Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

Taifa stars yaichachafya morocco 3-1 uwanja wa Taifa

0
0

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Thomas Ulimwengu akiwatoka Golikipa na Beki wa Timu ya Taifa ya Morocco wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia Mwaka 2014 kule nchini Brazil,uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda Bao 3 - 1,mabao mawili yaliyotiwa kimiani na Mshambuliaji Machachari,Mbwana Samatha huku moja likifungwa na Thomas Ulimwengu.
Beki wa Timu ya Morocco akiruka juu kuondosha hatari iliyokuwa ikielekeza langoni mwake.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Thomas Ulimwengu akiwatoka mabeki wa Timu ya Taifa ya Morocco wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Kombe ya Dunia Mwaka 2014 kule nchini Brazil,uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.
Hatari langoni mwa timu ya Morocco.............
Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),Shomari Kapombe akichuana vikali na Beki wa timu ya Morocco wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Kombe ya Dunia Mwaka 2014 kule nchini Brazil,uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.
Lango la timu ya Morocco ilikuwa ni hatari muda wote wa mchezo.
 Kipa wa Timu ya Morocco akiusindikiza kwa Macho mpira ulioingia wavuni,baada ta kuigwa na Mchezaji Mbwana Samatta wa Taifa Stars.
Mbwana Samatta akishangilia goli lake. wakimfukuzia.

Kikosi cha Taifa Stars.
Kikosi cha Morocco.
Mashabiki wa Taifa Stars wakiendelea kufurahia ushindi wa timu yao.
Wachezaji wa Taifa Stars wakimpongeza mwenzao Thomas Ulimwengu baada ya kufunga bao la kwanza.
Shangwe tupu uwanja wa Taifa.
Ulinzi wa nguvu uwanja wa Taifa.

Website ya Ngoma Africa Band aka FFU yaanza kurusha muziki hewani tena !

0
0


Website www.ngoma-africa.com ya Ngoma Africa Band aka FFU imeanza tena kurusha muziki hewani, baada ya marekebisho machache yanayo endelea kufanyika ili kubadili
sura yote  mtandao huo.

Tuvoti hiyo ya ilisimamishwa kurusha muziki hewani kwa muda wa siku nzima sasa inarusha tena muziki hewani na mnaweza kuendelea kupata burudani kamili tena kwa kusikiliza nyimbo aka (Virungu vya FFU) at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com Usikose kuwasiliana nao at contact@ngoma-africa.com.

MSTAHIKI MEYA WA ILALA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA MOROGORO YA MAGARI YAENDAYO KWA KASI.

0
0

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akijadili na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) Asteria Mlambo pamoja na watendaji wengine umuhimu wa kufanyika mkutano wa pamoja ili kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza wakati ziara yake ya kukagua ujenzi wa barabara ya magari yaendayo kwa kasi katika barabara ya Morogoro hadi Sokoine.
Picha juu na chini ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) Asteria Mlambo (aliyenyoosha mkono) akifafanua jambo kwa Mstahiki Meya wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo.
Muonekano wa Barabara ya Morogoro ambayo bado inayoendelea kukarabatiwa kwa ajili ya magari yaendayo kwa kasi ambayo imekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara na pia sasa imegeuka kuwa njia maarufu ya Bodaboda zinazoendeshwa kwa kasi na kuwa hatari kwa watembea kwa miguu ambao wamekuwa wakigongwa katika barabara hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumzia changamoto zinazojitokeza kufuatia ujenzi wa barabara ya Morogoro ambapo limejitokeza suala la wafanyabiashara kuona kwamba itakapo kamilika magari madogo yatakuwa hayapiti tena barabara hiyo hivyo hawajui hatma ya biashara zao haswa kuanzia Bibi Titi hadi Sokoine na kusema iko haja ya kukaa na wafanyabiashara hao kuwaeleza kuwa maendeleo hayakwepeki.

