Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

KUTANO WA TAKWIMU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAFANYIKA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuuwa Ofisi yaTaifayaTakwimu (NBS),kutoka Tanzania  Dkt. Albina Chuwa akifungua mkutano wa Wakurugenzi na Watalaam wa Takwimu kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili mausuala mbalimbali ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.6
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wataalam wa Takwimu wanchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia mausuala mbalimbali wakati wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Pichana Veronica Kazimoto.
…………………………………………………………
 
Na. Veronica Kazimoto, Dar es Salaam.

Wakurugenzi Wakuu wa Ofisi za Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Tanzania wamekutana leo  jijini Dar es salaam kujadili mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi katika kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

Akifungua Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa mkutano huo pamoja na mambo mengine unazileta pamoja Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya Takwimu na mchango wake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi hizo.

Amesema kuwa mkutano huo umelenga kuongeza na kuimarisha ushirikiano baina ya Nchi Wananchama wa Jumuiya hiyo katika matumizi ya Takwimu pamoja na kupitia mabadiliko ya sheria mbalimbali zinazosimamia masuala ya Takwimu kwa Nchi Wanachama.

Kwa upande wao wakurugenzi hao kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, na Burundi wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania kunatoa matumaini ya mwendelezo wa ushirikiano katika matumizi ya takwimu sahihi kutokana na mchango wake katika maendeleo ya nchi zao na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla. 

Wamesema kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana kikamilifu katika kuhakikisha kuwa kunakuwa na usimamizi mzuri wa takwimu mbalimbali zikiwemo za kilimo, Viwanda, Biashara, uchumi  na takwimu nyingine kwa manufaa ya wananchi wa Jumuiya hiyo.

Kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania ambao umehusisha wakurugenzi wakuu, wakurugenzi na maafisa wandamizi wa takwimu ni mwendelezo wa mikutano mbalimbali inayofanyika katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kujadili mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi katika kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

PAMOJA NA KUAIRISHWA TAREHE YA KURA YA MAONI, UMOJA WA MATAIFA WAFADHILI USAMBAZAJI WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA NJIA YA SAUTI

$
0
0
Pamoja na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kuahirisha  tarehe ya kupiga kura ya maoni, Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu na Utamaduni (UNESCO), kwa kushirikiana na Kampuni ya Focus Media pamoja na Mtandao wa radio za jamii  (COMNETA), limeamua kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti nchi nzima, ili wananchi wapate elimu  kuhusu maudhui yaliyomo ndani ya Katiba na kufanya maamuzi sahihi pindi siku ya kupiga kura itakapowadia. 

Aidha, mkakati huo wa kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti unajumuisha utoaji elimu kuhusu mfumo mpya wa kujiandikisha kwa njia ya kieletroniki (Biometric Voters Registration – BVR) pamoja na kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kutimiza haki yao ya kikatiba wakati wa upigaji kura.

Akipokea, nakala za CD zenye Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti, Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez, alipongeza Kampuni ya Focus Media kwa kuandaa matoleo hayo na kusisitiza radio za jamii kuzitumia ili kuwaelimisha wananchi mikoa yote juu ya Katiba inayopendekezwa.

 “Nimefurahi sana kuona hizi nyenzo za kisasa kama SD cards, kwa sababu tunaonesha kwamba radio za jamii ni njia bora zaidi za kutoa taarifa na pia zinawezesha kupata mrejesho kutoka kwa wananchi.” Bi Zulmira Rodrigez, ameongeza kusema “Hili ni jambo zuri sana kwa jamii, na inapeleka taarifa mpaka katika njia ya chini kabisa, vijiji vilivyoko ndani kabisa.”  

Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii Bwana Joseph Sekiku amewashuri watangazaji wa redio mbalimbali wliohudhuria semina hiyo amewaasa kutumia muda uliobai wa siku28 vizuri ili kuelimisha jamii maudhui ya Katiba inayopendekezwa ili wananchi wafanye maamuzi sahihi katika kura ya maoni na uchaguzi mkuu.

Sekiku ameongeza kwamba kwa sasa itapatikana kupia Focus Media pro ltd kwa kupitia mitandao yote ya kijamii na redio mtandao na wananchi wanaweza kuwasiliana kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba +255 772 55 55 53

WACHUNGAJI WATAKIWA KUWARUHUSU WAUMINI KUHUDHURIA TAMASHA LA PASAKA

$
0
0

Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel  ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste, David Mwasota akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka. Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama. (Picha na Francis Dande)
 Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamashas la Pasaka.
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamashas la Pasaka. Kulia ni Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel  ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste, David Mwasota.

