Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 527 | 528 | (Page 529) | 530 | 531 | .... | 1897 | newer

  0 0

    Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Joseph Kilangi akitoa hutuba yake ya ufunguzi katika Semina ya majadiliano ya “Rasimu ya Sera ya Urithi wa Utamaduni” iliyofanyika Forodhani Mjini Zanzibar,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi, Sera na Utafiti wa Wizara hiyo na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Dkt. Amina Ameir Issa. 
   Proff Shariff Mtaalamu wa Historia akitoa mchango wake katika Semina ya majadiliano ya ‘Rasimu ya Sera ya Urithi wa Utamaduni’ iliyofanyika Forodhani Mjini Zanzibar. 
   Mwalimu wa Historia Chuo Kikuu cha Taifa Suza Bi Zainab Othman akitoa mawazo ya kuiboresha Rasimu hiyo katika Semina ya kuijadili ‘Rasimu ya Sera ya Urithi wa Utamaduni’ Semina hiyo iliyofanyika Forodhani Mjini Zanzibar.
   Mjumbe kutoka Jumuiya ya Uokozi Zanzibar Omar Kombo akiijadili ‘Rasimu ya Sera ya Urithi wa Utamaduni’ katika Semina iliyofanyika Forodhani Mjini Zanzibar. Semina hiyo ya Siku mbili imefanyika kwa lengo la kupata maoni tofauti kutoka kwa Wadau mbalimbali nchini. Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar. 
   Mkurugenzi wa Sanaa Zanzibar Mdungi Ussi akichangia Rasimu ya Sera ya Urithi wa Utamaduni ambapo pamoja na mambo mengine ameshauri Sera hiyo isiingiliane na Sera zingine.Picha na Faki Mjaka
    Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na mambo ya kale Dkt Amina Ameir Issa akiwashukuru Washiriki kwa michango yao katika Semina ya Majadiliano ya Rasimu ya Sera ya Urithi wa Utamaduni iliyofanyika Forodhani mjini Zanzibar,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Uendeshaji, Sera na Utafiti wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mashaka Hassan Mwita na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Magofu Zanzibar Abdallah Khamis Magofu-Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
   Mkurugenzi wa Uendeshaji, Sera na Utafiti wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mashaka Hassan Mwita katikati akifunga Semina ya Majadiliano ya Rasimu ya Sera ya Urithi wa Utamaduni iliyofanyika Forodhani mjini Zanzibar,kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya kale Dkt Amina Ameir Issa na kulia ni Makamu Mwenyekiti ZATO Hassan Ali Mzee.


  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 12/05/15

  Urithi wa Utamaduni umeelezwa kuwa ni moja kati ya Vitega uchumi muhimu ambapo kama utatumika vyema utapelekea mchango mkubwa kwa Wananchi na Serikali kwa ujumla.

  Mchango huo unaweza kuwepo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ya Utalii,Teknolojia, Utafiti na Elimu.

  Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale Dkt. Amina Ameir Issa wakati wa mjadala wa Rasimu ya Sera ya Urithi wa Utamaduni uliofanyika Forodhani Mjini Zanzibar.

  Amesema Nchi nyingi duniani huingiza mapato kutokana na utalii ambao kwa kiwango kikubwa hutegemea vivutio vinavyotokana na urithi wa utamaduni.

  Dkt Amina ameeleza kuwa Utalii huchangia na kuongeza pato la Wananchi kutokana na kuuza bidhaa na huduma mbalimbali kwa watalii zinazotokana na Urithi wa Utamaduni zikiwemo Sanaa, Mikoba na Milango.

  Amesema kukamilika kwa Sera hiyo na utekelezaji wake kutawezesha watu kutambua na kuthamini utu wao, historia na utamaduni wao jambo ambalo litapelekea watu hao kuamua kuyalinda maeneo ya Uhifadhi na utamaduni wao.

  “Watu hufurahia kushuhudia Urithi wa Utamaduni wenye mahusiano na historia ya jamiii mablimbali kama vile maendeleo ya sayansi, mabadiliko ya sura ya nchi na viumbe,aina ya uburudishaji,ukarimu, huba na maisha ya watu kwenye maeneo hayo” Alisema Dkt Amina.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Joseph Kilangi amesema kukamilika kwa Sera ya Urithi wa Utamaduni kutaisaidia Serikali kuanzisha Utalii wa Utamaduni wa Zanzibar ambao utakuwa ni kivutio kwa Wenyeji na Wageni mbalimbali nchini.

  Amesema hatua hiyo ni miongoni mwa jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali katika kuimarisha Sekta hiyo ambayo ndio tegemeo la Uchumi wa nchi.

  Amesema Zanzibar ina utamaduni wake ambao unatofautiana na Nchi nyingine hivyo ipo haja ya Utamaduni huo kuenziwa na kufanywa uwe kivutio kwa Wageni ili waweze kuja nchini kwa ajili ya kujionea utamaduni huo.

  “Zanzibar tuna utamaduni wetu wa Asili ikiwemo Mavazi, Tabia njema, Ukarimu, kupendana,amani na utulivu,mambo ambayo tukiyaratibu vyema katika Sera hii itakuwa kivutio cha Utalii’’ Alisema Mkurugenzi Kilangi.

  Kwa upande wao Washiriki wa Semina hiyo wameipongeza Serikali kwa uamuzi wake na kuomba kufanyika kwa majadiliano mapana kutoka kwa Wadau mbali mbali hasa wa Vijijini ambao pia Sera hiyo inawahusu.

  Hata hivyo Wachangiaji hao wameiomba Idara ya Makumbusho ambao ndio Wasimamizi wakuu wa Sera hiyo kuhakikisha Sera hiyo haipingani na Sera nyingine.


  0 0


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  KUHUSU
  UTARATIBU WA UTEUZI WA WAGOMBEA NDANI YA CHAMA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015

  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza utaratibu wa uteuzi wa wagombea wake watakaokiwakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka huu. 

