Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

OFISI YA KIKUNDI CHA SANAA TARAB YATEKETEA KWA MOTO ZANZIBAR

$
0
0
 Vifaa vya muziki pamoja na pesa shilingi milioni 2.5 za Kikundi cha Utamaduni cha Sanaa Tarab vikiwa vimeteketea kwa moto pamoja na ofisi yao iliyopo Ngome Kongwe, Mjini Zanzibar usiku wa kuamkia jana. 
 Vifaa vya muziki pamoja na pesa shilingi milioni 2.5 za Kikundi cha Utamaduni cha Sanaa Tarab vikiwa vimeteketea kwa moto pamoja na ofisi yao iliyopo Ngome Kongwe, Mjini Zanzibar usiku wa kuamkia jana. 
 Katibu wa kikundi cha Utamaduni cha Sanaa Tarab Daudi Shadhil (kulia) akitoa maelezo kwa Mwandishi wa habari Miza Kona kuhusu kuteketea kwa moto ofisi yao hapo Ngome kongwe, kushoto ni Muongozaji msaidizi wa Kikundi hicho Yazid Mawiya.

Baadhi ya Wasanii wa kikundi hicho wakionekana katika hali ya huzuni nje ya ofisi yao baada ya kutekete kwa moto usiku wa kuamkia jana. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 

"HAPO HAPO ULIPO CAMPAIGN @AK CLASSIC COSMETICS"

$
0
0


 HAYA SASA WALE MAGWIJI WA VIPODOZI VYA UKWELI KUTOKA MAJUU KUANZIA BIDHAA ZA VICTORIAs SECRET,BBW,BIDHAA ZA NGOZI KAMA DAWA ZA CHUNUSI,STRETCH MARKS,BIDHAA ZA KUKUNG'ARISHA SASA WANAKWAMBIA UNAWEZA PATA BIDHAA ZAO HAPO HAPO ULIPO IWE OFISINI AU NYUMBANI!!!UNAAMBIWA UNALETEWA BIDHAA MPAKA MLANGONI!!TENA BILA GHARAMA ZA ZIADA!!
  CHA KUFANYA:



       1.INGIA KWENYE BLOG YAO (www.akclassic.blogspot.com) CHAGUA BIDHAA UNAYOIPENDA
       2.WAPIGIE KWENYE NAMBA ZAO (0713468393/0753482909) KUPATA MAELEZO YA BIDHAA HUSIKA NA BEI YAKE,TOA ADRESS YAKO KAMILI
       3.BIDHAA UTAKAYOORDER ITAKUFIKIA NDANI YA MASAA 2!!

  KWA MSAADA ZAIDI WATEMBELEEE www.akclassic.blogspot.com   0713468393/0753482909.

Mdau ANATAFUTA MCHUMBA/MUME WA KUANZA NAYE MAISHA YA NDO

$
0
0


Naitwa Anna Francis umri miaka 28
Ninatafuta mchumba mwenye mapenzi ya kweli na dhati, umri kati ya miaka 28 mpaka 40 ambaye yupo tayari kuingia kwenye ndoa,Ambaye hana mke,akiwa na mtoto au watoto sio kikwazo,

Awe mtanzania, Sichagui Elimu,dini,rangi  wala kabila,ambaye atakuwa tayari tuanzishe familia,.Mimi kwa sasa naishi na kufanya kazi hapa Marekani(USA),si lazima awepo hapa Marekani hata akiwa Tanzania au popote pale kwangu haina shida kwa sababu tutajitahidi kwa pamoja tuonane.

Tafadhali naomba kwa aliye serious tu aniandikie kwenye email hii; anneyfr@yahoo.com  au anitafute kwenye facebook kwa jina langu au pia unaweza kufuata link ifuatayo ya facebook ambayo ni; https://www.facebook.com/anna.kennedyfrancis

Rais Kikwete amtembelea Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Hospitali ya Taifa Muhimbili

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyepumzishwa katika chumba cha Dharura katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.Mzee Kingunge alikimbizwa Hospitalini Hapo Baada ya Kujisikia Vibaya.jopo la Madaktari Bingwa linamfanyia uchunguzi Mzee Kingunga ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.Aliyesimama Nyuma ya Rais ni mke wa Mzee Kingunge na kushoto ni Mtoto wa Mzee Kingunge Bwana Kinjekitile.(picha na freddy Maro)

MSTAHIKI JERRY SILAA ATAKA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA ELIMU KATIKA MANISPAA YA ILALA.

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza jambo na Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu iliyoenda sambamba na Kampeni ya Kutangaza FAO LA ELIMU.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya Kigilagila na kufafanua kuwa mambo yanayofanywa na Mfuko waPensheni wa PPF katika kurekebisha baadhi ya mafao yake haswa fao la kifo, si tu yatasaidia kuwapa elimu wanafunzi wanaoguswa bali yatatia mkono katika kuboresha elimu katika mfumo mzima wa taifa letu na moja kwa moja katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.

Aidha Mh. Silaa ametoa wito kwa watanzania akisema kwa kuwa sasa mifuko hii ya pensheni imefungua milango, sio kwa watu walioajiriwa pekee ndio wanaopaswa kujiunga na mifuko hii ya pensheni, lakini hata kwa watu waliojiajiri, wakulima na hata wafugaji wana uwezo kabisa kisheria kujiunga na mifuko ya pensheni na kunufaika nayo.

