Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 475 | 476 | (Page 477) | 478 | 479 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Msanii wa TOT Khadija Omary Kopa akiwasili uwanjani hapo.

  0 0

  Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers wakipiga picha ya ukumbusho na mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga (wa tano kulia) katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyokutanisha bloggers kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini, Muhidin Issa Michuzi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wageni waalikwa juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika juzi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini, Muhidin Issa Michuzi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wageni waalikwa juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika juzi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam

   BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limekubali kuanza ushirikiano na uhusiano mzuri na Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) mara kitakapo maliza mchakato wa usajili wake na kutambulika rasmi kisheria. MCT imesema kwa hatua ya kwanza itafanya mazungumzo na viongozi wa TBN na kujadiliana namna gani ya kuisaidia TBN.

   Kauli hiyo imetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mkajanga alipokuwa akizindiwa hafla ya kwanza ya mwaka 2015 ya wamiliki na waendeshaji wa blogu na mitandao mingine ya kijamii iliyofanyika katika Hoteli ya Serena. 

  Katibu huyo Mtendaji wa MCT alisema kwa maendeleo ya sasa ya teknolijia ya habari na mawasiliano ni vigumu kuzitenga blogu kama vyombo vya habari, hivyo kuahidi kushirikiana na TBN kuhakikisha inafikia malengo yake ya kuwaunganisha bloggers na kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili.

   Alisema MCT inasubiri TBN ipate usajili kisheria toka mamlaka husika serikalini na baada ya zoezi hilo itaanza kushirikiana maramoja na chombo hicho kilichoanzishwa kuwaunganisha wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii nchini na wale wanaofanya shughuli za nje ya nchi. 

  "...MCT ipo tayari wakati wowote kuanza kushirikiana nanyi kikazi, tunachosubiri ni TBN kusajiliwa rasmi...mtakapo maliza usajili tu njooni ofisi, tutazungumza na viongozi wenu ili kujua nini cha kuwasaidia. Naombeni msichelewe tuanze hili mara moja," alisema Kajubi Mkajanga akizungumza na wana-TBN kabla ya kuzinduwa sherehe hiyo. 

   Awali akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi alisema kwa sasa mitandao ya kijamii imekuwa ikitekemewa na kundi kubwa la jamii katika kusambaza taarifa kwa haraka licha ya uwepo wa changamoto kadhaa ndani ya tasnia hiyo. 

   Alisema pamoja na mambo mengine, TBN imeanzishwa kwa lengo la kuwaunganisha waendeshaji na wamiliki wa blogu pamoja na mitandao mingine ya kijamii, na pia kuhakikisha wana-TBN wanapata fursa ya kujifunza zaidi maadili ya tasnia ya habari na mawasiliano ili kufanya kazi zao kiufanisi zaidi. 


  Aidha aliishukuru Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania kwa kusaidia kufanikisha tukio la kukutana 'bloggers', pamoja na Benki ya NMB na makampuni mengine ya Coca Cola, AIM Group na kampuni ya huduma za intanenti ya Raha kufanikisha tukio hilo la kuwaleta pamoja bloggers wa Tanzania. 

   Akisoma risala ya wana-TBN kwa mgeni rasmi, Mjumbe wa TBN, Henry Mdimu alisema licha ya blogu kuwa chanzo kikubwa cha habari na mstari wa mbele kuwafikishia wananchi habari kwa haraka zaidi lakini bado zimekuwa hazitambuliwi na mamlaka zinazosimamia na kutetea tasnia nzima ya habari.

   "...Pamoja na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na 'bloggers' na waendeshaji wa mitandao ya kijamii, bado hawatambuliki rasmi na mamlaka husika pamoja na taasisi zinazohusika na usimamizi wa tasnia hii likiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Idara ya Habari (Maelezo), MISA-Tan na hata Mfuko wa Ruzuku kwa Vyombo vya Habari nchini (TMF). "..Tunasema hivi maana tunaona kwa namna moja ama ingine wadau hawa muhimu hawajumuishwi katika harakati au michakato yoyote ile mnayoifanya kwenye tasnia hii. 

  Mfano kupata semina za MCT, kupewa vitambulisho (Press card), kushiriki katika mafunzo na hata mashindano ya kila mwaka ya wanahabari yanayoandaliwa na MCT," alisema Mdimu akisoma risala ya TBN mbele ya mgeni rasmi Bw. Mkajanga. Kwa upande wa waalikwa rasmi kutoka ubalozi wa Marekani wakizungumza katika hafla hiyo kupitia kwa mwakilishi wao ameahidi kuisaidia TBN katika programu mbalimbali ili kuchochea uhuru wa habari nchini Tanzania. *Imeandaliwa na www.thehabari.com 

  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa hafla ya TBN, akizungumza machache katika hafla hiyo. Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa hafla ya TBN, akizungumza machache katika hafla hiyo.[/caption] [caption id="attachment_55612" align="aligncenter" width="800"]Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga moja ya dhawadi zilizotolewa na baadhi ya wadhamini wa hafla ya TBN. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga moja ya dhawadi zilizotolewa na baadhi ya wadhamini wa hafla ya TBN.[/caption] [caption id="attachment_55609" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.[/caption] [caption id="attachment_55610" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.[/caption] [caption id="attachment_55611" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.[/caption] [caption id="attachment_55613" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

  0 0

  Universal broadband is a real target to achieve through public private partnerships, says Etisalat Group CEO

  ·         Access to broadband is a basic right for everyone and it can be served smartly, where needed, says Ahmad Julfar
  ·         Artificial policies, long pay-back on infrastructure investments and diminishing returns impact ability of telcos to invest and innovate

  Abu Dhabi, March 2, 2015: Universal broadband is a real target that can be achieved through public private partnerships to promote greater digital, social and financial inclusion in the developing world, observed Mr. Ahmad Julfar, Chief Executive Officer of Etisalat Group.

