Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 511 | 512 | (Page 513) | 514 | 515 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Meza kuu toka kushoto ni Rais wa CHAUKIDU Prof.Lioba Moshi, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi wakuhudhuria sherehe ya Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani. Mhe. Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa mgeni rasmi sherehe iliyofanyika Silver Spring, Maryland nchini Marekani siku ya Alhamisi April 23, 2015 na kuhudhuriwa na wadau wa Kiswahili kutoka mataifa mbalimbali wakiwemo Wamarekani wanaozungumuza lugha ya Kiswahili.
  Dr. Hamza Mwamoyo mkuu wa idhaa ya Kiswahili Voice of Amerika (VOA) akimsabahi Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi huku wakipata picha ya kumbukumbu wenginine kwenye picha ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi.
  Farida(kulia) wa Farida Catering akiwaelekeza Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula aina ya vyakula alivyopika katika kuhitimisha sherehe ya CHAUKIDU siku ya Alhamisi April 23, 2015 Silver Spring, Maryland nchini Marekani. Hii ni mara ya pili kwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuonja mapishi ya Farida Catering mara ya kwanza ilikua katika shere ya miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyika mwaka 2013 Capitol Heights.
  Farida akiwaonyesha ustadi wa ukutaji matunda Rais mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi.
  Prof. Lioba Moshi akiongea machache ya kumshukuru Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuhudhuria sherehe ya CHAUKIDU tangia mchana na usiku bila kuchoka pia alimshukuru Balozi wa Tanzania nchini Marekani kwa kuwezesha kuja nchini kwa Rais Msataafu aliyependezesha na kunogesha sherehe ya chama chao na baadae alimkaribisha Balozi Liberata Mulamula kuongea machache.
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitoa shukurani zake kwa CHAUKIDU kwa kufanikisha sherehe yao na baadae aliwatambulisha maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani akiwemo Balozi wa heshima Ahmed Issa na wadau mbalimbali wakiwembo waandishi wa vitabu Kapuya kutoka California na Mzee Safari kutoka Maryland na baadae kumkaribisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuongea na wadau wa Kiswahili nchini Marekani.
  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiongea na wadau wa Kiswahili katika kuhitimisha sherehe ya CHAUKIDU iliyofanyika siku ya Alhamisi April 23, 2015 Silver Spring, Maryland. Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi mbali na kuwashukuru CHAUKIDU pia alitumia fulsa hiyo kuweka sawa baadhi ya maneno la lugha ya Kiswahili ambayo hukosewa kutamkwa ipasavyo kwa kutoa mfano alisema katika kiswahili kahuta tarehe 1 au tarehe 2 usahihi ni tarehe mosi na tarehe pili huku akitolea mfano kwa lugha ya kiingereza kwamba hata nao hutamka 1st na 2nd mfano mwingine alisema unaposema nawaahidini ni ahadi unayotoa kwa watu wasiokuwepo mbele yako lakini unaposema ninakuahidini ndio sahihi kwa ahadi unayotoa kwa watu waliopo mbele yako na mengine mengi.
  Kamati nzima ya CHAUKIDU ikipata picha ya kumbukumbu 

  0 0

  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Account - MCAT) Eng. Salum Sasilo (kulia) akimkabidhi funguo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya - MUST Prof. Joseph Msambichaka kama ishara ya makabidhiano rasmi ya kambi ya Kianda iliyokuwa ikitumiwa na Mkandarasi Aasleaf Bam International katika ujenzi wa barabara ya lami kuunganisha Mikoa ya Rukwa na Mbeya katika mradi wa Laela - Sumbawanga wenye jumla ya Kilomita 95. Chuo hicho Kikuu cha MUST kimedhamiria kubadilisha kambi hiyo yenye jumla ya ekari 118 na majengo ya kudumu zaidi ya 18 kuwa moja ya Kampasi zake itakayobobea katika sekta ya uhandisi ujenzi hususani ujenzi wa barabara.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa salamu zake katika hafla hiyo ambapo ameitaka taasisi ya MUST kuhakikisha kuwa inatunza miundombinu waliyokabidhiwa na kuiendeleza kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini kwa vizazi vilivyopo na vijavyo. Aliongeza kuwa dhamira ya Serikale yake ya Mkoa ilikua ni kuona kambi hiyo inakabidhiwa kwa moja ya taasisi kubwa za elimu nchini ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaamn na taasisi zingine ili kuinua sekta ya elimu nchini lakini imekuwa bahati kwa chuo cha MUST kupata nafasi hiyo ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya chuo chao na elimu kwa ujumla. Amekiomba Chuo hicho kuona uwezekano wa kuipa Kampasi hiyo ya Kianda jina la Rukwa kwa ajili heshma ya maeneo hayo ambayo yapo Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Sumbawanga. 
  Meza kuu.
   Miongoni mwa nyumba ndogo ndogo za makazi ambazo zipo ndani ya kambi hiyo.
  Sehemu ya washiriki katika hafla hiyo ya makabidhiano kutoka Mkoani Rukwa na Mbeya.
   Picha ya pamoja.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katikati akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya - MUST Prof. Joseph Msambichaka kulia na Meneja Mradi wa Kampuni ya Aasleaf Bam International iliyojenga barabara ya Lami ya Laela - Sumbawanga Ndugu Russel Rourke muda mfupi baada ya zoezi la makabidhiano ya kambi hiyo ya Kianda. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi ya Rasaisei English Medium ya mjini Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Aprili 24, 2015. Wapili kulia ni Rubani wa Ndege za serikali, Narzis Kisimbo , kulia ni Mwalimu Esther Minja na kushoto ni mwalimu Emmanuel Kubyo.Wanafunzi hao walikuwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ziara ya kujifunza.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Aprili 24, 2015.Kutoka kushoto ni Rubani Naeziz Kisimbo, Mhandisi, Dioniz Majogo na Afisa Uendeshaji, Mohammed Mwilima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

  0 0

  Kijji cha Amani kinavyoonekana
  Taasisi ya Better Living Aid kupitia kampuni ya Royal Nsyepa General Supplies ambayo mkurugenzi wake ni Bw Mgalula Fundikira za jijini Dar es Salaam leo imepeleka mtaalamu wa upulizaji madawa ya kuuwa wadudu kama kunguni na wengineo katika kijiji cha Amani kilichopo km 6 nje ya mji wa Tabora.

