Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA DKT. EDWARD HOSEA, JIJINI DAR.

$
0
0
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya marehemu Esther Gigwa, Mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili huo nyumbani kwa mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015.
 Wanafamilia wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya maziko.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkuruenzi huyo nyumbani kwake, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji, Familia ya wafiwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea na nduguze, waliofiwa na mama yao mzazi wakati Makamu alipofika kushiriki katika shughuli ya kuaga, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Ewdard Hose, Mama Esther Gigwa, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika nyumbani kwa Mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015.

NDEGE YA JWTZ YAPATA AJALI JIJINI MWANZA LEO

$
0
0
Ndegevita moja ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiteketea kwa moto huku jitihada za kuuzima zikiendelea katika ajali iliyotokea leo Februari 27, 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,  Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto. 

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda  alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu. 



Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.



BLOGGERS KUKUTANA KESHO KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA PATI YA KIHISTORIA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni  mjumbe wa TBN Mkala Fundikira,  Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya AIMS, Shafiq Mpanja wa AIM, Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na mjumbe wa TBN Khadija Kalili.
Katika mkutano huo TBN imesema kesho Jumamosi jioni Bloggers takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali nchini watakutanika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es salam kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa Bloggers.
 Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
 Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.
 Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Masaki jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea Msaki jijini Dar es salaam leo walipofika heshima zao za mwisho kwa mama yake mzazi Marehemu Esther Gigwa Hosea huko Masaki jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghariv Bilali, Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiwa pamoja na wafiwa wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Masaki jijini Dar es salaam leo.
Sehemu ya wafiwa na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Masaki jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

KIPINDI CHA “JICHO LETU MKURANGA” CHA REDIO UPENDO CHASAIDIA JAMII YA WENYE MAHITAJI MUHIMU MKURANGA

$
0
0
DSC_2663Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani akikabidhi madawati kwa Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bw.Benjamin Majoye yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding Company Limited ya jijini Dar es salaam pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo sare za shule, madaftari na viatu kutokana na msaada mkubwa wa kipindi cha “Jicho letu Mkuranga” kinachorushwa kila siku na kituo cha Redio cha Upendo Media cha jijini Dar es salaam kwa kuibua changamoto hizo na kuhamasisha taasisi na wananchi mbalimbali wenye uwezo kusaidia jamii masikini na zenye mahitaji muhimu, katika picha wa pili kutoka kulia ni Frank Mbando Mkurugenzi wa Kampuni ya FIFA Flow na katikati ni Ibrahim Mwangalaba Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo PLCDSC_2664Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la KKKT akikabidhi sare za shule  kwa Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bw.Benjamin Majoye zililzotolewa na Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding Company Limited ya jijini Dar es salaamDSC_2667 
Picha ya pamoja viongozi hao wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyokabidhiwa kwa wilaya ya Mkuranga.

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge tarehe 27.2.2015. Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere.mam9 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akimpongeza Mama Salma Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa kwenye hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwenye hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo tarehe 27.2.2015.mam8 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ta matiti kwa akina mama kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo. Hafala hiyo ilifanyika kwenye Kitengo cha Uzazi na mtoto cha hospitali hiyo kilichoko eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015.mam4 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupima saratani ya matiti kwa akina mama katika Hospitali ya Lugalo tarehe 27.5.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshauri Ndugu Peter Charles,28, baba mzazi wa binti Irene mwenye umri wa miezi 3 na mkazi wa Mikocheni kupunguza baadhi ya nguo alizomfunika mtoto wakati hali ya hewa ni ya joto. Mama Salma alimpongeza Ndugu Peter kwa kuambatana na mke wake kwenda kliniki.mam11 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Bibi Mariam Omar aliyemshika mtoto wake Jane Winston aliyekuwa akisubirim kupata huduma hospitalini hapo wakati Mama Salma alipotembelea sehemu mbalimbali za Kitengo cha Uzazi na Mtoto mara baada ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama tarehe 27.2.2015.

 mam3 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti (Mammograph) kwa akinamama katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kwenye kitengo cha Uzazi na mtoto kilichopo eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhmu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.mam6 
Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Ulinzi na wananchi waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama.mam5 
Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Ulinzi na wananchi waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama.
………………………………………………………..
Na Anna Nkinda – Maelezo.