NA LOVENESS BERNARD

Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly,  David Mwasota amewataka wachungaji wote nchini  kuwaruhusu waumini wao kuhudhuria katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika April 5 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Askofu huyo amewataka wachungaji wawaruhusu waumini waweze kusherehekea kufufuka kwake Yesu kristo kwa kusifu  na kuabudu pamoja na waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
 
Nawaomba wachungaji wawaruhusu waumini baada ya ibada waje uwanja wa taifa tumsifu muumba wa vyote kwa nyimbo na sala pamoja na waimbaji kutoka mataifa mbalimbali.

Naye Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama alisema waimbaji wameshaanza kuwasili nchini wakiongozwa na Faustine Munishi (Malebo) ambaye aliwasili jana huku Kerechi muimbaji kutoka Uingereza  akitarajiwa kuwasili Jumamosi.

Maandalizi tumekamilisha kwa asilimia 99 na waimbaji wameanza kuwasili nchini ambapo Faustine Munishi mtanzania aishie nchini Kenya na kesho tunatarajia kumpokea Ifeanyi Kerechi na Ephraim Sekeleti kutoka Zambia huku Rebecca Malope na Solly Mahlangu tukuwatarajia kuwasili Aprili 3 alisema Msama.

MKUTANO MKUU WA 31, TUZO ZA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA (MAYORS AWARD) NA MIAKA 30 YA ALAT KUFANYIKA APRILI 8-11, 2015JIJINI DAR

$
0
0


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini jana kuhusu Mkutano Mkuu wa 31 wa ALAT utakaokwenda sambamba na Tuzo za Viongozi wa Serikali za Mitaa ‘Mayors Award’ na Miaka 30 ya ALAT, utakaofanyika katika hoteli ya Kunduchi jijijni Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa ALAT, Habraham Shamumoyo na (kulia) ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB ambao ndio wadhamini wakuu wa mkutano huo, Waziri Barnabas. PICHA NA JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG.



Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 200, kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi kwa ajili ya kudhamini mkutano huo. Katikati ni Katibu Mkuu wa ALAT, Habraham Shamumoyo



XXXXXXXXXXXXXXX



Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) itafanya Mkutano wake Mkuu wa 31 katika hoteli ya Kunduchi jijijni Dar es Salaam. Kauli mbiu ya Mkutano huo unaodhaminiwa na benki ya NMB ni “Wananchi pigia kura katiba pendekezwa kuboresha Serikali za Mitaa na maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015”“.


Mkutano mkuu wa 31 unafanyika pamoja na mambo makubwa mawili yafuatayo; Moja ni Sherehe za Miaka 30 ya Serikali za Mitaa na ALAT ambayo itakuwa na kongamano la kutathmini tulikotoka, tulipo na kuangalia nini cha kufanya huko mbeleni ili kuziwezesha Serikali za Mitaa kutoa huduma kwa ufanisi zaidi. Pili, shaerehe za tuzo za viongozi bora wa Serikali za Mitaa (Mayors Award). Kwa mara ya kwanza ALAT itatoa tuzo kwa viongozi wa Halmashauri ambao wanafanya vizuri katika kusimamia Halmashauri zao. Katika mchakato wa kuwapata viongozi bora wananchi wameshirikishwa kwa kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu kwenda namba 15440. 


Kwa mwaka wa pili mfululizo, NMB wamekuwa wakidhamini mkutano wa ALAT na kwa mwaka huu, wametudhamini kwa shilingi milioni 200 ambapo milioni 150 ni kwaajili ya matayarisho ya mkutano na milioni 50 kwaajili ya ununuzi wa trekta ambalo litakabidhiwa kwa washindi wa tuzo ya uongozi bora wa Serikali za Mitaa (Mayors Award). Trekta hili tunaimani litasaidia shughuli mbalimbali za halmashauri iliyoshinda kama shughuli za ukandarasi ikiwemo utengenezaji wa barabara na urekebishaji wa miundombinu ndani ya halmashauri.


