Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 521 | 522 | (Page 523) | 524 | 525 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Naibu waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa serikali ya Zanzibar katika mradi wa ujasiriamali, ndugu Ameir Ali Ameir, ambaye ndiye Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma, Zanzibar.
   Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma, Zanzibar.ndugu Ameir Ali Ameir akizungumza na waandishi wa habari.
   Mkurugenzi Mkuu wa ILO Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda Bwana Alexio Musindo akizungumza na waandishi wa habari.
  Naibu waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari.
     Baadhi ya wahudhuriaji wa kongamano la kuadhimisha Miaka mitano ya mradi wa Ujasiriamali uliokuwa unaendeshwa na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO). 
   Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza wakati wa kongamano
    Mshauri Mkuu wa Ufundi wa Mradi, Bwana Jealous Chirove, akielezea mafanikio ya mradi

  ILO Tanzania yaadhimisha miaka 5 ya kuwawezesha vijana Tanzania kupitia ujasiriamali. Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) leo limeadhimisha miaka 5 toka kuanzishwa kwa mfuko wa ujasiriamali wa vijana (YEF) kwa kuandaa kongamano katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.

  Mfuko wa Ujasiriamali kwa vijana ulizinduliwa mwaka 2010 ukilenga katika kutengeneza ajira kwa vijana kwa kupitia ukuzaji wa sekta binafsi pamoja na kuongeza ushindani kwenye uchumi wa Afrika.

  Mradi ulijikita katika kuwatengenezea vijana ajira nzuri, kukuza ujasiriamali na kuwatengenezea fursa vijana wa kiafrika kupitia elimu, kuwaongezea ujuzi na uwezeshaji wa mtaji. Kwa kupitia mradi huu wa Kuwezesha Ujasiriamali, Mfuko wa Ujasiriamali kwa vijana ulilenga kutengeneza maelfu ya ajira kwa vijana katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda.

  Msingi mkuu wa mradi ulikuwa kukuza utamaduni wa ujasiriamali miongoni mwa vijana, kuingiza elimu ya ujasiriamali katika mitaala, kuongeza uwingi wa mambo yanayowezekana katika ajira kwa vijana, kuwezesha taasisi za vijana kutekeleza mawazo mazuri ya ujasiriamali na kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa vijana walio nje ya shule.

  Toka mradi umeanzishwa, umewezesha zaidi ya vijana 30,000 ambao ni wajasiamarali wapya na waliopo kupitia utoaji wa elimu ya biashara, kusaidia uanzishwaji wa biashara zaidi ya 17,000 pamoja na utengenezaji wa zaidi ya ajira 40,000 kwa vijana, ambayo vyote kwa pamoja vimevuka malengo ya mradi yaliyoaninishwa mwanzo.


  Pamoja na hayo, mradi pia umewezesha:
  ·        Zaidi ya biashara 16,000 zimeanzishwa ikiwa ni matokeo ya elimu ya biashara
  ·        Zaidi ya kazi 30,000 zimetengenezwa
  ·        Zaidi ya vijana1,000,000 wamefikiwa kupitia vyombo vya habari (radio, magazeti) na majukwaa mengineyo.
  ·        Zaidi ya wajasiariamali 30 wa mfano wametangazwa
  ·        Zaidi ya wanafunzi 50,000 wamepata elimu ya ujasiriamali
  ·        Zaidi ya walimu 340 wa shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo wameendelezwa
  ·        Jumla ya tathmini 6 zimefanyika pamoja makongamano 3 ya kisera
  ·        Miradi 33 imefanyika na taasisi za vijana
  ·        Zaidi ya vijana 30,000 wamepata elimu ya biashara

  Akizungumza wakati wa kongamano, Mshauri Mkuu wa Ufundi wa Mradi, Bwana Jealous Chirove alisema tathmini yao kwenye mradi imeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50% ya vijana waliopata elimu ya biashara wameweza kuanzisha biashara ndani ya miezi 12 huku wastani kila biashara ikitengeneza ajira mbili.

  ‘Mradi umepata mafanikio makubwa kwani kwa Tanzania pekee zaidi ya biashara 10,000 zimetengenezwa ambazo zimepelekea zaidi ya nafasi za ajira 20,000 ambazo kwa hakika ni mchango mkubwa katika kupambana na tatizo la ajira hapa nchini’ alisema Chirove.

  Mafanikio mengine ya mradi ni uanzishwaji wa mradi wa Kazi Nje Nje ambao unawatumia wahitimu kutoka vyuoni kuwafikia vijana walio mtaani na ujumbe kuhusu ujasiriamali pamoja na uanzishwaji wa mashindano ya kuandika mradi wa biashara uliowafikia moja kwa moja zaidi ya vijana 70,000.

  Mgeni rasmi wa Kongamano hili ambalo limehudhuriwa na wadau mbalimbali ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga amepongeza mchango wa ILO na Mfuko wa Ujasiriamali kwa mradi wao huu.

