Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 497 | 498 | (Page 499) | 500 | 501 | .... | 1898 | newer

  0 0

  AutoSueco is a subsidiary of Nors Group, the leading supplier of Trucks, Construction Equipment, Power Generators and Industrial Engines. Established since 1949 with HQ in Porto, Portugal; it has several brands worldwide.
  ……………………………………………………….
  AutoSueco Tanzania (Volvo) has appointed Alen Nkya as new Commercial Manager CE, a unit whose primary function is to run overall Construction Equipment business which also comprises of mining machines. He joins from April, this year.
  In a statement released today states that Mr. Nkya has over 10 years’ experience in the industry. Formerly a Sales Manager CE at Hyundai, he has an outstanding track record of achievements in Marketing, Business Development and Customer Relations.
  “I’m looking forward to this new challenge,” said Mr. Nkya. “Tanzania is one of the key markets with great potentials, so we must prosper in here and not just stay.”
  AutoSueco is a subsidiary of Nors Group, the leading supplier of Trucks, Construction Equipment, Power Generators and Industrial Engines. Established since 1949 with HQ in Porto, Portugal; it has several brands worldwide,

  0 0

  WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
  TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO
  (TaSUBa)
  timthumb

  TANGAZO LA KUJIUNGA NA CHUO
  TaSUBa inawatangazia umma nafasi za kujiunga na kozi kwa ngazi ya Cheti (Certificate) na Stashahada (Diploma) kwa mwaka wa masomo 2015 /2016
  Kozi hizo ni kama ifuatavyo:-
  1. Sanaa za Maonyesho (Performing Arts):-
  Muziki, Ngoma, Tamthiliya/Maigizo, Sarakasi na Sanaa za Ufundi
  1. Ubunifu na Uzalishaji wa Muziki (Music Design and Production)
  2. Picha Jongefu (Media Design and Film Production)
  - Masomo ya sayansi ya Jamii, ICT, Kiswahili na Kiingereza yatafundishwa kwa wote.
  - Mwombaji kozi namba mbili (2) na namba tatu (3) awe na ujuzi wa compyuta.
  unnamed (3)Pichani miongoni mwa walimu wa TaSUBa wakionyesha igozo la ubunifu jukwaani chuoni hapo.

  NGAZI YA CHETI KWA MIAKA MIWILI
  Sifa za Kujiunga

  - Aliyemaliza Darasa la Saba (Standard Seven) na ambaye hakuhitimu kidato cha Nne
  - Aliyehitimu kidato cha Nne na hakufanikiwa kupata wastani wa “D” nne (4)
  ANGALIZO:
  - Ngazi hii ni kwa Masomo ya Sanaa za Maonyesho TU.
  - Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM B
  IMG_0404.jpg wanafunziBaadhi ya wanafunzi wa wakiwa katika moja ya shughuli za ngoma katika jukwaa chuoni hapo.
  NGAZI YA CHETI KWA MWAKA MMOJA
  Sifa za Kujiunga
  - Aliyemaliza kidato cha nne na kupata wastani wa “D” nne (4)
  ANGALIZO:
  - Watakaofaulu wastani wa ‘B’ baada ya kuhitimu ngazi ya cheti wataruhusiwa kujiunga
  na Stashahada (Diploma) kwa miaka miwili.
  - Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM A
  a78f38f1d4L
  Wanafunzi wa TaSUBa wakiwa darasani chuoni hapo.
  NGAZI YA STASHAHADA (DIPLOMA)
  Sifa za Kujiunga
  - Awe amefaulu kidato cha sita na kupata principal pass 1 na subsidiary 1
  - Awe amehitimu ngazi ya cheti cha sanaa za maonyesho na ufundi kwenye chuo kinachotambuliwa na NACTE
  ANGALIZO:
  - Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM A
  IMG-20130928-WA0000Miongoni mwa wasanii Mahiri hapa Nchini Tanzania, Baba Haji akiwa katika pozi wakati wa kuhitimu masomo yake. Msanii huyo ni miongoni mwa wasanii waliopitia chuo hicho.
  MAELEZO MENGINE

  - FOMU za kujiunga zinapatikana Chuoni pia kwenye tovuti ya chuo www.tasuba.ac.tz
  - Kila mwombaji atalipia ada ya FOMU ya Tsh.15,000/=kupitia NMB BANK akaunti
  Na. 2101100012 yenye jina UTAWALA CHUO CHA SANAA
  - Maombi yaambatanishwe na stakabadhi ya malipo (Receipt/Bank Pay Slip) ya Tsh. 15,000 kwa ajili ya FOMU.
  - Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31/05/2015 na maombi yote yatumwe kwa; MTENDAJI MKUU, TaSUBa, S.L.P 32, BAGAMOYO, Tanzania.
  - Kwa MAELEZO zaidi wasiliana nasi kupitia namba za simu: 0715974100, 0763408792, na 0715394933 au Barua pepetaasisisanaa@gmail.com

  0 0

  Awali ya yote nirudie kutoa pongezi kwa serikali kwa hatua hii muhimu waliyofikia ya kuwasilisha mswada wa sheria mtandao ambao naimani kubwa itakua na majibu mazuri ya kudhibiti na kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao nchini. Naomba itambulike Tanznaia si ya kwanza kuwa na sheria za usalama mitandao na ukweli ni kwamba tumechelewa kwa kiasi Fulani. Nchi nyingi tayari zinasheria za usalama mitandao na zimeendelea kuboreshwa kadri teknolojia inavyo endelea kukua na kubadilika.


  Nitaanza na mifano michache kunasheria mitandao zilizopendekeza kifungo cha maisha kwa wahalifu mtandao nchini Uingereza. Na katika Kikao cha usalama mitandao kilichopita mshiriki aliyekua nami meza kuu katika kuongoza moja ya kikao aliyetokea “US Secret service” alipata kuainisha adhabu ya miaka kumi na sita bado imeonekana ni ndogo na inashauriwa kuongezwa makali.


  Aidha, Nieleze ushauri wa kuhakiki sheria mitandao zinaboreshwa na kuwa kali zaidi ni kutokana na athari ya uhalifu mtandao kua kubwa sana na imekua ikimgusa kila mmoja wetu – Kwan nje ya nchi kila siku tumekua tukipata habari mpya ya matukio ya kiuhalifu mtandao ambapo maelfu wamekua wakipoteza maisha, fedha na pia ufaragha wao umekua ukitumiwa vibaya na wahalifu mtandao.


  Tanzania pia hatuko salama – Nimekua nikipata malalamiko mengi ya watu kudukuliwa faragha zao, kuibiwa fedha nyingi sana na wengine kufikia hata kujitoa maisha kwa kudalilisha mitandaoni.


  Hayo yote yamekua yakisukuma wataalam usalama mitandao kuumiza vichwa kuhakiki wanakuja na mwarubaini wa uhalifu huu mtandao unaozidi kuota mbawa kila kukicha. Hapo ndipo mengi yakawekwa sawa katika kukabiliana na hali hii ikiwa ni pamoja na kukuza uelewa kwa watumiaji mtandao (Matumizi salama ya mitandao), Kuzalisha na kuongezea uwezo kwa wataalam wa usalama mitandao, kuwa na sharia stahiki za uhalifu mitandao, kukuza ushirikiano kutokana na uhalifu huu kutokua na mipaka, kuhimiza kupatikana kwa takwimu sahihi za uhalifu mitandao ili kuweza kutambua maeneo athirika zaidi.