  He was addressing an audience of some of the world’s leading figures in telecommunications at Mobile World Summit (MWS), the premier event of the ongoing 2015 Mobile World Congress in Barcelona. Mr. Julfar also holds the position of Vice Chair of the GSMA, which organizes the annual Congress and unites over 800 telecom operators and over 250 companies that operate in the broader mobile eco system.

  Mr. Julfar said that the public internet needs to evolve further and this requires investment in capacity, new solutions, technologies andinnovative business models. The telco sector will not be able to drive this alone, as they face the risk of a big disruption due to the shifts across the value chain.

  “Etisalat believes that access to broadband is a basic right for everyone and it can be served smartly, where needed,” he said. “But providing universal access to broadband poses a challenge for telcos because network investments not only have long pay-back periods and capex on infrastructure today yields diminishing returns.”

  Mr. Julfar said that “new investment models based on semi-public funding from governments or infrastructure-sharing models defined by regulators are urgently needed and should be encouraged.”

  Sharing his views on ‘connecting billions across the developing world,’ Mr. Julfar said: “The benefits of increasing connectivity are clear to see in economic, social and environmental fields, but there is a clear digital gap. Some 60 per cent of the world’s population remains unconnected, the majority of which is in rural areas of the developing world.”

  By 2020, approximately 3.8 billion men and women, or half of the world’s population will be connected to the internet via mobile and a vast majority of the new users will be in developing countries.

  “Telecommunications revolutionises everything we do; it is the industry that changes all other industries. Governments know it.  That's why, over the past 10 years, more than 150 governments have developed or are developing national broadband networks.  The primary goal is to make the country benefit from the economic impact of broadband. And we share a common interest to keep investing in the future internet.”

  Mr. Julfar proposed a number of changes the telecommunications ecosystem - Governments, Regulators, Internet companies and NGOs – should embrace. These include: new competitive models to allow telcos to focus on market value creation through collaboration between private and public sectors to distribute more choice, affordability and welfare to citizens.

  Mr. Julfar added: “Some of the most innovative models today come from emerging countries. Etisalat Group takes a different approach in various developing countries that it operates in, and not one size fits all. Our ability to be flexible to meet individual market need drives our growth across the region. This flexible approach has enabled Etisalat Group to extend service provision for millions of people.”

  Etisalat Group today encompasses 19 countries across two continents, and includes dynamic emerging markets across the Middle East, Asia and Africa serving over 182 million subscribers.

  Mr. Julfar was joined on the panel by HM Queen Maxima of the Netherlands, United Nations Special Advocate for Inclusive Finance for Development; Mr. Jon Fredrik Baksaas, Chairman, GSMA and President and CEO, Telenor Group, and Ms. Ann Cairns, President, International Markets, MasterCard.

  0 0

    Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Bi. Theresia Muhongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Haji Sajilo ambaye ni Kiongozi msimamizi wa Mipango wa NGO,s ya MOYODEI wakati alipotembelea kwenye mabanda yaliyoharibwa vibaya na mvua iliyonyesha jana jioni. Haya mabanda yalikuwa ni kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyotakiwa kuanza leo jumanne lakini kutokana na maafa hayo maonyesho hayo yamesogezwa mpaka tarehe 5/03/2014 kwa ajili ya ukarabati wa mabanda hayo.(Picha na Pamoja Blog)
   Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Bi. Theresia Muhongo akipata maelezo kutoka kwa mama kuhusu mabanda yaliyoezuliwa na mvua iliyokuwa na upepo mkali
   
   
  Baadhi ya Mabanda yakiwa yameharibika vibaya 

  0 0

  Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Triple A LTD na Mfanyabiashara wa Jijini Arusha, Papaa King Mollel (kulia) akimkabidhi pikipiki kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Novatus Makunga ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini kwa ajili ya kusaidia na kurahisisha shughuli za maendeleo katika kata ya KIA wilayani Hai mkoani Kilimanjaro . Hafla hiyo ilifanyika leo Sakina jijini Arusha.
   Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Triple A LTD na Mfanyabiashara wa Jijini Arusha, Papaa King Mollel (kulia) akikabidhi kadi ya pikipiki hiyo kwa Mkuu huyo wa Wilaya.
  Viongozi mbalimbali wa kata ya KIA wakishuhudia mkurugenzi mkuu wa Triple A LTD Papaking Mollel akimkabidhi pikipiki aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Novatus makunga kwa ajili ya kuchangia na kusaidia  shughuli za maendeleo ya kata ya KIA.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ametangaza kutobomoa nyumba zilizopo kando kando ya  barabara ya Mwanga-Kikweni/Vuchama-hadi Lomwe km 40.6 na kusema kuwa barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami kwa kutumia upana wake uliopo sasa hivi.

  Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo ya faraja kwa wakazi wa Kikweni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro kabla ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mwanga-Kikweni/Vuchama-Usangi hadi Lomwe(km 40) itakayojengwa kwa kiwango cha lami hivi karibuni.

  Waziri wa Ujenzi amechukua uamuzi huo kutokana na maeneo mengi ya milimani ambapo barabara hiyo inapita kuwa na mashamba ya watu tofauti na sehemu nyingine. “Nikiwa kama Waziri wa ujenzi katika maeneo haya ya milima sitatumia sheria ya mita 30 kila upande katika ujenzi wa barabara hii ili nyumba na mashamba ya wakazi wa huku yasiathirike”.

  Dkt. Magufuli aliongeza kuwa ujenzi wa Barabara una sheria zake ndio maana ameamua kutumia sheria ya barabara  namba 13 ya mwaka 2007 kifungu cha 13 na 20 kinachompa mamlaka kupunguza upana wa barabara.

