Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 476 | 477 | (Page 478) | 479 | 480 | .... | 1897 | newer

  0 0

    Mkurugenzi wa tigo nyanda za juu kusini, Jackson Kiswaga akikabidhi moja ya bati alizotoa kwa shule mbalimbali za jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa

  NA DENIS MLOWE, IRINGA.


  WANANCHI wa jimbo la Kalenga wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu, badala ya kujikita kuchangia sherehe za harusi na mambo mengine yasiyokuwa na tija katika maendeleo ya jimbo hilo.


  Hayo yamezungumzwa na mdau wa maendeleo, Jackson Kiswaga wakati akikabidhi mabati 50 na mifuko ya saruji 30 kwa shule ya sekondari ya Nyabula inayomilikiwa na kanisa katoriki parokia ya Nyabula katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa maabara ya Shule hiyo iliyoko katika wilaya ya Iringa vijijini.


  Kiswaga alisema kuwa urithi pekee kwa watoto ni elimu hivyo ni jukumu la wazazi kuchangia sekta ya elimu kuliko kusubiri serikali ambayo ina mzigo mkubwa kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo katika kukuza uwezo wa wanafunzi katika mambo ya masomo.


  “Mzazi unaweza kumwachia kijana wako mali, lakini itakwisha, ukimwachia elimu hakika huu ndiyo urithi pekee watanzania wenzangu, tujitoe kuchangia sekta ya elimu kama ambavyo tunafanya katika sherehe na kumbuka maisha ya sasa bila elimu utasababisha mwanao awe katika maisha magumu hapo mbeleni hivyo tusisubiri serikali tuwe na utamaduni wa kuchangia katika sekta hii ya elimu ndugu zangu,” alisema Kiswaga.


  Alisema kuwa juhudi za wananchi na mashirika pamoja na serikali zinahitajika ili kuwajengea wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia na ili waweze kufaulu vizuri katika masomo yao hivyo kuchangia maabara itasaidia sana kukuza uwezo wa mwanafunzi katika masomo ya sayansi pindi yakikamilika.


  Kiswaga aliongeza kuwa sekta ya elimu ni sekta muhimu sana kwa maendeleo ya nchi ambapo inabidi juhudi zaidi ziongezeke kuweza kuifanya elimu kuwa silaha bora itakayowasiadia  vijana kuondokana na umaskini.


  Naye Padri wa Parokia ya Nyabula Philipo Kindole alimshukuru Kiswaga kwa msaada wa mabati na saruji na kuwataka wananchi wengine kuiga mfano huo kwa maendeleo ya elimu katika mkoa wa Iringa.

  0 0

  ??????????
  Mkurugenzi wa kampuni ya vunja bei inayojihusisha na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya nyumbani Bw.Shija Ulaya Kamanija akimkabidhi zawadi ya dinner set Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Felix Ntibenda jana kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa mkuu wa mkoa huo ambapo pia aliwapatia watumishi zawadi ya chupa ya chai na vikombe vya chai kwa kuwapongeza kwa kufanya kazi kwa bidii shughuli hiyo ilifanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa Mkoa huku promosheni hiyo ikiwavutia wakazi wa jiji la Arusha
  ??????????
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Felix Ntibenda akimshukuru Mkurugenzi wa kampuni ya vunja bei inayojihusisha na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya nyumbani Bw.Shija Ulaya Kamanija baada ya kumkabidhi zawadi ya dinner set na jiko la gesi
  ??????????
  Watumishi mbalimbali wa serikali wakijipatia zawadi mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya vunja bei inayojihusisha na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya nyumbani Bw.Shija Ulaya Kamanija baada ya kufanya ziara jana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha
  ??????????
  Mkurugenzi wa kampuni ya vunja bei inayojihusisha na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya nyumbani Bw.Shija Ulaya Kamanija alisema pia atafanya ziara katika shule za serikali Sekondari na Msingi kwa kuwapatia zawadi ya sufuria za kupikia shule ikiwa ni sehemu yake ya kujitolea kwa jamii(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

  0 0

  Katika kujitetea mbele ya Baraza la Maadili kuhusu tuhuma dhidi yake za kugawiwa mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Escrow, mbunge wa Sengerema Bwana William Ngeleja alisema kuwa ni kawaida wabunge kupewa misaada na wafanyabiashara na taasisi za umma. Katika Maelezo yake alirudia tuhuma za kipuuzi dhidi yangu zilizokwisha tolewa huko nyuma kwamba
  1) nilipewa fedha na kampuni ya PAP na
  2) nilipewa fedha na shirika la NSSF.

  Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema “Hatutetereki”

  Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA.https://www.facebook.com/zittokabwe/posts/755794044441295

  MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI.


  Tuhuma zote hizo nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi wowote na zilikuwa siasa za majitaka. Hata hivyo bado zimekuwa zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo. Watuhumiwa wa ufisadi wa escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa na hivyo wanajaribu na watajaribu kubwabwaja na kuhangaika ikiwemo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao. Ndio maana Bwana Ngeleja ametaja msururu wa watu wakiwemo wafanyabiashara kwamba huwapa fedha wabunge bila chembe ya ushahidi.

