Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

onesho la Zari White party lazua gumzo jijini Dar,ni kuhusu kiingilio chake.!

$
0
0
 Watangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Powerbreakfast Gerald Hando pamoja na Hudson Kamoga wa Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 wakifanya mahojiano na Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini na kwingineko Diamond Platnum akiwa na mchumba wake Zari the bosslady,kuhusiana na mambo mbalimbali yakiwemo ya maisha yao na pia kuhusu onesho lao la Zari White Party wanalotarajia kulifanya usiku wa leo pale Mliman City,Jijini Dar.

Onesho hilo ambalo lilizua gumzo kila kona ya jiji la Dar likijulikana kwa jina la The White Party leo ndio kilele chake,kiingilio chake ukikisikia lazima usisimke,Kiingilio cha Onesho hilo kimevunja rekodi,haijawahi kutokea,kwa maana ya kwamba kiingilio kimepangwa kwa madaraja kuanzia Elfu hamsini,laki moja,milioni moja na milioni tatu,na huwezi amini tiketi sold out kitambo,imagine.

Katika mahojiano hayo Zari alieleza kuwa amefurahi kuonana na mtu kama Diamond,kijana anaejiamini,anaejituma na ni msanii anaefanya kazi zake kwa kujituma na juhudi kubwa,mwenye upendo na mapenzi ya kweli kutoka moyoni,alisema Zari huku akitoa tabasamu laini na kuongeza kuwa hajutii kumpata Diamond katika maisha yake.

Kwa upande wake Diamond nae alikiri wazi kumpenda Zari katika nyanja zote,amesema kwa sasa amekuwa na furaha kila wakati, kwa kuwa hivi karibuni anatarajia kupata mtoto wa kike kutoka kwa mchumba wake Zari. 
 Mtangazaji wa Clouds 360 Hudson Kamoga akimuuliza swali Bi.Zari ambae ni Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki na kwingineko. 
 Diamond akirekebisha jambo kwa mpenzi wake
 Ooh..relax baby.
 Ooh Shemejiiii......karibu..karibu Clouds FM/Clouds TV...! Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Power breakfast,Gerald Hando akimkaribisha Zari The Bosslady kabla ya kuanza mahojiano ya moja kwa moja kupitia Clouds FM na Clouds TV.


 Ooh Shemejiiii......karibu..karibu Clouds FM/Clouds TV...! Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Power breakfast,Gerald Hando akimkaribisha Zari The Ladyboss kabla ya kuanza mahojiano ya moja kwa moja kupitia Clouds FM na Clouds TV.
 Diamond akifafanua jambo.
 Kicheko kwa mbaaali






 Zari the bosslady katika ubora wake wa pozi.

TAARIFA YA MSIBA:Mwandishi mkongwe afariki dunia

$
0
0
Mwandishi wa habari mkongwe Kyaloeichi Oko Kessy (62) amefariki usiku
 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Pugu jijini Dar es Salaam.
Mpwa wa marehemu Tumaini Msengi ,alisema leo kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu na amekuwa akitibiwa katika hospitali mbalimbali za jijini Dar es Salaam hadi jana ambapo mauti yalimkuta.

Kabla hajaanza kuugua Kessy alikuwa mwandishi wa kujitegemea akiandika zaidi uchambuzi na makala katika vyombo mbalimbali vya habari nchini yakiwemo magazeti ya Motomoto,Shaba,Rai, na mengineyo mengi pia alikuwa ni mtunzi wa vitabu vya aina mbalimbali.

Msengi ameeleza kuwa  marehemu ameacha watoto wawili na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mdogo wake Chanika nje kidogo ya jiji na mazishi yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Marehemu ni mzaliwa wa kijiji cha Rosho Kilema mkoani Kilimanjaro.

ECONOMIC AND SOCIAL RESEARCH FOUNDATION (ESRF) GETS A NEW EXECUTIVE DIRECTOR

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO NA TUCTA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu toka kwa Gratian Mukoba, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) wakati wa kilele cha Mei Mosi Uwanja wa CCM Kirumbna jijini Mwanza leo mei 1, 2015. Picha na IKULU

