Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

TASAF, Wadau wa maendeleo wafanya tathmini

$
0
0
Mfuko wa Maendeleo ya jamii-TASAF kwa ushirikiano na wadau wa Maendeleo wameanza mkutano wiki mbili wa tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini -PSSN  unaosimamiwa na mfuko huo.

Zifuatazo ni picha zikionyesha wadau hao wa maendeleo na watendaji wa TASAF wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga katika ukumbi wa mikutani wa Makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia na taasisi zingine wakichangia mawazo kufuatia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga. 
 Baadhi ya watendaji wa TASAF na wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia na taasisi zingine wakisikiliza michango ya mawazo kutoka kwa washiriki kufuatia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga. 
 Baadhi ya wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia na taasisi zingine wakifuatilia kwa makini uchangiaji mawazo kufuatia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga 
Baadhi ya wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia na taasisi zingine wakipitia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga .

Kumbukumbu ya Amina Ngaluma J’mosi Dar

$
0
0
 KISOMO cha kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa mwimbaji mahiri nchini, marehemu Amina Ngaluma ‘Japanese’ kinatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii Kitunda, Machimbo Dar es Salaam.
 
Akizungumza na gazeti hili, baba mzazi wa marehemu,  Kassim Ngaluma, alisema kisomo hicho kitafanyika nyumbani kwa wazazi wake marehemu na kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali wa marehemu wakati wa uhai wake wahudhurie.
 
“Tunaomba wote tulioshiriki kwa namna mbalimbali wakati wa msiba wa marehemu mwanangu, tushirikiane pia katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo chake,” alisema Mzee Ngaluma na kuongeza kuwa kisomo hicho kitafanyika saa saba mchana baada ya swala ya adhuhuri.
 
Aliwaomba waliokuwa wanamuziki wenzake na marehemu, mashabiki wake, pamoja na wadau wengine wa muziki na marafiki wote, washirikiane katika tukio hilo.
 
Ngaluma aliyepata kung’ara na bendi mbalimbali nchini, alifariki dunia Mei 15 mwaka jana kwa shinikizo la damu akiwa Thailand alikokuwa akifanya shughuli za muziki katika bendi ya Jambo Survivor na kuzikwa Mei 24 mwaka huo, Dar es Salaam.
 
Wakati wa uhai wake alitamba na bendi mbalimbali zikiwemo African Revolution ‘Tamtam’, Double M Sound ‘Mshikemshike’ na TOT Plus zote za Dar es Salaam.Pia alipigia makundi ya Arusha Sangoma, Sayari Band na Less Mwenge yote ya Arusha na Mangelepa na Sky Sound za Kenya.
 
Baadhi ya nyimbo alizotunga wakati wa uhai wake ni Manyanyaso Kazini na Mapendo alizotunga akiwa Tamtam, wakati Double M Sound alitunga nyimbo za Wajane na Ukewenza.Pia alitoa albamu yake binafsi iitwayo Jitulize.
 
Baadhi ya nyimbo alizopata kuimba na kumpatia umaarufu mkubwa ni Mgumba, Maisha Kitendawili,  Ndugu Lawama, Zawadi ya Watanzania, Ugumu wa Maisha na Call Box zote zikitungwa na Muumin Mwinjuma ‘Kocha wa Dunia’.

MJADALA WA BAJETI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAFANYIKA DAR ES SALAAM

$
0
0
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Isaya Kisiri (wa pili kushoto), Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Bi Martha Tupa (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Sazi Salula na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Angelina Madete wakifuatilia kwa umakini mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika Ukumbi wa Hazina jijini Dar es Salaam, leo.( Picha na OMR)
02
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Isaya  Kisiri (kulia), akisikiliza kwa umakini  mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika Ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dar es Salaam, leo.  Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Sazi Salula na wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu  wa Ofisi hiyo, Bi Angelina Madete.

