Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 487 | 488 | (Page 489) | 490 | 491 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0
 • 03/18/15--04:24: Niambie Live Show....Ep1
 • Omby Nyongole, Salma Moshi na Queen Mkelemi
  Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
  Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.
  Ni Niambie Live....
  KARIBU

  0 0

  Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe  akiweka alama za  vidole katika mashine ya  BVR wakati  wa  kujiandikisha katika  daftari  la kudumu la  wapiga  kura  jana ,wa  pili  kulia ni kamishina wa  tume Prof Amone Chaligha
   Mkazi  wa  Ludewa  mjini  akipigwa  picha ya  kitambulisho  cha mpiga  kura
   kamishina wa  tume Prof Amone Chalighaakihojiwa na wanahabari kulia ni mbunge wa  Ludewa  Deo Filikunjombe akiwa na kitambulisho  chake  kipya  cha  kupigia  kura
   Mbunge  wa  Ludewa  Deo Filikunjombe akikabidhiwa kitambulisho  chake  cha kupigia kura  mara baada ya  kumaliza  zoezi la kujiandikisha  lililochukua  dakika 15
   Mkurugenzi  wa Halmashauri ya  Ludewa ambae ni msimamizi mkuu wa uchaguzi  wilaya ya  Ludewa Bw  Waziri  akichukua alama  za vidole wakati wa  kujiandikisha
   Mbunge  Filikunjombe  akipigwa  picha ya  kitambulisho cha mpiga  kura.

   Mkurugenzi wa  Ludewa akichukua alama  za  vidole wakati wa kujiandikisha
   Kamishina wa  tume Prof Amone Chalighakulia  akionyesha alama za sahihi ambazo mtu  akifoji sahihi katika  eneo  jingine  kikiletwa  kitambulisho  hicho  hubainika 
   Filikunjombe  kushoto  akikabidhiwa kitambulisho  chake  na  muandikishaji  kulia katikati ni kamishina  wa  tume Prof Amone Chaligha akimuelekeza alama maalum zilizopo katika kitambulisho  hicho
   Wananchi  Ludewa wakiwa katika  foleni ya  kujiandikisha

  Mmiliki  wa mtandao   huu wa matukio daima Francis  Godwin kushoto akimhoji kamishina  wa tume Prof Amone Chaligha (katikati)juu ya kasoro  za sugu katika  vidole zilizojitokeza awali makambako
  Mkazi  wa LudewaBw  Ernest Yohana  akionyesha  kitambulisho chake kipya.
  Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe (kushoto) akiweka sahihi  katika mashine ya kielektroniki za Biometric Voters Registration (BVR),wakati akijiandikisha katika daftari la kudumu la  wapiga  kura juzi katika  kituo cha shule ya msingi Ludewa mjini ,wa  pili  kulia anayeshuhudia ni kamishina  wa  tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC)  Prof Amone Chaligha(picha na 

  Na MatukiodaimaBlog, Ludewa

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema mchakato wa uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura  ulioanza kwa awamu ya  pili katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe umeanza  vyema na  sasa mashine hivyo za kielektroniki za Biometric Voters Registration (BVR), zinafanya kazi  vizuri hata kwa  wale  wenye vidole  vyenye sugu.

  Kauli  hiyo  imetolewa  jana   na kamishina  wa  tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC)  Prof Amone Chaligha wakati akizungumza na  wanahabari  nje ya  kituo  cha kuandikishia  wapiga kura cha Ludewa Shuleni wilani  Ludewa mara baada ya  mbunge wa jimbo  la  Ludewa  Deo  Filikunjombe na msimamizi wa  zoezi  hilo wilayani Ludewa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo  kumaliza  zoezi la  kujinadikisha .
  Alisema  kuwa kasoro za mashine za BVR ambazo awali zilikuwa zikisumbua  kutosoma alama za vidole  kwa baadhi ya watu hasa  wale  wenye sugu kwa  sasa kasoro  hizo  zimekwisha baada ya wataalamu wa mifumo ya Kompyuta kuzifanyia kazi ili  kufanya kazi kwa mazingira  yoyote yale .
  Prof.Chaligha alisema kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani zoezi hilo wilayani Ludewa litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo zoezi litahamia maeneo mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha  wala  kuhofu  mashine  kutofanya kazi .
  Alisema tokea zoezi hilo lianze wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama ilivyokuwa mji wa Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya kujipatia kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.

  “ Ni  kweli  siku  mbili tatu kasoro  za  sugu  katika  vidole  lilikuwa ni  shida  ila  wataalam wa IT  walilifanyia kazi na kwa  sasa  hakuna  kasoro kama  hizo na kuwa amepata  kuzungukia  vituo mbali mbali mjini Ludewa na  vijijini kasoro kama  hiyo haipo  tena kwa  sasa  hata  wakulima  wanajiandikisha bila shida.
    
