Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 531 | 532 | (Page 533) | 534 | 535 | .... | 1903 | newer

  0 0

    Diwani wa Soko la Tazara Vetenary, Zahoro Maganga akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu alipotembelea maeneo yaliyoharibiwa  na mvua akiongozana na  viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) jinsi maji yanavyotakiwa kufuata mfereji huo ambao haupitishi maji kupeleka katika mfereji huo .
   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads)  katika ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam (kushoto) ni Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama.
   Mhandisi Mradi Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Ngusa Julius (wa pili kulia)  akimwelekeza jambo Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (aliye vaa kofia) wakati wa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya jimbo lake yaliyo haribiwa na mvua na kusaidia kutowa Mashine ya kuondoa  maji hayo yaweze kuondolewa (kushoto) ni Katibu wa Kamati ya maafa na miundombinu ya Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke  Morocco Milanzi na kulia ni Naibu Meya Manispa  Temeke Juma Mkenga.
  Katibu wa Kamati ya maafa na miundombinu ya Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke  Morocco Milanzi (wapili kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (wa pili kushoto), wakati wa  ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam na mbunge huyo kusaidia mashine ya kuyaondosha maji hayo.
   Baadhi ya maeneo waliyo kumbwa na maji katika  Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke
  Mwenyekiti wa Serikali ya Mta wa Kilimahewa Tandika Devis Coner  Mfaume Mbonde (kulia)  akielekeza jambo wakati wa  ziara ya Mbunge na viongozi wa Tanroads wakiangalia maeneo yaliyoharibiwa na mvua nakuahidi kufanyia marekebisho maeneo hayo.
  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

  0 0

   Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, (kushoto), akipeana mikono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Juma Magahila, wakati akimkabidhi msaada wa mifuko ya saruji 100 na mabati 77 ili kusaidia ujenzi wa maabara za shule wilayani humo. Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika ofisi ya Halmashauri ya wilaya hiyo, Jumanne Mei 19, 2015. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Martha Mkupasi, (wapili kushoto), Afisa Elimu ya Sekondari wa wilaya, Benjamin A. Majuya, (watatu kushoto), na Afisa wa PPF, Kanda ya Temeke, Cecilia Makwaiya.(kulia). 
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani, Martha Mkupasi, (kulia), akizungumza jambo na Meneja wa PPF Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, (kushoto), na Afisa wa Mfuko huo, Cecilia Makwaiya
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mkoa wa Pwani Juma Magahila, (aliyekaa), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Martha Mkupasi, (katikati) na wageni wao, Erica Sendegeya (kulia), Meneja wa PPF Kanda ya Temeke, na Cecilia Makwaiya, Afisa wa Mfuko huo, katika picha ya ukumbusho.
   Erica akifurahia jambo, huku Cecilia naye akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.

  MFUKO wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Temeke, umeipiga jeki Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa kuipatia mifuko wa saruji 100 na mabati 77 kusaidia ujenzi wa maabara za shule za sekondari wilayani huko.


  Akikabidhi msaada huo, kwenye ofisi ya Halmashauri hiyo, Jumanne Mei 19, 2015, Meneja wa PPF Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, alisema, Mfuko wa Pensheni wa PPF, kupitia sera ya shirika ya uwajibikaji kwa jamii, (Corporate Social Responsibility-CSR), umetoa msaada huo ili kusaidia malengo ya wilaya katika kuhudumia jamii ambayo sehemu yake ni wanachama wa Mfuko huo.


  “Najua msaada huu hautamaliza kabisa mahitaji halisi ya ujenzi wa maabara, lakini bila shaka utasaidia kuongeza kasi ya kukamilisha ujenzi wa maabara hizo ili kusaidia watoto wetu kupata elimu iliyo bora” alisema Sendegeya, katika maelezo yake mafupi wakati wa makabidhiano hayo.


  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Juma Magahila, ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya viongozi wa wilaya, aliishukuru PPF kwa kutoa msaada huo kwa wakati muafaka, na kuongeza kuwa hatua ya Mfuko huo kusaidia juhudi za Halmashauri yake kukamilisha ujenzi wa maabara, ni faraja kubwa kwa wadau wa sekta ya elimu wilayani hapo.


  Afisa Elimu ya sekondari wa wilaya ya Mkuranga, Benjamin A. Majuya, alisema, mahitaji ya maabara katika shule 22 za wilaya hiyo ni maabara 66, maabara 3 kila shuke, na kwa sasa tayari maabara 16 zimekamilika katika hatua mbalimbali.


  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Martha Mkupasi, aliishukuru PPF, kwa kukubali maombi ya Halmashauri yake ya kupatiwa masada wa vifaa vya ujenzi wa maabara na hatua ya kukabidhi vifaa hivyo imekuwa ni faraja kubwa kwa Halmashauri yake.
  0 0

  Domain ni Nini?
   Ikiwa kuna mtu anataka kutembelea tovuti/website yako (kama wewe ulivyotembelea website hii) atahitaji kutumia domain yako au kwa kuiandika moja kwa moja au kupitia link kutoka kwenye search engine ili kuweza kuiona.
   Kompyuta huwasiliana kwa kutumia namba zinazoitwa anwani ya IP (IP Address). Hii  ni sawa na unavyo tumia namba ya simu fulani kuwasiliana na fulani. Jina la domain katika mtandao ni kama jina linaloendana na namba husika za simu katika simu yako.

  Badala ya kukariri namba za simu za watu wote, unaweka namba na jina kwenye simu yako maana majina unaweza kuyakumbuka kirahisi. Vivyo hivyo, badala ya kukariri IP address (ambazo) ni namba kwenye mfumo huu 123.456.789.123/ wateja wako watalijua tu jina lako/domain ambayo yaweza kuwa jinalako.co.tz  


  Jinsi ya kupata ‘domain name’

  Katika kufanya kuwa rahisi kwa wewe kuandikisha domain yako, Tanzania Network Information Centre (tzNIC) wamekupa njia mbili mbadala: -

  Njia ya kwanza ambayo ni rahisi tzNIC wamewapa vibali zaidi ya wasajili 20 nchi nzima ambao wanauwezo wa kukusaidia wewe kuandikisha domain yako kwa bei nafuu kabisa ya TZS 25,000 tu au USD 30 tu. 

