Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 515 | 516 | (Page 517) | 518 | 519 | .... | 1897 | newer

  0 0

   


   Na Woinde Shizza wa Libeneke la kaskazini blog.
  Jiji la Arusha bado linakabiliwa na changamoto ua ugonjwa ambao unaambukizwa kwa njia ya mkojo(U.T.I) ambao unakuwa siku hadi siku ambapo takwimu za mwaka 2014 zinaonyesha kuwa takribani wagonjwa 32085 walikutwa na ugonjwa huo hali ambayo inakwamisha jitihada za kujiletea maendeleo kutokana na ugonjwa huo.

  Ambapo alisema kuwa hadi hivi sasa hawajagundua tatizo na chanzo halisi cha ugonjwa huo ambao unakuwa kwa kasi sana katika jiji hili la Arusha, hali mabayo inakwamisha jitihada za kupambana na adui maradhi kwa wananchi wake.

  Hayo yameelezwa jana  na kaimu mganga mkuu wa jiji la Arusha Sr,Jane Balalukululiza wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake na kuweza kuelezea ugonjwa huo ambao umekuwa ni tatizo la jiji  kwa wananchi wake,mahojiano hayo yalifanyika ofisini kwake katika jiji hili, mkoa wa Arusha.

  Hata hivyo alisema kuwa rika linaloongoza kwa ugonjwa huo nikuanzia miaka mitano kuendelea hadi watu wazima ambapo hadi sasa hawajagundua chanzo hasa cha ongezeko hilo la ugonjwa wa u.t.i .

  Aliongeza kuwa ingawa kuna viashiria vya sababu vya ugonjwa huo kuwa ni kutoweka mazingira safi ya vyoo ,mazingira pia ya kujisaidia haja ndogo mahali amabpo si salama kwa afya ya mtumiaji eneo hilo hali ambayo inapelekea kupata kwa ugonjwa huo.

   Sr,Jane aliongeza kuwa bado pia kuna changamoto ya kujitokeza kwa wananchi kupima afya zao ili kujua kama afya ni nzuri ama imepata maambukizi yoyote ya magonjwa mbalimbali, ili kuchukua tahadhari na kupata matibabu ya ugonjwa husika.

  Mbali na jitihada za jiji hilo kupambana na adui maradhi ,wameunda mkakati wa kutumia kikosi kazi cha kukagua mazingira ya wananchi wake kuangalia namna ya kuweka mazingira safi ili kuepuka kupata maradhi na kuweka sheria ndogondogo endapo mtu atakiuka basi apelekwe kwenye vyombo vya sheria ili kudhibiti wananchi wakaidi wa taratibu za kuishi na nchi.

  Ameitaka jamii kwa ujumla kuweza kuwa na taratibu ya kupima afya zao kwani hivi sasa ugonjwa huo umekuwa ni kikwazo cha utekelezaji wa majukumu yao.

  Kwa upande wake mwakilishi wa wananchi Bi,Emiliani Msuya aliiomba Serikali kuweza kutenga fungu la kuweza kuwapa elimu wananchi wake ili kuweza kuwafundisha namana ya urtunzaji mazingira ili kuweza kuepuka kupata ugonjwa wa maambukizi ya njia ya mkojo ili kuweza kunausuru kurudisha nyuma jitihada za kujiletea maendeleo kupitia famili na wananchi wake.

  Aliongeza kuwa  wananchi wanatakiwa kuiunda vikundi vidogovidogo ili kuweza kusimsmiana katika kutunza mazingira na si kusubiri pindi Serikali mpaka ianze kampeni ya upimaji na kuweza kuhamasisha wananchi kupima afya zao.

  0 0

  Balozi Amina Salum Ali

  Na mwandishi wako, Washington, DC.

  Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

  Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.

  Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.

  Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika Mungu amlaze pema peponi, Amin.

  Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh.Subira Mgalu amezindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam kupitia kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na kumkwamua kiuchumi.

  Subira ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kumwezesha mwanamke katika kilimo na kumkwa mwanamke kiuchumi iliyofanyika  katika kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

  Subira amesema kufanyika kwa mashindano wilayani kwake ni fursa kwa wanawake kushiriki  kuchukua fomu za ushiriki na kuacha uvivu  na kutaka zawadi ya mshindi wa kwanza itokee wilyani humo.

   Aliongeza kuwa shindano hilo linawapa mwanamke uwezo wa kutambua haki zao umiliki wa ardhi na kuwa na ubunifu wa kuweza kubadilisha mbinu za kisasa za kilimo bora.

  Nae Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona amesema  kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa wenyeji wa shindano hivyo wanawake wa kisarawe wanahitaji kujituma katika kuchangamkia fursa hiyo.


  Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya fursa ambazo watazipata kupitia Shindano la  Mama Shujaa wa Chakula.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu  akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo wakati uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.
    Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam,Eluka Kibona akielezea Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
   Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akizungumza na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula.
   Kikundi cha sanaa cha Sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula.
   Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengine pindi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula litakapoanza.
   Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga Bwana Mohamed Mlembe Akiwashukuru Oxfam kwa kuleta Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Kijijini kwake.
    Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akifurahi kwa Burudani ya Muziki pamoja na wananchi baada ya uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kijijini Kisanga.
    Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua Mama kiuchumi.
    Mh. Subira Mgalu akifurahi pamoja na Baadhi ya kinamama wa kijiji cha kisanga Baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.

   Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu za kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.
   Baadhi ya Wageni waalikwa na wananchi wa Kisarawe wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo wakto akizindua shindano la Mama Shujaa lililofanyika leo katika Kijiji cha Kisanga wilayani humo.

  0 0

  Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale, kukabidhi barabara  ya magari yaendayo kasi kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART) ili zianze kutumika wakati sehemu zilizobaki zikiendelea kukamilika.


  Hayo ameyazungumza Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli katika hafla uzinduzi wa barabara ya Uhuru ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam iliyofanyika leo katika viwanja vya Karume.


