Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 533 | 534 | (Page 535) | 536 | 537 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem wa (kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia Maadhimisho ya Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani. Wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem wa (kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia Maadhimisho ya Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani. Wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi.
  Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia Maadhimisho ya Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem.
  Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia Maadhimisho ya Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem wa (kwanza kulia) akiwapongeza baadhi ya akinamama waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem wa (kwanza kulia) akiwapongeza baadhi ya akinamama waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakijitahidi kupata habari katika ukutano huo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakijitahidi kupata habari katika ukutano huo
  .
  Mmoja wa waathiriwa wa ugonjwa wa Fistula, Lidya Makanda aliyepata matibabu na kupona akionesha kipeperushi kilichookoa maisha yake baada ya kukisoma na kwenda hospitali kutibiwa ugonjwa huo.
  Mmoja wa waathiriwa wa ugonjwa wa Fistula, Lidya Makanda aliyepata matibabu na kupona akionesha kipeperushi kilichookoa maisha yake baada ya kukisoma na kwenda hospitali kutibiwa ugonjwa huo.
  Baadhi ya madaktari wanaotoa matibabu ya ugonjwa wa Fistula katika Hospitali ya CCBRT Tanzania wakiwa katika mkutano huo na wanahabari.
  Baadhi ya madaktari wanaotoa matibabu ya ugonjwa wa Fistula katika Hospitali ya CCBRT Tanzania wakiwa katika mkutano huo na wanahabari.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem na Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi wakipiga picha ya pamoja na akinamama waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem na Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi wakipiga picha ya pamoja na akinamama waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem (kulia) akihojiwa na moja ya wanahabari mara baada ya mkutano huo.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem (kulia) akihojiwa na moja ya wanahabari mara baada ya mkutano huo.
  Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV, Sam Mahela (mwenye kipaza sauti cha ITV) akipiga picha na akinamama waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.
  Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV, Sam Mahela (mwenye kipaza sauti cha ITV) akipiga picha na akinamama waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem na Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi wakipiga picha ya pamoja mara baada ya mkutano na wanahabari katika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam Tanzania.
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem na Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi wakipiga picha ya pamoja mara baada ya mkutano na wanahabari katika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam Tanzania.
  Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
  ZAIDI ya akinamama 3,000 nchini Tanzania huugua ugonjwa wa fistula mara baada ya kujifungua kila mwaka, huku sababu kubwa ya kupatwa na ugonjwa huo ikiwa ni huduma duni za afya ya uzazi hasa zile huduma za dharura kwa wajawazito wanapokuwa wakijifungua.
  Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya maadhimisho ya Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani.
  Lakini robotatu ya wagonjwa hao hawana uelewa wa kwamba wanaweza kupata matibabu na kupona kabisa ugonjwa huo. Ipo haja ya kuongeza bajeti ya huduma kwa wahusika na kutoa elimu zaidi ili kusaidia jamii hii inayoangamia kila kukicha kwa matatizo ya fistula. Wakinamama na wasichana ambao hukumbwa na matatizo ya fistula wamekuwa wakipata changamoto kubwa baada ya kutengwa na familia zao na wengine kuvunjika ndoa zao kutokana na hali ya kuvuja mkojo muda wote huku wakitoka na harufu kali. Alisema ili kuunga mkono juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa fistula.
  Hata hivyo ili kupambana na ugonjwa huo, Dk. Kanen alisema kuanzia mwaka 2003 UNFPA na wadau wenzake ilizinduwa kampeni ya dunia nzima kuhakikisha inazuia ugonjwa wa fistula (Grobal Campaign to End Fistula) mradi ambao kwa sasa unafanya kazi kwa zaidi ya mataifa 50 ulimwenguni huku ukijikita kwa kuzuia, kutibu na kuwasaidia kiuchumi waathirika wa ugonjwa huo.
  Hali hiyo imewafanya washindwe kujiendeleza katika shughuli zao za kila siku za kujiongezea kipato, Takribani akinamama 800 wanakufa kila siku dunia nzima kutokana na matatizo ya uzazi huku 20m kati yao wakijikuta wameathiriwa vibaya na ugonjwa hatari wa fistula. Inakadiliwa kuwa kati ya akinamama 50,000 hadi 100,000 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula ni 20,000 tu ndio hufanikiwa kupata matibabu ya ugonjwa huo kwa mwaka.
  Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi akizungumza na wanahabari kuzungumzia maadhimisho hayo yanayoanza tarehe 23 Mwezi Mai, 2015 alisema hospitali hiyo na washirika wake inasapoti maeneo manne ya wagonjwa wa fistula ambayo awali yalionekana ni changamoto kwao.
  Aliyataja maeneo hayo ni pamoja na Matibabu kwa wagonjwa, Gharama za Usafiri, Gharama za Chakula na Gharama za Malazi ili kumsaidia mgonjwa kuweza kukabiliana na changamoto hizo. “…Tunaomba kila mmoja kuanzia ngazi za familia watoe elimu kwa wahusika waje hospitalini kupata matibabu mapema kwani ugonjwa huu unatibika,” alisema Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi.

