Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 532 | 533 | (Page 534) | 535 | 536 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Balozi wa PSPF, Bi. Flaviana Matata akitoa elimu kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu (hawapo pichani) jijini Mwanza
   Afisa Mfawidhi Ofisi ya PSPF Mwanza, Bw. Salim Salim, akisalimiana na Balozi wa PSPF, Bi. Flaviana Matata, kabla ya kuanza semina ya siku moja kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu jijini Mwanza.
  Baadhi ya wanafunzi wakisoma vipeperushi vyenye taarifa kuhusu Mfuko wa PSPF wakati wa semina juu ya Mfuko huo iliyotolewa na Balozi wa PSPF, Bi. Flaviana Matata hivi karibuni.
  Mmoja wa wanafunzi waliohudhuria semina juu ya Mfuko huo iliyotolewa na Balozi wa PSPF, Bi. Flaviana Matata hivi karibuni akiuliza swali ili kapata ufafanuzi.
   Balozi wa PSPF, Bi. Flaviana Matata (mstari wa mbele katikati), katika picha ya pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wa elimu ya juu jijini Mwanza baada ya kuotoa elimu kwa wanafunzi hao juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana kwa kuwa mwanachama wa PSPF.

  0 0

  Magari yaliyokuwa yakitumiwa na watalii wa ndani waliokuwa wakipanda kwenda kilele cha Shira yakiwa yameegeshwa baada ya kushindwa kuendelea na safari kutokana na ubovu wa barabara .
  Baadhi ya watalii wa ndani wakiwa eneo la kambi ya Tembo wakisubiri magari madogo ya hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ajili ya kuwachukua kuwapeleka katika hifadhi hiyo.
  Watalii wa ndani walilazimika kupanda magari ya aina hii ili kufika katika kilele cha Shira.
  Safari ya kuelekea kilele cha Shira ikianza.
  Afisa Masoko wa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro Antypas Mgungusi akizungumza jambo mbele ya watalii wa ndani mara baada ya kufika Lango la Londros kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea kilele cha Shira.
  Baadhi ya watalii wa ndani.
  Hali ya hewa katika eneo hili ni ya kubadilika .
  Watalii wa ndani wakielekea katika kilele.
  Wengine walikuwa na furaha mara baada ya kufika katika uwanda wa Shira.
  Wengine waliamua kupumzika njiani.kama anvyoonekana m,wandishi James Paul wa ITV.
  Hatimaye magari yaliyokuwa yameshindwa kupita kutokana na ubovu wa barabara yalifanikiwa kupita na kupanda kuwachukua watalii wa ndani.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akipokea msaada wa sabuni kutoka kwa meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers,Christopher Loiruk kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea wilaya ya Moshi vijijini.
  Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akipokea msaada wa unga kutoka kwa Meneja mwajiri wa kampuni ya Bonite Bottlers,Joyce Sengoda kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko.
  Mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga akizungumza mara baada ya kupokea msaada kutoka kampuni ya Bonite Botttlers kwa ajili ya waathirika wa mafuriko.
  Eneomoja wapo ambalo wakazi wake wameathirika kwa mafuriko katika kijiji cha Kilungu.
  Msaada wa maji ambayo yametolewa kwa waathirika wa mafuriko katika vijiji hivyo ili kupunguza kutokea kwa maradhi ya tumbo yanayoweza kutokea kwa matumizi ya maji machafu.
  Unga wa ngano ukishushwa kwa ajili ya waathirika hao.
  Meneja mwajiri wa kampuni ya Bonite Bottlers ,Joyce Sengoda akiwasalimia wananchi katika vijiji vya Mikocheni ,Kilungu na Chemchem vilivyofikwa na mafuriko hivi karibuni wakati uongozi wa kampuni hiyo ulipofika kwa ajili ya kutoa msaada.
  Meneja Masoko na mauzo na wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd Christopher Loiruk akizungumza wakati wa kukabidhi msaada kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika vijiji hivyo.
  Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite,Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa sukari kilo 750 kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemi chemi.
  Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ,Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa maji zikiwa ni  katoni 500 kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemi chemi.
  Meneja muajiri wa Bonite Bottlers ,Joyce Sengoda akikabidhi ndoo za mafuta kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga ambazo zimetolewa 30 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemchem.
  Baadhi ya nyumba zilizo athirika na mafuriko hayo.
  Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo ambao baadhi yao bado wako katika kambi iliyopo kijiji cha Kilungu wakiishi katika zahanati ya kijiji hicho.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Meneja Mauzo wa Kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini A rusha ,kanda ya Kaskazini ,Edmund Rutaraka akikabidhi hundi ya kiasi cha sh Mil ,1.5 kwa mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro(KRFA) Gudluck Mushi kwa ajili ya kuisadia timu ya Kilimanjaro fc inayoshiriki ligi ya mabingwa wa mikoaikiwa kituo cha Lindi.
  Hundi iliyotolewa na kampuni ya Megatrade Investment Ltd.
  Menejamauzo wa kanda ya Kaskazini wa kampuni ya Megatrade,Edmund Rutaraka akizungumza jambo mara baada ya kukabidhi msaadawa kiasi cha sh Mil,1.5 kwa ajili ya timu ya Kilimanjaro fc.kushoto kwake mwakilishi wa kampuni hiyo mkoa wa Kilimanjaro Loseline Laiser.
  Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro Gudluck Mushi akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa pesa kiasi cha sh Mil,1.5 kutoka kampuni ya Megatrade kwa ajili ya timu ya Kilimnjaro fc.
  Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,Mohamed Musa akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada wa fedha toka kampuni ya Megatrade.
  Katibu wa kundi la mtandao wa Soka letu ,Godfrey Madegwa akizungumza namna ambavyo kundi hilo la wadau linavyo pambana kutafuta fedha za kuisadia klabu ya Kilimanjaro fc.
  Baadhi ya wadau waliofika ofisi za KRFA kwa ajili ya kushuhudia utolewaji wa hundi ya kiasi cha sh Mil,1.5 kwa ajili ya kuisadia timu ya Kilimanjaro fc. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini,

