Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 485 | 486 | (Page 487) | 488 | 489 | .... | 1898 | newer

  0 0

   WANANCHI  wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro wakiwamo wajasiliamali wadogo wamechangishana shilingi milioni tisa na kumkabidhi Naibu  Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Innocent  Melleck  kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao.

  Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye mji mdogo wa himo baadhi ya wananchi hao Halid Msango,Jonas Mamuya na Aisha Mkwizu walisema kwa pamoja wananchi wa jimbo la Vunjo bila kujali itikadi zao za vyama wamemchangia kiasi hicho cha fedha ili kimsaidie kuchukulia fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda utakapofika.
  unnamed Katika tukio hili tumeshiriki wananchi wa jimbo hili la Vunjo kwa umoja wetu bila kujali itikadi za kisiasa ambapo hapa pia wapo wanachama wa vyama vya NCCR Mageuzi,TLP,CHADEMA na CCM  soote tumeshiriki katika kuchanga fedha hizi lakini pia wapo makundi mbalimbali kama vile mama lishe, madereva wa Bodaboda, wauza mboga, na vijana wengine wanaofanya biashara ndogondogo na wapiga debe kwenye vituo vya mabasi ya daladala.

  Aidsha wananchi wao waliafikiana kuunda kamati ya kuzunguka jimbo zima kuhakikisha kuwa wanakusanya fedha za michango na kuhamasishana kwaajili ya kuhakikisha Melleck anapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
  Katika kamati hiyo mwenyekiti ni Mzee shayo na katibu wa mwika kuwa katibu huku katibu kata kata ya kilema kusini Shabani Kwezi kuwa mjumbe na wajumbe wawili toka kila kata za jimbo hilo hivyo kuwa na jumla ya wajumbe 36 katika kamati hiyo ambayo ilianza majukumu yake mara moja.

  Alisema zoezi hilo liliongozwa na zaidi ya wajumbe 1000 wa nyumba 10 wa CCM na kumtaka, Melleck kuchukua fomu ya kuwani nafasi hiyo ya uwakilishi katika uchaguzi ujao.
    Kwa upande wake Bwana Melleck aliwashukuru wananchi hao kwa ujasiri mkubwa na Imani kubwa walioonyesha kwake , nimefarijika sana kuona wananchi wenye kipato kidogo cha fedha wanachanga kiasi hiki cha fedha na kunikabidhi ili nichukulie fomu na mimi naahidi kutowaangusha kwa hilo, nitafanya hivyo muda ukifika,” alisema .


  Alisema jimbo la Vunjo linakabiliwa na changamoto nyingi hususan ukosefu wa ajira kwa vijana na kukosa mtetezi wa asilimia tano ya mapato  yatokanayo na Mlima Kilimanjaro ili yarudi kwa wananchi, Matatizo ya kielimu na maslahi ya walimu,Migogoro ya ardhi na miundombinu kuwa itakuwa kipaumbele chanya mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo mapema mwezi octoba mwaka huu.

  Melleck ambaye ni kijana alisema kwa umoja ulioonyeshwa na wana Vunjo anaamini kwamba utaendelea hivyo hivyo mpaka uchaguzi utakapomalizika na kuhakikisha CCM inashinda. Alisema amejiandaa kufanya mengi katika jimbo la Vunjo na kwamba njia pekee ya kupita ili kupata ushindi ni kuwashirikisha wananchi wote kwa kuwa anaamini kwamba jimbo hilo litakuwa huru kufungua fursa za kuichumi ikiwa atakuwa mwakilishi wake bungeni.

  “Vunjo kuna utajiri mwingi na kinachotakiwa ni mtu mwenye maono ya kuona fursa ili aweze kuwashirikisha wananchi kuzifikia kwa ajili ya maendeleio yao na watoto wao,” alisema .
    Melleck aliongeza kuwa wananchi wanayo nafasi ya kuona na kuwachuja wagombea wote ili waweze kupata mtu sahihi atakayeweza kuwavusha hapo walipo na kusonga mbele kwa manufaa ya wana Vunjo wote.

  0 0

   Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya NSSF Media Cup 2015, yaliyoanza kulindima katika viwanja vya Sigara, Chang’ombe Dar es Salaam leo asubuhi.
    Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akihutubia baada ya kufungua mashindano hayo.
   Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa mashindano hayo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Ludovick Mrosso, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF, Abubakar Rajab, Mkurugenzi Rasilimali Watu, Chiku Matessa na Mkurugenzi wa Uthamini na Usimamizi wa Hadhara, Sadi Shemliwa.

   Kikosi cha Timu ya Free Media kilichofungua mashindano hayo kwa kucheza na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC.
   Kikosi cha Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kilichomenyana na Free Media na kuibuka washindi wa bao 1-0 na kuendelea na mashindano hayo.
   wadau wa michezo wakifuatilia mashindano hayo.
   Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), akiwasalimia wachezaji wa timu ya Netball ya NSSF.
   Wachezaji wa timu ya Netball ya NSSF wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga.
  Mchezaji wa timu ya Free Media, Moses Magwai (kushoto), akimtoka Shaban Kassim wa TBC wakati wakimenyana leo viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam.

  0 0

  KAMA MNAVYOWATAMBUA #AKCLASSIC WAO NI MWENDO WA VITU VYA UKWEE NA ORIGINAL KABISA..

  SASA MALI MPYA IMEINGIA #TEAMNATURALHAIR MPOO? SAFARI HII HAMJASAHAULIKA!!

  PIA KUNA HABARI NJEMA KWA WADAU WOTE WANAOSUMBUKA NA MATATIZO MBALI MBALI KUHUSU NGOZI ZAO KAMA VILE KUUNGUA KWA MIKOROGO,WEUSI WA MACHONI(DARK CYCLE),KUSWEAT KULIKOPITILIZA,AKCLASSIC WAMEAMUA KUCHIMBA NA KUJA NA MAJIBU YA MATATIZO YENU TENA MADINI YASIYO NA MADHARA KABISAAA KWA NGOZI YAKO!!

     WALE WALIOTOKA KUJIFUNGUA NA YALE YOTE YATOKANAYO HATUJAWASAHAU PIA KUANZIA CORSETS,NYWELE(T444Z JBCO NA HAIRFINITY),WEUSI WA KWAPA NA SHINGO NA OFCOUZ NA BIDHAA ZA KUKUPIGA  MSASA!!
   KWA PICHA ZAIDI NA MAELEZO INGIA

            www.akclassic.blogspot.com

  TUNAPATIKANA KINONDONI KWA AMANYANYA NA MLIMANI CITY KWA NJE. 
   TUPIGIE  TUPIGIE /0753482909
  BIDHAA ITAKUFIKIA UPOPOTE ULIPO!!
   

  0 0

  unnamed 
  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiongoza Kikao cha kawaida cha Baraza la Mawaziri leo Jumapili Machi 15, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.PICHA NA IKULU.