  Hivyo narudia kutamka kwamba ninataka uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike mara moja, wenye ushahidi wapeleke kwenye vyombo vya uchunguzi na niitwe mbele ya Baraza la Maadili kujieleza. Nikiwa mbunge ambaye maisha yangu yote ya siasa nimeyatumia kupambana na ufisadi na kuchochea mabadiliko ili kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji na kuimarisha taasisi zake, nipo tayari kwa uchunguzi mahususi dhidi yangu dhidi ya tuhuma zilizotolewa na nyingine zozote ambazo mtanzania yeyote anazo dhidi yangu.

  Naunga Mkono kwa nguvu kubwa kazi inayofanywa na Baraza la Maadili. Ni kazi ambayo ilipaswa kuwa imefanyika kwa muda mrefu sana kwa kashfa mbali mbali ambazo viongozi wa umma wamepata kama vile ile ya rada, rushwa katika manunuzi ya mafuta mazito kuendesha mitambo ya Umeme, kujipatia mikopo kwenye taasisi za umma bila kulipa, kujilimbikizia Mali tofauti na kipato nk. Hivyo naiomba Sekretariat ya maadili iyachukue kwa uzito maoni ya Bwana Ngeleja na kama yana uzito kwa mujibu wa sheria na kanuni yafanyiwe uchunguzi. Nipo tayari kufanyiwa uchunguzi.

  Katika kujenga Misingi Madhubuti ya uwajibikaji nchini ni lazima kila kiongozi aheshimu taasisi kama Baraza la Maadili. Baraza likiendelea kufanya kazi kama inavyofanyika sasa, vita dhidi ya ufisadi itakuwa imepiga hatua na porojo za kuzushiana mitaani zitapungua.

  0 0

   
  General Manager, Etisalat Information Services Mr. Rashid Khusaif Al Naqbi shaking hands with Mr. Stefan Kercza, CEO & President of Eniro AB
  =====  ======  =======
  Abu Dhabi, United Arab Emirates, 3 March 2015: Etisalat Information Services (eIS), the UAE’s market leader in multiplatform information services and a subsidiary of Emirates Telecommunications Corporation-Etisalat, today announced the launch of “connect.ae”, the UAE’s first of its kind fully-digital, and multiplatform search service. 

  The launch marks an agreement between eIS and Eniro Global, the leading Nordic search company in the media industry, with operations in Sweden, Norway, Denmark, Finland and Poland. The service will initially cover the UAE, with the intention to launch the service in the other markets where Etisalat has operations.

  The “connect.ae” platform aggregates, organizes filters and distributes local data for all digital services, regardless of the user’s type of screen. “Connect.ae” is the UAE search engine; it collects, filters, classifies and presents local business information to the market. A smart shortcut to what you need, no matter where you are located in UAE.

  It is your tool to search for your favourite destinations for either business or pleasure offering routing guidance as well as many value added services for the search results. It offers search services by name/category/location, shopping, travel and hotel bookings, maps, location services, directions to the search results and much more served to the user regardless of the size of screen. It is available through online as well as Mobile App offerings. The service is available online in both English and Arabic languages.

  The service will be offered through the connect.ae portal as well as from the Arabic domain name of كونكت.امارات, a first for such a service in the UAE.

  Anyone can use the service, on the Internet or from the IOS or Android smartphones and tablets, to search for anything in the UAE such as finding that special restaurant and booking a table at it or getting the best hotel deals and making a booking. One can also find shopping malls and nearby stores, healthcare providers, amusement parks, etc. 

  The service would return all available results with filters based on relevance, proximity/distance or alphabetical sorting. The user will then be able to add such results to a phonebook, or get directions to the result’s location or simply call the business of interest. In summary, a simple-to-use service at your fingertips anywhere, anytime, with endless benefits and possibilities.

  “We searched for the best partner to develop a unique Local Search engine for all sorts of business and services as a complement to our telecom business,” comments Rashid Khusaif Al Naqbi, General Manager, Etisalat Information Services (eIS). “Eniro’s successful shift to digital distribution – and above all their strong position in mobile search – were decisive factors in our decision. We are looking forward to a successful launch in our home market, with a view to subsequently launching services in our other markets.”


  Commenting on the launch of this unique product, Mr.  Stefan Kercza, CEO & President of Eniro AB said “I am very excited to see the launch of “connect.ae”. The Eniro Global team have worked closely together with Etisalat Information Services in adapting our local search platform to the UAE market, and we now look forward to exploring the business opportunities in this positive and promising partnership."

  0 0  0 0


  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unaungana na watanzania wote kuomboleza kifo cha Makamu Mwenyekiti wao, John Komba aliyefariki Jumamosi na kuzikwa jana nyumbani kwao kijiji cha Litui, Mbinga mkoa wa Ruvuma.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib katika salamu zake za rambirambi alisema mtandao huo umempoteza kiongozi mwadilifu aliyetumia kipaji chake cha usanii kuwaunganisha makundi ya wanamichezo,waigizaji, wasanii wa luninga, bongo movie,wacheza sarakasi na waandishi wa habari kuunda mtandao huo.

