Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

TAHADHALI: HALI YA MVUA ZA MASIKA KATIKA MAENEO YA UKANDA WA PWANI


TAARIFA ZA UWEPO WA TSUNAMI SI ZA KWELI-MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

JUMUIYA YA VIJANA WASIO NA AJIRA YAZINDULIWA ZANZIBAR

$
0
0
 Mratibu wa Jumuiya ya Vijana wasio na ajira Tanzania Nd. Ussi Said Suleiman akitoa maelezo kwa Baadhi ya Vijana wasio na ajira waliohudhuria katika Mkutano wa kuitambulisha Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Water front Hall Rahaleo Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Vijana waliohudhuria katika Mkutano wa kuitambulisha Jumuiya mpya ya Vijana wasio na ajira Tanzania, wakimsikiliza Mratibu wa Jumuiya hiyo Nd. Ussi Said Suleiman (hayupo pichani). 
Mmoja wa Vijana wasio na ajira Zaituni Haji Mdigo  akiuliza swali katika Mkutano huo.  
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

KONGAMANO LA WAANDISHI NA MVIWATA

$
0
0
Mwenyekiti wa Mviwata Veronika Sophu akizungumza na waandishi wa habari wanaoandika habari za wakulima (kulia) ni Mkurugenzi wa Mviwata Stephen Ruvuga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mviwata Usi Haji Usi.
Pichani ni waandishi wa habari kutoa mikoa mbalimbali nchini wanaoandika habari za wakulima wakifuatia kongamano la waandishi wa habari marafiki wa wakulima lililowashirikisha waandishi mbalimbali kutoka vyombo na mikoa tofauti, lililofanyika mjini Morogoro na kuandaliwa na Mviwata.

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuwapa kipaumbele wakulima wadogo kwa kuandika habari zao kiundani kuliko kuegemea kwa wanasiasa peke yao.

Mwenyekiti wa Mtandao wa vikundi vya wakulima nchini (Mviwata), Veronica Sophu aliyasema hayo jana mjini Morogoro kwenye kongamano la waandishi wa habari wanaoandika habariza wakulima.

Sophu ambaye alikuwa mjumbe wa Bunge maalum la Katiba (BMK) kupitia kundi la wakulima  alisema wakulima nchini wanatakiwa wasikilizwe kwani wana changamoto nyingi zinazowakabili.

“Kuna changamoto ndogo kati ya waandishi wa habari na wakulima kwani vyombo vingi vya habari vimekuwa vinaegemea kwa wanasiasa na kutuacha wakulima bila kuwa na mahali pa kusemea,” alisema Sophu.

Alisema mara nyingi habari za wakulima wadogo hazipewi kipaumbele zaidi ya migogoro kati yao na wafugaji hivyo waandishi wa habari wabadilike kwa kuwatazama na wao.

“Asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima wadogo kwani kila kwenye watu 10 kati yao nane ni wakulima hivyo wapewe kipaumbele kwani bila mkulima mdogo hatuwezi kupata chakula nchini,” alisema Sophu.

Naye, Mkurugenzi mtendaji wa Mviwata Stephen Ruvuga alisema mchango wa waandishi wa habari nchini kwa upande wa wakulima mdogo ni wa muhimu hivyo uzingatiwe.

Ruvuga alisema wakulima wadogo wanatakiwa kuungwa mkono na waandishi wa habari kwa kusemewa kwa namna nzuri zaidi kuliko kuripoti tuu habari hizo bila kuingia kwa undani.

“Wakulima wadogo wana nafasi kubwa katika kuchangia uchumi wa Taifa na jamii kwa ujumla hivyo waandishi wa habari msiangalie tabaka la juu pekee na kuacha kutoa habari za wakulima,” alisema Ruvuga.

Mamilioni ya Kopa Bayport yazidi kupata wenyewe

$
0
0
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushaoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania. Picha zote na Mpiga Picha wetu.


======  ======  =========
SHINDANO la Kopa Bayport kwa njia ya mtandao linaloendeshwa na taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, limezidi kuchanja mbuga, baada ya wateja watatu wa mwezi Mei kuibuka na Sh Milioni moja kwa kila mmoja, huku mikoa ya Bukoba, Njombe na Dar es Salaam ikichanua katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam.

Wateja hao walioshinda katika shindano hilo ni Tryphone Mashamba mkoani (Njombe), Kisa Mboya (Dar es Salaam) na Oscar Gadawu (Bukoba) ambao wote kwa pamoja wameibuka na Sh Milioni moja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ikiwa ni huduma nzuri kutoka kwenye taasisi hiyo ya Bayport Financial Services.
Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Gladys John katikati akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa shindano la Kopa Bayport linaloendelea ambapo washindi watatu wamepatikana na kila mmoja kupata bahati ya kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, wakati kushoto ni Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema shindano lao limepokewa vizuri na wateja wao, waliopata urahisi wa upatikanaji wa huduma za mikopo kutoka kwenye taasisi hiyo. 
Tunatafuta washindi wa kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja kwa washindi watatu kutoka Bayport Financial Services. Ndivyo wanavyoonekana kusema katika droo hiyo ambapo washindi kutoka Njombe, Dar es Salaam na Bukoba wamechanua.