  ‘Tatizo la ajira kwa vijana bado ni changamoto kubwa kwa nchi zinazoendelea na bara zima la Afrika kiujumla hasa kutokana na ongezeko kubwa la wahitimu kutoka katika vyuo mbaliumbali hapa nchini, hivyo tunaishukuru ILO na serikali ya Denmark kwa juhudi zao za kuisaidia serikali kumaliza tatizo hili’ alisema Mheshimiwa Mahanga.

  Mheshimiwa Mahanga alisema mpaka sasa ni asilimia 25 tu ya watu wanaoingia kwenye soko la ajira ndio wanaajiriwa kwa mwaka kwenye sekta binafsi.   


  0 0

  SAM_2438
  Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini  wa wanahisa wa Benki ya Crdb  unatarajia kufanyika kesho  jijini Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog) .

  SAM_2443
  Baadhi ya sehemu ya waandishi wa habari kutoka jijini Arusha
  SAM_2437
  Godwin Semunyo Meneja mahusiano Benki ya CRDB
  SAM_2432
  Bi.Tully Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na huduma kwa wateja akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika maandalizi ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya CRDB
  SAM_2450
  Kulia ni Katibu wa bodi ya CRDB John Baptist Rugambo,katikati ni Mkurugenzi wa Fedha Frederick Nshekanabo,Kushoto Tully Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na huduma kwa wateja.
   
  Na Pamela Mollel-Arusha.

  Kufuatia anguko la shilingi ya Tanzania dhidi ya dola  wafanyabiashara nchini wametakiwa kuona kuwa ni fursa ya wao kijiinua kiuchumi katika biashara zao ndani  na nje ya nchi na kuachana na propaganda za wanasiasa ambapo wanalalamikia anguko hilo.
   
  Ambapo hali hiyo imesababisha kupanda kwa bidhaa mbalimbali nchini hali inayotajwa kuongeza ugumu wa maisha ya wananchi sambamba na wafanyabiashara nchini ambao wananunua na kuagiza bizaa kutika nje ya nchi.
   
  Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei wakati akiongea na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini  wa wanahisa wa Benki ya Crdb  unatarajia kufanyika kesho  jijini Arusha katika kituo cha mikutano cha  Kimataifa AICC.
   
  Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa Banki hiyo imeweza kupata faida ya shilingi bilioni 95.6 sawa na asilimia 14 kwa mwaka 2014 ambapo limekuwa ni ongezeko kubwa zaidi kutokea ambapo faida  hiyo itawasaidia kuweza kupatia wanahisa hao gawio la shilingi 15 kwa kila hisa na idadi ya wanachama hao.
   
  Ambapo mizania imeongezeka kwa asilimia 17 katika lengo lao katika mwaka huu ingawa soko limekuwa gumu kutokana na mfumuko wa bei uliopo sasa.
   
  Dr,Kimei aliongeza kuwa kutakuwepo na ajenda mbalimbali katika mkutano huo mkuu ambapo moja ya ajenda ni kuangalia namna ya kukua zaidi na kuongeza mtaji wao na kuboresha mfumo mzima wa Tehama ili kuweza kukabiliana na wizi wa kupitia mtandao ili kuweza kuwahakikishia usalama wa pesa za wateja wao.
   
  Aidha Banki hiyo inamkakati wa kuongeza mtaji wao ambapo wanatarajia kuongeza zaidi ya billion 100 ili kuongeza aman za banki na mtaji wao ili kuboresha huduma hizo  na kukuza rasilimali za banki hiyo.
   
  Dr,Kimei aliongeza kuwa wanamkakati wa kupanua huduma zao katika nchi ya Burundi na nchi jirani ili kuweza kuwarahishishia wateja wao pindi wanapotoka na kutembelea nchi hiyo na kupata huduma ya miamala ya fedha.
   
  Banki hiyo hivi sasa wanamawakala zaidi ya 575 ya fahari huduma na wanamashine ya zaidi ya 375 za kutolea pesa katika mikoa yote nchini ili kuwarahisishia wateja wao kupata huduma za kibenki.

  SAM_2456
  Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei,kushoto ni Naibu Mkurugenzi mtendaji huduma mtambuka benki ya CRDB Bi.Esther Kitoka,kulia ni Naibu Mkurugenzi mtendaji uendeshaji na Huduma kwa wateja CRDB Bw.Saugata Bandyopadhyay
  SAM_2454
  Mwandishi kutoka TV1 Arusha Jane Edward akijaribu kuchukua taswira katika mkutano huo
  SAM_2447
  Kulia ni Ena Mwangama Meneja kitengo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu na Edwin Nchimbi Afisa masoko wakifatilia mkutano huo
  SAM_2458
  Kulia ni Meneja Usajili wa Hisa kuotaka Benki ya CRDB Emmanuel Ng'ui na Dorice Ngikari kutoka ofisi ya Katibu wakifatilia jambo
  SAM_2449
  SAM_2460
  Mwandishi wa habari kutoka Mwananchi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Arusha Media Mussa Juma akiuliza swali kwa Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei

  0 0

  Aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshu (MUWSA) mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa kauli ya kuwaaga baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Mtendaji mkuu  DAWASCO.
  Kauli ya Mhandisi Luhemeja ya kuwaaga wafanyakazi hao ilionekana kama mwiba na kuzua simanzi kuu kwa watumishi hao waliofanya kazi na mkurugenzi huyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi 10.
  Mhandisi Luhemeja akijaribu kuwapatia wafanyakazi hao Lugha nzuri angalau wasibaki na majonzi.
  Meneja Fedha wa MUWSA ,Joyce Msiru akizungumza jambo katika kikao hicho.
  Hali ya huzuni ndio ilitawala katika viunga vya ofisi za Mamlaka hiyo.