MADEREVA NCHINI KUENDELEA NA UTARATIBU WA AWALI KUHUISHA LESENI ZAO

$
0
0
Mwenyekiti wa Madereva Tanzania, Clement Masanja (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo jijini Dar es salaam ili kuwajulisha madereva wote nchini kuwa mwaka huu wamekubaliana na Mamlaka husika kuwa hakutakuwa na mafunzo kama ilivyoelezwa hapo awali. Kulia ni Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.
…………………………………………………………………………..
Na Pius Yalula-MAELEZO-Dar es salaam
Serikali imesema hakutakuwa na mafunzo kwa madereva wa malori na mabasi na wala hawatakiwi kwenda kusoma kozi fupi ili kuhuisha leseni zao kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali na kusababisha mgomo.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga wakati akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari leo mjini Dar es salaam.
Alisema kuwa madereva wenye daraja E, C, C1, C2 na C3 walitakiwa kupata mafunzo ya muda mfupi kila baada ya miaka 3 kulingana na kanuni ziliandaliwa mwaka 2014 kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra),Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA),Chuo cha Taifa ya Usafishaji(NIT), Vyama vya Madereva , Ofisi ya Mwanasheri Mkuu wa Serikali na Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo Tanzania (TATOA) , lakini kwa mwaka huu hawatatekeleza kanuni hiyo.
Kamanda Mpinga alisisitiza kuwa kanuni hiyo hatatumika mwaka huu badala yake madereva wataendelea na utaratibu wao wa zamani wa kubadilisha na kuhuisha leseni zao kwa zile ambazo zitakuwa zimekwisha bila kuulizwa vyeti.
Aliongeza kuwa hadi hivi sasa mitala ya mafunzo hayo ya muda mfupi bado haijakamilika na wala Serikali haijawahi kupanga ada za mafunzo hayo , kwa hiyo utaratibu wa zamani utaendelea kutumika kama ulivyokuwa hapo awali.
Kamanda Mpinga alitoa wito kwa madereva wote kuwa wavumilivu kwa matatizo yao wakati Kamati ya kudumu ya kutatua matatizo ya sekta ya usafishaji ikendelea kuyatafutia ufumbuzi.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi na wasafiri kutoa taarifa kwa viongozi wa Jeshi hilo endapo wanaona Askari wao au dereva anatenda vitendo visivyo vya kimaadili ili aweze kuchukuliwa hatua.
Alisema kuwa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kipo wakati tayari kupokea malalamiko ya kuyachukulia hatua ili kulinda maisha ya wasafiri na mali zao , hivyo ni vizuri wakaripoti wale wote wanaohatarisha maisha ya wenzao.

WAZIRI WA FEDHA ZANZIBAR ASOMA BAJETI YA FEDHA YA MWAKA KWA MWAKA 2015/16 LEO

$
0
0
Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee akionesha Mkoba wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 leo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee akisoma Hutuba ya Mapato na Matumizi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 leo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee aliyokuwa akiisoma kuhusu Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 leo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Waalikwa walioshiriki wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee aliyokuwa akiisoma kuhusu Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 leo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

BAMAGA -AFRIKASANA SINZA TAABAN KWA MAFURIKO.!

$
0
0
 Pichani ni sehemu ya barabara kutoka Bamaga kuelekea Afrikasana Sinza jijini Dar ikiwa hoi bin taaaban baada ya kufunikwa na maji kufuatia mvua ambazo zimekuwa zikiendelea kunyesha jijini,aidha mafuriko hayo yamekuwa yakisababishwa pia na mitalo mingi ya eneo hilo kuzibwa na takataka zinazotupwa holela,matokeo yake maji yamekuwa yakikosa muelekeo.Idara husika wanapaswa kulifanyia kazi ipasavyo eneo hilo kwani limekuwa ni kero kubwa kwa wanaotumia barabara hiyo kila wakati kwenda kwenye shughuli zao za kila siku.
 Hali halisi ndio hivi mvua ikinyesha jijini Dar,kwa eneo la Bamaga.
Maji yakiwa yametuama tuliiii eneo la bamaga kuelekea Afrikasana.
 Sehemu ya soko la Mboga mboga na Matunda la Afrikasana-Sinza likiwa limezungukwa na maji,hali iliyopelekea biashara kuwa ngumu eneo hilo. 

