Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 477 | 478 | (Page 479) | 480 | 481 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na Greyson Mwase, Dodoma

  Meneja wa Shirika la Umeme Nchini  (Tanesco) mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu amesema kuwa Serikali imetenga  jumla ya shilingi  bilioni 43.89 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya  umeme katika mkoa wa Dodoma kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili.

  Temu aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Nishati na Madini  iliyopo  mkoani  Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi  ya umeme  ili kujionea utekelezwaji wake pamoja na kuzungumza na wawakilishi wa wananchi. Mbali na mkoa wa Dodoma, kamati hiyo  inatarajia kufanya ziara ya kukagua miradi ya umeme katika mikoa  ya Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na   kuzungumza na wadau wa madini katika mkoa wa Manyara.

  Akitoa  taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme katika mkoa wa Dodoma chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya  Pili, Temu alisema kuwa mradi  kabambe wa kusambaza umeme  vijijini  awamu ya pili  unahusisha wilaya  zote za mkoa wa Dodoma, wilaya za Chamwino, Kongwa zikiwa mojawapo.

  Akielezea kazi ya usambazaji wa umeme katika wilaya  ya Chamwino  Temu alisema kazi ya kupeleka umeme  itahusisha ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovolti 33 urefu wa kilomita 171.5 na  njia ya msongo  wa kilovoti 0.4 urefu wa kilomita 95.

  Alisema  ujenzi utahusisha pia ufungaji wa transfoma 22 za ukubwa mbalimbali  pamoja na kuunganisha wateja wapatao 1,195 kwa gharama inayokadiriwa kuwa shilingi za kitanzania bilioni 8.67.

  Aliongeza kuwa katika wilaya ya  Chamwino  hadi sasa ujenzi wa miundombinu  ya umeme  umefikia asilimia 52 na wateja 105 kati ya 1,195 wamekwisha unganishwa na huduma ya  umeme na kusisitiza kuwa mradi huu  unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.


  Alitaja maeneo yatakayofaidika na umeme huu kuwa ni pamoja na  vijiji  vya  Fufu, Masanze, Mloda, Handari, Chololo, Kikombo, Igandu, Msanga, Chinangali, Mwegamile, Mpera,  Chamwino Ikulu,  Solowu, Zajilwa,  Segala, Izava, Itiso, Magungu, Osteti, Dabalo, Nzali, Majeleko, Mlimwa, Igamba, Membe na Ikowa.

  Alitaja  vijiji  vingine ni pamoja na Msamalo, Makoja, Mnase, Mgunga, Mlebe, Ndebwe, Handali, Chanhumba, Matumbulu, Igogi, Chaludema, Sazima, Nkowe,  Chinyika, Chinyanguku, Nghaheleze, Ikombolinga, Idifu, Miganga, Muungano, Ilolo, Chalinze B, Azimio B na  Shule ya Msingi  Chinangali II

  Wakati huo huo akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika  wilaya ya Kongwa, Temu alieleza  kuwa kazi ya kupeleka umeme katika wilaya hiyo inahusisha ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovolti  33 urefu wa kilomita 197 na  njia ya umeme msongo wa kilovoti 0.4 urefu wa kilomita 66.

  Alisema  pia ujenzi huo unahusisha  ufungaji wa transfoma 51 za ukubwa mbalimbali  pamoja na kuunganisha wateja wapatao 1,195 kwa  gharama inayokadiriwa kuwa shilingi za kitanzania bilioni 9.24

  Alisema hadi kufika sasa ujenzi wa miundombinu  ya umeme umefikia kwa asilimia 68 na wateja 30 kati ya  1,640 wamekwisha unganishiwa umeme na kusisitiza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

  Alitaja vijiji  vitakavyonufaika na mradi huo kuwa ni pamoja na Manguto, Matongoro, Nororia, Mlanje, Manyata, Ngomai, Njoge,  Chiwe, Moleti, Pingakame,  Mlanje, Sejeli, Mkutani, Banyibanyi, Mageseni, Makawa, Mkoka na Magereza Vijiji vingine ni pamoja na Nilini, Ndurugumi,  Laikala, Mlali Ng’umbi, Mranana, Chingwilingwili, Ndalibo, Zoissa na Chitego.

