Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 544 | 545 | (Page 546) | 547 | 548 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Climate refugees in a temporary camp
  SOMETIMES it is very difficult to believe that in a free country like Tanzania, can have Refugees. May be it is sound very difficult. But let’s define Refugee according to the Oxford dictionary, “A person who has been forced to leave their country in order to escape war, persecution, or natural disaster”. Here we can find those factors lead to Refugees, then you will agree with me sometimes people can leave their homes even due to particular factors to find another home or remain homeless. One among the factors can be a natural cause in which most of phenomenons are due to climate Change and here we get Climate Refugees.
  Climate Refugees are those people who leave their homes due to climate change impacts or in simple words we can say are people who must leave their homes and communities because of the effects of climate change and global warming. I could not talk about others; I am confidently talking about my country Tanzania no matter how some people might think that, it is not necessary to talk about this. Regard once George Carlin said that “Those who dance are considered insane by those who cannot hear the music.”
  In Tanzania people have been much affected by climate change due to Floods that happening in different regions of Tanzania. Let’s talk about what happened December 2011, where Tanzania was very much affected by heavy rainfall for the first time since its independence 1961. It was reported about sixty seven thousand (67,000) people became homeless in Kilimanjaro, Arusha and Mbeya regions while in Dar es salaam about fifty thousand (50,000) people were affected.
  In March 2015 Tanzania also has faced a same challenge of Climate change through the floods that affected the coastal area of Lake Victoria and it was reported that about three thousand and five hundred (3,500) people were affected. It has been reported that most families became Homeless after floods that has been occurred in Tanzania. Mostly in Mwanza, Dar es salaam, Mbeya, Arusha and Kilimanjaro regions. Hence people became homeless and those people subjected as Climate refugees.
  Climate refugees in a temporary camp
  Climate refugees in a temporary camp
  Then there is no need to have those refugees regarding this is a free country. Then a government should work on those promises like to give a special place for those who are living in Areas that can be easily affected by climate change especially floods. It is true that our government have already prepare a special place for them but it has to improve the social services to those areas because it seems that is a big challenge for those places.
  As the year of Paris conference, UNFCCC COP 21 at France then all countries has to make sure that they participate active to make sure that they fight the climate change because it affects the whole planet. I believe that we can make it because climate change is real. Let’s echo the Bill Gates when he was saying “The climate change is terrible problem and it is absolute needs to be solved. It deserve to be a huge priority” that is one among a big quote that can be used to insist the United Nation.
  This is just a summary of what have been happen in Tanzania, and I know every where has been affected by climate change but let me remind you, if we cannot save a living Planet then we will never manage in dead planet like Mars”

  0 0

  ????????????????????????????????????
  Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini (Kushoto) akijadiliana jambo na Mtaalam mwelekezi kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh (Kulia) kwenye mafunzo yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodini nchini  yaliyofanyika  mjini Bagamoyo mkoani  Pwani.
  ????????????????????????????????????
  Sehemu ya washiriki wa mafunzo yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodini nchini  yaliyofanyika  mjini Bagamoyo mkoani Pwani  wakishiriki katika zoezi la kuandaa mpango wa mazingira kwa vitendo katika mafunzo hayo.

  ……………………………………..
  Na Greyson Mwase, Bagamoyo
  Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka nchini India (Centre for Science and Environment) kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini, imekamilisha mafunzo ya siku nne yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodi nchini ambapo wakaguzi walijifunza jinsi ya kuandaa miongozo mbalimbali kwa ajili ya kutumika kwenye ukaguzi wa mazingira kwenye migodi.
  Akizungumza katika mahojiano maalum wakati wa mafunzo hayo, Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje alisema lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa uelewa wakaguzi wa mazingira na migodi nchini wa kuandaa, kuchambua na kupitia taarifa za athari kwenye mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini. 
  Mhadisi Samaje alisema kuwa uelewa huu utawapa uwezo wakaguzi wa migodi kuchangia kikamilifu taarifa za athari kwa mazingira zinazowasilishwa na wawekezaji katika sekta ya madini kupitia Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC).
  Mhandisi Samaje ambaye pia ni Mkaguzi Mkuu wa Migodi aliendelea kusema kuwa mbali na kuwapa wakaguzi wa migodi uelewa wa kupitia taarifa za athari kwenye mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini nchini, mafunzo hayo yanawapa uwezo zaidi wa kukagua shughuli za utunzaji wa mazingira katika migodi kwa kuzingatia masharti ya mpango wa utunzaji wa mazingira ili kuhakikisha kuwa mazingira yanatunzwa ipasavyo.
  Alisema nchi ya Tanzania inahitaji miongozo mbalimbali iliyo bora katika usimamizi wa mazingira, na kusisitiza kuwa ili kukidhi haja hiyo, Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikiandaa mafunzo yanayohusiana na ukaguzi wa mazingira kwenye migodi ili kuhakikisha kuwa uchimbaji madini unakuwa ni salama.
  “ Kama Serikali tunataka kuhakikisha kuwa mbali na wachimbaji madini nchini kunufaika na kipato kutokana na shughuli za uchimbaji madini, tunataka wafanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa mazingira,” alisema Mhandisi Samaje.
  Alisisitiza kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine nchini katika kuhakikisha kuwa mazingira hususan kwenye maeneo ya migodi yanatunzwa ipasavyo.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo, walisema mafunzo hayo yaliwapa uelewa mpana katika usimamizi na ukaguzi wa mazingira kwenye migodi.
  Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Mhandisi Migodi Jones Mushi kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini alisema kuwa mafunzo hayo yamewawezesha kujifunza jinsi ya uandaaji wa taarifa za mazingira, pamoja na vigezo vinavyotumika katika kuchambua taarifa za mazingira.
  Mhandisi Mushi alisema mafunzo hayo yamewawezesha kufanya kazi kwa kujiamini kutokana na uzoefu walioupata kutoka nchi ya India ambao utawawezesha kuboresha utendaji kazi wao.
  Naye Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Cuthbert Cyprian aliongeza kuwa mbali na kujifunza uandaaji wa miongozo mbalimbali katika ukaguzi wa mazingira kweye migodi, wamejifunza namna ya uandaaji wa hadidu za rejea kwa ajili ya kuandaa tathmini ya athari za mazingira
  Mhandisi Cyprian alisema mafunzo hayo yaliwawezesha kujifunza jinsi ya kukabiliana na athari za mazingira kwenye migodi pamoja na ulipaji fidia kwa waathirika pindi migodi mipya inapoanzishwa.
  “Zoezi la ulipaji fidia lina changamoto zake, lakini uzoefu tulioupata kutoka nchi ya India kupitia mafunzo haya ninaamini utatuwezesha sisi kama wataalam kuboresha maeneo yenye kuhitaji maboresho ili kumaliza changamoto hizo,” alisema Cyprian.
  Cyprian aliiomba Serikali kuendelea kutoa mafuzo zaidi katika ukaguzi wa mazingira kwenye migodi pamoja na uboreshaji wa sheria na kanuni za mazingira ili kuhakikisha kuwa wachimbaji madini wanafanya shughuli zao katika mazingira ambayo ni bora na salama.
  Naye Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Fadhili Kitivai alisema kuwa mafunzo hayo yaliwawezesha kujifunza mikakati mbalimbali ya utunzaji wa mazingira hasa baada ya shughuli za madini kumalizika.
  Alisema mara nyingi baada ya shughuli za uchimbaji madini kumalizika nchini, migodi mingi imekuwa ikijitahidi kurudisha maeneo yake katika uasilia wake na kusisitiza kuwa kupitia mafunzo hayo, walijifunza mbinu mbadala za kuendeleza maeneo yaliyoachwa na migodi.

