ya watanzania wote milioni 47.


Amesema Ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi  inayopunguza umaskini kwa haraka na  huku  tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya serikali kutosheleza ubora wa  huduma za jamii kama vile afya, elimu na maji, hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshaji nchi uwe ni wa motisha kwa wazalishamali. 

Mifumo ya nchi zilizopiga hatua kubwa za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii  haijatimia  hapa kwetu.


Aidha Wafanyabiashara wakubwa wa ndani hawawekezi vya kutosha ndani ya nchi kuleta maendeleo ya haraka ya huduma, viwanda,kilimo na biashara. Baadhi yao, kwa hakika baada ya kuchuma fedha wanazihamishia nje ya nchi. Matokeo yake ni kwamba uchumi haukui kufikia kiwango cha kutosheleza vipato vya wakulima na wafanyakazi na wafanya biashara.Hatuna budi kujenga muafaka na wafanyabiashara hususani wazawa wa nchi yetu. Kazi hii ina hatua mbili:



Amesema wafanyabiashara watachukuliwa hatua kwa wasio waaminifu kwa kukwepa kodi, wanaotorosha fedha za kigeni na wanaoshiriki katika rushwa kubwa na biashara za magendo,kuwepo kwa mshikamano baina ya wafanyabiashara waovu na watendaji serikali kunachochea rushwa na kudumaza uchumi. Hali hii lazima irekebishwe.

TBS NA TFDA WATAKIWA KUDHIBITI BIDHAA ZISIZO NA UBORA ILI KULINDA UCHUMI

$
0
0
 Picha na maktaba
Na Woinde Shizza,Arusha 
Mamlaka ya Chakula na dawa(TFDA) na Shirika la Viwango nchini(TBS), wameshauriwa kuwadhibiti zaidi wafanyabiashara wasio waaminini ambao wanaingia nchini bidhaa sizizo na ubora kwani wanaporomosha uchumi.

Meneja masoko wa kampuni ya  Wrigleys (EA) Company Ltd, Emanuel Laswai, alitoa kauli hiyo juzi, katika uzinduzi wa bidhaa mpya za kampuni hiyo ya Doublemint  nchini Tanzania.

Laswai alisema, uingizwaji wa bidhaa feki na zisizo na ubora zina  athari za kiuchumi na kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.

“sisi kampuni yetu kwa mwaka tunalipa kodi Tsh 120 milioni, lakini inaumiza kuona kuna bidhaa zinaingizwa nchini kinyamela bila kulipiwa kodi”alisema

Alisema bidhaa zao zote kabla ya kuingia sokono lazima ziidhinishwe na vyombo vya ukaguzi wa serikali kama TBS na TFDA.

Mkaguzi wa vyakula, dawa, vipodozi ,wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA,kanda ya kaskazini, Barnabas Jacob, akizungumzia tatizo la uingizwaji bidhaa feki alisema Mamlaka hiyo, imeendelea kudhibiti na kukamata na kutekeleza bidhaa hizo.

Jakob alisema   milango ya TFDA, iko wazi kwa kila mwananchi kutoa taarifa ya kuwepo kwa bidhaa hatarishi katika mazingira yeyote ili ziweze kuchukuliwa hatua za kudhibiti  bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

Kwa Upande wake, Afisa uhusiano wa  shirika la viwango nchini(TBS) Roida Andusamile akizungumza na Mwananchi alisema TBS itaendelea kudhibiti bidhaa zisizo na ubora kuingia nchini   kwa kuanza kudhibiti bidhaa hizo kutoka nchi zinapotoka.

Hata hivyo, alisema ni wajibu wa wananchi pia kutoa taarifa TBS wanapobaini bidhaa zisizo na ubora katika soko au ambazo bado hazijaidhinishwa na vyombo vya serikali, ili kuweza kuchukuliwa hatua mara moja ya kuwadhibiti na kuwakamata wahusika.


MAPOKEZI YA DOKTA SLAA KATAVI

$
0
0
Msafara wa pikipiki na magari mjini Katavi jana wakati wanachama, mashabiki, wapenzi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walipojitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibroad Slaa ambaye yuko kwenye ziara ya mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR, kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa wingi kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura huku pia akikagua maandalizi ya chama kwenda kushinda uchaguzi mkuu mwaka huu.