  0 0
 • 03/15/15--20:27: NesiWangu Show...Albinism
 • Karibu katika kipindi cha NesiWangu.
  Katika kipindi hiki, Harriet Shangarai amezungumza na wanaharakati wa masuala ya Albinism. Sehemu ya kwanza ni mazungumzo na Daisy Makwaia wa Albino Charity Organization na sehemu ya pili ni mazungumzo yao na mwanaharakati mwenye Albinism Babu Sikare wa Afrobino Ltd
  Karibu

  0 0

  More 1 of 272 Web Clip CNN.com Recently Published/Updated - Elton John's boycott of Dolce & Gabbana spreads - 2 hours ago IDD AZZAN ATOA MSAADA WA KITI CHA MAGURUDUMU KWA MLEMAVU JIMBONI KWAKE Inbox x zainul mzige 6:26 AM (1 minute ago) to bcc: me Habari za asubuhi, Tafadhali pokea CODES hapo chini 0D6A5197
  Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan akikabidhi kiti maalum cha kujisaidia pamoja na kiti cha magurudumu kwa mama huyo mlemavu.

  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan (CCM) ametoa msaada wa kiti cha magurudumu kwa Rehema Nditi mkazi wa Magomeni Mwembe Chai kama msaada kutokana na taabu aliyokuwa akiipata.

  Idd Azzan ametoa msaada … ambapo baada ya kuona Rehema Nditi kupataa tabu ya kukosa kiti hicho. Mbunge huyo amekua akisaidia maendeleo mbalimbali ikiwemo shughuli za kijamii ndani ya jimbo lake hilo.

  Aidha, Mh. Iddi Azzan ametoa rai kwa Watanzania kuungana nae katika kuchangia pesa kwa ajili ya kununua Bajaji ambayo itafanya biashara ili waweze kuendesha maisha ya kila siku.
  “Watanzania tuungane kumchangia mama huyu kiasi chochote ilikununua bajaji kwa ajili ya kufanya biashara ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku kupitia kipato cha biashara hiyo ya Bajaji” alieleza Idd Azzan.

  Kwa upande wake, Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania, Kinachoerushwa na kituo cha Channel Ten, Hoyce Temu amefungua michango hiyo kwa kutoa kiasi cha Tsh. 500,000/- ili kuhamasisha na wengine kuchangia.

  Michango hiyo inaweza kuwasilishwa kwenye ofisi za Mbunge wa jimbo la Kinondoni ama unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Rehema Nditi kupitia namba TIGO PESA +255 719-543075 AU M-PESA +255 754 097 527
  0D6A5129

  0 0

    Mwanahabari Frank Kibiki, aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec.
  Wananchi wa manispaa ya iringa wamempongeza , Frank Kibiki kwa kuanzisha mashindano ambayo yalengo la kuwataka wakazi wa mkoa wa iringa kujua kuwa albino ni binadamu kama binadamu wengine hivyo tunatakiwa kuacha kuwauwa na kuwa nyanyasa kijinsia.

  Wakizungu kwa nyakati tofauti na blog hii wamesema kuwa wazo la mbunge mtarajiwa la kutoa elimu ya kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino)  kwa njia ya michezo yatawasaidia wakazi wa manispaa kwa kuwa wananchi wengi wanapenda michezo hivyo itakuwa rahisi kuwafikia.

  Pia walimtaka FRANK KIBIKI kuendelea na harakati za kupigania na kuwania ubunge wa jimbo la iringa mjini kwa kuwa anakila sababu ya kufanya hivyo kutokana na malengo pamoja na msimamo anaouonyesha kwa wakazi wa manispaa.
   Kwa upande wao viongozi wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)  mkoani iringa wamempongeza na kumuomba katika mashindano hayo wanaomba timu yao ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)kuwa moja kati ya timu itakayoshiriki katika mashindano hayo.

  “Tunaomba nasi kushiriki katika mashindano hayo ya Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 kwa kuwa ujumbe wa mashindano hayo unatulenga sisi, hivyo haitakuwa busara mashindano yaendelee bila sisi kuleta timu uwanjani”walisema viongozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

  viongozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) waliwataka wananchi wa manispaa ya iringa kumuunga mkono frank kibiki katika harakati zake za kugombea ubunge wa jimbo la iringa mjini kwa kuwa anaoneka kabisa kuwajari wananchi wenye kipato kidogo tofauti na wale wagombea wengine ambao wanatumia pesa nyingi kuutaka ubunge wa jimbo hilo.

  Walimalizia kwa kusema kuwa kesho watapeleka barua maalum kwa frank kibiki ya kumpongeza na kuwaomba wananchi wengine kumuunga mkono kibiki ili kuyafanya mashindano hayo kuwa bora zaidi.

  Naye Kibiki ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili kusaidia kuibua vipaji na kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.
  Alisema tayari shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi hilo, ambalo watoto wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao wenyewe watajiongoza.

  lakini kibiki hakusita kuwashukuru viongozi wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi(albino)mkoani iringa kwa kutambua lengo lake japo bado ajaletewa rasmi barua hiyo ya pongezi kwa naye amesikia tu kwa wananchi wakimshukuru kwa elimu na ujumbe aliouweka katika mashindano yake.

  Kwa upande wao wadau wa soka, manispaa yaa Iringa waliitaka serika kutambua mchango na kuwekeza kwenye soka ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea kuibu vipaji ikiwemo michuano ya watoto.

  0 0

  1
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mafia Dkt. Credianus Mgimba wakati alipokwenda kutembelea hospitali ya Wilaya, Kilindoni, kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi wa hospitali na kutembelea wagonjwa tarehe 14.3.2015. Aliyesimama katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Dkt. Nassor Ali Hamid.
  2
  Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya Wilaya ya Mafia wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati alipotembelea hospitali hiyo tarehe 14.3.2015.
  3
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Madaktari na wafanyakazi wengine wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia wakati alipotembelea hospitali hiyo kujionea shughuli mbalimbali za kitabibu zinazofanyika hospitalini hapo.

