Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

ZIARA YA WAZIRI MKUU TOKYO JAPAN

$
0
0
4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo  kutoka kwa Mbunge na Naibu Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Bw.Shigeki Iwai kuhusu kipeperushi chenye picha zinazoonyesha kilimo cha  chai kuzunguka mlima Fuji nchini Japan katika mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo  Machi 16, 2015.
(Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
1
Waziri mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya vyakula vya  Kitanzania vilivyosindikwa  kitalaamu, Afisa Mtendaji Mkuu  na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Kampuni ya Sumitomo ya Japan,Bw.Michihiko Kanegae baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo, Machi 16, 2015.  Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam hivi karibuni. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Masuala ya Miundombinu ya Umeme wa kampuni hiyo, Tsutomu Ben Akimoto.
2
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake wakiagana  na  Afisa Mtendaji Mkuu  na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Kampuni ya Sumitomo Corporation  Corporation ya Japan,Bw.Michihiko Kanegae (wapili kushoto) baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo, Machi 16, 2015.  Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyrezi jijini Dar es salaam hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan aliyemaliza kuda wake, Salome Sijaona, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Batilda Burian.
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipata Maelezo  kutoka kwa Ofisa wa Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, Noriko Tanaka kuhusu Treni inayofanyakazi bila dereva katika jiji la Tokyo wakatia lipotembelea Ofisi za Kampuni inayoendesha treni za aina hiyo ili kujifunza namna ya kusafirisha abiria kwa njia  ya reli katika majiji Machi 16, 2015.

Rais Kikwete awaapisha wajumbe wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha wajumbe saba wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam .Wajumbe wa tume hiyo walioapishwa leo ni pamoja na Mwenyekiti wake Bwana Edrissa Mavura,Paul Herbert Kinemela(Kamishna), Bwana Mathias Bazi Kabundunguru(Kamishna),Bwana Njaa Ramadhani(Kamishna)Bwana Jones Kyaruzi Majura(Kamishna), Bwana Jaffari Ally Omari(Kamishna) na Bibi Suzane Charles Ndomba.Pichani ni wajumbe wa tume hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wanne kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Edrissa Mavura.(Picha na Freddy Maro).

MOJA YA JENGO LA MABIBO HOSTEL JIJINI DAR LILIVYOSHIKA MOTO LEO ASUBUHI

$
0
0
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wanaoishi kwenye Hostel za Mabibo,wakiangalia moja ya majengo ya Hostel hizo likiwa limeshika moto asubuhi hii.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na msaada wa haraka unahitajika ili kuokoa mali zilizopo kwenye Jengo hilo.
Hakuna anaeamini anachokiona,kwani imekuwa ni tukio la ghafla sana.
Baadhi ya Wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye Jengo hilo wakiwa nje,huku wakiwa hawajui la kufanya wakati moto huo ukiendelea kuwaka.
Moshi unazidi kufuka na moto unaongezeka.

KINANA-WANANCHI WA KARATU WANA HAKI YA KUPATA HUDUMA MBALIMBALI ZA MAENDELEO

$
0
0

Hata hivyo Kinana amesema wananchi wa Karatu ni Watanzania na wana haki ya kupata huduma mbalimbali  za maendeleo na serikali ya CCM haitawaacha kama wanavyoachwa na viongozi wao wa CHADEMA waliowachagua wenyewe.



Baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo uwanja hapo
Katibu wa NEC Itaikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa Karatu waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo wa hadhara
Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano huo wa hadhara.
Wananchi wa kijiji cha Baray-Mbuga Nyekundu wakimshangilia Katibu wa NEC Itikadi na uenezi,Nape Nnauye alipozungumza kabla ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kushiriki ujenzi wa jengo la kituo cha upasuaji afya .
Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi kutoka Chadema kata ya Baray wilaya ya Karatu Juliana Israel akitangaza kujiunga na CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kata ya Baray.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Mbuga Nyekundu kata ya Baray.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwenye maeneo ya Mang'ola barazani mara baada ya kutemebelea miundo mbinu ya umwagiliaji ambayo imelalamikiwa na wananchi hao kwa kuwa ni mibovu na haiwasaidii wananchi hao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirki kupanda vitunguu pamoja na wananchi katika shamaba la Mang'ola Barazani.
Wananchi wa Kijiji cha Mang'ola wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu  Abdulrahman Kinana ,ambapo walimpa malamiko yao juu ya uongozi wao kufanya maamuzi bila kushirikisha wananchi,kubuni miradi hewa na kula fedha.

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM YAZINDULIWA RASMI,WANANCHI WATAKIWA KULINDA NA KUTUNZA MIUNDOMBINU.