   Hatua hiyo ya Better Living Aid ilifuatia ombi toka kwa wakazi wa kijiji hicho chenye wakazi wapatao 70 ambao baadhi yao ni wazee na wenye uathirika wa gonjwa sugu la ukoma, pamoja na changamoto ya kunguni pia wakazi wa hao wametoa maombi kwa taasisi hiyo nawasamaria wema wengine wajengewe vyoo zaidi kwani kwa sasa wana vyoo viwili tu vilivyo kwenye hali ya kutumika, huku vingine vikiwa vimejaa na haviwezi kunyonyeka. 

  Akiongea na mtandao huu mwenyekiti wa kijiji hicho Bw George Lusambilo alisema"kwa kweli tunaishukuru sana taasisi hii kwa kutuletea msaada huu, kwani tumekuwa tukilala kwa taabu sana, naona kuanzia leo tutalala kwa raha kama watu wengine" pia aliongeza "Ila tu jamani msituchoke, bado tunakumbushia ombi la kujengewa vyoo zaidi kwani idadi yetu na ukilinganisha na vyoo tulivyonavyo kwa kweli ni changamoto, lakini pia tunaomba tupate hata ka zahanati kadogo ili mganga na muuguzi wapate mahala maalum pa kutuhudumia hasa sisi wagonjwa wa ukoma"  Naye afisa ustawi wa jamii mkoa Bw Charles Makoye alisema "kwa niaba ya serikali naishukuru sana tasisi hii ya Better Living Aid kwa jitihada zao za kuboresha maisha ya wakazi wa hapa kijijni na napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kusaidia kijiji hiki kwani ustawi wa jamii si suala la serikali peke yake bali ni la jamii nzima inayotuzunguka kwani hawa wazee wametoka huko huko katika jamii zetu.
  Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid ametoa wito kwa makampuni na watu binafsi kuiunga mkono taasisi hiyo katika jitihada zake za kuwajengea vyoo na zahanati wakazi wa kijiji hicho. Vile vile ameeleza dhamira ya taasisi hiyo kutafuta wafadhili ili kujenga zahanati katika kijiji cha Masweya, wilayani Ikungi mkoa wa Singida alisema "Nilipata kufika kijijini Masweya mapema mwaka huu ambako nilipata kujua kwamba wakazi wa hapo hulazimika kutembea km 30 na ushee kwenda kjiji cha Mtunduru kupata huduma za matibabu. 

  Hivyo Better Living Aid itafanya kila liwezekanalo kijiji hicho kipate zahanati japo mdogo ya kuweza kuhudumia wagonjwa wa Malaria nk pia zahanati iweze kutoa huduma kwa wazazi, kitu mambacho kwa sasa hakipo kjijini Masweya. 


  Shukurani za dhati ziwaendee Mh Munde Tambwe (viti maalum Tabora), Mh Aden Rageh (Mbunge Tabora mjini) Bibi Joha Masawe, Bi Mtagwa Fundikira, Bibi Jamila Kaimika, Bibi Celina Koka na wanachama wote wa kundi la Better Living Aid Tunashukuru kwa msaada wa hali na mali iliyowezesha kijiji cha Amani kufanyiwa fumigation bila kumsahau mtaalamu Bw Selemani Muhogo wa kampuni ya SILVER ENTERTRADE LIMITED aliyepulizia dawa hiyo.
  Baadhi ya magodoro ya wakazi hao yakiwa yametayarishwa kwa kupuliziwa dawa

  Bw Muhogo akiandaa mashine ya kupulizia dawa
  Hpa akianza kunyunyiza dawa kwenye magodoro.

  Job DONE

  Baadhi ya vyoo vya hapo kijijini


  Mzee Hamisi Husseni akisubiri vifaa vyake vitiwe dawa
  Badhi ya mizigo ya wakazi wa kijiji hicho
  Afisa ustawi wa jamii Bw Charles Makoye akiongea na mkazi wa kijini hapo.

  Bibi Theresia Joseph akiwa nje ya chumba chake akisubiri huduma ya kupuliziwa dawa ya kuuwa  kunguni na wadudu wengine.
  Rundo la mahindi likiwa limotolewa nje kupisha upulizaji dawa ya kuua kunguni nani ya chumba yalimokuwa yamehifadhiwa.
  Baadhi ya panya waliokutwa ndani ya chumba cha mkazi mmoja wa kjijini hapo leo.
  Blogger wa Aloyson.com akiwa na Mzee Hamisi Husseni
  Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid Mkala Fundikira kushoto akiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Amani Bw George Lusambilo baada ya zoezi la upulizaji dawa ya kuuwa wadudu kunguni waliokuwa wakwasumbua mno wakazi wa kijiji hicho cha wazee wasiojiweza na waathieika wa ugonjwa wa ukoma.


  Baada ya ya kupuliziwa dawa baadhi ya kunguni wanaonekana wakiwa wamekufa.
  Blogger Juma Kapipi wa JHabari blog akiongea na mhanga wa kunguni baada ya kumhoji.
  Baadhi ya nguo zikichomwa moto baada ya kukutwa na kunguni wengi kupita  kiasi. 
  Habari na picha kwa hisani ya TBN Central zone!

