Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 528 | 529 | (Page 530) | 531 | 532 | .... | 1897 | newer

  0 0

  pichaaaaa
  Na Pamela Mollel wa jamiiblog
  Wasanii wawili wa kizazi kipya nchini Nurdin Billal maarufu kama Shetta na Abdulwaheed Sykes” Dully Sykes” kesho jumamosi  wanataraji kunogesha katika onyesho la kundi la marafiki wa waziri mkuu mstaafu,Edward Lowasa lililopewa jina la “ Usiku wa marafiki wa Lowasa” .

  Onyesho hilo limeandaliwa na kundi la marafiki hao wa Lowasaa chini ya umoja wao unaojulikana kama “4 U Movement” linataraji kufanyika katika ukumbi wa burudani wa Triple A uliopo jijini Arusha ambapo mbali na wasanii hao pia wasanii wengine wachanga wanataraji kulisindikiza .

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mratibu wa onyesho hilo,Jonathan Kassano alisema kuwa lengo kuu ni kuwakutanisha marafiki wote wa kiongozi huyo anayetajwa kuwania mbio za urais mwaka huu kufahamiana, kubadilishana mawazo pamoja na kubalishana ujuzi .

  Mratibu huyo alisema kuwa onyesho hilo litaenea katika mikoa mbalimbali nchini ambapo mnamo Mei 20 mwaka huu kuanzia majira ya saa 4;00 usiku litafanyika  pia katika mkoa wa Dodoma na kisha kuelekea jijini Mwanza kabla ya kusambaa kote nchini.

  Alisema kuwa kufanyika kwa onyesho hilo katika mikoa mbalimbali nchini kutawapa fursa marafiki wa kiongozi huyo ambaye  pia ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha kutawapa fursa marafiki hao kukutana na kufahamiana pia.

  0 0

  Na Takdir Ali –Maelezo Zanzibar.


  Viongozi wa vyama vya siasa na Dini wametakiwa kuwashajiisha wafuasi wao kushiriki katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kujikinga na matatizo mbali mbali yanayoweza kujitokeza ikiwemo kokosa haki zao.


  Amesema Daftari la kudumu la wapiga kura lipo kisheria si kwa matakwa ya kisiasa hivyo viongozi hao wanapaswa kutumia nafasi zao kuwaelimisha wafuasi wao kushiriki kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea kuboreshwa.


  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Ayub Mohd Mahmoud wakati alipokuwa akifungua semina ya kutoa elimu ya uandikishaji na uendelezaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa vijana wa Wilaya ya Magharib A na B hapa Mwera Wilaya ya Magharibi B.


  Amewaaleza vijana kuwa mara baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992,hali ya siasa Zanzibar haikuwa nzuri lakini juhudi za viongozi walizochukuwa zimepelekea hali hiyo kutulia, kwa hiyo si vizuri kwa wazee kuwaachia watoto wao au wajukuu zao Zanzibarisiokuwa na amani na utulivu.


  “Tumerithi nchi yetu kutoka kwa wazazi wetu ikiwa katika hali ya amani na utulivu sivizuri hata kidogo kuwaachia watoto na wajukuu zetu wakiwa katika nchi isiyokuwa na amani na utulivu,” alisema Ayub.  Aliongeza kuwa vijana kutoyajua yaliyopita  na kujua yaliopo  hivi sasa yanapelekea kukosa nafasi ya kufikiri zaidi katika kutoa maamuzi jambo ambalo amesema wanaweza kutoa maamuzi yasiyo sahihi.


  Mapema akitoa maelezo Afisa uandiskishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura Wilaya ya Magharibi Maalim Khamis Mussa  amesema ili kufanikisha Daftari hilo linaboreka zaidi  mashirikiano ya pamoja  ya  wadau mbali mbali ikiwemo  vyama vya siasa, vyama vya hiari na Wananchi wenyewe.


  Mwalimu Khamis amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa  wananchi kuwa kuna baadhi  ya majina ya  watu waliofariki ambao majina yao hayajaondolewa katika Daftari la kudumu  na kusema Tume ya Uchaguzi haina uwezo wa kuwaondoa waliokosa sifa katika daftari hilo bila ya wananchi kuenda kutoa vielelezo muhimu .


  Wakichangia katika semina hiyo washiriki wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Tume ya Uchaguzi kuandaa mazingira mazuri ya kuwawezesha wananchi kushiriki katika daftari la kudumu la wapiga kura bila vikwazo vyovyote sambamba na kuweka wazi kuwa watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ambao hawakupatata fursa hiyo muhimu ya kushiriki.
  0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akisisitiza jambo kwa wadau mbalimbali wa habari toka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo wakati akifunga kongamano la siku mbili la wadau wa habari liloandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye lengo la kuangalia mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
   Mhariri wa gazeti la Hoja toka nchini Tanzania Bw. Yassin Sadik  akichangia mada wakati wa kufunga kongamano la siku mbili la wadau wa habari liloandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye lengo la kuangalia mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw. Kajubi Mukajanga akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe kufunga kongamano la siku lilowashirikisha wadau mbalimbali wa habari toka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

   Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kufunga kongamano la siku mbili la wadau wa habari liloandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye lengo la kuangalia mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wadau wa habari toka nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika Mashariki wakiimba kwa pamoja wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa kufunga kongamano la siku mbili la wadau wa habari liloandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye lengo la kuangalia mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO


  0 0

   Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015. 
   Balozi wa Chini nchini Tanzania,Lu Youging akizungumza jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015,kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh.Anne Kilango Mallecela. 
   Baadhi ya Wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali mjini Dodoma waliohudhuria sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15,2015 .