  Akielezea changamoto katika utekelezwaji wa mradi wa REA  Awamu ya  Pili  Temu alieleza kuwa ni pamoja na wananchi wengi kuhitaji  huduma ya umeme katika awamu hiyo japokuwa  hawapo kwenye mpango huo  kwa sasa na  njia ya umeme  kutembea kwa umbali mrefu sana kupita kiwango cha kawaida na hivyo kuwa na  viashiria vya kupata umeme mdogo kwa muda mfupi. Aidha, alisisitiza kuwa katika utekelezaji wa mradi, baadhi ya wananchi wamekuwa wakijitokeza kudai  fidia.

  Alisema  ili kutatua changamoto hizo  kama shirika la Tanesco litaendelea kubaini maeneo  ambayo  yanahitaji umeme ili yawekwe kwenye  bajeti ya Tanesco inayoandaliwa kila mwaka na kwenye maeneo  ya  vijijini  shirika litaendelea kuweka miradi ya  REA kwa kadri itakavyokuwa inahitajika lengo likiwa ni kuhakikisha kila mwananchi anafurahia  huduma ya umeme.
  “Pia tutaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa miradi ya umeme   hususan  vijijini kwa maendeo ya taifa ili kuondokana na dhana ya kudai  fidia ambayo ni kubwa  kuliko  bajeti iliyotengwa”, alisisitiza Temu.

  0 0

  Abu Dhabi, March 4 2015: Etisalat, the leading telecommunications operator in emerging markets, has continued its recent history of success at the industry’s most prestigious annual awards. Etisalat came out on top of strong global competition to claim two highly sought-after awards for innovation at the GSMA’s Global Mobile Awards. Recognition in the GSMA’s 2015 annual awards brings to six the number of awards won by the company in the last three years.

  Etisalat won in “The Best Use of Mobile for Retail, Brands & Commerce” category for its Mobile Cashier product offering and “The Mobile Connect Award for Best Authentication & Identity Solution” for Etisalat Mobile Connect service. Following the judgment by a panel of independent and highly respected industry experts, the winners were announced at a big ceremony during the Mobile World Congress being held in Barcelona, Spain.

  “It’s tremendous to be honoured at the most important event in the global telecoms calendar,” said Ahmad Julfar, Etisalat Group CEO. “Innovation is key in today’s dynamic telecommunications sector and Etisalat is at the cutting-edge of finding solutions for all our customers. These awards recognize our commitment to keep innovating and introducing products that give businesses and communities the technology that enables their economies – and, therefore, societies – to progress, which is one of our core missions and winning this a global appreciation is a sign that we’re on the right track.”

  The award winning Etisalat Mobile Cashier enables businesses to accept credit card payments directly on their mobile phones, while Mobile Connect, helps customers to manage their Digital Identity and protect privacy on-line.  A member of the judging panel said the winning Etisalat products represented “a stand-out entry in terms of the scale of deployment and comprehensive suite of commerce offerings across so many countries and different verticals.”

  “We’ve had a phenomenal uptake for these products everywhere the service been introduced,” said Khalifa Al Shamsi, the Chief Digital Services Officer at Etisalat. “Through this new technology platform, we are integrating the power of mobile devices seamlessly into our customers’ every-day lives.”

  "Our warmest congratulations to all the winners of the 20th Global Mobile Awards," said John Hoffman, CEO of GSMA Ltd. “Our winners are in the esteemed company of the mobile innovators, pioneers and leaders that have won these coveted awards over the last two decades, many of whom have been game-changers in transforming the way that the world communicates.”