  Na Dixon Busagaga a Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDEKELEO

  (CHADEMA)

  RATIBA YA UCHUKUAJI FOMU, VIKAO VYA UCHUJAJI NA UTEUZI WA WAGOMBEA NDANI YA CHAMA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015.


  18/05 – 25/06/2015

  Kuchukua na kurejesha fomu za Udiwani Kata ambazo hatuna Madiwani.

  Makatibu Kata/Jimbo na Wilaya

  01/7 – 10/7/2015

  Kuchukua na kurejesha fomu Kata ambazo tuna Madiwani.

  Makatibu Kata/Jimbo na Wilaya.

  15/7 – 20/7/2015

  Uteuzi wa mwisho Wagombea Udiwani Kata pamoja na wale wa Viti maalum.

  Kamati Tendaji za Majimbo.
  18/5 – 25/6/2015

  Kuchukua na kurejesha fomu za Ubunge Majimbo ambayo hatuna Wabunge kwa sasa, pamoja na Fomu za Ubunge wa Viti Maalum.

  Makatibu wa Majimbo, Wilaya, Mikoa na Makao Makuu.

  6/7 – 10/7/2015

  Kuchukua na kurejesha fomu za Ubunge Majimbo ambayo tuna Wabunge kwa sasa.

  Makatibu wa Majimbo na Wilaya.

  20/7 – 25/7/2015

  Uteuzi wa awali wagombea Ubunge.

  Kamati Tendaji za Majimbo.

  20/7 – 25/7/2015

  Kuchukua na kurejesha Fomu za Mgombea Urais.

  Makao Makuu

  1/8 – 2/8/2015

  Uteuzi wa mwisho wa Wagombea Ubunge kufanyika.

  Kamati Kuu Taifa.

  3/8/2015

  Baraza Kuu Taifa

  Kamati Kuu

  4/8/2015

  Mkutano Mkuu Taifa

  Baraza Kuu


  0 0
 • 05/07/15--06:09: JIJI LA DAR LAJAA MAJI
 •  Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.

  MAFURIKO,Mafuriko,Mafuriko .! Jiji la Dar limejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha wengine kukosa makazi.

  Maeneo yaliyokumbwa kwa mafuriko ni Mnyamani (Ilala),Bonde la Mpunga (Kinondoni) ,Kigogo (Kinondoni),Mikocheni ( Kinondoni),Vingunguti (Ilala) Tabata Kisiwani (Ilala)na Kurasini (Temeke) na maeneo mengine ambayo hayajawahi kupata mafuriko yamefika.

  Mvua hizo zimeharibu miundombinu katika barabara ya Morogoro kwa kujaa maji na kufanya kutokuwepo kwa usafiri kuelekea katikati ya jiji la Dar es Salaam.

  Wilaya ya Kinondoni ndio inaongoza kwa maeneo mengi kukumbwa na mafuriko kutokana na watu kujenga katika mikondo ya maji na baadhi ya watu kujenga nyumba katika miundombinu ya maji mitalo ya  maji taka na  kufanya maeneo mengine kutapakaa maji na kuleta adha ya usafiri.

  Kwa Wilaya Ilala ni eneo moja ndilo limekuwa likisababisha mafuriko, ni kwa wale waliojenga karibu na bonde la mto Msimbazi  ndio wamekuwa waathirika wa mafuriko kila mwaka.

  Wananchi wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hawana msaada wowote huku mvua ikiendelea kunyesha kuanzia majira ya saa 10 jioni na kuamkia leo hadi katika muda huu mvua inatikisa.
  Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick amesema kuwa serikali msaada wake ni wale waliopata madhara kutokana na mvua hizo na sio kuwapa makazi na chakula kutokana na kukataa kuhama maeneo hayo na kuishia kuipeleka serikali mahakamani.

  Mkuu wa Mkoa amesema serikali ilitoa maeneo mbadala ya kwenda kujenga na kuishi kwa watu wa maeneo ambayo mara kwa mara wamekuwa wakipata mafuriko, walikataa na kuipeleka serikali mahakamani hivyo sasa haiwezi kuwasaidia.
  “Sasa sisi tufanye nini tutawaombea sala,lakini msaada kwetu ni wale waliopata madhara ya kiafya kwa ajili matibabu,Serikali ndio itafanya hivyo”amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema katika mvua zinazoendelea mtu mmoja amepoteza maisha kwa kuanguka katika mto ng’ombe uliyopo eneo la Mburahati jijini Dar es Salaam.