  Pia Dkt. Magufuli amemwaagiza  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART), Bi. Asteria Mlambo aharakishe kutafuta mabasi yaendayo kasi ili ifikapo Octoba Mwaka huu yawe yameanza kufanya kazi katika barabara ya Morogoro Road,jijini Dar es Salaam.


  Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.


  “Tatizo la wananchi wa Dar es salaam ni kutokutunza miundombinu pamoja na kutupa taka ovyo hali inayosababisha uharibifu wa miundombinu na kupelekea mafuriko wakati wa mvua”, alisema Meck Sadick.

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam jijini Dar es Salaam leo.
  Sehemu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
  Picha ya Pamoja ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Dar es Salaam pamoja na wananchi wa Manispaa ya Ilala waliohudhuria katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.

  Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Afrika (OAU) marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho .(picha na Freddy Maro).
   Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiuwasilisha mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo tayari kwa kuswaliwa mwili na kwenda kuuhifadhi kwenye nyuma yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo
   Waumini wa Kiislam kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita tayari kwa kuswaliwa mwili na kwenda kuuhifadhi kwenye nyuma yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo
   Sehemu ya waumini wa Kiislam wakisoma dua ya kumrehemu Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita aliezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Kitewita Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Pamoja nae ni Mkurugenzi Fedha, Regina Samakafu (katikati) na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Ngongi
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Katikati ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa benki hiyo, Peter Mapigano na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Teknolojia , Jema Msuya.
  Mkurugenzi wa Mipango wa Benki ya Posta Tanzania (TPB)Bernadethe Joseph Gogadi (kushoto) akifuatilia mkutano huo leo ambapo waandishi wa habari nao walikuwepo kuchukua taarifa kama wanavyoonekana pichani.

  0 0

  Waimbaji wa Glorious Worship Team (GWT) wakilishambulia jukwaa katika Sunday Celebration Season 6.
  Kiongozi wa Bendi ya The Jordan, Daniel Mbepera, akiimba kwa hisia sambamba na bendi yake.
  Wageni waliohudhuria wakisifu na kuabudu sambamba na GWT.
  Mjasiriamali mahiri Afrika na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akitoa somo la ujasiriamali.
  Wageni wakisikiliza somo la ujasiriamali kutoka kwa Shigongo.
  Waimbaji wa GWT wakizidi kutoa burudani kwa washiriki wa Sunday Celebration Season 6.

  KWA mara nyingine, kile Kikundi cha Kusifu na Kuabudu nchini cha Glorious Worship Team (GWT) Jumapili iliyopita kiliendelea na programu yake ijulikano kwa jina la 'Sunday Celebration' ambayo hufanyika kila Jumapili jioni.

  Wiki iliyopita ilikuwa ni Sunday Celebration Season 6 ambapo burudani mbalimbali pamoja na elimu ya ujasiriamali vilitolewa kwa watu waliohudhuria katika Ukumbi uliopo Victoria Service Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  Burudani ukumbini hapo ziliongozwa na Kundi la GWT likishirikiana na The Jordan Band huku elimu ya ujasiriamali ikitolewa na Mwalimu mahiri wa Ujasiriamali Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.
  (PICHA ZOTE NA GWT)

  0 0  0 0
 • 04/29/15--08:45: Article 12

 • 0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 50 kutoka Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) wa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yatakayoanza Juni 2015 katika wilaya hiyo.
   Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  Kinachosambazwa na Kampuni ya TSN, Khamis Tembo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda, akizungumza katika mkutano huo baada ya kutoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
    Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo (wa pili kulia), akimkabidhi jezi na vifaa vya michezo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yaliyoanzishwa na Makonda. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN , Koiya Kibanga.
  Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo akimvalishe moja ya jezi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya mashindano hayo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kushoto), akimkabidhi DC Makonda mpira mmoja kati ya 50 aliyoitoa kwa ajili ya mashindani hayo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN ambayo imetoa msaada wa vifaa hivyo vya michezo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo,Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN Group, Koiya Kibanga, Meneja Masoko na Mauzo wa TSN, Nafsa Soud na Mshauri wa TSN, Francis Bonda 'Kaka Bonda'
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kulia), ambaye ametoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiangalia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya TSN pamoja na Kampuni ya Smart Sports  ambayo imetoa mipira 50 kupitia Mkurugenzi wake, George Wakuganda.

   Suleiman Msuya

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea msaada wa jezi seti 100 na mipira 50 kutoka kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), ambavyo vina thamani ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya mashindano ya mpira wa netibali na mpira wa miguu yatakayoitwa Kinondano Cup.

  Akizungumzia msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondani, Paul Makonda alisema mikakati yake ni kuhakikisha kuwa vijana wa Wilaya hiyo wanatumia vipaji vyao kujikwamua katika umaskini.

  Makonda alisema mashindano hayo yatakuwa ni mpira wa miguu wanaume na wanawake, mpira wa kikapu wanawake na wanaume na mpira wa netibali ambao ni wanawake pekee.

  "Nimedhamiria kuhakikisha kuwa jamii inaondokana na dhana kuwa wakazi wa wilaya hiyo ni watumia madawa na uchangudoa na njia sahihi ni kuwahusisha vijana na kutumia vipaji vyao," alisema.

  Akizungumza baada ya kutoa msaada huyo Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy ambacho ndio wametoa mtaasa huo kupitia TSN, Khamis Tembo alisema msaada huo una lengo la kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

  Tembo alisema kampuni ya TSN inatambua umuhimu wa michezo hivyo kupitia Chilly Willy wameona ni muhimu kutoa msaada huo wa jezi seti 100 na mipira 50 ili kufanikisha malengo hayo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Smart Sport, George Wakuganda ambaye kampuni yake imetoa mipira 50 alisema wameamua kuungana na Mkuu wa Wilaya kwani wao ni wanamichezo.