Mkutano wa mwaka huu una umuhimu wa pekee katika historia ya Serikali za Mitaa na taifa letu kwa jumla. Mwaka huu ni mwaka wa 31 tangu kurejesha mfumo wa Serikali za Mitaa hapa nchini mwaka 1984; pili Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania inaadhimisha miaka 31 tangu kuanzishwa kwake tarehe 13 Disemba 1984. Tatu mwaka huu nchi yetu inapitia kwenye mchakato wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayotuwekea misingi na kanununi za uendeshaji wa nchi yetu kwa miaka 50 ijayo ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo ya Serikali za Mitaa itakayo jikita kwenye ugatuaji wa madaraka kupeleka kwa wananchi. 


Mkutano Mkuu wa kawaida wa Jumuiya hufanyika mara moja kila mwaka na wajumbe wake ni: Wenyeviti na Mameya 168 wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya, Wakurugenzi 168 wa Halmashauri, Wabunge 25 mmoja toka kila mkoa. Mkutano huu utahudhuriwa pia na Wizara, Idara za Serikali Kuu, Wakala za Serikali, Taasisi shiriki katika Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Balozi na Wabia katika Maendeleo, Mashirika ya Kimataifa na Jumuiya za Serikali za Mitaa za Afrika Mashariki na wadau wangine wa sekta ya Serikali za Mitaa. 

Aidha Mkutano huu utahudhuriwa na Asasi zisizo za Kiserikali, Mashirika na Makampuni na Wawakilishi wa Sekta Binafsi.  Inatarajiwa kwamba Mkutano huu utahudhuriwa na Washiriki takribani mia tano (550). Mkutano Mkuu wa ALAT ndiyo chombo cha juu kabisa cha maamuzi cha Jumuiya. 


Maandalizi yote kwa ajili ya Mkutanop yamekamilika kwa asilimia 95 na kwa namna ya pekee Kabisa tumemwalika Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mgeni Rasmi wa mkutano wetu Mkuu pamoja na kutoa tuzo za kwa Mameya/wnyeviti wa Halmashauri.


Niwashukuru wadau mbalimbali amabo wamejitokeza katika kufadhili na kusaidia Mkutano huu. Kwa namna ya pekee kabisa niwashukuru benki ya NMB kwa kuendelea kuwa mwenza (partner) katika Mkutano huu na tuzo za viongozi wa serikali za Mitaa. Niwashukuru pia PSPF, MABIBO BEER & WINE, MSD, NHC, NIDA, GF TRUCKS, PPF,TBA, TAA, LAPF, TSN, UTT.

Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ni chombo kinachoziunganisha Halmashauri zote za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji Tanzania Bara. Kwa sasa kuna Halmashauri 168 zinazounganishwa na chombo hiki.

WAIMBAJI KUTOKA UINGEREZA WATUA KUNOGESHA TAMASHA LA PASAKA JUMAPILI UWANJA WA TAIFA.

$
0
0
 Nyakwesy Mujaya akimpa au mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Uingereza, Ifeanyi
Kelechi, akipokea ua kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Msama Promotions, Nyakwesy Mujaya, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam le kwa ajili ya kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka. Kulia ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.
 Msama akipeana mkono na Ifeanyi Kelechi.
NA LOVENESS BERNARD
 
MWIMBAJI wa kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini
Uingereza, Ifeanyi Kelechi, ametua nchini kwa ajili ya kutumbuiza katika
Tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, siku ya jumapili.

Kelechi, aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA), jana saa mbili asubuhi kwa ndege ya Shirika la Qatar, akiongozana na wenzake wanne.

Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Kelechi
alisema lengo la ujio wake ni kuhakikisha tamasha hilo linanoga kuliko
yaliyowahi kufanyika, ndio maana amekuja na jopo la waimbaji watano.

“Namshukuru Mungu kutufikisha salama, nimefurahi
sana kufika Tanzania kwa mara ya kwanza, hasa kuja kuimba kwenye tamasha kubwa kama hili, ambalo naamini litakuwa chachu ya kumfanya kila mtu kuvutiwa nalo,” alisema. 
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, 
Alex Msama, alisema kuzidi kumiminika kwa waimbaji, kunaashiria tamasha hilo litanoga zaidi.

“Waimbaji wetu wameshaanza kuwasili nchini na kesho
waliobakia watawasili…Tunamshukuru Mungu kila kitu kinaenda sawa, tunaisubiria siku hiyo tu,” alisema Msama.

