Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 473 | 474 | (Page 475) | 476 | 477 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Wafanyakazi wa Uhuru FM, Redio ya wananchi wakiongozwa na Dj Fast Edie (kushoto) wakishow love wakati wa tafrija yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika Februari 27, 2015 katika ukumbi wa Tukuyu katika Hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam. 

  Tafrija hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mkurugenzi wao Angela Akilimali ilifana na kupongezwa na kila mfanyakazi kwa jambo hilo jema la kuwakutanisha wafanykazi na kufurahi pamoja. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angela Akilimali akizungumza machache wakati wa tafrija hiyo. Pamoja na mambo mengine aliwaasa wana Uhuru FM, Redio ya Wananchi kuzingatia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao hasa katika kipindi hiki cha Kura ya maoni ya katiba mpya pamoja na Uchaguzi mkuu.
   Picha ya pamoja ya wafanyakazi na wageni waalikwa katika tafrija hiyo.
   Viongozi wa Juu wa Uhuru FM, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi, Angel Akilimali (katikati).
   Burudaaaaaaniii ilitawala.
   Ni balaaa hakuna aliyekubali kukaa chini... na mambo ya Msondo hayo.
  Ilikuwa ni fulu rahaaa kwa wana Uhuru FM

  0 0

  Mgeni rasmi katika Mnuso wa bloggers ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akitoa mawili matatu kwa bloggers na kuahidi kuwa kuanzia mwaka huu bloggers wataingia katika tuzo mbalimbali zinazoendeshwa na MCT 
   Mrs Jeff (kushoto) akiwa na Mrs Ankal (Katikati) na Shamim Mwasha wa 8020 fashion blog wakati wa mnuso wa bloggers
   Gadiola kutoka Wazalendo 255 Arusha(Kulia) akiwa na Ankal (Katikati) na ZAinul Mzige kutoka dewji blog
   Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akisalimiana na Mmiliki wa Lukaza Blog, Josephat Lukaza wakati wa mnuso wa wamiliki wa Blog uliofanyika usiku wa Kuamkia Jana katika Hoteli ya Serena. Wanaoshuhudia pembeni Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Joachim Mushi na Mmiliki wa Michuzi Blog, Issa Michuzi
   Mgeni rasmi katika Mnuso wa Bloggers ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) akijadiliana jambo na Adela Kavishe ambae ni Mmoja kati ya wamiliki wa blog hapa Tanzania, Katikati ni Monica Joseph
   Baadhi ya Bloggers wakiwa katika picha ya Pamoja
   Cheers
   Khadija Kalili akisalimiana na Mgeni rasmi ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga wakati wa mnuso
   Mwenyekiti wa muda wa Mtandao wa Wamiliki wa Blog Tanzania (Tanzania Bloggers Network) Joachim Mushi akimkaribisha Mgeni rasmi kwaajili ya kutoa maneno mawili matatu kwa wamiliki wa blog.
   Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa akiongea jambo mbele ya Wanablog na wageni rasmi juu ya udhamini mkuu walioutoa katika mnuso huo kwa kutambua mchango wa blogs Tanzania
   Burudani kutoka kwa Jhikoman
   Mgeni rasmi akikata ndafu 
  Mwakilishi wa Bloggers akilishwa ndafu na mgeni rasmi Katika Mnuso huo.
   Adela Kavishe na Mdau Faustine Ruta wa Bukoba wadau Blog wakiwa mbele ya Ucanon wa Lukaza Blog
   Serebuka Serebuka unaweza pendwa tena........
   Faustine Ruta wa bukoba wadau blog katika ucanon wa Lukaza Blog na Josephat Lukaza
   Makala na Woinde kwa pamoja
   Monica Joseph na Mkurugenzi wa Masoko Wa Vodacom Kelvin Twisa
  Ankal akiwa na Faustine Ruta na Crant wakati wa mnuso wa bloggers.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  0 0

  indexSERIKALI imeyapokea maombi ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) cha Mkoa wa Mbeya yanayopendekeza mkoa huo ugawanywe na kupata mikoa miwili ya Mbeya na Songwe.

  Akizungumza na maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana (Jumamosi, Februari 28, 2015) kwenye uwanja wa Saba Saba wilayani Chunya, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema Serikali imeridhia maombi hayo kutokana na ukubwa wa mkoa huo ambao una kilometa za mraba 63,000.