  Another Etisalat product, Mobile Money service “Flous” was also nominated in the category “The best NFC & Mobile Money service”; Women empowerment program “Weena” in the category “Best Mobile Product, Initiative or Service in Emerging Markets”;  and integrated communication instrument C’me in the category “Best Mobile Network Product or Solution for Serving Customers”.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamishina Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya, wakati walipokutana baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Burn Ltd, Malaczynski Burn, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.


  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose aliyefika ofisini kwake leo kwa mazungumzo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose ofisini kwake,jijini Dar es salaam leo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

  0 0

  JUMLA dola za Kimarekani Milioni 31 (zaidi ya Sh. Bilioni 56 za Tanzania) zimetumika kutengeneza studio mpya za kisasa za Azam TV, zilizopo eneo la Tabata Relini, Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando wamiliki wa Azam TV leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Tabata, Dar es Salaam. 

  Mhando mwenye uzoefu wa kuongoza kampuni kubwa za vyombo vya habari zikiwemo Idhaa ya Kiswahili BBC, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na Mwananchi Communication Limited (MCL), amesema studio hizo zina ubora kuliko nyingine zote nchini.

  “Ni studio ambazo labda unaweza ukazifananisha na studio za kampuni kubwa kama CNN, Aljazeera BBC, na kwa kuwa za kwetu ni mpya, zinaweza kuwa na ubora kuliko hizo,”amesema.

  Tido amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa studio hizo, zoezi la uzinduzi wake rasmi litafanyika kesho, asubuhi mjini Dar es Salaam.

  Mhando ambaye alikuwa mtangazaji maarufu wa mpira wa miguu enzi zake nchini kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

  “Azam TV imeanza kufanya shughuli zake kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini tumekuwa tukiboresha mambo kadha wa kadha kuelekea siku ya kesho, ambayo tunaweza tukasema ndiyo mwanzo rasmi wa Azam TV,”alisema Tido.

  0 0

  Hivi ndivyo ofisi mpya ya tawi la 79 la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services wilayani Kwimba, mkoani Mwanza inavyoonekana kwa mbele siku lilipozinduliwa rasmi mapema wiki hii, huku mgeni rasmi akiwa ni Vicent Emmanuel, Katibu Tawala wa wilaya ya Kwimba, hayupo pichani.
  Katibu Tawala wa wilaya Mwanza, Vicent Emmanuel wa pili kutoka kulia, akiangalia matukio tofauti katika uzinduzi wa tawi la Bayport Financial Services, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Kushoto kwake ni Meneja Mauzo wa Bayport Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Kulia kwa Katibu Tawala ni OCS Adam Amir, akiafutiwa na Meneja wa Bayport Mwanza, August Tesha. Bayport wamezindua tawi la 79 nchi nzima kwa ajili ya kusogeza huduma karibu na wananchi.


  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua, kukuza na kuendeleza Sanaa kwa kushirikiana na taasisi ya Ako’mungoma Poverty Alleviation Organization (APAO) linaendesha programu ya wiki tatu ya Sanaa kwa watoto katika Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam. 

  Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 sura ya 9.6.16 Baraza linaelekezwa kushirikiana na wadau katika kuendesha matukio mbalimbali ya sanaa  kama programu hii ya watoto. 

  Programu hii ya Sanaa kwa watoto ambayo kilele chake kitakuwa tarehe 07/03/2015 na kuhusisha  maonesho, inatarajia kushirikisha watoto 215 ambapo 100 wanaishi katika mazingira magumu eneo la Mbutu - Kigamboni na wengine 100 kutoka shule za Msingi Gomvu na Mbutu. Aidha, watakuwepo wanafunzi waalikwa 15 kutoka shule ya msingi Msimbazi iliyopo wilaya ya Ilala. 

  Programu hii ambayo mwaka huu inadhaminiwa na Kampuni ya Mohamed Enterprises na Haakneel production (T) Ltd inalenga kukuza vipaji vya watoto katika fani za uchoraji, maigizo hususan majigambo na ngoma za asili. Pia tunatarajia udhamini toka wadau na makampuni mengine. 