  Aidha, kupitia mkutano na waandishi wa habari, Chadema pia imetangaza namna watia nia wa nafasi mbalimbali watakavyochukua na kurejesha fomu huku pia kikiweka wazi gharama za fomu kwa kila ngazi ya uteuzi yaani udiwani, uwakilishi, ubunge na urais 

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalim amesema kuwa utaratibu huo wa uteuzi katika ngazi ya ubunge na uwakilishi utahusisha hatua tatu katika ngazi ya jimbo/wilaya husika na hatua moja katika ngazi ya kitaifa huku ule wa udiwani ukiwa na sehemu mbili katika kata na moja wilayani/jimboni.

  “Kupitia mkutano wetu nanyi ndugu wanahabari, tunapenda kuutarifu umma wa Watanzania hususan wanachama wetu, wapenzi na wafuasi wote wenye sifa za kuwania uteuzi kupitia CHADEMA kuwa kwa kuzingatia matakwa ya katiba ya chama na kukuza demokrasia tukilenga kuhakikisha tunapata wagombea waadilifu, wenye uwezo wa kuwatumikia watu na wanaokubalika na wapiga kura, chama kimepanua wigo wa kupata maoni ya uteuzi,”alisema Mwalim.

  Akirejea maazimio ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama kilichoketi Mei 3 na 4 jijini Dar es salaam, NKMZ Mwalim amesema kuwa chama kimepitisha utaratibu huo utakaotumika kupata maoni na hatimaye kufanya uteuzi wa wagombea watakaosimama kugombea nafasi hizo tajwa kupitia CHADEMA katika ushirikano wa vyama vinavyounda UKAWA.

  Mwalim ameutaja utaratibu huo utakaotumika katika nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani, kuwa ni:

  Ubunge/Uwakilishi

  1. Mkutano Mkuu Maalum wa Jimbo

  Mkutano huu utafanyika kwenye kila jimbo la uchaguzi na utafanyika siku moja kwenye eneo moja ambalo ni makao makuu jimbo au eneo ambalo litaamuliwa na vikao vya chama. 

  Washiriki watatakiwa kuwapigia kura moja wagombea ambao wamejitokeza ndani ya chama na kura hiyo itakuwa ya siri .

  NKMZ amesema kuwa wasimamizi wa mikutano hiyo maalum ya kura ya maoni watatakiwa kuwa watu ambao hawana ‘maslahi’ kwenye uchaguzi huo yaani wasiwe wagombea au wasiwe na mgombea ambaye wanamuunga mkono kati ya wanaogombea nafasi hiyo.

  Kila mgombea atapewa fursa ya kujieleza mbele ya wapiga kura kwa dakika tano (5) na ataulizwa maswali yasiyozidi matatu kutoka kwa washiriki.

  Kura zitapigwa mwishoni baada ya wagombea wote kumaliza kujieleza mbele ya Mkutano Maalum wa Kura ya Maoni , na kila mgombea atakuwa na haki ya kuweka wakala wa kuhesabu kura zake.

  Matokeo ya kura hizi yatawasilishwa kwenye Kikao Cha Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya kabla ya kufanya kikao chake cha uteuzi.

  Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Kura ya Maoni Jimbo/Wilaya :

  (i) Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya Jimbo
  (ii) Wenyeviti wote wa kata za wilaya /jimbo
  (iii) Makatibu wote wa kata za wilaya/jimbo
  (iv) Makatibu waenezi wote wa kata za jimbo/wilaya
  (v) Wenyeviti na makatibu wa Mabaraza yote ya Chama Jimbo/Wilaya
  (vi) Wenyeviti wa Mabaraza yote katika Kata za wilaya/jimbo
  (vii) Makatibu wa mabaraza yote ya kata katika jimbo/wilaya
  (viii) Wenyeviti wa Serikali za Vijiji, Mitaa na Vitongoji watokanao na Chama kwenye Jimbo.

  2. Wagombea kujipigia kura wenyewe 

  Wagombea wote wapewe fursa ndani ya Mkutano Maalum ya kujipigia kura wenyewe na kila mmoja apige kura tatu, kura moja iwe yake binafsi na kura nyingine mbili atakiwe kuwapigia wagombea wengine waliopo.

  Matokeo ya kura hizi pia yatawasilishwa Kamati ya Utendaji na pia Ofisi ya Katibu Mkuu. 

  3. Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya

  Kamati ya Utendaji ya Wilaya /Jimbo itafanya uteuzi wa awali kwa mujibu wa Katiba ya Chama Ibara ya 7.4.10 (q).

  Kamati ya Utendaji itatakiwa kupiga kura za awali na kuwasilisha taarifa yake pamoja na Mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba ya Chama kwa ajili ya uteuzi mwisho.

  Utaratibu wa kuendesha vikao vya Kamati ya Utendaji Jimbo/Wilaya utazingatia Katiba na Kanuni za Chama.

  Udiwani 

  Katika nafasi ya udiwani Mwalim amesema kuwa kuwa utaratibu utakaotumika ni ule ule kama ilivyo katika nafasi ya ubunge isipokuwa hapa itakuwa katika ngazi ya kata kama ifuatavyo;

  1. Mkutano Mkuu Maalum wa Kata/Wadi 

  Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Kura ya Maoni kata/wadi:

  (i) Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya Kata
  (ii) Wenyeviti wote wa matawi katika kata
  (iii) Makatibu wote wa matawi katika kata
  (iv) Wenyeviti wote wa mabaraza ya wazee, wanawake na vijana katika kata
  (v) Diwani wa Chama wa Kata/Wadi, Diwani wa Viti Maalum, Mbunge/Mwakilishi anayeishi katika kata husika.
  (vi) Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Wenyeviti wa Kamati za Mitaa au Shehiya wanaotokana na Chama katika kata.
  (vii) Wenyeviti wa Serikali za Vitongoji, Mitaa na wajumbe wa serikali hizo katika kata wanaotokana na CHADEMA.

  2. Wagombea kujipigia kura wenyewe

  3. Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya

  Mwalim ameongeza kuwa tofauti na kwenye nafasi ya ubunge na uwakilishi ambayo uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Kamati Kuu ya Chama, kwenye ngazi ya udiwani uteuzi utafanywa na Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA.

