Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

TANZIA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
 

 
TANZIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Mhe. EUGEN ELISHIRINGA  MWAIPOSA  kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 June 2015 nyumbani kwake Dodoma ambako amekuwepo kushiriki Mkutano wa Bunge la Bajeti.

Mwili wa Marehemu utaagwa kesho tarehe 3 Juni 2015 kuanzia saa 4 asubuhi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, na baadaye mwili kupelekwa nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam.

BWANA alitoa, BWANA ametwaa. Jina la BWANA  lihimidiwe. Amina!

Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Dodoma,
2 Juni 2015. 


   

WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDERICK SUMAYE ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

$
0
0
 Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, akiingia ukumbini katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Dar es Salaam leo asubuhi akiwa ameongozana na mke wake Ester Frederick Sumaye kwa ajili ya kutangaza nia ya kuwania nafasi ya urais wakati ukifika iwapo jina lake litapitishwa na chama chake cha CCM. 
 Waziri Mkuu mstaafu  Sumaye akiwa na mke wake 
Ester Sumaye wakati wa mkutano huo wa kutangaza nia.
 Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (kulia), akizungumza na wanahabari na wadau wengine wakati akitangaza nia hiyo.
 Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (katikati), akiwa meza kuu. Kutoka kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kiluvya, Juma Semendu Nauchiwa. Kada wa CCM, Shabani Uronu, Mama Ester Sumaye na Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Charles Kaenja.
 Mwanahabari Ibrahim Yamola akimuuliza swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia ya nafasi hiyo.
  Mwanahabari Mariam Mziwanda akimuuliza swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia ya nafasi hiyo.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
 Msanii Oscar Nyerere akitoa burudani katika mkutano huo.
 Wananchi wakimpongeza Waziri Mkuu mstaafu Sumaye baada ya kuzungumza nao.
 Msanii Shafii Omari akitoa burudani.
Makada wa CCM na wadau wengine wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mhe. Fredrick Sumaye ametangaza nia ya kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar leo.
Sumaye amesema kuwa ameamua kutangaza nia akiwa Dar es Salaam maana anataka kuwatumikia Watanzania wote siyo wa nyumbani kwake pekee.Kauli mbiu yake ni ‘Uongozi Bora, Komesha Rushwa, Jenga Uchumi’.

Kiongozi huyo amesema ametangaza nia baada ya kujipima, akajitafakari na kujiridhisha kuwa anatosha kuwania nafasi hiyo.Sumaye amesema dira ya taifa katika miaka 10 ijayo ni kwamba Tanzania ifikie uchumi wa kati.

Aidha kiongozi huyo ametumia muda huo kuelezea kiongozi anayetakiwa na Watanzania kuwa:
-Kwanza ajipime, ajitafakari na ajiridhishe kuwa anatosha nafasi hiyo 
-Ajipime kiafya, kiakili, kimaadili na kidhamira

-Mzalendo, anayejua tulipotoka na tunapotaka kufika
-Kiongozi ambaye ni mtumishi atakayewatumikia wananchi na si bosi
-Kiongozi anayefikiri na kushauriwa 
-Kiongozi anayeweka maslahi ya Tanzania mbele na si yake binafsi
-Kiongozi atakayelinda amani ya Tanzania na Muungano wake.
-Mwenye uwezo wa kusimamia uchumi
-Atakayeboresha huduma za jamii zisizobagua watu.

-Atakayesimamia elimu ya Tanzania kurejea ilipokuwa hapo awali na kuiendeleza zaidi
-Atakayepambana na rushwa, ujangili na madawa ya kulevya.

Mhe. Sumaye pia amewatupia swali baadhi ya makada wa CCM waliotangaza nia na kudai kuwa wanauchukia umasikini hivyo kuamua kuutafuta utajiri Ikulu ambapo amewataka kama wanataka utajiri upo mitaani waende wafungue makampuni. (Habari wa Hisani ya Global Publishers). (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO NA WAFANYABIASHARA.