SHEREHE ZA MEIMOSI ZILIYOFANA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme(TANESCO) mkoa wa Kilimanjaro wakipita na gari lao mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu chaUshirika  mjini Moshi. 
Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCLwakipita katikamaonesho ya Mei Mosi
Chuo cha wauguzi Kibosho pia walipita mbele ya mgeni rasmi kuonesha nini wanafanya katika sherehe hizo za Meio Mosi.
Mtafiti kutoka kituo cha utafiti wa zao la Kahawa ncini cha TACri ,Jeremiah Magesa akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi namna ambayo  kituo  hicho kinavyo saidia katika upatikanaji wa mbegu bora ya zao la Kahawa.
Moja ya mtambo inayotumika kunyunyiza dawa katika Kahawa ikioneshwa mbele ya mgeni rasmi.
Kampuni ya Swissport pia walikuwepo kuonesha kazi wanayofanya katika viwanja vya ndege.
Kassim Mwinyi akitoa maelezo kuhusu kampuni ya Panone inavyosaidia katika utoaji wa huduma ya mafuta.
Magari ya kampuni ya TBL yakipita mbele ya mgeni rasmi.
Baaadhi ya wa wafanyakazi wakifuatilia maonesho hayo.
Afisa Masoko wa Hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)Antypas Mgungusi akitoa maelezo juu ya ofa iliyotolewa na hifadhi hiyo ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi kilele cha Shira kwa gharama za Kiasi cha sh 25.000ikijumuisha kiingilio hifadhini,usafiri wa kwenda na kurudi ofa inayotaraji kuanza rasmi Mei 15 mwaka huu.
Halmashauri ya manispaa ya Moshi wakionesha shughuli mbalimbali wanazofanya pamoja na kikombe cha mshindi wa pili wa usafi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akikabidhi kikombe cha ushindi wa nafasi ya pili katika usafi pamoja na cheti kwa mgeni rasmi kaimu mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Novatus Makunga katika shrehe za Meio mosi zilizofanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika.
Bodi ya Kahawa Tanzania TCB pia walikuwepo katika sherehe hizo.
Watengenezaji wa Highlife Gin pia waipita kutangaza bidhaa zao mele ya mgeni rasmi.
Kampuni ya SBC watengenezaji wa kinywaji cha Pepsi na jamii yake pia walipita kuonesha vinywaji vinavyo tengenezwa nakampuni hiyo.
Kampuni ya Sukari ya TPC ilitia fora baada ya kuingiza mitambo yake inayotumika katika kilimo,kunyunyiza dawa pamoja na kupakia miwa wakati wa uvunaji.
hata hivyo vijana walikosa uvumilivu wakalazimka kukimbilia miwa iliyoachwa uwanjani hapo kwa ajili ya maonesho.
Wafanyakazi wakiimba wimbo wa Solidarity katika shrehe hizo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Mwakilishi wa kampuni ya Bia Tanzania ,Pudensiana akitoa maelezo kuhusu kampuni hiyo.

WAFANYAKAZI WAHIMIZWA KUJITOKEA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura ili kuweza kupiga kura ya maoni na kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.

Hayo yamedhihirika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei 1, 2015 zilizofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wizara mbali mbali ikiwemo taasisi binafsi zilibeba mabango yenye ujumbe kuhamasisha wafanyakazi.

Mpaka sasa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linaendelea vizuri katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
 Wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) wakiwa katika maandamano kusherekea siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI huku wakiwa na bango lenye ujumbe wao mahususi kuwahamasisha wananchi kushiriki kujiandikisha na wapige kura kuchagua kiongozi bora.
 Wafanyakazi wa Mamlaka  ya anga nao  hawakuwa nyuma na mabango yao.
 Wafanyakazi wa Ofsi ya Rais - Ikulu...
 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege ya Air Tanzania...
Mabango mbalimbali yamebeba kaulimbiu juu ya kuhamasisha wafanyakazi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura km. Nikiripoti toka Uwanja wa Taifa wa Zamani (Picha na Christina Njovu).

RAIS DR. SHEIN AONGOZA KILELE CHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba aliposhiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,[Picha na Ikulu.]SH2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana Viongozi wa Chama CCM wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba aliposhiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba.SH3Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi   wakati alipowasili katika  Viwanja vya Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo.SH4Maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi Kisiwani Pemba yakiingia katika uwanja wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chakechake leo wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani na kupokelewa na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani).SH5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipunga mkono kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi za Serikali  na Binafsi kisiwani Pemba wakati akilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,[Picha na Ikulu.]SH6Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipunga mkono kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Taasisi za Serikali  na Binafsi kisiwani Pemba wakati wa Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba.
SH7Wafanyakazi wa Wizara ya Afya Kisiwani  Pemba wakipita mbele ya Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya  wafanyakazi wa Taasisi za Serikali  na Binafsi wakati wa Kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba.SH8Wafanyakazi wa ZSTC Pemba wakipita mbele ya  Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheinalipokuwa akipokea maandamano ya  wafanyakazi wa Taasisi za Serikali  na Binafsi wakati wa Kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Uwanja wa Kiwanja Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba.SH9Viongozi mbali mbali na wafanyakazi wakiwa katika ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba wakati wa sherehe za Siku ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo mgeni rasmi akiwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.SH10Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) pamopja na Viongozi wengine wakinyanyua mikono  juu wakati wakiimba wimbo maalum wa Mshikamano (Solidarity Forever) wakati wa kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani sherehe zilizofanyika leo Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chake chake Pemba.SH11Viongozi na Wafanyakazi Mbali mbali wakishikamana kunyanyua mikono juu wakiimba kwa pamoja na kuimba wimbo maalum wa Mshikamano (Solidarity Forever) wakati wa kusherehekea Siku yaWafanyakazi Duniani sherehe zilizofanyika leo Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Wilaya ya Chake chake Pemba.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI UKISHIRIKIANA NA PROIN PROMOTIONS WAZINDUA RASMI MANUNUZI YA FILAMU ZA KITANZANIA ONLINE