Akijibu baadhi ya kero na maswali ya wakazi wa jiji kuhusu kucheleweshwa na kuvurugwa kwa taratibu za barabara hiyo, Mstahiki meya amesema hiyo inatokana na watu haswa wafanyabisha kujijengea miundo mbinu bila kufuata taratibu za jiji, kitu ambacho kimesababisha mkandarasi anapofanya kazi yake anakutana na mitaro, bomba za maji safi na taka, mikongo ya mawasiliano ambazo haziko kwenye ramani na hapo lazima awatafute wahusika nao wanataratibu zao hivyo kuwa kikwazo kwake kukamilisha ujenzi huo.
Mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo Andrew John Shayo akielezea malalamiko yao kuwa tangu ujenzi wa barabara hiyo uanze biashara hazifanyiki kwa kuwa magari madogo hayapiti pia kumekuwa na tatizo la kupatikana kwa maji kutokana na mkandarasi huyo kukatakata mabomba ya DAWASCO na kuwa pindi mvua zinaponyesha maji yamekuwa hayaendi na kusababisha madimbwi na kushauri ukarabati huo uharakishwe kwa kuwa wao ndio waathirika wakubwa wa ujenzi huo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) Asteria Mlambo akifafanua kuwa mradi huo una mafungu saba ya utekelezaji na kati ya hayo fungu la saba lilishakamilishwa ambalo ni uhamishaji wa nyaya za Umeme lakini Kandarasi kuu tuliyonayo sasa hivi ambayo inawagusa watu wengi wa Dar es Salaam ni ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, na kuwataka watu kuwa wavumilivu kwa kuwa mkandarasi anashughulikia kwanza barabara kutoka Kimara hadi Kivukoni.
Picha Juu na chini ni Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa katika eneo lenye dimbwi la maji ameshauri Ili kupunguza msongamano tunafanya utaratibu angalao sasa tufungue barabara za India, jamhuri, Libya ili angalao kupunguza msongamano wa upande mmoja wa mji lakini baadae itabidi kujadiliana ili ujenzi huu ukikamilika mwezi Juni kutakuwa na changamoto za aina gani kwa pamoja na viongozi wa mitaa, wafanya biashara, wenzetu wa DART ili tuone biashara za watu zitaendelea kwa staili ya aina gani.

Amesema hatuwezi kubaki na jiji lilelile la zamani lazima tubadilike, kwa mradi wa kisasa kama huu Tanzania kwa maana ya jiji la Dar es Salaam ndio litakuwa la pili barani Afrika, mradi kama huu mpaka sasa uko Afrika Kusini peke. Na hizi barabara zinajengwa kwa kiwango cha zege hivyo zinadumu kwa miaka mingi.


Na.Mwandishi wetu
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa ameitisha mkutano wa pamoja na wafanyabiasha, wadau na watendaji wa idara mbalimbali za serikali ili kujadili changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi (DART).

Mstahiki Silaa amefikia uamuzi huo baada ya kujionea changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa mradi huo katika makutano ya barabara za Bibi Titi na Morogoro hadi barabara ya Sokoine ambazo zimekuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara na wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza baada ya kufanya ziara ya mradi huo katika barabara hizo, Silaa amesema kuna haja ya kuwepo kwa mkutano wa wadau mbalimbali kutoka Shirika la Nyumba (NHC), Mamlaka ya Maji Dar es Salaam (DAWASCO), Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na wafanyabiashara katika maeneo ya mradi huo ili kujadili na kufikia muafaka wa pamoja wa kutatua changamoto hizo.

Meya huyo amesema changamoto ni nyingi lakini zinaweza kutatuliwa ikiwa wadau wote wanaohusika katika mradi huu watakutana na kujadili kwa kina njia na hatua stahiki za kukabiliana na changamoto hizo.

Amezitaja changamoto ambazo zinajitokeza wakati wa mradi huo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa foleni baada ya njia nyingi kufungwa, kukosekana mahala pa kuegesha magari, kutokuwepo na njia za kupitisha magari ya zima moto na uharibifu wa miundombinu ya maji wakati wa ujenzi wa barabara.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Asteria Mlambo amesema kuwa pamoja na changamoto hizo zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi lakini jitihada za makusudi zinafanyika kuzitatua hasa zile zilizo ndani ya uwezo wetu.
Amesema mwenendo wa mradi huo unakwenda katika malengo yaliyopangwa kulingana na makubaliano ya mkandarasi wa mradi huo Strabag ili kutekeleza ahadi yake kwa Serikali ya kukamilisha mradi huo hadi ifikapo mwaka 2015.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi huu unaendelea vizuri pamoja na changamoto za hapa na pale, tunaomba ushirikiano wa wananchi na watumiaji wa barabara kwa ujumla kuheshimu na kufuata maelekezo ya barabarani yanayowakataza kutumia barabara zilizo kwenye matengenezo.