  0 0

  1
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, (pichani) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Mapanga na Nkome wakati wa ziara yake wilayani Bahi, Mkoani Dodoma. Waziri amefanya ziara Wilayani humo katika vijiji kadhaa kueleza hatua zilizofikiwa katika Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili, unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika na Umeme Nchini (TANESCO).
  2
  Meneja wa TANESCO Kanda ya Kati (Dodoma), Mhandisi Deogratius Ndamgoba akiwaeleza wananchi wa Vijiji vya Mapanga na Nkome wilayani Bahi, Mkoani Dodoma, kuhusu kuunganishwa na Huduma ya Umeme kwa vijiji hivyo wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene. Pamoja nae pichani ni Wataalamu kutoka Shirika hilo na nyuma yake ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati, Mhandisi Sosthenes Masolla.
  3
  Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Francis Mwonga, akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mtitaa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati). Waziri amefika katika Kijiji hicho kuwaeleza wananchi kuhusu hatua zilizofikiwa za kukiiunganisha Kijiji hicho na Huduma ya Umeme unaotekelezwa na Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili, unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na TNANESCO. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Bahi, Omar Badwel.
  4
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mtitaa wakati wa ziara yake kijijini hapo.
  5
  Mbunge wa Jimbo la Bahi, Omar Badwel, akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Kigwe, Wilaya ya Bahi wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene kijiji hapo. Waziri Simbachawene amefika Kijijini hapo ili kueleza wananchi hatua ya Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili kijijini ulipofikia kijijini hapo.

  ………………………………………………………………………
  Asteria Muhozya, Dodoma
  Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene amesema endapo utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Pili, inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), itakamilika kama ilivyopangwa ifikapo Juni mwaka huu, itawezesha kufikikiwa asilimia 40-45 ya Vijiji na Miji iliyounganishwa na Huduma ya Umeme kwa upande wa Tanzania Bara.
  Waziri Simbachawene ameyaeleza hayo wakati wa ziara yake katika Vijiji vya Mtitaa, Nkome, Mapanga, Kigwe na Mpamatwa Wilayani Bahi, Mkoani Dodoma, ambapo amefika katika vijiji hivyo kueleza hatua zilizofikiwa na Mradi huo wa kuviunganisha Vijiji hivyo na Huduma ya Umeme.
  “Tangu nchi yetu ipate uhuru, ilikuwa imeunganishwa na huduma ya umeme kwa asilimia 10, uongozi wa Awamu ya Nne ulilenga kufikia asilimia 30, lakini hivi sasa tumevuka na kufikia asilimia 36, haya ni mafanikio makubwa”,amesisitiza Simbachawene.
  Aidha, amewataka wananchi wanaopitiwa na Miradi hiyo, kuupokea vizuri uwekezaji huo kwani ni kichocheo kikuu cha uchumi na katika kuboresha maisha yao. “Uwekezaji huu muupokee uboreshe maisha yenu kwani umeme ni ajira, umeme ni maisha bora”,ameongeza Simbachawene.
  Katika ziara hiyo, Simbachawene ameambatana na Mbunge wa Bahi, Omar Badwel, Mkuu wa Wilaya ya Bahi Francis Mwonga na wataalamu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa Kampuni  ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China ikiongozwa na Mtendaji Mkuu Eng. Zhu Chunhua wa pili kulia  ofisini kwake leo tarehe22/05/2015. Kampuni hiyo inajenga barabara ya lami kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Katavi katika mradi wa Sumbawanga-Kanazi (KM 75). Mkuu huyo wa Mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ushirikiano wake mzuri na uongozi wa Mkoa katika shughuli zake za ujenzi wa barabara hiyo.
   Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akiongoza zoezi la utambulisho wa wageni na wenyeji katika kikao hicho.
  Mtendaji Mkuu  wa Kampuni  ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua wa pili kulia akizungumza katika kikao hicho ambapo ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano unaowapa katika kufanikisha ujenzi wa barabara ya lami ya Sumbawanga – Kanazi, aliongeza kuwa kampuni yake ipo tayari kufanya kazi zingine mbalimbali Mkoani Rukwa ikiwepo ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji taka pamoja na kuwekeza katika eneo la ufugaji. 
   Mtendaji Mkuu  wa Kampuni  ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua akimkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya walipomtembelea Ofisini kwake leo. Barabara ya Lami ya Sumbawanga – Kanazi – Namanyere – Kizi – Kibaoni inajengwa kwa fedha za Serikali ya Tanzania na ujenzi wake bado unaendelea.
   Picha ya pamoja.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akiteta jambo na Mtendaji Mkuu  wa Kampuni  ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua muda mfupi kabla ya kuagana mapema leo. (Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  WordEduForum-01-L

  Opening of World Education Forum 2015, Seoul. UN Secretary-General Ban Ki-moon centre, at the opening of the World Education Forum 2015, in Seoul. He is flanked by Hwang Woo-yea (left), Deputy Prime Minister and Minister of Education of the Republic of Korea; and Irina Bokova, Director-General of the UN Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO). 19 May 2015. Seoul, Republic of Korea. (UN Photo/Evan Schneider).

  Tanzania’s Minister for Education and Vocational Training (MoEVT), Honourable Dr. Jumanne Shukuru Kawambwa with a delegation of four most senior officials from Tanzania Mainland and Zanzibar and a representative from the Civil Society are attending the Third World Education Forum (WEF) from 19-22 May 2015 in Incheon, Republic of Korea. The 2015 WEF is the third after the Jomtien WEF of 1990 and the Dakar WEF of 2000. The 2015 forum takes stock of achievements and challenges since the Dakar WEF and deliberates on the education agenda for the next fifteen years (2015-2030).

  Tanzania was represented by a high profile delegation that consisted of two the Permanent Secretaries (from the Ministry of Education and Vocational Training and from the Prime Minister’s Office-Regional Administration and Local Governments), the Commissioner for Education from MoEVT as well as the Deputy Principal Secretary from MoEVT Zanzibar. The Civil Society is represented by HakiElimu which is a member organization of the Tanzania Education Network (TEN/MET).

  UNESCO is taking the lead in coordinating WEF with the collaboration of UNDP, UNHCR, UNFPA, UNICEF, UN Women and the World Bank (WB). The opening ceremony was attended by a number of high profile key speakers including Ms. Irina Bokova the Director General of UNESCO, representatives from the Government of the Republic of Korea and Mr Ban Ki-moon, the United Nations Secretary General, to mention but a few.