  “Lakini pia hapa kwenye udiwani, mkutano mkuu maalum wa kata ambao utawapigia kura za maoni wanaowania uteuzi wa udiwani, mbali ya kujumuisha wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa, utahusisha pia wajumbe wote wa serikali katika vitongoji, vijiji na mitaa wanaotokana na CHADEMA katika kata husika. Unaweza kuona tunavyopanua wigo wa demokrasia.

  “Jambo jingine ambalo tungependa kusisitiza kwa wote watakaojitokeza kuchukua fomu ni kuhakikisha wanazingatia utaratibu wa katiba ya chama, kanuni za uendeshaji chama na miongozo yetu na nyaraka mbalimbali za kiutendaji. Watambue kabisa kuwa kati ya mambo ambayo hatutakubali yatokee kwenye chama hiki ni vitendo vya rushwa kusaka nafasi. 

  “Tumeshasema na tunarudia tena kusisitiza kuwa watoa rushwa na wapokea rushwa hawana nafasi ndani ya CHADEMA. Tumekuwa wakali katika hili. Yeyote atakayebainika kuvunja kanuni za chama katika zoezi hili ikiwemo kujihusisha na vitendo vya rushwa hatutakuwa na msalie mtume katika kuchukua hatua stahiki ndani ya chama pamoja na vyombo husika vya kiserikali kuchukua hatua za kisheria,”amesisitiza Mwalim. 

  Gharama za fomu, utaratibu wa kuzichukua na kuzirejesha

  Kuhusu gharama za kuchukua fomu za uteuzi huo, Mwalim alisema kuwa baada ya Kamati Kuu kuamua tarehe za kuchukua na kurejesha fomu za uteuzi wa ndani ya Chama na mfumo mzima wa kuwapata wagombea ilikasimisha mamlaka kwa sekretarieti ya chama kufanya maamuzi na kuidhinisha kutolewa kwa fomu pamoja na gharama zake.

  Amesema kuwa sekretarieti ya chama taifa imeelekeza kuwa fomu zitaweza kuchukuliwa eneo lolote lile yaani kwenye ngazi zifuatazo; Taifa, Mkoa, Wilaya na Jimbo kwa upande wa fomu za ubunge na kwa upande wa udiwani fomu zitaweza kuchukuliwa kwenye ngazi ya wilaya, jimbo na kata.

  Aidha ameongeza kuwa fomu hizo pia zitapatikana mitandaoni kupitia website ya chama; www.chadema.or.tz, kwa ajili ya wale wote ambao kwa sababu moja ama nyingine wanaweza kushindwa kufika katika ofisi za chama. 

  Amesisitiza kuwa kuwa fomu hizo ni lazima zirejeshwe kwenye Ofisi ya Jimbo au Kata ambayo mgombea anagombea na ndipo atapaswakulipia gharama za fomu husika.

  Kwa upande wa Ubunge wa Viti Maalum, NKMZ amesema kuwa fomu zao zitalipiwa moja kwa moja kwenye Akaunti ya BAWACHA Taifa ambayo ipo kwenye fomu husika, hivyo wagombea wa nafasi hiyo watalazimika kuambatanisha fomu zao na risiti ya kibenki (Pay Slip) ambayo inaonyesha kuwa wamelipia fomu hizo. 

  Gharama za fomu hizo ni kama ifuatavyo;

  · Urais ni Tsh. 1,000,000/=
  · Ubunge/Uwakilishi wa Jimbo ni Tsh. 250,000/=
  · Ubunge Viti Maalum ni Tsh. 250,000/=
  · Udiwani wa Kata ni Tsh. 50,000/=
  · Udiwani wa Viti Maalum Tsh. 50,000/= 

  Imetolewa leo Alhamis, Mei 14, 2015 na;
  Idara ya Habari na Mawasiliano
  CHADEMA

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na madaktari wa Shirika lisilo la kiserikali la Al Muntada lenye makao yake makuu jijini London Uingereza wanaoendesha zoezi la upasuaji na tiba ya moyo kwa zaidi ya watoto 70 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza akiwa katika picha ya pamoja na madaktari wa Shirika lisilo la kiserikali la Al Muntada lenye makao yake makuu jijini London Uingereza wanaoendesha zoezi la upasuaji na tiba ya moyo kwa zaidi ya watoto 70 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Picha na Freddy Maro.

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubelgiji hivi karibuni.

  Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimefedhehesha na kuidhalilisha sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla.   

  Aidha, BASATA limepokea malalamiko kwa njia ya simu na mawasiliano ya internet kutoka kwa watanzania waishio ughaibuni wakilaani tukio la Msanii huyo. Katika mawasiliano yao wameeleza kwamba wamefedheheshwa na kudhalilika na tabia hiyo chafu iliyooneshwa na msanii huyu.

  Ikumbukwe kwamba, Shilole ni msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa, hivyo anapokwenda nje ya nchi kabla hajapata visa anapewa barua ya utambulisho kama msanii wa Tanzania, hivyo anapokuwa nje ya nchi anatambuliwa kama msanii Mtanzania, anapofanya kinyume na misingi ya kazi ya Sanaa, anajifedhehesha yeye mwenyewe, kazi ya Sanaa na nchi yetu pia.

  Aidha, ikumbukwe kwamba BASATA limeshapata kumwita na kumuonya msanii huyu kutokana na tabia yake ya kutokujiheshimu pale awapo jukwaani na yeye aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo chafu. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio hayo na kwa sasa katika ardhi ya nchi nyingine ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu Sanaa kama kazi nyingine.
  BASATA linapenda kueleza kwamba;
  1.Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla
  2.Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si Sanaa na hakina uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua.