Stanbic Bank Tanzania encourages women to use land as collateral

0
0
Stanbic Bank Tanzania Home Loan Manager Miranda Lutege, makes a presentation on how bankers avail opportunities to women to use land as collateral investment through Mortgage, during 2013 Annual General Meeting for Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA) and Continuing Legal Education sponsored by Stanbic Bank Tanzania, held at Bank of Tanzania hall at the weekend. The meeting had the theme; from being defensive to being proactive: Women, Land and Investment.

UMOJA WA SEREKALI ZA WANAFUNZI ZANZIBAR ZAHOJI JUU YA SABABU ZA KUFELI OVYO KWA MWAKA HUU.

0
0
  Mshereheshaji wa Umoja wa Serekali za Wanafunzi Zanzibar Hissham Muamed Abdukadir akisoma ratiba ya Kongamano linalouliza sababu zinazopelekea kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi wa Zanzibar.
 Katibu wa USEWAZA Salum Humoud Salum akinukuu badhi ya sababu zilizopelekea kushuka kwa ufaulu kwa wanafunzi wa Zanzibar zilizoandikwa kwenye gazeti la Zanzibar Leo.katika Kongamano lililofanyika Ukumbi wa Cafe Restaurant Bwawani Mjini Zanzibar.
 Msanii Ali Husen (wakulia) kutoka USEWAZA akimshawishi wanafunzi Abdallah Juma kutumia madawa ya kulevya,jambo ambalo hilikubaliki.Huko katika Ukumbi wa Cafe Restaurant Bwawani Mjini Zanzibar.
  Mwanafunzi Monika Samuel Makoya kutoka Skuli ya Kinuni akiuliza suali juu ya uhaba wa vifaa vya sayans na walim wake kwa Mkurugenzi wa Tasisi ya Elimu Zanzibar Huko katika Ukumbi wa Cafe Restaurant Bwawani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

 Mkurugenzi wa Tasisi ya Elimu Zanzibar wa pili (kushoto) Sleman Yahya Ame akijibu maswali alioulizwa na walim na wanafunzi waliofika kwenye Kongamano hilo,wakwanza (kulia) Haji Kutenga Mlezi USEWAZA,anaefata Abdulla Bakari Khamis Mahusiano (WEMA) na wakwaza kushoto,Sleman Takadir.

Neno La Leo: Yesu Akasema; " Simon, Acha Kuvua Samaki, E Nenda Ukawe Mvuvi Wa Watu"

0
0


Ndugu Zangu,
 Bwana Yesu alipotembelea mto Galilaya, aliwakuta wavuvi wakivua samaki, Simoni alikuwa ni miongoni mwa wavuvi hao. Yesu akasema; " Simoni, acha kuvua samaki,nifuate ukawe mvuvi wa watu.

Naam, watu wengi wanaangamia kwa kukosa uelewa. Kwa kutojitambua. Wanahitaji ukombozi wa kifikra. Na siku zote, haki uinua taifa, vivyo hivyo, dhulma huangamiza taifa. Na mahala pasipo na haki, basi, hapo hapatukuwa na amani.

Oneni, maovu yametamalaki katika dunia tunamoishi. Siku zote, kujipendelea ndilo shina la maovu. Si tuna mifano hai.
Oneni, wale wenzetu waliokaa na wakaamua kuuza nyumba za Serikali. Na Waziri mwenye dhamana  alisimamia utekelezaji wa dhulma ile kwa Watanzania, huku naye akiwa ameshajikwapulia nyumba yake. Lililopelekea uamuzi wa hila na ghilba wa kuuza nyumba za serikali ni ubinafsi na hulka ya baadhi ya viongozi kutaka kujipendelea.  

Karibu wote waliouziwa au kujiuzia nyumba hizo za Serikali, nyumba za wananchi, tayari walikuwa na nyumba kabla. Siku zote, hamu inakuwa ni jambo jema, endapo binadamu ataweza kuitawala hamu/tamaa yake.Wanadamu tusipoitawala hamu yetu, tukaanza kujipendelea, kuwasahau wengine, basi, hilo huwa ndio chimbuko la maovu.