  Aidha, Waziri Magufuli aliwatoa hofu wakazi wote waliowekewa alama ya X katika nyumba zao na kuwataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwasababu nyumba hizo hazitabomolewa.

  Katika hatua nyingine Dkt. Magufuli aliwataka watu wote waliojenga vibanda karibu na barabara ya zamani waanze kuondoka mapema kabla ya ujenzi wa barabara hiyo kuanza hivi karibuni.

  “Nawaomba wote mlioweka vibanda karibu na barabara mtoe kwa hiari yenu ili tutengeneze barabara hii bila vikwazo na kwa haraka tofauti na awali ambapo tulikuwa tunatangaza zabuni kwa kilomita chache” alisisitiza Waziri Magufuli.

  Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amemshukuru Waziri Magufuli kwa hatua yake hiyo na kusema kuwa kufunguka kwa barabara hiyo ni mkombozi mkubwa kwa wilaya ya Mwanga na Mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

  “Wilaya yetu hii inapakana na nchi jirani hivyo hata kiusalama ni vizuri barabara hii ikajengwa kwa lami ili irahisishe mawasiliano kwa haraka zaidi katika Wilaya yetu hii” alisema Mkuu wa Mkoa.

  Naye Mbunge wa Mwanga ambaye pia ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe ameishukuru Serikali na kusema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutawaondolea kero kubwa ya usafiri wananchi wa Usangi na mwanga na kuwasaidia kufanya biashara kwa urahisi zaidi tofauti na awali.

  “Kukamilika kwa barabara hii kutasaidia kuinua uchumi mkubwa uliopo huku Usangi tofauti na hali iliyopo sasa” Alisema Profesa Maghembe.

  0 0


  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itatumia shilingi bilioni 55 kuvipatia umeme vijiji 244 vya mkoa wa Mbeya kupitia Miradi ya Umeme Vijijini (REA).

  Ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Machi 2, 2015) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara yake ya siku saba kwenye mkoa huo. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mkapa, jijini Mbeya.

  “Nimeambiwa kuwa katika mwaka 2014/15, jumla ya vijiji 244 vitapatiwa umeme kupitia REA. Vijiji hivyo ni kama ifuatavyo: Chunya viko 13, Mbeya ni 32, Mbarali (56), Mbozi (14), Momba (15), Kyela (30), Ileje (18) na Rungwe (66) na jumla ya shilingi bilioni 55/- zitatumika kwa madhumuni hayo,” alisema.

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa mkoa huo kwa kusimamia suala la usambazaji wa umeme vijijini na kukamilisha awamu ya kwanza ya miradi ya umeme vijijini katika vijiji 17 vya mkoa huo.

  “Nimeelezwa kuwa miradi hiyo iliyogharamu ya shilingi billioni 7.6 katika vijiji 17 imekamilika kwa asilimia 100. Katika  Halmashauri ya Mbeya kuna vijiji vitano, Mbozi vijiji vinne, Chunya vijiji sita na Rungwe vijiji viwili; na imeweza kuunganisha wateja 650,” alisema.

  Alisema taarifa zinaonesha kuwa vijiji vilivyopangwa kupata umeme wa REA mwaka 2015/2016 ni 51 na kwamba hivi sasa ujenzi wa njia kubwa ya umeme wa 11Kv na 33Kv unaendelea. “Pia ujenzi wa njia ndogo ya umeme 400v unaendelea kujengwa na utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia 42.3,” aliongeza.

  Aliwahimiza viongozi wa mkoa huo kuongeza jitihada za kusambaza umeme kwa kuwa mahitaji ya umeme ni makubwa kwa wananchi wengi.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMANNE, MACHI 3, 2015.

  0 0


  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema mkoa wa Mbeya unaweza kupaa kiuchumi kama utazingatia fursa za kibiashara ilizonazo na kuwekeza zaidi kwenye viwanda vya usindikaji mazao ya kilimo na mifugo.

  Ametoa kauli hiyo  jana (Jumatatu, Machi 2, 2015) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara yake ya siku saba kwenye mkoa huo. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mkapa, jijini Mbeya.

  “Nguvu kubwa mnayo katika biashara hasa kama mtajitahidi kutumia vema fursa kubwa ya uwekezaji katika viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na mifugo mliyonayo,” alisema.

  Waziri Mkuu alisema mkoa wa Mbeya katika msimu wa 2013/2014 umeweza kuzalisha tani 4,159,907 za nafaka na kuuwezesha kuwa na ziada ya chakula ya tani 3,347,680.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema mkoa wa Mbeya bado una fursa nzuri ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na unaweza kuiwezesha kama nchi kuuza chakula katika masoko ya Afrika na Afrika ya Mashariki kama watajipanga vizuri.
  Wakati huo huo, Waziri Mkuu aliwapongeza viongozi hao kwa kuuwezesha mkoa wa Mbeya kutoa mchango mkubwa katika Pato la Taifa. “Katika taarifa ya mkoa, nimeelezwa kuwa mwaka 2013, mkoa huu ulichangia shilingi trilioni 3.951 na hivyo kushika nafasi ya tatu kati ya mikoa yote nchini ikitanguliwa na mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.”
  Alisema kutokana na ukuaji wa kasi wa idadi ya watu ambao ni asilimia 2.7, mtu akichukua pato hilo la mkoa na kuligawanya kwa idadi ya watu wa mkoa wa Mbeya anapata wastani wa pato la kila mwananchi kuwa ni sh. 1,420,427. “Kipato hicho, ni sawa na shilingi 118,369 kwa mwezi au shilingi 3,946 kwa siku sawa na Dola za Kimarekani (US $) 2.3,” alifafanua.