   “Tumekwishapokea maombi ya kuugawanya mkoa wa Mbeya kwa sababu mkoa huu una eneo la kilometa za mraba 63,617 zilizogawanyika katika Wilaya 8 na Halmashauri 10. Hili ni eneo kubwa sana kiutawala, siyo rahisi kuusimamia na kusukuma maendeleo,” alisema.

   Alisema kamati hiyo imeshauri mkoa huo ugawanywe katika wilaya nne nne ambapo mkoa mpya wa Songwe utakuwa na wilaya za Ileje, Momba, Mbozi na Chunya. Wamekubaliana kuwa makao makuu yatakuwa Mbozi lakini ninyi wa chunya mmeenda mbali zaidi kwa kuigawa Chunya kwenye wilaya mbili za Songwe na Chunya ambapo chunya itaenda Mbeya,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.


   Alisema katika kikao hicho ilikubaliwa kwamba makao makuu ya wilaya mpya ya Songwe yatakuwa Mkwajuni. “Nimekubali maombi haya kwa sababu yatapunguza gharama za uendeshaji, na kama itashindikana kupata wilaya mpya basi itabidi tuwape Halmashauri ya Songwe,” alisema.  Mkoa wa Mbeya una wilaya nane ambazo zimegawanyika katika tarafa 27, kata 262, vijiji 842 na mitaa 252. Idadi ya wakazi kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni 2,707,410.

  Akizungumzia kuhusu mpango wa maji katika wilaya hiyo, Waziri Mkuu alisema bado kuna changamoto kubwa ya kufikisha maji vijijini ambako upatikanaji wake uko kwenye asilimia 46. “Tuna mpango wa kuchimba visima vikubwa vitatu na mwakani tuna mpango wa kuchimba visima vingine virefu 11, tunachohitaji ni fedha na usimamizi,” alisema.

  Alivitaja vijiji viyakavyopata visima hivyo ni Makongorosi, Mkwajuni, Kapalala, Isangawana, Galula, Lupa na Matwiga. Vingine ni Kambikatoto, Tanile, Bitimanyanga na Mapogoro. Wakati huohuo, Waziri Mkuu amezindua maabara tatu katika shule ya sekondari ya Saza ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Shanta.

  Akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Chunya, Bi. Sophia Kumbuli alisema ujenzi wa maabara hizo tatu umegharimu sh. Milioni 268.5 vikijumuisha pia ununuzi wa samani, uwekaji wa mfumo wa maji na gesi. “Kati ya hizo sh. Milioni 23.5 ni za ununuzi wa vifaa vya maabara na kemikali na sh. Milioni 245 ni ujenzi wa jengo, samani na uwekaji wa mfumo wa maji na gesi,” alisema.

  Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya kwa kutembelea wilaya ya Mbozi ambapo mbali ya kuzungumza na wananchi, atazindua maabara Vwawa sekondari, atakagua ghala la nafaka la NFRA na kupokea taarifa ya uzalishaji na usambazaji wa miche ya kahawa kwenye kituo cha TACRI – Mbimba.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuna baadhi ya watu wamegeuza mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya kuwa wa kisiasa badala ya kujikita kuwafahamisha wananchi mazuri yaliyomo.
   
   Ametoa kauli hiyo  mwishoni mwa wiki wakati akiwahutubia wakazi wa Kata ya Lwangwa kwenye Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe akiwa kwenye siku ya nne ya ziara yake mkoani Mbeya kukagua shughuli za maendeleo. “Katiba inayopendekezwa imezingatia maslahi ya kila kundi kwenye jamii hivyo zipuuzeni kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa Katiba hiyo haijakidhi malengo ya Kitaifa,” alisema.

   Alisema mabadiliko yaliyofanywa kwenye Katiba hiyo ni asilimia 20, huku asilimia iliyobakia ni sehemu ya mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Jaji Warioba.  Alisema ili kukabiliana na kauli za kiupotoshaji, Serikali imeanza kusambaza nakala za Katiba inayopendekezwa hasa kwenye mikoa ya pembezoni.