  0 0

  SAM_2715
  Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_2723Umati mkubwa wa wananchi wa Arusha wakiwa wanampungia mkono Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee .
  SAM_2688
  Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa akiwa sheikh mkuu wa Bakwata mkoani  Arusha,Shaaban Juma wakifurahia jambo katika hafla ya harambe ya ujenzi wa  msikiti wa Patandi iliyofanyika jana katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha,jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana.
  SAM_2682Mkurugenzi wa kituo cha Redio 5 Arusha Francis Robart akiwa anawasilisha jumla ya fedha zilizopatikana katika harembee hiyo kwa Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa.
  SAM_2709Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa  msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee 
  ?????????????
  Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anasalimiana na baadhi ya wadau waliokuja kumuunga mkono katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee.
  SAM_2716Taswira ya picha wakati Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anaondoka katika uwanja wa msikiti mkubwa jijini Arusha
  SAM_2727
  ?????????????
  Msafara wa pikipiki 
  SAM_2695Mgombea anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini kupitia CCM, Mustafa Panju ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Bush Buck Safaris  akiwa anasalimiana na Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa baada ya kumkabidhi shilingi Milioni sita kwaajili ya ujenzi wa msikiti Patandi.
  SAM_2693Diwani Mathias Manga  akiwa anawasilisha mchango wa rafiki yake wa karibu Husein Gonga wa shilingi Milion saba.
  SAM_2679Mkurugenzi wa Redio 5 Arusha Francis Robart  kulia wakiwa wanapiga hesabu ya jumla ya fedha zilizopatikana
  SAM_2730Muonekano jiji la Arusha
  SAM_2660Kada maarufu wa chama cha CCM,Violet Mfuko katikati akiwa na diwani viti maalum Vick Mollel wakiwa wanamshangilia mgeni rasmi Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo 

  SAM_2669Kushoto ni mtia nia jimbo la Arumeru mashariki Solom Sioi pamoja na mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima wakifatilia jambo katika harambee hiyo

  SAM_2673Mbunge wa Kigoma mjini Peter Serukamba akiwasilisha mchango wake.
  SAM_2672
  SAM_2665Wananchi wakiwa wanamsikiliza Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa

  Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa anatarajia kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais kupitia CCM mnamo Mei 24 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.

  Lowasa,alitoa kauli hiyo leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo alifanikisha kuchangisha jumla ya zaidi ya kiasi cha sh,200 milioni ambapo watu mbalimbali walimuunga mkono katika harambee hiyo.

  Akizungumza katika hafla hiyo leo kwa mafumbo Lowasa alisema kuwa mnamo Mei 24 mwaka huu anataraji kusema neno ambalo atahitaji wananchi wamuunge mkono siku hiyo.

  "Niseme neno nisiseme,tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid siku hiyo nitasema neno ambalo nitahitaji mniunge mkono ambalo nitahitaji mniunge mkono "alisema Lowasa

  Lowasa kwa kujiamini aliwaomba kila mkazi wa Arusha siku hiyo kutoka na kuja uwanja huo na kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini.

  "Ukiulizwa unaenda wapi sema unakuja kuniunga mkono katika safari yangu ya matumaini"alisisitiza Lowasa 

  Hatahivyo,Lowasa aliipongeza kamati ya amani ya mkoa wa Arusha inayoundwa chini ya Askofu wa kanisa katoliki la jimbo kuu mkoani Arusha,Josephat lobullu kusimamia amani ya mkoa huo.

  Aliipongeza kamati hiyo na kusema kuwa amani ya mkoa wa Arusha ni muhimu kuliko jambo lolote kwa kuwa Arusha ni mji ambo ni chanzo cha utalii duniani.

  "Tuendelee kuheshimiana bila kujali misingi ya dini,kabila au rangi lakini niipongeze kamati ya amani ya hapa Arusha kwa kuwa Arusha ni mji wa kitalii bila amani hakuna utalii Arusha"alisema Lowasa na kuibua shangwe

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Dodoma unaojengwa na Chama Cha Mapinduzi CCM.kulia ni makamu mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na makandarasi wanaojenga ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Dodoma unaojengwa na Chama Cha Mapinduzi CCM, leo.Ukumbi huu upo karibu na Benki Kuu, njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma.

  Muonekano wa ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Dodoma.(picha na Freddy Maro).

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari leo (hawapo pichani) ,jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kubadilika kwa tarehe ya mkutano wao kufuatia kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape NnauyeAkizungumza na waandishi wa Habari leo ,jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kubadilika kwa tarehe ya mkutano wao kufuatia kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
  =========  ========  =======
  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  KAMATI kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inatarajia kukutana Mei 23 mjini Dodoma na kujadili ajenda mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu .

  Akizungumza na waandishi wa Habari leo ,jijini Dar es Salaam,Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kuwa kubadilika kwa siku ya mkutano imetokana na kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.

  Nape amesema kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kitafanyika Mei 22 ambapo ajenda mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na maoni ya Ilani ya CCM 2015-2020 ambayo itawasilishwa na Kamati iliyoundwa kwa kazi hiyo.

  Amesema kutakuwa na vikao vya kawaida Mei 21 hadi 22 ambavyo vitakuwa vinafanyika mkoani Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Kamati kuu  ya CC na Halmashauri Kuu (NEC).