Alisema awali wateja walilazimika kusafiri kuelekea kwenye tawi lao, lakini kuanzishwa kwa tovuti hiyo, kumetoa urahisi wa ukopaji kwa kiasi kikubwa mno, huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kushinda endapo ataamua kutumia huduma hiyo.

“Tunashukuru kuona Watanzania wenzetu wameendelea kupata urahisi wa huduma zetu za mikopo, maana anaweza kukopa mahala popote alipokuwapo, endapo ana kifaa kitachomuwezesha kuingia katika mtandao wetu wa www.kopabayport.co.tz, kama vile simu ya mkononi na kompyuta” alisema Cheyo.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania.


Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein, alisema promosheni hiyo ya kopabayport ni nzuri kwa wateja na Watanzania wote wanaoweza kujikwamua kwa kupata mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana kutoka Bayport.

“Sisi Bodi tunachoangalia ni kanuni na vigezo vya michezo ya kubahatisha kufuatwa, ikiwa ni upatikanaji wa washindi na namna walivyoweza kujiunga kwenye huduma hii ambayo kila mtu anaweza kuingia anapohitaji huduma yoyote,” alisema Abdulhussein.

Naye Meneja Huduma kwa Watejanwa Bayport Financial Services, Gladys John, aliwataka Watanzania kuendelea kuiunga mkono Bayport kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa mbalimbali za mikopo isiyokuwa na amana wala dhamana, bila kusahau Kopa Bayport inayoendelea kutolewa kwa ajili ya kuwapongeza wanaomua kutumia huduma hiyo nzuri.
Wateja hao watatu waliojinyakulia sh Milioni moja kila mmoja, wanaungana na Hyasint Mbunda Songea, Phaustine Mbilinyi Dar es Salaam na Allen Bishubo Bukoba ambao walishinda katika droo ya mwezi wa nne, ambapo Bayport Financial Services, imeshawapatia fedha zao za ushindi.

NAFASI ZA MASOMO NA FURSA ZA AJIRA

$
0
0
       Wewe   ni  kijana  wa  kitanzania ?

·       Unapenda  kufanya  kazi  kama    MTAALAMU  WA  CHAKULA  NA  LISHE ?

Kama  jibu  ni  ndio, basi  hii  ni  habari  njema  sana  kwako.
 Chuo  cha  NEEMA  HERBALIST  COLLEGE,  kinatangaza  nafasi  za  kujiunga  na  kozi ya   CHAKULA  NA  LISHE  katika  ngazi  ya  cheti  cha  msingi     yaani   BASIC   CERTIFICATE  IN  FOODS  AND  NUTRITION.
 Kozi  hii  itakupa  sifa  na  uwezo  wa   kufanya  kazi  kama  MUANDAAJI  NA  MTAYARISHAJI  WA  VYAKULA-LISHE  MAALUMU  KWA  WAGONJWA,   NA  WENYE  KUSUMBULIWA  NA  MATATIZO  MBALIMBALI  YA  KIAFYA, kwenye     maeneo  mbalimbali  kama  vile:
1.   Hotelini  na  kwenye   migahawa mbalimbali.
2.   Vituo  mbalimbali  vya  afya.
3.  Kwenye  shule  za  chekechea, msingi  na  sekondari.
 4.     Kwenye  vituo  vya   kulelea  na  kutunza   watoto ( Day  Care Centres   )
 5.   Kwenye  Vituo  vya  kutunza  wazee  na  watu  wenye  mahitaji  maalumu ya  kiafya.
6.      MAJUMBANI  : Kuhudumia  wagonjwa  na  wenye  mahitaji maalumu  ya  kiafya  waliopo  majumbani.
7.   Pamoja  na   kwenye  maofisi  mbalimbali.

MWOMBAJI  awe  na  Elimu  ya  kuanzia  darasa la saba, kidato  cha  nne  na  kuendelea.

FOMU  ZA  KUJIUNGA 
Fomu  za  kujiunga  na  kozi  hii  zinapatikana  chuoni kwetu  kwa  gharama  ya  shilingi  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU 
( Tshs.15,000/= )
Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM, katika  eneo  la  UBUNGO nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na  KAGAME HOTEL.

Mwisho  wa  kuchukua  fomu  ni  tarehe    12   JUNI  2015  saa nane  kamili  mchana.

ADA  YA   MASOMO 
Ada  ya  masomo  haya  ni  rahisi, na  inalipwa  baada  ya  mhitimu  kuingia  kazini.