  Alisema Kepteni Komba siku zote za maisha yake aliamini sanaa ni mkombozi wa wanyonge katika jamii ambako alitumia fani yake ya ualimu kufundisha wasanii wa fani mbalimbali alipokuwa na kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT), aliunda Kwaya, maigizo, sarakasi, taarab na muziki wa dansi.

  Marehemu Komba akiwa na kikundi chake cha TOT aliibua vipaji vya wasanii mbalimbali waliotamba zamani na wengine bado wanaendelea kutamba kama Nasma Hamisi Kidogo, Laila Khatib, Sheba Juma, Selemani Pembe, Banza Stone, Mohamed Mrisho, Badi Makule, Ali Star, Khadija Kopa, Othman Sudi, Abdul Misambano, Mwanamtama Hamisi na Haji Boha.

  Taalib alisema SHIWATA imempoteza kiongozi aliyekuwa msaada mkubwa katika kuimarisha mtandao huo kwa hali na mali na kuwashawishi wasanii wake wa TOT kujiunga na mtandao huo ili kushirikiana katika kujenga kijiji cha wasanii cha Mwanzega, Mkuranga.

  Marehemu Komba ambaye alikuwa mwanachama mwenye kadi namba moja wa SHIWATA kati ya wanachama 8,000 wa mtandao huo alikuwa akilipia michango yake na kuwa mfano kwa wengine.

  Taalib alisema SHIWATA imewapoteza wanachama maarufu katika kipindi cha karibuni na hivyo kuongeza pengo katika utendaji wake kama Ibrahim Muchacho, Fundi Said (Mzee Kipara), Seteven KAnumba, Hamisi Amigolas na Amina Ngaluma.

  Alisema katika uongozi wa marehemu Komba amesaidia kujengwa kwa nyumba 104 za wasanii katika kijiji cha Mwanzega ambapo wasanii wanaendelea na ujenzi.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha kawaida ambacho ufanyika kila baada ya miezi mitatuKikao hicho kimefanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Magreth Mtaki. hab3 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel akafafanua jambo wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Magreth Mtaki.
  hab4 
  Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Bibi. Magreth Mtaki na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakifuatilia mada kuhusu bajeti ya Wizara iliyowasilishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo Mwanzala Kayoka (hayupo pichani).

  hab5Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Mwanzala Kayoka akiwasilisha mada kuhussu uelekeo wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 na 2015/16 wakati wa kikao kazi cha kawaida baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na watumishi wote kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Liwa akielezea jambo wakati wa kikao kazi cha kawaida baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na hab7 
  Afisa Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Bib. Beatrice Sumari akielezea jambo wakati wa kikao kazi cha kawaida baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na watumishi wote kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.hab1 
  Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  hab8 
  Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (kulia) akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusiana na maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5. (Picha na Francis Dande)


  MWIMBAJI wa nyimbo za injili kutoka Zambia, Ephraem Sekereti yu miongoni mwa nyota wa kimataifa watakaopamba Tamasha la Kimataifa la Pasaka litakaloanzia Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam hapo April 5, kabla ya kuhamia mikoani.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo linalofanyika chini ya uratibu wa kampnuni ya Msama Promotions, Alex Msama, Sekereti anakuwa mwimbaji wa kwanza wa kimataifa kuthibitisha ushiriki. 

  Alisema mbali ya Sekereti ambaye mara kadhaa aliwahi kushiriki tamasha hilo na kuwa baraka kwa wapendwa na wadau wa Tamasha hilo, tayari ameanza maandalizi ya nguvu ili kuwa fiti katika tamasha hilo ambalo litabeba pia maadhimisho ya miaka 15.


  “Kwa upande wa waimbaji wa kimataifa, safari hii watakuwa wengi zaidi kutokana na ukubwa wa tukio lenyewe. Lakini hadi sasa Sekereti ndie wa kwanza kuthibitisha, wengine mazungumzo yanaendelea,” alisema Msama.

  Kwa upande wa waimbaji wazawa, Msama alisema nao wameongezeka na kufikia wawili kwani mbali ya Upendo Nkone aliyethibitishwa wiki iliyopita, mwingine ni Jesca Honoli na kusema wengine watazidi kujulikana kwa siku za usoni.

  Katika hatua nyingine, Msama alisema kwa vile ni tamasha linalokwenda na maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000, makundi maalumu katika jamii kama walemavu, yatima na wajane watashiriki katika kufurahia tukio ambalo ni faraja kwao.

  “Tamasha la Pasaka limekuwa pia baraka kwa makundi maalumu katika jamii kama walemavu, yatima na wajane, katika kuadhimisha miaka 15, makundi hayo yatakuwa na wawakilishi ili kuleta maana kamili ya nafasi yao katika tukio hilo la kimataifa,” alisema.

  Kuhusu mikoa ambayo itafikiwa na tamasha la mwaka huu, Msama alisema suala hilo bado linafanyiwa kazi na kamati yake kutokana na wingi wa maombio yaliyowafikia hadi sasa kwani ni mingi kuliko walivyotarajia kiasi cha kuipa kamati yake kazi ya ziada.