  Kuhusu  kasi  ndogo  ya  uandikishaji  alisema  imechangiwa na waandikishaji  wenyewe kuwa na kasi ndogo na kuwa kimsingi  kila mwananchi  anapaswa  kujiandikisha kwa dakika 3 hadi 4  na  kuwa kwa  siku moja mashine  inauwezo wa kuandikisha  kiwango  cha chini kabisa ni kati ya  watu 50 -80.
  Hata  hivyo alisema  wanaofanya kazi  hiyo  ya uandikishaji  ni  wale ambao wanataaluma ya IT na  walifanyiwa mchujo na  wale  walioshindwa waliachwa  hivyo  wamejipanga  kuna kazi hiyo  inafanikiwa vilivyo.
  Awali wakazi  wa Ludewa mjini  waliokutwa  kituoni  hapo  walielezea kero  kubwa ya  kukaa kwa muda mrefu  kituoni hapo  bila ya  kujiandikisha kwa madai ya  watoa huduma   hiyo  kufanya kazi kwa kasi ndogo  zaidi alisema mmoja kati ya  wakazi hao Bw  Ernest Yohana  .
  Alisema  kwa upande wake  alifika kituoni hapo  toka majira ya saa 4 asubuhi na  kukaa kwenye foleni  hadi saa 9 ;30  alasiri  alipofanikiwa  kujiandikisha na kuwa kwao  wakulima  wanapotezewa  muda  mwingi .
  Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Deo Filikunjombe ambae alifika  kujiandikisha akizungumza  mara  baada ya  kujiandikisha alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.
  “Mimi kama mbunge wajimbo la Ludewa leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata kitambulisho changu cha kupigia kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza wote bila kukosa ili kuweza katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha mpiga kura kitawasaidia kwa mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi ambaye mliniamini na mkanichagua kuwa mwakilishi wenu”,alisema Filikunjombe.
  Hata  hivyo  aliipongeza  NEC kwa  kufanya kazi kwa ratiba  na  kuwataka  kuendelea  kuifanya kazi hiyo kwa kuzingatia  muda  zaidi  ili  kuwawezesha  wananchi  kwenda katika  shughuli  nyingine za uzalishaji mali.
  Pia  alisema  kuwa  propaganda za  kuwa  vidole  vyenye  sugu mashine  haisomi   kuwa  hazina  ukweli kwani yeye  ni mbunge  mwenye sugu  katika  vidole pamoja na  wananchi wake  ila hakuna aliyelalamika  kushindwa  kujiandikisha  kwa ajili ya tatizo la  sugu .
  Alisema kama mtanzania unapaswa kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika kuipigia kura ya ndiyo katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi mnaowataka ifikapo oktoba mwaka huu.
  Filikunjombe aliyasema hayo katika kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.
   
  Zoezi la  kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limeanza tarehe 16/3/2015 litadumu katika  wilaya hiyo na nyingine kwa muda wa  siku saba kabla ya  kwenda  mikoa mingine ya  Katavi,Ruvuma,Lindi  na Mtwara .zinafanya kazi  vizuri hata kwa  wale  wenye vidole  vyenye sugu.

  Kauli  hiyo  imetolewa  juzi  na kamishina  wa  tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC)  Prof Amone Chaligha wakati akizungumza na  wanahabari  nje ya  kituo  cha kuandikishia  wapiga kura cha Ludewa Shuleni wilani  Ludewa mara baada ya  mbunge wa jimbo  la  Ludewa  Deo  Filikunjombe na msimamizi wa  zoezi  hilo wilayani Ludewa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo  kumaliza  zoezi la  kujinadikisha .
  Alisema  kuwa kasoro za mashine za BVR ambazo awali zilikuwa zikisumbua  kutosoma alama za vidole  kwa baadhi ya watu hasa  wale  wenye sugu kwa  sasa kasoro  hizo  zimekwisha baada ya wataalamu wa mifumo ya Kompyuta kuzifanyia kazi ili  kufanya kazi kwa mazingira  yoyote yale .
  Prof.Chaligha alisema kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani zoezi hilo wilayani Ludewa litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo zoezi litahamia maeneo mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha  wala  kuhofu  mashine  kutofanya kazi .
  Alisema tokea zoezi hilo lianze wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama ilivyokuwa mji wa Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya kujipatia kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.
  “ Ni  kweli  siku  mbili tatu kasoro  za  sugu  katika  vidole  lilikuwa ni  shida  ila  wataalam wa IT  walilifanyia kazi na kwa  sasa  hakuna  kasoro kama  hizo na kuwa amepata  kuzungukia  vituo mbali mbali mjini Ludewa na  vijijini kasoro kama  hiyo haipo  tena kwa  sasa  hata  wakulima  wanajiandikisha bila shida   
  Kuhusu  kasi  ndogo  ya  uandikishaji  alisema  imechangiwa na waandikishaji  wenyewe kuwa na kasi ndogo na kuwa kimsingi  kila mwananchi  anapaswa  kujiandikisha kwa dakika 3 hadi 4  na  kuwa kwa  siku moja mashine  inauwezo wa kuandikisha  kiwango  cha chini kabisa ni kati ya  watu 50 -80
  Hata  hivyo alisema  wanaofanya kazi  hiyo  ya uandikishaji  ni  wale ambao wanataaluma ya IT na  walifanyiwa mchujo na  wale  walioshindwa waliachwa  hivyo  wamejipanga  kuna kazi hiyo  inafanikiwa vilivyo.
  Awali wakazi  wa Ludewa mjini  waliokutwa  kituoni  hapo  walielezea kero  kubwa ya  kukaa kwa muda mrefu  kituoni hapo  bila ya  kujiandikisha kwa madai ya  watoa huduma   hiyo  kufanya kazi kwa kasi ndogo  zaidi alisema mmoja kati ya  wakazi hao Bw  Ernest Yohana  .
  Alisema  kwa upande wake  alifika kituoni hapo  toka majira ya saa 4 asubuhi na  kukaa kwenye foleni  hadi saa 9 ;30  alasiri  alipofanikiwa  kujiandikisha na kuwa kwao  wakulima  wanapotezewa  muda  mwingi .
  Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Deo Filikunjombe ambae alifika  kujiandikisha akizungumza  mara  baada ya  kujiandikisha alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.
  “Mimi kama mbunge wajimbo la Ludewa leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata kitambulisho changu cha kupigia kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza wote bila kukosa ili kuweza katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha mpiga kura kitawasaidia kwa mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi ambaye mliniamini na mkanichagua kuwa mwakilishi wenu”,alisema Filikunjombe.
  Hata  hivyo  aliipongeza  NEC kwa  kufanya kazi kwa ratiba  na  kuwataka  kuendelea  kuifanya kazi hiyo kwa kuzingatia  muda  zaidi  ili  kuwawezesha  wananchi  kwenda katika  shughuli  nyingine za uzalishaji mali.
  Pia  alisema  kuwa  propaganda za  kuwa  vidole  vyenye  sugu mashine  haisomi   kuwa  hazina  ukweli kwani yeye  ni mbunge  mwenye sugu  katika  vidole pamoja na  wananchi wake  ila hakuna aliyelalamika  kushindwa  kujiandikisha  kwa ajili ya tatizo la  sugu .
  Alisema kama mtanzania unapaswa kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika kuipigia kura ya ndiyo katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi mnaowataka ifikapo oktoba mwaka huu.
  Filikunjombe aliyasema hayo katika kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.
  Zoezi la  kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limeanza tarehe 16/3/2015 litadumu katika  wilaya hiyo na nyingine kwa muda wa  siku saba kabla ya  kwenda  mikoa mingine ya  Katavi,Ruvuma,Lindi  na Mtwara .
  Mwisho  0 0

   
  Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimekamilisha maadalizi ya kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo cha Takwimu cha nchini India.
   