$
0
0
1
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwaeleza wafanya biashara kuendelea kutoa ushirikiano, utakaojenga uhusiano wa kudumu kati yao na Serikali kwa maslahi na maendeleo ya Taifa, wakati akitoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam.
2
2- Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akimshukuru Waziri wa Fedha kwa ushirikiano wanaoendelea kuuonyesha kwa mamlaka hiyo hasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala la ukusanyaji Kodi nchini.
3
3- Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja akimueleza Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum kuridhishwa na utendaji wa serikali katika utatuzi wa changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kufikia malengo ya taifa ya kuwa na uchumi imara kupitia ukusanyaji wa Kodi.
4
4- Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu akipongeza kazi iliyofanywa Kamati ya uhamasishaji wa matumizi ya mashine za kielektroniki(EFDs) na kuwaasa kuendelea kutoa ushirikiano kwa maslahi ya Taifa kwa Ujumla.
5
 Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja wafanyabiashara alipotoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu.
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Serikali yafikia muafaka katika mgogoro wake na wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine za kieletroniniki EFD’s.
Hayo ameyasema jana Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari juu ya Serikali kufikia muafaka wa makubaliano yaliyofanyika kwa ushirikiano wa Kamati kuu ya Taifa iliyoshirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara katika ngazi ya Taifa.
“Matumizi ya mashine za EFD yalipoanza yalileta changamoto kwa wafanyabiashara ,hivyo niliunda kamati ya kitaifa pamoja na kamati katika ngazi za Mikoa na Wilaya pamoja na wenyeviti wakuu wa mikoa kutafuta suluhu la suala hili”alisema Mhe.Mkuya.
Waziri Mkuya aliendelea kusema Kamati imetoa mapendekezo mbalimbali kwa Serikali ikiwemo ya muda mfupi ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi na mengine ni yakisera ambayo yatahitaji muda mrefu yatafuata utaratibu unaopaswa katika utekelezaji wake,kwa ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu,kupitia kamati ya Kitaifa itakayodumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw.Johnson Minja aliipongeza serikali kwa kubali kukaa meza moja na wafanyabiashara katika kutatua mgogoro huo uliyokuwepo katika matumizi ya mashine za EFD na kuakukubali kupokea changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuzifanyia kazi.

RAIS KIKWETE ZIARANI NCHINI FINLAND

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata mapokezi Rasmi kutoka kwa mwenyeji wake, Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha mwenyeji wake, Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto kwa ujumbe alioambatana nao Ikulu ya Finland.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake, Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto.

BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA UKONGA EUGEN MWAIPOSA

$
0
0
7
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga marehemu Bi. Eugen Mwaiposa ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Taarifa za kifo chake zimetangazwa wakati bunge likiendelea na mjadala wa bajeti ya wizara ya afya hivyo kupelekea bunge hilo kuahirishwa hadi tarehe 4 mwezi huu.
1
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt Seif Rashid akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2015/2016 leo mjini Dodoma.
2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Jenista Mhagama (mwenye nguo nyekundu) akimfariji Mwenyekiti wa Bunge Bi. Lediana Mng’ong’o mara baada ya bunge kuahirishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Bi. Mary Nagu na kushoto ni wabunge James Mbatia na Goodluck Ole Medeye.
3
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjela Kairuki (kushoto) akitoka nje ya ukumbi wa bunge akiwa ameambatana na wabunge Bi. Mary Mwanjelwa na Rita Kabati baada ya bunge hilo kuahirishwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa.
45
Baadhi ya wabunge wakiwa kwenye hali ya simanzi baada ya kutangazwa kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa kilichotokea usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma.
6

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muuangano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Kiondo, wakati alipofika na ujumbe wake Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
li2
li3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Kombe kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani kutoka Kituo cha kuelelea watoto waishio katika mazingira magumu kilichopo Kigamboni, kinachosimamiwa na TBC. Mshana alifika na ujumbe wake Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar esSalaam, leo kwa ajili ya mazungumzo na kumkabidhi zawadi hizo. Picha na OMR
li4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Saa ya ukutani kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
li5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Khanga zenye Nembo ya TBC na zinazotangaza Utalii wa ndani  kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
li6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Tisheti  kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
li7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbi na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha kulelea Watoto waishio katika mazingira magumu, kilichopo Kigamboni baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
li8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib BIlal, akiagana na wajumbe walioongozana na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Kiondo, Omar Rajab (kushoto) na Maico Rugendo, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR

RAIS KIKWETE ZIARANI FINLAND

$
0
0
1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi Dorah Msechu katika uwanja wa ndege wa Helsinki alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu ya nchi hiyo
2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi wa FinladDorah Msechu katika uwanja wa ndege wa Helsinki alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu ya nchi hiyo
3
Rais Jakaya Kikwete akitembelea maabara ya majaribio ya kampuni ya kutengeza lifti ya KONE jijini Helsinki, Finland.
4
Rais Jakaya Kikwete akitembelea maabara ya majaribio ya kampuni ya kutengeza lifti ya KONE jijini Helsinki, Finland.
5
 Akipokea zawadi ya jezi ya timu ya taifa ya Finland ya basketball
6
JK akitoa zawadi ya mchoro wa Tingatinga kwa viongozi wa kampuni ya KONE
7
JK akitembelea  bandari ya Helsinki
9
Rais Kikwete akipata mapokezi Rasmi kwa mwenyeji wake Rais wa Finland Mhe Sauli Niinisto

10

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI LEO.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania, wakati walipomtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Juni 02,2015.

Asema :Jitahidini kuepusha migogoro-Dkt. Bilal awaasa wafugaji .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewataka wafugaji nchini kuhakikisha wanafuata sheria na kuachana na tabia ya kuchukua sheria mkononi ili kuhakikisha usalama wao na watu wanaopakana nao unakuwepo wakati wote. Mheshimiwa Makamu wa Rais amezungumza hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ujumbe kutoka Chama cha Wafugaji Tanzania ulioongozwa na Mwernyekiti wao Ally Hamis Lumiye.
 
Makamu wa Rais alisema, si busara kwa wafugaji kujichukulia sheria mkononi na kwamba matatizo yanayowakabili wafugaji ni muhimu yakatatuliwa kwa kufuata sheria za nchi. “Jitahidini kuepusha migogoro hasa ile inayosababisha watu kupoteza maisha. Tusichukue sheria mkononi, sote lazima tuwe watii wa sheria,” Makamu wa Rais alisema.
 
Awali akizungumza kwa niaba ya Baraza la Wazee wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Mwenyekiti wa Chama hicho Ally Hamis Lumiye alisema, chama cha wafugaji kwa sasa kinakabiliwa na changamopto kubwa hasa baada ya kuwepo mgawanyiko unaolenga kukimomonyoa chama hicho hasa kufuatia kujitokeza baadhi ya wafugaji kuamua kupora madaraka ya chama hicho na hivyo akaitaka serikali kuungana nao katika kuzima nguvu za waporaji hao.
 
“Mheshimiwa Makamu wa Rais leo hii tumekuja kwako kwa jambo moja nyeti. Wapo baadhi yetu wasiotaka kuona wafugaji tunajikomboa kwa kuwa na umoja kama huu. Wamefikia hatua ya kupora chama hiki na jitihada zetu za kutaka kuwadhibiti zinaonekana kuwa ngumu kufuatia baadhi ya viongozi wa serikali kuwatambua waporaji hao,” alisema mwenyekiti huyo.
 
Mheshimiwa Makamu wa Rais alisisitiza kuwa jambo la uporaji wa chama kamwe haliwezi kuachwa kimya kwa kuwa wafugaji na chama chao kimesajiliwa hivyo wafuate sheria hizo hizo ili kupata haki yao kama inaonekana kutokuwepo. Pili alisisitiza kuwa atalifanyia kazi suala hilo kupitia nafasi ziliozpo chini yake na kulipatia ufuimbuzi wa haraka.
 