SERIKALI IWEKE KIPAUMBELE KWENYE LISHE

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Shirika lisilokua la kiserikali la ANGONET lenye makao makuu  jijini Arusha ,Petter Bayo (kulia)  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya masuala ya lishe na kuitaka serikali iweke vipaumbele katika lishe ili kutokomeza matatizo ya udumavu na utapiamlo,Katikati ni Mratibu wa Angonet ,Petro Ahham ,kushoto ni Jovitha Mlay mwanachama wa shirika hilo(habari picha na libeneke la kaskazini blog)

Serikali imetakiwa kuweka vipaumbele katika masuala ya lishe ili kutokomeza matatizo ya udumavu na utapiamlo yanayosababishwa na lishe duni hivyo kuathiri maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Katibu Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali (ANGONET) ,Petter Bayo amesema kuwa kutokana na hali mbaya ya lishe nchini na kuongezeka kwa udumavu wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano 5 hadi kufikia asilimia 42% ya watoto hao kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2012.

Bayo alisema hayo jana akizungumza na Waandishi wa habari amesema   kuwa iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa athari zitakua kubwa katika shughuli za uzalishaji kutokana na lishe duni na pia kuathiri Nyanja za elimu na sekta mbali mbali kuwa  hayo jana akizungumza na Waandishi wa habari.

“Lishe ni kiini cha maendeleo ya jamii yoyote ile na nchi yoyote ile ni vyema serikali ikatilia mkazo suala la lishe kwani ni kichocheo muhimu cha maendeleo kwa kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi hasa waishio vijijini” Alisema Bayo

Mratibu wa Angonet ,Petro Ahham alisema kuwa Serikali inapaswa kutupia macho suala la upatikanaji wa chakula na kuangalia uhaba wa chakula unaoweza kusababisha watu kufa kwa kukosa chakula.

Ahham anaeleza kuwa ukosefu wa madini chuma kwa watoto umekua ukisababisha ugonjwa wa Anemia unaowapelekea watoto kusinzia wakiwa mashuleni hata kuchangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu  kutokana na Lishe duni.

Mwanachama wa Angonet ,Jovitha Mlay anaeleza kuwa shirika hilo kwa sasa linashirikiana Umoja wa mashirika yanayojihusisha na masuala ya  lishe Tanzania (PANITA) katika kutoa elimu juu ya lishe na kufanya uhamasishaji mashuleni na katika makundi mbalimbali ya jamii husasan kwenye Kanda ya Kaskazini,mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Manyara.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA KUANZA ZIARA KESHO KUELEKEA KAGERA, GEITA ,MWANZA

$
0
0
Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza mapema leo jijini Dar na Waandishi wa habari, alieleza kuwa wataondoka jijini Dar kesho kwa basi maalumu, ambapo watasimama njiani katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na mengineyo kwa ajili ya kusalimia wananchi.
 Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisisitiza jambo zaidi kwa Waandishi wa habari, kuhusiana na ziara hiyo itakayoanza kesho.


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana anatarajia kuanza ziara ya siku 28 kesho katika mikoa mitatu ya Kagera, Geita na Mwanza kukamilisha mikoa yote 30 nchi nzima.

Ziara hizo zenye malengo ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama zimekuwa na mafanikio kwa kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakumba wananchi hasa wa mikoani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo, Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema wataondoka jijini Dar kesho asubuhi kwa basi maalumu, ambapo watasimama njiani katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na mengineyo kwa ajili ya kusalimia wananchi.

“Ziara rasmi itaanza June 4 katika Wilaya ya Nyakanazi mkoani Kagera, lakini kesho tutakunywa chai Morogoro chakula cha mchana tutakula Dodoma halafu tutasalimia wananchi katika Mikoa ya njiani kama Singida, Nzega na tumepanga kulala Kahama mkoani Shinyanga, tukiamka ziara ndio itaanza rasmi,” alisema Nape.

Aliongeza kuwa katika ziara hiyo watatembelea majimbo yote ya uchaguzi hivyo amewataka wana-CCM na wananchi wengine kujitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu katika ziara hiyo ya kihistoria.