Hupelekea kutoelewana baina ya wanandugu, na hata kwa marafiki walioshibana. Hupelekea vurugu na machafuko katika jamii. Tunazungumzia uwepo wa upendo, haki na usawa. Dini nyingi zinazungumzia umuhimu wa upendo, haki na usawa katika jamii. Iwe ni Uislamu na Ukristo vivyo hivyo.

” Naapa kwa zama . Hakika binadamu wote wamo katika hasara isipokuwa wale walioamini na wakafanya matendo mema. Wakahusiana na haki na wakahusiana na subira” (Koran tukufu, Surat ASWR) Biblia nayo inasema; kuwa Kaini alikuwa mtu wa kujipendelea mno, akamwua nduguye. Mfalme Saulo alijipendelea mno, akamdhulumu Daudi. Yuda alijipendelea mno, akakubali kumsaliti Yesu kwa Vipande thelathini vya fedha. Hatimaye,  akamsaliti Yesu. 

Na ufufuko wa Bwana Yesu utukumbushe jukumu letu la kupambana na maovu katika jamii. Utukumbushe jukumu la kusaidia kazi ya kuwakomboa kifikra wanadamu wenzetu.
Kama Bwana Yesu alivyomkumbusha Simoni kwa kumwambia; ” Simoni, acha kuvua samaki. E nenda ukawe mvuvi wa watu.

Ni Neno la Leo.
Pasaka Njema.

Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam
0788 111 765

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kashfa ya vyeti vyake

0
0

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti.
Philipo Augustine Mulugo ndiyo jina lake halisi ambalo alilisomea mpaka alipohitimu darasa la saba kwa mara ya kwanza 1988, lakini kutokana na kwamba hakufaulu kwenda sekondari alirudia darasa hilo.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa takriban miezi mitatu sasa umebaini kuwa 1989, Mulugo alirudia darasa la saba katika Shule ya Msingi Rukwa ya mkoani Mbeya akitumia jina la Hamimu Hassan.
Imebainika kuwa kabla ya kuhitimu darasa la saba kwa mara ya pili, alibadili jina hilo (kutoka Hamimu Hassan) na kuwa Hamimu Augustino ambalo aliendelea nalo wakati akisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari kutwa ya Mbeya (Mbeya Day) mwaka 1990.
Hata hivyo, Mulugo mwenyewe akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam alipuuza tuhuma hizo kwa kusema kuwa ni njama za kisiasa zinazofanywa na maadui zake. Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule.
“Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo na kuongeza:
“Haya mambo kabla hata sijachaguliwa kuwa Mbunge, tulivyokuwa bado kwenye mchujo wa ndani, usiku wa manane watu walisambaza huu uvumi na nilivyoenda kwenye kikao nikatoa vyeti vyangu, wakaviona.”
Waliomfundisha
Baadhi ya walimu waliomfundisha Mulugo, watu waliofanya kazi naye pamoja na wakazi wa Kijiji cha Udinde alikozaliwa, maelezo yao yanathibitisha mabadiliko ya majina ya Mulugo kwa nyakati tofauti pia ngazi mbalimbali za kielimu.
Uchunguzi unabainisha kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne, alifaulu kwenda Shule ya Sekondari ya Wavulana, Songea ambako alisoma kati ya 1994 na 1996 akiendelea kutumia jina la Hamimu Mulugo.
Baada ya kuhitimu kidato cha sita, uchunguzi ulibaini kuwa Mulugo alirejea Mbeya na 1998 alilazimika kubadili tena jina pale alipotumia cheti cha mtu aitwaye Dickson Mulungu, kuombea kazi ya kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Southern Highlands.
Habari zinasema Mulugo alichukua hatua hiyo ili kumshawishi mmiliki wa shule hiyo mfanyabiashara, Gulnoor Dossa (sasa ni marehemu), kumpa nafasi ya kufundisha shuleni hapo.
“Mulugo alilazimika kutumia cheti cha rafiki yake aliyekuwa akiitwa Dick Mulungu ambaye alipata daraja la pili katika Shule ya Sekondari ya Songea Boys, hivyo ikawa rahisi kwake kupata kazi ya ualimu katika shule hiyo,” alisema mmoja wa waliofanya kazi naye shuleni hapo (jina tunalihifadhi kwa sasa).
Aliongeza kuwa Mulugo alianza kama mwalimu wa kawaida, lakini baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Shule (headmaster) wakati hakuwa hata na cheti cha ualimu. Alichukua nafasi hiyo ya ukuu wa shule baada ya aliyekuwapo kufariki dunia. ZAIDI ENDELEA HAPO CHINI KWENYE LINK

Dada Rachel anatafuta mwenza wa kuishi naye.

