Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Tamthilia ya "A Boys Mission" yahitaji Milioni 800 ili ikamilike

$
0
0
 Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye vituo vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha kutoka kulia ni Jesca haule na Aisha bakari.
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana katikati akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye vituo vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Brian daniel, Neema Mung'anya, Samuel katabazi, Jesca haule, Aisha bakari na Victor Casmir.

 Waigizaji wa tamthilia ya “A boys mission” inayoandaliwa na kampuni ya Forward Formidable Enterprises katika picha ya pamoja.
Kampuni mpya katika utengenezaji wa filamu nchini, Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” inahitaji kiasi cha Sh milioni 800 ili ikamilike.

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya FFE, Johnson Lujwangana alisema kuwa kwa sasa wameweza kutengeneza toleo la utangulizi "pilot episode' kwa ajili ya kuonyesha nini wanakifanya huku kila kitu kikiwa tayari kwa ajili ya kurekodiwa. Johnson alisema kuwa tamthilia yao inazungumzia changamoto na suluhisho mbalimbali kwa maisha ya vijana nchini na fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kughalimia gharama mbalimbali za kuzalisha rasmi tamthilia hiyo.

Baadhi ya gharama hizo kwa mujibu wa Johnson ni kulipa mtayarishaji bora, kuwalipa wasanii fedha kutokana na ubora wa kazi zao, kulipia vifaa vya kisasa, kulipa sehemu bora ya kurekodi tamthilia, usafiri, chakula na gharama nyinginezo.

“Kama msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond anatengeneza video ya dakika tatu kwa Sh Milioni 60, kwa nini tamthilia ambayo kila sehemu (episode) inatumia si chini ya dakika 45 hisifikia kiwango hicho cha fedha? Alihoji Johnson. Alisema kuwa wao wanataka kuwafaidisha wasanii wao kwa kuwalipa vizuri na kuendelea kudumu katika fani na kuwataka wadhamini kujitokeza kwa wingi kusaidia mradi huo.

“Hakuna hata msanii mmoja maarufu katika tamthilia hii, lengo si kama kuwatupa wasanii hao, bali ni kupanua wigo na kuwapa nafasi wasanii wengine, nataka kizazi kipya zaidi katika tasnia ili kuendeleza kuzalisha mastaa,” alisema. Alisema kuwa katika tamthilia imeonyesha na kutoa majibu ya nini vijana wanatakiwa kufanya hapa nchini na kuachana na fikra za kukimbilia nje ya nchi  kwa kudhani kuwa ndiko kutakuwa suluhisho la matatizo yao.

Alifafanua kuwa mara baada ya kufika huko, hali inakuwa tofauti na kukutana na changamoto nyingi zaidi za maisha na kuwaza kurejea nchini. “Tamthilia ni ya kisasa zaidi kwani lengo letu pia ni kuonyeshwa nje ya nchi na kuonyesha madhari ya kuvutia ya jiji letu la Dar es Salaam na kupromoti mji wetu tofauti na hali iliyozoeleka kwani tamthilia nyingi uonyesha maisha ya vijijini,” alisema Johnson.

Alifafanua kuwa kwa kuonyesha usafi wa mji, maeneo mbalimbali ya starehe ya hapa nchini, kutawavutia hata wasanii watayarishaji wa tamthilia nje ya nchi kuja kutayarishia kazi zao hapa nchini. Alisema kuwa tamthilia hiyo ina jumla ya sehemu 12 ambapo katika kila sehemu, muigizaji mkuu ma maudhui ya tamthilia pia yanabadilika.

MISS UNIVERSE NALE BONIFACE ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) CHA SALVATION ARMY

$
0
0
1
Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akikata  keki na wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakatialipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha  Salvatrion Arm jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya  siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi  watoto hao.
2
Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akiwalisha  Keki na wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakati  alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha  Salvatrion Arm jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya  siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi  watoto hao.
3
Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akigawa  madaftari kwa wanafunzi wenye mahitaji wakati alipotembelea  kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvatrion Arm
 jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya  kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi watoto hao.
4
Zawadi
6
Picha ya pamoja

Washindi wa Promesheni ya Airtel yatosha Zaidi wakabidhiwa magari yao

$
0
0
 Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kulia), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa mshindi huyo, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
 Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti akilijaribu gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana.
 Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akikabidhi kadi ya umiliki wa gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti katika hafla iliyofanyika, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (wa pili kushoto) ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.

 Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti akiteremka kutoka kwenye gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana.
 Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 464 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Wakala wa Mtandao huo, John Fred Kiwale katika hafla iliyofanyika, Mtaa wa Togo, eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando na (kulia) ni Mke wa mshindi huyo, Anna Kiwale na motto wake, Sylvia John.

 Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (katikati) akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Kondakta wa Malori, Jastini William Dodoo katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde.
 Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Jastini William Dodoo akiwa mwenye furaha ndani ya gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, baada ya kukabidhiwa na Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (kushoto), katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (katikati), akifafanua jambo kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Jastini William Dodoo (kulia), baada ya kumkabidhi gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.

PATO LA TAIFA LAONGEZEKA, LAFIKIA SHILINGI TRILIONI 21.2.

$
0
0
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Morrice Oyuke (Kulia)akitoa taarifa ya Pato la Taifa kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2014 leo jiji Dar es salaam. Pato hilo kwa mwaka 2014 limefikia kiasi shilingi trilioni 21.2  kutoka trilioni 19.8 za mwaka 2013, Kushoto ni  Mtakwimu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Gregory Milinga,.Picha na Aron Msigwa-MAELEZO.
PATO LA TAIFA LAONGEZEKA, LAFIKIA SHILINGI TRILIONI 21.2.
Aron Msigwa –MAELEZO.

Pato la Taifa (GDP)  katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2014 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 21.2  kutoka shilingi trilioni 19.8  za kipindi kama hicho kwa mwaka 2013.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jiji Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Morrice Oyuke, amesema kuwa katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2014 sekta nyingi za uchumi zimefanya vizuri katika uzalishaji ikilinganishwa na mwaka 2013.

Amesema katika kipindi hicho shughuli za uchimbaji wa Madini , Mawe na Kokoto zimekua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 3.3 za mwaka 2013, Uzalishaji wa bidhaa za viwandani  ukikua kwa asilimia 10.8 kutoka asilimia 10.4 pamoja na ongezeko la uzalishaji wa umeme kwa asilimia 10.7 kutoka asilimia 10.3 za mwaka 2013 kutokana na matumizi ya mafuta na Gesi.