   “Jumla ya nakala 300 za Katiba Inayopendekezwa zitasambazwa kwenye kila Kata ambapo makundi yenye uwezo wa kutoa elimu sahihi kuhusiana na Katiba inayopendekezwa yatapatiwa nakala hizo ili kuwaelimisha wananchi,” alisema Waziri Mkuu. 

   Wakati huohuo, akiwa Tukuyu mjini, Waziri Mkuu alizindua ofisi za Halmashauri hiyo baada ya jengo la zamani kupata nyufa kutokana na tetemeko la ardhi. Pia alizindua maabara tatu kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya Kayuki.

   Akizungumza na maelfu ya wakazi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Tandale jana jioni, Waziri Mkuu aliwataka wakazi hao kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha wakazi zoezi la uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakapoanza.


   Alisema ni muhimu wananchi watumie fursa hiyo ya kujiandikisha kwa sababu kadi zinazotolewa ndiyo zitatumika kwenye upigaji kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

   “Usipojiandikisha sasa hutaweza kupiga kura kumchagua kiongozi unayemtaka wakati huo ukifika. Hata ukiwa na kitambulisho au barua gani hutaruhusiwa kwa sababu taarifa zako zitakuwa hazimo kwenye daftari la wapigakura.” “Hili zoezi limeanza sasa pale Njombe na litafanyika nchini kote, ni vema tukijitokeza kwa wingi na kujiandikisha wakati waandikishaji watakapokuja hapa Tukuyu,” alisema Waziri Mkuu.

   Katika hatua nyingine, Mbunge wa Rungwe Magharibi, Prof. Mwakyusa aliiomba Serikali iingilie kati mradi wa maji wa masoko kutokana na mradi huo kukwama kwa muda mrefu.  “Mradi huu umelenga kuwanufaisha wanachi wa vijiji 15, mkataba ulisainiwa tangu 2009 na mradi ulipaswa kukamilika mwaka 2011 lakini hadi leo hakuna hata tone la maji,” alisema Prof. Mwakyusa.

   Aliiomba Serikali pia iingalie barabara ya kutoka Tukuyu hadi Busokelo yenye urefu wa km. 86 kwani ni mkombozi wa mazao mengi yanayozalishwa kwenye Halmashauri ya Busokelo. “Hii barabara ni ahadi ya Mheshimiwa Rais kwamba itajengwa kwa kiwango cha lami na imeingizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi. Kwa vile muda uliobakia ni mfupi, tunaomba iwekewe japo jiwe la msingi ili Rais ajaye akumbuke kuikamilisha,” alisema.

   Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya kwa kutembelea wilaya ya Chunya na kuzindua maabara, kufungua mradi wa maji wa Mbuyuni.
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, MACHI MOSI, 2015.

  0 0

  Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, almaarufu kama RED BRIGADE, wakila kiapo cha utii, mbele ya Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jijini Mwanza leo Jumamosi Februari 28, 2-015. Kiapo hicho kinafuatia kkamilika kwa mafunzo ya kiulinzi na usalama kwa vijana hao, ambapo nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2015.
  Vijana hao wakila kiapo mbele ya Mbowe, (kulia).
  Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), kiasoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigedi' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) akisikiliza kwa makini.
  Vijana hao wakitoa heshima mbele ya Mwenyekiti wao Mbowe.PICHA KWA HISANI YA KIVIS BLOG

  0 0

  • Watoto 4,220 waguswa, Waziri Mkuu akemea tabia hizo
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameendelea kukemea tabia za utoro na mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Chunya baada ya kupewa taarifa kwamba watoto 4,420 walitoroka shule na wengine 201 kupata mimba.

  Februari 26, mwaka huu, Waziri Mkuu aliwaagiza Mkuu wa Wilaya ya Kyela pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwasaka na kuwakamata wale wote waliohusika na utoro na ujauzito wanafunzi na kuwafikisha mahakamani mara moja ili liwe fundisho kwa wengine baada ya kuelezwa kwamba wanafunzi 94 walipata ujauzito na wengine 645 kuacha shule kwa sababu ya utoro.

  Akizungumza na maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana (Jumamosi, Februari 28, 2015) kwenye uwanja wa Saba Saba wilayani Chunya, Waziri Mkuu alisema haiwezekani kuiacha hali hiyo iendelee huku watoto wa wilaya hiyo wakiharibiwa maisha kwa kukosa masomo.