0
0

Mimi ni mwanamke, natafuta mwenza ambaye ni mcha mungu. Dini awe mkristo kutoka dhehebu lolote.awe na miaka kuanzia 33 mpaka 43. Nahitaji mtu aliye mcha Mungu, ambaye yupo tayari kutulia na kuanzisha familia. Ambaye hajawahi kuoa wala hana watoto. Nitashukuru ukiniwekea tangazo langu.
 
Mawasiliano yangu ni:


Greetings from JBG - Kibanda & Wife

0
0
 
Hope all is well.
Salamu nyingi saaana toka JBG!
I could not resist! Yes I cried! But Absalom is the same person I knew last two months! Amesimama! Mungu ni Mwema!!!
Anaomba watanzania wamwombee na amesema anaendelea vizuri kwa sasa…
Cheers,
Hoyce Temu.

Rais Kikwete apokea ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa julius Nyerere toka kwa Rais wa China Xi Jinping

0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Ukumbi huo umejengwa kwa ushirikiano kati ya Seriklai ya China na Tanzania.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Xi Jinping wa China wakishangilia jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia picha za matukio mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya China na Tanzania katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo wakati wa sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa China Mhe.Xi Jinping pamoja na Mkewe katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya sherehe za ufunguzi wa ukumbi huo leo.picha na Freddy Maro,Ikulu.

TIMU NNE ZAINGIA AWAMU YA PILI YA KIPINDI CHA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ WIKI IJAYO

0
0
Tarehe 20 mwezi Machi katika kipindi cha televisheni cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV kila Jumatano ikiwa ni Sehemu ya pili kati ya mfululizo vipindi hivyo halisia, Watanzania Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad walionyesha namna ambavyo mtu hapaswi kukata tamaa baada ya kushinda kwa kuwatoa wapinzani wao kutoka Kenya na Uganda katika raundi ya kwanza na kutinga nusu fainali, hatimaye kujinyakulia Dola za kimarekani 5,500 katika ukuta wa GUINNESS.

Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad wameonyesha namna gani kama mwanamichezo hapaswi kukata tamaa uwapo uwanjani na wanamatumaini makubwa kuwakilisha nchi katika mashindano ya Pan African ambapo wanaweza kushinda hadi dola za kimarekani 250,000.

Washiriki bora watakwenda kukutana ana kwa ana na mashabiki wa soka kutoka nchi za Cameroon,Ghana,Kenya, na Uganda ili atakayeonyesha ujuzi zaidi atavishwa taji la ubingwa wa` Pan-African’ na kupata kitika cha fedha kitakachobadilisha maisha yao.

Washiriki wote wana nafasi kuonyesha ujasiriwa kuipigania nchi yao. GUINNESS ilizunguka katika nchi yetu kusaka washiriki wazuri watakaonyesha umahiri wao wakiwa na matumaini lukuki na timu itakayoonyesha ujuzi zaidi itachaguliwa katika hatua nyingine ya kipindi hiki cha msimu wa pili.

Katika Episodi ya pili ya mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana siku ya Jumatano.

Hizi ndizo timu zitakazochuana vikali katika kipindi cha pili wiki hii cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.



Blue team – Tanzania – Magpies:

Simon Chimbo(21), Emmanuel Temu(20), wote kutoka Dar Es Salaam, ni mashabiki wakubwa wa Manchester United. Simon anasoma Teknolojia ya mawasiliano katika chuo cha Utawala wa Fedha IFM na Emanuel ni mcheza soka kutoka timu ya Mt. Camlius.