$
0
0
SD1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akitoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoani Dar es salaam.
SD2
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizindua mradi wa Maji ya Kisima mtaa wa Mongolandege, Ilala jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoani Dar es salaam. Mradi wa Kisima hicho umegharimu kiasi cha shilingi milioni 78.
SD3
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akifungua moja ya bomba la maji la mradi wa Maji ya Kisima mtaa wa Mongolandege, Ilala jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoani Dar es salaam.
SD4
Bi. Martha Singano, Mkazi wa Mongolandege akipokea ndoo ya maji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki mara baada ya  kuzindua  mradi wa Maji ya Kisima katika mtaa huo.
…………………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
.Dar es salaam.
Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Wiki ya maji kuanzia tarehe 16 hadi 22, Machi 2015 chini ya Kauli Mbiu isemayo Maji kwa Maendeleo Endelevu.
Maadhimisho ya mwaka huu yanatoa fursa kwa Mamlaka zinazohusika na usimamizi wa Maji nchini kutathmini huduma wanayoitoa kwa wananchi, kujenga na kuimarisha miundombinu iliyopo katika maeneo mbalimbali nchini. 
 
Akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Maji kwa mwaka 2015 katika Mkoa wa Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki amesema maadhimisho hayo katika jiji la Dar es salaam pamoja na mambo mengine yataambatana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) kuzindua miradi maji katika maeneo mbalimbali ya jiji, kutoa elimu kuhusu utunzaji wa vyanzo vya  maji, utunzaji wa miundombinu ya miradi inayojengwa, upokeaji wa maoni na kero za wananchi pamoja operesheni za kukamata baadhi ya watu wanaoiba na kuhujumu miundominu ya maji.
 
Amesema maadhimisho hayo  mkoani Dar es salaam yatazindua miradi  ipatayo 9 na kuweka mawe ya msingi katika miradi 2 na kuongeza kuwa chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) mkoa unatekeleza jumla ya miradi 41 ya Visima vya maji katika wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke.
 
Mhe. Saidi Meck Sadiki ameseama miradi mingine 14  iliyojengwa chini ya ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji (BTC) imekamilika na inaendelea kuwahudumia wananchi katika wilaya zote tatu za jiji la Dar es Salaam.
 
Amefafanua kuwa jiji la Dar es salaam linaongoza nchini kwa kuwa na mahitaji makubwa ya maji huku huduma ya Maji kwa wakazi hao  ikitolewa na Mamlaka ya Maji ya jiji la Dar es salaam (DAWASA) ambayo imekodisha shughuli za uendeshaji huduma kwa DAWASCO. Vyanzo vikuu vya maji katika jiji la Dar es salaam mto Ruvu, Kizinga pamoja na maji yanayopatikana chini ya ardhi.
 
Amesema mahitaji ya maji kwa wakazi wa jiji na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani kwa sasa ni wastani wa lita 450 kwa siku huku uwezo wa kuzalishaji maji kwa siku ni lita 300  ambazo ni sawa na asilimia 66.7 ya mahitaji yote.  
 
Ameeleza kuwa upungufu huo unaosababishwa na uwezo mdogo wa mitambo na miundombinu ya kuzalisha maji  na kuongeza kuwa Serikali kupitia sekta 6 zilizopewa kipaumbele chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, Maji yamepewa kipaumbele ambapo miradi ya maji 41 mkoani Dar es salaam itatekelezwa ili kufikia lengo la Serikali la uzalishaji wa lita 710 ambazo zitakua  ni zaidi ya mahitaji mwishoni mwa mwaka 2015.
“Matarajio yangu na mkoa ninaouongoza ni kuhakikisha kuwa tunawapatia watu milioni 3.8 ambao ni asilimia 90 ya wananchi katika jiji la Dar es salaam huduma ya majisafi na salama mwishoni mwa mwaka 2015” Amesisitiza.
 
Ameleza kuwa  DAWASA inatekeleza mpango maalum wa kuongeza upatikanaji wa maji jijini Dar es salaam kwa kupanua Mitambo ya Ruvu chini ambayo kazi yake imekamilika kwa asilimia 100, ujenzi wa bomba kuu kutoka Ruvu chini hadi chuo kikuu cha ardhi ambao umekamilika kwa asilimia 93, kazi ya upanuzi wa mtambo wa Ruvu juu na ujenzi wa bomba la maji hadi Kimara ambao umefikia asilimia 55 utakaokamilika mwezi Agosti, 2015.
 
Aidha, amesema kazi ya uchimbaji wa visima 20 katika awamu ya kwanza imeanza na itakamilika mwezi Agosti mwaka huu ikihusisha pia upanuzi wa mtandao wa usambazaji wa maji katika maeneo yaliyo kandokando ya mabomba makuu kutoka Ruvu chini na Ruvu juu na kunufaisha vitongoji vilivyopo kati ya mji wa Bagamoyo hadi eneo la Tegeta-Mpiji na vitongoji vilivyopo kati ya mji wa Mlandizi –Kiluvya na maeneo ya Mbezi, Kimara na Goba.
 
Awamu ya pili itahusisha upanuzi wa mfumo wa usambazaji wa maji katika maeneo yote ya jiji yatakayopata maji kutoka Kimbiji na Mpera na maeneo mengine ya jiji yasiyo na mabomba ya usambazaji.
 
Akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa visima vya dharula katika maeneo yasiyo na maji ya bomba amesema jumla ya visima 48 vimechimbwa katika maeneo mbalimbali ya jiji yakiwemo Kimara,Kimara, Kisukuru, Keko –Chang’ombe, Sandali, Mburahati, Mbagala, Mtoni, Kigamboni ,Gerezani na Ukonga.
 