  Wakuganda alitoa wito kwa wadau wengine kuungana na Mkuu huyo wa Wilaya kwani jitihada zake za kuhakikisha vijana wanatoka katika dibwi la umaskini ni za maana.
  (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungy (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) wakati akiwasilisha mada kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasanii kwenye Jukwaa la Sanaa lililofanyika Jumanne ya wiki hii makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala, Sharif Shamba. Kushoto ni Mwanasheria wa BASATA Deogratius Nchimbi.
  Mwanasheria wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Deogratius Nchimbi (Kushoto) akiongea jambo na wadau wa Sanaa (hawako pichani) mapema wiki hii wakati akihitimisha mjadala kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasanii uliowasilishwa na Meneja Mawasiliano wa mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza hilo kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala, Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
  Mmoja wa wadau wa Jukwaa la Sanaa akiuliza swali kwa Meneja mawasiliano wa TCRA juu ya athari za sheria mpya ya mitandao ya kijamii kwa wasanii na waandishi wa habari.
  Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza la Sanaa la Taifa mapema wiki hii.

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) mapema wiki hii wamelaani matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii miongoni mwa wasanii wakati wa programu ya Jukwaa la Sanaa iliyofanyika makao makuu ya Baraza hilo yaliyoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

  Akiongea wakati akiwasilisha mada iliyohusu ‘Matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasanii’, Meneja mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy alisema kuwa wasanii ni kioo cha jamii hivyo kwa namna yoyote ile hawapaswi kuwa sehemu ya uharibifu wa jamii inayowazunguka au kuharibu wajihi (taswira) yao kwa jamii yao.

  “Unapokuwa kioo cha jamii, unategemewa kuishi kwa kuwa mfano katika jamii yako. Vijana wengi wanaiga kutoka kwa wasanii ambao ni maarufu. Tunatarajia wasanii wawe mfano kwao” alisisitiza Mungi.

  Aliongeza kwamba, msanii anapotumia mitandao ya kijamii kwa kuweka picha chafu, zisizo na maadili au kitu chochote kisicho na staha ni kuchafua wajihi wake mbele ya jamii na hili linampotezea fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi maana hakuna kampuni au asasi itakayopenda kufanya kazi na msanii mwenye sifa mbovu.

  “Wasanii wanapotumia hovyo mitandao ya kijamii wanachafua wajihi wao katika jamii. Wanajikosesha fursa za kimapato. Mfano; mfanyabiashara anapotaka kutangaza shule yake ya watoto wa awali hawezi kutumia msanii mwenye wajihi mchafu na unaoharibu watoto” aliongeza Mungy.

  Alizidi kueleza kwamba wasanii hawana budi kutumia mitandao hii ya kijamii hususan facebook, twitter, instargram, u-tube na kadhalika katika kujitangaza na kuuza kazi zao na zaidi kutenga muda mwingi kutumikia jamii.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa na Masoko wa BASATA, Vivian Shalua alisema kwamba Baraza hilo muda wote limekuwa likisisitiza maadili mema miongoni mwa wasanii maana vijana wengi huwaangalia kama mfano katika maisha yao.

  “Kila mara BASATA limekuwa likisisitiza maadili kwa wasanii wote. Kazi hii ni ngumu na inataka wadau wote kushiriki katika kunyoosha maadili ya wasanii na vijana kwa ujumla” alimalizia Shalua

  0 0

  President of Zimbabwe and Chairman of Southern Africa Development Community (SADC), H.E Robert Mugabe delivers an opening speech at the SADC Extra Ordinary Summit of Heads of State and Government in Harare, Zimbabwe.
  Vice President of The United Republic of Tanzania, H.E Dr. Mohamed Gharib Bilal (R) represented President Jakaya Mrisho Kikwete at Summit.
  Part of the delegates who attended the Summit listen the official opening statement from Chairman of SADC, H.E Mugabe.
  Part of Heads of State and Government who attended the Summit follow up the opening statement. Right is the President of South Africa, H.E Jacob Zuma
  A Cultural group entertains the Heads of State and Government and other delegates in the Conference hall. 
  The story by Foreign Ministry's Staff.
  Heads of state of the Southern African Development Community (SADC) today adopted an Industrial Development Strategy to leverage the region's resources for sustainable development The strategic plan and roadmap was developed by a Ministerial Task Force mandated by the Heads of State last August. It is a three-phase programme emphasizing efficient use of resources, value edition, diversification and competitiveness to propel the region into a high tech industrial entity by 2063.

  The summit directed secretariat to compile the requisite budget and the Ministerial Council to prepare implementation plan. The Heads of State also approved revision of the Indicative Regional Development Plan, which now gives industrial development top priority.Development of infrastructure, including energy, water, roads and railways and ICT is ranked second while peace and security is third, followed by social services.

   

  The President of the United Republic of Tanzania, H.E. Jakaya Kikwete, was represented by the Vice-President, Dr. Mohamed Gharib Bilal at the Summit, which was attended for the first time by newly elected Presidents Edgar Lungu of Zambia, Philip Nyusi of Mozambique, Hage Geingob of Namibia and Lesotho Prime Minister Pakalitha Mosisili. The Summit chaired by Zimbabwe President Robert Mugabe was also attended by the President South Africa , Jacob Zuma, King Mswati of Swaziland and Mauritius Prime Minister Anerood Jugnauth.

  The Heads of State and Government Further endorsed a plan to inaugurate  the tripartite Free Trade Area (FTA) combining the SADC, EAC and COMESA blocks in June.

  They agreed that the creation of a continental FTA earlier scheduled for 2017 be pushed back to 2020.

  In her remarks to the Summit, the SADC Executive Secretary, Dr. Stergomena Lawrence Tax, said the Industrial Development Plan would boost the region's gross product and income per capital. Chairman Mugabe said member states should brace to finance the plan because western countries were unlikely to help. 

  "Those who benefit from our underdevelopment cannot be expected to help us," he said. He lamented that although SADC countries ranked highly in global mineral and agricultural output, more than two thirds of their population was below the poverty line.

  President Mugabe formerly handed over the Regional Peace Training Centre (RPRC) facility to Dr. Tax as part of the Summit opening ceremony. The facility for the training of military personnel, police and civilians has been donated to SADC by the Zimbabwe government.