  BASATA linawakumbusha wasanii wote nchini kuwa Sanaa ni kazi kama kazi zingine lakini siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa wakikiuka suala zima la maadili kwa kutengeneza kazi chafu zisizofaa mbele ya jamii ya watanzania wanaoipenda na kuiheshimu kazi ya Sanaa yenye staha. Tuungane kwa pamoja kukemea kazi chafu zinazozalishwa na wasanii wasiojitambua kwani suala la maadili ni suala mtambuka na linaanzia katika ngazi ya familia. 

  Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapopata mialiko ya kikazi kwenda nje ya nchi. Linawakumbusha kwamba haiwezekani msanii kutumia picha chafu na mavazi dhalili na kuonyesha utupu katika kuvuta mashabiki.

  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

  Godfrey Mngereza
  KATIBU MTENDAJI

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete maeno yaliyoathiriwa vibaya na mafuriko huko Tegeta wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.kw2
  .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maagizo kwa uongozi wa wilaya ya Kinondoni kuyaondoa kwa haraka maji yaliyozunguka makazi ya watu eneo la Tegeta wilayani Kinondoni kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
  kw3
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda pamoja na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akiwaagiza kutafuta mbinu za kuyaondoa kwa haraka maji yaliyozingira makazi ya watu eneo la Tegeta.kw6
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda pamoja na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akiwaagiza kutafuta mbinu za kuyaondoa kwa haraka maji yaliyozingira makazi ya watu eneo la Tegeta.kw7
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia makazi holela yaliyojengwa katika bonde la mkwajuni eneo la mto Msimbazi na kisha kuongea na wakazi wa eneo hilo akiwashauri kuhama kwakuwa eneo hilo si salama kwa maisha na mali zao(picha na Freddy Maro) .

  0 0
  0 0

  The Application for the Karibu Music Festival will be closed on Tuesday 30th June 2015 at 00:00 Midnight.

  The Karibu Cultural Promotions Organizational (KCPO) and Legendary Music Entertainment Tanzania (LMEP) Are highly encouraging Artists, Musicians, Groups and Bands of different genres to apply for the Golden opportunity of participating to a unique international platform of Music, Art and Cultural experience.

  0 0

  PROGRAMU ya Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo licha ya mafadikio mengi iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya nne ya utekelezaji wake. 

  Mratibu wa Mradi huo,Bwa.Sebastian Ndandala ametaja changamoto hizo leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni hatua ya kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo. 

   Mratibu huyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya kifedha inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze kuongea kwa pamoja, ugumu wa kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu kama E-procurement na ICTs, Uhaba wa ferdha za ndani katika kutekeleza program na changamoto nyingine katika utekelezaji mradi.

   Alisema mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na washirika wa maendeleo pamoja na Serikali ya Tanzania tayari umeingia awamu ya nne ambapo lengo kuu la awamu hii ni kudumisha nidhamu katika usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa umma ili kuleta maendeleo endelevu. 

   Aidha alisema licha ya changamoto zilizopo katika utekelezaji mradi huo yapo mafanikio hasa katika awamu ya nne ambayo ni pamoja na programu kufanikiwa kuunganisha mfumo wa usimamizi wa fedha nchi nzima katika serikali kuu na serikali za mitaa, kufanikiwa kufanya utafiti wa namna Halmshauri za Wilaya/Miji inavyoweza kuongeza mapato na kufanyika kwa zoezi la PEFA mwaka 2013 na hivyo kuibua mapungufu yaliyopo katika usimamizi wa fedha za umma.
  Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) ,Bwa.Sebastian Ndandala akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) ,Bwa.Sebastian Ndandala akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.  0 0  0 0

   Patients and relatives who went to seek medical attention at African Medical Investment Ltd (AMI Hospital, also known as Trauma Center) in Dar es Salaam were yesterday in shock to see court brokers attaching hospital belonging after AMI failed to pay its rental bills for the past 26 months that accumulated to $1.6million.

  Speaking to journalists who went to witness the eviction court broker from MEM Auctioneers and General Brokers Ltd, Mr Elieza Mbwambwa, said they were carrying out a court order issued by the High Court of Tanzania, Commercial Division, following a long commercial legal battle involving AMI and a local businessman, Mr Navtej Singh Bains, (the land Lord).

  He said that the court ordered for attachment of AMI hospital properties to compensate for the dept, mentioning that as at yesterday, a number of AMI properties were confiscated including three ambulances, one Saloon car (Mark II), special hospital beds, computers, chairs and other hospital gadgets.

  “Although we were given an order to confiscate everything at once after the elapse of 14 days notice, which falls today, we have considered humanity in executing this assignment because this is an hospital. We have only taken items that are not used by inn-patients (those who are already admitted).

  “We have given the hospital a notice to evacuate admitted patients by 22nd this month of May. If they don’t comply by this time, we will transfer them to other hospitals and hand over the building to the landlord. This has been done in a humanitarian level. We have not disturbed already-admitted patients, but from today onwards, not any other new patient will be allowed in,” he said.

  Mr Mbwambwa said that machines like city-scan, x-ray machines and others           that are still being used by in-patients have been recorded and will be attached immediately after transferring the patients.When contacted for his comments on behalf of AMI Hospital management, Mr Lawrence Ochola said briefly that they are still continuing to attend to admitted patients and that he could not comment further.


  Families and friend of patients admitted at AMI hospital were seen processing documents to transfer their patients. Those who were bringing in new patients were returned by the gate.  There is also information that AMI Hospital Bank accounts at EXIM Bank which were attached by the Courts were found to have been unfrozen and most funds emptied.

  It is now clear that AMI hospital will be closed down despites its several appeal attempts to stop eviction, leaving its loyal patients in limbo.
  The hospital had failed to comply with Tanzania Court of Appeal order that wanted it to deposit in court $1.514 million plus a monthly rent to a tune of $64,000 per month following a tenancy agreement dispute.

  AMI Plc Chief Executive Officer (CEO), Mr Theunis Peter Botha, also a Director and CEO of the local AMI Hospital in Tanzania, subsequently filed the Bankruptcy application in the High Court of Tanzania stating that it was operating insolvently having incurred losses for the past two years.