  0 0

  Mratibu wa Dhow race Omary Mdogwa akizungumza mbele ya waandhi wa habari hawapo pichani kuhusiana na mashindani ya Resi za Ngalawa yatakayofanyika Juni 6 mwaka huu,katika fukwe za Bagamoyo katika hoteli ya Millenium na kwa Dar es Saaam yatafanyika katika fukwe za Msasani bichi.Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza wa kutoka Bagamoyo na Dar es Salaam atapelekwa Zanzibar Juni 19 mwaka huu  kwaajili kufanya mashindano ya Majahazi mengine 10.  

  Mratibu wa kitengo cha Matangazo wa Dhow race, Issam Ramadhani Mussa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na mashindano ya Res za Ngalawa katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.(PICHA NA EMMENUEL MASSAKA.)

  0 0

   Afisa ustawi wa jamii  jiji la Arusha Saumu kweka akiwa anaongea  katika mkutano huo

  Na Woinde Shizza,Arusha
  Wito umetolewa kwa wazazi kutumia mda mwingi kukaa na watoto wao ili 
  kuwaepusha na vishawishi mbalimbali ambavyo wanaweza kuvipata.


  Hayo yamebainishwa na  Afisa ustawi wa jamii wa jiji la Arusha Saumu

  kweka wakati akiongea na wazazi ,walimu  na wanafunzi juu ya adhari
  zinazoweza kumapata mtoto wakati kipiondi ambacho autaweza kuwa nae.


  Alisema kuwa kumtelekeza mtoto kunaweza kusababishia vitu vingi

  vikiwemo mimba za utotoni kwa upande wa watoto wa kiume kulawitiwa
  pamoja na kujifunza tabia chafu ambazo zinamuharibu mtoto huyo.


  Alisema kuwa kumekuwa nawazazi wengi wamekuwa  wanafanya wafanyakazi wa ndani kama walezi hali ambayo inapelekea watoto kujifunza tabia chafu kwani wasichana wengi wamekuwa hawawafatilii watoto vizuri kama jinsi mzazi ungekuwa unamfatilia.


  “unakuta kipindi hichi wazazi wengi wanajidai wapo bize kutafuta hela

  hawezi ata kumuangalia mtoto  hawezi kufatilia mwenendo ya mtoto kitu
  ambacho mtoto inafikia mahali anafanya kitu anachokitaka  na hii
  inapelekea kwa mfano mtoto wa kike umemuacha umfatiliii wewe uko
  kazini umemuacha na mfanyakazi w akiume anaweza kumfanya chochote au
  pia mtoto unamuacha anazurura anaweza kukutana na wababa huko
  akawadanganya na vichipsi mayai akaenda na mtoto sababu ukai na mtoto
  ukampa maitaji anayoyataka sasa akienda kupew achipsi uko utajua
  mwishowe ndio unaletea mimba nyumbani saa nyingine watoto wa kiume
  ndio wanakuw amashoga”alisema saumu.


  Aidha aliwataka wazazi ambao ni wakali kupunguza ukali kwa watoto wao

  ili iwapo mtoto atafanyiwa kitu chochote au atakubwa na kitu chochote
  iwe rahisi kumuelezea mzazi kwani kuna wazazi wengine wanakuwa wakali
  mpaka watoto wanashindwa kuwaeleza matatizo ambayo wanayo.

  Kwa upande mwalimu mmoja wapo aliyejitambulisha kwa jina la Gwantu

  Mwakabungu aliwaomba wazazi wenyehela kupunguza kuwapa fedha nyingi.

  watoto wao kwani kitendo cha kuwapa fedha nyingi watoto wao
  kinawapelekea waatoto kuwa na zarau hata kwa walimu wao kutokana na
  fedha walizo nazo.

  Aidha aliiomba serekali kuunda sheria ambayo itazuia wanafunzi kuwa na
  simu mashuleni na hata manyumbani kwani kwa kufanya hivyo itasaidia
  kupunguza mmonyoko wa maadili kwani simu nyingi zimekuwa zikiwapotosha
  wanafunzi wengi.

  0 0

   Meneja Masoko wa Huwawei Bi Lydia Wangari, akionyesha kwa

  waandishi wa habari (hawapo pichani) simu aina ya Huwawei Met 7 ambayo
  zitauzwa katika Airtel Bazaar linalofanyika mlimani City ijumaa,

  jumamosi, na jumapili hii ikiwa na ofa ya simu ya bure aina ya
  'Huwawei Kishkwambi' iliyoshikiliwa na Meneja Masoko wa Airtel Bi
  Aneth Muga. Pia simu hiyo itaunganishwa na ofa kabambe ya kifurushi cha Airtel papo hapo.

   Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanahabari 
  (hawapo pichani) simu ya kisasa ya Airtel Red itakayopatikana kwa

  gharama nafuu katika Airtel Bazaar litakalofanyika wiki hii ijumaa,
  jumamosi, na jumapili hii pale mlimani City kwa gharama nafuu huku
  ikiwa imeunganishwa na kifurushi cha Airtel bure. Anaetazama ni Meneja
  Masoko wa Huwawei Bi Lydia Wangari.

  Meneja masoko wa Huwawei Bi Lydia Wangari akionyesha kati

  ya simu mbili zitakazouzwa na ofa ya 'Pata Moja BURE' siku ya ijumaa,

  jumamosi, na jumapili hii wakati wa Airtel Bazaar litakalofanyika pale
  Mlimani City wiki hii. Airtel Bazaar litawawezesha wateja wa Airtel
  kujinunulia simu kwa gharama nafuu huku zikiwa zimeunganishwa
  kifurushi cha ofa kambambe kwenye mtandao wa Airtel.
   * Ofa kabambe ya simu za Smart phone  kutoka Huawei zikiwa

  zimeunganishwa na Airtel.   *Simu kuuzwa bei poa zikiwa na ofa za vifurushi kabambe kutoka Airtel


  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ikishiriakiana na Huawei
   leo imetangaza kuanza Bazaar lake maalum litakalowawezeha watanzania
  kujipatia simu za kisasa za Smart phone na kuweza kufurahia huduma za
  zote za intaneti kupitia mtandao wa Airtel

  Bazaar la Airtel na Huawei  limepangwa kufanyika kuanzia ijumaa,
  jumamosi na jumapili hii kuanzia saa 3asubuhu hadi saa moja usiku
  katika eneo la ndani la Mlimani City  na litakuwa na muendelezo
  hapohapo na baadae litazunguka katika maeneo mbalimbali nchini.

  Akizungumzia Bazaar hilo Meneja masoko wa Airtel Bi Aneth Muga amesema
  "Bazaar letu litakuwa la kijanja zaidi kwani simu za smart phone
  zitakazouzwa ni bora na zitaambatana na ofa kabambe kuliko zote
  zinazopatikana sehemu yoyote".

  "Mteja wetu uliopo mahali popote tembelea BAZAAR la Airtel ujinyakulie
  simu bora na kisasa kama zile za Huawei au Airtel Red kwa punguzo
  kabambe zikiwa na  kifurushi cha intaneti kitakachokupa MB 120, SMS
  120 pamoja na muda wa maongezi 120 ofa ambapo huwezi kuipata popote
  zaidi ya kweye Airtel Bazaar" alisema Muga

  Meneja masoko kutoka Huawei Lyidia Wangari aliongeza kuwa licha ya
  simu za Smart phone za Huawei kuuzwa kwa gharama nafuu pia atakaenunua
  simu pale atajipatia simu nyingine ya bure au zawadi tofauti tofauti
  papo hapo kwa mfano "mteja yeyote kati ya 300 wa kwanza kununua simu
  ya Huwawei aina ya Met 7 DUAL atapata simu aina ya Kishkwambi bure
  kabisa na atakaenunua simu ya Huawei Met 7 atapata simu ya bure aina
  ya Y220 pale pale" alifafanua

  Kwa Upande wake Afisa Airte l wa kitengo cha Smartphone Bw, James
  Kagashe alisema "tunataka kudhihirisha kwa wateja wetu kuwa Airtel
  ndio mtandao sahihi kwa Smartphone yako popote ulipo,   nakuhakikishia
  kuwa kila simu inayouzwa katika Artel Bazaar inakuja na ofa kabambe ya
  kifurushi cha SMS, dakika za muda wa maongezi pamoja na intanet
  itakayokuwezesha kuperuzi upendavyo"

  Nawahamasisha wale wote mnaotaka kuenda na wakati kwa kumiliki simu
  bora na kuunganishwa na mtandao bora kwa Smartphone yako tembelea
  Airtel Bazaar la Airtel Mlimani City  ili tukuunganishe. Alimaliza kwa
  kusema Bw Mwanda.

  0 0

  mwenyekiti wa baraza la watoto wilaya ya Arusha Hassani Omary akizungumza wakati wa kongamano la  watoto ,walimu ,wazazi lililoandaliwa na shirikala intiative for youth (INFOY) kongamano lililofanyika ndani ya shule ya msingi ya uhuru jijini hapa

   baadhi ya wanafunzi ,wazazi na walimu waliouthuria katika kongamano hilo
  Mmoja wa mwanafunzi aliyeuthuria akieleza mathara ya mimba za utotoni

  Afisa ustawi wa jamii wa jiji la  Arusha Saum Kweka akichangia mada

  Na Woinde shizza,Arusha.

   Serekali  imetakiwa kuangalia upya sheria ya  mtoto ya mwaka 1971 
  kwani ndio  imebainika kuwa ndio chanzo kimoja wapo kinachoruhusu na

  kungangia ndoa za utotoni pamoja na mimba za utotoni.

  Akizungumza wakati  katika wa kongamano lililoandaliwa na shirika la

  intiative for youth (INFOY  )  mwenyekiti wa baraza la watoto wilaya
  ya Arusha Hassani Omary alisema kuwa ni wajibu wa serekali kuangalia
  upya sherika hii kwani sheria hii imekuwa ikiwaadhiri watoto wengi
  hapa nchini.


  Alisema kuwa sheria hii imekuwa ikiruhusu watoto hata wenye umri chini

  ya miaka 18 kuolewa  iwapo tu wazazi wake watakapo kubali kitu ambacho
  kinawaathiri watoto wengi katika masomo yao kwani wamekuwa
  wanakatishwa masomo yao  na  iwapo akitokea mtu mmoja kupeleka lala
  miko lake katika vyombo vya sheria amekuwa akishindwa kutokana na
  sheria hii inaruhusu mtoto huyo ata awe mdogo kuolewa mradi tu familia
  yake iwe imeafiki.