MTOTO WA BABA WA TAIFA JOHN GUIDO NYERERE AZIKWA LEO BUTIAMA

$
0
0
 Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila akisali mbele ya jeneza la marehemu John Guido Nyerere kabla halijaingia kanisani kwa ajili ya ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama.
 Viongozi na wananchi wakishiriki ibada ya kumuombea marehemu John Gaudo Nyerere katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama
 Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila akitoa heshima za mwisho kwa marehemu John Guido Nyerere baada ya kukamilika kwa ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowassa wakati wa mazishi ya John Guido Nyerere yaliyofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa ,Butiama.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu John Guido Nyerere likiteremshwa kaburini na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
 Mama Maria Nyerere akiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
 Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akiweka udongo kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
 Mtoto wa mwisho wa marehemu John Guido Nyerere anayefahamika kwa jina la Wanzagi akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na shangazi yake Anna Nyerere.
 Ni huzuni kwa kila mtu.
 Mama Maria Nyerere akiweka shada la mau kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
 Mtoto wa Marehemu anayeishi Lusaka Zambia, Sofia Nyerere Mwape akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yake marehemu John Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa heshima mbele ya kaburi la marehemu John Gaudo Nyerere mara baada ya kuweka taji la maua.
 Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Shyrose Bhanji akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu John Nyerere kwenye mazishi yaliofanyika nyumbani kwa marehemu Baba wa Taifa Butiama.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakishiriki kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
 Baadhi ya Watoto wa marehemu pamoja na ndugu wengine.
 Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akisoma salaam za rambi rambi kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wakati wa mazishi ya John Nyerere.
Emily Magige Nyerere akifafanua jambo wakati wa mazishi ya John Guido Nyerere. (Picha zote na Adam H. Mzee) .KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

NEWZ ALERT:UCHAGUZI MKUU WA BURUNDI WAAHAIRISHWA KWA MUDA USIOJULIKANA.

$
0
0
Rais kikwete alipohutubia waandishi wa habari Dar es Salaam akiandamana na Rais Nkurunzinza.PICHA KWA HISANI YA BBC SWAHILI

Uchaguzi mkuu wa Burundi umeahirishwa kwa muda usiojulikana,kwa sasa vyama vyote vya siasa vya Burundi vitaitwa kujadili mezani kwa amani na kisha utaitishwa mkutano wa wakuu wa EAC kupitia mapendekezo ya mkutano huo wa vyama vya siasa ili kufikia maafikiano,pia EAC wamelaani vikali jaribio la mapinduzi Burundi.@Jakaya Mrisho Kikwete.

Balozi mpya wa Malawi nchini Marekani atembelea Ubalozi wa Tanzania Washington DC

$
0
0
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi bi, Jane Nankwenya, kulia ni balozi wa Tanzania nchini Marekani Liberata Mulamula na Afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme.
 Mhe balozi mpya wa Malawi Nector Mhura akipokelewa na Afisa ubalozi Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi.
 Mhe, balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Malawi Nector Mhura.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani akiweka saini kwenye kitabu maalum cha wageni.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akimsikiliza kwa makini mwenyeji wake balozi Liberata Mulamula alipokua akijitambulisha.
  Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi bi, Jane Nankwenya.

                   PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.

WIZARA YA FEDHA YAWAPA SEMINA WAANDISHI WA HABARI JUU YA MRADI WA MABORESHO YA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma akifafanua jambo wakati wa warsha ya siku tano kuhusu mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli Njuweni Kibaha. Bi.Ingiahedi alisema kuwa Serikali ya Tanzania ilianzisha mradi huo kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya matumizi ya fedha katika ngazi zote.  Mradi huu umekuwa wa awamu 4 kutokana na mafanikio yanayojitokeza na changamoto.

Alisema kuwa Mpaka sasa mradi huo umepata mafanikio makubwa hasa ya  kuweka mfumo mzuri wa malipo, muda wa kupitishwa kwa bajeti ya Taifa umeimarika na fedha zinatoka kwa  wakati,Alibainisha kuwa bajeti ya mwananchi inatangazwa katika Tovuti ya Wizara ya fedha na kuwa mfumo wa malipo umefika mpaka katika Serikali za Mitaa.
Washiriki wa warsha kuhusu maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli ya Njuweni Kibaha.
 Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa katika warsha ya siku tano kuhusu kuhusu mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli ya Njuweni Kibaha. 