  AMI Tanzania is wholly owned by its London Company AMI Plc.
  In a bankruptcy petition filed in March this year before the High Court's Main Registry, the company alleges that it has been incurring losses in terms of billions to the extent of having several outstanding liabilities and debts which are now exceeding its ability to pay to different creditors.

  "The petitioner (AMI) incurred a net loss of $1.146 million in the year ended February 28, 2013, while in the year ended February 28, 2014, the petitioner incurred a net loss of 775,000 US dollars," reads a section of the petition document. 

  It is stated that the company was also required to pay outstanding dues to institutes, notably the National Social Security Fund (NSSF) and the Tanzania Revenue Authority (TRA) and individuals.

  According to the petition, given the value of the assets of the company and the amount of money owed to it by creditors, there was no way it would be able to raise enough funds for paying them as well as meeting her obligations.  
  There are also records showing that Lancet Laboratory (T) Ltd filed for an urgent application against AMI Hospital eviction claiming over Sh150 million owed to them by AMI Hospital.

  Inside information has it that several creditors are now in a limbo as the Hospital owes over $4m to them including the biggest creditor being the Landlord Mr Bains, Doctors, Staff, TRA, Pharmaceutical suppliers and other suppliers.

  0 0
 • 05/15/15--01:17: Mchuma unauzwa
 • Bei Milioni 6.5 ... Maelewano yapo. 
  Kwa maelezo zaidi cheki kwa namba hii: 
  0713262902. 
  Karibu.
  kwa nyuma
  kwa ndani
  Kwa mbele

  0 0

  Kinga ni bora kuliko tiba. Lakini kwa mti huu ulio katika barabara ya Kijichi, Dar es Salaam, kama inavyoonekana katika picha mbalimbali, inaelekea mamlaka zinazohusika ama zimepitiwa au zinachukulia poa. Picha zote na Nathan Mpangala.
  0 0

  Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Maua Seminary wakiimba wimbo wa taifa wakati wa mahafali ya kuhitimu kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo.
  Wahitimu wa kidato cha sita shule ya sekondari Maua Seminari.
  Mkuu wa shule ya sekondari Maua seminari ,Erastus Tesha akizungumza katika mahafali ya 33 kwa wahitimu wa kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo.
  Mgeni rasmi katika mahafali hayo ,mbunge wa kuteuliwa na rais ,Mh James Mbatia akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na wageni waalikwa .
  Baadhi ya wageni waliofika shuleni hapo kwa ajili ya mahafali ya ndugu zao wanaotarajia kuhitimu kidato cha sita katika shule ya sekondary ya Maua.

  Mbunge Mbatia akieleza mapungufu aliyoyaona katika kitabu cha sera ya elimu kilichozinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete.
  Mbatia akimkabidhi mkuu wa shule ya sekondari Maua Seminary kitabu cha sera ya elimu.
  Mkuu wa shule ya sekondari ya Maua Seminari akimkabidhi Mbatia zawadi kutokana na kazi anayoifanya ya kutetea elimu ya Tanzania.
  Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ,Mbunge Mbatia akitoa zawadi ya keki kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondary Maua Seminary.
  Mgeni rasmi katika mahafali ya 33 ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Maua,James Mbatia akiwa katika picha ya pamoja na walimu pamoja na wahitimu.
  Mbunge Mbatia akiongozwa na mkuu wa shule ya sekondari ya Maua Seminary,Erastus Tesha kutembelea maeneo mbalimbali ya shule hiyo.
  Baadhi ya majengo yaliyopo katika shule ya sekondary Maua Seminary.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Knada ya Kaskazini.

  0 0

  DSC_0252
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akimweleza yaliyomo kwenye taarifa ya ripoti ya hali ya Elimu ilivyo dunia (EFA Global Monitoring Report 2015) “Education For All 2000-2015” ambayo inaonyesha mafanikio na changamoto kidunia iliyoandaliwa na Shirika la UNESCO alipomtembelea ofisini kwake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja mjini Dodoma ambapo pia alikutana na wadau wa sekta ya elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Elimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  DSC_0254
  DSC_0258
  DSC_02611
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akimwonyesha takwimu za Tanzania zilizomo kwenye ripoti hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini.

  DSC_0276
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma.
  DSC_0273
  Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO, Zulmira Rodrigues (katikati) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) katika ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma.
  DSC_0069
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukutana na wadau wa elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Eimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
  DSC_0078
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) mjini Dodoma.


  Na Modewjiblog team
  KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini amesema elimu ya sasa inaelekezwa zaidi katika kumwezesha mtu kujitegemea. Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog kuhusu maendeleo na changamoto kwenye sekta ya elimu nchini katika wiki ya maadhimisho ya elimu inayofikia tamati leo mjini Dodoma.

  Alisema katika mahojiano hayo kwamba mfumo sasa unawaondoa watu kwenye ajira ya serikali na kutokana na hilo uimarishaji wa elimu ndio kitu cha msingi kabisa.
  Alisema katika maadhimisho ya elimu watu wanajifunza usimamizi kama msingi mkubwa wa maendeleo ya elimu nchini. Alisema kuna mambo mengi ambayo yanastahili kuangaliwa kwa sasa kutokana na vigezo vya ufanisi wa elimu kuonesha changamoto zinazokabili sekta hiyo pamoja na kuimarika kwake.

  Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupungua kwa uandikishaji wa watoto na mdondoko. Alisema viongozi, wazazi pamoja na walezi wamesahau wajibu wao na kumwachia mwalimu pekee katika kumlea mwanafunzi kimasomo na hii ndio chanzo kikubwa cha mdondoko na ufaulu mbaya. Alisema ni vyema watu wakajiuliza hawa wanaondoka wanakwenda wapi na wanafanya nini.

  “kuna sheria ambapo viongozi wa kata wanaruhusiwa kuwachukulia hatua na kuwafikisha mahakamani wazazi wanaokwamisha elimu, lakini watu hawachukia sheria hiyo” alisema.
  Aidha alisema ubora wa elimu una vigezo vingi ikiwa ni pamoja na kujituma kwa walimu katika ufundishaji na kuwa na dhamira ya kuwapa watoto vitu vyenye maana.

