Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

CHAWAKAMA YAFANYA ZIARA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akizungumza na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CHAWAKAMA, hawapo pichani) walipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof. Herman Mwansoko, na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo
2
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CHAWAKAMA) wakisikiliza kwa makini walipofanya ziara katika ofisi za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam.
3
Mkurugenzi Msaidizi Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akizungumza na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (hawapo pichani) walipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam.
4
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wanne kulia) katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof. Herman Mwansoko, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo na wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

Tazama sehemu ya pili ya kipindi cha ‘UBISHI’

$
0
0

Katika mwendelezo wa kipindi cha ‘Ubishi - Komaa Upate Pesa’, wiki hii Bwana Costantine Magavilla anakuletea sehemu ya pili iitwayo ‘Kazi ni Tabia’. Kazi ni gumzo kwa vijana wengi wa mjini ila ni kitu gani kinacho wachochea vijana kufanya kazi haswa na je madhara yake ni nini kwao. Pata majibu kwa kutembelea www.magavilla.com au kwa kubofya hapa https://www.youtube.com/watch?v=PY-QUloAZXY


Usikose kufuatilia vipindi hivi vinavyolenga kuelimisha, kukuhamasisha utazame upya maisha yako upateujasiri wa kubadili fikra na kufanya yako kila wiki siku ya Jumanne.


Bwana Costantine Magavilla ni mwandishi wa kitabu kiitwacho 'Life and You' na ni mhamasishaji maarufu Tanzania katika makongamano mbalimbali kuhusiana na maendeleo binafsi na mabadiliko ya kibiashara. Ni mdau mkubwa wa masuala ya masoko hususan katika kutangaza biashara na miongoni mwa kazi zake ni kuwahamasisha vijana kujituma na kuchangamkia fursa.


 Mwisho wa taarifa.

Imetolewa na Mancom Limited kwa mawasiliano zaidi tuandikie kupitia info@mancom.co.tz aucostantine@magavilla.com.

Ziara ya Mheshimiwa William Lukuvi Mkoani Mwanza hivi karibuni

$
0
0
  Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bw Manju Msambya (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bw Baraka Konisaga (Kulia),ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakimkaribisha Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi muda mfupi kabla ya Mheshimiwa Lukuvi kupoekea ripoti ya awali ya tume ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza leo 
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bw Baraka Konisaga akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi wakati wa kupokea taarifa ya tume ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza ambayo imekuwa kero kwa wananchi wa jiji hilo katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo.
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akijadiliana jambo na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bw Manju Msambya Kabla ya kuwasilishwa kwa ripoti ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza kufuatia tume iliyoundwa  na Mheshimiwa Waziri mwezi uliyopita. 
1.       Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akisisitiza jambo wakatyi alipozungumza na watendaji wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) mara baada ya kupokea ripoti ya kubaini vyanzo vya migogoro ya ardhi katika jiji la Mwanza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo.Picha/ Clarence Nanyaro

NMB YAKABIDHI HUNDI YA SH. BILIONI 1.5 KUCHANGIA MADAWATI

$
0
0
 unnamed
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa Kaimu Mtendaji  Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Tom Borghols  mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 1.5 ukiwa ni mchango wa Benki ya NMB kwa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili zisaidie kutatua tatizo la madawati kwa shle za msingi nchini. Kiasi hicho cha fedha kitatolewa kwa miaka mitano. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepokea hundi ya mfano (dummy cheque) yenye thamani ya sh. bilioni 1.5 kutoka benki ya NMB zikiwa ni mchango wa taasisi hiyo kwenye kampeni ya uchangiaji madawati kitaifa.

Akizungumza na Waziri Mkuu ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam jana jioni (Jumatano, Aprili 29, 2015), kabla ya kukabidhi hundi hiyo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Tom Borghols alisema wameamua kutoa mchango ili kusaidia kupunguza tatizo la uhaba wa madawati linalozikabili shule za msingi na za sekondari hapa nchini.

“Tunaelewa kwamba shule nyingi hapa nchini zinakabiliwa na uhaba wa madawati … tunaamini kuwa elimu bora inachangiwa pia na mazingira mazuri ya kusomea ikiwa ni pamoja na kukaa kwenye madawati wanapoandika. Kama sehemu ya mchango wetu kwa jamii (CSR), tumeamua kutenga sh. bilioni 1.5 ili zisaidie kupungua tatizo hilo,” alisema.