  0 0

  Askari watakaoshiriki kwenye Gwaride la heshima litakalohusisha vyombo vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakiwa wamebeba bendera za Majeshi ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe hizo uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.
  skari wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Maji wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo jijini Dar es salaam. 
   Askari wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Maji wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo jijini Dar es salaam. 
   Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kitengo cha Mawasiliano wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo jijini Dar es salaam. 
  Askari wa Kikosi Maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Komando) wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 

  Serikali imesema kuwa maandalizi ya Sherehe za Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yamekamilika na kwamba sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa Uhuru Aprili 26 mwaka huu. 
   Akitoa ufafanuzi kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya sherehe hizo kwa niaba Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam leo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema amesema maadhimisho ya mwaka huu yatapambwa na Kauli Mbiu isemayo Miaka 51 ya Muungano, Tudumishe Amani Na Umoja ,Ipigie Kura ya Ndiyo Katiba inayopendekezwa na Kushiriki Uchaguzi Mkuu. 
   Amesema Tanzania katika kipindi cha miaka 51 ya Muungano imepata mafanikio makubwa katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ya jamii, uchumi, Siasa,Ulinzi, Usalama na Uhusiano wa Kimataifa. 
   Bi. Mjema amefafanua kuwa maadhimisho hayo yataongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye atakuwa mgeni rasmi na kupambwa na michezo ya Halaiki, ngoma za asili, vikundi vya burudani na Gwaride la heshima litakalohusisha vyombo vya ulinzi na usalama. 
   Pia yatapambwa na Wimbo maalum utakaoimbwa na vijana wa halaiki na ndege vita za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zitakazopita mbele ya mgeni rasmi Kama sehemu ya shamrashamra ya sherehe hizo. 
   Ametoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuhudhuria maadhimisho hayo na kufafanua kuwa milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:30 asubuhi ili kuwawezesha wananchi kuingia kushuhudia sherehe hizo. Aidha, ameutaka uongozi wa SUMATRA na wamiliki wa vyombo vya usafiri (Daladala) kuelekeza magari yao ya abiria kwenda uwanja wa Uhuru ili kurahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi.

  0 0


  Majina yaliongia kwenye hatua ya tano bora kwenye Tuzo za Watu 2015 yametangazwa rasmi Ijumaa hii. Hiyo ni baada ya siku kadhaa za kuhesabu mapendekezo yaliyokuwa yakitumwa na wananchi kwa kipindi cha wiki tatu tangu kuzinduliwa kwa tuzo hizo.

  Zoezi la kupiga kura linafunguliwa rasmi Jumamosi hii, April 24.

  Haya ndio majina matano yaliyoingia kwenye tano bora:


  Mtangazaji wa redio anayependwa TZW1         

  Dida – Times FM
  D’Jaro Arungu – TBC FM
  Diva – Clouds FM
  Mariam Kitosi – Times FM
  Millard Ayo – Clouds FM

  Kipindi cha redio kinachopendwa TZW2

  Ala     za Roho – Clouds FM
  Amplifaya – Clouds FM
  Hatua Tatu – Times FM
  Papaso – TBC FM
  XXL – Clouds FM


  Mtangazaji wa runinga anayependwa TZW3     

  Abdallah ‘Dullah’ Ambua - EATV  
  Salama Jabir – EATV/Maisha Magic
  Salim Kikeke – BBC Swahili
  Sam  Misago - EATV
  Zamaradi Mketema – Clouds TV


  Kipindi cha runinga kinachopendwa TZW4

  Friday Night Live – EATV
  In My Shoes – EATV
  Mkasi – EATV
  Planet Bongo – EATV
  Take  One – Clouds TV

  Blog/Website inayopendwa TZW5

  Muongozaji wa video anayependwa TZW6

  Abby Kazi
  Adam Juma
  Khalfan
  Hanscana
  Nisher


  Muongozaji wa filamu anayependwa TZW7

  Jacob 'JB' Stephen
  Leah Mwendamsoke
  Timothy  Conrad
  Vincent ‘Ray' Kigosi
  William Mtitu


  Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa TZW8

  Elizabeth 'Lulu' Michael
  Irene  Uwoya
  Jacqueline  Wolper
  Riyama  Ally
  Wema Sepetu


  Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa TZW9
  Hemedi  Suleiman
  Jacob   'JB'    Stephen Mzee
  King Majuto
  Salim ‘Gabo’ Ahmed
  Vincent  'Ray' Kigosi

  Mwanamuziki wa kike anayependwa TZW10
  Lady  Jaydee
  Linah
  Mwasiti
  Shilole
  Vanessa  Mdee

  Mwanamuziki wa kiume anayependwa TZW11 
  Alikiba
  Barnaba
  Diamond  Platnumz
  Jux
  Ommy Dimpoz

  Filamu inayopendwa TZW12
  Chausiku
  Kigodoro
  Madam
  Mshale wa Kifo
  Sunshine

  Video ya muziki inayopendwa TZW13
           
  Akadumba -  Nay  wa        Mitego
  Kipi Sijasikia – Profesa Jay
  Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz   
  Wahalade -  Barnaba
  XO - Joh  Makini

  0 0

   KAIMU Katibu Mkuu wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John akiandika maswali aliyeulizwa na waandisshi wa habari (hawapo pichani ) juu ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam,Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani  -Tanzania ,Dk.Ritha Njau ,Kulia ni Naibu Mkurugezi Kituo cha Utafiti cha Ifakara,Dk.Abdulrazq Badru.
   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza siku ya malaria duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 25 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam,Kushoto ni  Naibu Mkurugezi Kituo cha Utafiti cha Ifakara (IHI),Dk.Abdulrazq Badru.
   .Meneja wa Mpango wa Kudhibiti Malaria wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,DK.Ben Mandike akisisitiza jambo  kwa waandishi  habari juu ya maadhimisho  ya siku ya malaria Duniania  iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam.
   Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Tanzania, Dk.Ritha Njau John akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza siku ya malaria duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 28 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam.
   Waandishi wa habari wakisikiliza taarifa ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Rasilimali Watu  wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John.
   Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John (hayupo pichani), akitangaza siku ya malaria duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 25 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam.
  Watalaam na watafiti wa malaria wakifatilia mada mbalimbali katika mkutano wa tano wa taarifa ya miaka mitano ya utafiti wa Malaria na hali halisi ya sasa iliyoandaliwa na Kituo cha Utafiti cha Ifakara na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  JAMII imeaswa kutumia elimu sahihi ya matumizi ya vyandarua katika kuweza kupambana na ugonjwa wa malaria.