   Waziri Mkuu alibainisha kwamba mtu akichukua wastani wa pato la kila mwananchi kwa mwaka 2013 na kupanga kwa mikoa yote, mkoa wa Mbeya unashuka na kushika nafasi ya sita kitaifa. Aliitaja mikoa inayowatangulia kuwa ni Dar es Salaam sh. 1,990,043/- ambao ni wa kwa kwanza; wa pili ni Iringa (sh. 1,660,532/-); wa tatu ni Arusha (sh. 1,448,782/-); wa nne ni Kilimanjaro (sh. 1,444,882/-); wa tano ni Ruvuma (sh. 1,438,392/-) na wa sita ni Mbeya (sh. 1,420,427/-).

   “Nawashauri muongeze juhudi za kuipita mikoa hiyo kwa kuwa mna fursa nyingi za kuongeza uzalishaji hasa katika mazao ya kilimo cha kahawa, kakao, mpunga, mahindi, viazi, pamoja na mazao ya maliasili kama vile mazao ya misitu, na uvuvi na uchimbaji madini,”.

  Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku saba mkoani Mbeya leo kwa kufanya majumuisho ya ziara yake na amerejea jijini Dar es Salaam jana jioni (Jumatatu, Machi 2, 2015) .


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMANNE, MACHI 3, 2015.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Hashimu Shaibu akila kiapo cha utumishi mbele ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda  jana katika hafla iliyofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huyo.chanzo libeneke la kaskazini blog

  0 0

   Kikundi cha ngoma cha watoto wa mitaani wakitumbuiza katika shughuli ya kuwakusanya watoto wa mitaani iliyofanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto wa mitaani kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao
  Baadhi ya Watoto wa mitaani waishio jijini Arusha waliokusanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto wa mitaani kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao


  Watoto wa mitaani wanaoishi  jijini Arusha katika mazingira hatarishi wanatarajiwa kujengewa Hostel zitakazowasaidia kuondokana na adha ya kupata sehemu za malazi hivyo kulazimika kulala maeneo ya stendi za mabasi na masoko.

  Mkurugenzi wa shirika la Gola linalojihusisha na masuala ya watoto wa mitaani jijini Arusha,Sawale Maghema  amesema kuwa mpango huo utasaidia watoto wa mitaani kuondokana na mazingira magumu yanayowapelekea kujiingiza katika vitendo vya uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya.

  Sawale alisema kuwa iwapo watoto wa mitaani watatelekezwa na jamii bila kusaidiwa wanaweza kugeuka na kuwa mwiba kwa jamii ya Watanzania hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuwasaidia watoto hao .

  "Watoto wa mitaani tuna mpango maalumu wa kuwakusanya na kuwakutanisha pamoja kujua mahitaji yao ,malengo na matarajio waliyonayo ili kuwasaidia kwa kushirikiana na jamii hata kwa hili la ujenzi wa Hostel litasaidia kuwaweka pamoja tukiwaacha waendelee kukaa mitaani hawatabadilika wataendelea kuwa na maisha mabaya" Alisema Sawale

  Mdau wa Masuala ya utalii Mustafa  Panju  alijitolea kuwasaidia watoto wa mitaani kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa watoto hao ili waweze kupata mahitaji muhimu  ,Ameeleza kuwa jamii inapaswa kuamka na kuwasaidia watoto hao badala ya kuwaacha waendelee kukaa kwenye mazingira hatarishi.

  Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Arusha ,Hassan Omari akizungumza kwa niaba ya watoto wa mitaani anaeleza kuwa watoto wa mitaani wana ndoto nyingi,vipaji na uwezo wa hali ya juu hivyo wakisaidia wanaweza kufika mbali na kulisaidia taifa .

  Chanzo:libeneke la kaskazini blog

  0 0

  Mshauri wa mambo ya Afya kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) Dk. Andemichael Ghirmay akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort na yamezaminiwa na WHO.za2 
  Mgeni rasmin Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed Jidawi akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kukabiliana na ugonjwa wa Ebola. za3 
   Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mgeni rasmin Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed Jidawi (hayupo pichani) wakati alipokua akifungua mafunzo hayo huko Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mjini Ungujaza5 
  Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mgeni rasmin Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed Jidawi (hayupo pichani) wakati alipokua akifungua mafunzo hayo huko Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mjini Unguja
  za6 
    Mmoja wawakufunzi kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) anaefanyia kazi Tanzania Dk. Grace Saguti akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha mada yake.
  za7 
  Mgeni rasmin Dkt. Jidawi katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

  NAPOKEA simu ambayo nashindwa kuielewa. Simu hii inatoka kwa rafiki yangu anayeishi mjini Dodoma, anayejulikana kwa jina Mustafa Mussa Seiph. Kijana huyu ananiuliza juu ya habari za kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni  John Komba.

  Komba amefariki Dunia  huku akiwa anategemewa kwa kiasi kikubwa kwa jimbo lake la Mbinga Magharibi, bila kusahau Chama Cha Mapinduzi kinachojiandaa na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwezi Oktoba mwaka huu nchini kote.

  Kuulizwa juu ya kifo cha Komba kiliendelea kutoka kwa watu tofauti waliokuwa wameshangazwa na habari hizo juu ya msiba wa nguli huyo wa muziki, ambaye mara kadhaa nyimbo zake zimekuwa zikitumika kwa matukio muhimu.

  Baada ya kufuatilia katika vyanzo tofauti, hatimae nilikubali matokeo kuwa Kapteni Komba hatupo naye duniani, yani ametangulia mbele ya haki, Februari 28 katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam, akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Ni majonzi makubwa kumpoteza mtu kama Komba, hii ni kutokana na umuhimu wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Katika kufuatilia suala la kifo cha Komba, mtu anaweza kufika mbali kwa kuona ni bora angebaki yeye na kuondolewa watu kadhaa ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wa kawaida ndani ya chama na serikali kwa ujumla.

