Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Mafuriko Dar es Salaam ni ushahidi wa athari za mabadiliko ya tabianchi

$
0
0
Mvua zinazoendelea kunyesha nakusababisha mafuriko na hasara kubwa jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini zimetajwa kuwa ni moja ya ushahidi wa udhaifu wa miundombinu ya kweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo ni janga kubwa duniani kwa sasa. Haya yalisemwa na FORUMCC; shirika linalijihusisha na masuala ya mabadiliko ya Tabianchi.

Watu zaidi ya 12 wameripotiwa kupoteza maisha mpaka sasa kutokana mafururiko hayo ambayo yameibua hisia na maswali mengi kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wengi wakihoji nani wa kulaumiwa kutokana na mafuriko hayo.

Afisa Miradi, Fazal Issa kutoka shirika la ForumCC ameitaka serikali na watu binafsi kuchukua hatua thabiti katika kukabiliana na mafuriko haya ambayo yanasababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema kuwa serikali na taasisi zake imekuwa na kawaida ya kuchukua hatua mara baada ya madhara kutokea badala ya kuweka mikakati ya muda mrefu ya kukabiliana na viashiria vya athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Taasisi zenye majuku ya kutoa tahadhari na kushughulikia majanga hasa ya mafuriko, mamlaka zinazohusika na ujenzi wa miundombinu katika jiji la Dar es Salaam, ukusanyaji na utoaji wa taka zinapaswa kufanyakazi kwa kushirikiana ili kutafuta suluhisho la kukomesha maafa haya kabla hayajaleta athari kwa watu” alisema Issa.

Alisema hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwani utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini unaonyesha kuwa mvua kubwa zitaendelea kunyesha hadi Mei 20 mwaka huu, hivyo kuwataka wananchi kutotupa taka hovyo na kufanyia usafi mifereji katika maeneo yao.

“Badala ya kulalamika na kuhoji nani wa kulaumiwa kutokana na mafuriko yanayojirudia jiji la Dar es Salaam, ni jambo la busara sasa kwa kila mwananchi kuwajibika katika nafasi yake katika kuzuia au kupunguza kutokea kwa mafuriko hayo” alisema Issa.  

Kwa upande wake Afisa Habari wa ForumCC, Tajiel Urioh Aliwataka Watanzania kutambua kuwa mvua na mafuriko makubwa yanayoendelea kutokea Dar es salaam na maeneo mengine yanamahusiano mkubwa na ongezeko la Joto duniani.

“Watu wanapuuza na kuchukulia mzaha mabadiliko ya tabianchi lakini wanapaswa kujifunza kutokana na mafuriko haya ambayo mbali na kusababisha vifo pia yameharibu miundombinu ya barabara, nyumba, madaraja” alisema Urioh 

Tafiti zinaonyesha kuwa joto limeongezeka kwa 0.850C duniani huku kwa Tanzania Joto likiongezeka kwa 10C tangu mwaka 1961 jambo ambalo linasababisha baadhi ya maeneo kupata mvua zinazozidi kiwango na kuwa na majanga kama vile mafuriko, vimbunga na ukame. 

Hata hivyo, repoti ya Jopo la wanasayansi duniani (IPCC 2007) inaonyesha, ili kukabiliana na uharibifu unaosababishwa na mafuriko, inategemea sana na mipango thabiti ya mipango miji, jinsi ya kutumia ardhi, ubora wa kuweza kutabiri kutokea kwa mafuriko, utoaji taarifa na jinsi ya kuchukua hatua.

Mafuriko ya namna hii yaliyoleta athari kubwa ni yale yaliyotokea mwaka 2011 katika Jiji la Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu  arobaini (40) huku yakiharibu vibaya miundo mbinu ya barabara, madaraja na makzi ya watu.


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Dk. Rehema Nchimbi afungua kikao kazi cha biashara ya kilimo