===========  =======  ========
Serikali ya Tanzania ilianzisha mradi huo kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya matumizi ya fedha katika ngazi zote.  Mradi huu umekuwa wa awamu 4 kutokana na mafanikio yanayojitokeza na changamoto.

Awamu ya kwanza (I) ilikuwa kutoka mwaka
1998 – 2004 huu ulikuwa na malengo ya kudhibiti matumizi,
kuweka nidhamu ya fedha pamoja na kukuzana kuimarisha uchumi mpana.

Awamu ya pili (II)
ilikuwa kutoka mwaka 2004 – 2008 malengo ya mradi huo yalikuwa ni kuimarisha na kuendeleza mifumo na njia zinazotumika katika malipo ya fedha za umma kwa kutumia njia rahisi na nyepesi. Aidha awamu hiyo ilizingatia pia uimarishaji wa njia ya ukusanyaji mapato na jinsi ya kuweka mbinu ya kuzitumia rasilimali fedha na kuweka mikakati ya kipi kianze kwanza.

Awamu ya tatu (III)
ilikua kuanzia 2008 – 2011, mradi huu ulikua na malengo ya kuhakikisha kuna kuwa na upatikanaji rasilimali fedha kutoka katikaTaasisi mbalimbali za kifedha.

Awamu ya nne (IV)
ya mradi ni kuanzia June 2012, mradi ulizinduliwa na kuanza rasmi tarehe 1 Julai, 2012. Madhumuni ya mradi huu katika awamu ya nne umelenga katika kuonge za nguvu ambayo itawezesha kufikia malengo ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, 
 hiyo inaenda sanjari na mpango wa maendeleo wa miaka mitano yaani 2011/2012 – 2015/2016 na MKUKUTA (MkakatiwaKukuzauchumi Tanzania)/ MKUZA (Mkakati wa Kukuza uchumi Zanzibar), ili kufika malengo ya ukuaji wa uchumi.


HABARI ZAIDI INGIA HAPA

MAPATO YA NDANI YAIMARISHWE KUFANIKISHA MALENGO YA MILLENIA

$
0
0
IMG_7697
Mkurugenzi wa kupunguza umaskini kutoka Wizara ya Fedha, Ana Mwasha (kulia) akifungua kongamano, linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dk.Oswald Mashindano na Katikati ni Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

MKURUGENZI wa Kupunguza Umasikini kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha amesema changamoto za uwezo wa kifedha kutekeleza miradi mbalimbali iliyokuwa katika Malengo ya Milennia, zinatoa ishara tosha ya kubadili mikakati ili kuwa na mafanikio katika Mipango ijayo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na washiriki wa kongamano, linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDGs ili kuhakikisha mafanikio.

Alisema ipo haja ya kuimarisha makusanyo ya fedha za ndani na kuacha kutegemea wahisani, kwa kuwa moja ya sababu za kushindwa kutekelezwa kwa Malengo ya Millenia ni ahadi za wahisani kutotekelezwa. Alisema kipengele cha nane katika Malengo ya Millennia, kiligusia ushirikiano wa kimataifa, ahadi ambazo amesema ukiachia nchi za Luxemburg, Denmark, Sweden na Norway, mataifa mengi hayakutoa asilimia 0.7 ya pato lao la ndani, ambalo lilikubalika kimataifa kusaidia Malengo ya Millennia kwa nchi masikini.

Alisema ili kuwepo na mafanikio katika miradi mipya na ile inayoendelezwa kutoka MDGs, iko haja ya kuangalia jamii iliyopo vijijini, ambako ndiko kwenye umasikini wa kutisha, ingawa Tanzania imefanya vyema kuondokana na umasikini wa chakula. Umasikini wa chakula umepungua hadi asilimia 9 wakati Malengo ya Millenia yalikuwa ni asilimia 11. Alisema ipo haja ya kufungua mawasiliano ya vijijini, kuinua kilimo, kuwapatia nafasi ya masoko na kuinua huduma za jamii.

Pamoja na kuzungumzia uwezo wa kifedha, alisisitiza haja ya wadau kuangalia namna ya kushirikisha sekta binafsi katika kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ili kukabili umasikini.
IMG_7692
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama akizungumza kwenye kongamano la siku moja linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF).