  Kwenye hili la Sheria ni hatua nzuri sana ambapo Tanzania imefikia ili kuweza kurahisisha mapambano dhidi ya uhalifu mtandao nchini na kuhakiki taifa linabaki salama kimtandao. Naimani Kila mmoja wetu ukizingatia wote ni wahanga kwa namna moja au nyingine ya uhalifu mtandao lazima tufurahie na kulipokea hili kwa mikono miwili. Wataalam wa usalama mitandao wamefurahishwa sana na hatua hii yetu na pongezi ni nyingi sana hadi sasa.


  Kuondoa hofu Watanzania naomba nieleze kwamba katika kuandaa muswada huu wataalam na wadau mbali mbali walishirikishwa na badae kuvuka mipaka kwa wataalam kutoka mataifa mbali mbali katika maswala haya ya usalama mitandao kutoa maoni yao na kuboresha – Haikukomea hapo imepitia hatua kadhaa na hata kupelekea kauli yangu niliyo itoa katika moja ya vikao vya wataalam wa usalama mitandao kueleza kuwa “ Hatua za kitaalam zimekwisha sasa ipo kwenye hatua za kisiasa kuweza kupatiwa Baraka kabla ya kuwasilishwa bungeni” – Kauli ambayo wataalam
  waliona taifa letu linachelewa sana kwani sharia zilikua hazina shaka na hata kupitiwa kwakwe kulipaswa kua kwa muda mfupi.

  Nimepata kufatilia kwa karibu kinachozungumzwa na wengi, Hofu kubwa nilizo ziona ambazo nimeona nizitole ufafanuzi ni kama ifuatavyo: -  MOJA, hofu kuwa uchunguzi wa makosa haya inaweza ikawa inakiuka faragha. Naomba nieleze kuna anaefahamu faragha yake iko dhaifu kiasi gani mara tu anavyo kua mtandaoni? Ni wazi kabisa unapaswa kujua faragha haiingi matatani tu kwa sababu ya sharia hizi mtandao.


  Uchunguzi wowote wa uhalifu mitandao duniani kote unahusisha uangalizi wa kina hatua kwa hatua kwa kila ushaidi wa kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupitia kwa karibu kila chembe ya shaka ya kile kinachoweza kuonekana kinaweza kuwa na chembe ya sababu ya uhalifu mtandao.


  Uchunguzi wa makosa ya digitali ni fani na ina maadili yake – Maadili ambayo yanasomewa darasani. Maadili hayo yana hakiki mchunguzi anafata masharti na vigezo stahiki vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kutotoa siri zisizoendana na uhalifu mtandao unaochunguzwa pamoja na kuwasilisha ushahidi kwa mhusika pekee bila kushirikisha kila mtu. Zaidi inawatu maalum si kila mtu anatakiwa kushiriki katika uchunguzi wa uhalifu mtandao. Na hili kuna moja ya masharti yana sisitiza kushirikisha idadi ndogo sana ya wachunguzi ni vyema zaidi.


  MBILI, kuna hofu kwanini makosa mtandao yanapatiwa ruhusa ya kuchunguzwa bila hata kusubiri ruhusa ya mahakama? Ikumbukwe kuwa kwanza uhalifu mtandao unafanyika kwa haraka sana na hauna mipaka. Ndio maana hili limeangaliwa sana na kuamua kutoa ruhusa kwa wapelelezi teule wa makosa ya uhalifu mtandao kupewa fursa ya kuazisha uchunguzi mara moja bila ya kungoja mahakama, Ikumbukwe kuna kinachoitwa “search warrant” ambacho mchunguzi wa makosa mtandao anakua nacho nahii inatolewa na kiongozi katika kitengo kinacho jihusisha na usalama mitandao katika taifa husika. Kusisitiza hili kama pangetolewa ruhusa kusubiri protokali za mahakama kufatwa kumbuka uhalifu mtandao unauwezekano mkubwa sana wa kupotezwa ushaidi wake na kusababisha ugumu kwenye kufikia malengo.


  TATU, Hofu ya faragha ya kupekuliwa mawasiliano – Niulize kama unatumia mtandao kuwasiliana vizuri hofu inatoka wapi kwenye hili. Kama unajua hunachembe ya uhalifu mtandao katika mawasiliano yako sidahani kuna haja ya kua na hofu kuchunguzwa. Na ikumbukwe yule aliyetiliwa mashaka pekee ndie anaye pekuliwa si kila mmoja atapekuliwa mawasiliano yake. Hii iko kila mahali duniani sisi sio wa kwanza.


  Mimi nadhani hofu kubwa tulitakiwa kuwa nayo ni kuhusu mamilioni ya pesa yanayo potea katika mabenki yetu, athari za lugha za uchochezi kwenye mitandao, athari za kuporomoka kwa maadili yetu, athari za mama na dada zetu kusambazwa picha zao za uchi mitandaoni, athari za wasanii wetu kutopata mapato kutokana na watu kuiba kazi zao mitandaoni, athari za kudukuliwa na wahalifu mitandao na taarifa zetu kutumiwa vibaya, athari za kuogopa kufanya miamala ya kifedha kupitia simu zetu, athari za kuogopa kuweka pesa benki inayo pelekea uchumi wa taifa kuyumba, athari zilizombele yetu zinazoweza kupelekea kuhatarisha maisha ( Kufa) kupitia uhalifu mtandao na athari nyingine nyingi.


  Ikumbukwe athari ni kubwa sana za uhalifu mtandao na hofu kubwa tulipaswa tuwe nayo na kwapamoja tuungane kuhakikisha sharia mtandao zinazidishwa makali na uchunguzi wake unafanywa kwa kina na utaalam wa hali ya juu. Hili ndilo linapelekea wataalam tunakutana mara kwa mara kuongezeana uwezo wa kuhakiki tuna tambua mbinu mpya za uhali mtandao na kujinoa kujua namna ya kuchunguza na kuweza kufikia malengo ya kudhibiti.


  Wabunge walionyesha hisia zao kutaka kupata ufumbuzi wa mabilioni ya pesa yanayopotea katika mabenki na makampuni ya simu kupitia uhalifu mtandao – Wanapaswa kukumbuka udhibiti unapaswa kwenda sambamba na kua na sheria madhubuti zinazoweza kuhimili hali mbaya ya uhalifu mtandao nchini.


  Naomba tu kusisitiza watanznaia kusoma na kuelewa na sio tu kufata mikumbo kwenye hili. Aidha, Hofu kubwa lazima iondoshe hofu ndogo. Nikiimanisha Uhalifu mtandao nitishio kubwa kuliko ugaidi na sheria zetu zanafanana kabisa na sheria nyingine za mataifa mbali mbali huku baadhi zikiwa kali zaidi kuliko tulizo nazo. 

  Nimalizie kwa kutoa wito wa matumizi salama ya mitandao ili kujiepusha na kuingia matatani bila sababu za msingi. Huku nikiwatoa watanznaia hofu juu ya uchunguzi wa dhati wa makosa haya uanafanywa na hakuana atakae ingia matatani kama si muhusika.

