Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA AENDELEA KUVURUGA MIPANGO YA WAPINZANI KATIKA JIMBO LA ISMANI

$
0
0
 Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, HASSAN MTENGA akijibu maswali ya wananchi wa tarafa ya pawaga.

Na Fredy Mgunda,Iringa

Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa, Hassani Mtenga amewataka wananchi wa tarafa ya Pawaga katika jimbo la Isimani kuendelea kumwamini Mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa anawatendea haki kwa kuwaletea maendeleo.

akizungumza katika mkutano huo, MTENGA amewataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kutokana na kutekeza ahadi zao ambazo wanakuwa wanaziahidi kwa wananchi.

Kwa upande wao wananchi kijiji cha boliboli kilichopo tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa Vijijini wanakabiriwa na matatizo ya kiafya pamoja na migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima hayo yamebaini katika mkutano ulifanyika katika kijiji hicho.

katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA
akiwapa vifaa vya michezo wananchi wa
 tarafa ya pawaga
wakizungunza wakati wa mkutano huo wananchi hao wamesema kuwa kijiji hicho hakina mganga wa kutoa huduma katika zahanati yao na kuongeza kuwa tatizo la migogolo ya aridhi limekuwa kubwa.

Akijibu maswali ya wananchi hao katibu wa ccm mkoa wa iringa hassani mtenga amewata viongozi wa chama hicho kufanya mikutano ya mara kwa mara na kupokea kero za wananchi na kuzitatua mapema ili kuendelea kukijengea imani chama chao.

Viongozi wengi wamekuwa hawawajali wananchi wao ambao wamewaweka matarakani na ndio imekuwa sababu ya matatizo mengi na migogolo mikubwa katika vijijini.

Lakini MTENGA amesema swala mfureji,tatizo la mganga,walimu kuwa walevi na mgogoro wa mbomipa anayachukua na kwenda kuyafanyia kazi na kuwaahidi kuwa matatizo yote waliomweleza yatatulika.

“Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuipigia kura katiba inayopendekezwa ili waweze kupata katiba ya wananchi na kuwaambia wananchi wa eneo hilo kuitumia fursa ya kuijiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura ambalo iringa litaanza tarehe 29 mwezi huu” alisema HASSAN MTENGA.

BASATA wampongeza Mayunga kwa kuwakilisha vyema Tanzania

$
0
0
Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (kulia)akipokea tuzo aliyoipata Nalimi Mayunga mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Afrika. Shughuli hii imefanyika jana katika halfa ya kumpongeza Mayunga kwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars iliyofanyika katika ofisi za BASATA. Akishuhudia kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (Katikati) akiongea katika halfa ya kumpongeza mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo na kuiwakilisha vyema Tanzania . halfa hiyo ilifanyika katika ofisi za BASATA Ilala Dar es Saalam. kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.

Baraza la sanaa Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano ya muziki yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika .

Mwisho mwa mwezi wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha kwenda kushiriki mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya  na kumtakia kila  laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu aliweza kufanya vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Star wa Afrika.

Habari njema kwa WanaBlogu waTanzaniania juu Uandikishaji Wanachama TBN

$
0
0
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili. 

Kwa wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na wanachama watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga uwanachama wa TBN. 

Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida), Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).

Kwa wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama wa TBN utafanyika kwa muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika kutathmini wanachama waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.

NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo wataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN. 

Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470 
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

LAPF YATOA MSAADA KUCHANGIA UJENZI WA MAABARA ZA SHULE-WILAYA YA ULANGA MASHARIKI.

$
0
0
 Meneja wa Kanda ya Mashariki ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yesaya Mwakifulefule  akikabidhi  msaada wa vifaa vya ujenzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mashahriki Bi. Christina Mndeme kwa ajili ya ukarabati wa maabara za shule katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mashahriki Bi. Christina Mndeme akizungumza jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya   Meneja wa Kanda ya Mashariki ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yesaya Mwakifulefule  kukabidhi  msaada wa vifaa vya ujenzi kwa kwa ajili ya ukarabati wa maabara za shule katika wilaya hiyo.

Picha ya pamoja baada ya makabidhiano hayo.

SEREKALI YAONYA WANAOTOROSHA MADINI

$
0
0
mmoja wa wakurugenzi wa  kampuni ya Tanzanite one Hussein Gonga akiwa anamuonyesha  Waziri wa nishati na majini George  Simbachawene madini ambayo yanachibwa na kampuni yao.

  Na Woinde Shizza,Arusha .

Serikali imewataka wachimbaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite nchini, kuacha tabia ya Utoroshaji wa madini hayo nje ya nchi huku,ikiagizwa kuachwa kuuzwa madini ghafi.

Katika kudhibiti biashara hiyo, serikali kwa kushirikiana na kituo cha mikutano cha Arusha(AICC) inakusudia kuanzisha kituo cha kisasa cha kimataifa cha ukataji wa madini hayo na kuuzwa nje.