  Nape amesema vikao hivyo vitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete katika kujadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya siasa ya chama hicho.

  Wakati huo huo Nape amesema kuwa wanachama sita  waliofungiwa  bado hatma yake kutokana na suala hilo linashughulikiwa na kamati mbili ambazo ndizo zinaweza kusema kifungo kinaendelea ama la,amesema na kuongeza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM)  kinaongozwa na kanuni ambazo yeye mwenyewe amezikuta hivyo ni lazima wanachama na makada wazifuate kanuni na miongozo ya chama.

  Amesema wanachama kutangaza nia ya kugombea sio tatizo lakini mazingira yanayoendana baada ya kutangaza nia hiyo ndipo kanuni na miongozo ya chama inaanza kutumika,amesema kanuni na miongozo ya CCM zinasema mtu ambaye yuko kwenye kifungo katika chama haruhusiwi kugombea nafasi yeyote ndani ya chama ambazo zipo wazi.

  Amesema mikutano hiyo itajadili jinsi gani watu watapochukua fomu,urudishaji wa fomu pamoja na njia ambazo zitatumika katika utangazaji nia kwa wagombea kutokana na mazingira yaliyopo.  0 0

  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa shirika hilo kutoka ofisi ya mkoa wa Temeke.
  Meneja Kiongozi mpya wa Ofisi ya NSSF Mkoa wa Temeke, Chedrick Komba akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa NSSF.

   Aboubakary Mshangama (kushoto) na Miraji Lipumba wakipeleka zawadi za wastaafu.
   Meneja Kiongozi mpya wa Ofisi ya NSSF Mkoa wa Temeke, Chedrick Komba akimkabidhi zawadi mstaafu wa NSSF, Mohamed Kilumike.
   Mstaafu wa NSSF, Brahan Newa kutoka Kitengo cha Takwimu akipokea zawadi yake kutoka kwa Meneja Kiongozi mpya wa Ofisi ya NSSF Mkoa wa Temeke, Chedrick Komba.
   Mstaafu wa NSSF, Brahan Newa kutoka Kitengo cha Takwimu akisalimiana na mstaafu mwenzake, aliyekuwa Meneja Kiongozi, Ofisi ya NSSF mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali wakati wa hafla ya kuwaaga iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
   Maofisa wa NSSF wakiwa katika hafla hiyo.
   Mstaafu, Brahan Newa akiwa na familia yake.
   Meneja Kiongozi mpya wa Ofisi ya NSSF Mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (kushoto) akiwa na aliyekuwa Meneja Kiongozi wa Ofisi hiyo, Yahya Mhamali wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa NSSF ofisi ya mkoa wa Temeke.
   aliyekuwa Meneja Kiongozi wa Ofisi hiyo, Yahya Mhamali wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa NSSF ofisi ya mkoa wa Temeke.
  Ofisa Mafao mstaafu wa NSSF, Margaret Mahege aakitoa neno la shukrani wakati wa hafla hyo.
  Mstaafu Kitengo cha Takwimu NSSF, Brahan Newa akitoa shikrani zake wakati wa hafla hiyo. 
  Ofisa Matekelezo mstaafu wa NSSF, Mohamed Kilumike akiwashukuru wafanyakazi wenzake kwa ushirikia wao wakati akiwa kazini. 
   Maofisa Waandamizi wa NSSF wakiwa katika hafla hiyo. 
  Ofisa Matekelezo mstaafu wa NSSF, Mohamed Kilumike (kulia) akiteta jambo na mstaafu Kitengo cha Takwimu, Brahan Newa
  Kutoka kushoto ni, Brahan New, Margaret Mahege na Yahya Mhamali wakikata keki wakati wa hafla ya kuwaaga.
  Yahya Mhamali akilishwa keki wakati wa hafla ya kuwaaga wafanyakazi wa NSSF ofisi ya mkoa wa Temeke.
  Margaret Mahege akilishwa keki.
  Abrahan Newa akilishwa keki.
  Picha ya pamoja. 
  Maofisa wa NSSF.
  Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF ofisi ya mkoa wa Temeke.
  Shukurani Masima (kushoto), Ummy Kimario wakifungua Shampeni.
  Wastaafu wakitakiwa afya njema na maisha marefu.
   Cheers
   Cheers
    Cheers
   Cheers mama.
   Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja.
   Ofisa Mafao mstaafu wa NSSF, Margaret Mahege aakitoa neno la shukrani wakati wa hafla hyo.
  Brahan Newa akishukuru kwa niaba ya wastaafu wenzake.
   Wastaafu pamoja na viongoi wa NSSF wakipata chakula.
   Wakati wa chakula.
   Ofisa Matekelezo mstaafu wa NSSF, Mohamed Kilumike akiwaongoza wafanyakazi wa NSSF kupata chakula.

  Wafanyakzi wa NSSF wakipata chakula.
   Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
   Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NSSF
  Muziki.

  0 0

  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Qaswida lililoandaliwa na Ulamaa Promotions Centre litakalofanyika  Mei 24 kwenye viwanja vya sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
  index
  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, ustadh Jumanne Ligopora.

  Ligopora alisema wamejipanga katika tamasha hilo kushirikisha madrasa zaidi ya 50 za jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa.
  Aidha Ligopora alisema hivi sasa wako kwenye mchakato wa kusambaza mialiko kwa madrasa za Dar es Salaama na mikoani.