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha EASTC Prof. Innocent Ngalinda amesema mkataba huo utasainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
   
  “Maandalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo cha Takwimu cha nchini India yamekamilika kwa kiasi kikubwa na ndio maana hapa mbele yenu mnamuona Naibu Balozi wa Ubalozi wa India hapa nchini amefika kwa ajili ya kujirizisha”, amesema Prof. Ngalinda.
   
  Prof. Ngalinda amesema kuwa mkataba huo una manufaa makubwa kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa wataalam wengi katika tasnia ya takwimu hapa nchini.
   
  Pamoja na ongezeko la watalaam wa takwimu hasa wakufunzi, kutakuwa na ukarabati wa miundombinu katika chuo hicho ambapo mabweni ya wanafunzi pamoja na ofisi za chuo hicho zitakarabatiwa.
   
  Prof. Innocent Ngalinda amefafanua kuwa katika mkataba huo, kutakuwa na mpango wa kubadilishana wanafunzi katika vyuo hivyo viwili ili kupanua uelewa wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi zaidi katika masuala ya kitakwimu.
   
  Kwa upande wake Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal amefurahishwa na maandalizi yaliyofanyika na kusema kuwa nchi yake iko tayari kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu kutoka chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na chuo cha Takwimu cha nchini India.
   
  “Nimefurahishwa na maandalizi yaliyofanyika katika chuo hiki na sasa tunamsubiri Waziri wa mambo ya Nje wa nchini India kwa ajili ya kutiliana saini ya mkataba huu ifikapo tarehe 28 Machi, 2015,” amesema Naibu Balozi Humpal.
   
  Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam na chuo cha Takwimu cha India vimekuwa vikishirikiana tangu mwaka 2012 lakini ushirikiano huo haukuwa rasmi hivyo vyuo hivyo vimeamua kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili kufanya ushirikiano huo kuwa rasmi.
   
   
  Na Veronica Kazimoto,
  Dar es Salaam,
  17 Machi, 2015.
   

  0 0

  Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

  NASHAWISHIKA kusema kwamba baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali katika wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, hawanazo kichwani. Na kama wanazo, basi wamegubikwa na maslahi zaidi. Wameshindwa kusimamia mambo yenye tija kwa wananchi na wakazi wao wilayani Handeni.

  Ndio hawanazo. Maana yapo mapungufu ya wazi ambayo kwa mtu mwenye akili hawezi kuyaacha yashamiri. Mtu mwenye nazo kichwani, atayafanyia kazi matatizo yanayowahusu watu, ukizingatia kwamba ndio kusudio la uwapo wake kwenye nafasi nyeti za serikali, kama ardhi, maji, afya, kilimo na mengineyo muhimu.

  Baadhi ya mambo hayo hayahitaji hata elimu ya kidato  cha nne kubaini mapungufu. Ni kutokana na hilo, nadiriki kusema viongozi wa serikali wamenyamaza, wakiwa na lengo la kuona Handeni inamwaga damu kutokana na migogoro ya ardhi.

  Katika kila kijiji cha wilaya ya Handeni kina migogoro mikubwa ya ardhi. Hali hiyo inatia hofu. Migogoro hiyo ni ile inayohusisha wakulima na wafugaji, wakulima wadogo na wafanyabiashara waliopewa jina la madalali wa ardhi, ama mipaka inayohusisha vijiji, bila kusahau wilaya kwa wilaya katika baadhi ya maeneo.

  Na migogoro hiyo imekuwa kero kiasi cha kuwafanya wananchi wakose imani na viongozi na watendaji wa serikali katika maeneo yao. Wanafanya hivyo kwa sababu kero zao hazitatuliwi.

  Kilio cha wananchi kimeendelea kuwa cha samaki, machozi yanakwenda na maji. Hii n hatari. Tulipofikia ni kubaya na wakati wowote wananchi wataanza kupigana.

  Watamwaga damu kama wanavyomwaga damu katika maeneo mengine ya nchi. Ajabu, licha ya wakulima na wananchi kulalamikia suala hilo, lakini hawasikilizwi. Watendaji wa serikali wamebakia kuwatumikia wenye nazo. Wanachumia tumbo.

  Machaguo yao ya kwanza ni wafugaji wakiamini kuwa watalipwa fedha au rushwa ya wanyama, kama vile ng’ombe, mbuzi na kondoo. Ama wale wakulima wakubwa wenye nazo. Hao ni rahisi kwenda Polisi na kupata askari wa kuongozana nao eneo la tukio kwa ajili ya kuwaogopesha wananchi.

  Hakuna haki anayeipata mlalahoi. Katika vijiji 112 vya wilaya ya Handeni hakuna kilichokuwa na ahueni. Huko watendaji wa vijiji baaadhi yao wamekuwa madalali wa kuuza ardhi. Na wenyeviti wengi wamefikia kughushi mihutsari inayogawa ardhi kwa wafanyabiashara bila kuangalia sheria ya ardhi.

  Kesi nyingi zipo kwenye makaratasi. Hazisikilizwi kwa wakati. Na zikisikilizwa, basi mwenye nazo anapewa haki wakati mkulima mdogo akiendelea kulia bila kupata msaada wowote.