Pia ameupongeza mfuko wa PPF kwa yale wanayoyafanya kwa watoto wa watu waliofariki wakiwa wanachama wa mfuko huo, ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2012 jumla ya wanafunzi 1, 333 wamelipiwa gharama mbalimbali zilizofikia jumla ya shilingi milioni 682.9 kitu ambacho ni jambo la kupigiwa mfano.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba akielezea nia ya kutembelea shule hiyo ni kutoa msaada wa vitabu kwa sababu tunaamini kwamba vitabu tutakavyo vitoa vitawasaidia wanafunzi waliopo hapa kuweza kupata elimu nzuri na kufanya vizuri katika mitihani yao na vilevile hawa ndio viongozi wa baadae. Vilevile katika hii shule ya Kigilagila sisi kama PPF tuna wanafunzi ambao tunawasomesha hivyo sisi ni wadau wa shule hii na tunatumia fursa hii kuwashauri waalimu na pia wazazi kujiunga na mfuko huu kwa manufaa ya baadae.
Meneja wa Penesheni PPF Bi. Chevu Sepeku akitoa elimu kwa wageni na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo kuhusiana na taratibu za utoaji wa mafao ya Elimu na kufafanua kuwa hutolewa ili kugharamia sehemu au gharama zote zinazohitajika katika elimu ya mtoto wa mwanachama aliyefariki ambapo gharama hizo ni kuanzia elimu ya chekechea hadi kidato cha nne.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi zawadi kwa mtoto wa darasa la Saba Ummy Abdalah kwa niaba ya wanafunzi wenzake. Ummy Abdalah ni miongoni mwa wanafunzi wanaosomeshwa na PPF kutumia FAO LA ELIMU baada ya wazazi waliokuwa wananchama wa mfuko huu kufariki dunia.
Mtoto Shakila Abdalah wa darasa la pili naye akipokea zawadi kutoka kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Veriana Mfugale akishihudia tukio hilo. 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwasili katika Shule ya Msingi Kigilagila iliyopo maeneo ya Gongo la Mboto kama mgeni rasmi katika hafla fupi iliyoandiliwa na mfuko wa Pensheni wa PPF ya kukabidhi vitabu kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akitambulishwa kwa Meneja wa Penesheni Bi. Chevu Sepeku( kushoto) mara baada ya kuwasili katika shule hiyo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba na Wa pili kulia ni Afisa Uhusiano wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele.

Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiteta jambo na mmoja wa wanakikundi cha kwaya cha shule hiyo mara baada ya kuwasili.

Kwaya ya Shule ya Msingi Kigilagila ikipiga wimbo wa Taifa kuashiria kuanza kwa hafla hiyo.

Meza kuu wakiupa heshima wimbo wa Taifa: Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa (wa pili kushoto), Meneja wa Penesheni Bi. Chevu Sepeku( kulia) , Wa pili kulia ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kigilagila Verian Mfugale.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kigilagila Verian Mfugale akiukaribisha ugeni katika shule hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi za vitabu shuleni hapo pamoja na kwa watoto wawili yatima ambao wazazi wao walikuwa ni wanachama wa mfuko wa Pensheni wa PPF na kuendelea kusomeshwa kupitia FAO LA ELIMU linatolewa na mfuko wa Penesheni wa PFF.Kwa picha zaidi bofya hapa

jiachie na jarida la Nathanmpangala live

$
0
0

magazine hewaniJarida la katuni linaloandaliwa na mchoraji katuni, Nathan Mpangala, limeanza kurushwa leo, Alhamisi, likiwa na sura mpya kwa kusheheni katuni kibao ili kukidhi haja ya wapenzi wa katuni wa ndani na nje ya nchi.
Jarida hilo ambalo litakuwa likipatikana kwenye link; www.nathanmpangala.blogspot.com, linatambulikwa kwa jina la ‘Jarida la Katuni la Nathan’ au kwa kidhungu; ‘Nathan Cartoons Magazine’ linalenga kuongeza wigo wa matumizi ya katuni nchini kwani kwa miaka mingi, katuni zimekuwa zikitumika zaidi kwenye zaidi kuliko njia zingine.
 Jarida hilo litakuwa likipambwa na katuni za kisiasa, uchumi, michezo na karakta maarufu zilizokuwa zikitoka magazetini siku za nyuma kama; Kijasti, Mzungu Mtaani, Daladala Laivu nk. Pia litakuwa na katuni mahsusi kwa ajili ya anga za kimataifa.
 Mbali na katuni pia litakuwa na habari mbalimbali za mashindano ya katuni yanayoendelea ulimwenguni ili kuwawezesha wachoraji wa Kitanzania kushiriki.

mpango mzima wa tamasha la pasaka

Mshindi wa tano wa DStv Rewards apatikana.

$
0
0
--IMG_9695
Mshindi wa tano wa DStv Rewards, Alphonce Mlekwa Omary (wa pili kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu(kushoto), Meneja Mahusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kutoka kulia) na Meneja Muajiri wa MultiChoice Tanzania, Tike Mwakitwange(kulia), mara ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Tshs Milioni 5 kuashiria ushindi alioibuka nao.

