Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

MGOMO WA MADEREVA WASABABISHA ADHA KUBWA KWA ABIRIA NCHINI.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva nchini, Rashid Saleh akizungumza na baadhi ya Madereva wenzake walioingia kwenye mgomo leo, kuishinikiza Serikali kuwatimizia matakwa yao waliyoyaomba kwa kipindi kirefu kilichopita.
Sehemu ya Umati wa Madereva hao ukimsikiliza kiongozi wao, mchana wa leo kwenye Stendi kuu ya Mabasi, Ubungo jijini Dar es salaam.
 Taswira ya kituo cha Simu 2000 Ubungo jijini Dar es Salaam leo baada ya mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria.Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
 Barabara ya Sam Nujoma eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
 Licha ya mgomo wa madareva Miundombinu ya maji machafu hakuna katika kituo cha Mabasi Yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
Hakuna kukanyaga maji ni kuruka mawe tuu.
 Mabasi yakiwa yameegeshwa katika Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoani-Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MOTO WATEKETEZA JENGO MOJA MTAA WA LIVINGSTONE NA NARUNG'OMBE, KARIAKOO JIONI YA LEO.

$
0
0

 
Moto mkubwa ukiendelea kuteketeza moja ya jengo lililopo kwenye makutano ya Mtaa wa LivingStone na Narung'ombe, Kariakoo jijini Dar es salaam muda huu. Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika mpaka sasa.
Globu ya Jamii inafuatilia tukio hilo taarifa kamili itawajia baadae kidogo.

mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria jijini Dar es salaam leo

MGOMO WA MABASI ABIRIA MOSHI,ABIRIA WAKWAMA STENDI, WAIGEUZA UKUMBI WA SINEMA...

$
0
0
Hivi ndivyo kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi kilivyoonekana.
Baadhi ya abiria wakiwa wamekaa kitako katika maegesho ya magari huku wakitizama Big Screen iliyopo jirani na kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
Baadhi ya abiria wakitizama kwa mbali screen hiyo.
Screen kubwa kwa ajili ya matangazo ya biashara iliyoko jirani na kituo kikuu cha mabasi ikionesha picha ya mashindano ya magari ambayo ilikuwa burudani kwa abiria baada ya kukosa usafiri kutokana na mgomo wa madereva uliotikisa nchi nzima.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MVUA YASABABISHA MAFURIKO MOSHI VIJIJINI,MBUNGE LUCY OWENYA AWAFARJI WAATHIRIKA.

$
0
0

Baadhi ya nyumba zilijaa maji hali iliyowalazimu wahusika kutoa itu vya ndani nje.
Wengine walilazimika kuweka vyakula juu ya mabanda ya kuku.
Baada ya maji kujaa wengine walilazimika kuhamishia magodoro yao juu ya paa la Choo.
Hata vyakula ambavyo vingi vyao vililowa na maji vilianikwa juu ya paa.
Mbunge Lucy Owenya akitizama namna ambavyo baadhi ya wananchi walivyoamua kuokoa vitu ya kwa kuianika juu ya paa.
Mifugo pia liathirika na mafuriko hayo.
Kutokana na hali hiyo Mbunge Lucy Owenya alilazimika kutoa msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko hayo
Mbunge Lucy Owenya akimfariji mmoja ya waathirika wa mafuriko hayo aliyekuwa akilia kwa uchungu baada ya kupoteza vitu vyake mbali,mbali ikiwemo vyeti vya taaluma ya utabibu.
Mbunge Lucy Owenya akikabidhi msaada wa chakula kwa wananchi walioathirika na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo.
Diwani wa kata ya Arusha Chini Rojas Mmari akizungumza jambo mara baada ya wananchi wake kukabidhiwa msaada huo.
Afisa mtendaji Utawala wa kiwanda cha sukari cha TPC ,Jafary Ally akizungumza kuhusu namna mafuriko hayo yalivyo athiri kiwanda hicho.
Mafuriko makubwa yamevikumba vijiji saba kikiwemo kiwanda cha sukari cha TPC na kuathiri miundombinu pamoja na makazi ya watu kujaa maji.
Mbunge wa viti maalumu ,Lucy Owenya (Chadema) (kulia)akiwa ameongozana na diwani wa kata ya Arusha Chini ,Rojas Mmari alipotembelea kujionea athari zilizotokana na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akitembelea maeneo yaliyo athirika na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akitizama sehemu ambayo wananchi walilazimika kuibomoa kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha TPC ili kuruhusu maji kupita.
Eneo lililobomolewa ili kuruhusu maji ya mafuriko kupita.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

ELIMU ZAIDI YATAKIWA KUBADILI JAMII KUTHAMINI MAALBINO

$
0
0
DSC_0016
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye akiwakaribisha mameneja wa Redio za jamii nchini (hawapo pichani) walioshiriki kwenye mafunzo ya siku moja ya kutoa elimu kwa Redio za jamii nchini juu ya kuandaa vipindi vyenye ujumbe sahihi wa masuala yanayohusu watu wenye Albinism iliofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema hivi karibuni. 

Katikati ni Afisa mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS), Kondo Seif na kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
DSC_0031
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akielezea dhima ya UNESCO kuwashirikisha shirika la Under The Same Sun (UTSS) kutoa elimu kwa Redio jamii ili kupaza sauti kwa jamii dhidi ya mauaji ya watu wenye Albinisim pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili walemavu wa ngozi.
DSC_0005
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa mwongozo kwa washiriki wa semina hiyo.
DSC_0199
Afisa mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS), Kondo Seif akiendesha mafunzo kwa mameneja wa Redio jamii nchini (hawapo pichani) kwenye semina ya siku moja iliyofanyika wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza. Katikati ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.