Amezitaja sekta nyingine kuwa ni usambazaji maji ambao umekua kwa asilimia 12.7 kutoka 6.9 za mwaka 2013, Habari na Mawasiliano kwa asilimia 11.9 kutoka 7.0, Shughuli za Fedha na Bima zikikua hadi kufikia asilimia 13.9 kutoka asilimia 6.8 za mwaka 2013.

Ameongeza  kuwa  katika kipindi hicho huduma za upangishaji wa nyumba zilikua  hadi kufikia asilimia  2.2 kutoka 2.1,  shughuli za kitaalamu, kisayansi, ufundi na utawala  zikifikia  asilimia 5.4 kutoka asilimia 1.0 ya mwaka 2013.

 Bw. Oyuke amezitaja  shughuli  nyingine kuwa ni uendeshaji wa Serikali ambazo zilikua  kwa asilimia 4.9 ikilinganishwa na 4.4, huduma za Elimu kwa asilimia 3.7 kutoka 3.5, Afya kwa asilimia 8.1 pamoja na shughuli za Sanaa na Michezo ambazo zilikua kwa asilimia 2.5 ikilinganishwa na 1.6 ya mwaka 2013.

Aidha, amebainisha kuwa uzalishaji wa Almasi katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2014 ulikuwa karatasi 66,508 ikilinganishwa na karatsi 27,828 zilizozalishwa katika kipindi kama hicho mwaka 2013.

Akizungumza kuhusu sekta ambazo hazikufanya vizuri katika kipindi cha Robo tatu ya mwaka 2014 Mkurugenzi huyo amesema kuwa  ni dhahabu  ambayo uzalishaji wake ulifikia Kilogramu 10,137 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na 11,010 za mwaka 2013,Madini ya Tanzanite kilogramu 1,449 kutoka 5140 zilizozalishwa mwaka 2013.

Amefafanua kuwa shughuli za Biashara za Jumla na reja reja, Ukarabati wa magari na pikipiki pamoja na vifaa vingine vya nyumbani zimeonyesha kukua kwa asilimia 6.0 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 6.7 ya mwaka 2013, shughuli za uhifadhi asilimia 13.9 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na asilimia 19.3 za mwaka 2013.

Aidha, amebainisha kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya mwaka 2014 kuanzia Julai mpaka Septemba, Pato la taifa kwa bei za mwaka 2007 limefikia kiasi cha Shilingi trilioni 10. 7 ikilinganishwa na shilingi trilioni 10.1 ya mwaka 2013.
 

Tanzania na Zambia zadhamiria kufufua Reli ya TAZARA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Zambia kwa ajili ya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Edgar Lungu ( mwenye suti ya kijivu aliyesimama mbele ya Rais Kikwete).
Rais Lungu akimkaribisha Rais Kikwete (hayupo pichani kuzungumza).
Mhe. Rais Kikwete akizungumza wakati wa mazungumzo rasmi na Rais Lungu na Ujumbe wake katika Ikulu ya Zambia. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Mebe na kulia ni Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma.

Rais Lungu wa Zambia aandaa Dhifa Kwa Heshima ya Rais Kikwete

$
0
0
1
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais wa Zambia Edgar Lungu pamoja na wake zao Mama Salma Kikwete na Mama Esther Lungu wakinyanyua glasi juu wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake ambao walifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Zambia.
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Edgar Lungu wa Zambia wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.
3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na Rais wa Kwanza wa taifa la Zambia Dkt.Kenneth Kaunda wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili nchini Zambia tayari amerejea jijini Dar es Salaam. (picha na Freddy Maro)

MWIJAGE AZITAKA KAMPUNI ZA MAFUTA KUBORESHA MAHUSIANO KWA JAMII

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (Kulia) akielekeza jambo kwa baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya Mafuta ya TIPPER alipotembelea Kampuni hiyo hivi karibuni wakati wa ziara yake kwa Kampuni mbalimbali zinazojishughulisha na biashara ya mafuta nchini.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (Wa pili kutoka Kushoto) akifuatana na baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO kukagua miundombinu ya kuhifadhia mafuta iliyoko eneo la Kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri alitembelea Kampuni mbalimbali zinazojishughulisha na biashara ya mafuta nchini kufanya mazungumzo na kukagua miundombinu inayotumiwa na Kampuni husika.
 Meneja wa Kampuni ya Mafuta ya HASS nchini Tanzania, Ali Hassan Ahmed (Kushoto), akisikiliza maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (aliyeinua mkono) kuhusu utekelezaji wa mambo mbalimbali unaotakiwa kufanywa na Kampuni hiyo, hususan kujenga mahusiano mema na jamii. Wa kwanza Kulia ni Mbunge wa Temeke (Viti Maalum – CCM), Mariam Kisaka.
 Joshua Mtunda (mwenye Fulana ya Njano), akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (wa Tatu kutoka Kushoto), kwa niaba ya Vijana wenzake wanaofanya biashara ya kusafirisha abiria kwa Pikipiki/Bodaboda kuhusu msaada wanaohitaji ili kuboresha biashara yao. Vijana hao wanafanya biashara yao eneo la Kigamboni karibu na ilipo Kampuni ya Mafuta ya HASS.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (wa kwanza – Kushoto), akikagua miundombinu ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya Mafuta ya PUMA katika eneo la Kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Pamoja naye pichani ni baadhi ya Viongozi wa Kampuni hiyo na Maafisa wa Serikali wanaoshughulikia Sekta ya Mafuta.



Na Veronica Simba
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage amezitaka Kampuni zinazojishughulisha na biashara ya Mafuta nchini, kutumia mbinu mbalimbali za kuboresha mahusiano mema na jamii zinazowazunguka ili kujenga imani kwa wananchi na hivyo kupata ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa miundombinu husika.
Aliyasema hayo katika ziara yake hivi karibuni alipotembelea Kampuni mbalimbali za Mafuta zilizoko jijini Dar es Salaam pamoja na kukagua miundombinu yao. 

Mwijage alisema, matatizo kama vile kuharibiwa kwa miundombinu ya kuhifadhia na kusafirishia mafuta, pamoja na wizi wa mafuta unaofanywa na baadhi ya wananchi unachangiwa na wananchi kutokuwa na imani na wafanyabiashara hao kwa kuwa hawaoni manufaa ya moja kwa moja kwa jamii kutoka Kampuni hizo.