  “Utoro kwenye shule za msingi, taarifa ya wilaya inaonyesha watoto 1,979 waliacha shule kati ya mwaka 2010 na 2014 ambao ni wastani wa watoto 395 kila mwaka na katika suala la mimba, taarifa hiyo inasema watoto 161 waliachishwa shule kwa sababu ya ujauzito,” alisema.

  “Haiwezekani kabisa! Hivi akinababa kuamua kutembea na mtoto shule ya msingi ni lipi hasa unalolitaka kwake… unamwachisha shule mtoto kwa lipi hasa, hapana. Nimeshatoa agizo wahusika wakamatwe. Wa zamani tunaweza tusiwapate, lakini hawa wa mwaka jana kwa shule za msingi wako 28, RC na watendaji wako fuatilieni na muwapeleke kwenye vyombo vya sheria,” alisisitiza.

  Akichanganua takwimu za sekondari, Waziri Mkuu alisema kati ya mwaka 2010 na 2014 wanafunzi 2,251 waliacha shule kwa sababu ya utoro na wengine 40 waliachishwa kwa sababu ya ujauzito.

  “Ninawasishi wazazi  na uongozi wa wilaya na mkoa tufanye jitihada kuhakikisha jambo hili linakomeshwa mara moja. Huwezi kununua madaftari an kumlipia ada tu halafu usitake kuona mwanao anamaliza shule. Kila mzazi ana jukumu la kuhakikisha mtoto wake anamaliza shule ili awe na maisha bora hapo baadaye,” alisema Waziri Mkuu.

  “Nirudie kuwakumbusha wazazi kwamba mtoto wa mwenzio ni mtoto wako, huwezi kukubali maisha yaharibike hivi hivi. Tuungane pamoja kuhakikisha tunashinda vita hii,” alisisitiza.

  Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya kwa kutembelea wilaya ya Mbozi ambapo mbali ya kuzungumza na wananchi, atazindua maabara Vwawa sekondari, atakagua ghala la nafaka la NFRA na kupokea taarifa ya uzalishaji na usambazaji wa miche ya kahawa kwenye kituo cha TACRI - Mbimba.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMAPILI, MACHI MOSI, 2015

  0 0


  0 0

   WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewatembelea askari wa Jeshi la Polisi waliolazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kutokana na ajali waliyoipata jana wakati msafara wake ukielekea Kata ya Galula wilayani Chunya.

  Waziri Mkuu aliwatembelea majeruhi hao na kuwapa pole leo asubuhi (Jumapili, Machi Mosi, 2015) kabla ya kuelekea wilayani Mbozi kuendelea na ziara yake ya Mkoa wa Mbeya. Alifuatana na mkewe Mama Tunu Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro na Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Seif Mhina.

  Akizungumzia hali ya majeruhi hao, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Ismail Macha alisema jana walipokea majeruhi tisa lakini watatu walifanyiwa uchunguzi wa afya zao na kuruhusiwa na wengine sita ilibidi wawalaze na kuwafanyia uchunguzi zaidi kutokana na hali zao zilivyokuwa.

  “Wengi wao walipata zaidi mshtuko ndiyo maana tukaamua kuwalaza ili tuendelee kuwapa uangalizi wa karibu… Mmoja tu ndiye amevunjika mkono wa kulia lakini wengine walipata michubuko miguuni, mikononi na usoni,” alisema.

  Aliwataja waliolazwa kuwa ni Deogratius Nandi (31), Paulin Masolwa (27), Omary Hussein (24), Hamisi Haji (29) ambao wote ni wanaume. Majeruhi wa kike ni Cecilia Mussa Kabona (28) na Mwazanije Hassan (23) ambaye amevunjika mkono wa kulia. Waliopata matibabu na kuruhusiwa ni Mashaka Shabani (42), Khalifa Rashid (26) na Joel Cheja (21).

  Dk. Macha alisema wanatarajia kuwaruhusu leo mchana ama kesho asubuhi kwani hali zao zinaendelea vizuri.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema chanzo cha ajali hiyo ni vumbi na kokoto barabarani ambazo zilifanya gari hilo la FFU lisesereke na kupinduka. Hata hivyo, alisema mwendo mdogo wa gari hilo ulisaidia kuokoa maisha ya askari hao.