IMG_7701
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano hilo.

Alisema mahitaji ya msingi katika kupunguza umasikini, hayajafikiwa kwani tumefikia asilimia 28.2 wakati tulitakiwa kuwa asilimia 19.
Alisema ipo haja kubwa ya kuangalia utekelezaji wa malengo endelevu kwa kuoanisha na mikakati mingine ya kidunia na ya kikanda, huku kazi kubwa ikiwa kuhakikisha malengo yote 17 yanatekelezwa katika muda uliopangwa.
Katika kongamano hilo, washiriki walipata nafasi ya kumsikia Balozi Celestine Mushy kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akichambua jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo anafikiri Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.
Pia katika majadiliano, washiriki waliozungumzia haja ya kuangalia takwimu kwa kuoanisha kwani zimekuwa zikitafutwa na kila mtu mpaka hazijulikani nani yuko sahihi.
Aidha, walitaka mkakati wa kiviwanda ndio uzingatiwe kwani ndio unaoonesha dira ya kufanikisha maendeleo ya kitaifa, kikanda na kibara.
Kongamano hilo liliendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Uchumi (ESRF) kwa ufadhili wa UNDP.
IMG_7742
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dk.Oswald Mashindano akizungumza kwenye kongamano hilo.
IMG_7724
Pichani juu na chini ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akiwasilisha mada jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.
IMG_7721IMG_7771
Dk. Kenneth Mdadila kutoka kitengo cha uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
IMG_7707IMG_7792
Pichani juu na chini baadhi ya wadau walioshiriki kwenye kongamano hilo wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
IMG_7800

BASATA YALAANI ONYESHO LISILO NA MAADILI LA MSANII SHILOLE NCHINI UBELIGIJI

$
0
0


BASATA YALAANI TABIA CHAFU NA ISIYO NA MAADILI ILIYOONESHWA NA MSANII SHILOLE KWENYE ONESHO LAKE NCHINI UBELIGIJI.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubeligiji hivi karibuni.
 Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimefedhehesha na kuidhalilisha sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla.   

Aidha, BASATA limepokea malalamiko kwa njia ya simu na mawasiliano ya internet kutoka kwa watanzania waishio ughaibuni wakilaani tukio la Msanii huyo. Katika mawasiliano yao wameeleza kwamba wamefedheheshwa na kudhalilika na tabia hiyo chafu iliyooneshwa na msanii huyu.


 Ikumbukwe kwamba, Shilole ni msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa, hivyo anapokwenda nje ya nchi kabla hajapata visa anapewa barua ya utambulisho kama msanii wa Tanzania, hivyo anapokuwa nje ya nchi anatambuliwa kama msanii Mtanzania, anapofanya kinyume na misingi ya kazi ya Sanaa, anajifedhehesha yeye mwenyewe, kazi ya Sanaa na nchi yetu pia.



 Aidha, ikumbukwe kwamba BASATA limeshapata kumwita na kumuonya msanii huyu kutokana na tabia yake ya kutokujiheshimu pale awapo jukwaani na yeye aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo chafu. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio hayo na kwa sasa katika ardhi ya nchi nyingine ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu Sanaa kama kazi nyingine.

BASATA linapenda kueleza kwamba;


1.    Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla
2.    Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si Sanaa na hakina uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua
 BASATA linawakumbusha wasanii wote nchini kuwa Sanaa ni kazi kama kazi zingine lakini siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa wakikiuka suala zima la maadili kwa kutengeneza kazi chafu zisizofaa mbele ya jamii ya watanzania wanaoipenda na kuiheshimu kazi ya Sanaa yenye staha. Tuungane kwa pamoja kukemea kazi chafu zinazozalishwa na wasanii wasiojitambua kwani suala la maadili ni suala mtambuka na linaanzia katika ngazi ya familia.
Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapopata mialiko ya kikazi kwenda nje ya nchi. Linawakumbusha kwamba haiwezekani msanii kutumia picha chafu na mavazi dhalili na kuonyesha utupu katika kuvuta mashabiki.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza

KATIBU MTENDAJI.