  Hayo ameyasema leo Kaimu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John wakati akitangaza siku ya malaria duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 25 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam,amesema jamii imetakiwa kutumia elimu sahihi katika kupambana na malaria.

  Amesema malaria imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2012 na kufikia asilimia 10 mwaka huu hiyo imetokana na juhudi za wizara ya afya na mashirika mbalimbali kutoa elimu juu kujikinga ugonjwa huo ambao awali ulikuwa ikichangia vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutokana na kutokana na kukosa vyandarua.

  John amesema katika madhimisho ya siku ya malaria ambayo itaadhimishiwa jijini Dar es Salaam yatakwenda sambamba na uzinduzi  wa ugawaji wa vyandarua milioni 24 vilivyotolewa na Wizara ya Afya ikiwa lengo kupambana na ugonjwa wa malaria. Amesema mikoa ambayo iko katika viwango vya juu vya ugonjwa wa Malaria ,Lindi,Geita ,Kigoma pamoja na Mara hali ambayo elimu inahitajika kwa mikoa hiyo katika matumizi sahihi ya vyandarua  kuweza kufikia asilimia sifuri.

  John amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Maralia ni Wekeza kwa Maisha ya Baadae ,Tokomeza Malaria na maadhimisho hayo itatumika sehemu ya kuelimisha juu ya kutambua dalili za malaria kuwahi katika kituo cha kutolea huduma,ili kupima na kudhibitisha uwepo wa vimelea kabla ya kuanza kutumia dawa kwa kuwa sio kila homa inasababishwa na Malaria.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA akizungumza mbele ya wakazi wa kijiji cha Sawala wilayani Mufindi (hawapo pichani),wakati akizindua  chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa.
   Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA akiwa amembeba mtoto mara baada ya kumpa chanjo.
  wakazi wa kijiji cha Sawala wilayani Mufindi wakimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita,mara baada ya kuzindua  chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa
   Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA akimpa chanjo mmoja wa watoto katika kijiji cha Sawala wilayani Mufindi mkoani Iringa

  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA amewataka wazazi na walezi Mkoani Iringa kutosikiliza maneno ya uzushi kuwa chanjo zinazotolewa kwa Watoto nchini huwa zinamadhara, badala yake wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kutolea chanjo ili kuwakinga watoto na uwezekano wa kushambuliwa na maradhi mbali mbali.

  Taarifa ya ofisi ya habari na mawasiliano ya halmashauri ya Wilaya  ya Mufindi, imeeleza kuwa ,Mkuu  wa wilaya aliyasema hayo katika kijiji cha Sawala Wilayani Mufindi Mkoani iringa wakati akimwakilisha Mkuu wa  Mkoa wa Iringa kwenye uzinduzi wa wiki ya chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5.

  Mhita amesema endapo wazazi na walezi watasikiliza maneno yasiyo na ukweli wowote, watakuwa wanahatarisha afya za watoto wao kwani kuzikosa chanjo hizo muhimu kwa ustawi wa Mtoto kutasababisha washambuliwe na maradhi, kitu ambacho kinahatarisha uhai wa Mtoto.

  Amesema chanjo ni mkakati muhimu na muafaka katika kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto lakini pia kupunguza gharama kubwa ambazo Familia na taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu maradhi yatokanayo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

  Wataalam ya afya wamethibitisha kuwa, chanjo huzuia  takribani vifo milioni mbili hadi tatu kila mwaka kutokana na maradhi yanayokigwa kwa chanjo ikiwa ni pamaoja na Ndui, Polio, Kifaduro na Pepopunda,ujumbe wa chanjo mwaka huu unasema Jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya huku kauli mbiu ikisema Chanjo ni zawadi ya Maisha.

  0 0


  diamond_platinumz-slider-2
  ZURII HOUSE OF BEAUTY AND BONGO DEEJAYS PRESENT!!
  Londons Rugby 7's After Party, Appearing Live, Bongo Flava recording artist from Tanzania most famous for his song "Number One". Diamond Platnumz will be preforming with his WCB dancers and special guests at the Royal Regency Banquet Hall for one night only.
  THE ROYAL REGENCY
  501 HIGH STREET NORTH
  MANOR PARK 
  For Front Row V.I.P Tables and Info Please Contact our Ticket Hotline: 07853482158 or 07421167123
  Dont be left out, tickets are running out quickly. We are counting down to the most Epic event of the Year!!

  IN SUPPORT OF ALBINO CRUELTY IN TANZANIA. TOGETHER WE SAY: "IMETOSHA"

  Follow the link below or clck "Buy Tickets" to get your tickets A.S.A.P

  http://buytickets.at/zurii-house-of-beauty-and-bongo-deejays/26052


  Buy tickets for Diamonds are forever UK live concert


  0 0


                               Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba shindano la urembo nchini maarufu kwa jina la Miss Tanzania limefunguliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kwamba Kampuni ya Lino International Agency LTD ambayo ni waendeshaji wa shindano hilo imewataka mawakala wake kuanza maandalizi ya shindano hilo.

  Taarifa hizo za kufunguliwa shindano hilo zilienda mbali kwa kueleza kwamba mawakala wametumiwa kalenda ya mashindano hayo kwa mwaka huu.