  “Ajali ilitokea saa 5:30 asubuhi eneo la Chang’ombe ya Mjele. Eneo lile lina kokoto kubwa kubwa ambazo zilisababisha gari lao kuserereka na kupinduka… gari halikuwa kwenye mwendo mkali ndiyo maana askari hao wamepata majeraha madogo madogo,” alisema.

  Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya kwa kutembelea wilaya ya Mbozi ambapo mbali ya kuzungumza na wananchi, atazindua maabara Vwawa sekondari, atakagua ghala la nafaka la NFRA na kupokea taarifa ya uzalishaji na usambazaji wa miche ya kahawa kwenye kituo cha TACRI - Mbimba.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMAPILI, MACHI MOSI, 2015

  0 0  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda yeye Mama Salma Kikwete kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo walipokwenda yeye na Rais Kikwete kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakimfariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakiwafariji wasanii wa Tanzania One Theatre kufuatia kifo cha kiongozi wao, Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.PICHA NA IKULU

  0 0

  Ankal akiwa na MD wa Michuzi Media Group (kulia kwake) pamoja na kikosi kazi cha Team Michuzi Production chini ya Production Manager Barbra Kilugira (wa tatu kushoto) ambayo ilipata heshima ya kurekodi mnuso wa kihistoria wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Meet and greet Party katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia March 1, 2015. Mnuso huu ulifanikiwa sana kwa udhamini mkubwa wa VODACOM TANZANIA (wadhaini wakuu), NMB, COCACOLA, RAHA.COM na SERENA HOTEL. 

  0 0

   Waziri Mkuu Mstaafu,Mh Edward Lowasa akisaini kitabu cha maombolezo alipofika nyumban kwa Marehem Capt. J komba kuwapa pole wanafamilia na ndg
   Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa Kapteni John Komba.
   Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akimpa pole mke wa marehemu Kapteni John Komba.
   Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akisalimiana na wasanii wa TOT wakati akiwasili msibani.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombelezo kwenye msiba wa Kapteni John Komba.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anna Makinda akisaini kitabu cha maombelezo ya msiba wa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba.

  0 0

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng. Mussa Natty akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa kwanza kushoto) ambapo alisema miradi ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari katika wilaya hiyo itagharimu zaidi ya sh. bilioni 2. na kuwa ujenzi wake unasimamiwa na waataalamu waliobobea katika shughuli hiyo.
  FUPA uliomshinda Waziri wa zamani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuhusu migogoro ya ardhi iliyokithiri katika Manispaa ya Kinondoni Mkuu mpya wa wilaya hiyo Paul Makonda ameahidi kuutafuna.
  Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mussa Natty alisema miradi hiyo yote ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari katika wilaya hiyo itagharimu zaidi ya sh. bilioni 2. na kuwa ujenzi wake unasimamiwa na waataalamu waliobobea katika shughuli hiyo.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng. Mussa Natty akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda jinsi maabara hiyo ilivyojengwa kwa ubora wa hali ya juu.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa kwanza kushoto) akiongea na baadhi ya madiwani wa Wilaya.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Manzese mara baada ya kumkaribisha shuleni kwake,
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiweka saini ya kumbukumbu mara baada ya kuwasiri.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng. Mussa Natty akiendelea kuelezea ujenzi wa maabara.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akishuka kutoka kukagua maabara ya ghorofa inayojengwa katika shule ya sekondari Manzese.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Manzese akitoa maelezo machache kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa kwanza kushoto) mara baada ya kuingia katika maabara inayotumiwa kwa sasa.
  Mara baada ya kumaliza ziara yake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa kwanza kushoto) alifanya majumuisho ya ziara, Ambapo ametoa onyo kwa wale wote waliojenga katika maeneo hayo kuanza kuondoka mara moja kabla hawajafikiwa.
  "Moto ninaokuja nao katika suala ili hautazimika nitasimamia mimi mwenyewe kwa kushirikiana na polisi ubomoaji wa majengo yote ambayo yamejengwa katika maeneo ya wazi na yale yaliyotengwa kwa ajili ya shule" alisema Makonda.
  Makonda alitoa maagizo hayo katika ziara ya siku moja ya kukagua shughuli za maendeleo katika wilaya yake Dar es Salaam jana.
  "Mimi simuogopi mtu nasimamia utendaji wangu wa kazi kila mtu anajua msimamo wangu wa kusimamia jambo na katika suala ili hakuna atakaye salimika " alisema Makonda.
  Makonda aliagiza migogoro yote ya ardhi ambayo ipo hivi sasa ianze kushughulikiwa na watendaji wanahusika katika manispaa hiyo kuanzia ngazi ya chini na ametenga kila Ijumaa migogoro ambayo inashindikana ipelekwe ofisini kwake ili kuzikutanisha pande zote zinazohusika kwa ajili ya kusuruhisha migogoro hiyo.
  Sambamba na agizo hilo Makonga amewataka wote wa manispaa hiyo kusimamia ujenzi wa maabara kikamilifu na kuagiza kuwa Aprili mwaka huu miradi yote iwe imekamilika."Hatutasubiri mpaka mwezi wa sita kama alivyo agiza wazirin mkuu kumaliza miradi yote ndani ya kipindi hicho nawaagiza mkamilishe maabara zote ifikapo mwezi wa nne na wale wote watakaoshindwa wajipime utendaji wao" alisema Makonda.

  Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni, Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni katika shule ya sekondari Turian iliyopo katika wilaya ya Kinondoni wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya Maabara katika sekondari za Wilaya yake. Aliyesimama nyuma yake ni Mkuu wa shule ya sekondari Turiani Mwalimu Betrice Mhando. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
  Mkuu wa shule ya sekondari Turiani Mwalimu Betrice Mhando akitoa maelezo machache juu ya shule yake mbele ya Mkuu wa Wilaya aliyeongozana na viongozi mbali mbali wa Wilaya.


  0 0

   Marehemu Kapteni Komba enzi za Uhai wake.

  Kesho tarehe 02/3/2015 saa 1 asubuhi misa parokia ya Mt. Bikira Maria Mpalizwa iliopo mbezi , saa 4 asubuhi mwili utaelekea Karimjee kwa ajili ya kuagwa, na saa 8 mchana mwili utaelekea airport tayari kwa safari ya Songea. Mazishi yatafanyika tarehe 3/3/2015 kijijini kwake Lituhi.

  Kufuatia Msiba huu shughuli za kamati hazitakuwepo kwa kesho tarehe 2/3/2015. Ukipata taarifa hii tafadhali mjulishe na mwingine.

  IMETOLEWA NA;
  OFISI KATIBU WA BUNGE
  1.3.2015

  0 0

  POSTPONMENT OF THE 1ST EAST AFRICA CONGRESS OF ACCOUNTANTS IN ARUSHA -TANZANIA
  Due to unavoidable circumstance the 1st East Africa Congress of Accountants which was scheduled to take place in Arusha from    5th to 7th  March 2015 has been postponed till further notice.
                                                                     
  We are very sorry for any inconvenience caused.


  Issued by:
  Executive Director
  NBAA,  Mhasibu House,
  P.O. Box 5128,
  Dar es Salaam.
  23rd February 2015


  0 0

  Napenda Kuchukua Fursa hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye Kurehemu kwa kunijaalia Uhai na afya njema hadi kufikia siku hii ya leo,ambapo ninayo furaha kubwa sana kwa kuongeza namba moja katika umri wangu,kwani bila yeye hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika.

  pia nitakuwa ni mchoyo wa Fadhila iwapo sitotoa shukrani za kipekee kwa ndugu zangu woote (wakiwemo wazazi wangu wawili,Ankal Issa Michuzi,Ahmad Michuzi,Karim Michuzi,Ramadhan Michuzi,Ismail Michuzi,Ankal Macheka,Ali Michuzi,Zahra,Tatu,Sellah,Bobby,Noreen,Adam,Saleh na wengine wengi ambao sijawataja majina yenu hapa ila moyoni ninayo,na bila kumsahau mtarajiwa wangu wa ubani bi. Farida) kwa kuwa pamoja nami katika makuzi yaliyo mema hadi leo hii kufikia hapa nilipo.