  Alisema kuna mambo mengi yanatakiwa kufanywa kuinua elimu na usimamizi unapokuwa mkali na wahusika kuadhibiwa ndio ufanisi unafanyika na mdondoko kuangaliwa.
  Alisema ipo haja kubwa ya kuwekeza kwenye elimu kwa viongozi na wadau kutimiza wajibu wao. Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Makuru Petro akitoa tathmini ya sekta ya elimu kwa wadau wa sekta ya elimu alisema pamoja na ongezeko la ufaulu ndani ya miaka miwili ipo haja ya kutathimini uimara wa mfumo katika kutoa huduma ya elimu.

  Alisema pamoja na ufanisi kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wanaokacha shule kunaonesha mfumo kuwa na kasoro na lazima uangaliwe. Aidha alisema sekta ya elimu wamepokea asilimia 97 ya bajeti yake na kwamba asilimia 70 imeenda kwenye halmashauri ambako ni watekelezaji wa miradi ya elimu. Tathmini hiyo inayowakilisha wizara zote zinazoshughulikia elimu kama TAMISEMI, Elimu na Maendeleo ya jamii na wadau wengine wa elimu ni sehemu ya shughuli inafanywa kila mwaka kwa lengo la kutambua kilichofanyika, changamoto na namna ya kukabiliana na tatizo hilo.

  Hata hivyo walisema kwamba ndani ya miaka miwili kumekuwepo na maendeleo makubwa katika sekta ya elimu hasa ufaulu na ubora wa elimu.

  0 0

  Siku 8 zimebaki kufikia kilele cha tuzo za filamu mwaka 2015.

  Ikiwa zimebaki siku chache kufikia kilele cha tuzo za filamu kwa mwaka huu ambapo Tuzo za Filamu Tanzania (TAFA) zinafanyika kwa mara ya kwanza nchini Mei 23, 2015 Mwalimu Nyerere International Conference Center jijini Dar es Salaam. 

  Haya ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini kwani ni kuonesha mafanikio. Ni vipengele mbalimbali vilivyopo katika kinyang’anyiro cha tuzo za filamu mwaka huu 2015. Tuzo hizo ambazo ni kubwa na zenye hadhi ya juu zimeandaliwa na Shirikisho la Filamu Tanzania na washirika mbalimbali .


   “Kazi kubwa ya Shirikisho la Filamu Tanzania ni kusaidia kukuza tasnia ya filamu na kuunga mkono jitihada za wasanii kwa namna mbalimbali. Mbali na hilo pia ni daraja linalowaunganisha wasanii wa tasnia ya filamu na Bodi ya Filamu nchini hivyo kurahisisha utendaji wa kazi zao. 

  Ninayo kamati ya maandalizi iliyo imara na thabiti ambayo imefanya kazi katika mazingira magumu usiku na mchana kuhakikisha tunapata halfa nzuri na ya namna yake ambayo haijawahi kutokea”, Alisema Simon Mwakifwamba, Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania.


  Aliongeza kwa kusema kuwa tasnia ya filamu nchini bado ina safari ndefu ukilinganisha na Hollywood ambao wameshapiga hatua kubwa. Tuzo hizi sasa ni jambo wanapaswa kujivunia kwa wasanii na watengeneza filamu kujivunia. 

  Imeripotiwa kuwa tasnia ya filamu imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa pato la taifa hili linathibitishwa na taarifa ya mapato nchini ya hivi karibuni, na hili linadhihirisha kuwa tasnia ya filamu inafanya kazi kubwa ya kupunguza tatizo la ajira nchini ambalo limekua ni tatizo kwa vijana wengi hapa nchini.


  Mara baada ya uzinduzi wa tuzo za Filamu mwishoni mwa mwaka 2014 uwasilishwaji wa kazi za filamu ulianza kwa wakati na baadae zilichaguliwa kwa ustadi mkubwa chache zilizoingia katika kinyang’anyiro cha tuzo hizi na hatua hiyo ilifanikiwa kikamilifu na baadae kutangaza washiriki wanaowania tuzo hizi za filamu. 

  Kuna filamu 24 ambazo zimeingia katika kinyang’anyiro cha tuzo hizi na kati ya hizo filamu 12 zitaibuka vinara wa tuzo za Filamu Tanzania 2015. Majaji nao wamefanya kazi kubwa na wana mchango mkubwa, kwani ushindi wa tuzo utategemea 70% kutoka kwa majaji na 30% zitakua ni kura za mashabiki. Majaji wote wanatoka katika Mtandao wa Filamu Afrika Mashariki ambapo Shirikisho la Filamu Tanzania ni mshirika.


  Wanatasnia wa filamu wanayo furaha kwa Shirikisho la Filamu kupiga hatua kubwa na hatua walizochukua hata kufanikisha kuwapo kwa tuzo hizi pia wamewashukuru wanakamati wa maandalizi ya tuzo hizi ambao wengi wao wamejitolea kuhakikisha tunapata kitu cha kujivunia.


  Nae Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tuzo hizo Bi Caroline Gul alisema, “tunategemea kuwa na hafla nzuri na ya kipekee.  Tumepokea maombi mengi kutoka kwa wanatasnia ya filamu ambao wanataka kuhudhuria kutoka sehemu mbalimbali za Afrika kuwaunga mkono wenzao. Mbali na hilo tumeanda burudani kabambe kwaajili ya siku hiyo. Tunachowaomba watanzania ni kutuunga mkono kwa kununua tiketi na kuhudhuria kwa wingi kwani ni kuonesha uzalendo kwa kupenda na kuunga mkono jitihada za kazi za wasanii wetu”  Pia alizungumzia swala la udhamini kwa kusema kuwa bado muda upo hivyo wadhamini wajitokeze kudhamini tuzo hizi kwani bado vitu vingi vinahitajika kufanyika. Alizishukuru taasisi zilizounga mkono tuzo za filamu ambao ni TCRA, International Eye Hospital na Foreplan Clinic bila kusahau EATV & EA Radio, Push Mobile na R&R Associates.