  The 2015 WEF seeks to take stock of achievements and shortfalls in the implementation of the Millennium Development Goals since the year 2000. The forum will also agree on a joint position for the education goal and targets in the post millennium development period (post 2015 development agenda). The agreements from the forum will be adopted by UN Member States at a Summit in September 2015;

  The forum will further agree on a framework to support the implementation of the future education goal which focuses on equitable and inclusive quality education and lifelong learning for all by 2030. UNESCO Dar es Salaam office, in collaboration with UNICEF, the WB and DFID are pleased to support the successful participation of the United Republic of Tanzania to the 2015 World education Forum

  0 0


  0 0

  1
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mwenyekiti Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein(kushoto), Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip Mangula(kulia) na katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana(watatu kushoto) wakati ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kinachofanyika katika ukumbi wa White House Mjini Dodoma.
  2
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo jioni.
  3
  Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM wakipitia ajenda za kikao hicho leo katika ukumbi wa White House Makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo jioni.
  4
   Stephen Wasirra na Adam Kimbisa, wakijadiliana jambo.
  5
  Mh.Jesniter Mhagama na Jerry Slaa, wakiteta jambo.mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kamti kuu mjini Dodoma leo.
  6
  Dkt.Emmanuel Nchimbi na Jenister Mhagama wakiteta jambo. (picha na Freddy Maro)

  0 0

  6Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Sheikh Abdulla Talib Abdulla amesema Taasisi za dini  hazipaswi  kuegemea upande wa chama chochote cha siasa ama kushiriki katika kampeni za uchaguzi lakini zinawajibu wa kujenga jamii ishiriki kikamilifu kufanyika uchaguzi huru na wa haki na kujenga matumaini makubwa ya kuwa na amani.
  Sheikh Abdulla Talib ameeleza hayo alipokuwa akiwasilisha mada ya nafasi ya Taasisi za kidini katika kufanikisha uchaguzi wa amani na uadilifu katika Semina ya kuhamaisha Viongozi wa dini ya Kiislamu  kusimamia amani wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
  Amesema dini inamisingi muhimu inayoweza kutumika katika kujenga  amani  kwani kuna uhusiano mkubwa wa kinadharia baina ya dini na uchaguzi wa amani na uadilifu.
  Ameongeza kuwa kufanya kazi ya kujenga amani ni kutekeleza dhamana ya dini kwani uislamu wakati wote unasisitiza umoja, upendo na  amani ya kila mtu.
   Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana amewaeleza washiriki wa semina hiyo ambao ni masheikh na wanazuoni kutoka mikoa mitatu ya Unguja kwamba wanadhima ya kusisitiza kufuatwa sheria na uadilifu kuanzia sasa mpaka  kutangazwa matokeo ya uchaguzi.

  “Uchaguzi wa amani unahitaji kuwepo uadilifu, kufuatwa taratibu na miongozo katika mchakato wote, ushirikishwaji wa pande zinazohusika  kwa mujibu wa matakwa ya kisheria, kutolewa elimu ya kutosha ya uraia, uwazi na uwajibikaji pamoja na kuyakubali matokeo,”alieleza Sheikh Abdulla Talib.
  Katika kufanikisha  uchaguzi  huru na haki Sheikh Talib ameshauri  kuwa na matumizi mazuri ya nyumba za Ibada na maeneo ya kidini  pamoja na matumizi mazuri ya aya, hadithi, nukuu za kihistoria na hekma nyengine.
  “Kwa kuzingatia uhalisia wa uchaguzi, taasisi za kidini zinapaswa kutumia mbinu na taratibu za kidini na nyenginezo katika kulingania uchaguzi wa amani, ”aliongeza sheikh Abdulla Talib.
  Aliwakumbusha wanazuoni hao kuwa Zanzibar ni nchi ndogo yenye watu wachache wenye uhusiano  wa karibu na tatizo linapotokea huzigusa familia nyingi hivyo amewashauri mahubiri yao  yalenge kufanyika uchaguzi katika misingi ya uhuru, uwazi, haki, amani na utulivu.
  Washiriki wa semina hiyo wameiomba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuwa waadilifu na kufuata taratibu na sheria zote za uchaguzi kuanzia hatua za kuliboresha daftari  la wapiga kura hadi kukamilika zoezi  la uchaguzi bila ya kuingiza  ushabiki wa kisiasa.
  Katika maazimio yao  masheikh hao wametaka kuhakikishiwa usalama wao wakati wa kutekeleza jukumu la kuwahubiria wafuasi wao kwani  wameingiwa na wasi wasi wa kukamatwa kutokana na  visingizio mbali mbali.
  Semina hiyo iliyofanyika katika jengo la Ofisi ya Bima Mperani, iliandaliwa na Jumuiya ya JUMAZA na UKUEM kwa kushirikiana na mtandao wa kimataifa wa dini kwa ajili ya kulinda watoto (GNRC)

  0 0

  1
  Mkurugenzi Mkuu na Muasisi wa Kampuni ya Compulynx Tanzania Bw.Sailesh Savani akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi Hundi kwa mtunzi wa wimbo wa kampuni hiyo Kanda ya Afrika Mashariki.
  2
  Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya Cumpulynx Tanzania) Bw. James Alvan (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kuhusu ya mashine za Eletronic Fiscal Device (EFD) zinazosambazwa na Kampuni hiyo kwa Tanzania.
  3
  Mkurugenzi Mkuu na Muasisi wa Kampuni ya Compulynx  Tanzania Bw.Sailesh Savani (kushoto) akikabidhi hundi kwa mshindi washindano la ubunifu kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa Afrika Mashariki Bw.Tulizo Kaduma (Kulia) na katikati ni Afisa Biashara wa Kampuni hiyo Bi.Genesis Mwaipopo.
  ………………………………………………………..
  Na Beatrice Lyimo- Maelezo.