  “Tunatarajia maelfu ya Waislamu kumiminika kwa wingi katika viwanja vya Benjamin Mkapa kwa lengo la kupata ladha mbalimbali za Qaswida,” alisema Ligopora,” alisema Ligopora.

  Mwenyekiti huyo wa Kamati ya maandalizi, alisema wameshapeleka taarifa kwa madrasa mbalimbali za jijini Dar es Salaam  na nyingine zilizoko mikoa jirani.

  0 0

  1
  Mgeni rasmi Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Faraji Abdalla akizindua Jumuiya ya watanzania wasio na ajira (TUEPO)  katika Ukumbi wa Water Front Rahaleo Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  5
  Mwenyekiti wa TUEPO Ussi Said Suleiman akimtoa maelezo mafupi ya Jumuiya hiyo na kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano huo.
  4
  Muongozaji wa Mkutano wa Uzinduzi wa Jumuiya ya Vijana wasio na ajira Tanzania TUEPO Msabah Ali Msabah akitoa maelezoa kwa washiriki wa Mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Water Front Rahaleo Mjini Zanzibar.
  3
  Picha ya pamoja  ya viongozi wa Jumuiya ya TUEPO wakiwa pamoja na Katibu Mtendaji Baraza la Vijana  Zanzibar (suti nyeusi)  baada ya kufungua mkutano huo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  2
  Mwenyekiti wa TUEPO Ussi Said Suleiman akiagana na Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Faraji Abdalla.
  ……………………………………………………………………….
  Na Maryam  Kidiko / Rahma Khamis  Maelezo  Zanzibar 
  Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar Nd. Khamis  Faraji Abdallah amewataka Vijana kujiunga  katika Taasisi zitakazo wawezesha kuwainuwa kimaisha.
  Hayo ameeleza katika Ukumbi wa Water front  Raha leo wakati alipokuwa akizindua Jumuiya  ya vijana wasio na ajira Tanzania  (Tanzania unemployed people organization) TUEPO .
  Amesema Baraza la Vijana Zanzibar lipo kwa ajili ya kuwasikiliza na kuwaelekeza vijana  ambao hawana ajira ili waweze kujiendeleza na kujiimarisha katika shughuli  mbali mbali za maendeleo ili  waweze kujiari  wenyewe .
  “ Ni lazima tufanye kazi kwa pamoja ili Baraza la Vijana Zanzibar  liweze kuimarika na kufanyakazi  kwa ufanisi,”  aliesema Katibu  Khamis.
  Akizungumzia   lengo la Baraza hilo amesema  ni kuwawakilisha Vijana   kufaidika na fursa zilizopo,  kuwawezesha   kujielewa,  pamoja na kuwashajiihisha kuwa na uwezo wa kuzalisha mali.
  “Ni vizuri kushirikiana  pamoja ili vijana waweze kuimarika katika maisha yao na Jamii kwa ujumla,” amesisitiza Khamis Faraji.
  Katibu huyo amewapongeza wanajumuiya hao kwa kufanikisha kuanzisha taaluma mbali mbali  ikiwemo  Ubaharia, Udereva, ushoni, Mapishi pamoja na kusomesha lugha ya kiengereza ambayo lengo lake ni kuwawezesha  vijana  kuajirika katika  Hoteli mbalimbali za  ndani na nje ya nchi.
  “Tutumie fursa iliyopo kwa ufanisi  zaidi bila ya kujali itikadi   ya vyama vya  siasa,”  ameongeza Khamis  Faraji.
  Nae Mwenyekiti wa Jumuiya  ya TUEPO  Ussi Saidi Suleiman  amesema wanatarajia  kuwapatia mafunzo ya ubaharia vijana watatu,  vijana 15  mafunzo ya mapishi, kumi  ushoni na vijana 20  wanatarajiwa kusomeshwa lugha ya kiengereza.
  Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kuwapatia mikopo ambayo itawawezesha vijana kuwaendeleza katika kukuzi vipaji na kujiendeleza kiuchumi sambamba na kuanzishwa viwanda ili vijana  waweze kupata ajira.
  Jumuiya hiyo  imeanzishwa  mwezi uliopita  na  ina wanachama 73 hadi hivi sasa. IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO -ZANZIBAR

  0 0

   Muonekano wa ndani wa ukumbi mpya wa mikutano uliojengwa na CCM mjini Dodoma ambao uko katika hatua za mwisho kukamilika kabla ya kuanza kutumika.Ukumbi huu upo karibu na jengo la  Benki Kuu, njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma - UDOM.

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Dodoma unaojengwa na  CCM.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Dodoma unaojengwa na  CCM. Kulia ni makamu mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na makandarasi wanaojenga ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Dodoma unaojengwa na  CCM, leo.Ukumbi huu upo karibu na Benki Kuu, njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma.

  Muonekano wa ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Dodoma. Picha na Freddy Maro.

  0 0

  MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions ambayo ndio inaandaa matamasha ya Pasaka na Krismasi, Alex Msama amekemea waimbaji wa muziki wa Injili Tanzania kufanya kazi ya Mungu na kuachana na siasa ambazo zinawaondoa kwenye uinjilishaji. 

  Msama ameyasema hayo wakati tukielekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na urais unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Msama anasema karipio hilo linawahusu pia viongozi wa dini wakiwamo Wachungaji na Maaskofu  ambao wanaonesha nia ya kutaka kuwania uongozi wa kisiasa katika nafasi hizo tatu.Sababu za Msama kukemea waimbaji wa Injili kujihusisha na Wanasiasa wakiwemo wagombea urais, kuna baadhi ya waimbaji wametunga nyimbo za ‘kuwatukuza’ wagombea urais wakati wao wanatakiwa muda wote kumtukuza Mungu na si binaadam wenzao.