“Mimi nami ni mfugaji, chama hiki ni muhimu kwa maslahi ya wafugaji. Kwa kuwa tuna katiba inayokiongoza na kwamba tunazo sheria ambazo zilifuatwa hadi kukipatia chama hiki usajili, basi hakuna haja ya kusikitika sana. Tutumie taratibu hizi hizi ili kuondokana na hao wanaotaka kupora mamlaka ya chama hiki,” alisema na kuongeza:
 
“Ni muhimu kiwepo chama imara kwa maslahi ya wafugaji wote. Chama hiki kinaweza kuwasaidia sana katika kukabiliana na changamoto mlizonazo maana kwa kuwa wamoja ni nguvu.”

Profesa Muhongo atangaza nia leo mjini Musoma

$
0
0
WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo, ametangaza nia rasmi ya kuwaomba Wana CCM kumteua kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, huku akisema ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuikwamua nchi katika hali mbaya ya umasikini na ukosefu wa wataalamu, hali inayoifanya nchi ishindwe kupiga hatua.

Pamoja na mambo mengine, Muhongo alitumia muda mwingi kutoa takwimu hali ya umasikini na utajiri kwa wananchi wa Tanzania, bila kusahau baadhi ya nchi ambazo zimeweza kupiga hatua kubwa kwa kujikita kwenye kuzalisha wataalamu na watafiti, akiwamo yeye, ambaye si tu ni Profesa, bali pia amebobea kwenye nishati kwa miaka mingi.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya wanachama wa CCM na Watanzania katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria, Musoma Mjini, Profesa Muhongo alisema kwamba anayo tiba ya umasikini wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba anatumia utaalamu wake kwa kusimamia mambo ya gesi, mafuta, umeme, bila kusahau elimu kwa ajili ya kuwakwamua wananchi wake.

“Nchi ina upungufu mkubwa wa takwimu hali inayowafanya viongozi washindwe kujua namna gani wanaweza kuondoa umasikini na kero zinazowakumba wananchi wake, hivyo hata wale wanaosema wanataka uongozi, hawajui wangapi wenye uhitaji.

KILELE CHA MAONESHO YA VIWANDA VIDOGO KANDA YA ZIWA (SIDO) YAFANYIKA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Moto ukiwa unawaka katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo Juni 2,2015 ndiyo kilele cha maonesho ya bidhaa za viwandani kanda ya ziwa yaliyoandaliwa na shirika la Viwanda Vidogo nchini SIDO.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ndiye aliyefunga maonesho hayo yaliyodumu kwa siku 5 yakihusisha wajasiriamali 260 kutoka ndani na nje ya Tanzania. 

Kabla ya kufunga maonesho hayo ambayo yamefanyika mkoani Shinyanga,mkuu wa mkoa huo Ally Rufunga alitembelea mabanda mbalimbali. Malunde1 blog,ilikuwepo eneo la tukio,mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha zifuatazo.......
Mwanafunzi Asha Hamis kutoka chuo cha VETA Shinyanga akipanda kwenye mtambo unaitwa Loader na kuonesha utaalam wake wa kufanya kazi kwa kutumia mtambo huo,baada ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kutembelea banda la chuo cha VETA
Mwanafunzi wa  chuo cha VETA akiendesha mtambo katika viwanja vya Shycom leo Juni 02,2015
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akimpongeza mwanafunzi wa VETA Asha Hamis  aliyeendesha Loader na  mwenzake Jafari ( katikati) aliyeendesha Greda  hapo uwanjani
Mkuu wa mkoa akiwa na vijana wa VETA ambao ni wataalam wa kuendesha magreda na Loader
Hapa ni katika banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga,moto ukiwa unawaka ikiwa ni sehemu ya maonesho ya jeshi hilo,ambapo baada ya moto kuwashwa ulizimwa kisha maafisa wa jeshi hilo kuonesha njia mbalimbali za kuzima moto mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga
Moto ukiwa unawaka katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizima moto huo
Maafisa wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyanga wakionesha kwa vitendo namna ya kuzima moto kwa kutumia maji
Afisa wa jeshi la zimamoto mkoa wa Shinyanga akionesha jinsi ya kuzima moto akiwa juu ya gari lao
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiwa ameshikilia kopo la dawa za asili katika banda la wataalam wa tiba za asili,kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,nyuma yake ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku,akifuatiwa na mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede
Mkuu wa mkoa akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa tiba za asili
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiulizia matumizi ya dawa ya Vidonda vya Tumbo katika moja ya mabanda ya tiba za asili
Mcheza ngoma ya Ugoyangi akiwa ameshikilia mnyama fisi katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Fisi akiwa eneo la tukio,huku mcheza ngoma ya wanunguli akionesha mbwembwe zake mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga
Burudani inaendelea
Jukwaa kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya 13 ya viwanda vidogo kanda ya ziwa.Pamoja na mambo mengine aliwataka Wajasiriamali nchini kuzingatia ubora wanazozalisha ili kuingia katika soko la ushindani wa bidhaa zao na kuongeza ufanisi wa bidhaa zao.