  0 0

  unnamed
  Waziri wa Nishati na Madini (wa pili Kulia) Mhe.George Simbachawene akizungumza na waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu Ugunduzi wa nane wa gesi asilia uliyofanywa na Kampuni ya Statoil katika eneo la Bahari Kuu,(wa kwanza kulia) ni Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt Charles Mwijage,na (wa kwanza kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Nishati na Madini Mhe.Richard Ndassa (Mb) wa Sumve CCM.
  Picha na Anitha Jonas – MAELEZO,Dodoma.

  0 0

  Na Greyson Mwase
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava amesema kuwa jumla ya leseni 3,449 zilitolewa katika mwaka wa fedha 2014/15 kwa wachimbaji wa madini ya aina mbalimbali nchini.
  Mhandisi Mwihava aliyasema hayo wakati akielezea mafanikio ya sekta za nishati na madini kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini uliofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam unaoendelea. 
  Lengo la mkutano huo ni kujadili mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Tasisi zake.
  Alisema kati ya leseni hizo leseni mbili ni za uchimbaji mkubwa, leseni za utafutaji wa madini ni 694, leseni za uchimbaji wa kati ni 21 na leseni za uchimbaji mdogo ni 2,732.
  Mhandisi Mwihava alieleza kuwa lengo la kutoa leseni hizo ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wanaendesha shughuli za uchimbaji katika maeneo rasmi yaliyopimwa na kuongeza pato la serikali.
  Alisema mbali na utoaji wa leseni hizo, wamiliki wa leseni 1,144 wa leseni za utafutaji madini, wamiliki 34 wa leseni za uchimbaji mkubwa na wamiliki 83 wa leseni za uchimbaji mdogo walisajiliwa kutumia mfumo wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao ujulikanao kama Mining Cadastre Portal.
  Alisema kuwa mfumo huo unawezesha wamiliki wa migodi hiyo kuhuisha leseni kwa kutumia mtandao badala ya kufunga safari hadi kwenye ofisi za madini.
  Mhandisi Mwihava akielezea mafanikio mengine katika sekta ya madini alisema kuwa mwezi Desemba, 2014 kampuni ya uchimbaji madini ya Resolute (T) Limited ilikabidhi miundombinu yote ya mgodi wa Golden Pride kwa Chuo cha Madini Dodoma ambayo itatumia kufundishia wanafunzi wa chuo hicho kwa vitendo. Aliongeza kuwa mafanikio mengine ni pamoja na uanzishwaji wa Ofisi mbili za Kanda na nne za Afisa Madini Mkazi ambazo zinafanya kazi.
  Alitaja ofisi hizo kuwa ni pamoja na Kanda ya Ziwa Nyasa – Songea, Kanda ya Ziwa Viktoria Mashariki – Musoma, Ofisi za Madini Mkazi zilizopo Bariadi, Moshi, Nachingwea na Njombe. Wakati huo huo akielezea mafanikio ya sekta ya nishati, Mhandisi Mwihava alisema kuwa hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu, utekelezaji wa mradi wa Kinyerezi 1 ulikamilika kwa asilimia 84 ambapo mitambo yote minne pamoja na mitambo ya kupooza injini imeshafungwa kwenye eno la mradi na kusisitiza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema Juni mwaka huu.
  Aliongeza kuwa mradi wa ujenzi wa bomba la gesi umekamilika kwa asilimia 97 na kuongeza kuwa mara baada ya ukamilishwaji wake wananchi wataanza kupata umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu.
  “ Pamoja na hayo, hadi kufikia Februari, 2015 jumla ya wateja wapya 131, 180 walio ndani na nje ya gridi ya taifa wameunganishwa na umeme ambayo ni sawa na asilimia 75 ya lengo la Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa mwaka ambalo ni kuunganisha wateja 175,000. “ Alisisitiza Mhandisi Mwihava.
  Alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa kampuni ya maendeleo ya joto-ardhi Tanzania ambayo ilianza kazi yake rasmi tangu Julai, 2014 na ukamilishwaji wa rasimu ya sera ya nishati na mafuta ambazo ziko kwenye hatua ya kuwasilishwa kwenye baraza la Mawaziri.

  0 0


  Katika jitihada za kupambana na uhalifu wa kimtandao ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kibenki katika mazingira salama zaidi, Benki ya Exim imetoa wito kwa wateja wake kuchukua kadi zao za ‘Faida chip and pin Debit Card’ zilizotambulishwa mapema mwezi Januari mwaka zilizochukua nafasi ya ‘Magnetic Stripe Faida Debit Card’.

  Kadi za ‘Faida chip and pin Debit Card’ hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja ikiwa na mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki ya Exim, Bw. Eugen Masawe jijini Dar es Salaam jana, mwisho wa kuchukua kadi hizo ni tarehe 15 Aprili, hivyo wateja wamebakiwa na siku zipatazo 13 kuanzia leo.

  “Tunatoa wito kwa wateja wetu kuchukua kadi zao za ‘Faida chip and pin Debit Card’ ambazo ni salama zaidi ukilinganisha na ‘Magnetic Stripe Faida Debit Card’ zilizokuwa zikitumika hapo awali.

  “Wateja hawatakuwa na uwezo wa kutumia kadi zao za zamani kuanzia tarehe 15 Aprili, kwani kadi hizo zitafungiwa. Hivyo wateja wanapaswa kutembelea matawi yao ili kuchukua kadi mpya,” alisema Bw. Masawe.

  Bw. Masawe alisema kuwa benki yake imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja na kusisitiza juu ya uchukuaji wa kadi hizo ambazo zitawasaidia wateja kufanya miamala yao ya kila siku katika mazingira salama zaidi.

  “Kwa kutumia kadi hii mpya ya kimataifa kutoka Benki ya Exim, mteja anaweza kuwa na uhakika kwamba miamala yake inafanyika katika mazingira salama kabisa,” alisisitiza.

  Aliongeza kuwa, Kadi hiyo mpya ya kimataifa inamuwezesha mteja kufanya miamala duniani kote katika mashine za ATM na POS zilizothibitishwa na MasterCard.


  0 0

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi na (kulia) ni Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti, Gaurav Dhingra.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati), ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi (kushoto) na Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti wa kampuni hiyo, Gaurav Dhingra wakionyesha ishara dole wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
  Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti, Gaurav Dhingra akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampunihiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akifatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

  MAONESHO YA KIMATAIFA YA VITO YA ARUSHA
  TAREHE 21-23 APRILI, 2015

  Wizara ya Nishati na Madini (MEM) kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), wanawaalika wadau wote wa Sekta ya Madini na wamiliki wa leseni za biashara ya madini, Masonara na wachimbaji wa madini ya vito kushiriki kwenye Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Vito ya Arusha (Arusha Gem Fair-AGF 2015). Maonesho haya yatafanyika katika hoteli ya Mount Meru ya Arusha, kuanzia tarehe 21 hadi 23 Aprili, 2015.

  Maonesho ya AGF kwa mwaka 2015 yanalenga kuendeleza azma ya kuifanya Arusha kuwa kituo cha madini ya vito Afrika. Pia maonesho haya yatawakutanisha washiriki (exhibitors) zaidi ya 100 kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini na wanunuzi wa kimataifa zaidi ya 1000 pamoja na wadau mahiri wa tasnia ya vito. Maonesho haya yanadhamiria kuendeleza biashara ya madini ya vito katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Mabanda ya maonesho yanapatikana kwa gharama za Dola za Marekani 1,000. Kamati ya Maonesho inasimamia ugawaji wa mabanda hayo kwa ushindani (first come-first be served).