Wateja wa DStv ambao wanalipia malipo ya mwezi ya akaunti zao kabla ya kukatika wanaendelea kubahatika na kuibuka washindi wa mamilioni ya pesa kila wiki. Hiyo ni kupitia droo maalumu ya DStv ambayo imepewa jina la DStv Rewards.   Mteja ambaye amebahatika kuibuka na kitita cha Tshs Milioni 5 wiki hii na hivyo kuifanya idadi ya washindi kufikia watano ni Bw. Alphonce Mlekwa Omary. IMG_9808
Tabasamu la ushindi. Ndivyo inavyoonekana katika picha kwa mshindi wa 5 wa DStv Rewards akifurahia kitita cha Tshs 5,000,000. Waliomzunguka pembeni ni ndugu zake ambao walimsindikiza na kufurahia pamoja naye ushindi.

OFISI YA KIKUNDI CHA UTAAMADUNI CHA SANAA TARAB CHAUNGUA MOTO.

$
0
0

Na Miza Kona-Maelezo Zanzibar      21-03-2013

OFISI ya Idara ya Utamaduni ya Kikundi cha Sanaa Taarab iliyopo Ngome Kongwe, Mjini Zanzibar, imeteketea kwa moto na kuharibu vitu vyote vilivyokuwemo ndani ya  ofisi hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika eneo la tukio, Katibu wa kikundi hicho Daud Shadhil AbdulMalik amesema moto huo ulitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 10.15 za alfajiri na kusababisha hasara kubwa.

“Vitu vyote vimeteketea kwa moto hakuna kilichobakia wala hakuna kinachofaa ” alisema Katibu huyo kwa huzuni. Alivitaja vitu vilivyoungua kuwa ni pamoja na fedha taslim shilingi milioni mbili na laki tano, majenereta mawili makubwa pamoja na vifaa vyote vya muziki vinavyotumiwa na kikundi hicho.

 “Kuna baadhi ya vifaa vilikuwa zaidi ya seti  moja na vyengine  vililetwa kwa ajili ya kuongezea uwezo, tunaviita vitu vya moto na baridi hivyo vyote pia vimeteketea”, alisikitika bwana Daud.

Aidha alisema kuwa chanzo cha moto na thamani ya vitu hivyo bado havijajulikana lakini vinakisiwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 70 na aliiomba Wizara husika kuwapatia ofisi na vifaa vyengine ili waweze kufanya kazi zao kama kawaida.

Hata hivyo ameishukuru Kikosi cha  Zimamoto na Uokozi  kufika kwa wakati sehemu ya tukio na kufanikiwa kuuzima moto huo.

Kikundi cha sanaa Taarab kina ofisi zake eneo la Ngome Kongwe ikiwa pamoja na  ghala na sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR. 

kumradhi wadau wetu hali ya mtandao si shwari

$
0
0
KUMRADHI WADAU WETU,HALI YA MTANDANO SI NZURI,TUMEFAHAMISHWA KUWA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO YA INTERNET (SEACOM) UMEKUBWA NA TATIZO,HIVYO WAHUSIKA WANALISHUGHULIKIA TATIZO HILO KWA UDI NA UVUMBA KUHAKIKISHA LINATENGEMAA NA KURUDI KAMA KAWAIDA,AIDHA WADAU WETU TUNAOMBA TUVUMILIANE MPAKA HAPO HALI YA MTANDANO UTAKAPOKUWA UMETENGEMAA BASI NASI TUTAKUWA HEWANI KAMA KAWAIDA,MTUWIE RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE ULE,TUKO PAMOJA.

JAMBO LEO, BTL MABINGWA NSSF MEDIA CUP 2013

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013 kwa naodha wa timu ya Jambo Leo, Said Mwishehe katika baada ya kuifunga Changamoto bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013 kwa nahodha wa timu ya Business Times Queens, Lulu Habibu baada ya kuifunga TBC 39-18 katika mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam. 

 Wachezaji wa Jambo Leo wakifurahia ushindi wa timu yao. 
Mashabiki wa timu ya Netiboli ya Business Times wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akikagua timu ya Business Times Queens kabla ya mchezo wao dhidi ya TBC.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akikagua kikosi cha timu ya TBC Queens.
Kikosi cha TBC Queens kikiwa katika picha ya pamoja.
Mabingwa wa Netiboli wa Kombe la NSSF Media Cup 2013 Business Times Queens kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuumana na TBC katika fainali.
 Mabingwa wa soka wa michuano ya NSSF Media Cup 2013 Jambo Leo, katika picha ya pamoja kabla ya mechi ya fainali dhidi ya Changamoto.
Kikosi cha timu ya Changamoto kilichoshika nafasi ya pili NSSF Media Cup 2013
Beki wa Changamoto John Robert akichuana na mshambuliaji wa Jambo Leo, Rogatius Katyali katika mchezo wa fainali ya michuano ya NSSF Media Cup 2013. 
 Wachezaji wa timu za TBC na (jezi nyeupe) na BTL wakichuanba katika mchezo wa fainali ya netiboli ya michuano ya NSSF Media Cup 2013. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau akizungumza wakati wa hafla ya kufunga michuano ya NSSF Media Cup 2013 leo. 
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akizungumza katika hafla ya kufunga michuano ya NSSF Media Cup 2013 leo.

DAR ES SALAAM, Tanzania

TIMU za Jambo Leo na Business Times (BTL), leo zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013, baada ya kushinda mechi zao za fainali ya soka na netiboli dhidi ya Changamoto na TBC.

Katika fainali ya soka, bao pekee la kipindi cha kwanza la mshambuliaji Julius Kihampa, lilitosha kuwapa Jambo Leo ubingwa wa pili wa michuano hiyo iliyofanyika kwa mwaka wa 10 na harakati za Changamoto kusawazisha hazikuzaa matunda.