  Kampuni ya COMPULYNX  Tanzania inayoshughulika na usambazaji wa mashine za Electronic Fiscal Device (EFD) imewashauri wafanyabiashara nchini kutumia mashine hizo ipasavyo kwani husaidia kukuza pato la Taifa.
  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw Sailesh Savani wakati akiongea na waandishi wahabari leo jijini  Dar es Salaam.
  “Wafanyabiashara wasiwe waoga kutumia mashine za EFD kwani huleta uhalali wa pande zote mbili ikiwemo Serikali na wafanyabiashara hivyo kupelekea maendeleo ya nchi kwani kodi zitakusanywa kihalali”aliongeza Bw Savani.
  Ameongeza kuwa mashine hizo husaidia kuweka kumbukumbu wa mfumo mzima wa biashara hivyo kuwasaidia wafanyabiashara kujua mapato na ulipaji wa kodi unaofanyika kihalali na kupelekea Serikali kujua mapato ya patika na yonchini.

  “Ukwepaji wakulipa kodi umechangia maendeleo duni katika sekta ya Miundombinu pamoja na ukosefu wa huduma za jamii zikiwemo Maji, Hospitali na Elimu bora nchini”, alifafanua Mkurugenzi huyo.
  Mbali na hayo kampuni hiyo inafanya shughuli mbalimbali zikiwemo kusambaza mitambo yakieletroni kiinayosaidia kukamata wahalifu katika maeneo mbalimbali ya biashara ikiwepo benki na maduka makubwa.
  Pia kampuni hiyo ilifanya mashindano yauimbaji iliyowashirikisha nchi tatu ikiwemo Tanzania, Kenya na Uganda na kumtangaza Bw. Tulizo Kaduma kutoka Tanzania kuwamshindi wa shindano hilo.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT)  Ezekiah Oluoch akizungumza juu ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kitaifa utakaofanyika Mei 28 katika mkutano Mkuu wa chama hicho utakaofanyika Mei 25 mpaka 28 katika ukumbi wa mikutano wa Ngurudoto,katika mkutano wake na waandishi wa habari jana uliofanyika katika ofisi za mkoa za chama hicho,kushoto ni Katibu wa chama mkoa Hassan Said

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa kitaifa May 28 mwaka huu ili kupata viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi  cha miaka 5 pamoja na kutetea maslahi ya walimu.  Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Ezekiah Oluoch amesema kuwa nafasi zinazogombaniwa ni Mwenyekiti wa chama,Katibu,Naibu Katibu mkuu pamoja na Mhazini wa chama hicho.  Ezekiah alisema hayo jana akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za  chama hicho Mkoa wa Arusha kuwa hadi sasa wana jumla ya wanachama  452 wamejitokeza kugombea nafasi hizo  na nafasi nyingine ikiwamo Mwakilishi wa Walimu wenye ulemavu  ,na kitengo cha Walimu wanawake.  “Wagombea ni wengi na nafasi ni chache tumeona tuache hivyo maana yake tukizuia idadi tutakua tumeminya demokrasia” Alisema Ezekiah  Ezekiah amesema kuwa jumla ya walimu 1000 wanatarajia  kushiriki uchaguzi huo wa kitaifa ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.  Mwenyekiti wa Chama hicho  Mkoa wa Arusha (CWT) Jevin  Buruya amesema kuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya uchaguzi huo hivyo amewataka walimu wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi huo.  Jevin amesema kuwa Chama cha Walimu Tanzania kitafanya mkutano mkuu utakaoanza May 25 hadi 28 ambapo agenda kuu ni Uchaguzi Mkuu,Mkutano huo unatajwa kuwa Mkutano wa Mwisho wa Raisi Kikwete kuwahutubuia walimu


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo akizungumza na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao. 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo akizungumza na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.

  CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kimepanga kuwajengea uwezo baadhi ya waandishi wa habari nchini juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kujiandaa na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2015. 

  Akizungumza katika mkutano na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo alisema mafunzo hayo yatawaongezea ujuzi wanahabari juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kwa ujumla kwa kuzingatia utoaji wa nafasi kwa makundi ya wanawake, 

  vijana na watu wenye ulemavu. Alisema kundi la wanawake wanaoshiriki kugombea katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi na walemavu wamekuwa wakikosa fursa kwenye vyombo vya habari kujinadi kutokana na mfumo na mazingira ya uchaguzi yalivyo, hivyo kuna haja ya kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuzipa kipaumbele pia na makundi hayo ambayo huachwa nyuma kwenye mchakato mzima.

   Kwa upande wake Mwandishi wa Habari Mkongwe na Miongoni mwa waanzilishi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga akitoa mada kwa wahariri juu ya umuhimu wa vyombo vya habari kutoa nafasi pia kwa wagombea wanawake watakaojitokeza kugombea katika Uchaguzi Mkuu; alisema hali hiyo itawafanya wagombea hao kujinadi kwa ufasaha kama ilivyo kwa wanaume hivyo kupata nafasi ya kusikika. Alivitaka vyombo vya habari kubadilika na kuandika habari za wagombea kwa kina, kufanya uchambuzi wa kutosha na kutumia takwimu zitakazo leta mvuto kwa wasomaji na hatimaye wao kufanya uamuzi sahihi baada ya kuwaelewa vizuri wagombea wao. 

   "...Binafsi naomba 2015 vyombo vya habari tuoneshe aina tofauti za kuripoti...turipoti habari zetu vizuri, tuandike kwa kuzingatia njinsia zote, tufanye uchambuzi wa kina, tuandike kwa kutoa takwimu zenye mvuto. Tuhakikishe wanawake nao watakaogombea wanapata nafasi sawa na kusikika kwa wapiga kura," alisema Bi. Sanga akizungumza. 