  Na zaidi sana kwa kutumia hao wasajili wenye vibali utapata pia huduma ya hiyo domain yako kuwa hosted ambayo kwa lugha rahisi ni eneo katika ulimwengu wa digitali unaloweza kufanyia lolote ikiwemo pamoja na kuuza bidhaa zako na kutuma na kupokea email.

  Hawa wasajili waliopewa vibali na tzNIC  pia watakupa huduma ya kusimamia website yako ili usiweze kupata tatizo lolote kwa kipindi chote cha matumizi yake. Tanzania Network Information Centre (tzNIC) pia wameweka huduma ya kujisajili na tzNIC moja kwa mojaingawa hawa shauri ufanye hivyo.

  Chaguo hili linahitaji kidogo kujua maarifa ya kiufundi katika field ya digitali. Ili kuwa na haki ya kujiandikisha moja kwa moja na tzNIC lazima kutoa anwani Itifaki ya Internet yani Internet Protocol yenye name servers mbili ambazo inabidi ziwe zimeunganishwa kwenye mtandao kwa kudumu pamoja na malipo ya TZS45,000.


  Wahi mapema kusajili jina la kampuni au biashara yako au hata kama ni mtu binafsi kabla mpinzani wako kibiashara hajasajili yeye. Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea kurasa za TzNic hapa chini  0 0

  NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM.

  INAHITAJI akili ya kiuwendawazimu kuaminishwa na kuamini kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepoteza mvuto. Kwamba vinavyokubalika ni Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, NLD, TLP na vinginevyo, ambavyo kwa udhaifu wao, wameona waungane baada ya kukosa dawa ya kukiangusha chama tawala.

  Si kweli, maana vipo viashiria vingi vinavyoonyesha kuwa chama hicho kikongwe Tanzania, kipo imara na kinaungwa mkono na watu wengi, wakiwamo watoto, wazee, vijana na wake kwa waume.

  Bado wapo watu wanaoamini kuwa mtu mtu anayepitishwa kugombea katika nafasi yoyote ndani ya CCM, basi huyo ndiye mshindi. Na yapo maeneo mengi ambayo watu wake hawajui chochote kuhusu vyama vya upinzani, isipokuwa CCM.

  Kuelekea katika Uchaguzi Mkuu, kumekuwa na kauli za hapa na pale zinazoshiria kuwa baadhi ya Watanzania wenzetu, hususan wanaotoka katika Chama Tawala wamedhamiria kuchukua fomu za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

  Ingawa wapo wengine wenye nia hiyo ya kutaka urais, ila ndani ya CCM hali hiyo imezidi. Ndani ya CCM kuna joto na mchuano mkali. Takribani miaka mitatu sasa tumeshuhudia mivutano ya kila aina.

  Wataka urais huo wamekuwa na vikao na safari za kutunisha makundi yao, bila kusahau kasi ya kuongeza ushawishi kwa vijana wao wanaoshindana katika mitandao ya kijamii kwa kujiita majina ya kila aina, kuashiria wapo kwenye msafara huo.

  Haya yote yanadhihirisha nguvu ya chama tawala. Kila mtu anaangalia nani ana mvuto zaidi ya mwenzake ndani ya CCM. Kila jina linalotajwa zaidi mtaani, basi linatokana CCM.

  Wapo wanaomtaja Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kwamba anayo haiba na uwezo wa juu ya kurithi kiti cha urais, kitakachoachwa na Rais, Profesa Jakaya Mrisho Kikwete, baadaye mwaka huu.

  Wanaoamini Membe anafaa wanafanya kila wawezalo ili jamii iwaelewe, bila kusahau wanaojiita wapo kwenye safari ya matumaini, nao wakichagiza Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli arithi mikoba ya JK.

  Si Lowassa au Membe tu, bali wapo wana CCM wengine kede kede walionyesha nia ya kutaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiamini uwezo na vigezo wanavyo.

  Vipi kuhusu January Makamba, Samuel Sitta, William Ngeleja, Emmanuel Nchimbi, Profesa Sospeter Muhongo, Dkt Asha Rose Migiro, Augustino Ramadhan, Stephen Wassira na majina lukuki yanayotajwa katika ndoto hizo za urais.

  Ingawa wenyewe hawajatangaza nia hiyo hadharani, lakini mwenendo wao, harakati zao na pengine matamshi kadha wa kadha yanaonyesha kiu hiyo ya kutakaa kuongoza taasisi nyeti na kubwa nchini Tanzania, kwa kofia ya urais.

  Kuwa na ndoto ya urais ni jambo moja na kuwa rais ni jambo jingine. Hii ni kwa sababu kunahitaji mipango na ridhaa ya kuaminiwa na Watanzania wote kwa kupitia sanduku la kura.

  Kura zitakazochanganya wagombea kutoka CCM na wale wa upinzani, huku kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Tanzania, ikidaiwa kuwa vyama vine vya siasa vitasimamisha mgombea mmoja kwa mgongo uitwao UKAWA.

  UKAWA ni msamiati ulioasisiwa katika Bunge la Katiba, ambapo vyama vine vya vya Chadema, CUF, NCCR MAGEUZI NA NLD, viliamua kuungana, muungano ulioendelezwa pia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na vijiji Desemba mwaka jana, wakisisitiza pia utaratibu huo utaendelea kwa madiwani, wabunge na urais.