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mheshimiwa Diodorus Kamala[l] akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali katika uzinduzi wa filamu za kitanzania ambazo sasa zitakuwa zikiuzwa online.sherehe hizo za uzinduzi ambazo zilifanyika jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
 Mwenyekiti wa Proin Group Tanzania ndugu Johson Lukaza akizungumza machache na kuwashukuru watu wote waliohudhuria uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online hapo jana katika ukumbi wa ACP House jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali.Uzinduzi huo ulifanywa na balozi wa Tanzania Mheshimiwa Diodorus Kamala.
Dr.Pendo akifanya mahojiano machache na Mheshimiwa Emmanuel kuhusiana na Filamu za kitanzania ambazo zitakuwa ziliuzwa mitandaoni pipote duniani.
Mwenyekiti wa Proin Promotion Tanzania ndugu Johson Lukaza [r] akiwa na viongozi wa Kitanzania nchi Ubelgiji katika sherehe za uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania onlione.
Kiongozi wa watanzania nchini Ubelgiji bwana Macha[r] akiwa na kiongozi wa watanzania jijini Antwerpen kwenye uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online popote duniani
Mwenyekiti wa Proin Promotion bwana Johnson Lukaza [l] akiwa na mmoja wa wageni waalikwa katika uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online jijini Brussel nchini Ubelgiji hapo jana.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Mheshimiwa Dr.Kamala akibadilishana mawazo na wageni wake mara tu baada ya uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online duniani kote.Balozi ni mmoja wa washiriki waliofanikisha shughuli nzima ya uzinduzi huo.
Warembo kutoka mataifa mbalimbali walikuwepo kwenye uzinduzi huo hapo jana.kwa manunuzi ya filamu zote za kitanzania sasa waweza kununua popote pale duniani kwa kutembelea website hii ya www.proinpromotions.co.tz 
Pendelea vya kwenu kwa kununua vyenu,sheme  Watanzania,Warundi,Wanyarwanda,Wakongo,Wazambia,Waganda,Wakenya na waafrika woote tunaomba ushirikiano wenu kwa kununua filamu zetu sasa.

UNESCO YAFURAHIA MABADILIKO REDIO JAMII

$
0
0
DSC_0107
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akiendesha mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
DSC_0025
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akitoa maelekezo kwa vikundi kazi wakati mafunzo hayo.

Miongoni mwa washiriki wa semina ya mwisho Pili Mlindwa wa redio jamii ya Panga FM akizungumzia mafunzo waliyopewa katika matumizi ya Tehama, alisema yamembadili sana katika utendaji wake na kumuongezea maarifa ya kazi. Alisema amefurahishwa sana na mafunzo ya Tehama ambayo sasa anaweza akafanya kazi nje ya studio na bado mhariri wake akawa na taarifa yake na kuitumia.

Alisema mafunzo mengi aliyopata katika mradi huo yakiwemo pia ya matumizi ya meseji Matrix, simu za mkononi kukusanya na kutoa taarifa kumemfanya awe wa kujiamini. Naye mwandishi wa habari, Bakari Khalid wa redio jamii Kaham FM ya Shinyanga akizungumzia Mafunzo ya Tehama alisema kwamba Unesco imefanya jambo la maana kuwapa mafunzo hayo ikizingatiwa kwamba redio nyingi zina watu wasiopitia chuo.

Alisema kwa sasa wanaweza kutengeneza vipindi bora vya kuhamasisha afya, elimu na kilimo na namna ya kuandika habari. Aidha alisema sasa wana uwezo wa kutumia kompyuta mpanguso (tablet) katika kuandaa vipindi na pia kuandaa taarifa mbalimbali.
DSC_0142
Wakala wa habari wa kituo cha Orkonerei Radio Service (ORS) cha wilayani Simanjiro, Nyangusi Ole Sangida akichangia mada kuhusu changamoto zinazowakabili Mawakala wa Redio Jamii katika ukusanyaji wa habari wakati wa mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
DSC_0019
Wakala wa habari wa kituo cha redio jamii Pangani FM, Pili Mlindwa akichangia mada wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku nne ikiwa ni sehemu ya mradi wa SIDA wa kuwajengea uwezo katika kuwawezesha kutengeneza vipindi bora.
DSC_0270
Wakala wa habari wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Paulina Juma akiwasilisha kazi ya kikundi ya kuandaa habari na kurekodi kipindi waliyofanya kwa vitendo katika Kompyuta mpanguso (Tablet) walizokuwa wakitumia kwenye mafunzo hayo.

DSC_0096
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
DSC_0122
Baadhi ya mawakala wa habari wa vituo vya redio jamii wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Kompyuta mpanguso (Tablet) wakati wa mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
DSC_0252
Baadhi ya mawakala wa habari kutoka vituo mbalimbali va redio jamii nchini wakiwa katika za vikundi.
DSC_0057
Wakala wa habari wa kituo cha Redio Jamii Pambazuko FM, Kaima Akida akifanya "Recap" ya mafunzo yaliyokuwa yakiendeshwa na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (hayupo pichani).
DSC_0292
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza machache wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa mawala wa redio jamii nchini ambapo aliwaasa kuyazingatia na kuyafanyia kazi waliyojifunza pindi warudipo kwenye vituo vyao vya kazi. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
DSC_0314
Wakufunzi na washiriki wa mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Na Mwandishi Wetu, Sengerema
AWAMU ya pili ya mradi wa kuwezesha redio za jamii kuhamasisha wananchi kushiriki katika kilimo, afya na elimu unatarajiwa kuanza Julai mwaka huu baada ya awamu ya kwanza ya miaka mitatu kuonesha mafanikio makubwa.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, wakati akihojiwa kuhusiana na mafunzo ya Tehama kwa Mawakala wa habari wa Redio za Jamii nchini yanayofanyika mjini hapa.