  0 0

  fl1
  Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima  (kulia)  akitoa maelezo kuhusu hali ya maendeleo ya mradi kwa wanajopo la ukaguzi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, pichani ni  Bibi. Florence Mwanri (Katikati), Ndg, Robert  Masatu na  Ndg. Aloce Shayo, kwa mfuatano.fl2
  Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Jilima akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji  Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango,  Bibi. Florence Mwanri, eneo likatalojengwa kituo cha Kinyerezi II mara baada ya Kinyerezi I kukamilika.fl3
  Sehemu za mashine za kuzalishia umeme wa gesi ambazo ziko tayari katika kituo cha Kinyerezi.fl4fl6
  Mwonekano wa kituo cha kuzalisha umeme wa gesi Kinyerezi kwa juu.
  …………………………………………………………..
  Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.
  Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo la ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango walipotembelea mradi huo.   
  “Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV 132 Kinyerezi hadi eneo la viwanda la Gongolamboto, alisema Mhandisi Jilima. Tayari nguzo za kusafirishia umeme kutoka Kinyerezi mpaka Kimara zimeshasimikwa vivyo hivyo kwa upande wa Gongolamboto.
  Naibu Katibu Mtendaji  Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango,  Bibi. Florence Mwanri, alisema iwapo mradi huu utakamilika na kuanza kuingiza umeme wake katika gridi ya taifa ni dhahiri kuwa gharama za uendeshaji wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa zitashuka, na pia kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.
  “Katika miaka mitano ijayo mpango wetu wa maendeleo umejikita zaidi katika uchumi wa viwanda hivyo ni  vema ujenzi huu ukamilika kwa wakati ili kutoleta changamoto katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa mwaka 2016/17-2020/21” alisisitiza Bibi. Mwanri.
  Ili kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo tayari Tanesco wameshanunua mitambo mingine mine ambayo itazalisha umeme kiasi cha kV 180.

  0 0

  gh1
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili kwenye Ukumbi Maalum kwa watu wa China. ‘Peoples Great Hall’, jijini Beijing China kwa ajili ya mazungumzo rasmi, alipoalikwa kwenye chakula cha jioni na Makamu wa Rais wa China baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo. jana Mei 20, 2015. Picha na OMR
  gh2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Serikali ya China, wakati alipowasili kwenye ukumbu Maalum wa watu wa China, ‘Peoples Great Hall’ kwa ajili ya mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo, jana Mei 20, 2015. Picha OMR
  gh3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati akikagua gwaride la heshima kwenye Ukumbi Maalum wa watu wa China, Peoples Great Hall, wakati alipofika kwa mazungumzo na mwenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo. Picha na OMR
  gh4
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakisimama kwa heshima wakati zikipigwa nyimbo za Taifa la Tanzania na China, kwenye mapokezi yake katika Ukumbi Maalum wa Watu wa China, kwa ajili ya mazungumzo baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Nchina. Picha na OMR
  gh5gh7gh8
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ujumbe wake (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao na ujumbe wake (kulia) kwenye Ukumbi maalum wa Watu wa China, ‘Peoples Great Hall’ baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini China. Picha na OMR