  4
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwangalia mtoto Naira Athuman aliyezaliwa tarehe 12.3.2015 katika hospitali ya Wilaya ya Mafia huku mama yake Fadhila Omar, mkazi wa eneo la Majengo, Kilindoni akiwa amempakata. Alisimama kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Zainab Vullu.
  5
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijiandaa kumchukua mtoto mchanga Sudi Ramadhani kutoka kwa mama yake akiwa ni mtoto wa tisa kuzaliwa kwa Mama Subira Haruni, 36, mkazi wa kijiji cha Mbwela, Kata ya Mbuchi katika wilaya ya Rufiji. Wakazi wengi kutoka maeneo ya Rufiji hasa waishio katika visiwa hupendelea kwenda Mafia kupata huduma za afya ambako ni karibu kuliko Utete.
  6
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Bibi Shamsa Bwaki huku akiwa amemshika mtoto wake aliyejulikana kwa jina la Mudhihir mwenye umri wa mwezi mmoja ambaye alionekana kama amezaliwa siku moja iliyopita. Hali hiyo ilipelekea Mama Salma kupitia ushauri uliotolewa na Dkt. Hadija Mwamtemi, ambaye ni daktari wake kuamuru mtoto huyo apelekwe Muhimbili leo hii kwa ndege ili akapatiwe matibabu ya haraka.
  8
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na akina mama, watoto waliokuwa maeneo ya hospitali ya Wilaya ya Mafia wakati Mama Salma alipotembelea hospitalini hapo tarehe 14.3.2015.
  9
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi, walimu na wananchi (hawapo pichani)  waliokuwa wamekusanyika katika Shule ya Sekondari Micheni iliyopo eneo la Kilindoni katika wilaya ya Mafia. Mama Salma alikwenda shuleni hapo kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi na walimu kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo ya shule hiyo.
  11
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi, walimu na wananchi waliokusanyika katika Shule ya Sekondari ya Micheni huko Mafia. Mama Salma alikuwa kisiwani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
  12
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari ya Micheni mara baada ya mkutano wake na wanafunzi wa shule hiyo tarehe 14.3.2015. Aliyekaa kulia kwa Mama Salma ni Mkuu wa Shule hiyo Ndugu Seif Mohamed Gadafi. Picha zote na John Lukuwi

  0 0  KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2015 imetangaza kiingilio cha chini kwa wakubwa katika tamasha hilo litakalofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni shilingi 5000.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Msama kiingilio kwa watoto watakaojitokeza kwenye onesho hilo watalipa shilingi 2000.

  Msama alisema VIP watachangia shilingi 10,000  na viti maalum watatoa shilingi 20,000.Msama alisema kuwa ameamua kuweka kiingilio kidogo ili iwe rahisi hata kwa walio na uwezo mdogo waweze kuhudhuria tamasha hilo.

  Tamasha hilo la mfano wake linalosubiriwa na wadau mbalimbali wa nyimbo za injili, litashirikisha wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili ndani na nje ya Tanzania.Aliwahakikishia usalama mashabiki wote wa muziki wa injili watakaojumuika kwenye tamasha hilo na kwamba usalama wa kutosha ambako alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi.

  Kupitia Tamasha la Pasaka Mwenyekiti huyo anawapa pole wakazi wa Mkoa wa Iringa kwa ajali iliyotokea wili iliyopita iliyohusiaha basi la Kampuni ya Majinjah na lori la mizigo na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 43.

  Ameongeza kuwa kupitia tamasha hilo anaendelea kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (albanism) na kulaani vikali unyanyasaji huo.

  0 0

  DSC_0015

  Mkufunzi ambaye pia ni mtaalamu mshauri wa Unesco, katika masuala ya utalii endelevu, James Banks akiendesha mafunzo kwenye warsha ya siku nne ya kutengeneza mkakati wa utalii endelevu hifadhi ya Ngorongoro iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha na kuandaliwa na Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA). Pichani chini kulia ni Mmoja wa wakufunzi wa warsha hiyo, Tamim Amijee.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

  Na modewjiblog, Karatu
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) likishirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wameandaa kongamano la siku nne lililofanyika mjini hapa kuangalia mkakati mpya wa kuendeleza utalii kama kitovu cha mapato katika hifadhi ya Ngorongoro. Kongamano hilo ni moja ya makongamano kadhaa ambayo yameandaliwa kwa pamoja kwa lengo la kutoa mwelekeo mpya katika hifadhi hiyo ambayo binadamu na wanyama huishi pamoja.

  Akizungumza na mtandao huu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, alisema kwamba kongamano hilo limeandaliwa kwa lengo la kujenga uwezo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kutambua haja ya utalii endelevu ambao pia utazingatia maslahi ya wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

  Alisema wakati NCAA inaangalia upya mkakati wake wa maendeleo katika hifadhi hiyo ambayo pia ni urithi wa dunia, UNESCO kama washirika wa karibu wamekubaliana kuendesha kongamano ambapo wadau wote kuanzia wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo na waendesha utalii zikiwemo hoteli na watawala kuangalia namna bora ya kuendesha hifadhi na kuneemesha wananchi.
  DSC_0207
  Zulmira alisema kwamba hifadhi hiyo inaingiza fedha nyingi ambazo zingeweza pia kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa kuanzisha mikakati ambayo inahusisha wananchi wenyewe na wadua mbalimbali wa sekta hiyo. Alisema kwamba idadi ya watalii wanaoingia hapo wanaingiza fedha nyingi serikali kuu lakini kiasi hicho hakionekani wazi wazi kwa wananchi na hivyo ipo haja ya kuangalia mwelekeo mpya ambao utaendelea kuhifadhi urithi huo huku wananchi wake wakifaidika na uwapo wa urithi huo.

  Wakati wa kongamano hilo washiriki walifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya kitalii kabla ya kufanya majadiliano na kuweka mwelekeo wa namna bora ya kutengeneza mkakati utakaoshirikisha wadau wote wa utalii katika eneo hilo. Alisema kwa muda mrefu tangu hifadhi hiyo iwe urithi UNESCO na NCAA walikuwa wakiangalia zaidi suala la hifadhi kiasi cha wananchi kuona kama wameachwa nyuma hivyo mkakati wa sasa ni kuwawezesha wananchi kufaidi matunda ya urithi huo kwa kila kada kupewa wajibu wake na kuona namna ya kuutekeleza ili ndoto iwe kweli.
  DSC_0030
  Mkufunzi ambaye pia ni mtaalamu mshauri wa Unesco, katika masuala ya utalii endelevu, James Banks akiwaelekeza jambo washiriki wa warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha.


  “Tumedhamiria kujenga uwezo… kusaidia wananchi kuongeza kipato chao kutoka kwa watalii … ukiangalia katika kreta unaweza kuona magari mengi yakiwa na watalii… tunataka watu wanaoishi katika eneo hili pia wafaidike …” alisema.Hifadhi hii inatambulika duniani kwa kreta yake kubwa, mbuga yenye wanyama wengi na eneo ambalo inasadikiwa binadamu wa kwanza aliishi kabla ya kutawanyika duniani Ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 8,300 Hifadhi ya Ngorongoro ndio hifadhi pekee duniani ambapo wanadamu wanaishi pamoja na wanyama kwa usalama.