  0 0

  Angelina Mziray Katibu Mkuu wa Women and Poverty alleviation in Tanzania  , Akiwakaribisha wageni Mbalimbali waliofika katika Sherehe za Kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo wao wameadhimisha mapema,Katika Ufunguzi Alisema kuwa Shirika lisilo ka Kiserikali la Waupata wakishirikiana na OXFAM wamesaidia Kijiji hicho katika kuleta maendeleo mbalimbali Tangu mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mpunga, Matumizi Bora ya Ardhi.

  Ambapo Pia aliwashukuru OXFAM kwa kuleta ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, na ujenzi wa masoko mawili ya kisasa, Pia kusaidia wanawake kupata hati milili za Ardhi ambapo wanawake 186 watapata Hati hizo. Mwisho alishukuru taasisi zengine zisizo za Kiserikali ikiwemo Mviwata,Ungo,Tupawaki pamoja na Mwayodeo kwa jitihada zao za kusaidia wanawake na wanakijiji cha Gongoni katika maendeleo ya kijiji hicho.
   Mmoja wa Mashuhuda Juliana Bi. Salum ambaye amepata haki Miliki ya Ardhi akielezea Jinsi gani ambavyo itamsaidia katika Maendeleo yake na jamii kwa ujumla.
  Mshereheshaji MC Chadieli G. Senzighe akiendelea kutoa Mwongozo katika Sherehe hizo.
   Elizabeth Luoga ambaye pia amepata Hati Miliki ya Ardhi akielezea Furaha yake na Ushuhuda wake kwa kuwashukuru OXFAM kwa jitihada kubwa walizo zifanya na wanazo zifanya ili wanawake wapate umiliki wa Ardhi amewashauri wanawake kuwa umiliki wa Ardhi unawezekana.
   Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Gongoni, Kilichopo Kata ya Rudewa Tarafa ya Kimamba Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Bi. Grace Robertson Kanwakaita akitoa utambulisho kwa wageni mbalimbali ambao walifika katika Sherehe ya wanawake wakiwemo, Wakulima na wamama wafugaji walio katika eneo hilo,Opata,shirikisho la Ardhi,OXFAM, Mviwata,Ungo na wagani wengine waalikwa.
   Profesa Majourin Mbilinyi Mwanamke mwanaharakati, Katika Sherehe hizo alisema kwamba wanawake wengi hawana kipato katika kupata umiliki wa ardhi, Ameipongeza Serikali ya kijiji ya Gongoni kwa kuwapatia Haki miliki ya ardhi wanawake alisema kuwa ipo haja ya kubadili mfumo wa umiliki wa ardhi kwa sababu ardhi ipo lakini wamiliki ni wenyefedha na iliyobaki kiasi ndio wanagombania wafugaji na wakulima wadogo wadogo na kusababisha Migogoro. Mwisho alisema kuwa wanawake wanahaki sawa ya kumiliki ardhi.
   Mama Shujaa wa Chakula 2012 Anna Oloishuro , Akiongea wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani katika kijiji cha Gongoni , alisema katika kazi zake kama mama shujaa wa Chakula anapigania wanawake wapate umiliki wa Ardhi kwa kuwa Ardhi ni uhai, aliongeza kuwa wanawake wananyimwa haki ya kumiliki ardhi jambo ambalo sio sahihi hivyo ni jukukumu lake kupigania hilo, Mwisho aliwapongeza wote waliopata hati miliki za Ardhi.
   Marcelina Charles Kibena Mwanachama wa Shirikisho la ardhi Morogoro akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani , katika maoni yake alizungumza juu ya mgawanyiko wa Rasilimali na ardhi haupo sawa kabisa amesema kuwa ardhi kubwa inamilikiwa na mabepari na wenye fedha ambao aidha ni watanzania au watu waishio nje ya Tanzania ambao hao ndio wanaleta mgongano mkubwa katika kumiliki ardhi,Alisema watu wanazidi kuongezeka lakini ardhi haiongezeki ambapo pia hilo ni tatizo la kuleta migogolo ya Ardhi. Mwisho alisikitika kuona watoto hawasomi na wamejikita katika kilimo na Ufugaji alisisitiza watoto hao wanahaki ya kwenda shule na kuja saidia maendeleo ya kijiji na jamii kwa ujumla hapo baadae.
   
  Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam  akiendelea kutoa mwongozo katika Sherehe hiyo
   Mratibu wa Mradi wa Haki za wanawake kumiliki Ardhi (WAOPATA) Joseph Pupa akielezea kwa ufupi maelezo ya Hati za Ardhi ambazo walipata wanawake mbalimbali pamoja na wanakijiji wengine wa Gongoni
   Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiongea na wanakijiji cha Gongoni pamoja na wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ikiwa ni wiki ya maadhimisho hayo, alipongeza harakati za kuwawezesha wanawake katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umiliki wa Ardhi, ambapo alisema kuwa OXFAM itahakikisha kila aliyeomba hati ya Kumiliki Ardhi ataipata, pia ameshukuru Taasisi zengine zisizo za kiserikali kuendelea kusaidiana ili kuleta maendeleo.

   
  Meza Kuu wakifurahia Burudani 
   
  Burudani ikiwa inaendelea 
   Baadhi ya wanakijiji wakipokea Hati Miliki za Ardhi
  Wanakijiji wakipata vijarida
   Wanakijiji cha Gongoni pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika Sherehe hizo.
  Hata watoto walikuwa bize wakisoma Vipeperushi na Vijarida.

