Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 512 | 513 | (Page 514) | 515 | 516 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana,viongozi wa CCM , wananchi na mafundi  wa mradi wa umeme kubeba nguzo za  umeme katika  kitongoji cha Ngalawale Ludewa kijijini kama  sehemu ya kuhamasisha wananchi kushiriki maendeleo

  Mbunge Filikunjombe wa kwanza  kulia na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya wa  kwanza  kulia wakishirikiana na mafundi wa maradi wa  umeme vijiji kuvuta kama kwa ajili ya kusimamisha nguzo ya  umeme

   mbunge Filikunjombe kulia  na diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchilo wakifukia  nguzo ya  umeme
  Wananchi na  mbunge  wakisaidiana kufukia nguzo ya  umeme

  wananchi na mafundi wa  umeme  wakijiandaa kubeba  nguzo

  mbunge Filikunjombe  akishiriki  kubeba  nguzo ya  umeme

  wananchi na  mbunge Filikunjombe wakiwa  wamebeba nguzo ya  umeme


  katibu  mwenezi wa CCM mkoa wa NJOMBE Honoratus Mgaya akichimba shimo la nguzo ya umeme

  mbunge Filikunjombe akiwa  chini ya shimo akishiriki  kuchimba shimo la nguzo ya  umeme  kitongoji cha ngalawale  kijiji  cha ludewa wengine ni diwani wa kata ya  Ludewa MONICA MCHILO ,katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya na katibu mwenezi  wa CCM ludewa FELIX Haule  wakishirikiana na mbunge  wao

   mbunge Filikunjombe akitoka  katika  shimo baada ya  kumaliza  kuchimba  shimo  moja la mfano kama kuhamasisha wananchi kushiriki katika maendeleo 

  0 0

  Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani akifungua mkutano wa Mabalozi wa Heshima uliofanyika siku ya Ijumaa April 24, 2015 Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Mkutano huo ulizungumzia  uwekezaji na Utalii zikiwemo Changamoto zake na jinsi ya kukabiliana nazo. Pia katika mkutano huo uliokua sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano uliudhuria pia na Viongozi wa Taasisi za Diaspora wa Tanzania ambao wanaguswa na kuiona nchi yao ikipiga hatua ya maendeleo katia sekta ya uwekezaji na Utalii.

  Abdul Majid mwanaDiaspora Mtanzania anayeishi California nchini Marekani akielezea huduma kwa wateja bado ipo kiwango cha chini nchini Tanzania na jinsi gani ikiboreshwa inavyoweza kunua uchumi wa Tanzania.

  Balozi wa Heshima Mhe. Kjell Berch akichangia na kuelezea majukumu ya Balozi wa heshima.

  Rais wa East Africa Diaspora Business Counsil Benedict Kazora ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas akichanganua na kutoa maelezo yanayoweza na kurahisiha maswala ya uwekezaji na kukosoa baadhi ya makampuni yanavyowekeza Afrika kwa kujinufaisha yenyewe.

  Karen Hoffman Rais wa The Bradford Group kutoka New York akielezea sekta ya Utalii na utangazaji wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani.

  Balozi wa Heshima Mhe.Cemil Teber kutoka New Mexico akichangia jambo.

  Balozi wa Heshima kutoka Ohio Mhe. Patrick Griswold akielezea sekta ya uwekezaji na changamoto inazokutana nazo huku akitoa mfano wake mwenyewe alipokua meneja mkuu wa General Tire miaka ya nyuma na tangia alipoondoka kiwanda kikafa na sasa anatarajiwa kwenda tena Tanzania kujaribu kukifufua upya kiwanda hicho.

  Mkutano wa Balozi Liberata Mulamula na Mabalozi wa Heshima ukiendelea

  Wakati wa chakula. Picha zote na Vijimambo, Kwanza Production

  0 0

  Katika shamrashamra za kusherehekea Miaka 51 kuungana Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Timu ya Zanzibar Diaspora​ nchini Marekani imeifunga bao 7-1 jirani zake timu ya Tanganyika USA.
  Kocha wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir pamoja na Kapteni Deddy Rouba​ wakikabidhiwa Kombe la Muungano.

  Mechi hiyo ambayo imehudhuriwa na mgeni rasmi rais mstafu wa awamu ya pili wa Tanzania Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi. ilifanyika katika viwanya vilivyopo Walker Mill Road District Heights Maryland, ambapo pia ilihudhuriwa na balozi wa Tanzania nchini Marekan Mhe. Liberata Mulamula.

  Mechi hizo hufanyika kila mwaka kwaajili ya kusherehekea kuungana kati ya Tanganyika na Zanzibar April 26, 1964.
  Rais mstafu wa awamu ya pili wa Tanzania Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi baada ya kusalimiana na wachezaji wa timu zote mbili

  Mapema Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi aliwataka waTanzania kuungana kwa pamoja bila ya kujali tafauti zao.Wakati huo huo kabla ya mechi kuaza Alhajji Ali Hassan Mwinyi alisalimiana na timu zote mbili na kuupiga mpira kuashiria kuaza kwa mechi hiyo.
  Kikosi kamili cha timu ya Zanzibar Diaspora
  Mashindao hayo ambayo yaliwapa ushindi mnono Timu ya Zanzibar Heroes baada ya kichapo cha 7-1 dhidi ya Timu ya Tanganyika katika mechi ya kutafuta Bingwa wa Kombe la Muungano, bao la kwanza kwa timu ya Zanzibar lilifungwa kwa njia ya Penalti mfungaji wa bao hilo alikuwa Yahya Kheri na magoli mawili ya lifungwa na Wingi machachari Abdulla J. Somania, mbao hadi timu kipindi cha kwanza kumalizika Timu ya Tanganyika ilifungwa 3-0