Rufunga aliwataka watanzania kuthamini bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali nchini kwani ni bora na zenye kiwango kinachotakiwa.Baada ya kutoa hotuba ya kufunga maonesho hayo,mkuu huyo wa mkoa alitoa vyeti kwa washiriki pamoja na zawadi kwa wajasiriamali walifanya vizuri katika maonesho hayo
Wajasiriamali kutoka Shinyanga wakiwa eneo la tukio
MC akiendelea kutoa miongozo mbalimbali
Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga Athanas Moshi akizungumza wakati wa kufunga maonesho hayo ambalo aliwaomba wajasiriamali kuacha kufanya biashara kwa mazoea na  waendelee kuzalisha bidhaa zenye ubora kama walivyoonesha katika viwanja vya Shycom.
Picha ya pamoja -baadhi ya washiriki wa maonesho hayo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga
Maonesho hayo ya Viwanda Vidogo kanda ya ziwa  yaliyoanza kufanyika mkoani Shinyanga tarehe 28 mwezi Mei na yamemalizika yakishirikisha wajasiriamali 260 kutoka ndani na nje ya Tanzania na kauli mbiu ya mwaka huu inasema; “Buni, Boresha, Jifunze biashara kupitia SIDO.”

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,LAZARO NYALANDU AUNDA TUME YA KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WANANCHI KUNYANYASWA

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi wa Kata ya Buger wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha leo katika ziara ya siku moja kuzungumza na wananchi baada ya mwananchi mmoja kuuawa kwenye msitu wa Marang unaohifadhiwa na Shirika la Hifadhi ya Taifa(Tanapa).Waziri Nyalandu ameunda Tume ya kuchunguza mgogoro huo ambayo itatoa mapendekezo serikalini kwa utekelezaji.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na mmoja  wa wananchi wa Kata ya Buger wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha leo baada ya kuhutubia wananchi hao na kuwahidi serikali kuwachukulia hatua askari waliokiuka taratibu za maadili.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha,Cesilia Paresso akihutubia wananchi wa Kata ya Buger na kuitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuzingatia sheria na wananchi kulinda Msitu wa Marang kwaajili vizazi vijavyo.
 Mkazi wa Kata ya Buger,Rehema Tango akitoa kero zake mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii.
sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huop ambao waliweza kutoa kero zao . 

SEHEMU YA HOTUBS YA MH.MWIGULU KUWANIA URAIS WA TANZANIA.

Niambie Live Show

$
0
0
Omby Nyongole, Dotto Maongo na Salma Moshi
Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.
Ni Niambie Live....
KARIBU

KUCHUKUA FOMU ZA URAIS CCM NI LEO MJINI DODOMA, SEIF KHATIBU NDIYE KAPEWA JUKUMU LA KUKABIDHI FOMU

$
0
0



Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Idara ya Oganezesheni Dr Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu Dodoma kuhushu ratiba ya kuchukua fomu leo  Wagombea Urais kupitia Chama hicho aliwataja kuwa ataanza Prof Mark  Mwandosya ,Stephen Wasira,Edward Lowasa, balozi Amina Salumu Ali na Charles Makongoro Nyerere  na Khatibu ndiye aliyepewa jukumu na Chama hicho kutoa fomu hizo.