  Pamoja na kuungana kwa vyama hivyo vine, bado hawakaribii nguvu inayotoka CCM. Wagombea wawili, Dk Willbroad Slaa kutoka Chadema na Profesa Ibrahimu Lipumba kutoka CUF ndio wenye kudaiwa wanao uwezo wa kusimama kwa upande wa Bara.

  Upande wa Visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ndiye atakayesimama kwa upande wa CUF ama UKAWA, kwa madai chama hicho ndicho chenye nguvu na ushawishi wa kuaminiwa na watu wa Zanzibar.

  Sawa, lakini vipi wanao uwezo wa kuitingisha CCM? Lipumba aliyegombea urais zaidi ya vipindi viwili Tanzania Bara na akaonekana kachokwa, anaweza kuitikisa CCM?

  Hata kama akiitikisa, UKAWA watamuanini na kumpa nafasi hiyo, huku akiwapo Dk Slaa, aliyeshika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010?

  Hili na mengine mengi yanawafanya hata wale wasioamini CCM, nao wanaingia kwenye wimbo wa nani bora kutoka chama tawala. Wanaamini huko ndiko kwenye mvutano mkubwa zaidi.

  Na mvutano huo unatokana na nguvu ya chama hiki kikongwe. Chama kitakachotoa rais mwingine baada ya Kikwete aliyeingia Ikulu huku akiungwa mkono na makundi mengi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

  Ni dhahiri wanaotaka kujua nguvu ya CCM waiangalie namna inavyoweza kumpata pia mgombea wake wa Urais. Ni jambo nyeti linalowekwa katika utaratibu mzuri na wa kueleweka. Hii inaonyesha ukomavu wa juu wa chama hiki.

  Hawa wote wanaotajwa kutaka urais, wameibuliwa na kukomazwa na chama hiki kikongwe. Waliaminiwa katika nafasi mbalimbali. Na pengine kila mmoja ana uwezo huo wa kusimama kama mgombea urais, huku akishinda kwa kishindo.

  Uzuri ni kwamba hadi mtu anapoweza kusimamishwa kama mgombea urais kwa tiketi ya CCM, anakuwa amepita katika vikaango lukuki kwa ajili ya kujiridhisha naye. Kwamba ni mtu safi? Ana nguvu na ushawishi mbele ya hadhira?

  Anaweza kuaminiwa na Watanzania wote, ukiacha hawa wanaopiga kelele kwenye mitandao ya kijamii, ambao ni dhahiri baadhi yao wanafadhiliwa na majina hayo?

  Je, anauzika, hana kashfa? Sifa hizi na nyingine kadha wa kadha zitaondoa wasiwasi na uwezekano wa kuungwa mkono na makundi yote nchini Tanzania. Na hapo ndipo panapojibu maswali ya wale wanaoamini mtu anayetoka CCM ndio kiongozi wao.

  Huu ndio ukweli wa mambo. Ukweli huu wanaujua pia hata wale walioibukia kwenye siasa za upinzani. Ndio hao hao wanaoanza kupiga porojo kwamba kuna uwezekano mtu anayetoswa ndani ya CCM, atahamia upinzani.

  Kama hiyo ni kweli, ndio kusema kwamba wagombea na wanaoapaswa kugombea nafasi hiyo ya urais wapo CCM. Na itaingia kwenye kumbukumbu mgombea wa CCM aliyetoswa kwenye urais, amekimbilia upinzani. Ataonyesha uroho wake wa madaraka.

  Ataonyesha hafai kuungwa mkono na Watanzania. Ikumbukwe kuwa urais ni nafasi moja inayotokea kwa Mtanzania mmoja kila baada ya miaka mitano au 10 kwa vipindi viwili.

  Hii inaonyesha kuwa Watanzania wote hatuwezi kuwa rais wa nchi hii. Hivyo ili iendelee, lazima tuache tamaa zetu. Wote hatuwezi kuwa rais kwa kipindi cha miaka mitano au 10.

  Tuvumiliane, tuheshimiane na pengine tuwe na uzalendo halisi wa  chi yetu Tanzania. Uzalendo uliochochewa kwa kiasi kikubwa na uwapo wa chama tawala CCM. Chama chenye nguvu na ushawishi kwa Watanzania wote.

  Ni nani anayeweza kusimama na kuthubutu kukisema chama hiki kuwa hakina mvuto, hali ya kuwa ndicho kinachosikilizwa kimtaje mtu wa kusimama kama mgombea urais?

  Chama kilichokufa kitatoaje rais kila msimu wa uchaguzi? Hata wale wanaosema hayo, nao hukaa chini na kusema fulani anafaa, yule akisimama atasumbua na maneno nk. La kushangaza, wote wanaotajwa kwa mazuri au kwa mabaya wanatoka CCM?

  Hii ni dalili ya wazi wazi kuwa mwenye uwezo wa kugombea urais wa Tanzania Bara na akaungwa mkono na Watanzania wote atatoka CCM na atakuwa rais wa Watanzania wote.

  Kama hivi ndivyo, basi ni jukumu la CCM wenyewe kuhakikisha kwamba mtu anayeweza kupewa nafasi hiyo ya kugombea urais ni sahihi na pengine asilazimike kusafishwa na dodoki ili aonekane msafi kwa Watanzania wote.