  Kilele cha programu hii yenye kauli mbiu ya “Amani na Uchaguzi 2015” kitapambwa na burudani ikiwemo mpira wa miguu kutoka kwa watoto wa Kituo cha APAO na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka jimbo la Kigamboni Mheshimiwa Faustine Ndugulile.

  Aidha programu hii ni mwendelezo wa programu ya Sanaa kwa watoto ya Baraza iliyoanza tangu miaka ya 80 ambayo ilipata kuibua na kukuza vipaji vya wasanii kama Mrisho Mpoto na Masoud Kipanya ambao hadi sasa wanafanya vizuri. 

  Kwa mwaka 2014 programu hii iliendeshwa katika wilaya ya Ilala kwa kushirikisha shule tano (5) ikiwemo ya Buguruni Viziwi na ilidhaminiwa na kampuni ya Msama Promotion. 

  Baraza linachukua fursa hii kuwaalika wananchi na wadau wote wa sanaa kufika kwa wingi kushuhudia vipaji vya sanaa walivyonavyo watoto.

  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Ayoob Omary akizindua vilabu vya wanafunzi vya Sumatra. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Oscar Kikoyo na kulia ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatan.
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
   Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano akizungumza.
   wanafunzi wakifuatilia hotuba za uzinduzi kutoka kwa viongozi.
   Mgeni rasmi pamoja na meza Kuu ikipiga picha na Vilabu mbalimbali kutoka shule za sekondari na msingi.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo (kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay, Dar es Salaam jana baada ya uzinduzi wa klabu za wanafunzi watumiaji wa huduma za usafiri mkoa wa Dar es salaam jana. Wengine ni  Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano na Mwenyekiti wa Baraza hilo Ayoob Omary. Picha na Sori: mrokim.blogspot.com

  0 0

  Na Chalila Kibuda 

  Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu amewataka watu wajitokeze katika  harakati za kupambana na watu wenye imani  potofu za kuwaua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

  Mdimu amesema uchunguzi umebaini ukosefu wa elimu kwa watu wenye imani hizo ndiyo hupelekea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo silaha ya elimu ni sehemu kubwa ya harakati hapa nchini.

  Hayo ameyasema leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kusema kuwa ana mpango wa kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha  jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

  Aidha,Mdimu ameahidi kutoa elimu hiyo kwa njia ya sanaa kwa kuwatumia baadhi ya wasanii kama Jhikoman,Kassim Mganga,Profesa J,Ray C,Fid Q,Roma Mkatoliki pamoja na Dami Msimamo.

  Pia amevitaka Vyombo vya Habari kutoa ushirikiano katika harakati hizo za  kuhakikisha wanatokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
   Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu (kati) azungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati azungumzia harakati zake za kutaka kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha  jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mwenyekiti wa Imetosha Movment,Masoud Ali "Kipanya" na kushoto ni Monica Joseph mjumbe wa Imetosha.
   Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni Wajumbe wa Imetosha,Joachim Mushi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
  Baadhi ya Wajumbe wa Imetosha wakiwa kwenye picha ya pamoja.

  0 0

   Baadhi ya maofisa wa TAMISEMI,TaGLA na mikoa ya Ruvuma, Mara na Mbeya wakishiriki kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference)
   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (katikati) akiongoza kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kilichofanyika kati ya Utumishi,TAMISEMI,TaGLA na mikoa ya Ruvuma ,Mara,Mbeya, Singida na Pwani.
  Baadhi ya Maofisa wa Ofisi ya Rais – Utumishi wakiwa katika kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kati ya Utumishi,TAMISEMI,TaGLA na mikoa ya Ruvuma ,Mara,Mbeya, Singida na Pwani.

  0 0

  Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum, Al Sheimar Kweigyir (Semeni Kingaru) mwenye shati la mikono mirefu, akiwa kwenye mazishi ya mama yake mzazi Bi Kibibi Haji Pembe, aliyezikwa Machi 3, kijiji cha Misugusugu, Kibaha, mkoani Pwani.