Alisema japo mradi huo umemalizika, kumekuwepo na mabadiliko mengi katika uendeshaji wa redio hizo za jamii ikiwa ni pamoja na matumizi ya Tehama katika kutengeneza vipindi na kuvirusha. Mradi huo wa uwezeshaji wa miaka mitatu ulimalizwa kwa mafunzo ya siku nne katika kituo cha redio jamii cha Sengerema Telecentre ambapo washiriki kutoka redio 9 walijifunza matumizi ya teknolojia katika kutengeneza vipindi, kukusanya taarifa kwa kutumia simu za kawaida na namna ya kuendesha redio hizo kuwa na mvuto na kutengeneza mpango kazi wa biashara.

Mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na Unesco na shirika la maendeleo la Sweden ( SIDA) limelenga kumwezesha mfanyakazi wa redio kutumia simu za mkononi kukusanya na kuboresha habari zake na kuzituma katika redio kwa matumizi ya ushawishi. “Tumeona mafanikio makubwa kwani kwa sasa wawakilishi wa redio hizi wanaweza kutengeneza vipindi kwa kuwashirikisha wanavijiji kutoa sauti zao ili zisikike,” alisema kutokana na hilo redio hizo sasa zimekuwa maarufu na za kuaminika.

Alisema nia ya Unesco ni kuhakikisha kwamba redio hizo zinashiriki kikamilifu katika kuhakikisha wananchi wanatoa na kupata taarifa zinazoweza kutumiwa na redio hizo kuhamasisha shughuli mbalimbali zikiwemo za kiafya, kielimu na kilimo.

Viongozi mbalimbali nchini Msumbiji wamkumbuka Brig. Jen. Hashim Mbita

$
0
0
Kitabu cha maombolezo ya Marehemu, Brig. Jen. Hashim Mbita kwenye Ubalozi wa Tanzania, Maputo Msumbiji.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Msumbiji, Mhe. Joaquim Chissano akiweka saini kitabu cha maombolezo ya Marehemu Brig, Jen. Hashim Mbita aliefariki dunia April 26, 2015.
Rais msataafu wa awamu ya tatu wa Msumbiji, Mhe. Armando Guebuza akiweka saini kitabu cha maombolezo ya Marehemu Brig, Jen. Hashim Mbita aliefariki dunia April 26, 2015.
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mh. Shamim Nyanduga akimkaribisha na Gen, Chipande (Mjumbe wa Kamati Kuu ya Frelimo) na ujumbe wake.
Gen.Chipande (Mjumbe wa Kamati Kuu ya Frelimo) akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo ya Marehemu Brig, Jen. Hashim Mbita aliefariki dunia April 26, 2015.
Camarada Sergio Pantie (Mjumbe wa Kamati Kuu ya Frelimo) akiweka sahihi kitabu cha maombolezo ya Marehemu Brig, Jen. Hashim Mbita aliefariki dunia April 26, 2015.

Wabunge wamkumbuka Marehemu Hashim Mbita

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Masuala ya Madawa ya Kulevya Mhe. Neema Mgaya Himid (Mb) na Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (Mb) wakisaini kitabu cha maombolezo.

Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya iliyopo ziarani nchini Zimbabwe hivi karibuni ilipata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania jijini Harare na kusaini kitabu cha maombolezo.
Marehemu Hashim Mbita aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. 

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWAFARIJI WAFIWA WA BRIGEDIA JENERAL HASHIM MBITA NA DKT ROBERT NTAKAMULENGA MKURUGENZI WA MAZINGIRA [NEMC]

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akitia saini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha ,Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Nyumbani kwa Marehemu Changmbe Jijini Dar es Salaam jana. 
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib  Bilal akiwafariji  watoto wa Marehemu rigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita alipokwenda Nyumbani kwa Marehemu Changombe Jijini Dar es salaam Jana aliyekaa Bw Mbita hashim naliyesimama  Iddi Hashim Mbita
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiwafariji Mjukuu wa Marehemu Brigedia Mstaafu Hashim Mbita kijana amal Iddi Hashim Wakati alipofika Nyumbani kwa Marehemu Changombe Jijini Dar es salaam Jana [PIcha na Ofisi ya Makamu Rais] 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilali akisalimiana na watoto wa Maerehemu Robert Ntakamulenga aliyekua  Mkurugenzi wa Mazingira {NEMC]  Nyumbani kwake Kimara Jijini Dar es salaam

NSSF Stakeholders meeting - postponed.