Waziri wa nishati na majini George  Simbachawene alitoa wito huo , wakati akifungua  maonesho ya Kimataifa ya  nne ya madini ya Vito jijini hapa yanayoendelea  Mount Meru hoteli.

Waziri Simbachawene alisema, tabia  utoroshaji wa madini hayo inaikosesha serikali mapato na pia inawapunguzia mapato wauzaji wa madini hayo na hivyo wote kupata hasara.
Akizungumza  juu ya kituo mauzo ya madini hayo, alisema, kinatarajiwa kuwa cha kisasa, kitakachokuwa na ofisi za kodi za mapato, kiwanja kidogo cha ndege na ofisi za wauzaji na wanunuzi wa madini. Wakizungumzia maonesho hayo, Wakurugenzi wa kampuni ya Tanzanite one, Faisal Juma na Hussein Gonga walieleza yamekuwa na manufaa makubwa na kuongeza wanunuzi wa madini.

Faisal alisema kampuni yake, imeanzisha mafunzo ya kufundisha vijana kukata madini hapa nchini ili kupunguza kuuzwa nje madini ghafi.
Naye Gonga alisema kuwa kampuni hiyo, pia itaendelea kushirikiana na serikali kuongeza ajira kwa vijana na pia kuzuia kutoroshwa nje madini hayo.

Kamishina wa madini,muhandisi Masanja amewata wamiliki wa madini,wachimbaji pamoja na wauzaji kutojiingiza katika utoroshaji wa madini kwakua unasababisha anguko la soko hilo kutokana na kupoteza bei halali ya madini hayo. Alisema serikali itaendelea kuboresha maonesho hayo, kila mwaka na kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara ya madini ya vito katika Afrika.

Maonesho hayo, yanashirikisha zaidi ya mataifa manane na wanunuzi kutoka nchi za Ulaya na Marekani mwaka  katika maonesho ya mwaka jana kiasi cha Tsh 3.4 bilioni kilipatikana 
habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog

MAADHIMISHO YA SIKU YA MALARIA DUNIANI

Shindano la TMT 2015 lazinduliwa rasmi leo, Mwanza kufungua pazia april 24 2015.

$
0
0
Afisa Masoko na Mahusiano wa Proin Promotions Ltd, Josephat Lukaza akizungumzia Uzinduzi wa msimu wa pili wa Shindano la TMT 2015 lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao pia ni wasambazaji, wauzaji na watengenezaji wa filamu za Kitanzania. Anayeshuhudia pembeni ni Mratibu wa Masoko wa ITV/Radio One ambao ni mmoja wa wadhamini wa Shindano la TMT 2015.
 Mratibu wa masoko kutoka ITV/Radio One (wa pili kulia) akizungumzia juu ya umuhimu wa wao ITV/Radio one kuwa washirika wa TMT 2015 na kuhaidi makubwa zaidi kwa mwaka 2015.P
 Mmoja wa majaji wa shindano la TMT 2015 Yvonne Cherry au Monalisa akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na shindano la TMT 2015 lililozinduliwa rasmi leo jijini Dar Es Salaam
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 limezinduliwa rasmi leo huku baadhi ya vigezo vikiwa vimeboreshwa, akizungumzia hayo Meneja wa Mradi wa TMT 2015, Saul Mpock amesema kuwa "Mwaka Huu Kigezo kimojawapo ni mshiriki kuwa na umri kuanzia miaka 16 na kuendelea huku fomu za kushiriki shindano hilo zikipatika siku ya usaili katika mkoa husika na bila gharama yoyote".

Shindano la Tanzania Movie Talents 2015 linaanza rasmi Kesho huku Kanda ya Ziwa ndio itakayofungua pazia la shindano hili kwa Mwaka 2015, Shindano hili linafanyika kikanda ambapo kanda sita za Tanzania zitafikiwa na shindano hili.

Kwa kanda ya Ziwa usaili utaanza tarehe 24 Aprili 2015 huku zoezi zima likifanyika mkoani Mwanza na hatimaye zoezi kuendelea kanda ya Kaskazini, Arusha, Kanda ya Kati, Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya, Kanda ya Kusini, Mtwara na Kumalizika Kanda ya Pwani, Dar Es Salaam.

Katika kanda zote tano ikiwa Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kati, nyanda za juu kusini na Kusini Washindi watakuwa ni watatu kutoka kila kanda ambapo kila mshindi ataibuka na kitita cha shilingi laki tano kila mmoja huku kanda ya Pwani itatoa washindi watano na kila mmoja kuondoka na shilingi laki tano pia na kupelekea Washindi kuwa 20 na kuingia kwenye nyumba ya TMT kwaajili ya Hatua ya Mchujo.TMT 2015 itarushwa na kituo cha ITV siku ya Jumapili saa tatu usiku huku kipindi cha kwanza kabisa cha TMT kikitarajiwa kuonekana tarehe 10 May 2015.