DSC_0055
DSC_0071
Meneja wa Redio jamii Mpanda FM iliyopo mkoani Katavi, Prosper Kwigize akichangia maoni yake kwenye semina hiyo namna ya kudhibiti mauaji ya watu wenye Albinism iliyofanyika hivi karibuni wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.
DSC_0076
Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akielezea jitahada za kituo chake cha Redio kinavyoshiriki katika kukemea mauaji ya watu wenye Albinism kwa kuendesha midahalo mbalimbali pamoja na makala maalum kuhusiana na walemavu wa ngozi.
DSC_0013
Baadhi ya mameneja wa vituo vya Redio jamii nchini walioshiriki semina hiyo ya siku moja wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Bwana Kondo Seif (hayupo pichani) wa Shirika la Under The Same Sun (UTSS).
DSC_0008
DSC_0042
DSC_0233
Mkufunzi wa semina ya siku moja kwa Mameneja wa Redio jamii nchini Kondo Seif akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo.

Na modewjiblog team, Sengerema
Ofisa mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS) Kondo Seif, ameitaka jamii kuungana kupiga vita imani potofu zinazosababisha mauaji kwa watu wenye albinism.

Alisema jamii ikiamka na kuamua kumaliza tatizo hilo, mauaji hayo yatakoma. Kauli hiyo aliitoa katika semina ya siku moja ya elimu kwa Redio za jamii nchini juu ya kuandaa vipindi vyenye ujumbe sahihi ya masuala yanayohusu watu wenye Albinism iliofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema mkoani Mwanza hivi karibuni.

Kondo alisema katika jamii kumekuwa na imani potofu ambapo Albinism wamekuwa wakiitwa majina yanayolenga kunyanyapaliwa na kusababisha kushamiri kwa vitendo vya ukatili na mauaji dhidi yao.

Aliitaka jamii kutambua kuwa albinism ni hali ya ukosefu wa rangi asilia mwilini inayoathiri ngozi, macho na nywele na ni nadra hali hiyo kupatikana na haiambukizi kama watu wengine wanavyodhani. Aidha ametaja jina sahihi la Kiswahili lililokubaliwa na baraza la Kiswahili Tanzania kuitwa watu wenye albinism kuwa ni watu wenye ualbino. Alisema watu wenye ualbino wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kukosekana kwa taarifa sahihi zinawagusa wao kama ngozi kushindwa kuhimili jua, uoni hafifu na kupungua kwa usalama.

Kwa mujibu wa Takwimu za shirika hilo watu wenye Albinism zaidi ya albino 70 nchini Tanzania wameuawa, zaidi ya 30 wamekatwa viungo vyao na makaburi ya watu wenye Albinism 20 yamefukuliwa. Ameviomba vyombo vya habari kushiriki kikamilifu kutoa elimu sahihi kwa jamii ili kustawisha maisha ya watu wenye Albinisms kuwa kufanya hivyo maendeleo yao, jamii na taifa kwa ujumla yataimarika.

Awali akizungumza na washiriki wa semina hiyo Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph aliwataka waandishi wa habari kuzingatia matumizi sahihi ya lugha wanapoandika habari na kuandaa vipindi vinavyozungumzia masuala ya Albinism.

Pia amesisitiza kuandaa vipindi vinavyobeba ujumbe sahihi wa kuelimisha jamii juu ya masuala yanayohusu Albinism ili kubadilisha mitazamo ya jamii ili kuwathamini, kuwalinda, kuwaheshimu na kuwashirikisha katika maendeleo.

Sambamba na hilo amevitaka pia kubeba jukumu kubwa la kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura na kutoishia kujiandikisha tu bali wajitokeze kupiga kura kuwachagua viongozi ambao ni Madiwani, Wabunge na Raisi October 2015 pamoja na kuipigia kura katiba inayopendekezwa wakati ukifika.

Ameongeza katika matukio hayo muhimu ya kitaifa watu wenye Albinism wahamasishwe kushiriki kikamilifu vile vile na makundi mengine kama wanawake, vijana, watu wenye ulemavu, wazee na makundi mengine maalum.

KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA ASIFU UTENDAJI KAZI WA WAZIRI LUKUVI JIMBONI NA WIZARANI ATOA AGIZO KWA VIJANA KUSAIDIA UJENZI WA BWENI IDODI SEKONDARI.

$
0
0


 katibu mkuu  UVCCM akiongoza wanachama  wapya  wa CCM kula  kiapo
Bw  Mapunda  akizungumza na  walimu  wa shule ya sekondari  Idodi  leo
Na matukiodaimaBlog

KATIBU  mkuu  wa   jumuiya ya  umoja  wa  vijana  wa  chama  cha mapinduzi (UVCCM) Taifa  Bw  Sixtus  Mapunda amempongeza  mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw  Wiliam Lukuvi kwa  kuwa  mbunge  wa  mfano katika  jimbo  lake na kuwa  waziri  wa  mfano  katika  baraza la  mawaziri kutokana na  utendaji kazi  wake  mzuri unaorejesha heshima  ya CCM kwa  wananchi hasa katika  kumaliza kero ya ardhi  hapa  nchini.

Mbali ya  pongezi  hiyo Mapunda ameeleza  kufurahishwa na mchango  wa mbunge  Lukuvi  wa bati 503 ,Saruji  mifuko 200  na  pesa  kiasi cha Tsh milioni 10  kwa ajili ya  kusaidia  ukarabati  wa  bweni la  wanafunzi  wa  shule ya  sekondari Idodi  lililoungua na moto  kutokana na hitirafu ya  umeme  hivi karibuni.

Bw  Mapunda  ameyasema  hayo  leo  wakati  akizungumza na wananchi  wa kijiji cha Idodi  jimbo la Ismani  wakati  wa  ziara  yake ya kichama katika jimbo    hilo kwa  ajili ya  kuhamasisha  wananchi  kujitokeza kwa wingi kujiandikisha  katika  daftari la  kudumu la  wapiga  kura.