FLOYD MAYWEATHER AMPIGA MFILIPINO MANNY PACQUIAO KWA POINTI

DR. SHEIN AZINDUA MFUKO WA UCHAGUZI MKOA MAGHARIBI KICHAMA.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda jana wakati wa Uzinduzi wa mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort.mo2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda(wa pili kushoto) Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha(kushoto) Mama Mwanamwema Shein (kulia) na Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharibi Yussuf Mohammed Yussuf wakiwa katika hafla ya  Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort jana.mo3Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika Uzinduzi wa mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort akiwepo Mke wa Mamako wa Pili wa Rais Mama Pili Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kushoto).mo4Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea taarifa kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Magharibi Aziza Mapuri jana wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort jana.mo5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza Viongozi mbali na wanachama wa CCM na Wafanyabishara katika chakula cha jioni wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort.mo6Kikundi cha Imarisha cha CCM MKoa Amani kikitoa burudani ya ngoma ya Tukulanga wakati wa 
Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
.mo7Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha tasilim shilingi Millioni Nne  kutoka kwa Waziri asiyekuwa na Wizara maalu na Mjumbe wa Halamashauri Kuu ya CCM NEC Machano Othman Said wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort.mo8Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha tasilim shilingi Millioni Tano kutoka kwa Waziri wa Fedha Omar Yussuf na Mkewe wakati wa Uzinduziwa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort,[Picha na Ikulu.]

Keeping the District Bagamoyo Hospital clean and tidy

$
0
0
Keeping the District Bagamoyo Hospital clean and tidy was the main activity conducted by the Minister for Education & Vocational Training Dr. Shukuru Kawambwa, CCM Party cadres and students from higher training institutes in Bagamoyo District.
CCM Cadres and Minister Dr. Kawambwa joined in by students and Bagamoyo Civilians keeping the hospital compound clean.

A new CCM Member Mariyam Hamadi, a student from Fisheries Research Institute, receives her membership card from Minister Dr. Shukuru Kawambwa. Four hundred new members took the allegiance oath to follow the membership code of conduct.

New Members of CCM Ruling Party, in all 400 from various institutions, taking the solemn allegiance oath to sincerely follow the code of conduct.

Minister Dr. Shukuru Kawambwa assisted by some CCM district and national leaders planting the Ashoka Tree seedling in the compound of the Bagamoyo District Hospital. Ten other leaders took the turn of planting the seedlings just near the main laboratory of the hospital.
For more CLICK HERE

KAMATI KUU CHADEMA KUKUTANA DAR ES SALAAM KESHO NA KESHOKUTWA

$
0
0

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa kuwa Kamati Kuu ya Chama, chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, itakutana Mei 3-4, katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

Katika kikao hicho cha siku mbili kitakachofanyika jijini Dar es Salaam, pamoja na masuala mengine ya kitaifa kuhusu hali ya kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu;

1.     Maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

2.     Taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama, kukiandaa chama kushinda dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

3.     Taarifa za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.

4.     Taarifa ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4 vinavyounda UKAWA.

5.     Taarifa za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la kudumu kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.


Imetolewa leo Jumamosi, Mei 2, 2015 na;

Tumaini Makene


Mkuu wa Idara a Habari na Mawasiliano- CHADEMA

WAZIRI MKUU AKABIDHI MADAWATI 45 KIEMBESAMAKI

$
0
0
*Aahidi kuchangia madawati 135 na viti vyake

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameahidi kuchangia madawati 135 na viti vyake kwenye shule ya msingi Kiembesamaki iliyoko wilaya ya Magharibi mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni mwitikio wa maombi aliyopewa na shule hiyo.

Ametoa ahadi hiyo jana (Jumamosi, Mei 2, 2015), wakati akikabidhi msaada wa madawati 45 na viti vyake yenye thamani ya sh. milioni 3.83/- yaliyotolewa na kampuni ya Jambo Plastics ya Dar es Salaam ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

“Tatizo la madawati ni la kitaifa… Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali ametuambia kwamba haya ya leo yatatosha darasa moja tu na bado kuna mengine matatu hayana kabisa madawati. Changamoto iliyopo hivi sasa ni kwamba haya madawati yatagawanywa vipi wakati watoto wengine bado hawana mahali pa kukaa?” alihoji Waziri Mkuu.

“Ili kuondoa tatizo hilo, mimi nitachangia madawati yaliyobakia kwa madarasa hayo matatu ili watoto wetu wakae vizuri, wazingatie masomo yao na pia wawe na miandiko mizuri,” alisema huku akishangiliwa na walimu, wanafunzi na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo waliohudhuria hafla hiyo.

Madawati hayo 135 na viti vyake vina thamani ya sh. milioni 11.5 kwa bei ya sh. 85,000/- kwa kila dawati na kiti chake.

Alipoulizwa ni lini madawati hayo yatakuwa tayari, Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bibi Rupa Suchak alisema yatawasilishwa shuleni hapo baada ya wiki moja kwa sababu wana madawati ambayo yamekwishatengenezwa kwenye bohari za kiwanda chao.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuongea na jumuiya iliyofika kushuhudia utolewaji wa msaada huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Bw. Ali Juma Shamhuna alisema yeye alisoma kwenye shule hiyo mwaka 1952 na kuainisha kwamba wana uhaba wa madawati kwa madarasa manne.