Tayari muimbaji Faustine Munishi ‘Malebo’ mtanzania
anayeishi nchini Kenya tayari kawasili tangu juzi huku Ephraim Sekeleti wa
Zambia, Rebecca Malope na Solly Mahlangu ‘Obrigado’ kutoka Afrika Kusini
watafuata. 
Mbali na waimbaji hao kutoka nje, watakuwepo pia wakali
wa hapa nchini wakiwamo Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro na wengineo.
 Msama akiteta jambo na Ifeanyi Kelechi,
 Ifeanyi Kelechi akiimba moja ya nyimbo zake.
 Miller Luwoye.
 Anthonia Nwafor.
 Msama akizungumza na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama (wa pili kulia) akiwa na waimbaji kutoka Uingereza.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakiwasubiri waimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza leo.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka wakiwa
katika picha ya pamoja wakati wakiwasubiri waimbaji wa nyimbo za injili
kutoka Uingereza leo. 
 Kutoka kushoto, Angela Kaonja, Nyakwesy Mujaya na Grace Khuni
 Angela Kaonja akimvisha skafu mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi.
……………………………………………………………..
 

PRESIDENT KIKWETE VISITS THE BILL GATES FOUNDATION AND BOEING PLANT IN SEATTLE

$
0
0
President Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation visit the Boeing planes manufacturing plant  in Seattle on April 2, 2015
STATE HOUSE PHOTOS.008
President Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation are shown around the offices of the  Bill and Melinda Gates Foundatio in Seattle on April 2, 2015.000000

Mh. Lowasaa katika Ibada ya Ijumaa Kuu leo

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwa ameungana na Waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front la Dar es Salaam leo.
Ibada ikiendelea.
Sehemu ya Waumini wa Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye Ibada ya Ijumaa Kuu leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiongoza Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika leo.

Igizo la Yesu likiongozwa na Bw. Moses Kombe alivyokuwa na wanafunzi wake kabla ya kuteswa hadi kutungikwa msalabani, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka kwenye Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam leo.
Mh. Edward Lowassa akifatilia igizo la mateso ya Yesu, lililoigizwa na Umoja wa Kwaya zote za Usharika wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Igizo likiendelea.
Mmoja wa watoto waliokuwepo Kanisani hapo akiangalia Igizo hilo.
Mmoja wa Waigizaji hao.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akipitia vifungu vya Biblia wakati Igizo la Yesu likiendelea.
Yesu akipelekwa kwa Pilato.
Vijana hao wakiigiza pale Yesu alipofikiswa kwa Pilato kuhukumiwa, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka kwenye Kanisa la KKKT Azania Front Dar es Salaam
Huzuni ilitawala wakati wa Igizo hilo.
Yesu akiwa amebebeshwa Msalaba katika Igizo hilo.
Muumini wa Kikristo, Moses Kombe akitungikwa msalabani kama Yesu katika igizo lililofanywa na Vijana wa Umoja wa Kwaya zote za Usharika wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Jijini Dar es salaam, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu leo.
Kuna waliomlilia na Wengine kufurahia.
+
?>

MASHABIKI WA SIMBA UKAWA WAPATA AJAKI,YADAIWA WATU WATANO WAMEPOTEZA MAISHA

$
0
0
kikundi cha ushangiliaji cha tawi la Simba la Mpira na Maendeleo maarufu kwa jina la Simba Ukawa  wamepata ajali  iliyotokea leo mjini Morogoro wakielekea mjini Shinyanga kuisapoti timu yao inayocheza mechi ya ligi kuu kesho dhidi ya Kagera Sugar.

Taarifa mpya na za uhakika zinasema watu watano (5) akiwemo kiongozi wa Simba Ukawa, Mohammed Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ wamefariki dunia na watu 15 wapo mahututi.

Ajali hiyo imetokea eneo la Mvomero ikihusisha basi dogo aina ya Toyota Costa lililopinduka na kuacha njia. Polisi bado hawajatoa tamko rasmi.