“Hii ni ziara ya kihistoria kwa sababu ya mambo matatu, kwanza tutatembelea visiwa vyote vya Ukerewe ambavyo ni nadra kutembelewa na viongozi, pili huu ni mwaka wa uchaguzi kuna masuala mengi yanahitaji ufafanuzi,” alisema.

Akitaja ratiba ya ziara hiyo Nape alifafanua kuwa, “Kuanzia Juni 5 mpaka Juni 15 tutakuwa Mkoa wa Kagera, Juni 16 mpaka 21 tutakuwa Mkoa wa Geita na Juni 22 mapaka Julai 2 tutakuwa Mwanza kuhitimisha ziara ya nchi nzima kwa mkutano mkubwa wa kihistoria.”

Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu faida za ziara hizi Nape alisema kuna masuala mengi ya kimaendeleo yalisimama lakini alipopita Katibu Mkuu Kinana ufumbuzi umepaikana, akitolea mfano mashamba yaliyobinafsishwa bila kufuata utaratibu alisema Rais Jakaya Kikwete, amefuta hati nyingi za mashamba ya wawekezaji na kurudishwa kwa wananchi.

“Kuna baadhi ya maeneo kulikuwa na zahanati zimeshajengwa lakini hakuna vibali, nimepata taarifa kuwa vibali vimeshapatikana na huduma zinaendelea, kulikuwa na matatizo ya ardhi za wananchi kuchukuliwa na wawekezaji katika maeneo ya Tanga, Arusha, Babati na maeneo mengine lakini kila kitu kipo sawa sasa na wananchi wanamshukuru Kinana,” alisema.

Aliongeza kuwa, “Nisisitize kuwa tumesema tutaondoka na basi maalumu kwa sababu kama kuna mwingine atafanya hivyo atakuwa ametuiga, mkumbuke hili wazo la kuondoka na basi ni la Katibu Mkuu.”.
Ikiwa ziara hizi zitamalizika salama Julai 2 mwaka huu, Kinana atakuwa Katibu Mkuu pekee wa CCM tangu kuanzishwa kwake Februari 5, 1977 kuzunguka nchi nzima kuangalia uhai wa chama na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.

Article 1

$
0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba
Mamia ya Waakazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake wakiwemo na Wageni mbalimbali kutoka nje ya Mkoa huu na nje ya Nchi wamejitokeza kwa wingi kumzika marehemu Samuel Luangisa leo Jumatano juni 3, 2015 nyumbani kwake Kitendaguro nje kidogo na Mji wa Bukoba. Marehemu Samuel Luangisa ni miongoni mwa waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi(Kagera) Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.

Mbunge wa muleba kusini Prof Anna Kajumulo Tibaijuka

Wanakwaya Mbalimbali walihudhuria Mazishi hayo

Baadhi ya Viongozi wa dini(katikati) ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini
Taswira za picha enzi ya uhai wa Marehemu Mhe. Samuel LuangisaMerehemu Samwel Lwangisa alizaliwa mwaka 1932 na mauti yalimkuta New York Marekani tarehe 25.05.2015 na kuzikwa leo Jumatano juni 3, 2015 Nyumbani kwake Kitendaguro Bukoba.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini


Mwanae na Marehemu akitoa neno lake


Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mhe. Samuel Ntambala Luangisa
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Kagera Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella akiwa sambamba na Mbunge wa Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki katika Mazishi Mhe. Samwel Ntambala Lwangisa leo Nyumbani kwake KItendaguro Nje kidogo ya Mjini wa Bukoba. Picha na Faustine Ruta

Le Mutuz nae alikuwepo katika Mazishi hayo ya Mhe. Samweli Ntambala Lwangisa.

Kushoto ni Bw. Willy O. Ruta mkurugenzi wa kampuni mpya ya utalii Bukoba Tour akishuhudia Mazishi hayo.
Mzee aliyekuwa karibu na marehemu Lwangisa akitoa neno Taswira
kulia ni Bi. Rukia Kassim kiwa na Mama Mwainunu







Wengi pia walifuatilia kupitia kwenye Tv Screen zilizokuwa ukumbini kutokana na wingi wa Watu hivyo Tukio zima kuwafikia kupitia kwenye tv katika sehemu walipokuwa maeneo hayo vyema.