Wanasiasa watano  wanatarajia kuchukua fomu ya kugombea urais  katika makao makuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma.

Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) wa Oganaizesheni, Dk Muhammed Seif Khatib, uchukuaji wa fomu hizo unaanza rasmi leo.

Amesema kwa mujibu wa orodha waliyonayo, wanachama watano watachukua fomu hizo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 10:30 jioni, na kila mmoja amepewa saa moja na wametenga muda wa kuzungumza na waandishi wa habari kwa wagombea ambao wataona inafaa kwao. Amemtaja wa kwanza kuchukua fomu kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya kuanzia saa 4 kamili hadi saa 5:30.

Profesa Mwandosya atafuatiwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira kuanzia saa 5:30 na atafuata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa atachukua fomu kuanzia saa saba kamili. Wa nne atakuwa Waziri wa zamani wa Muungano, Balozi Amina Salum Ali kuanzia saa 8:30 mchana na pazia la ufunguzi litafungwa saa 9:30 alasiri na mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere.

Baada ya kumaliza kuchukua fomu  kwa kundi la kwanza wanasiasa  wengine ambao wametangaza nia ya kuwania urais ni Lazaro Nyalandu, Frederick Sumaye, Profesa Sospeter Muhongo, January Makamba, Mwigulu Nchemba na Luhaga Mpina.Wanaotajwa ni pamoja Bernard Membe, William Ngeleja, Dk Titus Kamani, Luhaga Mpina, Mizengo Pinda, Dk Asha-Rose Migiro, Shamsi Vuai Nahodha, Dk Emmanuel Nchimbi na Dk Hamis Kigwangalla.

Katibu huyo wa Oganaizesheni amesema uchukuaji huo wa fomu utazingatia taratibu zilizowekwa na CCM na kutakuwa na fomu tatu zitakazopewa wagombea.Fomu  ya kwanza  itahusu maelezo binafsi ya mgombea, itahusu uzoefu na ujuzi wake, nyingine itakuwa ya kujaza orodha ya wadhamini wake na nyingine ya masharti kama yalivyokubaliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

Kwa upande wa wadhamini  amesema, mgombea atatakiwa kupata wadhamini 450 kutoka katika mikoa 15 ya Tanzania Bara na mikoa mingine mitatu ya Tanzania Zanzibar. wagombea hao watakapofika kuchukua fomu, wanapaswa kuwa na ada ya Sh milioni moja na watasaini daftari maalumu kuonesha ndio waliochukua fomu.

Amewataka  wagombea wengine wanaotaka kuchukua fomu hizo kuwasiliana mapema na ofisi yao kwani alisema wangependa kazi ya uchukuaji fomu kudumu kwa siku zisizozidi tano ili shughuli nyingine ziendelee.


HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA(TANAPA) KUPITIA UJIRANI MWEMA WAKABIDHI MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA ASHIRA WILAYA YA MOSHI

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika tanki la maji la mradi wa ujirani mwema uliotolewa na TANAPA kwa wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisoma kilichoandikwa katika vibao mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi huo.
RC ,Gama akinywa maji kwa kutumia mkono mara baada ya kufungua bomba la maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ashira katika wilaya ya Moshi ikiwa ni ishara ya kukabidhi mradi huo wa maji ulifadhiliwa na TANAPA kupitia mradi wa ujirani mwema.
Tanki la Maji la mradi wa ujirani mwema uliofadhiliwa na Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA).
Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Erastus Rufungulo akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi wakati wa kukabidhi mradi wa maji wa ujirani mwema uliofadhiliwa na TANAPA.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Meneja Ujirani mwema wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania(TANAPA) Ahmed Mbugi akizungumza kuhusu miradi ya ujirani mwema ambayo TANAPA imekuwa ikiitoa kwa jamii katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ashira  katika wilaya ya Moshi .
Kaimu Mkurugenzi mkuu TANAPA,Ibrahim Musa akitoa taarifa mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kuhusu ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi ,
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji uliofadhiliwa na TANAPA kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akiwahutubia wananchi waliofika katika makabidhiano ya mradi wa maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi ,uliofadhiliwa na hifadhi za taifa Tanzania (TANAPA) .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini, 