  Baraza linapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:


  1.     Wananchi wapuuze taarifa hizo kwani kusimamishwa kwa shindano la Miss Tanzania bado kuko palepale kama ilivyoelezwa katika barua ya BASATA ya tarehe 22/12/2014 waliyoandikiwa Lino International Agency LTD ambayo pamoja na mambo mengine iliwataka warekebishe kasoro kadhaa zilizojitokeza. Walisimamishwa kwa misimu miwili ya mwaka 2015 na 2016 ili kujipanga upya na kurekebisha kasoro husika.

  2.      
  2.      BASATA kama msimamizi na mratibu mkuu wa sekta ya Sanaa nchini ndilo lililolisimamisha shindano hilo baada ya kubaini mapungufu mengi. Kusimamishwa kwa shindano hili ilikuwa ni kwa njia ya kuufahamisha umma na kwa maana hiyo kama shindano litafunguliwa njia hiyo-hiyo ya  kutoa taarifa kwa umma itatumika na si vinginevyo.  


  3.      BASATA linatoa wito kwa Lino International Agency LTD kutumia muda wake mwingi kufanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza ili mashindano haya yatakaporejea yawe na mikakati na hadhi kuliko ilivyo sasa.


  4.      Aidha, Baraza linawataka wasanii na wadau wote kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika kuendesha shughuli za Sanaa sambamba na kufuata mifumo sahihi ya mawasiliano.

  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

  Godfrey Mngereza

  KATIBU MTENDAJI.
    


  0 0

  DSC_0089
  Pichani juu na chini ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza na katika mkutano uliohusisha wadau wa mashirika ya Kimataifa na asasi za kijamii ukiwa na lengo la ushirikishaji wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori uliofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House uliopo Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewji blog).
  DSC_0082
  DSC_0096
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akifafanua mazungumzo na wadau wa mashirika ya kimataifa na asasi za kijamii ukiwa na lengo la ushirikishaji wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori uliofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House uliopo Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam.
  DSC_0135
  Naibu Waziri wa Maliaisli na Utalii, Mahmoud Mgimwa akitoa salamu kwa wadau wa taasisi za kirai. Kushoto Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu.
  DSC_0124
  Mratibu wa Uhakiki wa Ubora kutoka Haki Elimu, Robert Mihayo akitoa maoni kwa Waziri Mh. Nyalandu ambapo amemuomba kushirikisha wadau wa elimu katika kutoa elimu ya uhifadhi wa wanyamapori kuanzia ngazi ya elimu ya msingi ili kuwaanda vijana ambao ni taifa la kesho.
  DSC_0110
  Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society, Francis Kiwanga akishiriki kutoa maoni katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori pamoja na kutokemeza ujangili wa Tembo.

  DSC_0105
  Mwandishi wa gazeti la Daily News, Diriham Kimathi akiuliza swali kwa Waziri Nyalandu (hayupo pichani).
  DSC_0129
  Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau kutoka asasi za kijamii na mashirika ya kimataifa waliohudhuria mkutano ulioitishwa na Waziri Nyalandu ambao umefanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House uliopo ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
  DSC_0131
  DSC_0059
  DSC_0005
  DSC_0143  DSC_0149 
  Waziri Nyalandu akisalimiana na baadhi ya wadau kutoka mashirika ya kimataifa na asasi za kijamii waliohudhuria mkutano huo.
    DSC_0158
  Mdau kutoka Tanzania Association on Climate Change, Ali Said Mosee akitoa maoni yake juu ya kuhusiana na nini kifanyike katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori katika mkutano uliotishwa na Waziri Nyalandu (hayupo pichani).

  Na Modewji blog team
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema kama watanzania wasiposhirikiana katika kudhibiti ujangili wa Tembo waliopo watatoweka kabisa katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

  Kauli hiyo ameitoa jana kwenye mkutano wa ushirikishwaji wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori uliofanyika wizarani kwake.
  “Uhifadhi kama tunavyoujua, hautaweza kufanikiwa kama kila mtu kwenye nchi hii atafikiria ni kazi ya serikali kuu peke yake. Na vilevile kama kila mtu atafikiria ni kazi ya wahifadhi peke yao”. alisema Nyalandu kwenye mkutano huo.

  Nyalandu alibainisha kuwa, majadiliano hayo, yatakuwa chachu kubwa ya maendeleo katika wizara hiyo huku akiwashukuru wadau hao mbalimbali wakiwemo wanahabari kwa kufika kwao, ili kuangalia suala la uhifadhi kwa mapana yake.
  Alisema wakati ujangili wa Tembo nchini umeshamiri sana, wakati umefika kwa watanzania kuhakikisha kwamba wanakomesha hali hiyo ili taifa kuendelea kuwa na wanyama wake.
  Alisema mathalani Tembo katika hifadhi ya Selous wamepungua kutoka Tembo 38,975 katika sensa ya mwaka 2009 hadi Tembo 1,384 kwa sensa ya mwaka 2014 na akasema kwa kasi hiyo katika miaka 10 ijayo Tembo Tanzania wataisha kabisa.
  “Hili ni muhimu watu wakafahamu, upana wa hivi vita ni mkubwa kiasi gani na watu wanaohusika ni wengi kiasi gani ndani na nje ya nchi," alisema Nyalandu akiongeza kuwa mitandao ya kihalifu imetanda ulimwenguni kote.
  Alisema suala la hifadhi halipo kwa wanyama pekee bali lipo katika upana wote na hata katika misitu.
  Alisema ili kukabiliana na ukatwaji hovyo wa miti kutoka katika misitu ya miombo wanajipanga kuhakikisha kwamba miombo inayodaiwa kuingizwa nchini kutoka Zambia inakamatwa ili kulinda miombo iliyopo magharibi ya nchi.
  Akizungumzia suala la mifugo na mbuga zinazopakana nazo amesema kwamba wanaanda rasimu ya kuhakikisha kwamba kuna mahusiano mazuri kati ya wenye mifugo na hifadhi wakiwa tayari kuyaachia baadhi ya maeneo kwa lengo la kuhakikisha kwamba wafugaji hawaingizi mifugo yao katika hifadhi.