Sehemu ya Baadhi ya Wanaumoja











Mwili ukisitiliwa kaburini
























Wageni Mbalimbali kutoka Nje ya Nchi walijumuika


Umati uliojitokeza katika mazishi.







bukobasports.com tunaipa pole Familia ya Marehemu Mh. Samweli Ntambala Lwangisa.
Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana....Warumi 14:8

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA WA FEDHA CHA FANYIKA MJINI MOROGORO

$
0
0

1
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe (katikati) akiwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kulia) wakiwasili kwenye ufunguzi wa kikao cha baraza la wafanyakazi la Wizara wa Fedha lililofanyika leo mjini Morogoro. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile.
2
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha baraza la wafanyakazi la Wizara wa Fedha lililofanyika leo mjini Morogoro.
3
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe akiwakaribisha wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Wizara wa Fedha kwenye ufunguzi wa kikao cha kikao cha baraza hilo lililofanyika leo mjini Morogoro.
4
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya Fedha ambaye pia ni Katibu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile akitoa neno kabla ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo lililofanyika leo mjini Morogoro.
5
Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya Fedha lililofanyika leo mjini Morogoro.

Waajiri na wafanyakazi wameaswa kutumia fursa ya kukutana mara kwa mara ili kujadiliana masuala mbalimbali ya kiutendaji yanayohusu maendeleo ya watumishi, kuongeza na kuimarisha bidii na utendaji wa kazi kulingana na sheria, kanuni na taratibu na kufikia azma ya nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025. Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya alipokuwa akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi la wizara hiyo leo mjini Morogoro.
Waziri Saada alibainisha kuwa lengo la kikao cha baraza hilo lilikuwa ni pamoja na kujadili na kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2014/2015 na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Fedha kwa mwaka 2015/2016 kabla ya kupitishwa Bungeni.
“Ili kuwa na mabaraza yenye tija mahali pa kazi, mabaraza ya wafanyakazi yanawajibu wa kuimarisha ushirikishwaji wa wafanyakazi katika uendeshaji wa shughuli za taasisi na hivyo kuwa na uongozi wa pamoja” alisema Waziri Saada.
Akisisitiza kauli ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete anayoituimia mara kwa mara, Waziri Saada amesema kuwa “Hazina ni moyo wa Serikali” na kuwaasa wafanyakazi wa Wizara hiyo watumie vema rasilimali rasilimali zilizomo, zinazokusanywa na zile za wahisani na hivyo kuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine za Serikali.
Aidha, Waziri Saada amewahimiza wajumbe hao wa kikao kutoka kutoka mikoa mbalimbali nchini kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi mkuu nchini ambapo wajumbe wamekumbushwa kutumia fursa waliyonayo na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura nchini ili waweze kuchagua viongozi watakaosaidia kusukuma maendeleo mbele maendeleo ya nchi.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe alisema kuwa mkoa wa Morogoro ni salama na ni mahali pazuri pa kuishi ikizingatiwa kuwa na hali nzuri ya kiulinzi na usalama mkoa mzima.
Mkuu huyo wa mkoa Dkt. Rutengwe aliwahakikishia wajumbe wa kikao hicho kuwa mkoa huo unahali nzuri ya usafi wa mazingira ukipambwa na safu za milima ya Uluguru ambazo zinaendelea kuhifadhiwa kwa hali ya juu ili kuendelea kuwa ni kivutio cha watu wengi wa nadani na nje ya nchi kuja Morogoro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa baraza hilo liliwahusisha wakuu wa idara mbalimbali ndani ya wizara ambalo linashirikisha wafanyakazi wote katika kuandaa bajeti yao na hivyo kuwa na bajeti shirikishi.

Sitta ajiweka mbali na lawama za wivu wa uwaziri mkuu!

$
0
0
Mh Samuel Sitta akitangaza nia leo mchana Itetemia Tabora
Mheshimiwa Samuel Sitta leo hii alitangaza rasmi nia yake kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Alitangaza nia yake hiyo mbele ya mamia ya wakazi wa kata ya Itetemia, Tabora mjini na wilaya za jirani na mji wa Tabora.
Mabango nayo yalikuwepo!

