Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 496 | 497 | (Page 498) | 499 | 500 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Sadolin bwana Pramod K. Tiwari(katikati)akimkabidhi mfano wa funguo mshindi wa kwanza wa promosheni ya Kwangua Ushinde bwana Abdul-aziz Massawe(46) mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam(kushoto)mara baada ya kujishindia pikipiki aliyokabiddhiwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia ni Mwakilishi wa mauzo wa kampuni hiyo kutoka Temeke bwana Mohamed Kibinda(wakwanza kulia). 
   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Sadolin bwana Pramod K. Tiwari(kulia)akimkabidhi mfano wa funguo mshindi wa kwanza wa promosheni ya Kwangua Ushinde bwana Abdul-aziz Massawe(46) mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam(kushoto)mara baada ya kujishindia pikipiki aliyokabiddhiwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
   Bwana Abdul-aziz Massawe(46) ambaye ni mshindi wa kwanza wa promosheni ya Kwangua Ushinde  inayoendeshwa na Kampuni ya rangi ya Sadolin akiwa mwenye furaha mara baada ya kukabidhiwa pikipiki yake jijini Dar es Salaam.

  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuvuta waya wa umeme kwenye mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Kirongo Samanga ikiwa sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji ikiwa sehemu ya uzinduzi wa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Kahe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Lembris Marangushi Kipuyo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi. Petronila Jakob kama ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma ya maji katika kijiji cha Kahe.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya namna uzalishaji unavyofanyika kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kutengeneza vinywaji ya Bellaview Fresh Fruits Processing Industry Ndugu Shanel John Ngowi.Kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tarakea wilayani Rombo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Tarakea Polisi.

  Katibu Mkuu wa CCM anaendelea na ziara za kujenga na kuimarisha Chama mkoani Kilimanjaro pamoja na kukagua, kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010. Katika ziara yake ya leo wilayani Rombo ,Katibu Mkuu alishiriki shughuli mbali mbali ,zikiwemo kufungua ofisi ya chama ya wilaya, kukabidhi Bima ya afya kwa vijana 900 wa boda boda,Kukabidhi mikataba na hundi ya vikundi 2o vya wanawake wajasiriamali. 
   Wakazi wa Tarakea wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya polisi Tarakea.
  Pichani kushoto ni aliyekuwa Katibu Mwenezi na Katibu wa Mbunge wa CHADEMA,wilaya ya Rombo John Tarimo akitangaza rasmi kurejea chama cha CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimsikiliza.
   Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wakirejesha kadi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo.


  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

  0 0

  unnamed222Na. Johary Kachwamba – MAELEZO, DODOMA
  …………………………………..
  Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetangaza ugunduzi wa gesi asilia katika Miamba ya Mchanga kwenye kisima kinachochimbwa na Statoil cha Mdalasini-1 kwenye bahari kuu ya Tanzania.

  Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene amebainisha hayo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma. Baada ya kuthibitishwa na Makamu wa Rais wa Statoil, Nick Maden pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

  “ugunduzi huo wa gesi asilia wa futi za ujazo trilioni 1.0-1.8, unaongeza kiwango cha gesi asilia iliyopatikana kwenye kitalu namba 2 kufikia futi za ujazo trilioni 22. Kisima cha Mdalasini -1 kimechimbwa katika urefu wa mita za maji ya bahari 2,296 kusini mwa kitalu namba 2” alisema Mhe. Simbachawene.

  “kuanzia mwanzo wa uchimbaji, Februari 2012, tumechimba visima 13 na tumefanya ugunduzi katika visima 8 ikiwemo Mdalasini-1. Bado tunaona uwezekano wa gesi zaidi katika eneo la Kitalu namba 2” aliongezea Mhe. Simbachawene.

  Statoil ni Mkandalasi katika Leseni ya Utafutaji ya Kitalu namba 2 kwa niaba ya TPDC na inayohisa ya asilimia 65% na mshirika wake ExxonMobil and Production Tanzania Limited inazo hisa asilimia 35%.
  Wakati wa uendeshaji baada ya Serikali kutoa Leseni ya uzalishaji, TPDC kulingana na mkataba inaweza kushiriki katika uendeshaji na uzalishaji kwa kutwaa asilimia 10% ya uwekezaji.