  0 0

  Wachezaji wa timu ya Umbrella Garden wakielekea katika lango kupiga mikwaju ya Penalti mara baada ya kutoka sare ya goli 1-1
  mchezaji wa Nyota Fc akipiga Penelti katika lango la Umbrela Garden
  Naibu Meya wa jiji la Arusha Prosper Msofe akifurahia mashindano ya Ndondo Cup katika Viwanja vya Aicc Jijini Arusha.
  .Mashabiki waliojitokeza Uwanjani hapo wakifuatilia meza kuu ambayo haipo Pichani
  Mashabiki wa Nyota Fc wakishangilia Ushindi mara baada ya timu yao kuinyuka Umbrella garden magoli 6-5
  Mlinda mlango wa timu ya Nyota Fc Hamis maarufu kama Dida akiwa anatizama mpira wavuni.

  Ashura Mohamed-Arusha

  Timu ya  Soka ya Nyota  Fc imeichapa timu ya Ambrella Garden Fc  kwa  Magoli  Sita kwa Matano na kufanikiwa kuondoka na kombe la Ndondo Cup  Sambamba na Kitita cha Shilingi  Laki  Tano Taslimu  katika fainali za Ndondo Cup zilizofanyika katika viwanja vya Aicc vilivyopo Jijini Arusha.

  Akizungumza wakati wa fainali hizo Naibu meya wa Jiji la Arusha Prosper Msofe alisema kuwa mashindano hayo ya ndondo Cup yamewakutananisha vijana wengi ambao wamepata fursa ya kuonesha vipaji  vyao.

  Prosper Msofe alisema kuwa mkoa wa Arusha una sifa nyingi lakini katika upande wa Soka kwa sasa Hakuna timu ambayo ipo imara ambao inafanya vizuri katika ligi mbali mbali hapa nchini.

  Aidha Msofe alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanaibua vipaji zaidi na kutengeneza timu moja ya mkoa Jiji la Arusha limepanga kununua eneo la kiwanja nje ya mji na kutengeneza uwanja bora wa kisasa ambao utawawezesha vijana wanaopenda kandanda mkoani Arusha kupata sehemu za kuonesha vipaji vyao na badae kuchuja vijana 20 ambao wataunda timu moja ambayo itawakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano mbalimbali hapa nchini.

  Kwa sasa hatuna maeneo ya wazi na hili ni changamoto kwetu vijana wetu wana vipaji lakini hawana sehemu ya konesha tumepanga kununua viwanja na kuvitengeneza ili tuanzishe mashindano mbalimbali ambayo yatapelekea tuapte timu bora itakayotuwakilisha vizuri mkoa wetu wa arusha alisema Msofe

  Kwa upande wake waandaaji wa  Ndondo Cup ambayo ni kampuni ya Tan Communication Media wamiliki wa redio 5, Mathew Philip alisema kuwa lengo la mashindano hayo ya ni kutoa burudani ya soka la Mchangani kwa wakazi wa Jiji la Arusha lakini pia kuwapa vijana nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika mchezo wa soka.

  Mathew alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa burdani mbali mbali kwa wakazi wa Jiji la Arusha huku akisema kuwa mkoa wa Arusha kwa muda mrefu hakukuwa na Soka la Mchangani ambalo lina vijana wengi ambao wana vipaji na kuwawezesha kuonesha uwezo wao kwa kuwa sasa mpira ni Ajira.

  Timu zilizoshiriki ni Pamoja na Nyota Fc ambao waliibuka washindi,Ambrella Garden ambao walishika nafasi ya Pili na kujinyakulia shilingi laki tatu,F.F.U Oljoro Fc,Njiro Sports,Tanzanite Fc,Red Star Fc,Lemara Boys,

  0 0

   Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya Alliance Insurance.
   Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi Fauzia Kullane.
   Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
   Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer.
   Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
   Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini Tanzania.
  Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Bwa.Godwin Gondwe

  KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.

   Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.

  Utafiti huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango  makao makuu nchini  Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko  na maoni ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.

  Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000 zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya jsu  kwa mwaka wa 2015 -2016.

  0 0

  Jaji Francis Mtungi akifunguja mkutano wa wadau wa siasa wa uimatishaji demokrasia ya vyama vingi

  Jaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.
  Mkurugenzi UNDP Philippe Poinsot akizungumza katika mdahalo
  Mkurugenzi wa Mkazi wa Shirika Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa na kiraia katika mkutano huo.

  Aidha alisisitiza kwamba demokrasia sio suala jepesi, lakini watanzania wanastahili kujivuna kwa hatuha waliyofikia katika mambo mbalimbali ambayo hata mataifa mengine ya Ulaya hayajafikia.

  Alisema mwaka 1994 wakati taifa linaingia katika vyama vingi taifa lilikuwa na vyama 13 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 1995 lakini sasa tunapozungumza kuna vyama 22 vyenye usajili wa kudumu, wigo wa kuwania dola ukiwa umetanuka zaidi.

  Pia alisema mafanikio mengine ni namna ambavyo vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuandika inavyoona sawa, japo kumekuwa na tukio la kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, Mtanzania na Mwananchi, lakini kadhia hizo haziondoi ukweli kuwa kumekuwepo na uhuru mkubwa wa vyombo vya habari.
  Dk bana akizungumza katika mdahalo
  Dk Benson Bana akizungumzia demokrasia ya vyama vingi.
  Alisema taifa hili halina sababu ya kuomba radhi kwa mafanikio yaliyopo na changamoto zake katika siasa kwani uelewa katika masuala ya siasa unazidi kutanuka.

  Alisema pamoja na mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na utamaduni wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na aidolojia (itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa ya siasa na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.
  Alisema kutanuka kwa wigo wa ushiriki wa kuwania dola (vyama vingi vya siasa) kunatakiwa kwenda sanjari na kujenga utamaduni huo wa kuimarisha ustawi wa utamaduni wa vyama vingi.