Mh Sitta akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Tabora leo mchana.
Mh Magreth Sitta akisalimia wananchi wa Itetemia


1.Muungano

Toka pande zetu mbili za muungano zinatolewa kauli na pia vitendo vyenye kuashiria nchi zetu zilizomo katika muungano yaani Tanganyika na Zanzibar zitengane. Kutoka Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai kuwa Zanzibar itanufaika zaidi ikiwa nje ya muungano na kuwa na uhuru kamili kama nchi. Na kutoka bara tunasikia.


2. Mchakato wa katiba

Pamoja na kuwa na muafaka kamili kuhusu katiba mpya haujapatikana, lakini katiba inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi ambayo yanaweza kutuleta karibu ikiwa ni hatua ya awali inayotuwezesha kusonga mbele kwa amani.


Mama Magreth Sitta akiwa na Mwenekiti wa UWT Mkoa wa Tabora Mama Mchemba.
Mtemi wa Unyanyembe Mtemi Msagata Fundikira, Mh Samuel Sitta na mwenekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini
Binafsi naamini kuwa pande zinazosigana kuhusu katiba zina wazalendo ambao wanaweza kukubaliana kuwa na kipindi cha mpito cha utulivu na maelewano kitakachotuwezesha kama taifa kusonga mbele. Viongozi a kijamii na ki saisa washawishiwe kukubali hoja mbili.


3.Mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda


Ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umasiikini kwa haraka na huku tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya aserikali kutosheleza  huduma za ubora wa huduma za jamii kama vile afya , elimu na maji,hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshaji uwe ni wa motisha kwa wazalisha mali. Mifumo ya nchi zilizopiga hatua za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira  chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii haijatimia hapa kwetu.




4.Mikakati ya dhati ya kupambana na rushwa

Rushwa kubwa zimekuwa na athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi yetu. Mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hata rushwa katika ajira, vimesababisha hasara ya matrilioni ya shilingi kwa taifa. Uchumi unakosa afya kutokana na kubanwa na rushwa ambayo sasa imeenea mpaka vijijini.



5. Kuimarisha CCM kiuchumi

Chama tawala madhubuti ni nyenzo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zote kwa ufanisi zilizoahidiwa kwenye ilani. Katika hili ni wajibu wa mwenyekiti wa chama kuhakikisha kwamba vitengo na vitega uchumi vya chama vinakuwa na tija inayokiwezesha chama kuendesha shughuli zake  kwa kujitegemea badala ya kutegemea ruzuku toka serikalini. Chama tawala kinachojitegemea ki uchumi ni kinga dhidi ya rushwa kwa sababu itazuia mazoea yaliyopo ya wafanyabiashara wasio waaminifu kujijenga kwa mwanya wa kuwa ni "wafadhili" 


Mh Magreth Sitta akifuatiwa na Mussa Ntimizi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui


Magreth Sitta Kijo akiwa na mumewe Kefa Kijoh Itetemia leo

Aidha Mh Sitta akijibu swali toka kwa mwandishi wa habari aliyeuliza "Mh Sitta unasemaje juu ya shutuma za waziri mkuu aliyejiuzuru wadhfa wake kuwa wewe na Mh Mwakyembe mlikuwa na wivu naye ndio maana mkamuonea mpaka ikabidi ajiuzuru? Mh Sitta akajibu "Bwana mwandishi kwa nini swali hilo humuulizi yeye mwenyewe aseme ni kipi alichoonewa? Mchakato wa uchunguzi ulifanyika mwaka 2008 mpaka sasa ni miaka 7 hivi sasa muda wote huu alikuwa wapi hata leo aseme alionewa? Jibu ambalo lilipelekea vicheko na vigerere toka kwa wananchi walioudhuria hafla hiyo. 

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenye basi kuwasalimia wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa wa Morogoro akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera.






 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa mkoa wa Morogoro waliojitokeza kuwasalimu wakati wa safari ya kuelekea Kagera.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi waliojitokeza kwenye kituo cha mabasi mjini Morogoro maarufu kama Msamvu ambapo aliwaambia wananchi hao huu ni wakati wa kuchagua kiongozi wa kutuongoza hivyo ni vyema wananchi kupima na kuacha ushabiki.