  gh9
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisindikizwa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Kushoto ni mkarimani wa Makamu wa Rais wa China. Picha na OMR
  gh10
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini China. Picha na OMR
  ………………………………………….
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatano Mei 20, 2015 amemalizia ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini China ambapo amekutana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China Mheshimiwa Li Yuanchao na kupata mapokezi Rasmi ya Serikali ya China katika ‘Ukumbi Maalum’ kwa wa Watu wa China. Makamu wa Rais katika mapokezi hayo alipata nafasi ya kukagua gwaride na kisha kuongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais Yuanchao katika ukumbi wa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa China alitumia nafasi hiyo kumshukuru Makamu wa Rais wa Tanzania kwa kukubali mwaliko wake na hivyo kufanya ziara ya kikazi nchini China na pia akaongeza kuwa, uhusiano wa China na Tanzania ni wa wakati wote na akasisitiza kwamba ushirikiano baina ya nchi hizi mbili unatoka katika mioyo ya wananchi. “Nilipokuwa Tanzania mwaka jana mwezi wa Juni niliona namna raia wa China anavyothaminiwa na kuheshimiwa nchini Tanzania. Jambo hili lilinipa furaha na kunielimisha kuhusu nchi zetu,” Makamu wa Rais Yuanchao alisema.
  Makamu wa Rais Dkt. Bilal alitumia nafasi hiyo licha ya kushukuru kwa Mwaliko pia kuzungumzia agenda za maendeleo ya Tanzania huku akisisitiza kuwa, anayo furaha kuhusu kukamilika kwa usimikaji wa mkondo wa Taifa kwa awamu zote mbili huku akiitaka serikali ya China kuendelea kuwa na Tanzania katika kukamilisha awamu ya tatu, jambo ambalo Makamu wa Rais Yuanchao alilikubali.
  Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alizungumzia pia ziara yake katika majiji ya Wuhan na Nanjing na akaelezea furaha yake kuhusu namna wananchi wa China wanavyoitazama Tanzania na namna walivyo tayari kushirikana nayo katika kukuza maendeleo ya viwanda sambamba na kutanua soko la biashara baina ya Tanzania na nchi zinazoizunguka. Pia alipata nafasi ya kuzungumzia kuhusu namna ya kuboresha reli ya TAZARA huku akimtaka Makamu wa Rais Yuanchao kusaidia kwa kuwaita Mawaziri wa Uchukuzi toka Zambia na Tanzania ili wakutane na wenzao wa China ili kuhakikisha kunapatikana mkakati mpya wa namna ya kuiendesha Reli hiyo kwa faida ya nchi washirika.
  “Reli hii ni moja ya viashiria vikubwa vya historia ya mahusiano yetu. Sisi Tanzania tusingependa kuona inakufa,” alisema Makamu wa Rais Dkt. Bilal na kuongeza kuwa mazungumzo kama hayo yanatakiwa kufanyika katika mradi wa ujenzi wa sehemu ya uwanja wa ndege wa Zanzibar ambao umesimama ujenzi kufuatia pande mbili kushindwa kuelewana.
  Kwa upande wake Makamu wa Rais wa China yeye aliihakikishia Tanzania kuwa China inao uzoefu mkubwa katika mambo mengi hivyo Tanzania inatakiwa kutumia urafiki wake na China katika kushirikiana kwenye masuala ya maendeleo. Pia alifafanua kuwa serikali za Tanzania, Oman na China zinatakiwa kuendelea kushirikana katika suala la Ujenzi wa Bandario na Bagamoyo na kwamba serikali yake imejipanga kuendelea kuwafadhili wanafunzi wa Kitanzania kusoma masomo ya Mafuta na Gesi.
  “Wakati nilipokuwa Tanzania nilifurahishwa na namna watu wenu wanavyoonesha uwezo wa kukabiliana na changamoto za sasa. Watu hawa wanaweza kabisa kufanya kazi za aina mbalimbali hivyo sisi tunaitazama Tanzania kama sehemu ya kuifanya Afrika itanuke na hivyo uhusiano wa China na Afrika ubakie kama ulivyokuwa katika kipindi cha Afrika kutafuta uhuru,” alisema.
  Mheshimiwa Makamu wa Rais amemaliza ziara yake na moja kwa moja kuanza safari ya kurejea nchini ambapo anategemea kushiriki mikutano ya Chama cha Mapinduzi inayofanyika mjini Dodoma. Katika ziara hiyo ya siku tatu nchini China, Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal aliambatana na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kutoka Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna. Mwingine ni Naib u Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim.
  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
  Mei 20, 2015
  Beijing, China

  0 0

   Pichani kati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre,Jumanne Ali Ligopora   akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam kuhusiana na tamasha la Qaswida,linalotarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe.Kulia ni Sheikh Muharami Pembe na kushoto ni Ustaadhi Jumanne Gereza.
   Mmoja wa watakaoshiriki katika tamasha hilo,Rahma Muhidin Kigora akighani Qaswida mbele ya waandishi wa habari  (hawapo pichani).
   Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo uliohusu 
  tamasha la Qaswida,linalotarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe.Kulia ni Sheikh Muharami Pembe na kushoto ni Ustaadhi Jumanne Gereza. 