  “Waimbaji tunatoka katika mstari, kwani Mungu anawategemea kufikisha ujembe wake kwa lengo la kuachana na machukizo ambazo yanapoteza mwelekeo wa jamii mbalimbali ambazo zinahitaji maono ya Wainjilisti,” alisema Msama na kuongeza. “Waimbaji ambao ninashirikiana nao katika kufikisha huduma ya neno la Mungu, nashangaa wanatoka katika mstari nawaomba wamrudie Mungu kwani wanapotea wakiwatumikia mabwana wengine.”  Alisema.

  Anasema kitendo wanachokifanya waimbaji na wachungaji ni kinyume na huduma ndani ya mioyo yao kwa sababu wanachokifanya si sahihi. Anafafanua kwamba kazi ya muziki wa injili ni kuhubirisha, waimbaji ni Wainjlisti wanawatoa waovu kwa shetani na kuwapeleka kwa Mungu ambaye ndiye tegemezi kwa binadamu wote.

  “Ni jambo la kusikitisha sana, wanamhuzunisha bwana Yesu, alipoondoka kwenda mbinguni aliwaambia wafuasi wake,  nendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili yangu, mwenye kuamini ataokoka na asiyeamini ameangamia,” alieleza Msama.

  Anasema kwa kufanya hivyo waimbaji hao ndio wanahubiri uovu kwa kuwapamba wachafu  na kuwafananisha na Yuda Eskariot aliyemsaliti bwana Yesu  kwa ajili ya pesa na kuwataka waliofanya hivyo waache mara moja.
   
  Msama anaendelea kueleza na kufafanua kupitia maandiko matakatifu  kwamba ya Kaisari wamuamuachie Kaisari, mwenye kupewa sifa na wao ni Mungu peke yake, mwanadam hawezi kupewa sifa na kuinuliwa kwa sifa.

  Pia anawakemea wagombea urais waache kuwatumia waimbaji  wa Injili na kujificha kwenye Kanisa kwamba ndio sehemu ya kuombea kura na kugawa pesa Makanisani, Mungu hahongwi na waache pia kumchokoza Mungu kwani akichukia zaidi mwisho wake ni mbaya.

  Anasema siasa na dini ni vitu viwili tofauti kwani kwenye siasa uongo ni mwingi ambao katika uinjilishaji hautakiwi kwa sababu unakwenda tofauti na maandiko matakatifu ya Mungu. “Nahuzunishwa na wanaotumia mfumo huo kwa sababu siasa inayohubiriwa ni ya kumjenga mgombea urais na kumpamba, wakati katika maandiko matakatifu hakuna mambo ya kupambana kama inavyofanyika sasa,” alisema.

  Anaeleza kwamba Wachungaji wanasahau kazi zao ambazo ni kuwachunga kondoo wa Mungu  na kuhubiri Injili na si lingine lolote. “Nia zao wakazitangaze huko na wakiendelea nitawaweka hadharani kwani nitawaumbua kwa kuwaeleza kwamba hawafai kuwa Marais kwa mtindo wanaoutumia,” alisema. Msama ndiye ‘anayedili’ na waimbaji wa muziki wa injili waache na watubu sambamba na kukiri makosa yao kwa Mungu na waachane na dhambi ambayo ni kero kwa Mungu.

  Wachungaji wanaojielekeza kwenye siasa waache mpangilio huo kwa sababu haiwezekani kuwatumikia mabwana wawili na kazi yao kwa Mungu ni Injili pekee. “Ukijikita huko utakuwa huna muda wa kumtumikia Mungu, siasa inasababisha kusema uongo wakati uchungaji una heshima kubwa,” alisema Msama.

  0 0  0 0


    Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mohamed Raza akionesha baadhi ya vifungu vya sheria vilivyopo kwenye kitabu kidogo cha sheria za Zanzibar,Mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
   Mtangazaji wa BB Swahili nchini Tanzania,Arnold Kayanda akifanya mahojiano mafupi na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Raza mara baada ya kuzungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Raza katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  MBUNGE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mohamed Raza amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kutafuta mgombea wa nafasi ya urais mwenye sifa na sio watu wanaotoa fedha kwa ajili ya kutaka kupendekezwa katika kiti hicho.

  Raza ameyasema  hayo leo  jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,amesema fedha nyingi zinamwagwa Zanzibar  kwa ajili ya watu wanaotaka Urais na fedha hizo zinatoka kwa wafanyabiashara ambao watataka zirudi au kumwamulia Rais katika nafasi za uteuzi wa baraza la mawaziri ambao watanufaika  katika kuhakikisha mambo yao yanakwenda.

  Amesema vyombo vya dola visaidie katika kupata rais mwenye sifa kwani ndiye Amiri Mkuu wa Ulinzi na Usalama, na bila kufanya hivyo wataakoumia ni watanzania huku viongozi wakijinufaisha wenyewe.

  Raza amesema kuwa CCM ikifanya vibaya katika kuchagua mtu sahihi, kuna upande wa pili wa UKAWA wana nguvu kutokana na mambo yanayoendelea nchini kutokwenda sawa na wanatumia hoja na hawawezi kuzuilika hata wamwagiwe maji ya pili pili wakitaka kufanya maandamano.