Shindano hili la TMT 2015 limedhaminiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Precision Air, I-View Studio, Global Publishers na Kituo cha ITV/Radio One ambao ndio watakaokuwa wakirusha matangazo ya TMT 2015. TMT ikiendelea kupata sapoti kutoka katika vituo mbalimbali za redio mikoani. Vilevile tunatoa nafasi kwa makampuni mengine ambao wangependa kushirikiana na TMT kwa mwaka 2015
Kauli Mbiu ya TMT 2015 ni Mpaka Kieleweke.

KAMBI MBWANA: Mdau wa maendeleo aliyeibuka na kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni

$
0
0
KULALAMIKA bila kutoa suluhisho ni kujipotezea muda. Ndivyo unavyoweza kusema unapoanza kuelezea wazo la kuandikwa kitabu cha Dira na Tumaini jipya Handeni, kilichoandikwa na Kambi Mbwana, moja ya wana harakati wa kimaendeleo hapa nchini.Mwandishi wa kitabu cha DIRA NA TUMAINI JIPYA HANDENI, Kambi Mbwana, pichani.


Kitabu hicho kilichoangazia mambo mengi ya kijamii kama vile kero ya migogoro ya ardhi, shida ya maji, ukosefu wa elimu ya uraia na namna bora ya kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana.
Kwa muda mrefu sasa, vijana wengi wamekuwa wakijiweka ‘busy’ katika kulaumu mifumo kadhaa, wakiwamo viongozi kama vile madiwani, wabunge na watendaji mbalimbali wa serikalini.



Katika kulaumu huko, baadhi yao wanakosa muda muafaka wa kufanya kazi nyingine za kuwakwamua kiuchumi au hata kutimiza wajibu wao kama wananchi, badala ya kuendelea kulaumu siku hadi siku.
Katika mazungumzo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Mbwana anasema kwamba wilaya ya Handeni ina changamoto nyingi zinazopaswa kuorodheshwa kwa ajili ya kuangalia namna bora ya kuzitatua.



Hali hiyo ilimfanya afanye ziara katika maeneo mengi ya wilaya hiyo kwa ajili ya kuandika kitabu ambacho kimeanza kuwafikia watu mbaalimbali wenye uelewa wa kusoma vitabu ili kutanua ubongo wao.



“Sijasubiri viongozi wa serikali au wanasiasa wafanye wao kila jambo, ndio maana nikapata wazo hili la kuandika kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni, ambacho kama wananchi watakielewa na kukisomaa, agharabu hata wale wenye kiu ya kuboresha maisha yao na si wananchi wao.



“Ukiacha hayo mambo ya kisiasa, bado wananchi hawaelewi namna gani wanaweza kuongeza kipato chao kwa kujihusisha na kilimo bora, ufugaji wa kuku, mbuzi, ng’ombe na shughuli nyingine halali kwa ajili ya kuwapatia maisha bora, badala ya kutegemea kilimo cha mazoea ambacho ni mahindi pekee na kuyategemea kwa chakula na biashara,” alisema.



Mbwana ambaye pia ni mwandishi wa habari za michezo anasema kitabu chake kimetaja kero kadhaa na namna ya kuzitatua, hivyo ni jukumu la kila mmoja kukipata kwa ajili ya kuona namna bora inavyoweza kumnufaisha kwa namna moja ama nyingine.



Anasema wazo la kuandika kitabu limetokana na umuhimu wakutoa elimu ya uraia kwa wananchi sanjari na kutumia kipaji chake kwa ajili ya kushirikiana na jamii yao, hususan kwa wilaya ya Handeni yenye uhitaji wa majarida, vitabu, makongamano na mikutano ya hadhara yenye dhamira ya kuwabadilisha kifikra na kimtazamo ili wapige hatua.



Wilaya ya Handeni licha ya kuwa kongwe, lakini ina changamoto nyingi, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kutimiza wajibu wake kwa ajili ya kuitangaza kwa kupitia sekta mbalimbali.
Kwenye suala la migogoro ya ardhi, wananchi wengi hawajui kama wanapaswa kuhoji au kusimamia watu wote waliopata ardhi kinyume cha sheria katika maeneo yao. Hii inawafanya watu wamiliki ardhi kinyume cha sheria na wengi wao wanawakandamiza walalahoi.



Mbwana pia anasema yapo maeneo ambayo viongozi wa serikali na wananchi wao hawana ushirikiano. Anaitaja Misima ambayo sasa inajulikana kama Kata ya Mabanda, upo mgogoro mkubwa unaoweza kuhatarisha usalama wa raia na mali zao, chanzo kikiwa ni eneo hilo kuingizwa kwenye Mamlaka ya Mji bila kushirikishwa.