TRA YAKUTANISHA WADAU KUJADILI SHERIA MPYA YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI YA MWAKA 2014 KABLA YA KUANZA KUTUMIKA

$
0
0
1c
Afisa Kodi Mwandamizi Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA) Bw. Richard Mwafongo akiwasilishaji kwa Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 ambapo alisema kuwa moja kati ya sababu ya kuandaa sheria hiyo ni kuongeza pato la taifa kupitia makusanyo mbalimbali wakati wa kikao kilichokutanisha wadau mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
2
3
Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja akichangia kwenye moja ya maeneo ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014, wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kujadili maboresho ya sheria hiyo
4
- Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba kuendelea kutoa ushirikiano kuelekea upatikanaji wa Sheria hiyo iliyoweza kutumika popote duniani hasa kwenye nchi zinazoendelea itayowezesha ukusanyaji dhabiti wa Kodi na hatimaye kuchangia maendeleo ya nchi.
5
- Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa Mkutano huo uliofanyika Leo Jijini Dar es Salaam
7
Baadhi ya wadau wakichangia kuhusu Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014
86
Baadhi ya wadau wakichangia kuhusu Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014
8a
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Afisa Kodi Mwandamizi Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA) Bw. Richard Mwafongo alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), Bw. Robert Senya (Katikati) na Bw. Abel Shirima.
Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya upakuaji wa mafuta kwa ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.

KWA HABARI ZA BURUDANI, SIASA, MASTAA NA MUZIKI ANGALIA GLOBAL TV ONLINE


BALOZI WA FINLAND NCHINI TANZANIA ,ANTILA SINIKKA AZINDUA KITUO CHA MSAADA KWA WAHANGA WA UKATILI.

$
0
0
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akikata utepe kuashiria kuazna kutumika kwa majengo hayo.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akifurahia jambo mara baada ya kufungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo hicho.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akiwa katika picha ya pamoja na watoa ushauri.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka alikabidhi kitabu cha "Politics of Gender "kwa mkurugenzi wa Kwieco ,Elizabeth Minde.
Maeneo mbalimbali ya kituo hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Mkurugenzi wa  Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO) akimpokea Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka aliyefika kwa ajili ya uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Watoa ushauri wa shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO)wakiimba wakati wa ufunguzi wa kituo hicho.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akifurahia jambo mara wakati akitembelea majengo ya kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ambayo yamejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo chini ya shirika la UKUMBI
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya KWIECO ,Clement Kwayu akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi Loe Rose Mbise wakai wa sherehe ya uzinduzi wa kituo hicho.
Mkurugenzi wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO) Elizabeth Minde akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Katika kituo hicho wahanga watapatiwa malazi ya muda na huduma zingine za kijamii km matibabu, chakula, msaada wa kisheria, mafunzo ya ujasiriamali n.k
Katibu tawala wa mkoa a Kilimanjaro ,Martha Ufunguo akitoa salama za mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Leonidas Gama wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia,mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Finland kupitia wizara ya mambo ya nje chini ya shirika la UKUMBI
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa KWIECO,Jaji Aishiel Sumari akitoa neno la shukrani mara baada ya hotuba ya mgeni rasmi ,Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka.
Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza kwa niaba ya wadau wa Kwieco wakati wa sherehe hizo.

UNIVERSAL BODY FITNESS, KUZINDULIWA RASMI KWENYE JENGO LA SHAMO TOWER, BAGAMOYO ROAD, MBEZI BEACH JUMAMOSI HII

WAZIRI MEMBE AANZA KUAGA WIZARA YAKE,AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA HIYO JIJINI DAR LEO.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ndio inapika viongozi bora hivyo watumishi wa wizara hiyo wametakiwa kufanya kazi kwa weledi  katika kupata mafanikio ya nafasi mbalilmbali.


Hayo ameyasema leo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernald Membe wakati wa akifungua Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo,amesema wafanyakazi wafanye kazi kwa weledi kutokana na wizara hiyo inavyopika watu kuwa viongozi.


Membe amesema sehemu kubwa ya wafanyakazi Ikulu wanatoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, hiyo ndio inaonekana ni jinsi gani viongozi wanapikwa katika wizara hiyo.