27/2/2015 Wanaume nchini wametakiwa kuwaunga mkono wake zao kupima saratani za matiti na shingo ya kizazi na pale watakapokutwa na maradhi hayo wasiwanyanyapae bali wawafariji kwani magonjwa hayo yanatibika kama yatagundulika mapema.

Rai hiyo imetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mashine ya kisasa ya upimaji wa saratani ya matiti (Mammography) katika Hospitali kuu ya Jeshi la  Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, kliniki ya Mama na Mtoto iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema unyanyapaa wa wanaume huwakwaza wanawake na kuwafanya baadhi yao kusita kujitokeza kupima na kupata tiba dhidi ya saratani.

“Nanyi wanawake msisubiri mpaka msikie maumivu ndipo mkapime maana wakati huo saratani itakuwa imeenea, jengeni tabia ya kupima saratani za matiti na shingo ya kizazi mara kwa mara wataalamu wanasema unapima  mara moja kila baada ya miaka mitatu”.
Bahati nzuri saratani ya shingo ya kizazi ina kinga kwa njia ya chanjo hivyo basi wazazi tuchangamkie kuwapeleka watoto wetu wa kike kupata chanjo hiyo, tutawapatia kinga ya kudumu ya maradhi haya hatari”, alisisitiza Mama Kikwete.

Alisema ugonjwa wa saratani ya matiti unaathiri wanawake wengi nchini na wataalam wa afya wanasema  saratani ya matiti ni ya pili kwa ukubwa nchini ikifuatiwa na  ya shingo ya kizazi.
Mama Kikwete alisema, “Niliamua kukabidhi mashine hii katika Hospitali hii baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wanatibiwa hapa pia huduma ya mama na mtoto hutolewa hapa.Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mashariki hivyo inastahili kuwa na mashine ya aina hii ambayo itawanufaisha wanawake wengi wanaokuja hapa kuhudumiwa”.

Kwa upande wa saratani ya tezi dume aliwahimiza wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wajitokeze kupima kwani ikigundulika  mapema inatibika. Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema, “Wanawake nasi tunao wajibu wa kuwahamasisha  waume zetu kupima saratani ya tezi dume na kuwafariji wakiwa wakiwa kwenye tiba. Tushirikiane kwa pamoja kuleta mabadiliko”.

Naye  Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Samuel Ndomba  alimpongeza Mama Kikwete kwa kazi anayoifanya ya kuiongoza Taasisi ya WAMA yenye lengo la kuinua ustawi wa watoto na akina mama hususani katika nyanja za afya, elimu na huduma za maji safi na salama. 

Alisema, “Juhudi kubwa unazozionyesha za kuboresha na kuendeleza huduma za afya ya mama na mtoto zinadhihirisha upendo wa dhati ulionao kwa umma wa watanzania”. 

Luteni Jenerali Ndomba  alisema tukio hilo la kukabidhiwa mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa Jeshi hilo ni la kihistoria na la kipekee na kumshukuru Mama Kikwete kwa kutambua umuhimu, kujali na kuthamini afya za wanajeshi, familia zao na akina mama wote.

“Ni dhahiri kuwa ulinzi imara wa taifa letu unategemea wanajeshi na wananchi wenye afya nzuri. Tunakuhakikishia kuwa mashine hii haitatumika kwa wanajeshi na familia zao tu bali itatumika kutoa huduma kwa wananchi wa Tanzania kwa kufuata kanuni na taratibu za huduma ya tiba Jeshini”, alisema Luteni Jenerali Ndomba .

Alimalizia kwa kusema Jeshi hilo litaweka kipaumbele katika mafunzo kwa wataalam ambao wataweza kuitumia na kuitunza vizuri mashine hiyo ili utoaji wa huduma kwa akina mama uwe endelevu.

Mashine hiyo imetolewa na kikundi cha wanawake wajasiriamali wa Tanzania waishio nchini Washington, nchini Marekani cha Wanawake watano (Tano Ladies) kwa kushirikiana na  Chama cha Wanawake wa Afrika na Uelewa wa Saratani (African Women Cancer Awareness Assossiation – AWCAA).
Wanawake hao walimkabidhi Mama Kikwete mashine hiyo ya kupimia saratani ya matiti mwishoni mwa mwaka jana alipokuwa nchini Marekani katika shughuli za kikazi  ili iweze kusaidia na  kuokoa maisha ya wanawake hapa nchini.