  Tamasha la Qaswida lililokuwa likitarajiwa kufanyika Mei 25,jijini Dar,sasa limepangwa kufanyika Mei 31 katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe.


  Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo,kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar, Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre,Jumanne Ali Ligopora amesema kuwa tamasha hilo limebadili tarehe ya onesho lake ili kuwa bora zaidi.

  Amesema kuwa tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake,tayari lmekwishawapata wadhamini watatu,amewataja wadhamini hao kuwa ni Gazeti la Dira ya Mtanzania, watengenezaji wa kinywaji cha Sayona na Madrasamtimun.

  Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa katika mashindano hayo kutakuwepo na watu wa benki za miamala ya kiislam,ambao wataonesha namna benki hizo zinavyofanya kazi na huduma kwa wateja wao.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu), George Mkuchika akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa uwazi na kusikilizana kati ya Serikali na taasisi zisizo za kiserikali barani Afrika mkutano uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
    Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Issah Mwambene akichangia  kwa upande wa serikali kuwa serikali ya Tanzania ni sikivu, wakati wa mkutano wa Uwazi na usikivu katika mambo ya uchumi serikalini pamoja na taasisi zisizo za kiserikali  katika bara la Afrika.
   Mkurugezi wa kampuni ya Compass Communications Ltd  Maria Sarungi akizungumza katika mkutano wa Uwazi na Usikivu  uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka bara la Afrika, mkutano hup umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugeni Mkuu wa TWAWEZA Aidani Eyakuza akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika kufunga mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya Wadau wa mkutano kutoka nchi mbalimbali  za Barani Afrika walihudhuria  mkutano uliofanyika  katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

  SERIKALI NA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZATAKIWA KUWA WAZI.
  Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  Serikali na Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali  Barani Afrika zimetakiwa kubadili maudhui yake kwa kuweka mipango ya  uendeshaji wa mambo yake kwa uwazi hasa kwenye sekta za uchumi.

   Hayo yamesemwa na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu),George Mkuchika wakati akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali Barani  Afrika  kutoka serikalini na Taasisi zisizo za kiserikali,mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijijini Dar es Salaam leo.

  Mkuchika amesema kuwa,mkutano huo utasaidia sana endapo yaliyozungumzwa kwa siku mbili katika mkutano huo yatafuatwa na wananchi wataweza kujua mambo mbalimbali katika nchi zao, pia kila mwananchi ashiriki vyema kufanikisha malengo ya nchi.

  Pia kwa upande wa serikali amesema kuwa  serikali ikiweka mambo yake kwa uwazi pia inaweza kukosolewa, sio kila jambo inalofanya ni sahihi inahitaji kukosolewa ili kuleta maendeleo, pia wananchi waweze kufahamu nini kinaendelea katika nchi husika.

  0 0


  Mwenyekiti   wa chama cha Tnzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo)   katika mkutano uiliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MELEZO kuhusu kukanusha  kuwa yeye amefukuzwa TLP,Kushoto Mkurugenzi wa Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo,Kulia ni Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mrikariya.


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.


  MWENYEKITI wa Chama cha Tnzania Labour Party (TLP) Agustino Mrema,amesema hajafukuzwa unachama katika chama hicho.


  Mrema aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana kuwa yeye ni mwenyekiti wa Chama hicho na hakuna mtu wa kumtoa kutokana na kuendesha chama hicho kwa kufuata katiba.


  Amesema kikundi kinachofanya hivyo na kusambaza taarifa kuwa kimemtoa kutokana na kufanya vikao hakitambui na kuwataka wanachama kuwabeza watu hao. 

  Mrema amesema yeye akiwa Mwenyekiti ataendelea kutetea jimbo lake la Vunjo,hivyo watu wanaosema amefukuzwa katika chama wapuuzwe.
  Aidha amesema biashara ya Urais ameachana nayo ,sasa kazi yake ni Ubunge kupitia jimbo la Vunjo na ameweza kuleta maendeleo ya wananachi katika jimbo hilo.


  0 0

  Muimbaji mahiri Vanessa Mdee amefiwa na dada yake mkubwa Anna Mdee, ambaye amefariki katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam,  jana Jumatano alfajiri. Anna ambaye alikuwa mfanya kazi wa kampuni ya sigara ya TCC na alikuwa katika kituo cha Dodoma kwa muda mrefu alikuwa India akipatiwa matibabu.