  Kwa mfano, katika Kata ya Kwamatuku, kijiji cha Komsala na Kwamatuku ambayo ni kata zipo kwenye mgogoro mkubwa mpaka uliosababisha ardhi kuporwa na kupewa mwekezaji anayejulikana kwa jina la Optimal. Shamba hili la Optima limechukua eneo kubwa, kiasi cha kuingia hadi Komsala bila kufuata sheria. Hapo hujaugusa mgogoro wa mpaka wa wilaya ya Korogwe uliyoingia hadi karibu na eneo la kijiji cha Komsala. Korogwe wameamua kujenga mnada wa ng’ombe katika eneo la kijiji cha Komsala.

  Aidha katika kijiji hicho pia kuna mivutano ya wenye nazo kupewa mashamba makubwa hali ya kuwa walalahoi wameachwa mikono mitupu. Hakuna kinachowafanya waendelee na kulima. Ardhi kubwa inamilikiwa na wenye nazo.

  Yupo mwanamama anayejulikana kwa jina la Amina Singa ambaye licha ya kuwa na eneo linalozidi heka 120 bila kujua sheria iliyompa ardhi hiyo, lakini bado ameingia kwenye maeneo ya wakulima wadogo wanaomiliki heka nne hadi tano.

  Huu ni zaidi ya ufisadi. Na kesi kama hizi hazitoi haki kwa masikini, wakiumizwa na msemo usemao mkono mtupu haulambwi. Kwa ujumla, kata zote za Handeni hususan zile za vijijini ni migogoro iliyostawishwa na viongozi. Katika Kata ya Misima ambayo leo inaitwa Mabanda ni mtihani mzito.

  Licha ya kesi kusikilizwa kwenye Baraza la Ardhi la wilaya Korogwe kutokana na Handeni kutokuwa na Baraza hilo, lakini bado wakulima wadogo wanakamatwa na kufunguliwa kesi katika mahakama ya mwanzo wilayani Handeni.

  Hii hutokea kinyume cha sheria. Hakuna sababu ya kufungua kesi mpya wakati kesi kama hiyo haijapatiwa ufumbuzi. Katika mgogoro mkubwa unaomuhusisha Michael Panga maarufu kwa jina la NADA katika Kata hiyo na wananchi ni unyanyasi mtupu.

  Kumbukumbu za kiofisi zinaonyesha NADA aliazimwa alime katika shamba ambalo uongozi wa mtaa wa Kwedigongo, kijiji cha Misima kwa kupitia mwenyekiti wake Idd Kisege, waliamua kuichota aradhi hiyo kwa ajili ya kupewa wakulima wadogo.

  Jambo hilo lilimfanya NADA akimbilie kwenye Baraza la Ardhi Machi 4 na kupewa Stop order, ambapo kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa mwezi Aprili mwaka huu. Kumbukumbu zinaonyesha waliopokea barua ya Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Korogwe ni pamoja na Mkurugenzi, Mkuu wa wilaya, OCD, OCS, Katibu Tawala Sindeni na WEO Kata ya Mabanda.

  Kama hivyo ndivyo, nani ameruhusu kumkamata Idd Kisege ambaye ni mwenyekiti wa Mtaa wa Kwedigongo na kumfungulia mashtaka wakati kesi kama hiyo itasikilizwa mwezi wa nne?

  Hii ni aibu kubwa. Viongozi na watendaji wa serikali wanaendelea kuikalia vikao migogoro ya ardhi kwa nia ya kuvuta posho na si kuchukua hatua kwa maslahi ya wananchi na wakazi wa Handeni. Wananchi wapo mashakani.

  Serikali inashindwa nini kuchukua hatua? Serikali hii sikivu inasubiri damu kumwagika? Kila uchao wananchi wanalalamika. Huko kwenye mabaraza la ardhi ya Kata ni mtihani mzito.

  Kumekuwa na kesi nyingi kiasi kwamba wajumbe hao wanashindwa kuyatatua, huku kelele za ugumu wa maisha na ukosefu wa weredi katika kuendesha kesi zenye utata zikiwagubika.

  Hii ni hatari kubwa. Wakati wowote damu itamwagika Handeni. Wakati wowote wananchi watatoana roho. Hii ni kwa sababu viongozi wao wamekosa busara.

  Viongozi wao wamekuwa wachumia tumbo. Wameona kwenye migogoro ya ardhi ndio mahali wanapoweza kuvuna fedha chafu kutoka kwa walalamikaji au walalamikiwa.

  Wakati hayo yakiendelea kutokea, wananchi nao wameanza kujiandaa kwa heri au kwa shari. Wameanza kunoa silaha zao, wakiamini kuwa yatakapotokea machafuko waweze kujihami.

  Vijana wanaharakati wamekuwa wakishawishiana namna bora ya kujihami dhidi ya kadhia ya ardhi. Swali la kujiuliza, unawezaje kumiliki heka 100 wakati wananchi wenyewe hawana hata robo heka kwa ajili ya kulima?
  Je, muhutsari wake unasemaje? Sheria gani imeruhusu kutoa ardhi kubwa kwa mtu bila kuangalia kitu wanachoweza kunufaika wananchi katika eneo hilo? Huu ni wizi na ufisadi.

  Ni wakati wa wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao wa vijiji kupambana usiku au mchana kuzikomboa ardhi zao. Waanze kuwanyang’aanya wale wote wenye ardhi inayozidi heka 50 na waliopewa bila kufuata sheria.

  Watu hao wapo wengi mno. Wamekwenda vijijini na visenti vyao kwa ajili ya kuwarubuni wakulima na viongozi wa vijiji ambao mwisho wa siku wametoa haki zao kwa matapeli hao.
  Hii haiwezi kukubalika. Wananchi wasikubali kupoteza haki zao za msingi, kama ardhi ambayo ndiyo inayoweza kuwapatia mwangaza wa kimaisha na kiuchumi.

  Haiwezekani kundi kubwa la wananchi likose mahala kwa kulima, wakati mtu mmoja ana heka zaidi ya 100. Mbaya zaidi amezipata kiwizi wizi, akishirikiana na viongozi wa vijiji wasiokuwa waaminifu.