KWA WAOMBAJI  WA  MIKOANI:
Kwa  wanafunzi  kutoka  mikoani, Hosteli  zipo  kwa  wanawake  na  wanaume.
  Kwa  waliopo  nje  ya  Dar  Es  salaam,kupata  fomu ya  kujiunga  na  kozi  hii, andika    maombi  ya  fomu  ya kujiunga  na  kozi   hii,kupitia  barua  pepe yetu  ambayo  ni :

Kwa  maelezo  zaidi, wasiliana  nasi  kwa  simu   0765103080.
 Au   tembelea ;

BODI YA UTT-PID NA MENEJIMENTI YAKE YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO CHINA

$
0
0
kwana Bodi ya UTT-PID ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wakiwa na wenyeji wao katika jiji la Chengdu ambapo walifanya ziara katika maeneo tofauti ya uwekezaji na manufaa wanayopata wananchi wa jiji hilo. Ziara hiyo ya siku Tano katika Miji tofauti inatarajia kukamilika Tarehe kumi kabla ya kurejea nyumbani.

Na Mwandishi Maalum
Bodi ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID), pamoja na Menejimenti yake ipo nchini China katika ziara maalum ya Mafunzo na kujenga uzoefu ya siku tano ikiwa na lengo la kuimmalisha utendaji kaziw wa taasisi hiyo.

Katika ziara hiyo, Bodi ya UTT-PID, ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wapo katika miji mbalimbali na kutembelea maeneo tofauti ya uwekezaji ilikushuhudia manufaa wanayopata wananchi wa maeneo hayo.

Kazi za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
pili
Bodi ya UTT-PID pamoja na Menejimenti ikipata Maelezo kutoka wataalum wa uzalishaji nishati toka mji wa Chengdu.
saba
Pichani Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID wakiwa na wenyeji wao ndani ya ukumbi wa mikutano nchini China katika ziara hiyo ya siku 5.
sita
Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID wakiwa na wenyeji wao ndani ya ukumbi wa mikutano nchini China katika ziara hiyo ya siku 5.
tano
Mkutano ukiendelea baina ya Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID wakiwa na wenyeji wao ndani ya ukumbi wa mikutano nchini China katika ziara hiyo ya siku 5.
tatuBodi ya UTT-PID ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. Elpina Mlaki (wa pili kushoto) pamoja na Menejimenti wakiwa na wenyeji wao katika jiji la Chengdu ambapo walifanya ziara katika maeneo tofauti ya uwekezaji na manufaa wanayopata wananchi wa jiji hilo.
nne
Wajumbe wa Bodi ya UTT-PID, wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka Zipingpu Hydropower mwenyeji wao, jinsi gani uzalishaji unavyofanyika na usambazaji wa nguvu za nishati. Mjumbe wa Bodi Mrs. J Mmari (kulia), akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dr. Gration Kamugisha mwenye shati jeupe na kushoto ni Mwanasheria wa Taasisi hiyo, Bi. Tuzo Mpiluka.

Tanesco toeni vibali kwa mafundi umeme wa REA - Simbachawene

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) akitoa maelekezo kwa Afisa Uhusiano - Huduma kwa Wateja wa Shirika la  Umeme Nchini (Tanesco) mkoa wa Dodoma, Innocent Lupenza (kulia) mara baada ya kuwasili katika wilaya  ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi ya  umeme vijijini. Waziri Simbachawene yupo mkoani  Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) Awamu ya Pili na Tanesco pamoja na kuzungumza na wananchi. Katikati ni Katibu wa Waziri Simbachawene Mhandisi  Joseph Kumburu.

 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia chini) akiangalia mafundi kutoka Shirika la  Umeme Nchini (Tanesco) waliokuwa wakiendelea na kazi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika Kata ya Mulunduzi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

 Diwani wa Kata ya Mulunduzi Hitler Chambilu akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata hiyo kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (hayupo pichani) ili aweze kuzungumza na wananchi wa kata hiyo (hawapo pichani)

 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akizungumza na sehemu ya  wakazi wa Kata  ya Mulunduzi pamoja na kusikiliza kero zao.

 Baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati, Sostenes Masolla (wa nne kutoka kulia) wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (hayupo pichani) katika kijiji cha Chinyanghuku wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Sehemu ya wakazi wa Kata ya Mulunduzi  wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (hayupo pichani).

 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akisalimiana na Diwani wa Kata ya Mulunduzi Hitler Chambilu (kushoto) mara baada ya kuwasili katika kata hiyo iliyopo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Chaludewa (hawapo pichani) mara alipotembelea katika kijiji hicho

 Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) akikabidhi mfano wa zawadi ya  jezi kwa mmoja wa wasanii wa kikundi cha sanaa kijulikanacho kama Neema Group, Ackley Mwaluka katika kijiji cha Chaludewa kilichopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Tanesco toeni  vibali kwa mafundi umeme wa REA - Simbachawene

Na Greyson Mwase, Dodoma.


Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameliagiza Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kutoa mafunzo  pamoja na  vibali kwa mafundi umeme nchini kote watakaofanya kazi ya kuweka mifumo ya umeme kwenye nyumba kabla ya kuunganishwa kwenye miundombinu  ya umeme inayojengwa na Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Tanesco.


Simbachawene alitoa  agizo  hilo katika ziara yake aliyoifanya katika wilaya  ya Mpwapwa mkoani Dodoma ya kukagua miradi ya umeme vijijini ili kujionea maendeleo yake, pamoja  na kuzungumza na wananchi. Miradi hiyo iliyopo chini ya Awamu ya Pili ya REA inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.


Alisema katika kujiandaa na huduma ya umeme, wananchi wa Mpwapwa wanatakiwa kuwekewa mifumo ya umeme (wiring) katika nyumba zao na wataalamu waliothibitishwa na Tanesco na kupewa leseni pamoja na mafunzo ili kuondokana na majanga ya moto yanayosababishwa na ufungaji holela wa mifumo ya umeme.


Alieleza kuwa katika utekelezaji wa miradi  ya REA kumekuwepo na mafundi wasiotambulika na Tanesco wanaojulikana kama vishoka ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye makazi ya watu na kudai kuwa ni mafundi kutoka Tanesco  na kuwawekea mifumo mibovu ya  umeme hali inayopelekea hasara kubwa ya kuunguliwa na nyumba baadaye.


Alisisitiza kuwa ili kukabiliana na mafundi ambao ni vishoka shirika la Tanesco linatakiwa kuchagua makampuni na mafundi binafsi ambao ni wataalamu wenye leseni na kutambuliwa na shirika hilo na kuwapa mafunzo  kabla ya kuanza zoezi la kuweka mifumo ya umeme kwenye nyumba za wananchi wanaotarajiwa kufungiwa umeme  chini ya mradi wa REA awamu ya pili. Aliongeza kuwa mara baada ya mafundi hao kupatiwa  mafunzo na Tanesco, watapewa barua maalum za utambulisho au hati maalum zitakazotumika wakati wa uendeshaji wa zoezi hilo.

Simbachawene alisema kuwa hatua hiyo inatokana na mikakati ya serikali katika kuwapunguzia wananchi  gharama na muda wa kufuatilia  huduma za kufungiwa mifumo ya umeme katika nyumba zao mijini.


Aliendelea kusema kuwa mbali na kuwapunguzia wananchi  gharama na muda wa ufuatiliaji wa kufungiwa mifumo  ya umeme katika nyumba zao, mpango huo utaleta ushindani wa gharama kati ya makampuni na mafundi  binafsi wenye leseni zinazotambuliwa na Tanesco.


Akielezea  hali ya  uunganishaji wa umeme nchini Simbachawene alisema mwaka 2005 wakati serikali  ya awamu ya nne inaingia madarakani, ni asilimia 10 tu ya wananchi walikuwa na umeme lakini hadi kufikia mwaka 2015 ni asilimia 36 ya  wananchi wana umeme na kusisitiza kuwa mara baada ya miaka mitano asilimia ya wananchi wenye umeme itakuwa ni 45 na kuifanya  Tanzania kuwa nchi  inayoongoza Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwaunganishia umeme wananchi  waishio  vijijini.


“ Hii ni  hatua kubwa ambayo tumepiga kama Serikali na bado tutaendelea kuhakikisha kuwa wananchi wote hasa waishio vijijini  wanapata umeme wa uhakika ingawa tutafanya kwa awamu tofauti tofauti,” alisema Simbachawene.

Simbachawene alifafanua kuwa ingawa sio  rahisi kuweka umeme katika vijiji  vyote kwa pamoja nchi nzima, miradi ya  REA itatekelezwa kwa awamu tofauti tofauti.

Simbachawene aliwataka wananchi kushirikiana na Tanesco pamoja na REA katika utekelezaji wa miradi ya  ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa kutoa sehemu ndogo ya mashamba yao ili ziweze kuwekwa nguzo za umeme ili waanze kunufaika na umeme huo mara moja.


Wakati huo huo Afisa Uhusiano - Huduma kwa Wateja wa Tanesco mkoa wa Dodoma Innocent Lupenza alisema kuwa kwa wananchi wenye  nyumba zenye  vyumba viwili hawatahitaji kufungiwa mifumo ya umeme, badala yake watawekewa kifaa maalumu kujulikanacho kwa jina la UMETA yaani Umeme  Tayari.


Akielezea kifaa hicho, Lupenza alisema kuwa kifaa hicho kitamwezesha mtumiaji kuwasha taa mbili pamoja na matumizi mengine madogo  kama pasi na kuongeza kuwa kifaa hicho kitauzwa kwa shilingi  42, 480.Akielezea taratibu za kufungiwa umeme kwenye nyumba Lupenza alisema wananchi waliopo  umbali wa mita 30  toka ilipo miundombinu ya umeme watalipia shilingi 27,000.