Akipokea mchango huo, Waziri Mkuu aliushukuru uongozi wa benki hiyo ulioambatana na Bw. Borghols kwa kuamua kusaidia juhudi za Serikali kutatua tatizo hilo. Alisema mchango huo ni mkubwa na anaamini kwamba utawachochea wadau wengine kuchangia juhudi za Serikali kutatua tatizo la madawati nchini.

“Nimecheki na watu wangu kwa kweli mahitaji ni makubwa lakini naamini mchango wenu utasaidia kupunguza tatizo la madawati kwa kiasi fulani. Tunawashukuru kwa uamuzi wenu wa kuchangia suala hili la kitaifa,” alisema.

Hadi sasa Serikali inahitaji kununua madawati 1,016,476 kwa ajili ya shule za msingi na za sekondari. Kati ya hayo, madawati 892,772 yanahitajika kwa ajili ya shule za msingi na madawati 123,704 yanahitajika kwa ajili ya shule za sekondari.

Madawati hayo yote yataigharimu Serikali kiasi cha sh. bilioni 91.4/- kwa gharama ya sh. 90,000/- kwa kila dawati.

Hata hivyo, Serikali iliamua kutenga fedha za chenji ya RADA ili zitumike kununua madawati na vitabu. Fedha hizo, zilisaidia kununua madawati 168,163 kwa bei ya sh. 90,000/- kwa dawati moja.

(mwisho)

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
ALHAMISI, APRILI 30, 2015.

UJUMBE WA BODI YA TRA WAKUTANA NA DR. SHEIN

$
0
0
tr1 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya TRA Benard S.Mchonvu wakati alipoongoza ujumbe wa Bodi hiyo leo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais.tr2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na ujumbe wa Bodi TRA ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais leo asubuhi ukiongoza na Mwenyekiti wake Benard S.Mchonvu (wa tatu kushoto) .tr2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na ujumbe wa Bodi TRA baada ya mazungumzo yaliyofanyika  Ikulu Mjini Zanzibar  leo asubuhi (kushoto)  Mwenyekiti wake Benard S.Mchonvu ( katikati) Rished Bad TRA Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.]

WAKIMBIZI KUTOKA NCHINI BURUNDI WALIOKIMBIA MWAKA 1972 WAPEWA URAIA

$
0
0

KT3Mmoja wa waliokuwa wakimbizi akiwa amebeba mwanaye kifuani kama anavyoonekana akielekea eneo la kupokelea cheti chake cha uraia na kuwa raia mpya wa Tanzania, hivyo kusahau yaliyopita na kuanza ukurasa mpya wa maisha katika nchi ya Tanzania.kama unavyomwona akiwa na furaha tele machoni kwa tabasamu lake.KT4Baada ya kukamilisha zoezi la ugawaji na upokeaji wav yeti vya uraia hawakuweza kumsahau mungu wao walikwenda kanisani na kukusanyika kumwomba mungu aweze kuwasaidi katika maisha mapya ya uraiani na kuepukana na taabu na adha za ukimbizi. Hapo wapo kanisani moja ya kanisa lililoko eneo la kijiji cha Lugufu Makazi hayo ya Mishamo.
 (Picha zote na Kibada Ernest Kibada. Makazi ya Mishamo Mkoani Katavi)

WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA DANGOTE

$
0
0

CBA YAHIMIZA WATANZANIA KUCHANGAMKIA MIKOPO YA NYUMBA

$
0
0
Meneja Masoko wa kampuni ya AVIC International,Bw.He Xianlong (katikati) akimwonyesha Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania,Bw.Julius Mcharo na maofisa alioambatana nao ramani za nyumba  zilizojengwa kwa ajili ya kuuzwa wakati wa ziara ya maofisa wa CBA walipotembelea mradi huo leo. CBA imeingia mkataba wa kutoa mikopo kwa wananchi wanaotaka kununua nyumba hizo kwa ajili ya makazi
Maofisa wa CBA Na Avic wakiangalia nyumba ambazo  zimejengwa kwa ajili ya kuuzwa kwa wananchi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CBA Tanzania,Bw.Julius Mcharo  na maofisa wengine wa benki hiyo wakiwasili katika eneo la Kigamboni walipofanya ziara ya kutembelea nyumba za mradi wa Avic International,CBA imeingia mkataba wa kutoa mikopo kwa wananchi wanaotaka kununua nyumba hizo kwa ajili ya makazi.Wengine pichani ni maofisa waandamizi ya Avic.
Meneja Msaidizi wa kampuni ya AVIC International,Bw.Li.Jiayin (katikati) akimwonyesha Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania,Bw.Julius Mcharo eneo la mradi  wa  uwekezaji wa ujenzi wa nyumba za kuuza wakati wa ziara ya maofisa wa benki hiyo kutembelea nyumba hizo. CBA imeingia mkataba wa kutoa mikopo kwa wananchi wanaotaka kununua nyumba hizo kwa ajili ya makazi.

KLABU YA MICHEZO YA RIADHA YA DAR ES SALAAM ‘DAR RUNNING CLUB’ YAANDAA MASHINDANO YA RIADHA YA MARATHON MEI 2 2015

$
0
0
Klabu ya michezo ya riadha ya Dar Es Salaam “Dar Running Club” (DRC) imeandaa mashindano  ya  mbio yajulikananyo kama “Mayday marathon” yatakayofanyika tarehe 02Mei 2015 yatakayoanza na kumalizika katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay (Police Officers Mess).
Mgeni rasmi atakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania  Inspekta Generali wa Police Ernest Jumbe Mangu (IGP).

Akizungumza na waandishi wa habari Mlezi wa Klabu ya DRC Mkuu wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni bwana Camillus Wambura) amesema DRC ni klabu ambayo ilianzishwa rasmi kutokana na makundi mawili tofauti yenye malengo sawa kimichezo, yaani Kinondoni police jogging club kutoka Polisi mkoa wa Kinondoni na Dar Es Salaam Athletic Club yenye washiriki kutoka maeneo mbali mbali ya Dar Es Salaam wakaamua kuungana na kuwa DRC. 

DRC ina madhumuni makubwa  ya kuendeleza michezo ya riadha nchini mpaka nje ya nchi na kuhimiza afya njema kimwili na kiakili, lakini pamoja na hayo muungano huu wa klabu unasaidia sana kuimarisha mahusiano  kati ya  Polisi na raia, hii inasaidia sana katika usalama na kukuza na kuendeleza dhana ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa jamii. Aliongezea…
 
Naye Captain wa DRC bi (Stella Mandago, na mratibu wa mashindano haya amesema kuwa Mashindano haya yanatarajia kushirikisha wanamichezo mbalimbali kutoka hapa nchini na  nje ya nchi pia, mashindano haya yatakuwa na washiriki watakao shiriki katika mbio za kilometa ishirini na moja nukta moja (21.1km) na kilomita kumi (10.0Km) yakiwa na lengo la kukuza na kuendeleza michezo ya riadha Tanzania na nje ya nchi ili kuwawezesha wanamichezo kufikia hatua za kimataifa na kuhimiza maisha yenye afya pia kudumisha mahusiano baina aya police na jamii.

 Klabu ya michezo ya Riadha “Dar Runing Club” inachukua fursa  hii kukukaribisha kushiriki mbio hizi zinazotarajiwa kuanza majira ya saa kumi na mbili asubuhi 12:00 katika viwanja tajwa hapo juu, aliongezea…..

Kutakuwa na zawadi kwa washindi kumi wa kwanza kwa wanawake na wanaume kama ifuatavyo kwa nusu marathoni ya km 21

 Mshindi wa kwanza  TZS 1,100,000
Mshindi wa pili   TZS 800,000
Mshindi wa tatu TZS 600,000
Mshindi wa nne TZS 350,000
Mshindi wa tano TZS 300,000
Mshindi wa sita TZS 250,000
Mshindi wa saba TZS 200,000
Mshindi wa nane TZS 1500,000
Mshindi wa tisa of TZS 100,000
Mshindi wa kumi of TZS 50,000