Kwa upande wa Netiboli, Business Times Queens ‘The Bize,’ ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mchezo huo kwa ushindi wa magoli 39-18 dhidi ya TBC, huku nyota wake Lulu Habibu akifunga mara 27.

Lulu alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo upande wa netiboli kwa kufikisha magoli 153 katika mechi nne alizocheza, huku tuzo hiyo kwa upande wa soka ikitwaliwa na Nurdin Msindo wa Tumaini Media, aliyefunga mabao manne.

Lulu na Nurdin kila mmoja alizawadiwa kiasi cha shilingi 300,000 ambayo ni zawadi kwa wafungaji bora, huku Sahara Media ikitwaa tuzo ya timu yenye nidhamu, ambapo walizawadiwa kikombe.

Kwa kutwaa ubingwa soka, Jambo Leo walizawadiwa kikombe na shilingi mil. 4, huku Changamoto wakitwaa shilingi mil. 3 kwa kushika nafasi ya pili na TBC wakizoa shilingi mil. 2 kwa kutwaa nafasi ya tatu - baada ya juzi Ijumaa kuwalaza IPP kwa penati 4-3.

‘The Bize Queens’, wamebeba kombe na shilingi mil. 3.5 za ubingwa wa netiboli, huku mshindi wa pili TBC wakilamba shilingi mil. 2 na mshindi wa tatu NSSF wakibeba kombe pekee na kitita chao cha shilingi mil. 1 wakikitoa kwa Tumaini iliyoshika nafasi ya nne.

NSSF Media Cup 2013 ni michuano iliyofanyika kwa wiki mbili kwenye viwanja vya TCC na DUCE vilivyoko Chang’ombe jijini Dar es Salaam, ikihusisha timu 17 za soka na 15 za netiboli zilizoundwa na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini.

Baada ya michuano hiyo kuzinduliwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaundencia Kabaka Machi 9, ilihitimishwa leo kwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla kukabidhi zawadi kwa washindi wapya.

WAZIRI MKUU PINDA ALIPOKUTANA NA PAPA FRANCIS WA KWANZA

$
0
0

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki  Duniani, Papa Francis 1  , Vatican City, Machi 21, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekutana na Papa Francis wa Kwanza na kufanya naye mazungumzo ya faragha ikiwa ni pamoja na kuwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete. 

Waziri Mkuu alipata fursa hiyo Alhamisi, Machi 21, 2013 alipofika kwenye makazi ya muda ya Papa Francis wa kwanza kwenye hosteli ya Mt. Martha mara baada ya kumaliza vikao na wawakilishi kadhaa wa mashirika ya kimataifa walioko mjini Roma, Italia. Papa Francis anakaa hosteli kwa sababu Ikulu yake ilifungwa mara baada a Papa Benedict XVI kujiuzulu na sasa inafanyiwa ukarabati mdogo.
 
Alipowasili Vatican City, Waziri Mkuu alipokelewa na Mkuu wa Itifaki wa Baba Mtakatifu (Chief of Protocol of the Holy See) Monsinyori Jose Avelino Bettencourt ambaye pia alimtambulisha kwa Katibu Mkuu wa Baba Mtakatifu, Kardinali Tarcisio Bertone kabla hajaonana na Papa Francis wa Kwanza.
 
Katika mazungumzo yao, Waziri Mkuu alimweleza Papa Francis wa Kwanza kwamba amefika kuwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais Kikwete. Katika salamu hizo, Waziri Mkuu Pinda alisema: “Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anakutakia heri katika jukumu hili jipya ulilopewa na Mwenyezi Mungu. Tunamshukuru Mungu kwa kukupa jukumu la kulea wanakondoo, nasi tutaendelea kukuombea katika kazi yako kubwa uliyonayo.”
 
Waziri Mkuu alimweleza Papa Francis wa Kwanza kwamba Rais Kikwete alitamani kuwepo kwenye ibada yake ya kusimikwa rasmi lakini kutokana na majukumu mengine ya kitaifa aliyokuwa nayo, hakuweza kufika na badala yake amemuomba Waziri Mkuu amuwakilishe.
 
Akipokea salamu hizo, Papa Francis wa Kwanza alisema anatambua fika jinsi Tanzania inavyojitahidi kuendeleza amani chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. “Tutaendeleza ushirikiano wa karibu uliokuwepo baina ya nchi zetu,” alimalizia Papa Francis wa Kwanza.

MAPATO YA TAMASHA KUJENGA KITUO CHA YATIMA DAR

$
0
0

 Mwenyekiti wa Maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kuhusu maandalizi ya tamasha hilo lenye kauli mbiu ya Amani na Upendo. Kulia ni Mdau wa muziki wa Injili, Mcharo Mrutu. 
WARATIBU wa tamasha la Pasaka litakalofanyika kwenye Uwanja
wa Taifa, jijini Dar es Salaam hapo Machi 31, wamepanga kutumia sehemu ya
mapato ya kiingilio kujenga kituo cha watoto yatima kama
ishara ya shukrani kwa jamii.(Picha na Francis Dande) 
======  ======  ======
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati
maalumu inayoratibu tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama, alisema kituo hicho kitakachokuwa chini ya kampuni ya Msama Promotions kitajengwa eneo la Pugu. 
Alisema uamuzi huo umefikiwa kwa lengo la kuwapa faraja
watoto yatima ambao nao wana haki ya kupatiwa matunzo na mahitaji muhimu katika makuzi yao ikiwemo elimu katika kujenga taifa bora la kesho.