Alisema katika hatua za awali wananchi watatakiwa kulipia fomu  kwa shilingi 5900 na baada ya hapo mkandarasi atafanya ukaguzi wa mifumo ya umeme iliyowekwa katika nyumba husika kabla ya kuiunganisha  nyumba hiyo na miundombinu ya  umeme.


MTEMVU ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MVUA TEMEKE

$
0
0
 Mtemvu akiitembelea Nyumba ya Bi Mwashamba Mwandoro maeneo ya Kurasini,  baada ya ukuta wa Nyumba kuanguka kutokana na Mvua zinazo endelea kunyesha Dar es Salaam na hapo akiongea akiwa katika nyumba hiyo, katika msafara huo aliongozana na Meya na Naibu Meya wa Temeke ,na Diwani wa maeneo hayo.
 Maji ya Mvua yakiwa yamezingira Nyumba maeneo ya Wailesi Temeke
 Mjumbe wa Shina kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM)  Juma Salum  (wakwanza kishoto) akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo hilo mara alipofika kuwaona
 Mtaa mzima ukiwa umefurika maji maeneo ya Wailesi kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Abdon Kidege, akimwelekeza jambo Mbunge wa Jimbo hilo Abbas Mtemvu wakati wa ziara ya kutembelea na kuwaona wananchi waliopatwa na mafuriko ya Mvua zinazo endelea kunyesha.

 Magari yakipita kwa shida na eneo hilo linauterezi kitu ambacho ni hatari sana kwa wanao tumia njia hiyo.
 Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na wananchi walio patwa na mafuriko maeneo ya Wailesi alipo watembelea
 Madereva wa Magari ya Abiria yanayo fanya safari kati ya Tandika - Yombo Kilakala kupitia Daraja la Tazara na Tandika kwa Limboa wakishirikiana kujaza viroba vya mchanga na kuweka sehemu yamaeneo ya  Barabara hiyo ili waweze kupita kwa urahisi     
 Madereva hao wakiwa wanapakia mchanga kwa kuweka katika maeneo nkorofi ambayo yanasababishwa.
 Magari mengine yalazimika kushushia katikati ya Daraja kitu ambacho ni hatari na wengine kupata nafasi ya kuosha Pikipiki zao

 Zaidi ya wanafamilia 55 kuyakimbia makazi yao katika maeneo ya Yombo Kilakala kwa Bongotonyo, kutokana na Nyumba zao kujaamaji
  Zaidi ya wanafamilia 55 kuyakimbia makazi yao katika maeneo ya Yombo Kilakala kwa Bongotonyo, kutokana na Nyumba zao kujaamaji
 Mbunge Mtemvu akiyapima maji kwa kuingia na kujionea
 Mbunge Mtemvu akiyapima maji kwa kuingia na kujione
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Yombo Relini Yusufu Marko (kulia) akimwelekeza jambo wakati alipo fika katika maeneo hayo baada ya kuzunguuka maeneo tofauti na  Mbunge Abbas Mtemvu 
 Mbunge wa Jimbo la Temeke na Mbunge wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu (kulia) akiongozana na Meya wa Temeke Maabad Suleimani (kati) na Naibu Meya wa Jimbo hilo Juma Mkenga  wakati wa ziara ya  kutembele walio athirika na Mvua zinazoendelea kunyesha
  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtevu akiyapima maji kwa kuingia katika dimbwi lililokuwa limejaamaji na kumlazim kushuka katika Gari alilokuwa amepanda na kumsaidia Dereva wa Gari  lenye usajili T 526 DDR lililonyuma ya Mbungehuyo kushindwa kupita na baada ya kufanyahivyo dereva huyo alionyeshwa njia ya kupita na kuendelea na safari ni baada ya mbunge huyo kuwa katika Ziara ya kuwatembelea waadhirika wa Mvua.
  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akimsaidia kumuelekeza Dereva wa Gari T 526 DDR baada ya uonekana kusuasua na akiwa anaziara ya kuwaona waadhirika wa Mvua
.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) 

AutoSueco (VOLVO) delivers Mining Equipments worth $2.9

$
0
0
 AutoSueco (VOLVO) Commercial Manager, Mr. Alen Nkya (right) proudly handing the keys for one of the Articulated Haulers when delivering mining equipments worth of US$ 2.9m to Namoya Procurement Manager, Mr. Serge Longo (centre) in Dar es Salaam recently. Witnessing (left) is Namoya Project Manager, Mr. Doyen Kwabo. 


AutoSueco (VOLVO) Commercial Manager, Mr. Alen Nkya (right) gestures with Namoya Procurement Manager, Mr. Serge Longo (centre) and Namoya Project Manager, Mr. Doyen Kwabo (left) after delivering several mining equipments in Dar es Salaam recently.