Red team – Kenya – Hawks:

Wawili hawa wanatoka Mombasa watavaa mashati mekundu kuonyesha upendo wao kwa mpira wa miguu katika sehemu ya pili Nyuma Donald Otieno( 36), atakuwa nguzo ya timu ,Awadh Mbarak(22), ataangalia masuala fiziki. Donald ni mwalimu wa soka na Awadh ni mwanafunzi

Green team – Uganda – Flex:

Mfanyabiashara Ibra Kawooya, (30), kutoka Namusuba na mwenzie Alex Muyobo(31) ambaye alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya mguu, wote ni mashabiki wa Manchester United .

Black team – Kenya – The Blues:

Francis Ngigi (23), kutoka Nairobi na Kepha Kimani (25), kutoka Thika watakaovalia fulana nyeusi watawakilisha Kenya katika sehemu ya 2. Francis ni Mfanyabiashara na ndo anatarajiwa kuwa kichwa cha Timu.

Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.

Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/ guinnesskenya Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufatilia ukurasa huu yaani ‘like’
na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga
yako.

Usisahau pia kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.

*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.

Compass yatahadharisha wanatumia jina la Flaviana kutapeli

0
0

KAMPUNI ya Compass Communications imewatahadharisha warembo  na wanamitindo wote nchini kutorubuniwa na genge la watu wanaotumia jina la Flaviana Matata kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai amesema jana kuwa kuna genge la watu wanaotumia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa facebook ujulikano kwa jina la Flaviana Matata’s  na kujipatika fedha kiasi cha sh. 200,000 kwa jila anayejiunga kwa lengo la kutafutiwa kazi au nafasi ya kufanya shughuli za wanamitindo nje ya nchi.
Maria alisema kuwa watu hao huwarubuni wasichana na kuwaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa mgongo wa Flaviana na mmoja wa vijana hao amejitambulisha kama ‘kaka’ yake mwanamitindo huyo, jambo ambalo si la kweli.
Alifafanua kuwa baada ya kukutana na wasichana waliongia katika mtego huo, huwa wanaawalaghai kwa njia mablimbali na baadaye kulipa kiasi hicho cha fedha. Alisema kuwa hali hiyo imewaletea usumbufu wasichana wengi na kujikuta wakihaha kutafuta ukweli baada ya kutapeliwa.
“Compass Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za Flaviana Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa njia yoyote na ukurasa huu au watu hawa.  Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe waangalifu kwani Flaviana Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu yoyote kazi ya  uanamitindo popote pake,” alisema Maria.
Maria alisema kuwa ukurasa halisi ya Flaviana Matata kwenye mtandaomwa Facebook ni “Flaviana Lavvy Matata” na kwa sasa wanendelea kushirikiana na vyombo husika kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu huo.

wema sepetu umetishajee..amlipia kajala faini ya sh mil 13 na kuachiwa huru.

0
0

MSANII nyota wa Filamu hapa nchini, Wema Sepetu amemlipia faini ya shilingi milioni 13 msanii mwenzake, Kajala Masanja, na kumfanya awe huru. Mapema leo, Kajala alihukumiwa kwenda jela miaka 5 au kulipa faini ya shilingi milioni 5. Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na tuhuma za kutakatisha fedha haramu. Faraji yeye amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 213.

Rais Kikwete na Rais Xi Jinping waweka shada la maua katika katika Makaburi ya wataalamu wa kichina huko Majohe ukonga

0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa China Xi Jinping wakiweka mashada ya maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA.Viongozi hao waliweka mashada hayo ya maua katika makaburi hayo yaliyopo katika kijiji cha Majohe,Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan wakiweka maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA huko katika kijiji cha Majohe,Ukonga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wa Rais Xi Jinping wakishuhudia(picha na Freddy Maro).