NASHINDWA NDANI YA DAR LIVE JUMAMOSI JUNI 6, 2015

Filamu ya MPANGO MBAYA kuzinduliwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani City

$
0
0
MPANGO MBAYA ni filamu iliyochezwa na washiriki 10 waliofanikiwa kuingia katika Fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) msimu wa kwanza 2014 na kushirikisha baadhi ya waigizaji mahiri kutoka katika kiwanda cha Filamu Tanzania.

Filamu ya Mpango Mbaya ni filamu ambayo imetengenezwa kwa viwango vya hali ya juu huku ikikidhi viwango vya kimataifa na ni filamu ambayo ina ubora wa hali ya juu kuanzia ubora wa picha, Sauti, rangi mpangilio wa matukio na upigwaji picha wake na ubora wa washiriki wa filamu hiyo
Filamu hii itazinduliwa mnamo tarehe 12 Juni 2015 Katika Ukumbi wa Mlimani City  na pia Filamu hii itaendelea kuonyeshwa kwa siku mbili mfululizo katika ukumbi huohuo.

Picha chini ni baadhi ya taswira za washiriki wa filamu hiyo

Makampuni, Wachimbaji madini watakiwa kuzingatia Sheria za Mazingira

$
0
0
 Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb) aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani, akimsikiliza  Mhandisi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Ephraim Mushi wakati alipotembelea banda la Wizara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea  katika viwanja vya Tangamano jijini  Tanga.
 Wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali jijini Tanga, wakiangalia madini ya ujenzi wakati walipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea  katika viwanja vya Tangamano jijiji Tanga.
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Mhe. Stephen Masele, akiongea jambo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Innocent Makomba (kulia) akiwaeleza akiwaonesha wananchi waliofika katika Banda la Wizara ya Nishati na Madini madini ya ujenzi  aina  Uranga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Dunian yanayoendelea katika Viwanja vya Tangamano Jijijini Tanga.

Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb) aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani, akisalimiana na wananchi na watumishi wa sekta mbalimbali baada ya kuwasili katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga kufungua maonesho ya Siku ya Mazingira .





Na Asteria Muhozya, Tanga.


Kampuni za uchimbaji madini, utafutaji mafuta na gesi wakiwemo wachimbaji wadogo nchini, wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za uhifadhi wa mazingira wakati wanapotekeleza shughuli zao, ili kuwezesha rasilimali zinazopatikana  ardhini ziweze kuwa endelevu  kwa manufaa ya vizazi vijavyo.


Rai hiyo imetolewa na   na Mhandisi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ephraim Mushi wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani yanayoendelea kufanyika  katika viwanja vya Tangamano  Jijini, Tanga.

Mhandisi Mushi ameeleza kuwa, kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu duniani hususan katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania    ni muhimu mahitaji yao yakaenda sambamba na rasilimali zilizopo.


“Nafahamu uelewa wa makampuni ya uchimbaji madini na utafutaji wa mafuta na gesi katika usimamizi na kutunzaji wa mazingira ni mkubwa, kwani tayari  kampuni hizo zina mpango wa usimamizi mazingira ambao umeeleza masuala yanayopaswa kuzingatiwa, lakini bado wanapaswa kuzingatia jambo hili wakati wote kutokana na umuhimu wa wake”, alieleza Mushi.


Kuhusu wachimbaji wadogo ameeleza kuwa, bado wanafanya shughuli zao za uchimbaji bila kuzingatia sheria na kanuni za usimamizi wa mazingira. “Wachimbaji wadogo bado hawazingatii suala hili lakini Wizara inafanya jitihada mbalimbali za mara kwa mara kuhakikisha wachimbaji wanafuata taratibu ikiwemo kuwaelimisha kuhusu usalama na mazingira”,aliongeza.