Benki ya Exim Ilivyoshiriki Katika Mbio za Magari Tanga

$
0
0
 Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Bw. Gabriel masanja  (wapili kulia) akipeana mkono na Bw. Rajpaul Singh Dhani (kulia) dereva wa gari ya mashindano iliyoiwakilisha benki hiyo katika mchezo wa mashindano ya magari uliyofanyika mkoani Tanga hivi katibuni. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Tanga.
Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Bw. Gabriel masanja  (wa kwanza kushoto) pamoja na Bw. Rajpaul Singh Dhani (Wa tatu kushoto) dereva wa gari (iliyopo mbele yao)ya mashindano iliyoiwakilisha benki hiyo katika mchezo wa mashindano ya magari uliyofanyika mkoani Tanga hivi katibuni. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Tanga. 

TAZAMA ATHARI YA MVUA ILIONYESHA JIJINI DAR NA KUPELEKEA UHARIBIFU MKUBWA WA MIUNDOMBINU KAMA HIVI.

$
0
0
Athari ya mvua hasa kwa miundo mbinu ni kubwa,pichani ni sehemu ya barabara ya mbezi chini ikiwa imekatika kufuatia mvua kubwa ilionyesha siku nzima ya jana.
Uchafu mkubwa uliokuwa umeziba daraja la mto mbezi chini ukiondolewa baada ya maji ya mto huo yaliyokuwa yakitiririka kwa kazi,kuziba kwa daraja hilo ilipelekea maji ya mto huo kupita juu ya daraja na kupelekea adha kubwa kwa wakazi wa eneo hilo na sehemu nyingine.
Athari kubwa ya mvua iliyopelekea kuleta adha kubwa katikati ya jiji la Dar na kwingineko.Pichani ni hali halisi ya maji kutuama mbele ya soko la Mboga mboga na Matunda eneo la Afrika Sana-Sinza,kufuatia mitaro ya eneo hilo kuzibwa na uchafu.
Pichani mkazi wa Bamaga akitazama athari ya mvua kubwa ilionyesha siku nzima ya jana jijini Dar



Soko la Mwenge nalo ilikuwa ni vigumu biashara kufanyika.
Kufa kufaaaana.


Sehemu ya Mto mbezi
Huyu jamaa sijui alikuwa anatafuta nini 




INTRODUCING Lady Jaydee - Give Me Love (Official Video)

TANZIA: MSIBA UK

$
0
0


 Nasikitika kutangaza kifo cha Mtanzania mwenzetu aitwaye Gertrude Matesh Hodgson. Ambaye alikuwa anakaa katika anuani 37 Cromer Street, Clifton,  York YO30 6DQ 

Marehemu amehifadhiwa katika hospitali ya  Cottingham, huko YORK.

Ameacha binti mmoja ambae anasoma chuo kikuu hapa UK.

Anategemea kuzikwa hapa hapa UK.

Msaada wa Ushauri na hali unahitajika sana.

Mawasiliano:-

Dada Kissa +447510145626

Mwanamisi 07448755475

Asante sana Mungu na awabariki nyinyi nyote.

Kwa niaba ya ndugu zetu wafiwa  naomba kuwasilisha kwenu account namba kwa msaada wenu watanzania wa UK

Account no:39860655
Sort Code: 56-00-70
Natwest Bank.
Name: Jacqueline E. Josephat

WAZIRI MKUU AISHUKURU LIONS CLUB KWA MISAADA YAKE

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameishukuru taasisi ya Kimataifa ya Lions Club kwa misaada ambayo imekuwa ikiitoa hapa nchini katika nyanja za afya, utunzaji mazingira na uokoaji wakati wa maafa.

Akifungua kongamano la 12 la mwaka linalojumuisha wadau wote wa Lions Club District 411 leo asubuhi (Jumamosi, Mei 9, 2015), Waziri Mkuu alisema anawashukuru wana Lions wote kwani miradi mingi wanayoifanya huwa ni kwa kujitolea tu.

“Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hii kwani kwa sehemu kubwa wanachokifanya ni kile ambacho sisi kama Serikali tulipaswa tukifanye. Wanatoa huduma bure za macho, matibabu ya moyo, wanatoa misaa ya mahema, vyandarua, vyakula pale tunapokumbwa na maafa. Wanafanya kazi nzuri,” alisema.

Akitolea mfano huduma za kijamii kama vile Heart Baby Project, Waziri Mkuu alisema: “Mradi wa Heart Baby Project umedumu kwa miaka karibu 30. Wameshawachukua watoto zaidi ya 3,000 wenye matatizo ya moyo na kuwapeleka India kuwapatia matibabu kwa gharama zao,” alisema.

“Jambo kubwa zaidi la kushukuru ni kwamba asilimia 99.5 ya watoto waliofanyiwa upasuaji, wamepona na hivyo kuweza kuokoa maisha ya watoto wetu,” alisema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wajumbe zaidi ya 500 waliohudhuria Kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Lions International, Raju Manwani alisema taasisi hiyo ina wanachama zaidi ya milioni 1.4 duniani waliosambaa katika nchi 210 ambao hufanya kazi kwa kujitolea.