  Taarifa kuhusu usajili zinapatikana katika Ofisi za Madini za Kanda zilizo katika Miji ya Arusha, Mwanza, Dar es salaam, Mtwara, Mpanda, Shinyanga, Mbeya, Musoma, Songea na Singida au Ofisi za TAMIDA. Wanunuzi wanatakiwa kujisajili kupitia tovuti ya maonesho: www.arushagemshow.com; au kwa barua pepe ya maonesho: info@arushagemshow.com; au kwa njia ya simu zifuatazo 0786366968, 0767498869 na 0767223387.

  KATIBU MKUU

  0 0

  EFM’s birthday cake.002
  Mkuu wa Mawasiliano na mtangazaji wa kipindi cha Joto la asubuhi Dennis Ssebo akiwa na Mkurugrnzi mkuu wa EFM redio bwana Francis Ciza.
  004
  Bwana Sukhwinder Bajwa,yeye ni mkuu wa masoko kutoka kampuni ya Zantel.Alikuja kuipongeza EFM siku ya leo.
  006
  Muheshimiwa David Kafulila alipokua akiongea moja kwa moja kutoka katika kituo cha 93.7 EFM siku ya leo.007
  Tunakata keki kwa pamoja.008
  Jeneral meneja wa EFM Geofrey Ndaula,alikipiga stori mbili tatu na Reuben Ndege(Ncha kali)pamoja Sostenas Ambakisye(Rdj-Kamokali).009
  Picha ya pamoja.
  …………………………………………………………………….
  WATANZANIA wameaswa kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Kituo cha Radio cha E FM kwa lengo la kuwasaidia kutimiza ndoto zao za maisha ya baadae pamoja na kuliletea Taifa maendeleo.
  Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa E FM,FRANCIS SIZA wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za urushaji wa matangazo ya Efm Radio. Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meya wa 
  Manispaa ya Kinondoni YUSUPH MWENDA, Mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa DAVID KAFULILA, Mheshimiwa ZITTO KABWE na Mkurugenzi wa Masoko kutoka Zantel, SUKHWINDER BAJWA.
  Katika hafla hiyo SIZA amesema kuwa ni muda muafaka sasa kwa Watanzania kubadili maisha yao kuwa chanya kupitia E FM na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano, kwani E FM ipo kw aajili ya Watanzania. Wakati huohuo,Mstahiki Meya wa MANISPAA ya Kinondoni YUSUPH MWENDA amesema kuwa, mbali na Efm kutoa Burudani pia imetoa mchango mkubwa kutatua changamoto kwa wananchi. MWENDA amewasihi wananchi hususani wa Kinondoni kutumia vyema matangazo ya Efm Radio ili iwe rahisi kutatua kero mbalimbali.
  Naye Mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa DAVID KAFULILA amesema kuwa, ameguswa kwa kiasi kikubwa na vipindi mbalimbali vinavyoendeshwa na Kituo hiki kwa kuwa vinaligusa Taifa. Akimzungumzia kumkumbuka ZITTO KABWE akiwa ni rafiki yake Bungeni na ni mmoja ya Wabunge wanaotoka wote mkoani wa Kigoma, Mheshimiwa KAFULILA amesema kuwa ,ZITTO alikuwa ni miongoni mwa Wabunge vijana walioleta mabadiliko makubwa ya Kisiasa nchini.
  Kwa upande wake Mheshimiwa ZITTO KABWE amesema, kwa kipindi kifupi, EFM imeonesha Taswira ya hali ya juu inayoakisi hali halisi ya chombo cha habari kinavyotakiwa kuwa. ZITTO amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kituo hiki kimeonesha utofauti na Vyombo vya Habari vingine kwa kuwa kinajali sauti za Wanyonge na si watu wenye nyadhifa Fulani katika jamii.

  0 0

  Kamati ya ufundi ya Trade Facilitation and Ports Community Systems ya Shirikisho la Bandari ulimwenguni " International Association of Ports and Harbours (IAPH)" inakutana Paris , Ufaransa kujadili mambo muhimu ikiwa ni pamoja na kutayarisha Mpango Kazi 2015-2017 wa Kamati hiyo, kupitia na kuandaa taarifa itakayowasilishwa kwenye World Ports Conference itakayofanyika Hamburg, Ujerumani June 2015 , ambapo pia tuzo kwa bandari bora zitatolewa. Ndg. Phares Magesa ni mjumbe wa Kamati hiyo na pia ni mmoja wa majaji wanne duniani watakaoamua na kutoa tuzo hizo. Mkutano wa Kamati hii unafanyika katika ofisi za makao makuu ya bandari ya Paris.
  Wajumbe wakiwa kwenye kikao
  Majadiliano yakiendelea.

  0 0

  Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka ambayo inaanza kesho Ijumaa Kuu, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi, kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao. Uzoefu unaonyesha kwamba, katika kipindi kama hiki cha sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. 
  Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mikoa yote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na pale vitakapoonyesha dalili ya kujitokeza viweze kudhibitiwa kwa haraka.
  Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
  Vilevile, Jeshi la Polisi linawataka madereva na watu wote watakaokuwa wakitumia barabara, kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuepuka kwenda mwendo kasi, kujaza abiria kupita kiasi na kutumia vilevi wawapo kazini. Wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao hususani katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi.
  Aidha, wazazi wawe makini na watoto wao, kutokuwaacha watembee peke yao ama kwenda disko toto bila kuwa chini ya uangalizi wa watu wazima ili kuepusha ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.
  Wananchi wakumbuke kutokuacha makazi yao bila uangalizi na endapo italazimu kufanya hivyo watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu watoe taarifa haraka kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu yao, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.
  Mwisho, Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya biashara hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, mahoteli na maeneo ya benki. Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji wa wahalifu hao endapo uhalifu unatokea.
  Tunawatakia watanzania wote Pasaka njema.
  Imetolewa na:-
  Advera Bulimba -SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.