“Ikiwa wananchi wataona manufaa ya uwepo wa Kampuni zenu katika maeneo yao, nina uhakika watajenga imani kwenu na hawatakuwa tayari kuona mnaharibikiwa kwa namna yoyote kwani wao pia watakuwa ni sehemu yenu,” alisema Mwijage.

Akifafanua kuhusu namna nzuri ya kujenga mahusiano mema na jamii, Mwijage alisema inafaa Kampuni hizo ziwasaidie wananchi kuinua vipato vyao kwa kuwapatia mitaji ya fedha na vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya biashara mbalimbali.

Naibu Waziri alitoa mfano wa biashara ndogondogo za kusafirisha abiria kwa kutumia Pikipiki maarufu kama Bodaboda zinazofanywa na vijana, pamoja na biashara ya kuuza chakula maarufu kama Mama Lishe kwa akina mama na mabinti. 

“Pamoja na mambo mengine makubwa mnayosaidia jamii kama vile kuchangia elimu, nashauri pia muone namna ya kusaidia mambo madogo madogo kama kuwanunulia bodaboda vijana pamoja na kuwapa mitaji akina mama lishe,” alisisitiza Mwijage.

Aidha, Mwijage alisisitiza Kampuni hizo kuwashirikisha Viongozi mbalimbali wa maeneo husika wakiwamo Wabunge, Madiwani, Viongozi wa Kata na Mitaa husika katika zoezi la kuainisha watu wanaohitaji misaada husika ili kuepuka utapeli kwa kuwapatia wasio na sifa zinazostahili kupata misaada hiyo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri aliagiza Barabara ya Mafuta iliyoko eneo la Mivinjeni-Kurasini jijini Dar es Salaam ifunguliwe ili kupunguza msongamano wa magari unaochangia magari makubwa yanayosafirisha mafuta kwenda sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi kutokusafiri kwa wakati hivyo kusababisha hasara kwa Kampuni husika.

“Ninaomba Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iangalie uwezekano wa kuifungua njia hii ambayo wameifunga, ili itumike kama ilivyokuwa ikitumika awali; magari yaingie na kutoka kwa urahisi ili kuepusha msongamano uliopo,” alisisitiza Mwijage.

Naibu Waziri alilazimika kutoa agizo hilo kufuatia hali ya msongamano mkubwa wa magari aliojionea kwa baadhi ya Kampuni alizotembelea ikiwemo Kampuni ya GAPCO iliyoko eneo la Kurasini.

Kwa upande wao, wawakilishi wa Kampuni zilizotembelewa na Naibu Waziri, waliahidi kuzingatia ushauri uliotolewa katika kuboresha mahusiano yao kwa jamii husika.


CHID BENZ ALIPA FAINI 900,000/=, AACHIWA HURU NA MAHAKAMA

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya.

Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo misokoto ya bangi.

Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.

CHIDI BENZ HURU:Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya 900,000/= kwa kukutwa na madawa ya kulevya.

POSTPONEMENT OF THE 1ST EAST AFRICA CONGRESS OF ACCOUNTANTS IN ARUSHA-TANZANIA

$
0
0
POSTPONMENT OF THE 1ST EAST AFRICA CONGRESS OF ACCOUNTANTS IN ARUSHA -TANZANIA
Due to unavoidable circumstance the 1st East Africa Congress of Accountants which was scheduled to take place in Arusha from    5th to 7th  March 2015 has been postponed till further notice.
                                                                   
We are very sorry for any inconvenience caused.


Issued by:
Executive Director
NBAA,  Mhasibu House,
P.O. Box 5128,
Dar es Salaam.
23rd February 2015

Mh. Al Shaimar Kweigyir amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino)

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir, amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino,Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.

Katika ziaraa hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, Crencencia Joseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Bayport Financial Services mkoani Mwanza. 
Wakiwa Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana nao alipata fursa ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Ersther ambaye ni wa Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha yake pamoja na kulia msiba wa mwanae.

Tukio la utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi limezidi kushika kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau, hususan wale wenye ulemavu wa ngozi wakiamini kuwa serikali imeshindwa kuwapatia ulinzi wa kutosha.

Akiwa jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba kwa ajili ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili kati ya watano waliobaki wakiwa ni albino.
Mbunge wa kuteuliwa Shaimar Kweigyir katikati akiwa na bibi wa Yohana Bahati (Tabu Maganiko) kulia ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyeuawa hivi karibuni mkoani Mwanza, huku mama yake akiachwa na majeraha makubwa wakati wanagombania mtoto katika tukio hilo la kusikitisha. Kushoto kwake ni Mweka Hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdullah Omari.
Katibu wa Mheshimiwa mbunge, Semeni Kingalu, kulia akipiga picha wakati walipomtembelea majeruhi Ester Maganiko, ambaye mtoto wake Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi aliuliwa katika tukio hilo la kusikitisha. Anayefuata ni Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Bugando na Clencencia Joseph, Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

MKURUGENZI WA TAMWA ATUNUKIWA TUZO YA CEFM CHAMPION

$
0
0
DSC_01311-1024x681 (1)
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mh. Alexandre Lévêque akimkabidhi tuzo ya kwanza Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA,Bi. Valerie Msoka kwa kufanikisha kampeni dhidi ya ndoa za utotoni.(Picha zote kwa hisani ya mtandao wa hivisasa.co.tz).
DSC_01341-1024x681
Mmoja wa wafanyakazi wa Chama cha wanahabari wanawake Tanzania TAMWA akiwakilisha zawadi ya ua kwa Mkurugenzi wao Valerie Msoka baada ya kukabidhiwa tunzo ya umahiri na utambuzi wa kupinga ndoa za utotoni na Ukeketaji nchini Tanzania kutoka nchini Canada.
DSC_02031-1024x681
Wapili kutoka kushoto ni Balozi wa Canada nchini Tanzania Alexandre Lévêque , Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Valerie Msoka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe na wawakilishi mbalimbali kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa wa masuala ya wanawake, UNFPA na UN Women.
DSC_01191-1024x681 (1)
Wadau mbambali wa masula ya wanawake na waandishi wa habari wakongwe (Ma-Veterans), kutoka kushoto ni Fatuma Aloo pamoja na Mama Rose Haji Mwalimu wakihsuhudia tukio hilo.





Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) Valerie Msoka, amekuwa mtu wa kwanza kutunukiwa tuzo ya CEFM Champion, na Ubalozi wa Canada nchini.

Katika sherehe fupi iliyofanyika Serena Hotel 24 Februari 2015, Balozi wa Canada nchini Bwana Alexandre Leveque alisema kuwa Valerie Msoka amekuwa mwanaharakati wa kwanza kutunikiwa tuzo hiyo na ubalozi wake kama ishara ya kukubali mchango wake kupiga vita ndoa za utotoni, za kulazimishwa na ukeketaji kwa watoto wa kike nchini.

“Watoto wa kike na wanawake wamevumilia machungu ya ndoa za utotoni na za kulazimishwa hivyo wanahitaji mtu wa kuwasemea: mtu ambae ataelezea taarifa zao zinakazosaidia kuwaweka watu pamoja na kuleta mabadiliko yenye tija,”amesema Balozi Lévêque. Valerie Msoka atakuwa mtetezi. Ninafuraha kumtangaza kuwa Mtetezi wa CEFM wa Ubalozi wa Canada nchini Tanzania.”

Valerie ametumia ujuzi wake kama mwanahabari aliyebobea, mwanaharakati na mpenda maendeleo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali bila kujali litakalomtokea au kueleweka vibaya na jamii.
Ameandika taarifa zenye kuvuta hisia, huruma na kuhamasisha kasi ya mabadiliko Katika jamii na watunga sera,” alisema Balozi Leveque.

Watoto wa kike milioni 14 duniani huozeshwa kila siku katika umri mdogo chini ya 18 jambo ambalo ni kinyume cha haki za mtoto na ukiukwaji wa haki za binadamu. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa ndoa za utotoni na mikoa husika ni Shinyanga, Tabora, Mara, Lindi, Mbeya na Morogoro.

Balozi Leveque ameahidi kuunga mkono jitihada zinazomlinda mtoto wa kike ili kuendeleza kampeni ya Zero Marriage kwa mkoa wa Mara iliyozindiliwa mwaka 2014 na aliyekuwa mke wa Hayati Rais wa Kizalendo wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela, Graca Machel.

Akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo hiyo, Valerie Msoka alisema kuwa ndoa za utotoni za kulazimishwa na ukeketaji vyote vinaenda pamoja na ni wajibu wa wadau mbalimbali ikiwemo serikali na vyombo vya habari kuendeleza kutoa elimu, kufanya tafiti ili kuwa na rekodi inayofahamika kuhusu ukubwa wa tatizo, kufuatilia mwenendo na mafanikio ya kampeni mbalimbali na kuendeleza hamasa kwa jamii kwa nini ndoa za utotoni zikomeshwe.

“Tukitaka kufanikisha kampeni hii ni lazima tufanye kazi kwa pamoja na kwa moyo mmoja, kuelewa nani anafanya nini kwa kiwango gani. Serikali nayo bado tunaitegemea sana kwa hali na mali katika kubadilisha sera zinazomkandamiza mtoto wa kike kwa kuzingatia mabadiliko ya katiba mpya”, alisema Valerie.

“Tuzo hii ni yetu wote, kama sio kwa ushirikiano wenu wadau wa maendeleo, vyombo vya habari ambavyo tumefanya kazi kwa karibu sana na jamii kwa ujumla. Ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushikamana kuhakikisha kuwa hadhi ya mtoto wa kike inalindwa ipasavyo”.

Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) kupata tuzo ya kutambulika. Mwaka 2010 Ubalozi wa Marekani ulimtunuku Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Ananilea Nkya tuzo ya Mwanamke Jasiri kutokana na mchango wake wa kuendeleza usawa, fursa na haki kwa wanawake wa wasichana wa Kitanzania.

Akitoa nasaha zake kwa niaba ya serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Jinsia Bi Anna Maembe amempongeza Msoka kwa kazi nzuri na chama anachokiendesha kwa ujumla na kusema kwamba tuzo hii imetolewa wakati ambapo dunia na taifa kwa ujumla linatafakari matokeo ya Beijing +20 ambako Katika maazimio 20 yaliyoainishwa, Tanzania ilipendekeza kulifanyia kazi azimio moja ambalo ni la kumlinda mtoto wa kike.

Maembe amesema tuzo hii itatoa hamasa kwa wengine na itakuwa kielelezo cha serikali Katika jitihada za kutekeleza tamko la CEDAW linalolenga kumlinda mwanamke na mtoto wa kike.

Amesema serikali itaendeleza jitihada hizo kwa kuhakikisha watoto wa kike hawaolewi katika umri mdogo kwa kulazimishwa kwa kujenga mazingira mazuri shuleni yatakayovutia watoto wa kike kubaki mashuleni, kuongeza hamasa za uelewa wa tatizo na kuhakikisha wale wote wanaohusika na kuwalazimisha watoto wa kike kuolewa Katika umri mdogo wanachukuliwa hatua za kisheria. Lakini pia kuharakisha kubadilisha sharia ya Ndoa ya mwaka 1971 ambayo haimlindi mtoto wa kike chini ya umri wa miaka 18 kuolewa.

“Watoto 2 kati ya 5 hujikuta wako Katika mazingira ya kuozeshwa kwa nguvu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kutokuwa na elimu ya kutosha, maisha duni vijijini, umaskini na mila na desturi potofu zinazoendelezwa na baadhi ya makabila na mahari”, amesema Maembe.
Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 39 ya watoto wa kike wenye elimu ya msingi wameolewa katika umri usiotarajiwa chini ya miaka 18 wakati wale wenye elimu ya kutosha wa mjini wameolewa baada ya kufikisha miaka 18.
DSC_02181-1024x681
Mkurugenzi wa mtendaji wa TAMWA akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Chama hicho. 

Ndoa za utotoni ni pale mtoto wa kike anapoozeshwa kwa lazima akiwa katika umri chini ya miaka 18 na wakati mwingine yuko shuleni. Madhara yake ni makubwa kwa afya ya mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kupoteza uhai wake na mtoto mwenzake, kukosa maendeleo kimaisha na kuendeleza utamaduni wa kuwa tegemezi na kudumaza fikra na kumfanya kuwa duni Katika taifa.