  0 0

  Wafanyakazi wa kampuni ya Mafuta ya Panone wakiwa katika picha ya Pamoja na watoto wanao lelewa katika kituo cha Gabriela cha mjini Moshi.
  Afisa uhusiano wa timu ya soka ya Panone fc Kassmi Mwinyi akitoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Panone Frank Mwaikatale akigawa zawadi ya mikate kwa watoto wanaolelewa katika  kituo cha Gabriela cha mjini Moshi.
  Mlinda mlango wa timu ya Panone fc ya mkoani Kilimanjaro Ben Haule maarufu kama Yaw Berko akigawa zawadi kwa watoto wanao lelewa katika  kituo cha Gabriela.
  Watoto pamoja na walezi wao wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Panone ya mjini Moshi.
  Watoto wa Kituo cha Gabriela na wafanyakazi wa kampuni ya Panone wakifurahia zawadi kwa pamojana .Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii Kanda ya kaskazini.

  0 0

   Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakiwa katika mistari wakisubiri huduma ya kupima macho inayotolewa kwa ushirikiano na madaktari kutoka Shirika la Spacsaver la Sweeden na madaktari wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika Skuli ya  Sekondari ya Kiembesamaki.
   Daktari wa macho kutoka Shirika la Spacsaver Petter Daniesin akimfanyia vipimo  mtoto  Sabrina Abdalla Salum katika zoezi linalofanyika  Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki.
  Daktari wa Shirika la Spacsaver Ingrid Stenersen akimfanyia uchunguzi mmoja ya wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki waliofika Skuli ya Sekondari ya eneo hilo kupatiwa huduma ya macho. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakimjulia hali Meja Peter Lyamuya aliyelazwa katika hospitali kuu ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam akiuguza jeraha la mguu alilopata baada ya ndege ya kivita aliyokuwa akiiendesha kuanguka na kulipuka wiki iliyopita.

  Askari huyo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) alinusurika kifo baada ya kufanikiwa kujiokoa katika ajali hiyo iiyosababishwa na ndege mnyama kuingia kwenye injini na kusababisha hitilafu iliyopelekea kushika moto, kuanguka na kulipuka.Ndege hiyo ilikuwa katika mazoezi ya kawaida kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.(picha na Freddy Maro)muh3

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa Mpwapwa mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa.Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuiarisha uhai wa chama,kukagua,kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
    Baadhi ya Wananchi na wanachama wa CCM,wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia katika uwanja wa Mashujaa,wilayani Mpwapwa leo jioni 
   Baadhi ya Wananchi na wanachama wa CCM,wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia katika uwanja wa Mashujaa,wilayani Mpwapwa leo jioni 
  Wakazi wa Mpwapwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi-Taifa,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mpwapwa mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa mkoani Dodoma.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa mifereji ya umwagiliaji katika shamba la Umwagiliaji katika kijiji cha Msagali kata ya Chunyu.Kinana alikagua na kushiriki ujenzi wa ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji skimu ya Msagali
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa sambamba na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Mh.Adam Kimbisa wakishiriki ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Kisoke,Wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua na kushiriki ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM wilaya ya Mpwapwa.   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikatiza kwenye moja ya mtaro alipokwenda kukagua na kushiriki kulima katika shamba la mkulima bora wa mwaka 2014,Bi.Anna Mlewa katika kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa.
   Sehemu ya ujenzi na ukarabati wa mfereji wa umwagiliaji
   Pichani Kati ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongoza na Mkulima bora wa mwaka 2014,Bi.Anna Mlewa na Mumewe pichani kulia,ambapo Ndugu Kinana alikwenda kukagua na kushiriki kulima katika shamba la mkulima huyo katika kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa tatu kushoto) akishiriki kulima shamba la karanga la Mkulima bora wa mwaka 2014 mkoa wa Dodoma,Bi.Anna Mlewaka katika kijiji cha Berege Wilayni Mpwapwa mkoani Dodoma.Mkulima huyo alieleza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuwa 2012/13 alifanikiwa kulima ekari 30 na kuzalisha kiasi cha gunia 300 za mtama,mnamo mwaka 2014 alihamasika kuongeza eneo kufikia ekari 130 ambazo alizalisha gunia 650.Mkulima huyo alisema kuwa mpaka sasa amefanikiwa kununua power tiller 1,ameanzisha biashara ya duka na mashine ya kusaga,anasomesha watoto shule ya msingi,sekondari na chuo.

  0 0

  DSCN9215

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), Dk Ali Mzige (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Kambi ya kupima afya bila malipo kwa watoto wadogo, itakayofanyika Jumapili ya Machi 8 mwaka huu. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy na kulia ni mwakilishi wa shule ya Kibugumu, Mwalimu Mzamili Ally.

  Na Andrew Chale modewji blog
  Imeelezwa kuwa, Sensa ya mwaka 2012 ilionesha kuwa asilimia 42 ya watoto chini ya miaka 5 hapa Nchini Wamedumaa, asilimia 16 wana uzito pungufu (wako underweight), asilimia 5 wamekonda (marasmic) wako kwenye kadi nyekundu ya mtoto.