JAJI KIONGOZI ATOA SOMO KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA, VYAMA VYA WAAJIRI NA WAAJIRIWA.

$
0
0

JA1
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akifungua mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini.
JA2
Baadhi ya washiriki wa mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
JA3
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa – MAELEZO
Dar es salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila ametoa wito kwa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini  kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, viwango na uadilifu ili mahakama hiyo iendelee kuwa kimbilio la wananchi wanaotafuta haki.
 
Akizungmza wakati wa wakati wa kikao cha wadau wa Mahakama kujadili uboreshaji wa utendaji kazi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kilichowahusisha watendaji wa Mahakama ya Kazi , Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) leo jijini Dar es slaam, Mhe.Shaaban Lila amesema kuwa  msingi mkuu wa Mahakama ya Tanzania nikuhakikisha kuwa inatoa maamuzi kwa wananchi kwa haki na wakati.
 
Amesema  iwapo waajiri na waajiriwa kote nchini haki watazingatia wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao kulingana na kanuni na taratibu zinazosimamia maeneo ya kazi migogoro  mingi inayopelekwa mahakamani baina ya waajiri na waajiriwa itapungua nchini.
 “Kila upande ifanye kazi yake kwa haki ,kumekuwa na mrundikano wa mashauri  ya kazi yanayokwenda mahakamani kwa ajiri ya utatuzi na usuluhishi ,mengi ya mashauri hayo hayahusiani na kufukuzwa kazi isipokuwa yale ya kukosa uaminifu, wizi na ubadhirifu sehemu za kazi” Amesisitiza.
 
Amebainisha kuwa Mahakama ya Tanzania lazima iheshimiwe kutokana na misingi yake kwa kuweka msisitizo katika kushughulikia masuala ya msingi na kutatua kero za wananchi hususan usimamizi na utoaji wa haki kwa wakati.
 
Mhe. Shaaban amefafanua kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya maboresho na mabadiliko katika kushughulikia mashauri ya muda mrefu yaliyoko mahakamani huku akieleza kuwa mkakati wa sasa ni kupunguza umri wa mashauri ya muda mrefu ya miaka 5 hadi 10 yanayofikia 265  na yale ya umri wa miaka 3 yapatayo 201 yaweze kushughulikiwa ndani ya mwaka 1 hadi 2 ifikapo June 2015.
 
“Lengo letu ni kushughulikia mashauri haya haraka kwa muda mfupi, muhakikishe mashauri haya mnayamaliza kwa sababu yanagusa uzalishaji na maisha ya watu, kuchelewa  kuyasikiliza  kunaathiri  uchumi ” Amesisitiza.
 
Aidha,amewataka wadau wanaoshiriki mkutano huo kujipima katika malengo wanayojiwekea pamoja na kusimamia utekelezaji wa hukumu na maamuzi yanayotolewa na mahakama na kueleza kuwa ofisi yake inaandaa mkakati wa usimamizi wa suala hilo.
 
 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri nchini Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mulimuka akizungumza katika mahojiano maalum amesema kuwa mbali na mkutano huo kuwaweka pamoja wadau  hao kwa maana ya Mahakama, Waajiri (Serikali) na waajiriwa unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini. 
 
Amesema asilimia 70 ya mashauri yanayokwenda  mahakama Kuu Divisheni ya Kazi yanahusu migogoro ya waajiri  kuwasimamisha kazi wafanyakazi wao kutokana na makosa mbalimbali na kuongeza  kuwa mengi ya makosa hayo hayasababishi mtu afukuzwe kazi.Ametoa wito kwa pande zote kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kufuata haki ili mashauri yote yanayopelekwa mahakamani yaweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuondoa migogoro ya kazi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini.