Katika hatua nyingine Mhe. Saidi Meck Sadiki ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa baadhi ya watu wanaorudisha nyuma juhudi za Serikali za kuwapatia wananchi maji safi kwa kuhujumu miundombinu ya maji ya DAWASCO kwa kuendesha vitendo vya wizi wa maji, mambomba na miundombinu mingine.
 
Pia ameitaka DAWASCO na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kuanza kuwafuatilia na kuwadhibiti baadhi ya wafanyabiashara wanaowaibia wananchi kwa kununua maji ya DAWASCO kwa gharama nafuu ya shilingi 1 kwa lita na kuyauza kwa zaidi ya shilingi 50.

mkutano wa kuimarisha ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini uliofanyika jijini Mwanza.

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Charles Kitwanga, akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kuimarisha ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya  madini unaofanyika jijini  Mwanza.
Baadhi wa washiriki wa mkutano wa kuimarisha ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya  madini  wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga anayeshughulikia Nishati  (hayupo pichani).

Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Migodi Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha taarifa wakati wa mkutano wa kuimarisha ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya  madini unaofanyika jijini  Mwanza.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Charles Kitwanga (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kuimarisha ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya  madini

Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Paul Masanja (wa pili kulia) akiongea jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Charles Kitwanga wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kuimarisha ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya  madini.

ZIARA YA WAHARIRI KIWANDA CHA BIA TBL MBEYA

$
0
0

 WAHARIRI 22 wa Vyombo vya habari mbali mbali nchini jana walifanya ziara kwenye Kiwanda cha Kampuni ya  Bia Tanzania(TBL) wakiongozwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF).
Katika ziara hiyo Wahariri hao walipata maelezo mbali mbali kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Roberto Jarrin kuhusu hali ya kibiashara ya kampuni hiyo pamoja na bidhaa zinazozalishwa kisha kutembelea mitambo ya kutengeneza Bia.

Meneja wa Kiwanda cha Bia Mbeya, Waziri Jemedari aliwaambia Wahariri Changamoto ambazo Kiwanda hicho kinakabiliana nazo kuwa ni pamoja na umeme wa grid ya taifa kuwa na nguvu ndogo ya kutokutosha kuendesha mitambo, ubovu wa barabara ya kuingilia kiwandani pamoja na upatikanaji wa maji.

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Wahariri, Mwenyekiti wa TEF, Absolom Kubanda, aliishukuru Kampuni ya TBL kwa kuwathamini na kuwaalika katika ziara hiyo na kuongeza kuwa watakuwa mabalozi wazuri kutangaza hali halisi waliyoiona kiwandani hapo tofauti na maneno ya watu mitaani.

Alisema watu wengi hudhani mazingira ambayo vinywaji vinatengenezwa hayafai jambo ambalo sio la kweli kutokana na kujionea wenyewe mlolongo mzima tangu uoshaji wa chupa hadi kinywaji kinavyojazwa kuwa katika hali ya usafi.

Kwa upande wake Meneja uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Editha Mushi alisema lengo la kuwaalika Wahariri wa Vyombo vya habari ni kudumisha uhusiano baina ya TBL na Vyombo vya habari.

Aliongeza kuwa lengo lingine ni kutoa mrejesho kwa jamii juu ya hali ya kibiashara ilivyosasa na awali kupitia kwa Wahariri wa Vyombo vya habari ili iwe wazi kwa kila mtu.










      Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Bia(TBL) na SUBMiller East Africa Operesheni, Roberto Jarrin, akiwasilisha Mada kwa Wahariri wa Vyombo vya habari nchini waliofanya ziara katika kiwanda cha Bia Tawi la Mbeya.


   Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari akitoa maelezo kuhusu kiwanda hicho kwa Wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini.


Meneja wa Kampuni ya Vinywaji ya Konyagi(TDL) akifafanua jambo kwa Wahariri wa vyombo vya habari.


 Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Bia(TBL) na SUBMiller East Africa Operesheni, Roberto Jarrin, akionesha kitu ubaoni kwa Wahariri wa Vyombo vya habari nchini waliofanya ziara katika kiwanda cha Bia Tawi la Mbeya.


  Steve Kilindo (Corporate affairs& legal director) akitoa maelezo kwa Wahariri.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa TBL, Editha Mushi akibadilishana mawazo na mmoja wa watumishi wa TBL Mbeya.




Wahariri wakifuatilia kwa makini mada zinazowasilishwa.




Meneja Viwango wa TBL Esther Mmari akitoa maelezo juu ya viwango vya bia zinazozalishwa kwa Wahariri.


Baadhi ya Watumishi wa TBL wakikagua makaratasi yaliyojazwa na Wahariri baada ya kupewa kazi ya kuchagua Bia aina ya Kilimanjaro yenye ubora.




Baadhi ya Wahariri wakiangalia kwa makini Bia zilizo kwenye grasi ili kugundua bia yenye ubora unaotakiwa.




 Wahariri pamoja na Watumishi wa TBL wakielekea kutembelea mitambo ya kutengenezea vinywaji katika kiwanda cha Bia cha TBL tawi la Mbeya.




Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Mbeya Waziri Jemedari akitoa maelezo kwa Wahariri wakiwa wanatembelea na kuangalia mitambo mbali mbali kiwandani hapo.






Wahariri wakiwa Kiwandani wakiangalia mitambo mbali mbali.







Mmoja wa Wahariri akiuliza swali kutoka kwa Uongozi wa TBL.

100 kupewa tuzo Tamasha la Pasaka

$
0
0
WADAU 100 waliofanikisha kwa namna mbalimbali  katika kipindi cha miaka 15 tangu kuanzishwa Tamasha la Pasaka nchini wanatarajiwa kupewa tuzo wakati wa tamasha la mwaka huu.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa wadau hao ni wanasiasa, viongozi wa dini, wafanyabiashara na waandishi wa habari.
 
“Wapo wengi waliotusaidia kufikia hapa tulipo, lakini tumeteua 100 hawa watapokea kwa niaba ya wengine, ikiwa ni shukrani kwa kutusaidia kwa namna mbalimbali.
 
“Wapo waliotusaidia wanatoka Dar es Salaam na wengine mikoani, hivyo wale wa mikoani tutawapa tuzo zao wakati tukienda katika matamasha ya huko na wale wa Dar es Salaam watapokea siku yenyewe ya Pasaka,” alisema Msama.
 
Alieleza kuwa si kazi rahisi kuweza kusimamisha tamasha kubwa kama hilo kwa miaka 15, pia si kazi ya yeye peke yake bali ni ushirikiano wa watu mbalimbali ambao anaona kuna umuhimu wa kuwashukuru.
 
Alisema watawapa tuzo maalum pamoja na vyeti ambavyo anaamini kwa kiasi fulani vinaweza kuwafanya wahisi kweli mchango wao umetambuliwa.
 
Mwaka huu Tamasha la Pasaka linatimiza miaka 15 tangu lianzishwe, ambapo waandaaji wamepanga tamasha kubwa la kuendena na sherehe hizo.
 
Tayari wasanii maarufu kutoka nje ya Tanzania wameshathibitisha kushiriki  wakiwemo Rebecca Malope na  Solly Mahlangu ‘Obrigado’ wote kutoka AAfrika Kusini na raia wa Uingereza Ifeanyi Kelechi

MAKALA YA SHERIA: SHERIA HAILAZIMISHI KUTOA MATUNZO YA MTOTO KULIKO UWEZO WAKO

$
0
0

Suala la matunzo ya watoto/mtoto lim ekuwa ni suala ambalo wasomaji wengi wamekuwa wakiniuliza sana. Wengi wao wanaouliza ni wale ambao wamezaa nje ya ndoa na hivyo kuna utata wa matunzo ya watoto na wale ambao wamekuwa wana ndoa lakini sasa tayari wametengana aidha kwa talaka au bila talaka. Niseme tu kwa ufupi kuwa suala la matunzo ya watoto linajumuisha mambo mengi nami nitaeleza baadhi tu.

1.HUWEZI KUMLAZIMISHA MTOA MATUNZO KUTOA AMBACHO HANA.

Kumekuwepo na tabia ya wazazi hasa upande wa wazazi wa kike kuwalazimisha wanaume ambao wamezaa nao na kutengana nao kutoa matunzo ya watoto kwa kiwango cha juu kabisa ambacho pengine kinazidi hata kipato cha mtoaji. Hili si sawa. Ni kweli sheria inamlazimisha mwanaume kutoa matunzo ya mtoto lakini haimlazimishi kutoa kuliko anachopata. Sheria haiseme kwakuwa mwanamke anaishi na mtoto wa mtu basi mwanaume ndio sasa afanywe kitega uchumi. Inafikia hatua mwanamke hafanyi kazi yoyote isipokuwa anategemea ile pesa ya matunzo ya mtoto ndio iwe kila kitu katika maisha yake.

Hii ndio sababu hata akipewa kiasi kinachotosha haoni kama kinatosha kwakuwa kinakuwa na njia nyingi kama saluni, nguo za kuvaa, pesa ya upatu, michango ya harusi na kitchen party na kila kitu kinachohusu maisha yake binafsi. Ieleweke wazi kuwa kwa mujibu wa sheria pesa ya matunzo ya mtoto haihusiki na haya. Pesa ya matunzo ya mtoto ni pesa ya matunzo ya mtoto kama neno lenyewe lilivyo na linavyojieleza si vinginevyo.

2.INARUHUSIWA KUKATAA IKIWA UNALAZIMISHWA KUTOA MATUNZO YANAYOZIDI UWEZO WAKO.

Ikiwa mwanaume analazimishwa kutoa kuliko kipato chake basi anaruhusiwa kukataa hata kama amri hiyo imetolewa na mahakama. Wengine huandikishana polisi lakini bado haibadili maana kwakuwa mtu anatakiwa kutoa kulingana na uwezo wake au kipato chake. Wapo wazazi hasa wa kike ambao huwalazimisha wanaume kutoa matunzo ya kuwasomesha watoto international schools wakati kipato cha mwanume ni shule ya kata. Sheria inachokataza ni kukataa kabisa kutoa matunzo ya mtoto lakini haimlazimishi mtu kutoa kilichomzidi. Au wengine hulazimisha kuwekewa mpaka wafanykazi wa ndani( house girl) wakati kipato cha mwanaume hakiruhusu jambo hilo.