  Tanzania Bloggers Network (TBN) pia naomba mpokee shukrani zangu za dhati kwa kuwa pamoja nami kama mwanachama hai siku zote na bila kunitupa,pia nichukue fursa hii kutoa pongezi kwa uongozi wa TBN na wanachama wenzangu kwa kuungana pamoja katika tafrija ya kihistoria  iliyotukutanisha pamoja,kiukweli ile ilikuwa ni siku muhimu sana kwetu kwa kutukutanisha pamoja na kufahamiana zaidi,ile ilikuwa ni bonge la heko kwani kuna wengine walitamani kuwa na umoja kama wetu lakini hawafanikiwi.

  pia nawashukuru marafiki,jamaa zangu pamoja na Wadau woote popote pale mlipo ambao kwa namna moja ama nyingine mmekuwa ni mchango mkubwa katika maisha yangu na kunifanya kila siku niwe bize kuhakikisha libeneke halilali mpaka kieleweke.Nawashukuruni sana tena sana na Mungu awabariki nyoote. Nawapenda sana wote na tuko pamoja sana.


  TEMBELEA BLOG YA MTAA KWA MTAA Inayomilikiwa na Besdei boy Othman Michuzi kwa kufuata link hii.
  http://othmanmichuzi.blogspot.com
   
  Hapa ni dole tupo,nikiwa na wadau wangu Anganile na Hellen Kiwia.

  0 0

   Mratibu wa programu ya Wafanye Watabasamu na mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, akimwonesha mtoto Maurine jinsi ya kuchora katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita. Mpangala na wenzake walitembelea watoto wanaotibiwa saratani ili kuchora nao na kuwapa zawadi mbalimbali. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu
   Nguvu ya sanaa tiba kama inavyooneshwa na Clara.
   Sanaa tiba ikawasahaulisha maumivu, wakajihisi wako nyumbani. Baadhi ya watoto wakijiachia na marafiki wa Wafanye Watabasamu waliokwenda kuwatabasamisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita.
   Mtoto Nico akienda sambamba na marafiki wa Wafanye Watabasamu. Kutoka kulia ni Sia Marupa, Masoud Junior na Cloud Chatanda.
   Ha ha ha haaaaaa. Hili ndilo lengo hasa la Wafanye Watabasamu. Mungu akupe nafuu ya mapema Nico. 


  Marafiki wa Wafanye Watabasamu Jumamosi iliyopita waliwatembelea tena watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, ambapo waliwapa zawadi mbali mbali kisha kuchora nao ikiwa ni sehemu ya sanaa tiba (art therapy). 
   Akizungumza na blogu hii, mratibu wa programu hiyo ambaye pia ni mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, alisema, ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kutumia sanaa tiba kukabiliana na msongo wa mawazo, kusahaulisha maumivu na kuwapa nafasi watoto waweze kufanya shughuli walizokuwa wakifanya majumbani. 
  Ziara hiyo imewezekana kutokana na michango ya marafiki wa ndani na nje ya nchi ambao walichangia fedha na vitu mbali zikiwamo sabuni, dawa za meno, miswaki, mafuta ya kupakaa, toilet papers, matunda, vifaa vya kuchorea nk. “Tiba sanaa ni sanaa mpya nchini, baadhi ya nchi inatumika mahospitalini, magerezani, makambi ya wakimbizi, mashuleni, kwenye vituo vya kulelea watoto wenye mazingira magumu, majumbani nk. Si kwa watoto tu hata watu wazima inawahusu pia,” Alisema Mpangala. 
   Mpangala alisema programu hiyo imepokelewa vizuri na watoto hospitalini hapo na inaratibiwa kupitia mitandao ya kijamii. Kwa watakaopenda kuungana na programu hii watembelee ukurasa wa Wafanye Watabasamu katika facebook. 
   Mpangala amewashukuru, wasanii wenzake, marafiki wa Wafanye Watabasamu, Hospitali ya Taifa Muhimbili, ndugu jamaa na marafiki kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika. Pia vyombo vya habari kwa kupaza sauti za watoto hao.

  Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Karibu katika sehemu hii ya kwanza kati ya mbili za mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.