Katiba ya nchi inamlinda mtoto wa kike kwa kutambua kwamba mtoto ni yule ambaye huko chini ya miaka 18 na hana sifa za kupiga kura. Lakini wakati huo huo Sheria ya Ndoa 1971 inasema mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 16 anaweza kuoa na msichana mwenye miaka 14 anaweza kuolewa kwa ridhaa ya wazazi.

Sheria hizi mbili zinakinzana na hivyo hazimlindi mtoto wa kike moja kwa moja. “Tutahakikisha kwamba sheria ya ndoa inafanyiwa marekebisho ili iende pamoja na Katiba ya nchi, jitihada zinaendelea kwa kuungana na wanaharakati wote nchini kuleta mabadiliko hasa baada ya kuzindua kampeni ya “Ukanda Huru wa Ndoa za Utotoni” (Child Marriage Free Zone) na Graca Machel.

Tuzo ya CEFM Champion ilishuhudiwa na wadau mbalimbali kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa kuchangia maendeleo, Umoja wa Kimataifa, waandishi wa habari na wanajamii.

JAHAZI NA MASHAUZI KUTIFUANA USIKU WA BABA NA MWANA

$
0
0
jaha1
Usiku wa Baba na Mwana.

Hatimaye makundi mawili yanayoaminika kuwa na mashabiki wengi zaidi katika taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic yatafanya onyesho la pamoja mwezi ujao. Onyesho hilo litafanyika Travertine Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam, Jumapili ya tarehe 22 mwezi Machi.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa makundi hayo mawili kufanya onyesho la pamoja (bila kushirikishwa makundi mengine).Onyesho la kwanza lililopewa jina la Usiku wa Baba na Mwana lilifanyika miaka minne iliyopita ndani ya ukumbi huo huo na inaaminika kuwa hadi leo bado rekodi yake ya mahudhurio pale Travertine haijavunjwa.

Mzee Yussuf na Isha Mashauzi ambao ni wamiliki wa makundi hayo, wameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo ni “Usiku wa Baba na Mwana …Season 2”.Viongozi hao wamesema onyesho hilo ni la kukuza udugu pamoja na kuwakutanisha pamoja mashabiki wao na kamwe halina hata chembe ya wala mpambano.

BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YAANGAMIZA UNGA WA NGANO TANI 70 AMBAO HAUFAI KWA MATUMIZI YA BINADAM.

$
0
0
Mtambo aina ya Kijiko likichukua mchanga kuchanganya na unga ulioharibika kwa lengo la kuangamiza katika kijiji cha Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini ”B” Unguja.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. NGA3NGA2 
Unga wa ngano mbovu tani 70 uliokamatwa ukiwa sokoni na mafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar ukimwangwa eneo la Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini ”B” Unguja tayari kawa kuangamizwa. NGA1 
Magari yakipakia Unga wa ngano mbovu katika godauni lililokuwa la Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) Mnazi mmoja, unga huo haufai kwa matumizi ya binadam.

Wasanii 87 watajwa Tamasha la Pasaka

$
0
0
WASANII 87 mahiri wa muziki wa Injili wa hapa nchini na nje ya nchi wamependekezwa na wadau washiriki kwenye miaka 15 ya Tamasha la Pasaka mwaka huu.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa wadau wa muziki huo wameomba waandaaji wahakikishe wasanii hao wanakuwepo mwaka huu.
 
“Kama mnavyofahamu Kampuni yangu ya Msama Promotion mwaka huu inafanya onesho kubwa la miaka 15 tangu tuanze Tamasha la Pasaka, wadau wetu mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao namna ya kuboresha na wamekuwa wakitutajia aina ya wasanii wanaotaka waje, idadi yao mpaka leo asubuhi (jana) imefikia 87, ni idadi kubwa ambayo haijapata kutokea kuombwa na mashabiki.
 
“Kati ya wasanii hao, 27 ni wa hapa nchini, 15 ni nchi nyingine za Afrika Mashariki , tisa Afrika Kusini, 14 sehemu nyingine za Afrika,  nane Uingereza na waliobaki ni kutoka Marekani,” alisema Msama.
 
Hata hivyo alisema kwa mazingira yaliyopo kamati yake haiwezi kuwaleta wasanii wote hao badala yake watakachofanya ni kukutana na kuteua wachache watakaokuja kutumbuiza kutokana na vigezo vyao.
 
 “Kuna vitu vingi vya kuangalia kabla ya kumpa nafasi msanii, lakini kubwa ni nafasi yake siku ya tamasha, maana wengine wana ratiba zao ndefu kidogo,” alisema Msama.
 
Mwaka huu Tamasha la Pasaka linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam na limekuwa likijiongezea umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa kiroho kupitia matamasha hayo.
 
Umaarufu wa matamasha hayo pamoja na mambo mengine, unatokana na ukweli kuwa yamekuwa yakifanyika kwa ubunifu na umakini mkubwa huku kila mwaka yakiongezeka na kubadili waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi.
 
Baadhi ya nyota waliowahi kutumbuiza katika matamasha hayo ni marehemu Angela Chibalonza kutoka Kenya,nguli wa kutoka Afrika Kusini, Solly Mahlangu ‘Obrigado’, Sipho Makhabane na Rebeka Malope.
 
Wengine ni Ephraim Sekeleti kutoka Zambia, Ambassadors of Christ (Rwanda), Faraja Ntaboba na Solomoni Mukubwa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), 24 Elders  (Uganda) na Anastazia Mukabwa (Kenya).

WAKUTANA KUJADILI MKAKATI WA MRADI WA KIJIJI CHA DIGITALI

$
0
0
DSC_0113
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada ya mchanganuo wa ufumbi wa changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali.

Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
WADAU mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi ambao wamo katika mradi wa kijiji cha dijiti cha Ololosokwan kilichopo wilayani Monduli Arusha wanakutana kwa warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji hicho nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Al Amin Yusuph warsha hiyo imelenga kuangalia changamoto na namna ya kuzitatua ili mradi kuwa na tija kwa wananchi wake.
Yusuph alisema kwamba wadau hao wanapanga mkakati kuangalia vipaumbele na changamoto katika utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitatu.

Alisisitiza kwamba kwa kuwa mradi huo utakuwa na mawasiliano ya kisasa, masomo kwa njia ya Tehama, tiba kwa kutumia mtandao wadau wamekusanyika mjini Bagamoyo kuangalia namna bora ya kuufanya mradi huo uwe endelevu hata kama UNESCO na mbia wake Samsung watajiondoa huko mbeleni.