$
0
0
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Dk. Rehema Nchimbi akifungua kikao kazi cha biashara ya kilimo kwa kongani ya Ihemi iliyoandaliwa na SAGCOT (Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania) kwa ushirikiano na UONGOZI Institute (Taasisi ya Uongozi Afrika kwa Maendeleo Endelevu) mapema leo Iringa mjini. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kilimo wa TCCIA Bi. Magadalena Mkocha, Mwenyikiti wa Bodi ya Agricultural Council of Tanzania Dk. Sinare Y. Sinare, DC wa Iringa Mh. Angeline Mabula, DC wa Mufindi Mh. Mboni Mhita na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Philemon Luhanjo. 
 Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Philemon Luhanjo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya UONGOZI Institute akitoa salaam kwa niaba ya taasisi hiyo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha biashara ya kilimo kwa kongani ya Ihemi inayoendelea Iringa mjini. UONGOZI Institute imeshiriki katika kuwezesha kikao kazi hicho.
  Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Bw. Geoffrey Kirenga akitoa utangulizi wa mada ya biashara ya kilimo kwa nyanda za juu kusini. Mkutano huu wa siku mbili unakutanisha  viongozi wa serikalini, sekta binafsi, mashirika ya kimataifa pamoja na wakulima kwa ajili ya kujadili kuhusu kuboresha biashara ya kilimo nchini kwa nyanda za juu kusini.
 Picha ya pamoja ya wageni waalikwa na washiriki wa kikao kazi cha biashara ya kilimo inayoendelea Iringa mjini. Mada zinazojadiliwa ni pamoja na wajibu wa viongozi katika kuleta mageuzi katika kilimo. 

NCCR-MAGEUZI WASHAMBULIA JIMBO LA VUNJO

$
0
0
Mwenyekiti wa kitengo cha kina mama Jimbo la vunjo na Katibu wa Chama cha NCCR Mageuzi kata ya Kilema, Leah Mudy akizungmza wakati wa mkutano uliofanyika katika eneo la Lyamombikatika jimbo la Vunjo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo ,Dauson Lyimo akizungumza katika mkutano huo.
Mjumbe wa Mkutano mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi taifa,Hemed Msabaha akihutubia katika mkutano huo.
Wananchi wakijibu salamu ya chama hicho.
Baadhi ya wananchi wakirejesha kadi za vyama mbalimbali wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lyamombi.
Baadhi ya kadi zilizo rejeshwa. Na Dixon Buagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini,

Maofisa wanane wa Benki Kuu Tanzania (BOT) kizimbani kwa mashitaka 14 ya kufoji vyeti vya kidato cha nne

$
0
0
Habari na Mwene Said wa Globu ya Jamii .
 Maofisa wanane wa Benki Kuu Tanzania (BOT) wamekutwa na kesi ya kujibu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salam, dhidi ya mashitaka 14 ya kughushi na kuwasilisha vyeti vya kidato cha nne vilivyoghushiwa. 
 Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao, dhidi ya washtakiwa Justina Mungai, Christina Ntemi, Siamini Kombakono, Janeth Mahengena Beatha Masawe, Jacquiline Juma, Philimina Mutagurwa na Amina Mwinchumu. 

 Hakimu Mwaseba alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wa Jamhuri bila kuacha shaka washtakiwa wana kesi ya kujibu na kwamba wanatakiwa kupanda kizimbani kujitetea dhidi ya mashitaka yao.
Hakimu alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa utetezi wao Juni 16 hadi 17, mwaka huu. Watumishi hao wa Benki Kuu wanadaiwa kuwa katika kitengo cha kuhesabu fedha vya BoT. Mapema Septemba 19, mwaka 2008, upande wa Jamhuri uliwasomea washtakiwa hao mashitaka yao . 
Ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2001, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Mungai alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba S.342/43 kilichotolewa Februari 26, 1980. 
Aidha, ilidaiwa kuwa cheti hicho kilitolewa na Baraza la Mitihani la Taifa. 
Katika shtaka la pili, mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2001, jijini, aliwasilisha cheti hicho huku akijua ni cha kughushi.
 
Katika shtaka la tatu na nne, ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2002 jijini, mshtakiwa wa pili alighushi cheti cha kidato cha nne chenye namba za usajili S.0222/42 kikionyesha kimetolewa Novemba 26, mwaka 1999 na kwamba aliwasilisha Benki Kuu. 
Katika shtaka la tano na sita, ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2001 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Komakono, alighushi cheti cha kidato cha nne chenye namba za usajili S.238-0076 kilichotolewa Machi 14, mwaka 1997 akionyesha kuwa kimetolewa na Baraza la Taifa ambapo walikiwasilisha Benki Kuu. 
Upande huo wa Jamhuri uliendelea kudai kuwa katika shtaka la saba na nane, mshtakiwa wa Mahenge, anadaiwa kuwa alighushi cheti cha kidao cha nne, chenye namba za usajiliS.311/0071 kikionyesha kimetolewa Machi 14, mwaka 1997, na Baraza la Taifa ambapo aliwasilisha benki kuu. 
Aidha, shtaka la tisa na kumi, ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika jijini, mshtakiwa Massawe, anadaiwa kuwa 2001 benki kuu, alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba za usajili S.331/0071 kikionyesha kimetolewa Aprili 22, mwaka 2000, na Baraza la Taifa ambapo alikiwasilisha Benki Kuu. 
Ilidaiwa kuwa, shtaka la 11 na 12, mshtakiwa Juma, anadaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2000 jijini, alighushi cheti cha kidato cha nne chenye namba za usajili S.375/020 kikionyesha kimetolewa Machi 14, mwaka 1999 na Baraza la Taifa ambapo alikisilisha Benki Kuu. 
Pia, shtaka la 13 na 14, mshtakiwa Mutagurwa anadaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2002, alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba za usajili S.0764/0012 kikionyesha kimetolewa Machi 14, mwaka 1997 na Baraza la Taifa ambapo alikiwasilisha Benki Kuu. Katika shtaka la 15 na 16, mshtakiwa Mwanchungu anadaiwa kuwa siku isiyofahamika, 2001 jijini, alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba za usajili S.0307-004 kikionyesha kimetolewa Machi 28, mwaka 1991 na Baraza na Taifa, ambapo aliwasilisha Benki Kuu. Washtakiwa wote walikana mashtaka yao na wako nje kwa dhamana. 