  Ni wakati huu wa Mkuu mpya wa Wilaya ya Handeni, Husna Rajab, akaliangalia suala hilo kwa mapana yake. Hatuwezi kulalamikia ugumu wa maisha kwa wananchi wetu, wakati fursa zinazotoa ajira kama kilimo hazifanyiwi kazi kutokana na nguvu kazi kubwa kukosa eneo la kulima.

  Tunaweza kupiga soga sana. Tunaweza kulala katika majumba na ofisi za umma, lakini lazima tufahamu kwamba damu inaweza kumwagika wakati wowote, chanzo kikiwa ni migogoro ya ardhi isiyopatiwa ufumbuzi na inayochochewa na viongozi wezi, watendaji mafisadi waliokubali migogoro iwe njia ya kuwapatia rushwa kubwa na ndogo kwa manufaa yao binafsi.
  kambimbwana@yahoo.com+255712053949
  Mwisho

  0 0

  Moses Mashalla,Arusha

  Baadhi ya watumishi katika hoteli yenye hadhi ya nyota nne ya Snowcrest Hotel ya jijini Arusha wameushutumu uongozi wa hoteli hiyo kwa kushindwa kuwalipa mishahara yao tangu mwezi Januari hadi sasa.

  Pia wameiangukia serikali  kwa kuitaka iingilie kati suala hilo kwa kuwa pamoja na kuwasilisha madai yao katika idara mbalimbali za serikali mkoani hapa lakini hadi sasa wameshindwa kupatiwa ufumbuzi wa madai yao.

  Hoteli hiyo ni ile ambayo ilizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete  mwaka 2009 na kisha kuvunjwa ghafla na Wakala wa barabara mkoani Arusha(Tanroads) baada ya ukuta wake kudaiwa kujengwa katika eneo la hifadhi  ya barabara ya Arusha-Moshi.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti watumishi hao kwa sharti la kutotajwa majina yao hadharani kwa sababu za kiusalama walidai kuwa uongozi wa hoteli hiyo umeshindwa kuwalipa mishahara yao tangu mwezi Januari hadi sasa.

  Wakiongea kwa nyakati tofauti na gazeti hili walidai kuwa kitendo cha wao kutolipwa mishahara yao kimechangia ukali wa maisha kwa kuwa baadhi yao wameshindwa kuwapeleka watoto wao mashuleni na hata kushindwa kumudu kulipia kodi za nyumba zao.

  “Tunadai mishahara yetu tangu mwezi Januari hadi sasa hatujalipwa na hali ni mbaya kwani  wengine tunadaiwa kodi za nyumba na  ada mashuleni sasa tutaishi vipi”walihoji kwa nyakato tofauti

  Hatahivyo,walisisitiza kwamba pamoja na kufikisha malalamiko yao mbele ya Chama Cha Wafanyakazi wa hifadhi ya mahoteli , majumbani ,huduma ya jamii na ushauri (Chodau) mkoani Arusha lakini hadi sasa suala lao halijaweza kupatiwa ufumbuzi wa kina na kuiomba serikali iingilie kati.

  Meneja wa hoteli hiyo,William Mollel alipotafutwa na gazeti hili alikiri kuhusu madai hayo na kudai kwamba kuyumba kwa biashara pamoja na janga la ugonjwa wa Ebola limechangia kwa kiasi kikubwa hoteli yao kushindwa kujiendesha kwa kuwa wamekosa wateja hususani raia wa kigeni.

  Naye,Katibu wa Chodau mkoani Arusha,Jeremiah Meliary alikiri watumishi hao kuwasilisha madai yao mbele ya chama hicho na kusisitiza kwamba wao waliyapeleka mbele ya tume ya Usuluhishi na Uamuzi(CMA) mkoani hapa ili yaweze kushughulikiwa.

  Hatahivyo,mkuu wa tume hiyo mkoani hapa,Sifuni Mnzava alipoulizwa juu ya suala hilo alisema kuwa apewe muda ili aweze kuwasiliana na maofisa wake ili kujua kama madai hayo yaliwasilishwa kwao au la.

  0 0

  TAREHE ya leo ni ndio aliyo zaliwa Mama mzazi wa Blogger na Mpigapicha nguli Tanzania, Mroki Mroki, Bi. Mary O.Nathan  (pichani) wa Kinyenze, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambaye leo anatimiza miaka 63 tangu kuzaliwa kwake tarehe kama ya leo. 
  Kipekee anamshukuru Mungu kwa kumjalia umri huo alionao hivi sasa. Anawashukuru wote ambao wamechangia yeye kuishi vyema. Anaishukuru sana Familia yake yote kwa umoja na upendo walio nao jambo mabalo anasema linamfanya aishi kwa furaha na amani. 
  Aidha watoto wake wote wanampa Pongezi za dhati na Kumuombea Mungu amjalie zaidi Afya njema, akimpa zawadi ya Hekima na Busara katika kipindi hiki cha maisha yake ya utu uzima ambao Busara yake na Hekima vinahitajika sana ndani ya Familia yake na Jamii kwa ujumla.
  Wajukuu zako na Vitukuu wako pia wanakusalimia sana na wanakuimbia kale kawimbo ka Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!!
  Happy Birthday Bibi!!! Dear Bibi Happy birthday to youuuuuuuu!!!!
  Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kinyenze ,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakutakia heri na fanaka.
  HAPPY BIRTHDAY MAMA TUNAKUPENDA SANA NA TUNAJIVUNIA KUWA NA MAMA WA NAMNA YAKO, MUNGU AKUJALIE HEKIMA NA BUSARA ZAIDI KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.
  BY: FAMILIA YAKO.

  0 0

  Na Bakari Issa,Dar es Salaam

  Naibu Kamanda wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),Wilaya ya Moshi vijijini,Innocent Melleck amempongeza Rais Jakaya Kikwete na Serikali kwa ujumla kwa kuwajali wananchi wa kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga waliopatwa na janga la kubomokewa na nyumba zao kutokana na mvua iliyoambatana na mawe makubwa na upepo mkali.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Melleck amesema kitendo cha Rais Kikwete kuahidi kuwajengea nyumba wananchi hao kinaonyesha namna anavyowajali wananchi hao.