Kutakuwa pia na washindi wa 3 kwa mbio za Km 10 kama ifuatavyo

Mshindi wa Kwanza  TZS 500,000
Mshindi wa PIli  TZS 300,000



Mshindi wa tatu  TZS 200,000

WATAALAMU WA KUJITOLEA WAKIKARIBISHWA NCHINI

$
0
0
1
Mtaalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani Bw. Shota Yanagisawa (aliyesimama) akijitambulisha kwa Kaimu Katibu Mkuu – Utumishi Bw. HAB Mkwizu katika hafla fupi ya kukaribishwa nchini iliyofanyika Utumishi mapema leo.
2
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akiwakaribisha wataalamu wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kuja kujitambulisha Utumishi.
3
Wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani wakishukuru baada ya kukaribishwa.
4
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akiagana na Wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha iliyofanyika Utumishi.

WAKUU WA TAASISI ZA TAKWIMU WA NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA JIJINI DAR

$
0
0

th5Mtendaji Mkuu wa  Taasisi ya  Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi  za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.
th2Bw. Andry Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la  watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za Afrika linalojadili masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania wenyeji wa mkutano huo.th3Baadhi ya watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala linaloendelea jijini Dar es salaam.th4Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Takwimu Barani Afrika (AFRISTAT) pia mtaalam wa Takwimu kutoka nchini Cameroon Bw. Martin BALEPA akiwasilisha mada kuhusu namna nchi za Bara la Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kutumia takwimu sahihi.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AREJEA NCHINI BAADA YA KUHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC, JIJINI HARARE, ZIMBABWE.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake walioshiriki katika Mkutano wa dharura wa SADC, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo kwenye Hoteli ya Rainbow Jijini Harare, Zimbabwe, jana Aprili 29, 205. Makamu wa Rais amerejea nchini jana kuendelea na majukumu ya Kitaifa. 
R2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na baadhi ya viongozi wenzake wakitoka kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa dharura wa SADC jana. 
R3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya Zimbabwe, huku akipunga mkono kuaga wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Zimbabwe jana Aprili 29, 2015 kurejea nchini. Kushoto kwake ni mkewe mama Zakhia Bilal. R4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajab, wakati akiondoka kurejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC, jijini Harare, Zimbabwe jana April, 29, 2015. R6Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akimkabidhi Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax, mfano wa funguo kama ishala ya makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, wakati wa Mkutano wa dharura uliofanyika jana Aprili 29, 2015 kwenye Hoteli ya Rainbow jijini Harare, Zimbabwe.
Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika. Picha na OMR 

UFAFANUZI WA SSRA KUHUSU KANUNI YA UWIANISHAJI WA MAFAO YA PENSHINI YA MWAKA 2014

IFIKAPO MACHI MWAKANI TATIZO LA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM LITAKUWA HISTORIA

$
0
0
 Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
IFIKAPO machi mwakani tatizo la umeme jijini Dar es Salaam itakuwa historia  kutokana na kukamilika  kwa miundombinu  ya mitambo ya  umeme ifikapo machi mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene katika ziara ya  ukaguzi wa miradi ya umeme ya  Kurasini, Mbagala pamoja na Kinyerezi  jijini Dar es Salaam leo.

Ziara hiyo  iliyoanzia katika mitambo ya Umeme Wizarani hapo na kuelekea,Kurasini na Mbagala ikiwa na lengo la  kusogeza miundombinu ya umeme karibu na watumiaji wa umeme.

Simbachawene amesema kuwa  kuna miradi minne ambayo mpaka sasa inafanyiwa kazi kwa uhakika  inayotegemewa kusambaza Umeme kwa watumiaji bila kuwa n amatatizo ya  umeme.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  amesema kuwa matatizo mbalimbali ya  ununuzi wa Luku za umeme nayo yanafanyiwa kazi kwa  kuyahimiza makampuni nayoshirikiana na TANESCO katika uuzaji wa umeme ili waweze kuimarisha huduma hizo.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akipewa maelekezo leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  kuhusiana na uboreshaji wa  Mtambo wa umeme uliopo katika wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene  akikagua Mtambo wa umeme uliopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
 Mitammbo ya umeme iliyopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KIFO CHA MBITA: CCM YATOA SALAAM ZA RAMBIRAMBI