  Anna na Vanessa ni watoto wa marehemu Sammy Mdee, aliyekuwa mwandishi mkongwe aliyewahi kuongoza gazeti la Daily News, Katibu wa Mwalimu Nyerere na pia mkurugenzi wa kituo cha AICC. Mazishi ya Anna yatakuwa Same Jumamosi saa 8 mchana.

  Mungu Amlaze Pema Anna Mdee

  0 0
 • 05/22/15--00:07: Article 9


 • 0 0

  MWL. ERNEST MWAMKAI KIONDO

  Mpendwa Baba, tarehe 22 May 2015 umetimiza mwaka mmoja tangu ututoke hapa duniani kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu.

  Tunakukumbuka sana kwa malezi, upendo na ushauri wako  ambao daima ndio dira yetu na kumbukumbu yetu.

  Unakumbukwa sana na Wazazi wenza Mama Anna na Mama Agatha, Dada zako na sisi wanao, wakwe zako, wajukuu wote pamoja na ukoo wote wa Kiondo, Bendera, Mbaruku, Msangazi, Bila, Mjata na  Nyangasa.

  Japo haupo tena pamoja nasi kimwili, lakini kiroho tuko pamoja nawe kila siku.
  Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kukuhifadhi  mahali pema peponi.

  AMEN.

  Kutakuwa na misa ya kumuombea Marehemu Mzee wetu Jumamosi  tarehe 6/6/2015 katika Kanisa la Mtakatifu Yohana  Krisostomo, Majani Mapana, Tanga.

  Misa inategemewa kuanza saa 3 asubuhi na kabla ya hapo, Ijumaa tarehe 5/6/2015 kutakuwa na mkesha  nyumbani kwa Marehemu Kwaminchi Tanga, karibu na Uwanja wa saba saba.
  Karibuni sana.

  MPENDWA BABA TUTAKUKUMBUKA DAIMA

  0 0

   Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa akisalimiana na Mzee Masoud Ali Chitende Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mtama mara baada ya kuwasili kwenye kata ya Mtama ambapo alipata nafasi ya kuwasalimu wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata Mtama na Majengo, Mtama mkoani Lindi.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mtama Mzee Said H. Maluma,kushoto ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Majengo Mzee Omari Mataka.
   Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata ya Mtama na Majengo wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye .


  0 0

  Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Wakili wa Kujitegemea, Elias Nawera (katikati), akizungumza na wanachama hicho na viongozi mbalimbali wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Kawe Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kawe, Athumani Athumani na Katibu wa CCM wa kata hiyo, Said Kheri.
  Kada huyo, Elias Nawera (katikati), akizungumza na wanachama wa CCM
  na viongozi mbalimbali (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Kawe Ukwamani, Chande Mbonde, Diwani mstaafu wa Kata ya Mikocheni (CCM), Harold Maruma ambaye ni kampeni Meneja wa Elias Nawera, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe, Lilian Mkotani na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kawe, Athumani Athumani.
  Diwani mstaafu wa Kata ya Mikocheni (CCM), Alord Maluma ambaye ni kampeni Meneja wa Elias Nawera akimtambulisha mgombea huyo mbele ya viongozi wa kata hiyo na waandishi wa habari (hawapo pichani)
  Mjumbe wa Propaganda wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa ni Mshereheshaji (MC), wa shughuli hiyo, Muhidini Mtengereka,  akitoa mada mbalimbali.
  Viongozi mbalimbali wa CCM wa Kata hiyo waliokuwepo kwenye shughuli hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Kata ya Kawe, Joseph Maliwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), wa Kata hiyo, Sharifa Ngongolo na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa Kata hiyo, Siri Gongo.
  Makada wa CCM wa Kata ya Kawe wakiwa kwenye mkutano huo.
  Makada wa CCM wa Kata ya Kawe wakiwa kwenye mkutano huo
  Kada wa CCM wa Kata ya Kawe akiserebuka katika mkutano huo.
  Wanahabari waliokuwepo kuchukua taarifa hiyo.
  Na Dotto Mwaibale
  KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Kawe jijini Dar es Salaam,  Elias Nawera, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Kawe katika uchaguzi mkuu unatorajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwa tiketi ya chama chake.
  Akitangaza nia yake mbele ya wanachama na viongozi wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Nawera ambaye ni Wakili wa kujitegemea alisema anayo nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.
  Alisema anaamini kuwa anatosha kuliongoza jimbo hilo kwakuwa amekuwa kada kwa muda mrefu na kwamba wakati wa kuwania nafasi hiyo ukifika atakuwa miongoni mwa watakaojitokeza kuchukua fomu ndani ya chama kwa lengo la kugombea kuchaguliwa ili kuwa miongoni mwa wawania ubunge jimboni humo.
  “Nataka kulirudisha jimbo ili mikononi mwa Chama cha mapinduzi, hivyo ndugu zangu nimesimama mbele yenu kutangaza nia yangu ya dhati ya kutaka kuwania jimbo ili pale muda utakapofika na mimi nitakuwa miongoni wa nitakaoomba ridhaa kwa chama changu”
  “Ndugu zangu nitaomba ushirikiano wenu pale muda utakapofika na kwa pamoja tuhakikishe kuwa jimbo hili linarejea CCM kwa ushindi wa kishindo”alisema Nawera.
  Kwa upande wake Meneja Kampeni wake Harold Maruma alisema kwamba anaamini kuwa wakati wa mchakato wa kugombea ndani ya chama utakapofika, Nawera atakuwa miongoni mwa watakaoomba ridhaa ya kuwa mgombea kwa tiketi ya chama hicho.
  Alisema kwamba nia ni moja kuhakikisha kuwa CCM inapata ushindi wa kishindo na kwamba kwasasa kinachofanyika ni kuweka nia ukizingatia kuwa  jimbo hilo linaongozwa na upinzani hivyo kwa CCM linahesabika kama lipo wazi. (Imeandaliwa na mtandao wahttp:www.habari za jamii.com)