Huu nao ni unayanyasaji kwa upande wa wanaume na haukubaliwi na sheria. La msingi ni kuwa iwapo utalazimishwa kutoa kuliko uwezo wako we kataa. Na kama uamuzi huo umetolewa na mahakama basi kataa kwa kukata rufaa kupinga kabisa jambo hilo. Sheria inaposema matunzo ya watoto haisemi kuwa watu watoe kuliko uwezo wao hapana. Sheria ni haki na haki huzingatia ukweli na hali halisi ya jambo.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Muadhama, Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akizungumzia kuhusu tamko la Maaskofu juu ya katiba pendekezwa

VIDEO YA SEHEMU YA HOTUBA YA KINANA AKIHUTUBIA KARATU MJINI

Imetosha Movement Kufanya Matembezi Hisani Machi 28

$
0
0
Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya 'Imetosha Movement' na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni. Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya 'Imetosha Movement' na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni.

 ASASI ya Harakati za Imetosha ilioanzishwa kupinga mauaji na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye u-albino inatarajiwa kufanya matembezi makubwa ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa uma juu ya imani potofu zinazoendelea za mauaji ya albino. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu amesema matembezi ya hisani kuchangia fedha zitakazowezesha kutolewa kwa elimu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa juu ya imani potofu zinazoendelea na mauaji ya albino yanatarajia kufanyika Dar es Salaam Machi 28, 2015.

 Alisema matembezi hayo yataanzia katika Viwanja vya Leaders na kuzunguka maeneo yaliyopangwa kisha kurejea viwanjani hapo kwa ajili ya shughuli maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya harakati maalumu za imetosha zitakazo kwenda kwa jamii ya kawaida na kueneza elimu ikiwa ni juhudi za kuhamasisha kila mwana jamii kupaza sauti na kusema 'Imetosha Mauaji ya Albino'.

 "...Baada ya taratibu kukamilika, matembezi sasa yatafanyika Tarehe 28 Machi kuanzia saa 12 Alfajiri, kutoka Leaders Club tutazunguka na kurudi hapo, karibuni sana tuchangie harakati hizi zenye lengo zuri kwa mustakabali wa Taifa letu lenye sifa ya amani na utulivu," alisema Mdimu katika taarifa yake. 

Aidha akizungumzia uvumi ulioenea hasa katika nchi za nje, unaodai kwamba serikali imekataza watu wenye ulemavu wa ngozi kuandaa matembezi au maandamano alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuongeza kuwa kuna taratibu za kufuata kabla ya uandaliwa shughuli hizo. "...Hili suala sio kweli, ili ufanye mambo kama haya ni lazima upitie taratibu za kisheria ili upate kibali. Hii ni nchi na ina taratibu zake kwa hiyo tulipaswa kuzifuata na ndio kilichosababisha hata matembezi yetu kuahirishwa. 

"Tulikuwa tunafuata taratibu na leo rasmi tumepata usajili wa Imetosha...sasa imetosha imekuwa taasisi kamili inayoitwa IMETOSHA MOVEMENT. Napenda kuchukua wasaa huu kuwashukuru marafiki wote wanaoniunga mkono, na kunipa moyo, msinichoke kwa sababu safari bado ni ndefu," Hata hivyo aliwataka wananchi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni kujitokeza katika matembezi hayo ya hisani ili kuunga mkono juhudi sa mapambano ya kukomesha mauaji na vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa watu wenye ualbino maeneo mbalimbali ya nchi.

18 wahitimu mafunzo ya uongozi bora waliyoanzishwa na Rais Obama

$
0
0
 Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress akisisitiza jambo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya  uongozi bora kwa vijana yaliyoanzishwa na Rais wa Marekani, Barrack Obama kuptia taasisi ya Mandela Felloship, Ohio University na Institute for International Journalism.
 Mkurugenzi wa mafunzo ya Yali Connect Camp, Dk Yusuf  Kalyango akizungumza na wahitimu 18 wa mafunzo hayo.
 Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akipozi katika picha na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress mara baada ya kukabidhiwa cheti cha uhitimu.
Vijana kutoka mataifa manne wakimsikiliza Balozi wa Marekani nchini Tanzania (hayupo pichani) wakati wa  hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi bora kwa viongozi vijana wa baadaye yaiyomalizika hivi karibuni jijini.


Jumla ya vijana 18 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Mauritius, Seychelles na Tanzania wemehitimu mafunzo ya wiki mbili ya uongozi bora yaliyoanzishwa na Rais wa Marekani, Barrack Obama.

Mafunzo hayo yaliendeshwa nchini chini ya programu ya Connect Camp chini ya  Mandela Washington Fellowship, Chuo Kikuu cha Ohio na Taasisi ya Kimataifa ya Uandishi wa Habari (Institute for International Journalism) yenye malengo ya kuwapa uwezo vijana wa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress aliwataka vijana hao kutumia mafunzo hayo kwa mafanufaa katika fani zao na nchi husika kwani ni nyenzo ya kuwa viongozi bora wa baadaye hapa duniani. Childress alisema kuwa Rais Obama ameanzisha mafunzo hayo kutokana na kutambua umuhimu wa uongozi bora na kuamini kuwa vijana ndiyo taifa la kesho.