“Tunayo madarasa matupu manne na hii ndiyo skuli yangu niliyosoma tangu mwaka 1952. Ni kweli tunakua na tunaongezeka lakini bado tuna watoto wanakaa chini… wananchi wa Zanzibar wanajitolea kujenga shule lakini inapofika kwenye madawati imekuwa ni tatizo. Tunaomba kuungwa mkono zaidi”, alisema.


Naye, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi, Bw. Ayoub Mahmoud Jecha alisema shule hiyo ina shule za Serikali 64 lakini ni shule mbili tu ndizo zina madarasa yaliyokamilika na yote yakiwa na madawati. Alisema wilaya hiyo ina jumla ya wanafunzi 114,000 ambapo 79,000 kati yao wanasoma kwenye shule za Serikali na 35,000 wanasoma kwenye shule za binafsi.

“Wilaya hii ina upungufu wa madawati 5,700. Kwa uwiano wa dawati moja kwa kila watoto watatu, ina maana kuwa watoto 17,100 wanasoma wakiwa wamekaa chini. Tunashukuru mchango huu wa Jambo Plastics lakini tunaomba wahisani zaidi wa kutusadia ili watoto wetu wapate mazingira mazuri ya kujifunzia,” aliongeza.

Awali, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Jambo Plastics, Bibi Rupa Suchak katika taarifa yake alisema kampuni yake imeamua kutumia plastiki kutengeneza madawati kwa sababu imedhamiria kuhifadhi mazingira lakini kuokoa kudorora kwa uchumi.

“Haya madawati ni imara na yanadumu kwa muda mrefu tumeshayasambaza kwenye shule zaidi ya 400 huko Tanzania Bara na tumeona matokeo mazuri… pia yanasaidia kuhifadhi mazingira kwa kuzuia ukataji miti ovyo. Takwimu zinaonyesha miti zaidi ya 100,000 inakatwa kila mwaka kwa ajili ya kupata mbao za kuetengezea madawati,” alisema.

“Madawati haya yanaweza kuongezwa au kupunguzwa urefu kulingana kimo cha mtoto lakini pia yana uimara wa pekee ambao unaokoa mamilioni ya fedha ambazo zingetumika kununua madawati mengine pindi yale ya mbao yanapovunjika,” alisema.

Waziri Mkuu alirejea jijini Dar es Salaam jana jioni.


IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, MEI 3, 2015.

Benki Kuu ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua hizi kufuatia kushuka kwa shilingi nchini-Zitto Kabwe.

$
0
0
Yaliyojificha kuporomoka kwa shilingi dhidi ya Dola ya Marekani
Shilingi inahujumiwa na Mabenki? – Zitto Kabwe[1].

Katika ukurasa wangu wa facebook mnamo tarehe 25 Aprili 2015 niliandika kuhusu sababu za shilingi kuporomoka thamani na majawabu ya namna ya kurejesha thamani halisi ya sarafu yetu. Nilieleza “Shilingi kuporomoka dhidi ya dola na kuvuka 1$/2000TS kunasababishwa na sababu kadhaa 1) Woga wa uchaguzi na hivyo Dola nyingi kutoingia nchini (FDI etc) kusikilizia Serikali ijayo inaundwaje 2) Woga wa uchaguzi na hivyo matajiri kununua dola kwa kasi (too many Tshs chasing too few $) ili kuzificha (hoard) nje 3) kutouza mazao nje na kuagiza bidhaa nyingi kutoka nje ( current account deficit) 4) Benki Kuu kutoachia $ nyingi kwenye soko kutokana na akiba ya fedha za kigeni kupungua 5) Kuongezeka kwa huduma ya Deni la Taifa ambapo malipo ni kwa fedha za kigeni kwa madeni yaliyo wiva.

Niliendelea kushauri majawabu “Suluhisho 1) Benki Kuu kuachia $ za kutosha kwenye soko katika muda mfupi na wa kati (Mwezi Februari BoT ilifanya hivi na kuongeza $64 milioni kwneye soko bila mafanikio[2] 2) Kuongeza mauzo nje hasa ukizingatia kwa sasa ‘our exports becomes cheaper vis a vis foreign exchange) 3) Malipo ya kodi ya Ongezeko la Mtaji kutoka BG (Shell transaction ) na Ophir (Pavilion transaction), malipo haya kwa fedha za kigeni 4) Punguza kununua vitu vya anasa kutoka nje 5) Unafuu wa huduma kwa Deni la Taifa ( Debt relief ) 6) Punguza ujazo wa fedha nchini (mop tshs out)”.

Mjadala mkali umeendelea kuhusu suala hili katika majukwaa mbali mbali. Ni dhahiri kuporomoka kwa shilingi kunaathiri sana Watanzania wa ngazi ya kati hasa wafanyabiashara wa kati wenye kununua huduma na bidhaa kutoka nje. Wenye viwanda wanaotegemea malighafi kutoka nje gharama zao za uzalishaji zimeongezeka zaidi na hivyo kuhatarisha uzalishaji mali nchini. 