  Alisema pia kuna haja ya kuimarishwa kwa taasisi zinazosaidia utamaduni huo kama Tume huru ya Uchaguzi, Bunge na hata mfumo wa utawala ambapo wakuu wa mikoa na wilaya wasiwe katika hali ya kikada bali wale wanaoweza kutekeleza majukumu yanayostahili katika maeneo yao.

  jaji Mutungi akiwa na Mkurugenzi UNDP Poinsot
  Jaji Mutungi akiteta jambo na Mkurugenzi UNDP, Bw. Poinsot.
  Aidha alisema kwamba vyama vingi vya siasa vinafanyakazi ya uanaharakati badala ya kuwa na itikadi ya kuifuata .

  Alizungumzia pia haja ya vyama vya upinzani kujivunja na kuanzisha chama kimoja na kutengeneza mkakati wa kutwaa dola huku akisema muungano wa Ukawa kwa sasa una mushkeri zaidi badala ya kusaidia kujiandaa kutwaa dola.

  Katika mdahalo huo ambao ulielezwa na Msajili wa vyama vya Siasa jaji Francis Mutungi, si mkusanyiko wa kufanya kampeni ya uchaguzi bali jukumu la ofisi ya msajili hasa kuelekea uchaguzi mkuu, washiriki wake pia walielezwa changamoto za siasa za vyama vingi.

  Profesa Rugumamu alisema kwamba katika tafiti aliyoifanya yeye na wenzake katika nchi 15 za bara la Afrika wamekumbana na changamoto takribani saba ambazo ni kikwazo katika kupata na kukuza utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
  IMG_4917
  Jopo la wanazuoni kuanzia kulia Dk Bana, Profesa Meena, Profesa Rugumamu na mwishoni ni msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
  Miongoni mwa changamoto hizo ni vyama vikongwe na utamaduni wake kushindwa kuainisha kati ya mamlaka ya dola na vyama vyenyewe, kuwepo kwa vyama vya kikanda na kidini katika kipindi cha mpito katika demokrasia ya vyama vingi, wanasiasa kubadili katiba waendelee kutawala, vyama na wanachama kutojua haki na wajibu wao kutokana na kutofundishwa uraia tangu awali.

  Pia alizungumza uadui unaojijenga kwa nchi ambazo zimetoka vitani na uanzishaji wa makundi ya ulinzi ya vyama ambavyo husababisha mitafaruku wakati wa uchaguzi au kwenye uchaguzi na matumizi ya fedha yasiyojulikana kwa ama kukosa sheria au sheria kuwapo na watu kutoizingatia.

  Alisema dosari zote hizo zinatikisa ujenzi wa utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi. Awali akimkaribisha Jaji Mutungi kufungua mkutano huo Mkurugenzi wa UNDP nchini, Philippe Poinsot alisema Umoja wa mataifa umefurahishwa kwa wadau wa siasa nchini Tanzania kuwa na mazungumzo yenye lengo la kustawisha amani kuelekea uchaguzi na kutengeneza mfumo wa majadiliano kama kukiwepo na kutokuelewana.

  Alisema mkutano huo walioufadhili ni sehemu ya makubaliano ya Ofisi ya Msajili na UNDP kupitia mradi wake wa kuimarisha demokrasia (DEP) yenye kulenga kujenga uwezo na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na kuleta maelewano ndani ya vyama na kitaifa wakati nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
  IMsimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian
  Msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
  Alisema ni matumaini yake kwamba mkutano huo utatengeneza mustakabari bora wa Tanzania kuwa na uchaguzi huru na wa amani.
  Alisema kutokana na ushindani, uchaguzi unaweza kuleta matata kwa hiyo ni vyema kama wadau wataliangalia hilo na kuona namna ya kutanzua matata ili taifa libaki na amani na kusonga mbele katika maeneo yote ya jamii.
  Naye Jaji Mutungi aliwaasa washiriki kutambua kwamba hakuna sababu ya kukamiana na kukomoana miongoni mwa vyama vya siasa kwani wote wanajenga nyumba moja na kimsingi hawana sababu ya kugombania fito.
  Alitaka wadau kucheza mchezo wa siasa kwa maridhiano ili wasibomoe misingi ya amani ya taifa na mafanikio yake.
  Alisema lengo la mkutano huo ni kuweka sawa dhana ya demokrasia ya vyama vingi na kutafuta majibu ya changamoto zinazokabili pasipo kuvunja amani ya nchi.
  Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi
  Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi.
  Profesa Rugumamu akizungumza
  Profesa Rugumamu akizungumza.
  IMG_4861
  Baadhi ya washiriki wakijadiliana.
  IMG_4879
  Washiriki wa mkutano wakijadiliana.
  wanamdahalo wakiwa makini
  Wanamdahalo wakiwa makini.

  Dk. Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa amewataka wadau wa siasa na wananchi kwa ujumla kuzuia uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu kwa kufuata Sheria na kutobeza mamlaka.

  Dk Bana alisema hayo jana akijibu swali la msimamizi wa mdahalo wenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi ulioandaliwa na Msajili wa Vyama vya siasa kwa ufadhili wa UNDP, Profesa Bernadetta Killian.

  Profesa Killian alitaka kujua baada ya maelezo ya awali ya Dk Bana juu ya mtazamo wake kuhusu ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania , nini kinastahili kufanya kuepuka uvunjifu wa amani hasa katika muda huu ambapo viashiria vipo.

  Dk Bana alisema kama watu hawatafuata utamaduni wa vyama vingi, utamaduni wa kufuata sheria na kutobeza mamlaka, taifa litaingia katika machafuko.

  Alisema watu kama wanaona wanaonewa wanatakiwa kufuata taratibu na kama taratibu hizo zinaonekana ni tatizo bado wanatakiwa kuwa na subira na kuondoa taratibu hizo zenye matatizo kwa kufuata utaratibu.

  Katika shauri hilo la viashiria vya mizozo Profesa Rugumamu, aliyebobea katika masuala ya kutanzua mizozo aliihimiza Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutengeneza mfumo wa utambuzi wa viashiria vya hatari (early warning) ili iweze kukabiliana navyo mapema.