  Hata hivyo, wakati tunaendelea kuomboleza kifo cha Komba, wanajitokeza wachache wenye roho mbaya na kufurahia kifo chake. Kwanini? Ni binadamu gani mwenye roho ya utu anayeweza kufurahia kifo cha binadamu mwenzake?
   
  Hata jamii hiyo inatofautiana kisera, kidini au kiitikadi bado si sababu ya kuona mtu anashangilia kifo cha mwenzake, kama anavyoweza kushangilia mnyama aliyeangushwa. Nchi yetu yenye amani na utulivu, watu wa aina hii wanatokea wapi.

  Inashanaza na kuumiza. Ni punguani pekee anayefurahia kifo cha Kapteni Komba. Ingawa alikuwa mwana CCM, lakini pia alikuwa mbunge na mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Mbinga Magharibi Tanzania Bara.

  Hakuwa na uadui kiasi hicho. Ndio maana tulishuhudia watu wengi wakipokea kifo cha Komba kwa masikitiko makubwa. Nani atairithi sauti yake. Nani atatumia muda mchache kutoa nyimbo bora zinazosimamia uzalendo na kuhamasisha mengi nchini kwetu.


  Inasikitisha kuona siasa zinaondoa utu wetu. Kama viongozi wa upinzani wote wameumizwa na kifo cha Komba, mfuasi gani anayeweza kuwa tofauti na wakubwa wao? Hata kama alikuwa na jambo lisilofurahisha wachache wao, bado sio sababu ya kuanza kumdhihaki kwa namna moja ama nyingine, hata pale tunapoliona jeneza lake.

  Binadamu duniani tunapita tu. Safari yetu ni moja. Unapoona mwenzako ametangulia mbele za haki, jua na wewe unafuata. Huo ndio ukweli. Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa, alizungumzia kifo cha Komba kwa huzuni za aina yake.

  Kama hivyo haitoshi, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alionyesha mapenzi kwa Komba. Idadi kubwa ya viongozi kutoka vyama vya upinzani walionekana kwenda kwa wingi kumuaga marehemu Komba, aliyezikwa jana kijijini kwao Lituhi.

  Hii ni kuonyesha kuwa upinzani na kushindana ni kwenye siasa tu. Inapotokea suala la kifo, hakika kila mmoja wetu anapaswa kuumia. Kama hivyo ndivyo, hakika nawashangaa wanaotumia muda mwingi kumdhihaki, wakitumia mwanya huo kutokana na misimamo yao tofauti.

  Hizo sio siasa. Angalia, Komba alikuwa akiamini kuwa anayestahili kumrithi Rais, Dr Jakaya Mrisho Kikwete ni Edward Lowassa tu. Alilisema hili mchana na usiku. Alisimamia kwenye hoja yake hiyo bila woga wowote. Lakini kuonyesha ukomavu wa kisiasa na pia huzuni katika matatizo, bado haikuwa sababu ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuacha kuhudhuria msiba wa mwanasiasa huyo.

  Si Membe tu, kundi la wagombea urais wengi ndani ya CCM walimiminika kwa wingi kuomboleza msiba huo bila kuangalia Komba aliwaunga mkono au aliwapinga. Ndio siasa zinavyotaka moyo na uzalendo wa hali ya juu.

  Ukiacha katika majukwaa ya kisiasa, bado sote ni binadamu na Watanzania halisi. Tunapaswa kuishi kwa upendo. Hatupaswi kufurahia matatizo yanayotokea wenzetu. Huo si ubinadamu. Ni zaidi ya unyama usiostahili kuungwa mkono.

  Mara baada ya kupata taarifa za msiba huo, sikuridhishwa hata kidogo juu ya watu waliokuwa wakisambaza picha mbaya za marehemu Komba. Wengine walifika mbali kwa kusambaza picha ya saa chache baada ya kifo chake.

  Bado najiuliza. Watu wa aina hii hawajui uchungu wa kufiwa? Hivi kama aliyefariki ni baba zao, mama zao au mtu wao wa karibu anaweza kupata ujasiri wa kuisambaza picha ya marehemu? Hata kama anao moyo huo, bado hauwezi kumtuma awatumie picha isiyoridhisha wengine.

  Huu si uungwana. Fikiria usambaziwe picha ambayo kiuhalisia tu haifai, utajisikiaje? Kama sababu ni siasa, je picha hizo za marehemu zimesambazwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu au viongozi wengine?

  Upuuzi huo unafanywa na watu wasiofahamu hata gharama za ada ya uanachama wa Chadema kwa kipindi cha mwaka mmoja. Watanzania tusifike huko. Msiba wa Komba si wa CCM na familia yake tu, ila Watanzania wote wameguswa.

  Kabla ya kuingia kwenye siasa, Komba alikuwa mwalimu. Pia akawa mwanajeshi. Nafasi zote hizo zilikuwa ni za kuwatumikia Watanzania wote. Na kama kelele zinakuja kwa sababu ya kupingana juu ya maoni ya Katiba, sidhani kama ni sahihi.

  Hii ni kwa sababu kila mtu alikuwa na ruhusa ya kutoa maoni yake aliyoona yanafaa kwa ajili ya kujenga mustakabali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na si Komba tu, ila inapotokea msiba, hakuna haja ya kuonyesha chuki dhidi ya wenzetu hao.