ZIARA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA WILAYANI KYELA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa chelezo ya kuundia meli kwenye bandari ya Itungi,  Kyela akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo  Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) ky8Mwendesha baiskeli akipita katika daraja la zamani la Mwaya wilayani Kyela huku wakitazama daraja jipya  (kulia) lilozinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)ky3 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari  26, 2015. Wapili kulia ni mkewe Tunu na wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kyela anayeoondoka, Margareth Malanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  ky12 
Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Zamani wa Mbeya Mzee  John Mwakipesile baada ya kuwasili kwenye  makazi ya  Mkuu wa Wilaya ya Kyela kwa ziara ya siku moja wilayani humo Februari 26, 2015. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) ky15Wanafunzi wakimpungia mkono Waziri Mkuu Mizengo Pinda hayupo pichaniky16 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana  na  Katibu wa CAHDEMA wa kata ya Mwaya, Ageni Pamesa  kabla ya kufungau maabra ya  shule ya sekondari ya  Mwaya akiwa katika ziara ya Mkoa wa  Mbeya Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu) ky17 
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  na mkewe Tunu (wapili kulia) akitazama mafunzo kwa vitendo wakati alipokagua maabara ya Kemia katika shule ya seondari ya Mwaya wilayani Kyela Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kyela baada ya kufungua ukumbi wa  Halmashauri hiyo wakiwa katika ziara ya wilaya  hiyo Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) ky14 
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, MizengoPinda wakati aliozungumza baada ya kufungua mashine ya kukoboa nakuchambua mpunga mjini Kyela Februari 26, 2015. (PIcha na Ofisi  yaWaziri Mkuu)
ky11 
Daraja la Mwaya  wilaya ni Kyela ambalozo lilizinduliwa na Waziri Mkuu, mizengo Pinda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakitazama  eneo itakapojengwa chelezo na bandari ya  Itungi  wilayani Kyela wakiwa katika ziara ya wilaya hiyo, Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu) ky6 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na watalaamu wa kampuni ya kichina ya CHICCO kabla ya kufungua daraja  la Mwaya lililojengwa na kampuni  hiyo wilayani Kyela Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) ky4 
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Mama Mlemavu, Lesia Kambungwe baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Kyela akiwa katika ziata ya wilaya hiyo Februari 26, 2015<(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DKT.MAGUFULI AFANYA UKAGUZI WA KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM

$
0
0

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwaita wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika eneo la Ferry kwa ajili ya safari ya kwenda Bagamoyo na kurudi kwa safari ya majaribio kwa kutumia kivuko cha MV Dar es Salaam alichokikagua leo.
Kivuko cha MV Dar es Salaam kikiwa njiani kuwasili eneo la Magogoni kwa ajili ya kuanza safari ya kwanza ya majaribio ya kwenda Bagamoyo mkoani Pwani.Kivuko hiki kinauwezo wa kubeba abiria zaidi ya 300.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakipanda kivuko cha MV Dar es Salaam kwa ajili ya Safari ya majaribio ya kwenda Bagamoyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akimpokea Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili Bagamoyo na Kivuko cha MV Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi kushoto wakiwa safarini kuelekea Bagamoyo Mkoani  Pwani, akiwa na Kamanda wa Navy, Meja Jenerali Rogastian Laswai.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliopata fursa ya kupanda kivuko hicho wakitazama madhari ya jiji wakati wakiwa safarini

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amekagua kivuko cha MV Dar es salaam kinachotarajia kutoa huduma zake kati ya Dar es salaam na Bagamoyo na kuahidi kuwa kivuko hicho kitaanza kazi siku chache zijazo mara baada ya kukamilika kwa vituo vya maegesho. 

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Waziri Magufuli amewataka wakazi wa Dar es salaam na Bagamoyo kukitumia kivuko hicho ambacho kitawawezesha kufika katika maeneo yao kwa haraka na kuepuka usumbufu wa msongamano katikati ya jiji la Dar es salaam. 

“Tumieni kivuko hiki kwa uangalifu ili kidumu kwa muda mrefu, na sisi Serikali tutahakikisha tunaweka nauli nafuu ili kuwezesha wananchi wengi kumudu kutumia usafiri wa kivuko hiki, amesema Waziri Magufuli”. 
Waziri Magufuli amemtaka mkandarasi wa Ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho ambae ni Kamandi ya Wanamaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kukamilisha ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho mapema iwezekanavyo ili huduma za usafirishaji zianze mara moja. 

Kwa upande wake Mkuu wa MKoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo ameipongeza Wizara ya Ujenzi kwa kuwezesha kupatikana kwa kivuko cha MV Dar es salaam ambacho kitafungua fursa za kiuchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi. Aidha, Eng. Ndikilo ameiomba Wizara ya Ujenzi kuiendeleza barabara ya Bagamoyo- Zinga hadi Mbegani na kuhakikisha kuwa na usafiri wa basi moja kutoka Bagamoyo kwenda Mbegani na kuwepo maegesho ya magari yenye usalama. 

 Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) Eng. Marceline Magessa, amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya kuanza kazi kwa kivuko hicho yamekamilika ambapo tayari manahodha, mabaharia na mafundi watakaohudumia kwenye kivuko hicho wameshaajiriwa. 
 Aidha Eng. Magessa alibainisha kuwa Kivuko cha MV Dar es salaam kimetengenezwa na kampuni ya Western Marine Shipyard kutoka Denmark kwa takriban Shilingi bilioni 8 na kina uwezo wa kubeba abiria 300 wakiwa wamekaa. 

 Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ya JWTZ Meja Jenerali Rogasian Laswai, amemshukuru Waziri kwa kupewa kazi ya kujenga maegesho hayo na kuahidi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ili wananchi wanufaike na huduma za kivuko hicho mapema. 

Takriban vituo saba vinatarajiwa kujengwa kwa ajili ya maegesho ya kivuko hicho ikiwemo Magogoni, K awe, Jangwani, Rungwe Oceanic, Mbweni, Kaole na Mbegani. 
 IMETAYARISHWA NA KITENGO 
CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI.


KINANA AKUTANA NA KAMATI KUU YA CHAMA CHA SPLM CHA SUDANI YA KUSINI

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzana na Kamati Kuu ya Chama Cha SPLM ambapo alipeleka ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,kikao hicho kilikuwa chini ya Mwenyekiti wa chama cha SPLM ambaye pia ni Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir, Ikulu mjini Juba.
 Mwenyekiti wa chama cha SPLM ambaye pia ni Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ambacho Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihudhuria.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu cha chama cha SPLM ,kikao hicho kilimalizika usiku wa manane mjini Juba ,Sudan.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati Kuu ya chama cha SPLM mjini Juba,kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa SPLM ambaye pia ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo James Wani.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za watumishi zililizojengwa na NHC Busokelo

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akifungua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo.mi2 
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio wakati akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wialaya ya Busokelo, Mbeya. mi4 
mi8Mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Busokelo zinazojengwa na NHC kama zinavyoonekana leo.mi9 
Bango la Kumkaribishs Waziri Mkuu mi10 
Msoma Hotuba wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Bw. Sanga akisoma hotuba hiyo mbele ya Waziri Mkuu leo. mi11 
Msoma Hotuba wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Bw. Sanga akisoma hotuba hiyo mbele ya Waziri Mkuu leo. mi13 
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki , Profesa Mark Mwandosya katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wialaya ya Busokelo.
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki , Profesa Mark Mwandosya katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wialaya ya Busokelo. mi15 
Baadhi ya Watendaji wa NHC na viongozi wa Wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya wakiwa wamejipanga kumkaribisha Waziri Mkuu mi16 
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akikaribishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki , Profesa Mark Mwandosya wakati akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Mbeya. mi18 
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki , Profesa Mark Mwandosya katika eneo la nyumba za gharama nafuu za watumishi za Busokelo, Mbeya zinazojengwa na Shirika hilo kabla ya kuwekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda.mi19 
Baadhi ya Wafanyakazi wa NHC wakifuatilia uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi huo wa nyumba za watumishi wilayani Busokelo. mi20Wafanyakazi wa NHC Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya shughuli ya uwekaji jiwe la msingi

WAVAMIZI NA WAMILIKI WA ARDHI KINYUME CHA SHERIA JIJINI DAR KUKIONA, KUKUMBWA NA BOMOA BOMOA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Alphayo Kidata (kulia) bakitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa awamu ya tatu linaloendelea katika Manispaa ya Kinondoni  jana jijini la Dar es salaam.Kulia ni Muhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Baraka Mkuya.bom2 
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bw. Alphayo Kidata  (hayupo pichani) alipokuwa akitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa kwa wananchi waliovamia maeneo yanayomilikiwa kisheria na watu wengine katika manispaa ya Kinondoni  jana jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wananchi katika manispaa ya Kinondoni wakiondoa bidhaa zo katika maduka eneo la Tegeta Machakani kupisha zoezi la bomoa bomoa kufuatia maduka hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.
bom6 
Moja ya ukuta uliojengwa kinyume cha sheria katika eneo lisiloruhusiwa eneo la Tegeta ukibomolewa jana.
……………………………………………………………
Na. Aron Msigwa –MAELEZO, Dar es salaam.
 Dar es salaam.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kuwa itaendelea na zoezi la kuvunja  nyumba zilizojengwa katika maeneo ya wazi na yale yaliyochukuliwa kwa nguvu kinyume cha sheria kutoka kwa wananchi wanaoyamiliki kihalali katika maeneo mbalimbali nchini.
 