  0 0

   Sehemu ya umati wa wanachama wa VIKOBA mkoa wa Arusha wakifuatilia kwa makini Kongamano la Vikoba lililofanyika katika ukumbi wa Olasiti garden na kudhaminiwa Mfuko wa Taifa wa  bima ya Afya  (NHIF).Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni "Vikoba Chachu ya Maendeleo ya Kweli".
  Maafisa kutoka Mfuko wa Taifa wa  bima ya Afya  (NHIF)wakifuatilia kwa makini Kongamano la Vikoba lililofanyika katika ukumbi wa Olasiti garden na kudhaminiwa Mfukohuo.Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni "Vikoba Chachu ya Maendeleo ya Kweli".Picha na woinde shizza

  0 0

  Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Harrison Mwakyembe akihutubia wajumbe wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaofanyika Mjini Addis Ababa –Ethiopia.
  Naibu Katibu Mkuu –Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nd. Armantius C.Msole (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua wakifuatilia hotuba ya Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr.Harrison Mwakyembe (Hayupo pichani) katika Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango wa Afrika unaofanyika Mjini Addis ababa – Ethiopia.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua akipata maelezo kuhusu utaratibu wa Mkutano kutoka kwa kamishina msaidizi wa Fedha za nje Bi.Judica Omari baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaoendelea Mjini Addis Ababa – Ethiopia. Katikati ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr.Albina Chuwa.

  0 0


  Mwenyekiti wa TUICO mkoa wa Kilimanjaro,Renatus Chimola akizungumza mara baada ya uchaguzi kukamilika.
  Mwenyekiti mpya wa Chama cha Wafanyakazi TUICO tawi la MUWSA ,Maulid Barie akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo.
  Viongozi na wananchma wa Chama cha Wafanyakazi TUICO tawi la MUWSA wakiimba wimbo wa Solidarity.
  Viongozi wapya wa Chama cha Wafanyakazi (TUICO) tawi la MUWSA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuchaguliwa kuongoza tawi hilo kwa kipindi cha miaka mitano.   Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  Baadhi ya wanachama wakijiandaa kwa ajili ya kuchagua viongozi wa TUICO,tawi la MUWSA.

  Mwenyekiti wa TUICO mkoa wa Kilimanjaro,Renatus Chimola akikusanya kura kwa nafasi ya Uenyekiti.
  Wanachama wakisikiliza sera toka kwa wagombea.
  Baadhi ya wanachama wakijinadi mbele ya wanachama wa TUICO tawi la MUWSA ,kuomba ridhaa ya kuingoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
  Mmoja wa wagombea wa nafasi ya Ujumbe wa kamati ya utendaji ya TUICO tawi la MUWSA ,Esther Massawe akiomba kura wakati wa uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo.
  Kamati ya Uchaguzi wa Viongozi wa TUICO tawi la MWSA wakiendelea na zoezi la kuhesabu kura.
  Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa Viongozi wa TUICO,tawi la MUWSA ,Rashid Nachan akitangaza matokeo .
  Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira MUWSA ambao ni wanachama wa TUICO wakifurahia mara baada ya kutangazwa kwa washindi.

  0 0


  AMI Hospital or Trauma Center at Msasani Dar es Salaam is facing imminent closure after it failed to comply by Tanzania Court of Appeal order that wanted it to deposit in court USD 1,514,000 plus a monthly rent to a tune of USD 64,000 per month following a tenancy agreement dispute.

  A panel of three Court of Appeal judges, Justices Mbarouk Mbarouk, Salum Massati and Katherine Oriyo ordered African Medical Investments (T) Ltd (AMAI) to make the deposits a month after the ruling which was issued on the 12th day of February 2015, an order that has not been honored. 

  The court made their ruling on civil application No. 185 of 2014 filed by AMI in protest against execution of a ruling on main commercial suit No. 104 of 2013 that it lost to its Landlord (local business man Navtej Singh Bains) in respect of a building where the company is conducting its business.

  AMI Hospital had lost the case filed by the landlord for failure to pay rent for the past 26 months in a legal battle at the Tanzania Commercial Court in November 2014 and were issued with a Notice for Eviction by the landlord.
  AMI subsequently filed for Bankruptcy protection to the High Court of Tanzania last Friday stating that it was operating insolvently having incurred losses for the past two years.

  AMI Plc Chief Executive Officer (CEO), Mr Theunis Peter Botha, also a Director and CEO of the local AMI Hospital in Tanzania, filed the Bankruptcy application in the High Court of Tanzania.

   AMI Tanzania is wholly owned by its London Company AMI Plc which was kicked out of the London Stock Exchange in February 2014 for trying to sell its assets in Maputo without shareholder disclosure.

  Through a notice released last week on Wednesday (25th March), Mr Lawrence Ochola, a Kenyan National working as Hospital Accountant, appealed for all stakeholders to stay cool and that AMI Hospital is operating normally.

  “The management of AMI hospital –Dar es Salaam wishes to take this opportunity to acknowledge to its various stakeholders that we are aware of their fears and concerns that have been elicited by news that appeared in a section of local media to the effect that AMI has filed for bankruptcy.

  In a bankruptcy petition filed last week before the High Court's Main Registry, the company alleges that it has been incurring losses in terms of billions to the extent of having several outstanding liabilities and debts which are now exceeding its ability to pay to different creditors.