  Kipindi cha pili kuaza, Tanganyika waliingia kwa kasi, na katika mchezo waliocheza haukuwasumbua sana timu ya Zanzibar kutokana na udhibiti wa wachezaji wanne  ambao wazoefu wa zamani katika funi ya soka waliweza kuumiliki mchezo huo, mmoja wao alikuwa Captain Deddy Rouba​ ambae alikuwa Super Middlefield wa mchezo huo, aliposaidiana na Yussuf Mecca kutoka Columbus,Ohio,Yahya pamoja na Ally, ambao wametawala ngome ya timu ya Tanganika, bao la nne na la tano yalifungwa na Mshambuliaji hatari Lodi Mohammed, na bao la sita na  lasaba, lilifungwa na wingi hatari na mchezaji nyota ambae amechukua tunzo la mchezaji bora katika mchezo huo Abdulghan Ali Himid ambae baada ya mchezaji Yussuf Mecca kupata Redcard kwa kosa la kulalamika kwa goli la offside lilifungwa dakika ya 76 za mchezo huo na kujikuta timu ya Tanganyika kuambulia kipigo cha magoli 7-1, chini ya Kocha Seif Ameir wa Timu ya Zanzibar Diaspora Nchini Marekan.
   Kikosi cha timu ya Tanganyika 
  Tanganyika na Zanzibar kama ishara ya Muungano
  Abdulghan Ali Himid akipokea tunzo la uchezaji bora 
  Ally akishangilia Ushindi wa ZADIA
  Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Omar Ally Kocha Seif Ameir wa Timu ya Zanzibar Diaspora Nchini Marekani wapili kushoto akipata picha na wachzaji wa Zanzibar Diaspora

  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika  kwenye Uwanja wa Mongella mjini Nansio wilayani Ukerewe mkoani Mwanza. 


  Mbowe akisalimiana na mlemavu wa viungo alipowasili kwa chopa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mongella mjini Nansio Ukerewe mkoani Mwanza juzi.

  0 0

  Mzee Yusuf akiimba ndani ya Dar Live.
  Mashabiki wakiserebuka huku wakiwa na picha ya Mzee Yusuf.
  Leila Rashid akipagawisha mashabiki.
  Mashabiki wakiserebuka kwa raha zao.
  Shabiki (aliyeinama) akionyesha kipaji cha kukata viuno.
  Wanenguaji wa Jahazi wakipozi mbele ya kamera.
  Shabiki akimtunza pesa Hadija Yusuf.
  Musa Musa akilicharaza gitaa.
   
  Shabiki aliyetaka kuingia bure ukumbini baada ya kutaitiwa na walinzi.
  \Fatma Kassim akiimba.
  MASHABIKI wa taarab nchini jana walipata walichokitaka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani  wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

  Katika onyesho la jana, Kundi la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf lilimwaga burudani ya nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki kibao waliofurika katika ukumbi huo ambao una kila aina ya ‘mafuraha’ ikiwa ni pamoja na makulaji na vinywaji licha ya hali ya hewa kujenga tishio la mvua kila mara. (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL) 

  0 0

  Afisa Uhakiki, Neema Chilipweli (kushoto) akiihakiki familia ya Yohanna Bukuru (watatu kulia), pamoja na mkewe na watoto wao sita kutoka Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda Vijijini, Mkoa wa Katavi, ikiwa ni hatua ya awali ya uhakiki ili familia hiyo iweze kupewa vyeti vya uraia wa Tanzania. 
  Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania.
   Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo ambapo wiki hii zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo nchini, linatarajiwa kukamilika. Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hivyo.

  Na Felix Mwagara, Mishamo.
   ZOEZI la ugawaji wa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa waliokuwa Wakimbizi wa Burundi zaidi ya 152,572 walioingia nchini mwaka 1972 linatarajiwa kumalizika wiki hii katika Makazi ya Mishamo mkoani Katavi.
  Wakimbizi hao ambao waliomba uraia wa Tanzania mwaka 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, sasa watakuwa raia halali wa Tanzania kwa kuwa na uwezo wa kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo za Udiwani na Ubunge. 
  Akizungumza wakati wa ugawaji wa vyeti hivyo, Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile alisema ugawaji wa vyeti hivyo ulianza Novemba 24 mwaka jana, katika Makazi ya Katumba yaliyopo mkoani Katavi, ambapo watu 56,554 walipewa vyeti vya uraia na baadaye zoezi la ugawaji likahamia katika Makazi ya Ulyankulu mkoani Tabora, ambapo watu 43,453 tayari wamepewa vyeti hivyo.
  Nisajile alisema katika makazi yake ya Mishamo ambapo ugawaji wa vyeti hivyo unaendelea na unatarajiwa kumalizika ifikapo Aprili 30 mwaka huu, ambapo katika makazi hayo zaidi ya raia wapya 52,565 wanatarajiwa kupewa vyeti vyao. 
  “Mpaka leo hii (jana) katika makazi haya ya Mishamo kama unavyoshuhudia ndugu mwandishi umati wa watu wakizidi kuingia katika kituo hiki, mpaka sasa tayari tumegawa vyeti 131,351 kwa raia hawa wapya, na tunatarajia ifikapo wiki ijayo Aprili 30 tutakuwa tumemaliza ugawaji wa vyeti hivi katika vijiji vyote, na zaidi ya raia wapya 152,572 katika Makazi ya Katumba, Ulyankulu na Mishamo watakuwa wamepewa vyeti hivi na zoezi litakuwa limekamilika” alisema Nisajile.
  Alisema Serikali ndiyo inatoa vyeti hivyo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), ambapo wote kwa pamoja wamejipanga kikamilifu ili ugawaji huo unamalizika salama na kwa umakini wa hali ya juu.  Hata hivyo, Nisajile alisema kuwa, makazi yake ya Mishamo Ya vijiji 16, hivyo kabla ya kuanza kugawa vyeti hivyo, huwa wanatoa elimu kwa kuwahamasisha wakazi wa kijiji ambacho kinatarajia siku ya pili yake kwenda kugawiwa vyeti hivyo. Alisema katika uhamasishaji huo, yeye Mkuu wa Makazi anaambatana na Maafisa Uhamiaji na UNHCR ili waweze kuhamasisha mambo mbalimbali kuhusiana na umuhimu wa vyeti hivyo.
  Aliongeza kuwa, vyeti hivyo vinatolewa kwa mtu mmoja mmoja ambapo raia mpya anatakiwa aje na karatasi ya uthibitisho wa picha za wanafamilia ili kuiwezesha Serikali na UNHCR kutambua kabla ya kutoa cheti kwa wahusika hao na kila anayepewa cheti hicho anatakiwa kusaini. Zoezi la ugawaji wa vyeti vya uraia kwa raia hao wapya lilikuwa la miezi mitano, ambapo lilianza Novemba 24 mwaka 2014, na Aprili 30 wiki hii, linatarajiwa kukamilika.