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Alphayo Kidata alipokuwa akitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa awamu ya tatu linaloendelea katika Manispaa ya Kinondoni  jijini la Dar es salaam. 
 
Alisema  kuwa wizara imekuwa ikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ambao maeneo yao yamevamiwa na watu wengine kinyume cha sheria ambayo wao wanayoyamiliki kihalali. 
 
Alieleza  kuwa  kutumia kanuni na taratibu zinazosimamia umiliki na matumizi ya ardhi nchini wizara hiyo itaendelea kuchukua hatua na kuyabaini maeneo yote yenye migogoro inayosababishwa na baadhi ya  wananchi wasio na nyaraka halali za umiliki kisheria kuingia kwenye viwanja vya wananchi.
 
“Sisi kama wizara tumekubaliana kuwa zoezi hili litakuwa endelevu, wale wote waliovamia maeneo ambayo sio yao yakiwemo maeneo ya wajane na kujenga majengo yao Serikali itayabomoa kwa nguvu hata kama wamejenga maghorofa na Hoteli” Amesisitiza.
Alisema kwa muda mrefu pamekuwa na wimbi kubwa la migogoro ya ardhi inayosababishwa na tabia ya wananchi wasio na nyaraka kisheria kuingia kwenye viwanja vya watu wengine wenye hati za kumiliki ardhi kihalali na kuviendeleza kiuvamizi pasipokuwa na vibali vyovyote vya ujenzi.
 
Bw. Kidata alibainisha  kuwa vitendo wanavyofanya wananchi hao ni kosa la jinai na  kinyume cha sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu namba 175(1) kinachozuia mwananchi yeyote kuingia na kuendeleza  kwenye ardhi asiyoimiliki kisheria.  
 
Alisisitiza kuwa hakuna raia yeyote wa Tanzania aliye juu ya sheria hivyo watanzania bila kujali hali walizo nazo wanao wajibu wa kutii na kufuata sheria za nchi zinazosimamia sekta ya ardhi na kuongeza kuwa Serikali haitamvumilia yeyote atakayeendesha vitendo vya kuhujumu maeneo ya wazi, kujenga kuta katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuvamia maeneo ya hidhadhi ya Bahari.
 
Kwa upande wake Muhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya ambaye zoezi hilo lilifanyika katika manispaa anayoisimamia ameeleza kuwa awamu ya tatu ya zoezi la bomoa bomoa katika manispaa hiyo limehusisha  ubomoaji wa kuta, majengo  na  maduka katika maeneo ya tofauti ya kata Mikocheni B na  Tegeta.
 
Aliongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maenedeleo kwa kushirikiana na manispaa ya Kinondoni na vyombo vya ulinzi na usalama itaendelea na zoezi hilo ili kusimamia sheria za nchi kutokana na baadhi ya wananchi kwa makusudi kuendesha vitendo vya hujuma na vurugu miongoni mwa jamii.
 
“Kwa upande wetu kama manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara na vyombo vya ulinzi na usalama, tutalifanya zoezi hili kuwa endelevu ili tuweze kuondoa kabisa migogoro ya ardhi katika manispaa yetu” Alisisitiza.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AZINDUA HUDUMA ZA “DUTY FREE SHOP” MAGEREZA UYUI TABORA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashilia uzinduzi rasmi wa “Duty Free Shop” ya Magereza Mkoani Tabora leo februari 28, 2015. Kamishna Jenerali Minja amesema kuwa Huduma hiyo itatolewa pia kwa Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mkoani Tabora(kulia) ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji.min2 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiangalia bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika  “Duty Free Shop” ya Magereza Mkoani Tabora mara tu baada ya uzinduzi rasmi leo februari 28, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Uyui, Tabora. min3Muonekano wa Jengo la “Duty Free Shop” ya Magereza Mkoani Tabora ambalo limzunduliwa leo februari 28, 2015 na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani)
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi wa “Duty Free Shop” ya Magereza Mkoani Tabora. min5 
Kikundi cha ngoma za asili ambacho kinaundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoani Tabora kikitumbuiza katika hafla ya “Duty Free Shop” ya Magereza Mkoani Tabora. min6 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora(wa pili kulia) ni RPC Tabora, ACP Suzani Kaganda(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga, SACP. Anet Laurent(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Tabora, SACP. Rajab Mbilo(wa tatu kushoto) ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji(wa tatu kulia) ni Katibu Tawala Mkoani Tabora, Bi. Kudra Mwinyimvua(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