Hali hiyo inawafanya viongozi washindwe kuzungumza na wananchi wao kwa hofu ya kuzua mtafaruku au aibu, pale anapopita viongozi wa juu wa serikali, jambo linalohitaji kuangaliwa upya.



“Wilaya hii yenye shida lukuki inapaswa kwanza kutambua changamoto hizi, kuzikubali na kushirikiana pamoja kwa ajili ya kuzitatua kwa kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza wajibu wake.



“Hata hili wazo la kuandika kitabu ni kwa sababu nahitaji kutimiza wajibu wangu, nikiamini kuwa watu hawana uelewa wa mambo mengi, hivyo endapo watasoma machapisho mbalimbali wanaweza kufika mbali,” alisema Mbwana.



Aidha Mbwana anawataka watu kufahamu umuhimu wa kusoma vitabu na jinsi vinavyoweza kuwakomboa wananchi katika kukuza mitazamo yao, bila kusahau namna bora ya kuweza kubadilisha mitazamo yao.



Anasema kitabu hicho kimeandikwa na kuelemea zaidi katika wilaya ya Handeni, ingawa baadhi ya kero au maudhui ya yaliyoandikwa humo yanashabihiana katika maeneo mengi ya Tanzania.



Anawataka wadau wote, wakiwamo viongozi wa serikali na vyama vya siasa kukubaliana na matokeo ya umuhimu wa kuelimisha wananchi wanaoshiriki kuwaingiza watu wengi kwenye nafasi za uongozi, ingawa mara kadhaa wamekosa faida ya jambo hilo.



Mbwana ambaye pia alishiriki kuanzisha wazo la kuundwa kwa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation yenye Makao yake Makuu wilayani Handeni, mkoani Tanga, anasema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni kuona baadhi ya watu hawakitaki kitabu hicho kwa faida wanazojua wenyewe.



Hii ni kwa sababu watu hao wanaona kilichoandikwa kwenye kitabu hicho kikitumiwa vyema na wananchi kinaweza kuleta athari kutoka kwa baadhi ya watu wasiokuwa na dhamira ya
kuwakomboa wananchi wao.



“Nimeweza kuchapa nakala 1000 za kuanzia ambapo nimejibana mno katika kuandaa kitabu hiki, hivyo kwa bei ya Sh 3500 kwa kitabu kimoja, niliamini kuwa endapo kitanunuliwa vizuri, ningeweza kuchapa nakala nyingine ili kiweze kusambaa katika maeneo mengi zaidi, maana lengo si kutajirishwa na kitabu hiki, ila kuwaelimisha wananchi wenzangu.



“Wakati ambao naendelea kukisambaza, ni wakati wa wadau kukinunua au kunisaidia namna ya kukisambaza kwa wananchi, yakiwamo mashirika, taasisi za serikali, wadau wa maendeleo kwa mmoja kwa mmoja, bila kusahau vyama vya siasa ambavyo navyo vinapaswa kusambaza nakala ya kitabu hiki, ukizingatia kuwa lengo ni moja kuwazindua wananchi, maana kwa miaka kadhaa sasa wananchi wameendelea kudidimia licha ya kuwa kwenye wilaya yenye rasilimali nyingi, kama vile ardhi, dhahabu nk,” alisema.



Maeneo ambayo tayari kitabu hicho kinapatikana ni Handeni Mjini kwa Ayubu Magazeti, Misima, Sindeni, Kwamatuku, Komsala, wakati Korogwe Mjini kinapatikana Kituo cha mabasi karibu na lango la kutokea kwa Bony muuza magazeti, Tanga Mjini kikipatikana stendi ya zamani, bila kusahau katika baadhi ya maeneo ya jijini Dar es Salaam.



Hata hivyo Mbwana anasema kwamba licha ya kitabu hicho kuuzwa kwa bei ndogo tu ya Sh 3500, lakini bado inaonekana ni kubwa, hivyo anajaribu kuwatafuta wadau wengine wa kimaendeleo katika kushirikiana nao ili watafute namna bora ya kuwapatia kitabu hicho.



Habari za kitabu hicho cha Dira na Tumaini jipya Handeni zimeanza kuenea siku chache zilizopita katika mitandao ya kijamii facebook na blogs na baadhi ya magazeti, huku wahitaji wa kitabu hicho wakiombwa kuwasiliana na mwandishi wa kitabu hicho anayepatikana kwa namba +255 712053949 au barua pepe yake kambimbwana@yahoo.com.



Kwa mujibu wa Mbwana, kitabu hicho ni sehemu ya kuwakomboa wananchi na wakazi wa Handeni, ambao kwa miaka kadhaa wameshindwa kupata mwangaza na kuendelea kudidimia kwa kuhakikisha kuwa wanayatumia maandishi yaliyomo kwenye kitabu hicho kupata ufumbuzi wa changamoto zao za kimaisha, hususan katika kipindi hiki ambacho wanasiasa waroho watakapoanza kupitisha fedha chafu, zawadi ambazo zote ni rushwa inayopaswa kupigwa vita.