  Tuwaombee dua tukiamini nasi tunaelekea huko. Hakuna atakayeishi milele. Leo ni Komba, kesho ni wewe au mimi. Pamoja na mambo hayo machache ambayo wasiojua nini maana ya siasa wanalalama, bado Komba alikuwa mmoja wa viongozi makini na wenye mchango katika Taifa letu.

  Komba aliweza kusimamia hoja zake bila haya wala soni.  Siasa sio chuki wala uadui. Mtu anayeweza kuudhihaki mwili wa marehemu huyo ana walakini. Ni punguani pekee anayeweza kufurahia msiba wa Komba au binadamu mwenzake yoyote.

  Watanzania sisi wote ni wamoja. Rais Kikwete alidhihirisha namna gani kifo cha Komba kimemgusa yeye na Watanzania wote baada ya kushindwa kujizuia kutoa chozi. Wengine walionekana kutoa chozi ni Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba na wengineo wengi waliomiminika katika Viwanja vya Karimjee kumuaga Kapteni Komba.

  Huenda viongozi hao wa CCM walijaribu kuvuta picha katika kampeni zijazo. Lakini pia wengine wanajaribu kuangalia namna gani umuhimu wa Komba ulipaswa kuendelea kuwapo katika nchi yetu inayopambania maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Ni kutokana na hilo, naomba Watanzania tuwe wamoja katika kumuombea marehemu Komba akapumzike kwa amani, sanjari na kuomba dua kwa viongozi na wananchi wote katika sekeseke la uchaguzi lililozidi kushika kasi.

  Hakuna haja ya kumdhalilisha marehemu hata kama kuna aliyokuwa akiyafanya huvutiwi nayo, hii ni kwa sababu hakuna aliyekamilika hapa chini. Nenda Komba. Tutakumbuka, ila ni punguani pekee anayefurahia kifo chako. kambimbwana@yahoo.com
  +255712053949

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Kwimba
  TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo imepongezwa na serikali kwa hatua yake ya kufungua tawi wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
  Meneja Mauzo wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, akimuelekeza jambo Katibu Tawala wa Wilaya Kwimba, Vicent Emmanuel, katika uzinduzi wa tawi jipya wilayani humo, uliofanyika Machi 2 mwaka huu. Wengine ni maofisa wa taasisi hiyo, Ramadhan Hanafi na Monica Mwangoka. Picha na Mpigapicha Wetu.

  Shughuli za uzinduzi huo zilifanyika Machi 2 mwaka huu, huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, akiongozana na viongozi mbalimbali wa serikali wilayani humo.
  Katibu Tawala wa wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, kushoto akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi tawi jipya la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Kulia ni Meneja Mauzo wa taasisi hiyo Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Picha na Mpigapicha Wetu.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Tawala huyo wa wilaya Kwimba, Emmanuel alisema kwamba kufunguliwa kwa tawi hilo kutatoa huduma karibu na wananchi, kama njia ya kukuza uchumi wao kwa ujumla, zikiwapo fursa za kukopeshwa bidhaa mbalimbali, vikiwamo vyombo vya usafiri.

  Alisema kwamba awali watu wa Kwimba walilazimika kusafiri umbali mrefu kupata huduma za mikopo, lakini sasa wamesogezewa huduma karibu, hivyo ni jukumu lao kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujinufaisha kwa ajili ya maisha yao.

  “Serikali tunaipongeza Bayport Financial Services kwa hatua ya kuanzisha tawi hapa Kwimba, hivyo tunaamini kwa pamoja tutafanikisha maendeleo kwa watu wote kwa kupitia njia ya mikopo kwa watumishi wa umma na wafanyakazi waliodhinishwa,” alisema Emmanuel.

  Naye Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, alisema kwamba tawi lao limejipanga kutoa huduma bora kwa wakazi na wananchi wa Kwimba waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kupata huduma zao.
  “Huu ni mwendelezo wa Bayport Financial Services kuhakikisha kwamba tunaendelea kufungua matawi katika sehemu mbalimbali, ambapo sasa tumefikisha matawi 79 nchini kote, ambapo uwapo wa taasisi yetu umerahisisha maisha kwa watumishi wa umma na wafanyakazi waliodhinishwa na taasisi yetu.

  “Tunaomba wachangie fursa za mikopo mbalimbali kama ile ya bidhaa, mikopo ya fedha, bima ya elimu kwa uwapendao, ambapo katika mikopo ya bidhaa, mteja anaweza kukopeshwa bodaboda, vifaa vya ujenzi, injini za boti, pembejeo za kilimo na huduma nyingine nzuri na muhimu kwa Watanzania wote,” alisema.

  Kwa mujibu wa Kasambala, huduma za Bayport ni rahisi kupatikana ndani ya saa 24, huku zikiwa hazina amana wala dhamana, jambo linaloonyesha mafanikio makubwa kwa wateja wetu watakaoamua kupata huduma katika taasisi yao.

  Bayport Financial Services ni taasisi inayojihusisha na mikopo, huku ikiwa na matawi katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, ambapo kwa kupitia tawi la Kwimba, wateja wao hawatalazimika kusafiri ili wapate huduma za taasisi hiyo.