  Mungu ibariki Tanzania.
  Mwisho


  0 0

  WADAU WA TANZANIA WAISHIO USA ILE TOUR YA "MoFLAVA ALL WHITE PARTY" FT. TANZANIAN BORN & #1 USA INT'L VERSATILE DJ  "DJ KAYCEE MoFLAVA" SASA IMEWADIA. KAA TAYARI KWANI HIVI KARIBUNI THE PARTY WILL BE IN YOU CITY.  TAREHE ZA TOUR NI HIZI HAPA CHINI AND MORE WILL BE ADDED SOON! SO SAVE THE DATE FOR YOUR CITY OR CITY NEAR YOU. LETS ENJOY TOGETHER THIS SUMMER!
  MORE DATES & CITIES FOR MoFLAVA "ALL WHITE" USA TOUR:
  06/06/2015 CINCINNATI OHIO 
  O6/20/2015 DALLAS TEXAS W/ 
  07/11/2015 HOUSTON TEXAS 
  07/18/2015 MINNEAPOLIS MN 
  07/30/2015 COLUMBUS OHIO 
  08/01/2015 WASHINGTON D.C
  08/22/2015 WICHITA KS 
  09/05/2015 ANTLANTA GA 
  MORE DATES COMING SOON. 4 BOOKING CALL OR TXT 2812365204
  To listen to DJ Kaycee Moflava Mixes go to www.hulkshare.com/djkaycee  0 0

   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba akiwaonyesha waandishi wa habari jinsi mji wa Kisarawe utakavyojengwa, katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe na Katibu mkuu wa kamati kuu ya Miradi,Mwanamvua Mrindoko na kushoto  ni Afisa Mradi wa Maliasili wa Wilaya ya Kisarawe,Cheyo Nyegele.

  Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe
  wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,ambapo wilaya ya Kisarawe inatarajia kuuza viwanja zaidi ya 291 kwa wewekezaji wa viwand.
   Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa  kazini
   Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali sambamba na Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

  Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakisoma vipeperushi vinavyoeleza namna ya mji wa kisarawe utakavyojengwa.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe imetangaza viwanja 291 vilivyopimwa  kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda katika Wilaya hiyo.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Adamu Ng’imba amesema Halmashauri ya Kisarawe ina mazingira rafiki kwa uwekezaji wa viwanda kutokana na maeneo hayo yalivyopimwa.

  Ng’imba amesema kuwa mradi wa viwanja hivyo umeshirikisha wananchi wa maeneo hayo ili kuweza kuondokana na migogoro baina ya wawekezaji na wananchi ili kuepuka malengo yaliyokusudiwa yasifanikiwe.

  Amesema katika viwanja vilivyopo katika mradi wa viwanda asilimia 63 ya fedha zitazopatikana katika uuzaji wa kiwanja kwa zitakwenda kwa mwananchi ni katika kuepuka migogoro hiyo. Amesema wawekezaji baada ya kukamilisha taratibu zote za umiliki wa ardhi ni miaka mitatu kama ameshindwa kuendeleza Halmashauri itachukua na kuuza kwa mtu mwingine.
  Ng’imba amesema katika kuondokana na migogoro na ujenzi holela wa Halmashauri imeamua kushirikisha wananchi katika maeneo husika. Amesema watakaopata maeneo ya uwekezaji katika Halmshauri ya Kisarawe watapata hati ndani ya siku saba na wananchi ndiyo watakaonufaika na mradi huo.

  0 0

  Kwa hili jipya la ‘StarTimes’ mawe yameiva na kuni zimebaki. Waswahili wanasema ukichemsha mawe kuni zinaisha kumaanisha kuwa kuna vitu haviwezekani, lakini Startimes wamekuja kivingine kabisa na kuonyesha kumbe mawe yanaweza yaaiva, kuni ndio zikabaki. 

  Startimes Tanzania, wale magwiji wa dijitali wametuletea watanzania Androi Application ambayo inakuwezesha kufuatilia chaneli uzipendazo huku ikikupa taarifa za vipindi vyako usivikose. Kama hiyo haitoshi, Tenbre itakuwezesha kuchat na watazamaji wengine wa vipindi uvipendavyo, manatazama kipindi kisha mastory yanafuata. Hili ni jiwe la moto kutoka Startimes, linaitwa Tenbre linapatikana kwenye Google Play au bofya hapa.

  Kama hiyo haitoshi, unaweza kukusanya sarafu au ‘coins’ kwenye app hiyo ambazo unaweza kuzibadili na kulipia king’amuzi chako. Fanya fasta, fuata hatua hizi Download Tenbre kwa kutembelea Play Store kwenye simu yako ya Android au bofya hapa .Install na jisajili kupitia simu yako ya mkononi.

  Umemaliza, anza kufuatilia vipindi vyako, chati na marafiki na kusanya coins…ni rahisi tu kama hivyo. Narudia tena Bofya, download, Install, Jisajili, Furahia kila kitu kiganjani mwako.
  Kama una swali au ungependa kujua zaidi, tembelea kurasa za Startimes hapa chini.


  0 0

  Na Lorietha Laurence-Maelezo
  Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) itaadhimisha wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika Mei 25 hadi 29 mwaka huu.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bw. Assah Mwambene ,amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe.
  katika ufunguzi huo, Mkurugenzi ameeleza kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa na uzinduzi wa Mradi wa Nyaraka za Urithi wa Tanzania (TAHAP) ikiambatana na maonyesho ya picha ya kumbukumbu mbalimbali zinazoelezea ukombozi wa bara hilo.
  “Mradi wa nyaraka za urithi wa Tanzania unatarajia kuweka na kutunza kumbukumbu mbalimbali zinazohusu ushiriki wa Tanzania katika harakati za zinazohusu ukombozi wa nchi za Bara la Afrika” alisema Bw.Mwambene.
  Naye Mshauri Mkuu wa masuala ya Uhifadhi wa Nyaraka kutoka UNESCO, Bw.Philippe Roisse ameeleza namna shirika hilo lilivyojidhatiti katika kuhakikisha kumbukumbu hizo zitakavyohifadhiwa kwa usahihi na manufaa ya kizazi kijacho.
  “UNESCO imeazimia kusimamia suala hili la uhifadhi wa nyaraka za kumbukumbu Barani Afrika kuhusu harakati za ukombozi na hasa ukizingatia shirika hili limefikisha miaka 17 katika kutoa huduma” Alisema Bw. Roisse.
  Kwa Upande wa Mshauri Mwelekezi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Dkt. Dinah Mbaga ameeleza kuwa mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Afrika ni muhimu sana kwa kizazi cha sasa, na kuongeza kuwa ni muhimu kukumbushana.
  Aidha, Mshauri kutoka UNESCO Bw. Daniel Ndagala, ameongeza kwa kueleza kuwa mradi wa uhifadhi wa kumbukumbu mbalimbali na nyaraka za urithi ni chombo muhimu sana katika utekelezaji wa utambuzi wa juhudi za Tanzania kwa nchi za Bara la Afrika.
  Wiki ya maadhimisho ya Ukombozi wa Bara la Afrika utaenda sambamba na midahalo mbalimbali ikiwemo, mdahalo wa mchango wa vyama vya siasa katika harakati za ukombozi, Mchango wa wanajeshi katika harakati za ukombozi
  Mingine ni mchango wa wanawake katika harakati za ukombozi, mchango wa wasanii na watunzi na mchango wa vyombo vya habari yote ikilenga suala zima la harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.
  Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufungwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni naMichezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.