  Kamanda Kova amesema aliyepoteza maisha ni Shaban Idd (73) Mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam na mwili wake umeopolewa na kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.

  0 0

  WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda amewataka Watanzania wenye uwezo wa kifedha waangalie uwezekano wa kuanzisha viwanda hapa nchini badala ya kuendelea kuwa wachuuzi wa kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi na kuziuza hapa nchini.

  Ametoa wito huo jana jioni (Jumatano, Mei 6, 2015) baada ya kutembelea maonyesho ya biashara ya Syria yanayoendelea kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania pamoja na wafanyabiashara kadhaa, Waziri Mkuu Pinda alisema mtindo unaoendelea wa kuuza mazao ghafi nje ya nchi hauisaidii Tanzania kama nchi na badala yake unanemeesha viwanda na uchumi wa nchi zinazonunua mazao hayo.

  “Watazania lazima wajiulize hivi bidhaa zote wanazoagiza kutoka nje ya nchi haziwezi kabisa kuzalishwa hapa nchini ili kupunguza matumizi mkubwa ya fedha za kigeni, kukuza uchumi na kuongeza ajira?,” alihoji Waziri Mkuu.

  Alisema wakati umefika sasa wa Tanzania kufikiria kuanzisha mpango mahsusi wa kulinda viwanda vya ndani kwa kuweka vivutio vitakavyowashawishi wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuanzisha viwanda vitakavyotumia malighafi inayozalishwa hapa nchini hatua ambayo itawafanya wafanyabiashara wasiende nje kununua bidhaa ambazo zinaweza kuzalishwa hapa nchini.

  Mapema, Balozi wa Syria nchini, Mhe. Abdulmounem Annan alimweleza Waziri Mkuu kuwa nchi yake inavyo viwanda vya nguo za pamba zaidi ya 100 na pamba ghafi yote inayotumika kwenye viwanda hivyo inalimwa nchini humo.

  Balozi Anan alisema yuko tayari kuandaa utaratibu utakaowawezesha wafanyabiashara, wawekezaji na viongozi wa Serikali kwenda Syria ili kukutana na wenzao kwa lengo la kujifunza na kuwashawishi waje kuwekeza Tanzania kwenye viwanda vya nguo na vya kusindika vyakula.

  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  ALHAMISI, MEI 7, 2015.

  0 0

    Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza wakati wa kuzindua timu ya wataalam wa mazungumzo katika mikataba ya gesi na mafuta kutoka serikalini na mafunzo yao maalum yaliyofanyika katika hoteli ya Park Hyatt kisiwani Zanzibar jana. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Bi. Sheila Khama Mkurugenzi wa Kituo cha Rasilimali za Afrika katika Benki ya Maendeleo ya Afrika. 
   Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa katika uzinduzi wa timu hiyo ya wataalam wa mazungumzo katika mikataba ya gesi na mafuta ambao umeenda sambamba na mafunzo maalum ya siku mbili kisiwani Zanzibar. UONGOZI Institute ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Columbia (Taasisi ya Uwekezaji Endelevu) na Mradi wa Wanasheria Waandamizi wa Kimataifa ndio waandaji wakuu wa timu hiyo ya wataalam ambao watapitia mafunzo ya miezi sita katika masuala ya yatakayowanoa kupata mikataba bora ya mafuta na gesi asilia kwa manufaa bora ya nchi. 
   Taswira ya wageni waalikwa pamoja na washiriki wa mafunzo ya wataalam wa mazungumzo katika mikataba ya gesi na mafuta. Wataalam ishirini na tano waliochaguliwa kuingia katika timu ya mazungumzo wanatoka katika ofisi na taasisi mbali mbali kama Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, Wizara ya Kazi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, TANESCO, TPDC, Tume ya Mipango, STAMICO, Ofisi ya Waziri Mkuu, Benki Kuu, TRA, Wizara ya Viwanda na Biashara, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, TAMISEMI na NEMC.
  Mjadala wa mafuta na gesi ukiendelea.   Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania leo imezindua timu ya wataalam ambao wamechaguliwa kwa ajili ya kuwakilisha serikali katika mazungumzo ya mikataba ya gesi asilia na mafuta na kampuni za kimataifa ya gesi asilia na mafuta ili kuweza kuleta mikataba yenye manufaa makubwa kijamii na kiuchumi kwa ajili ya taifa la Tanzania na watu wake kwa ujumla. 

   Timu hii ya wataalam inajumuisha watu 25 wenye utaalam mbali mbali waliochukuliwa kutoka ofisi na taasisi tofauti za serikali ili kuhakikisha kwamba masuala katika uchumi endelevu wa gesi na mafuta yanatatuliwa ipasavyo. Wataalam hao wametoka katika ofisi na taasisi mbali mbali kama Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, Wizara ya Kazi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, TANESCO, TPDC, Tume ya Mipango, STAMICO, Ofisi ya Waziri Mkuu, Benki Kuu, TRA, Wizara ya Viwanda na Biashara, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, TAMISEMI na NEMC. 