  Raza ambaye ni Mbunge Muwakilishi wa Jimbo la Uzini amesema kuwa hali inayokwenda sasa sio nzuri kutokana bajeti ya Zanzibar kukosa wafadhili kutokana na watu waliojipatia fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow wakati wazanzibar hawajahusika kujipatia fedha hizo.

  Amesema kutokana na kukwama kwa wafadhili, wanaoathirika ni wananchi kwani posho ya mbunge ya siku ndio fedha ya mwananchi ya mwezi mmoja hivyo kutokana na dola kushuka wataathirika kwa kiwango kikubwa.

  "Aidha kutokana mambo yanayoendelea tunahitaji kuwa na viongozi ambao wanaangalia wananchi na sio wale ambao wanajiangalia wenyewe kwa masilahi yao binafsi huku wanaowagua wakiwa na hali mbaya",alisema Raza. 

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kushoto) akizungumza na wandishi wa Habari (pichani hawapo)  baada ya hitimisho la  Mkutano wa nne wa mafunzo ya Upasuaji wa Ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya fahamu, Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid, uliomalizika hivi karibuni. ambapo wakishirikiana na Wataalamu  madaktari bingwa wa Chuo cha Weill Cornell toka Marekani kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya kisasa, ambapo Watanzania  21 wamefanyiwa  upasuaji wa magonjwa hayo wakishirikiana na madaktari toka Tanzania , Uganda, Rwanda, Southi Afrika, Marekani na Ulaya. Dokta Othman Kiloloma, alimshukuru Rais Jakaya Kikwete ambaye aliye waweka karibu na wenzao wa Chuo cha Marekani na kuwashukuru wenzao wa chuo cha marekani kwa kuwawezesha kufanyika upasuaji huo. (wakwanza kulia) ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani,ambaye aliwaeleza waandishi hao kua mgonjwa mmoja kufanyiwa upasuaji anagharimu kiasi cha dola elfu moja za upasuaji huo nahaihusiani na mambo mengine.na katikati ni Profesa Philip Steg toka Chuo cha Marekani nayeye alipata nafasi ya kuongea na waandishi hao na kuwashukuru Wataalamu wa Moi (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (wapili) kushoto na kuanzia kulia ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani anaye fatia ni Profesa Philip Steg toka  Chuo cha Weill Cornell  Marekani na kushoto ni Menneja ea Taasisi ta Moi Almas Jumaa.
   Madaktari wakiwakatika Upasuaji na ikiongozwa Dk, Japhet Ngerageza
   Mashine ya kisasa yenye thamani shilingi mil. 700 iliyotolewa msaada na Weill Cornell toka Marekani ikikumika kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania kwa Muungano wa jitihada za Rais Jakaya Kikwete.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  TU2
  Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Alhaji Mussa Salum akizungumza katika sala ya hitima ya marehemu Abdallah Rehani, baba mzazi wa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Tabata jijini Dar es salaam Mei 17, 2015.Kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim na kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa katavi, Dkt. Ibrahim Msengi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  TU3
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika sala ya hitima ya marehemu Abdallah Rehani, baba mzazi wa  mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Tabata jijini Dar es salaam Mei 17, 2015. TU4
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim baada ya hitima ya marehemu Abdallah Rehani, baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu, Tabata jijini Dar es salam Mei 17, 2015. 
  TU5
  Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal akiagana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya sala ya hitima ya marehemu, Abdallah Rehani, baba mzazi wa mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Tabata jijini Dar es salam Mei 17, 2015. 

  TU1
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akifarijiwa na Mke wa makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha  Seif Iddi katika Sala ya Arobaini ya kifo cha Baba mzazi wa mke wa Waziri Mkuu, Marehemu Abdallah Rehani iliyofanika nyumbani kwa Marehemu, Tabata jijini Dar es salaam Mei 17, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  NU1
  Rais Kikwete akimpokea Rais Filipe Jacinto Nyusi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini  Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
  NU2
  Rais Kikwete akimpokea Rais Filipe Jacinto Nyusi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini  Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
  NU3
  Rais Filipe Jacinto Nyusi akipokea shada la maua baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.NU4
  Rais Filipe Jacinto Nyusi akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.NU5
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi wakiangalia ngoma  baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.NU6
  Rais Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu jijini Dar es salaam katika siku ya kwanza ya  ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
  NU7
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake  Rais Filipe Jacinto Nyusi wakishangiliwa na mamia ya wakazi wa Dar es salaam waliojitokeza kwa wingi kumlaki Rais huyoanayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu
  NU9
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake  Rais Filipe Jacinto Nyusi na ujumbe wake katika mazungumzo rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo
  NU10
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe na Waziri wa Masuala ya Ndani wa Msumbiji wakitiliana saini mkataba wa makubaliano mbele ye marais  Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake  Rais Filipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji.
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ambaye ni Mwanamitindo na Mbunifu Mavazi maarufu nchini Tanzania,  kwa sasa akifanyia kazi zake nchini Marekani, akizungumza wakati wa semina ya siku moja, iliyowaleta pamoja, wanamitindo "kinda" wa Tanzania, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Jumapili Mei 17, 2015. 

  Semina hiyo ililenga kuwafunza na kubadilishana uzoefu juu ya tasnia hiyo inayokuwa kwa kasi. Semina hiyo ya siku moja, ilitayarishwa kwa pamoja na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na mwanamitindo huyo nguli. Katika maelezo yake, Flaviana,  alisema yeye binafsi ni mwanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa hiari yaani "PSPF Supplementary Scheme-kwa kifupi PSS", na kuwataka wanamitindo waliohudhuria semina hiyo, kufuata nyayo zake. 