  Akizungumzia kama Tanzania ni nchi ya demokrasia Dk. Bana alisema kwamba kuna maendeleo makubwa yamepatikana tangu mtindo wa vyama vingi kuingia nchini miaka 23 iliyopita.

  Alisema demokrasia haijengwi kwa siku moja, ina safari ndefu yenye milima na mabonde na wakati mwingine watu wasifike.


  0 0

   Meneja wa Kanda ya Mashariki Bw. Yesaya. Mwakifulefule  akikabidhi hundi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Bw. Nicolaus Kombe wakati wa sherehe za makabidhiano zilizofanyika jana Ruangwa mkoani Lindi. Hii ni mikopo ya wanachama kupitia SACCOS zinazotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF  ili kuwawezesha kutimiza malengo yao mbali mbali wakati wakiwa bado kazini au kabla ya kusataafu. Hadi kufikia sasa LAPF imetoa mikopo ya zaidi ya sh, 2.2 bilioni.LAPF imeikopesha Saccos ya Walimu katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni mia moja (100,000,000). 
    Meneja wa Kanda ya Mashariki Bw. Yesaya. Mwakifulefule  akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa sherehe za makabidhiano ya hundi,ambazo hutolewa kama sehemu ya mikopo ya wanachama wa SACCOSS na mfuko wa pensheni wa LAPF ili kuwawezesha kutimiza malengo yao mbalimbali wakati wakiwa bado kazini au kabla ya kustaafu,hafla hiyo ilifanyika jana Ruangwa mkoani Lindi.

   LAPF imetoa mikopo ya zaidi ya sh, 2.2 bilioni.LAPF imeikopesha Saccos ya Walimu katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni mia moja (100,000,000).  
    Mkurungezi wa Halmashauri ya Ruangwa Bw. Nicolaus Kombe akimkabidhi hundi Mwenyekiti wa Saccos ya Walimu Ruangwa Bw. Hamisi Salum Marungu wakati wa Makabidhiano hayo.
    Afisa wa Mipango na Uwekezaji Bw. Filbert Francis akitoa maelezo kuhusu Mikopo ya SACCOs wakati wa sherehe za makabidhiano. 
    Mkurungezi wa Halmashauri ya Ruangwa Bw. Nicolaus Kombe akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa sherehe za makabidhiano ya hundi,ambazo hutolewa kama sehemu ya mikopo ya wanachama wa SACCOSS na mfuko wa pensheni wa LAPF ili kuwawezesha kutimiza malengo yao mbalimbali wakati wakiwa bado kazini au kabla ya kustaafu,hafla hiyo ilifanyika jana Ruangwa mkoani Lindi.

   LAPF imetoa mikopo ya zaidi ya sh, 2.2 bilioni.LAPF imeikopesha Saccos ya Walimu katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni mia moja (100,000,000).  

  0 0

  Taarifa “INAYOSOMEKA HAPA” ilitolea ufafanuzi wa Nchi ya India inavyo pambana ili kuweza kufikia malengo katika kuboresha usalama mitandao hasa katika wizi unaofanywa kupitia ATM. Na baada ya kupata kutolea ufafanuzi muswada wa sharia mtandao, taarifa “INAYOSOMEKA HAPA”  Ilifafanua yamuhimu kuzingatia ili sheria hiyo iweze kupelekea kufikiwa kwa malengo kusudiwa ya kupata Tanzania salama kimtandao na kupunguza wimbi la makosa mtandao nchini.

  Baada ya hayo nilipata kuhudhuria mikutano kadhaa katika nchi mbali mbali ambapo nilifanikiwa situ kuwasilisha mada kwa wataalam wengine wa maswala ya usalama mitandao bali pia kujifunza mengi kutoka kwao katika maswala mbali mbali ya msingi ya kufanyiwa kazi ili kuweza kuboresha usalama mitandao situ katika ngazi ya kitaifa bali na kibara pamoja na  Dunia kwa ujumla.

  Makubwa matatu ambayo nimeona niyazungumzie leo ni pamoja na kuhakiki kuna njia madhubuti na zenye mpango stahiki za kukuza ulewa kwa watumiaji mitandao jinsi ya kujilinda na kulinda wengine watumiapo mitandao, Kuhakikisha Taifa linakua na mikakati endelevu ya kutengeneza na kuongeza uwezo wataalam wa maswala ya usalama mitandao pamoja na kupatikana na ufumbuzi wa kudumu wa kukabiliana na wimbi la wizi wa fedha kupitia mashine za ATM.


  0 0

   29 April 2015: MultiChoice Africa would like to inform the general public and all television broadcasters that ONLY SuperSport International has rights to air the ‘Fight of the Century’ bout taking place this weekend between Floyd Mayweather and Manny Pacquiao in Sub-Saharan Africa.

  From this Saturday, 2ndof May, DStv will air the super-fight on SS6 and SS6 HD to enable all DStv Premium viewers to watch the action in High Definition. The build-up to the live event will begin at 8pm and headed by former boxer, Brian Mitchell, with a professional record of 45-1-3 and a panel that includes Phillip Ndou, who fought Mayweather in 2003, and legendary referee Stan Christodoulou. Viewers will also be treated to breaking news, extensive behind-the-scenes coverage, documentaries, one-on-ones with Mayweather and Pacquiao, plus past fight highlights involving the pair.

  The rights also include live streaming, which is available to Premium subscribers on the SuperSport app. The build-up will culminate in The Fight of the Century which will air from the early hours of Sunday on May 3rd.
  No other television station/event organiser or entity shall screen this boxing match on any other programme or channel in a public place or free-to-air, live or repeated, without the authorisation of MultiChoice since this will be in violation of the directives governing the distribution of programmes and television channels. It furthermore interferes with and infringes upon the programme and channel distribution rights and arrangements of third parties.