Aliwataja baadhi ya wadau kuwa ni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Afya na ustawi wa jamii, Samsung, Unesco, wanakijiji wa Ololosokwan, waganga wa jadi wakunga, Taasisi ya elimu na Chuo cha Ufundi cha DIT.
Alisema changamoto ambazo zinaonekana ni lazima ziangaliwe ni pamoja na matumizi ya lugha hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa wengi wa wananchi wa Kimasai hawazungumzi Kiswahili fasaha.

“tunategemea sana Tehama kufanikisha mradi huu, na lugha inayoweza kutumiwa ni Kiswahili, sasa hili ni changamoto ni lazima kuangalia mawasiliano” alisema Yusuph na kuongeza kuwa kuwapo kwa radio ya jamii kutachangia kwa kiasi kikubwa kutoa nafasi ya wananchi wengi kujifunza Kiswahili.

Aidha alisema kwamba mambo mengine ambayo yanaangaliwa katika warsha hiyo ni matumizi ya Tehama (intaneti) na kutoa mafunzo ya namna ya kuhudumia na kufanyia matengenezo mitambo mbalimbali iliyomo katika mradi huo.
DSC_0141
Mwenyekiti wa kikundi cha elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akishiriki kutoa maoni wakati wa warsha hiyo inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani. Aliyesimama ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Alisema nia kubwa ya kukusanya wadau mbalimbali ni kuangalia utekelezaji wa nia ya mradi ya kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwa jamii ya kimasaii ambayo kwa sasa utamaduni na uchumi wake unatishiwa na mabadiliko ya tabia nchi.
“Tunataka maendeleo haya yasaidiwe na mawasiliano. Tunaangalia jinsi ya kutumia mawasiliano kuleta maendeleo” alisema Yusuph.
Alisema ni matumaini yao kwamba wabia wengine wa mradi huu ambao ni kampuni ya simu ya Airtel watatumia uwezo wao kuhakikisha kwamba kijiji hicho kinakuwa hewani muda wote kwa lengo la kurahisisha huduma zinazopatikana kwa njia ya mtandao hasa tiba.
Aidha alisema kwamba pamoja na kuleta maendeleo mradi huo unakusudiwa kuhamasisha amani kati ya koo na makabila mbalimbali yaliyopo wilayani Ngorongoro.
DSC_0082
Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Peter Kitenyi (wa kwanza kulia) akichangia maoni kwenye kikundi cha sekta ya Afya wakati wa kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili jamii ya wafugaji wa kijiji cha Ololosokwan katika utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali huku Mwenyekiti wa kikundi hicho kutoka UNESCO, Bw. Mathias Herman(katikati kulia) akiorodhesha maboresho ya changamoto hizo.
Katika warsha hiyo ambapo wadau wamegawanyika makundi mbalimbali ili kutengeneza hoja za kufanyia kazi kwa ajili ya kufanikisha masuala ya elimu na afya.
Katika elimu wameangalia vikwazo ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni na watoto kuacha shule kwenda kuchunga mifugo.
Ili kukabiliana na kiwango kikubwa cha kutojua kusoma na kuandika kipaumbele kinachofikiriwa ni kuwafikia vijana hao wakiwa machungani kwa kuwapelekea mafunzo kwa njia ya mtandao.
Afisa Mipango wa Elimu wa Unesco, Jennifer Kotta alisema changamoto ya elimu katika kijiji hicho na majirani ni kubwa na kwamba wanachofikiria ni kutumia Tehama ambapo sasa watawafikia vijana kule waliko.
DSC_0110
Wadau mbalimbali wa Elimu, Afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi wanaoshiriki warsha ya wiki moja inayofanyika wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji cha dijiti cha Samsung cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Aidha wamepanga kufunza lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kutanua wigo wa majadiliano wa wakazi wa eneo hilo na watalii wanaofika na kupenda kununua kazi zao.
Warsha hiyo iliyofunguliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini inafanyika wakati vifaa vya kutengeneza kijiji hicho vikiwa vimeshaondoka katika bandari ya Dar es salaam.
Katika masuala ya Afya wadau wameangalia vipaumbele vinavyostahili sasa ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mimba na mtoto.
Wamesema wanawake wa kimasai wanafanya shughuli nyingi kuanzia ujenzi wa makazi na ukamuaji wa maziwa hadi ulezi wa watoto na kusema katika mazingira hayo wanahitaji sana elimu ya uzazi salama.
DSC_0088
Mwenyekiti wa kikundi cha Sanaa na ubunifu kutoka UNESCO, Courtney Ivins (wa pili kushoto) wakijadiliana na wanakikundu wenzake kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utamaduni hususani kwa wakimama wa kimasai wanaotengeneza bidhaa za shanga jinsi ya kuziboresha na kuvutia watalii wanaotembelea hifadhi ya Ngorongoro mpaka kijiji cha Ololosokwan pamoja na jinsi ya kutatua migogoro ya ardhi iliyopo kwenye jamii za wafugaji.
DSC_0084
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye majadiliano na kikundi chake huku wakiangalia changamoto mbalimbali za masuala ya Tehama zinazoikabili kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya kuziboresha ikiwa ni maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali.
DSC_0092
Mwenyekiti wa kikundi cha elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa elimu ya msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sarah Mlaki (wa kwanza kushoto) na wadau kutoka Ololosokwan wakianisha changamoto na utatuzi wa changamoto kwenye sekta ya elimu katika kuboresha utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigiti cha Samsung cha Ololosokwan wakati wa warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
DSC_0097

Mashindano ya gofu NIC Corporate Lugalo Challenge 2015 kufanyika kesho viwanja vya TPDF

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi Shemweta akikabidhi zawadi kwa Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo tayari kwa mashindano ya NIC Corporate Lugalo Challenge 2015 yanayofanyika kesho February 28 kuanzaia saa 7:00 asubuhi kwenye viwanja hivyo yakishirikisha wachezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.


Shindano la NIC Corporate Golf Chalennge linaandaliwa na shirika la bima la taifa NIC na linafanyika kila mwaka kuanzia tangu lilipoanzishwa mwaka 2013 na linashirikisha wachezaji wa rika zote na jinsia zote NIC imeandaa zawadi mbalimbali kwa washindi, ambapo mshindi wa kwanza atapata jiko kubwa la umeme. 