  Akizindua timu hiyo ya wataalam wa mazungumzo ya mikataba ya gesi asilia na mafuta kutoka serikalini iliyoenda sambamba na mafunzo ya mazungumzo ya awali ya siku mbili iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) katika Hoteli ya Park Hyatt kisiwani Zanzibar, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alisema  kwamba mpango huo itawawezesha kuwapatia wataalam wa kufanya mazungumzo yenye ueledi na mafanikio kwa taifa. 

   “Ni matumaini yangu kwamba mafunzo haya yatawawezesha wahusika kuweza kupata ujuzi na umahiri wa kutosha kufanya mazungumzo yatakayoleta manufaa makubwa kwa ajili ya taifa letu sasa na kwa ajili ya vizazi vijavyo pia,” alisema. Balozi Sefue aliwashauri pia hii timu mpya ya wataalam .

  “kujitolea kujifunza, kuelewa, kufikiria kimkakati, kusimamia, kutafiti, kuchunguza na muhimu zaidi kufanya mazungumzo vizuri kwa niaba yetu wote, kwa ajili ya maslahi ya Tanzania kwa sasa na hata baadaye.” Balozi Sefue aliendelea, 

  “Kufanya mazungumzo ya mikataba ya mafuta na gesi asilia na kampuni za kimataifa ya mafuta ni changamoto kubwa kwa serikali za nchi zilizobarikiwa na rasilimali nyingi kutoka Afrika, changamoto ambayo lazima itatuliwe.” Balozi Sefue alisema kwamba kampuni hizi za kimataifa za mafuta zinauwezo mkubwa wa kuleta wataalam wao waliobobea katika fani za uhandisi, kiuchumi na kisheria kutoka duniani kote na wenye uzoefu wa muda mrefu sana. 
  Kwahiyo, changamoto ya kwanza kabisa ambayo serikali za Afrika inakumbana nayo ni hii ya kutokuwa na wataalam wenye uwezo wa kutosha ukilinganisha na kampuni za kimataifa ya mafuta na gesi asilia. 

   Aliongeza, “Tayari ugunduzi wa futi za ujazo trilioni 50 za gesi asilia zinaweza na inapaswa kuleta chachu ya kufanya mageuzi ya kiuchumi katika nchi yetu ili iweze kuwa nchi endelevu yenye kipato cha kati katika miaka ya hivi karibuni. Lakini ili hii ifanyike, tunapaswa kuiga yale mazuri, kutokurudia makosa ambayo nchi zingine wamekwisha yafanya huko nyuma na pia inatubidi tufanye mazungumzo mazuri ili kupata mikataba bora.” 

  Balozi Sefue aliwasihi timu hiyo ya wataalam kupitia na kuelewa jitihada za serikali zilizokwisha fanyika huko nyuma na zinazoendelea ili kuweza kupata muundo mzuri wa jinsi ya kusimamia vizuri sekta hii ya mafuta na gesi asilia. “Kwa mfano kuna mengi ambayo yamefanywa kama kutengeneza sera, mikakati na sheria, na zote hizi lazima zieleweke na zizingatiwe katika mafunzo yenu na mazungumzo mtakayokwenda kuyafanya,” alisema.
  Aliongeza, “Itabidi wataalam wetu wajiandae vizuri kwa ajili ya kufanya mazungumzo yenye ueledi mkubwa itakayo kuwa na malengo ya kuleta usawa katika pande zote mbili wa serikali na kampuni za kimataifa ya gesi asilia na mafuta.” 

  Kutokana na maelezo ya Katibu Mkuu Kiongozi kuna umuhimu wa kufanya mipango kwa ajili ya kufikia aina ya taifa tunayoitaka. Kama hatutakuwa na maamuzi ya kimkakati na ambayo yatafanywa katika hatua hizi za awali, kutakuwa na hatari ya kutokea kwa matabaka ya kiuchumi na kijamii na mwishowe kuzaa laana ya rasilimali. 

   “Lazima tuepukane na laana ya rasilimali ambazo nchi zingine zimesha tumbukiza humo. Serikali ya Tanzania imedhamiria kwamba uwepo wa gesi asilia lazima iwezeshe mageuzi ya kijamii na kichumi kwa ajili ya kuifanya nchi yetu kuwa ya kipato cha kati na ukuaji endelevu na mpana kwa manufaa ya wengi na maendeleo ya watu wote kama ilivyoainishwa katika dira ya maendeleo ya Tanzania ya 2025.”

  0 0

   The Chairman of the UN High Level Panel on The Global Response to Health Crisis President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete leads a discussion during a panel retreat held at New York’s Long Island this morning. Other panel members in the picture from second left are Marty Natalegawa from Indonesia, Rajiv Shah from USA, a member of the UN  secretariat, Micheline Calmy Rey from Switzerland, and Celso Amorin from Brazil. 