 Hivyo, amewataka wachimbaji wadogo kuwa na mpango wa utunzaji mazigira kwa kuwa utaonesha namna ya  kuhifadhi na kutunza mazingira na hivyo kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na kanuni husika.


Akieleza zaidi kuhusu jitihada zinazofanywa na wizara katika kusimamia masuala ya   uhifadhi na utunzaji wa mazingira, hususan katika sekta za nishati na madini,  ameeleza kuwa, Wizara imeshatoa mafunzo kadhaa kuhusu masuala hayo kwa maafisa mazingira mazingira wa halmashauri katika Wilaya mbalimbali za  mikoa ya Mwanza, Iringa  na Mbeya kuhusu sheria na kanuni za madini na athari za uchimbaji usiozingatia uhifadhi mazingira.


Vilevile ameongeza kuwa,  wizara mafunzo mengine ni pamoja na mpango kazi wa mazingira wa wizara ambapo maafisa mazingira hao wanatakiwa kuingiza masuala ya madini kwenye mpango kazi yao. Mafunzo hayo pia yanatarajiwa kuendelea kufanyika katika miningine katika mwaka wa fedha ujao.


Aidha, ameeleza  kuwa, wizara imekuwa ikishirikiana na taasisi kadhaa zenye uhusiano wa masuala mazingira kama vile Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira  (NEMC) na wizara nyingine katika masuala yanayohusu  miradi ya nishati na madini jambo ambalo limeleta matokeo mazuri kwa kuwa miradi yote ya nishati na madini haiwezi kuanza   bila kufanyiwa tathmini ya athari kwa mazingira.


Siku ya mazingira duniani huazimishwa kila mwaka tarehe 1 - 5 Juni, ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu “ Ndoto Bilioni  Saba. Dunia Moja. Tumia Rasilimali kwa Uangalifu”. Aidha, maonesho hayo yalifunguliwa  rasmi na tarehe 1 Mei,2015, na Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta  (Mb)kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal.

NEW SONG: SAI SHAN'OKUZANA - DAT

EXCLUSIVE: TANZANIAN RAPPER FID Q ALBUM LISTENING PARTY AT NAIROBI RAPSODY - THUR JUNE 4TH

$
0
0
After a successful event with Brooklyn, NY hip hop artist Yasiin Bey (Mosdef) in his first East African showcase, Nairobi Rapsody is back this Thursday (4th June) with Tanzania’s hip hop wordsmith -  FID Q.


Welcome to Ebony Lounge from 10:00 p.m. (Thursday 4thJune) for an exclusive night with Coke Studio Africa season 3 artist: FID Q of the hit Bongo Hip Hop. He will be in Nairobi, Kenya hosting a Listening Party of his upcoming third album Kitaaolojia (Streetology) for the first time. The album is set for release in July.


Kitaaolojia album is about what’s happening on the streets and inspires the youth to be in control of their lives. It features 10 songs including Ielewe Mitaa, Neno featuring Lord Eyez, Sihitaji Marafiki featuring Yvonne Mwale from Zambia, Siri ya Mchezo featuring Juma Nature, Bendera ya Chuma with Ben Pol and Bongo Hip Hop with the producer P Funk Majani. FID Q has also worked with BET Nominated Kenyan group Sauti Sol in a song that will feature in Kitaaolojia album.


“The first album Vina Mwanzo Kati na Mwisho was about FID Q’s prose and writing. Propaganda was a political album.  Now Kitaaolojia edutaines. It highlights FID Q’s motive to help youth and the young people from the street to make sense of their lives,” said a statement from his management.


Welcome to a chilled-out affair with the FID Q nicknamed “The Swahili Kid” by New York hip hop artist Fat Joe. Gates open at 8:00 p.m. Entrance Free. Good vibes. FID Q will also play some of his past songs from the other albums. He will be joined on the decks by Kenya’s DJ Finalkut.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images