Alisema  kuwa hakuna  sababu ya  wananchi  wa Isimani  kuhangaika na  mbunge  zaidi  ya  Lukuvi  kutoka na kazi kubwa ya  kimaendeleo ambayo  mbunge   huyo  ameifanya  ndani ya jimbo  hilo na  kuwa hadi  sasa hakuna mbunge ambae upepo  wa  kisiasa kwa wananchi wake ni mzuri kama  ilivyo kwa  mbunge  Lukuvi .

Kwani  alisema  pamoja na  Lukuvi ambae ni  waziri  wa ardhi  kuleta  maendeleo  katika  jimbo lake  bado  amekuwa ni  waziri  mchapakazi  kwa  kufanya kazi kwa  vitendo  zaidi  kwa  kuwasaidia  wananchi  wenye  kero mbali mbali  za ardhi  kupata  haki  yao .

"Nawaombeni  kama  kuna  mpinzani wa Chadema anakuja  kutaka  ubunge  Isimani muulizeni anataka  kuwafanyia  nini  cha  kimaendeleo  na amefanya  nini ikiwa hata  saruji  mfuko  mmoja sekondari ya  Idodi ameshindwa  kupeleka  ......nawaombeni sana msimpoteze  Lukuvi ni   mbunge mchapa  kazi" alisema

katika  kuunga  mkono  jitihada  za mbunge  Lukuvi na  jitihada za  wadau mbali mbali ambao  wamejitokeza  kuchangia  maafa katika  shule  ya sekondari  Idodi kwa upande  wake anawaagiza  vijana wote  wa UVCCM mkoa  wa  Iringa kuandaa kambi ya kufyatua  tofari za  kujengea bweni mmoja  katika  shule   hiyo ya sekondari  Idodi   kuanzia  mwezi  ujao  ili  kuwezesha  wanafunzi kupata  bweni la  kuishi .

Mapunda  alisema  kuwa  kwa upande  wake  atasaidia bati  770  kwa  ajili ya ujenzi  wa  bweni   hilo na  kuwataka  wananchi  kujenga  utamaduni wa  kuendelea  kushiriki  shughuli za kimaendeleo na  kuchagua CCM ambao  wanatenda kwa  vitendo  badala ya  wapinzani  ambao wao kazi yao ni kufanya maandamano  na  sio  maendeleo .

Kuhusu  suala la  majanga  ya  moto  katika  shule ya  sekondari  Idodi  aliuagiza  uongozi  wa shule  hiyo  pamoja na  serikali ya  wilaya  kwa  kushirikiana na shirika la umeme  Taifa Tanesco  kufanya uchunguzi  wa  kina  ili  kujua  chanzo  cha moto wa  mara kwa mara  shuleni hapo  na  kuwa  yawezekana  chanzo  si mfumo  wa  uunganishaji wa umeme katika  bweni ila  upo   kwa Tanesco  wenyewe kwa  umeme  kuzidi na  kupungua .

katika   ziara   yake hiyo  pia katibu  huyo na msafara  wake  walipata  kutembelea  makaburi  ya  wanafunzi  12  walioteketea kwa moto  katika  shule  ya  sdekondari  Idodi  na  kufanya  sala  fupi ya  kuwakumbuka wanafunzi hao ambao  hadi  sasa majina  yao wote yamepatikana  baada  ya  vipimo  vya  DNA kurudi kutokana  na  awali  kuzikwa bila  kutambuliwa na  kuona  jinsi  ambavyo   serikali  ilivyoboresha  eneo  hilo kwa kuweka  uzio  ili  kuwaondoa hofu  wanafunzi wengine.

Katika  risala  yake  kwa  katibu  mkuu  huyo mkuu  wa shule ya  sekondari  Idodi  Bw  Christopher Mwasomola alisema  kuwa  mbunge  wa  jimbo  hilo Bw  Lukuvi ndie  aliyekuwa mtu wa  kwanza kusaidia ukarabati  wa mabweni  yaliyoungua moto  kwa  kutoa Saruji  mifuko 200, bati 503  ,madogoro 100 na fedha  kiasi  cha Tsh milioni  10  na  kuwa bila jitihada  hizo  za mbunge  wao yawezekana hadi  sasa ukarabati  huo  usingefanyika .

Aliwataja   wadau  wengine  waliofika  kusaidia  kuwa ni pamoja na  Ruaha Carnivores Project waliotoka  madogoro 48, Paroko Salvatory   Tsh  milioni 1, Askofu wa  kanisa la RC jimbo la  Iringa Tsh  milioni 1  na  sabuni kwa  wanafunzi wote , TOHASSA Iringa  Tsh  900,000, Shule  mbali mbali  za  sekondari zilichangia vitu  mbali mbali zikiwemo kalamu ,sabuni  na  vifaa  vingine  , Shule ya msingi Idodi Tsh 100,000, Balozi  wa Dubai  Tsh 9,927,000  na mbunge  wa viti maalum  mkoa  wa Iringa Bi  Chiku  Abwao(Chadema) Tsh milioni 1

Hata   hivyo  alisema  changamoto  kubwa ni  kukosekana kwa  bweni la  wasichana  shuleni  hapo na  kupelekea  wanafunzi kwa  sasa  kulala jengo  la mazingira  ukumbi wa mikutano  pia  kukosekana kwa utulivu kwa  wanafunzi  shuleni hapo .