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA BAJAVERO DAR WAPATA MAFUNZO JUU YA HEDHI SALAMA.

$
0
0
 Mratibu wa Mradi wa Afya wa Help Kids Edith Peter Mziray akiwasihi wanafunzi kuwa wasikivu wakati wa semina ya Hedhi salama
Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambao pia ni waandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akiwauliza wanafunzi wa Darasa la tano hadi la saba changamoto wazipatazo wakati wanapoingia katika siku zao na pia kuwaelimisha juu ya Hedhi salama. 
 Mwanafunzi wa Darasa la Tano Anitha Norbart (12) akiuliza swali kama ni sahihi kutumia Mdalasini wakati akiwa katika siku zake?
 Daktari Edna Kiogwe akitoa elimu juu ya umuhimu wa kujitambua wakati wakiwa katika Hedhi na njia mbadala za kujiweka sawa pindi wanapokuwa katika kipindi hicho

 Wanafunzi wakiwa wanafundishwa moja ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya na Daktari Edna Kiogwe.
 Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la Tano sita na saba wakiwa wanafurahia Jambo wakati wa mafunzo
 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa Makini Semina Hiyo
 Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi ya Bajavero akipewa zawadi ya Glory Pads ikiwa ni sehemu ya kusherekea siku ya Hedhi Duniani.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bajavero zamani Wamato  wakifurahia Pads za Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi Duniani.

****
Kuelekea Kilele cha siku ya Hedhi Duniani ambayo itakuwa tarehe 28.05.2015 Mtandao wa Hedhi salama www.hedhisalama.com  umeendelea kutoa mafunzo juu ya Hedhi salama ikiwa ni pamoja na changamoto,Magonjwa na mambo mbalimbali ambayo yanamtokea mwanamke anapokuwa katika Hedhi pamoja na ushiriki wa wanaume katika kujua maswala ya hedhi katika shule ya msingi ya yatima ya Bajavero,

Akitoa mafunzo ya Semina hiyo Daktari Edna Kiogwe alieleza kuwa kuna haja ya vijana tangu wakiwa wadogo wakapata Elimu juu ya Hedhi ili wanapokuwa wasijeshtuka pindi hali hiyo inapo wajia.

Alieleza juu ya umakini na ufaulu mashuleni kuwa Wasichana wengi  huahirisha shughuli za kimasomo  kama kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao


Aliongeza ili Binti apate kuendana na hali hii anatakiwa ajivunie na kufurahia kipindi chote anachokua hedhi, atambue kwamba kila mwanamke hupitia kipindi hicho na hata wenzake darasani huvipitia vipindi hivyo vya hedhi, si yeye
peke yake anaeingia hedhi. 



Pia Dkt. Edna alisisitiza kuwa  Wanaume na wavulana wanahitajika kuelimishwa juu ya hedhi, wengi wao hawajui chochote juu ya hedhi na hua wanadhani mwanamke peke yake ndo anapaswa kufahamu juu ya hedhi. "Tukiwaelimisha wanaume juu ya hedhi, watakua msaada mkubwa kwa wake zao, watoto wao, dada zao,mama zao na ndugu zao wa kike. Kulingana na tamaduni zetu za kiafrika baba ndo mtafutaji na mwenyekauli ya mwisho katika familia" Alisema Dkt. Edna


Nao wanafunzi wa shule ya msingi ya  Bajavero  walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na kupata majibu pia kufurahishwa na elimu bora  na kujitambua zaidi, pia walishukuru kupata zawadi za Pads aina ya Glory  ikiwa ni kuelekea katika siku ya Hedhi duniani.

MAADHIMISHO SIKU YA MALARIA DUNIANI KITAIFA KUFANYIKA MNAZI ,MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani mwaka 2015 alipokutana na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuwakumbusha na kuwaelimisha wananchi juu ya athari za Malaria na mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo.
Tanzania itaungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Malaria duniani Aprili 25 mwaka huu ili kutathmini mafanikio ya utekelezaji wa mikakati  mbalimbali ya kupambana na ugonjwa huo hapa nchini.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani mwaka 2015, leo jijini Dar es salaam amesema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuwakumbusha na kuwaelimisha wananchi juu ya athari za ugonjwa wa Malaria na mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo.

Amesema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam chini ya kauli mbiu isemayo Wekeza kwa Maisha ya Baadaye, Tokomeza Malaria huku msisitizo mkubwa ukilenga kuikumbusha na kuielimisha jamii kuepuka athari na madhara yanayotokana  na ugonjwa huo.