“Tangu kuasisiwa kwa tamasha la Pasaka mwaka 2000, tumekuwa
tukirejesha sehemu 
ya mapato ya viingilio kwa jamii kwa njia ya misaada kwa 
yatima, wajane na walemavu, lakini safari hii tumeona twende zaidi ya hapo kwa kujenga kituo cha watoto,” alisema. Alisema lengo ni kujenga kituo hicho cha kisasa ambapo kama mipango itakwenda vizuri, kitakamilika kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake kwani wangependa ndiye akizindue kwa kutambua mchango wake kwa tamasha hilo.

“Mwaka 2011, Rais Kikwete ndiye alikuwa mgeni rasmi wa
tamasha letu pale 
Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. “Kitendo cha Rais kuacha kazi nyingi na kuja kutuunga mkono kwenye shughuli hii  ya kiroho, kwetu ni jambo kubwa sana ambalo kamwe hatutalisahau, hivyo tumeona tumpe heshima hiyo ya kuzindua kituo hicho akiwa bado madarakani,” alisisitiza.

Msama ametoa wito kwa wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki
wa injili kujitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za kampuni yake kuandaa tamasha hilo kwa malengo mbalimbali ikiwemo kueneza injili ya Mungu na kusaidia makundi maalumu. 
Kuhusu waimbaji, Msama alisema wale wa nje wataanza kuwasili wiki ijayo na kuongeza kuwa hadi kufikia Ijumaa, waimbaji wote  watakuwa wamefika tayari kwa tukio hilo mbalo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Aliongeza kuwa idadi ya waimbaji imeongezeka baada ya kujitokeza
kwa mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Ntutuma kutoka nchini Kenya.
Baada ya kishindo cha tamasha hilo kutikisa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, itakuwa zamu ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Mwanza kabla ya mashambulizi kuhimishwa mkoani Mara.

WFP, IFAD NA FAO ZAAHIDI USHIRIKIANO NA TANZANIA

$
0
0

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekutana na wakuu wa taasisi za kimataifa za WFP, IFAD na FAO na kufanya nao mazungumzo kuhusu namna ya kuendeleza kilimo nchini Tanzania.
 
Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao Alhamisi (Machi 21, 2013) alipowatembelea kwenye ofisi zao jijini Roma, Italia kila mmoja kwa nyakati tofauti.
 
Mkurugenzi Mtendajiwa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Bi. Ertharin Cousin, alimweleza Waziri Mkuu kwamba shirika lake litaendelea kutumia bandari ya Dar es Salaam kusafirishia vyakula kwenda nchi zenye uhitaji wa chakula ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa ununuzi wa bidhaa kwa maendeleo (Purchase for Progress Programme).
 
“Tumekubaliana na wadau tunaoshirikiana nao, tuendelee kutumia bandari ya Dar es Salaam kupeleka mizigo Sudan ya Kusini na Uganda kwa sababu ya amani iliyopo nchini Tanzania. Kwa hiyo muamini kwamba sisi ni wadau wenu wa karibu na wa kuaminika,” alisema Bi. Cousin.
 
Akitoa mfano, Bi. Cousin alisema: “Kuna wakati kulikuwa na njaa kubwa kule Somalia na Zambia wakawa na hifadhi kubwa ya mahindi, lakini tulishindwa kusafirisha mahindi kutoka huko na kuyapeleka yanakohitajika kwa sababu ya hali mbaya ya usalama kwenye ukanda wa magharibi,” alisema.
 
Akizungumzia kuhusu ukuaji wa miji na kasi ya watu kuhamia mijini, Bi. Cousin alionya kwamba kuna haja ya kuwianisha uendelezaji wa miundombinu kwenye maeneo ya mijini na yale ya vijijini ili kuepuka tatizo la msongamano mkubwa wa watu mijini linalozikabili nchi nyingi zinazoendelea.
 
Alisema shirika lake limefanya utafiti nchini India na kubaini kuwa kadri kiwango cha ukuaji wa miji kinavyoendelea ndivyo kasi ya wakazi kuongezeka inavyozidi. “Tumeziainisha nchi za Kenya, Tanzania na Ethiopia na kuziweka kwenye mpango maalum ili zijipime jinsi zitakavyokuwa katika miaka 20 ijayo ili zisije kuwa na hali kama ya India hivi sasa,” aliongeza.
 
Naye, Rais wa Shirika la Kimataifa Kuendeleza Kilimo na Chakula (IFAD), Dk. Kanayo Nwanze alimweleza Waziri Mkuu kwamba shirika lake limeandaa mpando wa miaka mitatu ambao utazihusisha nchi 30 ikiwemo Tanzania ambazo zitafanyiwa impact evaluation kulingana na misaada ambayo zimekuwa zikipatiwa na shirika hilo.
 
“Tunataka tuangalie hali halisi kule Vijijini, je maisha ya wananchi yamebadilika kulingana na misaada ambayo tumekuwa tukiitoa? Je, wakulima wameongeza uzalishaji? Je wakulima wameunganishwa na masoko? Je, taasisi za kifedha zinawajali wakulima wadogo?” alifafanua Rais huyo wa IFAD.
 