Amesema ikitokea anapata ajira baada ya hapo atatafuta wafanyakazi wa wizara ya mambo ya nje kutokana na upukwaji wa bora wa uongozi katika wizara hiyo.


Membe ametumia baraza hilo kwa kuaga na kuwataka wafanyakazi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura  ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernald Membe akizungumza wakati akifungua Barazala Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernald  akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi wakiwa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu Ya Jamii. 

MKAPA AWATAKA WAKANDARASI NCHINI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA WELEDI.

$
0
0
 RAis mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa akifungua Mkutano wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi leo jijini Dar es salaam
 Rais mstaafu wa awamu ya Pili Mhe.Benjamin Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB).
  Rais mstaafu,Benjamin Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi/wakandarasi waliofanya vizuri na kupewa zawadi mbalimbali na vyeti na Bodi ya Wasajili wa Wakandarasi (CRB).
  Baadhi ya Wahandisi waliohudhuria mkutano huo wakiapishwa leo jijini Dar es Salaam. 
  Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia masuala mbalimbali. Picha/Aron Msigwa -MAELEZO. 


Na.Aron Msigwa -MAELEZO.
14/5/2015.Dare es salaam.


Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin Mkapa amewataka Wakandarasi kote nchini kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ujenzi ili miradi wanayoisimamia na kuitekeleza iweze kuwa na manufaa kwa taifa.

Mhe.Mkapa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) uliowawajumuisha pia wadau wa sekta ya Ujenzi kutoka nchini Malawi na Kenya.

Amesema umakini katika usimamizi wa kazi za wakandarasi na uwepo wa wataalam waliobobea katika sekta ya ujenzi umechangia kwa kiasi kikubwa kasi maendeleo inayotokea sasa nchini Tanzania.

Ameeleza kuwa sekta ya ujenzi ndiyo iliyolifikisha taifa hapa kutokana na mchango wake katika Pato la Taifa unaofikia asilimia 14.1 ikifuatiwa na sekta nyingine na kuongeza kuwa ili nchi iweze kuendelea lazima wakandarasi wazalendo wajengewe uwezo ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa katika sekta ya ujenzi zinabakia Tanzania na kuwanufaisha wazawa badala ya wageni.

Amesisitiza kuwa uchumi wa Tanzania lazima ubakie mikononi mwa watanzania wenyewe na kutoa wito kwa Serikali kuendelea kutoa kipaumbele kwa wakandarasi wa ndani ili wawe na uwezo wa kujiendeleza na kujitegemea kwa kutengeneza ajira nyingi zaidi na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati.


Amewataka wakandarasi wa ndani kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi, kuzingatia kanuni na taratibu zinazosimamia sekta hiyo ili taaluma yao iendelee kuheshimiwa ndani na nje ya nchi huku akisisitiza umuhimu wa wakandarasi hao na kuungana ili kujenga uwezo wa kushindana na makampuni mengine kutoka nje.

Kwa upande Waziri wa Ujenzi Mhe.John Magufuri akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa ili taifa liweze kupata maendeleo endelevu katika sekta ya ujenzi lazima wataalamu wanaohusika na sekta hiyo wafanye kazi zao kwa kuzingatia kanuni, miiko na sheria zilizowekwa.

Amesema taaluma ya uhandisi nchini Tanzania imechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha miundombinu ya barabara, madaraja,majengo,vivuko mbalimbali na miundombinu mingine muhimu ya kuwarahisishia wananchi huduma bora ya usafiri.

Aidha, amesema uwepo wa sheria na 15 inayosimamis sekta hiyo hapa nchini na ongezeko la wakandarasi waliosajiliwa wanaofikia 15,062 kutoka ndani na nje ya nchi, wengi wao wakiwa watanzania linaonyesha maendeleo makubwa yaliyopigwa na sekta hiyo ikilinganishwa na miaka 15 iliyopita.