  NCA ilianzishwa mwaka 1971na kutangazwa kuwa urithi wa dunia na UNESCO mwaka 1979 lakini kwa muda sasa kumekuwepo na mawazo kwamba dhima kubwa imekuwa kulinda wanyama na mazingira na kusahaua kwamba pale pana binadamu ambao wanamahitaji na wanataka kufaidika pia na mazingira ambayo wanayalinda.
  DSC_0164
  Pichani juu na chini ni washiriki na wadau wa sekta ya utalii kwenye warsha ya siku nne ya kutengeneza mkakati wa utalii endelevu hifadhi ya Ngorongoro iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha na kuandaliwa na Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA).
  Kwa mwaka zaidi ya watalii 450,000 huzuru Ngorongoro ikiwa ni asilimia 60 ya watalii wanaofika nchini.
  Mtaalamu mshauri wa Unesco, James Banks, ameelezea kufurahishwa kwake na kongamano hilo na kusema kwamba linatoa mwanya wa wadau mbali mbali muhimu Ngorongoro kuona mwelekeo mpya unaostahili kuchukuliwa ili kuwa na utalii endelevu.
  Alisema matokeo ya mkakati huo sio tu utaongeza mapato serikalini bali pia utaimarisha utalii kutokana na ushiriki wa moja kwa moja wa jamii zinazoishi ndani ya hifadhi hiyo.
  Mshiriki mwingine wa kongamano hilo Flora Assey, Afisa Utalii kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha alielezea kufurahishwa na kongamano hilo hasa kwa kuchukua mlengo wa masomo kwa vitendo hali ambayo anaamini itabadili kabisa utekelezaji wa mkakati unaobuniwa kwa sasa.
  DSC_0035
  Naye Meneja mkuu wa Ngorongoro Serena Safari Lodge, Dismas Simba alielezea kuridhishwa kwake na kongamano hilo na kusema litawezesha wadau wote kufanyakazi kwa pamoja kuhakikisha kwamba utalii unakuwa endelevu katika eneo hilo hasa kwa kuzingatia kwamba eneo hilo ndilo pekee duniani ambako wanyama na wanadamu wanaishi pamoja.
  Naye Ofisa Mwandamizi wa Miradi na Mratibu wa UNESCO katika masuala ya urithi wa dunia na utalii endelevu, Peter DeBrine amepongeza hatua iliyofikiwa na wadau katika kongamano hilo na kusema raundi ya pili Juni mwaka huu itatoa mwangaza zaidi kwani utarejesha majibu ya maswali ambayo kila mtu amepewa kuyafanyia kazi.
  Alisema amefurahishwa na kiwango cha kujituma cha wajumbe waliofika katika kongamano hilo na kusema kwa jinsi ilivyo mabadiliko yanayofikiriwa na NCAA yatafanikiwa ili wananchi nao wawe wanafaidika moja kwa moja na uwapo wa urithi huo wa dunia katika maisha yao.
  DSC_0042
  DSC_0233
  Flora Assey, Afisa Utalii kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha akinakili mambo muhimu wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya siku nne iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Kudu Lodge and Campsite iliyopo mji mdogo wa Karatu mkoani Arusha.
  DSC_0106
  Mwenyekiti wa Baraza la wakina Mama kata ya Oloirobi, Kijiji cha Mokilal mkoani Arusha, SEKETO OLDUMU akishiriki kwenye kikundi kazi wakati wa warsha ya siku nne ya kutengeneza mkakati wa utalii endelevu hifadhi ya Ngorongoro iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha na kuandaliwa na Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA).
  DSC_0057
  Meneja Mkuu wa Ngorongoro Crater Lodge | &BEYOND, Markus Schroeder (kulia) akishiriki kuchangia maoni wakati wa warsha ya siku nne ya kutengeneza mkakati wa utalii endelevu hifadhi ya Ngorongoro iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues.
  Kwa matukio zaidi bofya hapa

  0 0

  photo 4

  Pichani juu na chini ni baadhi ya majengo yaliyokamilika ya Shule ya msingi Kakuni yaliyojengwa na Waziri Mkuu Pinda kupitia michango ya wadau wa maendeleo.

  Na Andrew Chale wa modewji blog
  Kila mmoja wetu anatambua mchango mkubwa wa elimu hasa ile inayotolewa ikiwemo ngazi ya Awali, Msingi, Sekondari na elimu ya juu ikiwemo chuo. Pia katika hilo ni jamb la msingi sana na la maana hasa unapokumbuka mahala ulipopatia elimu husika. Mtandao huu wa Mo dewjii blog tunapenda kuungana na kumpongeza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa juhudi zake za dhati kabisa katika kuhakikisha shule yake aliyowahi kusoma hapo inasaidiwa na kufikia malengo yake.

  Waziri Mkuu alipaata elimu yake katika Shule ya msingi Kakuni. Kwa kusoma hapo darasa la kwanza hadi la nne. Lakini kwa mapenzi mema na juhudi za kutaka kuona watoto wa hali ya chini hasa wa wakulima wanapata elimu bora, kwa juhudi zake binafsi, ameweza kusaidia shule hiyo ikiwemo kutafuta wafadhili mbalimbali wa kuipiga tafu, akiwa kama Mizengo Pinda. Ambapo unaweza kusoma kiunganishi hichi hapa cha mtandao ili kusoma habari hiyo zaidi ya wadau kumuunga Waziri Mkuu Pinda katika kuisaidia shule ya Kakuni: http://dewjiblog.com/2015/03/11/japan-yachangia-sh-milioni-160-shule-ya-msingi-kakuni/
  photo 1
  Mtandao huu unapongeza juhudi hizo za Waziri Mkuu Mizengo Pinda hivyo pia nawe ukiwa ni miongoni mwa unayeguswa na maendeleo ya elimu hapa nchini, ni wakati wa kutembelea shule yako uliosoma awali iwe elimu ya ‘vidudu’ yaani Chekechea/Awali, Shule ya Msingi ama Sekondari basi ni wakati wa kurejea na kusaidia chochote kile ili kuendeleza Elimu hapa Nchini.


  Bila shaka kama Watanzania tutaiga juhudi hizi za Waziri Mkuu Mizengo Pinda, bila shaka elimu ya Tanzania itapanda maradufu kwani tumeweza kushuhudia kwa upande wa juhudi hizo za Mizengo Pinda ikiwemo kushawishi wadau ikiwemo Serikali ya Japan, kutoa msaada wa dola za Marekani, 90,286, ambazo ni sawa na Sh. Milioni 160. Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Awali kwenye Shule ya Msingi, Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi.
  PM-PINDA
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda.
  Juhudi za Mizengo Pinda za kuanzisha wazo hilo la kusaidia kuijenga shule yake ni kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo.
  Kwani alipata kusoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.
  Hivyo, tunatambua wapo wasomi wengi, wapo wabunge, wapo Mawaziri, wapo Wakurugenzi na wengine wenye vyeo vikubwa Serikali, sekta binafsi na waliopo ndani nje ya nchi, shime tujitokeze kwa wingi kwa kila mmoja kwenda kwenye shule aliyosoma na kuchangia chochote.
  Tunatambua sisi tumepata elimu wakati gani na kiwango cha elimu wakati huo kilikuwaje, hivyo tutakapojitokeza kama alivyofanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, hii itasaidia kukuza elimu yetu hapa Nchini.
  photo 3
  Muonekano wa majengo yaliyokamili ya shule ya msingi Kakuni alipopata elimu ya msingi Waziri Mkuu Pinda na kuamua kuijenga upya kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.3/- kutokana na michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo.
  photo 5

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Swissport Tanzania Bw. Gaudence Temu (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya utendaji wa kampuni yake mara baada ya mkutano mkuu wa kampuni hiyo kumalizika uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Pamoja nae kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Swissport, Bw. Juan Jose Andres Alvez na Bw, Jeroen L. de Clercq ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo nchini Kenya. 