Alisema hivi sasa wameanza kukusanya takwimu za awali (baseline data) katika nchi husika kabla ya kuanza kufanya tathmini itakayoanza mwaka huu hadi mwaka 2016.
 
Mapema, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), Bw. Jose Graziano da Silva alimweleza Waziri Mkuu kwamba shirika lake limetiliana saini makubaliano na benki ya Rabo (Rabobank) ili iweze kuwasaidia wakulima waliojiunga kwenye vyama vya ushirika.
 
“RaboBank imekubali kufanya kazi hiyo na imeichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zitakazokuwa waanzilishi wa mpango huo (pilot project)… watawasiliana nanyi muda si mrefu kuhusiana na suala hili,” alisema.Aliomba wakati mpango huo utakapoanza, wakulima wa Tanzania wawe tayari kushiriki kwenye mpango huo.
 
Waziri Mkuu Pinda kwa upande wake, katika nyakati tofauti aliwaarifu wakuu wa taasisi hizo za kimataifa juu ya hali ya uchumi wa Tanzania, Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP), Ukanda wa Kilimo wa Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT) na mchakato wa kuandaa Katiba mpya.
 
Alisema ili kuendeleza kilimo, ipo haja ya kushirikiana na wadau kutoka sekta binafsi kama njia ya kuleta maendeleo ya haraka nchini Tanzania. Bado tunayo changamoto ya kukabiliana na umaskini, lakini tunaamini kuwa kilimo ndiyo jawabu la tatizo hili,” alisema.
 
Waziri Mkuu alikwenda Roma, Italia kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye ibada maalum ya kumsimika Papa Francis iliyofanyika Jumanne, (Machi 19, 2013) kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Mt. Petro mjini Vatican, kisha akaamua kukutana na viongozi wa taasisi hizo.
 
Waziri Mkuu alirejea nchini Ijumaa, Machi 22, 2013).
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
JUMAMOSI, MACHI 23, 2013.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA SERIKALI YA UINGEREZA NA UJUMBE WAKE

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kulia kwake) aliyeongozana na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kushoto kwake) aliyeongozana na ujumbe wake wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013 kwa amazungumzo. Picha na OMR
======= ====== ======
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA
DAR ES SALAAM, MACHI 22, 2013
 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Ijumaa, amekutana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Bwana Mark Simmonds ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo sambamba na masuala mengine akaelezea shukrani zake kwa serikali ya Uingereza kwa kuwa na mahusiano mazuri na Tanzania na kwa kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
 Mheshimiwa Makamu wa Rais aliyekuwa anamuwakilisha Rais katika mapokezi hayo alisema, Tanzania inathamini mchango wa Uingereza katika sekta za elimu na afya na sasa ambapo kampuni za Uingereza hasa British Gas inajihusisha katika utafutaji wa Gesi katika bahari ya kina kirefu Kusini mwa Tanzania. Pia alizungumzia kuhusu mchango wa Uingereza kimataifa hasa katika masuala ya Mazingira na akamueleza Waziri Simmonds kuwa, Uingereza inaweza kusaidia nchi zinazokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa yenyewe kushirikiana na nchi kubwa duniani katika kuhakikisha kuwa zinatimiza wajibu wao katika kulinda mazingira.
 Kwa upende wake Waziri Simmonds yeye alimshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa mapokezi mazuri na kisha akaelezea furaha yake kwa mchango wa Tanzania katika kusaka amani katika nchi za Maziwa Makuu hasa DRC, Madagasca na Zimbabwe na kisha akafafanua kuwa, Tanzania ni mshirika mzuri wa Uingereza na kwamba nchi hii ni mfano wa kuigwa kutokana na ushiriki wake katika kusaidia amani kwa majirani zake sambamba na hatua zake za kuwapatia maendeleo wananchi wake.
 Waziri huyo alibainisha kuwa Uingereza iko tayari kuendelea kusaidia katika suala zima la uwazi na uwajibikaji na hasa katika maeneo ya Kodi na akashauri juu ya kuzidi kuwa na mashirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika shughuli za maendeleo.
Waziri Simmonds anakaa nchini kwa siku mbili na katika mkutano huu na Mheshimiwa Makamu wa Rais alifuatana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diana Melrose.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam, Tanzania

Novelist Chinua Achebe dies, aged 82

$
0
0

Chinua Acebe

Novelist Chinua Achebe dies, aged 82 Nigerian author  recognised for key role in developing African literature has died in Boston, where he was working as a professor