  Aidha aliongeza  kuwa  mbali na sheria hii pia serekali ikinatakiwa

  kutilia  mkazo sana katika mila mbalimbali na desturi zetu kwani mila
  zingine zimekuwa zikichangia pia kwa kiasia kikubwa watoto wadogo
  haswa wakike kukosa haki zao za msingi kwa kuwalazimisha kuolewa iwapo
  tu viongozi wa mila zao wakitaka huku akitolea mfano kwa kwa kabala la
  kimasai ambalo linaishi hapa Arusha na kudai kuwa wamekuwa wakisimamia
  na kulazimisha watoto wao kuolewa pindi tu pale atakapo kuwa amevunja
  ungo tu au pale atakapo uonekana amekuwa kidogo.


   Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa  kulinda  na kutetea haya ya

  sheria ya mtoto Laurent Sabuni alisema kuwa ni wajibu wa serekali
  kutaangalia kwa makini sheria hii kwani imekuwa ikiweaathiri watoto
  kwa kiasi kikubwa  kwa kuwakosesha haki zao .


  Alisema kuwa  kumekuwepo na matatizo  ya watoto wadogo kupata mimba zautotoni kutokana na pale wanapopeleka mashitaka katika vyombo vya
  sheria  ,sheria hii imekuwa ikiwatetea wahalifu  hali ambayo imekuwa
  ikiwapelekea watoto kukata hata tamaa ya kwenda kushitaki katika
  vyombo vya sheria.


  Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii  manispaa ya Arusha Saum Kweka

  alisema kuwa  katika kipindi hichi ni wajibu wakila mzazi kuhakikisha
  anamlinda mtoto wake anampa elimu mtoto wake kuhusiana na mimba za
  utotoni .

  Alisema kuwa kumekuwepo na watoto wengi wanapewa mimba wakiwa wadago 
  lakini kutokana na kutopata ushauri kutoelimishwa kutokaa karibu na
  wazazi wao hivyo ni wajibu wa kila mzazi kuahakikisha anamuelimisha
  mtoto wake kuhusiana na mazingira yanayomzunguka.


  Aidha saum alisema kuwa ni wajibu wa kila mzazi kutambua kuwa

  kumuozesha mtoto mdogo ni hatari na pia ni ukiukwaji wa sheria ,pia ni
  kumkosesha haki za msingi mtoto hivyo ni wajibu wa kila mzazi kupiga
  vita vikali  ndoa za utotoni pamoja na mimba za utotoni huku akigusia
  kwa kusema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni tokomeza mimba na ndoa za
  utotoni sote kwa pamoja tunaweza.

  0 0


  Mshauri mkuu wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA, Gerard Govaeas akizungumza na baadhi ya waandihsi wa habari katika Ukumbi wa mikutano katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam leo\, Kushoto ni Mkuu wa Hati Miliki wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA,Asnath Heriel na kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa RIGHT HERE TANZANIA Jenny Woodier.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhurika katika mkutano wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA mkutano uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam leo.

  Kampuni ya matangazo ya FLAMETREE iliyojikita Africa mashariki sasa imezinduliwa upya na kupewa jina jipya la RIGHT HERE TANZANIA, mabadiliko haya yametokana na kuingia kwa mwekezaji mpya wa kimataifa ambaye ameonyesha nia ya dhati ya kuwekeza kwenye kampuni hii kufuatia utendaji mzuri aliouona kwenye kampuni hiyo na kuamua kuongeza nguvu zaidi katika kuinua utendaji, uwekezaji huu unatarajiwa kuongeza tija na muamko wa wafanyakazi na wateja wao. Kufuatia mabadiliko haya sasa kampuni ya RIGHT HERE itaweza kuhudumia wateja wake kwa viwango vya juu zaidi huku idadi ya wabunifu na vitendea kazi vikiongezwa.

  RIGHT HERE imechaguliwa kuwa mwakilishi kwa Tanzania wa kampuni kubwa ya matan- gazo ya PUBLICIS ambayo ni moja kati ya makampuni makubwa manne duniani kama WPP, Interpublic na Omnicom.

  Akizindua jina hilo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwekezaji huyo Bwana Gerald Govaerts amesema, “nia na madhumini ya uzinduzi huu ni kuitambulisha kampuni hii kwa upya kwa watanzania, licha ya kuwapo hapa nchini kwa zaidi ya miaka mitatu.

  Gerald aliendelea kusema “soko la Tanzania kwa sasa linakua kwa kasi na sekta ya ushirikiano inazidi kukua kwa viwango vya juu, hivyo umuhimu wa kutangaza masoko na bidhaa zinazozalishwa ni mkubwa mno, kwa kufanya hivi tunatoa nafasi kwa makampuni mengine kutambua uwepo wetu hapa Tanzania na Afrika mashariki na wao kuweza kuzitambua kazi tunazozifanya. 

  ”Kufuatia uwekezaji huu mpya na ubia kwa kampuni ya kimataifa, nia kubwa ni kukuza sekta ya masoko kwa Afrika mashariki huku tukifanya kazi kwenye viwango vya kimataifa. Tunayofuraha kubwa kwa uwekezaji huu kwani utaongeza tija kwa watanzania wenye vipaji.

  Kampuni ya RIGHT HERE inatoa huduma mbalimbali kama kuandaa matangazo ya biashara kwa niaba ya wateja, kununua nafasi za matangazo kwenye vyomba vya habari,kuandaa mikakati ya jinsi ya kukuza bidhaa yako, kuwatangazia wateja bidhaa zao kwenye mitandao mbalimbali na kuwashauri hali halisi ya masoko na ushindani ilivyo duniani kwa sasa.

  “Ni furaha kubwa kuitambulisha kwenu kampuni ya RIGHT HERE” alisema Bi Jenny Woodier, meneja mkuu wa RIGHT HERE Tanzania, huku tukijivunia timu yenye wafanyakazi bora na kazi nzuri ambazo tumeshazifanya mpaka sasa kwa wateja wetu,licha ya kuandaa kazi nzuri zilizoendana na soko la wateja wetu lakini pia tumeonekana kimataifa na kupata nafasi ya kuwa wawakilishi wa kampuni kubwa yenye nia ya kuwekeza hapa Tanzania kwa hapo baadaye. Ubia huu na kampuni ya Publicis Africa Group utakuwa na manufaa makubwa kwa wateja wetu na kutuwezesha sisi kama RIGHT HERE kupanua wigo wetu wa kufanya kazi kimataifa.