  KAMPUNI ya Swissport Tanzania Plc imepata ongezeko la faida kwa asilimia 73 (baada ya makato ya kodi na gharama nyingine zote), mafanikio yaliyotokana na maendeleo makubwa ya Sekta ya Usafiri wa Anga hapa nchini.

  Kampuni hiyo  inayotoa huduma zake kwenye viwanja vya ndege vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro  pamoja na ule wa Mtwara, ilitangaza mafanikio hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake mkuu  wa thelathini.

  Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Bw Juan Alvez alitaja sababu za mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa mashirika ya ndege yanayofanya safari zake katika viwanja vya ndege vya Tanzania na ongezeko la wingi wa safari kwa mashirika yaliyopo.

  “Ongezeko hili la asilimia 73 ni matokeo ya ongezeko la faida kutoka sh. bilioni 7.496 mwaka 2013 hadi kufikia sh. Bilioni 12.937 iliyoripotiwa  mwaka 2014,’’ alisema.

  Akifafanua zaidi Bw Alves alisema jumla ya abiria 1,111,156 walihudumiwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 23 ikilinganishwa na idadi ya abiria 905,347 waliohudumiwa katika kipindi cha mwaka 2013.

  Kufuatia mafanikio hayo ambayo pia yameonekana kwenye idara nyingine ikwemo ya ubebaji wa mizigo, Bw Alves alisema wana hisa wa kampuni hiyo  wana kila sababu ya kutabasamu kwa kuwa watapokea Sh287.50 ya gawio kwa kila hisa ikilinganishwa na sh 166.58 ya mwaka 2013 ili kuhakisi ongezeko hilo la asilimia 73.

  Akizungumzia uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo kwa 2014, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Gaudence Temu alisema kampuni hiyo ilifanikiwa kununua vifaa vya usaidizi ardhini (GSE) vyenye thamani ya sh. Bilioni 1.7huku akiongeza kuwa vifaa hivyo tayari vimeshafika na vimeanza kutumika.

  “Ongezeko lingine la sh. bilioni 2.7 katika uwekezaji  linatarajiwa kufanyika ndani ya mwaka huu na litahusisha mabasi mawili ya kubebea abiria katika viwanja vyetu sambamba na kifaa cha kupakia na kushusha mizigo mizito chenye uwezo wa hali ya juu,’’ alibainisha Bw. Temu.

  Kampuni hiyo inajumuisha pia wanahisa wa Kitanzania wapatao 11,500 ambao wanamiliki asilimia 49 ya hisa zote huku asilimia 51 zikiwa zinamilikiwa na kampuni ya Swissport International.


  0 0

  1
  Mwasibu wa Kampuni ya Nivanaa Quality service and catering, Bi.Magreth Tairo akizindua kampuni hiyo City Louge jijini Dar es salaam ambayo Kampuni hiyo inajishugusha na upikaji wa vyakula katika sherehe mbalimbali yenye makao yake makuu Kinnondoni Manyanya Dar es Salaam.
  2
  Wadau walioudhuria katika hafla hiyo wakifuatilia uzinduzi huo.
  3
  Timu nzima ya waanzilishi na wamiliki wa Kampuni ya Nivanaa Quality service and catering wakiwa kwenye picha ya pamoja.
  4
  Mwasibu wa Kampuni ya Nivaana Quality service and caterin, Bi.Magreth Tairo (wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.

  5
  Mwasibuwa Kampuni ya Nivaana Quality service and catering, Bi. Magreth Tairo.akiteta jambo na wadau wakati wa hafla hiyo.
  6
  Kushoto ni Mkurugenzi wa oasis of sivana tz ltd,Alfa Minga akiwa kwenye picha ya pamoja na Magreth Minga ambaye ni mkewe.
  7
  Timu nzima ya NIVANAA wakiwa kwenye picha ya pamoja.na familia yao wakati wa hafla hiyo iliofanyika jijini dar es salaam hivi karibuni.
  8
  Wageni waalikwa.
  Endelea kuangalia picha za tukio hilo
  91011
  14
  Hii ni moja wapo ya bidhaa zinazotengenezwa na Kampuni ya Nivaana Quality service and catering.
  1213
  1516

  0 0


  1.DHAMANA NININI.

  Dhamana ni hatua ambapo mtu ambaye tayari ni mtuhumiwa wa kosa fulani huachiwa huru kwa muda ili kusubiri hatua za kufikishwa mahakamani au kama tayari amefikishwa mahakamani husubiri kuendelea kwa kesi yake. Kwahiyo ili lije suala la dhamana ni lazima uwe umetuhumiwa polisi au tayari umefikishwa mahakamani. Ieleweke kuwa kuna aina kuu mbili za dhamana. Kwanza dhamana ya polisi na pili dhamana ya mahakamani.Hapa tunazungumzia dhamana ya polisi.

  2.UKIOMBWA HELA KWA AJILI YA DHAMANA KATAA.

  Dhamana hutolewa bure. Ieleweke wazi kuwa hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa ili mtuhumiwa au mshtakiwa akubaliwe dhamana. Mchezo huu wa kuomba hela ili mtu apate dhamana umetamalaki zaidi vituo vya polisi. Wewe kama raia unalotakiwa kujua ni moja tu kuwa hakuna sheria inayomtaka raia kutoa hela ili apate dhamana. Serikalini hakuna risiti ya malipo ya dhamana. Kama wewe utaamua kutoa hela hiyo ujue umetoa kwasababu zako lakini sheria iko hivyo.Ifikie hatua raia wajisimamie kwa kukataa kutoa hela kununua dhamana.

  Hakuna kitu ambacho askari anaweza kukufanya ikiwa utakataa kutoa hela kwa ajili ya dhamana. Hakipo kabisa kinachohitajika ni ujasiri wako tu kwa kumwambia askari kwamba sikupi hela kwakuwa dhamana hainunuliwi. Usikubali kutoa hela kwa ajili ya dhamana ndugu ni kosa na hela hizo ni rushwa. Na hiyo ni kwa dhamana zote ya polisi pia ya mahakamani. Katika taratibu za kupata dhamana hamna kulipa hela.