RAIS WA MSUMBIJI AWASILI ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume akiwa nchini kwa ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi alipokuwa akisalimiana na Mawaziri wa Zanzibar mara alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume akiwa nchini kwa ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitambulishwa na Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi aliposalimiana na Mawaziri mbali mbali wa Serikali ya Msumbiji walioungana na Rais Filipe mara baada ya mapokezi walipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume kwa ziara ya kikazi Nchini.
Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi akikagua Gwaride la JWTZ mara baada ya kupokea salamu ya Heshma alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume akiwa nchini kwa ziara ya kikazi wakati wa mapokezi yake ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi mbali mbali walifika uwanjani hapo kwa mapokezi maalum.
Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi akiangalia ngoma ya kibati akiwa naMwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume akiwa nchini kwa ziara ya kikazi.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya mapokezi akiwa na ujumbe wake walipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume akiwa nchini kwa ziara ya kikazi.
Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi akipokea salamu ya Heshma ya Gwaride la JWTZ akiwa naMwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume akiwa nchini kwa ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi alipofika Ikulu Mjini Zanzibar katika ziara ya kikazi nchini akiwa na ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar katika ziara ya kikazi nchini akiwa na ujumbe wake,[Picha na Ikulu.] 

NENO LA SHUKURANI KUTOKA KWA FAMILIA YA BWA UWESU MASUMI WA MBEZI BEACH JIJINI DAR

$
0
0
Familia ya  Bw. Uwesu Y.Mssumi wa Mbezi Beach Dar es Salaam inatoa shukurani za dhati kwa ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa   misaada ya hali na mali wakati  na maobolezo na  hatimaye mazishi ya mke wake mpendwa  Mwalimu  Hidaya U. Mssumi  ( mama ya Fatuma, Mwanana, Bibie na Mariam) kilichotokea  tarehe 27 April na kuzikwa tarehe 28 April, 2015.

Shukurani za pekee ziwafikie wanajumuiya wa masjid Akram, Taqwa, Noor  na Fauz  Mbezi Beach, masjid Maamur- Upanga, Dr. Halid Gongoro, Ofisi za CCM Mkoa wa Pwani na  wilaya ya Rufiji,  Menejiment za kampuni ya Export Trading Group,  Mgodi wa Acacia North Mara, Chuo Kikuu Dodoma na Takukuru Mkoa Manyara bila kuwasahau wanafunzi waliomaliza shule ya msingi Muhimbili mwaka 1988.

Haitakuwa rahisi kuwataja wote waliotusaidia na kushirikiana nasi ila kwa ujumla wenu tunawashukuru sana kwa  kutupa faraja wakati wa kipindi hiki kigumu.

Tunawakaribisha na tunaomba tushirikiane nanyi katika arobanini ( Duah) ya kumwombea marehemu itakayofanyika tarehe 6 Juni, 2015 baada ya swala ya Adhururi ( saa saba mchana) . Duah hii itafanyika nyumbani Mbezi Beach kitalu J   plot na 229/30 mtaa wa Mufindi  (off Mwai Kibaki Road)  
Inna Lilah waina Lilah Rajuhun.

UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU HAPA NCHINI

$
0
0
Godfrey Haongo mkufunzi kutoka Open University nchini Tanzania akitoa elimu ya njia ya mtandao.
Head of India Tanzania Center of Excellence in ICT (DIT), Dr. Amos Nungu akiwakaribisha wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), wakufunzi pamoja na walimu waliofika kwenye mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao.(Picha zote na Geofrey Adroph wa pamoja blog).
Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo akimkaribisha Ofisa anayeshughulikia na masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (wa kwanza kutoka kushoto) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao kwa walimu wa vyuo vya elimu
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari akifungua mafunzo kupitia njia ya mtandao iliyoandaliwa na UNESCO yaliyofanyika jijini Dar.
Bi. Eunice Gachoka kutoka Kenya Institute of Curriculum Development akijitambulisha kwa walimu (hawapo pichani) waliofika kwenye mafunzo ya kupitia mtandao.
Daudi Mbona mkufunzi kutoka chuo cha DIT akiendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya walimu walioudhuria mafunzo ya kupitia njia ya mtandao yaliyofanyika kwenye chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) hapa jijini Dar.

Baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo.Na Geofrey Adroph, Pamoja blogUNESCO imeaandaa mafunzo ya uboreshaji wa elimu kwa walimu hususani katika somo la Tehama kwa vyuo mbalimbali vya hapa nchini vinavyotoa elimu ya ualimu. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania yamefanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) ili kuweza kuwapa fursa hiyo waalimu wa vyuo mbalimbali katika ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya Tehama. Hii inatokana na baada ya mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini Tanzania hivyo kuona kama kuna mapungufu katika masuala la uelewa na matumizi ya Tehama hasa katika vyuo hivyo.Baada ya kuona kuna mapungufu hayo UNESCO waliamua kuanzisha mradi uitwao UNESCO-China Funds in Trust Project (CFIT) wakishirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini Tanzania waliamua kuanzisha mradi huo kwa malengo makuu matatu ambayo ni kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu wanapofundisha katika Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuwanunulia vifaa vya Tehama ambavyo vitasaidia katika kufundishia na kujifunzia, Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo alivitaja vifaa hivyo kwa kuviorodhesha kuwa ni pamoja na kompyuta, Projecta, na Sola ili kuhakikisha hakuna tatizo la umeme katika ufundishaji wa masomo hayo .Kupitia mradi huo wa (CFIT), UNESCO imeandaa mafunzo ya siku tano kwa walimu wa vyuo vya ualimu kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu hapa nchini Tanzania ili kuongeza ujuzi na ufanisi katika ukuzaji wa Tehama hasa kupitia kwenye njia ya mtandao na pia kuendana na wakati kutokana na mabadiliko pamoja na ukuaji wa matumizi ya Teknolojia Mafunzo haya yaliyoandaliwa na UNESCO yanafanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa ajili ya kuwapa elimu kwa baadhi ya walimu wa vyuo ili kupata uelewa zaidi juu ya Tehama.Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Daudi Mboma ambaye ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka (DIT) na Godfrey Haongo kutoka Open University of Tanzania ambao wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa .Waalimu tisa kutoka chuo cha ualimuTabora, waalimu tisa kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne kutoka chuo cha ualimu Morogoro, mmoja kutoka Shule direct, wawili kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso District, pia kuna baadhi ya watakao pata mafunzo hayo wanatokea Wizara ya elimu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano na UNESCO ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini.Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma za kitehama katika taifa la Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.

KIKAO CHA BAJETI CHA OFISI YA RAIS UTUMISHI

$
0
0

Watendaji wa Ofisi ya Rais wakisikiliza uwasilishaji wa Bajeti ya Ofisi ya Rais kupitia Runinga.
 5&6 MAELEKEZO: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) pamoja na Waheshimiwa Mawaziri walio Ofisi ya Rais, wakikutana na watendaji wa Ofisi ya Rais wakati wa kuwasilisha bajeti ya Ofisi ya Rais Bungeni-Dodoma.

RAIS KIKWETE kufungua mkutano wa Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete anatarajia kufungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa  Shughuli za Serikali kwa uwazi (OGP).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu inaeleza kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” utafanyika Mei 20 hadi 21, 2015 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Aidha, imeeleza kuwa dhumuni la  mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uwajibikaji na utawala wa Serikali ili kutoa mrejesho kwa wananchi pamoja na uwazi kuhusu masuala ya ardhi.

“Kupata uzoefu wa utekelezaji wa OGP kutoka nchi wanachama katika bara la Afrika nan je ya Afrika kama vile taarifa za uwazi zinazoimarisha uwajibikaji” iliongeza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema  kuwa mkutano huo ni wa kwanza kufanyika nchini Tanzania na ni wa pili kwa Kanda ya Afrika ambapo kwa mara ya kwanza  ulifanyika nchini Mombasa nchini Kenya mwaka 2013.