  Aidha amesema kwamba wanajipanga namna ya kuhakikisha kwamba hakuna mgongano wa maeneo kati ya wanyama na binadamu na kwamba wanavijiji wanafundishwa namna ya kuishi na wanyama katika maeneo yenye mwingiliano mkubwa. Aidha alisema kwamba meno ya Tembo kilo 1,763 yalikamatwa mwaka jana na jitihada zinaendelea za kukabiliana na majangili kwa kutanua mtandao wa kiintelejensia ndani na nje.

  Alisema kwa sasa wanamsaka raia wa China anayeshutumiwa kutorosha nyara za serikali kwa kushirikiana na jeshi la Polisi la Kimataifa (Interpol).
  Kwa nje ya nchi, meno ya Tembo yaliyokamatwa, Kilo 40 katika miji ya Hong Kong, China.

  Aidha alisema watuhumiwa 1,711, walikamatwa kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana na kesi zao zinaendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini. Pia silaha 85 zimekamatwa ikiwemo silaha za kivita ambazo walikuwa wakizitumia mbugani.

  Alisema ukichanganya na silaha zilizokamatwa kwenye operesheni tokomeza, jumla silaha 1,199 zimekamatwa. Kwa upande wake, Ali Said Mosee aliyehudhuria mkutano huo kutoka Tanzania Association on Climate Change, alishauri ushirikishaji wa wadau mbalimbali kutatua migogoro kwenye mipaka ya mbuga na pia mgongano wa kimaslahi kati ya hifadhi na wanadamu.

  Aidha wadau walishauri Wizara kuhakikisha inapunguza misafara ya wanyama ya kuhamahama kutoka sehemu moja hadi nyingine ikiwemo kwa kuzalisha miti na mazao yanayopendwa na wanyama hao. “Wanyama wetu wanatakiwa wafanyiwe utafiti na kujua nini Nyati anapendelea kula porini, basi wapande hiyo miti na vyakula vyake kwa ujumla hata kwa Tembo hivyo hivyo.Wapande hiyo miti hapa hapa kwani hata siye binadamu tunavyovyakula tunavyovipenda, naamini hata kwa wanyama ni hivyo hivyo, rai yangu ni kuwa tufanye utafiti na kujua ili kuzuia misafara hii” alisema Ali Said Mosee.

  Tanzania inahifadhi za taifa 16 na asilimia 40 ya ardhi ya nchi ni maeneo yaliyohifadhiwa. Kati ya maeneo hayo yaliyohifadhiwa hadi mwezi uliopita mwaka huu 2015, maeneo 19 yanamilikiwa na wananchi na yameshasajiliwa. Pia alisema kwamba kuna mapori ya akiba, 28 nchi nzima.

  “Watu wengi wanadhani kwamba misitu yote inamilikiwa na serikali kuu. Ukweli ni kwamba serikali kuu inamiliki asilimia 35 tu ya misitu ya nchi yetu, misitu mingine yote inamilikiwa na vijiji, wilaya na watu binafsi asilimia 7. " alibainisha waziri huyo. Aliwataka watendaji wa Serikali za mitaa kukabiliana na changamoto ya kutoweka kwa kasi kwa misitu ili taifa lisitumbukie katika jangwa. 

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu juzi.it1Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wakimshangilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (hayupo pichani), katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani humo juzi.it02Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akizungumza na halaiki ya vijana wa chama hicho muda mfupi baada ya kuifunga kambi ya mafunzo ya vijana hao iliyofanyika Kijiji cha Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu juzi.it2Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wakimshangilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (hayupo pichani), katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani humo juzi.it3Wazee wa kabila la wasukuma wakimkabidhi zana za asili  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ili yeye na chama chake aweze kutawala nchi. Mbowe alisimikwa na kupewa zana za kitemi za kabila hilo na kuitwa jina la Mayego kabla ya kuanza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima mkoani Simiyu juzi.it4Wazee wa kabila la wasukuma wakimuombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ili yeye na chama chake aweze kutawala nchi. Mbowe alisimikwa na kupewa zana za kitemi za kabila hilo na kuitwa jina la Mayego kabla ya kuanza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima mkoani Simiyu juzi.

  0 0

  indexKundi la Watanzania 26 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.
  Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
  Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.
  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
  25 Aprili 2015

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo   Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kutoka kushoto) Kamishna Mkuu wa UhamiajiTanzania Sylvester Ambokile Mwakinyule na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Perera A.Silima. 
  uh2
  uh4Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia hatua za utengenezaji wa PassPort za Uraia wa Tanzania wakati alipotembelea sehemu mbali mbali baada ya kulifungua Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo   Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Perera A.Silima na (kulia) Inspekta wa Uhamiaji Hassan Suleiman Ameir.[Picha na Ikulu].uh5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Asistance Inspekta Khamis Ali Haji (katikati)wakati alipotembelea katika chumba cha kumbukumbu za picha kwa Wananchi walioomba Passpoti za Uraia baada ya kulifungua Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo   Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Utoaji Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari, iliyofanyika jana usiku April 24, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. tu2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milion tatu na Laki Nane (M.3.8) mshindi wa jumla katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, Mkinga Mkinga, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. Kushoto ni Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Robert Mihayo na Generali Ulimwengu. tu3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milion tatu na Laki Nane (M.3.8) mshindi wa jumla katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, Mkinga Mkinga, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. tu4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo  mshindi wa pili wa jumla katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Mwandishi wa habari wa Gazeti la The Citizen, Lucas Liganga, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. Picha na OMRtu5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni kumi (M. 10) Mwandishi wa habari wa siku nyingi mkongwe, Generali Ulimwengu, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. Kushoto ni Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Robert Mihayo na (kulia) ni Mke wa Generali Ulimwengu. tu6Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari waliopata Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa habari, zilizotolewa jana usiku Aprili 24, 2015 wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. tu8Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wanakamati wa maandalizi wa hafla hiyo baada ya kumalizika hafla hiyo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam jana usiku Aprili 24, 2015. Picha na OMR