  0 0

  Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba(katikati) akielezea jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao katika ofisi zake kuelezea siku ya tuzo za filamu zitakazofanyika jumamosi hii jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Bwana Ezekiel kutoka Push Mobile na kushoto kwake ni Meneja Masoko wa EATV na EAR Happy Shame.
   Meneja Masoko kutoka EATV na EA Radio Happy Shame(kulia)akielezea jambo kwa Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba wakati wa mkutano na wana habari kuhusu Tuzo za Filamu Tanzania 2015 leo jijini Dar es Salaam ambapo EATV na EAR ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo.

  Mei 23, hapatoshi Mwalimu Nyerere Internnational Conference Center;


   Ni siku moja tu imebaki kufanyika kwa tuzo kubwa za filamu nchini ‘Tanzania Film Awards’ 2015(TAFA). Ni tuzo kubwa ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam tarehe 23 Mei 2015, Mwalimu Nyerere International Conference Center. Haya ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini na kila mmoja ana shauku ya kushuhudia tuzo hizo zitakazo wapa wasanii wetu amsha amsha ya mafanikio katika tasnia yao.


  Akiongea na wana habari katika ofisi zake raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba alisema, “Maandalizi yote yapo tayari na tumejipanga kikamilifu kufanikisha tuzo hizi. Kutakuwa na burudani mbalimbali kusherehesha tuzo hizi zikiongozwa na mzee Kikii, Mwasiti na Barnaba, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wana tasnia ya filamu watakaowakilisha vizuri kabisa tasnia yao kwa kutufanya tucheke na tufurahi. 

  Yote hii ni kuwaburudisha wageni wetu watakaokuja kutuunga mkono katika siku hii muhimu kwa wana tasnia ya filamu.Tuna wageni mbalimbali ambao wameshafika kutoka nchi tofauti za Afrika ili kutuunga mkono katika hafla hii”.


   “Napenda kuwashukuru waisani mbalimbali waliojitolea kutuunga mkono Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TRA, EATV na EAR, International Eye Hospital, Foreplan Clinic, R&R Associates, Simu Tv na Barazani Production. Kwa namna ya pekee nashukuru vyombo vyote vya habari kwa sapoti kubwa waliotupa kipindi chote cha mchakato wa tuzo hizi tangu wakati wa uzinduzi hadi sasa bado wapo nasi bega kwa bega.”


  “Wito wangu kwa watanzania na wana Afrika Mashariki kwa ujumla kutuunga mkono kwa kununua tiketi za hafla hii ili waweze kufika kushuhudia tuzo hizi za kipekee zitakazo andika historia mpya katika tasnia ya filamu. Tiketi zinapatikana kwa bei ya 50,000/= kawaida na VIP ni 100,000/= katika vituo vifuatavyo;Shear Illussion - Mlimani City and Millenium Towers, Robby One Fashion- Kinondoni and Sinza Africasana, B&B Boutique- Dar Free Market duka namba 46 na Viva Towers duka namba 31, Secky Bureau de Change - Big Bon Sinza Mori,  Save Mart wholesalers - Mikocheni kwa Nyerere EATV na ITV.  Karibuni sana tufurahie na kuunga mkono kazi za wasanii wetu.” Alisisitiza Mwakifwamba.


  Tuzo za Filamu Tanzania 2015 zitakua na ‘surprises’ za kutosha hasa kushuhudia mastaa kutoka nchi za Ghana na Nigeria na mengine kibao. Watanzania wajitokeze kwa wingi kuunga mkono kazi za wasanii wetu hii ni kuonesha uzalendo kwa kupenda kazi za wasanii wetu.