  "The petitioner (AMI) incurred a net loss of 1.146 million US dollars in the year ended February 28, 2013, while in the year ended February 28, 2014, the petitioner incurred a net loss of 775,000 US dollars," reads a section of the petition document.

  It is stated that the company was also required to pay outstanding dues to institutes, notably the National Social Security Fund (NSSF) and the Tanzania Revenue Authority (TRA) and individuals.

  According to the petition, given the value of the assets of the company and the amount of money owed to it by creditors, there was no way it would be able to raise enough funds for paying them as well as meeting her obligations.  

  There are also records showing that Lancet Laboratory (T) Ltd filed for an urgent application against AMI Hospital eviction claiming over TSh 150m owed to them by AMI Hospital.

  Inside information has it that several creditors are now in a limbo as the Hospital owes over $4m to them including the biggest creditor being the Landlord Mr N Bains, Doctors, Staff, TRA, Pharmaceutical suppliers and other suppliers.

  Learned counsel Dilip Kesaria, who represented the Landlord, asked the court to issue a final notice of eviction which has been outstanding since September 2014 against AMI Hospital.


  0 0

  IMG_8866
  Watangazaj wa kituo cha Radio 5 wakimkabidhi dereva wa daladala ya via samunge stendi ya daladala Bw, Juma Ramadhani kapu  la zawadi za pasaka baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa kuwa msikilizaji wa kituo hicho katika gari lake.,Kulia ni Wilfredy ,Hilda Kinabo na kushoto Mkuu wa vipindi vya Radio5  Mathew Phillip zoezi hilo lilifanyika leo jijini Arusha(Habari Picha na http://jamiiblog.co.tz)
  IMG_8870
  Hapa Bw.Juma Ramadhani akifanyiwa mahojiano na watangazaji wa kituo cha Radio 5 leo jijini Arusha
  IMG_8907
  Mama Hadija wa Unga  LTD jijini Arusha akiwa anaangalia zawadi la kapu baadaya kuibuka mshindi kwa kusikiliza Radio 5 kipindi cha taarifa ya habari na matukio,pembeni ni watoto wakiwa wanashuhudia zawadi hizo
  IMG_8909 
  Watangazaji wa kituo cha  Radio 5 wakamkabidhi mshindhi wa pili mama Hadija wa Unga LTD  kapu la zawadi baadaya kuibuka mshindi kwa kusikiliza Radio 5 kipindi cha taarifa ya habari na matukio.
  IMG_8926
  Kulia ni Hilda Kinabo,kushoto Wilfredy watangazaji mahiri wa kituo cha Radio 5 wakimkabidhi mama Ruthi Sumary mkazi wa Sokon 1 zawadi ya Pasaka
  IMG_8928
  Watangazaji wa kituo cha Radio 5 wakimkabidhi mshindi wa 3 mama Ruthi Sumary mkazi wa Sokon 1 Kapu la zawadi ya Pasaka baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kusikiliza kipindi cha mkasa,kulia ni Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo 
  IMG_8938
  Watangazaji wa Radio 5 wakimkabidhi mshindi wa 3 Bwana Paskal Raimond Wenga kutoka Olorien Kijenge Kapu la zawadi  ya pasaka baada ya kuibuka kuwa mshindi kwa kusikiliza vipindi vyote vya Radio 5,

  0 0

   2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki, waratibu wa mkutano Mkuu wa Sita wa majadiliano ya kukuza maendeleo endelevu ya mifumo ya Elimu ya Juu na Maendeleo ya Kiuchumi. Mkutano huo ulifunguliwa leo Machi 31, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  1
  Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua rasmi mkutano Mkuu wa Sita wa majadiliano wa Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) wenye lengo la kukuza maendeleo endelevu ya mifumo ya Elimu ya Juu na Maendeleo ya Kiuchumi, uliofanyika leo Machi 31, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  34
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo.
  6
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, baada ya kuufungua ramsi, leo Machi 31, 2015.
  5
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo baada ya kufunguliwa rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

  0 0

  Meneja ukuzaji biashara na Masoko wa Selcom Tanzania, Juma Mgori kushoto akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya uzinduzi wa promosheni ya ‘Shinda na Selcom’ inayomwezesha mtumiaji wa huduma za kampuni hiyo kujishindia Tsh 100,000 ambapo washindi kumi watajishindia kitita hicho kila wiki na shindano hilo litadumu hadi mei 31 kulia ni Meneja Miradi wa Kampuni hiyo Gallus Runyeta
  Meneja ukuzaji biashara na Masoko wa Selcom Tanzania, Juma Mgori kushoto akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi
   wa promosheni ya ‘Shinda na Selcom’ inayomwezesha mtumiaji wa huduma za kampuni hiyo kujishindia Tsh 100,000 ambapo washindi kumi watajishindia kitita hicho kila wiki na shindano hilo litadumu hadi mei 31 katikati ni Meneja Miradi wa Kampuni hiyo Gallus Runyeta na Meneja wa huduma za Ziada ‘VAS’, Chia Ngahyoma
  Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom Gallus Runyeta kushoto akimwelekeza Meneja ukuzaji biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Juma Mgori jinsi shindano linavyo endelea katika mtandao