  Aliketi nasi kuzungumzia zaidi suala hili la Katiba hii pendekezwa, na mchakato mzima wa kuipata
  Karibu

  0 0

   
  Kikosi cha Timu ya Benki ya Exim Tawi la Babati katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa kirafiki kuanza kati ya timu hiyo ya Benki na timu ya Babati Citizens FC wakati wa Bonanza la michezo lililofanyika mwishoni mwa wiki Babati. Bonanza hilo liliandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa mkoani Manyara lilikiwa na lengo la kukuza michezo mkoani hapo.

  0 0

    Meneja wa Airtel Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo (kushoto)  akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Saidi Juma Alli (Kulia) mkazi wa kondoa baada ya kuibuka mmoja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani katikati akishuhudiaAfisa Uhusiano na matukio wa Airtel bi Dangio Kaniki .
   Meneja wa Airtel Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo (kushoto)  akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Saidi Juma Alli (Kulia) mkazi wa kondoa baada ya kuibuka mmoja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani katikati akishuhudiaAfisa Uhusiano na matukio wa Airtel bi Dangio Kaniki .
   Mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli akilijaribu gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 778 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.
   Wafanyakazi wa Airtel wakisherehekea kwa pamoja na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli (mwenye shati jekundu), baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.
  Wafanyakazi wa Airtel wakisherehekea kwa pamoja na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli (mwenye shati jekundu), baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.


  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imemkabidhi gari aina ya Toyata IST kwa Bwana Juma Said Alli mkazi wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma mara baada ya kuiba mshindi katika droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha zaidi.
  Zawadi hiyo yenye thamani ya Shilingi Milioni 15 ilikabidhiwa kwa Alli mwishoni mwa wiki na Meneja wa Airtel Kanda ya Kati, Stephen Akyoo. Akizungumza mbele ya vyombo vya habari wakati akikabidhiwa gari hiyo aina ya IST, yenye namba za usajili T778 DCZ, Alli alisema shughuli zake ni ukulima wa mazao mbalimbali katika Kijiji cha Ololimo na ana mke mmoja na watoto wawili. 
  “Sikutegemea kushinda ingawa nimekuwa nikijiunga mara kwa mara na kifurushi cha Yatosha, kila ninaponunua vocha za Airtel na ninamshukuru Mungu nimeshinda kutokana na Yatosha ya Shilingi 500 tu. Hivyo nawahimiza watanzania wenzangu wasikate tamaa kwani na wao wanaweza kubahatika kama mimi na kujishindia gari hili zuri,”alieleza Alli.
   Kwa upande wake Meneja wa kanda ya kati bwana Stephen Akyoo alisema "tunao washindi wengi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam, Kagera, Mtwara, Mbeya, Tanga,Mwanza,katavi na sasa Dodoma. 
   Promosheni hii bado inandelea ni rahisi sana kwa kutumia vifurushi vya Airtel yatosha vya siku, wiki au mwenzi moja kwa moja unaunganishwa kwenye droo ya Airtel yatosha na kupata nafasi ya kujishindia Toyota IST kila siku. 
  Vifurushi vya Airtel yatosha vinapatikana kwa kupiga *149*99# , au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha au kununua kupitia Airtel Money kwa matumizi yako ya kawaida kabisa unapata nafasi ya kujishindia gari " 
   Wakati huo huo Airtel imetangaza washindi saba wa wiki ya nne ya promosheni ya Airtel yatosha waliopatikana kupitia droo iliyofanyika siku ya ijumaa katika makao makuu ya Airtel Moroco, washindi hao ni pamoja na Juma Mapande (30) mkazi wa Pwani, Eusedio Onesmo Kipalile(48) mkazi wa Njombe, Suleiman Daudi Onesmo (20) Mkazi wa Mwanza, Seleman Kikondi Kimu (29) Mkazi wa Morogoro, Hassan Saidi Kimbe(28) Mkazi wa Dar es Saalam, Mohamed Ahmed Hamis (47) mkazi wa Manyara pamoja na Aivan Mbogambi Saigwa (35) Mkazi wa Dodoma 
   Washindi hawa watakabithiwa magari yao wiki hii pindi taratibu zote za makabithiano zikikamilika

  0 0
 • 03/02/15--03:10: Article 10


older | 1 | .... | 473 | 474 | (Page 475) | 476 | 477 | .... | 1897 | newer