  Aliwaeleza umuhimu wa wanamitindo hao ambao wengi ni vijana, kujiunga na mpango huo kwa faida yao ya sasa na baadaye, kwani yeye anafaidika sana kuwa mwanachama wa Mfuko huo. Baada ya maelezo hayo yaliyofuatiwa na balozi mwingine wa Mfuko huo, Msanii maarufu wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, naye aliwapa "doze" wanamitindo hao juu ya ukuhimu wa wao kuchangamkia fursa mapema kwani ndio mtindo wa kisasa. 

  Hali kadhalika afisa masoko wa Mfuko huo Magira Werema, aliwahakikishia wanamitindo hao kuwa Mfuko huo ni Mfuko bora na wala hawatajuta waingiapo kuwa wanachama. Baada ya hotuba hizo, wanamitindo hao walizichangamkia fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko huo amba;po karibu washiriki wote zaidi ya 100 walijiunga na Mfuko huo.
  Wanamitindo wakiwa kwenye foleni ya kupiga picha tayari kujipatia vitambulisho baada ya kukamilisha zoezi la kujaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS wa Mfuko huo.
  Wanamitindo wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS.
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Magira Werema, akitoa maelezo ya kina kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na Mfuko huo.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akizungumza jambo na wenzake, Magira Werema, (kushoto), na Colleta Mnyamani, ambaye ni Afisa Uhusiano wa Mfuko huo.
  Flaviana (kulia) na Zuli Remtula,(katikati),  mwanamitindo mwingine nguli nzhini,na washiriki wengine wa semina hiyo, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Afisa wa PSPF, Magira Werema.


  0 0

  Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho (wapili kushoto) akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM), Profesa Idris Kikula (Kulia) ikiwa ni sehemu ya mchango wa benki hiyo katika mfuko maalum wa chuo hicho maarufu kama Endowment Fund, wakati wa hafla fupi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Akishuhudia ni Meneja Msaidizi wa Masoko wa Benki hiyo, Bi Anita Goshashy 

  BENKI ya Exim Tanzania imechangia fedha kiasi cha shilingi mil. 10/- kwenye mfuko maalumu  wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) maarufu kama “UDOM Endowment Fund”  ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo kusaidia sekta ya elimu nchini.

  Mfuko huo ulianzishwa na chuo hicho hivi karibuni kikilenga kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia baadhi ya mahitaji muhimu ya chuo sambamba na uwekezeaji  katika fursa za kitaaluma hususani kwenye masuala ya tafiti za kisayansi.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki mara tu baada ya kupokea hundi ya kiasi hicho cha pesa,Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof Idris Kikula alisema kwa sasa pesa yote inayopatikana inahifadhiwa kwenye akaunti maalumu ya uanzishwaji wa mfuko huo.

  “Hadi kufikia sasa tumefanikiwa kupokea takribani milioni 500/-ikiwa ni pesa taslimu pamoja na ahadi kutoka kwa wachangiaji  mbalimbali.Tukishakamilisha mipango yote kuhusu aina za uwekezaji ndipo tutajua kila uwekezaji utatengewa kiasi gani japo kwa kiasi kikubwa pesa nyingi itaelekezwa kwenye miradi ya tafiti,’’ alisema.

  Katika kuthibitisha kuwa uwekezaji kwenye tafiti za kisayansi  unaweza kuwa na tija zaidi Prof Kikula alitolea mfano mafanikio ya hivi karibuni waliyoyapata baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho ambao wameweza kubuni program maalumu inayoweza kuendesha zoezi za chaguzi mbalimbali.

  “Kwa sasa programu hiyo bado inaendelea kufanyiwa majaribio na zaidi tunarajia kuitumia kwenye chaguzi zetu za wanafunzi pale pale chuo,’’ alisema Prof. Kikula huku akitoa wito kwa taasisi nyingine za fedha kuiga mfano wa benki ya Exim kwa kuchangia kwenye mfuko huo na maendeleo ya elimu kwa ujumla.

  Aidha, Prof. Kikula alibainisha kuwa chuo hicho kitakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa kitaendelea kuwajulisha wachangiaji wote wa mfuko huo kuhusiana na mwenendo mzima wa mfuko huo yakiwemo mafanikio yake.
  Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkuu wa Hazina wa benki  ya Exim Bw.  George Shumbusho  alisema benki yake iliamua kuunga mkono jitihada za chuo hicho ikiwa ni namna ya kuthibitisha umakini wake kwenye masuala yote yanayohusu sekta ya elimu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

  “Exim kamwe tusingeweza kuvumulia kuona kwamba kuna programu muhimu kama hii inaendelea ndani ya taifa letu bila kutuhusisha kwa namna yoyote ile,’’ alisema Bw. Shumbusho huku akiahidi kwa niaba ya benki hiyo kuendelea kuwezesha mfuko katika siku zijazo kulingana na matokeo na ufanisi wa mfuko.