$
0
0
SALAAM ZA RAMBIRAMBI ZILIZOTOLEWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI NDUGU ABUDLRAHAMAN KINANA WAKATI WA KUAGA MWILI WA BRIG. GEN. HASHIM MBITA (Mst)
TAREHE 29 APRILI, 2015 – LUGALO DAR ES SALAAM

Ndugu Rais, Amiri Jeshi Mkuu na Ndugu Waombolezaji,

Maisha ni safari na kila safari huwa na mwisho wake,  Tuko hapa kwa kuwa safari ya Brig. Gen. Hashim Mbita duniani imefika ukingoni.  Tumekusanyika hapa siyo kuhuzunika bali kujivunia safari ya mafanikio makubwa ya Mwanamapinduzi, Mpiganaji, Mwanadiplomasia, Mwanahabari, Mwanasiasa na Mzalendo wa mfano.

Mwanasayansi mashuhuri Albert Enstain aliwahi kusema kuwa, thamani ya mtu itapimwa kwa mchango wake kwa jamii siyo kwa kile alichokipata kutoka kwa jamii yenyewe.  Hakuna ubishi, Brig. Gen Mbita alitoa mchango mkubwa kwa Watanzania na Waafrika.  Aliipenda na kulitumikia Taifa lake.  Alishiriki kikamilifu kulijenga na kuliimarisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika miaka ya awali na aliongoza Chama cha TANU kwa ufanisi.  Lakini mchango na umahiri wake ulidhihirika katika kuiongoza Kamati ya Ukombozi ya Bara la Afrika.

Kwa kumbukumbu zilizopo kila kazi na jukumu alilopewa Brig. Gen. Mbita iwe Jeshini, Serikalini, katika Chama, katika kuongoza Ukombozi na baadaye kuandika historia ya Ukombozi, aliteuliwa kwa makusudi maalum na kwa malengo maalum.  Alipelekwa Uingereza kutoka Ikulu kwa lengo la kusaidia kulijenga Jeshi la Wananchi Tanzania liwe la kizalendo baada ya maasi ya mwaka 1964. Kwa kuamini kuwa Chama imara ndicho kinachotoa uongozi bora kwa Taifa, Brig. Gen. Mbita aliteuliwa kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa TANU ili kuleta ufanisi na nidhamu katika Chama.

Kuna msemo maarufu jeshini usemao Kamanda aliye jasiri anaweza kuwa na bahati. Lakini hakuna Kamanda anayeweza kuwa na bahati bila ya kuwa jasiri. Ujasiri aliokuwa nao Brig. Gen. Mbita ndiyo iliyokuwa sababu ya kuteuliwa kwake kuiiongoza Kamati ya Ukombozi wa Afrika.   

Alishiriki kuvijenga vikosi vya Frelimo (Msumbiji), ZANU-PF (Zimbabwe), SWAPO (Namibia), ANC (Afrika Kusini), MPLA (Angola), MOLINACO (Comoro), PAIGC (Guinea Bissau, Cape Verde)  na vyama vingine.  Aliviandaa vikosi hivi kupambana na majeshi makubwa yenye silaha nzito na za kisasa na yenye nguvu nyingi.  Lakini mwaka 1994, Brig. Gen Mbita alihitimisha kazi ya Ukombozi wa Afrika kwa ushindi mkubwa.

Chama Cha Mapinduzi kinatambua na kuthamini mchango na kazi kubwa iliyofanywa na Brig. Gen. Mbita katika kukiendeleza na kukiimarisha Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi. Katika maisha yake kazini na hata baada ya kustaafu aliendelea kutoa ushauri, maoni na wakati mwingine kutoa uzoefu wake ndani ya Chama. 

Tutauenzi mchango wake, tutajifunza utendaji wake, tutajitahidi kuiga mwenendo wake na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na ardhi na mwenye kutupa na kutuondolea uhai, ili amuonee huruma mja wake huyu.  Brig. Gen. Mbita atabaki kuwa na nafasi muhimu katika historia ya mapambano dhidi ya ukoloni, ubeberu, ubaguzi wa rangi na uonevu.