Amesema Serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete iko katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo miradi mikubwa ya barabara za mzunguko katika jiji la Dar es salaam Barabara, madaraja makubwa, reli na miradi mingine ambayo itaifungua nchi ya Tanzania kitaifa na kimataifa na kuimarisha sekta usafirishaiji

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa kipaumbele kwa Wakandarasi wazalendo kote nchini Ili waendelee kunufaika na zabuni mbalimbali zinazotangazwa kote nchini kwa asilimia 45 na kuongeza kuwa malengo yaliyopo ni kufikia ongezeko la asilimia 70 ili uchumi wa sekta ya ujenzi uendelee kubaki nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Dkt.Ambwene Mwakyusa amesema mkutano huo umeandaliwa na Bodi ya Wakandarasi Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta ya ujenzi Chini ya kauli Mbiu isemayo Changamoto na Mustakabali wa Sekta ya Ujenzi katika Kutimiza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Amesema licha ya sekta ya ujenzi nchini Tanzania kuendelea kupata mafanikio nchini bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kihandisi zikiwemo za mazingira yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi katika kuathiri ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo madaraja na barabara ambazo zimekua zikiathoriwa na mvua.

Amesema wakandarasi wanakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ucheleweshwaji wa malipo yao na madeni makubwa wanayoidai Serikali kutokana na miradi waliyofanya katika maeneo mbalimbali nchini.

Amefafanua kuwa mkutano huo wa mwaka umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo kutoka Kenya na Malawi pamoja na kampuni mbalimbali zipatazo 95 zinazojihusisha na ujenzi zilizoshiriki kuonesha namna zinavyotekeleza majukumu yao, kuonesha bidhaa wanazozalisha,vifaa vya ujenzi na mitambo mbalimbali inayotumika katika ujenzi hapa nchini.

Katika hatua nyingine Bodi ya Usajili wa Wakandarasi imewaapisha Wahandisi waliohudhuria mkutano huo ili kulinda weledi na ufanisi wa kazi zao na kuwakumbusha wahandisi hao kutumia utaalam wao katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia viwango ,sheria na taratibu zilizowekwa.

Aidha Bodi ya Usajili wa Wakandarasi imetoa zawadi mbalimbali ikiwemo vyeti kama motisha ya kutambua mchango wa makampuni na wakandarasi wazalendo waliofsnya vizuri katika sekta hiyo nchini Tanzania kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo suala la uzingatiaji wa Afya na usalama mahali pa ujenzi,viwango vya ubora wa ujenzi na vifaa wanavyotumia katika miradi mbalimbali wanayotekeleza.

DKT. MWAKYEMBE AFUNGUA KONGAMANO LA VYOMBO VYA HABARI DAR

$
0
0
3
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Harrison Mwakyembe akifungua kongamano la siku mbili mapema hii leo jijini Dar es Salaam linalotathmini mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
7
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisikiliza kwa makini michango mbalimbali ya wadau wa habari wakati wa kongamano la siku mbili mapema hii leo jijini Dar es Salaam linalotathmini mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki, kushoto ni Katibu wa bunge la Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera na kulia.
4
Baadhi ya Mabalozi na wadau wa habari wakimfuatilia kwa makini Waziri wa Ushirikianno wa Afrika Mashariki Dkt. Harrison Mwakyembe wakati akifungua kongamano la siku mbili mapema hii leo jijini Dar es Salaam linalotathmini mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
8
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Harrison Mwakyembe ( mwenye tai ya njano mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa habari wakati wa wa kongamano la siku mbili mapema hii leo jijini Dar es Salaam linalotathmini mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki, kushoto ni Katibu wa bunge la Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera na kulia.Picha zote na Eliphace Marwa – MAELEZO


1
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT), Kajubi Mukajanga (pichani)akiwashukuru washiriki wa kongamano la vyombo vya habari litakalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, kongamano hilo linaloratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki linalenga kutathmini mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika ukanda wa afrika Mashariki.
2 
Katibu wa bunge la Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera akitoa neno la shukrani kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe kufungua kongamano la siku mbili linalotathmini mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki, kongamano hilo linaloratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 5
Mmoja wa wadau wa habari Dkt. Ayoub Rioba akichangia katika kongamano la siku mbili mapema hii leo jijini Dar es Salaam linalotathmini mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
6
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene akijibu maswali mbalimbali ya washiriki wa kongamano la siku mbili mapema hii leo jijini Dar es Salaam linalotathmini mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live


Latest Images