  0 0

   Maaskofu na wachungaji wa makanisa ya kipentekosti wakiingia ukumbini katika Hoteli ya Tamari iliyopo Mwenge tayari kwa kutoa tamko lao.
  Katibu wa Maaskofu wa makanisa ya Kipentekosti Dk. Damas Mukassa akisoma tamko la maaskofu hao Dar es Salaam jana, kuhusu sakata la kukamatwa kwa Askofu wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ambalo leo hii wanatarajia kwenda kumuona Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Mangu kuzungumzia suala hilo. Kulia ni Askofu Dk.Mgullu Kilimba na Askofu Mwaviga Mwafululila.
   Askofu Dk. Paul Shemsanga akizungumza katika mkutano huo ambapo maaskofu hao walitoa tamko lao.
   Wachungaji mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
   Wachungaji mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.


   Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo.
   Baadhi ya maaskofu wakiwa kwenye mkutano huo.

  Mpiga picha wa gazeti la Mtanzania, Hamphrey Shao akipiga picha katika mkutano huo.
   Na Dotto Mwaibale MAASKOFU wa makanisa mbalimbali ya Kipentekoste nchini wamesema wanatarajia kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ili kulimaliza sakata la Askofu Josephat Gwajima, kwani kuliendeleza ni kuleta mpasuko wa kidini katika jamii.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Maaskofu hao, Askofu Dk. Damas Mukassa alisema hakuna sababu ya jambo hilo kukuzwa, kwani mhusika amemsamehe Askofu Gwajima.
  Dk. Mukassa alisema ni vema Serikali na vyombo vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi, kwani yanaweza kusababisha chuki baina yao.
  “Tunaomba Serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu, na busara itumike ili kuepusha uvunjifu wa amani katika jamii,” alisema Mukassa.
  Katibu huyo alisema wanasikitishwa kukamatwa kwa wasaidizi wa Gwajima, kwa kisinginzio kuwa, walitaka kumtorosha, jambo ambalo haliwezekani.
  Alisema wamekaa na kutafakari kilichomkuta Askofu Gwajima, kwani kiuhalisia afya yake ilikuwa salama, hivyo wamebaki na shaka, kama vyombo vya usalama si sehemu salama kama zamani.
  Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwajima aliyelazwa katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam amejitokeza hadharani na kusema kuwa, hakuna njama  ya yeye kutoroshwa na wachungaji wake na amekiri kuwa, bastola iliyokutwa katika begi ni yake na anaimiliki kihalali.
  Alisema iwapo angekuwa na lengo la kutoroka nchini angeondokea Arusha, ambapo alikuwepo, lakini aliamua kuitikia mwito wa jeshi la Polisi na kurejea Dar es Salaam.
  Askofu Gwajima alisema baada ya wachungaji wake kupata taarifa  ya kuwa, amefariki ndipo walikwenda kumwona na kumpelekea silaha hiyo ili aweze kujilinda.
  “Kwa kuwa, palikuwa na mpango huo nikawaambia wachungaji wangu waende nyumbani kwangu na kuchukua begi lililokuwa chumbani, ambapo ndani yake palikuwa na baadhi ya nguo na bastola  ninayoimiliki kihalali, kwani humo ndani kulikuwa na nyaraka zilizokuwa zikionesha umiliki na vitu vingine,” alisema Gwajima.
  Alisema alishangaa kuona Askari wakiwavamia wachungaji wake na  kuwafikisha kituoni kwa kosa la kutaka kumtorosha, jambo ambalo si la kweli.
  Gwajima alisema walipofika hospitalini usiku, wachungaji wake walimfikishia begi na kuliweka ndani ya chumba, lakini walitokea watu ambao walijitambulisha kuwa, ni askari na kuomba mzigo ulioingizwa ndani na hapakuwa na ushindani akawapa.
  Kuhusu kuzimia kwake, alitoa taarifa ya kusumbuliwa na kichwa kwa muda mrefu bila ya kusikilizwa ili apatiwe huduma, ambapo kilichotokea ndiyo hicho walichokiona.