Alikuwa kiongozi mwenye msimamo na mwenye kuelewa mambo mengi lakini msikivu. Inawezekana Watanzania wengi hatukumjua kwa kuwa hakushughulika kujulikana. Alikuwa jasiri na vile vile alikuwa na wingi wa unyenyekevu. Ujasiri wake ulidhihirika katika kufanikisha majukumu aliyokabidhiwa lakini unyenyekevu ulimzuia kujinadi.   

Alitanguliza utumishi na kujiepusha na utukufu. Nafasi alizoshika zilikuwa za juu na zenye kuheshimika.  Kama angependa angeweza kupata umaarufu mkubwa katika nafasi aliyokuwa nayo lakini hiyo haikuwa hulka yake.  Maisha na Utumishi wake ni darasa kamili kwetu sote.

Tunawashukuru viongozi waliokuja kuwakilisha vyama mbalimbali kuungana na Watanzania kumuenzi Brig. Gen. Hashim Mbita.  Wanafalsafa wanatuambia ushindi wa kumbukumbu za wale tutakaowakumbuka zitadumu katika mioyo ya watu na katika historia ya Taifa walilolitumikia. Sihitaji kuwashawishi Ndugu waombolezaji wenzangu kukiri kuwa Brig. Gen Mbita atabaki kwenye mioyo yetu na kuendelea kukumbukwa na wananchi wengi wa Bara la Afrika alioshirikiana nao kuwarudishia Uhuru wao na heshima yao.

Kwa kumalizia, kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi natoa pole kwa Mama Mjane, Watoto, Ndugu na Jamaa, Marafiki na kwa Jeshi la Wananchi Tanzania.

Mwenyezi Mungu amfungulie milango ya Pepo.

Imetolewa na:
 
Idara ya Itikadi na Uenezi
Chama Cha Mapinduzi
30/04/2015

Launch of the Tanzania Photographic Journey- 50 Years of the United Republic of Tanzania

$
0
0
Book Launched: Photographic Journey - 50 years of United Republic of Tanzania 
Deputy  Minister of Finance, Hon Adam Milama launched the much anticipated book,  Tanzania Photographic Journey - 50 years of  United Republic of Tanzania (The Union between Tanganyika and Zanzibar 1964 -2014 ) at Serena Hotel this week.
The book celebrates and covers the historic journey of the 50 years of the United Republic Of Tanzania. The book, which comprises of over 444 pages describing in detail the historic journey of Zanzibar and then Tanganyika (Tanzania Mainland), covering the rich historical background and the political journey prior to the Union in 1964 and also the political journey of the factual events from 1964 until 2014.
Javed Jafferji who is the publisher of the book said" It took 17 months to publish this book and it is the best book I have worked in the last 25 years out of 70 books i have published. I am proud that this book will remain a reference manual  for generations of Tanzanians to come"
This book has been blessed by both the existing Presidents, Dr Jakaya Mrisho Kikwete and Dr. Ali Mohamed Shein by both having agreed to do the foreword for this book. Furthermore, it remains to be the only book that carries the foreword of both the Presidents of the United Republic of Tanzania and Zanzibar respectively and furthermore they are the current Presidents in power.
 Left JAVED JAFFERJI and Right Simai Mohammed Said.
 Launching of the book.
Presenting a copy to Daimond who appears in the book as Icons of Tanzania.
 Presenting a Book to Mama Zakia Meghji.
 Signing of the book.
 Diamond proudly showing  the book.

RAIS KIKWETE ATEUA MAJAJI WAWILI WA MAHAKAMA YA RUFAA TANZANIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kuanzia Jumamosi iliyopita, Aprili 24, 2015, taarifa iliyotolewa Dar es Salaam, leo, Alhamisi, Aprili 30, 2025 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) imesema.


Taarifa hiyo imewataja wajaji hao kuwa ni Jaji  Augustine Gherabast Mwarija na Jaji Stella Ester Augustine Mugasha, ambao wote wamekuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tokea walipoteuliwa Novemba 28, 2006.

Kabla ya uteuzi wake, Jaji Mwarija alikuwa Jaji Mfawadhi, Kitengo cha Biashara, Mahakama Kuu, Dar Es Salaam. Kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kati ya mwaka 2003 na 2006.