  Melleck ambaye  amejitolea kuingia katika kinyanganyiro cha kuwania ubunge jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),amesema Serikali ya Rais Kikwete imewasaidia wananchi waliopatwa na majanga mbalimbali wakiwamo wananchi wa Mbagala na Gongo la Mboto waliolipukiwa na mabomu.

  Aidha,Melleck amewapongeza viongozi wa CCM kwa juhudi kubwa zinazofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Abrahamani Kinana na Katibu Mwenezi na Itikadi,Nape Nnauye ambao wamefanya kazi kubwa ya kuimarisha Chama huko mikoani na kuweza kuwa viongozi wa kwanza kuzunguka na kuwafikia wananchi.

  Pia,Melleck amesema viongozi wamekuwa kiungo kikubwa sana kwa vijana na kutoa mwanga mpya wa nafasi za vijana katika nafasi za uongozi kuwa kubwa pasipo kuwa na upendeleo wowote,na kusema kuwa juhudi na ushirikiano wao ndiyo unaoleta taa ya kijani kwa vijana kuanzia ngazi za chini hadi ubunge.
  Naibu Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Moshi vijijini, Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari.

  0 0

  6
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Mhe.January Makamba (kulia)pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe(kushoto) wakifurahi pamoja na Walimu na Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Dar es Salaam Independent nje ya Bunge mara baada ya kikao cha bunge, leo tarehe 18/03/2015 Mjini Dodoma.
  7
  Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.Aggrey Mwanri akijibu swali la Mhe. Dkt Festus Limbu Mbunge wa Magu,lilikuwa likihoji ni kiasi gani cha kodi ya Majengo kimekusanya katika kipindi cha miaka mine na nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2014/2015.
  1
  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Juma Nkamia akijibu swali la Mhe.Haroub Shamis Mbunge wa jimbo la Chonga kuhusu jinsi gani serikali inawasaidia waadishi kuandika habari za kibiashara,Mjini Dodoma.
  2
  Mhe.Victor Kawawa akichangia hoja juu ya Muswada wa sheria ya udhibiti wa Ajira za wageni wa mwaka 2014 uliyosomwa na Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka, leo tarehe 18/03/2015 bungeni Mjini Dodoma.
  3
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janet Mbene akijibu swali la Mhe.Philipa Mturano Mbunge wa viti maalum lililokuwa likihoji ni namna gani Serikali imejipanga kuthibiti biashara ya vyuma chakavu kutokana na kuwepo na wizi wa mabomba.
  4
  Waziri wa Kazi na Ajira Mhe.Gaudensia Kabaka akisoma muswada wa sheria ya Udhibiti wa Ajira kwa Wageni ya mwaka 2014 kwa mara ya pili ndani ya Bunge, leo tarehe 18/03/2015 Mjini,Dodoma.
  5
  Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya (kushoto) akizungumza naWaziri wa Habari, Wizara wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Fenella Mukangara nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kikao, Mjini Dodoma.


  0 0


  imagesAli Issa  Maelezo- Zanzibar
  Hakuna sababu itayoifanya Zanzibar kushindwa kuitumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia wanafunzi Skuli kwani Zanzibar inahazina kubwa ya watalamu na  ndio chimbuko la   Kiswahili katika Nchi za Afrika na Dunian kwa ujmlai.

  Hayo yamesemwa leo huko Eacrotanal Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Mohamed Seif Khatib  wakati wa ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Kiswahili Duniani yalio fanyika hapo.

  Amesema inawezekana kabisa na frusa hiyo ifanyiwekazi kwa kukaa pamoja Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja  na Wizara ya Habari UtAMADUNI Utalii na Michezo Zanzibar kuzipitia sera zilizo tangulia kulipatia mamuzi suala hilo. Amesema kunanchi nyingi tu duniani ambazo zinasomeshwa kwakutumia lugha zao na haijawa tatizo katika nchihizo.
  “Kuna nchi kama China,Uholazi na nyengnezo wanatumia furusa ya kusomeshea wanafunzi kupitia lugha zao,”

  Nae Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakar na Naibu Katibu Mkuu Wiara ya Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Zanzibar Issa Mlingoti alisema watakaa pamoja na wizara zao kulijadili suala hilo kwani hadi sasa kuna sera mbilizo pingana.
  Wamesema wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wao wamelikubali hilo kuwa wanafunzi wafundishwe kupitia lugha ya Kiswahili la kini Wizara ya Elimu wao wanalipinga,hivyo watakaa pamoja na kusawazisha ili waendesambamba na wezao wa Tanzania Bara.

  Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) pia mjumbe wa baraza la kiswahili Zanzibar Mmanga M. Mjawiri amesema kuna umuhimu mkubwa wanafunzi Skuli wafundishwe kupitia lugha yao ya kishwahili kwani kiengereza Tanzania bado kikwazo. Hakuna masiliano mazuri kati ya walimu na wanafunzi wakati wa kufundisha hivyo Kiswahili ndio suluhisho la wanafunzi kumuelewa mwalimu.

  0 0

  3
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya kutengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu, Kaono Yono baada ya kuzungumza na viongozi wa kampuni hiyo . Kampuni hiyo   nashirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)  katika  suala la ufundi na vifaa, wakati alipotembelea Ofisi za Kampuni hiyo jijini Tokyo Machi 18, 2015. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya NEC Kaono Yono.
  4
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akigana na Rais wa Shirika la Misaada la Kimataifa la Japan (JICA), B.  Akihiko Tanaka baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo Machi 18, 2015
  5
  Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akizungumza na Mbunge wa Bunge la Japan kutoka Chama Tawala cha Liberal Democratic Party, Koya Nishikama (katikati) kwenye Ofisi za Bunge la Japan jijini Tokyo Machi 18, 2015. Wengine pichani ni maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Japan.
  1
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake wakizungumza na  Viongozi wa kampuni ya Japan ya  kuengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu ya NEC  ambayo inashirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)  katika  suala la ufundi na vifaa, wakati alipotembelea Ofisi za Kampuni hiyo jijini Tokyo Machi 18, 2015. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya NEC Kaon Yono.
  6
  Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akiagana na Mbunge wa Bunge la Japan kutoka Chama Tawala cha Liberal Democratic Party, Koya Nishikama  baada ya mazungumzo yao kwenye Ofisi za Bunge la Japan jijini Tokyo Machi 18, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  unnamed 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wapya wa wilaya aliowateua hivi karibuni baada ya kufungua semina elekezi ya uongozi mjini Dodoma jana katika ukumbi wa St.Gaspar..Wengine katika picha walioketi mbele ni Waziri wa TAMISEMI Mh.Hawa Ghasia(Watatu kushoto),Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh.Aggrey Mwanri(Wapili kulia),Katibu Mkuu TAMISEMI Bwana Jumanne Sagini(kushoto), Mwenyekiti wa wakuu wa mikoa ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro(wapili kushoto), na watano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa(picha na Freddy Maro)