   
  SuperSport’s knock-out build-up programming to ‘The Fight of the Century’ includes:
  ·         Studio analysis headed by former boxer, Brian Mitchell and a panel that includes Phillip Ndou and legendary referee Stan Christodoulou on SS6 from 10pm CAT on Saturday.
  ·         Updates on the biggest fight in boxing history plus “Big Fight Special” on SuperSport Blitz at 7am, 1pm and 7pm CAT daily.

  ·         Wall-to-wall big-fight programming on Friday, 1stMay on SS6 from 6am to 5.30pm CAT.
  ·         SS6 will cross live to the MGM Grand Garden Arena in Las Vegas at midnight on Friday for the pre-fight weigh-in. 

  ·         After the weigh-in, Pacquiao’s six-knockdown defeat of Chris Algieri will be broadcast on SS6 to remind fans of his power and excitement. SS6 will cross to Las Vegas for the tournament at 3am CAT on Sunday morning. The undercard features WBC super-bantamweight champion Leo Santa Cruz against Jose Cayetano, plus WBO featherweight champion Vasyl Lomachenko against Gamalier Rodriguez.

  ·         In the unfathomable possibility of missing the live fight action, DStv subscribers can catch the repeat the fight on SS6 at 7am CAT on Sunday and again on SS5 from 9pm CAT. Repeats will continue throughout the week.

  ·         The bulk of the programming will also be available on the Video on Demand service.
  PLEASE NOTE: SuperSport advises fight fans to set their alarm clocks for 4:30am CAT as the big Las Vegas bouts typically start at any time between 5:15am and 6am CAT.  For more information about this much-anticipated #MayPac bout, please visit www.dstv.com.

  0 0

  01
  Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.02
  Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.0304
  Baadhi ya Wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya  uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
  07
  Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akimpongeza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kushoto) mara baada ya kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
  08
  Naibu Katibu Mtendaji (Sekta za Uzalishaji) kutoka  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy (Kulia) akimpongeza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kushoto) mara baada ya kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
  09
  Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiongea na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila (Kulia) mara baada ya uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima. Anayewasikiliza ni Naibu Katibu Mtendaji (Sekta za Uzalishaji) kutoka  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy.