  0 0  JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

  KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO


  Simu ya Upepo   : “N G O M E”          Makao Makuu ya Jeshi,

  Simu ya Mdomo : DSM  22150463      Sanduku la Posta 9203,

  Telex                     : 41051                       DAR ESSALAAM,    15, May 2015

  Tele Fax                : 2153426

  Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk

  Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz

                    

  Taarifa kwa Vyombo vya Habari


  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linasikitishwa na  taarifa za uvumi zilizotolewa  kuenea kwenye mitandao ya kijamii face book, whatsapp na twitter zikieleza kuwa JWTZ inafanya usaili leo tarehe           15 May 2015 katika Chuo cha Dar es SalaamInstitute of Technology (DIT) kwa wale waliosoma fani ya Computer science, IT, Electronics na Mechanical Enginering.

  JWTZ linapenda kuwajulisha wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo si za kweli ni uvumi, JWTZ lina utaratibu wake wa kuandikisha Jeshini ambapo hutoa taarifa katika vyombo vya habari kwa utaratibu ulio sahihi.


     Aidha, Jeshi linaendelea kusisitiza wananchi kuwa halina akaunti za mitandao hiyo na ni kinyume cha sheria kusambaza ujumbe kwa kutumia jina au nembo ya JWTZ watakao bainika watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.


     
  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

  Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963.
  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es slaam,Saidi Meck Sadiki akitoa taarifa ya ziara ya siku tatu ya Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi nchini Tanzania atakayoifanya kuanzia Mei 17 hadi 19, 2015.


  Na.Aron Msigwa -MAELEZO.
  15/5/2015.DAR ES SALAAM.

  Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi anatarajia kuwasili nchini Tanzania Mei 17 mwaka huu kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine anatarajia kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.

  Akitoa taarifa ya ziara hiyo leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki amesema kuwa Rais Filipe Nyusi atawasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam, Mei 17,2015 majira ya saa 6.

  Amesema mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Rais huyo atalakiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, kupata mapokezi ya burudani ya ngoma za asili na kukagua gwaride la heshima litakaloandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzanian(JWTZ) na baadaye kupigiwa mizinga 21.

  Mhe.Sadiki amesema kuwa mara baada ya shughuli ya mapokezi ya Rais huyo uwanja wa ndege ataelekea Ikulu ambako atapokewa rasmi na mwenyeji wake,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete na baadaye viongozi hao wawili watakua na mazungumzo ya faragha.

  Amesema Mei 18, 2015 Rais Filipe Nyusi atafanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Msumbiji waishio nchini Tanzania na kisha kuendelea na ziara yake Visiwani Zanzibar ambako atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.

  Ameeleza kuwa baada ya kukamilisha ziara yake kisiwani Zanzibar Mei, 19 mwaka huu, Rais Filipe Nyusi ataelekea mjini Dodoma ambako atakutana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,Rais Jakaya Mrisho Kikwete yalipo Makao Makuu ya Chama cha hicho na baadaye ataelekea Ukumbi wa Bunge kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Amesema ,Mhe.Filipe Nyusi atahitimisha ziara yake na kurejea nchini kwake Mei 19,2015 na kuwaomba wananchi hususan wakazi wa jiji la Dar es salaam kuwa wavumilivu kutokana na usumbufu utakaotokana na baadhi ya barabara zikiwemo Nyerere, mzunguko wa Kamata, Barabara ya Sokoine ,Luthuli na Barabara ya Kilwa kufungwa mara kwa mara kupisha msafara wa kiongozi huyo.

  0 0  “Nimesikitishwa sana na kauli ya Mhe. Joshua Nassari ambayo ameongea kwa kudhalilisha  utendaji wangu  serikalini.  

  Naomba  Mh. Nassari  afahamu kuwa  kunikashifu pasipo  kueleza masuala  ya kisera  au ya kiutendaji ni  kupungukiwa na busara  ya kawaida kwa kiongozi aliyepaswa kuwawakilisha wapiga kura wake kwa hoja.

  Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Mhe. Nassari aliniita Jimboni kwake  Arumeru Mashariki akiniomba nitatue  tatizo  lililohusu wananchi  wa  jimboni kwake waliokuwa wanahitaji matibabu katika  hospitali  ambayo ilikuwa sharti  upitie ndani  ya hifadhi  ili ufike kutibiwa.

   Nilikwenda kuwaona wagonjwa na kuitembelea hospitali hiyo na kulitatua tatizo hilo  siku hiyo hiyo.  Kwangu  kama Waziri, halikuwa suala  la  kufanyia  siasa  afya za Watanzania, pamoja na yeye kuwa Mbunge wa upinzani. 

  Nilimheshimu na kukubali wito wake kwa niaba ya wananchi.  Nimewatembelea na kuwatia  moyo maaskari wetu  nchi nzima  na kuwapelekea  vitendea kazi. Nimefurahi pamoja nao  na kulia pamoja nao. Nimeenda kuwafariji familia za wapiganaji  wetu waliopoteza maisha kwa kuuawa wakilinda raslimali za Taifa, watu ambao  Mhe. Nassari anawabeza. 


  Tumepambana na ujangili na tunaendelea kuushinda. Tumeleta magari, silaha,  ndege, helicopters, na raslimali nyingi ili kulinda raslimali za Taifa.  Busara haisomewi ila ni kumshukuru Mungu  akusaidie kujua  matumizi ya ulimi. Nimesikitishwa sana na kauli  za uongo na kuzusha za Mhe. Nassari. Imeandikwa, usimsingizie jirani yako  uongo.”


  Mh. Lazaro Nyalandu.