Waliotangulia mbele ya haki mpaka sasa ni:
Waluya, Rehema, Ali Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ Wabi na dereva wa gari Abdallah Fundi.maandishi picha  na Shafih dauda.com 



PRESIDENT KIKWETE ADRESSES WORLD AFFAIRS COUNCIL, MEETS WITH TANZANIANS LIVING IN SEATTLE

$
0
0
President Jakaya Mrisho Kikwete addresses a meeting of the World  Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
jk 2
President Jakaya Mrisho Kikwete chats with Carmen Hummel who had asked him a question on how his childhood was during a meeting of the World  Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
jk3
President Jakaya Mrisho Kikwete is mobbed by excited stidents after addressing a meeting of the World  Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
jk4jk5jk6
President Jakaya Mrisho Kikwete greets members of the Tanzanian Community based in Seattle  during his one-day visit of the city on Thursday April 2, 2015
STATE HOUSE PHOTOS

EFM yapiga stori na Wadau wa Tasnia ya Habari za Mitandao

$
0
0
 Mtangazaji wa Radio 93.7 EFM ya jijini Dar es salaam, Samira Kiango (pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Tasnia ya Habari za Mitandao (Social Media), Clarence Mulisa kutoka Global Publishers (kulia), Fredrick Bundara kutoka Bongo Five (pili kushoto) pamoja na Othman Michuzi MTAA KWA MTAA BLOG chini ya Michuzi Media Group, mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha Mezani, kilichokuwa kikijadili swala zima la Muswada wa Sheria za Makosa ya Mtandao 2015, kilichoruka hewani mapema leo asubuhi.Alieketi ni Johnbosco Kamili wa EFM.

Kampuni ya TTCL yatoa msaada kituo cha watoto yatima Chamazi

$
0
0
Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka. Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka.Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa kwa mmoja wa walezi wa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'. Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa kwa mmoja wa walezi wa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'.Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'. Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'. Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund.
Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakiteremsha sehemu ya msaada uliyotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka. Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakiteremsha sehemu ya msaada uliyotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka.Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka. Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka.Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'. Kushoto ni MKuu wa Kituo hicho, Wilfrida Lubanza. Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'. Kushoto ni MKuu wa Kituo hicho, Wilfrida Lubanza.Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka. Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya PasakaPicha ya pamoja na watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi baada ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kukakabidhi sehemu ya msaada kwa watoto hao jana jijini Dar es Salaam. Picha ya pamoja na watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi baada ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kukakabidhi sehemu ya msaada kwa watoto hao jana jijini Dar es Salaam.


  Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa zawadi ya Siku Kuu ya Pasaka kwa kutoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa 'Yatima Group Trust Fund'. TTCL imekabidhi msaada huo wa mchele kilo 150, maharage kilo 100, unga sembe kilo 125, mafuta ya kula ndoo nne, maji katoni 25, juisi katoni 15 pamoja na chumvi mifuko 2 jana kituoni hapo na kupokelewa na MKuu wa Kituo hicho, Wilfrida Lubanza.

  Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, Meneja wa TTCL Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo aliziomba taasisi anuai na jamii kwa ujumla kuwakumbuka yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu hasa kipindi hiki cha siku kuu ambapo nao wangependa kufurahi pamoja. Alisema jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wengine waliopo katika mazingira hatarishi si kazi ya vituo vilivyojitolea au serikali tu bali kila mwanajamii hasa wale wenye uwezo. 

Alisema TTCL itaendelea kuyakumbuka makundi anuai yenye uhitaji kila ipatapo nafasi kwani hilo ni moja ya jukumu lao kurejesha sehemu kidogo kwa jamii kwa njia ya kusaidia popote, kwani wao ni sehemu ya jamii. "...Kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Kamugisha Kazaura na wafanyakazi wote napenda kutoa msaada huu wa vyakula kwa ajili ya kituo chako cha kulelea watoto yatima katika kuelekea katika sherehe za siku kuu ya Pasaka," alisema Matondo akikabidhi msaada huo. 

 Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Yatima Group Trust Fund, Lubanza aliishukuru TTCL kwa moyo huo wa kujitolea kwa kuwakumbuka watoto wanaolelewa katika kituo hicho hasa kipindi hiki cha siku kuu ya pasaka. Alisema wanafarijika sana wanapoona jamii na taasisi mbalimbali zikishiriki kuwasaidia watoto yatima na wengine walio katika mazingira hatarishi kwani ishara hiyo ni kuonesha kila mmoja anawajibika katika suala hilo ambalo ni changamoto kubwa nchini.