  0 0

  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akichangia na kufunga Semina maalum ya siku moja iliyoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuwaelimisha wadau wa vituo mbalimbali vya kutolea huduma za matibabu Mkoani Rukwa juu utaratibu wa Mfuko huo katika kutoa mikopo ya vifaa tiba, dawa na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za matibabu. Lengo kuu la utaratibu huo ulioanzishwa na Mfuko wa Bima ya Taifa ni kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wake na watanzania kwa ujumla. Semina hiyo imefanyika leo tarehe 02/03/2015 katika ukumbi wa RDC Mkoani Rukwa, Ndugu Pangisa amewaasa wadau hao kuchangamkia fursa hiyo kuimarisha huduma katika vituo vyao.
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Rukwa Ndugu Abdiel Mkaro akizungumza katika semina hiyo. Ndugu Mkaro alisema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanza utaratibu wa kuwakopesha wadau mbalimbali wanaotoa huduma za matibabu Mkoani Rukwa, lakini jambo la kushangaza wengi wao wamekuwa hawatumii fursa hiyo vizuri kwani baadhi yao wamediriki hata kutofuatilia maombi yao na kutelekeza barua zao ambazo wameshakubaliwa. Aliwaasa wadau hao kutumia fursa hiyo ili kuboresha huduma katika vituo vyao.
  Mtoa mada mkuu katika Semina hiyo ndugu Yesaya Irira (Kulia) ambaye ni Afisa Mipango na Uwekezaji Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Makao Makuu akizungumza katika Semina hiyo ambapo amesema mikopo hiyo inatolewa kwa vituo vyote vya Serikali, vya Binafsi na vya Kidini kwa kigezo kikuu kuwa kituo hicho kiwe kimesajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kutoa huduma kwa wanachama wake. Aliongeza kuwa miongoni mwa taratibu za kupewa mkopo ni pamoja na Mkopaji kujaza fomu ya maombi ambapo kiwango cha Mkopo kitategemea wastani wa madai ya kituo kwa huduma zitolewazo kwa wanachama wa Bima ya Afya ambayo pia yatakuwa dhamana kuu ya Mkopo husika katika madai ya kila mwezi. Kwa Mkopo unaozidi Milioni tano Mkopaji atatakiwa kuweka dhamana yenye thamani ya mkopo na kwa upande wa mkopo wa kifaa tiba hufanyika kuwa dhamana ya mkopo mpaka marejesho ya Mkopo yatakapokamilika.
   Dkt. Dunstan Tendwa, Afisa Mhakiki wa Ubora wa Huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Rukwa akiwa na wadau wengine walishiriki semina hiyo.
   Wadau kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Manispaa ya Sumbawanga wakifuatilia semina hiyo.
   Bi Safi Julius, Afisa Mipango na Uwekezaji Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wajumbe wengine waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa RDC Mkoani Rukwa.
   Sehemu ya wajumbe katika semina hiyo.
  Sister Helena Katebela wa Kituo cha Afya Katandala akiuliza swali katika Semina hiyo. Alitaka kujua endapo dawa anazohitaji Mkopaji hazipo kwa wakala wa usambazaji ambaye ni MSD itakuwaje? Alipata jibu kuwa mkopaji huyo ataelekezwa kwa msambazaji mwingine aliyejiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afta tofauti na MSD. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

   Kwa mara nyengine tena Mwanamitindo afanyae kazi zake za uanamitindo nchini Marekani Flaviana Matata amepata deal ya kutangaza vipodozi vya Kiko Milano vya nchini Italy .Flaviana na wanamitindo wenzie wanatangaza kampeni iyo iliyopewa jina la Modern Tribe
  flavy 

  0 0

  Kama inavyofahamika, chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997 na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 2010, jukumu la Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kusimamia na kuendesha Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani kwa Tanzania Bara. 

  Aidha, Sheria ya Kura ya Maoni imezipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar jukumu la kuendesha Kura ya Maoni kwa ajili ya kuhalalisha Katiba Inayopendekezwa. Kwa mujibu wa Katiba na Sheria, Tume hizi huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na mamlaka nyingine yeyote.

  Ni jambo linaloeleweka kwamba, zoezi lolote la Uchaguzi huanzia na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Wapiga Kura wote wenye sifa za Kikatiba na Kisheria ya Kupiga Kura ni lazima kwanza waandikishwe katika Daftari na kupata Kadi kama Kitambulisho kinacho thibitisha kuwa ameandikishwa na ndicho atakachotumia kujitambulisha siku ya kupiga kura. Hivyo, ni muhimu sana kuwa na Daftari la Wapiga Kura linaloaminika ili kuhakikisha kuwa wote wanaopiga kura kweli ni wale tu walioandikishwa.

  Kutokana na chaguzi zilizopita, za mwaka 2010, Chaguzi Ndogo za Igunga, Arumeru Mashariki, Kalenga na Chalinze, Daftari lililokuwa linatumika limekuwa lilalamikiwa Tume imelalamikiwa sana hivyo, linahitaji kuboreshwa.

  Hivyo, Tume ilifanya tafiti za kutosha katika nchi mbalimbali ikiwemo wenzetu wa Zanzibar na tuliridhika kwa dhati kuwa, Kuboresha Daftari kwa mfumo wa BVR unafaa. Hata hivyo, kwa Tanzania mfumo huo utatumika kwa Kuandikisha Wapiga Kura tu na siyo kwa shughuli nyingine za Mchakato wa Kupiga Kura.

  Kwa kuwa kazi ya kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni ya msingi kabla ya zoezi la Kupiga Kura, Tume wakati wote imesisitiza kuwa jukumu lake la kwanza ni kukamilisha kazi ya Kuboresha Daftari. Mengine yatafuata baada ya hapo.


  Kama inavyofahamika, zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilizinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu tarehe 24 Februari, 2015 katika Halmashauri ya Mji wa Makambako, Mkoani Njombe. Zoezi lilianza kwa kutumia vifaa 250 vya BVR vilivyokuwa vimefika nchini na ndivyo pia vilitumika wakati wa Zoezi la Majaribio katika maeneo ya Kawe Dar es Salaam, Kilombero Morogoro na Mlele Mkoani Katavi.


  Pamoja na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika matumizi ya mfumo huu, kwa ujumla zoezi limeendelea vizuri. Mwitikio wa wananchi ni mkubwa sana. Kwa mfano katika maeneo fulani ya Kata mbili tumeongeza muda ili kumaliza Uandikishaji kwa wananchi waliojitokeza.

  Inatarajiwa kwamba, zoezi litakamilika Mkoani Njombe tarehe 18/04/2015. Hadi kipindi hiki kwa Kata ambazo Tume imeishapita, hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza Kituoni ambaye aliachwa kuandikishwa. Tume inawahakikishia wananchi kuwa wakati ambapo vifaa vingine vya BVR vinaendelea kupokelewa na Tume wanachi wote watakaojitokeza katika Mikoa mingine nchini wenye sifa wataandikishwa. Baada ya zoezi kukamilika Mkoani Njombe, kwa tarehe zitakazo ainishwa, Tume itaendelea na Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Mikoa ya Ruvuma, iringa, Mtwara, na Lindi.

  Kama ilivyofanyika Mkoani Njombe ni tegemeo la Tume kuwa Mikoa inayofuata itawahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yao na kujiandikisha kwa tarehe zitakazotangazwa kwenye Mikoa husika. Ni upotoshaji kwa wananchi kwamba mistari/foleni ni dalili ya ubovu wa mfumo wa BVR badala ya kuonyesha kwamba ndiyo kukolea kwa demokrasia nchini.

  Mara kwa mara, Tume imeulizwa itakuwaje kama tarehe 30 April, 2015 inakaribia na Tume haijakamilisha Uboreshaji wa Daftari. Wakati wote Tume imesema, ikitokea hivyo itawaarifu wananchi
  haijakamilisha Uboreshaji wa Daftari. Wakati wote Tume imesema, ikitokea hivyo itawaarifu wananchi kwa jumla hali itakavyokuwa.


  Kwa muktadha huo leo tarehe 02/04/2015, Tume inapenda kuwaarifu wananchi kama ifuatavyo;

  i. Kwa vile kazi ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni ya msingi kabla ya Zoezi la Kupiga Kura na kutokana na uzoefu tuliopata Mkoani Njombe, Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura bado halijakamilika Mkoani Njombe na katika Mikoa mingine. ii. Kwa vile zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijakamilika, Tume haitaweza kuendelea na zoezi la upigaji wa kura ya maoni.


  Hivyo, kwa heshima na taadhima Tume inawaarifu kuwa Zoezi lililotangazwa awali la Kura ya Maoni kufanyika tarehe 30 Aprili, 2015 limeahirishwa hadi tarehe itakapotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kushauriana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.