  Gwajima alisema alikuwa akihojiwa na Kamanda wa Upelelezi wa Kanda (ZCO), ambapo aliendelea kumhoji huku akimpa taarifa ya kuumwa kichwa, lakini hakumsikiliza, hivyo mpaka anaanguka na kuzimia hakujua kilichoendelea hadi alipofikishwa hospitalini.
  Askofu Gwajima alisema hana mgogoro wowote na Askofu mwenzake na anampenda, kilichotokea alikuwa katika kazi yake ya kukemea aliyoyasema.
  Kwa upande, Dk. Willibrod Slaa, mara baada ya kumtembelea Askofu Gwajima hospitalini hapo, alisema haingilii ugomvi wa Askofu Pengo na Gwajima, bali anachokipinga ni upotoshaji unaofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia.
  Dk. Slaa alisema polisi waache maneno yao ya kusema mtu anajifanya anaumwa, kwani ni kitendo ambacho kinaonesha kuwa, halithamini utu wa mtu.
  Aidha, alisema mambo anayofanyiwa Askofu Gwajima hata yeye aliwahi kufanyiwa akiwa Arusha, baada ya umma kupotoshwa kuwa, alikamatwa na silaha kana kwamba yeye ni jambazi.
  “Nilikamatwa na jeshi la polisi huko Arusha, ambapo kisheria unapokuwa na silaha unaisalimisha, nilifanya hivyo na nikaambiwa nijisajili, lakini siku iliyofuata taarifa ikatolewa kuwa, nimekamatwa na silaha, hivyo inaonesha jinsi gani jeshi la polisi linavyofanya hila kwa raia,” alisema.
  Dk. Slaa alisema mahakama ndiyo itakayotoa ukweli wa jambo hilo kama ilivyotokea katika kesi ya ugaidi dhidi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati fulani.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba alisema kinachoonekana kwa sasa ni ukiukwaji wa haki za binadamu ambao unaendelea kufanywa kwa vyombo vya usalama.
  Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema anatarajia kufanya mazungumzo na Askofu Gwajima kutokana na kauli yake ili kujua nini kilimsukuma kutoa kauli hiyo.
  Akizungumzia sakata hilo la kukutwa na silaha na kuendelea kuwashikilia wachungaji na wafuasi wa Gwajima, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema silaha hiyo haimilikiwi kihalali na Gwajima.
  Kova
  Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa, silaha zilizokamatwa hospitalini katika njama za kumtorosha Mchungaji Josephat  Gwajima hazimilikiwi kihalali.
  Aidha, jeshi hilo lilisema kuwa, linaendelea na upelelezi wa watu 15 waliohusika na tukio la kufanya njama za kutaka kumtorosha Gwajima na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
  Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova alisema wanafanya uchunguzi ili kujua kwanini walikula njama na mbinu gani walitumia.
  Alisema silaha hiyo ambayo ni bastola aina ya Berreta yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu iliyokamatwa juzi, imebainika kuwa, inamilikiwa kinyume cha sheria na wamiliki si halali.
  “Silaha zilizokamatwa hazimilikiwi kihalali na wahusika akiwemo Gwajima, hawamiliki kihalali, hivyo kuna kesi ya kupatikana na silaha, ambapo ni kinyume cha sheria.”
  “Pale ambapo tutagundua kuwa, kuna makosa yaliyotajwa atachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema.
  Alisema kuhusu ni kwanini alipata mshtuko kuhusu suala hilo litajulikana na daktari kwa kushirikiana na mahakama.
  Kamishna Kova aliongeza kuwa, upelelezi utakapokamilika na wakili wa Serikali akikubali,  washtakiwa hao watafikishwa mahakamani.
  Wakati huohuo, Methusela Gwajima ambaye ni Mwanafamilia amekemea vikali kitendo cha kutukanwa kwa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na kwamba ni kinyume cha sheria.
  Alisema kitendo hicho ni cha fedheha, ni kinyume cha sheria ya nchi na kwamba, alitakiwa kumfuata na kumweleza na si kumtukana matusi makubwa na kumsababishia aibu kubwa.
  Aliongeza, Gwajima abebe msalaba wake mwenyewe kwa kwenda kuomba msamaha, kwani aliamua kumchafua kiongozi huyo wa kiroho, na kwamba itamsaidia kurudisha heshima ya mwanzo aliyokuwa nayo. 