Licha ya kwamba kuporomoka kwa shilingi kunafanya bidhaa zetu za kuuza nje kuwa rahisi, lakini huchukua muda kuzalisha bidhaa hizo na hasa kilimo kuweza kufaidika hali hiyo. Kwa hiyo ni faida kwa nchi kwa sasa kuwa na sarafu stahmilivu ( stable) iliyojengwa kwenye misingi imara ya Uchumi. Hata hivyo, inaonekana kuwa sarafu ya Tanzania inahujumiwa. Kuporomoka kwa Shilingi katika wiki za hivi karibuni sio matokeo ya nguvu za soko bali ni matokeo ya hujuma ( currency manipulations).

Mabenki makubwa ya kigeni nchini, inasemekana, katika miezi ya karibuni yamefanya currency manipulations na kupelekea dola chache kukimbizwa na shilingi nyingi na hivyo bei ya dola kupanda bei. Hii inatokana na ukweli kwamba Benki zetu kubwa tatu zinazoongoza zinaendeshwa na wageni. Inasemekana biashara hii hufanyika kati ya matawi ya Benki za kigeni hapa nchini na makao makuu yao. 


Kuporomoka kwa shilingi kunakotokea hivi sasa hakuendani na kuporomoka kwa miaka ya nyuma kipindi kama hiki (ambacho ki kawaida ni miezi shilingi hushuka thamani kwa sababu ya watalii kuwa wachache na mauzo ya bidhaa nje kuwa madogo sana). Wastani wa miaka 10 iliyopita inaonyesha kuwa kipindi hiki shilingi hushuka kwa kati ya 8% mpaka 13% na sio kuporomoka kwa zaidi ya 20% kulikotokea hivi sasa. Kwa mfano mwaka 2011 miezi kama hii ( Februari – Mei) Shilingi iliporomoka kutoka shs 1,380 kwa dola 1 mpaka shs 1,570 sawa na mporomoko wa 12%. Hata hivyo kuanzia mwaka huo mpaka mwaka 2014 shilingi imekuwa ikishuka thamani kwa kiwango kidogo sana. Mwaka 2013 thamani ya shilingi ilishuka kwa wastani wa asilimia 1.7 tu.

Uchambuzi huu wa thamani ya sarafu yetu unaonyesha kuwa kuna zaidi ya nguvu ya soko kunakotokana na mauzo yetu nje kuwa machache. Vile vile kupanda kwa thamani ya dola ya marekani duniani hakutoshi kuelezea mporomoko huu wa kasi wa shilingi kuanzia mwezi Disemba mwaka 2014 mpaka sasa. Tuhuma za mabenki kuwa yanahujumu shilingi (currency manipulations) zaweza kuwa na ukweli.

Vile vile, inasemekana kumekuwa na utoroshaji mkubwa wa dola kutoka nchini kwenda nje ya nchi. Utoroshaji huu unafanyika kupitia wasafiri wanaopita ukumbi wa VIP uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam. Utoroshwaji huu unatokana na hofu isiyo ya msingi kwamba uchaguzi utakuwa na vurugu. Utoroshwaji wa fedha ni kinyume sheria zetu. Sheria zetu za fedha za kigeni zinazuia mtu kubeba zaidi ya dola 10,000 za kimarekani zikiwa taslimu, kuingia nazo nchini au kutoka nazo nchini. Tafiti za haraka zinaonyesha kuwa huu umekuwa ni utaratibu wa kawaida kila mwaka wa uchaguzi tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

Benki Kuu ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua zifuatazo;
1.     Kufanya uchunguzi wa kushtukiza mara moja dhidi ya benki zote za kigeni zilizopo hapa nchini. Uchunguzi huu utazame biashara ya fedha za kigeni ya benki hizi kwa lengo la kuzuia ‘ currency manipulations’ na kuchukua hatua madhubuti dhidi ya Benki yeyote itakayokutwa imehujumu biashara ya fedha za kigeni kwa lengo la kushusha thamani ya shilingi dhidi ya dola za kimarekani.
2.     Jeshi la Polisi na kitengo cha kuzuia utoroshaji wa fedha ( anti money laundering unit) kufanya ukaguzi wa lazima wa watu wote wanaosafiri kwenda nje ikiwemo wanaopita sehemu ya watu mashuhuri (VIP Lounge) ili kudhibiti utoroshaji wa fedha za kigeni kwenda ughaibuni.
3.     Watanzania tufikirie upya nafasi ya Mabenki katika uchumi wa nchi na kufanya maamuzi magumu ya kurejesha baadhi ya Benki katika umiliki mpana zaidi wa Watanzania. Kwa malengo ya muda wa kati, Benki kubwa 3 nchini ilazimu kuwa na umiliki unaozidi 51% wa Watanzania. Bila ya kushika mabenki nchi itachezewa sana.
4.     Suluhiho la kudumu la sarafu stahmilivu ni kuongeza uzalishaji wa bidhaa za kuuza nje ya nchi na kupunguza manunuzi ya bidhaa kutoka nje. Urari wa Biashara wa Tanzania umepanuka kutoka $1bn mwaka 2004 mpaka $6bn mwaka 2013 (BOT 2013) kutokana manunuzi yetu nje kukua kwa kasi kutoka $2.5bn mpaka $11bn wakati mauzo yetu nje yakikua kwa kasi ndogo kutoka $1.4bn mpaka $5bn katika kipindi hicho. Isingekuwa uimara katika urari katika uwekezaji na uhamisho wa mitaji, Tanzania ingekuwa na sarafu yenye thamani sawa na takataka. Serikali ihimize uzalishaji mali mashambani na viwandani na kuuza nje biadhaa zilizoongezwa thamani. Zama za kutegemea dhahabu zimekwisha na sio endelevu. Turudi kwenye misingi: Bidhaa za Kilimo na Viwanda.