   TAMWA imekubali kuwajengea uwezo baadhi ya waandishi wa habari juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kwa kuzingatia makundi mbalimbali hasa ya wanawake na walemavu ili nao waweze kusikika kama ilivyo kwa kundi la wanasiasa wa kiume. Tayari maandalizi yanafanywa kukamilisha zoezi hilo mapema kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.
  Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kushoto) akizungumza na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kushoto) akizungumza na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya maofisa wa TAMWA (kushoto) wakichukua taarifa muhimu katika mkutano huo.Baadhi ya maofisa wa TAMWA (kushoto) wakichukua taarifa muhimu katika mkutano huo.Mwandishi wa Habari Mkongwe na Miongoni mwa waanzilishi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao.Mwandishi wa Habari Mkongwe na Miongoni mwa waanzilishi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao.

  0 0


  Mmoja wa watalii wa ndani ,Dkt Gaspaer Mpehongwa ,(Kulia) akizungumza jambo na wageni wakati akiwaonesha moja ya picha inayoonesha namna ambavyo volcano ilivyo ripuka na kutengenza uwanda wa Shira.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.


  Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika Prof,Faustine Bee akizungumza jambo kuhusu miamba iliyoko katika mapango hayo.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mwanga wakiongozwa na meneja wao ,Innocent Silayo(wa pili toka kulia) wakishuka mara baada ya kutembelea vivutio  katika uwanda wa Shira.
  Baadhi ya watalii wa ndani wakiwa katika gari kuelekea kilele cha Shira katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
  Kundi la Pili la watalii wa ndani wakiwa katika eneo la uwanda wa Shira mara baada ya kufika kwa usafiri wa gari hadi katika eneo hilo.
  Afisa Masoko wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro akizungumza na watalii wa ndani kabla ya kuendelea na safari ya kutembelea vivutio mbalimbali viyoko katika uwanda wa Shira yakiwemo mapango ya Shira Caves.

  Safari ya kuelekea katika vivutio vya asili katika uwanda wa Shira ,hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
  Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU),Faustine Bee akitizama mandhari katika uwanda wa Shira wakati akipanda mlima huo kuelekea katika mapango ya Shira.
  Raia wa kigeni wakipata kumbukumbu katika maeneo mbalimbali ya hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
  Watalii wa ndani wakichukua taswira mbalimbali mara baada ya kufika kilele cha Shira ndani ya Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
  Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU) Faustine Bee akichukuliwa taswira na kijaa wake baada ya kufika eneo la Shira hut.
  Safari ya kuelekea kutizama mapango ikiendelea.
  Watalii wa ndani wengine waliweka kumbukumbu.
  Safari ikaendelea.
  Baada ya kupanda vilima watalii wa ndani pia walipata nafasi ya kupumzika.
  Watalii wa ndani wakiwa katika mapango ya Shira ambayo yalitumiwa na wapagazi wakati wa zoezi la kupandisha watalii wakati wa safafri ya kuelekea kilele cha Uhuru,
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MOCU) Prof,Faustine Bee akifurahia mara baada ya kuingia katika mapango ya Shira.

  0 0

  Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya matumizi ya Tehama katika ufundishaji kwenye vyuo vya ualimu.Na Geofrey Adroph, Pamoja blog

  Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu ya Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limejikita katika uboreshaji wa elimu kwa kuwapa mafunzo walimu katika somo la Teknnolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama). 

    Akizungumza leo katika Ufungaji wa Mafunzo yaliyoandaliwa na UNESCO wakishirikiana na China Funds in Trust Project (CFIT) yaliyofanyika kwa siku tano katika Ukumbi wa DIT, Jijini Dar es Salaam, Ofisa Miradi wa UNESCO, Faith Shayo amesema mafunzo waliopata walimu wa vyuo vya walimu mbalimbali nchini itawasaidia katika uboresha wa elimu ikiwa ni pamoja na kuwapa vifaa vitakavyotumika katika kufundishia somo hilo. 


    Faith amesema ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya Tehama hiiinatokana na baada ya mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini kuona kuna mapungufu katika masuala la uelewa na matumizi ya Tehama katika vyuo vilivyopo nchini.Amesema katika kufikia malengo ya mradi wa UNESCO-China Funds in Trust Project (CFIT) wanaoshirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini kwa malengo makuu matatu.

  Aliyataja malengo hayo ni kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu wanapofundisha katika somo la Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuwanunulia vifaa vya Tehama ambavyo vitasaidia katika kufundishia.Faith amesema baada ya mafunzo hayo vyuo vitapata vifaa mbalimbali ambayo ni kompyuta, Projecta,ya na vifaa vya kuzalisha umeme wa jua (Solar Energy) kwa ajili ya kuondokana na tatizo umeme unaokatika katika mara kwa mara. 

    Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka (DIT), Daudi Mboma pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Godfrey Haongo ambao wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa .Waliopata mafunzo hayo Waalimu tisa wa Chuo cha Ualimu Tabora, na tisa wengine kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne kutoka chuo cha ualimu Morogoro, na mmoja kutoka Shule direct, wawili kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso District. 

    Mafunzo hayo yametolewa kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya elimu ambao wana mchango mkubwa hasa katika ukuzaji wa Tehama wakishirikiana na wanafanya kazi wa UNESCO ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini. 

  Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma za kitehama katika taifa kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.

  0 0


  Court broker from MEM Auctioneers and General Brokers Ltd Mr. Elieza Mwambo (second right) hands over door keys to Bains Holdings Limited Site Manager Mr Zulfiqar Hassanali (left) as a sign of handing over a premise where AMI hospital used to operate its business, back to the landlord, after AMI was evicted for nun-payment of $ 1.75 million as rent due for 3 years. Right is MEM Operation Manager, Mr. Protches Moshi.
  Court broker from MEM Auctioneers and General Brokers Ltd Mr. Elieza Mwambo, speaks to journalists (not in picture) during a handover a premise where AMI hospital used to operate its business, back to the landlord, after AMI was evicted for nun-payment of $ 1.75 million as rent due for 3 years. Right is MEM Operation Manager, Mr. Protches Moshi. 