  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Tobacco Lifes Company TLTC na Tanzania Tobacco Procesing Company TTPL wakishindana kunywa soda na kula mkate wakati wa bonanza la siku ya familia iliyofanyika Morogoro..
  Wafanyakazi wa kike wa kampuni ya Tanzania Tobacco Lifes Company TLTC na Tanzania Tobacco Procesing Company TTPL wakishindana kuvuta kamba wakati wa bonanza la siku ya familia iliyofanyika wiki iliyopita katika viwanja vya Magadu
   Wafanyakazi  wa kampuni ya Tanzania Lefes Tobacco Company TLTC na Tanzania Tobacco Procesing Company TTPL wakishindana kukuna nazi wakazi wa bananza la siku ya familia ya kampmuni hizo yaliyofanyika wiki iliyopita katika viwanja vya magadu Manispaa ya Morogoro.  Manispaa ya Morogoro.
  Mkurugenzi wa sheria na mahusiano wa kampuni hizo Richard Sinamtwa akiwasalimia watoto wa wafanyakazi wakati wa bonanza la siku ya familia lililofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya magadu manispaa ya Morogoro. Picha na Hamida Shariff, Morogoro
  Morogoro.Wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Lifes Tobacco TLTC na Tanzania Tobacco Procesing  TTPL wametakiwa kudumisha michezo mbalimbali baada ya saa za kazi ili kujenga mahusiano mema baina yao pamoja na kuwa na afya bora.
  Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi wa Sheria na mahusiano wa kampuni hizo Richard Sinamtwa wakati akifungua bonanza la siku ya familia kwa wafanyakazi wa kampuni hizo lililofanyika katika viwanja vya Magadu, Maniaspaa ya Morogoro.
  Sinamtwa alisema kwa kutambua michezo ni muhimu sehemu za kazi hivyo uongozi wa kampuni hizo uliamua kutenga siku ya maalumu kwa ajili ya bonanza la wafanyakazi.
  Alisema kuwa bonanza hilo pia linashirikisha watoto wa wafanyakazi hao ambao nao wamekuwa wakicheza michezo mbalimbali na hivyo kufahamiana na kujenga urafiki.
  Hata hivyo aliwataka wafanyakazi hao kudumisha suala la usalama kazini ili kuepuka na majanga na ajali zinazoweza kutokea kazini endapo suala la usalama kazini halitazingatiwa.
  Pia aliwataka wafanyakazi kujituma, kudumisha uadilifu, uaminifu na kuongeza ufanisi wa kazi ili kampuni hizo ziweze kuongeza uzalishaji.
  Naye Mwenyekiti wa bonanza hilo Dkt. Mose Makawu alisema kuwa siku hiyo ya familia kampuni hizo zimekuwa zikitoa zawadi kwa wafanyazi bora na waliofanyakazi kwa muda mrefu na kwa uadilifu.
  Dkt. Makawu alisema kuwa kampuni hizo pia zimekuwa zikitoa zawadi kwa watoto wa wafanyakazi walioshinda kwenye michezo mbalimbali.
  Kwa upande wake mfanyakazi bora wa kampuni hiyo Mhina Katongo alisema kuwa siri kubwa ya yeye kuwa mfanyakazi bora ni kujituma na uadilifu hivyo aliwataka wafanyakazi wenzake kufanyakazi kwa kuzingatia maadili na pia kudumisha nidhamu ya kazi.

  0 0

  KAMPUNI tanzu ya Bharti Airtel inayoongoza katika utoaji wa huduma za
  simu za mkononi ikifanyakazi katika nchi 20 Asia na Afrika, leo
  imemteua Balozi Juma Volter Mwapachu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
  Wakurugenzi ya Airtel Tanzania.

  Balozi Mwapachu ni Katibu Mkuu aliyepita wa Jumuiya ya Afrika
  Mashariki, nafasi aliyoishika kati ya Aprili 2006 na Aprili 2011.
  Kabla ya uteuzi huu, Mwapachu alikuwa Balozi Mwakilishi Ufaransa na
  UNESCO.

  Mwapachu ni mhitimu wa shahada ya sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  (UDSN). Pia ni mhitimu wa Diploma ya Juu ya Sheria ya Kimataifa,
  Masuala ya Diplomasia ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Sheria za
  Kimataifa na Diplomasia huko New Delhi, India.

  Pia ana shahada mbili za heshima katika fasihi na sayansi ya siasa za
  UDSM na Chuo Kikuu cha Taifa Rwanda.

  Akizungumzia uteuzi huo, Christian de Faria, Ofisa Mtendaji Mkuu wa
  Airtel Africa, alisema: “Ni faraja kwetu Balozi Mwapachu kuiongoza
  Bodi yeti ya Wakurugenzi nchini Tanzania. Uzoefu wake mkubwa utaongeza
  thamani kubwa kwa Bodi yetu na kutoa miongozo bora ya kimkakati katika
  shughuli zetu nchini Tanzania. Tunaamini pia kuwa atadumisha mahusiano
  na wadau mbalimbali nchini.”

  Kwa upande wake, Balozi Mwapachu alisema: “Ninaipokea kwa heshima
  kubwa fursa hii ya kujiunga na Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel, na, kwa
  pamoja na wajumbe wenzangu wa Bodi hii ya wakurugenzi wa Airtel,
  tutashirikiana  kujenga kampuni thabiti yenye misingi imara ili
  kuendelea  kutoa huduma bora ya mawasiliano nchini Tanzania.


  “Sekta ya mawasiliano ina mchango mkubwa katika kukua kwa uchumi wetu
  ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wananchi kila mahali. Pia ukuaji wa
  teknolojia ya hali ya juu na ubunifu katika masoko ikisaidiwa na mfumo
  mzuri wa usimamizi wa sekta hii ni dhahiri kutakuwa na uwezekano kwa
  sekta hii ya mawasiliano  kuendelea kutoa mchango mkubwa zaidi katika
  maendeleo ya taifa.”

  Balozi Mwapachu ana uzoefu mkubwa katika masuala ya kuongoza bodi
  mbalimbali kwani amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya
  Rasilimali Tanzania (TIB) na Shirika la Reli Tanzania (TRC). Pia
  alikuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya East African Breweries
  Limited, Kenya.

  Kwa sasa yumo katika bodi kadhaa za taaasisi binafsi ndani na nje ya
  nchi. Ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo Kikuu cha Dodoma
  (UDOM). Uzoefu wake wa kiuongozi katika mashirika na sekta binafsi
  Tanzania na eneo la Afrika Mashariki utaleta  tija katika uongozi wake
  wa Airtel Tanzania.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dk. Gration Kamugisha (kulia) akielezea juu ya Taasisi hiyo juu ya utendaji wa kazi zake hapa Nchini, kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa ya Lindi, Amida Abdala

  Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dk. Gration Kamugisha (kulia) akielezea juu ya Taasisi hiyo juu ya utendaji wa kazi zake hapa Nchini, kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa ya Lindi, Amida Abdallah na pichani chini kulia ni Mstahiki Mstahiki Meya wa manispaa ya Lindi, Frank Magali.
  UTT-PID
  Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi, wakiendelea na mafunzo hayo kutoka kwa maofisa wa UTT-PID (hawapo pichani)
  Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi, wakiendelea na mafunzo hayo kutoka kwa maofisa wa UTT-PID (hawapo pichani).