  0 0

  Faraja Nyalandu - Executive Director of Shule Direct speaking on entrepreneurship and its' challenges in Tanzania and promoting self employment during the Innovation week organised by Human Development innovation Fund (HDIF) in Dar es Salaam earlier this week. From left Benedict Tesha - Founder of Jamaa Technology, Nisha Ligon - CEO of Ubongo Limited, Taha Jiwaji - CEO of Bongo Live and Co Founder of KINU.
  Benedict Tesha - Founder of Jamaa Technology speaking on entrepreneurship and its' challenges in Tanzania and promoting self employment during the Innovation week organised by Human Development innovation Fund (HDIF) in Dar es Salaam earlier this week. From left Nisha Ligon - CEO of Ubongo Limited, Taha Jiwaji - CEO of Bongo Live and Co Founder of KINU and Faraja Nyalandu, Executive Director of Shule Direct.
  Dr Jacqueline Thomas, senior Scientist at Ifakara Health Institute (IHI) speaks about the Kigamboni sludge treatment plant during the Innovation Week that was organised by Human Development Innovation Fund earlier this week in Dar es Salaam.
  Mr. David McGinty, Team Leader of Human Development Innovation Fund ( HDIF) speaks during the innovation week that was held at Nafasi Art Space in Dar es Salaam.
  Andrew Mahiga, Managing Director at Maanisha! speaks on Innovation during the Innovation that was held at Nafasi Art Space earlier this week in Dar es Salaam. To the left Gadi Ramadhani ( An artist), Paul Ndunguru ( An artist at Alama) and to the far right is David McGinty, Team Leader at Human Development Innovation Fund ( HDIF)
  David McGinty, Team Leader at Human Development Innovation Fund (HDIF) creating an object with match sticks and a match box that was an exercise during the innovation week held at the Nafasi Art Space earlier this week.
  ---
  The Human Development Innovation Fund (HDIF) convenes entrepreneurs, researchers, academics, creatives & development professionals to collaborate and create social impact through innovation.
  Last week, HDIFcollaborated with BUNI Innovation Hub, KINU Innovation Hub, DFID, World Bank, Commission for Science and Technology (COSTECH), Deloitte and Nafasi Art Space to curate a series of interactive events, exploring innovation in research, development, entrepreneurship, technology and the arts. Individuals and organizations shared their insights on innovation respective to their field of expertise for audiences and collaborators from across sectors. This inaugural Innovation Week was designed to catalyze on the innovation process in Tanzania and provide inspiration and connections to individuals and organizations on innovation.
  HDIF challenges Tanzanians to implement and scale innovative ideas for more positive sustainable development impact and remove barriers to reach innovation.Over 500 Tanzanians participated in the week-long events that offered interactive seminars, workshops and trainings. David McGinty, HDIF Team Leader commented, ‘We wanted to inspire the current and future leaders in Tanzania to take risks on new ideas, collaborate across sectors, and transform Tanzania through the scaling of innovation.’ He explained ‘Strengthening Tanzania in innovation is a way to create growth, raise the global profile of Tanzania, and tackleTanzania’s social and economic challenges.’
  Dr. Donath Olomi, Partner of Tanzania Renewable Energy Business Hub was a panelist during the week. He said ‘I have been genuinely surprised at the attendance throughout this innovation week. It is clear that Tanzanians believe they have potential innovative ideas and are looking for partners, be it in the private or public sector, that can nurture and support their ideas as they develop.’ He added ‘Events like these will help stimulate cross-sector collaborationsin Tanzania to innovate and find profitable ways of addressing key issues in Tanzania.’
  Tanzania ranks 123 out of 143 countries according to the Global Innovation Index 2014. Despite its many endowments, Tanzania remains a poor country by both local and international standards. A mapping study conducted by Sosthenes Sambua, Executive Director of Tanzania Entrepreneurship and Competiveness Center (TECC)indicated that the lack of competitiveness in Tanzania is attributed to three factors. The first is lack of innovation policy comprehensive enough to catalyze innovation system in the country. The second factor is lack of linkages between industry, academia and government. The third factor is inadequate funding available to commercialize innovative ideas. Mr. Sambuasays‘Platforms like the Innovation Week that bring together policy makers, private sector actors &entrepreneurs from across all sectors, creates dialogue that will help lead to new orimproved policies that will catalyze the innovation system in Tanzania.’
  HDIF was launched to fund innovative and sustainable solutions to create social impact in education, health and WASH (water, sanitation and hygiene) across Tanzania. The second funding round is scheduled for mid-2015. Guidelines and important dates will be posted on the HDIF website www.hdif-tz.org.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye ni Katibu wa Tume Bi. Agnes Mgeyekwa akitoa hotuba fupi katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi TUMESHERIA.
  2
  Mwenyekiti wa Tume Mh. Jaji Aloysius Mujulizi akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi
  3
  Wajumbe wa Baraza wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza.
  4
  Mwenyekiti wa TUGHE tawi la TUMESHERIA Bw. Fredy Kandonga akizungumza katika kikao cha Baraza.
  5
  Wajumbe wa Baraza wakiwa katika kikao hicho.
  6
  Katibu wa Kikoa cha Baraza Bi. Marlin Komba akitoa ufafanuzi wakati wa kikao cha Baraza.
  7
  Wajumbe wa Baraza pamoja na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Tume wakiimba wimbo wa Mshikamano katika kikao cha Baraza la wafanyakazi TUMESHERIA .