Bw. Mushi amesema maadhimisho ya mwaka huu  yamelenga kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kutambua dalili za malaria na kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma pindi wasikiapo dalili za ugonjwa huo ili waweze kupima afya zao  na kupatiwa matibabu.

“Ugonjwa wa malaria kwa muda mrefu umekuwa na athari kwa nguvu kazi ya taifa na utekelezaji wa mikakati mbalimbali, hivyo ni wajibu wetu kushirikiana kuwaelimisha wananchi kuwahi katika vituo vya afya pindi wasikiapo dalili za malaria” Amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji Mpango wa Udhibiti wa Maambukizi ya Malaria Dkt. Linda Nakara akizungumza kuhusu maadhimisho hayo amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na wadau mbalimbali wa huduma za afya kufanya maonyesho ya huduma wanazotoa kwa jamii.

Ameongeza kuwa wadau hao pia wataendesha shughuli za uchunguzi wa vimelea vya malaria kwa kutumia vipimo vinavyotoa majibu kwa haraka (MRDT) na matibabu ya ugonjwa wa malaria kwa wale watakaogundulika kuwa na malaria.

RAIA WAPYA WA TANZANIA WASHANGILIA KUPEWA VYETI VYA URAIA

$
0
0
Raia wapya wa Tanzania, wakazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Shukuru Nzokila (kulia) na Anicet Yohanna wakishangilia baada ya kupokea vyeti vyao vya uraia wa Tanzania, katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. 
Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo.
5
Baadhi ya raia wapya wa Tanzania, wakazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, wakionyesha vyeti vyao kwa furaha baada ya kupokea vyeti hivyo vya uraia, katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo.1
 Kiongozi wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) katika Makazi ya Mishamo, Adolph Bishanga akimkabidhi chandarua na shuka raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses (kulia) baada ya kujifungua mtoto wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na UNHCR kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya kupokelea vyeti. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.2
2. Mkuu wa Makazi ya Ulyakulu, Abdulkarim Mnacho (kushoto) akimpongeza raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses baada ya kujifungua mtoto wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya kupokelea vyeti.
  3
Raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses akiwa na mtoto wake mara baada ya kujifungua mtoto huyo wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya kupokelea vyeti.6
 Afisa Uhakiki, Maharusi Nasibu (kushoto) akichukua alama ya vidole kwa raia mpya wa Tanzania, Mandaakiza Severin kabla ya kupewa cheti chake cha uraia katika ugawaji wa vyeti hivyo kwa raia wapya zaidi ya 52,565 katika Makazi ya Mishamo yaliyopo wilayani ya Mpanda Vijijini, Mkoa wa Katavi. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo.

WARSHA YA MPANGO KAZI YA MAADILIKO YA TABIANCHI YAFANYIKA DAR ES SALAAM

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Angelina Madete akifungua Warsha ya kukamilisha Mpango kazi wa kuhuhisha masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi katika maeneo ya Pwani ya Dar es Salaam. Warsha hiyo ya siku mbili inafanyika katika Hotel ya Stella Maris, Bagamoyo na inahusisha wadau kutoka Vyuo Vikuu, wadau wa maendeleo na Manispaa za
Dar es Salaam.
5
Mratibu wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi katika maeneo ya pwani ya Dar es Salaam Mhandisi Ladislaus Kyaruzi (kulia) akifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mgeni Rasmi (hayupo pichani). Kushoto ni Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Patrick Ndaki.
  3
Washiriki wakiwa katika vikundi wakipitia na kurekebisha Mpango kazi.4
2
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Angelina Madete akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu waliohudhuria Warsha katika Hotel ya Stella Maris, Bagamoyo.

MANISPAA YA ILALA YAELEZEA UBORESHAJI WA UKUSANYAJI WA MAPATO YAKE

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri hiyo. Kulia ni Meneja Kodi Majengo, Stellah Mgumia.
 Meneja Kodi Majengo wa Manispaa hiyo, Stellah Mgumia akitoa ufafanuzi mbalimbali wa ukusanyaji wa mapato.
 Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa Manispaa hiyo, Francis Luambano (kushoto), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.
 Ofisa Biashara wa Manispaa hiyo, Dennis Mrema, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale

MANISPAA ya Ilala imewaonya wafanya biashara wanaotumia madalali kulipia huduma zinazopatikana katika manispaa hiyo waache maana wamekuwa chanzo cha upoteaji wa mapato katika manispaa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Meneja Uhusiano wa Manispaa hiyo Tabu Shaibu  alisema uboreshaji wa mapato unategemea sana uaminifu wa walipa kodi kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato vinavyotegemewa katika manispaa hiyo.

"Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inategemea mapato yake kutoka kwa wafanya biashara na wamiliki wa nyumba waaminifu wanaolipa kodi kwa wakati ili kutekeleza shughuli za maendeleo".