  Dhamira yetu ni kuona ushindani wa matangazo ya bidhaa kwa Tanzania unakua na kufikia viwango vya kimataifa. Mpaka sasa tumeweza kushinda tuzo mbali mbali za kimataifa.

  Bi Jenny aliendeela kusema “ Kama kampuni tumefanya kazi hapa Tanzania kwa miaka mitatu na makampuni ya ndani na nje ya Tanzania ikiwamo makampuni ya simu, benki, taasisi zisizo za kiserikali,kampuni za samani za ndani, kampuni za sola na nyingine nyingi. Kwa miaka hiyo michache ya kufanya kazi kwa bidii na kutambulika kimataifa,kampuni ya RIGHT HERE sasa inasababu ya kujivunia ujuzi wa kufanya kazi za wazawa huku tukizifanya kwa viwango vya kimataifa. Kama wadau wa matangazo tunaamini ubunifu bora unaleta ushindani katika soko na kuweza kuifikisha bidhaa kwenye viwango vya kimataifa.

  KUHUSU KAMPUNI YA RIGHT HERE.
  Jina la RIGHT HERE linatoa maana halisi ya jinsi sisi tunavyofanya kazi kwa kuangalia walengwa wanataka nini na kufahamu umuhimu wao, lakini pia kama unatafuta mdau mwenye ujuzi na mwenye viwango vya kimataifa, watanzania wenye ubunifu na wanaoendana na hali ya soko, suluhisho pekee ni “RIGHT HERE”

  0 0

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzomna Spika wa Bunge la nchi ya Finland Mhe Maria Lohela siku alipotembelea bunge la nchi hiyo.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya mchoro kutoka kwa Msanii wa Kimataifa wa Kitanzania aishiye Sweden Bw. Charles Njau alipomutana na  Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mtaalamu wa kimataifa wa mambo ya mapishi aishiye Sweden Chef Issa Kipande ambaye mwaka jana alikuwa katika tiu ya taifa ya Sweden kwenye mashindano ya kombe la dunia la mapishi walikoibuka na medali ya dhahabu. Chef Issa, ambaye pia anaedeesha hoteli Mtwara, hivi karibuni amefungua mgahawa mkubwa mkubwa kuliko yote wa Ki Afrika katika Ulaya yote mjini Trolhattan, nje kidogo ya jiji la Stockholm, wenye uwezo wa kuchukua watu 400 kwa wakati mmoja
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa jumuiya ya watanzania waishio nchii Sweden jijini Helsinki

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa 16 wa Sweden katika kasri la Mfalme jijini Stockholm, Sweden

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa SIDA Bw. Torbjorn Petterson makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyakazi wa SIDA  katika makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mahojiano na wanahabari jijini Helsinki, Finland.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonganisha glasi na Mari Kiviniemi, Waziri wa Masuala ya Nje wa Finland wakati wa dhifa iliyoandaliwa kwa hashima yake jijini Helsinki
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mabalozi wa sasa na wa zamani waliopata kuiwakilisha Finland nchini Tanzania
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania waishio Finlan
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyabiashara wa Finland pamoja na washirika wao wa Tanzania baada ya mkutano wao jijini Helsinki, Finland
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo alipotembelea kiwanda cha METSO cha  kutengenezea vipuli vya mitambo ya gesi na mafuta katika jiji la Helsinki, Finland.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika wa Bunge la Sweden Mhe Urban Ahlin alipotembelea Bunge la nchi hiyo jijini Stockholm.

  0 0

                             Othman Khamis Ame,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
  Maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Jamii katika kijiji cha Kiwengwa Kiliomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “ B “ yanaendelea vyema katika hatua za mwisho zitakazoiwezesha skuli hiyo kuanza kuchukuwa wanafunzi wa Elimu ya maandalizi kuanzia mwezi Januari Mwaka ujao wa 2016.

  Ujenzi wa skuli hiyo uliohusisha pia vyoo na Tangi la Kuhifadhia maji ambavyo vinajengwa kwa kutumia Taaluma ya Chupa za Maji  zilizotiwa mchanga unafadhiliwa na Mradi wa Kimataifa wa Give kutoka Nchini Marekani.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Skuli hiyo Bwana Tahir Ali alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyepeta fursa ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo kwamba Kamati hiyo kwa kushirikiana na Wananchi kupitia ushauri wa Wizara husika ya Elimu wanatarajia kuanza usomeshaji mapema mwakani kwa hatua ya watoto wa maandalizi.

  Bwana Tahir alisema juhudi za Wanakijiji kwa kuungwa Mkono na Shirika la Kimataifa la Give la Marekani zimelenga kuwakomboa Watoto wa Kijiji hicho ambao kwa muda mrefu walikuwa wakikosa fursa muhimu za kielimu.

  Naye Meneja Mpya wa Mradi wa Kimataifa wa Give kutoka Marekani Bwana Joshi Winter alisema Uongozi wa Mradi huo umejipanga vyema katika kuhakikisha ujenzi wa Skuli hiyo unakamilika vizuri na kutoa fursa kwa watoto wa Kijiji hicho kupata Elimu.

  Meneja wa Mradi huo wa Give ameuomba Uongozi wa Kijiji hicho kwa kushirikiana na Serikali Kuu kuandaa mazingira ya kupata eneo kubwa zaidi kwa ajili ya matayarisho ya ujenzi wa Majengo ya Sekondari katika Skuli hiyo ya Jamii Kiwengwa ambapo Taasisi yake itakuwa tayari kusaidia ufadhili.

  Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Taasisi hiyo ya Kimataifa inafaa kupongezwa na wapenda Elimu hapa Nchini kutokana na hatua yake ya kuunga mkono makundi ya jamii katika kujikomboa kielimu.

  Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi za taasisi na mashirika ya maendeleo ndani na nje ya nchi yaliyojitolea kusaidia Wananchi hasa wanaoishi katika mazingira magumu ya kimaisha ambayo huwa kikwazo cha kupata elimu.