  Hayo yamesemwa jana Machi 4, jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), Dk Ali Mzige mbele ya wandishi wa habari wakati wa kutoa taarifa juu ya kambi ya upimaji wa afya kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 5, itakayofanyika Jumapili ya Machi 8, katika shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni, wilaya ya Temeke.

  Dk. Mzige alibainisha kuwa kama ilivyo kwa watu wazima, upimaji wa afya ya watoto wenye umri chini ya miaka 5 una manufaa makubwa kwa mtoto, familia na jamii ya watanzania wote.

  Ambapo alibainisha kuwa, tatizo la utapia mlo kwa watoto hapa nchini imepelekea Tanzania kuwa nafasi ya tatu katika Bara la Afrika, Lishe duni kwa watoto na wajawazito huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ikiongoza na Ethiopia ikiwa ni ya pili kwa tatizo hilo la utapiamlo.

  DSCN9217
  Hata hivyo Dk. Mzige alibainisha kuwa, utapiamlo huo unaonekana nchini upo kwenye mikoa inayozalisha chakula na matunda kwa wingi ikiwemo ya Morogoro, Mbeya, Tanga, Rukwa, Iringa na Manyara.

  Pia alieleza kuwa tatizo lingine ni la utapiamlo la kula chakula kupita kiasi kama vyakula vyenye wanga na sukari kwa wingi, mafuta kwa wingi na kuleta maradhi/magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa watoto na watu wazima.

  Aidha, Dk. Mzige alisema kuwa elimu sahihi dhidi ya kupambana na maradhi hayo ya utapiamlo, yatatolewa kwenye kambi hiyo huku akisisitiza wazazi kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kwani itakuwa ni ya kipekee na faida kwao na kwa watoto wao.
  “Tujitokeze kupima afya zetu na pia watoto hasa wadogo. Hivyo kambi hii itakuwa msaada mkubwa kwani tutachunguza yale magonjwa mengi yanayowakabili watoto wengi hapa nchini.” Alisema Dk. Mzige.
  DSCN9242
  Dk. Mzige akionyesha mswaki wa mti ambai ni wa asili, ambapo alishahuri watanzania kuwa na tabia ya kubadilisha miswaki yao kila baada ya miezi mitatu, ama kutumia miswaki ya miti ambayo inasaidia kuboresha meno.

  Akitoa baadhi ya takwimu zinazowakabili watoto wengi hapa nchini, ni pamoja na :
  Watoto 130, walio chini ya umri wa miaka 5 hufa kila siku hapa Nchini kwa ajili ya utapiamlo (Malnutrition-Lishe duni).

  Upungufu wa wekundu wa damu asilimia 59 kwa watoto wenye miezi 6 hadi 59. Asilimia 33 ya watoto chini ya miaka 6 wana ukosefu wa vitamin A. BANGO SANGHO, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy alisema kuwa kwa kushirikiana na Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), ya Jijini Dar es Salaam ambapo wameandaa kambi hiyo ya kupima afya bila malipo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 ni faraja kwa jamii hiyo kwani watoto wengi hapa Nchini wamesahulika katika kupimwa afya zao.
  DSCN9265
  Dk. Mzige akionesha Yai ambapo alibainisha kuwa Yai sio zuri kwani lina Cholesterol hivyo mtu anashahuriwa kula mayai matatu kwa wiki hasa ya kuchemsha.

  Amit Nandy aliwataka wananchi wa Kigamboni na maeneo mbalimbali kuwapeleka watoto wao katika shule ya Msingi, Kibugumu kwa ajili ya kupimwa afya zao hizo ikiwemo magonjwa yanayowakabili watoto wengi. “wazazi wote tunawaomba kujitokeza kwa wingi, Machi 8, katika shule ya Msingi Kibugumu mukiwa na watoto wenu pamoja na makadi ya kliniki ilikuweza kupata huduma ya matibabu bure.