Pia wshindi wengine watapata zawadi mbalimbali zilizotayarishwa kwa ajili yao ambazo ni meza kubwa ya ofisini, mikoba ya akina mama, mabegi ya wanafunzi, Feni , Friji, Microwave na zawadi nyingine nyingi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)5 

Wafanyakazi Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waelezea namna wizara yao inavyoweza kufanikisha Mkakati wa Kitaifa kuhusu matumizi ya Kondomu

$
0
0
 Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Mussa Varisanga akielezea jambo wakati wa kikao cha pamoja na washauri kuhusu masuala ya Kondomu wakati wakijadili Mkatati wa Taifa wa Matumizi ya Kondomu unaoratibiwa na TACAIDS leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mshauri wa Kimataifa kutoka Uganda Bw.Moses Muwonge
 Mshauri wa Kimataifa kutoka Uganda Bw.Moses Muwonge akizungumza na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha pamoja kujadili kuhusu Mkatati wa Taifa wa Matumizi ya Condom unaoratuibiwa na TACAIDS leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshauri kutoka taasisi ya AMCA Bw. Patrick Kauyamwenge.
 Mwakilishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Ngaiza Alex akizungumza wakati wa kikao cha pamoja baina ya maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na washauri kuhusu masuala ya Kondomu wakati wakijadili Mkatati wa Taifa wa Matumizi ya Kondomu unaoratibiwa na TACAIDS leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mshauri wa Kimataifa kutoka Uganda Bw. Moses Muwoge na  Mshauri kutoka taasisi ya AMCA Bw. Patrick Kauyamwenge.
 Afisa Habari wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Zawadi Msalla (katikati) akielezea jambo wakati wa kikao cha pamoja na washauri kuhusu masuala ya Kondomu wakati wakijadili Mkatati wa Taifa wa Matumizi ya Kondomu unaoratibiwa na TACAIDS leo jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM

SERIKALI KUFUFUA BANDARI 14 ZA ZIWA NYASA – WAZIRI MKUU

$
0
0
*Apewa jina la Chifu wa Wanyakyusa, aitwa Mwakabulufu
WAZIRI MKUU Mizengo amesema Serikali imeamua kufufua bandari ndogo 14
kwenye mikoa mitatu inayozunguka Ziwa Nyasa ili kuimarisha usafiri wa
majini kwa wakazi wa Ruvuma, Njombe na Mbeya.

“Tangu mwaka 2006 bandari za kwenye mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya
zilikufa na hivyo kuleta shida ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo
lakini Serikali imeamua kuzifufua bandari hizo na Itungi itakuwa ndiyo
kituo kikuu cha bandari zote katika Ziwa Nyasa,” alisema Waziri Mkuu.

Alikuwa akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Kyela kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika jana jioni (Jumatano, Februari 26, 2015) kwenye
uwanja wa michezo wa Mwakangale na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa
wilaya hiyo.

Alizitaja bandari hizo kuwa ni Ndumbi, Lundu, Njambe, Mkili, Liuli, na
Mbamba bay ambazo ziko mkoani Ruvuma. Nyingine ni Lumbila, Ifungu,
Nsisi, Lupingu na Manda ambazo ziko Njombe wakati bandari za Mbeya ni
Itungi, Kiwira na Matema.

Alisema ili kufanikisha hilo, Serikali imehamisha chelezo (Dry Dock)
kutoka bandari ya Mwanza na kwamba mkandarasi kutoka Kampuni ya
Songoro Marines, ameshaanza  ujenzi wa chelezo hiyo.

“Baada ya kukamilika, Chelezo hiyo, itatumika kutengenezea meli mpya
yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo na kufanya
ukarabati wa meli pindi zinapohitaji matengenezo. Nimeambiwa na
mkandarasi kutaka watamaliza hii kazi ifikapo Juni, mwaka huu,”
alisema huku akishangiliwa na umati huo.


Waziri Mkuu alisema, mbali ya hilo, chelezo hiyo pia itatumika
kutengeneza matishari mawili ya kubebea mizigo ambayo yatakuwa na
uwezo wa kubeba mizigo tani 1,000  kila moja.

“Yatatumika kusafirisha mizigo hiyo hususan mazao ya wakulima kupitia
bandari ndogo zilizopo lakini pia yatasafirisha tani 60,000 za makaa
ya mawe, tani 72,000 za saruji kutoka Mbeya kwenda Malawi na mikoa
jirani; tani 10,000 za mbolea kutoka Dar es Salaam pamoja na chuma
kutoka Liganga na Mchuchuma,” alisema.

“Chelezo hiki kitakapokamilika kitakuwa kikubwa na cha aina yake…
hakuna kingine cha kulinganishwa nacho katika nchi jirani za Malawi,
Zambia na Msumbiji. Itumieni fursa hii kwa kutunza ule mto kwenye
mdomo wa kuingilia bandari ya Itungi, msilime kwenye kingo za mto,”
aliongeza.

Mapema, akizungumza na wakazi wa kata ya Lusungo mara baada ya kuweka
jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Lusungo, Waziri Mkuu Pinda
alisema daraja hilo ni kiungo muhimu kwenye barabara hiyo iendayo
kwenye bandari ya Matema.

Aliwataka wakazi wa kata hiyo walitunze daraja hilo ili liweze
kuwasaidia kusafirisha bidhaa na mazao wanayolima. Ujenzi wa daraja
hilo, ambalo limejengwa kupitia mfuko wa barabara, lina urefu wa mita
50 na upana wa mita 7.3 pamoja barabara yenye urefu wa mita 600 kutoka
kwenye maingilio ya daraja hilo, limegharimu kiasi cha sh. bilioni 3.7
huku ujenzi wake ukiwa umekamilika kwa asilimia 99.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Pinda alipewa jina la MWAKABULUFU
na Chifu Ernest Mwailemale wakati akisimikwa kuwa kiongozi wa eneo
hilo la Lusungo. Waziri Mkuu alivishwa mgolole na kupewa mkuki ili
autumie kuilinda nchi dhidi ya maadui kutoka pande zote.

Akizungumza mara baada ya kumsimika Waziri Mkuu, Chifu Mwailemale
mwenye umri wa miaka 91, alisema jina hilo ni la babu yake mzaa baba
ambaye aliwahi kutawala eneo hilo. Hata hivyo, hakutaja ni mwaka gani.