Mkuu  huyo  pia  alimpongeza  katibu  mkuu  huyo  wa vijana  kwa  kuwa  kiongozi  wa  mfano katika  jamii na  kuwa alichokifanya katika shuleni  hiyo ndicho  ambacho  wananchi  wanapenda  na  sio maneno  bila  vitendo .
Katibu wa  UVCCM Taifa  Bw Sixtus  Mapunda  mwenye  kofia ya ccm  akishiriki   mchezo wa   kimasai  leo  wakati  wa uzinduzi  wa tawi la  CCM eneo  la  wafugaji kijiji  cha  Idodi 
mjumbe  wa  baraza  kuu la  utekelezaji  la UVCCM Taifa  Secky Kasuga kulia akishiriki na  viongozi  wa  kitaifa  kucheza ngoma ya  kimasai
viongozi  wa  kitaifa  wa UVCCM Taifa  wakishiriki kucheza na masai.
Wananchi  wakiwa  juu ya  miti  wakimsikiliza katibu  mkuu wa UVCCM taifa  leo kijiji cha Idodi
wananchi  wa  Idodi  wakiwa katika mkutano wa katibu  wa UVCCM Taifa
katibu  wa UVCCM taifa  kulia akimpongeza kada wa CCM
Masai  wakiwa cheza  ngoma
katibu  mkuu  wa  UVCCM Taifa Sixtus Mapunda  akisimikwa  kwa  mlezi  wa tawi la Uvccm kulia ni Bi Secky Kasuga
kada  wa CCM Bi Juliana Shonza  akicheza  ngoma  ya  kimasai  leo Idodi
katibu  mkuu  UVCCM Bw Sixtus Mapunda  akimpokea  kada  wa Chadema  Idodi aliyejiunga na  CCM leo
Mkuu  wa  shule ya  sekondari  Idodi  akitoa taarifa ya kuungua kwa mabweni ya  wanafunzi 
Kada  wa Chadema  akivishwa kofia ya  CCM na katibu  mkuu wa UVCCM Taifa  Bw Mapunda leo
diwani  wa Idodi  Bw  Onesmo Mtatifikolo akijibu maswali ya  wananchi  leo 
Bweni la sekondari ya  Idodi  ambalo mbunge  wa  jimbo   la Ismani wiliam Lukuvi na  wadau  mbali mbali  wamelikarabati  baada ya  kuungua  moto
katibu  mkuu  wa UVCCM Taifa  Bw Sixtus Mapunda  akiwahutubia  wananchi  wa Idodi  jimbo la Isimani  leo
katibu  mkuu  wa UVCCM Taifa  akifurahi jambo na katibu tarafa ya  Idodi  leo
viongozi  wa CCM wilaya  ya  Iringa ,mkoa na  taifa  wakiungana na katibu  mkuu wa UVCCM Taifa  kufanya  sala katika makaburi ya  wanafunzi 12  walioteketea kwa  moto  shule ya  sekondari  Idodi  mwaka  juzi
mkuu  wa  shule ya sekondari  Idodi  akimkabidhi taarifa ya  shule katibu mkuu  wa UVCCM Taifa  Bw Mapunda  leo
Mratibu  wa  wana CCM  wa  vuyuo  vikuu Bw  Ramadhan  Baraza   kulia akiwa katika  kibao  chenye majina ya wanafunzi  waliokufa  moto Idodi  sekondari
katibu  mkuu  wa UVCCM taifa  akiwa  na  viongozi wengine  kwenye  kibao  chenye majina  ya  wanafunzi  waliokufa kwa  moto  Idodi  sekondari  mwaka  juzi
Katibu  wa UVCCM mkoa  wa  Iringa E. Mwampashi akimtambulisha  Juliana Shonza
Walimu  Idodi wakiwa katika  kikao na  katibu  mkuu wa UVCCM leo
Mkuu  wa  shule  ya  sekondari  Idodi  Bw  Cristopher Mwasomola  akitoa  taarifa ya  shule  hiyo
katibu mkuu  akikagua  jengo  la  bweni  lililoungua  moto   Idodi  sekondari
Hili  ndilo  bweni  lililowaka  moto 
Katibu  mkuu  UVCCM taifa  akimsikiliza  mkuu  wa  shule ya  sekondari Idodi  leo
Wananchi  Idodi  wakimsikiliza katibu mkuu  wa  UVCCM Taifa 
katibu  mkuu  UVCCM Bw  Mapunda  akikabidhi kadi kwa wanachama  wapya wa CCM Idodi

MAHOJIANO YA KHADIJA KIMOBITEL NA ZENJ FM,

$
0
0
Katika mahojiano na Redio Zenj FM na mmoja ya wa wanamuziki nguli wa muziki wa dansi Bi.Khadija Mnoga aka Kimobitel kwenye kipindi maalumu cha wakongwe wa muziki  wa dansi na vijana wa enzi zile, kinaongozwa na mtangazaji mahiri bwana Mustapha Mussa siku ya jumamosi 2 Mai 2015.
Mwanamuziki  Khadija Mnoga Kimobitel amefunguka kwa kusema kile kinacho
ukwamisha muziki wa dansi “Bongo Dansi” na kuurudisha nyuma juhudi za wanamuziki na muziki huo ni kubaniwa kwa kutopewa Promotion na kutopigwa mara kwa mara maredioni hapa nchini,Khadija Kimobitel ambaye ni mmoja wapo wa wanamuziki wachache wa kike  waliobobea katika muziki wa dasni alifunguka kwa kusema “Hakuna mchawi wa muziki wa dansi” bali ni baadhi ya redio zilizopo
hapa nchini kwa makusudi wameamua kutopiga mara kwa mara na kutozipa Air time ya kutosha nyimbo za muziki wa dansi .

Khadija Kimobitel alizitaja bendi kama Mlimani Park Orchestra ziliweza kufanya vizuri enzi zile za Radio Tanzania (RTD),kwa sababu RTD ilitoa muda mwingi na wa kutosha kwa kupiga muziki wa dansi, aliongeza kwa sasa Redio nyingi lakini kumekuwa na ubaguzi Muziki wa dansi unabagulia kwa nia ya kuuchimbia kaburi.