“Nimefurahishwa na mwamko wa mafunzo haya, nawaomba myatumie kwa ajili ya maendeleo yenu na kwa nchi husika, hii ni nyenzo pekee katika kufikia lengo mlilojiwekea,” alisema Childress.

Mafunzo hayo yanayojuliana kwa jina la  ‘Young African Leadership Initiative (Yali) yalishirikisha vijana  nane (8) wa Kitanzania, wanne Uganda, huku Kenya, Mauritius na Seychelles zikiwakilishwa na watu wawili wawili.

Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo ni Mbunge wa Chadema jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nasari ambaye alisema atatumia mafunzo hayo kujihimarisha kisiasa na kushinda kiti ha ubunge katika jimbo hilo.
 
Alisema kuwa mafunzo hayo yamepanua ufahamu wake katika siasa na hiyo ndiyo itakuwa silaha kubwa katika uchaguzi ujao. “Najua kuwa nitapata upinzani mkubwa katika uchaguzi huo, nipo kidete kwa ajili ya kutetea kiti hicho na kupitia mafunzo haya, hakuna atakayenizuia kushinda,” alisema Nasari.

Kipindi kipya cha Niambie Live kuanza kurushwa kesho

$
0
0
Hiki ni kipindi kitakachozungumzia baadhi ya mambo ambayo yametawala kwenye mitandao ya kijamii.
Kitawajia punde
USIKOSE kukifuatilia

walimu wa jimbo la uzini wafanya ziara ya kimasomo mkoani Lindi

$
0
0
                                                                                                                                                                                             
Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete amefurahishwa na hatuwa iliyochukuliwa na Walimu wa Jimbo la Uzini Zanzibar ya kufanya ziara ya kimasomo Mkoani Lindi kwani ni njia moja wapo ya kujifunza na kujiongezea elimu kwa vitendo.

Hayo ameyasema Jana wakati akiwakaribisha walimu wa Jimbo hilo Mkoani hapo kwa ajili ya kuanza rasmi ziara yao ambayo inatarajiwa kuchukuwa takribani wiki moja.   
 
Aidha Mama Salma amesema ziara za kimasomo ni njia moja ya kuleta mashirikiano na kudumisha Muungano wa Watanzania katika kuboresha Sekta ya Elimu Nchini hiyo ni kwa sababu  Elimu ya Juu na Sekondari nchini Tanzania ni moja ya mambo yaliyo chini ya Serikali ya Muungano.
                                                        
Akizungumzia Changamoto zinazowakabili Walimu hao  katika Sekta ya Elimu  kwa upande wa Mkoa wa Lindi ni upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi jambo ambalo  husababisha kukosekana kwa wataalamu wa fani mbalimbali za Kisayansi kwa maendeleo ya Taifa ambapo  hurudisha nyuma jitihada zao za kutaka kuzalisha wataalamu watakaokwenda sambamba na ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia.
                                                                                                                                                    
Nae Afisa Uendeshaji wa Wizara ya Elimu Zanzibar Nd. Muhussin Sufiani Mkanga amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kujifunza njia mbalimbali zilizobora za kielimu ikiwa ni njia za kuwafundishia wanafuzi wa Zanzibar katika kuimarisha ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne.

Hata hivyo amewataka walimu wenzake waliopata fursa kuwepo katika ziara hiyo kuwa makini katika kujifunza masomo hayo kwa lengo la kupata njia zilizo bora za  utoaji wa  elimu kwa  wanafunzi wao ikiwa ni mfano mzuri wa kuigwa na walimu wengine Nchini.
 
Jumla ya walimu 36 kutoa Zanzibar wamepata fursa ya ziara ya kimasomo Mkoani Lindi na wanatarajiwa kuwa mabalozi wazuri kwa walimu wenzao waliokosa fursa hiyo kwa kuwapa yale yote mazuri waliyoyapata na kuyafanyia kazi kwa maendeleo ya Nchi yao.

                                                                                      IMEHARIRIWA NA HABARI MAELEZO-ZANZIBAR


jamii inapaswa kuwekeza katika sayansi na teknolojia - Balozi Sefue

$
0
0
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na wajumbe wa warsha wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya ubunifu wa sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya ubunifu wa sera ya Taifa katika Sayansi na Teknolojia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(katika) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu(kushoto), na Naibu Katibu Mkuu wa Hiyo John Mngodo,warsha hito iliandaliwa iliandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.

Na May-Zuhura Simba

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa ili jamii iweze kukua kwa kasi na kupata maendeleo haina budi kuwekeza katika sayansi na teknolojia.

Aliongea hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

“ubunifu katika sayansi na teknolojia ni kitu muhimu katika kupata uvumbuzi wa vitu mbalimbali muhimu vinavyoleta maendelao kwa jamii husika hivyo kuna umuhimu wa kuwafungia wanasayansi katika atamizi ili kupata matokeo mazuri ya utafiti” alisema Balozi Sefue.