  0 0

  unnamed634
   Michuano ya NACTE INTER COLLEGE CHAMPIONSHIPS TANZANIA-DAR ES SALAAM 2015, Leo imeendelea tena kwenye Viwanja vya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambako Timu za kundi A zimecheza na mchezo uliokuwa gumzo ni baina ya Chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere dhidi ya Chuo cha Bandari, ambapo hadi Mwisho wa Mchezo Timu hizo zimeweza kufungana 3-3.

  Timu ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ndiyo waliokuwa wa kwanza kupachika mabao 2 kipindi cha kwanza, ambapo hadi timu hizo zinakwenda Mapumziko Mwalimu Nyerere ilikuwa mbele kwa 2-0.
  kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote zilifanya mabadiliko ya hapa na pale lakini ni ya Mwalimu nyerere tena iliyoweza kupata bao la tatu kabla ya Timu ya Bandari Kusawazisha mbao yote kwenye dakika za Mwisho za mchezo huo  ambao hakika ndiyo uliokuwa gumzo katika siku ya leo.

  Mchezo mwingine ilikuwa ni kati ya IFM dhidi ya chuo cha Taasisi ya  Elimu ya Watu wazima, ambapo mchezo huo timu hizo zimekubali kugawana pointi moja moja sambamba na wenzao wa chuo cha Kilimanjaro kwa mama ngoma waliogawana pointi na chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT). Matokeo ya kundi la Uwanja wa Ustawi wa Jamii timu ya Chuo cha Biashara CBE, wamefanikiwa kujipatia Pointi zao 3 na magoli mawili baada ya timu ya chuo cha Uhasibu kushindwa kutokea Uwanjani katika kipindi kilichopangwa.

  mchezo mwingine ilikuwa ni baina ya timu ya Chuo cha kodi ambao wamecheza na timu ya kitivo cha engeneering ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam zimeweza kugawana Pointi baada ya timu zote kushindwa kufika Uwanjani.
  wakati mchezo wa Mwisho wenyeji timu ya chuo cha ustawi wa jamii imeweza kujipatia Ushindi mnono wa Mabao mawili na hivyo kujizolea pointi zote tatu dhidi ya timu ya chuo cha Wauguzi wa Muhimbili, ambapo michezo hiyo awali ilipangwa kufanyika kwenye Viwanja vya chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini imelazimu kubadili Uwanja kutokana na Viwanja vya Chuo Kikuu kuwa na ratiba katika kipindi hiki hivyo michezo yote sasa itafanyika kwenye viwanja vya Ustawi wa jamii katika hatua hii ya makundi.

  Kundi B ambao michezo yake inafanyika kwenye Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mchezo wa kwanza ulizikutanisha timu za chuo cha St.Joseph, ambapo katika mchezo timu ya St. JOSEPH ilifanikiwa kuibua na ushindi wa mabao mawili kwa bila (2-0) dhidi ya timu ya chuo cha Njuweni Insititute. mchezo mwingine Timu ya chuo cha Wauguzi Tumbi ikafanikiwa kupata Point 3 baada ya kujipatia mabao mawili dhidi ya kitivo cha UDBS ambao walishindwa kutokea uwanjani kabla ya DACICO kidedea dhidi ya timu ya chuo cha taifa cha Teckinolojia (D.I.T) .