Chinua Achebe: 'grandfather of African fiction'.
Chinua Achebe, the Nigerian novelist seen by millions as the father of African literature, has died at the age of 82.
African papers were reporting his death following an illness and hospital stay in Boston this morning, and both his agent and his publisher later confirmed the news to the Guardian. Simon Winder, publishing director at Penguin, called him an "utterly remarkable man". "Chinua Achebe is the greatest of African writers and we are all desolate to hear of his death," he said.
In a statement, Achebe's family requested privacy, and paid tribute to "one of the great literary voices of all time. He was also a beloved husband, father, uncle and grandfather, whose wisdom and courage are an inspiration to all who knew him."
A novelist, poet and essayist, Achebe was perhaps best known for his first novel Things Fall Apart, which was published in 1958. The story of the Igbo warrior Okonkwo and the colonial era, it has sold more than 10m copies around the world and has been published in 50 languages. Achebe depicts an Igbo village as the white men arrive at the end of the 19th century, taking its title from the WB Yeats poem, which continues: "Things fall apart; the centre cannot hold."
"The white man is very clever. He came quietly and peaceably with his religion. We were amused at his foolishness and allowed him to stay. Now he has won our brothers and our clan can no longer act like one," says Okonkwo's friend, Obierika, in the novel.
The poet Jackie Kay hailed Achebe as "the grandfather of African fiction" who "lit up a path for many others", adding that she had reread Things Fall Apart "countless times". "It is a book that keeps changing with the times, as he did," she said.
Achebe won the Commonwealth poetry prize for his collection Christmas in Biafra, was a finalist for the 1987 Booker prize for his novel Anthills of the Savannah, and in 2007 won the Man Booker international prize. Chair of the judges on that occasion, Elaine Showalter, said he had "inaugurated the modern African novel", while her fellow judge, the South African Nobel laureate Nadine Gordimer, said his fiction was "an original synthesis of the psychological novel, the Joycean stream of consciousness, the postmodern breaking of sequence", and that Achebe was "a joy and an illumination to read".
Nelson Mandela, meanwhile, has said that Achebe "brought Africa to the rest of the world" and called him "the writer in whose company the prison walls came down".


The author is also known for the influential essay An Image of Africa: Racism in Conrad's Heart of Darkness (1975), a hard-hitting critique of Conrad in which he says the author turned the African continent into "a metaphysical battlefield devoid of all recognisable humanity, into which the wandering European enters at his peril", asking: "Can nobody see the preposterous and perverse arrogance in thus reducing Africa to the role of props for the break-up of one petty European mind?"
According to Brown University, where Achebe held the position of David and Marianna Fisher university professor and professor of Africana studies until his death, this essay "is recognised as one of the most generative interventions on Conrad; and one that opened the social study of literary texts, particularly the impact of power relations on 20th-century literary imagination".
Born in 1930 in Ogidi, in the south-east of Nigeria, the author won a scholarship to the University of Ibadan, and later worked as a scriptwriter for the Nigeria Broadcasting Service. He chose to write Things Fall Apart in English – something for which he has received criticism from authors including Ngugi wa Thiong'o – but Achebe said he felt "that the English language will be able to carry the weight of my African experience. But it will have to be a new English, still in full communion with its ancestral home but altered to suit its new African surroundings".
His fourth novel, 1966's A Man of the People, anticipated a coup that took place in Nigeria just before the book was first published. "I'd ended the book with a coup," Achebe told the Guardian, "which was ridiculous because Nigeria was much too big a country to have a coup, but it was right for the novel. That night we had a coup. And any confidence we had that things could be put right were smashed. That night is something we have never really got over."
His most recent work was last year's mix of memoir and history There Was a Country, an account of the Nigerian civil war of 1967 to 1970.
Achebe was a supporter of Biafran secession, but after the end of the civil war in 1970 he took what he described as a "sojourn" in politics. There he found that "the majority of people … were there for their own personal advancement", deciding instead to devote himself to academia.
He went on to write what he called a "limited harvest" of five novels – the most recent of which was 1987's Anthills of the Savannah. "I go at the pace of inspiration and what I can physically manage," he said.
In 1990 a car accident in Nigeria left him paralysed from the waist down, and forced his move to the US. "I miss Nigeria very much. My injury means I need to know I am near a good hospital and close to my doctor. I need to know that if I went to a pharmacist, the medicine there would be the drug that the bottle says it is," he said in 2007.
Achebe has twice rejected the Nigerian government's attempt to name him a Commander of the Federal Republic – a national honour – first in 2004, and second in 2011. In 2004 he wrote that "for some time now I have watched events in Nigeria with alarm and dismay. I have watched particularly the chaos in my own state of Anambra where a small clique of renegades, openly boasting its connections in high places, seems determined to turn my homeland into a bankrupt and lawless fiefdom. I am appalled by the brazenness of this clique and the silence, if not connivance, of the presidency … Nigeria's condition today under your watch is, however, too dangerous for silence. I must register my disappointment and protest by declining to accept the high honour awarded me in the 2004 honours list."

Ras Inno kutambulisha rasmi bendi yake

$
0
0

MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya reggae hapa nchini, Ras Inno Nganyagwa,anatarajia kuitambulisha rasmi bendi yake katika onesho mahsusi linalotarajiwa kufanyika katikati ya mwezi ujao jijini Dar es Salaam.

Akizungumza hapa jamvini, Ras Inno alisema kwamba huo ni mwanzo wa kutimiza mikakati yake ya harakati za kurudi kwenye fani baada ya kujiweka pembeni kwa muda mrefu. Alisema kwamba, onesho hilo licha ya kuitambulisha bendi hiyo, lakini pia litakuwa mahsusi kwa ajili ujio wake mpya wenye mbinu za kisasa za kiweledi za kufanya kazi.

Nguli huyo ambaye pia ni mtafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii na mwandishi maarufu wa safu mbalimbali katika magazeti ya hapa nchini, alibainisha kuwa baada ya kuwa nje ya ulingo kwa muda mrefu.

“Nimeamua kurudi rasmi kivingine kwenye fani baada ya kuusoma muziki wa reggae nikiwa pembeni na kubaini mapungufu kadhaa niliyotathmini, hivyo nimebuni mikakati mbadala tofauti ya namna bora ya kurudi jukwaani kwa dhamira ya kuipaisha reggae, pia kukonga nyoyo za mashabiki wake ambao hawajamuona jukwaani kwa muda mrefu,” alisema.