KIKUNDI CHA WANAWAKE CHA WOMEN WITH VISION WATOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA KATIKA MSIMU HUU WA PASAKA

$
0
0

Wanakikundi wa women with vision wakiongozwa na mwenyekiti wao Herieth Makombe  wakiwa katika kituo cha msimbaz centre walipofika na kutoa misaada ya baadhi ya mahitaji katika kuwakumbuka watoto yatima katika msimu huu wa sikukuu za pasaka .


Baadhi ya mahitaji ambao walitoa katika kituo cha msimbaz centre katika kuawajali watoto yatima wa vituo vya msimbaz centre na mburahati .


Baadhi ya wakinamama wa kikundi cha women with vision wakiwa katika picha ya pamoja na mlezi wa kituo cha watoto yatima Msimbazi centre wakati walipotembelea na kutoa  msaada wa baadhi ya mahitaji kwa ajili ya kuwafariji na kuwajali katika msimu huu wa sikukuu za pasaka ambapo walitoa msaada katika vituo viwili vya Msimbaz centre na Mburahati .

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAMWAGA MISAADA KWA VITUO SABA VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR

$
0
0

 Baadhi ya Vyakula mbalimbali vikishushwa kwenye gari kwa ajili ya kuvikabidhi vituo vya wataoto waishio katika mazingira magumu vipatavyo saba,msaada huo una thamani ya shilingi milioni sita.
 Bwa.Alex Msama akikabidhi msaada vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kwa Msimamizi wa kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa,Bi.Halima Ramadhan,kilichopo Boko jijini Dar.
Watoto wakipokea zawadi kutoka Kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd.Alex Msama
 
======== ========  =========

NA LOVENESS BERNARD.

Kampuni ya Msama Promotions imetoa msaaada wa vitu mbalimbali kwa vituo 7 vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Alex Msama alisema kuwa misaada hiyo ni sehemu ya mapato yatokanayo na Tamasha la Pasaka.

‘’Misaada hii ni mapato ya Tamasha la Pasaka mwaka jana  ,tumewapa watoto zawadi hizi ili washiriki vema katika kusheherekea sikukuu ya Pasaka na wajisikie kama watoto wengine’’, alisema Msama.

Kwa upande wake mmoja wa walezi wa vituo hivyo Honoratha Michael ambaye ni mlezi wa kituo cha Honoratha kilichopo Temeke, alisema kuwa anaishukuru  Kampuni ya Msama Promotions kwa kuwapa misaada hiyo wanaomba nawatu wengine wajitolee kuwasaidia.

‘’Tunamshukuru Msama na kampuni yake na hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuombea Baraka kutoka kwa Mungu baba pia tunawaomba watanzania wengine wajitolee kwani tunazo changamoto nyingi katika vituo vyetu’’alisema Honoratha.

Misaada hiyo iliyotolewa jijini Dar es Salaam imegharimu million sita imewanufaisha watotowa vituo vya Honoratha (Temeke),Malaika kids (Kinondoni),  Umra(Magomeni),Mwandaliwa( Boko), Zaidia (Sinza)na kituo cha Rahman kilichoko Magomeni. 

Taarifa kutoka Sikika kuhusu upotoshaji wa mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015

$
0
0
Naomba nifafanue kuhusu propaganda inayoenezwa na maafisa wa TCRA kupitia CloundsFM kuhusu Sikika na Mswada wa ‪#‎CyberCrimeBill‬.

Sikika haikuhudhuria mkutano wa wadau unaodaiwa kufanyika Dodoma kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na leo maafisa wa TCRA.

Sikika haikutoa maoni kuhusu Mswada wa miamala ya kielektoniki kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na pia leo maafisa wa TCRA.

Sikika ilituma maoni ya pamoja ya wadau kwa niaba ya wadau kuhusu #CyberCrimeBill kwa njia ya email kwa Mwenyekiti wa Kamati Mh Peter Serukamba.

Maoni hayo hayakutumika kuboresha #CyberCrimeBill bali kuongeza tu orodha ya wadau wanaodaiwa "kushiriki" kwa lengo la kuonesha kuridhia.

Kwa kuwa maoni ya wadau hayakuzingatiwa na kwamba ‪#‎CiberCrimeBill‬ iliyopitishwa ina mapungufu mengi, Sikika na wadau bado wanaipinga.

Mwisho tunaomba jina la Sikika lisiendelee kutumika kuhalalisha upitishwaji wa sheria hii.

Irenei Kiria
Mkurugenzi wa Sikika
4 Aprili 2015.