Mkutano huo unatarajiwa kuwa na washiriki 200 kutoka Serikalini, Asasi za kirai, Washirika wa Maendeleo wakiwemo Mawaziri kutoka ndani na nje ya nchi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa baadhi ya Taasisi za Serikali, wawakilishi kutoka Nchi wanachana wa OGP kutoka bara la Afrika.

Washiriki wengine ni kutoka nchi za Botswana, Zambia, Uganda, Marekani, Zimbabwe pamoja na washirika wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia, UNDP, UNICEF, UNESCO, MCC, USAID, DFID na JICA.

Uandikishaji Wanachama 'Tanzania Bloggers Network' (TBN),

$
0
0
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN kilichosajiliwa rasmi na Serikali Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. 

Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo ambayo ipo hai. Kwa wakazi wa Dar es Salaam wenye sifa na wanataka kujiunga na TBN fomu zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. 

Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media Group, mjini Jengo refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili. 

Kwa wanachama wa mikoani juu na namna ya kujiunga wasiliana nasi kwa barua pepe; mushijoa@gmail.com  au  piga namba; 0756469470. 

Kwa wanaoitaji kujiunga mnaombwa kuchukua fomu mapema kabla ya zoezi la usaji lililoanza 22 Aprili, 2015 halijafungwa.

NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo wataigharamia wenyewe. Hata hivyo utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy katiba hiyo na itatumwa mikoani kwa gharama za TBN. 

Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470 
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

MBUNGE FILIKUNJOMBE AKIPIGA KAZI LUDEWA

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana na Wapigakura wake kushusha rola la Nyaya za umeme kwenye kijiji cha Luhana kata ya Luana wilayani Ludewa  jana kwa ajili ya mradi wa umeme  vijijini ambapo kijiji hicho pia kinatarajiwa kupata umeme  hivi karibuni.
 Mbunge jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana na wapiga kura wake kushusha Transfoma jana kwa ajili ya kufungwa kwenye mradi wa umeme unaotekelezwa kwenye  kijiji cha Luana wilayani Ludewa mkoani Njombe. 

SELCOM YAWEZESHA MALIPO YA PANGO YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Selcom Tanzania Sameer Hirji akimuonyesha mashine ya POS ya Selcom Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu. Mashine hizo zitatumika katika ulipaji wa kodi za majengo ya NHC.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Selcom Tanzania Sameer Hirji akimuonyesha risiti za malipo ya pango za nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa malipo kwa njia ya mtandao wa Selcom
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Selcom Tanzania Sameer Hirji akielezea kwa waandishi wa habari jinsi huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya Simu na akaunti za Benki inavyofanya kazi.


BENKI YA DCB YATOA ZAWADI KWA WAFANYAKAZI NA MATAWI YALIYOFANYA VIZURI JULAI HADI DESEMBA 2014

$
0
0
 
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Raymond Mushi akizungumza na wadau mbalimbali wa benki ya DCB wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya Mwenyekiti wa Bodi ya DCB kwa Tawi lililofanya vizuri kwa mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2014.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya DCB,Balozi Paul Rupia akizungumza jambo kwa niaba ya benki hiyo na kwa niaba ya kumkaribisha mgeni rasmi,Mkuu wa Wilaya ya Ilala.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB,Bw.Edmund Mkwawa akipokea cheti cha kutambulika katika mafunzo ya Ukurugenzi wa benki hiyo. 

 Meneja Masoko wa benki ya DCB,Boyd Mwaisame(kulia) akipokea cheti cha utumishi wa muda mrefu na maendeleo ya benki ya DCB kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Raymond Mushi.

 Baadhi ya wadau na wafanyakazi wa benki ya DCB wakiserebuka kwa pamoja katika hafla ya kukabidhi zawadi ya Mwenyekiti wa Bodi ya DCB kwa Tawi lililofanya vizuri kwa mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2014.

  
Na Bakari Issa.


Wanahisa na wadau mbalimbali wametakiwa kuitumia kikamilifu benki ya DCB ili kuiwezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa benki hiyo.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Raymond Mushi katika hafla ya kukabidhi zawadi ya Mwenyekiti wa Bodi ya DCB kwa Tawi lililofanya vizuri kwa mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2014.


Katika hafla hiyo,Mhe.Mushi ameisifu benki hiyo ya DCB kutoa huduma zake kwa njia ya kisasa(Mtandao wa Intaneti) na kusema kuwa ni benki ambayo huduma zake ndiyo silaha kubwa katika ushindani wa mabenki.