  Fate of employees of Medical Investment Ltd (AMI Hospital, also known as Trauma Center) in Dar es Salaam, is hanging in a balance as the hospital officially closes business in Tanzania.

  This was evident yesterday when tens of neglected AMI employees gathered in front of the then hospital building to voice their frustration on how AMI hospitals management was treating their case after the High Court ordered the hospital to vacate premise for nun-payment of approximately $ 1.75 million as rent due for 3 years.

  Speaking on behalf of other demanding employees, Roslyn Sesoa who worked for the hospital as a nurse said the management has stopped picking their calls, nobody is communicating to them on what will happen to their contribution to the National Social Security Fund (NSSF) pension funds as well as salary arrears.

  “We have gone to NSSF to check how much we have contributed to the fund, but to our surprise, AMI management was deducting our part of the contribution from our salaries, but not remitting the same to NSSF. This leaves a big question on our fate as the hospital is now closed and the management does not want to say anything. 


  We are also demanding salary arrears which were being paid in discrimination. We want NSSF management to take action on these private employers who do not remit employees contributions, and when they close business, employees remain stranded,” said Ms Sesoa.

  She mentioned that doctors, nurses, receptionists, cleaners and other AMI employees are now stranded as their employment has been cut short without any compensation. This includes local employees and expatriates.           

  Implementing the courts order issued earlier this month, AMI assets and the premise were yesterday handed over to the landlord Mr Navtej Bains whom AMI owes approx a sum of $ 1.75 million, due to not paying rent for 3 years.

  Speaking to journalists at the premise yesterday during the handover, Mr. Elieza Mwambo, court broker from MEM Auctioneers and General Brokers Ltd, said they had followed all eviction procedures as per the court order by issuing an eviction notice to the hospital and proceeded to give another grace period of one week for the hospital to transfer admitted patients, something which was done in a humanitarian grounds.  

  “We have done a very peaceful eviction and we thank God that no patient lost a life in the process. This is because we handled the case carefully knowing that this facility was occupied by a hospital. We have attached all AMI assets which include CT-scan, x-ray machines, three ambulances, one Saloon car (Mark II), special hospital beds, computers, chairs and other hospital gadgets, which will be auctioned to recover part of the rent,” said Mr. Mwambo.

  He added that during the auction, they will give priority to an investor who will be interested in renting the premise to use as a hospital. He said the landlord is already in talks with other reputed medical institutions and is eager to get a medical facility running in the same premises so that residents there should continue having medical services next to their door steps.

  Mr. Mwambo rubbished the issue of handing over the property back to AMI saying that it would morally be wrong to place a humanity service in the hands of a management whose integrity is questionable. Sources say that AMI was the most expensive hospital in terms of consultation and in patient services in Tanzania.

  It is claimed that the court had frozen the AMI's account since January this year and the management was dealing only with cash payments thereafter. Even after the inflow of such huge amounts it is unfortunate that the staff of the hospital have not been paid their salaries and 2 years contributions to NSSF has not been remitted.

  The question here is where all the money went if neither the landlord, nor the staff nor the creditors were not being paid, as there is a long line of creditors daily outside AMI hospital building coming to get their dues, but are dodged by the management. 
  Inside information has it that several creditors are now in a limbo as the Hospital owes over $4m to them including the biggest creditor being the Landlord Mr Bains, Doctors, Staff, TRA, Pharmaceutical suppliers and other suppliers.
   ENDS…..


  0 0

  Mkurugenzi wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa ya Mei 22, katika Hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa serikali. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.


  KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, inayojihusisha na mikopo, imeanzisha huduma mpya ya kukopesha viwanja watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni za kawaida na wajasiriamali wa aina zote.

  Kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kumetokana na taasisi hiyo kupania kuboresha maisha ya Watanzania, likiwamo kundi la wajasiriamali ambalo limeendelea kusahauliwa na kampuni nyingi kupewa mikopo.
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, akizungumza katika uzinduzi huo, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, alisema kuwa ni kusudio lao kutoa fursa ya watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni na wajasiriamali kupata nafasi ya kutimiza ndoto za kumiliki ardhi nchini Tanzania.
  Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Kibaha, Obed Katonga, kulia akijadiliana jambo na Meneja Uzalishaji wa Bayport Financial Services, Mashaka Mgeta kulia kwake na Mkuu wa Kanda ya Pwani, David Ndiega.

  “Huduma yetu katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani, fomu zake zinapatikana katika matawi yote ya Tanzania Bara, ambapo kwenye matawi yetu yote fomu hizo zitakuwapo, huku fomu hizo za kukopeshwa viwanja zikipatikana kwa wiki mbili, kuanzia Mei 22 hadi Juni 10 mwaka huu.

  “Si lazima uwe mtumishi wa umma ili uwe na sifa ya kukopeshwa viwanja, ila hata wajasiriamali nao wamekumbukwa katika huduma hii nzuri kwa Watanzania wote, hivyo ni wakati wao sasa kuiunga mkono taasisi hii ili iweze kuwakomboa na kuwakwamua pia,’ alisema Mbaga.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda mwenye shati jeupe mbele akiwa katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja kutoka kwenye taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana jijini Dar es Salaam. Mwenye miwani ni Ruth Bura, mtumishi wa taasisi hiyo anayehusika na mambo ya Bima.

  Akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kibaha katika uzinduzi huo, Afisa Mipango wa wilaya hiyo, Obed Katonge, alisema kwamba Bayport imebuni huduma nzuri inayofaa kuungwa mkono na Watanzania wote, hasa kwa kuingia kwenye sekta ya ardhi inayopanda thamani siku hadi siku duniani kote.
  Wadau wanafuatilia uzinduzi huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akiendelea kufafanua katika uzinduzi wa mikopo ya viwanja, katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kushoto akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa serikali.
  Meneja Masoko wa Property International, Zora Moore, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, huku wao wakiwa ni kampuni iliyohusika na upimaji wa viwanja hivyo vya Vikuruti, Wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
  Mambo yamekwenda poa. Ndivyo wanavyoonekana kusema Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga kulia na Meneja Masoko wake na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo, katika uzinduzi wa mikopo ya viwanja. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
  Mwandishi wa Clouds Tv na Radio, Salehe Masoud, akibadilishana mawazo na mdau wa maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, mwenye shati jeupe na Mwandishi wa redio ya Times FM, Phillip Daudi.
  Staff wa Bayport Financial Services wakijadiliana katika uzinduzi wa huduma yao.
  Wadau wanafuatilia kwa makini kilichokuwa kinaendelea katika uzinduzi huo.
  Baada ya kuzindua, wadau walikuwa wakibadilishana mawazo kama hivi.


  “Serikali hususan kwenye wilaya yetu ya Kibaha tumepokea huduma hii kwa mikono miwili, ukizingatia kuwa wilaya yetu ni kati ya maeneo yanayokuwa kwa kasi, hivyo tunaamini tutaendelea kushirikiana na Bayport kwa ajili ya kuwapatia mwangaza wateja na wananchi wote kwa ujumla,” alisema Katonge.

  Habari; napenda kuiwasilisha kwako stori ya uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja kutoka Bayport Financial Services, yenye maskani yake, jijini Dar es Salaam, Tanzania. Wageni mbalimbali walialikwa akiwamo Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paulo Makonda. Uzinduzi huo ulifanyika jana ijumaa ya Mei 22 katika Hoteli ya Serena. Tunaomba sapoti yako ili Watanzania waone na waweze kuchangamkia fursa hii ya mikopo ya viwanja kutoka mradi wa vikuruti, uliopo Kibaha. Kambi Mbwana, +255 71205949.

  Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya ni njia ya kunapanua wigo wao na shabaha ya kuwafaidisha wateja wao na Watanzania wote kwa huduma na bidhaa zilizothibitishwa kwa ubora zaidi. 

  “Bayport ilikaa na kufanya tafiti kadhaa zenye nia ya kujenga jamii na kuinua uchumi wa Watanzania wote, hivyo tukaona ipo haja ya kufungua ukurasa huu wa kukopesha viwanja, huku wateja wetu wakitakiwa kulipa kila mwezi katika vipindi vya miezi 24, ambapo kiwanja cha chini kabisa kinapatikana kwa Sh 1,700,000 na nzuri zaidi wateja wetu wanaweza kuona huduma nyingine nzuri za mikopo kwa kupitia tovuti yetu ya www.kopabayport.co.tz ,” alisema Cheyo.

  Naye Meneja Bidhaa wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema makato ya kiwanja chenye thamani ya Sh 1,400,000 kwa mjasiriamali ni 105,181.55, wakati mtumishi wa umma akilazimika kukatwa Sh 73,684.49, huku akiongeza kuwa mtu anaweza kupata kiwanja kwa malipo ya fedha taslimu. “Naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kukopeshwa viwanja hivi ili watimize ndoto zao za ujenzi wa nyumba, maana Bayport imekuja kwa ajili ya kuboresha maisha ya Watanzania wote, maana tangu sasa kila mtu anaweza kuwa baba au mama mwenye nyumba,” alisema Cheyo.

  Mbali na huduma ya mkopo wa viwanja, Bayport pia inatoa mikopo mbalimbali ya bidhaa, mikopo ya fedha taslimu, bima ya elimu kwa uwapendao, huku mikopo yote hiyo ikiweza kupatikana kwa njia ya mtadao wa www.kopabayport.co.tz.

  0 0

  Kamati Kuu imepokea na kutafakari taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili ambayo ilipitia adhabu waliyopewa wanachama sita waliokiuka kanuni za Maadili na kupewa Onyo Kali, adhabu iliyodumu kwa kipindi kisichopungua miezi 12
  Wanachama hao sita ni;-
  i. January Makamba
  ii. William Ngeleja
  iii. Steven Wassira
  iv. Bernard Membe
  v. Edward Lowassa
  vi. Fredrick Sumaye

  Kamati Kuu imepokea na kukubali pendekezo la Kamati ya Usalama na Maadili ya kumalizaka kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hawa. Kwa hiyo adhabu hiyo kwa sasa imemalizika, na wanachama hao wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao katika Chama.

  Hata hivyo Kamati Kuu inawataka wanachama hawa na wale wengine wenye nia ya kugombea Urais kupitia CCM Kuzisoma , Kuziheshimu na Kuzizingatia Kanuni za Maadili za CCM na kanuni zingine zinazoongoza mchakato ndani ya Chama, ili wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni hizo.

  Wale wote wanaotaka kugombea, yaani waliokuwa kwenye adhabu na wengine watakaojiingiza kwenye kampeni mapema na hivyo kukiuka maadili na miiko ya Chama, taarifa za kukiuka kwao zitatumiwa wakati wa kuchuja majina ya wagombea utakapofika.

  Taarifa hizo zitatumika katika kuwapima na kuamua iwapo wana sifa za kutosha na wanafaa au hawafai katika kupata uteuzi wa nafasi wanayoiomba.

  Imetolewa na;-
  Nape Moses Nnauye
  Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM
  22/05/2015

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akizungumza wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kujadili na kufanya uamuzi wa kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi katika wilaya ya Sumbawanga na Kalambo leo tarehe 23 Mei 2015. Kikao hicho kimeridhia mapendekezo hayo ya Halmashauuri husika baada ya kukidhi vigezo ambapo yatapelekwa ngazi za juu kwa uamiuzi zaidi. 