  0 0

    Mkurugenzi wa kampuni ya 4Beli, Gilbert Herman (kulia) akihutubia wakati uzinduzi wa mashindano ya  Mbio Ndefu ya Bagamoyo Historical Marathon 2015 yanatarajiwa kutimua vumbi Juni 14 mwaka huu mjini Bagamoyo Mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Bagamoyo, Pwani leo. Wengine kutoka kushoto ni, Kaimu Ofisa Michezo Wlaya ya Bagamoyo, Hamisi Kimenya, Mwenyekiti wa Riadha Tanzania Mkoa wa Pwani, Joseph Luhende na Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Hudumaza Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Eliudi Eliakimu aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo katika uzinduzi huo.
   Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Hudumaza Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Eliudi Eliakimu aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo katika uzinduzi huo akisoma hotuba ya mheshimiwa waziri.

   Kaimu Ofisa Michezo Wlaya ya Bagamoyo, Hamisi Kimenya (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon yanaandaliwa na kampuni ya 4Beli ya jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti chama cha Riadha Mkoa wa Pwani, Joseph Luhende (wa pili kushoto) akizungumzia maendeleo ya riadha katika mkoa huo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mbio Ndefu ya Bagamoyo Historical Marathon 2015 yanatarajiwa kutimua vumbi Juni 14 mwaka huu mjini Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua taarifawakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon mjini Bagamoyo, Pwani leo.

  0 0

  4
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akielezea mambo mbalimbali yahusuyo ardhi na mipangomiji kwawatendaji wa Mkoa wa Arusha(hawapo pichani) alipozungumza nao kwenye hoteli ya Naura Springs Arusha jana. Waziri Lukuvi amesisitiza nidhamu ya kazi na kufuata sheria katika kuhudumia wananchi masuala yahusuyo ardhi.
  5
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akikabidhiwa makabrasha yenye kero mbalimbali za ardhi zilizowasilishwa kwake kwa ufasaha mkubwa na Mkoa wa Arusha kupitia Mpima Ardhi wa Mkoa wa Arusha Bw. Hamdoun Mansoor.
  6
  Mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe. Goodluck Ole Medeye naye alikuwepo hoteli ya Naura Spring kuzungumzia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi kwenye mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
  7
  Mbunge wa Arusha Mhe. Godbless Lema naye alikuwepo hoteli ya Naura Spring kuzungumzia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi kwenye mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
  8
  Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari naye alikuwepo hoteli ya Naura Spring kuzungumzia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi kwenye mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
  9
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda akiwakemea watendaji wa ardhi Mkoani Arusha kutokana na umangimeza wao unaowafanya kushindwa kutatua kero za ardhi na kusababisha migogoro mingi ya ardhi mkoani humo. Alisema maafisa ardhi na mipango miji wanalalamikiwa sana na wananchi.
  10
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akiongea na waandishi wa habari katika eneo lenye mgogoro wa ardhi lililoko mpaka wa Longido, Monduli na Arumeru eneo la Oldonyosambu Arusha. Waziri ameahidi kukutana na wanasiasa wa Mkoa wa Arusha ili kumaliza mgogoro huo.
  New Picture
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akionyeshwa na Mpima Ardhi wa Mkoa wa Arusha Bw. Hamdoun Mansoor ramani yenye mipaka katika maeneo yanayobishaniwa kwenye mgogoro wa ardhi kati ya Wilaya za Arumeru, Monduli na Longido.
  1
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akiingia jengo la Utawala la Mkoa wa Arusha ili kukutana na Uongozi wa Mkoa huo kupata taarifa ya Mkoa inayohusu migogoro ya ardhi.
  2Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akipokelewa na Uongozi wa Mkoa wa Arusha alipowasili kufanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za ardhi zilizoko katika Halmashauri mbalimbali za Mkoa huo.
  3
  Baadhi ya watendaji na viongozi mbalimbali wa Halamashauri za Mkoa wa Arusha wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alipowakutanisha katika Hoteli ya Naura Springs kuzungumzia kero na migogoro ya ardhi katika mkoa huo kwa nia ya kuipatia ufumbuzi wa haraka.

  0 0

  3
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mafunzo ya wakuu wa  wilaya wapya yanayofanyika katika ukumbi wa hosteli ya St.Gaspar mjini Dodoma leo jioni.Kushoto ni Waziri wa TAMISEMI Mh.Hawa Ghasia,Watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa na kulia ni Naibu waziri TAMISEMI Mh.Aggrey Mwanri
  12
  Baadhi ya wakuu wa wilaya wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo kwa wakuu wapya wa wilaya mjini Dodoma leo jioni. (picha na Freddy Maro)