Aliajiriwa kama Hakimu Mkazi Daraja la Tatu Februari 2, mwaka 1987, baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka 1986.

Naye Jaji Mugasha, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Jaji Mfawidhi, Dar es Salaam. Alikuwa Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha na awali Kanda ya Moshi tangu 2009 hadi alipohamishiwa Mahakama Kuu, Dar Es Salaam.



Aliajiriwa kama Wakili wa Serikali mwaka 1983 baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka huo huo, 1983.


 Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.



30 April, 2015

WARSHA YA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI DAWA ZANZIBAR (ELMIS) KWA WAKURUGENZI NA MAAFISA WA WIZARA YA AFYA.

$
0
0
1
Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad akitoa maelezo na kuwakaribisha washiriki wa warsha ya usambazaji dawa kwa njia ya kielectroniki iliyofanyika Park Hyatt Hotel Shangani mjini Zanzibar.
2
Mfamasia mkuu Zanzibar Habib Ali Shariff akitoa maelezo kuhusu mfumo huo mpya wa kielectroniki ulivyoanza kufanyakazi Zanzibar.
3
Waziri wa Afya Zanzibar Rashid Seif ambae alikuwa Mwenyekiti wa warsha hiyo akitoa muongozo kwa washiriki .
4
Mkurugenzi Usimamizi wa Mifumo ya kielectroniki kutoka Shirika la John Snow Incoparated (JSI) akizungumzia uimarishaji wa mfumo na mafanikio yake kwa washiriki wa warsha hiyo.
5
Meneja wa Zoni ya Unguja ya mfumo mpya wa usambazaji dawa kwa njia ya kielectroniki Biubwa Khamis (aliesimama) akitoa uzoefu wa usambazaji wa  mfumo zamani na huu wa sasa katika warsha hiyo.
6
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya siku moja ya usambazaji dawa kwa njia ya kielectroniki iliyofanyika Park Hyatt Hotel Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

UZINDUZI WA KITABU CHA KUJIFUNZA KILINGALA CHA TSHIMANGA KALALA ASSOSA NA KAVASHA CLUB…

$
0
0
unnamed
Jumapili hii tarehe 03-May-2015, mwanamuziki mkongwe Tshimanga Kalala Assosa atazindua kitabu kilichokuwa kikisubiriwa na watu wengi sana kwa muda mrefu mno.
Ni kitabu cha “kuJifunza LINGALA kwa Kiswahili”.
Uzinduzi huo utaambatana na tukio kubwa sana la wana Dar Kavasha Club pamoja na chakula cha jioni cha pamoja (dinner).
Ni ndani ya ukumbi wa MRC Jumapili (03-May-2015) kuanzia saa 12 hadi saa 3 jioni. MRC ndio ukumbi ambao “Club Raha Leo Show” ya TBC1 ilikuwa inafanyikia.
Tshimanga Kalala Assosa amepata kupiga bendi nyingi kubwa hapa Afrika kama Negros-Success (akiwa na Bolhen na Bavon Marie), Orchestre Lipua Lipua, Orchestre Les Kamale (akiwa na Nyboma, Mulembu na Kizunga) pamoja na Fukafuka zote za Congo DRC. Kwa hapa Tanzania amefanya kazi na Mlimani Park Orchestra, Marquis Original, Orchestre Makassy, Orchestre Mambo Bado, Legho Stars na Bana Maquis.
Mgeni rasmi wa tukio atatangazwa.
Wote mnakaribishwa. Wahi bila kukosa. Kiingilio ni BURE.

Mratibu wa asasi ya Better Living Aid atoa wito kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi!

$
0
0
Watangazaji Hamisa Mussa Lubilo na Deogratius Yagomba wa VOT fm 89.0 wakimuuliza maswali mratibu wa asasi ya Better Living Aid walipomualika leo asubuhi katika kipindi cha Meza huru!
Mratibu wa asasi ya kiraia ya Better Living AidBw Mkala Fundikira leo akiwa amavalia fulana ya mkakati wa Imetosha unaopinga mauaji dhidi ya watu wenye ualbino ambao yeye ni mjumbe wa kamati kuu, ametoa wito kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi mjini Tabora waiunge mkono asasi yake inayodhamiria kujenga vyoo na zahanati katika kijiji  cha Amani kilichopo Ipuli Tabora, kijiji chenye wakazi wazee na wasiojiweza na waishio na gonjwa sugu la ukoma. 