Khadija Kimobitel alifunguka zaidi kwa kusema wanamuziki wa dansi na bendi za Tanzania zinajitahidi kufanya kazi nzuri ..lakini kazi hiyo inachimbiwa kaburi nakukosa Promo ya kutosha kwa makusudi.
Ameziomba Redio mbali mbali na wadau wa muziki kuweza kuzipiga nyimbo za muziki wa dansi na kuzipa air time ya kutosha.

Bumbuli wampokea January Makamba kishujaa; Wambariki Urais.

$
0
0
 Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia, January Makamba akipokelewa na wazee mara baada ya kuwasili jimboni kwake.
 Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia, January Makamba akipokelewa na akina mama na kupewa baraka zake.
Na Raisa Said, Bumbuli. 

 Wakazi mbalimbali wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoani Tanga wamesema kuwa wapo tayari kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba kama ataamua kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa Uraisi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.  Wakazi hao ambao walionyesha nia yao hiyo katika sehemu mbalimbali alizopita Mbunge huyo katika ziara yake ya siku sita kutembelea jimbo lake iliyoanza Machi 30. Makamba ni mmojawapo wa watu wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ya Urais.

 Alipokuwa katika kata ya Tamota, viongozi wa dini walimfanyia maombi maalum ambayo yaliongozwa na  Mchungaji Amasia Mweta na Sheikh Amiri Yahaya Shekibula mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutumbiwa na Mbunge huyo kijana. Akihutubia mamia ya wakazi wa Bumbuli katika  maeneo yote  aliyopita  kwenye ziara yake, Makamba aliwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kusema kama sio wao asingeweza kuonekana na kutajwa katika kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa CCM. 

 Makamba, huku akishangiliwa na wakazi hao wa maeneo  hayo, alisema kuwa hakuna namna ambayo unaweza kutengeneza watu kukutaja katika nafasi za juu bila kupitia kwa wananchi kukuchagua katika nafasi ya kuwawakilisha. “Kutajwa si dhambi na kwa kuwa fomu za uchaguzi sio sumu si dhambi  pia kuchukua na kuingia katika kinyang’anyiro hicho,” alisema na kuongeza kuwa sasa hivi kuna kiu kubwa ya uongozi wa aina mpya na kuna watu wamemuona na kumtaja yeye jambo ambalo si baya. 

 Nao wananchi , wakiwemo vijana, kina mama na wazee katika maeneo mbalimbali aliyopitia Makamba, walimhakikishia Mbunge huyo kuwa hivi sasa hawatampokea mtu yeyote ambaye atakuja kujipitisha katika jimbo hilo hadi hapo watakapojua hatma ya utekelezaji wa nia ya Mbunge huyo kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa Urais kupitia  CCM. Nao waumini wa Usharika wa Bumbuli walimtaja Mbunge huyo kuwa jasiri, mweledi na mwenye maono mapana na wakasema wanaahidi kuwa bega kwa bega katika harakati hiyo  ya kuwania kuwa mgombea wa CCM.

VIDEO AUDIO NEW: MUNA - KALALA JUNIOR

ILO Tanzania to celebrate five (5) years of empowering youth through entrepreneurship in Tanzania

$
0
0
 International Labour Organization (ILO) has announced today that the National Capstone Conference in Tanzania will take place on the 7th of May at the Julius Nyerere International Convention Centre aiming to showcase the success of The Youth Entrepreneurship Facility (YEF) and its partners over the past five years and celebrate the achievements with its young beneficiaries and partners.

Since its inception, the YEF has unleashed entrepreneurial potential of more than 30,000 emerging and existing entrepreneurs through the business development training, supported the start- up and growth of 17,000 businesses and the creation of 40,000 jobs for young people, by far exceeding the initial outreach and impact targets.


Speaking about the upcoming conference ILO Tanzania Country Director, Mr. Alexio Musindo, said the program will be closing in June 2015 and the Capstone Conference in Tanzania will present results from country-level activities, and investments on skills and entrepreneurship; on improving the productivity of young people, and on sustainable business models and offshoots that are expected to carry forward some activities of the project.


‘The Conference will be a platform to convene a variety of 300 stakeholders, partners and beneficiaries who are committed to entrepreneurship, promoting policies and programs to enhance employment, especially among youth’ said Mr. Jealous Chirove, Chief Technical Advisor.


Conference participants will include policy makers; representatives from different ministries ( e.g. Ministry of Labour and Employment; Ministry of Information, Youth ,Culture and Sports; Ministry of Education and Vocational Training); representatives from donor community ; private sector, industry representatives; civil society youth serving-organizations; researchers; and YEF beneficiaries among many others. These include;


·        promoting a culture of entrepreneurship

·        integrating entrepreneurship in education system

·        increasing the evidence base on what works on youth employment

·        facilitating youth led organizations to implement innovative solutions to youth entrepreneurship

·        facilitating access to business development services and finance for young people


The participants especially the project partners will be expected to make presentations and facilitate discussions based on specific initiatives implemented in collaboration with the project.



The Guest of Honour is expected to be the Hon. Minster of Labour and Employment, Ms. Gaudencia Kabaka,

RITA YAENDELEA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WILAYA YA KINONDONI

$
0
0
01
Meneja Masoko na Mawasiliano kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani} leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya kampeni ya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi za Manispaa ya Kinondoni ambapo amesema hadi sasa zaidi ya wanafunzi Elfu 5 wamesajiliwa na kupata vyeti. Kulia ni Msajili wa Vizazi na Vifo Wilaya ya Kinondoni Bi. Mariam Ling’ande.
02
Msajili wa Vizazi na Vifo Wilaya ya Kinondoni kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bi. Mariam Ling’ande akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani} leo Jijini Dar es Salaam kuhusu taratibu za kufuata ili kupata cheti cha kuzaliwa na kutoa rai kwa wananchi kuacha kutumia vishoka ambao hutoa vyeti bandia badala yake wafike kwenye ofisi za RITA zilizopo kote nchini. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro.
03
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA FATMA SALUM – MAELEZO