RAIS WA ZANZIBAR,DK. SHEIN AKUTANA NA RAIS WA CHINA WAZUNGUMZA,LEO SERENA HOTEL DAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping,katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam,walipokutana leo asubuhi ikiwa ni hatua ua ushirikiano katika nchi mbili hizi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Balozi Mdogo wa China anyeishi Zanzibar Bibi Chen Yiman,baada ya mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping,leo asubuhi katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping,katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam,walipokutana kwa mazungumzo ya Kiutendaji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akimtambulisha Waziri wa Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee,kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping,katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam,walipokutana kwa mazungumzo ya Kiutendaji.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

KITABU CHA KIFO NI HAKI YANGU CHAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR LEO

0
0
Mtunzi mashuhuri wa vitabu kutoka kampuni ya Mkuki na Nyota, Mzee Walter Bgoya, akikata utepe pamoja na mtunzi wa kitabu cha 'Kifo ni Haki Yangu', Eric James Shigongo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo. Mtunzi wa kitabu cha 'Kifo ni Haki Yangu', Eric James Shigongo, akiongea na wadau (hawapo pichani) waliofika katika uzinduzi wa kitabu chake katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar.
Mtunzi Eric Shigongo akimpatia kitabu mtunzi mwenziye, mzee Walter Bgoya.
Mzee Walter Bgoya akiongea na wanahabari wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Eric Shigongo cha 'Kifo ni Haki Yangu'.
Afisa wa polisi Patrick Massawe ambaye pia ni mtunzi mashuhuri wa hadithi za magazeti nchini, akisainiwa kitabu na Shigongo wakati wa uzinduzi.
Eric Shigongo (kushoto), akibadilishana mawazo na msomaji wa hadithi zake, Ahmed El Maamry, wakati akimsainia kitabu.
Eric Shigongo akimsainia kitabu mwanaye, Samwel Shigongo.
Eric Shigongo akisaini kitabu kwa ajili ya mwandishi wa Nipashe, Somoe Ng'itu.
Shigongo akiwasainia vitabu baadhi ya wasomaji waliohudhuria uzinduzi huo.
Waratibu wa uzinduzi wa kitabu cha 'Kifo ni Haki Yangu', Abdallah Mrisho (kulia) na Angela Msangi wakisubiri uzinduzi.
Afisa wa polisi Patrick Massawe na msomaji mwingine wakipitia baadhi ya kurasa za kitabu cha Eric Shigongo aliyesimama kulia.
Baadhi ya wasomaji waliohudhuria uzinduzi huo.
Shigongo akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa duka la TPH.
MTUNZI mahiri wa vitabu nchini, Eric James Shigongo, leo amezindua rasmi kitabu chake cha 'KIFO NI HAKI YANGU' katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House (TPH) lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, wasomaji 50 wa mwanzo walipata fursa ya kupata zawadi ya kitabu hicho bure kilichosainiwa na mtunzi. Kujipatia nakala ya kitabu hicho na vinginevyo, wasiliana au fika katika vituo tajwa hapo chini:
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)

CHINESE PRESIDENT XI JIN PING MAKES MAIDEN SPEECH ON AFRICA IN DAR ES SALAAM TODAY

0
0

 President Jakaya Mrisho Kikwete listen keenly as  his guest Chinese President Xi Jinping makes  his maiden speech in  Africa during the handing over ceremony of the Mwalimu Julius Nyerere Convention Centre.


The Visiting Chinese President delivered an important speech, expounding on China-Africa relations and China's Africa policy. 


President Xi arrived in Dar Es Salaam on Sunday for a state visit to Tanzania, the second leg of his first foreign trip after he assumed presidency earlier this month.

 President Jakaya Mrisho Kikwete and his guest Chinese President Xi Jinping applaud to the mammoth crowd. 
President Jakaya Mrisho Kikwete speaks as his guest Chinese President Xi Jinping during the handing over ceremony of the Mwalimu Julius Nyerere Convention Centre. For more photos CLICK HERE

PARTY KUBWA ya PASAKA kudondoshwa MZALENDO PUB, Millennium towers J'PILI ya PASAKA katika kusheherekea SIKUKUU ya PASAKA

0
0

Utafiti wa Tamwa wamrudisha mwanafunzi shuleni

0
0

 Mwenjuma Magalu (wa kwanza kulia mstari wa pili) ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha  pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo akiwa darasani na baadhi ya wanafunzi wenzake  alipotembelewa na mwandishi wa habari hizi.
Bibi wa mwanafunzi Mwenjuma Magalu, Amina Mohamed (kulia) akizungumza na Mhariri wa mtandao wa  Thehabari, Joachim Mushi kijijini Msasa, wilayani Handeni juzi. 
======  =====  =======
Utafiti wa Tamwa wamrudisha mwanafunzi shuleni 

Na Thehabari.com, Handeni

UTAFITI wa kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 umefanikisha kumrudisha shuleni mwanafunzi wa sekondari aliyekuwa ametelekezwa yeye pamoja na familia yao.