  Madaktari bingwa na matabibu watapima magonjwa mbalimbali ikiwemo Afya ya kinywa, Uzito, Ukaguzi na ushauri wa lishe. Pia watakaobainika kuwa na matatizo maalum ya kiafya watapewa rufaa” alieleza Amit Nandy. Ambapo alibainisha kuwa, huduma hizo za matibabu zinatarajiwa kutolewa kuanzia asubuhi ya saa tatu hadi saa saba mchana. (Saa 3:30 asubuhi-Saa 7-30 mchana).
  DSCN9264
  Dk Mzige akionyesha soseji ambapo alisema kuwa ulaji wa soseji sio mzuri kwa afya hivyo watu wanatakiwa kuepuka ama kupunguza.
  DSCN9252
  Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakiingia kwa maandamano mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo. Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakiingia kwa maandamano mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo.Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam waifuatilia mada anuai katika maadhimisho hayo. Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam waifuatilia mada anuai katika maadhimisho hayo.
  Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakiingia kwa maandamano mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo. Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakiingia kwa maandamano mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es SalaamBaadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa hafla ya maadhimisho. Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa hafla ya maadhimishoBaadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada anuai. Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada anuai.Baadhi ya washiriki wenye ulemavu wa kusikia wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam waifuatilia mada anuai katika maadhimisho hayo. Baadhi ya washiriki wenye ulemavu wa kusikia wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam waifuatilia mada anuai katika maadhimisho hayo.Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam waifuatilia mada anuai katika maadhimisho hayo. Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam waifuatilia mada anuai katika maadhimisho hayo.Meza kuu katika maadhimisho hayo. Meza kuu katika maadhimisho hayo.Vikundi vya maigizo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam vikitoa burudani katika hafla hiyo. Vikundi vya maigizo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam vikitoa burudani katika hafla hiyo.Baadhi ya wanaharakati toka meza kuu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakizungumza na wananchi. 
  Baadhi ya wanaharakati toka meza kuu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakizungumza na wananchi.Baadhi ya washiriki wenye ulemavu wa kusikia wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam waifuatilia mada anuai katika maadhimisho hayo. Baadhi ya washiriki wenye ulemavu wa kusikia wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam waifuatilia mada anuai katika maadhimisho hayo.[/caption] [caption id="attachment_55658" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa hafla ya maadhimisho. Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa hafla ya maadhimisho.[/caption] [caption id="attachment_55675" align="aligncenter" width="600"]Baadhi ya wanaharakati toka meza kuu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakizungumza na wananchi. Baadhi ya wanaharakati toka meza kuu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakizungumza na wananchi.[/caption] [caption id="attachment_55674" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya wanaharakati toka meza kuu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakizungumza na wananchi. Baadhi ya wanaharakati toka meza kuu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakizungumza na wananchi.[/caption] [caption id="attachment_55673" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya wanaharakati toka meza kuu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakizungumza na wananchi. Baadhi ya wanaharakati toka meza kuu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam wakizungumza na wananchi.

  0 0

  IMG-20150304-WA0003
  Hugoline Martin Mtambachuo au unaweza kumuita DJ CHOKA aka Mr Appetite baada ya kukaa kimya kwa muda wa mwaka mmoja bila kuendelea na mix tape zake, mwaka huu amehamua kurudi tena.
  Dj Choka anasema alikuwa kimya mwaka 2014 kwa kuwa alikuwa busy akimlea mtoto wake na familia yake, wimbo wa mwisho kuutoa ulikuwa unaitwa STINGA LI ambao ulikuwa umetengenezwa na Prod Pancho Latino kutoka Bhitz Music Group.

  Mwaka huu 2015 Dj Choka anaanza na wimbo wake wa kwanza alioupa jina la NITALALA UZEENI huku akiwa amewashirikisha wasanii kama Country Boy, Climax Bibo, Young Lunya, Bgway na Deddy. Wimbo huu umesimamiwa na Prod mchanga anayekuja vizuri anajulikana kwa jina la GARD kutoka A.M Record.

  Wimbo huu unatarajiwa kutoka siku ya Ijumaa tarehe 13 mwezi huu wa 3, na matarajio ya video yako mbioni kufanyika na kampuni ya utengenezaji video kutoka hapa hapa Tanzania.
  _MG_2680
  Pichani ni Dj Choka akiwa na Deddy
  IMG_2636
  Pichani kuanzia kushoto ni Prod Gard, Prod Maneck na Dj Choka wakiwa studio ya A.M Rec
  _MG_2674
  Dj Choka, Deddy, Young Lunya & Prod Gard

  0 0

  Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni urban and rular engineering ndugu Awadh Zuberi ,pamoja na wasaidizi wake walipomtembelea balozi mstaafu Mustafa nyang'anyi nyumbani kwake Washington, kuanzia kushoto ni Awadh Zuberi, Shemuni Halahala,Balozi Nyang'anyi, Zuberi Athumani


  0 0

  mar1 
  Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark Childress akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Leo Jijini Dar es Salaam.
  mar2Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na balozi   wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark Childress(wa pili kulia) mara baada ya mazungumzo.
  mar3 
  Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark Childress akimuaga Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju alipomtembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Leo Jijini Dar es Salaam

  0 0

  mna1
  Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman akikata utepe kuzindua mpango wa upimaji usikivu wa watoto wachanga katika hafla iliyofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar, wa kwanza (kushoto) mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael na (wakatikati) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
  mna2
  mna3
  Wafanyakazi wa Afya waliopatiwa mafunzo maalum ya kuwapima usikivu watoto wachanga wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.
  mna6
  Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga. (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam Taib na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
  mna5
  Baadhi ya wageni walioalikwa katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Hospitali ya Mnazimmoja.

  …………………………………………………………………….
  Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.  
  Waziri wa Afya wa Zanzibar  Rashid Seif Suleiman amesema sikio,  mdomo  na macho ni sehemu muhimu sana katika maisha ya  binaadamu hivyo unapokuwa na   wataalamu wa  kushughulikia viungo hivyo ni neema kubwa inayopaswa kuenziwa.

  Haya ameyasema jana katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar wakati wa uzinduzi  wa kuwapima usikivu watoto wachanga mara  baadaya kuzaliwa ili kujua matatizo yao.

  Amesema uchunguzi  wa watoto wachanga kujua usikivu wao  mapema ni mpango mzuri  ambao utalisaidia Taifa kuwa na   watoto wenye usikivu  mzuri na njia rahisi  ya kuwapatia matibabu kwa watakaogundulika na matatizo hayo.