  Washindi wawili katika kila kundi ndiyo watakaoingia hatua ya Robo fainali itakayoshirikisha jumla ya timu nane huku timu mbili zikipewa nafasi ya kuingia kwa njia ya upendeleo(Best Looser). Michezo hii inaratibiwa na Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Enter tainment C.o Ltd, ya jijini Dar es Salaam

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye koti) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Usalama wa Hotel ya New Afrika Hotel ya Jijini Dar es Salaam, Bw. Isack Kabugu kuhusu hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika mtungi wa kuhifadhi moto katika Hoteli hiyo ambayo ilileta athari katika majengo ya ofisi zilizopo jirani na hoteli hiyo ikiwemo ofisi ya Idara ya Habari na Ofisi ya Bodi ya Filamu Tanzania zilizopo chini ya Wizara hiyo leo (Jumapili April 26, 2015).
  ng2Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye koti) akijionea athari mbalimbali zilizosababishwa na hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika mtungi wa kuhifadhi moto katika Hoteli hiyo hatua iliyosababisha uharibifu wa majengo ya ofisi zilizopo jirani na hoteli hiyo ikiwemo ofisi ya Idara ya Habari na Ofisi ya Bodi ya Filamu Tanzania zilizopo chini ya Wizara hiyo leo (Jumapili April 26, 2015).
  ng3Mafundi mitambo wa katika hoteli ya New Afrika ya Jijini Ddar es Salaam akiangalia athari zilizotokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika mtungi wa kuhifadhi moto katika Hoteli hiyo ambayo ilileta athari katika majengo ya ofisi zilizopo jirani na hoteli hiyo ikiwemo ofisi ya Idara ya Habari na Ofisi ya Bodi ya Filamu Tanzania zilizopo chini ya Wizara hiyo leo (Jumapili April 26, 2015).
  (Picha na MAELEZO)

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo  kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akienelea kuwapungia mkono kwa furaha kuwasalimia wananchi
   Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa na Viongozi wengine wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR

  0 0

   Mandhari ya nje ya Hoteli ya Kisasa ya Shangani Hotel Apartments iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego usiku jana mjini Mtwara. Pia ulizinduliwa Mgahawa wa kisasa ambapo wageni waalikwa walifaidi kula chakula cha usiku kilichopikwa na wapishi waliobobea kwa mapishi yenye vionjo vya kila aina.

  Wageni wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa hoteli hiyo itakayozidi kuongeza hadhi ya Mji wa Mtwara ni, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara, Seleman Mtalika na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma S. Ally.Pia waliwepo wageni wengine kutoka taasisi mbalimbali pamoja na wafanyabishara. Hoteli hiyo inamilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji Akida Zidikheri.
  Akida Zidikheri (kushoto) mmiliki wa Shangani Hotel Apartments na . Said Aboud (kulia)pamoja na Mstahiki Mayor wa Manispaa ya Mtwara, Selemani Mtalika ndani ya mgahawa huo wa kisasa uliopo katika hoteli hiyo.
   Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri wakiwa ndani ya moja ya Apartments pamoja naMkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego (kulia), na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara  Fatma S. Ally (kushoto).

   Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri wakiwa ndani ya moja ya Apartments pamoja naMkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego (kulia),
   Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri akiwaonesha wageni waalikwa sehemu ya kutengenezea mikate (bakery), iliyomo kwenye jiko la mgahawa huo.
   Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara, Seleman Mtalika akimkaribisha mkuu wa Wilaya ili aweze kumkaribisha rasmi Mkuu wa Mkoa ili azungumze na wageni waalikwa.

   Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri akitoa shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria ufunguzi huo.
   Wakipata mlo wa usiku kwenye mgahawa huo, kutoka kushoto ni;Mstahiki Mayor wa
  Manispaa ya Mtwara, Selemani Mtalika, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego Mwajuma Mchuka Station Manager wa ATC Mtwarana.

   Wageni waalikwa wakipta chakula cha usiku kwenye mgahawa huo
  Ni kula kwa kwenda mbele

  0 0

  DSC_0351

  Cake maalum iliyoandaliwa kwenye sherehe za uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
  DSC_0354
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins kabla ya zoezi la kuwasha mishuma 70 kwenye cake hiyo ikiwa ni uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Mshehereshaji wa sherehe hizo Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
  DSC_0382
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins wakiwa wamejumuika na wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye mnuso huo.
  DSC_0361
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiwasha nakshi nakshi zilizowekwa kwenye cake maalum ya uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini. Anayemkingia upepo ni walioandaa Cake hiyo kutoka kampuni ya M.E Gift Wraps and Delivery huku Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins naye akijianda kufanya zoezi hilo.
  DSC_0372
  Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakishiriki kuwasha mishumaa 70 iliyowekwa kwenye cake hiyo.
  DSC_0380
  IMG_0162
  DSC_0388
  Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakikata cake kwa niaba ya wafanyakazi wenzao.

  DSC_0396
  DSC_0404
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akila kipande cha cake kwenye mnuso huo.
  DSC_0407
  Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakilishana cake kabla ya kupata chakula cha usiku wakati wa shamra shamra za uzinduzi wa miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  DSC_0412
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi wenzake.
  IMG_0172
  Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakijumuika kwenye chakula cha usiku wakati wa sherehe za uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
  IMG_0179
  IMG_0188
  IMG_0225
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifuatiwa na Afisa Habari wa UNIC, Usia Nkhoma Ledama wakipakua chakula cha jioni kwenye mnuso huo.
  IMG_0190
  IMG_0193
  Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakijisevia nyama choma ndani ya hoteli ya White Sands.
  IMG_0220
  IMG_0197
  IMG_0202
  IMG_0213
  IMG_0207
  IMG_0222
  BAADA YA KUPATA BUFEE LA NGUVU ULIWADIA ULE WASAA WAKUFANYA DIGESTION YA CHAKULA KWA KUSAKATA RHUMBA...
  IMG_0253
  Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakisakta rhumba kwenye hafla ya uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
  IMG_0303
  Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakionyesha ufundi wa kusakata rhumba kwenye mnuso huo.
  DSC_0502
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye shati ya kijivu) naye hakubaki nyuma alionyesha umahiri wake.
  DSC_0493
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins naye alionyesha ufundi wake kama anavyoonekana pichani.
  DSC_0484
  Usia Nkhoma Ledama naye akasema hata wasinichezee hawa.... akajibu mapigo.
  DSC_0487
  Burudani ikiendelea kwa furaha na amani.
  DSC_0533