  0 0

  Smart Codes now a full service digital company has been nominated again in the 2015 Awwwards from awwwards.com as one the best website around the world.  www.smartcodes.co.tz  has been placed in a queue to appear as “Site of the Day”. If successful, it will also be included in Awwwards book "The Best 365 Websites Around The World"in 2015. The awwwards Team pointed out that, Smart Codes site will be fully checked and tested by their submission team, and then posted in their nominees section and will be evaluated over 7 days by their international jury and Awwwards’ users.  If the submission (Smart Codes site) is awarded a high score will be the best 365 website around the world in 2015.
  Smart Codes team is thrilled by being given this honor for the second time. Being nominated again as the best site from Tanzania, we hope to present our country well in this prestigious award. At Smart Codes we believe that “Technology is for Everyone” and therefore we are excited by this and we will strive to make our tagline (Technology for Everyone) more so.


  You can vote for Smart codes by clicking VOTE here: http://www.awwwards.com/best-websites/smart-codes-1/


  0 0


  0 0

  UKIWA NI MWAKA WA 19 TANGU AJALI YA MV BUKOBA ITOKEE FLAVIANA MATATA KUPITIA MFUKO WA FLAVIANA MATATA FOUNDATION AMBAYO IMEKUWA IKIADHIMISHA KWA KUSOMA IBADA NA KUKUMBUKA WAHANGA HAO AKIWEMO MAMA YAKE MZAZI. 

  MWAKA WA NNE SASA FMF IKIWA INAFANIKISHA IBADA IYO AMBAPO ILISOMWA KATIKA KANISA LA NYAKAHOJA JIJINI MWANZA NA KISHA KUMALIZIA IBADA IYO KATIKA MAKABURI HAYO YALIYOPO IGOMA JIJINI MWANZA
  FLAVIANA MATATA FOUNDATION INAPENDA KUWASHURU TEAM YA ZALENDO TANZANIA , MARINE SERVICE KWA KUSHIRIKIANA NASI KATIKA IBADA IYO PAMOJA NA NDUGU ,JAMAA NA MARAFIKI SAMBAMBA NA FAMILIA ZA WAFIWA.flavian31
  flavian 19IMG_5925 
   TEAM ZALENDO TANZANIA WALIKUWAJA RASMI NA T-SHIRT ZAO ZA HATUTASAHAU MAY 21IMG_5937 MUANZILISHI WA ZALENDO TANZANIA MIRAJI KIKWETE NAE ALIKUWEPO NA TEAM YAKE NZIMA IMG_5948
  IDRISSA, MWANAFA , AY NAO WALIKUWEPO ZALENDO TANZANIAflavian33flavian27flavian30flavian23flavian25flavian28flavian29  flavian22flavian20flavian21flavian34flavian26

  0 0

   The CRDB management has donated ten desk top personal computers to Dar Es Salaam Institute of Technology (DIT), Mwanza campus, to be used in trainings by  footwear and leather goods producers so as to develop their technical skills. Above, Ms  Mary Maro (2nd right), CRDB SAUT Agency In charge, handing over part of the consignment to Dr. Albert G. Mmari (2nd left), Head of DIT Mwanza campus, at a  ceremony held recently in Mwanza. Looking on, are CRDB officials.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


  TAARIFA KWA UMMA


  KUHUSU KAMPENI YA UGAWAJI WA DAWA ZA KUKINGA NA KUTIBU MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE   KATIKA MKOA WA MWANZA


  Ndugu Wananchi,

  Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, hususan Kichocho na Minyoo ya tumbo yameathiri sehemu kubwa ya jamii katika mkoa wetu wa Mwanza. Magonjwa haya huleta mahangaiko makubwa kwa wananchi  hasa kwa watoto ikiwemo upungufu wa damu, kuzorotesha ukuaji, kupunguza mahudhurio ya watoto shuleni na pia kutofanya vizuri katika masomo yao. 

  Ugonjwa wa Kichocho husababisha Saratani ya Kibofu cha mkojo ambayo haina tiba hadi sasa. Minyoo ya tumbo inaweza kusababisha Utumbo kuziba na mtu kulazimika kukatwa utumbo, Minyoo ikiingia kwenye ubongo huleta dalili  kama za kifafa vilevile minyoo huathiri Ini na  endapo muathirika hatawahi kupata  matibabu, dalili zote hizi husababisha Mauti. 