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola na akisalimiana na baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa mgeni rasmi katika wa mahafali hayo shuleni Jangwani sekondari iliyopo manispaa ya Ilala Jijini Dare s salaam.
  ja2 - CopyMkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola (wa katikati) na baadhi wa viongozi wa shule wakielekea eneo la mahafali ya kidato cha sita ya shule ya sekondari Jangwani yalifanyika mwishoni mwa wiki ambapo Mkurgenzi huyo alikuwa mgeni rasmi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Shule ya sekondari Jangwani Geraldine Mwanisenga.
  ja3 - CopyBaadhi ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu wa Shule ya sekondari Jangwani wakielekea eneo la mahafali yao.
  ja4 - CopyMkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya kidato cha sita shule ya sekondari Jangwani mwishoni mwa wiki na kuwaasa watumie nidhamu bora ambayo itawasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea maishani mwao. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya sekondari Jangwani Geraldine Mwanisenga.
  ja5 - CopyMwanafunzi aliyepata vyeti mbalimbali vya taaluma takribani saba kwa kufanya vizuri katika masomo ya Kemia, Biyolojia, Fizikia, Hesabu, cheti cha kuwa mwanafunzi bora katika masomo, uongozi, uongozi bora pamoja na zawadi Rosemary Mushi akipongezwa na Mgeni Rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola na kukabidhiwa vyeti vyake wakati wa mahafali ya kidato cha sita yalifanyika shule ya sekondari Jangwani mwishoni mwa wiki.

  ja6ja7Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu wa Shule ya sekondari Jangwani wakimsikiliza Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola wakati wa mahafali yao shuleni hapo mwishoni mwa wiki.
  ja8Baadhi ya burudani zinaoongozwa na wanafunzi picha ya 08, msanii Barnaba Boy picha 09a na b na Msanii Masami picha 10 walivyopamba mahafali ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Jangwani kwa burudani murua.
  ja9ja10Msanii Barnaba Boy akiimbaja11ja12Kikundi cha wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani wakionesha ukakamavu wao huku mmoja wao alyekuwa juu ya wenzake akimakabidhi MC mic kwa ujasiri.
  ja13Baadhi ya walimu na wageni waalikwa wakimfuatilia mambo mbalimbali wakati wa mahafali ya kidato cha sita shule ya sekondari Jangwani yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
  (Picha na Eleuteri Mangi)
  ……………………………………………………………………..
  Na Eleuteri Mangi 
  Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Jangwani wameaswa kutumia muda wao vema wakiwa shuleni kwa kuwekeza kwenye elimu ambayo inasaidia kumbadilisha mtu na hatimaye kubadilisha jamii nzima. 
  Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Jangwani iliyopo manispaa ya Ilala Jijini Dare s salaam.
  “Ukizaliwa mwanamke, tambua kuwa wewe ni kiongozi wa kwanza katika jamii, hivyo tumia vipaji vyako kama ulivyojaliwa na Mwenyezi Mungu ukizingatia suala la nidhamu ambayo ndiyo msingi wa mafanikio yote yatakayowasaidia katika maisha yenu ndani ya jamii” alisema Tausi. Tausi alisisitiza kuwa watu wengi duniani wanaofanikiwa wanaongozwa na nidhamu bora waliyonayo ambayo imewasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea, wanafunzi hao wametakiwa kuiga mfano huo ili waweze kufanikiwa maisha yao kwa manufaa yao binafsi, jamii na taifa kwa ujumla.
  Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya sekondari Jangwani Geraldine Mwanisenga alipokuwa akitoa taarifa fupi ya shule kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo alisema kuwa shule yake ni miongoni mwa shule kongwe nchini ambazo zinazofanya vizuri kitaaluma na masuala mengine yasiyo ya kitaaluma.
  Kuhusu taaluma, Mkuu huyo alisema kuwa shule yake imeendelea kufanya vizuri na kushika nafasi ya juu katika matokeo ya mitihani ya taifa ambapo mwaka huu imeshika nafasi ya kwanza kwenye matokeo ya kidato cha nne miongoni mwa shule za sekondari za serikali katika Mkoa wa Dar es salaam. 
  Mkuu huyo wa shule alisema kuwa siri kubwa ya mafanikio yao inatokana na kujiweka malengo, mikakati na kuhakikisha vyote inatekelezwa kwa wakati.
  Miongoni mwa mikakati hiyo ni kufundisha masomo ya ziada na rekebishi, kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo, ushirikiano baina ya Bodi ya shule, wazazi, wafanyakazi wanafunzi na wadau wengine wa elimu ikiwa ni chachu ya mafanikio ya shule. Aidha, Mkuu wa shule mwalimu Geraldine amewaasa wahitimu hao watumie elimu waliyoipata wakiwa shuleni hapo kama silaha ya ukombozi kwenye jamii, maana jamii inahitaji wasomi ili kuikomboa kifikra, kiuchumi, kijamii na kisiasa.
  Naye mwanafunzi aliyepata vyeti mbalimbali vya taaluma takribani saba kwa kufanya vizuri katika masomo ya Kemia, Biyolojia, Fizikia, Hesabu, cheti cha kuwa mwanafunzi bora katika masomo, uongozi, uongozi bora pamoja na zawadi Rosemary Mushi alibainisha kuwa ilikuwa ndoto yake kuja kuwa mwanafunzi bora maana alipokuwa kidato cha nne zawadi hiyo ilienda kwa mwanafunzi mwingine ambapo hatua hiyo ilimpa hamasa ya kusimamia azma yake kwa moyo wote.
  “Leo ninafuraha sana maana ilikuwa ndoto yangu kuja kuchukua vyeti vyote ambapo ilinilazimu kusoma sana na kufaulu vizuri ili nifikie ndoto yangu ya maisha ya kuwa daktari wa watoto” alisema Rosemary.
  Rosemary aliushukuru uongozi wa shule, walimu, wafanyakazi wasio walimu na wanafunzi wenzake kwa ushirikiano mzuri alioupta kutoka kwao wakati wote alipohitaji masaada wao ili kufikia malengo yake ya kufaulu vizuri masomo yake na kumuwezesha kusonga mbele katika hatua nyingine ya elimu.
  Shule ya sekondari Jangwani ilinzishwa kwa historia ya kuwekwa jiwe la msingi liliwekwa mnamo Mei 28, mwaka 1928 na Kiongozi Mkuu wa ukoloni wa Mwingereza wakati huo Sir Donald Cameroon na kuifanya shule hiyo kuwa na umri wa miaka 87 ambapo kwa sasa ina jumla ya walimu 102, wafanyakazi wasi walimu 21, wanafunzi 1150 miongoni mwao wanafunzi 70 ni wenye mahitaji maalum kulingana na mahitaji ya sera ya elimu chini ya mataala wa elimu jumuishi uliohimiza kusomesha wanafunzi wenye mahitaji maalum.