ZIARA YA WAZIRI MKUU PINDA WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Misingi  la ujenzi wa nyumba za  watunmishi wa Halmashauri ya  Busokeleo wilayani Tukutu  unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika kijiji cha Rungwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Beya Februari 27, 2015. Wapili kushoto ni mkewe Tunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akigua nyumba zinazojengwa na Shirikal la Nyumba la Taifa (NHC) karika kijiji cha Rungwa kwa ajili ya watumishi wa Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari 27, 2015. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mark Mwandosy na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa NHC, Haikaman Mlekio. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)mw2 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiweka jiwe la msingi  la mradi wa umwagiliaji wa Katerantamba katika halmashauri ya  Busokeleo wilayani rungwe akiwa katika ziara ya mkoa wa beya Februari 28, 2015.
 mw5 
Mke wa Waziri Mkuu, Mamam Tunu Pinda akivalishwa kitenge na bibi Hilda Mwasikili katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mjini Tukuyu Februari 27, 2015.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS, IKULU NA UTAWALA BORA DKT. MWINYIHAJI MAKAME MGENI RASMIN TUZO ZA WASANII BORA WA MUZIKI WA ZANZIBAR MWAKA 2015.

$
0
0
Meneja wa Fedha Z.M.C.L Bi. Saide Moh’d akimkabidhi tunzo Mwanamuziki bora wa mwaka wa kizazi kipya Riko Singo katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar.
med7Mwanamuziki bora wa mwaka wa kike wa kizazi kipya Baby J akipokea tunzo kwa Meneja wa Z.M.C.L Tawi la Dar es Salam mara baada ya kuipuka kidedea tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Midia Corporation LTD iliopo Zanzibar.
Baadhi ya wageni waalikwa na wadau mbali mbali wakishuhudia wasanii wa Zanzibar wakipewa tunzo katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar. med9'
Wasanii wa kikundi cha Smart Comed Zanzibar wakitoa Burudani.
med10 
Msani Mr Blue akitumbuiza katika Tamasha la Wasanii wa Zanzibar.
Mgeni Rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikiulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akimkabidhi tunzo ya muandaaji bora wa Tamasha Zanzibar Music Award mwaka 2015 Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa Redio ya Zenji FM Mohamed Seif Khatib katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar.  med12 
Mgeni Rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikiulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Zanzibar Midia Corporation LTD. Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

Waziri Fenella akutana na wasanii nchini

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na wasanii nchini na kuwaasa wasanii kuielimisha na kuhamasisha Jamii kuhusu Katiba Inayopendekezwa kupitia kazi mbalimbali za sanaa, wakati wa mkutano na wasanii nchini uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimueleza jambo Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Francis Michael wakati wa mkutano na wasanii uliofanyika katika ukumbi wa uwanja mpya wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko akiongea na wasanii nchini na kuwaeleza kuhusu umuhimu wa sekta hiyo kushiriki kikamilifu katika masuala ya kitaifa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea upatikanaji wa Katiba Mpya, Kulia ni Katibu wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo.


Rais Kikwete aongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM ikulu Dar es Salaam

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya taifa ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wapili kulia ni Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein na wawatu kulia ni makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal.Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwaongoza wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kusimama kwa dakika chache kumkumbuka mjumbe wa baraza la wawakilishi wa jimbo la Magomeni Zanzibar ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati hiyo leo wakati wa kuanza kikao cha kamati hiyo ikulu jijini Dar es Salaam.(picha na Freddy Maro)

Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa yamsaidia mama aliyeporwa mtoto wake mwenye ulemavu wa ngozi na kuuwawa

$
0
0

Meneja Mauzo wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugaano Kasambala, akimpa pole Ester Jonas, mama wa Yohana Bahati, mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino, aliuawa mkoani Mwanza, hivi karibuni. Mama huyo anatibiwa katika Hospitali ya Bugando baada ya kupata mareraha katika tukio la kuvamiwa na kuporwa mtoto wake. Kulia kwa Kasambala ni Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir mwenye miwani waliyeambatana katika safari hiyo kwa ajili ya kuwapa pole na kuwafariji.