  Majimbo hayo yatazaliwa katika majimbo yaliyopo hivi sasa ambapo kwa jimbo la Kwela ambalo lipo katika Wilaya ya Sumbawanga litazaa jimbo la Ziwa Rukwa baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi ikiwemo ya idadi ya watu na ukubwa wa jografia. Kwa upande wa jimbo la Kalambo ambalo lipo katika Wilaya ya Kalambo linatarajiwa kuzaa Jimbo jingine la Mambwe. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
   Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
   Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa taarifa iliyopokelewa na ofisi yake kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya maelekezo ya kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo ya Uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Kushoto ni muwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Clemence Bakuli ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama hicho Mkoa.
   Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifafanua jambo katika kikao hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta.
   Sehemu ya wajumbe na waalikwa wa kikao hicho.
   Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

   Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akimkabidhi Mkuu wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Akina mama wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dokta Mathew Kallaga (aliyepokea kwa niaba ya uongozi) vifaa mbali mbali vyenye thamani ya Tshs. Milioni saba alivyotoa kwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitatu ya kipindi hicho. 

  Kila mwaka Kipindi cha Mboni huwa kinaadhimisha kwa kutoa msaada sehemu mbali mbali ikiwa ni mpango wake wa kurudisha fadhira kwa jamii ambapo mwaka huu aliungwa mkono na PSPF, Nakiete Pharmacy, Fadhaget Sanitarium Clinic pamoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
   Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akipongezwa meneja wa Jengo la Wazazi, Sister Amina Mwakuluzo kwa moyo aliyouonyesha. Kila mwaka Kipindi cha Mboni huwa kinaadhimisha kwa kutoa msaada sehemu mbali mbali ikiwa ni mpango wake wa kurudisha fadhira kwa jamii ambapo mwaka huu aliungwa mkono na PSPF, Nakiete Pharmacy, Fadhaget Sanitarium Clinic pamoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. (Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.)
   Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akitoa shukrani zake kwa uongozi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuweza kumpokea na kukubali vifaa alivyotoa ili viweze kuendelea kusaidia jamii. Mboni alitoa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya Tshs. Milioni saba alivyotoa kwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitatu ya kipindi hicho. 

  Kila mwaka Kipindi cha Mboni huwa kinaadhimisha kwa kutoa msaada sehemu mbali mbali ikiwa ni mpango wake wa kurudisha fadhira kwa jamii ambapo mwaka huu aliungwa mkono na PSPF, Nakiete Pharmacy, Fadhaget Sanitarium Clinic pamoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
   Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akimkabidhi kikombe Mkuu wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Akina mama wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dokta Mathew Kallaga.
   Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akitoa zawadi mbali mbali kwa akinamama aliyowakuta katika wodi ya wazazi. Kipindi cha Mboni huwa kinaadhimisha kwa kutoa msaada sehemu mbali mbali ikiwa ni mpango wake wa kurudisha fadhira kwa jamii ambapo mwaka huu aliungwa mkono na PSPF, Nakiete Pharmacy, Fadhaget Sanitarium Clinic pamoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
   Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akimkabidhi nguo kwa mama aliyejifungua mtoto wa kike. Pembeni anayeshikilia nguo ni Mkurugenzi wa Fadhaget Sanitarium Clinic, Dokta Fadhili Emily.

  ... Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akiwa amebeba mtoto kwa furaha.

   Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akitoa zawadi ya Nakiete Baby Diaper ambazo hutengenezwa na Kuuzwa na Nakiete Pharmacy ambao nao waliungana nae kutoa msaada huo.

   Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba (katikati) akiongea machache mara baada ya kukabidhi vifaa vyenye thamani ya Tshs. Milioni saba alivyotoa kwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitatu ya kipindi hicho. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Fadhaget Sanitarium Clinic, Dokta Fadhili Emily, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Nakiete Pharmacy, Dorine Mzava na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Akina mama wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dokta Mathew Kallaga na Dokta Vicent Tarimo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiongea wakati alipounga mkono Kipindi cha Mboni Show katika utoaji wa Misaada katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Nakiete Pharmacy, Dorine Mzava na Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba.
  Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akitia shukrani kwa wauguzi wa hospitali hiyo.
  Picha ya Pamoja...
  Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutoa msaada katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akishow ndugu zake na Emma Kahere na Mariam Masimba.
  Timu ya Mboni Show ikifurahia pamoja madokta.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 23 Mei 2015  kuelezea juu zoezi la uandikishiaji wa Wananchi kwenye daftari la kudumu la Mpigakura litakaloanza rasmi kesho tarehe 24 Mei 2015 Mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
  Mkutano na waandishi wa habari ukiwa unaendelea. Kwa taarifa kamili SOMA HAPA CHINI:-

  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti leo kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma, tarehe 23 Mei 2015.

  Kamati Kuu katika kikao chake cha tarehe 22/05/2015 mjini Dodoma pamoja na mambo mengine imepokea na kutafakari kwa kina taarifa ya maandalizi ya mchakato wa kupiga kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa.

  Baada ya kutafakari na kwa kuzingatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika maandalizi hayo, Kamati Kuu ya CCM inaishauri serikali kwa kushauriana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakizingatia changamoto zilizopo na hali halisi ya mchakato huu, kutafuta njia muafaka ya kulishughulikia na kulihitimisha jambo hili kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

  Imetolewa na:-
  Nape Moses Nnauye
  Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM (T).
  23/05/2015.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) leo, Jumamosi, Mei 23, 2015 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Seif Shariff Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Ikulu Ndogo, Dodoma. Rais Kikwete akimwaga Mheshimiwa Hamad baada ya kumalizika kwa kikao hicho. 
  Picha na John Lukuwi, Maelezo.

older | 1 | .... | 533 | 534 | (Page 535) | 536 | 537 | .... | 1903 | newer