Alitoa wito huo akiongea katika kipindi cha meza huru cha Vot fm89.0 alisema "nawaomba wenye maduka ya vifaa vya ujenzi watuunge mkono kwa kuchangia hata mifuko mitano ya simenti, bati mbili au hata kifaa chochote cha ujenzi ambacho kitataumika katika ujenzi wa vyoo na zahanati katika kijiji hicho alimradi tunahitaji michango ya aina yeyote ile" 
Mkala Fundikira akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na watangazaji wa kipindi cha Meza huru, kipindi kinachoruka ktk kituo cha redio cha VOT fm 89.0 ya Tabora leo asubuhi.
Pamoja na kueleza kuwa asasi yao inayoundwa na marafiki toka mitandao ya jamii kama Facebook  na Viber pia alieleza kuwa tangu waanze kusadia kijiji hicho washapeleka vyakula, vyandarua na masweta kwa nyakati tofauti, pia ikiwemo kulipia upulizwaji wa dawa za kuuwa wadudu pamoja na kunguni ambao walikuwa wakisumbua wakazi wa kijiji cha Amani. 
Mkala akiwa amevalia fulana yenye ujumbe wenye kupinga mauaji kwa watu wenye ualbino ya mkakati wa Imetosha.
Alipoulizwa dhamira ya asasa yao ni kusaidia Tabora tu au na mikoa mingine? Mratibu huyo alijibu "Hapana, Better Living Aid itasaidia na kwingineko pia, kwa mfano tunatafuta wahisani ili tukajenge zahanati kijijini Masweya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Masweya hakuna zahanati pamoja na kuwa pana wakazi zaidi ya 7000, nafikiri wa Tanzania tuwe wahalisia kuwa serikali yetu haitoweza kukidhi mahitaji ya wa Tanzania wote kwa wakati mmoja hivyo basi ni wakati muafaka wa sisi kama jamii kuanza kujitolea na kuwezesha asasi kama yetu kupeleka huduma za afya sehemu kama Masweya"

Fundikira pia alimshukuru Mh Munde Tambwe Abdallah kwa kutoa ahadi ya Mifuko 50 ya simenti, lori 10 za mchanga pamoja na tano za mawe na kokoto , alisema "Tena kabla sijasahau nimpongeze na kumshukuru sasa sana sana Mh Munde Tambwe kwa kutupa msaada ambao ni msingi, kwa maana ya kuwa ahadi yake ndiyo itaanzisha ujenzi wa majengo hayo ya vyoo na zahanati, hivyo basi na wengine wajitolee ili tusonge mbele" 
Hoteli ambamo chakula cha usiku cha uchangishaji fedha kwa ujenzi wa vyoo na zahanati utafanyika baadae mwezi huu jijini Dar es Salaam iliyopo maeneo ya Ocean road.
Aidha asasi hiyo ina mpango wa kuandaa chakula cha usiku jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Southern Sun baadae mwezi huu ambapo Mh Samuel Sitta(waziri wa uchukuzi) amekubali kuwa mgeni rasmi, karamu hiyo itaandaliwa ili kuchangisha fedha za kuwezesha miradi hiyo iweze kukamilika. 

"Bado tupo kwenye hatua za mwanzo za maandalizi lakini tunataraji karamu hiyo ya uchangishaji pesa ifanyike ama mwishoni mwa mwezi wa MEI au mwanzoni mwa mwezi Juni 2015. Pia Fundikira aliwashukuru Mh Aden Ragen(Mbunge wa Tabora mjini), Mh Munde Tambwe(Viti maalum), Sylvester Koka(Mbunge wa Kibaha) na wanachama na wote wa Better Living Aid kwa kuwezesha kifedha upulizwaji wa dawa kijiji cha Amani uliogharimu Tsh Laki 980.

Tembelea mtandao wa betterlivingaid.Blogspot.Com ujue zaidi kuhusu asasi hii na malengo yake au piga namba 0754 666620 kwa maelezo.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>