Aidha aliongeza kuwa nchi kama Korea na Singapore waliwekeza katika sayansi,technologia na ubunifu na hivyo kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa jamii zao.

Vilevile alisisitiza kuwa ubunifu ukisimamiwa dhabiti utasaidia katika kuleta mageuzi kwenye sekta muhimu ikiwemo elimu, afya,biashara,kilimo na miundombinu na hivyo kutatua matatizo ya kijamii.

“Mfano mzuri ni Max malipo ambalo ni zao la vijana wa kitanzania waliokuwa wamewekwa katika atamizi na kuleta uvumbuzi huu kwa kutumia sayansi na teknolojia ” alisema Balozi Sefue.

Aidha aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo,makampuni binafsi, na serikali kushirikiana kwa pamoja kufungua vituo atamizi zitakavyosaidia vijana kuvumbua teknolojia mbalimbali.

MAKALA YA SHERIA: ILI KUBADILI HATI YA NYUMBA / KIWANJA KWA HARAKA ANDAA NYARAKA HIZI

$
0
0

Watu wengi wanaonunua ardhi wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa katika kubadili majina yaani kutoka mmiliki wa mwanzo kwenda kwa mmilki mpya aliyenunua. Upo usumbufu ambao husababishwa kwa makusudi na maafisa wanaohusika lakini pia upo usumbufu ambao husababishwa na watu wenyewe wanaotaka kubadili majina. Awali ya yote lazima nikiri kuwa baadhi ya maafisa wa mamlaka za ardhi husababisha uchelewaji kwa makusudi kabisa na lengo likiwa kujenga mazingira ya kupozwa kidogo. Hili lipo na kila mtu ambaye amekuwa akishughulikia masuala ya hati na kubadili majina miliki kama mimi atakiri kukutana na haya. Hao tuwaache mimi leo nazungumzia maandalizi ambayo ukiyafanya mapema utafanikiwa kwa urahisi na haraka kubadili jina la kiwanja au nyumba kutoka kwa mtu akiyekuuzia kuingia jina lako.

1.UMUHIMU WA KUBADILI JINA HARAKA BAADA YA MANUNUZI.

Sheria iko wazi kuwa ambaye jina lake linaonekana kwenye hati ndiye mmiliki.

Kwa kauli hii mnunuzi anatakiwa kufanya jitihada za haraka na za makusudi kubadili jina mara tu baada ya kununua kiwanja au nyumba. Sikatai kuwa kunakuwa na mkataba wa mauziano lakini lazima ieleweke kuwa mbele ya macho ya sheria jina lililo kwenye hati lina uzito kuliko mkataba wa mauziano. Usiridhike kukaa na mkataba wa mauziano ikiwa hujabadili jina. Hii ni kwa ajili ya ulinzi wako na wa ardhi yako. Utakapotokea mgogoro wa umiliki ikiwa hujabadili jina waweza kuwa katika hatari kubwa ya kupoteza hasa kama mgogoro huo umeanzishwa na aliyekuuzia. Huu ndio ukweli na lazima tuonyane ili tuwe salama na mali zetu. Lakini pia hata ukitokea mgogoro mwingine wowote wa umiliki kuna mambo ndani ya sheria yataufanya kuwa mgumu kutokana na sababu tu kuwa ulikuwa hujabadili jina. Hapo sijaongelea faida nyingine za kubadili jina kama kukopa n.k. Nishauri tu kwa ufupi kuwa unapojiandaa kununua nyumba au kiwanja jiandae pia na kubadili jina moja kwa moja. Hakikisha haya mawili yanakwenda pamoja.

2. ILI KUBADILI HATI KWA URAHISI NA HARAKA HEBU ANDAA NYARAKA HIZI.

( a ) NYARAKA ZA UHAMISHO
Nayaraka za uhamisho zinajumuisha fomu namba 29 ijulikanayo kama fomu ya kusudio la uhamisho( notification of disposition) ambayo hueleza nia na lengo la muuzaji kutaka kubadili jina au kuondoa jina lake katika hati. Hii utaandaa nakala tatu . Pili ni fomu namba 30 ambayo hujulikana kama fomu ya idhibati ya uhamisho ( application for approval of disposition). Katika fomu hii muuzaji pia atakuwa anatoa idhini kwa mamlaka za ardhi kuidhinisha hiari yake ya kuachia umiliki kutoka kwake kwenda kwa mtu mwingine ambaye ndiye mnunuzi. Mwisho ni fomu namba 35 ijulikanayo kama fomu rasmi ya kuhamisha umiliki ( transfer of a right of occupancy) ambayo ndiyo rasmi sasa huhamisha umiliki kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi. Hii ndiyo humpa mnunuzi umiliki rasmi . Pia mkataba wa mauziano ni nyaraka ambayo itaambatanishwa hapa.