MBUNGE wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir kwa ushirikiano na Taasisi ya Kifedha, inayojihusisha na mikopo ya Bayport Financial Services yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, Tanzania, walifanya ziara ya siku mbili jijini Mwanza kwa ajili ya kutembelea familia mbili zilizopoteza watoto wao wawili ambao ni walemavu wa ngozi.
 
Familia hizo ni ya Ester Jonas, mama wa marehemu Yohana Bahati na ile ya Sofia Juma mama wa mtoto Pendo Emmanuel, wote wakiwa ni watu wenye ulemavu wa ngozi, huku familia zote mbili zikipewa Sh Milioni 2 kila moja.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir mwenye miwani akimfariji mama wa Yohana Bahati (Ester Jonas) aliyelazwa Hospitali ya Bugando, Mwanza, pamoja na kumpaa mafuta ya kupaka kwa ajili ya watoto wake wawili ambao nao ni albino,. Kushoto kwa Mh Shaimar ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala na wafanyakazi wengine wa Bayport waliombatana pamoja kwenye msafara huo wa kutoa pole.
 
Akizungumza katika safari hiyo, Mbunge Shaimar alisema
ameendelea kusikitishwa na mauaji hayo ya albino yanayotoa haki ya kuishi ya watu wote wenye ulemavu wa ngozi, huku akiitaka jamii kuacha kufavya vitendo hivyo visivyokuwa vya kiungwana kutokana na kudhulumu haki za kuishi za binadamu wenzao.
 
“Naumia juu ya vitendo hivi kwasababu na mimi nipo kwenye
kundi hili lawatu wenye ulemavu wa ngozi wanaoendelea kupukutika siku hadi siku, hivyo tupambane na majangili haya, maana najua Mheshimiwa Rais, Dr Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wamekuwa wakiguswaa mno na matukio haya yanayoichafua nchi yetu,’ alisema Shaimar, ambapo pia aliishukuru Bayport Financial Services kuingia katika harakati za 
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyri (katikati), akizungumza
na binti aliyekutwa nyumbani kwa Ester Jonas, mama wa albino Pendo Bahati aliyeporwa na haijulikani alipokuwa. Kulia kwake ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services, Lugano Kasambala, aliyeambatana na mbunge huyo.
 
Naye Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, alisema taasisi yao imeguswa na mauaji hayo na kuitaka jamii kushirikiana na viongozi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama katika kupambana vikali na watu wanaoendeleza kufanya unyama wa kuteka watu wenye ulemavu wa ngozi kwa sababu wanazojua wenyewe.
 
Alisema hali hiyo waliamua kufanya safari moja na mbunge Shaimar ambaye kiuhalisia ni balozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi, huku akiamini kwa ushirikiano huo unaweza kupunguza au kuondosha kabisa vitendo hivyo vya mauaji ya albino yanayoendelea kushika kasi katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara.
 
Wengine waliombatana kwenye ziara hiyo ni pamoja na Afisa
Ustawi wa Jamii Mwanza, Leah Linti, Katibu Tawala Msaidizi Crecencia Joseph, Mweka Hazina wa Chama cha Albino Taifa (TAS), Abdullah Omari, Jeshi la Polisi wilayani Misungwi, huku safari zote zikiwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanzaa, Magesa Mulongo.

kapteni John komba afariki Dunia jijiNI dar

$
0
0
Hayati John Komba enzi za uhai wake

Mbunge wa Nyasa (Mbinga Magharibi) mkoani Ruvuma na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Capt. John Komba amefariki dunia jioni hii katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam, mtoto wa Marehemu Bw. Herman Komba amethibitisha. Taarifa zaidi tutawaletea hapa hapa kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI- AMIN.

HAYA HAPA NDIO MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KILICHOFANYIKA LEO JIJINI DAR

Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images