  The panel appointed by the UN Secretary General Ban ki Moon has been charged with the responsibility to come up with recommendations aimed at strengthening national and international systems to prevent and manage future health crises taking into account lessons learnt from the response to the outbreak of Ebola Virus disease(Photo by Freddy Maro)

  0 0


   Pichani ni mtungo wa foleni ya magari mtaa wa Chimala almaarufu eneo la Ocean Road,jioni ya leo jijini Dar.  0 0
 • 05/08/15--05:23: Happy Birthday MO
 • DSC01228-Edit

  MODEWJI BLOG TEAM:Thanking you for being a great boss just isn't enough for your special day! Thank you for inspiring us to be our best! Happy birthday, boss! 

  And below is a small gift from us!
  IMG_9643 
  Please join us to wish him a Happy Birthday by follow him on his twitter@moodewjiand instagram@moodewji

  0 0

  DSC_0080
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo kabla ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome na Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi. Waliosimama wakishuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Joel Nanauka wa UNESCO, Afisa tawala msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem, Afisa mipango wa utamaduni wa UNESCO, Rehema Sudi, Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing, Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja na Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha.
  DSC_0084
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome wakitiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China. Wanaoshuhudia tukio hilo waliosimama ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. LU Youqing (wa pili kushoto), Ofisa anayeshughulikia masuala ya elimu kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar (wa pili kulia), Afisa mipango wa utamaduni wa UNESCO, Rehema Sudi (kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha na Kulia aliyeketi ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
  DSC_0086
  Zoezi la kusaini mkataba likiendelea.
  DSC_0089
  Wakifurahi kwa pamoja mara baada ya zoezi la kutia saini kukamilika.
  DSC_0090
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome wakibadilishana hati za mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. LU Youqing(wa pili kushoto) pamoja na Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia).
  DSC_0091
  DSC_0103
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo baada ya kutiliana saini mkataba huo.

  DSC_0068
  Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia) akizungumza jambo na Afisa wa ubalozi wa China (katikati) na Kushoto ni Afisa Utawala msaidizi wa UNESCO, Rahma Islem.
  DSC_0023
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (wa pili kulia), Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia), Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja na mkalimani wa Balozi wa China wakifurahi jambo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani) akiwasili kwenye chumba cha mikutano Wizara ya Elimu kwa ajili ya hafla fupi ya kutiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

  Na Modewji blog team.
  SERIKALI na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jana wametiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini.

  Akizungumza baada ya kutiwa saini kwa mkataba huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema mradi huo ni mkombozi mkubwa katika maandalizi ya kufundisha kwa kutumia Tehama nchini.

  Alisema mpango huo wenye kuwezesha walimu kujifunza Tehama unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China ambao ndio wamepitisha fedha zao UNESCO.Katika utiaji saini huo ambapo Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing alikuwepo, katika jumla ya uhai wa mradi ambao ni miaka miwili , miundombinu ya ufundishaji masomo ya sayansi na hesabu katika vyuo vya walimu vya Monduli na Tabora itaboreshwa.
  Katika mradi huo walimu watafundishwa elimu ya Tehama, namna ya kufundisha na kujifunza.

  Katibu mkuu Mchome alisema kwamba vyuo hivyo viwili vitawezeshwa kuwa na mtandao ambao utaunganishwa na vyuo vingine vinane vya masomo ya sayansi na hesabu kwa ajili ya kubadilishana taaluma. Pia vyuo hivyo vitawezeshwa kuandaa programu zenye kuelezea mfumo wa utoaji huduma za Tehama kwa ajili ya walimu wa masomo ya sayansi na hesabu.
  DSC_0037
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akisalimina kwa furaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (kulia) na kushoto ni Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (aliyeipa mgongo kamera).

  Profesa Mchome alisema ili taifa liweze kusonga mbele katika mpango wake wa kufundisha kwa kutumia Tehama ni vyema kuandaa walimu na fedha za China kupitia Unesco zitasaidia maandalizi hayo. “Tunaamini tukiwekeza katika vifaa vya kupromoti Tehama, walimu wakifundishwa na kuandaliwa vyema, wataenda kusaidia kufundisha na kuwezesha matumizi ya Tehama katika shule zao.” Alisema Profesa Mchome.

  Alisema japo zipo program ndogo nyingine , program waliyotia saini jana ilikuwa kubwa na yenye tija itakayoimarisha ubora wa elimu kwa kuwapa wanafunzi elimu ya kujitegemea, elimu yenye kuwakwamua kiujuzi na kuutumia ujuzi huo kwa maendeleo yao na taifa.
  Tanzania ni miongoni mwa mataifa barani Afrika ambayo mapema wametambua thamani ya kufundisha kwa njia ya Tehama ili kuboresha elimu na mfumo wa elimu.

  Taasisi zitakazohusika na mradi huo ni pamoja na Chuo Kikuu Huria (OUT) na Taasisi ya Elimu nchini(TIE) kwa kuratibiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
  DSC_0074
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) pamoja na Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (kushoto) kabla ya kutiliana saini mkataba huo.