Shaibu alisema manispaa inategemea vyanzo vinne vya mapato ambavyo ni kodi ya majengo, leseni za Biashara, ushuru wa mabango na kodi ya huduma za jiji.

Kodi nyingi imeishia mikononi mwa watu wanaojiita madalali au vishoka sababu ya kukosa uaminifu kwa wale waliowatuma na kuingiza waliowatuma katika hatia ya ukwepaji kodi, aliongeza Shaibu.

"Walipa kodi wengi wamejikuta hatiani baada ya kuwatumia madalali au vishoka wasio waaminifu kulipa kodi na kujikuta stakabadhi zao hazipo katika kumbukumbu ya stakabadhi za manispaa za walipa kodi na kusababisha walipe faini mara tatu ya kodi au kushtakiwa mahakamani kwa kosa la kughushi".

Shaibu alielezea zoezi la tathmini ya majengo ya biashara na makazi linaliendelea katika manispaa hiyo ili kujipanga ma ukusanyaji wa kodi wa mwaka wa fedha 2015/16 unaoanza tarehe mosi julai.

"Tunaomba ishirikiano kutoka kwa wakazi wa wilaya ya Ilala ili tuweze kupata makadirio ya kodi ya kodi ya majengo ambayo ni asilimia 0.15 kwa jengo la makazi na asilimia 0.20 kwa jengo la biashara".


Shaibu ametoa wito kwa walipa kodi kuhakikisha wanalipa kodi kwenye mamlaka husika na kama walishatumia madalali au vishoka wakahakiki nyaraka zao manispaa ili wasije kuingia matatizoni." 

(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/

AMIRI JESHI MKUU RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA KYERWA LUTENI KANALI BENEDICT KITENGA (MSTAAFU) LEO MKOANI MOROGORO

$
0
0

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete (pichani kati)  na Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda  (pichani shoto) wakishuhudia askari wa jeshi la Wananchi (JWTZ) wakipiga risasi hewani kama sehemu ya heshima ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera leo,Marehemu Luteni Kanali Benedict Kitenga (mstaafu) huko kwenye makaburi ya Mlima Kola Kigurunyembe mkoani Morogoro. PICHA NA IKULU.

WADAU WA KISWAHILI SIKU YA CHAUKIDU CHUO KIKUU CHA HOWARD

$
0
0

 Asha Nyang.anyi akiwa kwenye meza akikagua majina ya wadau wa Kiswahili kwenye sherehe ya  Chama Cha Ukuzaji Wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) inayoendelea sasa hizi chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC na Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi atakua mgeni rasmi.
Wadau wa Kiswahili wakiendelea kuingia ukumbini.
 Wadau kutoka Zanzibar wakipata picha
 Walimu wa kiswahili wa vyuo mbalimbali wakipata picha ya pamoja.
 wadau wa Kiswahili wakihudhuria sherehe ya CHAUKIDU
 Walimu na maporofesa wa vyuo wakiwa ndani ukumbi wa Blackburn Center siku ya Alhamisi April 23, 2015 chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.
 Wadau wa Kiswahili wakibadilishana mawili matatu.
Wadau wa Kiswahili wakilonga Picha zaidi Baadae

SHEREHE YA CHAUKIDU YA MCHANA CHUO CHA HOWARD YAFANA

$
0
0
Rais wa CHAUKIDU Prof Lioba Moshi watatu toka kushoto akimkaribisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi mara tu alipowasili kama mgeni rasmi chuo kikuu cha Howard Washington, DC katika sherehe ya chama cha ukuzaji wa Kiswahili Duniani siku ya Alhamisi April 23, 2015 kulia ni Prof Venessa White Jackson 
 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimtambulisha mkewe mama Sitti Mwinyi kwa mwenyeji wao Prof Lioba Moshi pia na yeye akimtambulisha mama Sitti Mwinyi kwa Prof Venessa White Jackson kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula .  
Prof Lioba Moshi Rais CHAUKIDU akielezea historia fupi ya CHAUKIDU na baadae kumkaribisha Rais mstaafu kuongea na wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya chama hicho iliyofanyika siku ya Alhamisi April 23, 2015 katika chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.

Ms Mamburi Lyambaya (kushoto) akimtambulisha Prof Venessa White Jackon na yeye kuwasalimia wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya CHAUKIDU iliyofanyika katika chuo kikuu cha Howard Washington, DC.


Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa meza kuu kulia ni prof Venessa White Jackson '

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba kwa kuwashukuru CHAUKIDU kwa kummpa mwaliko na kwa kuwa yeye ni mdau mkubwa wa lugha ya Kiswahili hakusita kukubali kuja kujumuika nao pia Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliwapongeza kwa kuitangaza lugha ya Kiswahili nchini Marekani.