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA AFRIKA KUSINI REBECCA MALOPE AWASILI USIKU HUU KUTUMBUIZA KESHO TAMASHA LA PASAKA JIJINI DAR.

$
0
0

Happy Easter

Rais Kikwete atoa Mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow Wilson International Centre) tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC nchini Marekani. PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow Wilson International Centre) tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC nchini Marekani. 
Sehemu ya wahudhuliaji katika mhadhara huo wakimpigia makofi Rais Kikwete (hayupo pichani). 
Serikali ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia madarakani Mwaka 2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza Mkakati wa Maendeleo wa Mwaka  2025 (Tanzania Development Vision 2025) ambao  unalenga  kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye  uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow Wilson Centre.

 "Naamini mrithi wangu atayaendeleza na kujifunza kutokana na mafanikio haya na kuendeleza kutoka pale tutakapoachia" Rais amesema na kuongeza kuwa pia anatarajia kuwa Tanzania itakuwa na sera na sheria ya kusimamia Gesi na mapato yake kwa vile inatarajiwa kuanza kupatikana ifikapo Mwaka 2020. 

Katika mhadhara huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Mabalozi, wasomi na viongozi wa taasisi hiyo, Rais  Kikwete ameelezea mafanikio na changamoto katika uongozi wake wa miaka 10 katika elimu, siasa, uchumi na maendeleo ya jamii. 

 "Najivunia kuweza kuendelea kuliweka Taifa katika hali ya Umoja pamoja na changamoto zote, tumepambana na vitisho pale vilipojitokeza na pia tumetoa mchango mkubwa katika harakati za kisiasa zilizopelekea vyama viwili kutiliana saini maridhiano na kupata muafaka Mwaka 2010". 

 Rais ameelezea na kuongeza kuwa makubaliano hayo yalipelekea Zanzibar kufanya uchaguzi kwa amani na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina ya vyama vya CCM na CUF. "Natumaini tutafanya uchaguzi huru, haki na amani ili niweze kumkabidhi Urais mrithi wangu katika hali ya utulivu" Rais ameongeza.

 Imetolewa na; 

 Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Washington DC - Marekani4 Aprili, 2015.

MAMA TUNU PINDA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

$
0
0
Spika wa Bunge Anne Makinda akimpa pole mke wa Waziri Mkuu,  Mama Tunu Pinda  (kulia) ambaye alifiwa na baba yake Mzazi, Mzee Abdallah Rehani , Nyumbani kwa marehemu,Tabata  jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015 . Wengine pichani ni ndugu wa karibu wa Mama Pinda.2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, DR. Wilbroad Slaa katika mazishi ya babamkwe wake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015..  Kushoto ni Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sjharif Hamad.3
Waombolezaji wakisoma dua ya kumwombea marehemu Abdallah Rehani, Baba Mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, nyumbani kwa Marehemu, Tabata jijini Dar es sAlaam Aprili 4, 2015.4
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Seif Sharif Hamad (katikati) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi katika mazishi ya Baba mkwe wake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Segerea Jijini Dar es salaam Aprili 4, 20155
Waombolezaji wakizika mwili wa baba mzazi wa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda , Marehemu  Abdallah Rehani kwenye  Makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam, Aprili 4, 2015.
6
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda    akishiriki katika  mazishi ya Baba  Mkwe wake , Marehemu Abdallah Rehani kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili  4, 2015.
7
Makamu wa Kwanza  wa Rais wa Zanzibar,  Seif  Sharif Hamad  akishiriki katika  mazishi ya Baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Marehemu Abdallah Rehani kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili  4, 2015.
8
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi  akishiriki katika  mazishi ya Baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Marehemu Abdallah Rehani kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili  4, 2015.
9
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr. Wilbroad Slaa akishiriki katika mazishi ya    baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Marehemu Abdallah Rehani yaliyofanyika kwenye makaburi ya  Segerea jijini Dar es salaam Aorili 4
10
Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali walioshirikikatika mazishi ya Baba Mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Marehemu Abdallah Rehani yaliyofanyika kwenye  makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015.
11
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanziba Seif Sharif Hamad wakitoka kwenye eneo la makaburi ya Segerea jijini Dar es slaam baada ya mazishi ya baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Marehemu Abdallah Rehani Aprili 4, 2015. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mstaafu, Frederick Sumaye na  na mwenye koti jeusi katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi.