  Taaluma ya matumizi ya chupa za Maji zinazotiwa mchanga iliyobuniwa Nchini Nicaragua Amerika Ya Kusini katika ujenzi wa majengo mbali mbali ya makazi na huduma za Kijamii inatumika kwa lengo la kutunza  mazingira.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akikagua maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya Jamii katika Kijiji cha Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Skuli hiyo Bwana Tahir Ali, Kulia yake Balozi Seif  ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi ambapo nyuma yao ni jengo la Vyoo lililojengwa kwa kutumia chupa za maji zilizotiwa mchanga.
   Balozi Seif Ali Iddi wa kwanza kulia akimpongeza Meneja wa Mradi wa Kimataifa wa Give kutoka Nchini Marekani Bwana Josh Winter kutokana na Taasisi yake kusaidia maendeleo ya Elimu Zanzibar.Picha na –OMPR – ZNZ.

  0 0  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida jioni hii ambapo aliwahutubia wananchi na kuwaeleza kuwa huu ni wakati wa kuchagua kiongozi wa kutuongoza hivyo ni vyema wananchi kupima na kuacha ushabiki.
    Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia na Mkuu wa mkoa wa Singida,Dkt.Parseko kone mara baada ya kuwasili mkoani humo na kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera akiwa ameambatana Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Maofisa wengine wa chama.
  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya Wanachi wa Mkoa wa Singida jioni hii alipowasili katika ofisi za mkoa za CCM,na pia alipata fusra ya kuwahutubia wananchi,Ndugu Kinana na ujumbe wake wako njiani kuelekea mkoani Kagera kwa ziara ya siku 28. 
   Baadhi ya wafuasi wa Chama cha CCM wakiwa wamekusanyika jioni hii wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana,alipowahutubia kwa muda mfupi nje ya ofis za mkoa wa Singida jioni hii.

  0 0

  01Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Bi Samia Suluhu Hassan akitembelea fukwe za mto Pngani kukagua shughuli za mazingira katika fukwe hizo katika Wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
  03Picahani ni sehemu ya ukuta wa Mto Pangani unaojengwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais ili kuzuia maji yanayoshambulia sehemu ya Nchi kavu.
  04Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Bi Samia Suluhu Hassan akiangalia ujenzi wa ukuta wa kingo za mto Pangani wakati wa ziara ya kutembelea Pangani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira duniani.
  …………………………………………………………………….
  Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais
  Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais washirikiana na wananchi wa mkoa Tanga katika kufanya usafi wa mazingira ya maeneo mbalimbali mkoani humo ikiwa ni kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika kila tarehe 5 ya mwezi Juni duniani kote ambapo kitaifa mwaka huu yatafanyika mkoani Tanga .
  Wakiongozwa na Naibu Katibu wa Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Angelina Madete wafanyakazi hao walitembelea Kituo cha Afya cha Ngamia na kutembelea maeneo mbalimbali ya mazingira ya kituo hicho kwa ajili ya kufahamu uhifadhi wa taka kabla na baada ya teketezwaji wake kituo humo.
  Wakati huo huo pia wafanyakazi hao walitembelea Soko la Mpwapwani liliopo eneo la Uzunguni mkoani humo ambapo waliwaelimisha wafanyabiashara pamoja na wanachi waishio karibu na maeneo hayo kutohifadhi taka katika eneo moja ili kuhepusha uharibifu wa mazingira.
  Aidha Injinia Madete alifafanua kuwa baadhi ya taka huweza hutumika tena kama malighafi hivyo ni vizuri kutozihifadhi taka hizo katika sehemu moja na taka zingine ambazo hupelekwa dampo huku akiongeza kuwa baadhi ya taka hizo pia huwa haziozi hivyo hupelekea dampo kujaa kwa haraka pamoja na uharibifu wa mazingira.
  Katiaka majumuisho ya ziara hiyo wafanyakazi hao walitembelea fukwe za Bahari katika eneo la Raskazone na kutoa wito kwa maafisa mazingira wa mkoa wa Tanga kuotesha miti ya mikoko katika baadhi ya maeneo ya wazi ndani ya hifadhi ya fukwe hizo kwa ajili ya kuzuia bahari kuharibu eneo la kuta za kingo katika fukwe hizo.

  0 0

  1
  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mkoani Dodoma kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika nchini. Kushoto kwake ni Idd Mruke, Meneja Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mkoa wa Dodoma.2
  Meneja wa Takwimu za Biashara na Utalii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ambaye ni Msimamizi wa Sensa ya Viwanda nchini akiwaelezea waandishi wa habari leo mkoani Dodoma kuhusu vigezo vilivyotumika katika kuchagua sampuli ya viwanda vilivyochaguliwa kufanyiwa utafiti. Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda.3
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda wakati akizungumza nao leo mkoani Dodoma kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika nchini.

  …………………………………………………
  Na Veronica Kazimoto, Dodoma
  Wito umetolewa kwa wamiliki wote wa viwanda kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wasimamizi na wadadisi wanaokusanya taarifa za Sensa ya Viwanda inayoendelea hapa nchini.
  Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dododoma ambapo amesema ukusanyaji taarifa kwa nchi nzima umefikia wastani wa asilimia 80.5.
  “Hadi kufikia tarehe 24 Mei, 2015 jumla ya viwanda vidogo 9,540 sawa na asilimia 82 pamoja na viwanda vya kati na vikubwa 1,158 sawa na asilimia 79 vilikamilika kukusanywa taarifa zake. Hii inafanya ukusanyaji Takwimu kwa nchi nzima kuwa wastani wa asilimia 80.5″, amesema Dkt. Kigoda.
  Aidha, Waziri Kigoda amesema licha ya mafaniko hayo, bado kuna kazi kubwa ya kukamilisha viwanda vilivyobaki ambavyo ni takriban 2,032 sawa na wastani wa asilimia 19.5.
  “Hivyo, nawaasa wamiliki wote wa viwanda hususani katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Morogoro, Tabora, Kigoma na Manyara kutoa ushirikiano zaidi na wa kutosha kwa zoezi hili ili ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Juni, 2015, tuweze kuhitimisha”, amesisitiza Dkt. Kigoda.
  Waziri Abdallah Kigoda amesema lengo kuu la Sensa ya Viwanda ni kukusanya takwimu sahihi zinazohusu Sekta ya Viwanda nchini ambazo zitawezesha kupata viashiria sahihi vya uchumi pamoja na taarifa muhimu za viwanda kama vile orodha ya viwanda kimkoa, anuani na mahali vilipo, aina ya umiliki na utaifa wa wamiliki.
  Taarifa nyingine ni pamoja na mwaka ambao viwanda hivyo vimeanza uzalishaji, shughuli kuu ya viwanda husika, idadi ya wafanyakazi, gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mapato yanayotokana na uzalishaji na gharama za uzalishaji.
  Lengo lingine la Sensa ya Viwanda ni kupima na kufuatilia mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Viwanda ili kuiwezesha Serikali kuboresha sera na programu za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya Tanzania, 2025, Malengo ya MKUKUTA na Mpango wa Taifa wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN).
  Jumla ya Wadadisi 198 wameajiriwa kwa ajili ya kufanya kazi ya kukusanya Takwimu na taarifa viwandani ambapo wanasimamiwa na Mameja Takwimu wa Mikoa, Watakwimu kutoka Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Maafisa kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