Naye Mwenyekiti wa Lions Multiple Council, Bw. Teja Kalsi alisema wanapojiandaa kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa kwa Lions Club, wamejiwekea lengo la kuhakikisha wanatoa huduma kwa watu milioni 100 kwa katika Nyanja zao nne kuu. Hivi sasa taasisis hiyo imetimiza mika 98 tangu kuanzishwa kwake.

“Uanachama ndiyo nguzo yetu kuu lakini pia tuna shauku ya kutimiza watu milioni 100 waliopata huduma zetu katika nyanja za vijana, afya na hasa huduma ya macho, utunzaji wa mazingira na kuwalisha wenye njaa. Tujielekeze huko ili tutimize kaulimbiu yetu isemayo palipo na uhitaji, mwana-lion yupo (Where there’s a need, there’s a lion),” alisema.

Kongamano hilo limehudhuriwa na washiriki kutoka Kenya, Uganda, Ethiopia, Seychelles, Sudan Kusini, India na wenyeji Tanzania.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAMOSI, MEI 9, 2015.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA LIONS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia mkutano wakati alipofungua kongamano la 12 la Lions Club kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam  Me 9, 2015.
 Baadhi ya washiriki wa kongamano la 12 la Lions Club wakimsikiliza Wairi Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua  kongamano hilo kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam Mei 9, 2015.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongea   na viongozi wa Lions Club  baada ya kufungua kongamano lao la 12 kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana  na viongozi wa Lions Club  baada ya kufungua kongamano lao la 12 kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MKUU WA WILAYA MISSENYI MH.FADHIL NKURLU AKAMATA SHEHENA LA NGOZI ZA MAGENDO

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh. Fadhil Nkurlu (kushoto) akimhoji dereva wa lori aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Kabyemela (mwenye tisheti jekundu) baada ya kuwekewa mtego na kukamatwa na shehena ya ngozi ya magendo iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea nchi jirani. Shehena hiyo ilikamatwa katika kizuizi cha Kyaka.

 Baadhi ya ngozi ya magendo iliyokamatwa baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuweka mtego kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. Shehena hiyo ya ngozi ya magendo inakisiwa kufika uzito wa takribani tani 10.
--------------------------------------------------------------- 
Missenyi. 8 Mei, 2015 - Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh. Fadhil Nkurlu amekamata shehena kubwa ya ngozi ya magendo yenye uzito unaokisiwa tani 10 ikisafirishwa kwenda nje ya nchi bila kibali wala nyaraka zozote za serikali.  
Kwa mujibu wa  taarifa za ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Missenyi ngozi hiyo ilitokea Kahama ikiwa inaelekea nchini Uganda na ilikamatwa katika kizuizi cha Kyaka, wilayani Missenyi.  
"Tulipata taarifa kutoka kwa raia wazalendo tangu jana yake kwamba kuna bidhaa za magendo ambayo huwa yanapita usiku, ndipo nikawapanga vijana kutoka vikosi vyote vya ulinzi na usalama kuweka mtego huu," alisema DC Nkurlu.


"Hiki ni kipindi ambacho magendo ya kahawa husafirishwa kwa wingi kwenda nje ya nchi na hivyo hukosesha serikali mapato yake stahiki. Lakini tumejipanga ipasavyo na tutahakikisha tunakamata kila aina ya magendo. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayejihusisha katika biashara hii," alisisitiza. 

"Napenda kutoa rai kwa wananchi wote wa Missenyi kuendelea kutoa ushirikiano wao kwa serikali ili kuweza kukamata bidhaa hizi za magendo na kudhibiti mtandao huu haramu," alisema Mh. Nkurlu.  

Hii ni mara ya pili ndani ya wiki hii magendo yanakamatwa ambapo Jumatatu shehena kubwa ya mbao zilikuwa zikisafirishwa kinyemela zilikamatwa na bado zinashikiliwa katika kituo cha polisi cha Kyaka.

CHADEMA WAFANYA MKUTANO WAO JIJINI ARUSHA.

$
0
0
Mheshimiwa Tundu Lissu akiwahutubia wakazi wa Arusha Mjini katika mkutano mkubwa ulioambatana na mvua kubwa hapo jana.
Wakazi wa Arusha wakiwa katika mkutano mkubwa ulioambatana na mvua lakini wamesema hawataondoka hata kama mvua ya mawe itanyesha
Makamanda wakiwa wamelowa chapa chapa lakini bila kujali mvua wameweza kufanya mkutano kama kawaida.