Pia,amewahimiza wafanyakazi na matawi ya benki hiyo kufanya kazi kwa ari na nguvu mpya ili waweze kufanya vizuri ili baadae wapate zawadi kama wafanyakazi wa tawi la Ukonga walioshika nafasi ya kwanza kwa asilimia 80 kwa mwaka 2014.


Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,Bw.Edmund Mkwawa amesema benki imepata faida ya Sh.3.7Bilioni kwa mwaka 2013 kutokana na ongezeko la matawi kama tawi la Kariakoo,Mabibo na Chanika.


Hata hivyo,Mkwawa ameyataja matarajio ya benki hiyo kwa mwaka 2015,kuwa ni kuongeza amana kwa (33%),kuongeza mikopo kwa wateja pamoja na kutoa huduma bora naza haraka zaidi kwa wateja. 

UCHAGUZI MKUU WA BMT KUFANYIKA JUNI 10 MWAKA HUU.

$
0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limesogeza mbele siku ya kufanya uchaguzi  wa Chama cha Mchezo wa Vinyoya Tanzania (TBA) ambapo unatarajiwa kufanyika 10 Juni mwaka huu katika ukumbi wa Baraza hilo.

Hayo yamesemwa na  Afisa habari Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Najaha Bakari wakati akizungumza na Mwandishi wetu kwa Njia ya simu.

 Pia Najaha amesema kuwa Baraza hilo linaongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu za Uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Mchezo wa Vinyoya Tanzania   (TBA) hadi  Juni 5 mwaka huu.

Amesema kuwa Fomu zinapatikana ofisi za Baraza la Michezo na kwenye tovuti ya Baraza, gharama ya  fomu ni shilingi elfu 10,000/=,Amesema kuwa nafasi ya Mwenyekiti nafasi 1,Makamu Mwenyekiti nafasi 1,Katibu Mkuu nafasi 1,Katibu Mkuu Msaidizi nafasi 1,Mweka Hazina nafasi 1,Mweka Hazina Msaidizi nafasi 1na Wajumbe nafasi tano  wakuchaguliwa.

WAFUGAJI WAPATIWA NA TAWLA ELIMU YA KISHERIA NA USHAURI

$
0
0
Mwenyekiti wa wasaidizi wa kisheria wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Ibramih Melita akizungumza na wafugaji wa kijiji cha Nanja kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa kisheria yaliyotolewa na Chama cha wanawake wanasheria nchini (TAWLA) jana.
 Askari wa dawati la jinsia na watoto wa Mkoa wa Arusha, Baltazar Kitiku akizungumza na jamii ya wafugaji wa Kijiji Cha Nanja, Kata ya Lepruko Wilayani Monduli Mkoani humo, kuhusiana na kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia kwenye mafunzo yaliyotolewa na Chama cha wanawake wanasheria nchini (TAWLA) kwenye maadhimisho yao ya miaka 25.
 Jamii ya wafugaji wa Kijiji cha Nanja Kata ya Lepruko Wilayani Monduli Mkoani Arusha, wakiwasikiliza wanasheria wa Chama cha wanawake wanasheria nchini (TAWLA) Tawi la Arusha, ambao wameadhimisha miaka 25 ya kuanzishwa kwa chama hicho kwa kutoa elimu na ushauri wa kisheria jana kwenye vijiji vya Nanja na Meserani (Duka bovu) Wilayani Monduli.
Baadhi ya jamii  ya wafugaji wa Kijiji cha Nanja, Kata ya Lepruko Wilayani Monduli Mkoani Arusha, wakiwasikiliza wanasheria wa Chama cha wanawake wanasheria nchini (TAWLA), ambao jana walitoa elimu na ushauri wa kisheria kwenye kijiji hicho.

RAIS WA MSUMBIJI AHUTUBIA WANA CCM MJINI DODOMA LEO

$
0
0

 Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akihutubia kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akijaribu kofia ya CCM ikiwa sehemu ya zawadi alizopewa na CCM.
 Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi pamoja na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akiwaaga wana CCM mara baada ya kuwahutubia ambapo alisisitiza kuwa Frelimo itaendelea kudumisha mshikamano wao na CCM.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.
 Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akisalimiana na wanachama na wapenzi wa CCM waliojitokeza kumpokea na kumkaribisha Dodoma.
 Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akivishwa skafu na vijana wa Chipukizi wa CCM mkoa wa Dodoma wakati wa mapokezi kwenye Makao Makuu ya Chama.

 Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ,pamoja na viongozi wengine wa CCM mkoa wa Dodoma wakiimba wakati wa kumkaribisha Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi kwenye makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa neno la kumkaribisha Rais wa Msumbiji na Mwenyekiti wa Chama cha Frelimo Mhe. Filipe Nyusi kwenye makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Msumbiji kuhutubia viongozi mbali mbali wa CCM wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu
 Mpigania Ukombozi wa Msumbiji Mzee Aberto Chipande akizungumza kabla ya Rais Filipe Nyusi kuhutubia wana CCM ambapo alielezea namna harakati za kuikomboa nchi yao zilivyoanza, kupangwa na kuratibiwa Kongwa Dodoma na kuanza safari ya kuelekea vitani mwaka 1963 na kusema Dodoma ni nyumbani kwake.
 Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu, Viongozi wa CCM mkoa wa Dodoma pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Rais Filipe Nyusi kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.

NHC Yafungua Rasmi Kituo Cha Huduma Kwa Wateja

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.

Mkurugenzi waShirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Mkurugenzi waShirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Wakurugenzi wa Shirika hilo wakishuhudia tukio la kuzinduliwa kwa tukio hilo
Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
Picha zaidi za tukio la uzinduzi huu tutawaleteeni baadaye.

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA KWA NJIA YA SIMU NA MALIPO YA KODI KWA MFUMO WA SIMU ZA KIGANJANI – MEI 19, 2015
.................................................................................................
Katika jitihada za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuboresha huduma kwa wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja, leo Shirika la Nyumba la Taifa linazindua huduma mbili, ambazo ni kituo cha huduma kwa wateja na pili ni mfumo wa kulipa kodi za nyumba kwa kutumia simu ya kiganjani.

Kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kitatumika kuhudumia wateja wetu wote kwa kupiga simu pale wanapohitaji kufahamu juu ya huduma zetu na bidhaa mbalimbali pamoja na kutoa taarifa mbalimbali za shirika zinazohusu huduma kwenye makazi yao. Wateja wataweza kupata huduma hii kupitia nambari +255 784 105 200 na + 255 222 162 800. Kupitia kituo hiki Shirika linawaahidi kwamba maulizo na taarifa zozote zitakazoripotiwa zitapewa kipaumbele kwa kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Katika kuendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji kodi kutoka kwa wapangaji wetu, Shirika limeanzisha mfumo wa kulipa kodi kupitia simu za kiganjani ili wapangaji waweze kufanya malipo ya kodi zao bila ya usumbufu wowote kupitia tigopesa, mpesa na airtel money.

 Kupitia mfumo huu, wapangaji wataweza kufanya malipo kwa kutumia simu zao na wataweza kuhamisha fedha kutoka kwenye benki akaunti zao na kwenda Shirika la Nyumba mahali popote walipo na kwa muda wowote ambao ni muafaka kwao bila ya kufika katika vituo vyetu vya makusanyo ya kodi.

MANISPAA YA KINONDONI YAENDELEA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA KUONDOA MAJI KATIKA MAKAZI YA WATU TEGETA,BUNJU NA KUNDUCHI NA KUJENGA MFEREJI WA KUDUMU KUPITISHA MAJI YA MVUA KUELEKEA BAHARI YA HINDI

$
0
0
AT1
Mkuu wa mkoa wa Dar es slaam,Saidi Meck Sadiki(katikati) akiangalia athari ya maji yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar es slaam akiwa ameambatana na wakazi wa eneo hilo la Kunduchi Ununio.Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na DAWASA inaendelea na zoezi la kuyaondoa maji hayo pamoja na ujenzi wa mfereji mkubwa kuelekea baharini utakaokusanya maji kutoka Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya Hindi.AT2
Kazi ya ujenzi wa mfereji huo mkubwa wenye urefu wa kilometa 2.1 ikiendelea katika eneo la Kunduchi Ununio.AT3
Maji yaliyotuama yakiwa bado yamezingira nyumba na makazi ya watu eneo la Boko jijini Dar es salaam ambayo harakati za kuyaoondoa zinaendelea kufanywa na manispaa ya Kinondoni.AT4
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki ( katikati ) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Musa Nati wakati akikagua utekelezaji wa zoezi la kuondoa maji katika makazi ya watu eneo la Basihayo Tegeta.