Wafanyakazi wa Benki ya CBA washerehekea pasaka na watoto yatima

$
0
0

Benki ya Commercial Bank of Africa (CBA) leo imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Msimbazi kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wafanyakazi hao walishiriki kulea na kucheza na  watoto hao ikiwa ni njia ya kuwaonyesha upendo.

Akizungumza kituoni hapo Meneja wa benki hiyo wa tawi la Nyerere ,Nuru Mwangulangu,ambaye aliongoza wafanyakazi wenzake waliofika kituoni hapo alisema wamefanya hivyo kama sehemu ya utaratibu wao wa kuchangia makundi yenye mahitaji maalumu kwenye jamii hususani watoto ambao ndio tunaamini wanapaswa kuandaliwa vizuri na kupata mahitaji muhimu na haki wanazostahili kwa kuwa ndio taifa la kesho.

“CBA leo tumekuja kuwaona vijana, kufurahi nao,na kuwapatia zawadi ili kuwawezesha kufurahia sikukuu ya Pasaka kama watoto wengine waliopo majumbani.watoto kama hawa wanahitaji upendo,faraja na kupatiwa misaada mbalimbali ya kuwawezesha kujisikia kuwa nao ni sehemu ya jamii na kusaidia jamii ni sehemu ya sera yetu ndio maana tumekuwa tukisaidia jamii katika Nyanja mbalimbali hususani elimu na afya”.Alisema Mwangulangu.

Pia alisema kufika kwao wameweza  kuangalia mazingira, kufahamu changamoto zinazowakabili walezi wa kituo hicho na kuona wapi benki inaweza kusaidia katika siku za usoni na aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia kutoa msaada na kutumia muda wao kusaidia makundi mbalimbali yenye mahitaji kwenye jamii.


Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa kituo hicho,Sista Ana Marandu,aliwashukuru wafanyanyakazi wa benki hiyo kwa kutoa msaada wa chakula ,nguo,kuwafungia watoto michezo ya burudani na kutumia muda wao kucheza nao. “Tunatoa shukrani kwa upendo mkubwa mlioonyesha siku hii ya leo na tunawaomba siku zote mtupe ushirikiano kama huu”.Alisema Sista Marandu.

WAZIRI MEMBE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE KUHIMIZA VIJANA WAIPENDE DINI KUDUMISHA AMANI NCHINI

$
0
0
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akionyesha tuzo yake mbele ya umati wa watu (hawapo pichani),aliyotunukiwa kwa mchango wake mkubwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii,katika tamasha la pasaka.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea katika tamasha la 15 la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. Pembeni ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa rai kwa viongozi wa dini zote pamoja serikali kuhimiza vijana waipende dini ili kudumisha amani, utulivu na uadilifu.Mhe Membe amesema hayo wakati akihubutubi maelfu ya watu waliohudhuria Tamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.

Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba  amempongeza Mhe Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka.Katika Tamasha hilo la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions, ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo, wamemtunuku Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika kukuza tasnia ya Sanaa nchini.

Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.Tuzo zimetolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa michango yao katika kutangaza Tamasha la Pasaka.

Viongozi wa Serikali waliohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Mhe. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.Tamasha hilo lilihudhuriwa na viongozi wa kidini wakiwemo, Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly na Mchungaji Mwasota.

Tamasha la Pasaka lilianzishwa rasmi mwaka 2000 na huwashirikisha Waimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini na nje ya nchi ambapo mwaka huu limewashirikisha waimbaji kutoka hapa nchini, Afrika Kusini, Uingereza  na Zambia.
 Mwanamuziki wa Kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca Malope akicheza na shabiki wake kwa staili ya pekee kabisa,huku uwanja ukilipukwa na mayowe kila kona.
 Mwimbaji nguli wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini, Mchungaji Solly Mahlangu pichani kulia akiwa na skwadi lake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja  katika lamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
 Mdau wa muziki wa Injili Emmanuel Mbasha akipa kitu cha Selfie na rafiki yake ndani ya uwanja wa Taifa wakati wa tamasha Pasaka lililofanyika April 5 jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.
 Kwaya ya Kijitonyama wakiimba katika tamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
  Sehemu ya umati wa Watu waliohudhuria tamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na mkewe wakimkaribisha jukwaani Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe pichani kulia ni Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly.

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images