DC ILALA, ORIJINO KOMEDI WASHIRIKI WIKI YA MAZINGIRA KATA YA KIVUKONI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akishiriki zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala jana asubuhi. Wa pili kushoto ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya  Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.
 Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (kushoto) akifanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi  kata ya Kivukoni karibu na maeneo ya Aga Khan sambamba na wafanyakazi wenzake pamoja na Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' (wa kwanza kulia) katika kuadhimisha wiki ya Mazingira.

 Wadau mbalimbali kutoka Green WastePro Ltd, Manispaa ya Ilala, Forum CC pamoja na wasanii mbalimbali wakiendelea kufanya usafi kwenye fukwe ya bahari ya Hindi kata ya Kivukoni katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira.
  Hali ilivyokuwa kabla ya kufanya usafi
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shay o(kulia) wakati wa zoezi la kusafisha fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Kushoto ni Msanii maarufu wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi, Lukac Mhavile "Joti"
  Wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd wakiendelea zoezi la usafi katika fukwe za bahari ya Hindi eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akizungumza jambo na Afisa Mazingira Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda wakati wa zoezi la kufanya usafi kwenye fukwe ya bahari ya Hindi eno la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akisitiza jambo kwa wadau walioshiriki zoezi la usafi katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Aga Khan na kuwaomba waendelee na kufanya usafi na hata kuwahamasisha watu wengine kuwa mabalozi wa mazingira ili kufikia malengo waliyojiwekea katika manispaa ya Ilala.
Baadhi ya wadau waliofika kwenye zoezi la usafi katika wiki ya Mazingira lililoendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd.

BENKI YA EXIM TANZANIA YASHIRIKI MAONYESHO YA 18 YA WIKI YA MAZIWA KWA MAFANIKIO MAKUBWA.

$
0
0
 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr, Titus Kamani, (kulia) akisalimiana na Meneja Uendeshaji na Huduma kwa wateja wa benki ya Exim Tanzania tawi la Babati mkoani Manyara Bw. John Ndyebonera ,alipotembelea kwenye banda la maonyesho la benki hiyo ambayo ilishiriki kwenye maadhimisho ya 18 ya wiki ya maziwa yaliyofanyika kitaifa wilayani Babati hivi karibuni. Wengine ni wafanyakazi pia wa benki hiyo.
 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr, Titus Kamani, (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kwenye banda la maonyesho ya benki ya Exim Tanzania tawi la Babati mkoani Manyara ambayo ilishiriki kwenye maadhimisho ya 18 ya wiki ya maziwa yaliyofanyika kitaifa wilayani Babati. Anayeshuhudia kwa karibu zaidi ni Meneja Uendeshaji na Huduma kwa wateja wa benki hiyo tawi la Babati  Bw. John Ndyebonera. Wengine pia ni wafanyakazi wa benki hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Babati mkoani Manyara wakiongozwa na Meneja Uendeshaji na Huduma kwa wateja wa benki hiyo tawi la Babati  Bw. John Ndyebonera (Wa pili kulia), kwa pamoja wakishuhudia mmoja wa washiriki wa maonyesho ya 18 ya wiki ya maziwayaliyofanyika kitaifa wilayani Babati (wa kwanza kulia) akisaini kitabu cha wageni waliotembelea banda la maonyesho ya benki hiyo ambayo pia ilishiriki maonyesho hayo kwa mafanikio makubwa. 

MBUNGE JOSHUA NASSAR ASHIRIKI UJENZI WA CHANZO CHA MAJI KIJIJI CHA KARANGAI KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI.

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akishirikiana na wananchi katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar aiwa amepanda kwenye Lori lililokuwalikibeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji kwa ajili ya kumwagilia katika kijiji cha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo.
Mbunge Nassar akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza na mmoja a wanakiji cha Karangai huku akiwa amembea mtoto muda mfupi baada ya kumaliza hatua za awali za uwekaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza na baadhi ya kina mama ambao mingoni mwao wanajishughulisha na shughuli za kilimo alipotembelea kijiji cha Karangai kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya umagiliaji katika kijiji hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.



MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar jana ameungana na mamia ya wananchi katika kijijicha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo kufanya shughuli za awali za ujenzi wa chanzo kipya cha Maji kwa ajili ya umwagiliaji.