  0 0

  Mjane wa marehemu Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita, Ngeme Mbita (katikati) akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu, Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo.  Brigedia Mbita amefariki leo katika Hospitali ya Lugalo. (Picha na Francis Dande)
   Mjane wa marehemu Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita, Ngeme Mbita (katikati) akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu, Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo.  Brigedia Mbita amefariki leo katika Hospitali ya Lugalo.
   Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba akiwa nyumbani kwa marehemu, Brigedia Jenerali Hashim Mbita Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Heshima waShirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Said El Maamry na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku.
  Waombolezaji
   Ndugu na jamaa wakiwa katika msiba wa Brigedia Hashim Mbita.
   Waombolezaji wakiwa na huzuni nyumbani kwa marehemu.
  Baadhi ya ndugu na jamaa wakiwa na majonzi.
  Wanafamilia wakiwa katika hali ya huzuni leo.
  Baadhi ya ndugu na jamaa wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu.
   Mtoto wa marehemu, Idd Mbita akitoa taarifa za shughuli za mazishi ambapo marehemu atazikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano saa 10 jioni.

  Na Mwandishi Wetu
  Rais Jakaya Kikwete amepokea kwa majonzi makubwa kufuatia kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), Chama cha TANU na Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Africa – Liberation Committee of the African National Unity (OAU), Brigedia Jenerali Hashim Mbita.


  Rais Kikwete amemwelezea marehemu Mbita kama mmoja wa viongozi ambao wameifanyia Tanzania mambo  mengi na kwa miaka mingi.   Kutokana  na taarifa za msiba huo, Rais Kikwete ameelekeza Serikali na Jeshi kushirikiana na familia kusimamia msiba huo na kuandaa mazishi yake.


  Rais Kikwete alipokea taarifa hiyo ya msiba alipoingia tu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kuongoza maelfu ya wananchi kuadhimisha miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliuelezea msiba huo kama msiba wa simanzi kubwa.


  “Ni wachache katika nchi yetu wanaoweza kulinganishwa na Mzee Hashim Mbita kwa kiwango cha utumishi uliotukuka, wa miaka mingi na usiokuwa na kasoro. Katika utumishi wa Serikali alipata kuwa Mwandishi wa Habari Mkuu wa Idara ya Habari na pia kuwa Mwandishi wa Habari wa Rais kabla na baadaye kuwa Balozi wa Tanzania katika Zimbabwe. Kazi zote alizifanya kwa ufanisi mkubwa sana,”alisema Rais Kikwete na kuongeza:


  “Katika Chama cha TANU alikuwa Katibu Mtendaji wa Chama na katika Jeshi letu makini, Mzee Mbita alipata na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali, yote mambo makubwa kweli kweli.
  “Lakini ilikuwa katika nafasi ya Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Afrika ambako Mzee Mbita alikamilisha utumishi wake kwa kusimamia shughuli nzito ya kuwasaidia ndugu zetu Kusini mwa Afrika kwa miaka 20 mfululizo, miongo miwili, na kuweza kupata uhuru wao. Hakuna mpigania uhuru katika Msumbiji, Zimbabwe, Namibia, Angola na hatimaye katika Afrika Kusini ukiondoa nchi nyingine kama Cape Verde, asiyejua mchango wa Mzee Mbita. 

  Wote hawa amewatumia vizuri, kwa ufanisi, kama mlezi, kama kiongozi, kama kamanda hadi wakafanikisha kazi ya ukombozi. Huu ni mchango mkubwa kweli kweli.   “Kitendo chake cha mwisho cha utumishi, kilikuwa kuongoza shughuli za Mradi wa Hashim Mbita wa Kuweka Kumbukumbu za Harakati za Ukombozi Kusini mwa Afrika na Kuenzi Viongozi Wakuu (Hashim Mbita Project to Honour Outstanding Leaders), kazi ambayo nayo aliifanya kwa uwezo na ufanisi mkubwa na ripoti yake tukaizindua mwaka jana pale Victoria Falls, Zimbabwe wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),”alisema Rais Kikwete.  Alisema Zimbabwe ilitangaza kumpa Mzee Mbita Nishani ya The Royal Order Munhumutapa yenye kutambua mchango wake katika harakati za ukombozi wa Zimbabwe.  Mzee Mbita amekuwa raia wa sita wa kigeni, na wa kwanza asiyekuwa rais, kupata heshima hiyo ya juu kabisa ambayo hutolewa na Taifa la Zimbabwe kwa wageni ambao wamechangia Uhuru wa Zimbabwe. 


  Viongozi watano wa mwanzo kupata Nishani hiyo, mwaka 2005, walikuwa ni Marais na Viongozi Waanzilishi wa Kundi la Nchi za Frontline States dhidi ya Ukoloni na Ubaguzi wa Rangi, Marehemu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Kenneth David Kaunda wa Zambia, Marehemu Sir Seretse Khama wa Botswana, Marehemu Samora Moises Machel wa Musumbiji na Marehemu Augustinho Neto wa Angola.  Brigedia Jenerali mstaafu, Hashim Mbita amefariki dunia katika Hospitali ya Kuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, Dare es Salaam. Mbita ambaye alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), alifariki dunia leo majira ya saa 3 asubuhi.

  Akizungumza nyumbani kwa marehemu Chang’ombe, Temeke, mtoto wa marehemu, Iddi Mbita amesema baba yake alifariki kutoka na kusumbuliwa na shinikizo la damu,
  “Mzee alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu na leo (jana) ameamka salama, akanywa chai na dawa, kisha akaomba kupumzika. Baada ya muda mfupi akafariki dunia asubuhi muda saa 3,” alisema Iddi.