Mwenjuma Magalu ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo alitelekezwa na babayake yeye pamoja na mamayake mwaka jana, hivyo kushindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo licha ya kuchanguliwa kuendelea na masomo.

Hata hivyo baada ya utafiti wa kihabari kufanyika kijijini Msasa Wilaya ya Handeni na taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na sekondari baada ya mamayake (kwa sasa marehemu) kukosa uwezo kuripotiwa, alijitokeza mfadhili wa kumsomesha ambaye anagharamia masomo yake hadi sasa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi akiwa shuleni Komnyang’anyo, mwanafunzi huyo aliishukuru TAMWA kwa kuibua tatizo la familia yao kwa umma na kupatikana kwa mfadhili ambaye amemrudisha masomoni licha ya familia yao kutelekezwa.

“Binafsi nawashukuru sana hao (TAMWA) waliopaza sauti hadi mjuu wangu kurudi shuleni…hii kwetu ilikuwa ni ndoto kwetu maana mtoto mwenyewe alikuwa amekata tamaa kabisa kurudi shuleni na alikuwa kaanza kufanya vibarua mitaani huku wenzake wakiendelea na shule,” alisema bibi wa mtoto huyo, Amina Mohamed akizungumza. Bibi huyo akizungumzia maisha ya sasa ya familia hiyo alisema bado wanahitaji msaada wa huduma hasa baada ya mwanaye kufariki dunia mwaka jana na kumuachia watoto wake.

Aliongeza kwa sasa yeye ni mgonjwa wa TB anayetumia dawa hivyo kwa hali yake ameshauriwa kupumzika jambo ambalo limempa mzigo mkubwa kimajukumu mwanafunzi (Mwenjuma), kufanya kazi za nymbani kama kupika kulima na shughuli nyingine.

Hata hivyo mama wa mtoto huyo (Hadija Magalu) ambaye alitelekezwa na mzazi mwenzake alifariki dunia mwaka jana kwa tatizo la uzazi na kuiacha tena familia hiyo ya watoto watatu katika hali ngumu zaidi chini ya malezi ya bibi mzaa mama.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa kushirikiana na TAMWA

MPAMBANO WA MASUMBWI KUFANYIKA JITEGEMEE ULIYOKO WILAYA YA MUHEZA MKOA WA TANGA

0
0


IDDY MKWELA
BONDIA Iddy Mkwela wa Dar es salaam anatarajia kuoneshana kazi ya kurushiana makonde na Lucas Ndula wa Muheza wakati wa kusherekea sikukuu za pasaka jumapili ya march 31 katika viwanja vya wazi vya Jitegemee vilivyopo wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga

akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa mpambano huo wa raundi 6 kg,60 bondia wa siku nyingi ambae kwa sasa ni kocha wa mchezo huo Muheza, Chalres Muhilu ' Spins' alisema mpambano huo wa wazi umeandaliwa kwa ajili ya kutoa burudani wilayani hapo na kuhamasisha mchezo wa masumbwi

ambapo kutakuwa na mapambano mengi ya mchezo huo yatakayoanza saa kumi jioni ikiwa kiingilio ni miguu yako tu amewataka wapenzi wa mchezo huo kujitokeza kuangalia mabondia kutoka Dar wakipambana na Muheza pamoja na kutoa rai kujitokeza kwa wafadhili kudhamini mchezo huo unaopendwa na vijana wengi wilayani humo ndio mana tumeamua kuweka katika viwanja vya wazi ili watu wote wajionee wenyewe mchezo wa ngumi unavyo endeshwa katika mazingira magumu

Nae Kocha wa kimataifa  wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' aliyepewa jukumu la kwenda na vijana kutoka Dar ili wakalete changamoto na kuleta amasa ya mchezo huo amesema atakwenda na Nassoro Mbwiga atakayemenyana na Bakari Sendekwa katika uzito wa kilo 52 na Iddy Mkwela atakaepambana na Lucas Ndula mpambano wa raundi 6
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images