  0 0

  Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari za mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jiji. Mvua hizo zinazonyesha kwa siku tatu mfululizo zimesababisha vifo vya watanzania hawa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam kama ifuatavyo:

  1.    Mnamo tarehe 06/05/2015 majira ya saa moja kamili usiku huko maeneo ya Magomeni Kinondoni jijini Dar es Salaam mtu mmoja jina SHABAN S/O IDD, Miaka 73, Mkazi wa Manzese alisombwa na maji ya mto ng’ombe alipokuwa akijaribu kuvuka mto huo. Mwili wake ulipatikana siku iliyofuata 07/05/2015 akiwatayari amekwishafariki dunia na umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.

  2.    Kifo kingine kilitokea tarehe 07/05/2015majira ya  saa sita kamili mchana huko maeneo ya Mwananyamala Mbuyuni Kata ya Mwananyamala, OysterBay, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo mtu mmoja aitwaye MASUMBUKO S/O DOUGLASS @ LIMAMU, Miaka kati ya 50-55, mkazi wa Mwananyamala Mbuyuni, alianguka na kufariki dunia ghafla wakati anatoa maji yaliyoingia nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa hivyo wakati akihangaika kutoa maji, ugonjwa huo ulimpata na kuanguka kwenye maji na kufariki dunia baada ya kukosa msaada wa haraka. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.


  0 0

  Ratiba Ya Mkutano Wa 20 

  0 0

   Mkurugezi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa AICCjijini Arusha leo. 
   Mwrnyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza wakati wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB.
   Mwanahisa akiuliza swali.


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akitoa maelezo wakati wa kumpatia zawadi za kimila, Shuka ya rubega, mkuki na ngao, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (kulia), wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu kwenye kampuni hiyo, na wengine 10 walizawadiwa kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera mpya ya Acacia ya tabia sita (six desired behavior), kama kipimo cha utendaji bora wa kazi ambapo ni pamoja na kushirikiana na kufanya kazi kwa uwazi, kutambua ubora wa mfanyakazi na kumuwajibisha anapokengeuka, kupanga kazi na kutenda, kufanya kile ulichopanga kufanya, kufanya kazi kwa wepesi, na kujiendeleza ili kuwa bora katika utendaji wa kazi wa kila siku. 

  Katika hotuba yake, Mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa mgeni rasmi, kwenye sherehe hiyo ambayo ilikuwa maalum kuwatunuku wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, na kufanyika Alhamisi usiku wa kuamkia leo Ijumaa Mei 8, 2015, aliwamwagia sifa wafanyakazi wa mgodi huo hususan uongozi mpya chini yaa Brad, kwa kuja na sera mpya ambayo sio tu inawajali wafanyakazi bali pia wananchi wanaozunguka mgodi huo ikiwemo serikali.
  Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia udthabiti wa kampuni hiyo, (GM-Organizational Effectiveness), Janet Reuben-Lekashingo, (kulia), akimkabidhi cheti Isack John Nkulu, kwa utumishi wa muda mrefu kwenye kampuni hiyo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Mwenyekiti wa Proin Group Tanzania ndugu Johnson Lukaza akizungumza machache na kuwashukuru watu wote waliohudhuria uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania kupitia mtandao (online) hapo jana katika ukumbi wa ACP House jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali.Uzinduzi huo ulifanywa na balozi wa Tanzania Mheshimiwa Diodorus Kamala.


  0 0

  Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha mafuriko yaliyong'oa miti na kuharibu kingo za daraja la Kikuletwa wilayani Hai.
  Mti mkubwa ulizolewa na maji na kisha kugota katika daraja la Kikuletwa.
  Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Kikuletwa wakivuka katika daraja hilo.
  Baadhi ya vijana wakiangalia namna ambayo wataweza kuondoa miti hiyo.
  Mawe pia katika barabara inayounganishwa na daraja hilo yamezolewa na maji.
  Mwenyekiti wa Kijiji cha Chmka Jacob Idd akipita katika daraja hilo kujionea athari za mafuriko hayo.
  Baadhi ya wananchi wakitizama eneo ambalo ulikuwepo mti ulisombwa na maji
  Miundo mbinu ya maji ya mradi wa Losaa Kia ambao ulikuwa unapeleka maji katika kijiji hicho ikiwa imechukuliwa na maji pia.
  Waanchi katika kijiji hicho wakijadili ni cha kufanya.
  Wakazi wa maene hayo bado wameendelea kupita katika daraja hilo kwa mashaka.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini 

  0 0

    Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Gwesigabo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kupanda kwa mfumuko wa bei wa huduma na bidhaa. Kushoto ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei, Luth Minja.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

  Na Dotto Mwaibale

  OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.3 kwa Machi mwaka huu ambapo umeongezeka kwa asilimia 0.8 kutoka asilimia 0.7 Machi,2015.

  Ongezeko hilo limechangiwa na kasi ya upandaji bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia Aprili, 2015 kuongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo ya Machi, 2014.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo alisema farihisi za bei zimeongezeka hadi 157.21 Aprili,
  mwaka huu kutoka 150.50 Aprili mwaka jana.

  "Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa Machi mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 7.1 kutoka asilimia 5.9 Machi mwaka jana, hii imetokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kinachoishia Aprili, 2015," alisema.