  Baadhi ya Madiwani kutoka Halmashahuri ya Lindi wakifuatilia mafunzo ya elimu juu ya ufanyaji wa kazi wa UTT-PID
  Baadhi ya Madiwani kutoka Halmashahuri ya Lindi wakifuatilia mafunzo ya elimu juu ya ufanyaji wa kazi wa UTT-PID.
  Baadhi ya Wahandisi wa Halmashahuri ya Manispaa ya Lindi wakifuatilia mafunzo hayo ya UTT-PID
  Baadhi ya Wahandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakifuatilia mafunzo hayo ya UTT-PID.
  Diwani akifuatilia mafunzo ya UTT-PID
  Diwani akifuatilia mafunzo ya UTT-PID.
  madiwani wa Manispaa ya Lindi wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID jijini Dar es Salaamk
  Madiwani wa Manispaa ya Lindi wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID jijini Dar es Salaam.
  madiwani wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID uliokuwa unafanyika jijini Dar es Salaam
  Pichani juu na chini ni madiwani wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID uliokuwa unafanyika jijini Dar es Salaam.
  madiwani wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID
  madiwani wa Manispaa ya Lindi wakiendelea kufuatilia mkjutano huo wa UTT-PID
  Mdiwani wakiendelea na mfunzo haayo ya UTT-PID
  Madiwani wakiwa kwenye mafunzo hayo ya UTT-PID.

  Na Andrew Chale wa Mo dewji blog
  Madiwani wa Manispaa ya Lindi wapo jijini Dar es Salaam katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo mbinu iliyo chini Wizara ya Fedha (UTT-PID), iliyopo jijini Dar es Salaam na nje ya Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kuelewa utendaji wa kazi wa taasisi hiyo hapa nchini.

  Katika ziara hiyo inayotarajia kumalizika Machi 19, mwaka huu. Mapema leo Machi 16, Madiwani hao wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaaa ya Lindi, Frank Magali waliweza kupatiwa elimu juu ya utendaji kazi wa taasisi hiyo ya UTT-PID na miradi inayoendesha hapa nchini.

  Miongoni mwa elimu hiyo ni pamoja na ufanyaji wa kazi wa UTT-PID na wadau wanaoshirikiana nao huku hadi sasa ikiwa inasimamia miradi mbalimbali ikiwemo mikoa ya Pwani, Morogoro, Kagera, Dar es Salaam, Lindi na mikoa mingine hapa nchini.

  Awali akiwakaribisha madiwani hao wa Manispaa ya Lindi, Mkurugezi Mkuu wa UTT-PID. Dk. Gration Kamugisha alieleza kuwa, UTT-PID imekua ikifanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa Siasa, wananchi, wadau na wabia binafsi pamoja na serikali katika kutekeleza mipango yake.

  “Karibu sana UTT-PID, miradi yetu tunafanya kwa kushirikiana na watu mbalimbali. Wakiwemo wanasiasa, ndio maana leo tupo nanyi Madiwani ambao munawawakilisha wananchi huko munako toka” alieleza Dk. Gration Kamugisha.

  Aiadha, kwa upande wa Madiwani hao walipongeza UTT-PID kwa hatua hiyo ya kuwapa elimu sambamba na kutembelea baadhi ya miradi inayoendeeshwa na taasisi hiyo.

  0 0

   Sijambo la ajabu kwa wasomaji wa habari za kila siku kujikuta wakichagua baadhi ya kurasa au kutilia maanani zaidi habari za aina fulani, na hapa ina maana kuwa kuna vichwa vya habari vitakavyo wavuta kusoma habari yake mwanzo hadi mwisho.

  Harakati za kutetea haki za watoto na wanawake ndio eneo langu. Ndio maana habari hii haikunipita, habari iliyoandikwa kwenye habari iliyoandikwa kwenye gazeti la the Guardian,  na nitaandika sehemu ya habari hii ili nanyi msome:
  “’Nilipokuwa mdogo sana mama yangu alinipeleka nikafanyiwe ukeketaji na sikugundua hadi nilipofika umri wa miaka mitano, pale nilipoanza kupata matatizo ya kwenda haja ndogo, hali ambayo huwa inawapata wasichana na wanawake wengi waliokeketwa,’ anasimulia  Jazira.”
  And somewhere else in that story the journalist, Rose Mwalongo  as she recounts the story of  Jazira Ramadhani, now a mother of three, she wrote:“’I really don’t know what my father told my aunt I can only guess he mentioned my problem to her and a few days later, I was sent for yet another mutilation to supposedly heal my ailment.’”
  Students in Singida in a rally to demonstrate their feelings against FGM--Photo from IPP Media
  I read that story to the end, wondering why this practice never seems to go away, despite interventions from many activists and the government. But at the same time I was thinking of how I could influence more reporting of this dangerous ritual. I was looking for ways be a catalyst for have more journalists keep stories of women like Jazira in the media or simply find ‘rewards’ for  reporters like Rosemary so that they keep writing.
  Then I learnt that every year on International Women’s Day, Women Deliverhonours different organisations, people or groups who work tirelessly to deliver for women and girls across the globe. It turned out that this year Women Deliver chose to honour journalists. You should have seen me frantically searching for relevant details to fill nomination forms for Rosemary
  Today I am happy to report here that Women Deliver has announced the honoured 15 journalists and Rose’s name was selected  as well, from a pool of 100 journalists nominated by Women Deliver partners around the world.  
  Awesome!
  Next step is now crucial. We all need to vote for Rose so that she emerges among top 3 who will receive a scholarship to attend  the Women Deliver 2016 Conference in Copenhagen, Denmark. Voting closes on March 20th. SoVOTE NOW and spread the word.
  For more information, and to read Rose’s and other contestant’s profile click here.
  ACT NOW  by voting for this champion for our mothers and babies. Deadline is March 20

  0 0

  indexNa Kijakazi Abdalla- Maelezo Zanzibar
  …………………………………………..Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo amesema hospitali za Zanzibar hazifanyi biashara ya vipimo vya aina yoyote katika maabara zake bali huwataka wananchi kuchangia kwa baadhi ya vipimo hivyo na kupewa risiti mara baada ya kuchangia huduma hiyo.

  Hayo ameyaeleza wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Mhe. Jaku Hashim Ayoub katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi huko Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja.