  0 0

  1
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (katikati) akiwasili katika Bandari ya Nchi Kavu ya TRH katika ziara ya wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo kontena mbili zilikamtwa ambapo moja ilikutwa na bidhaa za tv na nyingine biskuti huku nyingine mbili   hazikuweza kupatikana mahali zilipofichwa.
  2
  Kamishna Msaidizi wa Forodha wa Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bw. Tiagi Kabisi kushoto akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Road Haulage (TRH) Bw. Ali Lilani katika ziara ilifanywa na Waziri wa Fedha leo jijini Dar es Salaam.
  3
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (kushoto) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Kamishna Msaidizi wa Forodha wa Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bw. Tiagi Kabisi katika ziara ya wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo kontena mbili zilikamtwa ambapo moja ilikutwa na bidhaa za tv na nyingine biskuti huku nyingine mbili   hazikuweza kupatikana mahali zilipofichwa.
  4
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (katikati) akiangalia mbidhaa za tv zilizokutwa katika mojawapo ya kontena zilizokuwepo katika Bandari ya Nchi Kavu ya TRH katika ziara ya wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  5
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (katikati) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha (kulia) Mhe.Dkt.Servacius Likwelile na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo(kushoto) wakati wa ziara ya wizara hiyo katika Bandari ya nchi Kavu ya Tanzania Road Haulage(TRH) leo jijini Dar es Salaam.

  6
  Kontena mbili zenye bidhaa za Tv na Biskuti zilizokamatwa katika Bandari ya Nchi Kavu ya Tanzania Road Haulage (TRH) wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya leo jijini Dar es Salaam.
  ………………………………………………………………….
  Na Lorietha Laurence- Maelezo
  Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya amesema kuwa serikali itawashughulikia wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi kwa kuwachukulia hatua stahiki ikiwemo kunyang’anywa leseni ya biashara na kulipa faini.
  Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika ziara ya kukagua bandari kavu ya kampuni ya THR ambapo ni mjumuisho wa ziara iliyoanza jana jioni kutembelea Bandari za nchi kavu. 

  “Tumekamata jumla ya kontena nane ambazo katika taarifa za awali zilieleza kuwa zina bidhaa za gypsum powder na gysum plasta lakini tulipozifungua tumekutana na bidhaa tofauti na kile tulichoambiwa” alisema Mhe. Mkuya
  Aidha aliongeza kuwa bidhaa zilizokutwa katika kontena hizo ni pamoja na spea za pikipiki,vitenge ,Tv na biskuti ambazo zilitakiwa kulipia ushuru tofauti na zile ambazo ziliandikwa katika taarifa ya kupokea mzigo.

  Mhe. Mkuya alisema kutokana na udanganyifu huo takribani shilingi milioni mia tatu zimepotea na hiyo ni mojawapo ya vikwazo vinavyokwamisha shughuli za maendeleo kusonga mbele kwa ukosefu wa fedha.
  Naye Kamishana Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Tiagi Kabisi ameeleza kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali wakati wa utendaji wao wa kazi ikiwemo udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara ikiwemo hili la kutokulipwa kodi.

  “Hii ni mojawapo ya changamoto ambazo tunakutana nazo katika kazi zetu ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za udanyifu ili kukwepa kulipa kodi” alisema Bw.Kabisi
  Ziara hiyo ni mojawapo ya mikakati ya Wizara ya Fedha katika kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanawajibika katika suala la ulipaji wa kodi nia ni kuhakikisha nchi inaweza kujitegemea kupitia vyanzo mbalimbali vya uchumi ili kukuza na kuendeleza ustawi wa nchi.

  0 0

   
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.  
    Nyumba za gharama nafuu za NHC Mwongozo, Kigamboni Dar es Salaam zinavyoonekana leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea.  
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo ya Injinia wa NHC, Elisante Ulomi anayesimamia Mradi wa Mwongozo Housing Estate mchana wa leo. Mojawapo ya Nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada, Kigamboni Dar es Salaam inavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea.  
    Nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada, Kigamboni Dar es Salaam zinavyoonekana leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea.
   
    Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.  
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.  
    Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo.  
    Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea.  
    Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea.  
    Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri alipozitembelea. Nyumba ya mfano itakayojengwa katika kitalu nambari 300 kona ya kuelekea kwenye Hospitali ya Mikocheni jijini, Dar es Salaam leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya Nyumba ya mfano itakayojengwa katika kitalu nambari 300 kona ya kuelekea kwenye Hospitali ya Mikocheni jijini, Dar es Salaam leo. Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria kutoka kwa Mkurugeni wa Ubunifu wa NHC, Issack Peter alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Mmojawapo wa mafundi wajenzi wanaojenga nyumba hizo za Victoria akiwa kazini wakati wa ziara ya Waziri.