  0 0

  Mdau wa maendeleo wa wilaya za Handeni na Kilindi, mkoani Tanga, bwana Amiri Mganga, mwenye t-shirt nyekundu, akikabidhiwa nakala ya KITABU CHA DIRA NA TUMAINI JIPYA HANDENI, kilichoandikwa na Kambi Mbwana, kutoka kwa Msemaji wa Coastal Union, Assenga Oscar ambaye pia ni Mwandishi wa habari wa New Habari 2006 Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa na The African, leo jijini Tanga, Tanzania.

  Kitabu hicho kinapatikana kwa Sh 3500 tu. Maeneo yanapopatikana kitabu hicho ni pamoja na Handeni Mjini kwa Ayubu Magazeti soko la zamani, Misima, Sindeni, Kwamatuku, Komsala, Korogwe, Tanga Mjini na Dar es Salaam. Kama unahitaji kitabu hicho wasiliana nasi kwa simu +255 712053949, kambimbwana@yahoo.com.
  Picha na Mpigapicha Wetu.

  0 0

  11081279_10153671778293368_2618536340363672919_n (2)

  Na Andrew Chale wa Modewji blog
  Msanii mkali wa maigizo na vichekesho, Nchini, Amri Athuman a.k.a King Majuto anatarajiwa kufanya shoo maalum ya vichekesho katika viwanja vya kufurahia watoto Kariakoo, Aprili 7, mwaka huu Mjini Unguja, Zanzibar.
  Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo kampuni ya Bond Entertainment Limited, kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), walieleza kuwa gwiji huyo wa vichekesho King Majuto ambaye pia ni mkongwe anayetamba ndani na nje ya Tanzania ataonyesha vichekesho vyake hivyo hiyo Aprili 7, katika mapumziko ya siku ya Karume (KARUME DAY).
  KingMajuto“Ni wakati wa familia kujitokeza kwa wingi siku ya Jumanne ya tarehe 7/4/2015, kuja kumshuhudia King Majuto na kufurahia vichekesho vyake” ilieleza taarifa hiyo.
  mzee
  Ambaapo katika siku hiyo ya Aprili 7, kwenye shoo hiyo ya vichekesho, kiingilio kwa wakubwa ni Tsh.2,000/= huku kwa watoto itakuwa ni sh 1,000.
  wema_2Pichani ni baadhi ya vichekesho vyaa gwiji huyo, King Majuto katika moja ya kazi zake akiwa na msanii Wema Sepetu.

  Onyesho hilo lenye vionjo vya “Njoo uvunje mbavu na King Majuto!!. Taarisha mbavu zako” limedhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya tigo Tanzania.

  0 0

  IMG_1562

  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa tatu kushoto) akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (wa tatu kulia), Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia), Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuwasili kwenye mnuso wa uzinduzi wa mgahawa huo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

  Na Mwandishi Maalumu, Trollhattan-Sweden
  MGAHAWA mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa’, umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya dunia.
  Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.

  Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.

  Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.

  Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande.
  IMG_1477
  Wadau wakiwa nje ya ukumbi tayari kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
  IMG_1567
  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) pamoja na Chef Issa Kapande (kulia) wakielekea kwenye eneo la tukio.

  Alisema Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.

  Alisema hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto.
  "Ni dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan."

  Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara.
  Katika mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana na juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine katika mitandao ya wapishi wakuu.
  IMG_1577
  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia) wakielekea eneo la tukio.

  Kapande ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya dhahabu katika upishi akiwa na timu ya Sweden magharibi alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wapishi wa nyumbani kukubali kubadilika na kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kujifunza na kufunza ili kuwa na aina nyingine ya mapishi katika kuendeleza sekta.

  Alisema akiwa amefanyakazi katika nchi 17 na tayari akiwa na vitega uchumi nchini alianzia nia ya kuwekeza Sweden mwaka 2009 wakati alipohamia nchini humo akitokea Uswisi. Alisema alianza kwa kuomba vibali, lakini mchakato kamili ulianza mwaka 2013.

  "Tulilazimika kufanya utafiti kidogo" alisema na kuongeza kuwa katika utafiti huo walihoji watu 300 na kujua mwelekeo hasa wa shughuli yao unastahili kuwaje.

  Kapande ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan na Chuo kikuu cha kimataifa cha menejimenti ya hoteli cha Uswis amesema amepambana vikali na mkewe hadi kufikia hatua ya kuanzisha mgahawa huo ambao upo katika eneo la ukubwa wa skwea mita 810.
  IMG_1587
  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa pili kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia). Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto), Makamu mwenyekiti wa kamati ya elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Trollhattans Stad, Fahime Nordborg (katikati).

  Ndani ya mgahawa huo pia watu mbalimbali watapatiwa taarifa za utalii Tanzania. Katika kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani, baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya), Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton, Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Laura Bush.

  Wengine ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide, Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine wengi.
  IMG_1590
  IMG_1592
  IMG_1598
  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiongozana na Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande kwenye sehemu maalum aliyoandaliwa.
  IMG_1484
  Pichani juu na chini ni wadau kutoka kila kona ya dunia waishio nchini Sweden walihudhuria.
  IMG_1551
  IMG_1487
  IMG_1538
  IMG_1495
  IMG_1512
  IMG_1625
  Bw. Per R. Bostrom akisalimiana na Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (aliyeketi). Kulia ni Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
  IMG_1627
  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund wakiwa meza kuu.
  IMG_1875
  Meza kuu.
  IMG_1629
  Mwenyekiti wa awali wa Chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Tengo Kilumanga (katikati) akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa mgahawa huo.
  IMG_1647
  Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande akizungumza machache na wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa risala ya ufunguzi.
  IMG_1656
  IMG_1926
  Meza kuu wakifuatilia historia ya Chef Issa Kapande (hayupo pichani) wakati akizungumza na wageni waalikwa.
  IMG_1980
  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akisoma risala mara baada ya kuzindua mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande.
  IMG_1951
  Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago akitambulishwa kwa wageni waalikwa.
  IMG_1650
  Baadhi wageni waalikwa wakisikiliza historia ya Chef Issa Kapande kabla ya mgeni rasmi kusoma risala ya ufunguzi.
  IMG_1669
  Ukumbi mzima ulionekana kuvutiwa na historia ya maisha na mafanikio ya Mtanzania Chef Issa Kapande (hayupo pichani).
  IMG_1685
  Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Chef Issa Kapande ambapo alimuomba aitafutie nafasi ndani ya mgahawa wake kama kumbukumbu.
  IMG_1699
  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (kushoto) na mwenyeji wake Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund pamoja na Makamu mwenyekiti wa kamati ya elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Trollhattans Stad, Fahime Nordborg (kulia) wakiongoza wageni waalikwa 300 kushiriki chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mmiliki wa mgahawa huo Chef, Issa Kapande.
  IMG_1700
  IMG_1708
  Chef Issa Kapande akikata nyama ya Mbuzi kwa ajili ya mgeni rasmi, Mh, Balozi Dora Msechu.
  IMG_1712
  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akifurahi jambo na Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, Khamis Mwinjuma Simba (kushoto).
  IMG_1715
  Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund akijisevia minofu ya nyama ya Mbuzi wakati wa uzinduzi wa mgahawa huo.
  IMG_1742
  Wageni wakiendelea kupakua chakula.
  IMG_1769
  IMG_1775
  IMG_1798
  IMG_1816
  IMG_1821
  IMG_1756
  Mwenyekiti wa awali wa Chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Tengo Kilumanga (kulia) na mkewe wakishiriki chakula cha jioni kwenye mgahawa wa Mtanzania mwezao.
  IMG_1824
  Katibu wa Chama cha Watanzania Sweden (TANRIKS), Mathias Pembe (kushoto) pamoja na Mhasibu wa chama hicho, Bw. Emmanuel Ntundu ni miongoni kati ya wageni waalikwa 300 waliohudhuria uzinduzi huo.
  IMG_1835
  IMG_1838
  Katibu wa Chama cha Watanzania Sweden (TANRIKS), Mathias Pembe (kulia), Mhasibu wa chama hicho, Bw. Emmanuel Ntundu (kushoto) pamoja na mtoto wa Mwenyekiti wa chama hicho, Grace Saulli wakijichana msosi uliondaliwa na Chef Issa Kapande.
  IMG_1866
  Wageni waalikwa wakiendelea kupiga msosi uliofurahiwa na wengi ambao utakuwa unapatikana kwa chakula cha mchana kwa kipindi cha mwezi mmoja na hapo baadae itakuwa mpaka chakula cha usiku ndani ya mgahawa wa "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food).
  IMG_1869
  Mh. Balozi Dora Msechu na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund.
  IMG_2028
  Mgeni rasmi Mh. Balozi Dora Msechu kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
  IMG_2080
  Mgeni rasmi Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mh. Dora Msechu (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Daniel Saulli (kushoto), Mhasibu wa chama hicho, Emmanuel Ntundu (kulia), Katibu wa chama hicho, Mathias Pembe (wa pili kulia) pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago.
  IMG_2265
  Mgeni rasmi Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mh. Dora Msechu (wa pili kulia) na Mtanzania ambaye ni mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden, Chef Issa Kapande katika picha ya pamoja kikundi cha burudani.........
  IMG_2216
  Mtanzania ambaye ni mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden, Chef Issa Kapande katika picha ya kumbukumbu na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago.
  IMG_2237
  Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago, Chef Issa Kapande katika picha ya pamoja na timu yake kwenye mgahawa huo.
  IMG_2041
  Mdau Abraham Juma Ndwatta wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden akiwa na Grace Saulli kwenye hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
  IMG_2074
  Wadau wakiendelea kupiga picha na Mh. Balozi Dora Msechu.
  IMG_2125
  Mh. Balozi Dora Msechu akisakata rhumba kwenye uzinduzi huo.
  IMG_2093
  Chef Issa Kapande akicheza muziki na wageni waalikwa.
  IMG_2119
  IMG_2106