  010
  Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiongea na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara baada ya uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
  011
  viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 uliokuwa ukifanywa na Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
  ……………………………………………………………………….
  Na Saidi Mkabakuli
  Serikali imesema kuwa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha miradi ya kitaifa ya kimkakati iliyoibuliwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo unaofikia kikomo mwaka ujao wa fedha wa serikali.
  Hayo yalisemwa na Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
  Dkt. Nagu alisema kuwa mpaka kufikia mwezi machi mwaka huu, serikali imefanikiwa kutandika reli za uzito wa ratili 56.12 kwa yadi kwa umbali wa km 9 kati ya stesheni za Lumbe, Mto Ugalla na Katumba; kukamilisha malipo ya ununuzi wa mabehewa 274 ya mizigo ambapo mabehewa yameshaanza kupokelewa Novemba 2014; kukamilika kwa matengenezo ya njia ya reli iliyoharibiwa na mafuriko katika maeneo ya Ruvu – njia panda ya Mruazi.
  Waziri Nagu aliongeza kuwa kwa upande wa Barabara hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa kilometa 502.6 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kilomita 560, na ukarabati wa kilomita 78.8 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kukarabati kilomita 131.5. Kwa upande wa madaraja hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa madaraja ambapo daraja la Kigamboni limefikia asilimia 75, Sibiti asilimia 22, Kilombero asilimia 26, Mbutu asilimia 99, Lukuledi II asilimia 25 na Kavuu asilimia 36.
  Katika sekta ya Uchukuzi, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuongezeka kwa shehena iliyohudumiwa katika bandari ya Dar es Salaam kufikia tani milioni 14.3 Machi 2015 dhidi ya lengo la tani milioni 13.0 kwa mwaka 2014/15; kuongezeka kwa ufanisi wa bandari katika kupakua magari kwa kila shifti moja ya saa 8 kufikia magari 886 kwa shifti kufikia Machi 2015 ikilinganishwa na lengo la magari 600 kwa shifti katika mwaka 2014/15; kupungua kwa muda wa meli kupakia na kupakua mizigo bandarini kutoka lengo la wastani wa siku 5 mwaka 2013/14 hadi wastani wa siku 3.7 kufikia Machi 2015; kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa malipo kwa njia ya mtandao mwezi Julai, 2014; na kuanza  kutoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam kwa masaa 24 kwa siku zote za juma. Aidha, kwa upande wa bandari ya Bagamoyo, hatua iliyofikiwa ni kusainiwa kwa makubaliano ya ujenzi wa bandari; na kutangazwa kwa zabuni kwa ajili ya kupata wawekezaji katika bandari za Mtwara na Mwambani -Tanga.
  “Katika sekta ya nishati, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542) Machi 2015, na ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi Madimba (Mtwara) na Songosongo (Lindi) umefikia asilimia 86.9 ambapo unatarajiwa kukamilika Juni 2015. Kwa upande wa usambazaji wa umeme vijijini, wateja wapya 2,602 wameunganishiwa umeme katika mikoa ya Simiyu, Singida, Kagera, Tanga, Ruvuma, na Iringa,” alisema Dkt. Nagu.
  Kwa mujibu wa Waziri Nagu, shughuli nyingine zilizotekelezwa nia katika sekta ya nishati, ni pamoja na kukamilika kwa usimikaji wa mitambo 4 ya kufua umeme yenye uwezo wa jumla ya MW 150, kuendelea na ujenzi  wa vituo vya kupoza na njia za kusafirisha umeme, na kuendelea na ujenzi wa  karakana, majengo ya utawala, na barabara za ndani katika mradi wa Kinyerezi I; kukamilisha ulipaji fidia kwa eneo la Makambako katika mradi wa usafirishaji umeme wa Makambako – Songea;  na kuanza ujenzi wa nguzo za njia ya umeme katika mradi wa msongo wa kV 400 wa Iringa – Shinyanga.
  Akiwasilisha kazi zilizotekelezwa katika sekta  ya Maji, Dkt. Nagu alisema kuwa  ulazaji wa mabomba katika mradi wa maji Ruvu Chini kutoka Bagamoyo hadi Dar es Salaam kazi ambayo imekamilika kwa kilomita 52.43 kati ya kilomita 55.93 za mradi sawa na asilimia 93.8; kwa upande wa mradi wa maji Ruvu Juu: mkandarasi amekamilisha utafiti wa udongo na uchunguzi wa awali wa mahali yatakapojengwa matanki Kibamba na Kimara; na kwa upande wa mradi wa Bwawa la Kidunda,  wananchi wamelipwa fidia ya shilingi bilioni 7 kupisha ujenzi wa barabara na eneo litakapojengwa bwawa.
  “Kwa upande wa miradi ya maji vijijini, jumla ya miradi 123 ya maji ilijengwa na kukamilika. Idadi hii imenufaisha wananchi wapatao 463,750 na kuongezeka kwa ufanisi katika masuala ya ununuzi wa huduma katika mikataba kutoka siku 265 hadi siku 90. Aidha, Serikali imeendelea na ujenzi wa mabwawa ambapo bwawa la Iguluba (Iringa) na Wegero (Mara) yamekamilika. Vile vile, ujenzi wa bwawa la Kawa (Rukwa) umefikia asilimia 95, bwawa la Sasajila (Dodoma) asilimia 66.09 na Mwanjoro (Shinyanga) asilimia 45.4,” aliongeza Waziri Nagu.
  Katika sekta ya kilimo, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na: kupatikana kwa hati za mashamba mawili ya Bagamoyo na Mkulazi; maghala 30 yamekarabatiwa na kupatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbozi na Momba.  
  Vile vile, skimu 30 za umwagiliaji zimepatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbarali, Kyela na Iringa; na mafunzo juu ya kubaini na kudhibiti visumbufu, matumizi bora ya maji, utunzaji na matengenezo ya miundombinu ya umwagiliaji na kutumia mwongozo wa uendeshaji skimu za umwagiliaji yametolewa.  Aidha, ujenzi wa maghala 2 katika Wilaya ya Mlele umekamilika.
  Vile vile katika sekta ya viwanda, Waziri Nagu alizitaja kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya Itoni – Mkiu – Liganga na Mchuchuma kwa kiwango cha changarawe ili kuwezesha mitambo kufika maeneo ya Mchuchuma na Liganga; na kuanza uthamini wa mali za wananchi watakaohama eneo la Mchuchuma. 
  Vile vile, fidia shilingi bilioni 53 imelipwa katika eneo la kujenga kituo cha Biashara na Huduma Kurasini; na fidia ya shilingi bilioni 7 imelipwa katika eneo la uwekezaji Bagamoyo na Serikali imesaini mkataba na kampuni ya China Mechants Holding International kwa ajili ya kujenga bandari na eneo la viwanda. Aidha, katika kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua viluwiluwi wa mbu, Kibaha, kazi ya ufungaji wa mitambo na ujenzi wa miundombinu inaendelea na inatarajiwa kukamilika kabla ya Julai, 2015.
  Akizungumzia upande wa maendeleo ya rasilimali watu, Dkt. Nagu alisema kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na kuendelea kugharamia wanafunzi 159 wanaoendelea na mafunzo katika fani za mafuta na gesi kwa ngazi mbalimbali za mafunzo ndani na nje ya nchi ambapo wanafunzi 124 wanagharamiwa na Serikali na wanafunzi 35 wanagharamiwa na nchi wahisani; na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vikuu na vyuo vya ualimu, ufundi na ustawi wa jamii.
  Kwa upande wa utafutaji wa rasilimali fedha, Waziri Nagu alisema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania inatumia kanzidata bora inayohifadhi taarifa inayoweza kuthaminisha bidhaa na hivyo kutoa makadirio bora zaidi ya viwango vya kodi. Vilevile, alisema kuwa tozo kwa ajili ya uwekezaji katika elimu umeanza Julai 2013 ikiwa asilimia 2.5 ya mapato ghafi ya kampuni za simu.
  “Katika sekta ya fedha, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuongezea Benki ya Maendeleo ya Kilimo mtaji wa shilingi bilioni 60; kuendelea kuongeza mtaji wa Benki ya Rasilimali kufikia shilingi bilioni 212 ambapo mtaji kutoka Serikalini ni shilingi bilioni 152.2 na shilingi bilioni 59.8 zimetokana na malimbikizo ya faida; na  mali za Benki ya Maendeleo ya Wanawake Tanzania ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 26.5 mwaka 2013 hadi shilingi bilioni 34.8 mwaka 2014,” alisema Dk. Nagu.
  Kuhusu eneo la huduma za utalii, Dkt. Nagu aliongeza kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na usanifu wa ujenzi wa Utalii House awamu ya pili na kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji mapato (utalii, uwindaji na upigaji picha). Aidha, idadi ya watalii kutoka nje iliongezeka kutoka watalii 1,090,905 mwaka 2013 hadi watalii 1,102,026 mwaka 2014. Vile vile mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 1.81 mwaka 2013 hadi dola za Marekani bilioni 1.98 mwaka 2014.
  “Kwa upande wa Biashara, hatua iliyofikiwa ni kurekebisha sheria ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kutoa  elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu mfumo huo; kuanzishwa kwa kampuni ijulikanayo kamaTanzania Mechantile Exchange plc kusimamia na kuendesha soko la mazao ya bidhaa na kuhamasisha matumizi ya fursa za masoko ya mipakani, Kikanda na Kimataifa,” aliongeza.
  Kwa mujibu wa Dkt. Nagu maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2015/16 yamezingatia maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16). Aidha, Mpango huu umezingatia Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini – MKUKUTA II (2010/11 – 2014/15), Malengo ya Milenia, Mwongozo wa Mpango na Bajeti  kwa mwaka 2014/15; Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2014/15 yaliyojadiliwa na Bunge Novemba, 2014; Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2010 – 2015); na sera na mikakati ya kisekta.

older | 1 | .... | 515 | 516 | (Page 517) | 518 | 519 | .... | 1897 | newer