Akifafanua zaidi alisema kuwa licha ya kuitambulisha bendi yake ya kudumu atakayokuwa akitumbuiza nayo, tofauti na zamani ambapo alitumbuiza zaidi kama mwanamuziki huru anayepiga na kundi la wapiga vyombo bila jina rasmi la bendi.

Onesho hilo mahsusi pia litakuwa maalum katika kuitambulisha taasisi yake aliyoiunda itakayosimamia kazi zake ikiwemo bendi, pamoja na miradi aliyoibuni yenye lengo la kuupromoti muziki wa reggae ili kuhakikisha vijana wengi wanavutika na kujitosa kwenye miondoko hiyo, ili kupanua wigo wa idadi ya wanamuziki wa reggae kwa kuibua vipaji vipya.

Alisema onesho hilo litakalohudhuriwa na wadau wa muziki watakaoalikwa ambao taasisi yake inatarajia kushirikiana nao siku za usoni, litatumika pia kuitambulisha rasmi albamu yake mpya ya nne aliyoirekodia katika studio za Soundcrafters zilizopo Temeke hapa jijini, anayotarajia kuizindua hivi karibuni.

“Katika onesho hilo nitapiga nyimbo zangu zilizonipatia umaarufu miaka ya nyuma ukiwemo wimbo wa ‘Gila’ kutoka albamu ya Money-Pesa (1994), pamoja na nyimbo nyingine kutoka albamu zangu mbili zilizofuata na nyimbo mpya kutoka katika albamu mpya ya ‘Kwa Nini’.”

Utambulisho huo ni mwanzo wa maandalizi ya uzinduzi utakaofuatiwa na ziara ya maonesho yasiyopungua 10 katika awamu ya kwanza, itakayoanzia hapa jijini kabla ya kuelekea nyanda za juu Kusini na baadaye awamu ya pili itahusisha kanda ya Kaskazini na ziwa katika mfululizo wa maonesho ya kupromoti albamu yake mpya na muziki wa reggae kwa ujumla.

Katika onesho la utambulisho atasindikizwa na kundi la Kizazi Kipya cha Reggae, bendi ya Fimbo inayopiga miondoko ya asili, mwimbaji wa muziki wa gospo Mrs Annette Mwasambogo na Dj maarufu wa disco la reggae hapa nchini Aluta Warioba kutoka redio ya Times FM. 

Rose Muhando kutambulisha mambo mapya Pasaka

$
0
0
MWIMBAJI nguli wa muziki wa kiroho, Rose Muhando amejipanga kisawaswa katika Tamasha la Pasaka mwaka huu na anatarajia kutambulisha albamu yake mpya iitwayo Tazama Mungu Anacheka.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa mwimbaji huyo amemuhakikishia kuwa amewaandalia mashabiki wake vitu vikubwa kwenye tamasha hilo litakalofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumapili wiki hii na siku inayofuata Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Msama alizitaja nyimbo zilizopo katika albamu hiyo kuwa ni Mungu Anacheka, Tenda Wema, Mungu Unshangaza, Mwanamke Mbaya, Sema Nami, Penye Raha,Heri Wenye Moyo, Shujaa wa Msalaba na Tembea Baba. 

Akizungumzia maandalizi ya onesho hilo, Msama alisema yanaenda vizuri na kwamba wasanii wan je ya nchi wanatarajiwa kuanza kuwasili Alhamisi wiki hii na kuwaomba mashabiki wakae mkao wa kula kupata mambo mazuri.

Wasanii wan je ya Tanzania watakaotumbuiza ni kundi la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda  ambalo pia linatarajia kuzindua albamu yao mpya iitwayo Kaeni Macho. Wasanii wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.

Wasanii wa Tanzania waliothibitisha licha ya Rose Muhando ni Upendo Nkone, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival, Bonny Mwaitege, Upendo Kilahiro na kundi la Glorious Celebration.Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NYUMBANI KWAKE

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Kulia ni Mke wa Mzee Kingunge
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Picha na OMR

NEW PRESIDENT OF CHINA XI JINPING RECEIVES ROUSING WELCOME IN DAR ES SALAAM

$
0
0
 China's new President Xi Jinping arrived in Tanzania today ahead of   a three-nation Africa tour also taking in South Africa and the Republic of the Congo. 
President Xi  flew into  Dar es Salaam with his wife from Moscow. After holding official talks scores of ministers and CEO of Chinese companies signed a totalo of 16  accords before the new President of China gave  a keynote speech on relations with Africa during a state banquet later on.


He is scheduled to head to Durban, South Africa, tomorrow  for a summit of leaders of the world's major emerging economies, known as the BRICS, on Tuesday and Wednesday, and could endorse plans to create a joint foreign exchange reserves pool and an infrastructure.


 Banners with smiling faces of the two presidents
 Welcome to Tanzania a girl greets the President of China and his wife after she and the boy gave the visiting dignitaries bouquet of flowers
 President Jakaya Kikwete welcomes President Xi Jinping and his wife to Dar es salaam
 A warm welcome for President Xi Jinping at the Serena Inn in Dar es salaam
 President Xi Jinping's motorcade arrives at the Eastern Gate of the State House 
 Guest and host work the crowd of hundreds of Dar es salaam residents
 The two Presidents wave to the huge crowd below
 Official talks

Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images