Kwa kiwanja au eneo ambalo halijaendelezwa ( halijajengwa) huandaliwa kitu kiitwacho commitment bond kikiwa kama ziada ya nilivyotaja hapo. Fomu zote hizo pamoja commitment bond hupatikana katika ofisi za wanasheria na huandaliwa na wanasheria.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA INAYOENDESHWA NA UTT AMIS YAPATA FAIDA KUBWA

$
0
0
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa UTT AMIS Bw.Simon Migangala akiongea na waandishi wa habari jana Dar es salaam kuhusiana na ufanisi wa mifuko kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

UTT AMIS ndiyo waendeshaji na waanzilishi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja nchini.Mpaka sasa wanaendesha mifuko mitano ya uwekezaji ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa wekeza Maisha,Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye zaidi ya shilingi bilioni 227.

Bwana Migangala aliwaambia waandishi wa habari kuwa kwa ujumla ukuaji wa mifuko umekua mzuri na umewezasha kutoa faida nzuri kwa wawekezaji wake zaidi ya 100,000 kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Mfuko uliotoa faida nzuri zaidi ni Mfuko wa Watoto ambao ulitoa asilimia 51.19 ukifuatiwa na Wekeza Maisha uliotoa asilimia 45.23

Mfuko wa tatu ni Umoja ambao ulikua kwa asilimia 38.46, wanne Kujikimu alikua kwa asilimia 36.77 na Ukwasi kwa asilimia 11.46

Alisema kimsingi wanafurahia na wanajivunia faida hiyo waliyopata wawekezaji wao.Ukuaji huu umechangiwa na ufanisi mzuri wa soko la Hisa la Dar es salaam , masoko ya fedha ambako mifuko pia huwekeza na weledi wa meneja wa Mifuko (UTT AMIS) katika kuwekeza na kusimamia mifuko.

Katika kipindi hicho cha miezi sita thamani halisi za vipande vya mifuko viliongezeka kama ifuatavyo;

Kipande cha Mfuko wa Umoja kiliongezeka kutoka shilingi 365.6892 hadi shilingi 435.9008,Wekeza Maisha kilitoka shilingi 237.5386 hadi 291.1558 kwa Mfuko wa Watoto kiliongezeka kutoka shilingi 213.72 hadi shilingi 268.3172

Mfuko wa Kujikimu kutoka shilingi 118.1779 hadi shilingi 131.1440(ukijumuisha na gawio la shilingi 4 kila baada ya miezi mitatu) na mwisho Mfuko wa Ukwasi toka shilingi 114.3608 hadi shilingi 120.9362.

Ongezeko hilo linathibitisha ukuaji wa mifuko yetu na tunawahamasisha watanzania wajiunge katika mifuko hii waweze kuwekeza fedha zao na kupata faida maridhawa.Tunaendelea kuwaambia kuwa ni fedha zako,ni akiba yako,ni uwekezaji wako, faida ni yako! UTT AMIS tunawezesha! Hakika tutaendelea kuwa ‘Mshirika hakika katika uwekezaji’

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE NDANI YA JIMBO LA LONGIDO MKOANI ARUSHA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi na bendera za aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Longido ambaye amejiunga na CCM kwenye mkutano uliofanyika Eworendeke.Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako kwenye ziara ya siku tisa mkoani Arusha ya Kuhimiza,kuimarisha na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010 ikiwemo pia na kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
Wananchi wa kijiji cha Eworendeke wakiwa wamekusanyika wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia wilayani humo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Eworendeke ambapo alitoa salaam za shukrani kwa CCM wilaya ya Longido kwa kuipa ushindi mzuri wakati wa uchaguzi.
Wananchi wakisikiliza hotuba kwa makini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya katika kijiji cha  Lesingeita,wilayani Longido.Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Longido Mh.Lekule Laizer.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Eworendeke ambapo alimpongeza mbunge wa jimbo la Longido kwa uamuzi wake wa kutogombea uchaguzi ujao na kusema wanasiasa wengi wanajua kuingia kwenye siasa lakini wakisahingia hawajui wakati gani wa kutoka.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Engikareti wilaya Longido.
Mzee Kitasho Simel Nakutamba akimpa mkono Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika hoteli yake ya Longido kama ionekanavyo pichani.
Pichani ni jengo la kituo cha mafunzo cha Learning In Longido (LIL),ambapo  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliweka jiwe la msingi na kushiriki kupaka rangi kwenye majengo hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi kwenye majengo ya kituo cha mafunzo cha Learning In Longido (LIL).



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiandaa sindano ya chanjo tayari kwa kumchoma ng'ombe.,Pichani shoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha,Ndugu Onesmo Ole Nangolo akishuhudia tukio hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kumchoma ng'ombe chanjo kwenye mradi wa ufugaji wa madume bora katika kijiji cha Ketumbeine.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa jengo la hoteli katika kijiji cha Kitumbeine,kushoto ni mmiliki wa hoteli hiyo Ndugu Halifa Juma.
Mbunge wa Viti Maalumu Vijana,Catherine Magige akiwahutubia wakazi wa Eworendeke,Wilayani Longido.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vijana wa kimasai alipowasili  kwenye kituo cha mafunzo Learning In Longido

KITABU KIPYA CHA MHAMASISHAJI MAHIRI ZAIDI AFRIKA, ERIC SHIGONGO KUINGIA MTAANI MEI 1, 2015

Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images