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AHUTUBIA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI- MUSOMA

$
0
0
Waziri mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wanawake waliofika kwenye viwanja vya mukendo mjini Musoma kuhudhuria Maadhimisho ya  ya siku ya wakunga dunia yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mukendo, Musoma Mei 6, 2015.2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia wakati muuguzi, Naomi Sarali  alipompima mapigo ya moyo, Mwajuma Juma ikiwa ni moja ya madhimisho ya siku  ya wakunga duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mukendo mjiniMusoma Mei 5, 2015.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Zilote Stephen.
3
Msanii Magesa Julius wakikundi cha sanaa cha Egumba cha mkoani Mara akiongoza kundi hilo kutumbuiza katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani zilizofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mukendo mjini Musoma, Mei 5, 2015.
4
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakunga waliozawadiwa zawadi mbalimbali kutokana na mchango wao katika kuwahudumia wajawazito wanaojifungua katika meneo mbalimbali nchini. Mheshimiwa Pinda alikuwa mgeni rasmi katika  sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani zillizofanyika kitaifa kwenye viwanjavya Mukendo mjini Musoma Mei 5, 2015.

………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imeanzisha Kurugenzi ya Wauguzi na Wakunga katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazowakabili kwenye utoaji wa huduma kwa umma.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 5, 2015), wakati akizungumza wauguzi na wakunga pamoja na wakazi wa mkoa wa Mara kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mkendo, mjini Musoma.
“Nina taarifa kuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha (2015/2016), Kurugenzi hiyo itakuwa na bajeti yake yenyewe itakayotumika kuboresha huduma za wauguzi na wakunga nchini. Haya yote yanafanyika kwa kuwa Serikali inatambua na kuthamini shughuli za wauguzi na wakunga hapa nchini,” alisema.
Alisema mafanikio yaliyofikiwa ya kupunguza vifo vya watoto na vifo vya wanawake yamechangiwa na kazi nzuri zinazofanywa na wakunga licha ya kuwa kada hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi.
Alisema ili kukidhi mahitaji ya wakunga nchini, Serikali imeongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na fani ya uuguzi na ukunga. Akitolea mfano, Waziri Mkuu alisema: “Mwaka 2009 tulikuwa na wanafunzi wa uuguzi na ukunga 617 wa ngazi ya Cheti na 925 wa ngazi ya Diploma. Kufikia mwaka 2014 idadi hiyo iliongezeka kufikia wanafunzi 2,566 wa Cheti sawa na ongezeko la asilimia 315 na wanafunzi 2,294 wa Diploma sawa na ongezeko la asilimia 141 katika kipindi cha miaka mitano.”
Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhara hiyo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi Jamii, Dk. Stephen Kebwe alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi tano barani Afrika ambazo zimeweza kupunguza vifo vya watoto na kuvuka Malengo ya Milenia.
Alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanaume wa mkoa huo na wanaume wote nchini kukubali kutumia njia za uzazi wa mpango ili wawasadie wenza wao kuwa na afya imara. Pia aliwataka waachane na dhana potofu za mitaani bali wafuate tiba na huduma sahihi uzazi wa mpango kwenye vituo vya afya.
“Inashangaza kuona baadhi ya wanaume wanawaacha wake zao eti kwa sababu hawazai, lakini wakiwaacha baada ya muda unasikia yule mama amepata ujauzito, hapo kosa ni la nani?” aliuliza.
“Pia ninawasihi akinababa waachane na dhana potofu kuhusu njia ya kufunga kizazi. Ninawahimiza washiriki njia hii ya kufunga kizazi wanaposhauriwa kufanya hivyo kwa sababu kufunga ule mrija hakumuondolei mwanaume hadhi ya kufanya tendo la ndoa, bado inawezekana hata baada ya kufunga mrija,” alisisitiza.
Mapema, akitoa salamu kwenye maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mkazi wa taasisi ya Mama Ye, Bw. Craig Ferla aliitaka Serikali na wadau waliangalie suala la vifo vya akinamama na watoto kwa jicho la tofauti na kulipigia kelele zaidi ili uwekezaji kwenye fani ya ukunga na uuguzi uweze kuongezwa.
Bw. Ferla ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utepe Mweupe wa Muungano wa Uzazi Salama Tanzania, alisema Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakipigia kelele idadi ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani lakini hakuna mtu anayesema chochote kuhusu vifo vya wanawake na watoto wachanga.
“Watu wanapiga kelele kuwa Taifa limepoteza watu 972 kati ya Januari na Aprili mwaka huu, lakini hatujui kwamba katika kipindi hicho hicho Taifa limepoteza wanawake na watoto 15,000 kutokana na matatizo ya uzazi na hii ni mara 15 zaidi lakini hakuna anayepiga kelele,” alifafanua.
Alisema wanawake 8,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na uzazi wakati watoto 40,000 hupoteza maisha wakiwa katika mwezi wao wa kwanza duniani. “Vifo vya ebola tangu ianze vimefikia 10,000 lakini dunia nzima imeitikia lakini hivi vya akinamama hakuna anayesema chochote.”
“Kuna tatizo jingine ambalo linakwenda kimyakimya nalo ni la vifo vya watoto wanaozaliwa wafu. Hawa wanafikia 47,000 kwa mwaka ambao ni karibu watoto 15,000 kwa miezi minne lakini nalo pia hakuna anayelisemea licha ya kuwa ni janga kubwa kitaifa,” aliongeza.
“Ninaiomba Serikali na wadau wawekeze zaidi katika kada ya wakunga ili tuweze kuokoa maisha ya akinamama na watoto,” alisema Mkurugenzi huyo ambaye kwa muda wote alitumia Kiswahili fasaha na kuufanya mkutano mzima umshangilie kwa nguvu.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
  1. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 5, 2015.