………………………………………………………………….
Na.Aron Msigwa- MAELEZO
.Dar es Salaam.
Manispaa ya Kinondoni inaendelelea kujenga mfereji wa kudumu wenye urefu wa Kilometa 2.1 ili kuondoa maji yaliyojaa kwenye makazi ya watu, eneo la Basihayo -Tegeta,Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya Hindi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa hivi karibuni mara baada ya kuwatembelea wananchi katika maeneo hayo walioathiriwa na mafuriko.
Akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo kujionea utekelezaji wa agizo hilo leo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki amesema kazi ya ujenzi wa mfereji huo utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 900 inafanyika kwa kasi inayoridhisha licha ya ugumu uliopo wa kutafuta uelekeo wa maji hayo kutoakana na uwepo wa makazi ya watu.
Amesema ujenzi wa mfereji huo mkubwa unakwenda sambamba na kazi ya uondoaji wa maji ya mvua yaliyojaa katika makazi ya watu katika eneo la Basihaya inayofanywa na Shirika la maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam huku Manispaa ya Kinondoni chini ya usimamizi wa Muhandisi wake Baraka Mkuya ikiendelea na uchimbaji wa mfereji wa juu na ule utakaopita chini ardhi kuelekea baharini.
Amesema kuwa katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa ufanisi mkubwa bila kuathiri makazi ya watu na kulazimika kulipa fidia kwa wananchi Manispaa hiyo inaendelea kuzungumza na baadhi ya wananchi ambao maeneo yao yatatumika kupitisha mfereji huo waruhusu kazi hiyo iendelee huku taratibu nyingine zikiendelea kufanyika.
Aidha amesema kwa baadhi ya wananchi waliojenga kuta na nyumba kwenye mkondo wa maji hususani eneo la Kunduchi Ununio na kuzuia maji kuelekea baharini maeneo yao yatabomolewa na baadhi ya hati za viwanja kufutwa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mussa Nati akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo kushuhudia zoezi la uondoaji wa maji na ujenzi wa mfereji huo amesema kuwa fedha zinazotumika katika kazi hiyo zinatolewa na manispaa ya Kinondoni, na kazi hiyo itafanywa na wataalam wa Manispaa hiyo na kufafanua kuwa kukamilika kwake kutaondoa adha ya muda mrefu ya mafuriko waliyokuwa wanaipata wakazi hao kipindi cha mvua.
“Manispaa ya Kinondoni tumetenga kiasi cha shilingi 900 kwa ajili ya kufungua maji na kujenga mifereji ya kudumu inayoelekea baharini katika ili wananchi waweze kuishi bila usumbufu wowote,na kazi hii tutaimaliza ndani ya mwezi mmoja” Amesisitiza.
Naye Muhandisi wa Manispaa hiyo Baraka Mkuya amesema kuwa kazi ya uondoaji wa maji na ujenzi wa mifereji ya wazi na ile inayopita chini ya ardhi kutokea eneo la Basihayo Tegeta na kukatisha barabara ya Bagamoyo kuelekea bahari ya Hindi urefu wa kilometa 2.1 itakamilika ndani ya mwezi mmoja.
Kwa upande wao madiwani wa eneo hilo Bw.Majisafi Sharifu,Diwani wa Kata ya Bunju (CHADEMA) na Bi.Janet Lite kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema kazi ya utekelezaji wa agizo la Rais la ujenzi wa mfereji huo inakwenda na kueleza kuwa itakuwa faraja kwa wakazi wa kata hizo kutokana na adha kubwa ya mafuriko ya maji waliyokua wanaipata wakati wa msimu wa mvua.

MATUKIO BUNGENI LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri Mkuu, Mstaafu, Edward Lowassa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 19, 2015. pin1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge  kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 18, 20154, Victor Mwambalaswa wa Lupa, Sylvester Mabumba  wa  Dole na Dkt. Hamisi Kigwangalla wa Nzega. pin2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 18, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

VIONGOZI MBALIMBALI WAJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA MASHAURIANO KUHUSU AMANI, UMOJA NA UTULIVU WA NCHI YETU

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungungumzwa katika mkutano wa siku mbili wa mashauriano kuhusu amani, umoja na utulivu wa nchi yetu ulioanza leo ambao utamalizika kesho. Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), ulifanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam leo asubuhi.
 Brigedea Jenerali mstaafu, Francis Mbena akihutubia kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia.
 Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Jaji mstaafu, Joseph Warioba, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo, Salim Ahmed Salim,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, Brigedea Jenerali mstaafu, Francis Mbene na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.
 Viongozi wakiwa kwenye mkutano huo.

 Viongozi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Viongozi wa vyama vya siasa wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Willibrod Slaa.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto),akiteta jambo na na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Salim Ahmed Salim (waliokaa mbele katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha mkutano huo.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad (kulia), akisalimia na mama Balozi Getrude Mongela katika mkutano huo. Katikati ni
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Salim Ahmed Salim.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Salim Ahmed Salim (katikati), akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye wakati wakitoka kupiga picha ya pamoja nje ya ukumbi huo. 
(Imeandaliwa na mtandao wa http: www.habari za jamii.com)
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images