  0 0


  0 0

   Rais wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani leo jijini Dar es Salaam, kuhusu Mkutano wa tatu wa Shirikisho la Vyama  vya Wataalamu wa Masuala ya Chakula na Lishe Afrika ambao unalenga kutoa fursa kwa wanasansi wa masuala ya lishe ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Joyceline Kaganda  na Afisa Mawasiliano wa taasisi hiyo Herbert Gowelle (kushoto).

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Joyceline Kaganda  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu namna taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia umuhimu wa lishe nchini  kama moja ya masuala muhimu ya kimaendeleo. Kushoto ni  Rais wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo.
  Rais wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu kupunguza viwango vya ukondefu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwa asilimia 50 mwishoni mwa mwaka huu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dkt. Joyceline Kaganda.

  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa taasisi ya chakula na lishe uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anne Kilango Malecela akizungumza na walimu (hawapo pichani) waliohuduria mafunzo ya Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.
    Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania na Mratibu wa Basic Support Program Julius Lugemalila akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same. 
   Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Elimu ya msingi TAMISEMI Kassim Kaoneka akiongea na naibu Wazirir wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ,viongozi wa elimu na walimu walioshiriki mafunzo ya Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.
   Baadhi ya walimu wa shule za msingi wilayani Same walioshiriki mafunzo ya  Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same. 
  Mwalimu Ruth Elifuraha akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anne Kilango Malecela amewataka walimu wanaofanya kazi katika maeneo wanayotoka kuwa na nidhamu ya kazi ili kuendelea kuinua ubora wa Elimu nchini. 

  Akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same amesema sababu kubwa ya kushuka kwa taaluma katika wilaya hiyo ni kutokana na walimu kufundisha katika maeneo ya nyumbani. Kitu kinachosababisha  muda mwingi kushughulikia matatizo ya familia zaidi. 

  "Walimu wanaofundisha maeneo ya nyumbani mara nyingi hukosa nidhamu ya kazi kwa kutofanya kazi uadilifu na badala yake kuishia kutatua matatizo yanayozunguka ndugu na jamaa" alisema Naibu Waziri.Aidha, amewataka kuwa na nidhamu ya hali ya juu ili kuhakikisha wanawatendea haki watoto wanaowafundisha na kuheshimu muda wa serikali kwa kufanya kazi kwa masaa wanayopaswa kufanya kazi.

   Serikali ilianzisha Programu ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi ili kukabiliana na changamoto za kushuka kwa kiwango cha ufaulu. Programu hii iitwayo Programu ya Mafunzo ya Kujenga Uwezo kwa Walimu na Wanafunzi katika ujifunzaji na ufundishaji inalenga kuongeza kiwango cha ufaulu.

  Mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi ngazi ya shule  yanasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Srikali za Mitaa (TAMISEMI). Ufuatiliaji wa mafunzo unafanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. 

  Baada ya mafunzo haya walimu wanapaswa kuanzisha madarasa rekebishi ili kuinua kiwango cha taaluma na ufaulu kwa wanafunzi kulingana na mazingira yao.   

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielezea jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Mjumbe kutoka Liberia akitoa vote of  thanks baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua  rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
      Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015.
   Mjumbe kutoka Liberia akitoa vote of  thanks baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua  rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
   Mshereheshaji wa mkutano huo Mhe. Maria Sarungi-Tsehai akitoa maelezo baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua  rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Mkurudenzi Mtendaji wa taasisi ya Twaweza Bw. Brian Eyakuze akimkaribisha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kupokea tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
     Mkurudenzi Mtendaji wa taasisi ya Twaweza Bw. Brian Eyakuze akimkabidhi  Rais Jakaya Mrisho Kikwete  tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akishukuru kwa kupewa tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015

    Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
   Rais Kikwete akisalimiana na Balozi wa Ujerumani nchini ambaye ameshiriki katika mkutano huo na mabalozi wengine wengi
    Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
   Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa mabalozi ambaye  ameshiriki katika mkutano huo na mabalozi wengine wengi
    Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015.

    Rais Kikwete na viongozi wengine wakijiandaa kupata picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
    Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
  Rais Kikwete akiagana mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.

  0 0

   Baadhi ya wakimbizi wakiwa wamewasili Kigoma
   Wakimbizi kutoka Burundi wakisubiri huduma mbalimbali za kijamii
   Mmoja wa wakimbizi akiwa anapata matibabu
   Hapa watoto wa wakimbizi wakijipikia Chakula , katika mazingira hatarishi
   Mamia ya wakimbizi wakiwa wanatafakari hatima yao
   Hii ndio hali halisi ya vyoo ambavyo vimechangia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
  Wafanyakazi wa Shirika la Oxfam wakishusha vifaa kwa ajili ya vifaa vya upatikanaji wa maji na vyoo ili kubabiliana na Kipindupindu. 
   Hiki ni moja ya chanzo cha maji
   Wakimbizi wakiwa ndani ya Meli

  Ongezeko la wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi pamoja na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo maji safi linamaanisha kuongezeka kwa hatari ya mlipuko wa magonjwa ya kuambukizwa hasa kwa wakimbizi takribani 40,000 walioko Kagunga mpakani mwa Tanzania. 