  0 0

  1
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani moja ya fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati alipofika Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo Juni 4, 2015 kwa ajili ya kuchukua fomu hizo. Kushoto ni Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni ,Seif Khatib. Picha na OMR
  4
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, baada ya kukabidhiwa mkoba huo na Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni , Seif Khatib, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo, Juni 4, 2015.
  6
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa Fomu hizo. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.
  7
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuchukua fomu, leo Juni 4, 2015. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.

  9
  Baadhi ya wana CCM waliohudhuria Mkutano wa Makamu wa Rais Dkt. Bilal. alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
  101112
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanachama wa CCM na wanahabari, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu za kuwania urais.
  14
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Fomy za kusaka wadhamini, mmoja kati ya vijana waliojitolea kusambaza fomu za kutafuta wadhamini, Saada Ilasi, baada ya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma.

  0 0

  Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi nia ya kuwania urais, Ngeleja  
  amesema wananchi wengi wamekuwa wakidhani kuwa aliondolewa katika wadhifa huo kwa kutumia madaraka vibaya jambo ambalo si sahihi. 


  Ameongeza utaratibu uliofanyika kumuondoa ni utaratibu wa kawaida na kuwa unaweza kutumika hata bila ya kuwa na udhaifu katika uongozi.

  Ameongeza kumekuwa na baadhi ya baadhi ya watu wanaoeneza habari hizo kwa leo la kumchafua.
  Willim Ngeleja anaungana na viongozi wengine wa siasa kutangaza nia ya kugombea urais. BOFYA VIDEO JUU KUMSIKILIZA.Hebu tujiulize. Kwa nini Takwimu za uchumi nchini zinaonyesha Uchumi ukikuwa kwa wastani wa asilimia 7% takribani kwa muongo mzima wa takribani miaka 10 mfululizo lakini umasikini umekuwa ukipungua kwa asilimia 2% tu? BOFYA VIDEO JUU KUSIKILIZA

  Ingawa nafasi ya Urais imeombwa na wanachama wengi, Ngeleja atoa fursa kwa watanzania kumtathimini, na si kwa maneno ya mtaani bali kwa takwimu za utendaji kazi ikiwa ni sambamba na kuifuatilia ripoti ya CAG na ESCROW kuisoma kurasa hadi kurasa.

  0 0

  5
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia wakati alipofungua Mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa nchi za bonde la  mto Nile kwenye Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma Juni 4, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    34
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa Nchi za Bonde la Mto Nile wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati alipofungua mkutano wao kwenye  Kituo Cha Mikutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma Juni 4, 2015.
  1
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) wakimsikiliza Dkt. Mohsen Alarabawy  (kulia)   katika maonyesho yalikwenda sambamba  na Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za Bonde la Mto Nile  kwenye Kituo cha Mikutano cha Hoteli ya Saint Gaspa mjini Dodoma Juni4, 2015.
  2
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) wakimsikiliza Nakaraga Juliet kutoka Uganda (kulia)  katika maonyesho yalikwenda sambamba  na Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za Bonde la Mto Nile  kwenye Kituo cha Mikutano cha Hoteli ya Saint Gaspa mjini Dodoma Juni4, 2015.

  0 0

  Mfalme wa Masauti Bongo, Christian Bella ‘Obama’ akiwa ndani ya Global TV Online.
  Christian Bella akiimba wimbo wake mpya wa 'Nashindwa' ndani ya studio za Global TV Online leo.
  Malaika Band chini ya uongozi wa Christian Bella katika moja ya shoo yao, Dar Live patakuwa hapatoshi Jumamosi hii.
  Mfalme wa Masauti akiimba.
  Christian Bella akiimba kwa hisia.
  MFALME wa Masauti asiye na mpinzani Bongo, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuutambulisha Usiku wa Nashindwa, Juni 6, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
  Akizungumza na mtandao huu, Bella ambaye ni kiongozi wa Bendi ya Malaika Music alisema kuwa kuanzia saa mbili usiku wa Jumamosi utakuwa wa aina yake kutokana na walivyojiandaa na bendi yake.
  Staili mpya
  Bella aliwataka mashabiki wengi kujitokeza kwa wingi kwani mbali na kuzindua wimbo huo, mashabiki watapata burudani ya kuoneshwa staili zao mpya.
  “Bella na Malaika tumewaandalia staili tatu mpya na za kitofauti ambazo kila mmoja atazipenda na kuzicheza kwani tutazizindua kwa mara ya kwanza,” alisema Bella.
  Sapraiz kumiminika
  Bella aliongeza kuwa yeye pamoja na Malaika Music wameaandalia sapraiz kibao kwa wakazi wote wa Mbagala, Temeke na pande zote jijini Dar watakaojitokeza.
  “Mara ya mwisho kupiga shoo Dar Live ilikuwa ni Usiku wa Wapendanao ‘Valentine’s Day’ na usiku ule ulikuwa maalum kwa kina mama wote nakumbuka niliwaita mashabiki wote jukwaani na kuimba nao Wimbo wa Nani Kama Mama, walifurahi sana.
  “Niwaambie safari hii ni ya kitofauti kwani nakuja na Nashindwa hivyo mashabiki wote kila mmoja nitapanda naye jukwaani na kuimba naye Wimbo wa Nashindwa.”
  Ladha ndani ya ladha
  Ukiachana na wimbo wa Nashindwa usiku huo Bella alisema utakuwa wa ladha ndani ya ladha kwani kwa mara ya kwanza atawaonjesha wimbo mwingine mpya.
  “Kuna wimbo mpya ambao nimefanya na msanii mkubwa wa kimataifa na siku hiyo mbali ya kuburudika na Wimbo wa Nashindwa pia nitawaonjesha kipande cha wimbo huo.”
  Burudani mwanzo mwisho
  Kuhakikisha burudani haikauki, kwa wale mashabiki 500 wataofika wa kwanza ndani ya Dar Live watapata bahati ya kupiga picha ‘red carpet’ na Bella sambamba na kuzungumza naye machache.
  “Hakuna msanii ambaye amewahi kufanya hivi kama nilivyofanya Valentine’s Day na safari hii natoa nafasi hii kwa mashabiki wote watakaofika mapema.”
  Mashabiki pia watarajie kupata nyimbo mpya kutoka kwa Malaika Music pamoja na nyimbo nyingine zote kali kutoka kwa Bella kama vile Nani Kama Mama, Msaliti, Nakuhitaji na nyingine nyingi.