  0 0

  *AUNDA KAMATI YA KUSHUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI KINONDONI
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. 
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema kuwa wilaya ya Kinondoni inakabiliwa na changamoto migogoro ya ardhi ambayo inatakiwa kila mtu ambaye amenyimwa haki ya ardhi watapata kutokana na utaratibu uliopo.
  Makonda aliyasema hayo hivi karibuni wakati ziara ya kutembelea wilaya hiyo, Makonda alisema asili ya migogoro hii inatokana hasa na mgongano wa uhalali wa umiliki pamoja na uvamizi wa maeneo ya wazi yaliyotengwa maalumu kwa shughuli za jamii ni changamoto ya muda mrefu na natambua juhudi nyingi zilizofanyika katika kutatua.
  Makonda alisema moja ya mkakati wangu ni kufanya utatuzi unaohusisha taasisi zote muhimu ili kufupisha mlolongo unaowapotezea muda walioko kwenye migogoro na kuhakikisha mwenye haki anapewa haki yake bila kuyumbishwa.
  Alisema anatenga siku moja ambayo ni ya Ijumaa kuwa siku maalumu ya kukutana na wananchi na kusikiliza matatizo yanayohusiana na Ardhi na utaratibu huu utaanza machi 6 mwaka huu na zoezi la uandikishaji kwa wale wanaohitaji kusikilizwa matatizo yao utaanza majira ya saa 3.
  Makonda alisema Ili kupata ufumbuzi usio na shaka kamati ndogo itakayohusika katika kushughulikia matatizo hayo itaundwa na Katibu tawala wilaya (DAS) akiwa ni katibu, Mwanasheria wa Manispaa, Afisa Mipango miji, Afisa Ardhi.
  Aidha alisema ili kufanya zoezi hili liwe na ufanisi na mafanikio ningeomba wananchi wafuate utaratibu kuanzia ngazi za watendaji wa chini kabla ya kufikisha kila muhusika ahakikishe amekuja na vielelezo vyote halali vinavyoweza kutumika katika kufikia uamuzi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Balozi wa Japan nchini, anayemaliza muda wake, Mhe.  Masaki Okada wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kumkabidhi zawadi ya kitabu chenye picha na ramani ya jiji la Dar es salaam wakati Balozi huyo alipokwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 2, 2015 kuaga. (picha na ofisi ya Waziri mkuu)MIZ3 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akikabidhi zawadi ya kinyago Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake, Masaki Okada  ambaye alikwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es salaam Machi 2, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbinga Mhashamu John Ndimbo akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma leo.(picha na Freddy Maro).
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa ,Mkoani Ruvuma.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa ,Mkoani Ruvuma. Habari na picha na IKULU.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Machi 3, 2015, ameungana na mamia ya waombolezaji kumzika Mbunge wa Jimbo la Nyasa na msanii mahiri wa muziki nchini, Mheshimiwa Kepteni John Damiano Komba, kwenye makaburi ya Kanisa Katoliki katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma. 

  Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, akitokea Dar es Salaam, kiasi cha saa tano na robo asubuhi, Rais Kikwete amekwenda moja kwa moja Lituhi, karibu kiasi cha kilomita 140 kutoka mjini Songea, kwa ajili ya mazishi ya Mheshimiwa Komba ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM). 

  Rais Kikwete amejiunga na waombolezaji akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kiasi cha saa tisa mchana kwa ajili ya mazishi ya mmoja wa wasanii ambao walijijengea heshima kubwa kwa nyimbo zake za uhamasishaji. 

  Wakati wa shughuli za mazishi ambazo kidini zimeongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki Mbinga, waombolezaji walisomewa salamu za rambirambi ambazo zimetumwa na Rais wa Pili wa Malawi, Mheshimiwa Bakili Muluzi ambaye sasa amestaafu. 

  Katika salamu hizo, Mheshimiwa Muluzi amesema: “Nilimjua Komba kama rafiki na taarifa za kifo chake cha ghafla zimenistua sana.” 

  Mwili wa Marehemu Komba uliteremshwa kaburini saa 9:30 mchana huku ukishuhudiwa na mjane wa marehemu Salome Komba na watoto wake 11. 
  Rais Kikwete ameondoka Lituhi mara baada ya mazishi kurejea mjini Songea kumalizia ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani Ruvuma.


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa uwanja wa ndege mjini Dodoma mapema leo asubuhi na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Mh. Adam Kimbisa,tayari kwa kuanza ziara ya siku tisa, yenye lengo la kukagua, kuhimiza miradi ya maendeleo ya wananchi pamoja na kuangalia uhai wa chama, ambapo mara baada ya kuwasili amefanya mkutano wa ndani na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mpwapwa yenye majimbo mawili ya Uchaguzi.Kinana ametokea Mkoani Ruvuma mara baada ya kushiriki mazishi ya aliekuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi,Marehemu Kapteni John Komba aliyezikwa kijijini kwao Lituhi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akilakiwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma,Mh.Chiku Galawa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Dodoma mapema leo asubuhi,kulia kwake ni  Katibu wa CCM Mkoa,Albert Mgumba
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.Chiku Galawa mapema leo asubuhi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege,tayari kwa kuanza ziara ya siku 9 mkoani humo,
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa,Mh.Addam Kimbisa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake pamoja na baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM Wilaya ya Mpwapa mapema leo asubuhi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Wanachama wa CCM waliofika mapema leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mpwapwa kumpokea Ndugu Kinana na Ujumbe wake,ambapo anaanza rasmi ziara yake wilayani humu na vitongoji vyake.
  PICHA NA MICHUZIJR-MPWAPWA.

  0 0

  DSC_0003

  Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya Tehama, Al Amin Yusuph akiwasilisha mrejesho wa kazi ya kikundi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.(Picha na zote Zainul Mzige wa modewjiblog)

  Na Mwandishi Wetu
  WAKAZI wa kijiji cha Ololosokwan wamesema kwamba ujio wa kijiji cha digitali katika kijiji chao ni neema kwao kwani kitawasaidia kukabiliana na changamoto kubwa za maisha zinazowakabili.

  Kauli hiyo wameitoa mwishoni mwa wiki wakati wa kuhitimisha warsha ya siku saba ya kuangalia fursa na changamoto zitakazoambatana na mradi huo wa miaka mitatu unaodhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung.

  Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake waliohudhuria warsha hiyo ambapo wataalamu mbalimbali wanaohusika na mradi huo walikutana kujadili changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Salangat Mako, alisema kwamba tatizo la miundombinu, Afya na Elimu wanaamini litakabiliwa na mradi huo.
  Alisema kuna shida kubwa ya elimu kutokana na mazingira yaliyopo ambapo wanafunzi wanalazimika kutembea kilomita 14 kwenda na kurudi shule hali inayodhoofisha ari ya kujifunza.
  DSC_0044
  Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akitoa mrejesho wa kilichojadiliwa na kikundi chake.
  Aidha alisema kwamba kuna changamoto katika zahanati yao yenye wauguzi wawili huku hospitali ya wilaya ikiwa kiasi cha kilomita 50 hali inayowafanya watu wengi kutegemea mitishamba katika matibabu mbalimbali pamoja na wanawake kusaidiwa uzazi na wakunga wa jadi.

  Alisema kuwepo kwa mradi huo kutasaidia wanafunzi kuweza kujisomea kwa kutumia mfumo wa mtandao wa intaneti na hivyo kuwa katika nafasi ya kuelimika vyema kutambua wajibu wao na fursa zilizopo zinazowazunguka kwa kuwa hifadhini.

  Aidha kuwepo kwa kiliniki ya mtandao kutaongeza ufanisi wa zahanati iliyopo pamoja na kuipa mkono katika tiba na kuondoa watu kutegemea tiba za asili.Akizungumzia fursa za kiuchumi alisema ni matarajio yao kwamba kuwepo kwa kijiji hicho na utamaduni wake, kutawezesha kutumia vyema fursa za kitalii ili kukua kiuchumi kwa kujua mipango inayostahili katika kuendeleza utamaduni kwa jicho la kibiashara zaidi.
  DSC_0036
  Mratibu wa shirika la IrikRAMAT Foundation, Salangat Mako akitoa mrejesho wa suluhu za changamoto mbalimbali za kikundi cha uchumi na utamaduni wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya wiki moja.

  Naye Mganga mfawidhi wa zahanati ya Ololosokwan Obeid Laizer ambaye yupo katika kijiji hicho kwa miaka 15 amesema ana matumaini makubwa na mradi huo kwa kuwa mchanyato wake unaonekana kujali zaidi sosholojia za watu na afya zao hasa kwa kuwa na kliniki inayotembea na tiba kwa intaneti itakayomuwezesha kuwasiliana na madaktari wenzake ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya afya.

  Alisema kwamba kijiji hicho kina magonjwa mengi japokuwa makubwa ni nyumonia, ukosefu wa damu, magonjwa ya zinaa, majereha ya wanyama kutokana na kuchunga mbugani na ugonjwa wa kuhara damu.
  Alisema uwapo wa maabara utawasaidia kupata uhakika wa tiba kuliko sasa ambako wanafanya kwa kukisia zaidi.
  DSC_0018
  Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya afya kutoka UNESCO, Bw. Mathias Herman akiwasilisha mrejesho wa kikundi kazi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

  Naye Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro Beneth Bwikizo amesema kwamba mradi huo utaleta mabadiliko makubwa kwa wanakijiji hapo kutokana na shughuli nyingi za hapo kuhusanishwa na mradi huo.

  Alisema mradi huo ambao unaangalia zaidi kukabili utamaduni unaokwamisha maendeleo kwa kutoa elimu na kuiunganisha na dunia nyingine kwa mawasiliano unaonekana utafanya maisha ya wakazi wa hapo kuboreka.
  Alisema mradi huo wa kwanza nchini Tanzania na watatu bara la Afrika umempa hamasa kubwa baada ya kuona unaangalia changamoto zilizopo Ololosokwan ambazo ni za miundombinu katika elimu, afya na uchumi na kuzifanyia kazi.
  DSC_0051
  Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro, Beneth Bwikizo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya ujumbe wa kijijini cha Ololosokwan uliohudhuria warsha hiyo ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
  DSC_0054
  Afisa Miradi msaidizi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko (kushoto) na Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Teresia Irafay wakinakili yanayojiri wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji cha kidigital (Unesco - Samsung digital village) katika kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
  DSC_0057
  Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la IrikRAMAT linalomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maoni yake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi kijiji cha Kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Warsha hiyo ya wiki iliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini.
  DSC_0066
  Pichani jii na chini ni wadau mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi waliohudhuria warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
  DSC_0034
  DSC_0008
  Kutoka kushoto ni Mathias Herman wa UNESCO, Mkurugenzi wa elimu ya msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sarah Mlaki pamoja na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ololosokwan, Emmanuel Madeje.
  DSC_0064
  Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akionesha kwa mifano baadhi ya bidhaa za nje zikivyokuwa na ubora kwenye vifungashio wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha digitali (Unesco-Samsung digital village) kwa wakazi wa kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
  DSC_0118
  Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisikiliza baadhi ya maboresho ya changamoto zilizojadiliwa na kikundi kazi cha sekta ya elimu na wadau mbalimbali wa elimu.
  DSC_0070
  Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akitoa maboresho ya kazi za vikundi vilivyokuwa vikijadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo katika kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali.
  DSC_0070
  Picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo ya wiki moja iliyomaziki mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akimsikiliza Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga (wa pili kulia) akimuelezea mikakati ya ushirika huo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio, akifuatiwa na Katibu wake Bw. Benedicto Damiano na kulia ni Mtunza Hazina Bi. Judith Medson.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu chake cha uanachama toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio (wa tatu toka kulia). Wengine ni Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto Damiano (wa pili kulia), Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) na Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha kitabu chake cha uanachama baadas ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio wakishuhudiwa na Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto Damiano, Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.


older | 1 | .... | 475 | 476 | (Page 477) | 478 | 479 | .... | 1898 | newer