  Tayari watu 20 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo ya Kagunga na katika kambi ya Nyarugusu ambapo wakimbizi hupelekwa kwa ajili ya makazi.

  Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) limeripoti uwepo wa watu 1057 wenye dalili za kuharisha waliopo Kagunga ambapo wakimbizi husubiria usafiri wa boti zinazowasafirisha kwenda Kigoma. 

  Kuna uhitaji wa haraka sana wa huduma za msingi ikiwemo maji safi na vyoo. Shirika la Oxfam linafanya kazi na shirika la TWESA ili kutoa ufumbuzi wa haraka kukidhi mahitaji hayo kwani kuna uhitaji wa haraka sana wa maji safi, huduma za matibabu pamoja na vyoo. 

  Shirika la Oxfam tayari limeanza maandalizi ya haraka ili kuongeza upatikanaji wa maji safi na kujenga vyoo vya dharura katika kambi ya Nyarugusu ili kukabiliana na ongezeko kubwa la wakimbizi. 

  Inakadiriwa takribani wakimbizi 22,000 wamesafirishwa kutoka Kagunga kwenda katika kambi ya Nyarugusu ambapo wanapewa makazi ya muda mfupi katika shule na makanisa wakati mashirika mbalimbali ya misaada yakiendelea kutoa vifaa vya ujenzi wa makazi ya muda mrefu. 

  Huduma za matibabu katika makambi ya wakimbizi zinasua sua kutokana na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa mbalimbali.

  Uhitaji wa haraka wa huduma za msingi ni muhimu ili kuzuia ongezeko la magonjwa yanayosambaa kama kipindupindu.   0 0

    Waziri  wa Maliasili  na  Utalii  Lazaro  Nyalandu  (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk (wa tatu kulia), wengine ni wawakilishi kutoka balozi huo. (Picha  zote na Loveness  Bernard)
  Waziri  wa Maliasili  na  Utalii  Lazaro  Nyalandu  akiwa  amebeba  ndoo  ya maji  kichwani  alipokuwa  akikabidhiwa  visima  33 vilivyochimbwa kwa msaada  wa Watu  wa Falme  za Kiarabu  na Balozi  wa Falme  hizo.
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifungua bomba la maji kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji katika Kata ya Olosokwani, Loliondo wilayani Ngorongoro, juzi. Mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya Falme za Kiarabu (UAE) ambayo imewekeza wilayani humo. Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa UAE nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk.
   WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akijindaa kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kata ya Olosokwani, ambako alizindua mradi mkubwa wa maji ya visima virefu wilayani Ngorongoro, juzi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro,Hashimu Shaibu.
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifurahia jambo na wakazi wa kijiji Olosokwani, baada ya kuzindua mradi wa maji wa visima virefu wilayani Ngorongoro juzi. Kushoto ni Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk.


  Na Loveness Bernard

  Wafugaji kutoka nchi za jirani  waliovamia katika eneo la Loliondo  wametakiwa kuondoa mifugo yao mara moja ili kuliacha eneo hilo kubaki na amani.

  Akizungumza na wananchi na wafugaji wa kijiji cha Ololosokwani, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema wakazi wa Loliondo wanauwezo wa kutatua migogoro yao wenyewe ila wanaosababisha migogoro hiyo isiishe na kuibuka mara kwa mara ni wageni wanaoingia katika eneo hilo na kuchungia mifugo yao.

  “Ninatoa tahadhali kwa wageni wanaoitazama loliondo kwa jicho la husda waache kufugia mifugo yao loliondo, kila mmoja afugie kwao ardhi ya loliondo ni ya wana loliondo na sio wageni” alisema Nyalandu.

  Alisema changamoto kubwa inayoikabili eneo hilo la Loliondo ni ongezeko la watu na mifugo wakati ardhi ikibaki kuwa ile ile.

  Nyalandu alisema kuna haja ya kuendeleza uhifadhi ili eneo la Loliondo liendelee kustawi na wageni waendelee kuja Loliondo ambapo watachangia utalii endelevu katika shughuli kama za utalii wa picha na uwindaji.

  Akizungumzia kuhusu miradi ya maji aliyoikabidhi kwa wananchi wa loliondo jana kutoka kwa Balozi wa Falme za Kiarabu waliofadhiri ujenzi wa miradi hiyo iliyogharimu sh bilioni 1.6 Waziri Nyalandu alisema hayo ni matunda  ya ushirikiano mzuri baina ya Rais Jakaya Kikwete na Mfalme wa Dubai Shekh Makthum na Jumuiya  ya falme za kiarabu.

  Alisema utekelezaji wa miradi hiyo ni ahadi ya Rais Kikwete kwa maeneo ya wafugaji ambapo alisema azma yake ni kuona tatizo la maji katika maeneo ya wafugaji linamazika na kuona mifugo na wafugaji wakinenepa.

  Aliwataka wananchi wa Loliondo kuitunza miradi hiyo kwa faida yao na mifugo yao huku wakitumia muda mwingi kwa kazi za maendeleo ya loliondo.