Zoezi hilo lilo anza majira ya saa 3 asubuhi na kumalizika majira ya saa 12 jioni ilishuhudiwa Mbunge Nassar akishiriki kazi za mikono ikiwemo kubeba mawe na kuayapanga katika eneo la mto kwa ajili ya ujenzi wa chanzo hicho.

Akizungumza katika eneo hilo ,Nassar alisema lengo la ujenzi wa chanzo hicho kipya ni harakati za kuokoa mazao kwa baadhi ya mashjamba ambayo yameanza kukauka kutokana na kukosekana kwa maji ya kutoshja.
“Nilijitolea kulipia malori matatu kwa siku nzima kufanya kazi hii na ununuzi wa nyaya maalum (chain link) kwa ajili ya kufungia/kujengea Mawe kwenye eneo ambalo chanzo cha maji haya kinaanzia lakini pia kwa sababu ilikuwa ni kazi ya kutwa nzima tulihakikisha hakuna anayeondoka katika eneo hili hivyo tuliamua kuchinja mbuzi ,tukapika ugali  na kazi ikaendelea”alisema Nassar.

Nassar aliwashukuru ijana zaidi ya 300 pamoja na kina mama waliofika katika zoezi hilo kwa lengo la kuendelea kumtia moyo.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA UKUMBI WA CHAKULA ULIOFADHILIWA NA TANAPA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akihutubia wananchi waliofika katika hafla fupi ya makabidhiano ya ukumbi wa chakula uliojengwa katika shule ya Sekondari Olele Wilayani Rombo kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro ,Leonidas Gama akikagua jengo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na Mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakifurahia nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanafunzi wa shule ya  sekondari ya Olele wakati alipofika kwa ajili ya uzinduizi na makabidhiano rasmi ya ukumbi wa chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Rombo mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari Olele iliyopo kata ya Olele kwa ajili ya kukabidhi Mradi wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa , Tanzania (TANAPA).
RC ,Gamana viongozi wengine wakiskiliza nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na kwaya ya shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Kutokana na hali ya mvua iliyokuwepo wakati wa makabidhiano ya ukumbi wa chakula,mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama alilazimika kubadili meza kuu na wao wakaa eneo ambalo pia lilikuwa na mvua huku akisema ni vyema mvua ikawanyeshea wote pamoja na wananchi.
Jengo la Ukumbi wa Chakula lililojengwa kwa ufadhili wa Shirika la  Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Meneja Ujirani Mwema kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ahmed Mbugi akitoa taarifa kuhusiana na ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Olele. 
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania,TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mradi wa ujirani mwema wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
RC,Gama na DC,Kipuyo wakilowa kutokana na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Wanafunzi katika shule ya sekondari Olele wakifuatilia hotuba ya viongozi waliofika shuleni hapo kwa ajili ya makabidhiano ya ukumbi wa chakula uliojengwa na TANAPA.
Mkuu wa wilaya ya Rombo ,Lembris Kipuyo akizungumza katika hafla hiyo.
Wakazi wa kata ya Olele.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

TAASISI YA WOINSO KUZINDUA FILAMU YA MAADILI KWA WATOTO JUNI 6 MWAKA HUU.

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ndani ya Taasisi ya wanawake katika jamii(WOINSO),Juliana Madeleke akizungumza kuhusiana na siku ya uzinduzi wa filamu ya "THAMANI YETU LEO" filamu inayoelezea changamoto mbalimbali ambazo zinafanya watoto wasifikie malengo yao katika jamii,katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Milenium Tower jijini Dar es Salaam leo,kushoto ni Mjumbe wa Maendeleo ya  Bodi ndani ya Taasisi ya wanawake katika jamii(WOINSO),Zenais Mtebe.Filamu hiyo itakayozinduliwa katika ukumbi wa mikutano wa Milenium Tower Juni 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam, Mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo ni Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Afya ya uzazi na Maendeleo hapa nchini(UMATI)lulu Ng'wanakilala.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ndani ya Taasisi ya wanawake katika jamii(WOINSO),Juliana Madeleke  katika mkutano ambao ulikuwa ukielezea mambo mbalimbali yanayowakabili watoto katika jamii na kuhusiana na uzinduzi wa Filamu ya "THAMANI YETU LEO" itakayozinduliwa Juni 6 mwaka huu.(PICHA NA EMMENUEL MASSAKA.)
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images