RAIS KIKWETE AWASILI ALGIERS, ALGERIA, KWA ZIARA RASMI YA SIKU TATU

$
0
0
 Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.ab2
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.ab3
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.ab4
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.ab5
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
ab6
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
ab7
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
ab8ab9
Bendera za Tanzania na Algera zikiwa zimepamba jiji la Algiers, Algeria, ambako Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
ab10ab11
………………………………………………………………….
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
Rais Kikwete amewasili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria akitokea New York, Marekani, ambako kwa wiki nzima amekuwa anaendesha vikao vya Jopo la Watu Mashuhuri Duniani ambao wanatafuta jinsi gani dunia inaweza kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na majanga ya afya, na hasa magonjwa ya milipuko, katika siku zijazo kufuatia balaa la ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene mjini Algiers, Rais Kikwete amepokelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal kabla ya kuelekea kwenye Kasri ya Kirais ya Zeralda ambako amefikia.
Baadaye jana jioni, Rais Kikwete ameweka shada la maua kwenye Mnara wa Taifa kwa heshima ya wanamapinduzi waliopoteza maisha yao katika vita vya ukombozi wa kuwania uhuru wa Algeria kutoka kwa Wafaransa.
Algeria ilipata uhuru kutoka kwa Wafaransa mwaka 1962 baada ya vita kali ya ukombozi ya miaka minane, ambako pia wananchi wanaokadiriwa milioni mbili walipoteza maisha yao.
Baadaye, Rais Kikwete pia amembelea Jumba la Makumbusho la Mashujaa wa Vita ya Ukombozi mjini Algiers.
Kesho, Jumapili, Mei 10, 2015, Rais Kikwete atahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo itaandaliwa kwa heshima yake na Waziri Mkuu ambaye atafanya naye mkutano rasmi kabla ya dhifa.
Baadaye, Rais atakwenda kwa mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Rais Abdelaziz Bouteflika, ambaye mwaka jana alichaguliwa tena kwa mara ya nne kuongoza Algeria tokea alipochaguliwa kuwa Rais  kwa mara ya kwanza mwaka 1999 baada ya kutumikia kama Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi yake kwa miaka mingi. Tokea 1999, alichaguliwa tena 2004, mwaka 2009 na mwaka jana.
            Tanzania na Algeria zimekuwa marafiki wa karibu kwa miaka mingi tokea uhusiano ulipoanzishwa na waanzilishi wa mataifa hayo mawili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Ben Bella. Kwa hakika, Algeria ilikuwa moja ya nchi chache duniani zilizoisaidia sana Tanzania wakati wa Vita ya Kagera dhidi ya Idi Amin.
Tanzania pia imekuwa inapata misaada mikubwa kutoka Algeria katika sekta za gesi a elimu na katika kitendo kilichothibitisha ukaribu kati ya Tanzania na Algeria, mwaka 2010, Algeria iliifutia Tanzania kiasi cha dola za Marekani milioni 144. Kiasi hicho kilikuwa ni pamoja na deni la awali la dola milioni 58.03, deni ambalo liliongezeka kwa sababu ya mikopo ya mafuta ambayo Tanzania ilikuwa inapata kutoka Algeria na riba.

TIMU TANZANIA YASHIRIKI MATEMBEZI YA SUSAN G. KOMEN WASHINGTON, DC

$
0
0

Timu Tanzania ikipata picha ya pamoja kabla ya kuanza matembezi ya saratani ya matiti ya Susan G. Komen yaliyofanyika Washington, DC siku ya Jumamosi May 9, 2015.

Wanusurika wa saratani ya matiti wakipata picha ya pamoja.

Matembezi yakianza.

Kushoto ni msaniii toka uingereza Matt Goss aliyeimba wimbo maalum wa Strong kwa ajili ya matembezi haya ya Susan G. Komen ambaye mwaka jana mama yake mzazi alifariki kutokana na maradhi ya saratani ya matiti akipeana mkono na watembeaji wa saratatani ya titi. Kati ni Nancy G. Brinker mdogo wake Susan G. Komen akipeana mkono na watembeaji siku ya maadhimisho ya matembezi ya saratani ya matiti kwa kumuenzi dada yake kwa kuanzisha oganaizesheni ya kupigana na gonjwa hili hatari mwaka 1982 kama ahadi aliyomwekea dada yake.

Mmoja ya watembeaji na mnusurika wa saratani ya titi akipatiwa huduma ya kwanza na watembeaji wenzake baada ya kuanguka na kupata majeraha kwenye paji la uso huku wakisubili gari la wagonjwa.

Timu Tanzania ikichanja mbuga kwenye matembezi hayo.

Mwanahabari wa Kwanza Production na Vijimambo Media Mubelwa Bandio(kulia) akiwa sambamba na mwimbaji Matt Goss na Nancy G. Brinker CEO wa Susan G. Komen

Timu Tanzania ikiwa imemaliza matembezi yao ya maili 3 takribani na kilomita 5

Watoto wa wazazi Watanzania wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza matembezi hayo na wazazi wao.

Picha ya pamoja ya kumaliza matembezi hayo pamoja na mmoja wa kikosi cha zima moto wa TDF aliyejumuika kupiga picha na timu Tanzania.

Picha zote na Kwanza Production na Vijimambo Media & Entertainment.
Kwa picha zaidi bofya HAPA
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images