  "Nashukuru Watanzania wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha msiba na mazishi ya mama yetu kwa kutufanyia mambo mengi yenye kuleta ushirikiano kwa jamii kwa rambimbari zilizoonyesha kuguswa na msiba huu. Familia haina cha kuwalipa, isipokuwa kwa Mungu pekee.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuwa Serikali itahakikisha kuwa
  sekta na miradi inayotambuliwa na kuingizwa kwenye Mfumo wa Tekeleza
  kwa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now au BRN) ni ile yenye manufaa
  makubwa nay a haraka kwa wananchi walio wengi.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Machi 5, 2015) wakati
  akizungumza wa wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa taarifa ya
  mwaka wa kwanza ya utekelezaji wa Mfumo wa Tekeleza kwa Matokeo
  Makubwa Sasa kwenye uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini
  Dar es Salaam.

  “Vigezo hivi ndivyo vilivyotumika kutambua sekta sita za mwanzo ambazo
  ni kilimo, elimu, nishati, uchukuzi, utafutaji rasilmali fedha na maji
  ambazo leo ndiyo tunapokea taarifa ya utekelezaji wake kwa mwaka wa
  kwanza,” alisema.

  Alisema vigezo hivyo pia vilitumika kuchagua mazingira ya biasharana
  huduma za afya kuziingiza kwenye utaratibu wa BRN. “Serikali inaamini
  kwamba kuimarika kwa mazingira ya biashara, hasa biashara ndogondogo,
  kutatoa fursa za watu wengi zaidi kujiajiri na kuajiri na kuajiri
  wengine,” aliongeza.

  Alitoa wito kwa watendaji wote kujifunza na kuutumia mfumo huo ili
  waweze kufikia malengo waliyojiwejkea kwa  haraka zaid. “Mambo matatu
  yanayoupa mfumo huu uwezo mkubwa zaidi ni kupanga kipaumbele; kuwa na nidhamu na uwazi; na haya mambo yako ndani ya uwezo wa kila Mmoja wetu ,” alisema.

  Alisema Serkali itaendelea kuchukulia utekelezaji wa mfumo wa Tekeleza
  kwa Matokeo Makubwa Sasa kama jambo la kipaumbele katika kutekeleza
  majukumu yake.

  “Haitoshi kwamba tumepata mafanikio haya katika mwaka Mmoja. Ni lazima sasa tuazimie sote kuchukua kanuni hizi na kuzitumia katika kila eneo
  la maisha yetu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha tumetoa mchango
  kamili kwa Taifa letu kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya
  Taifa ta Maendeleo hadi mwaka 2015,” alisema.

  Alitumia fursa hiyo kuwashukuru Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa
  halmashauri, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri kwa kusimamia vema
  utekelezaji wa BRN katika maeneo yao.


  Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuukuzungumza na washiriki kabla ya
  kuzindua taarifa hiyo, Mtendaji Mkuu wa Presidential Delivery Bureau,
  Prof. Issa Omari alisema utoaji wa taarifa hiyo ni hatua mojawapo kati
  ya hatua nane za mfumo huo. Aliwataka watendaji wanaotekeleza mfumo
  huo wahakikishe wanafuata hatua zote nane.

  Alisema kwamba jambo msingi katika utekelezaji wa BRN ni kubadilisha
  maisha ya wananchi na siyo tu kupima utendaji kazi wa mawaziri wa
  sekta husika.

  Alisema mojawapo ya mafanikio ya utekelezaji wa mfumo huo ndani ya
  mwaka mmoja ni ushirikishwaji wa jamii kwa kiwango kikubwa kiasi cha
  kusaidia kasoro za kijamii. “Kwa mfano katika sekta ya elimu, watu
  wanashangaa ufaulu kupanda haraka… lakini tuna shuhuda za utoro
  kupungua kwenye shule moja kutpoka watoto 500 hadi sifuri…. Hii ni kwa
  sababu tuliishirikisha jamii hadi ngazi ya chini,” alisema.