  0 0
 • 04/03/15--00:21: TAARIFA KWA UMMA
 • KUMUOMBA MH. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ASIPITISHE
  MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015

  Mtandao wa waandishi kupitia mitandao nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake vyema kwa kutokupitisha muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 unaokandamiza uhuru wa mawasiliano mitandaoni. 

  Muswada wa sheria ya makosa ya Mtandaoni unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, na kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.

  MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015
  Umoja huu (TBN) ulishtushwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali kupitisha Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 kwa hati ya dharura kitendo ambacho hakikutarajiwa kutokana na kuwa mitandao bado ni kitu kipya nchini hivyo tulihitaji maridhiano na wadau na elimu kati ya raia na Serikali ili wengi watambue yapi ni makosa kwa kutumia mitandao na yapi yanakubalika.

  Kimsingi TBN haipingi Tanzania kuwa na Sheria ya Makosa ya Mtandao bali inaiomba Serikali kuwashirikisha wananchi na hasa wadau wa habari na wanamitandao ya jamii ili kuridhiana kwa vipengele ambavyo vinaonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Na hatimaye kutoka na sheria isiyo na viashiria kandamizi juu ya uhuru wa kupata na pokea habari.

  Hali kadhalika tulishuhudia watetezi wa haki za binadamu pamoja na wawakilishi wa watumiaji wa Mtandao wa intaneti nchini wakitoa sababu zenye uzito za kwanini sheria hii isipite kwa hati ya dharura na kuhoji kwanini sheria hii ipite kwa dharura bila ya kupata majibu.

  Muswada huu ambao kati ya makosa mengi uliyonayo kubwa moja wapo ni majukumu makubwa aliyopewa Mkuu wa Kituo chochote cha Polisi kuwa na uwezo wa kupekuwa na kuchukua vielelezo/data pale anaposhuku kuna suala la uhalifu unaohusu mtandao. Swali ni kuwa kwanini polisi apewe mamlaka ya kumsulubisha mtuhumiwa katika hatua ya mwanzo bila uthibitisho wa sahihi?

  Mbali na hapo, sisi kama waandishi ulimwenguni kote tunatakiwa kufuatilia maadili ya kazi zetu. Maadili ya mwandishi yeyote yule ni kutunza usiri wa chanzo cha habari yake pale inapotakiwa lakini katika sheria hii sisi kama bloggers, sheria hii inakiuka hili kwa kutulazimisha kutaja vyanzo vya habari.

  Kupitia sheria hii, bloga yeyote yupo hatarini kutokana na kwamba sheria inaainisha ni kosa la jinai kutoa ujumbe unaoweza kumuudhi mtu kihisia.

  Aidha, tunamuomba Mheshimiwa Rais pia asipitishe Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2013.

  Muswada huu unavinyima uhuru vyombo vya habari vinavyotangaza takwimu mbalimbali. Kama ilivyo Ibara ya 7(4) ‘‘Chombo chochote cha habari ambacho kinachapisha taarifa za kitakwimu za uongo au upotoshaji, au kinatangaza kipindi chochote kinachohusu shughuli za ukusanywaji wa taarifa ambayo imefanywa au inafanywa na Ofisi, na hatimaye kusababisha wananchi wasishiriki kwenye shughuli hiyo ya ukusanywaji wa taarifa au wasishirikiane na maafisa wa Ofisi, kinatenda kosa.’’

  Hii iki maanisha kuwa hata blog zetu ziko hatarini kuelekea katika kulazimika kufanya kazi za kuisifia serikali na kutangaza takwimu zilizopitiwa na serikali tu, jambo ambalo litaharibu ukuaji wa uhuru wa habari nchini.

  Tunamkumbusha mwananchi wa kawaida anayetumia mtandao wa intaneti kuwa hayuko salama kwani sheria hii inamlazimisha mtoa huduma wa mtandao kutoa taarifa za wateja wake jambo ambalo linahatarisha uhuru wa kutoa na kupokea habari.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

  IMETOLEWA NA;
  Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network-TBN)
  04/03/2015.