Kutoka kushoto ni Balozi wa Umoja wa Afrika Mhe. Amina Salum Ali, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na mama Sitti Mwinyi wakifuatilia hotuba ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Howard wakiimba nyimbo za Kiswahili kwa ustadi mkubwa kuliko wastajabisha Watanzania na wadau wengine wa Kiswahili.

Wadau wa Kiswahili wakifuatilia sherehe ya CHAUKIDU

WATUMISHI WA UMMA WASHAURIWA KUZINGATIA KANUNI NA MAADILI YA KAZI.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam

ms5Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Margareth Mtaki akitoa salamu za kwa niaba ya wafanayakazi wa Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa.
ms6Mjumbe wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutoka Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya akielezea jambo wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam
ms7: Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika mkutano wa Baraza hilo jana jijini Dar es Salaam.

Mzee Mwinyi ahutubia wadau wa Kiswahili Washington DC

$
0
0
Ifuatayo ni hotuba ya Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi alipohutubia mkutano wa nne wa Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) uliofanyika tarehe 23 Aprili 2015 katika Chuo Kikuu Cha Howard jijini Washington DC
KARIBU


WAZIRI MKUU PINDA ASHIRIKI MAZISHI YA LUTENI KANALI MSTAAFU KITENGA

$
0
0
01
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimfariji Mama Francisca Kitenga baada ya mazishi ya mumewe, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, , marehemu,Luteni Kanali Benedict Kitenga  yaliyofanyika kwenye makaburi ya  Kola , Morogoro mjini Aprili 24,(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).02
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitupa mchanga kaburini katika mazishi ya  aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, , marehemu,Luteni Kanali Benedict Kitenga  yaliyofanyika kwenye makaburi ya  Kola , Morogoro mjini Aprili 24, 2015
03
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telesphor Mkude baada ya mazishi ya  aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, , marehemu,Luteni Kanali Benedict Kitenga  yaliyofanyika kwenye makaburi ya  Kola , Morogoro mjini Aprili 24, 2015.
040607
Wazirii Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na  baadhi ya Wakuu wa Wilaya walioshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, , marehemu,Luteni Kanali Benedict Kitenga  yaliyofanyika kwenye makaburi ya  Kola , Morogoro mjini Aprili 24, 2015.

WAZIRI MAHENGE AFANYA ZIARA MACHINJIONI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, Mh. Binilith Mahenge , akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo kabla ya kuanza ziara yake ya Ukaguzi wa Mazingira ya Machinjio, jijini humo na kulia katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. ( Picha na OMR)
bl2Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, Mh. Binilith Mahenge , akikagua machinjio ya Vingunguti leobl3Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mh. Binilth Mahenge (wa tatu kulia), akikagua mazingira ya Machinjio ya Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. (Picha na OMR)
………………………………………………………….
Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais
Baadhi ya machinjio jijini Dar es Salaam hayakidhi vigezo vya mazingira ya machinjio, hali ambayo huatarisha afya za wakazi wanaozunguka maeneo hayo ikiwemo pamoja na wafanyakazi machinjioni humo.
Hayo yalibainika wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu ya Rais – Mazingira, Mh. Binilith Mahenge alipofanya ziara ya ukaguzi mazingira katika baadhi ya machinjio hayo jijini humo leo.
Katika ziara hiyo, Mh. Mahenge alitembelea machinjio ya Ukonga na kubaini kuwa, machinjio hayo hayajakidhi vigezo vya mazingira ya machinjio ambavyo ni kuwepo kwa mabwawa maalum ya kuhifadhi majitaka yatokanayo na shughuli hizo ikiwemo na kusakafiwa kwa saruji eneo hilo.
Ilihali machinjio hayo huchinja ng`ombe 200 hadi 250 kwa siku ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Ilala hutoza ushuru wa shilingi 2500 kwa kila ng`ombe na mmiliki wa machinjio hayo hutoza shilingi elfu 2 kwa kila ng`ombe kama gharama za uendeshaji shughuli hiyo.
Aidha Mh. Mahenge, alimtaka mmiliki wa machinjio hayo kutekeleza vigezo hivyo vya mazingira kwa kuwa suala hilo linaweza kufanyika kupitia mapato yatokanayo na shughuli za uendeshaji wa machinjio hayo.
Wakati huo huo pia, alitembelea machinjio ya Vingunguti ambapo Taarifa ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilieleza kuwa mazingira ya machinjio hayo hayaridhishi kutokana na uchakavu wa miundombinu yake.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa miundombinu iliyopo bado inaendeleza mfumo wa kizamani katika uendeshaji wa shughuli hizo hivyo kupelekea usafi wa maeneo hayo kuwa mgumu na usiokidhi vigezo vya mazingira.
Kufuatiwa Taarifa hiyo ya Halmashauri, Mh. Waziri alishauri na kuutaka uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuweka bajeti maalum ya kutunza na kuboresha mazingira ya machinjio hayo.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images