  0 0

  New Picture (10)
  New Picture (11)
  Kiongozi wa kikundi cha vijana 40 cha Wajenzi Isoso, Wilayani Kishapu akisoma risala kwa Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya (wa pili kushoto walioketi) mara baada ya Meneja huyo kumaliza mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Bi. Jane Mutagurwa ambaye alimhakikishia ushiriki makini wa Halmashauri hiyo katika kuwasaidia vijana kazi, mtaji na maeneo endelevu ya kufanyia kazi yao ya kufytaua matofali yanayofungamana. Aliishukuru NHC kwa msaada wa mashine kwa Halmashauri hiyo ambazo zimewapa vijana ajira.
  New Picture (12)
  Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya na Meneja wa NHC Mkoa wa Shinyanga Bw. Ramadhani Macha (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Festo Kang’ombe mara baada ya kufanya mazungumzo naye ya kuhamasisha Halmashauri hiyo kutoa ushirikiano kwa vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC ya kuytatulia matofali yanayofungamana.
  New Picture (13)
  Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akiwa katika eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga maarufu kwa ajili ya vijana wa Juakali wanaotengeneza matofali ya kufinyanga na kuchoma, ambapo aliendesha zoezi la kukinyang’anya mashine iliyotolewa na NHC kama msaada kikundi cha vijana cha Amanias katika Manispaa hiyo baada ya kugundua kuwa kikundi hicho kimeacha kutumia mashine hiyo na kujiunga na kazi za juakali za kutengeneza matofali ya udongo wa kufinyanga.
  New Picture (14)
  Wakufunzi wa VETA Shinyanga wakiwa eneo la Kata ya Usanda wakimueleza Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya namna wanavyoshiriki kurekebisha hitilafu ndogondogo zinazojitokeza katika mashine za vijana za kufytatua matofali yanayofungamana alipokagua vikundi vya vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
  New Picture (15)
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Bi. Isabella Chilumba akiueleza ujumbe wa NHC na watendaji wake namna Halmashauri hiyo inavyoshiriki kikamilifu kuwawezesha vijana waliopewa msaada na NHC wa mashine ya kufyatulia. Halmashauri hiyo imewapa vijana mtaji, maeneo ya kufanyia kazi na kazi za kujenga maabara, kuta za shule mbalimbali na majengo mengine ikiwa ni sehemu ya kusaidia kikundi hicho chenye vijana 70 kuwa na ajira endelevu.
  New Picture (16)
  Kikundi cha vijana katika Halmashauri ya Ushetu kikijenga ukuta wa shule ya Sekondari Ukune iliyoko kilometa 70 kutoka Kahama kwa kutumia matofali yanayofungamana baada ya kupewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali hayo na NHC mwaka 2014.

  New Picture (17)
  Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akiwapa zawadi ya fedha za kuwaongezea hamasa vijana wa kikundi cha vijana wapatao 70 Wilayani Ushetu kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zao baada ya kukagua shughuli za maendeleo walizofanya kwa kutumia mashine za kufyatulia matofali yanayofungamana walizopewa na NHC ili kujiajiri.
  New Picture (18)
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bw. Patrick Kalangwa akitoa maelezo ya jinsi kikundi cha vijana waliyopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali na NHC kinavyosaidiwa na Halmashauri hiyo. Hata hivyo, alikiri kuwa shughuli za migodi ya madini zinafanya baadhi ya vijana hao kuacha kutengeneza matofali na kujihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini.
  New Picture (19)
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kahama Mji Bw. Michael Nzengula akitoa maelezo kwa viongozi wa NHC waliomtembelea Ofisini kwake kufahamu namna Halmashauri hiyo inavyoshiriki katika kusaidia vijana wanaotengeneza matofali ya kufungamana kwa kutumia msaada wa mashine walizopewa na NHC.
  New Picture (20)
  Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora Bw. Erasto France Chilambo akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bw. Florence Mwale ya nia ya NHC ya kuinyang’anya Halmashauri hiyo mashine za kufyatulia matofali walizopewa na NHC baada ya Halmashauri hiyo kutosimamia kikamilifu vijana.
  New Picture (21)
  Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kaliua Bw. Mabula Isambula akieleza ujumbe wa NHC namna Halmashauri hiyo mpya inavyowawezesha vijana mitaji na maeneo ya kufanyia kazi za kufytaua matofali yanayofungamana kwa kutumia mashine walizopewa na NHC ili kuwezesha vijana kujiajiri.
  New Picture (22)
  Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akizungumza na kikundi cha vijana Wilayani Kaliua waliopewa msaada wa mashine na NHC ili kujiajiri alipowatembelea kuwapa hamasa na kukagua shughuli zao.
  New Picture (23)
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bw. Gervas Magashi aklipokutana na ujumbe wa NHC na kuueleza mkakati wa Halmashauri hiyo wa kusaidia vijana waliyopewa mashine kutengeneza matofali yanayofungamna na NHC ili kujiajiri.
  New Picture (24)
  Ofisa Miliki wa NHC Bw. Rockussy Sanka na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Bw. Muungano Saguya wakikagua ubora wa matofali yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana cha Tujiajiri na Miti ni Mali Wilayani Nzega.
  New Picture (25)
  Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa akimpa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Iramba Bi. Halima Mpita hundi kwa ajili ya kusaidia vijana waliyopewa msaada na NHC wa mashine za kufyatulia matofali yanayofungamana
  New Picture (26)
  Meneja waHuduma kwa Jamii na Meneja wa Mkoa wa Singida wakiwa katika Halmashauri ya Ikungi kuhakiki shughuli za vijana za kutengeneza matofali yanayofungamana. Vijana hao wameshajenga jingo la Ofisi yo ya kuendeshea kazi zao.

older | 1 | .... | 528 | 529 | (Page 530) | 531 | 532 | .... | 1897 | newer