  0 0

  Mbunge  wa  jimbo la kalenga  Godfrey  Mgimwa  akishiriki  kucheza  kwaito na wanafunzi wa  shule ya  sekondari ya  wasichana Ifunda  leo

  Mkuu  wa  shule ya  sekondari ya  wasichana  Ifunda akimpongeza mwalimu  wa kujitolea  wa Hesabu Shuleni  hapo  mbele ya  mbunge Godfrey Mgimwa
  Mbunge  wa Kalenga  Godfrey Mgimwa kushoto  akikavbidhi  zawadi  kwa  walimu  wa  shule ya  sekondari ya  wasichana Ifunda
  Wanafumnzi  wa  kidato cha  sita  wakikabidhiwa  vyeti  na  mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa
  Wanafunzi  wa  shule ya  sekondari  ya  wasichana  Ifunda  wakimpokea  mbunge  wa  jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa kwa  gwalide  maalum
  Mbunge  Mgimwa wa tatu  kulia  akiongozana na mwenyekiti wa bodi  ya shule hiyo  Abed  Kiponza  kulia na viongozi mbali mbali wa  shule  hiyo ya  serikali ya  kijiji  cha Ifunda
  Mbunge  Mgimwa  akivishwa  skafu 
  Mbunge  Mgimwa  akitazama  mwanafunzi  wa  Ifunda akimpasua Simbilisi 
  Baada ya  upasuaji  kufanyika
  Mwenyekiti  wa bodi ya  shule ya  sekondari ya  wasichana  Ifunda Abed  Kiponza akimpongeza mbunge Mgimwa
  Mbunge  Mgimwa  akiwahutubia  wanafunzi  na  wazazi
   Na MatukiodaimaBLOg
  BAADA ya  wanafunzi kukosa darasa  kubwa la  kusomea ,mbunge   wa  jimbo la  Kalenga  Godfrey  Mgimwa amejitolea kuanza ujenzi  wa darasa  hilo kuahidi kuchangia   mifuko  200  ya  Saruji  yenye  thamani ya  zaidi ya Tsh milioni 3 kwa  ajili ya  kusaidia  ujenzi  wa  darala litakalotumiwa na  wanafunzi  zaidi ya 200 katika  shule ya  sekondari  ya wasichana  Ifunda  katika  wilaya ya Iringa   mkoani  Iringa.

  Mbunge   Mgimwa ambae  alikuwa  mgeni  rasmi  katika  mahafali ya  9  ya  shule   hiyo  ametoa ahadi   leo   kufuatia  maombi ya  uongozi  wa  shule   hiyo  .

  Alisema  kuwa lengo lake  kuona  kiwango  cha  elimu  katika  jimbo lake  kinaendelea  kukua  zaidi na  ndio  sababu  ameendelea  kusaidia  ujenzi  wa maabara pamoja na  kuchangia shughuli  mbali mbali  za  kimaendeleo zinazofanywa na  wananchi  wake  zikiwemo  za ujenzi  wa  shule ,nyumba  za  walimu pamoja na  ujenzi  wa maabara zinazojengwa kufuatia  agiza  la   Rais  Dkt  Jakaya  Kikwete.

  "Leo  hapa  nimeelezwa  changamoto   mbali  mbali  zinazoikabili  shule  hii  kwanza  juu ya  uchakavu  wa majengo ,uhaba  wa  walimu  wa masomo ya  Hisabati na  Sayansi lakini  pia  ukosefu  wa darasa  kubwa  litakaloweza  kuchukua  wanafunzi  200  kwa  wakati mmoja  na mmeomba  kusaidiwa   kati ya  bati 200 ama  Saruji  .......sasa   ili  ujenzi  huu  uanze mimi  nitachangia saruji  mifuko  yote  200  ila rai yangu  kwa  wazazi tuungane  katika  ujenzi  huu"

  Kuhusu tatizo la  uhaba  wa  walimu  alisema  kuwa  hiyo ni  changamoto  ya  nchi  nzima  japo  alisema  lazima  atalifikisha kwa  mkurugenzi mtendaji wa  Halmashauri  ya  wilaya  ya  Iringa  ili  kuweza  kuitazama  shule   hiyo  kwa  jicho  la tatu  .

  Pia  mbunge   huyo  alisema  kuwa  toka  ameingia  madarakani mwaka  jana  kuna baadhi ya  kazi  kubwa  amepata  kuzifanya katika  jimbo  hilo  na  kuwa   wananchi  wa  jimbo  hilo  ni mashahidi  katika suala  hilo na  kuwa akiwa  kama mwakilishi  wa  wananchi  wa Kalenga atahakikisha kwa  muda  uliobaki kuona anatafuta  majibu ya  changamoto mbali mbali  za  jimbo  hilo.

  Aidha  mbunge  huyo  aliupongeza  uongozi  wa shule  hiyo kwa kazi nzuri ya  ukuzaji  wa taaluma  shuleni hapo na hata  kuifanya  shule   hiyo  kuwa  moja kati ya  shule  zenye sifa  nzuri ya  kufaulisha ndani ya  wilaya ya  Iringa ,mkoa na taifa   na  kuwataka   wahitimu  wa  kidato cha  sita  kutumia  muda  uliobaki kujisomea  zaidi  ili  kuendeleza  rekodi ya  kufaulu  vema  katika  mitihani ya kidato  cha sita.

  Mwenyekiti  wa  bodi ya  shule  hiyo  Abed Kiponza akimshukuru  mbunge  Mgimwa  alisema  kuwa msaada  huo  ni  ukombozi  mkubwa wa maendeleo ya  ujenzi  wa  darasa  hilo   pia  aliwaomba  wazazi na  wadau mbali mbali  kujitolea  kushiriki  ujenzi  wa  darasa  hilo  pamoja na uboreshaji  wa majengo  ya  shule  hiyo .

  Kiponza  alisema  kuwa  shule  hiyo  ni   shule  ambayo  imekuwa  ikiendeshwa  kwa misingi  bora ya  kitaaluma na  kuwa  haijapata  kuwa na mgomo  wa  wanafunzi  wala  walimu  tofauti na  shule  nyingine .

  Mkuu  wa  shule   hiyo  Bi Zaina  Salingwa katika  taarifa  yake  kwa wazazi na  mgeni  rasmi  alisema  kuwa  shule   hiyo  ilianza mwaka 2005  baada ya  kufungwa kwa  kilichokuwa  chuo  cha ualimu  Ifunda na  kuwa hali ya majengo  hayo ni chakavu  zaidi  baada ya majengo hayo  kujengwa  toka mwaka 1985.

  Alisema  kuwa  shule  hiyo ni  shule ya  bweni  yenye  uwezo  wa  kuchukua  wanafunzi 640  lakini ina  wanafunzi 653  wakiwepo  wanafunzi 440  wa  kidato cha tano na wanafunzi 213 wa kidato cha sita na  kuwa asilimia 90 ya  wanafunzi  wanasoma  masomo ya  Sayansi na jumla ya  michepuo  waliyonayo  ni  saba   yani CBG, PCB, PCM, PGM,EGM,HGK na HGE na  kuwa  walimu   waliopo  ni 23 huku masomo ya Sayansi  na  Hesabu  yakiwa hayana  mwalimu hata  mmoja  zaidi ya  kukodi  walimu  kutoka nje.

  Mkuu   huyo  alisema  kuwa hadi sasa  shule   hiyo  imefanikiwa  kuwa na gari la  mkuu  wa  shule  ambalo limenunuliwa kwa  kiasi  cha Tsh milioni 20   fedha  zilizochangwa na  wadau mbali mbali  akiwemo kamanda  wa UVCCM mkoa  wa Iringa  Salim Asas .


  0 0

  indexBaraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.
  Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu.
  Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.
  Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kumezwa na faida katika biashara zao kiasi cha kuandaa madisko ya watoto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa makubwa ambayo yangedhibitika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.
  BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.
  BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa Sanaa sherehe njema ya Pasaka yenye furaha tele. 
  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
  Godfrey Mngereza
  KATIBU MTENDAJI

older | 1 | .... | 497 | 498 | (Page 499) | 500 | 501 | .... | 1898 | newer