  Alisema marehemu Mbita alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la hilo tangu Agosti mwaka jana, hivyo kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). 
  Alisema akiwa katika hospitali hiyo, aliwekwa chini ya Uangalizi Maalum wa Daktari (ICU).

  Alisema alikaa katika hospitali hiyo kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu na ilipofika Oktoba mwaka jana alipelekwa nchini India kwa matibabu zaidi. 

  Iddi alisema alikaa nchini India kwa miezi miwili na Januari mwaka huu alirudishwa nchini na kuendelea na matibabu nyumbani kwake Chang’ombe jirani na Klabu ya TCC Chang’ombe.

  Alisema kwamba Machi 23 mwaka huu Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ walimfuata na kumchukua kwa ajili ya kumpatia matibabu zaidi.

  Alisema baada ya vipimo mdaktari katika Hospitali ya Lugalo walibaini kuwa kuna matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakimsibu hivyo aliendelea kupata matibabu hadi alipoaga dunia.

  “Unajua ugonjwa ulikuwa umemla sana hivyo kusababisha organ (mfumo wa viungo vya mwili)  mbalimbali kupata hitilafu,” alisema Iddi.   
  Alisema marehemu ataswaliwa nyumbani kwake Chang’ombe na mwili utapelekwa katika msikiti wa kwa Mtoro, Kariakoo na baadaye mazishi yatafanyika siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu saa 10 jioni.


  0 0

   mwanahabari frank kibiki  , aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec akiwa na  watoto waliofanyiwa ukaliti wa kijisia pamoja mkuu wa kituo cha matumaini centre
  mwandishi wa habari wa gazeti la mzalendo na uhuru TUMAINI MSOWOYA KIBIKI akiwa na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia
  mwandishi wa habari wa gazeti la mzalendo na uhuru TUMAINI MSOWOYA KIBIKI akiwa na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia pamoja na mkuu wa kituo cha matumaini centre.

  Na fredy mgunda,iringa

  Ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike ndio inaonekana kuwa sababu  ya mkoa wa iringa kuzalisha wafanyakazi wengi wa kazi za ndani

  akizungumza na blog hii mwanahabari frank kibiki  , aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec.amesema kuwa watoto wengi wa kike hawapewi nafasi ya kwenda kusoma kutokana na tamaduni potofu hivyo waandishi wa habari tunatakiwa kuungana kuwapigania watoto hawa.

  Aidha KIBIKI amewataka wananchi wa mkoa wa iringa kushirikiana na mkuu wa kituo cha matumaini centre ili kuwasaidia watoto wa kike ambao wanaishi katika kituo hicho.

  lakini KIBIKI amewaomba viongozi mbalimbali na waandishi wa habari kupaza sauti zetu ili kukomeshakabisha suala la ukatili wa kijinsia ambao bado unaendelea hapa mkoani kwetu.

  Wananchi mkoani iringa wametakiwa kuwathamini na kuwapa elimu watoto wa kike ili kupunguza unyanyasaji wa kijinsia unaoendelea kwa sasa.

  Kwa upande wake mkurugenzi kituo cha matumaini centre HELLEN NKUNDA amesema kuwa amekuwa akipokea watoto wengi wa kike ambao wamefanyiwa ukatili wa kijinsia  na amekuwa akiwapokea na kuwapa elimu ya ufundi.

  Lakini NKUNDA amewataka watoto hao kuwa makini na waaminifu katika maisha yao ili wasirudie yale ambayo yalimtokea hapo awali na wasikubari kudanganywa tena.

  NKUNDA ameitaka serikali  kutoa elimu kuanzia shule ya msingi juu madhara ya ukatili ili kujenga jamii ambayo itakuwa na elimu juu ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsi hasa kwa watoto wa kike.

  Alimalizia kwa kumshukuru mwandishi wa habari frank kibiki kwa kutoa msaada wake kwa mtoto ambaye aliyekuwa amefanyiwa ukatili wa kijinsia.

  0 0

  Karibu katika sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout, Ameeleza mengi kuhusu kazi yake na familia kwa ujumla.

  Anavyokabiliana na kazi zake, changamoto za afanyalo, tuzo alizopata nk
  Na pia, kaeleza kuhusu mtazamo wake juu ya waTanzania (hasa wa Diaspora) na ushauri kwa kinamama wote 
  KARIBU.

  0 0

  Zilikuwa siku thelathini (haiyumkini kana kwamba ni zilizozidi masaa ya kawaida yazungukapo bila kubaini) zilizojaa majuto, maumivu makali yasiyomithilika wala kuelezeka.  Nilijiuliza kwa nini?  NIlijiona kana kwamba thamani ya utu wangu imetoweka.  Niliomba Mungu usiku na mchana ingali nikishindwa hata maneno wakati wa sala.

  Majuto ni mjukuu na ingali ya jana kamwe haiwezi kuwa kesho, achilia mbali ya leo.  Nimeamka kwani natambua kuna maelfu, mamia elfu ama hata mamilioni duniani kote wapitiao makubwa zaidi ya yangu yaliyojiri.

  Nimeamua, nimekata shauri, nimesimama, nimefuta chozi, sitaishi kwa kuwaza ikiwa kama ni njonzi;


  ‘NIMEAMUA KUPAZA SAUTI, NIMEAMUA KUWA SAUTI’.

  Haya ni machache latika kitabu chake kipya kikiitwa – Chozi la Sitti……Kwa nini ukose kuwa sehemu ya HISTORIA?