  Alisema bei za vyakula kama mchele umepanda kwa asilimia 23.3, unga wa mihogo kwa asilimia 8.4, nyama kwa asilimia 4.9, samaki kwa asilimia 5.8 ambapo maharage yamepanda kwa asilimia 6.8 na sukari kwa asilimia 5.6.

  Kwegisabo aliongeza kuwa mfumuko huo kwa Aprili, 2015 umeongezeka kwa asilimia 0.8 ukilinganisha na asilimia 0.7 Machi, 2015 ambapo farihisi za bei zimeongezeka hadi 157.21 Aprili, 2015 kutoka 155.88 Machi, 2015.

  "Vyakula vilivyochangia kuongezeka kwa farihisi za bei ni pamoja na mchele kwa asilimia 5.8, mahindi kwa asilimia 6.3, unga wa mahindi kwa asilimia 5.0, samaki waliokaushwa kwa asilimia 3.1, ambapo maharage kwa asilimia 2.9, na viazi mviringo kwa asilimia 7.0, mihogo kwa asilimia 6.4 pia viazi mviringo kwa asilimia 4.0," alisema Kwesigabo.

  Aidha uwezo wa shilingi 100 kununua bidhaa na huduma imefikia shilingi 63 na senti 61 Aprili, 2015 kutoka Septemba, 2010 ikilinganishwa na shilingi 64 na senti 15 Machi, 2015.

   Alisema mfumuko huo unamwelekeo unaofanana na nchi za Afrika Mashariki ambapo Uganda umeongezeka kwa asilimia 3.60 kutoka asilimia 1.90 Machi, 2015, Kenya umepanda kwa asilimia 7.08 Aprili, 2015 kutoka 6.31 Machi, 2015.  
   (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

  0 0

   Mwananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu ambacho ni maarufu kwa ulimaji wa zao la Shayiri akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin mara baada ya kukabidhi Kituo  cha Afya cha Kijiji hicho vifaa mbalimbali vya matibabu.
   Maofisa wa TBL wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo wilayani Karatu, katikati ni Afisa Uhusiano Dorris Malulu, kushoto kwake ni Mkurugenzi Jarrin na kulia kwake ni Meneja mradi wa Kilimo cha Shayiri Dk. Basson

   Mkurugenzi wa Kiwanda cha TBL Robert Jarrin akiwa anangalia baadhi ya vifaa na Mganga wa Hospitali ya wi;aya ya Karatu Dk. Lucas wakati wa makabidhiano ya vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba Kata ya Mbulumbulu.
   Mwenyekiti wa Kijiji cha Kambi ya Simba Damian Anatholi akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya Kituo cha Afya cha Kijiji hicho ambacho ni maarufu sana kwa kilimo cha Shayiri.


   Mwenyekiti wa Kijiji cha Kambi ya Simba Damian Anatholi akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrinwakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya Kituo cha Afya cha Kijiji hicho ambacho ni maarufu sana kwa kilimo cha Shayiri.

   Mganga wa Mfawidhi wa wilaya ya Karatu Dk. Lucas akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya hospitali kwa ajili ya kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani Arusha.

   Mkurugenzi wa TBL Robert Jarrin akiwa pamoja na Meneja Mradi wa Kilimo cha Shayiri Dk. Basson wakitembelea jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Simba kilichopo Kata ya mBULUMBULU wilayani Karatu wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali kwenye kituo hicho.
  Mganga wa wilaya ya Karatu Dk. Lucas akibadilishana na mawazo pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali kwa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani Arusha.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin akipokea zawadi ya fimbo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kijiji wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu ivi karibu, ambapo Kiwanda hicho kilikabdhi vifaa vyenye thamani ya Sh. Milioni 22.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin akikabidhi baadhi ya vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba wilayani Karatu mkoani Arusha kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji hicho, ambapo Kampuni hiyo ya Bia ilitoa vifaa vyenye thamani ya Sh.Milioni 22.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin Robert Jarrin akipokea zawadi ya fimbo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kijiji wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu ivi karibu, ambapo Kiwanda hicho kilikabdhi vifaa vyenye thamani ya Sh. Milioni 22.
   Afisa Uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na baadhi ya viongozi Serikali ya Kijiji pamoja na uongozi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya kituo hicho vyenye thamani ya Sh. Milioni 22, Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin na kushoto kwake ni Meneja Mradi Kilimo cha Shayir Dk. Basson Bennie.

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid (wapili kulia), akipiga makofi mara baada ya kuzindua mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini, ambapo vituo vya Afya 13 vinanufaika na mradi huo.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid, akizindua mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini, ambapo vituo vya Afya 13 vinanufaika na mradi huo.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid (wapili kulia), akiwa na baadhi ya watendaji wa Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini wakishudia uzinduzi wa mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na shirika hilo katika vituo vya Afya 13.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid (katikati), akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya kuzindua mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini, ambapo vituo vya Afya 13 vinanufaika na mradi huo.

older | 1 | .... | 521 | 522 | (Page 523) | 524 | 525 | .... | 1897 | newer