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAFANYA MKUTANO MAALUM WA BARAZA LA WAFANYAKAZI

$
0
0
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi wakifuatilia mada katika mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika hoteli ya J.B Delmonte mapema leo.
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwa katika mkutano maalum wa Baraza la wafanyakazi uliofanyika hoteli ya J.B Delmonte mapema leo.
 Kaimu Katibu Mkuu - Utumishi Bw.HAB Mkwizu (aliyesimama)  akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika ukumbi wa hoteli ya J.B Delmonte mapema leo. Kulia kwake ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Lilian Denis.
 Kaimu Katibu Mkuu - Utumishi Bw.HAB Mkwizu (aliyesimama)  akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma uliofanyika hoteli ya J.B Delmonte mapema leo.
Kaimu Katibu Mkuu - Utumishi Bw.HAB Mkwizu (aliyesimama)  akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma uliofanyika hoteli ya J.B Delmonte mapema leo.

KONYAGI WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KITUO CHA POLISI CHANG’OMBE

$
0
0
 Askari wakisaidia kushusha kwenye gari saruji iliyotolewa msaada na Kampuni ya Konyagi ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL), kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe, kitengo cha upelelezi. Hafla ya utoaji wa vifaa vya ujenzi vikiwemo pia mabati, misumari na fedha ya mafundi vilikabidhiwa jana katika kituo hicho kilichopo Temeke, Dar es Salaam.
 Askari wakisaidia kushusha kwenye gari mabati yaliyotolewa msaada na Kampuni ya Konyagi ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL), kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe, kitengo cha upelelezi. Hafla ya utoaji wa vifaa vya ujenzi vikiwemo pia saruji, misumari na fedha ya mafundi vilikabidhiwa jana katika kituo hicho kilichopo Temeke, Dar es Salaam.
 Askari wakisaidia kushusha kwenye gari mabati yaliyotolewa msaada na Kampuni ya Konyagi ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL), kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe, kitengo cha upelelezi. Hafla ya utoaji wa vifaa vya ujenzi vikiwemo pia saruji, misumari na fedha ya mafundi vilikabidhiwa jana katika kituo hicho kilichopo Temeke, Dar es Salaam.
 Inspekta John Mkweru (kushoto) akiangalia msaada wa misumari uliotolewa na Konyagi kwa kituo hicho.

  Mkaguzi wa Hesabu wa Konyagi, Thomas Munema (kulia), akikabidhi MISUMARI YA KENCHI  KWA DEPUTY RCO WA CHANG’OMBE SP RAMADHANI KINGAI.
Gari la Konyagi lililobeba msaada huyo.
 Mkaguzi wa Hesabu wa Konyagi, Thomas Munema  (kushoto), akimkabidhi nyaraka za msaada huo, Inspekta Philip Bura.
 Mkaguzi wa Hesabu wa Konyagi, Thomas Munema (kushoto), akimkabidhi fedha Inspekta Philip Bura kwa ajili ya  mafundi watakaojenga kituo hicho.
Jengo la ofisi ambalo vifaa hivyo vitatumika kujengea.

MGOMO WA MADEREVA WAPATA MUAFAKA,MABASI YAANZA SAFARI

$
0
0
Na Bakari Issa,wa Globu ya Jamii-Dar es Salaam. 

 Mgomo wa Madereva uliodumu kwa takriban siku moja na ushee, hatimaye umepata muafaka baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni,Paul Makonda kuusuluhisha kwa kusaini makubaliano na Uongozi wa Chama cha Madereva. 

 Makubaliano hayo yaliitaka Serikali kuboresha Mikataba kwa Madereva,malipo kwa madereva hao,pamoja na tatizo la ukaguzi wa magari ili kuondoa usumbufu kwa madereva hao,na kuiomba Serikali kufanya ukaguzi huo kwa siku moja tu. 

 Akizungumza na Madereva hao,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda amewataka Madereva hao kuachana na mgomo huo na kuwaahidi Madereva hao kuyafanyia kazi madai yao katika muda ambao wamekubaliana usiozidi saa 4 asubuhi kesho. 

 Aidha,Makonda amesema katika madai hayo imeundwa Tume ambayo itashughulikia madai hayo pamoja na kuwahakikishia Madereva hao kuwepo na mwakilishi katika Tume hiyo iliyoundwa,ambayo itajadili masuala ya Mkataba,malipo,matibabu pamoja na suala la kusoma kwa Madereva hao. 

 Pia,Makonda amelitaka Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni kuwaachia Madereva ambao tayari walikua wamekamatwa kutokana na kuonekana kufanya fujo katika mgomo huo katika Soko la Urafiki jijini Dar es Salaam. Kwa Upande wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Madereva,Rashidi Salehe amemuomba Mkuu wa Wilaya kutatua madai ya Madereva hao ili kuondoa mgomo ambao unakwamisha usafirishaji wa abiria. 

 Baadhi ya Madereva na Makondakta wa Mabasi wanaondelea na Mgomo, wakiwa wamekaa juu ya Kontena zilizopo kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es salaam kusubiria mustakabali wao, huku ulinzi Mkali wa Jeshi la Polisi ukiwa umetawala eneo hilo. 