  02.05.2015 kuanzia saa moja usiku @Mlimani City Conference Hall…..Pata tiketi yako SASA: 0685 01 07 17


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano Dk.Mohammed gharib Bilali pamoja na Viongozi wengine wakiwa  katika picha ya pamoja baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Bw.Damian Zefrini Lubuva baada ya kumvalisha  Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha nishani Bw.Aboud Talib Aboud wakati wa hafla ya kutunuku Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu katika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akivalisha Nishani Bw,Mohammed Seif Khatibu wakati wa hafla ya kutunuku  Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu  katika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Cpl Laura Philip Mushi  Nishani ya Ushupavu wakati wa utoaji wa Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Madaraja mbali mbali katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Tanzania wakisimama wakati wimbo wa taifa ukipigwa baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares Salaam
   Miongoni mwa Wananchi na Viongozi walioteuliwa kutunikiwa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kutunikiwa nishani zao,[Picha na Ikulu,]
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) na makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika sherehe za utoaji wa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali  katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana
   Miongoni mwa Viongozi na Wananchi  walioteuliwa kutunikiwa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kutunikiwa nishani zao ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jana,[Picha na Ikulu,]
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Bw.Mabrouk Jabu Makame Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam


  0 0

   Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki akisalimiana na baadhi ya Wakufunzi wa chuo cha Polisi Moshi (CCP) wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua mafunzo yanayoendelea chuoni hapo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)

   Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki (kushoto) akiwasili katika chuo cha Polisi Moshi (CCP) wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua mafunzo yanayoendelea chuoni hapo.Katikati ni Mkuu wa Chuo hicho, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi na Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Omar Rashid (Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)
   
  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Moshi.
   
  Wakufunzi wa Chuo cha Polisi Moshi (CCP) wametakiwa kuendelea kutoa mafunzo kwa weledi ili kuweza kupata askari bora ambao watashirikiana na jamii katika kupambana na uhalifu hasa katika kipindi hiki ambapo kumeibuka uhalifu mpya kwa njia ya mitandao na unaovuka mipaka.
   
  Wito huo umetolewa jana mjini moshi na Naibu Inspekta Jenerali wa  Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi chuoni hapo ambapo alizungumza na wakufunzi hao na kuweka mikakati mbalilmbali ya kuboresha mafunzo katika chuo hicho.
   
  Naibu IGP Kaniki alisema, askari wakipata mafunzo bora wataongeza mbinu zitakazowezesha kukabiliana na  uhalifu huo na hivyo kuendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kushirikiana na jamii ambayo imekuwa msaada mkubwa wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
   
  “Ili kuhakikisha kwamba raia wa Tanzania na mali zao wanalindwa ipasavyo, Jeshi la Polisi hatuna budi kuendelea kubuni mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu wa kila aina unaobadilika mara kwa mara na hilo linawezekana kwa kuendelea kuwapatia askari wetu mafunzo yenye viwango vya kupambana na uhalifu unaokua kwa kasi”alisema Kaniki.
   
  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Polisi moshi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi alisema wanaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa mafunzo wanayotoa yanalenga katika mitaala ambayo wamekuwa wakiiboresha mara kwa mara ili kuendana na wakati kulingana na mazingira ya uhalifu unaotokea katika jamii.
   
  Alisema, mbinu za uhalifu zimekuwa zikibadilika kila siku hivyo, na wao kama chuo wamejikita kuhakikisha kuwa askari wanaopita katika chuo hicho wanazipata mbinu mpya na hivyo kuwa zaidi ya wahalifu ili waweze kupambana nao. 

  0 0

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa matibabu ya watoto 400 wenye matatizo ya kupinda miguu. Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah. (Picha na Francis Dande)
   Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kusaidia matibabu ya watoto 400 wenye matatizo ya kupinda miguu. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans 
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya kupinda miguu katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa  huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akionyesha picha za watoto wenye matatizo ya kupinda miguu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia matibabu ya watoto 400 wenye matatizo yakupida miguu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akionyesha picha za watoto wenye matatizo ya kupinda miguu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia Hospitali ya CCBRT katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa  huo.


  NA FRANCIS DANDE  BANK OF AFRICA-TANZANIA, leo imezindua rasmi kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia Hospitali ya CCBRT katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kupinda miguu.


  Msaada huu kwa Hospitali ya CCBRT utawezesha watoto kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kupata matibabu bure au kwa gharama nafuu ili kuwawezesha kutembea sawa sawa.


  Ugonjwa wa kupinda miguu unaweza kuathiri mguu mmoja  au yote miwili. Miguu iliyopinda huonekana kuingia ndani hasa katika goti.


  Bila kupatiwa  matibabu, wagonjwa wa aina hii mara nyingi hutembea kwa kutumia magoti au au pande wa pili wa nyayo zao, lakini wakipatiwa matibabu mapema wakati wa utotoni watoto hao huweza kutembea vema na hata kushiriki mchezo wa riadha.


  Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa BANK OF AFRICA-TANZANIA, Owusu- Amoah, alisema benki yake itaendelea kuisaidia CCBRT kwa kila hali, ikiwamo hilo suala la matibabu  kwa watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu ili kuboresha maisha ya  Watanzania.


  Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemann, alisema kuwa CCBRT imekusudia kuyabadili maisha ya Watanzania, lakini hawatafanikiwa kufikia lengo lao bila kupata msaada kutoka kwa washirika wakarimu kama BANK OF AFRICA-TANZANIA.