  0 0

  kombe 3
  Mfadhili wa michuano ya kombe la Ng'ombe  ambaye pia mkurugenzi wa kampuni ya  East Link Tanzania Ltd,Kim Fute wapili kutoka kushoto akibadilishana mawazo na baadhi ya vijana waliofika kushuhudia michuano hiyo ,michuano hiyo itahitimishwa mapema siku ya jumapili wiki hiii katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni ambapo Timu ya Zamzam na Nyota watachuana.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).
  kombe na view meru mlimaTaswira ya muonekano wa mlima Meru unavyoonekana pichani,hii ilikuwa juzi katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha.
  kombe 2
  Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Zamzam FC wakimwangalia mlinda mlango wao ,Seleman Casillas mara baada ya kuanguka na kulalamika kuua mguuni juzi katika mechi baina yao na Parrot katika kombe la Ng"ombe iliyochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha,klabu ya Zamzam ilifanikiwa kutinga fainali katika mchezo huo ambapo itakutana na Nyota siku ya jumapili

  Soka  ni mchezo wa ajabu embu sikia hii mlango wa klabu ya Parot FC,Sacrifice Adam juzi  alijikuta akiangua kilio uwanjani mara baada ya kushuhudiwa timu yake ikitolewa katika michuano ya kombe la ng’ombe linaloendelea  kuwaka moto katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha.

  Adam,aliangua kilio wakati alipokuwa akishuhudia timu  yake ikiondolewa na klabu ya Zamzam FC juzi katika viwanja hivyo katika hatua ya matuta baada ya timu yake kuchapwa kwa jumla ya penati 5 kwa 4.

  Hatahivyo,hapo awali Adam alifanikiwa kuokoa mipira mingi ya hatari iliyokuwa ikipigwa na washambuliaji wa klabu ya Zamzam hususani wakati timu hizom zinakkwenda kumalizia kipindi cha pili.

  Kwa hatua hiyo klabu ya Zamzam sasa imefanikiwa kukata tiketi ya kuingia katika hatua ya fainali ambapo itakutana na Nyota siku ya kesho (jumapili) katika viwanja hivyo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mdau wa michezo jijini Arusha na  mkurugenzi wa kampuni ya  East Link Tanzania Ltd,Kim Fute.

  Hatahivyo,jambo la kuvutia katika mechi hiyo ni pale paliposhuhudiwa watu wa kada zote wanafunzi,wanawake,wazee pamoja na watoto wadogo walipokusanyika kwa pamoja kushuhudia mchezo huo jambo lililoashiria kwamba mchezo wa soka bado unachukua nafasi ya kupendwa kwa kiasi kikubwa kupendwa tofauti na michezo mingine.

  0 0

   Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo (Kulia) akifungua kikao kati ya wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Kamati ya maandalizi ya Tuzo za TAFA leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.

   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akizungumza na wadau wa filamu waliofika katika Ofisi za Wizara hiyo kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchiniitakayofanyika tarehe 23 Mei mwaka huu. Kulia niKatibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo

   Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA Bibi. Caroline Gachara Gul (kulia) akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchini kwa Uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na watendaji kutoka Bodi ya Filamu nchini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo Bibi. Siima Rubibira.

   Wajumbe kutoka Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA pamoja na maafisa wanaosimamia Filamu nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini mjumbe aliyekua akichangia (hayupo pichani) wakati wa kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo hizo kwa uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

   Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Saimon Mwakifwamba (kushoto) akichangia wakati wa kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchinikwa uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na watendaji kutoka Bodi ya Filamu nchini leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Bw. John Kalage.

  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Mchezo Prof. Elisante Ole Gabriel (waliokaa katikati), Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof Elimas Mwansoko (wapili kushoto), na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo (wapili kulia) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA na watendaji wanaosimamia shughuli za filamu nchini. Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo.


  Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Filamu Tanzania yashauriwa kutangaza Tasnia ya Filamu kimataifa


  Na Lorietha Laurence-Maelezo

  Kaimu  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel  ameishauri kamati ya maandalizi ya  Tuzo ya Tanzania Film Awards kuhakikisha kuwa wanaitanganza tasnia ya filamu kimataifa. Akiongea na kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha kupokea taarifa ya Maandalizi ya   Tuzo hizo kilichofanyika katika ukumbi wa wizara ambapo aliwapongeza viongozi wa kamati hiyo kwa juhudi walizozifanya.

  “kazi mnayoifanya ni nzuri kwa kuwa inasaidia kukuza na kuitangaza tasinia ya filamu  na hivyo  kuwavutia wadau mbalimbali kuwekeza zaidi” alisema Prof.Elisante

  Aidha  amewataka viongozi wa kamati hiyo kuhakikisha kuwa tuzo zitakazotolewa siku hiyo ziwe za ubora na kiwango cha juu ili kuwahamasisha waandaji wa filamu kuandaa filamu zenye viwango vizuri zaidi.


  Naye Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Tuzo hizo Bibi. Caroline Gul ameeleza kuwa mpaka sasa wamefanikiwa katika maandalizi mbalimbali ikiwemo ukumbi,tuzo zitakazotolewa na amajaji.

   “Mpaka sasa tumefanikisha  katika suala la ukumbi na kupokea filamu 300 ambazo zipo katika vipengele 12  zenye jumla ya washiriki 50 watakaoshindanishwa siku hiyo” alisema Bibi. Caroline.Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fisoo ameishukuru kamati hiyo kuweza kushirikiana na Serikali kwa kila hatua wanayoifanya katika maandalizi ya tuzo hizo.

  “Serikali inatambua mchango wenu katika kukuza na kuendeleza tasnia ya filamu nchini ni jambo zuri kwa kuwa inasaidia  kukuza soko la tasnia hii kimataifa” alisema Bi.Fisoo.


  Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia nia Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Saimon Mwakifwamba ameeleza kuwa wamefanikiwa  kualika  majaji kutoka  East Africa Film Network  ambao watasaidiana na majiaji wa hapa nchini  katika  kupata washindi.


  Tuzo za Tanzania Film  Awards   zinatarajiwa kufanyika tarehe 23 May katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa  Mwalimu Nyerere ambapo tikite zitauzwa kuanzia elfu 50 mpaka laki moja kwa VIP.

  Mwisho.older | 1 | .... | 527 | 528 | (Page 529) | 530 | 531 | .... | 1897 | newer