  0 0

  001002Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano  unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu  (Achieving sustainable development through employment creation and decent work) tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani. 
  003Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiondoka baada ya yeye kuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano  unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu  (Achieving sustainable development through employment creation and decent work) tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani.
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ukiwasili Moshi Mjini kutokea Wilaya ya Rombo kwa Ziara ya siku kumi  ndani ya mkoa wa Kilimanjaro.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wamekamilisha ziara yao ya miko mitatu ikiwemo Dodoma,Arusha na Kilimanjaro,Ziara hiyo ililenga Kuimarisha,kutekeleza na kuhimiza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ya CCM,ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Moshi mjini kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambia kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.
  wananchi wa Moshi mjini wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia,ambapo aliwaeleza kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.
  wananchi wa Moshi mjini wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela,wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye huku wameweka mikono kichwani kuashiria kuwa miaka 20 kwa upinzani jimbo la  Moshi mjini imetosha.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Moshi mjini mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambie wastuke sasa wasiendelee kukandamizwa na viongozi wasiojali maendeleo yao.
  Wakazi wa Moshi mjini wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia,ambapo aliwaeleza kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.
   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya Moshi mjini Ndugu Aggrey Marealle akihutubia wananchi wa Moshi mjini ambapo aliwaambia kuwa wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya kweli kwa kuchagua CCM kuongoza mji wa Moshi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatiza kwenye maji wakati akielekea kwenye eneo la mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa akina mama Lishe wa Njoro,Moshi mjini.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali baada ya kutembelea kikundi Vijana cha Kata ya Miembeni.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wanachama wa Vikoba kata ya Makongoroni ambapo alishiriki kuzindua vikoba 11 vyenye wanachama 330,Kata ya Makongoroni,Moshi mjini.
  Jengo la soko la kati Moshi mjini likiwa liemacha kama pagala baada ya wafanyabiashara wa soko hili kuondolewa na kuachwa kama lilivyo mpaka sasa
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa soko la kati ambalo limefungwa kwa mwaka mzima sasa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanya biashara ambao soko lao limefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye mabango na wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia vijana wa boda boda ,Stendi Kuu kata ya Mawenzi ambapo aliwaambia kuwa boda boda ni sehemu ya kupata kipato hivyo inabidi wafanye shughuli yao hiyo kwa umakini mkubwa ,ikiwa kudumisha umoja, kufuata sheria, kujisajiri na kutambulika na mamlaka husika ,kuaminika ili waweze kukopesheka.

  0 0

  AutoSueco is a subsidiary of Nors Group, the leading supplier of Trucks, Construction Equipment, Power Generators and Industrial Engines. Established since 1949 with HQ in Porto, Portugal; it has several brands worldwide.
  ……………………………………………………….
  AutoSueco Tanzania (Volvo) has appointed Alen Nkya as new Commercial Manager CE, a unit whose primary function is to run overall Construction Equipment business which also comprises of mining machines. He joins from April, this year.
  In a statement released today states that Mr. Nkya has over 10 years’ experience in the industry. Formerly a Sales Manager CE at Hyundai, he has an outstanding track record of achievements in Marketing, Business Development and Customer Relations.
  “I’m looking forward to this new challenge,” said Mr. Nkya. “Tanzania is one of the key markets with great potentials, so we must prosper in here and not just stay.”
  AutoSueco is a subsidiary of Nors Group, the leading supplier of Trucks, Construction Equipment, Power Generators and Industrial Engines. Established since 1949 with HQ in Porto, Portugal; it has several brands worldwide,

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Kushoto) na  Kaimu Katibu Mkuu  wa Wizara  ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) wakiingia kwenye  ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini unaoanza tarehe 01 hadi  tarehe 02, Aprili 2015 wenye lengo la kujadili mafanikio na changamoto  katika utendaji  kazi wa Wizara pamoja na taasisi zake.
  2
  Mwenyekiti  wa Chama cha Wafanyakazi wa  Afya na Serikali Kuu (TUGHE) Wizara  ya Nishati na Madini, Marcelina  Mshumbusi akisoma hotuba ya kumkaribisha  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava  (hayupo pichani) katika mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.

  3
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi  wa Wizara  ya Nishati na Madini  wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (hayupo pichani)
  4
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi  Ngosi  Mwihava (kulia)  akisoma hotuba ya kumkaribisha  Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa kwanza kushoto). Katikati ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
  5
  6
  Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini.
  8
  Baadhi  ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara  ya Nishati na Madini wakiimba wimbo wa kuonyesha mshikamano ujulikanao kwa jina  la “solidarity forever
  9
  Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Mhasibu Mkuu Mfawidhi wa Wizara  ya Nishati na Madini, Michael Marandu (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano ili kufungua mkutano huo.
  10
  Naibu  Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga  (katikati, waliokaa mbele) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi, Wizara ya Nishati na Madini.

older | 1 | .... | 496 | 497 | (Page 498) | 499 | 500 | .... | 1897 | newer