  0 0

  1
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ujio wa sheria mpya ya Takwimu  ya mwaka 2015 iliyopitishwa na Bunge Mwezi Machi mwaka huu leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi hiyo Bw. Morrice Oyuke.
  23
  Wadau mbalimbali na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ujio wa sheria mpya ya Takwimu  ya mwaka 2015.
  ………………………………………………………….
  Na. Veronica Kazimoto. Dar es salaam.
  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Sheria Mpya ya Takwimu ya mwaka 2015 haina lengo la kuzuia Taasisi au watu binafsi kufanya tafiti zao hapa nchini bali inalenga kuweka misingi imara ya shughuli za kitakwimu na tafiti zenye ulinganifu unaotokana na mfumo rasmi  utakaoondoa uwepo wa takwimu zinazokinzana.
   Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ujio wa sheria hiyo mpya iliyoridhiwa na Bunge Mwezi Machi mwaka huu.

  Amesema kuanzishwa kwa sheria hiyo kunalenga kutoa mwongozo kwa Taasisi za Serikali na Mashirika mbalimbali yanayozalisha takwimu hapa nchini ili yaweze kuendesha shughuli za ukusanyaji na usambazaji wa takwimu kwa kuzingatia sheria hiyo mpya na kuwa huru kutoa takwimu sahihi  zinazoendana na uhalisia wa Tanzania.

  “Sheria hii hailengi kuondoa uhuru wa taasisi nyingine za utafiti zilizopo kisheria kufanya kazi zao, taasisi hizo zitaendelea kuwa huru kufuata taratibu zao ilimradi hazikiuki sheria hii” Amesisitiza Dkt.Chuwa.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa. 
  Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ngabo Ibrahim, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Katikati ni Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji SSRA, Sarah Kibonde na kulia ni Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo, wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu jijini leo.


  0 0

  DSC_0369
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akiendelea na maongezi na ugeni huo ofisini kwake jijini Mwanza.
  DSC_0377
  Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia), akielezea nia ya Shirika lake kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji na dhuluma zinazofanywa jamii dhidi ya watu wenye albinism nchini alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo ofisini kwake jijini Mwanza.

  SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeahidi kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji na dhuluma zinazofanywa jamii dhidi ya watu wenye albinism. 

   Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues wakati akizungumza na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo.
   Mwakilishi huyo wa Unesco amesema hayo alipomtembelea Mkuu wa mkoa kumsalimia na kumweleza hatua zinazochukuliwana Unesco katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watu wenye albinism. 

   Akifafanua zaidi alisema kwamba UNESCO haijatenga fedha zitakazotumika kuendesha kampeni mahsusi bali itatumia uwezo wa kiufundi uliopo kwa wataalamu walionao na kwamba wanakusudia kuona kwamba miaka 15 ijayo watoto wanaozaliwa nchini Tanzania wanakuwa huru pasipo na viashiria vya kuhatarisha maisha vinavyosababishwa na mauaji ya watu wenye albinism. 

  Akimkaribisha Bi Zulmira ofisini kwake, Mkuu wa mkoa Magesa Mulongo alisema kwamba ingawa kuna utulivu katika kipindi hiki mkoani Mwanza, bado mkoa wake unaendelea kukabiliana na viashiria vinavyosababisha ukatili kwa watu wenye albinism na wazee.
   Bwana Magesa alisema imani potofu zilizopo zinazosadikika kufanikisha biashara za uvuvi wa samaki, uchimbaji wa madini na wanasiasa kuendelea na madaraka ni miongoni mwa sababu kubwa za mauaji hayo yaliyoitia doa jeusi jamii ya kitanzania nje ya mipaka.

   Alisema kwamba jitihada zinafanywa kukabiliana na imani hizo potofu kwa kuihamasisha jamii kutoziamini na kwamba madaraka na utajiri unatokana na juhudi, kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo. 

   Aidha amesema mkoa wake umekuwa ukihakikisha kwamba makundi yanayotumika kuua watu wengine kwa kushirikisha jamii yanavunjwa na pia kuwachukulia hatua kali wote wanaobainika kushiriki kwa njia moja au nyingine. 

   Hata hivyo mwakilishi wa umoja wa mataifa alisema kwamba hali ya amani  itatawala pale tu watu watakapobaini kwamba kuua ni ukiukwaji wa haki za binadamu na ni kosa la jinai. 

   Alisema pindi binadamu watakapokiri kwamba binadamu wote ni sawa na kuishi na albinism sio ‘mzimu’ watabadili mwelekeo mzima wa fikra potofu kimaisha na kuishi kwa amani na kuthaminiana. 

   Bi Zulmira alimwambia mkuu wa mkoa kwamba UNESCO kwa kushirikiana na wadau wengine wataendesha makongamano yenye lengo la kushirikisha jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayo changia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhuluma zinazofanya dhidi ya watu wenye albinism.

  0 0

   Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akitoa maelezo ya taarifa zake muhimu wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa Afisa Mwandikishaji Msaidizi Shaibu Chitala kwenye shule ya msingi Mbagala  Majengo B,jimbo la Mtama mkoani Lindi.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akichukuliwa alama za vidole wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwenye shule ya msingi Mbagala  Majengo B,jimbo la Mtama mkoani Lindi.
   Katibuwa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akipigwa picha na
  mwendeshaji wa mashine ya  wa BVR Mzee Mohamed   wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwenye shule ya msingi Mbagala Majengo B,jimbo la Mtama mkoani Lindi.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitia saini wakati wa kukamilisha taratibu za kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ,Mtama mkoani Lindi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha kadi yake mpya ya kupiga kura mara baada ya kumaliza kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura Majengo B, Mtama mkoani Lindi.
  Picha na Adam Mzee.
   Wananchi wa kitongoji cha Dodoma B,kijiji cha Majengo B wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
  Mkazi wa kijiji cha Majengo B,Mtama mkoani Lindi ,akipigwa picha kukamilisha taratibu za kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

  0 0

  PG4A5948
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, DKt. Fenella Mukangara akizungumza katika ibada ya kumwombea marehemu Samweli Chamulomo iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, eneo la Mlezi, Dodoma, Mei 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  4
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, DKt. Fenella Mukangara akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Samweli Chamulomo baada ya ibada ya kumwombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, eneo la Mlezi, Dodoma, Mei 20, 2015.
  5
  Mke wa Waziri mkuu,Mama tunu Pinda akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Samweli Chamulomo baada ya ibada ya kumwombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, eneo la Mlezi, Dodoma, Mei 20, 2015.