  0 0

   Mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa katikati akizungumza na Vijana wa Kata ya Selela (hawapo pichani) wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga
   
   Vijana wa Kata ya Selela wakisikiliza kwa makini mada zilizokua zikitolewa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.
   Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Mesha Singoyo akifafanua jambo kwenye semina ya vijana wa Kata ya Selela kuhusu Ujasiriamali, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha

   Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga (kulia) akizungumza na wanakikundi cha Naisho wanaomiliki mradi wa kunenepesha ng’ombe na kuziuza wakati wa kutembelea miradi ya vijana wa Kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Wapili kushoto ni mhamasishaji kutoka Wizara hiyo Bibi. Ester Riwa na wanne kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.

   Baadhi ya ng’ombe zinazomilikiwa na vijana wa Naisho Group zikiwa machungani katika kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.
   Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele (wapili kulia) akifafanua jambo walipotembelea mradi wa kikundi cha Songambele kinachojishughulisha na kilimo katika Kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Kulia ni mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa.

  Moja ya shamba la mahindi linalomilikiwa na kikundi cha Songambele katika kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Mondili Mkoani Arusha. Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Monduli

  0 0

  Rais mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiingia chumba cha mkutano cha Nyerere ndani ya mjengo wa Ubalozi Washington, DC siku ya Ijumaa April 24, 2015 kulikokua na kikao cha Mabalozi wa heshima kilichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Balozi Liberata Mulamula kwa ajili kuongelea maswala mbalimbali zikiwemo changamoto za utalii na uwekezaji nchini Tanzania na jinsi gani ya kukabiliana nazo, mbali na Mabalozi hao wa heshima na marafiki zao wengine waliohudhuruia kikao hicho ambacho kilikua sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano ni wawakilishi wa Taasisi za Diaspora za Kitanzania zinazopigana kusaidia maswala ya uwekezaji na Utalii kwa nchi yao Tanzania. Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi pia aliongozana na mkewe Mama Sitti Mwinyi.
  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakiwemo Mabalozi wa heshima wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa za Tanzania na Marekani.

  Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Mabalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa  taasisi mbalimbali za Kimarekani zinazotangaza utalii wa Tanzania nchini Marekani na baadae kumkaribisha kuongea nao.

  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani anyoamtambulisha mbele ya mabalozi wa heshima na kwamba yeye Rais mstaafu ndiye aliyefanya mageuzi ya mfumo wa uchumi Tanzania tunaoendelea nao hivi sasa.

  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiongea na Mabalozi wa Heshima kuwashukuru kwa kuipenda na kuitangazaTanzania nchini Marekani na kuwaasa wasichoke kwa wao wamekua chachu ya maendeleo ya nchi aipendayo Tanzania.

  Mbalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa taasisi zinazotangaza Utalii na uwekezaji Tanzania wakimsuikiliza Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
   Picha ya pamoja.
  Mayor De  Andre Windom wa mji wa Highland Park jimbo la Michigan akipata picha na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimuaga Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi wakati walipokua waiondoka baada ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kumaliza kufunga kikao cha Mabalozi wa Heshima Ubalozini hapo. Picha zote na Vijimambo, Kwanza Production

  0 0

  Mwandishi wa vitabu Yasin Kapuya akimwelezea Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ya jinsi gani vitabu vyake vinavyoweza kumkwamua mwananchi wa hali ya chini na kumfikisha juu katika kumboreshea maisha mapya. Akijitolea mfano wake mwenyewe alipoanzia shimoni Kariakoo mpaka kufika nchni Marekani na sasa kualikwa katika mikutano mikubwa ya kutoa semina ya jinsi gani unavyoweza au kampuni inavyoweza kuwa namba moja katika sekta ya biashara.
  Mwandishi wa vitabu Yasin Kapuya akichangia jambo na Katibu Mkuu wa Rais mstaafu Bwn. Abdallah Makame (kulia) aliokua akiongea na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi siku ya Ijumaa April 24, 2015 jijini Washington, DC nchini Marekani.
  Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya wakiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakishikilia bango la kitabu chake kipya kitakachotoka hivi karibuni.

  Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya akimkabidhi Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi moja ya vitabu vyake.

  Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya akiagana na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Picha na Vijimambo, Kwanza Productionolder | 1 | .... | 511 | 512 | (Page 513) | 514 | 515 | .... | 1897 | newer