Tutaendelea kufuatilia thamani ya shilingi mpaka ifikapo mwezi Julai ambapo ndipo kipindi kigumu kwa shilingi huwa kihistoria. Hatua zilizoainishwa zisipotazamwa na mamlaka tajwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani yaweza kufikia tshs 3000!
[1] Zitto Kabwe ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo. Amepata kuwa Waziri Kivuli wa Fedha na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC.

[2] Benki Kuu kuingiza $ kwenye soko kuna hatarisha kupunguza Akiba ya fedha za Kigeni. Kutokana na ujinai unaoendelea kwenye soko la fedha za kigeni nchini, BoT kuendelea kumwaga fedha za kigeni inaweza kuwa ni mkakati wa kudumu wa wanaofaidika na ‘currency manipulations’. Kushinikiza Benki Kuu kuendelea kubomoa foreign reserve ni kutokuona mbali na kujaribu kujiridhisha kwa kutibu dalili za ugonjwa badala ya ugonjwa wenyewe.

UN na EU Wavutiwa na Programu za Radio za Jamii Morogoro

$
0
0
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza na kikundi cha akinamama kinachotengeneza vikoi na bidhaa mbalimbali mjini Ifakara. Kikundi hicho kimewezeshwa na EU na Umoja wa Mataifa UN. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza na kikundi cha akinamama kinachotengeneza vikoi na bidhaa mbalimbali mjini Ifakara. Kikundi hicho kimewezeshwa na EU na Umoja wa Mataifa UN.Akinamama wa kikundi cha utengenezaji vikoi na bidhaa nyingine za nguo wakiendesha moja ya mashine yao rahisi kutengeneza nguo hizo. Balozi Filiberto Sebregondi na Alvaro Rodriguez walitembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na taasisi hizo. Akinamama wa kikundi cha utengenezaji vikoi na bidhaa nyingine za nguo wakiendesha moja ya mashine yao rahisi kutengeneza nguo hizo. Balozi Filiberto Sebregondi na Alvaro Rodriguez walitembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na taasisi hizo.Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakisaidiana kuendesha moja ya mashine rahisi za ufumaji vitambaa eneo la Ifakara, mkoani Morogoro. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakisaidiana kuendesha moja ya mashine rahisi za ufumaji vitambaa eneo la Ifakara, mkoani Morogoro.Mmoja wa akinamama wa kikundi cha ufumaji na kudarizi vitambaa mbalimbali akiendesha moja ya mashine rahisi kuandaa vitambaa. Mmoja wa akinamama wa kikundi cha ufumaji na kudarizi vitambaa mbalimbali akiendesha moja ya mashine rahisi kuandaa vitambaa.Mmoja wa akinamama wa kikundi cha ufumaji na kudarizi vitambaa mbalimbali akimpongeza Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi mara baada ya kupewa zawadi ya vitambaa na umoja wa akinamama alipotembelea mradi wao. Mmoja wa akinamama wa kikundi cha ufumaji na kudarizi vitambaa mbalimbali akimpongeza Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi mara baada ya kupewa zawadi ya vitambaa na umoja wa akinamama alipotembelea mradi waoBalozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi (wa kwanza kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipata maelezo kutoka katika kikundi hicho cha uvumaji na uandaaji vitambaa. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi (wa kwanza kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipata maelezo kutoka katika kikundi hicho cha uvumaji na uandaaji vitambaa.Baadhi ya vitambaa na bidhaa zilizoandaliwa na kikundi cha ufumaji na kudarizi vitambaa mbalimbali Mjini la Ifakara, mkoani Morogoro. Baadhi ya vitambaa na bidhaa zilizoandaliwa na kikundi cha ufumaji na kudarizi vitambaa mbalimbali Mjini la Ifakara, mkoani Morogoro.Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika moja ya vituo vya radio jamii Ifakara. 
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika moja ya vituo vya radio jamii Ifakara.Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi wakiuliza maswali kwenye moja ya vituo vya radio za jamii Ifakara jana. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi wakiuliza maswali kwenye moja ya vituo vya radio za jamii Ifakara jana.Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi wakiwa katika kituo cha Redio Pambazuko Mjini Ifakara walipotembelea radio za kijamii na kujua namna zinazofanya kazi kwa jamii. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi wakiwa katika kituo cha Redio Pambazuko Mjini Ifakara walipotembelea radio za kijamii na kujua namna zinazofanya kazi kwa jamii.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images