  Waziri Mkuu ameenda Kahama, mkoani Shinyanga kuwapa pole waathirika wa maafa ya mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa kuamkia jana. Mvua hiyo
  imesababisha vifo vya watu 92 na kujeruhi watu 98 huku mamia watu
  wakiwa hawana mahali pa kuishi.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  ALHAMISI, MACHI 5, 2015.

  0 0

  Pichani Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Abdulrahman Kinana ukielekea jimbo la Kimbakwe  Wilayani Mpwapwa mapema leo asubuhi kuendelea na ziara yake ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi ikiwemo na kuzitafutia ufumbuzi.
  Mwenyekiti wa kikundi cha Mkombozi,Bwa.Athanas Kigosi akitoa maelezo mafupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,kuhusiana na shamba la mfano ambalo limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha Kibakwe,Wilayani Mpwapwa.Bwa.Athanas alieleza changamoto wazipatazo katika maandalizi yao ya kilimo kuwa suala la pembejeo limekuwa tatizo kubwa kwao,kwani zimekuwa zikiletwa kinyume na wakati,hali inayowapelekea ugumu wa kuendelea na kilimo kwa wakati,mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo sambamba na mazao yao kutopandishwa bei,Hivyo Bwana Athanas ameiomba serikali kuwasaidia wakulima kupelekewa pembejeo kwa wakati ili kuhakikisha maandalizi ya kilimo yanakwenda kwa wakati.
  Katibu Mkuu wa  CCM,Ndugu Kinana akifafanua jambo kwa Wanahabari katika shamba la mfano ambalo limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha Kibakwe,Wilayani Mpwapwa.Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Kibakwe,jimbo la Kibakwe wilaya ya Mpwapwa,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoa wa Dodoma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe wilayani Mpwapwa.
   Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo husika.

  PICHA NA MICHUZI JR-KIBAKWE MPWAPWA


  0 0

        Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark Childress akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Leo Jijini Dar es Salaam.
       Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na balozi   wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark Childress(wa pili kulia) mara baada ya mazungumzo.

  Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark Childress akimuaga Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju alipomtembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Leo Jijini Dar es Salaam


  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Mzee  Donald Lubunda ambaye  amepoteza watoto wane katika maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha  katika  eneo la Mwakata wilayani Kahama Machi 3 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kuwapa pole waathirka leo
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa pole wanafamilia wa MzeeZakaria  Limbe ambao wamepoteza wototo wane katika mafa ya mvua kubwa yenye upepo na  mawe iliyonyesha katika eneo la Mwakata Machi  3 usiku. Alikwenda katika maeneo yaliyoathirika leo  kuwapa pole wananchi. 
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipa pole Shoma Petro  ambaye ni mmoja wa majeruhi wa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa yenye upepo na mawe iliyonyesha kwenye  eneo la  Mwakata wilayani Kahama Machi 3, 2015 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kwenye hospitali a wilaya ya Kahama kuwapa pole  majeruhi waliolazwa hospitalini hapo
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu, Jenista Mhagama  (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa ShinyangaDr Rufunga kukagua maeneo yalyoathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana  na upepo mkali na mawe katika eneo  Mwakata wilayani Kahama usiku Machi 3, 2015. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametembelea baadhi ya familia zilizopoteza
  wapendwa wao pamoja na majeruhi waliolazwa kwenye hospitali ya wilaya
  ya Kahama kutokana na maafa ya mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa
  kuamkia jana.

  Akizungumza na wafiwa katika vijiji vya Mwakata na Magugung’hwa katika
  kata ya Mwakata wilayani Kahama leo mchana (Alhamisi, Machi 5, 2015)
  Waziri Mkuu alisema Serikali haitawaacha katika kipindi hiki kigumu
  walichonacho.

  Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuwafikishia wafiwa na waathirika
  wa maaafa hayo salamu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye aliwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

  Akiwa katika shule ya msingi Mwakata ambako watu 250 wanahifadhiwa
  hapo kwa muda, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao pamoja na wananchi
  waliofika kumsikiliza kwamba Serikali imepanga kuleta vyakula, mahema,
  mablanketi na madawa ya hospitali ili kuwasaidia waathirika hao.
  “Serikali haitaacha mtu afe kwa njaa,” alisema.

  Pia aliagiza maghala ya NFRA yaliyoko Isaka yatumike kupokea misaada
  ya chakula kwa sababu yako karibu sana kata ya Mwakata. “Ili uratibu
  wa misaada uweze kufanyika hapa kijijini, ni vema maghala ya kuhifadhi
  chakula cha msaada yakahamia hapa Isaka kwa sababu ni karibu sana na
  hapa Mwakata,” alisema.

  “Yakiwa hapa itasaidia usimamizi na uhakika wa huduma zinazotolewa kwa
  waathirika. Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya simamieni hilo kwa sababu
  janga hili ni letu na linabebwa na Serikali,” aliongeza.

  Alisema ameongea na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid
  na kumwagiza atume watu wake wafanye tathmini ya hali ya afya kwani
  katika hali ya majanaga kama haya, ni lazima kuna hatari ya kutokea
  kwa magonjwa ya mlipuko.

  Mapema, Mbunge wa Msalala, Bw. Ezekiel Maige aliiomba Serikali itume
  misaada ya haraka ya vyakula na mahema kwa waathirika hao lakini pia
  ipeleke kikosi cha wanajeshi ili wasaidie kujenga nyumba za watu
  walioathirka kama ambavyo ilifanya kwa watu wa Kilosa mwaka 2009.

  Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
  Uratibu na Bunge), Bibi Jenista Mhagama ambaye anasimamia idara ya
  maafa ameuagiza uongozi wa wilaya ya Kahama kuhamishia timu ya
  waratibu wake kwenye eneo la tukio badala ya kufanyia kazi kutoka
  makao makuu ya wilaya ambako ni zaidi ya km. 30.

  “Misaada iasche kuratibiwa wilayani bali ihamie hapa Mwakata,  na hao
  wanaotoa misaada waambiwe wailete hapa kwenye eneo la tukio … uratibu
  ukifanyika kule hakuna atakayekuwa na picha halisi ya nini kinaendelea
  kwenye kijiji hiki,” alisisitiza.

  Mvua hiyo imesababisha vifo vya watu 42 na kujeruhi watu 98 huku mamia
  watu wakiwa hawana mahali pa kuishi. Pia watu 52 kati ya 112 waliokuwa
  wamelazwa hospitalini wameruhusiwa kurudi majumbani huku majeruhi 60
  wakiendelea kupatiwa matibabu.

  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, MACHI 5, 2015.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo. Walioketi kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo wakati akiongea na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania baad ya kukutana nao pamoja na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo Ikulu jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

  0 0

  gab1 
  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi Leah Kihimbi akimkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha kumi cha Sekta ya Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel na katikati ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo.
  gab2
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwasalimia wadau wa Utamaduni huku akiwa ameshika moja ya dhana za utamaduni alipokua akifungua kikao cha kumi cha Sekta ya Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo. gab3 
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na wadau wa Utamaduni alipokua akifungua kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo.

  gab4 
  Afisa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya Bw. Godfrey Msokwa akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo.
  gab5 
  Mmoja wa washairi (kushoto) akiburudisha wadau wa Utamaduni wakati wa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Kikundi cha ngoma kijulikanacho kama Jivunie Sanaa Tanzania kikitumbuiza wakati wa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. gab8 
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (waliokaa mwenye suti) katika picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya Utamaduni baada ya kufungua kikao kazi cha kumi cha Sekta hiyo jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)………………………………………………………………………
  Na: Genofeva Matemu – Maelezo
  Maafisa Utamaduni na wadau wa utamaduni wametakiwa kutumia sanaa kupitia fani mbalimbali kuhamasisha juhudi za kuifahamu na kuipokea katiba inayopendekezwa ili jamii ya watanzania kuweza kujipatia katiba inayokidhi mahitaji yao.

  Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua kikao kazi cha kumi cha Sekta ya Utamaduni, Uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.

  Profesa Gabriel amesema kuwa lengo la kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni ni kutanabaisha maudhui ya Katiba inayopendekezwa hivyo kuwataka wadau wa utamaduni kutumia tasnia ya sanaa inayoumbwa na herufi K tatu zinazolenga Kuhabarisha, Kuelimisha na Kuburudisha jamii katika masuala mbalimbali.

  “Utamaduni ni kama inta inayoshikamanisha watu, ni vyema wadau wa utamaduni mkatumia talanta mliyonayo kufikia fikra za watu kwani suala la katiba pendekezwa ni letu sote kama watanzania hivyo tujivunie kwa kuweka mambo kwenye vitendo na kuishi yale tunayoyasema” amesema Profesa Gabriel.

  Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi. Leah Kihimbi amesema kuwa sanaa imekua ikitumika kusaidia makundi mbalimbali katika jamii kutoa sauti zao kwenye mambo mbalimbali na kuamini kuwa sanaa ina nafasi kubwa ya kuhamasisha na kuelimisha jamii maudhui ya katiba inayopendekezwa.

  Bibi. Kihindu amesema kuwa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kimewashirikisha maafisa utamaduni kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara kikiwa na madhumuni ya kueleza mchango wa fani za sanaa katika kuelimisha umma maudhui ya katiba inayopendekezwa na kutoa ufafanuzi wa masuala ya Sekta ya Utamaduni yaliyozingatiwa katika Katiba inayopendekezwa.
   Akizungumza kwa niaba ya maafisa Utamaduni kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara, Afisa Utamaduni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw. Godfrey Msokwa amesema kuwa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kitawawezesha wadau wa utamaduni kutumia sanaa kuifikia jamii na kutekeleza maazimio yatakayokusudiwa na kikao hicho.

  Kikao kazi cha 10 cha Sekta ya Utamaduni chenye kauli mbiu isemayo Fani za Sanaa zielimishe Umma Maudhui ya Katiba Pendekezwa kimelenga kutumia sanaa kama kichocheo na mbinu mojawapo ya kuelimisha, kuonya na kuelekeza mambo mbalimbali yanayoihusu jamii.

  0 0
 • 03/05/15--21:01: Viwanja vinauzwa


 • 0 0

   
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye sambamba viongozi mbalimbali wa chama mkoani Dodoma jana wamemaliza ziara ya Kikazi katika jimbo la Mpwapwa na Kibakwe mkoani Dodoma,ambapo leo wanaanza ziara katika jimbo la Kongwa.Kinana anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.

  0 0

   
  Muimbaji wa Nyimbo za Injili Rehema Chawe

  MSANII wa nyimbo za Injili, nyanda za juu kusini Rehema Chawe ambaye ni Mwanachama wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA), anatarajia kuzindua albamu yake ya kwanza, inayoitwa Kusamehe ni afya.
  Uzinduzi huo unatarajia kufanyika Jumapili, March 8, mwaka katika kanisa la EAGT, Frelimo kwa mchungaji Mwenda, ambaye ni Mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste mkoani Iringa.
  Akizungumza na wanahabari, Chawe alisema uzinduzi huo utapambwa na waimbaji wengi toka nje na ndani ya mkoa wa Iringa.
  Alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa, ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Iringa, Enock Ugulumo.
  Mwenyekiti wa CHAMUITA mikoa ya nyanda za juu kusini, Tumaini Msowoya Kibiki aliwataka wanachama wote kuwepo kwenye uzinduzi huo ili kumsindikiza mwenzao.
  “Ni jukumu la waimbaji wote hususani wanachamuita kuhakikisha wanakuwepo siku ya uzinduzi ili kumuunga mkono mwanachama wenzetu,”alisema Kibiki.

older | 1 | .... | 477 | 478 | (Page 479) | 480 | 481 | .... | 1898 | newer