  0 0  ZILE GUMZO ZA JIJI ZILIZOKUWA ZIMEADIMIKA MUJINI SASA ZIMEINGIA @AK CLASSIC COSMETICS #MLIMANI CITY..
   
  KUANZIA JUU (UNYWELENI) UTAPATA HAKI YAKO.. 1.T444Z 2.JBCO 3.HAIRFINITY 4.KINKY CURLY 5.SHEA MOISTURE 6.CANTU
  WEUSI WA MACHONI 1.MELADERM
  LIPS YAKE LIPGLOSS TENA YA UKWEEE

  MWILINI NA TUMBO #BODYSHAPER SASA ZIMEKUJA ZA KUTOSHA ZOTE ZA MAZOZEZI NA KUVAA OFISINI

  WALE WA KUNG"AA 1.MAKARI 2.GLOWs 3.HT.26 4.OTENTIKA
  WEUSI WA MAPAJANI 1.EXPERT SCAR SERUM

  PITIA BAADHI YA MAMBO YAO HAPA....


  TUNAPATIKANA KINONDONI KWA MANYANYA NA
   MLIMANI CITY MKABALA NA SUBWAY..;.  
   TUPIGIE  TUPIGIE /0753482909
  BIDHAA ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO NDANI NA NJE YA DAR!!  0 0

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na kamati ya Ulinzi na Usalama usiku huu ndani ya wilaya Kahama mkoani Shinyanga tayari kwa mapumziko,ambapo kesho ataianza rasmi ziara yake katika kijiji cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera,Ndugu Kinana ndani ya Biharamulo atapokea taarifa za chama na Serikali na baadae kuzungumza na Wafugaji wa kanda ya Ziwa (Mikoa ya Geita,Kagera,Mwanza na Shinyanga)  na baadae kueleke Bukoba mjini.

  Ndugu Kinana amewasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha uhai wa chama,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama. 
   KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa jimbo la Nzega usiku huu Dkt.Hamis Kingwangalla,mara baada ya kuwasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama. 
    KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akipokelewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho usiku huu wilayani Nzega mkoani Tabora akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama. 
    KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali mara baada ya kuwasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana pia aliwashukuru wakazi wa wilaya hiyo kwa kumpokea vyema na kumtakia kheri katika safari yake ya kujenga chama na nchi kwa ujumla
   KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwashukuru wapenzi na washabiki wa chama hicho wilayani Nzega usiku huu kwa kumpokea vyema na kumtakia kheri katika safari yake ya kukijenga na kukiimarisha chama na nchi kwa ujumla
   KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akimshukuru Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla kwa mapokezi mazuri wilayani humo,ndugu Kinana amewasili wilayani humo mnamo majira saa nne usiku na ushehe akitokea jijini Dar kwa basi maalum akiwa emeambatana na ujumbe wake akielekea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi
   Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla  akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana .

  PICHA NA MICHUZI JR.KAHAMA.

  0 0

  Irina_Bokova

  Director-General of UNESCO. Irina Bokova.

  Seven Billion Dreams. One Planet. Consume with Care.
  We live in a world transforming deeply, rocked by multiple crises, on a planet facing rising pressure.

  Environmental change has never been so deeply interconnected with our societies as it is today, in this era that many scientists call the Anthropocene, when human activity is the major force shaping the planetary system. The impact that individual women and men are having on the sustainability of the planet may not always be visible -- but consider the impact of seven billion women and men, and it becomes clear that daily choices matter.

  Environmental change is not just about carbon – it is, fundamentally, about women and men, it is about how we produce and consume in society. The environment is intertwined with human values and behaviour, directly linked to our livelihoods, urban development and nature conservation as well as migration patterns, affecting also the use of water and land, impacting on species survival.

  Sustainability cannot be crafted through technological or economic solutions alone. We need green societies to build green economies. We must act in a holistic manner, across the board, starting with individual women and men. 

  This year, the international community has an historic opportunity to adopt a new sustainable development agenda and to reach a global agreement on climate change. UNESCO is bringing the full force of its mandate and experience to make both a success. 

  We are promoting education for sustainable development to shape the new values, skills and knowledge that all societies need today. Sustainability will be built on the benches of schools, starting as early as possible. We work also to harness the power of science, technology and innovation to strengthen knowledge, to safeguard biodiversity through Biosphere Reserves, and to strengthen the links between the sciences and policy.

  This is one goal of the Scientific Advisory Board, an initiative of the United Nations Secretary General for which UNESCO is the Secretariat, to craft a new unity among all sciences and catalyze new synergies across disciplines, policy lines and borders, including to inform the 21st Session of the Conference of the Parties to the UN Framework Convention on Climate Change (COP21) that will be held in Paris later this year.

  There is strong global momentum – we need to act on this promise and make a new one, for development that is sustainable, in harmony with the planet. This responsibility cannot wait -- we must act now.

older | 1 | .... | 544 | 545 | (Page 546) | 547 | 548 | .... | 1897 | newer