  6
  Baadhi ya Waandishi wa habari wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Samweli Chamulomo baada ya ibada ya kumwombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, eneo la Mlezi, Dodoma, Mei 20, 2015 7
  Mkurugenzi wa TBC, Clement Mshana akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Samweli Chamulomo baada ya ibada ya kumwombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, eneo la Mlezi, Dodoma, Mei 20, 2015.
  8910111213
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, DKt. Fenella Mukangara , akiweka shada la maua katika kaburi la mwandishi wa habari  wa TBC< marehemu Samweli Chamulomo yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kikuyu mjini  Dodoma, Mei 20, 2015.

  0 0

  Na. Andrew Chimesela – Morogoro.


  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajab Rutengwe ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kutumia sheria zilizopo katika kusimamia vema suala la usafi wa mazingira.


  Dkt. Rutengwe ametoa agizo hilo jana (19 Mei, 2015) wakati wa kikao maalum cha uhamasishaji wa kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira kilichofanyika katika ofisi za mkoa huo.


  Kiongozi huyo wa  ngazi ya mkoa alibainisha kuwa zipo baadhi ya sheria ambazo ni nzuri  na endapo zitafanya kazi mji wa Morogoro utakuwa safi  muda wote kwani sheria hizo zinaelekeza kila mwananchi kufanya usafi katika eneo analoishi.


  “Kila mwananchi anatakiwa kufanya usafi wa mazingira umbali wa mita kumi kila upande kutoka eneo analoishi, yaani mbele ya eneo lake, nyuma, kushoto na kulia kwa eneo lake, sheria, taratibu na kanuni za usafi zisimamiwe kikamilifu” alisema.


  Aidha, Dkt. Rutengwe alikwenda mbali zaidi ya kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa mazingira na kutaka juhudi zaidi zifanyike ili kung’arisha mji wa Morogoro hasa Manispaa ya Morogoro kwa kuwa Halmashauri hiyo ndio uso wa mkoa wa Morogoro.


  ’’Ndugu wadau, Mimi ninaheshimu sana mashindano haya lakini nimeona tuende zaidi ya mashindano ya usafi kwa kulenga mambo makuu yafuatayo;

  Kuufanya mji wa Morogoro kuwa kijani wakati wote (Greening), Kuupendezesha mji wa Morogoro wakati wote (Beutification) na Kuwa na uendelevu wa usafi baada ya mashindano”, Dkt. Rutengwe alisisitiza.


  Katika hatua nyingine Dkt. Rutengwe amewaomba Wanahabari Mkoani humo kutumia taaluma yao kuwaelimisha wananchi umuhimu wa usafi wa mazingira na hivyo kuuboresha mji wa Morogoro huku akiwataka Wasanii ambao ni wazawa wa mkoa huo nao wabuni na kutunga nyimbo zinazohamasisha, kuboresha na kutangaza vivutio vilivyoko katika Mkoa wa Morogoro.


  Naye Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Amir Nondo, alisema katika kuendeleza Usafi wa mazingira wa Manispaa ya Morogoro muda wote, kuna sheria ndogo ambazo wanazitumia.


  Nondo alibainisha kuwa moja ya sheria hizo ni kutoza faini ya shilingi elfu hamsini (Sh. 50,000/=) kwa kila mwananchi anayekamatwa akichafua mazingira kwa namna yoyote na faini hiyo anatozwa wakati huo huo.


  Aidha, alisema wanatoa motisha ya shilingi elfu ishirini na tano (Sh. 25,000/=) kwa mwananchi yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa wanaovunja sheria zilizopo na kuchafua mazingira ya halmashauri hiyo,


  Awali, wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kwenye kikao hicho, mbele ya wadau wa usafi wa mazingira Ofisa Afya wa Mkoa wa Morogoro Bwana Carle Lyimo alisema, lengo la kikao hicho ilikuwa ni kutoa mrejesho kwa viongozi wa Mkoa kazi zilizofanyika kwenye Kampeini ya Usafi wa Mazingira katika Mkoa wa Morogoro na kuongeza ushiriki kwa viongozi pamoja na jamii katika utekelezaji wa Kampeini hiyo. 


  Aidha, kikao hicho kililenga kujadili mikakati ya namna ya kuboresha usafi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa ili ifikapo wakati wa maadhimisho ya usafi kitaifa Mkoa uweze kushika nafasi ya juu kitaifa.


   Kwa Mkoa wa Morogoro Halmashauri zote zimekuwa zikishiriki kwenye mashindano hayo isipokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ambazo zimeanza kushiriki kwenye mashindano hayo mwaka 2014/2015.


  Takwimu zinaonesha Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imekuwa na rekodi nzuri katika mashindano hayo hususani miaka ya hivi karibuni kama inavyooneshwa hapa chini mwaka na nafasi iliyoshika kwenye mabano;


  Mwaka 2007 ilishika nafasi ya 18 kati ya Halmashauri 20, 2008 (15), 2009 (15), 2010 (12), 2011 (7), 2012 (12), 2013 (3) na 2014(3). mwaka 2015?


  Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira ilizinduliwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 5 Juni mwaka 2012 lengo likiwa kuboresha miundo mbinu ya usafi wa mazingira katika ngazi ya kaya na shule ili kuweza kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa ambapo mashindano hayo ya Usafi Kitaifa yanatarajiwa kufanyika tarehe 5 Juni mwaka huu. 

older | 1 | .... | 531 | 532 | (Page 533) | 534 | 535 | .... | 1903 | newer