 Ghafla likazuka tukio la kurushwa mawe kutoka kwa watu wasiojulikana waliokuwa nje ya Stendi hiyo na kupeleke watu wote waliokuwa kwenye eneo hilo kukusanyika sehemu moja ili kujinusuru. Hali ilikuwa tete pale mawe yalipokuwa yakirushwa, na kupelekea baadhi ya viongozi pamoja na wanahabari waliokuwepo kwenye eneo hilo kukusanyika sehemu moja. hivyo polisi walilazimika kutumia mbinu zao na kufanikiwa kulituliza tukio hilo. 
 Baadhi ya Madereva na Makondakta wa Mabasi wanaondelea na Mgomo, wakiwa wamekaa juu ya Kontena zilizopo kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es salaam kusubiria mustakabali wao, huku ulinzi Mkali wa Jeshi la Polisi ukiwa umetawala eneo hilo.
 Ghafla likazuka tukio la kurushwa mawe kutoka kwa watu wasiojulikana waliokuwa nje ya Stendi hiyo na kupelekea watu wote waliokuwa kwenye eneo hilo kukusanyika sehemu moja ili kujinusuru.
 Hali ilikuwa tete pale mawe yalipokuwa yakirushwa, na kupelekea baadhi ya viongozi pamoja na wanahabari waliokuwepo kwenye eneo hilo kukusanyika sehemu moja. hivyo polisi walilazimika kutumia mbinu zao na kufanikiwa kulituliza tukio hilo.

 Baadhi ya wanahabari wakinawa maji kufuaria moshi wa Mabomu ya Machoni yaliyokuwa yakipigwa Ubungo mchana wa leo.
 Ulinzi ulitawala eneo lote la Ubungo leo.
 Baadhi ya Madereva na Makondakwa wao wakimzogoa mmoja wa Viongozi wao alikubali kuzungumza na Viongozi wa Serikali waliofika eneo hilo.
 Muda mfupi baadae, Aliwasili Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe ambaye alipokelewa kwa shangwe na Madereva hao.

Shangwe zikiendelea.
Mmoja wa viongozi wa Madereva akiwasihi wenzake kutulia ili kuwasikiliza viongozi waliokwenda kuwasiliza.

PRESIDENT KIKWETE MEETS RAJIV SHAH

$
0
0
unnamed
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets former USAID Administrator Rajiv Shah in New York shorlty before the commencement of the first meeting of the High Level Panel on The Global Response to Health Crisis.The panel chaired by President Kikwete was appointed by the UN Secretary General Ban Ki Moon on April this year to make recommendations to strengthen national and international systems to prevent and manage future health crises taking into account lessons learnt from the response to the outbreak of Ebola.The panel is expected to submit its report to the Secretary General at the end of December this year.
(photo by Freddy Maro)

RAIS WA ZANZIBAR DK.ALI MOHAMED SHEIN AWAFARIJI WALIOPATWA NA MAAFA YA MVUA ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimfariji Bibi Fatma Abdalla Turufino Mkaazi wa Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea wananchi wa sehemu hiyo  waliopatwa  na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua   iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora, [Picha na Ikulu.)
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na wasaidizi wake alipofika Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar leo wakati alipofanya ziara ya hafla kutembelea wananchi wa sehemu hiyo  waliopatwa  na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua   iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora,
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wa Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar wakati alipofanya ziara ya hafla leo  kutembelea wananchi wa sehemu hiyo  waliopatwa  na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua   iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora,
4
Hapa  ni Mtaa wa Mwanakwerekwe ambapo pamefanyika shimo kubwa akama linavyoonekanwa kutokana na mvua  iliyonyesha juzi na kupelekea uharifu ambao fedha nyingi zitatumika kufukia eneo hili pia Rais wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  alitembelea wakati alipofanya ziara ya makusudi leo kutembelea maafa mbali mbali yaliyotokea kutokana na Mvua hiyo.
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Injinia Ramadhan China wa Idara ya Ujenzi wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia maafa mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa sehemu hiyo  kwa kuvunjikiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali, 
6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed  leo wakati  wakati alipofanya ziara ya hafla ya  kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia maafa mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa sehemu hiyo  kwa kuvunjikiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,
7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed  (kulia) wakati  wakati alipofanya ziara ya hafla ya  leo  kutembelea Bwawa la Maji la Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia namana lilivyofurika Maji ya  mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali kwa Wananchi,
8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Tomondo Mohamed Iddi (kulia) alipofika leo kuangalia maafa yaliyomkuta Bibi Mwanahamis Takrima Mohammed (aliyekaa) kwa kuvunjikiwa na nyumba yake  kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali (wa pili kulia) Mkuu wa Wilaya Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,
9
Baadhi ya Nyumba za wananchi wa Ziwamaboga Wilaya ya Magharibi zilizoathirika kwa kuingiliwa na maji ya mvua mkubwa iliyonyesha juzi na kepelekea  hasara mbali mbali kwa Wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni mwa ziwa hilo ambapo leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alitembelea na kuona hasara zilizotokea akiwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali.
10
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimueleza jambo Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud wakati alipotembeleabaadhi ya Nyumba za wananchi wa Ziwamaboga Wilaya ya Magharibi zilizoathirika kwa kuingia na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kepelekea  hasara mbali mbali, katika ziara hiyo Mhe, Rais alifuatana na Viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,

PRESIDENT KIKWETE CHAIRS THE HIGH LEVEL PANEL ON THE GLOBAL RESPONSE TO HEALTH CRISIS

$
0
0
2
The UN Secretary General Ban Ki Moon welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to his New York Office where the President chaired The High Level Panel on Global Response to Health Crisis.(photos by Freddy Maro)

PRESIDENT KIKWETE MEETS ANTI EPIDEMIC HIGH LEVEL PANEL MEMBERS IN NEW YORK.

$
0
0
4
The Chairman of the High Level Panel on The Global Response to Health Crisis President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, The Un Secretary General Ban Ki Moon(Third Left) pose fro a group Photo with other panel members at the UN Headquarters in New York this afternoon. Other panel members in the picture from left are, Marty Natalegawa(Indonesia), Micheline Calmy Rey(Switzeland) fourth left,Celso Amorim from Brazil(second right) and Rajiv Shah(right).
On April this year the UN Secretary General Ban Ki Moon appointed a six member High Level panel to make recommendations to strengthen national and international systems to prevent and manage future Health Crises taking into account lessons learnt from the response to the outbreak of Ebola Virus disease.
(photo by Freddy Maro)  
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images