  “Kujua tatizo la kiafya mapema na kuanza kulishughulikia kunapunguza gharama za matibabu hivyo nawanasihi wazazi kuwapeleka watoto wenu mara baada ya kujifungua, ”alisisitiza Waziri wa Afya.
  Amesema  maradhi ya usikivu  yamekuwa yakiwasumbua watoto wengi Zanzibar na iwapo kila mzazi atatimiza wajibu wake wa kumpeleka  mtoto wake  kupata vipimo yataweza kupungua.

  Waziri wa Afya aliwataka wazazi  kuwa na utamaduni wa kuzalia Hospitali  ili kupata huduma hiyo kwa urahisi na watakaozalia majumbani  kuwapeleka watoto wao kuchunguzwa usikivu mara baada ya kuzaa.
  Aidha Waziri huyo aliwataka madaktari  waliopatiwa mafunzo ya kutoa huduma hiyo kuwa waadilifu katika kutekeleza kazi zao kwani huduma za watoto wachanga  na wazazi zinahitaji uvumilivu.

  Waziri alisema tatizo la uskivu huazia  mtoto  anapochelewa kulia mara baada ya kuzaliwa ama wanapopata homa ya manjano, kutopatiwa chanjo, mzazi kuchelewa kuzaa baada ya uchungu wa muda  mrefu na kuzaliwa mtoto bila ya ya kufika muda wa kuzaliwa.

  Nao madaktari walio patiwa mafuzo hayo walisema kuwa wana uwezo mzuri wa kuwapima usikivu watoto  na kubaini matatizo yao  na kuishauri Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa kuwafikia watoto watakaozaliwa vijijini.
  Mradi huo wa kupima watoto usikivu ulipokea msada wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi kutoka Jumuiya ya Madaktari wanotoa huduma za matibabu vijijini ( ZOP) ambavyo vina thamani vya Dola elfu 50 za kimarekani.

  0 0

  DSCN9299
  Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Komputa wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC), January Ntisi akizindua kitabu cha ripoti ya Bodi ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Umoja wa Mataifa, kwenye hafla ya uzinduzi uliofanyika Machi 4, MAELEZO, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Afisa Mipango wa Umoja wa Mataifa, Immaculata Malyamkono-Nyoni na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupambana na Watumiaji wa Madawa ya Kulevya,Very Kunambi. (Picha na Andrew Chale).
  DSCN9305
  Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa ripoti ya Kupambana na dawa za kulevya ya Umoja wa Mataifa. Kulia ni mgeni rasmi Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC), January Ntisi na kushoto ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama.
  Na Andrew Chale wa Modewji blog.
  Uongozi wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataaifa (UNIC) umezindua ripoti ya Kupambana na dawa za kulevyaa ya Umoja wa Mataaifa, Uzinduzi uliofanywa Machi 4, Jijini Dar es Salaam.

  Wakizungumza mbele ya wandishi wa habari kwa upande wake, Afisa Habari wa Kituo Cha Habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo alibainisha ripoti hiyo imeweza kuchambua mambo mbalimbali dhidi ya dawa za kulevya na mikakati iliyofikiwa.

  Ambapo alisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na kupungua kwa wimbi la kuingia kwa dawa za kulevyaa nchini hasa kupitia njia za bahari ya Hindi huku mji wa Mexico wa America, ukipunguza kwa asilimia kubwa matumizi ya dawa za kulevya.

  Vuzo alibainisha kuwa, pia mikakati iliyofikiwa ambayo pia imo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na mfumo wa kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya wanaoacha kwa kuwapatia dawa maalum za kupunguza taratibu matumizi hayo.

  ‘Mipango ya kuwapatia wale wanaocha dawa maalum za kusaidia utumiaji wa madawa na pia dhidi ya kupambana na dawa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi wa watumiaji” alisema Vuzo. Aidha, alibainisha kuwa, Afrika Kusini katika bara la Afrika ndio inayoongoza kwa kuwa na njia nyingi za usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine na Heroine .
  DSCN9301
  Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC), January Ntisi akionyesha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

  Kwa upande wake Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya kudhibiti Ukimwi DCC, January Ntisi ,amesema wanashirikiana katika kupambana na dawa za kulevya na umoja huo kwani Tanzania ni miongoni nchi ambazo pia zinakabiriwa na tatizo hilo.
  Alisema mwaka jana walikamata dawa tani 2.3 ambazo zingeingia nchini kungekuwa na kundi kubwa ambao wanatumia dawa hizo.

  Kwa upande wake, Immaculate Nyoni ambaye ni Project officer UNODC alibainisha juhudi mbalimbali zinafanywa katika kukabiliana na wimbi la dawa za kulevya duniani kote ambapo kwa sasa angalau matumizi hayo yakiendelea kupungua.
  DSCN9317
  Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC), January Ntisi akifafanua jambo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.
  DSCN9311
  Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa kupambana utumiaji wa Madawa ya Kulevya waliohudhuria uzinduzi huo.

older | 1 | .... | 476 | 477 | (Page 478) | 479 | 480 | .... | 1897 | newer