  Amesema kuwa ipo haja kwa wananchi kudai risiti ya malipo wakati wanapochangia huduma hiyo ili iwe ndio uthibitisho wa malipo hayo na endapo ikitokea kwa mwananchi yoyote kutopewa risti hiyo kwa ajili ya huduma aliyochangia anatakiwa kutoa taarifa kwa uongozi wa hospitali aliyolipia au kutoa taarifa kwa watendaji wa wizara hiyo.

  Aidha amesema kuwa uongozi wa Wizara hiyo hauna taarifa juu ya kuwepo kwa wizi wa baadhi ya vifaa vya matibabu na kuuzwa kwa wananchi kutoka kwa watendaji wa wizara hiyo hivyo amesema Wizara yake italifanyia kazi tatizo hilo ipasavyo ili kulipatia ufumbuzi unaofaa na kuwataka wananchi kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa pindi wanapobaini kuwepo kwa tatizo hilo kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.


  Wakati huohuo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kuwa kupitia Wizara yake ya Biashara, Viwanda na Masoko inafanya juhudi za makusudi kwa lengo la kuwasaidia Wajasiriamali kuweza kuuza bidhaaa zao katika masoko ya ndani na nje Nchi.

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi huko Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja, wakati akijibu swali la mwakilishi wa nafasi za wanawake Mhe. Shadya Mohammed Suleiman.

  Mhe. Kisasi amesema Wizara yake imekuwa ikichukuwa juhudi mbalimbali katika kuzitafutia masoko ya nje bidhaa zinazozalishwa Zanzibar, juhudi hizo ni pamoja na kutumia soko la Jumapili ambalo lilianzishwa rasmi huko Pemba kwa Wajasiriamali wanaouza bidhaa zao ndani ya Kisiwa cha Pemba.

  Aidha amesema kuwa Soko hilo lina jumla ya vikundi 28 hadi sasa ambavyo vinashiriki kikamilifu katika maonyesho mbalimbali ya biashara pamoja na kuandaa na kuratibu ushiriki Wajasiriamali wa Zanzibar katika maonesho hayo na Matamasha ya Biashara ya ndani na nje ya Zanzibar.

  Hata hivyo Naibu Waziri huyo amesema kuwa katika maonesho ya Sabasaba yaliyofanyika Mwaka jana jumla ya wajasirmali 48 kutoka Zanzibar walishiriki maonyesho hayo ambapo wajasiriamali 19 kutoka Pemba na 29 kutoka Unguja, pamoja na hayo juhudi hizo zimeshaanza kuzaa matunda na wajasiriamali wameanza kupata masoko zaidi kwa kwa ajili kuuza bidhaa zao.

  0 0


  1
  Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ally Idd akisalimiana na wasanii wakati akiwasili katika uwanja wa Amani Zanzibar kw ajili ya ufunguzi wa Tamasha la wasanii la kuimarisha uzalendo Tanzania.
  2
  Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif ally Idd akizungumza katika tamasha la wasanii ambapo aliwataka kutumia karama zao kuhamasisha uzalendo kwa watanzania hasa katika kipindi hiki cha kuelekea upatikanaji wa Katiba Mpya pia kutumia nafasi yao katika jamii kuelimisha jamii kuisoma na kuielewa Katiba Inayopendekezwa ili kuona ni jinsi gani imegusa maisha ya watanzania ili waweze kufanya uamuzi sahihi wakati wa kupiga kura ya maoni.
  3
  Msanii wa kizazi kipya nchini Nickson Simon a.k.a Nikki wa pili akizungumza kwa niaba ya wasanii na kueleza ni jinsi gani haki za wasanii zimetambuliwa kwa mara ya kwanza katika Katiba Inayopendekezwa, wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
  4
  Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif ally Idd.

  5
  Msanii wa Kizazi kipya kutoka Zanzibar Jamila Abdallah (Baby J) akitumbuiza wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
  6
  ‘Zuwena Mohamed A.KA. Shilole akitumbuiza wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
  7
  Nikki wa pili akipagawisha maelfu ya mashabiki waliohudhuria Tamasha hilo.
  8
  Wasanii wa kundi la Navy Kenzo wakiwa jukwaani wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
  9
  Vijana waliohudhuria tamasha hilo wakisoma Kijarida cha maudhui ya Katiba Inayopendekezwa kilichoandaliwa kwa lugha nyepesi wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar.
  ………………………………………………………………………………….

  Watanzania wameaswa kuisoma ili waweze kuielewa Katiba Inayopendekezwa na kufanya uamuzi sahihi wakati wa kuipigia kura ya maoni.Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Idd wakati wa Tamasha la kuhamasisha uzalendo lililofanyika Zanzibar Machi 7, 2015.
   Balozi Seif alisema kuwa huu ni wakati wa Watanzania kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kuona ni jinsi gani haki za makundi mbali mbali katika jamii zilivyoainishwa na namna watakavyonufaika“natoa wito muisome Katiba Inayopendekezwa ili kuona jinsi haki za makundi mbalimbali katika jamii zilivyoanishwa na muweze kutumia fursa hiyo kufanya maamuzi sahihi wakati wa kuipigia kura ya maoni wakati utakapofika” Alisema Balozi Seif.

  Aidha Balozi Seif alisema kuwa huu ni wakati wa wasanii kutumia nafasi yao katika jamii kuelimisha juu ya maudhui ya Katiba Inayopendekezwa kwa kutumia kazi zao za sanaa.
   Akiongea kwa niaba ya wasanii katika Tamasha hilo msanii wa kizazi kipya Nickson Simon a.k.a Nikki wa Pili alisema kuwa wasanii wamefarijika sana hasa baada ya Katiba Inayopendekezwa kutambua haki za wasanii kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.

  Nickson aliongeza kuwa walianza mchakato wa kupigania haki za wasanii kwa kutoa maoni wakati wa Tume ya warioba lakini hazikuingizwa katika Rasimu iliyotolewa na tume hiyo hivyo kuwabidi kupeleka maoni yao kwenye Bunge Maalum la Katiba na hatimaye zimejumuishwa ndani ya Katiba Inayopendekezwa.

  “Baada ya haki za wasanii kutokuwepo kwenye Rasimu ya Katiba iliyotolewa na tume ya Jaji warioba wasanii tuliamua kwenda kupeleka maoni yetu kwa mara nyingine kwa mwenyekiti wa Bunge Maalum na baada ya kutoka kwa Katiba hii Inayopendekezwa haki za wasanii zimeweza kutambulika”. Alisema Nickson.

  Tamasha hilo linadhumuni la kuhamaisha uzalendo kwa watanzania hasa kwenye masuala ya kitaifa ikiwemo mchakato wa upatinaji wa Katiba Mpya na uchaguzi Mkuu

older | 1 | .... | 485 | 486 | (Page 487) | 488 | 489 | .... | 1898 | newer