  “Kwa kusaidia matibabu ya  ya ugonjwa wa kupinda miguu, BANK OF AFRICA-TANZANIA itasaidia kuzuia  ulemavu miongoni mwa mamia ya watoto, hivyo kuboresha nmaisha yao,” alisema Telemann.


  Kampeni hiyo itahusisha wafanyakazi wa benki hiyo hapa nchini, wateja na wale wote wanaosambaza bidhaa mbalimbali kwao.Telemann aliongeza kuwa dhamira hii itasaidia  kuhakikisha  watoto wetu wanakuwa na maisha bora siku za baadaye na kuzifikia ndoto zao.


  Vilevile kutasaidia  kujenga jamii iliyo imarika kiafya, yakiwamo maisha ya wenye ulemavu.

  0 0
 • 04/27/15--06:49: Article 21
 •  Mwenyekiti wa ACT-Tanzania,  Lucas Kadawi Limbu.
    Mwenyekiti wa ACT-Tanzania,  Lucas Kadawi Limbu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ambapo alipinga Msajili wa Vyama Siasa Nchini, Jaji Francis Mtungi kubadilisha jina la chama cha ACT-Tanzania na kuwa ACT-Wazalendo bila ya kufuata utaratibu. Kulia ni Katibu Muenezi wa chama hicho, Fredy Kisena na Katibu Mkuu wa chama hicho, Leopold Mahona.
   Viongozi wa chama hicho wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto Kaimu Katibu wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam, Peter Katunka, Kaimu Katibu Mkuu, Leopold Mahona, Mwenyekiti, Kadawi Lucas Limbu na Katibu Muenezi Fredy Kisena.
    Mwenyekiti wa ACT-Tanzania,  Lucas Kadawi Limbu.
   Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  Mwenyekiti wa ACT-Tanzania,  Lucas Kadawi Limbu (kulia) akisisitiza jambo.

  Na Dotto Mwaibale

  MWENYEKITI wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), Lucas Kadawi Limbu amemlalamkia Msaji wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Mstaafu Francis Mtungi kwa madai ya kukiuka utaratibu wa kubadilisha jina la chama hicho na kuwa ACT-Wazalendo.

  Limbu alitoa malalamiko hayo mbele za waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kuhoji nyuma ya ACT-Wazalendo kuna nini.

  "Tunashangazwa na jaji Mtungi kwa kubadili jina la chama chetu bila ya kufuata taratibu huku akijua fika kuna kesi ya msingi ipo mahakama kuhusu mwenendo wa chama hicho. Alisema Limbu

  Aliongeza kuwa kuna njama za makusudi zilizofanywa za kubadilisha jina la chama hicho kwani haiwezeka na haiingii akilini kubadilisha jina la chama kwa kipindi kifupi na haraka kiasi hicho.

  "ACT-Tanzania ni chama chetu sio cha Zitto na kama anahitahi siasa safi aanzishe chama chake kwani nafasi hiyo ipo wazi kwa kila mtanzania.

  Alisema ni jambo la ajabu kuona chama kinafanya mkutano wake mkuu wenye nia hofu na kumpatia mtu madaraka ya kioongozi mkuu na kubadilisha jina lake huku msajili wa vyama akishuhudia.

  Alisema msajili wa vyama vya siasa alitoa tamko la kubadilishwa jina la chama hicho tarehe 20-4-2015 wakati tayari kiongozi mkuu wa chama hicho kilichobadilishwa jina akiwa katika zaira ya kichama mikoani aliyoianza tarehe 10-4-2015 huku wakigawa kadi kwa kupitia chama cha ATC-Wazalendo.

  Limbu alihoji fedha zinazotumika kwenye ziara hiyo na za kuchapa kadi, bendera za chama na vifaa vingine kuwa zinatoka wapi kama hakuna watu wenye nia mbaya na chama cha ATC-Tanzania.

  (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

  0 0

     Meneja  wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari MAELEZO Ajijini Dar es Salaam leo kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa kulia ni  Afisa masoko  wa NHBRA Zubeda Salum.
   Meneja  wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akionyesha aina  ya kwanza ya kigae  cha kupaulia nyumba,kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa kulia ni  Afisa masoko  wa NHBRA Zubeda Salum.
   Meneja  wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akionyesha aina  ya pili ya kigae  cha kupaulia nyumba,kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa.
    Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa kuonyesha aina mbalimbali za vigae vinavyoweza kutengenezwa na kila mwananchi hapa nchini katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)
   
  Na Avila Kakingo,Globu ya Jami.
  WAKALA Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wamegundua njia rahisi ya kuboresha makazi kwa kutumia vigae kwa gharama nafuu ambazo kila mwananchi anaweza kuzimudu. 

  Hayo yamesemwa na  Meneja  wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo. Kwemana amesema kuwa utengenezaji wa vigae hivyo ni rahisi na gharama hafuu kwani bidhaa zote za kutengeneza vigae hivyo zinapatikana hapa hapa  nchini.
  Hifaa hivyo  vinavyotumika kutengenezea vigae hivyo ni mchanga sementi na  nyuzi za katani bidhaa  hizo zote zinapatikana hapahapa nchini, ikiwa kuna  mashine inayotumika kushindilia mchanga uliochanganywa na sementi nayo ni gharama nafuu ukilinganisha na faida zinazopatikana.


  Kwemana amesema kuwa  njia ya kutengeneza vigae hivyo vitasaidia  kutumika kama njia nyingine ya kupaua nyumba zetu ambapo vigae hivyo huu kaa muda mrefu kuliko kutumia Nyasi au Bati.

older | 1 | .... | 512 | 513 | (Page 514) | 515 | 516 | .... | 1897 | newer