  0 0

  002
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kufungua rasmi Kituo cha Taifa Cha Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini Dodoma leo.
  003
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia jalada la mwaka 1940 ambapo alisoma utendaji kazi wa Babu yake Chifu  wa Kabila la Wakwere Mrisho Kikwete wakati huo.Jalada hilo ni moja ya majalada ya zamani yaliyohifadhiwa kutumia teknolojia ya kisasa katika Kituo Cha Taifa Cha Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini Dodoma.Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa kituo hicho Rais Kikwete ametoa agizo la kuanzishwa maktaba za Viongozi wa kitaifa hususan marais wastaafu ili kuhifadhi vyema historia ya nchi.
  001
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Taifa Kumbukumbu huko kisasa mjini Dodoma leo.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, watatu kushoto ni Mwenyekiti wa BungeMh. Zungu na kulia ni Waziri wan chi Ofisi ya Rais Utawala BoraMh.George Mkuchika. (picha na Freddy Maro)

  0 0

  Mfanyabiashara mashuhuri katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,Vicent Laswai akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofsi za Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
  Mfanyabiashara Vicent Laswai akijadiliana jambo na Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) ,Erastus Rufungulo kabla ya kuaza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro. kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya Topi Raisen Richard Mardai 
  Mfanyabiashara Vicent Laswai akiwa na Mhifadhi mkuu KINAPA ,Erastus Rufungulo wakati akifanya maandalizi ya Kupanda Mlima Kilimanjaro ,shoto mwa Laswai ni Charity Githinji meneja masoko wa Kibo Palace. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Tuhakikishe ushindi unarudi nyumbani!!! Mpigie kura Mayunga Tuma SMS yenye neno YUN kwenda 15594 au Piga 0901002233 kisha chagua 1 #‎TeamMayunga #‎AirtelTRACEStar.

  Video link, Instagram: https://instagram.com/p/0XCapjGBUb/?taken-by=airtel_tanzania

  0 0

  WAANDAAJI wa Tamasha la Pasaka wamemualika Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi kushuhudia tamasha la mwaka huu.
   
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa wamemualika Mzee Mwinyi kwa sababu ana historia kubwa na tamasha hilo.“Mzee mwinyi alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha letu la kwanza, hivyo tumemualika aje aone vijana wake tunavyoendelea baada ya kutupa baraka wakati huo.
   
  “Bado hatujapata majibu, lakini naamini yatakuwa mazuri na atakuja kama mgeni wetu, maana tumealika wageni wengi sana wakiwemo viongozi wastaafu, viongozi wa sasa na makundi mbalimbali ya kijamii,” alisema Msama katika taarifa hiyo.
   
  Mwaka huu Tamasha la Pasaka linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam na limekuwa likijiongezea umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa kiroho kupitia matamasha hayo.
   
  Umaarufu wa matamasha hayo pamoja na mambo mengine, unatokana na ukweli kuwa yamekuwa yakifanyika kwa ubunifu na umakini mkubwa huku kila mwaka yakiongezeka na kubadili waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi.
   
  Baadhi ya nyota waliowahi kutumbuiza katika matamasha hayo ni marehemu Angela Chibalonza kutoka Kenya, nguli wa kutoka Afrika Kusini, Solly Mahlangu ‘Obrigado’, Sipho Makhabane na Rebeka Malope.
   
  Wengine ni Ephraim Sekeleti kutoka Zambia, Ambassadors of Christ (Rwanda), Faraja Ntaboba na Solomoni Mukubwa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), 24 Elders  (Uganda) na Anastazia Mukabwa (Kenya).

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Al-Shaymaa Kwegyir, akizungumza na wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki hawapo pichanai, katika kongamano la kujadili nini kifanyike kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) lililofanyika jana chuoni hapo. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Keto Mshigeni na Kulia ni Kokushubika Kairuki.
   
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  MBUNGE wa Viti Maalum ambaye pia ni mlemavu wa ngozi (albino), Al -Shaimaa Kweigyir, amekemea vikali unyanyapaa unaofanywa na baadhi ya Watanzania juu ya jamii yenye ulemavu wa ngozi na kusema kwamba inawafanya watu hao waishi kwa unyonge.

  Mbunge huyo aliyasema hayo jana katika kongamano la kujadili nini kifanyike ili kutokomeza mauaji na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa walemavu wa ngozi llilofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo wanazuoni.
  Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Al-Shaymaa Kwegyir, katikati akiwa kwenye kongamano la wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki kujadili nini kifanyike kutokomeza mauaji ya albino. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Keto Mshigeni na Kulia ni Kokushubika Kairuki.

  Akizungumzia unyanyapaa huo, Shaimar alisema kwamba bado baadhi ya wana jamii wamekuwa wakiendeleza vitendo vya unyanyapaa vinavyofanywa na watu ambao wamekuwa na mtizamo hasi juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

  Alisema kwamba jamii ikielimika na kutambua haki sawa kama walivyokuwa nazo wao juu ya ndugu zao albino, hata mauaji yatapungua kama sio kwisha kabisa, hususan kwa kuhakikisha kwamba wanawalinda na kuwathamini wakati wote.
  Mbunge wa Viti Maalum CCM, AL Shaimaa Kweigyir kushoto akizungumza na Kokushubika Kairuki katika kongamano hilo lililohudhuriwa na watu mbalimbali.
  Baadhi ya wahudhuriaji wa kongamano hilo wakisikiliza mada zilizokuwa zinazungumzwa.
  Watu wanasikiliza kwa makini katika kongamano hilo la kujadili juu ya mauaji ya albino yanayoendelea kutokea hapa nchini.

  “Wapo watoto wanaozaliwa katika hali ya albino ambao wamekuwa wakiishi kwa mashaka makubwa kutokana na unyanyapaa dhidi ya jamii nyingine ambayo ukiangalia kwa kina hakuna tofauti yoyote kati ya albino na wengineo.

  “Naomba jamii ione albino ni watu kama wao kwa kuhakikisha kwamba wanawathamini, wanawajali na kuwalinda wakati wote, huku wakianzia kwenye uondoaji wa fikra mgando na unyanyapaa wanaofanya kwa baadhi ya kaya,” alisema.

  Mbunge Shaimar ni miongoni mwa viongoz wa serikali waliojiweka busy katika kutafuta mbinu za kuweza kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino yanayoendelea kutokea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

older | 1 | .... | 487 | 488 | (Page 489) | 490 | 491 | .... | 1897 | newer