  Magonjwa haya ni moja kati ya vyanzo vikuu vya umasikini katika familia, jamii, na taifa kwa ujumla. Aidha, takwimu zinaonesha kuwa wagonjwa walioathirika kwa saratani ya kibofu cha mkojo na hasa wakazi wa kanda ya ziwa kwa asilimia kubwa chanzo chake ni maambukizi ya kichocho.


  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhia tamko la Shirika la Afya Duniani linalokusudia kudhibiti au kutokomeza magonjwa haya ifikapo mwaka 2020, na ili kutekeleza azma hiyo. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetengeneza mpango kazi wa miaka mitano wa Utekelezaji wa shughuli mbalimbali za udhibiti wa magonjwa haya.

  Ndugu Wananchi,


  Tafiti zilizofanyika mwaka 2005 zimeonyesha uwepo wa maambukizi ya ugonjwa wa  Kichocho mkoani Mwanza yapo juu kuliko maeneo mengine nchini. Utafiti huo ulionyesha maambukizi ya Kichocho yapo kati ya asilimia 12.7 hadi 87.6 nchini. Utafiti huo unaonesha kwamba ugonjwa wa kichocho umeenea zaidi maeneo ya kando kando ya ziwa Viktoria na kiwango cha maambukizo ni zaidi ya 80% na kwa minyoo ya tumbo ni hadi 100%.

  Na katika jamii za watoto wenye umri wa kwenda shule, tafiti kwa njia ya parasitologia, maambukizi ya ugonjwa huu ni zaidi ya 50%. Kwa kiwango hicho cha maambuzi, kwa mujibu wa tafiti na maelekezo ya kitaalam ya Shirika la Afya Duniani (WHO), jamii inapaswa ipewe dawa za kukinga na kutibu.


  Tangu mwaka 2009 wizara ilizindua mpango wa udhibiti wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika mikoa ya mitano kwa kuanzia, na hadi mwaka 2012 mpango huu tayari ulikuwa umetekelezwa katika mikoa 14 na hadi mwishoni mwa mwaka jana (2014) umekuwa ukitekelezwa  katika mikoa 17 ikiwemo Mwanza iliyoingia katika mpango mwaka 2013. 

  Hadi sasa, mpango huo unaratibu shughuli zake katika mikoa 21 ikiwemo Kilimanjaro, Arusha, Simiyu na Geita iliyoingizwa katika mpango mwaka huu wa 2015. Lengo la mpango kwa sasa ni kuifikia mikoa ya Shinyanga, Mara na Kagera mapema iwezekanavyo ili kudhibiti magonjwa haya ifikapo mwaka 2020.  Ndugu Wananchi,


  Mkoa  unawajulisha wananchi na wakazi  wote wa mkoa wa Mwanza  kuwa tarehe 26   na 27 Mei 2015 tutaendesha kampeni ya  ugawaji  dawa za kukinga na kutibu magonjwa ya Kichocho na Minyoo ya Tumbo. Walengwa wa kumeza dawa hizi ni watoto  wote wenye umri wa kuanza shule ya msingi walioandikishwa na wasioandikishwa.


  Kampeni hii itaendeshwa na watalaam wa huduma za afya wakishirikiana na Walimu katika shule zote za msingi waliopatiwa mafunzo maalumu ya ugawaji wa dawa hizi. Kabla ya unywaji wa Dawa hizi Mtoto anatakiwa ale chakula na katika muda usiozidi  masaa 2 baada ya kula awe amepatiwa dawa hizi; chakula hicho kitaandaliwa shuleni.


  Hivyo kila Mzazi  katika mkoa wa Mwanza  anaombwa  amruhusu mtoto wake aende kumeza dawa hizi muhimu ili ajikinge na kupata tiba ya magonjwa haya hatari kwani huduma hii  ya dawa za kinga tiba inatolewa bila malipo kwa kila mtoto.


  Dawa hizi zimethibitishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa ni salama, na hazina madhara yoyote kwa afya ya binadamu zinapomezwa kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa afya na Walimu waliopatiwa mafunzo.


  Dawa zitakazohusika ni za Praziquantel za kudhibiti Kichocho na Albendazole za kudhibiti  Minyoo ya tumbo ambazo zitatolewa kwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule, walioandikishwa na ambao hawakuandikishwa.


  Ndugu Wananchi,

  Ni matumaini yetu  kuwa Wazazi mtawaruhusu watoto wajitokeze kwa wingi ili kumeza dawa hizi kwa maendeleo ya afya za watoto wetu na Jamii kwa ujumla. Nawaombeni sana, muendeleze sifa nzuri ya Mkoa wetu kwani umekuwa ukifanya vizuri miaka yote katika suala zima la chanjo.

  Asanteni sana kwa kunisikiliza.


  IMETOLEWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA MWANZA


older | 1 | .... | 532 | 533 | (Page 534) | 535 | 536 | .... | 1903 | newer