Alipoulizwa maana ya jina hilo, Chifu Mwailemale ambaye wakati wote
alikuwa akizungumza Kiswahili kwa ufasaha alisema: “Jina hili halina
maana maalum bali na heshima kwa sababu lilikuwa la Chifu aliyetawala
eneo hili,” alisema na kufafanua kuhusu umri wake: “Nina miaka 91 kwa
maana nilizaliwa tarehe 25 Septemba mwaka 1924,” alisema Chifu huyo
ambaye anaelezwa kupigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, FEBRUARI 27, 2015.

Maofisa wa Ofisi ya Rais - Utumishi wakiwa katika kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kati ya Utumishi na mikoa ya Mtwara,Lindi, Kilimanjaro na Dodoma.

$
0
0
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) akiongoza kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kilichofanyika kati ya Utumishi na mikoa ya Mtwara,Lindi, Kilimanjaro na Dodoma. 
 Baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kilichofanyika kwa kuunganisha mikoa ya Mtwara, Lindi, Kilimanjaro  na Dodoma.
 Maofisa wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao kazi kwa njia ya video (Video Conference) kati ya Utumishi na mikoa ya Mtwara,Lindi, Kilimanjaro na Dodoma. Uendeshaji wa vikao kwa njia ya mtandao umepunguza gharama na muda uliokuwa unatumika kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

MIMBA, UTORO KYELA VYAMTISHA WAZIRI MKUU

$
0
0

* 94 wapewa ujauzito, 645 watoroka shule wilayani humo
* Aaagiza waliohusika wasakwe, wafikishwe mahakamani

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Kyela pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwasaka na kuwakamata wale wote waliowapa ujauzito wanafunzi na kuwafikisha mahakamani mara moja ili liwe fundisho kwa wengine.

Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye shule ya sekondari ya Mwaya,
kwenye kata za Ikusya na Lusungo na wakazi wa mji wa Kyela, jana
(Jumatano, Februari 26, 2015), Waziri Mkuu alisema elimu ni jambo la
msingi sana kwa kizazi cha sasa na kijacho na Serikali haiwezi kuona
fursa za elimu zikichezewa kiasi hicho.

“Haiwezekani hata kidogo! Serikali hatuwezi kuwa tunahimiza ujenzi wa
madarasa kila kukicha halafu watoto wanaopaswa kusoma kwenye hizo
shule wao wanatoroka. Hawa watoto wana wazazi, iweje kuwe na utoro
kiasi hiki?” alihoji.

“DED na DC wabaneni wazazi na mabinti walioharibiwa masomo, ni lazima
watawataja wanaume waliohusika kuwapa mimba. Kwa kuanzia anzeni na hao wa mwaka jana ambao ni wasichana 11. Wakiwekwa ndani wachahe itakuwa fundisho kwa wengine,” alisema.

Akielezea ukubwa wa wa tatizo hilo kwenye shule za sekondari peke
yake, Waziri Mkuu alisema mwaka 2010, wasichana 26 walipewa ujauzito;
mwaka 2011 (wasichana 22); mwaka 2012 (wasichana 19); mwaka 2013
(wasichana 16) na mwaka 2014 (wasichana 11). “Jumla yao ni 94, hii ni
idadi kubwa sana. Akina baba waacheni watoto hawa wamalize masomo,
msiwaharibie maisha,” alikemea.


Akichanganua takwimu za utoro kwa wanafunzi haohao wa sekondari,
Waziri Mkuu alisema mwaka 2010 walitoroka wanafunzi 95; mwaka 2011
(wanafunzi 160); mwaka 2012 (wanafunzi 212); mwaka 2013 (wanafunzi 90)
na mwaka 2014 (wanafunzi 88).

“Katika kipindi cha miaka mitano, jumla yao wote hawa ni 645. Hali hii
haivumiliki na jambo liko ndani ya uwezo wa Halmashauri yenu.
Fuatilieni wazazi wa hawa watoto na DC na DED ni lazima tabia hii
ikomeshwe mara moja,” alionya.

Aliwaasa watoto wa wilaya wawe makini na masomo na waache tabia ya
utoro na kupenda mambo ya maisha. “Wanangu someni kwa bidii, achaneni
na haya mambo mengine. Ukipoteza nafasi masomo kidato cha tatu au cha
nne, maisha yako yanakuwa yameharibika,” aliwaasa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwageukia wanaume wanaowafuata watoto wa
shule na kuwataka kimapenzi wakati wanawake wa wilaya ni wengi kuliko
wanaume. “Wlaya hii ina wanaume 106,012 na wanawake 115,478. Sasa ni
kwa nini msiwafuate hao akinamama wakubwa ambao ni wengi kuliko ninyi?
Acheni huo mchezo, waacheni hawa watoto wa kike wamalize masomo yao,”
alisisitiza.

Mapema, akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Wilaya ya Kyela,
Bi. Margareth Malenga alisema kushamiri kwa biashara kwenye mpaka wa
Kasumulu, mkoani Mbeya, kumechochea kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi
wanaotoroka shuleni na kwenda kujishughulisha na biashara ndogondogo
mpakani hapo.

“Aidha, kukosekana kwa chakula kwenye baadhi ya shule za msingi na
sekondari wilayani hamu, ni sababu nyingine inayofanya wanafunzi
waache masomo na kwenda kufanya biashara ndogondogo kwenye mpaka wa Kasumulu,” aliongeza.

Alisema hali hiyo imechangiwa na kuwepo kwa baadhi ya kaya masikini
zinazoshindwa kuwalipia gharama za masomo watoto wao.

Akifafanua, Bi. Malenga alisema katika kipindi cha mwaka 2012 hadi
2014, wavulana 414 na wasichana 159 waliochaguliwa kujiunga na elimu
ya sekondari waliacha shule kwa sababu za utoro.

Kuhusu elimu ya msingi, Bi. Malenga alisema, wanafunzi wapatao 711
wametoroka shule lakini kutokana na jitihada zilizofanyika, wanafunzi
155 wamerudishwa shuleni. “Wanafunzi 556 waliobakia wanaendelea
kutafutwa kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji ili waweze
kuwarudishwa kuendelea na masomo,” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alisema wameanzisha utaratibu wa kila Mkuu wa
Shule kuwasilisha ripoti ya mahudhurio ya wanafunzi kwa watendaji wa
kata na vijiji kila Ijumaa ambapo tangu utaratibu huo uanze,
wamefanikiwa kudhibiti utoro kwa asilimia 91.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, FEBRUARI 27, 2015.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images